Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1661 | 1662 | (Page 1663) | 1664 | 1665 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mmoja wa abiria akikaguliwa na mashine ya mkono, iliyoshikwa na Afisa Afya wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Bw. Peter Maseke, ikiwa ni moja ya njia za kudhibiti wagonjwa wa Ebola wasiingie nchini. Ugonjwa huo umetangazwa hivi karibuni kusambaa nchini Kongo.
  songwe1Afisa Afya wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Bw. Peter Maseke (katikati) akikagua hati za kusafiria za mmoja wa abiria aliyekuwa akisafiri kuelekea Dar es Salaam, ambapo (kulia) ni mashine maalum inayotambua abiria wenye homa kali, ambayo ni moja ya dalili za ugonjwa wa Ebola.
  songwe3Abiria wakiwa katika eneo la nje la kuondoka kwenye Kiwanja cha Ndege cha Songwe

  Na Mwandishi Wetu
  UONGOZI wa Viwanja vya Ndege vya Songwe na Kigoma, umejiandaa kwa kushirikiana na maafisa afya, kuhakikisha hakuna mgonjwa mwenye dalili za Ebola anaingia nchini, akitokea maeneo ya Tunduma na nchini Burundi.

  Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Bw. Pius Kazeze alimwambia Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bi.Bahati Mollel kwa njia ya simu kuwa, tayari Maafisa wa Afya wameshafunga mashine maalum (thermo scanners) inayotambua joto la mwili la abiria ambaye anasafiri kwa kupitia kiwanja hicho, na likizidi 38 anatakiwa kutoa taarifa za afya yake.

  Bw. Kazeze amesema Kiwanja cha Songwe ni tofauti kidogo na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo zaidi wanakagua abiria wanaoondoka kwa kuwa wengi wanatoka mpakani maeneo ya Tunduma na kwenda maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

  “Tayari maafisa Afya wamefunga mashine ya ukaguzi wa afya eneo la nje la kuondokea abiria kwani kwetu huku tunapata abiria wengi wanaotoka nchi jirani wanaopitia mpakani Tunduma, hivyo wengi wao wanatoka nchi zinazopakana na Kongo, ambayo inasadikika ugonjwa wa Ebola umeibuka kwa kasi kubwa,” alisema Bw. Kazeze.

  Hatahivyo, amesema mbali na mashine hiyo kubwa iliyowekwa sehemu maalum, pia wanamashine mbili ndogo zinazotumiwa kwa kushikwa mkononi na maafisa Afya, lakini wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa Watumishi wa afya, ambao tayari wameshaomba kuongezewa mmoja ili kufanikisha kazi hiyo kuwa rahisi.

  Naye Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Kigoma, Bw. Theophan Bileha amesema wapo mbioni kiweka kifaa hicho kwa kuwa wanatarajia abiria kutoka Burundi watakaowasili kwa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), itakayoanza safari zake kuanzia Agosti 30, 2018.

  “Tumeshafanya kikao na wenzetu wa Afya, na wameahidi kuleta mashine mojawapo, tunatarajia abiria wanaotoka Bujumbura, kwani tumeambiwa ATCL itaanza kwenda huko kuanzia tarehe 30, na hawa wapo watakaoshuka hapa na wengine wanakwenda kwenye viwanja vingine kulingana na ratiba ya ndege hii,” alisema Bw. Bileha.

  Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigoma, Dk. Peter Nsanya amesema mashine hiyo itawekwa kiwanjani hapo kwa kipindi, ambacho ndege zinatua na baada ya ratiba za ndege kumalizika, wanahamishia eneo la Bandarini kwa kuwa pia kuna abiria wanaotoka maeneo mbalimbali.

  “Sisi tumejipanga kukabiliana na maradhi haya ikiwa na kuhakikisha hatutaruhusu uingie nchini, na ndio maana tunaratiba za ndege, ambapo tutakuwa tunakwenda kutoa huduma, na baadaye kuhamia bandarini,” amesema.
  Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, Mohamed Maulid amesema wamejiandaa kwa kushirikiana na Maafisa Afya wamekuwa wakitumia mashine ya mkono kwa ukaguzi wa abiria wanaotoka nchi za Uganda, Nairobi na Kongo.

  Ugonjwa wa Ebola unaosambazwa kwa virusi vya Ebola, husababisha homa kali inayoweza kuambatana na kutokwa damu mdomoni, puani, masikioni, machoni na sehemu nyingine za wazi na unaenea kwa haraka. Hivi karibuni  umetangazwa kutokea nchini Kongo na kusababisha vifo.Dalili za Ebola ni pamoja na homa kali, maumivu ya kichwa na misuli, mwili kulegea, kutapika, kuharisha, vipele na kutokwa damu.

  Juzi Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kilitangaza kuchukua hatua kali za kuweka zuio kwa abiria wanaongia nchini kupitia Kiwanja hicho, ambapo kumefungwa vifaa ambavyo vinabaini joto la abiria na endapo litazidi nyuzi joto 38, atatakiwa kutoa maelezo zaidi ya maisha yake.
  Pia abiria wote wanaowasili kwa ndege zinazotoka nchi jirani na Kongo wanatakiwa kupitia eneo maalum ambalo hutakiwa kunawa mikono yao kwa dawa maalum ili kuua vijidudu mbalimbali.

  IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO CHA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA)

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mswenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (,kushoto) na Mwakilishi Mkaazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) Bw.Alvaro Rodriguez wakifungua pazia kuashiria Uzinduzi wa PROGRAMU ya Pamoja Zanzibar uliofanyika leo Ukumbi wa Idrisa Abduwakil Mnazi Mmoja mjini Zanzibar ambapo mpango huo utafanikisha maendeleo kwa wananchi wa Zanzibar,[Picha na Ikulu.]28 Aug 2018.
  Rais wa Zanzibar na Mswenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi wengine wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa katika hafla ya Uzinduzi wa PROGRAMU ya Pamoja Zanzibar iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Idrisa Abduwakil Mnazi Mmoja mjini Zanzibar akiwepo na Mwakilishi Mkaazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) Bw.Alvaro Rodriguez (wa tatu kushoto),[Picha na Ikulu.]28 Aug 2018.
  Rais wa Zanzibar na Mswenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake katika hafla ya Uzinduzi wa PROGRAMU ya Pamoja Zanzibar uliofanyika leo katika Ukumbi wa Idrisa Abduwakil Mnazi Mmoja mjini Zanzibar (wa tatu kushoto)Mwakilishi Mkaazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) Bw.Alvaro Rodriguez,[Picha na Ikulu.]28 Aug 2018.
  Rais wa Zanzibar na Mswenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimkabidhi zana za Kazi Bibi.Mwanaisha Makame (Topu) (wa pili kulia) katika hafla ya Uzinduzi wa PROGRAMU ya Pamoja Zanzibar uliofanyika leo Ukumbi wa Idrisa Abduwakil Mnazi Mmoja mjini Zanzibar (katikati) Mwakilishi Mkaazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) Bw.Alvaro Rodriguez,[Picha na Ikulu.]28 Aug 2018. 

