Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live

MAADHIMISHO YA WIKI YA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KITAIFA YAFUNGWA JIJINI DODOMA.

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CGF Thobias Andengenye, akitoa taarifa ya Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa, wakati wa kufunga maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri uliopo Jijini Dodoma jana.

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kitengo cha Maokozi toka Makao Makuu wakimuonesha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala, jinsi wanavyoweza kufanya maokozi kwenye majengo marefu pindi ajali inapotokea, alipotembela Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma wakati wa kufunga maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yaliyoanza Agosti 29, 2018 Jijini humo jana.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala, akipokea zawadi ya kizimia moto cha awali (Fire Extinguisher) kutoka kwa Mkaguzi Msaidizi wa Zimamoto Philibert Chaki, alipotembelea banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati wa kufunga maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yaliyoanza Agosti 29, 2018 Jijini Dodoma jana.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamto na Uokoaji, CGF Thobias Andengenye akimkabidhi cheti mwakilishi wa TCRA, ambaye jina lake halikupatikana kwa mchango wake wa kufanikisha Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa, wakati wa kufunga maadhimisho hayo yaliyoanza Agosti 29, 2018 katika Uwanja wa Jamhuri uliopo Jijini Dodoma jana.


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamto na Uokoaji, CGF Thobias Andengenye akimkabidhi zawadi ya kikombe Konstebo wa Timu ya Polisi Dodoma, Ally Juma mara baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa bao moja dhidi ya wapinzani wao Timu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Jamhuri, wakati wa kufunga maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yaliyoanza Agosti 29, 2018 Jijini Dodoma jana.

Msanii Mrisho Mpoto na kundi lake wakitumbuiza wimbo maalum wenye maudhui ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji, mbele ya Mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamto na Uokoaji, CGF Thobias Andengenye, wakati wa kufunga maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yaliyoanza Agosti 29, 2018 katika Uwanja wa Jamhuri uliopo Jijini Dodoma jana. (Picha zote na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)



Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yalizinduliwa rasmi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola (Mb) Agosti 29, 2018 katika Uwanja cha Jamhuri Jijini Doodma na kufungwa jana Agosti 31, 2018 na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CGF Thobias Andengenye. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa mwaka huu ni “SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA KUFUNGA VING’AMUAMOTO VIWANDANI”

MKUU WA OPERESHENI MAALUM ZA JESHI LA POLISI AKITOA ELIMU JUU YA KUKABILIANA NA UHALIFU KATIKA KIJIJI CHA MASUGURU MKOANI MTWARA.

$
0
0
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, akisalimiana Kamandani Jawapi mwanakijiji wa Masuguru wilayani Masuguru mkoani Mtwara baada ya kumalizika mkutano na wananchi wa eneeo hilo.( Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, akizungumza na wanakijiji cha Masuguru wilayani Masuguru mkoani Mtwara juu ya kukabilina na kuwafichua wahalifu wanaokimbilia kijijini hapo wakitokea nchini Msumbiji.( Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, akizungumza na wanakijiji cha Masuguru wilayani Masuguru mkoani Mtwara juu ya kukabilina na kuwafichua wahalifu wanaokimbilia kijijini hapo wakitokea nchini Msumbiji.( Picha na Jeshi la Polisi)

TANZANIA INAONGOZA KWA UWEKEZAJI UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI-WAZIRI MKUU MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania inaongoza kwa kupokea uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki. 

“Mtiririko wa uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja nchini umeongezeka kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita na sasa wawekezaji wameipa kipaumbele Tanzania kama kitovu cha uwekezaji barani Afrika.”

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Septemba 02 ,2018) wakati akihutubia Kongamano la Biashara kati ya Tabnzania na China kwenye Hoteli ya Winstin jijini Beijing nchini China.Waziri Mkuu amesema Tanzania imethibitika kuwa ni Taifa lililodhamiria kwa dhati kujenga uchumi wa viwanda , pamoja na kulinda na kudumisha amani na utulivu.

Amesema ripoti ya uwekezaji duniani iliyotolewa mwaka 2018, inaonesha kuwa Tanzania inaongoza kwa kupokea uwekezaji katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na imepokea kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.2 mwaka 2017.Waziri Mkuu amesema Tanzania inafanya juhudi kubwa ili iweze kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, hivyo imeweka mkazo mkubwa katika kujenga msingi imara wa viwanda.

“Ili kufanikisha hilo tumeandaa Ukanda wa Kuzalisha kwa ajili ya mauzo ya Nje na Ukanda maalum wa Kiuchumi tukilenga kutimiza mkakakati wetu wa kukuza uchumi wa viwanda na biashara.”Akizungumzia kuhusu sekta ya fedha, Waziri Mkuu amesema Tanzania inawakaribisha wawekezaji kuanzisha Taasisi za Kifedha kama vile benki kwa ajili ya kutoa mikopo midogo midogo, benki za uwekezaji, benki za kilimo na benki za biashara.

Kuhusu uwekezaji kutoka China uliosajiliwa na Kituio cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kati ya Novemba 2015 hadi Oktoba 2017, Waziri Mkuu amesema umefikia thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.077 na umejikita katika meneo ya kilimo, majengo ya biashara, rasilimali watu, viwanda na utalii.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema kuna fursa nyingi kwenye sekta ya huduma hususan katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambayo ni miongoni mwa sekta ndogo zinazokuwa kwa haraka nchini Tanzania. 

Pia kumekuwa na ukuaji na mageuzi ya haraka katika soko la TEHAMA nchini kwa miaka 10 iliyopita. “Soko la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano limekuwa kwa ongezeko la watumiaji, aina ya huduma zinazotolewa pamoja na kupanuka kwa eneo ambalo huduma hizo hutolewa.”Waziri Mkuu ameongeza kuwa, “Tanzania kuna fursa zisizo na ukomo katika eneo hili huku kukiwa na matarajio ya kukuwa kwa soko la kikanda.”

