Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

WAKANDARASI MIRADI YA UMEME WATAKIWA KUANZISHA YADI MAALUM

$
0
0

Na Veronica Simba – Chato

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewataka wakandarasi wote nchini wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini, kuwa na Yadi maalum za kuhifadhi vifaa katika maeneo wanakotekeleza miradi hiyo, ili kuondoa kisingizio cha kutowaunganishia wananchi umeme kutokana na kutokuwepo na vifaa.

Aliyasema hayo, jana Septemba 16, 2018 katika Kijiji cha Kahumo wilayani Chato, akiwa katika ziara ya kazi, ambapo pia aliwasha umeme rasmi kijijini hapo. “Kuanzia sasa nawaelekeza muwe na Yadi zenu ambapo mtahifadhi vifaa vyote vya kazi na sisi Serikali tutazikagua. Maneneja wa TANESCO kagueni Yadi hizo.”

Waziri alitaja vifaa vya kazi vinavyotakiwa kuwepo katika Yadi hizo kuwa ni pamoja na nyaya za umeme, nguzo, transfoma pamoja na mita za Luku.

Aidha, akiwa katika Kijiji cha Magiri wilayani humo, ambako pia aliwasha umeme rasmi, Waziri Kalemani aliwaasa wananchi kuepukana na vishoka wakati wanapotaka kutandaziwa mfumo wa nyaya za umeme katika makazi yao.

Aliwataka wananchi kujiridhisha na uhalali wa mafundi watakaowatumia kuwatandazia mfumo wa nyaya, katika Ofisi za TANESCO zilizopo katika maeneo yao. Akifafanua, alisema majina ya mafundi wenye sifa yatatundikwa katika Ofisi hizo ili kuwarahisishia wananchi kuwatambua hivyo kuepukana na vishoka.

Waziri aliwahamasisha wananchi kuhakikisha wanalipia huduma ya kuunganishiwa umeme huo wa bei nafuu, ambao ni shilingi 27,000 tu ili wanufaike na Mradi husika wa Umeme Vijijini (REA), kwani Mradi huo utakapoisha, watalazimika kuunganishiwa umeme kwa bei ya kawaida, ambayo ni kubwa.

Akizungumza na wananchi wa Chato Mjini katika mkutano wa hadhara, Waziri alitoa maelekezo kwa wakandarasi wa REA, kuhakikisha wanawaunganishia umeme wananchi wasiopungua 10 kwa mkupuo kila siku, tofauti na ilivyo sasa ambapo wengi wao wamekuwa wakiwaunganishia umeme wananchi wachache tu katika maeneo wanakotekeleza miradi hiyo.

“Natoa rai kwa wataalam wangu wa TANESCO na REA nchi nzima kuhakikisha wakandarasi wanaotekeleza miradi hii nchi nzima, wanawaunganishia umeme wananchi wasiopungua 10 kwa mkupuo kwa siku moja, kila tunapokwenda kuwasha umeme.”

Hata hivyo, Waziri Kalemani aliwapongeza watendaji wa TANESCO na REA kwa kazi nzuri wanayofanya ambapo alisema kuwa hali ya umeme nchini imeimarika na kwamba umeme haukatiki-katiki.

Waziri Kalemani yuko katika ziara ya kazi Kanda ya Ziwa, ambapo mbali na Mkoa wa Geita, atatembelea pia Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme pamoja na kuzungumza na wananchi.


Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Magiri wilayani Chato, Mkoa wa Geita akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme, Septemba 16, 2018.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akiwasha umeme katika moja ya nyumba za wakazi wa Kijiji cha Kahumo wilayani Chato, Mkoa wa Geita, kuashiria kuwashwa rasmi kwa umeme kijijini humo. Tukio hilo lilifanyika Septemba 16, 2018, wakati Waziri akiwa katika ziara ya kazi.
Wananchi wa Kijiji cha Kahumo wilayani Chato, Mkoa wa Geita, wakimpokea kwa bashasha Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (mwenye shati la bluu-kulia), alipowasili kijijini hapo jana, Septemba 16, 2018, kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo.
Kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati na Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani, Mbunge wa Nyang’hwale Hussein Kassu na Mbunge wa Igunga Seif Gulamali; wakifurahia jambo, wakati wa Mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Kalemani Chato Mjini, akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme na kuzungumza na wananchi, jana Septemba 16, 2018.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Chato, Elias Makory, akizungumza wakati wa mkutano wa Waziri wa Nishati, Dkt, Medard Kalemani (hayupo pichani) na wananchi wa Kijiji cha Kasenga, wilayani humo; jana Septemba 16, 2018 akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.
Kutoka kushoto ni Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Ziwa, Mhandisi Macleen Mbonile, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Geita, Mhandisi Joachim Ruweta na Mhandisi wa Umeme kutoka Wizara ya Nishati, Salum Inegeja, wakijadiliana jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) wilayani Chato, kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme, jana Septemba 16, 2018.

Waziri wa Nishati, Dkt, Medard Kalemani (kulia), akiwaonesha wananchi wa Kijiji cha Kasenga wilayani Chato, kifaa cha Umeme Tayari, kinachotumika kuunganisha umeme pasipo kutandaza mfumo wa nyaya (wiring). Waziri alikuwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme pamoja na kuzungumza na wananchi, jana Septemba 16, 2018. Pamoja naye pichani (kutoka kushoto) ni Meneja wa TANESCO Wilaya ya Chato, Nyabingiri Nyaonge na Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini katika eneo hilo, Ibrahim Saidi.

SERIKALI YAANZA KUTOA MSAMAHA WA KODI KWA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (wa pili kulia), akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Singida Mhandisi Leonard Kapongo (wa pili kushoto), wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja katika kijiji cha Muhalala, wilayani Manyoni, mkoani humo.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Singida Mhandisi Leonard Kapongo (kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia), wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja kilichopo wilayani Manyoni, mkoani Singida.
Mhandisi Mshauri kutoka kampuni ya NIMETA Consult anayesimamia ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja wilayani Manyoni, Mhandisi Patrick Lujinya (kulia), akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (wa pili kulia), kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa kituo hicho ambao ujenzi wake umefikia asilimia 60 mpaka sasa, mkoani Singida.
Muonekano wa baadhi ya nyumba za watumishi watakaoishi mara baada ya ujenzi wa Kituo cha Ukaguzi wa Pamoja kukamilika katika kijiji cha Muhalala, Wilayani Manyoni, Mkoani Singida. Ujenzi wa kituo hicho utakamilika mwezi Februari mwakani.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano



Serikali imesema imeshaanza kutoa misamaha ya kodi kwa mikataba ya ujenzi na matengenezo ya miradi ya maendeleo ikiwemo barabara, viwanja vya ndege na madaraja ambayo ilitakiwa kusamehewa kulipa kodi ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo. 

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akikagua hatua za ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja (One Stop Inspection Station), wilayani Manyoni mkoani Singida, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kuwa mradi huo umechelewa kukamilika kutokana na mkandarasi kutopata msamaha wa kodi kama jinsi ilivyopangwa na hivyo kuathiri mtiririko wa fedha katika utekelezaji wa wake. 

"Serikali imeanza kutekeleza misamaha ya kodi iliyokwama katika miradi inayoendelea na inayotarajiwa kuanza hapa nchini ikiwemo huu mradi na mingine mingi", amesema Waziri Mhandisi Kamwelwe. Mhandisi Kamwelwe amemtaka mkandarasi wa Kampuni ya Impresa di Construction Ing E. Mantovani S. p. A con socio unico Via Belgio anayejenga kituo hicho kuhakikisha anakamilisha mradi huo ndani ya muda aliyoomba kuongezewa kwani hataongezewa muda mwingine. 

"Nahitaji kituo hichi kikamilike ifikapo mwezi Februari mwakani, kwani haya ni maazimio ya pamoja ya nchi za wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kupunguza ucheleweshwaji wa usafirishaji wa mizigo kupitia barabara ya kati kuelekea nchi jirani", amesisitiza Mhandisi Kamwelwe. 

Aidha, Waziri Kamwelwe ameeleza kuwa ukamilikaji wa vituo hivyo utapunguza muda na gharama za usafirishaji wa mizigo kupitia barabara ya Ukanda wa Kati (Central Corridor) kwani hadi sasa magari makubwa yanasimama vituo 31 kutokea Dar es Salaam hadi mipaka ya Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). 

Awali akitoa taarifa ya mradi kwa Waziri huyo, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Singida Mhandisi Leonard Kapongo ameeleza kuwa maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha Manyoni umefikia asilimia 60 na ujenzi huo unaenda sambamba na ujenzi wa kituo kilichopo Nyakanazi mkoani Kagera. 

Ameongeza kuwa ujenzi wa kituo hicho utahusisha uwekaji wa mizani ya mwendo, ofisi za Mamlaka ya Mapato (TRA), Polisi, Uhamiaji, kituo cha mapumziko na mafunzo kwa wasafirishaji, maegesho ya magari makubwa na nyumba za watumishi. 