  Rais wa Zanzibar na Mswenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwakilishi Mkaazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) Bw.Alvaro Rodriguez alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Idrisa Abduwakil Mnazi Mmoja mjini Zanzibar leo katika hafla ya Uzinduzi wa PROGRAMU ya Pamoja Zanzibar katika kuleta maendeleo mbali mbali ya Kijamii,(katikati) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud,[Picha na Ikulu.]28 Aug 2018. 

  Baadhi ya Mawaziri wa Wizara mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa wakiwa katika hafla ya Uzinduzi wa PROGRAMU ya Pamoja Zanzibar iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Idrisa Abduwakil Mnazi Mmoja mjini Zanzibar,mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mswenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.]28 Aug 2018.
  Baadhi ya Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa wakiwa katika hafla ya Uzinduzi wa PROGRAMU ya Pamoja Zanzibar iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Idrisa Abduwakil Mnazi Mmoja mjini Zanzibar,mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mswenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.]28 Aug 2018.
  Wananchi na Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa wakiwa katika hafla ya Uzinduzi wa PROGRAMU ya Pamoja Zanzibar iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Idrisa Abduwakil Mnazi Mmoja mjini Zanzibar,mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mswenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.]28 Aug 2018.

  0 0

  Kuhusu BROKEN HEART: Hakuamini mahusiano yake na mtu aliyempenda yaishe kwa yeye kudumbukizwa kwenye dimbwi la msongo wa mawazo, aliyempenda aligeuka kuwa adui.
  'Mapenzi ni kitu ambacho kinaweza kukufanya chizi, sihitaji tena mwanaume maishani mwangu.' Alizungumza.
  Lakini maisha ni safari, na akiwa katika safari ya maisha alijikuta akizama kimapenzi kwa mwanaume mwingine, mwanaume aliyedhani ni tofauti na waliopita.
  Shilole A.K.A Shishi Baby Kulia akiwa pamoja na Jackson  Fute kuzindua rasmi riwaya waliyo andilka pamoja inayokwenda kwa jina la Broken Heart, uzinduzi huo ulifanywa ndani ya Duka la vitabu la Mak Books and Brains Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
  Bwana Jackson Fute (Kushoto) akiongea na waandishi wa Habari Mara baada ya kuzindua riwaya waliyo andika na Shilole.
  Msanii maarufu wa Muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva, Bongo Movie na sasa Mtunzi wa vitabu Bi. Zena Yusuf Mohamed Maarufu kwa jina la Shishi Baby, akielezea kwa ufupi namna alivyopata wazo la kuandika Riwaya ya Broken Heart kuwa inalenga historia yake ya kweli kabisa na kuongeza kuwa amefurahi kumshirikisha mwandishi chipukizi Bw. Jackson Fute na kazi imeenda vizuri. pia aliwaomba watanzania wamuunge mkono kwani kitabu kinauzwa kwa Tsh 15,000 tu na Online Ebook ni Tsh 3,000 kinapatikana kote Duniani.
  Mhariri wa Riwaya ya Broken Heart Bi Zuhura Seng'enge maarufu kwa jina la The African Lioness ambaye pia ni Mshairi, Mtunzi, Mwandishi na Mfasiri akielezea namna alivyo ipokea kazi ya kuhariri Riwaya hiyo na kukili kwamba ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufanya kazi hiyo. "Moja ya changamoto nilizozipata wakati nahariri Riwaya hii ilikuwa ni utamu wa simulizi zilizokuwemo ndani mpaka nikachelewa kumaliza kazi hiyo kwa muda kutokana na kunogewa na visa mkasa"
  alisema Zuhura.
   Waandishi wa Habari wakiendela kufanya mahojiano na Shishi Baby pamoja na Jackson Fute wakati wa uzinduzi wa Riwaya hiyo.
   Mhariri wa Riwaya hii  Bi. Zuhura Seng'enge akipokea Riwaya yake kutoka kw Shishi Bby
   Mmoja wa wadau Bw. Hassan A.K.A Double D wa Uswahilini Matola  nae akipokea Riwaya yake
   Bw. David Kisamfu  Akipokea Riwaya yake kutoka kwa Shishi Bby
   Mtaalam wa picha za mnato Bw. Zajilu Zaid nae akionesha Riwaya yake ya Broken Heart baada ya kuinunua
   Anaitwa Silver (kushoto) Akipokea Riwaya yake kutoka kwa Shishi Bby
  Bw. Francis nae Akipokea Riwaya yake kutoka kwa Shishi Bby
   Ukiingia tuu katika Duka la vitabu la Makbooks Brains Mlimani City  utakutana na Riwaya ya Broken Heart
   Mmoja wa wanunuzi akiwa anasoma Dibaji
   Kulia ni mmoja wa wafanyakazi katika Duka la vitabu la Mak Books and BrainsBi. Fina akimpa mfuko wenye Riwaya ndani Shishi Baby ili amkabidhi mnunuzi.
  Hili hapa ndio duka la vitabu la Mak Books and Brains lililopo Mlimani City hapa ndipo utapata Riwaya ya Broken Heart.
  Picha zote na Fredy Njeje  0 0


  0 0

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amejitolea kumsomesha na kumlea mtoto Christopher Edward kutokea kijiji cha Mtita, Wilaya ya Bahi jijini Dodoma ambaye amekatwa miguu yote miwili katika Hospital ya kibingwa ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma kufuatia kupatwa na ugonjwa wa kupooza miguu.

  Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo jana katika Hospital hiyo ya kibingwa wakati akikabidhi kiti cha matairi (wheelchair) kwa mtoto Christopher kilichotolewa na Hospital ya Benjamin Mkapa ikiwa ni njia ya kumrahisishia usafiri kumtoa sehemu moja kumpeleka sehemu nyingine katika kutimiza majukumu yake ya kila siku ikiwemo elimu.

  Kutokana na changamoto hizo zinazomkabili mtoto Christopher, Naibu Waziri Mavunde akishirikiana na Mbunge wa Bahi Mh Omary Badwell wameahidi kumsaidia miguu ya bandia miwili na pia kumsomesha katika shule ya Fountain Gate Medium School iliyopo Miyuji Jijini Dodoma ili kumsaidia mtoto kutimiza ndoto zake za kielimu na maisha kwa ujumla.

  Akitoa maelezo ya awali Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Benjamin Mkapa Dr Alphonce Chandika alisema Hospital imeona imsaidie mtoto Christopher kiti hicho cha kutembelea ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano katika kuwajali na kuwasaidia watanzania wenye vipato vya chini.

