Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1663 | 1664 | (Page 1665) | 1666 | 1667 | .... | 1896 | newer

  0 0

  0 0  0 0


  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa George Simbachawene wakifuatilia Uwasilishwaji wa Taarifa ya utekelezaji wa kazi za Sido Mkoa wa Singida kwa kipindi cha mwaka 2016 hadi Juni 2018.
  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa George Simbachawene wakikagua maeneo mbalimbali ya hatua za uzalishaji katika kiwanda cha Mafuta ya Alizeti cha Mount Meru kilichopo Mjini Singida, Kamati hiyo ipo katika ziara ya kutembelea Viwanda mbalimbali Mkoani humo.
  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakiashuhudia bidhaa ya mafuta ya Alizeti iliyo tayari kwa ajili ya kupelekwa sokoni walipotembelea Kiwanda cha Mount Meru kilichopo Mjini Singida hii leo. Picha na Ofisi ya Bunge

  0 0   Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC) baada ya Kamati hiyo kumtembelea ofisini kwake leo. Kamati hiyo iko ziara Mkoani Morogoro.
  MOROGORO 2
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mhe. Vedasto Ngombale akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo na watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa LAAC, Mhe. Abdallah Chikota. Kamati hiyo ilikwenda kumtembelea Mkuu wa Mkoa kabla ya kuanza ziara yake ya kikazi mkoani humo
  MOROGORO 3
  Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Stephen Kabwe na watendaji mbalimbali wa Mkoa huo.Kamati hiyo ilikwenda kumtembelea Mkuu wa Mkoa kabla ya kuanza ziara yake ya kikazi mkoani humo

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola akipata maelezo kutoka kwa Annastazia Daniel,Msanifu Majengo katika banda la TBA kwenye maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola akipokea Zawadi kutoka kwa Ngeta Mwaitande Katibu Msaidizi Baraza la Wafanyakazi wa TBA katika banda la TBA kwenye maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola akiwasili katika banda la Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwenye maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola akisaini kitabu cha wageni banda la Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwenye maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma


  Bw.Baltazar Kimangano,Mkurugenzi wa Idara ya Mliki wa Wakala wa Majengo Tanzania akizungumza na Askari ambaye alitembelea banda la TBA kwenye maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodomaa  Bw.Baltazar Kimangano,Mkurugenzi wa Idara ya Mliki wa Wakala wa Majengo Tanzania katika akiwa kwenye picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Wakala wa Majengo Tanzania kwenye maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma  Afisa Miliki wa TBA Bw.Fredy Magula akifafanua jambo kwa wananchi waliotembelea banda la TBA kwenye maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma  Maofisa wa TBA wakiwa katika picha ya pamoja kwenye maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma  Maofisa Miliki wa TBA wakiendelea kutoa Elimu kwa wananchi waliotembelea banda la TBA kwenye maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma  Baadhi ya Wananchi waliotembelea banda la TBA wakiendelea kupata maelezo kutoka kwa Maofisa kwenye maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma  Afisa Utumishi wa TBA Bw.Lumuli Mwangosi akipokea Cheti cha Ushiriki wa maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma


  Afisa Utumishi wa TBA Bw.Lumuli Mwangosi akionesha Cheti cha Ushiriki wa maadhimisho ya Jeshi la zimamoto na uokoaji yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma

  …………………….

  Na.Alex Sonna,Dodoma

  Katika kukabiliana na upungufu wa nyumba za watumishi wa serikali wanaohamia jijini Dodoma, Wakala wa majengo nchini (Tba) wameanza ujenzi wa nyumba 100 za watumishi wa umma katika eneo la Nzuguni Jijini hapa.
  Hayo yamebainishwa leo na Ofisa Milki wa TBA, Fred Mangula wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya wiki ya zimamoto yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri . 

  Mangula amesema kuwa TBA ina jumla ya ekari 600 za ardhi zilizopo Nzuguni ambazo wanatarajia kujenga nyumba kwa ajili ya kuwauzia na kuwapangisha watumishi wa umma wanaohamia Dodoma.“Sisi kama wakala wa majengo wa serikali tumejipanga kutatua changamoto ya uhaba wa makazi kwa watumishi wa umma wanaohamia makao makuu Dodoma, na kwa kuanza tutajenga nyumba 100 eneo la Nzuguni kwa ajili ya watumishi wa umma,” amesema Mangula.

  Pia amongeza kuwa siyo hapo tu bali hata katika eneo la Itega lililopo jijini hapa wana eneo la ardhi ambalo watajenga nyumba kwa ajili ya viongozi ambapo ujenzi wa nyumba hizo utaanza hivi karibuni.Aidha amesema TBA ipo katika mchakato wa kujenga nyumba za bei nafuu kwa ajili ya kuziuza na kuzipangisha kwa watumishi wa umma.

  Naye Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano wa TBA, Edina John amesema kuwa katika ujenzi wa majengo wanazingatia miundombinu ambayo haitasababisha nyumba kushika moto hata kama utatokea.“Kwa hiyo kwenye nyumba tunazojenga tunahakikisha kuwa tunaweka miundombinu ambayo itawezesha nyumba kutoshika moto hata kama utatokea, na hii tumeifanya kwenye majengo mengi ambayo tumeshayajenga na ndiyo maana hakuna kesi za moto katika majengo yetu,” amesema John.

  Kufika mpaka sasa wakala wa Majengo Tanzania wameshajenga majengo mengi nchini kwa kuwa ina rasilimali za kutosha kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao ikiwemo rasilimali fedha.Naye Rachel Kyando ambaye ni mpangiliaji majengo kutoka TBA amesema kuwa wakala huo ndiyo wakala pekee wa serikali katika ujenzi ambao hutoa ajira kwa jamii inayozunguka miradi inayotekelezwa na wakala huo.

  Amesem TBA inatekeleza miradi mingi ya ujenzi hapa nchini kwa hiyo huwa inatia ajira kwa jamii husika kwa kushiki katika ujenzi wa miradi hiyo.