Mradi wa ujenzi wa vituo vikuu vya ukaguzi wa pamoja wa magari makubwa yanayoenda nje ya nchi unahusisha vituo vitatu ambavyo ni Vigwaza, Manyoni na Nyakanazi kwa umbali wa takribani kilomita 500 kutoka kituo kimoja hadi kingine ikiwa na lengo la kuondoa msongamano wa magari makubwa kwenye vituo vilivyopo. 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

WANANCHI WAELEZA FURAHA YAO YA BARABARA YA JUU (FLYOVER) YA TAZARA

MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA YAPUNGUA KWA 90%-MAJALIWA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Vyombo Vinavyopambana na Biashara ya Dawa za Kulevya kutoka nchi za Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam Septemba 17, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Vyombo Vinavyopambana na Biashara ya Dawa za Kulevya kutoka nchi za Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam Septemba 17, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Vyombo Vinavyopambana na Biashara ya Dawa za Kulevya kutoka nchi za Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam Septemba 17, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Vyombo Vinavyopambana na Biashara ya Dawa za Kulevya kutoka nchi za Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam Septemba 17, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Bibi Jo Dedeyne ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Taasisi za Umoja wa Mataifa zinazoshughulikia dawa za kulevya na uhalifu (United Nations Office on Drugs na Crime – UNODC) baada ya kufungua Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Vyombo vinavyopambana na Dawa za Kulevya kutoka nchi za Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Septemba 17, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WAZIRI MKUUKassim Majaliwa amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini yamepungua kwa asilimia 90 baada ya Serikali kufanikiwa kudhibiti biashara hiyo.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Septemba 17, 2018) baada ya kufungua mkutano wa 28 wa wakuu wa vyombo vinavyopambana na dawa za kulevya kutoka nchi za Afrika ujulikanao kama (28th HONLEA- Afrika), jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere(JNICC), unashirikisha wajumbe zaidi ya 120 kutoka nchi 54 za Afrika unatarajiwa kutoka na maazimio ya namna ya kutokomeza biashara ya dawa za kulevya katika mataifa hizo.

Waziri Mkuu amesema lengo la mkutano huo ni kubadilishana uzoefu na kupanga mikakati ya pamoja kuhusu udhibiti na mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya katika nchi hizo. “Ni lazima tuwe na mikakati ya pamoja ya kudhibiti uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya barani Afrika. Hata hivyo ni muhimu kudhibiti njia zote zinazotumika kusafirisha dawa za kulevya.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Tanzania inaendelea na mikakati ya kupambana na uzalishaji wa dawa hizo ikiwemo mirungi na bangi, ambayo inapandwa kwa kuchanganywa na mazao ya chakula. Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Tanzania ni nchi ya kwanza katika bara la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuanzisha vituo vya utoaji wa matibabu kwa waathirika wa dawa za kulevya mwaka 2011.

Amesema hadi kufikia mwishoni mwa 2017, jumla vituo sita vya kutolea matibabu vilianzishwa, ambapo zaidi ya waathirika 6,500 wa dawa za kulevya aina ya heroin walijiandikisha na kupatiwa matibabu. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini yameathiri sekta mbalimbali ikiwemo ya afya, uchumi na jamii, uchunguzi umebainisha kuwa kati ya asimilia 20 hadi 50 ya watumiaji wanamaambuzi ya ugonjwa wa ukimwi.

Amesema ni muhimu kwa nchi zote kuunga mkono na kuimarisha mifumo ya kisheria ya kimataifa katika udhibiti wa biashara za dawa za kulevya, ambao hutegemea mikataba yote ya msingi ya Umoja wa Mataifa.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, SEPTEMBA 17, 2018.

TRA YATOA ELIMU YA MAADILI, MABADILIKO YA SHERIA ZA KODI KWA WATUMISHI WAKE TANGA

$
0
0
Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi Diana Masalla kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu akiwasilisha mada kuhusu mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa watumishi wa TRA mkoani Tanga kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao ili waweze kutekeleza na kusimamia sheria za kodi kwa ufanisi na kutoa huduma stahiki kwa wateja.

Na Veronica Kazimoto, Tanga

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa elimu ya maadili na mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa watumishi wake mkoani Tanga kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao ili waweze kutekeleza na kusimamia sheria za kodi kwa ufanisi na kufuata maadili ya kazi ipasavyo.

Akizungumza wakati akiwasilisha mada ya Mabadiliko ya Sheria ya Kodi ya Mwaka 2018, Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi Diana Masalla kutoka TRA Makao Makuu amesema kuwa, kila mtumishi wa TRA anapaswa kujua sheria za kodi na mabadiliko yake kwa undani ili aweze kutoa huduma stahiki kwa wateja.

"Kila mwaka wa fedha unapoingia, Serikali kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hufanya mabadiliko mbalimbali ya sheria na kanuni za ukusanyaji wa kodi, hivyo ni muhimu kila mtumishi wa TRA kujua mabadiliko na kanuni hizo kwa lengo la kutoa huduma stahiki kwa wateja wetu,"  alisema Masalla.

Aidha, Meneja huyo wa Elimu kwa Mlipakodi amewataka watumishi hao kufuata sheria na kuepuka upendeleo wakati wote wanapotoa huduma kwa wateja wanaotembelea ofisi za TRA.

Naye, Afisa Maadili Mwandamizi Adelaida Rweikiza kutoka TRA Makao Makuu, amewaambia watumishi hao kuwa, ni muhimu kuzingatia maadili kila wanapotimiza wajibu wao ili kuondoa malalamiko ambayo yanaharibu taswira nzuri ya TRA.

"Kila mmoja wetu ana jukumu la kuilinda taswira ya mamlaka yetu, hivyo ni wajibu wetu kuzingatia maadili ikiwa ni pamoja na kutumia lugha nzuri kila tunapowahudumia wateja," alisema Rweikiza.

Timu ya Maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania inaendelea kutoa elimu ya maadili na mabadiliko ya Sheria za Kodi ikiwa ni pamoja na Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi kwa watumishi wa TRA na wafanyabiashara wa Mikoa ya Kanda ya Kasikazini.
Afisa Maadili Mwandamizi Adelaida Rweikiza kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu akizungumza na watumishi wa TRA mkoani Tanga wakati wa utoaji elimu ya Maadili na Mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa watumishi hao kwa lengo la kuwajengea uwezo ili waweze kutekeleza na kusimamia sheria za kodi kwa ufanisi na kutoa huduma stahiki kwa wateja.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Tanga Masawa Masatu akizungumza wakati wa utoaji elimu ya Maadili na Mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa watumishi TRA mkoani hapo kwa lengo la kuwajengea uwezo ili waweze kutekeleza na kusimamia sheria za kodi kwa ufanisi na kutoa huduma stahiki kwa wateja.
Afisa Kodi Mwandamizi Gelas Kinabo wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Tanga akichangia hoja wakati wa utoaji elimu ya Maadili na Mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa watumishi TRA mkoani hapo kwa lengo la kuwajengea uwezo ili waweze kutekeleza na kusimamia sheria za kodi kwa ufanisi na kutoa huduma stahiki kwa wateja.

QNET: Kusaidia Maendeleo ya Michezo Afrika

$
0
0

Sekta ya michezo barani Afrika inakua kwa kasi sana. Iwe katika michezo ya riadha (ambayo Afrika ya Mashariki na pembe ya Afrika huwa wanaongoza katika bara zima na hata katika mashindano ya kiulimwengu kwa ujumla), au michezo mingine. Bara la Afrika linabadilika taratibu kuwa mabingwa katika shughuli mbalimbali za michezo ambayo mpaka hivi karibuni zimetawaliwa na nchi za ulaya na Asia.

Kwa ujumla katika mchezo wa mpira wa miguu Afrika imeonyesha viwango vikubwa kwa timu za kiafrika kufanya vizuri katika mashindano ya kidunia. Tunashukuru umaarufu wa mchezo wa mpira wa miguu miongoni mwa mashabiki ndani ya Afrika na wadhamini wapya wenye mapenzi mema wanaojitokeza, wapenzi wa michezo na wadau mwengine.

Miongoni mwa wale ambao wameingia katika ushirika na vyama vikubwa vitatu vya mpira wa miguu barani Afrika ni QNET, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja yenye asili ya Asia ambayo biashara yake iko Afrika na ambayo kwa hakika dunia nzima inaichukulia kuwa ni miongoni mwa mashirika makubwa katika tasnia hiyo.

Mapema mwaka huu, QNET ilisaini mkataba wa ushirikiano wa muda wa miaka miwili na mabingwa wa ligi za vilabu vya Afrika: Ligi ya Mabingwa CAF, Ligi ya Kombe la Shirikisho na Ligi ya Kombe la Super Cup katika mpango wa udhamini unaolenga katika wigo mpana wa kidigitali na shughuli ambazo zinalenga kukuza ushirikiano wa mashabiki na wawakilishi wa QNEt (IRs) Afrika.