  "Kweli tumeokoa maisha ya Christopher tena bila kumtoza gharama, lakini tusingeishia hapo kwasababu tayari ni mhitaji, hivyo tumempatia kiti hiki na sasa tunawaomba watanzania wamsaidie miguu bandia, suala elimu na mahitaji mengine muhimu ili ajimudu katika maisha yake" alisema Dkt Chandika.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde (pichani kati) akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),kuhusu kujitolea kumsomesha na kumlea mtoto Christopher Edward kutokea kijiji cha Mtita, Wilaya ya Bahi jijini Dodoma ambaye amekatwa miguu yote miwili katika Hospital ya kibingwa ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma kufuatia kupatwa na ugonjwa wa kupooza miguu.
  Naibu Waziri Mavunde akikabidhi kiti cha matairi (wheelchair) kwa mtoto Christopher kilichotolewa na Hospital ya Benjamin Mkapa ikiwa ni njia ya kumrahisishia usafiri kumtoa sehemu moja kumpeleka sehemu nyingine katika kutimiza majukumu yake ya kila siku ikiwemo elimu. 
  Picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa akizungumza na viongozi wa bodi ya Korosho nchini ambao hawapo pichani wakati wa ziara ya ya kutembelea maeneo mapya yanayolima korosho nchini yaliyofanyiwa utafiti na kubainika yanaweza kustawi zao hilo na hivyo uhamasishaji wa kilimo hicho ukafanyika akielezia mikakati ya wilaya yake kupanda zaidi ya ekari 5000 za mikorosho Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Charles Fussi kushoto akimsikiliza kwa umakini Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana wakati wa ziara ya viongozi wa bodi kuhamasiha kilimo cha zao la Korosho kwenye maeneo mapya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Charles Fussi kushoto akisistiza jambo kwa viongozi wa bodi ya Korosho nchini Afisa Kilimo Frank Mfutakamba kulia na Afisa Uhusiano Bryson Mshana kushoto wakati walipofanya ziara wilaya ya Manyoni kuhamasisha kilimo cha zao hilo. Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana kulia akisisitiza jambo kwa Afisa Kilimo ,Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni Fadhili Chimsala Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa bodi ya Korosho waliotembelea wilaya hiyo kushoto ni Afisa Uhusiano Bryson Mshana kulia ni Afisa Kilimo Frank Mfutakamba Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa kushoto akiagana na Afisa Kilimo wa Bodi ya Korosho Frank Mfutakamba mara baada ya viongozi wa bodi ya korosho kumaliza mazungumzo naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Charles Fussi wa pili kutoka kushoto akisisitiza jambo na viongozi wa bodi ya Korosho mara baada ya kumalizia mazungumzo nayo kushoto ni Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana na kulia ni Afisa Kilimo wa Bodi hiyo Frank Mfutakamba Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana akitazama moja ya mikorosho mipya iliyopandwa kwenye shamba mfano ambalo walilitembelea ili kuweza kuhamaisha zao hilo liliopo Kijiji cha Masigati

  WILAYA ya Manyoni mkoani Singida imetenga zaidi ya ekari 5000 kwenye Kijiji cha Masigati kwa ajili ya kupanda mikorosho mipya baada ya wananchi kuhamasisha kupanda zao hilo.

  Hayo yalisemwa na Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa wakati wa ziara ya viongozi wa bodi ya korosho nchini ya kutembelea maeneo mapya yanayolima korosho nchini ambao yalifanyiwa utafiti na kubainika yanaweza kustawi zao hilo na hivyo uhamasishaji wa kilimo hicho.

  Viongozi wa bodi hiyo ambao walifika kwenye shamba la mfano lililopo katika Kijiji cha Masigati kwenye Halmashauri ya Manyoni ambalo lilianza mwaka jana ni Afisa Kilimo wa Bodi hiyo Frank Mfutakamba na Afisa Uhusiano Bryson Mshana wakiwa kwenye uhamasishaji wa kilimo hicho kwenye maeneo mapya.

  Mkuu huyo wa wilaya alisema kati ya hizo ekari zilizopandwa ni 1250 kwa msimu uliopita wa kilimo na msimu umekaribia mwezi Desemba mwaka huu wataanza tena kuendelea na upandaji wa mikorosho mipya.

  “Pamoja na kwamba tumetenga ekari 5,000 kwa ajili ya kulima kilimo cha Korosho lakini mipango yetu ni kufikia ekari 10,000 alisema pamoja na hayo tutaendelea kufanya uhamasishaji kwa wananchi kuweza kuchangamkia fursa ya zao hili na kupanda mikorosho kwa wingi “Alisema.

  Alisema wananchi wake wamehamasika baada ya kuwepo kwa uhamasishaji mkubwa kupitia mikutano mbalimbali huku akiwataka wananchi wa wilaya hiyo kutumia fursa ya kilimo hicho kutokana na kwamba maeneo yote yana uwezo kustawi zao hilo hivyo walipande kwani litawasaidia na kuwa mkombozi wa maisha yao.

  “Lakini pia nisema kilimo hiki kimeweza kutoa fursa kwa watu kutoka mikoa mingine wameanza kulima korosho Manyoni hamasa bado inaendelea kwa halmshauri mbili za Manoyoni na Itigi licha kwamba hawajafanya kilimo cha pamoja lakini watu wanalima Korosho”Alisema

  Alisema Halmashauri ya Manyoni wamekuwa na mpango wa kilimo cha pamoja kupitia ekari hizo elfu tano jambo ambalo limesaidia wananchi kupata ajira na hivyo kukuza uchumi wao kutokana na shughuli za upandaji zinazofanyika.

  Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Charles Fussi aliishukuru bodi ya korosho kutokana na kwamba wao ndio wamekuwa chachu ya kuzalisha korosho kama zao la mkakati kwenye halamshauri yao limeanza na wao kama bodi walikuwa wa kwanza kuhamasisha wananchi.

  Alisema kabla ya kuanza kilimo hicho Utaftiti ulifanyika na baada ya kugundua korosho inaweza kufanya vizuri hivyo bodi ya korosho waliomba ardhi na wazo lao kubwa lilikuwa la kwanza kupitia Halmshauri walifika Kijijini Masigati kuzungyumza na wananchi waliomba ardhi wakapewa eka 2000 wahamasisha vikundi vikaundwa wakaanza kugawa ardhi kwa vikundi.

  Alisema kila kikundi kina ekari si chini ya 100 wameanza kusafisha mashamba wanalima korosho lakini wameamua mradi huo upanuliwe kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi huku akiwakaribisha watanzania wengine kuchangamkia fursa hiyo.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  REDCROSS Tanzania imedhamiria kuleta mapinduzi kwa wananchi kuhakikisha kila mmoja anawajibika kutoa msaada wa majanga yanayojitokeza ili kusaidia waathirika wa majanga hayo wasipoteze maisha kwa kukosa huduma ya kwanza.

  Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Katibu wa Redcross Julius Kejo wakati akizungumza na waandishi habari kuhusiana kazi zinazofanywa na Redcross Tanzania na namna kuhakikisha jamii inawajibika kusaidia kuwa mstari wa mbele katika majanga mbalimbali yanayotokea na kuachana na tabia ya kukimbilia kuona bila ya msaada wa huduma ya kwanza.

  Amesema bado kuna tatizo kubwa kwa jamii kutowajibika pale yanapotokea majanga ikiwamo ya ajali na mengineyo kwa kushindwa kuwasaidia kwa haraka watu wanaopata athari katika majanga hayo badala yake kubaki washudiaji tu na kupiga picha.

