Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Vyama visivyokuwa na Ruzuku vyaitaka Chadema iache kuingilia wagombea wake

$
0
0

Katibu Mkuu wa Chama cha AFP Taifa, Rashid Mohamed akizungumza na waandishi wa habari kupinga Tamko la ubalozi wa Marekani kuhusu uchaguzi wa Igunga na kutaka Chadema isiwaingilie kwenye maamuzi yao




NA Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Umoja wa vyama visivyokuwa na Ruzuku nchini ikiwemo chama cha AAFP, DP pamoja na Chama cha Demokrasia Makini wamelaani vitendo vya wagombea wa vyama hivyo kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kulalamikia tume ya uchaguzi kutotenda haki kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge kwenye jimbo la Korogwe vijijini.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari leo, Katibu mkuu wa chama cha AAFP Rashid Mohamed Rai amesema kuwa baada ya kukagua fomu ya mgombea wa chama chake alibaini kuwa kuna baadhi ya tozo ambazo mgombea huyo alikuwa hajalipia licha ya kutumiwa fedha hizo na baada ya hapo akalalamika kuwa miongoni mwa watu ambao fomu zao hazijapokelewa wakati alikuwa hana vigezo na fomu yake ingekataliwa kwasababu hakulipia fedha za baadhi ya ada za uchaguzi.

“Kuna baadhi ya magenge ya matapeli ambao wamevamia hivyi vyama kwa nia tofauti, kuna watu wanachukua fomu kwa nia ya kugombea wanaweka mfukoni halafu baada ya muda wanaanza kulalamika ukimwambia lete fomu uangalie unakuta yeye mwenyewe hakujaza fomu aliiweka tu” alisema

“Mfano mzuri ni Mgombea wangu, hata ile hela ya uchaguzi ya tume hakulipa halafu siku ya uchaguzi ananiambia fomu haipokelewi na mkurugenzi hayupo mpaka mida ya saaa 9 nauliza wenzake pale wananiambia bado mgombea huyo hajafika eneo la kurudisha fomu, anaingia pale saa 10 na yeye anaungana na hao wanaolalamika kuwa wamefamnyiwa ubaya” aliongeza Rai.

Amebainisha kuwa uchukuaji wa fomu na urejeshaji ni tofauti lakini baadhi ya watu walikuwa wakidanganya ili kutengeneza mazingira ya kugombanisha tume na vyama vya siasa kwa nia mbaya, ambapo CHADEMA waliungana na Mgombea wao na kuanza kutumia maneno makali akilalamikia tume jambo ambalo ni uongo.

“Kama hata ada hakulipa lakini na eye anaungana kwenye mkutano wa Chadema halafu anatoa povu hapo unajua kabisa kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiwaambia wasirudishe fomu” aliongeza Rai kwenye taarifa yake

Kwa upande wake Naibu katibu mkuu wa chama cha DP Abdul Mluya amesema kuwa alipokea simu kutoka kwa mgombea wake majira ya saa saba akilalamika kuwa hamuoni mkurugenzi lakini baada ya hapo alikuja kupata kipande cha video ya mgombea wake akiwa kwenye ofisi ya Chadema akilalamika wakati CHADEMA haina mahusiano mazuri na chama cha DP.

“Sisi DP na Vyama wenza ambavyo havina ruzuku tutaungana wakati tukienda kwenye uchaguzi wa Monduli kushiriki uchaguzi wa marudio lazima tupite korogwe tuonane na mkurugenzi tukajue tatizo lilikuwa ni lipi kisha tutatoa tamko pamoja au chama kimoja kimoja” alisema Mluya

Aidha amebainisha kuwa kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiwapigia simu wagombea wa vyama hivyo wanaoshiriki uchaguzi wa marudio kwenye Jimbo la Monduli, wakiwatishia na kuwaambia wajiunge na vyama vyao na wawaunge mkono na kusema kuwa vyama hivyo vitaenda kushughulika na kuhakikisha wanakabiliana na watu hao wenye nia mbaya ya kugombanisha tume na Vyama Vyao.