  0 0

  Na Fatma Salum-MAELEZO
  Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni linawashikilia watuhumiwa watatu kwa tuhuma za kumshambulia na kumsababishia maumivu makali mtu anaetambulika kwa jina la Robson Orotho ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Bunju A Jijini Dar es Salaam.
  Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Murilo Jumanne Murilo, imebainishwa kuwa sababu ya kushambuliwa kwa mfanyabiashara huyo ni kutokulipa faini ya usafi kiasi cha shilingi elfu 50.
  Watuhumiwa hao watatu ni Kelvin Edson, Gudluck Festo na Rehema Nyange ambao wote ni Askari Mgambo wa Wilaya ya Kinondoni.
  Aidha imeelezwa kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kulitokana na taarifa mbalimbali zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii ambazo zilionesha kukiukwa kwa sheria za nchi, hivyo kupelekea Jeshi la Polisi kufanya ufuatiliaji wa haraka na kuwatia mbaroni watuhumiwa wote waliohusika na tukio hilo. 
  Pia taarifa hiyo imesema kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.
  Jeshi la Polisi linatoa wito kwa vyombo vyote vya umma na visivyokuwa vya umma kufanya kazi kwa kufuata misingi ya sheria, taratibu na kanuni za nchi.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akizungumza wakati wa mkutano wa utoaji wa taarifa ya uchunguzi wa kamati iliyoundwa na mkuu huyo kuchunguza ubadhilifu wa fedha za Ushirika wa watumia maji katika kijiji cha Mijongweni.
  Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akiwahoji baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji cha Mijongweni kuhusiana na ubadhilifu uliofanyika katika Ushirika huo.
  Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya ,akizungumza juu ya maamuzi yaliyochukuliwa mara baada ya kamati aliyoiunda kuwasilisha taarifa yake.
  Baadhi ya wananchi wakisikiliza kwa makini juu ya maamuzi yaliyochukuliwa na Mkuu huyo wa wilaya .
  Baadhi ya wananchi wakionesha mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa mkutano huo.
  Katibu tawala wa wilaya ya Hai,Upendo Wera akizungumza katika mkutano huo.
  Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Mijongweni ,Omary Mohamed akizungumza kwa niaba ya wananchi wengine katika mkutano huo.
  Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akitizama baadhi ya mashine zilizotolewa kwa Ushirika huo ambazo zinatajwa kutumika huku mapato yake hayajulikani yalipo.
  Moja ya Mashine hizo ikiwa tayari imeharibika baada ya kuondolewa Roller inayotumika kwa ajili ya kutembelea.
  Mashine mpya ya Ushirika huo ambayo haijaanza kutumika bado.
  Baadhi ya watuhumiwa wa ubadhilifu wa fedha za Mradi wa Ushirika huo wakiwa kwenye gari la Polisi mara baada ya kukamatwa wakiwa eneo la mkutano.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.


  -WADAIWA KUFANYA UBADHILIFU WA ZAIDI YA MIL 200.
  -WENGINE WAUZA VIPURI VYA MASHINE.
  WATU 16 wakiwemo viongozi wa Bodi ya Ushirika wa Umoja wa watumia maji katika kijiji cha Mijongweni (UWAMI) wanashikiliwa na Jeshi la  Polisi kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya  wakituhumiwa kuhusika na ubadhilifu wa fedha za mradi zaidi ya Sh Mil 200.
  Mbali na Viongozi wa Bodi ya ushirika huo wakiongozwa na Mwenyekiti wake ,Nuru Ndoma pia wamo baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji, Viongozi wa kamati ya mpito ya kusimamia mradi huo ikiongozwa na Alex Mkwizu.
  Kukamatwa kwa Viongozi hao kunatokana na taarifa ya uchunguzi uliofanywa na kamati iliyoundwa na  Mkuu huyo wa wilaya kuchunguza madai ya ubadhilifu wa fedha baada ya kukataa taarifa yaawali ya  kamati kama hiyo iliyoundwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo Gelasius Byakanwa.
  Tuhuma zinazowakabili watu hao zimetajwa kuwa ni pamoja na kuuzwa kinyemela kwa Mashine ya kulimia (Power tiller ) aina ya Kubota iliyotolewa na Wizara ya Kilimo kwa kijiji cha Mijongweni ambayo inatajwa kuuzwa kwa mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Yusuph Losindilo.
  Baadhi ya viongozi hao pia wanatajwa kutakatisha fedha za malipo ya ukodishwaji wa mashine ya kuvunia Mpunga kwa kuziingiza katika akaunti ya kijiji na kasha kuzitoa wakati huo huo na kuzipangia matumizi yasiyokuwa na maelezo ya kutoshereza.
  Aidha watu hao pia wanadaiwa kuuza baadhi ya vipuri vya Mashine hizo na baadae kuonesha kuwa wamenunua vipuri kwa ajili ya matengenezo ya mashine hizo huku ikionyesha vipuri vinavyodaiwa kununuliwa ni vile vilivyoletwa pamoja na mashine.
  Katika taarifa yake ,Mwenyekiti wa kamati hiyo maalumu ya uchunguzi ,Valeria Banda alisema wizara ya Kilimo ,chakula na Ushirika kupitia Halmashauri ya wilaya ya Hai ilipeleka mashine tano za kuvuna na moja ya kupura mpinga kwa lengo la kupunguza adha ya wananchi kuvuna na kupura mpunga kwa kutumia mikono.
  “Lengo jingine la kutolewa kwa mashine hizi ilikuwa ni kuongeza chanzo cha mapato kwa wananchi wa kijiji cha Mijongweni ,mashine tatu zenye thamani ya Sh Mil 222.5 zilikuwa ni Combine Harvester aina ya Kubota , mbili aina ya Daedong na moja ya Kupura mpunga (Paddy thresher) zenye thamani ya Sh Mil 152.8”alisema Valeria.
  Alisema katika kuendeleza ubadhilifu watu hao wanadaiwa kushindwa kusimamia matumizi ya mashine hizo  ambapo inadaiwa wajumbe wa bodi walipangiana zamu ya kusimamia mashine izo wakati wa zoezi la uvunaji kwa maslahi yao binafsi huku wengine wakivuna nyakati za usiku bila kuwasilisha hesabu za mavuno hayo kwa uongozi.
   “Mfano Mayunga Mathayo anatuhumiwa kuvuna nyakati za usiku na kutowasilisha hesabu za fedha alizokuwa anapata ,hali iliyosababisha afukuzwe kuwa mjumbe wa bodi.Mayunga pia aliuza Hydrolic pump (Orignal) aina ya Kubota yenye thamani ya sht Mil 5 ya mashine namba tisa ya kuvuna mpunga na kufunga pump isiyo na ubora kwenye mashine hiyo ambayo kwa sasa imeharibika.”alisema Valeria.
  Valeria alisema fedha zilizokuwa zinapatikana shambani zaidi ya asilimia 50 zilifanyiwa matumizi shambani na wakati mwingine fedha zote zilitumika huko huko shambani bila kufikishwa ofisini na hata zilizofikishwa bado zilipangiwa tena matumizi.
  “Baada ya fedha kufanyiwa matumizi zilizobaki zilipelekwa SACCOS ya jitegemee na kutolew wakati huo huo kwa matumizi mengine yasiyo na kibali wala vithibitisho vyovyote ,mfano Oktoba 18 ,2016 kiasi cha sh 810,000 ziliingizwa kwenye akaunti na tarehe hiyo hiyo Sh 800,000 zikatolewa ,katibu wa Bodi Severa Kimati aliyehusika kuziweka na kuzitoa hakuwa na maelezo ya kutosha zaidi ya kusema alitumwa na mwenyekiti wa Bodi Nuru Ndoma”alisema Valeria.
  Alisema fedha ambazo zingetakiwa kuwekwa katika akaunti ya kijiji toka Machi,2016 wakati mashine hizo zikianza kufanya kazi hadi kufikia Juni ,2018 kipindi ambachowalifanya kazi wajumbe wawili kutoka kwenye jamii zilipaswa kuwa Sh Mil 285.6 lakini kiasi kilichopo ni Sh Mil 10.9 ambazo zilipatikana baada ya afisa mtendaji na afisa ugani kuamua kusimamia mashine moja katika kipindi cha mwezi mmoja.
  Akizungumza baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo ,Mkuu wa wilaya ya Hai,Lenga Ole Sabaya alimuagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Hai,Lwelwe Mpina kumkamata aliyekuwa Mkuu wa idara ya Ushirika wa wilaya hiyo , Raphael Mbwambo ambaye alitajwa pia kuhusika katikaubadhirfu huo.
  Alisema viongozi wa Bodi, ya Ushirika huo hawakuwa na uhalali kutokana na kwamba hakuna wanahisa wala wanachama waliokaa  na kuwachagua  na kwamba waliteuana kwa maslahi yao binafsi huku akitaka fedha zote zilizopotea kurejeshwa.
  “HAwa viongozi wa Bodi kwa kushirikiana na wajumbe wa serikali ya kijiji warudishe fedha walizoiba za wananchi wanyonge wa kijiji cha Mijongweni ,Nimeelekeza wasiingie kwenye ofisi yoyote ya umma,hawa ni waharifu kama waharifu wengine hadi itakapothibitika vinginevyo.”alisema Ole Sabaya.
  Wanaoshikiliwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya ushirika huo ,Nuru Ndomba  na Katibu wake wake  Severa Kimati  pamoja na wajumbe wengine, Salama Amani,Sadiki Msangi, Abuu Musa na D eogratius Bruno,.
  Wengine ni Alex Mkwizu, Mashati Amani, Bakari Malola, Adamu Mdaki,Mayunga Mathayo ,Abdalah Dhamiri,Richard Msele,Ramadhan Miraji ,Miraji Araba na Koswai Mrisho.
  Mwisho.