Akizungumzia kuhusu udhamini huo, CEO wa QNET bwana Trevor Kuna alisema kwamba ushirikiano huo na CAF ni uwekezaji muhimu sana kwa kampuni, ambayo unaendana na wateja wake na jamii ya Afrika kwa ujumla. Ikiwa inawianisha bidii za kimichezo na biashara ya QNET. Bwana Kuna alihamasisha: “Kama mpira wa miguu, QNET inaunganisha dunia na kuhamaisha ari ya kufanya kazi kwa pamoja kama timu miongoni mwa wawakilishi wake (IRS) na kila mmoja anayehusika katika biashara yetu. Kufanya kazi kama timu na utendaji thabini ni mambo ambayo yako sambamba katika mpira wa miguu na biashara ya masoko ya mtandao”

Udhamini huu pia ni kilemba kingine katika kofia ya QNET na inaonyesha tena jitihada za kampuni ya mauzo ya moja kwa moja katika kuthamini maadili ya michezo: Umakini, kufanya kazi kwa bidii na kuongeza bidii mpaka kiwango cha mwisho. Ushirikiano huu unakuja kama jukumu la QNET kama mshirika rasmi wa mauzo ya moja kwa moja wa Klabu ya Mpira wa Miguu wa Manchester City, shughuli ambayo imeiwezesha QNET kuunganisha msisimko wa mpira wa miguu na shauku ya mashabiki katika msisimko wa mauzo ya moja kwa moja na msukumo wa wawakilishi (IRs) wa QNET

Aliongeza kwamba ushirikiano wa kampuni hii na CAF umepelekewa zaidi na shauku ya kampuni hii kutengeneza fursa za ushiriki ikiwa inalenga mashabiki wa mchezo wa mpira wa miguu katika bara la Afrika pamoja na kuandaa matamasha ya kuangalia mechi kwaajili ya wasambazaji na IRs katika nchi mbalimbali barani Afrika.

Ushirikiano huu pia ni ushahidi wa kuuzika kwa mchezo wa mpira wa miguu wa Afrika kama bidhaa – jambo ambalo limehamasisha makampuni ya kiwango cha kimataifa kama QNET kuonyesha nembo yao katika mchezo ambao unatazamwa zaidi duniani.

QNET ina maono bora ya kibiashara katika bara la Afrika ambayo ina endesha shughuli zake katika maeneo ya Afrika ya Magharibi na Afrika ya Mashariki ambako kampuni ya mauzo ya moja kwa moja imetoa fursa za ujasiriamali kwa maelfu ya watu kupitia bidhaa zake zinazoweza kubadilisha maisha zinazotolewa kupitia mfumo wao wa biashara ya mtandao (e-commerce) kwenda kwa wateja na IRs.

Bidhaa za kampuni zinajumuisha pamoja na bidhaa za huduma binafsi, bidhaa za majumbani, saa, vito, safari za mapumziko, elimu na zingine nyingi – ambazo zinauzwa kupitia ofisi za QNET na mawakala wao walioko duniani kote, pia kutoka kwa waendeshaji walioko ndani ya maeneo tofauti katika nchi mbalimbali.

QNET ambayo inasherehekea kutimiza miaka 20 mwaka huu, na ambayo inajigamba kwa kukua kwake kutoka kuwa kampuni ndogo yenye bidhaa moja kwenda kuwa kampuni yenye zaidi ya bidhaa 100 za aina mbalimbali tofauti, inabakia kuwa imejidhatiti kutoa programu za mafunzo ya mara kwa mara, kuhamasisha mwenendo imara wa maadili ya utendaji, kuwasaidia wasambazaji wake kwa kuwapatia vifaa vya matangazo na vifaa vya kufanyia biashara na kuendelea kutafuta au kutengeneza bidhaa sahihi kwaajili ya wateja wao walioko dunia nzima.

Janja janja ya Tanzania Remix watapeli bilioni 3.7 serikali

$
0
0
  Naibu waziri wa uchukuzi Mhandisi Atashazita Nditiye akitembelea viwanja vya fidia kwa wananchi waliopisha upanuaji wa uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
TANZANIA Remix watapeli bilioni 3.7 fedha za serikali ambazo zilikuwa kwaajili ya fidia kwa wahanga wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Fedha hizo zilkuwa kwaajili ya kununua maeneo ya wananchi waliokuwa wananishi kipunguni A na Kipunguni Mashariki.

Akizungumza na wanachi wa kata ya Luhangwa Kata ya Msongola manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaamleo, Naibu waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye alipotembelea viwanja vya fidia vya Luhangwa amesema kuwa serikali inataka viwanja ambavyo havina mgogoro na vilivyolipiwa kwa kuwa serikali ishalipia fedha viwanja vyote 537 ambavyo vinadhamani ya shilingi bilioni 3.7.

" Tanzania Remix ninawapa wiki moja kupima na kuwalipwa wananchi fedha zao za viwanja kulingana na mkataba wao. Msipofanya hivyo Jumatatu ya Septemba 24,2018 hamtaru nyumbani mtaenda sehemu tofauti na nyumbani " Amesema Nditiye.

"Tanzania Remix imelipwa Fesha ya viwanja 537 ambavyo  vinatakiwa kuwapa  wananchi wa kipungunj A na Kipunguni Mashariki kama ya fidia kwaajili ya upanuzi wa uwanja wa ndege na kwakuwa hawajawalipa wenyevinjwa leo tuhairishe shughuli ya ukaguzi wa viwanja na tuwape muda Tanzania Remix kuwalipa wenye viwanja kwa kadili ya walivyosaini mkataba".

Nditiye ameiagiza Tanzania Remix ifikapo Septemba 24 mwaka huu iwalipe fedha wananchi atakagua viwanja visivyo na mgogoro na wananchi vilivyopangiliwa vizuri kila kiwanja kikijitegemea na vyenye barabara zinazoeleweka.

Wananchi wa Luhangwa  wanena.
Mwenyekiti wa mtaa wa  Luhangwa, Salum Kipendo amesema kuwa yeye pamoja na anaowaongoza hatujalipwa fedha za viwanja kadiri ya mkataba unavyosema kwa asilimia 40 kwa Asilimia 60.

Nae Mrisho Hasimu miliki wa shamba amesema kuwa mimi na baadhi ya wenzangu hatujalipwa fedha za ununuzi wa viwanja kadili ya mkataba tuliosaini sisi na serikali kwaajili ya viwanja vya wananchi waliopisha  upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
 Naibu waziri wa uchukuzi Mhandisi Atashazita Nditiye akizungumza na wananchi wa Luhanga kata ya Msongola Manispaa ya Ilala jijni Dar es Salaam alipotembelea viwanja vya fidia za wananchi  waliopisha upanuzi wa uwanja wa ndege na kuwapa  Tanzania Remix wiki moja kwaajili ya kuwalipa wananchi stahiki zao kwani serikali imeshatoa fedha kwaajili ya ununuzi wa viwanja hivyo.
Mmilikiwa shamba eneo la Luhangwa,Seif Mbonde  akizungumza na Naibu waziri wa uchukuzi Atashazita Nditiye wakati alipotembelea eneo la viwanja vya fidia za wananchi walipisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa malimu Julius Nyerere Luhanga kata ya Msongola manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja wa ndege (TAA) Richard Mayongela akizungumza na wanachi wa Luhangwa Kata ya  Msongola jijjnj Dar es Salaam na kuwaambia kuwa wao mamlaka ya viwanja vya ndege wameshalipa fedha zote kwaajili ya viwanja waliobakia ni Tanzania Remix ambao wanatakiwa kuwalipa fedha hizo.
Mmiliki wa shamba katika eneo la Luhangwa Mrisho Hashim akizungumza na waandishi wa habari katika eneo Luhangwa kata ya Msongola jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kutolipwa sitahiki yake kadili ya Mkataba wao kati ya Tanzania Remix na baadhi ya wananchi wenye mashamba eneo la Luhangwa kata ya Msingola  Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam ikiwa bado hawajalipwa fedha za viwanja vyao kadili ya mkataba unavyosema.  



TBL YAADHIMISHA SIKU YA UNYWAJI BIA KISTAARABU DUNIANI KWA VITENDO

$
0
0
Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL Group), chini ya kampuni mama ya ABInBev, mwishoni mwishoni mwa wiki iliadhimisha siku ya Unywaji wa Pombe Kistaarabu diniani kwa kushiriki kampeni mbalimbali za kuhamashisha matumizi ya vinywaji vizuri kwenye jamii. Mbali na uhamasishaji huo uliofanyika katika mikoa mbalimbali nchini ambako kampuni inaendesha biashara zake pia kampuni ilitoa vifaa vya kupima kiwango cha ulevi kwa madereva kwa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani. Akiongea wakati wa kukabidhi vifaa hivyo katika hafla iliyofanika mwishoni mwa wiki,Afisa Mawasiliano wa TBL, Amanda Walter alisema kuwa kupitia sera ya kampuni ya Smart Drinking Goals,siku zote itahakikisha inahamasisha matumizi ya vinywaji vyenye kilevi kiafya na burudani na sio kuleta athari kwa jamii.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la polisi (SACP), Fortunatus Muslim, (watatu kutoka kulia) akiongea wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya kupima ulevi kwa madereva vilivyotolewa na TBL Group katika maadhimisho ya Siku ya Unywaji bia kistaarabu,mwishoni mwa wiki, wengine pichani (wa nne kutoka kulia ) ni Afisa Mawasiliano wa TBL, Amanda Walter na Maofisa wengine kutoka Jeshi la Polisi. 3.Afisa Mawasiliano wa TBL Group, Amanda Walter akiongea wakati wa hafla hiyo. Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la polisi (SACP), Fortunatus Muslim katika picha ya pamoja na askari waliohudhuria hafla hiyo pamoja na Afisa Mawasiliano wa TBL,Amanda Walter.