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAJESHI NCHINI

MADIWANI WANNE WA CHADEMA ,MOSHI WAUNGANA NA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA KILIMANJARO KUHAMSISHA MAENDELEO KATIKA KATA YA SHIRIMATUNDA

$
0
0
Diwani wa kata ya Shirimatunda katika Manispaa ya Moshi,Fransic Shio (CHADEMA) akizungumza wakati wamkutano wa kata uliolenga kujadili masuala ya maendeleo pamoja na kutambulisha wajumbe wanaounda kamati ya maendeleo ya kata hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro,Patrick Boisafi akizungumza katika mkutano  wa kata ya Shiriamtunda ambapo yeye amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata hiyo.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi .
Naibu Meya wa Manispaa ya Moshi na Diwani wa kata ya Njoro,Jomba Khoi akizungumza katika mkutano huo ambapo yeye na madiwani wenzake walifika kumuunga mkono Diwani wa kata hiyo katika kuchangia shuhghuli za maendeleo .
Baadhi ya wananchi waishio kata ya Shirimatunda wakiwa katika mkutano huo.
Diwani wa kata ya Kiboriloni,Frank Kagoma ni miongoni mwa madiwani walifika kuhamsisha shghuli za maendeleo katika kata ya Shrikamtunda.
Baadhi ya wawananchi waliofika katika mkutano huo.
Diwani wakata ya Soweto,Collins Tamimu pia ni miongoni mwa Madiwani waliofika katika mkutano huo.
Baadhi ya wananchi waishio katika kata ya Shirimatunda.
Diwani wa kata ya Ng'ambo katika manispaa ya Moshi ,Genesis Kiwhelu akiwa mmoja wa madiwani waliofika kuhamisisha shughuli za maendeleo katika kata hiyo.
Baadhi ya wananchi wakichangia hoja mbalimbali wakati wa mkutano huo ikiwemo ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa darasa kwa ajili ya shule ya awali katika kata hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini,