  0 0
  Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabia kizungumza na waajiriwa wa kampuni ya Professional Cleaner watakaokuwa wanatoa huduma kwa mteja (customer care) kwa wadau wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mafunzo mafupi ya utoaji wa huduma bora kwa mteja leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Taasisi hiyo Agnes Kuhenga
  Picha 2
  Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga (kushoto) akitoa maelekezo ya namna ya kutoa huduma bora kwa waajiriwa wa kampuni ya Professional Cleaner watakaokuwa wanatoa huduma kwa mteja (customer care) kwa wadau wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mafunzo mafupi ya utoaji wa huduma bora kwa mteja leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
  Picha 3
  Mkurugenzi Idara ya Uuguzi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya (kulia) akitoa mada ya namna ya kupokea wagonjwa kwa waajiriwa wa kampuni ya Professional Cleaner watakaokuwa wanatoa huduma kwa mteja (customer care) kwa wadau wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mafunzo mafupi ya utoaji wa huduma bora kwa mteja leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
  Pix 4
  Mfanyakazi wa kampuni ya Professional Cleaner ambaye ni mmoja kati ya watoa huduma kwa mteja (customer care) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Khadija Abeid akielezea namna ambavyo atakua akitoa huduma bora kwawatejawakatiwamafunzomafupiyautoajiwahuduma bora kwamtejaleokatikaukumbiwaTaasisiyaMoyoJakayaKikweteJijini Dar es Salaam.
  Pichana: Genofeva Matemu
  ………………………….
  Na:Salome Majaliwa
  Wafanyakazi kutoka kampuni ya Professional Cleaner ambao watakua wakitoa huduma kwa mteja (customer care) katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wametakiwa kufanyakazi kwa bidii kwa kutoa huduma bora kwa wateja ili kuboresha huduma za Taasisi hiyo.
  Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati wa mafunzo mafupi kwa watua huduma hao leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
  Prof. Janabi amesema katika kuboresha huduma zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Taasisi imeanzisha kitengo cha Huduma kwa Mteja (Customer Care) ili kupunguza msongamano wa foleni kwa wagonjwa wakati wa matibabu na kuongezatija katika utoajiwa huduma.
  “Taasisi hii inaona wagonjwa wa nje kati ya 150 mpaka 300 kwa siku; ili Kuboresha huduma tunazozitoa Taasisi imeona ni vyema tuwe na kitengo cha huduma kwa mteja kitachoratibu utoaji wa huduma kwa wagonjwa kwa kufuata taratibu zilizopo” alisema Prof. Janabi
  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kutoka Taasisi hiyo Agnes Kuhenga amewataka watumishi wa kitengo cha huduma kwa mteja kuwa hudumia wagonjwa kwa kufuata haki na wajibu wa mtoa huduma kwa mteja.
  Naye Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delila Kimambo amewahasa watumishi wa kitengo cha huduma kwa mteja kuwa na upendo kwa wagonjwa, kuwa sikiliza na kuwajali pale wanapohitaji msaada kutoka kwao.
  “Wagonjwa hawafanani kuna wengine wanakuja wakihitaji huduma ya haraka zaidi; nyie mkawe msaada kwao kwa kuwa wabunifu ili huduma zinazohitaji kazi weze kupatikana kwa wakati na kuweza kuokoa maisha ya wagonjwa wetu” alisema Dkt. Delila

  0 0   Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa akitolea ufafanuzi tukio la ajali iliyohusisha gari la kubebea wagonjwa(ambulance), Mali ya JWTZ na gari aina ya Toyota canter yenye namba za usajili T.764 ACK ,huko eneo la Kibiki ,Bwilingu Chalinze Mkoani Pwani .
  Picha na Mwamvua Mwinyi
  …………………
  NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
  ELINIKUNDA Mushi (50) ,amefariki dunia baada ya gari la kubebea wagonjwa (ambulance) mali ya jeshi la wananchi wa Tanzania  (JWTZ) , lililokuwa likimuwahisha hospital ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu kupata ajali eneo la Kibiki, kata ya Bwilingu, Chalinze mkoani Pwani.
   
  Katika ajali hiyo watu wengine wanne walijeruhiwa baada ya dereva wa ambulance kudaiwa kuligonga gari nyingine kwa nyuma,lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara kwa ajili ya matengenezo .
   
  Akitoa taarifa kuhusu tukio hilo, kamanda wa polisi mkoani Pwani, (ACP) Wankyo Nyigesa ,alisema ajali hiyo imetokea alfajiri agost 31 mwaka huu.Alieleza, gari namba 3489 JW 12 aina ya Ashok Leyland inayomilikiwa na kikosi cha jeshi 911 KJ cha Ihumwa Dodoma, mali ya JWTZ, lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Dar es salaam aliligonga gari lingine lenye namba za usajili T. 764 ACK aina ya Toyota canter na kusababisha kifo cha mtu mmoja .
   
  Nyigesa alisema, aliyepoteza maisha ni Elinikunda ambae alikuwa mgonjwa akipelekwa kwenye matibabu katika hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi. 
  “Watu wanne walijeruhiwa ambao ni pamoja na Beatrice Shidodolo (56)muuguzi wa hospital ya hospital ya Dodoma, Ufo Swai (48) mkazi wa Ngerengere yeye alikuwa akimhudumia mgonjwa akiwa Dodoma “alisema Nyigesa. Nyigesa aliwataja majeruhi wengine kuwa ni Justine Patrick (28)ambae alikuwa dereva wa gari namba T. 764 ACK iliyokuwa imeegeshwa kwa matengenezo na Rashid Rais (35) alikuwa fundi wa gari hilo wakazi wa Chalinze. 
   