“Maeneo ya kuwekeza ni pamoja na utoaji wa huduma za simu hususan katika maeneo ya vijijini, utoaji na uendeshaji wa huduma za mtandao pamoja na ukarabati na matengenezo ya vifaa vya mawasiliano. Tunawakaribisha wawekezaji kuwekeza katika maeneo haya.”

Amesema kwa wale ambao nia yao ni kuwekeza katika kilimo, Tanzania ina hekta milioni 44 za ardhi inayofaa kwa kilimo na takribani hekta milioni 29.4 kwa ajili ya umwagiliaji.

“Ninawakalibisha wawekezaji kuja kuwekeza katika kilimo cha biashara kwa mazao kama miwa, mpunga, ngano, kahawa, chai na mahindi. Tuna fursa kubwa ya kuwekeza katika kilimo cha miwa na uzalishaji wa sukari.”

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, SEPTEMBA 02, 2018.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya Wafanyabiashara wa nchini China, wakati akizungumza nao leo jijini Beijing ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC),unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa China Xi Jinping kesho jumatatu Septemba 3, 2018 ambapo utafanyika kwa siku mbili. Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Joh Pombe Magufuli, katika mkutano huo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Group,Mohamed Kiluwa ambaye ni mmoja ya baadhi ya Wajumbe kutoka Tanzania waliopo nchini China kuhudhuria Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC),unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa China Xi Jinping kesho jumatatu Septemba 3, 2018.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya Wafanyabiashara wa nchini China,mara baada ya kuzungumza nao leo jijini Beijing ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC),unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa China Xi Jinping kesho jumatatu Septemba 3, 2018 ambapo utafanyika kwa siku mbili. Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Joh Pombe Magufuli, katika mkutano huo.

Balozi wa Tanzani chini China, Mbelwa Kairuki akimtambulisha mmoja wa wafanyabiashara wa China kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Godfrey Mwambe baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzungumza nao leo jijini Beijing, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa China, Xi Jinping kesho jumatatu Septemba 3, 2018 ambapo utafanyika kwa siku mbili.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Godfrey Mwambe akibadilishana kadi na baadhi ya Wafanyabiashara wa nchini China.









WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHI CHINA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watanzania waishio nchini China Kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing, Septemba 2, 2018. Pichani kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini China,Mh Mbelwa Kairuki.
Baadhi ya Watanzania wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao Kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing nchini China, Septemba 2, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies Naima Mohamed Kiluwa,alipozungumza na Watanzania waishio China wakiwemo na wageni waalikwa mbalimbali kutoka Tanzania kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing nchini China Septemba 2, 2018. Pichani kati ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies Mohamed Kiluwa na kulia ni Mfanyabiashara maarufu kutoka Tanzania,Mh John Cheyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga wakati alipowasili kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing nchini China, Septemba 2, 2018. Kushoto ni Waziri wa Madini, Angela Kairuki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mke wa Balozi wa Tanzania nchini China na Waziri wa Madini, Angela Kairuki wakati alipowasili kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing China kuzungumza na Watanzania, Septemba 2, 2018. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania waishio nchini China baada ya kuzungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing nchini China Septemba 2, 2018. Kulia kwake ni Waziri wa mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga na kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki. 


