RC MAKONDA APONGEZA JESHI LA POLISI KWA KUSIMAMIA AMANI NA UTULIVU UCHAGUZI JIMBO LA UKONGA

$
0
0

index
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amelipongeza Jeshi la Polis kwa kazi kubwa ya kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kipindi chote cha kampeni za uchaguzi Jimbo la Ukonga hadi uchaguzi uliofanyika siku ya Jana na kumalizika salama pasipo uvunjifu wa amani.
1
RC Makonda ametoa pongezi hizo leo alipokutana na Makamanda na maafisa wa polisi ambapo amesema anajivunia kuona uchaguzi wa Ukonga umemalizika salama bila fujo wala uvunjifu wa amani.
2
Aidha RC Makonda amewapongeza wananchi kwa kulinda aman na kulifanya jiji la Dar es salaam kuzidi kuwa na amani masaa 24.
3
Pamoja na hayo RC Makonda amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro na Kamanda wa Polis Kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa kwa kuwa na vijana shupavu, wakakamavu na wenye morali ya kuwatumikia wananchi.
DAR ES SALAAM NI KITOVU CHA AMANI NA USALAMA MASAA24.

WAZIRI JENISTA MHAGAMA AZIAGIZA TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI ZINAPOSAIDIA JAMII ZIKUMBUKE MAHITAJI YA MAKUNDI MAALUM

$
0
0

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (wapili kulia), Naibu Wake, Mhe. Stella Ikupa (wakwanza kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba (mwenye miwani), wakiangalia jinsi wanafunzi wasioona wanavyotumia mashine maalum za kuandika nukta nundu, kwenye chuo cha walemavu Yombo jijini Dar es Salaam Septemba 17, 2018. Waziri Jenista amepokea mashine hizo maalum Braille Machines,  11 zilizotolewa na WCF ikiwa ni utekelezaji wa sera ya kusaidia jamii (CSR) ili zitumike kwanye taasisi za wanafunzi wasioona.
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, (pichani), ameziagiza taasisi za umma na binafsi nchini zinapotoa fedha za kusaidia jamii (CSR), zikumbuke kuna kundi maalum la walemavu nchini ambao nao wanahitaji huduma maalum kama wanavyohitaji wengine.
Mheshimiwa Waziri aliyasema hayo jioni ya Septemba 17, 2018 wakati akipokea mashine maalum za kuandika kwa wanafunzi wasioona (Braille Machines) kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwenye chuo cha walemavu Yombo jijini Dar es Salaam.
“Tunapoona kwenye shule za msingi wanahitaji madawati, tukumbuke kwamba, wapo wanafunzi kwenye vyuo,  wapo wanafunzi kwenye shule za msingi, ambao ni wenye ulemavu ambao pengine badala ya madawati, wao wanahitaji viti vya kuwaongezea mwendo, au kama tunatoa computer mpakato, tukumbuke kwamba tunazo shule na vyuo watoto wetu, vijana wetu wanasoma wenye ulemavu wangehitaji mashine hizi zenye kuandika nukta nundu ili kuwasaidia wenye ulemavu ili na wao wafaidike na elimu katika nchi yetu ya Tanzania.” Alisema Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama wakati akihutyubia kwenye hafla ya kukabidhi mashine hizo.
Alisema, Amefarijika kuona maagizo ya Ofsii ya Waziri Mkuu, yameweza kutekelezwa na taasisi ambayo iko chini ya ofisi ya Waziri Mkuu, kwa kusaidia kundi hilo la wenye ulemavu.
“Vifaa nitakavyovikabidhi leo ni maalum kwa wenzetu wasioona  na ni vya wanafunzi walioko katika vyuo mbalimbali kwenye nchi yetu siyo hapa Yombo peke yake.” Alifafanua.
Aliupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa msaada huo mkubwa na kwamba fedha walizotumia kununua vifaa hivyo ni kuwekeza kwa vijana ili kujiandaa kuwa na utashi na weledi na kujiandaa kuingia kwenye soko la ajira nchini.
Akimkaribisha Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, ameitaka jamii ya watu wenye ulemavu nchini kujiamini, kujitambua, kujikubali na kutioa bidii katika kazi wanazofanya.
“Kama ni mwanafunzi weka bidii katika masomo, na kama ni mwajiriwa weka bidii katika kazi yako kwani huo ndio ukombozi kwa mtu mwenye ulemavu.” Aliasa Mhe. Ikupa.
Alisema vifaa vilivyopokelewa ni muhimu sana kwa watu wenye ulemavu hususan kwa kundi la wasioona, kwani vitawawezesha katika dhama  nzima ya ujumuishwaji mtu mwenye ulemavu anapopatiwa vifaa vinavyoweza kutekeleza majukumu yake anakuwa anawezeshwa kuwa katika ujumuishwaji kwa hiyo atajumuishwa katika elimu lakini hatimaye atajikuta amefikia kwenye eneo la ajira na hatimaye kujikomboa na kuon dokana na utegemezi na uombaomba.
“Nikiwa kama Naibu Waziri ninayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, nitoe pongezi za kipekee kwa uongozi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa tendo hili kubwa ambalo mmelifanya.” Alipongeza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) Bw. Masha Mshomba alisema, Mwaka jana (2017) WCF ilifanya Mkutano wa kwanza wa mwaka na katika mkutano ule Mfuko uliahidi kupitia mpango wake wa kusaidia jamii (CSR) utasaidia watu wenye ulemavu na kwamba ahadi hiyo imetekelezwa.
“Tumetoa msada wa mashine hizi maalum (Braille Machines) 13 zenye thamani ya Shilinhgi Milioni 33.8 na tunaimani kwamba zitawasaidia sana wenzetu wasioona ili kuwafanya washiriki kwa ufanisi katika kujifunza.” Alisema.
Alisema, Sekta ya Hifadhi ya Jamii, WCF ikiwa ni miongoni mwa sekta hiyo, moja ya majukumu ambayo serikali inasisitiza ni kuhakikisha ushiriki wa sekta katika kuondoa changamoto kwenye makundi maalum na hatua hiyo ya kutoa msada ni utekelezaji wa maagizo hayo ya serikali.
Katika awamu hii ya kwanza taasisi zilizofaidika ni pamoja na Chuo cha Ufundi kwa Walemavu, Yombo na Sabasaba kilichoko Singida, Shule za Uhuru Mchanganyiko ya Dar es Salaam, Shule ya Msingi Ndanda, iliyoko Mkoani Mtwara, Shule ya msingi Biharamulo, Shule ya Msingi Mgeta Mseto Bukoba Mkoani Kagera. 

 
Mhe. Waziri Jenista Mhagama (kushoto), akiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Anayeshughulikia masuala ya wenye ulemavu), Mhe. Stella Ikupa, wakati akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba akizungumza kwenye hafla hiyo
 Mhe. Stella Ikupa, (Kulia), akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba
 Baadhi ya wanafunzi wanaosoma kwenye chou cha ufundi kwa watu wenye ulemavu Yombo jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye hafla ya kupokea msada wa mshine za kuandika nukta nundu (Braille Machines)
 Baadhi ya wanafunzi wanaosoma kwenye chou cha ufundi kwa watu wenye ulemavu Yombo jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye hafla ya kupokea msada wa mshine za kuandika nukta nundu (Braille Machines)
 Wanafunzi wakijadiliana wakati wa hafla ya kupokea msaada wa mashine za kuandika nuka nundu (Braille Machines) Septemba 17, 2018.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (anayeshuhulikia masuala ya Wenye ulemavu), Mhe. Stella Ikupa, akilakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF Bw. Masha Mshomba na viongozi wengine, wakati akiwasili kwenye hafla hiyo.
 Waziri Mhe. Jenista Mhagama, (katikati), akipokelewa na Kaimu Mkuu wa Chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu Yombo jijini Dar es Salaam, (Kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, wakati akiwasili chuoni hapo Septemba 17, 2018.
 Wanafunzi wakishangilia
 Bw. Mshomba akijadiliana na wasaidizi wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Bi. Laura Kunenge, na Afisa Uhusoiano Mwandamizi, Bw. Fulgence Sebera.
 Waziri Mhagama, akimkabidhi mashine hiyo, Kaimu Mkuu wa Chuo cha ufundi kwa wanachuo walemavu Yombo, Bi. Mariam, wapili kushoto), huku Naibu Waziri Mhe. Stella Ikupa (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa WCF Bw. Masha Mshomba wakishuhudia.
  Waziri Mhagama, akimkabidhi mashine hiyo, Kaimu Mkuu wa Chuo cha ufundi kwa wanachuo walemavu Yombo, Bi. Mariam. Kushioto ni Bw. Masha Mshomba.
 Kaimu Mkuu wa chuo cha ufundi kwa walemavu Yombo, Bi. Mariam, (kushoto) akitoa neon la shukrani.
 Picha ya pamoja.
 Mmoja wa wanafunzi akionyesha kipaji cha kusakata muziki wa Bongo Flava
 Mhe. Jenista Mhagama, akikishajihisha kikundi cha kwaya ya 
 Mhe, Waziri akimkabidhi mbunge wa Ndanda Mhe. Cecil Mwambe.
Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi mashine mwakilishi kutoka Shule ya Uhuru Mchanganyiko ya Dar es Salaam, Bi.Mwilongo Mtamike.