  Uchunguzi wa awali umebaini katika ambulance hiyo ilikuwa imepakia watu wengi wanne ambao hawakuweza kupata majeraha yoyote ambao ni MT. 3480 SGT Elimasa Mushi (40) askari wa JWTZ makao makuu ya Jeshi (MMJ). Nyigesa aliwataja wengine kuwa ni MT 95881 PTE Taulin Kaira (30) askari wa  911 KJ aliyekuwa msindikizaji wa gari hilo la wagonjwa, Eveline Stanley (25) alipewa msaada wa usafiri na mtoto wake wa miezi 11 anaitwa Nicholous Petro na dereva wa gari hilo MT. 67451 SGT Shaban Mpwate. 
   
  Kamanda huyo alifafanua, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospital ya Jeshi ya Lugalo na majeruhi wamepelekwa katika hospital hiyo. Dereva wa ambulance Shaban Mpwate,anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi. Nyigesa aliwaasa madereva wa magari ya dharura kama magari ya wagonjwa kuhakikisha wanachukua tahadhari kubwa wanapokuwa wamepewa kipaombele na watumiaji wengine wa barabara ili kuweza kuepuka ajali zembe. 

  0 0


   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI, Mkapa House jijini Dodoma leo.
  Picha na ofisi ya Makamu wa Rais
  ………………..

  Na Judith Mhina-MAELEZO
  Kitendo cha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushtakiwa mara nyingi zaidi katika Mahakama ya Afrika ya Haki ya Binadamu ni ushahidi tosha kuwa Serikali imetoa uhuru wakushtakiwa kutokana na makubaliano ya Kimataifa yaliyosainiwa na Serikali yenyewe.

  Maneno hayo yamethibitishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye amesema kuwa, Serikali itahakikisha Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu (AfCPHR) kuwa itatekeleza kwa ukamilifu amri na hukumu mbalimbali zinazotolewa na mahakama kama ambavyo imeainishwa katika mkataba wa kuridhia mahakama hiyo.
  Kutokana na taarifa iliyoripotiwa na gazeti la Mtanzania, toleo Na. 9013 la tarehe 25 Agosti 2018 lenye kichwa cha Habari “Tanzania yaongoza kwa kushtakiwa Afrika ” ambapo Serikali ya Tanzania imedhihirika kuwa na mashtaka 117 katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu yenye jumla ya kesi 180.

  Tanzania kama nchi ni kinara wa kulinda haki za binadamu Afrika Mashariki na kati na ndio maana Makamu wa Rais, Mhe Samia amesema “Serikali itaendelea kushirikiana na mahakama hiyo katika kulinda haki hizo.  Hivyo kitendo cha kuwa na mashauri mengi zaidi katika mahakama hiyo inatokana na uelewa mkubwa wa wananchi katika kutafuta haki zao pia urahisi wa kuifikia mahakama hiyo. Uhuru wa kuishtaki Serikali upo katika nchi ambayo ina uhuru wa kweli na Utawala wa Sheria na hili ni jambo muhimu sana Watanzania kulifahamu. Nchi ambazo hazijali Haki za Binadamu huwezi kuishtaki Serikali, ndio maana Tanzania imeridhia makubaliano mbalimbali ya Kimataifa na kikanda.

  Baadhi ya mikataba hiyo ambayo imeandaliwa na Chama Cha Wanasheria Tanzania Bara “ Zijue Haki za  Binadamu, Sheria katika lugha  rahisi ni kama vile “Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu la Mwaka 1948”.  Tamko hili limekubaliwa na kupitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 10 Desemba, mwaka 1948.Hivyo, Tamko hilo ndilo chimbuko la kulindwa kwa haki za binadamu duniani kote. Tamko hili linajumuisha, kwa pamoja, aina zote za haki za binadamu, yaani haki za kiraia na kisiasa, na haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

  Tamko la Kimataifa la haki za binadamu ni “tamko” halina masharti ya kuzibana nchi kutekeleza haki za binadamu kisheria. Pamoja na kuwa halina nguvu kisheria. Tamko hili linaheshima kubwa sana kimataifa na nchi nyingi wamelitambua na kuingiza kwenye katiba zao. Tanzania imefanya hivyo katika Ibara ya 9 (f) ya Katiba ya nchi ya mwaka 1977.

  Nyingine ni “Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa wa Mwaka 1966. Ambao ulipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1966 na kuanza kutumika Machi, 1976. Tanzania imeukubali na kuuridhia mkataba huo tarehe 11 Septemba 1976.Kama nchi Tanzania ina jukumu la kuheshimu na kuwahakikishia watu wote uwepo wa haki hizi bila ubaguzi wa aina yoyote, kama vile rangi, kabila, lugha, dini, asili au utaifa wao; Kupitisha sheria na hatua nyingine za kulinda haki zilizomo kwenye mkataba pale ambapo sheria au hatua zozote hazijafanywa;
   Aidha, sheria zimeweka utaratibu kuhakikisha mtu yeyote aliyeingiliwa au kukiukwa kwa haki na uhuru wake anapata ufumbuzi kama vile kulipwa fidia;  Kuhakikisha usawa kati ya wanaume na wanawake katika kufaidi haki za kiraia na kisiasa zilizoorodheshwa kwenye mkataba.
  Vilevile, kuna Mkataba wa Kiafrika wa Haki za Binadamu na Haki za Watu wa Mwaka 1981 Mkataba huu ulipitishwa na wakuu wa nchi na serikali za Umoja wa Nchi za Afrika (OAU), Nairobi – Kenya mwaka 1981.

  Hadi leo nchi zote za Afrika ni wanachama wa Mkataba huu. Nchi wanachama zina wajibu wa kutambua haki, uhuru na wajibu uliomo kwenye mkataba na kuchukua hatua za kisheria kuzipa nguvu haki. Mkataba wa Kiafrika wa Haki za Binadamu na Haki za Watu unatambua na kulinda aina zote za haki za binadamu yaani haki za kisiasa, kiraia, kiuchumi, kiutamaduni na kijamii.
  Mfano wa haki za binadamu zinazotambuliwa na kulindwa kwa Haki za Binadamu ni pamoja na Haki ya kutobaguliwa, usawa, haki ya Zijue Haki za Binadamu  7 kuheshimiwa, haki na uhuru ya kuabudu na kujumuika na wengine. Ulinzi wa Haki za Binadamu Mlinzi wa kwanza wa haki hizi ni binadamu mwenyewe.