LUGOLA AKERWA MGAMBO KUMPIGA KIKATILI MWANANCHI JIJINI DAR ES SALAAM, ATOA ONYO KALI KWA WATU WANAOCHUKUA SHERIA MKONONI

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amelaani tukio lililofanywa na Mgambo wa Jiji la Dar es salaam akisema ni la kihuni, kishenzi na kinyama na halipaswi kufumbiwa macho na wapenda amani, watetezi wa haki za binadamu na wananchi wote kwa ujumla.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Lugola alisema Serikali inalaani vikali tukio hilo ambalo lililotokea wiki iliyopita jijini humo, na kutokana na unyama huo tayari hatua za kisheria zimeanza kuchukuliwa.
“Jeshi la Polisi tayari limewakamata wahusika kama Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni tarehe 31 Agosti, 2018 ilivyoeleza. Natumia fursa hii kuwakumbusha tena Mgambo wote kuwa makini katika utekelezaji wa maagizo wanayopewa na kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu,” alisema Lugola.
Pia kutokana na tukio hilo, Lugola alisema anazitaka Mamlaka za Majiji, Manispaa na Halmashauri kufikiria kuanzisha Huduma ya Polisi Wasaidizi (Auxiliary Police) katika maeneo yao kwa mujibu wa Sheria ya Polisi na Polisi Wasaidizi Sura ya 322 ili kuepuka matukio ya uvunjifu wa haki za Binadamu kama tukio la Mgambo watatu  jinsi lilivyo tokea.
Aidha, Lugola pia alizungumzia kuhusu baadhi ya matukio mengine ambayo watu  wanajichukulia Sheria mkononi na kuwaadhibu kwa kuwapiga watu wengine kwa sababu mbalimbali.
Aliyataja matukio hayo ni pamoja na ugomvi wa kifamilia ndani ya ndoa ambao huhusisha Wanaume kuwapiga wake zao au wake kuwapiga waume zao, pia  wananchi kuwapiga watu wanaowatuhumu kwa makosa mbalimbali, pamoja na walimu kuwapiga wanafunzi kinyume cha sheria.
Pia Lugola aliwaonya baadhi ya Askari Polisi ambao wanatumia nguvu isiyo ya kadiri kulingana na mazingira halisi wanapowadhibiti watuhumiwa.
“Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi inalaani vikali matukio ya kujichukulia Sheria mkononi na kupitia kwenu Wanahabari nawataka Watanzania kufuata sheria za nchi kwa kuacha vitendo vya kujichukulia Sheria mkononi. Vitendo hivi pamoja na kusababisha uvunjifu wa amani vinaweza kuleta madhara kwa watu ambao hawana makosa na kuichonganisha Serikali na wananchi wake,” alisema Lugola.
Kutokana na matukio hayo, Lugola aliwataka wanandoa wanakumbushwa kutumia Dawati la Jinsia katika Vituo vya Polisi kote nchini ili kuwasilisha malalamiko yao ya unyanyasaji wa kijinsia ndani ya ndoa ili hatua stahiki zichukuliwe.
Pia aliwataka wananchi waendelee kuheshimu sheria za nchi na kuepuka kujichukulia unakuta mtu anapigwa hata haulizi anayepigwa amekosa nini nae anajiunga nao na kumpiga hali ambayo imesababisha majeraha, vilema vya kudumu na vifo kwa watu wasio na hatia.
Hata hivyo, Lugola aliwaonya walimu kwa kufanya matukio kujirudia kwa kuwaadhibu wanafunzi kwa kuwachapa na kuwapiga hovyo kiasi cha kusababisha maumivu makali, ulemavu na vifo.
“Natumia fursa hii kuwakumbusha Walimu kote nchini kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ya Adhabu kwa wanafunzi ambayo imetolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili kuepuka madhara yake, kuondoa hofu kwa wazazi na kufanya shule zetu kuwa mahali salama kwa watoto wetu,” alisema Lugola.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, jijini Mwanza leo. Katika hotuba yake kwa waandishi hao, Lugola alilaani tukio la askari mgambo wa Jiji la Dar es Salaam kwa kumpiga kikatili mwananchi eneo la Bunju, wilayani Kinondoni. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WATANZANIA WAISHIO NJE WATAKIWA KUSHAWISHI WAWEKEZAJI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatakaWatanzania waishio nje ya nchi wahakikishe wanashiriki kikamilifu kujenga uchumi wa nchi yao kwa kushawishi wawekezaji wenye mitaji mikubwa waje kuwekeza nchini na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Magufuli inaamini kuwa Tanzania itapata maendeleo makubwa ya kiuchumi endapo wananchi wake watatekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya “Hapa Kazi tu”.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumapili, Septemba 02 ,2018) wakatiakizungumza na Watanzania waishio nchini China kwenye ofisi za Ubalozi wa Tanzani uliopo jijini Beijing. 

Alisema nchi zote zilizoendelea zilihakikisha kuwa wananchi wake wanaelewa na kutekeleza matamko yanayowahamasisha kufanya kazi, hivyo alitumia fursa hiyo kuwahamasisha Watanzania popote walipo kutekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu.’

Waziri Mkuu alisema China ambayo imefanikiwa kuwa moja kati ya nchi zenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani, imefika hapo kutokana na mchango mkubwa uliotolewa na wananchi wake, ambao waliamua kuunga mkono juhudi za Serikali yao kwa kufanya kazi kwa bidii na weledi wakiwa ndani au nje ya nchi. 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwataka Watanzania waishio nje ya nchi wajiepushe na vitendo vya uhalifu hasa biashara ya dawa za kulevya ambayo inachafua jina na heshima ya nchi yao kimataifa. “Tanzania ni nchi nzuri na inaheshimika duniani, nawasihi wote mnaoishi nje muachane kabisa na biashara haramu ya dawa za kulevya kwa sababu inalitia doa Taifa na adhabu yake katika baadhi ya nchi ni kifo,” alisisitiza Waziri Mkuu.

Awali, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga alisema mwelekeo wa Diplomasia ya Tanzania Kimataifa hivi sasa ni kiuchumi (economic diplomacy), hivyo Watanzania waishio nje wanapaswa kuwa wabunifu, makini katika kutafuta fursa zenye manufaa kwa nchi yao.

Alisema Diplomasia ya Uchimi si kupeleka Tanzania wawekezaji tu bali wawekezaji katika viwanda ambavyo kila vinapojengwa vinachangia kuinua uchumi wa Taifa.Kwa upande wake,Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki aliwaasa vijana kuitumia teknolojia ya mawasiliano na mitando ya jamii kutafuta habari na taarifa muhimu hasa nafasi za masomo ili kujiendeleza kielimu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, SEPTEMBA 03, 2018.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini afanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa Polisi.

MTENDAJI MKUU TFS ATOA NENO KWA WASHIRIKI MISS TANZANIA 2018

$
0
0
*Awataka wawe mabalozi kuhimiza uhifadhi wa misitu,utalii wa ndani
 Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.

WAREMBO wa Shindano la Miss Tanzania 2018 wametajwa kuwa mabalozi wazuri wa Vivutio vya Utalii nchini ikiwemo Rasilimali za Misitu na Nyuki pamoja na Maporoko.

Akizungumza na Warembo hao jijini Dar es Salaam wakati anawaaga wakielekea katika hifadhi ya Amani mkoani Tanga, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS), Profesa Dos Santos Silayo amewataka walimbwende hao kutumia weledi, uwezo Kitaaluma na nafasi katika jamii kusaidia uhifadhi wa misitu.

Prof. Silayo amewataka warembo hao kutangaza Misitu hiyo mazuri yake ili iweze kutumika kutoa huduma za kiutalii na kuonesha thamani yake iliyosimama.Amesema uhifadhi wa misitu unaifaida nyingi na moja ya faida misitu ni cha chanzo uhifadhi wa maji na kuongeza pamoja na hewa safi.