MADIWANI wanne kutoka  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika manispaa ya Moshi  pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro Patrick Boisafi wamejitokeza kumuunga mkono Diwani wa kata ya Shirimatunda ,Francis Shio (Chadema) kuhamasisha uchangiaji katika shughuli za maendeleo.
Madiwani waliojitokea katika mkutano maalumu wa Diwani  kata na wananchi wa kata hiyo ,ni pamoja na Diwani wa kata ya Soweto,Collins Tamimu,Diwani wa kata ya Njoro na Naibu Meya wa manispaa ya Moshi,Jomba Khoi ,Diwani wa kata ya Ng’ambo Genesis Kiwhelu na Diwani wa kata ya Kiboriloni ,Frank Kagoma.
Akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ofisi ya kata ya Shirimatunda  ,Diwani wa kata ya Shirimatunda ,Fransic Shio alisema maendeleo ya wananchi katika maeneo yao yataletwa na wananchi wenyewe na si itikadi za kisiasa kama baadhi ya wanasiasa wanavyoamini.
“Shirimatunda yetu ni ya kwanza kuliko vitu vingine,haya ninayo yasema ni ya uwazi tukikubali kuyaingiza mambo ya kisiasa katika maendeleo ya kata yetu ,yapo mambo mengi sana yatasimama  ,ni lazima kaul yetu ya wana Shirimatunda,umoja ya wana Shirimatunda na amani yetu tuweze kuilinda kwa gharama yoyote”alisema Mh Shio.
Shio aliwataka wakazi wa Shirimatunda kuwaondoa katika misingi ya umoja wa wakazi wa kata ya Shirimatunda huku akiwaomba kupitishwa azimio la kuchangisha fedha kwa kila familia katika kata hiyo kutoa kiasi cha Sh 10000 kwa ajili ya ujenzi wa darasa la wanafunzi wa shule ya awali.
Kwa upande wao ,Madiwani waliofika kumuunga mkono Diwani huyo,walisema ili kushawishi wadau mbalimbali pamoja na serikali kujitokeza kuchangia maendeleo katika kata hiyo wakazi wa eneo hilo wanapaswa kuwa wa kwanza katika kuchangia.
“Mgeni akija nyumbani akakuta wewe mwenyewe hujielewi ,hata kama amekuja na zawadi atarudi nayo ,watu wa Shirimatunda wanaangaliana nani anatoa nini ,endapo kila mkazi wa Shirimatunda akiguswa na hiki tunachokifanya basi angechangia katika eneo hili la elimu”alisema Diwani Kagoma.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia amechaguliwa kuwa mwenyekiti ya maendeleo ya kata hiyo ,Patrick Boisafi alisema kuchangia ujenzi wa Madarasa kwa wanafunzi wa elemu ya awali ni jambo la Kihistoria katika kata hiyo.
“Hakuna mashamba tena hata ya kuwagaiwa watoto wetu ,shamaba lililobaki ni moja na la muhimu sana ambalo ni Elimu,kuna watu ambao wamekuja hapa kutuunga mkono wakasema wafanye jambo ambalo litaacha Historia na ni hili la kuchangia shule ya awali name naunga mkono jambo jema kama hili “alisema Boisafi.
Kwa upande wake ,Naibu Meya wa Manispaa ya Moshi na Diwani wa kata ya Njoro alisema Halmashauri itatoa kipaumbele katika ujenz wa Madarasa hayo kwa kutenga Fungu hasa kutokana na hamasa walioyoionesha wakazi wa kata ya Shirimatunda kw akuanza kuchangia.
 “Niliwaambia nimekuja kujifunza kutoka kwenu na nimeona jinsi mlivyo weza kuanzisha michango na kuonyesha mahitaji yenu kwamba shule ya awali imeonekana kuwa kipaumbele ,ni lazima na mimi kwenye halmashauri yangu tutaipa kipaumbele tutatoa Sh Mil 10 kwa mwaka wa fedha ujao wa 2018/2019.”alisema Khoi.
Katika hatua nyingine wananchi  wa Kata hiyo wameiomba serikali kupitia Wakala wa Barabara vijijini na Mjini  (TARURA) pamoja na Halmashauri ya manispaa ya Moshi kutoa kipaumbele cha barabara kwa kata hiyo ambayo haina kipande hata kimoja cha barabara ya Lami .

Serikali yawatoa hofu wavuvi kuhusu vibali vya nyavu.

$
0
0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega amesema Serikali inaratibu vyema upatikanaji vibali vya kuagiza nyavu bora kwa ajili ya shughuli za uvuvi.

Ulega ametoa kauli jana katika mkutano wa hadhara na wakazi wa kisiwa cha Gana kilichopo wilayani Ukerewe alipofanya ziara ya kutembelea na kusikiliza kero za uvuvi.

Ulega ambaye pia ni mbunge wa Mkuranga amewaeleza wanakisiwa hao wa Gana kuwa Serikali imeshaanza kutoa vibali vya kuagiza nyavu kwa utaratibu unaofaa.

Wakazi hao walitumia fursa hiyo kumuuliza Ulega kuhusu hatima ya samaki aina ya Furu, Gogogo, Nembe na Ningu ambao hawatajwi na sheria ya uvuvi.

Ulega amewajibu "Serikali inaanda muongozo utakaowasaidia kuvua samaki hawa kwa uhuru " amesema .Pia amewataka wavuvi wa Gana wajiunge kwenye vikundi vya ushirika ili wapekelekewa mradi wa Mfuko wa Hifadhi ya Taifa ya Jamii (NSSF) wa wavuvi skimu.