  Akitembelea Mahakama hiyo Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Julius Mashamba na Naibu wake Dkt Ally Possi, wametimiza wajibu wao wa kufuatilia mahakama hiyo, kujua nini kimejiri ili kuhakikisha kila Mtanzania ana haki ya kusikilizwa na kutendewa haki.“Wengi wanaolalamika haki zao katika kesi za jinai hazijatekelezwa kwa namna kesi zilivyosikilizwa na kuchelewa kupata nakala za mwenendo wa kesi ili wakati rufaa au kunyimwa msaada wa sheria” amesema Dkt. Mashamba
  Dkt Mashamba ameongeza kuwa, jambo kubwa lililofanya kutembelea Mahakama hiyo ni wingi wa kesi hizo na hasa zikichukuliwa kama zimekuwa zikifanana kwani wengi hudai kutopata masaa wa kisheria wakati mahakama za ndani zilizotoa uamuzi wake.

  Chimbuko na Utambuzi wa Haki za Binadamu kwa kipindi kirefu haki za binadamu zimekuwepo na kuongoza maisha ya mwanadamu kulingana na asili ya kila mwanadamu. Kukua na kutambulika kwa haki za binadamu kumepitia madaraja kadhaa kulingana na hatua kadhaa za kukua kwa jamii.
  Kabla ya karne ya 19 haki hizi zilikandamizwa na kupuuzwa na jamii, serikali iliyotawala katika jamii husika na wakati mwingine mataifa yaliyoingia kutawala mataifa mengine. Hali hii ililawalazimisha watetezi wa haki za binadamu kufanya kazi ya ushawishi ili kuanza hatua ya kuainisha na kuzitambua haki za binadamu.

  Hatua ya kwanza kabisa ya utambuzi wa haki za binadamu ilitokana na kuzidi kwa vitendo vya ubaguzi, ukatili, unyanyasaji, kutumikisha watu kwa kuwaita watumwa na uonevu dhidi ya binadamu na matendo mengine ya aina hiyo.

  0 0   Kaimu Kamishna wa Fedha na Lojistiki, DCP Leonard Paul na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Mhimbili Prof. Andrea Pembe wakisaini makubaliano ambapo Chuo hicho kimelipatia Jeshi la Polisi eneo la ekari mbili katika Kampasi ya Mloganzila kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi.Makubalino hayo yalisainiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.(Picha na Jeshi la Polisi)
  2 (11)
  Kaimu Kamishna wa Fedha na Lojistiki, DCP Leonard Paul na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Mhimbili Prof. Andrea Pembe wakibadilishana nyaraka baada ya kusaini makubaliano ambapo Chuo hicho kimelipatia Jeshi la Polisi eneo la ekari mbili katika Kampasi ya Mloganzila kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi.Makubalino hayo yalisainiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.(Picha na Jeshi la Polisi)
  3 (9)
  Kaimu Kamishna wa Fedha na Lojistiki, DCP Leonard Paul na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Mhimbili Prof. Andrea Pembe wakionyesha nyaraka baada ya kusaini makubaliano ambapo Chuo hicho kimelipatia Jeshi la Polisi eneo la ekari mbili katika Kampasi ya Mloganzila kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi.Makubalino hayo yalisainiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.(Picha na Jeshi la Polisi)
  5 (6)
  Kaimu Kamishna wa Fedha na Lojistiki, DCP Leonard Paul na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Mhimbili Prof. Andrea Pembe wakizungumza baada ya kusaini makubaliano ambapo Chuo hicho kimelipatia Jeshi la Polisi eneo la ekari mbili katika Kampasi ya Mloganzila kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi.Makubalino hayo yalisainiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.(Picha na Jeshi la Polisi)
  4 (9)
  Maofisa kutoka Makao Makuu ya Polisi na viongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Mhimbili  wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kusaini makubaliano ambapo Chuo hicho kimelipatia Jeshi la Polisi eneo la ekari mbili katika Kampasi ya Mloganzila kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi.Makubalino hayo yalisainiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.(Picha na Jeshi la Polisi)

  0 0  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde ameishukuru sekta binafsi kwa mchango mkubwa inaoutoa katika sekta ya Uchumi wa Viwanda na fursa za Ajira inazozitengeneza kupitia uwekezaji.
  vu2Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo katika uzinduzi wa muonekano mpya wa kinywaji kikali cha K-VANT katika Hotel ya Serena Jijini Dar es salaam ambapo pia amechukua fursa hiyo kuipongeza kampuni ya MEGA BEVERAGES kwa kutoa fursa za AJIRA kwa wananchi zaidi ya 1000 na pia kwa uwekezaji wa kiwanda cha kuzalisha vinywaji na kuitaka kampuni hiyo kuzingatia ubora ili kuifanya bidhaa yao kuwa shindani na kuvuka mipaka ya Tanzania.
  vu3Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni MEGA BEVERAGES Bw. Francis Kimaro ameishukuru Serikali kwa mazingira wezeshi yaliyofanikisha uwekezaji huo wa kiwanda na kuahidi kuzalisha bidhaa zenye ubora.

  0 0

  Maadhimisho ya Juma la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Maonesho ya wadau wa jeshi hilo yamefungwa leo Dodoma, ambapo msisitizo ulikuwa ni kwa watanzania kushiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa kufunga ving'amuamoto viwandani.
   Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala akisindikizwa na Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwenda kutembelea mabanda ya wadau wakati wa maazimisho ya Juma la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yalifanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
   Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, akioneshwa kifaa mahsusi kiitwacho "king'amua moto" kitumikacho kugundua moto ukiwa hatua za awali na kuwezesha kukabiliwa kwa urahisi  wakati akitembelea mabanda ya wadau wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwenye maonesho yaliyoandaliwa sambamba na maazimisho ya Juma la Jeshi hilo yalifanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
   Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala akipata maelezo ya namna ya utoaji wa huduma mbalimbali  za kiuhamiaji mbalimbali toka kwa Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji, Alice Mhoja wakati akitembelea mabanda ya wadau wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwenye maonesho yaliyoandaliwa sambamba na maazimisho ya Juma la Jeshi hilo yalifanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
   Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakionesha namna ya kuokoa mtu aliyenaswa katika jengo refu.
  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala akipata maelezo ya namna ya kutumia zana mbalimbali  zinazotumika kuzima mioto ya aina tofauti toka kwa Luteni Kalalawina wakati akitembelea mabanda ya wadau wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwenye maonesho yaliyoandaliwa sambamba na maazimisho ya Juma la Jeshi hilo yalifanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.

  0 0


  Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Amina Salum Ali akitoa hutuba yake katika kilele cha Maadhimisho ya 16 ya siku ya Tiba asili Afrika.  Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya afya Zanzibar Dkt. Mayasa Salum Ali na kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Mzee Mohamed Kheri. Maadhimisho hayo yalifanyika Ukumbi wa Shekh Idrisa Abdul Wakili Kikwajuni mjini Zanzibar. Picha na Abdalla Omar-Maelezo Zanzibar. 
  2 (10)
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya afya Zanzibar Dkt. Mayasa Salum Ali akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya 16 ya siku ya Tiba asili Afrika yalifanyika Ukumbi wa Shekh Idrisa Abdul Wakili Kikwajuni mjini Zanzibar. Picha na Abdalla Omar-Maelezo Zanzibar. 