Amesema kuwa TFS itatumia sehemu ya washiriki hao wa Miss Tanzania mwaka huu kwa ajili ya kuwa malozi ambao watashiriki kikamilifu kuhimiza uhifadhi misitu.Amefafanua watawajengea uwezo katika kuhakikisha wanaifanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa na zaidi kuna maeneo mengi ya misitu ambayo imehifadhiwa ambayo inahitaji mabalozi wa kutangazwa.

"TFS pamoja na wadau wengine wakiwamo wa utalii nchini ambao wapo Wizara ya Maliasili na Utalii tumeamua kushirikiana na  ya Miss Tanzania kuhakikisha washiriki watano wa Miss Tanzania tunawatumia kuutangaza vivutio vya utalii na uhifadhi misitu,"amefafanua Profesa Silayo.

Amesema katika kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri warembo hao watatembelea baadhi ua misitu iliyohifadhiwa ukiwamo hiyo hifadhi ya msitu Amani.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basilla Mwanukuzi amesema kuwa lengo la ushiriki wa taasisi za utalii katika Shindano hilo la Ulimbwende ni kukuza utalii wa ndani.

Mwanukuzi ameeleza kuwa taasisi za utalii zimeunga mkono kuhakikisha Utalii unatangazwa na hivyo washiriki watano kati ya 20 waliopo kwenye shindano hilo watapata fursa ya kuwa mabalozi wa utalii na uhifadhi wa misitu.

Mwanukuzi amesema kutakuwa na mabalozi watano katika Shindano hilo la Miss Tanzania 2018 wamegawanyika katika sehemu tano.Ametaja kutakuwa na Miss Domestic Tourism, Miss Ruaha, Balozi TANAPA), Miss Ngorongoro, Miss Seleu(Tanzania World Life Authority) na  Miss Equal Tourism chini ya Forest Services.

Kuhusu shindano la Miss Tanzania ,Mwanakuzi amesema wameshusha bei ya kiingilio ili kutoa fursa ya watanzania wengi kushuhudia.Ametaja viingilio hivyo ni kwamba  VVIP 70,000, VIP 50,000 na kawaida 30,000.

Amesema lengo la mashindano hayo si kupata faida bali kuhakikisha jukwaa hilo linatoa fursa kwa watoto wa kike kuwa daraja katika kutimiza ndoto zao kwani anaamini baada ya mashindano hayo watashiriki kufanya kazi za kijamii kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.
 Washiriki wa Miss Tanzania mwaka 2018 wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza safari ya kuelekea Msitu Amani mkoani Tanga.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo(wa pili kulia)akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Miss Tanzania mwaka 2018 baada ya kuzungumza nao kuhusu umuhimu wa warembo hao kuutangaza uhifadhi wa misitu na utalii nchini
 Muandaji wa Mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2018 Basila ambaye pia amewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1998 akiwa na Mtendaji Mkuu wa TFS Profesa Dos Sontos Silayo wakati wakizungumza na washiriki wa mashindano hayo jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI MKUTANO WA JUKWAA LA USHIRIKIANO KATI YA CHINA NA AFRIKA ULIOANZA JIJINI BEIJING

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Afrika uliofunguliwa na Rais huyo kwenye ukumbi wa Great Hall of the People uliopo Beijing, Septemba 3, 2018. Mheshimwa Majaliwa amemwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wakuu wa Afrika na China baada ya Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping kufungua Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya Tanzania na China Kwenye ukumbi wa Mikutano wa Great Hall of the People uliopo Beijing, Septemba 3, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

LUGHA YA KISWAHILI CHANGAMOTO YA UTABIBU WILAYANI KYERWA MKOANI KAGERA

$
0
0

 Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Dkt. Diocles Ngaiza, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu upatikaji wa dawa kutoka Bohari ya Dawa (MSD), mkoani humo mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mfamasia wa wilaya hiyo,  Dominic Malabeja. 
 Wauguzi wa Zahanati ya Kaisho iliyopo wilayani Kyerwa mkoani Kagera, wakisaidia kubeba maboksi yenye  dawa baada ya kupelekewa na Bohari ya Dawa (MSD) wilayani humo mwishoni mwa wiki. Kutoka kulia ni Devotha Maganga, Editha Nyaruzi na Yolanda Joseph.

 Jengo la Zahanati ya Kata ya Kaisho.
 Taswira ya moja ya Jengo la Kituo cha Afya cha Murongo wilayani Kyerwa.
 Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Cornelia Mwillawi (kushoto), akimuonesha fomu maalumu ya kujaza baada ya kukabidhiwa dawa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Murongo, Dkt.Rashid Eid (kulia), baada ya kukabidhiwa dawa mwishoni mwa wiki. Katikati ni Tabibu wa kituo hicho, Denis Rugemalira.
Tabibu wa kituo hicho, Denis Rugemalira (kulia), akijadiliana jambo na Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Cornelia Mwillawi baada ya kukabidhi dawa katika kituo hicho.

Na Dotto Mwaibale, Kyerwa Kagera

KUTOKUFAHAMU Lugha ya Kiswahili imekuwa ni changamoto kubwa ya upatikanaji wa matibabu katika Kituo cha Afya cha Murongo kilichopo mpakani mwa Tanzania na Uganda wilayani Kyerwa mkoani Kagera.

Hayo yalielezwa na Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dkt. Rashid Eid, mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao walikuwepo mkoani Kagera kuangalia taratibu za usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenye vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Kagera zinazofanywa na Bohari ya Dawa (MSD)

"Changamoto kubwa tuliyonayo ni wagonjwa wetu tunaowapatia matibabu katika hiki kituo chetu cha afya cha Murongo kutojua lugha ya kiswahili hivyo ulazimika kutumia lugha ya alama kuweza kuelewana kama vile kama mgonjwa anaumwa kichwa basi atashika kichwa na kama tumbo vilevile atashika tumbo" alisema Dkt. Eid.

