Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Kilimo wa China, Bw. Han Changfu wakati alipotembelea Wizara ya Kilimo ya nchi hiyo iliyopo Beijing Septemba 3, 2018. Majaliwa yupo nchini China kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya Afrika na China – FOCAC
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Kilimo wa China, Bw. Han Changfu (kushoto) wakati alipotembelea Wizara hiyo iliyopo Beijing, Septemba 3, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Kilimo wa China, Bw. Han Chanfu wakishuhudia utiaji saini wa Makubaliano ya Ushirikiano katika masuala ya Uvuvi kati ya China na Tanzania kwenye ukumbi wa Wizara ya Kilimo ya China katika jiji la Beijing, Septemba 3, 2018. Wanaotia Saini ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Rashid Ali Juma (kushoto) na Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Qu Dongyu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo wa China, Bw. Han Chanfu (wanne kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) baada ya mazungumzo yao kwenye ukumbi wa wizara hiyo jijini Beijing, Septemba 3, 2018. Wengine pichani ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Rashid Ali Juma. (wapili kushoto), Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke (watatu kushoto), Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki na Naiba Waziri wa Kilimo wa China, Qu Dongyu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na ujumbe wake wakiagana na viongozi wa Wizara ya Kilimo ya China baada ya mazungumzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Wizara hiyo, Beijing nchini China, Septemba 3, 2018. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Jimbo la Jiangsu nchini China katika sekta ya kilimo na viwanda utaiwezesha nchi kufikia malengo yake ya kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2020 na ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Amesema jimbo la Jiangsu ni miongoni mwa majimbo yaliyopiga hatua kubwa ya maendeleo kwenye teknolojia na viwanda duniani na Tanzania inahitaji wawekezaji wa uhakika katika sekta ya kilimo hususani watakaowekeza kwenye viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo, kuongeza thamani na kutafuta masoko.
Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumatatu, Septemba 03, 2018) wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Gavana wa Jimbo la Jiangsu nchini China, Bw. Guo Yuan Qiung kwenye ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini China.
“Tunathamini mchango wa Jimbo la Jiangsu katika uchumi wa Tanzania, ambapo sasa wawekezaji kutoka jimboni humo, waliowekeza kwenye viwanda mbalimbali kama cha kuchambua pamba, kutengeneza nyuzi na kukamua mafuta ya kula kwa kutumia mbegu za pamba cha Jielong kilichopo wilayani Shinyanga na kiwanda cha nguo cha Urafiki cha jijini Dar es Salaam.”
Kadhalika, Waziri Mkuu alisema bado mchango wa jimbo hilo unahitajika katika uendelezaji viwanda hususan katika masuala ya teknolojia ya viwanda, kuimarisha utafiti kwenye sekta ya kilimo na kuisaidia Tanzania kupata masoko ya mazao kama mbaazi, muhogo na soya. “Tunaomba uendelee kuhamasisha kampuni nyingi zaidi kutoka jimboni kwako kuja kuwekeza nchini.
Kuhusu kiwanda cha nguo cha Urafiki cha jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu na Naibu Gavana huyo walikubaliana kuangalia uwezekano wa kufanya mapitio ya changamoto za uendeshaji wa kiwanda hicho ili kutafuta suluhisho la mapungufu yanayojitokeza katika kiwanda hicho.
Kwa upande wake, Bw. Qiung alimhakikishia Waziri Mkuu ushirikiano wa hali ya juu hasa katika uwekezaji wa viwanda na kwamba anaamini kuwa mkutano wa FOCAC utatoa dira ya maendeleo kwa Tanzania na Bara zima la Afrika.
Aliongeza kuwa jimbo lake lipo tayari kushirikiana na Tanzania katika masuala ya elimu kwani lina vyuo vingi vinavyotoa kozi mbalimbali na aliwakaribisha wanafunzi kutoka Tanzania kwenda jimboni humo kusoma.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, SEPTEMBA 04, 2018.
UWEKEZAJI KUTOKA CHINA KUTUFIKISHA UCHUMI WA KATI-MAJALIWA