  “Ajali ikitokea, badala ya watu kutoa msaada wa huduma ya kwanza kuokoa maisha yao, watu wanawazunguka kuwashangaa, na wengine wanatumia muda huo kuchukua picha kutuma kwenye mitandao na kuacha wenzao wakihangaika au baadhi ya wengine wanapoteza maisha wakati huo huo kwa kukosa huduma ya kwanza wakati pengine wangewasaidi kuokoa maisha yao ,” amesema Kejo

  Amesema umefika wakati watanzania kubadilika kujitoa katika kupata elimu ya huduma ya kwanza ambayo itatumika katika kuokoa maisha ya watu katika majanaga mabalimbali kwani kusaidia mtu katika majanga ni haki kwa yule yaliyompata.

  "Tuwe na huruma kila mmoja awajibike tusikubali kuwapoteza ndugu nzetu na nguvu kazi ya taifa letu kwa vitu ambavyo hata sisi tunaweza kutoa msaada bila kutegemea msaada kutoka kwa watu wengine kutoka nje.”

  Amesema kwa sasa Redcross watahakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa kila mmoja kuanzia ngazi ya familia, mikoa yote, mijini na vijijini kuhakikikisha kila mmoja anawajibika kutoa msaada wa huduma ya kwanza katika majanga ili kupunguza idadi ya watu wanaopata matatizo ama kufariki kutokana na kukosa msaada huo wa kwanza.

  kwa upande wake, Kheri Ngwere, Mratibu wa Huduma ya Kwanza, Redcross, amesema wako kwenye mchakato wa kuandaa mtaala wa namna ya utoaji wa huduma ya kwanza ambao unatarajiwa kutumika katika taasisi mbalimbali hasa zinazotoa mafunzo ya ufundi stadi na usalama balabalani.

  Amesema wanatarajia mtaala huo utaanza kutumika Septemba mwaka huu kwa majaribio kwa kipindi cha miezi sita na baadae kuanza kutumika rasmi na kwamba lengo ni kuwajenhea uwezo jamii kuokoa maisha ya watu kwenye majanga kupitia huduma hiyo ya kwanza.
   Katibu Mkuu wa Recross Tanzania Julius Kejo akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na kazi ya Redcross katika utoaji wa huduma wakati wa Majanga yanapotokea, mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi wa Ubelgiji Red cross Tanzania An Vanderheyden akizungumza uzoefu wa Redcross katika kujitoa katika uchangiaji.

  0 0  Na Dotto Mwaibale, Kagera

  Mtoto wa Jinsia mbili ya kike na kiume amezaliwa katika Hospitali Teule ya Rubya iliyopo wilayani Muleba mkoani Kagera.

  Kuzaliwa kwa mtoto huyo kumethibitishwa na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt.Geore Kasibante (pichani),  ambaye alisema hali ya mtoto huyo kuwa inaendelea vizuri na kuwa wakati wowote atapelekwa hospitali kubwa kwa ajili ya uchunguzi ili afanyiwe upasuaji kwa vile katika hospila hiyo hawana madaktari bingwa wa kuweza kufanya upasuaji huo.


  0 0

  Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashantu Kijaji akizungumza katika mkutano wa 41 wa umoja wa kikanda wa makampuni ya Bima kutoka nchi 39 za Mashariki na Kusini mwa Afrika (OESAI) .Picha na Vero Ignatus. 
  Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa BIMA nchini (TIRA) Dk, Baghayo Saqware akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus
  Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo,Khamis Suleiman akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha. 
  Wapili kutoka kushoto ni Naibu waziri wa Fedha Dkt. Ashantu Kijaji, aliyepo kulia kwake ni Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa BIMA nchini (TIRA) Dk, Baghayo Saqware, akifuatiwa na Rukia Adam Mjumbe kutoka (TIRA) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka baadhi ya matataifa 39 Duniani. Picha na Vero Ignatus.   Na.Vero Ignatus.Arusha


  Mkutano wa 41 wa umoja wa kikanda wa makampuni ya Bima kutoka nchi 39 za Mashariki na Kusini mwa Afrika (OESAI) umefunguliwa  rasmi mkoani Arusha.

  Mkutano huo umefunguliwa na Naibu waziri wa fedha Dkt. Ashatu Kijaji ambapo ameyataka makampuni ya Bima kutoa huduma za Bima kwa wakulima ili kufikia uchumi wa kati. 

  Dk, Kijaji amesema asilimia 75 ya Watanzania ni wakulima ambao bado hawana elimu kuhusu bima ikiwemo kupata mikopo ya bei nafuu kwaajili ya kutatua changamoto za kilimo na kufikia katika uchumi wa kati. 

  Ameyataka makampuni ya bima nchini kuangalia kundi hilo la wakulima ili nao waweze kunufaika na bidhaa wanazozalisha kwakuwa kundi hilo ni kubwa na ni fursa kwa makampuni ya bima nchini kuongeza idadi ya watumiaji wa bima. 

  Amesema watanzania wanaotumia bima hapa nchini ni chini ya asilimia moja idadi ambayo hairidhishi kabisa kwakuwa watanzania wapo zaidi ya milioni 45 kwa mujibu wa ofisi ya Takwimu za Taifa. Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa BIMA nchini (TIRA) Dk, Baghayo Saqware amesema mkutano huo wa 41 unatoa fursa kwa kampuni za bima zilizopo hapa nchini kujifunza jinsi kampuni za nje za bima zinavyofanya kazi kwa ufanisi. 

  Aidha amesema kampuni hizo zitapata fursa ya kujifunza uboreshaji wa huduma kwa kutumia mfumo wa Tehama unaoleta mageuzi katika utoaji wa huduma bora zako bima, rasilimali watu na kuongeza wigo wa kutafuta watu mbalimbali kwaajili ya kulipia bima ya maisha. 

  Hata hivyo Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo,Khamis Suleiman amesema lengo la mkutano huo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 asilimia 50 ya watanzania wawe na aina yoyote ya bima kwani kwa sasa Tanzania ipo kwenye nafasi ya pili kwa nchi za Afrika Mashariki kwa kutoa huduma za bima.

  0 0

  NEC – Dodoma.

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16 mwaka huu katika Majimbo ya Ukonga, Korogwe Vijijini, Monduli na kwenye Kata 23 za Tanzania Bara kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni wakati wa uchaguzi.

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi Uchaguzi huo mdogo jijini Dodoma.Jaji Kaijage amewataka Wasimamizi hao kuepuka kufanya kazi kwa mazoea ili wapunguze na kuondoa malalamiko yanayojitokeza wakati wa uchaguzi.

  Amesema Uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali zinazopaswa kufuatwa na kuzingatiwa akisisitiza kwamba hatua na taratibu hizo ndiyo msingi wa uchaguzi mzuri wenye ufanisi usio na malalamiko au vurugu.

  “ Tunakutana hapa kwa muda wa siku tatu (3) ili kwa pamoja tubadilishane uzoefu, tujadili namna ya kufanikisha zoezi la uchaguzi lakini pia namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika hatua zote za uchaguzi,” Amesema Jaji Kaijage.

  Aidha, amewataka Wasimamizi hoa waepuke madhara yanayotokana na ukiukaji wa Sheria, Kanuni na taratibu za Uchaguzi na akisisitiza kwamba katika kipindi hiki chaguzi zinafanyika katika mazingira ambayo yana hamasa kubwa ya Kisiasa, kutoaminiana na wakati mwingine hutawaliwa na mihemko ambayo imekuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.