Alisema katika eneo hilo kunamuingiliano mkubwa wa watu kutokana na kuoleana kwani kuna Waganda waliooa Tanzania na Watanzania waliooa Uganda na kuwa kwa pande zote hizo mbili wananchi wake hawajui kuzungumza kiswahili zaidi ya makabila yao ya Kiganda, Kinyankole, Kihaya na Kinyambo.

Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo kuna wakati hulazimika kuwaita wafanyakazi wa kituo hicho wanao elewa kiswahili kutafsiri lugha wakati wanapozungumza na mgonjwa  ambaye hajui kiswahili ili kubaini ugonjwa wake.

Akizungumzia upatikanaji wa dawa kutoka MSD alisema zinapatikana kwa wakati na kuwa pamoja na kituo hicho kuwepo na muingiliano huo wa watu kutoka nchi jirani ya Uganda hawana ubaguzi wa kutoa huduma kwao.

"Kituo chetu kinatoa huduma kwa watu wote bila ya ubaguzi na hatujawahi kupungukiwa dawa kwa vile tunapo agiza dawa tunakuwa na idadi ya pande zote mbili na kuongeza za ziada jambo ambalo limsaidia tusiwe tunapungukiwa kwa dawa zote muhimu" alisema Dkt.Eid.

Alisema katika kituo hicho cha afya kwenye mwezi wa sita wagonjwa wanaotibiwa ni kati ya 50 hadi 80 kwa siku lakini kwa hivi sasa ni wagonjwa kuanzia 20 hadi 40 ingawa hakufafanua kwanini idadi hiyo inapungua katika kipindi hicho.

Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Dkt. Diocles Ngaiza alisema upatikana wa dawa katika wilaya hiyo kutoka MSD ni mzuri ukilinganisha na miaka 2015 ambapo walikuwa wakipata asilimia 30 lakini sasa hivi ni zaidi ya 70.

Katika ziara hiyo wilayani Kyerwa MSD ilikabidhi dawa katika Kituo cha Afya cha Murongo na Zahanati ya Kaisho.

CHINA KUTOA DOLA BIL. 60 KWA MAENDELEO YA AFRIKA

$
0
0
RAIS wa China, Xi Jinping amesema China itatoa jumla ya dola bilioni 60 za Marekani kwenye mpango wake wa miaka mitatu ya ushirikiano na Afrika katika shughuli za maendeleo.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Septemba 03 ,2018) wakati akifungua Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaofanyika jijini Beijing nchini China.

Rais Jinping ameahidi kuwa nchi yake itatoa ushirikiano ili kuhakikisha kwamba amani ya kudumu inapatikana Barani Afrika, hatua ambayo ni muhimu kwa ustawi wa nchi za Afrika.

Maeneo mengine ambayo Rais huyo ameahidi kuwa China italisaidia Bara la Afrika ni pamoja na ujenzi wa miundombinu, ushirikiano katika sekta ya biashara na huduma za afya.

Kadhalika, Rais Jinping amesema China itatoa nafasi za mafunzo ya kilimo bora na mafunzo ya ufundi kwa watalaam kutoka nchi za Afrika ili kuchangia katika maendeleo ya uchumi. 

Amesema hivi sasa anaamini kwamba China na nchi za Bara la Afrika wako karibu zaidi na wanashirikiana vizuri sana katika shughuli za kimaendeleo ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Mkutano huo ulianza kwa sherehe ya ukaribisho na baadae viongozi kutoka nchi mbalimbali barani Afrika na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antyonio Geterres walipata fursa ya kupiga picha ya pamoja na mwenyeji wao Rais wa China. 

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa ambaye anamuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano huo alisalimiana na Rais Jinping baada ya ufunguzi. Mkutano huo utaendelea kesho ambapo viongozi wengi kutoka Bara la Afrika watapata nafasi ya kuzungumza.

RAIS DKT. MAGUFULI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA YA UJENZI WA MELI MPYA, CHELEZO, UKARABATI WA MELI YA MV VICTORIA NA MV BUTIAMA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia zoezi la utiaji saini Mikataba mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Meli mpya ya abiria na mizigo, Chelezo, ukarabati wa Meli za Mv Victoria na Mv Butiama, Mikataba ambayo ilisainiwa kati ya Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania Marine Services Company (MSCL) na Kampuni tatu za Korea Kusini ambazo ni M/S STX engine Co ltd, Saekyung Construction ltd na KTMI Co ltd. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika Bandari ya Mwanza Kusini mara baada ya kushudia utiaji saini wa Mikataba mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Meli mpya ya abiria na mizigo, Chelezo, ukarabati wa Meli za Mv Victoria na Mv Butiama, Mikataba ambayo ilisainiwa kati ya Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania Marine Services Company (MSCL) na Kampuni tatu za Korea Kusini ambazo ni M/S STX engine Co ltd, Saekyung Construction ltd na KTMI Co ltd.
Mfano wa Meli mpya itakayojengwa ambayo Mkataba wake umesainiwa. Meli hiyo itakuwa na Urefu wa Mita 90, Kimo mita 10, uwezo wa kubeba abiria 1200 magari madogo 20, mizigo tani 400 na itakuwa ikisafiri kwa muda wa masaa sita tu kutoka Mwanza mpaka mkoa wa Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Balozi wa Korea Kusini hapa nchini Song Geum Yong watatu kutoka kushoto waliokaa,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella wakwanza kulia waliokaa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe watatu kutoka kulia pamoja na wabunge mbalimbali wa mikoa ya Kanda ya ziwa.