  4 (8)
  Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Amina Salum Ali akiangalia Dawa asili kutoka kwa Vikundi mbalimbali vya Wajasiriamali waliofika Zanzibar kushiriki Maadhimisho ya 16 ya siku ya Tiba asili Afrika ambapo kwa Zanzibar yalifanyika Ukumbi wa Shekh Idrisa Abdul Wakili Kikwajuni mjini Zanzibar. Picha na Abdalla Omar-Maelezo Zanzibar 
  5 (5)
  Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Amina Salum Ali akiangalia Dawa asili kutoka kwa Vikundi mbalimbali vya Wajasiriamali waliofika Zanzibar kushiriki Maadhimisho ya 16 ya siku ya Tiba asili Afrika ambapo kwa Zanzibar yalifanyika Ukumbi wa Shekh Idrisa Abdul Wakili Kikwajuni mjini Zanzibar. Picha na Abdalla Omar-Maelezo Zanzibar 
  6 (1)
  Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Amina Salum Ali akiangalia Dawa asili kutoka kwa Vikundi mbalimbali vya Wajasiriamali waliofika Zanzibar kushiriki Maadhimisho ya 16 ya siku ya Tiba asili Afrika ambapo kwa Zanzibar yalifanyika Ukumbi wa Shekh Idrisa Abdul Wakili Kikwajuni mjini Zanzibar. Picha na Abdalla Omar-Maelezo Zanzibar 1 (11)
  Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Amina Salum Ali akiangalia Dawa asili kutoka kwa Vikundi mbalimbali vya Wajasiriamali waliofika Zanzibar kushiriki Maadhimisho ya 16 ya siku ya Tiba asili Afrika ambapo kwa Zanzibar yalifanyika Ukumbi wa Shekh Idrisa Abdul Wakili Kikwajuni mjini Zanzibar. Picha na Abdalla Omar-Maelezo Zanzibar 

  0 0   MKUU wa wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Jabiri Shekimweri kushoto akizungumzia na Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana mikakati yao katika zao la Korosho wakati wa ziara ya viongozi wa bodi hiyo kutembelea maeneo mapya kuhamasisha kilimo hicho
   Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana kulia akisisitiza jamabo kwa Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kuhusu ziara yao wilayani humo
    Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana kulia akiagana na Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodomaa mara baada ya kumaliza mazungumzo
   Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Jabir Shekimweri katika akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa bodi ya Korosho kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Mpwapwa Sarah Kombakulia  ni Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana na Afisa Kilimo wa Bodi hiyo Frank Mfutakamba

   Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana kulia akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwapwa Paul Mamba Swea wakati wa ziara hiyo
   Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana katikaati akiwa na Kaimu Kaimu Mkuu wa Gereza la Mpwapwa mkoani Dodoma Mratibu Magereza Joseph Mwita Sabayo kushoto wakitembelea shamba la mfano la Magereza
   Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana katikati akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo ya kutembeleaa shamba la mfano la magereza wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma kushoto ni Kaimu Kaimu Mkuu wa Gereza la Mpwapwa mkoani Dodoma Mratibu Magereza Joseph Mwita Sabayo
   Afisa Kilimo kutoka Bodi ya Korosho nchini Frank Mfutakamba kushoto akimueleza kitu kwenye mmea wa Korosho Kaimu Mkuu wa Gereza la Mpwapwa mkoani Dodoma Mratibu wa Magereza Joseph Mwita Sabayo
  Wakiwa kwenye picha ya pamoja.

  NA MWANDISHI WETU, MPWAPWA.

  MKUU wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Jabiri Shekimweri amesema wanalitumia zao la Korosho kujenga uchumi,kuimarisha mapato yao sambamba na vyanzo vyengine vya Halmashauri kutokana na kwamba bado ni zao jipya kwao.

  Shekimweri aliyasema hayo  wakati akizungumza na viongozi wa bodi ya Korosho nchini waliofanya ziara ya kutembelea wilaya hiyo ambapo pia waliweza kuwatembelea wakulima ikiwa ni mpango wao kupita kwenye maeneo mapya yanayolima zao hilo kuwahamasisha wakulima ikiwemo shamba la mfano la magereza wilayani Mpwapwa.

  Alisema hilo linatokana na kwamba agenda ya zao la Korosho ndio wanalisimamia kwa wigo mpana na walikubaliana kwenye Halmashauri ikiwemo Baraza la madiwani ,Vikao vya Kamati ya Ushauri ya wilaya hiyo (DCC) wakiwemo wadau mbalimbali kwamba wajenge uchumi wa wilaya hiyo kwa kutumia zao la mkakati la Korosho.

  Alisema katika agenda ya zao hilo wilayani humo hakuna namna nyengine watapata maendeleo kama hawatalichukua kama zaoi lao la uchumi na kuendelea kuhimiza wananchi kujikita kwenye kilimo hicho kutokana na kuwa na faida lukuki.

  “Kwa kweli agenda hizi tatu ni kubwa kujenga uchumi kupitia korosho,kuimarisha mapato ya wilaya yao kupitia Korosho na vyanzo vyengine vya halmashauri kwa sababu ni zao jipya,kupitia korosho mnyororo mrefu wanakwenda kutekeleza falsafa pana ya hapa kazi tu ya Mh Rais wetu Dkt John Magufuli”Alisema DC Jabiri.

  Alisema uanzishwaji wa zao hilo unafaida nyingi ikiwemo kutengeneza ajira ya kilimo cha biashara pia zao hilo litavutia viwanda vya ubanguaji korosho na hivyo utajibu Tanzania ya viwanda.

  “Kwani ukishakuwa na uzalishaji mkubwa sekta nyengine zitakuja zikiwemo za usafirishaji zitaamka na kuinua uchumi wa wilaya ya Mpwapwa,mkoa na Taifa kwa ujumla “Alisema.

  Aliongeza kwamba agenda ya pili ni kuanzisha mashamba darasa ambapo vijana wa Boda boda wana ekari 12 ambazo wanalima korosho lakini pia kuanzisha mashamba darasa ili watu waweze kujifunza ili waweze kulima zao hilo.

  Hata hivyo alisema mkakati tatu ni kushawishi namna bora ya upatikanaji wa miche kwani wilayani hapo walikuwa na vikundi saba vya uzalishaji ya miche kwa vitalu mwaka jana walizalisha miche 480,000 huku miche 100,000 ikisomwa na maji baada ya mvua kubwa kuonyesha.

  Kaimu Mkuu wa Gereza la Mpwapwa Mratibu Magereza Joseph Mwita Sabayo aliishukuru bodi ya Korosho kwa kuwatembelea kwenye shamba lao ambalo lilianzishwa mwaka 2009 likiwa limetueliwa na wilaya hiyo kuwa shamba darasa ambalo wananchi walikuwa wanajifunza kupitia shamba hilo.