"Mradi huu utakaokopesha na utawasaidia kuimarisha shughuli zao kupitia vikundi watakavyoviunda,"amesema Ulega.
Pichani kati ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Abdallah Ulega akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wa chama cha CCM,Ulinzi na usalama wilaya,wakienda kwenye mkutano mara baada ya kuwasili katika kisiwa cha Ghana wilayani Ukerewe Pichani kati ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Abdallah Ulega akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wa ulinzi na usalama wilaya,wakiwa ndani ya boti kueleka kisiwa cha Ghana wilayani Ukerewe kukutana na wananchi wakiwemo wavuvi katika ziara yake ya kutembelea na kusikiliza kero zao

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Abdallah Ulega akizungumza na Wananchi wa kisiwa cha Ghana wilayani Ukerewe katika mkutano wa hadhara,alipofanya ziara ya kutembelea na kusikiliza kero za Wavuvi

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Abdallah Ulega akiagana na baadhi ya viongozi (hawapo pichani),wakati akipanda boti kuelekea kisiwa cha Ghana wilayani Ukerewe kukutana na wananchi wakiwemo wavuvi katika ziara yake ya kutembelea na kusikiliza kero za Wavuvi hao.

JAMHURI KUWASILISHA MASHAHIDI 34 NA VIELELEZO 15 LIKIWEMO PANGA LINALOTAJWA KUTUMIKA MAUAJI YA MWANAFUNZI SHULE YA SCOLASTICA.

$
0
0
Na Dixon Busagaga,MOSHI

JUMLA ya Mashahidi 34 wanatarajia kutoa ushahidi katika shauri la mauaji ya kukusudia ya mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Scholastica iliyopo Himo,Humphrey Makundi.

Mbali na Mashahidi hao pia upande wa Jamhuri umepanga kuwasilisha vielelezo 15 vikiwa katika mfumo wa nyaraka pamoja na Panga linaloaminika kutumiwa na mshtakiwa wa kwanza katika shauri hilo.

Hayo yamo katika maelezo ya awali yaliyosomwa jana Mahakama Kuu ,Kanda ya Moshi na Wakili Mkuu wa Serikali,Joseph Pande mbele ya jaji wa mahakama kuu ,kanda ya Moshi,Haruna Songoro.Miingoni mwa mashahidi hao ni baba mzazi wa marehemu,Humphrey,Bw Jackson Makundi,madaktari kutoka hosptali za rufaa za KCMC na Mawenzi,maofisa wa jeshi la Polisi kutoka ofisi ya mkuu wa upelelezi wa mkoa (RCO) na kituo cha Polisi Himo.

Mashahidi wengine ni wahudumu chumba cha kuhifadhia maiti ,hosptali ya rufaa ya mkoa ,Mawenzi na mfanyakazi wa kampuni ya mawasiliani ya simu za mkononi ya Vodacom kutoka Dar es Salaam.Upande wa vielelezo vilivyopangwa kuwasilishwa ni pamoja na simu saba za mkononi zikiwemo za washtakiwa ,ripoti ya uchunguzi wa mawasiliano ya simu pamoja na ripoti ya uchunguzi wa mwili wa marehemu na taarifa ya vina saba (DNA).

Kwa upande wa utetezi unatetewa na wakili Elikunda Kipoko akisaidizana na Wakili Gwakisa Sambo ulieleza mahakama kuwa ushahidi wao utawasilishwa kabla kesi haijaanza.Shauri hilo lilikuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa kosa lao pamoja na maelezo ya mashahidi ambapo washtakiwa wote watatu walikana shtaka lao.

Washtakiwa katika shauri hilo ni pamoja na mlinzi wa shule hiyo Hamisi Chacha ambaye anatajwa kama nshtaliwa wa kwanza,Mkurugenzi wa Shule za Scholastica, Edward Shayo ambaye anatajwa kama mshitakiwa wa pili na Mwalimu wa nidhamu, Laban Nabiswa anayetajwa kama mshitakiwa wa tatu.

Katika maelezo yake mbele ya mahakama hiyo Wakili Mkuu wa Serikali, Joseph Pande aliieleza kwamba washtakiwa hao kwa pamoja walitekeleza kosa hilo la mauaji ya kukusudia Novemba 11 mwaka 2017, huku wakijua kwamba kufanya hivyo ni kosa kinyume cha kifungu cha 196 cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 ya Sheria iliyofanyiwa Marejeo Mwaka 2002.