MGAHAWA MPYA WA FOOD POINT WAZINDULIWA NAMANGA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia akizungumza na wanahabari katika mgahawa wa Food Point uliopo Namanga Mkabala na Benki ya Exim wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo mchana akiwa ni mmoja wa waalikwa katika chakula cha mchana wakati mgahawa huo ukifunguliwa rasmi leo, Ukihitaji chakula safi na kilichopikwa na wataalamu wa maakuli nenda Food Point utafurahia chakula chao.
23
Mgahawa wa Food Point unavyoonekana kwa nje.
5
Baadhi ya wageni walioalikwa wakisubiri huduma ya chakula mara baada ya kuagiza chakula.
6
Baadhi ya wafanyakazi wa Food Point wakiwahudumia wateja waliofika katika mgahawa huo kupata chakula cha mchana.
78
Baadhi ya wateja wakisubiri kupata chakula.
9
Nyama choma za kutosha kabisa
1011
Huduma ya vinywaji kama Juice, Soda na vyakula mbalimbali vinapatikana.
12
Bw. Alex Msama akiwa ni mmoja wa wageni waliopata huduma kwa mara ya kwanza katika mgahawa huo.
13
Baadhi ya wateja wakipata chakula.

China Kushirikiana na Nchi za Afrika Katika Mambo Nane

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, MAELEZO

Beijing-CHINA

RAIS wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping amesema, Serikali ya nchi hiyo ipo tayari kushirikiana na Afrika katika maeneo makubwa nane katika kipindi cha miaka mitatu ijayo itayojikita katika masuala ya viwanda, miundombinu, biashara, kilimo, ulinzi na usalama pamoja na mazingira. 

Akifungua Mkutano wa Tatu wa Jukwaa la Ushirikiano wa China na Bara la Afrika (FOCAC) leo Beijing China na Rais Xi Jinping ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa hilo amesema katika masuala ya viwanda, uchumi wa Bara la Afrika na usafirishaji wa bidhaa utaendelea kupewa kipaumbele na Serikali ya China pamoja na makampuni yake yanahimizwa kuwekeza katika nchi za Afrika.

Kuhusu sekta ya kilimo, Rais Xi Jinping alisema Serikali ya China imepanga kuanzisha miradi 50 itayogharimu kiasi cha Yuan Bilioni 1 (Dola Milioni 147) itayosaidia masuala ya dharura na majanga mbalimbali ya kibinadamu sambamba na hilo, Rais Xi Jinping ameahidi kupeleka wataalamu 500 wa masuala ya kilimo ili kusaidia maendeleo ya sekta hiyo Barani Afrika.

Akizungumzia kuhusu masuala ya miundombinu, Rais Xi Jinping amesema Serikali ya China itafanya juhudi na Umoja wa Afrika kuunda mpango wa ushirikiano wa Miundombinu baina ya Bara la Afrika na China na kusaidia makampuni ya Serikali ya China kupata fursa ya ujenzi wa miradi mbalimbali.

Katika masuala ya Biashara, Rais Xi Jinping alisema China itaongeza uingizaji wa bidhaa zinazotoka nchi za Afrika ili kuweza kuzisaidia kukuza biashara za kimataifa na kuahidi kupunguza kodi mbalimbali za bidhaa kutoka Bara la Afrika.

Aidha Rais Xi Jinping alisema katika eneo la uhifadhi na ulinzi wa Mazingira, Serikali ya China imepanga kuanzisha miradi 50 itayosaidia mfumo wa bioanuai na ulinzi wa mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kulinda uifadhi wa wanyama pori.

Akifafanua Zaidi, Rais Xi Jinping alisema China pia imekusudia kuwajengea uwezo vijana wa Bara la Afrika katika mafunzo ya ufundi stadi ambapo imepanga kutoa nafasi 1000 katika hadhi ya juu, nafasi za ufadhili wa masomo 50,000 pamoja na kuwakaribisha vijana 2000 kutembelea masuala mbalimbali.

Katika eneo la afya, Rais Xi Jinping alisema Serikali ya China imepanga kuendeleza miradi 50 katika sekta ya afya, hususani vituo vinavyolenga kupunguza magonjwa mbalimbali ikiwemo ukimwi, kifua na malaria.

Kuhusu mahusiano ya mtu mmoja mmoja Rais Xi Jinping alisema Serikali ya China imepanga kuanzisha taasisi ya mafunzo kwa watu wa Bara la Afrika na kubadilishana fikra na mitazamo. Aidha Rais Xi Jinping alisema katika Nyanja ya Amani na Usalama, China itaendelea kuweka mfuko maalum wa fedha na kusaidia Jeshi la Umoja wa Afrika ikiwemo kuanzisha miradi 50 ya kusaidia katika masuala ya kulinda amani, kupambana na uharamia na ugaidi.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Afrika uliofunguliwa na Rais huyo kwenye ukumbi wa Great Hall of the People uliopo Beijing, Septemba 3, 2018. Mheshimwa Majaliwa amemwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