SERIKALI ITUUNGE MKONO WAWEKEZAJI -MULOKOZI

$
0
0
kurugenzi wa kampuni ya kiwanda cha pombe kali cha Mati Super Brands Ltd cha mjini Babati mkoani Manyara, David Mulokozi (kulia) akitoa maelezo kwa viongozi wa mkoa huo walipotembelea kiwanda chake hivi karibuni.PICHA: GIFT THADEY
Wafanyakazi wa kampuni ya kiwanda cha pombe kali cha Mati Super Brands Ltd cha mjini Babati mkoani Manyara, wakiendelea na shughuli za uzalishaji kwenye kiwanda hicho.PICHA: GIFT THADEY

NA GIFT THADEY

“Rais John Magufuli amekuwa akitangaza kila wakati kuwa serikali yake ni serikali ya viwanda, hivyo viongozi wa serikali wanapaswa kutuunga mkono sisi wawekezaji na siyo kutukandamiza kwani tunalipa kodi pindi tukizalisha bidhaa zetu na kuziuza, tunawalipa mishahara wafanyakazi wetu na pia sisi wenyewe kama kampuni tunanufaika kupitia uwekezaji tulioufanya, tunanufaika wote,” hivi ndivyo anavyoanza kuzungumza mkurugenzi wa kiwanda cha pombe kali cha Mati Super Brands Ltd cha mjini Babati mkoani Manyara, David Mulokozi.

Mulokozi anasema kuna mamlaka zinapaswa kutoa ushirikiano kwa wawekezaji tangu awali, wanapoanzisha kiwanda na kuwapa elimu juu ya nini wanapaswa kufanya na siyo kusubiri mara baada ya kuanza uzalishaji wanajitokeza na kudai kuwa wamekosea hivyo watozwe faini na kufungia uzalishaji bila sababu ya msingi.

Anasema mamlaka za serikali zilizopo kisheria ikiwemo mkemia mkuu wa serikali, mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) mamlaka ya mapato nchini (TRA) na shirika la viwango nchini (TBS) zinapaswa kutoa elimu kwa wawekezaji ili wafuate hatua zinazopaswa kufuatwa pindi wanapotaka kuanza uwekezaji ili waeleweshwe juu ya mchakato huo.

Anasema TRA ndiyo mamlaka ya mwisho kutoa kibali cha kufanya shughuli za biashara nchini hivyo walisikitishwa kiwanda chao kufungiwa na mamlaka nyingine bila sababu za msingi ili hali walikuwa wanalipa kodi serikali na walifuata hatua zote zinazotakiwa.

“Tangu tuanze kufanya shughuli kwenye hiki kiwanda chetu hatujawahi kulipa kodi TRA chini ya shilingi milioni 30 kwa mwezi na pia tumesababisha kuwepo kwa ajira kwa wananchi wa mkoa wa Manyara hivyo wakati kiwanda kilipofungwa kwa miezi mitatu watumishi wetu pia waliathirika kwani walikosa kazi kwa muda huo,” anasema Mulokozi.

Anasema kutokana na sera nzuri za Rais John Magufuli waliamua kuanzisha kiwanda hicho wakati ambapo kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda iliposhika kasi illi kuunga mkono kauli mbiu hiyo hivyo wanatakiwa kuungwa mkono kwani miongoni mwa viwanda vilivyoanzishwa kipindi cha utawala wake ni kampuni ya Mati Super Brands Ltd.

Mikakati yao

Mulokozi anasema wanatarajia kufungua kiwanda kingine ambacho kitakuwa cha kuzalisha dawa za binadamu katika eneo hilo hilo la Babati mkoani Manyara na hivi sasa wapo kwenye mchakato wa utafiti kupitia wataalamu waliobobea kwenye fani hiyo waliopo hapa nchini na nje ya nchi.

“Bado kuna changamoto ya urasimu kwa baadhi ya watumishi wa idara za serikali kwani mara nyingi tunapokwenda kwa maofisa wa serikali ili watupatie ushirikiano juu ya unanzishwaji wake inatupa wakati mgumu kwani badala ya kutuambia tupite hapa na pale wenyewe wanakuwa wageni kama sisi kwani hawatambui lolote,” anasema.

Anasema wameanzisha kiwanda kingine kupitia kampuni nyingine ya Manyara Breweries iliyosajiliwa miezi miwili iliyopita kwa ajili ya kufanikisha kiwanda kingine na pia wao ni wakulima wakubwa wa mazao ya mtama, mahindi, maharage na dengu kwenye mashamba yao yalliyopo eneo la Galapo wilayani Babati.

Uboreshaji maslahi ya wafanyakazi wao

Meneja uzalishaji wa kiwanda hicho, Gasper Mlay anasema kupitia kampuni hiyo, wafanyakazi wao wamepatiwa mtaji wa kuanzisha kikundi cha kuweka na kukopa (Saccos) hivyo kuboresha maslahi ya watumishi ambao kutokana na hali hiyo wanakuwa wanapata muda mzuri wa kupumzika baada ya kutoka kazini.

Mlay anasema wana wafanyakazi wengi na wanapokuwa nao lengo siyo kuwaajiri na kuwapa mishahara pekee, pia wanawapa elimu ya malezi ya familia na utawala wa fedha zao, kwani ni taaluma waliyoipata vyuoni ambayo wafanyakazi wengine hawana.

Anasema wanahakikisha kuwa wanachokipata kinakuwa na tija na pia wanapokuwa na tafrija huwa wanawaalika familia za wafanyakazi wao na wenzi wao ili kuhakikisha upendo, mshikamano na ukaribu unakuwepo kwa familia ikiwemo mahusiano mazuri ya baba, mama na watoto.

“Tukiona sehemu kuna tatizo kuna daktari wa kampuni ambaye yupo na timu yake ataweza kuisaidia familia hiyo kwa namna mbalimbali ikiwemo ushauri nasihi kwa lengo la kuboresha maisha yao na pia kuendelea kufanikisha kampuni,” anasema Mlay.


Historia ya kiwanda

Mulokozi anasema yeye kwa kushirikiana na wenzake wawili ambao awali walikuwa waajiriwa, walisajili kampuni yao Octoba mwaka 2017 na kuanzisha kiwanda hicho kinachozalisha pombe kali za ZEC na Strong katika ujazo tofauti tofauti kwenye kata ya Bagara mjini Babati.

Anasema uwepo wa kiwanda hicho umewanufaisha wananchi wa eneo hilo ikiwemo kutoa ajira kwa mafundi kwani tangu ujenzi wake uanze wametoa ajira za kudumu 31 na ajira za muda mfupi 19 hivyo jumla wana wafanyakazi 50.

Anasema kupitia Saccos ya kampuni hiyo wafanyakazi wake wanaboresha yao ikiwemo kusomesha watoto na pia wamewapa maagizo ndani ya muda wa miaka mitano wafanyakazi wake wamenunua viwanja na wajenge nyumba kwa lengo la kuboresha maisha yao.

KATIBU MKUU WA UVCCM KUZINDUA ALBAM YA MSANII MGEGO SEPTEMBA 30/2018 MKOANI IRINGA

$
0
0
NA FREDY MGUNDA,IRINGA

KATIBU mkuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) taifa kuwa mgeni rasmi katika uzindua albam ya nyimbo za injili ya msanii James Mgego wa mkoani Iringa  inayoitwa “Achani Mungu Aitwe Mungu” na uzinduzi huo utafanyika katika ukumbi wa HIGHLAND HALL uliopo mjini iringa tarehe 30 /09 /2018.

Akizungumzia uzinduzi huo msanii wa nyimbo za injili James Mgego alisema kuwa anatarajia kuzindua albam yenye nyimbo tisa zilizotengenezwa katika studio za Nice zilizopo mkoani Iringa.


Mgego alisema kuwa mgeni rasmi atakuwa katibu mkuu wa umoja wa vijana ndugu Raymond Mwangwala(MNEC) na viongozi wengi wa serikali na wakisiasa kutoka mkoani Iringa na nje ya mkuoa wa Iringa.


Katika uzinduzi huo kutakuwa na kwaya mbalimbali ambazo zitatumbuiza kama vile TAC kwaya Anglicana, Nuru kwaya Anglicana,TAG Mlandege,Mhimidini Mlandege,Kwaya ya vijana kanisa kuu,kwaya mkuu kihesa,uinjilisti KKKT Ipogolo, uinjilisti KKKT PHM frelimo,kwaya ya vijana kitwilu,RC Mshindo,ACT fellowship,Faith kwaya tumain, RC kichangani kihesa,Sayuni Anglican Ipogolo na Elishadai Anglican Ilula.