  Jaji Kaijage amewaeleza Wasimamizi hao kwamba wameaminiwa na kuteuliwa katika nafasi hizo za usimamizi wa Uchaguzi kwa kuwa wana uwezo wa kufanya kazi hiyo hivyo wajiamini na kujitambua.Amaetoa wito kwa Wasimamizi hao kuhakikisha kuwa wanayaelewa vema maeneo yao ya kazi na kuhakikisha kwamba wanawatumia vizuri wasaidizi walio nao katika maeneo yao kwa matokeo bora.

  “Mjue mna jukumu la kuimarisha imani ya wananchi pamoja na wadau wote wa uchaguzi kwa Tume. Hivyo mfanye kazi kwa ufanisi wa hali ya juu, bila kuegemea upande wowote. Kufanya kazi kwa uhuru na kwa uwazi kutasaidia kudumisha amani katika maeneo yenu ya Uchaguzi” Amesisitiza.

  Kuhusu kufanyika kwa Uchaguzi huo mdogo Septemba 16 mwaka huu, Jaji Kaijage amesema kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 37 (1) (b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 kikisomwa pamoja na kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Serikali za Mitaa, Sura 292, ni jukumu la Tume kusimamia, kuendesha na kuratibu uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi.

  Amesema kwa nyakati tofauti Tume imepokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa kuzingatia Kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Ubunge katika Majimbo ya Ukonga, Korogwe Vijijini na Monduli.

  Pia amefafanua kuwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa, ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali ya Mitaa, Sura, 292 alitoa taarifa ya uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata 23 kutoka katika Halmashauri 15 zilizopo katika Mikoa 10 ya Tanzania Bara.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Waziri wa Fedha na Mipango , Dkt Philip Mpango amewaaga watumishi watano wa wizara hiyo wanaosafiri kwenda nchini Uingereza kwa ajili ya ufadhili wa Masomo, uliotolewa na DFID Kupitia mfuko wake wa UKAID.

  Akizungumza na Michuzi Media Group katika Mkutano wa kuwaaga watumishi hao, Waziri Mpango aliwataka Vijana hao kuwa wazalendo kwa nchi yao na kutokubali kuyumbishwa na jambo lolote la ujanja kutoka kwa watu wa Mataifa mengine.

  “Hii nafasi niliomba mimi kwa ajili ya watumishi wa Wizara muende kujifunza na hili ni kundi la pili ,hivyo naomba mkafanye kile kilichowapeleka kwani watanzania  zaidi ya Milioni Hamsinii wanategemea kuja kunufaika na ujuzi mlioupata kutoka huku ili muweze kuja kuendesha taasisi hii,ambayo ndio Ubongo wa uchumi wa nchi yetu” alisema Dkt. Mpango.

  Dkt MPango alisisitiza kuwa yeye kama  Waziri anajivunia sana kuona Vijana wanapanua maarifa kwa kujiongezea elimu kutoka sehemu nyingine ,kwani kunasaidia kujiamini na kuzungumza kwa hoja za uhakika mbele ya umati wa watu.Alisema kuwa kama watalaamu wote hao kutoka wizara ya fedha watafanikiwa kufanya vizuri, watazidi kuiongezea sifa nchi yetu kuendelea kupata nafasi ya kupeleka vijana wengi kwenda kujifunza.

  Ameweka wazi kuwa yeye atakuwa Waziri mwenye furaha sana kwa kuona kila idara katika Wizara yake ina vijana makini ambao ni weledi katika kazi zao.
  Waziri wa Fedha na Mipango , Dkt Philip Mpango akizungumza na Vijana watano kutoka Wizara hiyo ambao wamepata ufadhili wa masomo nchini Uingereza 
  Waziri wa Fedha na Mipango , Dkt Philip Mpango akisisitiza jambo kwa Vijana hao 
  Waziri wa Fedha na Mipango , Dkt Philip Mpango akiagana na Vijana hao na kuwatakia Safari Njema
  Wafanyakazi wa Wizara ya fedha , Sudah Joseph, Peter Kalugwisha,Morick Mwasagwa,Eliud Mkilamweni na Tunsume Mlawa wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango , Dkt Philip Mpango 
  Waziri wa Fedha na Mipango , Dkt Philip Mpango akiwa katika picha ya Pamoja na Wanufaika wa Ufadhili wa Masomo wa DFID kupitia Mfuko wa UKAID

  0 0
 • 08/28/18--22:45: Muhimbili yapokea vifaa tiba
 • Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea vifaa tiba 69 ambavyo vimefanyiwa matengenezo na kurejea katika viwango vyake vya matumizi.

  Vifaa tiba hivyo (Screen) ambavyo vilikua chakavu vimetengenezwa upya na familia ya Bwn. Khakoo bila malipo yoyote, ambavyo hutumika kumsitiri mgonjwa akiwa kitandani huku akipatiwa huduma hospitalini na kwamba matengenezo yake yamegharimu shilingi milioni 2. 7.

  Katika matengenezo hayo familia ya Khakoo imejitolea kulipa wafanyakazi , kununua vitambaa pamoja na mashono huku MNH ikiunga mkono jitihada hizo kwa kutoa mashine ya kuchomelea na vifaa vya kupakia rangi. Akipokea vifaa tiba hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru ameishukuru familia ya Bwn. Khakoo kwa msaada huo na kueleza vifaa hivyo ni muhimu kwa kutolea huduma hospitalini hivyo vitatumika kwa uangalifu.

  ‘‘Tunashukuru sana kwa msaada huu mkubwa kwakweli tumejifunza kwamba vifaa vilivyochakaa vinaweza kutengenezwa upya na vikakutumika tena, hili tumelichukua na tutalifanyia kazi kadiri inavyowezekana’’.Amesema Prof. Museru. Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa huduma za uuguzi, Sista Zuhura Mawona amesema kila wodi inahitaji screen 6 ambazo hutumika kumsitiri mgonjwa wakati akihudumiwa hivyo zitagawiwa kulingana na mahitaji.

  Kwa upande wao familia ya Bwn. Khakoo imesema wameamua kutengeneza vifaa hivyo kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuboresha huduma za afya nchini na kutoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huo.

  ‘‘ Tuliviona vifaa hivi vikiwa chakavu tukaona kwamba kuna uwezekano wa kuvitengeneza na vikaendelea kutumika kwa wagonjwa , sisi ni watu binafsi tumeamua kama familia kujitolea na hivyo tumeokoa fedha nyingi takribani shilingi milioni 30. Amesema Bwn. Khakoo.

  Vifaa hivyo endapo vingenunuliwa vipya kimoja kingegharimu shilingi laki nne hadi laki tano.   Familia ya Bwn. Khakoo ikimkabidhi vifaa tiba Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prf. Lawrence Museru mapema leo , kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa huduma za uuguzi Sista Zuhura Mawona


  Baadhi ya vifaa tiba (Screen) ambavyo hutumika kumsitiri mgonjwa wakati akipatiwa huduma.