TANZANIA YAPATA MWAKILISHI WA HESHIMA HONG KONG NA MACAO

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki kwa pamoja na Bibi Annie Suk-Ching Wu wakisaini Mkataba kumwezesha Bibi Wu kuwa Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania huko Hong Kong na Macao. Tukio hilo lilifanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Beijing, China na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda pamoja viongozi wengine ambao wapo nchini China kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC).
Balozi Mbelwa na Bibi Wu wakibadilishana mkataba mara baada ya kuusaini
Mhe. Waziri Mahiga akitoa hotuba kumpongeza Bibi Wu kwa kukubali kuiwakilisha Tanzania kwenye maeneo hayo na kumtaka kuiwakilisha vema nchi
Mhe. Waziri na viongozi wengine wakisubiri kuanza kwa ratiba
Mhe. Waziri Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Mbelwa na Bibi Wu mara baada ya kushuhudia uwekwaji saini wa mkataba wa kumwezesha Bibi Wu kuiwakilisha Tanzania Hong Kong na Macao
Picha ya pamoja na viongozi na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo
Katibu Mkuu, Prof. Mkenda akiteta jambo na Mhe. Balozi Mbelwa
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bibi Justa Nyange akiwa na Maafisa ambao walikuwepo kushuhudia uwekwaji saini wa mkataba wa kumwezesha Bibi Wu kuwa Mwakilishi wa Heshima kwenye majimbo ya Hong Kong na Macao ya nchini China

Rais Magufuli atengua na kuteua Katibu Mkuu na Kamishna wa Kazi

UTPC:WAANDISHI SIYO MAADUI BALI NI WADAU WA MAENDELEO

$
0
0
 Rais wa Klabu za waandishi wa habari nchini Deogratius Nsokolo akizungumza katika mkutano wa UTPC unaofanyika Jijini Arusha katika ukumbu wa Lush Garden. Picha na Vero Ignatus.
 Mkurugenzi wa idara ya Maendeleo ubalozi wa Sweden Ulf Kallsting
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza na viongozi wa Klabu za waandishi wa habari kutoka mikoa tofauti hapa nchini. Picha na Vero Ignatus.
Afisa program, Mafunzo, Utafiti na Uchapishaji kutoka UTPC Victor Maleko akizungumza na viongizi wa Klabu za waandishi wa habari kwenye mkutano mkuu uliofanyika Mkoani Arusha.
 Mkurugenzi wa UTPC Abubakari Karsan akiwa na Mkuu wa idara ya Maendeleo ubalozi wa Sweden Na. Vero Ignatus. Arusha

RAIS wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania Deogratius Nsokolo ameiomba serikali  kuwaangalia waandishi wa habari kwa jicho la tofauti ili kuwalinda kwa kuwa tasnia hiyo sio adui bali ni wadau muhimu wa maendeleo ya Nchi. 

Amesema hayo  katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania unaofanyika Jiini Arusha,ambapo amesema ndani ya miaka miwili waandishi  57 wamepata matatizo ya kupigwa,kuumizwa na kunyang'anywa vifaa vya kazi na baadhi kupote jambo ambalo linaleta woga katika utendaji kazi.

Nsokolo amesema hawawezi kutupia lawama kwa serikali kwa sababu hawajafanya uchunguzi wa kutosha,bali wanaomba kulindwa ili waweze kuchangia maendeleo kupitia kalamu zao.''Napenda ifahamike pote kuwa waandishi wa habari sio maadui bali ni wadau muhimu wa maendeleo hivyo vema kushirikiana na sio kuonana maadui,"alisema

Aidha amemshauri Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Magufuli kuangalia aina ya viongozi anaowateua kutokana na hivi karibu kujitokeza hadharani baadhi ya kiongozi mmoja kutoa kauli tata kwa mwandishi wa habari aliyepigwa uwanja wa mpira Dar es Salaam.Ni wazi tukio hilo la kulaaniwa na halipaswi kufumbiwa macho tunaomba wahusika wachukuliwe hatua maana tunafahamu kabla ya kuingia uwanjani kuna kukaguliwa hivyo huwezi kuingia mtu na silaha,"alisema

Pia alisema katika mkutano huo iliohudhuriwa na wajumbe 81 toka Klabu 28  Tanzania Bara na Visiwani watatoa Tuzo ya tatu ya Daudi Mwangosi kama ishara ya kuonyesha waandishi hawako salama."Lakini tunaomba wafadhili wetu SIDA waangalie jinsi ya kusaidia Klabu ya Dodoma na tutapeleka andiko maalum ili wajengewe ofisi zenye hadhi kulingana na hali ilivyo sasa na kuwapatia mafunzo wanahabari ili wafahamu jinsi ya kuandika habari za viongozi mbalimbali wanaotembelea Dodoma,"alisema

Naye Mkuu wa Idara ya ushirikiano wa Balozi wa Sweden Tanzania (SIDA) Ulf Kastig alipongeza Klabu ya Arusha na Morogoro kubuni miradi kwa ajili ya kujiongezea kipato kwa ushirikiano na wadau wa mikoa yao.Aliwakumbusha wanahabari kuhakikisha wanaandika habari za utafiti ili kuepuka kuleta shida katika nchi."Lakini ili Klabu zenu ziendelee kuwa na vyanzo vingi vya mapato vema mkaongeza idadi ya wanachama,"alisema.Alipongeza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Klabu za wanahabari na UTPC na kusema jambo la kuigwa kwani linajenga Demokrasia ya kweli.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro aliwaasa wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao licha ya kukabiliana na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa ajira.Amesema Wilaya yake inakabiliwa na changamoto kubwa ya migogoro ya ardhi ambayo sehemu kubwa inasabishwa na ukosefu wa uelewa wa sheria ya umiliki ardhi na baadhi ya wanasiasa kuitumia kujipatia kura.

"Mimi sitakubali kabisa kuachia wanasiasa wajinufaishe na migogoro hii lazima nibadilishe badala ya ardhi kuwalaana bali iwe baraka hasa Halmashauri ya Meru, na hili nimeanza kuzungumza na viongozi wadini tusaidiane kulimaliza," Picha na Vero Ignatus.