Wakisoma maelezo hayo kwa kupokezana, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Abdalah Chavula alidai kuwa mwanafunzi huyoaliyekuwa akikaa bwenini aligundulika kutokuwapo shuleni hapo jioni ya Novemba 6, mwaka jana.

"Jioni ya Novemba 6, mwaka 2017, mwanafunzi huyo hakuonekana katika mazingira yasiyoeleweka shuleni hapo na baada ya kukamatwa mshtakiwa wa kwanza alieleza siku ya tukio hilo alisikia kishindo na alipomulika kwa tochi alimuona mtu anashuka katika fence na alipoanza kumkimbiza ili amkamate alishindwa na ndipo alipompiga kwa panga na kurudia mara nyingi,"alidai Chavula .Zaidi aliendelea kudai kuwa baada ya hapo, mshtakiwa wa kwanza alimpigia simu mwalimu na mmiliki wa shule na kumueleza kilichotokea.

Kwa upande wake, Wakili wa Utetezi, Elikunda Kipoko anayesaidiwa na Wakili Gwakisa Sambo alisimama na kueleza mahakama hiyo kwamba hawapingi majina ya washtakiwa na kwamba kweli wameshtakiwa na wanakabiliwa na kesi hiyo, isipokuwa mtiririko, maelezo na vingine vyote na wanatambua majukumu ya upande wa mashtaka ni kuthibitisha hayo.

Kutokana na maelezo hayo ya upande wa mashtaka na utetezi, Jaji Songoro alisema tarehe rasmi ya kuanza kwa kesi hiyo itapangwa na Msajili wa Mahakama Kuu na pande zote zitajulishwa lakini washtakiwa watendelea kukaa rumande hadi hapo kesi yao itakapomaliza kusikilizwa.


MSHINDI MASHINDANO YA MISS TANZANIA 2018 KUJULIKANA SEPTEMBA 8 JIJINI DAR

$
0
0
Na.khadija Seif,Globu ya jamii

Muandaaji wa kinyang'anyiro cha Wanamitindo nchini ambae pia alishawahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1998, Basilla mwanukuzi amezungumza jijini Dar es salaam na wanahabari kuhusu hafla ya mashindano hayo yanayotarajiwa kufikia kilele septemba 8 mwaka huu katika ukumbi  wa Julius Nyerere international convention Centre (JNICC).

Aidha Mwanukuzi ametoa shukrani kwa Waziri wa Sanaa,utamaduni na michezo Mh.Harrison Mwakyembe kwa kushirikiana na mashindano hayo tangu yalipoanza mchakato wake  April mwaka huu, na kufungua rasmi kwani kulikuepo na changamoto mbalimbali hapo awali likiwemo suala la kufungia mashindano hayo kutokana na sababu mbalimbali, ambapo kimsingi ziliwanyima warembo wengi fursa ya kushiriki.

"Hivyo basi kwa sasa wamepatiwa fursa hiyo na tunategemea tutapata mshindi ambae ataipeperusha bendera yetu Kwenye mashindano ya miss World ambayo yatafanyika nchini China ",alieleza Basilla.Pia ametolea ufafanuzi kuhusu vigezo ambavo vimewekwa bayana kwa mrembo atakaeshinda taji hilo, ikiwemo umri pamoja na uraia wa Tanzania sambamba ukiwekwa mbele zaidi .

Mshindi wa miss Tanzania atapatiwa taji lenye thamani ya shilingi za kitanzania millioni 6 pamoja na gari lenye hadhi nzuri na viwango pamoja na kupata fursa ya kusaidia jamii yake.
Muandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania Basilla Mwanukuzi akizungumzaa na wanahabari jijini Dar es salaam kuhusu mashindano ya warembo hao yanayotarijiwa kufikia kilele chake mwanzoni mwa septemba mwaka huu

DIWANI MAMUYA ACHAGULIWA MAKAMU MWENYEKITI HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI.

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

DIWANI wa kata Marangu Mashariki katika jimbo la Vunjo,Mh Exaud Mamuya amechaguliwa kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi baada ya kushinda kwa kura 45 zilizopigwa .