  Pichani ni vifaa tiba vilivyokuwa chakavu kabla ya kufanyiwa matengenezo na familia hiyo.
  Prof. Museru akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Bwn. Khakoo na baadhi ya wakurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.


  Bwn. Khakoo akimuelezea Prof. Museru jinsi walivyofanyia matengenezo vifaa hivyo.

  0 0

  Na Richard Bagolele – Chato 

  Serikali Wilayani Chato imeziagiza shule zote kuanzia msimu ujao kuhakikisha zinalima zao la Pamba na Mtama kuanzia ekari mbili kwa kila shule. 

  Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri Semeon wakati akiongea na walimu wakuu, wakuu wa shule na waratibu wa elimu kata za Chato kwenye hafla fupi ya ugawaji wa pikipiki 23 zilizotolewa na serikali kupitia wizara ya elimu, sayansi, na ufundi stadi hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato. 

  “Tunahitaji shule na taasisi zote ni lazima muwe na ekari zisizopungua mbili za pamba na zinatakiwa kusimamiwa na wagani waliopo huko vijijini” amesisitiza Mkuu wa Wilaya. 

  Mkuu wa Wilaya amesema fedha zitakazopatinaka kutokana na zao la pamba ziwe na lengo la kumnufaisha mwanafunzi kwa kuwaandalia chakula ili kumpunguzia mzigo mzazi ambao wamekuwa wakichangia huduma ya Chakula kwa wanafunzi. Akikabidhi pikipiki hizo Mkuu wa Wilaya amewataka waratibu wa elimu kata kuzitembelea shule zilizopo maeneo yao mara kwa mara na si kusubiri wakati wa mitihani tu kwani sasa wamepata usafiri. 

  Mkuu wa Wilaya pia amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji kutenga bajeti kwa ajili ya kununua pikipiki za watendaji wa kata kwa awamu ili nao waweze kutimiza malengo yao sambamba na kuwafikia wananchi kilahisi. 

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Eliurd Mwaiteleke amesema Wilaya ya Chato imekuwa ikifanya vizuri kwenye matokeo ya elimu hivyo uwepo wa pikipiki hizo kutasaidia katika kuboresha upatikanaji wa elimu ili kuongeza tija na ufaulu ambapo shule zote zitafikiwa kirahisi. 

  Amewaasa waratibu elimu kata kuzitumia vizuri pikipiki hizo kwa kufanyia kazi za kuboresha elimu na si kufanyia shughuli zao binafsi na kuepuka kuendesha wakiwa wamelewa. Naye mratibu wa elimu kata ya Bukombe Mwalimu Ernestina Athanas amesema amefurahishwa na ujio wa pikipiki hizo ambapo kwa sasa atazifikia shule 7 za kata hiyo na amesema anategemea matokeo mazuri kwa matokeo yajayo. 

  Jumla ya pikipiki 23 zimekabidhiwa kwa waratibu wa elimu wa kata za Wilaya ya Chato ambao kuna jumla ya shule za msingi 139 na shule za sekondari 28.
  Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri Semeon akiongwa na walimu wakuu, wakuu wa shule na waratibu wa elimu kata za Chato
  Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri Semeon (kulia) akikabidhi ufunguo wa pikipiki kwa mratibu elimu kata ya Bwanga Venance Bahati
   Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Eliurd Mwaiteleke akiongea na wakuu wa shule, walimu wakuu na waratibu elimu kata za Chato
  Mkuu wa Wilaya ya Chato (katikati) akiwasha pikipiki kama ishara ya kukabidhi pikipiki hizo kwa waratibu wa elimu kata 23 za Wilaya ya Chato.
  Watendaji mbalimbali wa idara ya elimu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Chato (hayupo pichani).

  0 0

  Dar es Salaam. Bendi kongwe nchini, The African Stars (Twanga Pepeta) imeandaa onyesho maalum la kutimiza miaka 20 tokea kuanzishwa kwake Septemba 29.

  Bendi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1998, itafanya onyesho lake kwenye ukumbi wa Club Legends uliopo Namanga na maandalizi yake yameanza.

  Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka alisema kuwa sambamba na onyesho hilo, shughuli mbalimbali zitafanywa na wanamuziki wa bendi hiyo ikiwa pamoja na kutembelea ofisi za vyombo vya habari mbalimbali, kusaidia watoto yatima na wagonjwa.Baraka alisema kuwa kudumu kwa miaka 20 katika muziki wa dansi si kazi ndogo kwani kuna bendi nyingi zilizoanzishwa baada ya bendi yao kuanzishwa zimeshindwa kuendelea na shughuli za muziki. Bendi hiyo ilifanikiwa kuzindua albamu 14.

  Alisema kuwa bendi yao imepitia changamoto nyingi kwa kipindi chote hicho ikiwa pamoja na kupanda na kushuka, lakini uongozi wa kampuni inayomiliki bendi hiyo, African Stars Entertainment Tanzania (Aset) ilisimama kidete kuhakikisha wanadumu katika soko la muziki tofauti na bendi nyingine.

  “Miaka 20 si midogo kudumu katika shughuli za muziki, kwa kweli tumepitia changamoto nyingi sana, wanamuziki kuhama, soko la muziki wa dansi kushuka kutokana na mabadiliko ya sekta hiyo ikiwa pamoja na kuibuka kwa muziki wa kizazi kipya (bongo fleva), taarab na Singeli. Mashabiki walibadili muelekeo, lakini sasa mambo yamerejea,” alisema Baraka.

  Alisema kuwa kwa miaka hiyo 20, wameweza kupata mafanikio mbalimbali ikiwa pamoja na kuanzisha bendi nyingine kama African Revolution enzi ya Chumvi Chumvi mpaka Tam Tam na baadaye kubadilishwa jina na kuwa Vibration Sound.

  “Pia tuliweza kuanzisha studio (Aset Production), gazeti (Zeze), kituo cha kuibua vipaji (Aset Academia) na kuibua wanamuziki nyota kama Totoo Kalala ambaye kwa sasa anatamba na bendi ua Bogos ya Musica na wanamuziki wengine wengi sana,” alisema.Alifafanua kuwa pia waliwekeza katika sekta ya filamu na kufanya kazi na waigizaji mbalimbali nchini ikiwa pamoja na marehemu, Steven Kanumba na wengineo huku wakisaidia wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya kupata maonyesho ya nje kama Uingereza na nchi nyinginezo.

  “Bendi yenyewe ilifanya maonyesho nje ya nchi mbalimbali za Scandinavia kama Norway, Sweden, Denmark na Finland, pia bendi ilifanya maonyesho kadhaa nchini Uingereza na kushiriki katika tamasha la mfalme wa Oman,” alisema.
  Mkurugenzi wa bendi ya African Stars (Twanga Pepeta), Asha Baraka (wanne kutoka kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana sherehe maalum ya miaka 20 ya bendi hiyo iliyopangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Le Legends Septemba 26. Picha na Mwandishi wetu.

  0 0

  Na Veronica Kazimoto-Tabora.