Aidha Mgego alisema kuwa kutakuwepo na waimbaji maalufu na mashuhuri wa nyimbo za injili ndani na nje ya mkoa wa Iringa watakuwepo kama vile DR Tumaini Msowoya,Nesta Sanga,Ntimiza Rwiza,Samson Kihombo,faraja kigula,Mwl Senje,mama masawe mwamvita,Petro Chetenge,Raymond Mwalisu,Tukuswiga Ikoso na wengine wengi.


Mgego alisema kuwa anawakabiribisha wananchi wote katika uzinduzi huo ambapo hakutakuwa na kiingilio chochote kile.

MFAHAMU BWANA MAHER ALBARWANI, ALIYESAFIRI NA PIKIPIKI TOKA OMAN MPAKA TANZANIA KUSHUHUDIA TAMASHA LA URITHI JIJINI DODOMA

$
0
0
Bw. Maher Albarwani (aliyevaa kofia) akiwa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Urithi Festival.
Hii ndio Pikipiki aliyosafiri nayo Bw. Maher Albarwani kutoka Oman mpaka Tanzania akipita nchi mbalimbali Duniani

Balozi wa Heshima kutangaza Pori la Akiba-Selous Miss Journalism Tanzania Witness Kavumo(kushoto) akiwa na Bw. Maher Albarwani wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Urithi jijini Dodoma 
Mdau wa mambo ya Utalii Bw. Festo Mazuguni (Kushoto) akiwa na Bw. Maher Albarwani uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Kutoka kushoto ni Balozi wa Heshima kutangaza Pori la Akiba-Selous Miss Journalism Tanzania Witness Kavumo, Bw. Maher Albarwani aliye safiri na pikipiki kutoka Oman mpaka Tanzania na Naomi Mbilinyi ambaye ni Afisa Utalii kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) wakiwa katika Banda la Utalii.
Picha na Fredy Njeje

KAMPENI YA 'LET'S DO IT' YAWAKUTANISHA PAMOJA WATANZANIA KUFANYA USAFI

$
0
0
 Wadau mbalimbali wa Mazingira wakifanya usafi kwenye ufukwe wa Coco, Kinondoni Jijini Dar es salaam katika kuadhimisha siku ya usafi duniani iliyofanyika mwishoni mwa wiki kupitia kampeni ya ‘Let’s Do it’ iliyolenga kuondoa taka kutoka kwenye mazingira ya asili. #KINONDONI
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akizungumza na wadau mbalimbali wa Mazingira kwenye ufukwe wa Coco katika kuadhimisha siku ya usafi duniani iliyofanyika mwishoni mwa wiki kupitia Kampeni ya ‘Let’s Do it’ iliyolenga kuondoa taka kutoka kwenye mazingira ya asili. #KIGAMBONI
 Wadau mbalimbali wa Mazingira wakifanya usafi eneo la Ferry Sokoni, Kigamboni jijini Dar es salaam katika kuadhimisha siku ya usafi duniani iliyofanyika mwishoni mwa wiki kupitia kampeni ya ‘Let’s Do it’, iliyolenga kuondoa taka kutoka kwenye mazingira ya asili.
#MBEZI MWISHO - UBUNGO
Ilikuwa ni siku ya kuadhimisha siku ya Usafi Duniani iliyofanyika mwishoni kwa wiki iliyopita wakazi wa Mbezi Mwisho, Ubungo jijini Dar es Salaam walikufanyika na kufanya usafi katika maeneo yao ya biashara na majumbani kupitia kampeni ya #LetsDoit. Zoezi hili la usafi kwa Tanzania lilifanyika katika miji 33 ikiwa na Temeke, Kinondoni, Morogoro, Arusha n.k. 
Kila mmoja akiwajibika kukusanya pamoja taka taka ili kuweka mazingira yao salama.
Uongozi wa Kata ya Msigani ukiwa mbele ya vifurushi vya taka taka walizokusanya pamoja na wananchi wao.
Moja ya vibao vilivyowekwa mitaani kuzuia utupaji wa taka taka ovyo.
Vijana waliojitokeza katika suala la usafi wa mazingira.

SOKONI KIWALANI

$
0
0
 Mfanyabiashara  wa samaki waliokaushwa katika soko  la Kiwalani Dar es Salaam akiwawauzia samaki wananchi wa eneo hilo  ambapo samaki mmoja huuzwa kati ya shilingi elfu moja ( 1000) hadi 6000 (Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)

Mfanyabiashara wa viungo vya mboga  katika soko la Kiwalani jijini Dar es Salaam akiwauzia  wananchi  ambapo fungu la nyanya anauza 200 hadi 300

WAZIRI MBARAWA AZINDUA MRADI WA MAJI WA KIWALANI LEO JIJINI DAR

$
0
0
*Awataka Dawasa wawaunganishie maji wananchi walipe kidogo kidogo

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amezindua mradi wa maji wa Kiwalani  na kuwataka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) kuhakikisha wanawaunganishia wananchi wa eneo hilo maji kwa mkataba ili walipe kidogo kidogo kwakuwa serikali imetumia fedha nyingi sana kufanikisha mradi huona Malengo ya Serikali ni kuona watanzania wanapata maji kwa asilimia 90.

Amezungumza hayo wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliokuwa umekamilika tayari na wananchi wa Kiwalani wakianza kupata maji safi na salama kuitia vizimba vitano vilivyokuwa vimeshajengwa tayari.


Profesa Mbarawa amesema, kumalizika kwa mradi huu ni moja ya ahadi ya serikali ya kuhakikisha kila mwananchi na eneo la Kiwalani wana zaidi ya miaka 30 hawajawahi kuwa na maji safi ya Dawasa  na wamekuwa wanatumia  chumvi katika kipindi chote hicho.

Amesema Profesa Mbarawa, ukiachana na mradi huo mpaka sasa serikali bado ina miradi mingine ikiwamo mradi wa Bilioni  133.2 ambao ni mradi wa kutoka Benki ya dunia na maji yatakayozalishwa hapo yatapatikana maeneo ya Dar es Salaam na Bagamoyo.

Amesema, Mradi mwingine ni wa Usambazaji maji wa Kiluvya, Salasala, Kimara na Goba utakaogharimu Bil 74.46, huku akisisitiza zaidi katika miradi ukiwamo mradi wa maji taka wenye thamani ya Bil 156.64 ambao yote kwa amoja ikikamilika itahakikisha inaleta manufaa kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani.

"kuna Visima 21 katika  mradi wa Kimbiji Mpera tayari vimeshakamilika  na kabla ya 2020 maji yatapatikana kwa maeneo yote ikiwamo Kigamboni ambapo kumekuwa na changamoto ya maji safi kwa muda mrefu sasa,".

Waziri Mbarawa ameeleza kuwa, anatambua kuna baadhi ya maeneo yana changamoto ya maji na baadhi ya maeneo hayo ni Gongo la Mboto, Pugu,Kinyerezi na maeneo ya karbu  na kwa namna Dawasa mpya inavyofanya kazi kwa kasi inaonesha changamoto ya maji itakuwa ni historia ndani ya Mkoa wa Dares Salaam na Pwani.

Amemalizia kwa kuwaasa wananchi kununua maji ya Dawasa yenye gharama nafuu  na kuchana kununua maji ya maboza wanayouziwa kwa ei kubwa tofauti na Dawasa anbao wanauza Unit moja sawa na  lita 1000 kwa sh 1664 na sasa kununua maji ktk magari umekwisha.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi  na Maji Taka Mkoa wa Dar es Salaam (Dawasa) Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa miradi yote itakapokamilika wakazi wa Dar es Salaam na Pwani watapata maji ya uhakika.

Luhemeja amesema kuwa, ndani ya siku 100 za Dawasa Mpya watahakikisha miradi inakamilika na mingine wakandarasi wakiingia kazini ili kufanikisha upatikanaji wa maji kwa wakazi wote na wakitimiza hitaji la kuongeza wateja wapya 200,000 kutokana na miradi hiyo  ya maji.

Pamoja na hilo, Luhemeja amesema kuwa moja ya mkakati mwingine wa Dawasa  mya ni kuona wanaongeza ukusanyaji wa mapato kwa kufikia Bilioni 12 ikiwamo kuwafuatilia wale wote wenye madeni.

Mratibu wa Mradi wa Kiwalani Mhandisi Ramadhani Mtindasi amesema kuwa mradi wa Kiwalani ni Km 13.32 ukiwa na vizimba vinane lakini mpaka sasa tayari wameshajenga vizimba vitano na karibuni watamalizia vitatu. na ukiwa umekamilika mwishoni  wa mwezi wa nane.