  Alisema hapo mwanzo mikorosho ilikuwa ikionekana kulimwa mikoa ya kanda ya lakani baadae zao hilo liliweza kuenea maeneo mbalimbali huku gereza hilo wakilima ekari elfu hamsini na tisa wamejidhatiti kuhakikisha wanakuwa shamba la mfano

  0 0


  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe  akifurahi pamoja na viongozi wengine wa Wizara  leo Jijini Dodoma baada ya  kupokea kombe kutoka kwa Nahodha wa timu ya mpira wa miguu wanawake Bi. Asha Rashidi (hayupo katika picha) .

  Pix 2 (4)
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe  akisisitiza jambo kwa wachezaji walioshiriki mashindano ya Jumuiya ya Afrika Masharik (hawapo katika picha), wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji hao leo Jijini dodoma, kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Zanzibar Bw.Hamis Alli Mzee,anayefuata ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Susan Mlawi na  kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo.

  Pix 1 (5)
  Katibu Mkuu  Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi   akizungumza leo Jijini Dodoma na wachezaji walioshiriki mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  (hawapo katika picha) ambapo timu ya mpira wa miguu wanawake waliibuka washindi wa kwanza, katikati ni Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Harrison Mwakyembe na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo.
  Pix 4 (3)
  Baadhi ya wachezaji wa Twiga Stars wakimsikilza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika picha) wakati wa halfa ya kuipongeza timu hiyo leo Jijini Dodoma .
  Pix 5 (2)
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa timu  zilizoshiriki  mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo timu ya mpira wa miguu wanawake waliibuka washindi wa kwanza.
  Pix 6 (1)
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja  na wachezaji wa timu ya Karate .

  0 0

  Serikali imesema iko tayari kutangaza katika Gazeti la Serikali msitu wa Mwalimu Nyerere uliopo Butiama Mkoani Mara kama eneo lindwa kimazingira, kufuatia ahadi iliyotolewa mwaka jana wakati wa kilele cha Siku ya Mazingira Duniani iliyofanyika Butiama Mkoani Mara.

  Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba mara baada ya kutembelea eneo hilo na kuzungumza na mwakilishi wa familia hiyo Bw. Madaraka Nyerere. 

  Bw. Nyerere amesema kuwa kama familia watafurahi sana kwa eneo hilo kutangazwa kama eneo lindwa ikiwa ni pamoja na kuweka taratibu za matumizi sahihi ya uvunaji wa rasilimali ndani ya msitu huo na kutoa zuio kwa baadhi ya shughuli za kibinadamu isipokuwa kwa kibali maalumu tu. Akiwa katika mwendelezo wa ziara ya kukagua masuala ya usimamizi na uzingatiaji wa Sheria ya mazingira nchini, Waziri Makamba amesema kuwa lengo la kuhifadhi baadhi ya maeneo nchini ni kuhakikisha kuwa yanakuwa na usimamizi endelevu kwa manufaa ya wote. 

  Awali akiwa katika Manispaa ya Musoma Mkoani Mara Waziri Makamba ametembelea Mlima Mukendo uliopo Mtaa wa Nyerere, Kata ya Mukendo na kuridhia ombi wa Baraza la Madiwani la kuomba msitu huo uhifadhiwe kwa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004. 

   “Nawapongeza sana Uongozi wa Mkoa wa Mara, wao wameenda mbali zaidi kwa kupitisha azimio hili katika Baraza la Madiwani, hii inatupa sisi msukumo wa kufanya jambo hili kwa haraka zaidi, sisi kama Serikali tutaleta rasimu ya tangazo la gazeti mapema iwezekanavyo ili tukubaliane masharti na vigezo tutakavyoweka kabla ya kulitangaza rasmi katika gazeti la Serikali” Makamba alisisitiza. 

  Waziri Makamba ametoa rai kwa ungozi wa Mkoa wa Mara haraka iwezekanavyo kupendekeza majina ya maafisa wanaofaa kuteuliwa kuwa wakaguzi wa mazingira na kuliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Nchini (NEMC) ndani ya mwezi mmoja kutoa mafunzo kwa wakaguzi wa Mazingira walioteuliwa na watakaoteuliwa ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu. 

  “Mratibu wa Mazingira Kanda ya Ziwa, isipite tarehe 30/09/2018 kabla ya wakaguzi hawa kupatiwa mafunzo na vitambulisho” Makamba alisisitiza. 
  Nae Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima amesema Mkoa wake unalenga kutekeleza kwa vitendo kampeni ya kuifanya ‘Mara kuwa ya kijani’ na mikakati waliyojiwekea ni pamoja na kupanda miti milioni 10 ndani ya miaka miwili. 

  Katika kuunga mkono jitihada kubwa za Mkoa wa Mara katika kampeni ya kupanda miti Waziri Makamba ameahidi kutoa viriba Milioni Moja vyenye thamani ya Shilingi Milioni 5 na laki 5. Waziri Makamba anaendelea na ziara yake Mkoani Mara kwa kutembelea Wilaya ya Serengeti.
   Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima (kushoto) akimkaribisha mgeni wake Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba mara baada ya kuwasili Mkoani hapo kwa ziara ya kikazi ya kukagua, kutathmini na kuzungumza na viongozi, kuhusu maeneo yanayopendekezwa kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira na Kufuatilia utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi Mazingira ya 2004 katika ngazi za Serikali za Mitaa.
   Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na viongozi na watendaji katika ngazi mbalimbali Mkoani Mara. Pamoja na mambo mengine Waziri Makamba amewataka kuanzisha kamati za usimamizi wa mazingira katika ngazi za vijiji, vitongoji, Mitaa na Kata.
   Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na viongozi na watendaji katika ngazi mbalimbali Mkoani Mara. Pamoja na mambo mengine Waziri Makamba amewataka kuanzisha kamati za usimamizi wa mazingira katika ngazi za vijiji, vitongoji, Mitaa na Kata.
   Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (kulia) akizungumza na Bw. Madaraka Nyerere mara baada ya kutembelea katika makazi ya Hayati Mwl. Julius Nyerere Wilayani Butiama na kuona namna ya kuhifadhi msitu wa Mwalimu kwa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004.
   Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwa na viongozi wa Wilaya na Manispaa akipanda Mlima Mukendo ili kujionea namna ya kuuhifadhi ikiwa ni miongoni mwa maeneo yaliyopendekezwa na Baraza la Madiwani kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira.  0 0

    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela (wakwanza kulia) akiwaongoza wafanyakazi wa Mamlaka hiyo, Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa chas Julius Nyerere (JNIA) Bw. Paul Rwegasha (watatu kulia) na Afisa Uhusiano Bi. Bahati Mollel (wapili kulia) kukabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 5 (5,000,000/=) kwa mgeni rasmi kwenye hafla ya bunge kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule nchi nzima, Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda (wapili kushoto) na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya hafla hiyo, Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka. Hafla hiyo ilifanyika usiku wa kuamkia leo Septemba 1, 2018 jijini Dar es Salaam.

    NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
  MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imeunga mkono juhudi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Umoja wa Wabunge Wanawake wa Bunge hilo, (TWPG) kukusanya fedha kwa ajili ya kujenga vyoo salama vya shule nchi nzima kwa mtoto wa Kike kwa kutoa mchango wa kiasi cha Shilingi Milioni Tano (5,000,000).
  Katika hafla ya kuchangisha fedha kwa dhumuni hilo, iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela, alikabidhi msaada huo wa fedha kwa mgeni rasmi, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda.
  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa (TWPG), ambaye pia ni Mbunge wa Urambo, Mhe.Margareth S. Sitta, wazo la kutafuta fedha za ujenzi wa vyoo hivyo ni katika jitihada za kuhakikisha wanafunzi wote hususan wa kike, wanafurahia haki yao ya msingi ya kupata elimu katika mazingira rafiki na masafi bila kujali changamoto zinazosababishwa na tofauti zao za kimaumbile.
  Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Wabunge, Wakuu wa Taasisi za Umma na Binafsi, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, aliwapongeza Wabunge hao kwa hatua hiyo ya kuhakikisha kunakuwepo kwa  mazingira bora shuleni ili kutoa haki sawa ya kupata elimu kwa wanafunzi wote.
  “Wazo hili litasaidia sana serikali katika kuhakikisha mazingira ya shule yanaboreshwa ili kutoa nafasi sawa kwa wanafunzi wote wa kike na kiume” alibainisha Spika Ndugai.
  Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amefurahishwa sana na kitendo hicho na kwamba ameshindwa kuhudhuria hafla hiyo kwa vile bado yuko kwenye msiba wa dada yake huko Chato Mkoani Geita. 
  Kwa upande wake, mgeni rasmi Mhe. Anne Makinda aliwapongeza wabunge hao wanawake kwa hatua hiyo ya kuunga mkono juhudi za serikali na kuwataka Wabunge wanaume kuwaunga mkono wenzao katika kufanikisha kampeni hiyo inayolenga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 3.5 zitakazowezesha kujenga vyoo vya shule kwenye majimbo yote 264 nchi nzima.
  Taasisi mbalimbali zilichangia kwenye harambee hiyo.

   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai, akizunhgumza.
   Mwenyekiti wa Kundi la Wabunge Wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Urambo, Mhe. Margareth S. Sitta, akitoa hotuba yake.
   Mgeni rasmi kwenye hafla ya bunge kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule nchi nzima, Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda, akitoa nasaha zake.
   Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya hafla hiyo, Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, akitoa nasaha zake.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela, akifuatilia kilichokuwa kikizungumzwa na viongozi.
   Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha akifurahia jambo.
   Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama wakifuatilia hafla hiyo.
   Meza ya wafanyakazi wa Idara ya Uhamiaji nchini.
   Spika Ndugai akiongoza wabunge wengine kusakata rhumba
   Mbunge wa Viti Maalum ambaye pia ni msanii wa muziki, Mhe. Martha Mlata akiimba kwenye hafla hiyo.
   Wabunge wa Viti Maalum wakisakata rhumba.
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, akiongozana na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson wakati wakiingia ukumbini.
  Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kiwkete akiwa na Mbunge wa jimbo la Segerea, Mhe. Bonner Kalua

  0 0

   Fatma Salum- MAELEZO

  TRENI ya kifahari inayojulikana kwa jina la ROVOS ambayo ni miongoni mwa treni tatu bora duniani imewasili jijini Dar es Salaam kwa kutumia reli ya Tazara ikiwa na watalii 64

  Watalii hao wamekuja Tanzania kwa ajili ya kutembelea maeneo mbalimbali yenye vivutio vya utalii hapa nchini ikiwemo mbuga za wanyama na visiwa vya Zanzibar.Akizungumza katika hafla fupi ya kuwapokea watalii hao iliyofanyika stesheni ya TAZARA Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa TAZARA Tanzania, Fuad Abdallah alieleza kuwa treni hiyo iliondoka mji wa Cape Town nchini Afrika ya Kusini Agosti 18, mwaka huu.
   
  “Watalii mbalimbali huja nchini mara tano kwa mwaka kwa kutumia ROVOS kupitia reli ya TAZARA na nchi yetu hunufaika na ujio huu hasa faida za kiuchumi,” alisema Fuad.Aidha alibainisha kuwa treni ya ROVOS ni miongoni mwa treni tatu bora duniani, hivyo ujio wa treni hiyo na watalii unatokana na vivutio bora vya utalii na miundombinu mizuri ya reli ya TAZARA.
   
  “Treni hii inatumia reli ya TAZARA kuleta watalii kwa sababu nchi yetu imekidhi vigezo vya utalii na reli yetu imekidhi vigezo vya usalama na mawasiliano ya uhakika,” aliongeza Fuad. Alisema kuwa katika safari hiyo ya treni watalii hao pia walipata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Selous iliyopo kusini mwa Tanzania na kuona wanyama mbalimbali wanaopatikana kwenye hifadhi hiyo.
  Wakizungumza kwa furaha ya kuwasili Tanzania, watalii hao wa kijerumani walisema kuwa wamefurahia sana safari hiyo na mapokezi mazuri ya watanzania na kuahidi kurudi kwa mara nyingine.
   
   Kwa upande wake mfanyakazi wa treni ya ROVOS, Monica Rieder mwenye asili ya Ujerumani alisema kuwa amewahi kufika Tanzania mara 14 na anavutiwa na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo yanayofanyika hapa nchini siku hadi siku.
  TAZARA ni shirika la reli ya pamoja ya Tanzania na Zambia iliyoanza mwaka 1976 na inamilikiwa kwa asilimia 50 kila upande.
   Meneja Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) Fuad Abdallah (kulia), akizungumza na Waandishi wa Habari katika makao makuu ya shirika hilo Jijini Dar es Salaam kabla ya kuwasili kwa treni ya kitalii ya ROVOS kutoka Afrika ya Kusini.
   Baadhi ya watalii kutoka Ujerumani wakifurahia buradani ya bendi ya Polisi baada ya kushuka kutoka kwenye treni ya ROVOS moja kati ya treni ya kifahari duniani, watalii hao wamekuja nchini kutembelea vivutio mbalimbali.
   Mama wa Kijerumani Linde Erdmann (katikati) akifurahia kuwasili Tanzania kwa mara ya kwanza akitokea Afrika ya Kusini kwa kutumia treni ya ROVOS kupitia reli ya TAZARA.
  Moja ya mgahawa unaopatikana katika treni ya kifahari ya ROVOS iliyowasili leo hapa nchini ikitokea Afrika ya Kusini kupitia reli ya TAZARA.
  (Picha na Paschal Dotto- MAELEZO).


  0 0

   Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakifuatilia kwa karibu Uwasilishwaji wa Taarifa ya Ukaguzi katika Mkoa wa Singida walipotembelea Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Singida.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mheshimiwa George Simbachawene akifuatilia Uwasilishwaji wa Taarifa kutoka kwa Naibu wa Mdhibiti Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Ndg. Wendy Massoy katika Kikao kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida hii leo, Kamati hiyo ipo katika Ziara Mkoani humo.


  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa George Simbachawene wakiwa katika kikao na Watendaji Wakuu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida hii leo Kamati hiyo ilipofanya ziara yake Mkoani humo.

older | 1 | .... | 1663 | 1664 | (Page 1665) | 1666 | 1667 | .... | 1896 | newer