  WAFANYABIASHARA wenye malimbikizo ya madeni ya kodi wametakiwa kutuma maombi ya msamaha maalumu wa riba na adhabu kwenye malimbikizo hayo mapema kabla ya tarehe 30 Novemba, 2018 ili waweze kunufaika na msamaha huo ambao umetolewa kwa lengo la kutoa unafuu kwa kuwapa fursa ya kulipa kodi ya msingi  ndani ya mwaka wa fedha wa 2018/19.

  Wito huo umetolewa na Afisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Rose Mahendeka wakati wa semina elekezi kwa wafanyabiashara, wadau na washauri wa wafanyabiashara kuhusu msamaha huo iliyofanyika leo mkoani Tabora. 

  "Nachukua fursa hii kutoa wito kwenu wafanyabiashara kutuma maombi ya msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi ambapo mwisho wa kutuma maombi ya msamaha huu ni tarehe 30 Novemba, 2018," alisema Mahendeka. 

  Mahendeka aliongeza kuwa "Mara nyingi wafanyabiashara huwa mnajitokeza mwishoni kabisa mwa tarehe zinazoonyesha mwisho wa kulipa, kuwasilisha au kutuma maombi fulani suala linalosababisha foleni na msongamano mkubwa katika kutoa huduma katika ofisi zetu. Nachukua fursa hii kuwaomba msisubiri tarehe za mwisho kuleta barua za maombi ya msamaha huu wa riba na adhabu ya madeni ya kodi na naomba mjue kwamba, huu ndio muda muafaka wa kila mwenye malimbikizo ya madeni kutuma maombi Ofisi ya TRA katika mkoa wake kikodi."

  Naye, Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka hiyo Chama Siriwa alisema muombaji wa msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya kodi anapaswa kutoa maelezo na vielelezo vya ukweli na uhakika wakati wa uwasilishaji wa maombi yake.

  "Kila muombaji anatakiwa kutoa taarifa za ukweli wakati anaomba msamaha huu na endapo itabainika kuwa muombaji ametoa taarifa za udanganyifu, Kamishna Mkuu anayo haki kisheria kubatilisha na hivyo kupelekea muombaji kupoteza sifa za kufaidika na  msamaha huu, " alifafanua Siriwa.

  Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mihayo iliyopo mkoani hapa inayomilikiwa na Taasisi ya Dini ya Kanisa Katoliki Padri Salvatory Maganga, ameishukuru TRA kwa kutoa Elimu ya msamaha wa riba na adhabu ya madeni ya malimbikizo ya kodi na kuomba elimu hii iendelee kutolewa kwa wafanyabiashara katika maeneo mbalimbali nchini.

  Mamlaka ya Mapato Tanzania inaendelea kutoa elimu ya msamaha huu hususani kwa wafanyabiashara, wadau na washauri wa wafanyabiashara kwa lengo la kuwahamasisha kutuma maombi ya msamaha huu kabla ya muda uliopangwa haujamalizika ambao ni tarehe 30 Novemba, mwaka huu. 
   Afisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Rose Mahendeka akitoa elimu juu ya msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi wakati wa semina elekezi kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali (hawapo pichani) iliyofanyika mkoani Tabora kwa lengo la kuwahamasisha wafanyabiashara hao kutuma maombi ya msamaha huo kabla ya tarehe 30 Novemba, 2018.

  0 0

   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akiiongoza Wizara yake kutoa majibu ya hoja za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika leo Jijini Dodoma.
   Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Sheria Ndogo wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi alipokuwa akitoa majibu ya hoja za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika leo Jijini Dodoma.

  0 0

  Na WAMJW Dodoma
  Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba ameyataka wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutilia mkazo katika kutekeleza Sera za Maendeleo zilizopo katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) ili kufanikisha juhudi za Serikali katika kuletea wananchi Maendeleo.

  Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza Sera zinazosimamiwa na kuratibiwa na chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii leo Jijini Dodoma.

  Bw. Katemba amesisitiza kuwa Mashirika hayo yanapaswa kuwasilisha mipango yao kwa Msajili ili kuweza kuwa na Mpango mkakati mmoja wa kuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi.

  Ameongeza kuwa suala la Maendeleo ni mtambuka na linapaswa kutekelezwa kwa ushirikiano baina ya Serikali, Wadau na wananchi ili kufanya shughuli za Maendeleo kuwa endelevu.
   Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba akizungumza na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Jijini Dodoma katika kikao cha ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza Sera zinazosimamiwa na kuratibiwa na chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii.
  Watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Idara Kuu Maendeleo ya Jamii pamoja na wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakisikiliza mada zilizokuwa zikiwasilishwa kuhusu ushirikiano kati ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Serikali katika kikao cha ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza Sera zinazosimamiwa na kuratibiwa na chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW


  0 0

   Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya sukari ya Kilombero Sugar, Fimbo Butallah akizungumza na wananchi wa Mbagala siku ya uzinduzi wa paketi ndogo za sukari ya 'Bwana Sukari' inayozalishwa na kiwanda hicho. Paketi hizo zitauzwa kwa shillingi 500/- na shillingi 1000/-.
   Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya sukari ya Kilombero Sugar, Fimbo Butallah akimkabidhi paketi mpya za Bwana Sukari mkazi wa Mbagala Zena Athumani siku ya uzinduzi wa bidhaa hiyo uliofanyika viwanja vya Mabagala Zakeem hivi karibuni.
  Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya Sukari ya Kilombero Sugar, Fimbo Butallah akizungumza na waandishi wa habari siku ya uzinduzi wa paketi ndogo za sukari ya Bwana Sukari itakayouzwa kwa shillings 500/- and shillingi 1000/-. 

  Na Mwandishi Wetu.
  KAMPUNI ya Sukari ya Kilombero (KSC) imezindua paketi ndogo za sukari yake ijulikanayo kama ‘Bwana Sukari’, ikiwa ni jitihada za kuhakikisha watanzania wengi zaidi wanamudu kununua sukari hiyo kutokana na unafuu wake wa bei.

  Paketi mpya za sukari chapa ya ‘Bwana Sukari’ zinapatikana kwa ujazo wa gramu 350 maarufu kama ‘Robo Plus’ na paketi za gramu 160 maarufu kama ‘Booster’. 

  Paketi za ‘Robo Plus’ zitauzwa shilingi 1,000/ kwa kila paketi, na paketi za ‘Booster’ zitauzwa kwa shilingi 500/-kwa kila paketi.

  Uzinduzi wa paketi mpya za ‘Bwana Sukari’ uliofanyika maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam ni sehemu ya mkakati wa kampuni ya KSC kuhakikisha sukari yake inawafikia watanzania wa hali mbalimbali za kiuchumi. 

  Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), Chama cha Wazalishaji wa Sukari Tanzania (TSPA), viongozi na wafanyakazi wa KSC.

  Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi wa Biashara wa KSC, Fimbo Butallah alisema kampuni ya sukari ya Kilombero imekua ikipanga mikakati ya kuhakikisha bidhaa ya ‘Bwana Sukari’ inawafikia watanzania wengi zaidi hapa nchini.