Kutoka katikati ni Rais wa RAIS wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania Deogratius Nsokolo, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ubalozi wa Sweden Ulf Kallsting, wakwanza kushoto ni Kaimu mwenyekiti wa wa umoja wa Klabu za waandishi wa habari nchini Jane Mihanji. Picha na Vero Ignatus.
 Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Arusha Press Klab Cloud Ngwandu,akiwa na Katibu wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha Mustafa Leu katika mkutano mkuu UTPC.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA NAIBU GAVANA WA JIMBO LA JIANGSU NCHINI CHINA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Gavana wa Jimbo la Jiangsu nchini China, Bw. Guo Yuan Qiang kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing, Septemba 3, 2018. Waziri Mkuu yupo nchini China kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika - FOCAC. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Gavana wa Jimbo la Jiangsu nchini China, Bw. Guo Yuan Qiang (kushoto) kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing nchini China, Septemba 3, 2018. Waziri Mkuu yupo nchini China kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika - FOCAC. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Gavana wa Jimbo la Jiangsu nchini China, Bw. Guo Yuan Qiang kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing, Septemba 3, 2018. Waziri Mkuu yupo nchini China kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika - FOCAC. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TMA KUCHOCHEA MATUMIZI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KWA SEKTA MBALIMBALI ZA KIUCHUMI NA KIJAMII

$
0
0
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeandaa mkutano wa wadau mbalimbali kwa ajili ya msimu wa mvua za Vuli (Oktoba hadi Desemba, 2018) ambao unalenga kupata maoni ya wadau jinsi utabiri wa Msimu wa Mvua za Vuli utakavyoweza kutumika katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ushirikishwaji wa Wadau Katika Kuchochea Matumizi Ya Taarifa Za Hali Ya Hewa”.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dkt. Agnes Kijazi alisema kuwa lengo kubwa la mkutano huo ni kuchochea matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii hapa nchini.

‘lengo kubwa la mkutano huu kama ilivyo katika kauli mbiu ni kuchochea matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii, ambapo katika mkutano huu, mtapata fursa ya kuona utabiri wa hali ya hewa wa msimu wa Oktoba hadi Disemba, 2018 na hivyo kuwa na majadiliano yenye lengo la kuchangia juu ya athari zitakazopatikana katika sekta zenu kutokana na utabiri huo na hatimaye kuandaa mbinu na mipango ya kukabiliana na athari hizo’. Alisema Dkt.Kijazi. 

Aidha aliongezea kuwa mkutano huo ni sehemu ya kubadilishana uzoefu kati ya wataalamu wa TMA, Sekta mbalimbali na Washirika wa Maendeleo hivyo basi ni sehemu muhimu ya ushirikishwaji wa wadau katika kujenga na kuimarisha utoaji na matumizi ya huduma za hali ya hewa katika jamii akisisitiza kuwa kauli mbiu imechaguliwa ili kuakisi jitihada za Mamlaka katika uandaaji na utoaji wa huduma shirikishi. 

Akifanunua umuhimu wa tarifa za hali ya hewa katika kuchangia azma ya serikali ya kufikia uchumi wa viwanda Dkt. Kijazi alisema huduma za hali ya hewa ni muhimu katika uzalishaji wa mali ghafi za viwanda na utunzaji wa miundo mbinu ya usafirishaji wa mali ghafi hizo pamoja na utunzaji wa miundo mbinu ya viwanda vyenyewe. Aliwataka wadau kutumia huduma za hali ya hewa katika sekta zao ili kumuunga mkono Mhesmiwa Rais katika kufikia malengo hayo ya uchumi wa viwanda.

Kwa upande Wake mwakilishi wa mradi wa kilimo himilivu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Bw. Diomedes Kalisa alisema kupitia mkutano huo wa wadau ni dhahiri malengo ya FAO ya kuboresha mfumo wa utoaji taarifa za hali ya hewa yatafikiwa hususan katika kilimo ili kubadilisha kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kwenye kilimo cha biashara katika kuboresha maisha ya wakulima na nchi yote katika kufikia malengo ya uchumi wa viwanda.

Nao wadau kutoka sekta mbali mbali wakijadili taarifa ya utabiri wa hali ya hewa uliotolewa na TMA katika msimu wa Machi hadi Mei, 2018 ambao usahihi wake ulifikia asilimia 96 waliipongeza Mamlaka kwa ongezeko hilo la usahihi wa utabiri. Hata hivyo walizungumzia changamoto ya utabiri kutowafikia wananchi wengi hasa wakulima na kuishauri TMA kuona uwezekano wa kuwatumia maafisa ugani kuhakikisha wakulima wengi wanapata taarifa za utabiri kwa wakati. Akijibu hoja hiyo Dkt. Agnes Kijazi alisema TMA imejipanga kuihusisha Wizara husika ili kuona utaratibu mzuri wa kutoa mafunzo kwa maafisa ugani na kuhakikisha wanapata utabiri mara unapotolewa.

Mkutano huo umefanyika tarehe 03 Septemba 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Taasis ya mafunzo ya uanasheri kwa vitendo Tanzania chini ya udhamini wa TMA na FAO na kuwashirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali zikiwemo maji, Nishati, maafa, mazingira, kilimo,tawala za mikoa, afya, elimu, Asasi zisizo za Kiserikali, wana habari na mashirika ya maendeleo ya Kimataifa

KUTOKA BEIJING CHINA

$
0
0

 Kwa mujibu wa wenyeji wanaeleza kuwa hili ndilo jengo refu zaidi kuliko yote jijini Beijing,lina ghorofa 108
Mandhari tulivu  ndani ya mtaa  wa Xinyuanxili middle street,Chaoyang  jijini Beijing,utunzaji wa mazingira na usafi katikati ya mji ni wa hali ya juu kabisa
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live




Latest Images