Amesema mradi huo mpaka sasa umeweza kuata Wateja wapya 450  na waliounganishwa ni  246 ila wakati wa ujenzi wa mradi huu waliata Changamoto kubwa sana kwa kuwa eneo hilo lina mkondo wa maji  wakati wa umewakaji mitaro mitaro 

Amemalizia kwa kusema mradi huo una awamu tatu, na tayari awamu ya kwanza na ya pili umekamilika kwa  asilimia 100 limekamilika. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa (wapili kushoto) kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah  Kaluwa (wakwanza kushoto) wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa mradi wa maji Kiwalani Bom Bom jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa wakifungua  mradi wa maji Kiwalani Bom Bom jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza machache na kumkaribisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, kuzungumza  wananchi wa Kiwalani  Bom Bom leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame  Mbarawa, (wapili kushoto), akionyeshwa ramani ya mradi wa maji  katika kata Kiwalani Bom Bom na  Mratibu wa Mradi wa Kiwalani Mhandisi Ramadhani Mtindasi leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, akiwa ameambatana na watendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa),wananchi wa Kiwalani Bom Bom wakielekea sehemu ya mrad wamaji.
Baadhi ya watendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa)   (Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)

NDITIYE AITAKA TAA IPATE VIWANJA VYAKE 537 VYA FIDIA KWA WANANCHI WALIOPISHA UPANUZI WA UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU JULIUS NYERERE

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (mbele katikati) akikagua eneo lenye viwanja 537 vilivyopo eneo la Msongola wilayani Ilala, Dar es Salaam kwa ajli ya kuwapatia wananchi walipoisha upanuzi wa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mawalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Richard Mayongela


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akimsikiliza mmoja wa wananchi wenye mashamba eneo la Msongola, Ilala, Dar es Salaam, Mrisho Kawete (wa kwanza kushoto) ambao hawajalipwa na Kampuni ya Tanzania Remix iliyochukua mashamba yao kwa ajili ya kuwapatia wananchi waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Richard Mayongela (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa wananchi wa maeneo ya Msongola, Ilala, Dar es Salaam wanaodai malipo ya maeneo yao kwa Kampuni ya Tanzania Remix ili yaweze kugawiwa kwa wananchi waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) akisikiliza kwa makini
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akikagua orodha ya majina na taarifa ya wananchi waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wanaotakiwa kupatiwa viwanja na kampuni ya Tanzania Remix. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Richard Mayongela (wa kwanza kushoto) akionesha taarifa hiyo na katikati ni Afisa Ardhi Mkuu wa TAA Bi. Sesilia Mwing’uri

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) akimsikiliza mwakilishi wa Tanzania Remix (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo kuhusu viwanja 537 wanavyotakiwa kuwapatia wananchi waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Richard Mayongela

………………….

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameielekeza Mamlaka ya Viwanja va Ndege Tanzania (TAA) kufuatilia na kupata viwanja vyake 537 kutoka kwa kampuni ya Tanzania Remix kama makubaliano ya mkataba yalivyo kwa ajili ya kuwapatia wananchi waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam (JNIA)

Nditiye ameyasema hayo katika ziara yake ya kukagua viwanja 537 kwenye eneo la Msongola lililopo wilaya ya Ilala, Dar es Salaam ambapo kampuni ya Tanzania Remix ilipewa jukumu na TAA ya kuandaa viwanja hivyo takribani miaka mitano sasa ili viweze kugawiwa kwa wananchi waishio maeneo ya Kipunguni A na Kipunguni Mashariki, Dar es Salaam waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam kwa nia njema ili Serikali iweze kuendeleza na kupanua uwanja huo.

Nditiye amesema kuwa atafika tena kwenye eneo hilo baada ya wiki moja kukagua hatua iliyofikiwa ya upatikanaji wa viwanja hivyo kwa kuwa jambo hilo limechukua muda mrefu na Serikali haiko tayari kuona jambo hilo likiendelea pasipo kufika mwafaka kwa kuwa lina sura ya ujanja ujanja na uongo uongo ambao hauko wazi ambapo wananchi wasio na hatia wanaumia bila sababu

Amefafanua kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia TAA imeilipa Kampuni ya Tanzania Remix kiasi cha shilingi bilioni 3.7 ili waweze kuandaa viwanja ambavyo vitakabidhiwa kwa wananchi hao waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa JNIA. “Tumetembelea eneo hilo, tumejionee wenyewe, mmesikia wananchi wakiwa wanalalamika kuwa Tanzania Remix hawajawalipa wananchi mashamba yao ili yapimwe viwanja na kugawiwa wananchi waliopisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa JNIA. TAA wana mkataba kati yao na Tanzania Remix na ninaamini TAA wamewavumilia sana Tanzania Remix. Nadhani sasa ni wakati TAA washikilie mkataba unasemaje na muanze kuchukua hatua kwa kuwa jambo hili limechukuwa muda mrefu, wananchi wako tayari kuachia viwanja na kupokea viwanja, hatuwezi kuona wananchi wananyanyaswa,” Nditiye amesema.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Bwana Richard Mayongela amesema kuwa hadi hivi sasa kampuni ya Tanzania Remix imegawa viwanja 58 tu kwa wananchi kati ya viwanja 537 vinavyohitajika kugawiwa kwa wananchi na kazi hiyo imechukua muda mrefu kukamilika na hivyo wanaichonganisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi walioridhia na kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa JNIA kwa nia njema. Mayongela amewaomba wananchi waendelee kuwapa ushirikiano na kuvumilia jambo hili ili liweze kufanyiwa kazi na hakuna haki ya mwananchi yeyote itakayopotea kwa kuwa wananchi kwa uzalendo wao wamepisha eneo husika ili waweze kuona maendeleo ya taifa lao. “Mkataba huu ulikuwa ni wa miaka miwili ila bahati mbaya huu ni wa mwaka wa nne au wa tano unaenda na mkataba umeisha muda wake japo sisi tulilipa pesa nao watupe viwanja. Nimeelekeza wanasheria wapitie mkataba husika na kama utakuwa haujatekelezwa, TAA na wananchi tutachukua hatua ya kudai kampuni ya Tanzania Remix, hatutaki kesi na wananchi hawatak kesi ila wanataka haki yako,” amesema Mayongela.

Akiwa ziarani humo, Nditiye amezungumza na baadhi ya wananchi ambao maeneo yao ya Msongola yametwaliwa na Kampuni ya Tanzania Remix ili yaweze kuchukuliwa, kupimwa, kuwekwa miundombinu mbali mbali na kugawiwa kwa wananchi waliopisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa JNIA . Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake mbele ya Mhandisi Nditiye, Bwana Mrisho Kawete amesema kuwa kampuni hiyo haijakamilisha malipo yote kwa wananchi hao hivyo hawako tayari kwa maeneo yao kuchukuliwa na kupatiwa wananchi waliopisha upanuzi. Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Luhanga, Kata ya Msongola iliyopo wilayani Ilala, Dar es Salaam Bwana Lwembu Henjewele amesema kuwa wananchi wanaunga mkono jitihada za Serikali za kupanua uwanja huo na wameridhia maeneo yao wapatiwe wananchi wanaohitajika kulipwa fidia ila tu kampuni ya Tanzania Remix ikamilishe malipo kwa wananchi wake

BancABC Tanzania partners with MasterCard and Vodacom to introduce online payment solutions

$
0
0


Mkuu wa Kitengo cha Hazina BancABC Tanzania Barton Mwasamengo akiongea na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki baada ya kuzindua huduma ya Vodacom MasterCard Virtual card. Huduma ya Vodacom Virtual Card ni maalum kwa kulipia huduma na bidhaa kwa kupitia M-Pesa kwa njia ya mtandao na itatumika ndani na nje ya nchi ikiwa ni ushirikiano baina ya BancABC, Vodacom Tanzania na MasterCard.

Mkuu wa Kitengo cha Hazina BancABC Tanzania Barton Mwasamengo (kushoto), Raghav Prasad Rais wa MasterCard Ukanda wa Sub African Sahara (kati kati) na Hisham Hendi Kaimu Mkurugenzi Vodacom Tanzania (kulia) wakipiga makofi baada ya kuzindua kuzindua huduma ya Vodacom MasterCard Virtual card jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Huduma ya Vodacom Virtual Card ni maalum kwa kulipia huduma na bidhaa kwa kupitia M-Pesa kwa njia ya mtandao na itatumika ndani na nje ya nchi ikiwa ni ushirikiano baina ya BancABC, Vodacom Tanzania na MasterCard.

Mkuu wa Kitengo cha Hazina BancABC Tanzania Barton Mwasamengo (kushoto), Raghav Prasad Rais wa MasterCard Ukanda wa Sub African Sahara (kati kati) na Hisham Hendi Kaimu Mkurugenzi Vodacom Tanzania (kulia) wakishikana mikono baada ya kuzindua kuzindua huduma ya Vodacom MasterCard Virtual card jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Huduma ya Vodacom Virtual Card ni maalum kwa kulipia huduma na bidhaa kwa kupitia M-Pesa kwa njia ya mtandao na itatumika ndani na nje ya nchi ikiwa ni ushirikiano baina ya BancABC, Vodacom Tanzania na MasterCard.
 

BancABC Tanzania, which is part of Atlas Mara a London listed entity, has made yet another step ahead of the market by partnering with MasterCard and Vodacom Tanzania through M-Pesa service to introduce online payment solutions – The Vodacom MasterCard Virtual card for both local and international purchases. The service will enable local businesses and merchants to accept interoperable digital payments, many for the first time. Consumers are now able to make quick, easy and secure payments with their mobile money wallets at any time.