  “Sukari ni moja ya bidhaa muhimu kwa matumizi ya kila siku ya nyumbani na sukari ya Bwana Sukari ni moja ya sukari inayopendwa zaidi na watumiaji wengi, tunawashukuru wateja wetu kwa kuikubali bidhaa yetu na kuifanya ifanye vizuri sokoni, kuonyesha shukrani zetu tumeamua kuwaletea paketi hizi ndogo ili wateja wetu wawe na uhuru wa kuchagua ujazo upi utawafaa kwa matumizi yao,” alisema Fimbo.

  Akiongeza kuwa, paketi mpya za ‘Bwana Sukari’ zitakidhi mahitaji ya watumiaji wengi zaidi, “kwa mfano paketi za ‘Booster’ ambazo zitauzwa kwa shilingi 500/-zitawafaa zaidi wale wanaohitaji sukari lakini kwa wakati huo hawana uwezo wa kumudu kununua paketi kubwa au kwa wale wenye familia ndogo.”

  “Kwa ufupi, kupitia paketi hizi ndogo za Bwana Sukari tunawapa wateja wetu uhuru wa kununua sukari ya ujazo mdogo lakini iliyofungwa kwa hali ya usafi na usalama kabisa na kwa bei nafuu.”

  Kwa kuanzia, paketi mpya za ‘Bwana Sukari ’zitapatikana katika maduka yote ya rejareja mkoani Dar es Salaam na wilayani Kilombero mkoani Morogoro wakati KSC inaendelea kufanya mikakati kuhakikisha bidhaa hii inasambaa nchini kote siku za usoni.

  0 0

  Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utetezi kutoka ACT Bw Timothy Mmbaga akichangia mada kwenye Mkutano wa wadau wa Kilimo uliokuwa ukijadili usalama wa Chakula na Masoko kwa wakulima ulioandaliwa na Baraza la Kilimo chini ya Mradi wake wa Ubia wa Kilimo Tanzania (TAP) uliofanyika jana mjini dodoma. 
  Katibu Tawala Msaidizi Sekta za Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dodoma Bi Aziza Mumba akichangia Mada kuhusu Nafasi ya NFRA na CPB katika kuimarisha Usalama wa Chakula, Bei za vyakula na Masoko kwa wakulima ulioandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) chini ya Mradi wake wa Ubia wa Kilimo Tanzania (TAP) uliofanyika jana Mjini Dodoma
  Mratibu wa taifa wa ubia wa kilimo Tanzania TAP, Bw. Mark Magila akichangia mada wakati wa mkutano wa wadau wa kilimo uliokuwa ukizungumzia usalama wa chakula na masoko kwa wakulima ulioandaliwa na baraza la kilimo Tanzania chini ya mradi wake wa TAP na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo uliofanyika mjini Dodoma jana. 
  Sehemu ya washiriki wa warsha ya wadau wa kilimo nchini wakifuatilia kwa ukaribu mjadala wa nafasi ya NFRA na CPB katika kuimarisha usalama wa chakula bei za vyakula na masoko ya wakulima, ulioandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania ACT, Chini ya Mradi wake wa Ubia wa Kilimo Tanzania TAP, uliofanyika jana mjini Dodoma.
  Afisa Sera kutoka Baraza la Kilimo Tanzania (ACT), Bi Laetitia Wiliam akisikiliza kwa makini uwasilishwaji wa Mada ya iliyokuwa ikihusu Nafasi ya NFRA na CPB katika kuimarisha Usalama wa Chakula, Bei za vyakula na Masoko kwa wakulima, katika walisha iliyoandaliwa na ACT chini ya Mmradi wake wa Ubia wa Kilimo Tanzania (TAP) uliofanyika jana Mjini Dodoma.
  Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utetezi kutoka ACT Bw Timothy Mmbaga akiwa katika Picha ya pamoja na baada ya kumalizika kwa Mkutano wa wadau wa Kilimo uliokuwa ukijadili usalama wa Chakula na Masoko kwa wakulima ulioandaliwa na Baraza la Kilimo chini ya Mradi wake wa Ubia wa Kilimo Tanzania (TAP) uliofanyika jana mjini dodoma.

  0 0

  NEC – Dodoma.
  TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16 mwaka huu katika Majimbo ya Ukonga, Korogwe Vijijini, Monduli na kwenye Kata 23 za Tanzania Bara kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni wakati wa uchaguzi.

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi Uchaguzi huo mdogo jijini Dodoma.

  Jaji Kaijage amewataka Wasimamizi hao  kuepuka kufanya kazi kwa mazoea ili wapunguze na kuondoa malalamiko yanayojitokeza wakati wa uchaguzi.

  Amesema  Uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali zinazopaswa kufuatwa na kuzingatiwa akisisitiza kwamba hatua na taratibu hizo ndiyo msingi wa uchaguzi mzuri wenye ufanisi usio na malalamiko au vurugu.

   “ Tunakutana hapa kwa muda wa siku tatu (3) ili kwa pamoja tubadilishane uzoefu, tujadili namna ya kufanikisha zoezi la uchaguzi lakini pia namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika hatua zote za uchaguzi,” Amesema Jaji Kaijage.

  Aidha, amewataka Wasimamizi hoa waepuke madhara yanayotokana na ukiukaji wa Sheria, Kanuni na taratibu za Uchaguzi  na akisisitiza kwamba katika kipindi hiki chaguzi  zinafanyika katika mazingira ambayo yana hamasa kubwa ya Kisiasa, kutoaminiana na wakati mwingine hutawaliwa na mihemko ambayo imekuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.

  Jaji Kaijage amewaeleza Wasimamizi hao kwamba wameaminiwa na kuteuliwa katika nafasi hizo za usimamizi wa Uchaguzi kwa kuwa wana uwezo wa kufanya kazi hiyo hivyo wajiamini na kujitambua.

  Amaetoa wito kwa Wasimamizi hao kuhakikisha kuwa wanayaelewa vema maeneo yao ya kazi na kuhakikisha kwamba wanawatumia vizuri wasaidizi walio nao katika maeneo yao kwa matokeo bora.

  “Mjue mna jukumu la kuimarisha imani ya wananchi pamoja na wadau wote wa uchaguzi kwa Tume. Hivyo mfanye kazi kwa ufanisi wa hali ya juu, bila kuegemea upande wowote. Kufanya kazi kwa uhuru na kwa uwazi kutasaidia kudumisha amani katika maeneo yenu ya Uchaguzi” Amesisitiza.

  Kuhusu kufanyika kwa Uchaguzi huo mdogo Septemba 16 mwaka huu,  Jaji Kaijage amesema kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 37 (1) (b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 kikisomwa pamoja na kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Serikali za Mitaa, Sura 292, ni jukumu la Tume kusimamia, kuendesha na kuratibu uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi.

  Amesema kwa nyakati tofauti Tume imepokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa kuzingatia Kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Ubunge katika Majimbo ya Ukonga, Korogwe Vijijini na Monduli.

  Pia amefafanua kuwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa, ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali ya Mitaa, Sura, 292 alitoa taarifa ya uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata 23 kutoka katika Halmashauri 15 zilizopo katika Mikoa 10 ya Tanzania Bara.

older | 1 | .... | 1661 | 1662 | (Page 1663) | 1664 | 1665 | .... | 1897 | newer