The virtual card will allow M-Pesa mobile wallet holders to make payments on any local or international website or app so long as MasterCard is accepted for payment without the need for a bank account or credit card. Customers can request the virtual card from the M-Pesa USSD menu or soon on the M-Pesa app and top the card up via the wallet. Once the card is topped up with funds, the virtual card is ready for use.

Speaking in Dar es Salaam during the launch of the Vodacom MasterCard Virtual card, the BancABC Tanzania Head of Treasury Barton Mwasamengo said currently we are living in a world where payments are processed every fraction of a second, financial institutions are increasingly challenged to improve the profitability of today’s business whilst they accommodate a steady stream of new transactions, channels and technologies. Due to that factor, BancABC is striving to expand the various channels of its transactions processing systems to new levels by collaborating with other partners in the market to increase its penetration with an objective of taping into the unbanked, Mwasamengo said.

Through partnerships like these, we will be able to accomplish our digital channels vision by providing tailor made solutions for our customers. The Vodacom MasterCard Virtual card is one of the many digital initiatives to be rolled out in the Country, added Mwasamengo.

He added that collaboration between industry leaders in payments, technology and financial services means life-changing solutions can be developed and rolled out rapidly to make a tangible difference in the lives of Tanzanians by allowing them to buy and pay for goods and services more easily than ever before.

Speaking at the same event, BancABC Tanzania Head of Digital Silas Matoi said that the Vodacom MasterCard Virtual card extend convenience on payment methods as it is a hustle free solution whereby the user will not be required to go through any other additional procedures to get a card, as long as one is M-Pesa registered customer can quickly create a card and use the card details to pay for your online purchase.

The service we have launched today provide interoperability to the Global E-commerce as M-Pesa customers easily access to Global MasterCard E-commerce merchants. (Paying world-wide to all MasterCard enabled merchant site), said Matoi adding that the service is affordable and cost effective solution to the citizens.

Due to its free nature, where there are no charges associated during card issuance and upon performing transaction online in comparison to other existed card products added Matoi

Tigo na Clouds Wazindua Msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote

$
0
0
Tamasha la kusisimua zaidi la muziki na utamaduni Afrika Mashariki na Kati, Tigo Fiesta 2018 – Vibe Lama Lote sasa lipo tayari kukonga mioyo na 100% mziki wa nyumbani katika mikoa 15 ya nchi. Kauli mbiu ya Tigo Fiesta 2018 ni Vibe Kama Lote, ikiashiria burudani maridhawa na ladha ya kumbukumbu zisizofutika zinazoendana na msimu huu nchini kote.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga alibainisha kuwa, msimu wote wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote utashuhudia burudani 100% kutoka kwa wasanii wa kitanzania, kufuatia mafanikio makubwa ya mfumo uliotumika mwaka jana. 

Shangwe zinatarajiwa kuanza mjini Morogoro siku ya Jumamosi tarehe 29 Septemba.‘Muziki ni nguzo muhimu ya kampuni yetu, kwa hiyo Tigo Fiesta 2018 itadumisha asili yake ya kuvumbua na kukuza vipaji vya Kitanzania. Lengo letu kuu ni kukuza tasnia ya muziki na kutoa fursa za ajira kwa vijana na jamii yote kwa ujumla’ William alisema. 

Naye Katibu Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, Gardner G. Habash alisema kuwa katika historia yake ya miaka 17, Tigo Fiesta imekuwa jukwaa la kukuza muziki wa nyumbani. ‘Tigo Fiesta inawapa fursa wasanii kuonesha uwezo wao na kuongeza idadi ya mashabiki ndani na nje ya nchi. Kuna maelfu ya mashabiki wanaohudhuria matamasha yenyewe au kufuatilia matukio kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,’ alisema.
Mbali na kutoa burudani ya uhakika, Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote pia itaibua fursa nyingi za kujiongezea kipato kwa wasanii pamoja na wakaazi wa maeneo mbali mbali yatakayoshuhudia shamrashamra za msimu huu.


Pia katika msimu huu wa burudani, Tigo inatoa tiketi za watu mashuhuri (VIP) za kuhudhuria Tigo Fiesta 2018 kwa wateja ambao watanunua vifurushi vya Tigo VIP Pack ambavyo vinawapa wateja huduma bora zaidi za sauti, SMS na data kuanzia TSH 30,000/-. Vile vile, wateja wote wa Tigo pia watapata nafasi ya kujishindia zawadi kem kem kama vile pesa taslim na simu janja kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta Chemsha Bongo ambapo watatakiwa kujibu maswali yanayohusu Tigo Fiesta 2018 - Vibe Kama Lote.
‘Wasanii wenyewe pamoja na jamii yote kwa ujumla katika mikoa 15 itakayotembelewa na msimu huu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote watapata fursa kubwa za kiuchumi zinazoendana na msimu wenyewe,’ William alisema. Wafanya biashara mbali mbali ikiwemo wamiliki wa hoteli, migawa, kumbi za starehe, mama niitilie, wauzaji wa nguo na wamiliki wa vyombo vya usafiri huongeza kipato kutokana na biashara zao kuchangamka kutokana na idadi kubwa ya wateja wanaohudhuria matamasha ya Tigo Fiesta.

Gardner aliongeza kuwa msimu huu wa Tigo Fiesta 2018 - Vibe Kama Lote utajumuisha miji ya Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu msimu mpya wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote kupata vibali kutoka kwa baraza hilo. Tigo Fiesta 2018 inatarajiwa kuwapa fursa wasanii wa nyumbani kutoa burudani za muziki katika mikoa 15 ya nchi, kuanzia Morogoro tarehe 29 Septemba. Pamoja naye ni Katibu Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner Habash (katikati) na Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga (kulia).
Katibu Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner Habash (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu maandalizi ya msimu mpya wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote unaotarajiwa kuwapa fursa wasanii wa nyumbani kutoa burudani za muziki katika mikoa 15 ya nchi, kuanzia Morogoro tarehe 29 Septemba. Pamoja naye ni Katibu Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner Habash (katikati) na Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga (kulia) .
Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar Es salaam katika uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote unaotarajiwa kuwapa fursa wasanii wa nyumbani kutoa burudani za muziki katika mikoa 15 ya nchi, kuanzia Morogoro tarehe 29 Septemba. Pamoja naye ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner Habash (katikati).

MAPINDUZI YA SEKTA YA UVUVI WILAYA YA PANGANI, ZIARA YA MBEGANI INJINI ZA BOTI ZENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 80 ZAPATIKANA

$
0
0

  KAIMU Mtendaji Mkuu wa FETA kulia akiteta jambo na uongozi wa wilaya ya Pangani kushoto anayemsikiliza ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa na kushoto ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso wakati walipofika ofisini kwake
 KAIMU Mtendaji Mkuu wa FETA akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso  kulia ni Mkurugenzi wa Mafunzo FETA  kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah na anayefuatia ni Afisaa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson
Siku chache baada ya kikao na Waziri wa Uvuvi na Ufugaji; Mh. Luhaga Mpina na Uongozi wa wilaya ya Pangani chini ya Zainab Abdallah na Mbunge wa Jimbo la Pangani Jumaa Aweso wamefanya ufatiliaji wa haraka sana kupelekea ufanikishaji wa upatikanaji wa Mashine Engine za boti za kuvua mazao ya baharini.

Hatua hiyo ni baada ya kufanya ziara kwenye Chuo cha Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (Fisheries Education and Training Agency - FETA); makao makuu wilayani Bagamoyo (Mbegani) walipokwenda kufatilia, na kupata uhakika wa Engine zenye thamani ya takribani sh.Milioni 80 kwa ajili ya wana Pangani wanaojihusisha na sekta hii ikiwa ni matokeo chanya ya haraka sana. Tunamshkuru Katibu Mkuu (Uvuvi) Dr Rashid Tamatama kwa kufanikisha hatua hii muhimu.

Akizungumza baada ya hatua hiyo muhimu Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa alisema  hayo  ni mapinduzi makubwa ambapo engine hizi zinaenda kuwasaidia vijana wengi na kuimarisha zaidi sekta hii.

Alisema pia ni kujifunza na kujionea namna chuo kinavyo endeshwa ikiwa ni sehemu ya kujiandaa ufanikishaji wa mafunzo yanayotolewa hapo kutolewa Chuo Cha KIM kilichopo Pangani baada ya kupata suluhu ya sintofahamu ya muda mrefu iliopo.

Hata hivyo viongozi wa wilaya ya Pangani  walitoa  shukrani za dhati kwa Wizara ya Uvuvi kwa namna walivyo na utayari mkubwa wa kushughulika na changamoto za watanzania ikiongozwa na Waziri Mpina na Naibu Waziri Ulega ambae wiki ijayo atafika Pangani kuweka sawa mengine mengi kuelekea uimarishaji wa sekta hii tegemezi No.1 la mapato ,uchumi na ajira Pangani.
#Panganiyetu
#SektakwaSekta
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images