Katika kinyang’anyiro hicho ,Mh Mamuya alikuwa akichuana na wagombea,Filbert Shayo kutoka chama cha NCCR-Mageuzi na Chata Madata wa Chama cha Mapinduzi ambaye hata hivyo baadae alienguliwa.

Akizungumza wakati wa Uchaguzi huo, Afsa Uchaguzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Patrick Nyavanga alitoa ufafanuzi wa namna mshindi anavypatikana katika uchaguzi huo ikiwemo mshindi kupata kura za ndio zisizopungua asilimia 50 ya kura zote zilizopigwa.

Alisema uchaguzi huo unafanyika kwa mujibu wa kifungu namba 6 cha kanuni za kudumu za Halmashauri na baraza la madiwani wa Halmashauri wa Wilaya ya Moshi likaridhia kufanyika kwa uchaguzi wa Makamu mwenyekiti.Uchaguzi huo ulilazimika kufanyika kwa awamu mbili baada ya awamu ya kwanza kukosekana mshindi baada ya wagombea wote kutofikisha zaidi ya nusu ya kura zote zilizopigwa.

Katika marejeo ya awamu ya piliya zoezi la upigaji kura jumla yakura 45 zilipigwa ambapo Mh,Mamuya alipata kura 45 baada ya mgombea kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi Mhe,Shayo kuamua kujitoa wakati wa uchaguzi wa marudio na Mhe.Chata kuenguliwa.

Msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi Peter Malendecha alimtangaza Mhe.Exaud Willison Mamuya mgombea kwa tiketi ya CHADEMA kuwa Makamu Mwenyekitiwa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kwakipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019.

Akizuzngumza mara baada ya kumtangaza mshindi,Malendecha alisema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki na umeendeshwa kwa amani na utulivu kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya uchaguzi.
Mbali na uchaguzi huo baraza la madiwa wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi limeunda kamati na kufanya uchaguzi wa wenyeviti wa kamati mbalimbali za kudumu za Halmashauri ikiwemo kamati ya Elimu ,afya na maji, kamati ya maadili, kamati ya mipango miji na kamati ya Uchumi, ujenzi na mazingira.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Exaud Mamuya (katikati) akiwakatika vazi maalumu baada ya kuchaguliwa kwamara nyingine kushika nafasi hiyo.

FILAMU YA BAHASHA YAPATA MAPOKEZI MAKUBWA TOKA KWA WANANCHI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Valentino Mlowola amesema njia nzuri ya kusambaza na kupeleka ujumbe kwa wananchi kuhusu mapambano dhidi ya rushwa ni kutumia sanaa.

Mlolowa amesema hayo wakati wa uzinduzi wa filamu inayojulikana kwa jina la BAHASHA iliyoandaliwa na ubalozi wa Uswisi na Uholanzi kwa kushirikiana na Takukuru inayozungumzia madhara yanayojitokeza katika sehemu mbalimbali inayosababishwa na rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa filamu hiyo, Mlolowa amesema sanaa ni njia nzuri ya kuweza kufikisha ujumbe kwa urahisi kwakuwa wananchi wanapenda sana sanaa na filamu hii itawasaidia zaidi katika kuona madhara yanayokuja baada ya rushwa.

Amesema kuwa, filamu hii ina ujumbe mzuri sana na wanatarajia mwakani katika mbio za mwenge isambazwe ili nchi nzima ili wananchi waelewe madhara yatokanayo na rushwa na wananchi wameipokea kwa muitikio mkubwa sana.

Kwa upande wa Ubalozi wa Uswisi Florence Tinguely Mattli amesema kuwa nchi yao imekuwa inashirikiana na Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa na wanaunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli katika kupinga na kupambana na rushwa. Balozi Mattli amesema kuwa filamu hii ya BAHASHA ni mali ya taasisi ya Takukuru na wao ndiyo watakaoisambaza kwa wananchi nchini na watashirikiana na serikali katika kupambana na rushwa kwenye nyanja zote.

Muandaaji wa Filamu hiyo Louise Kamin amesema kuwa filamu hii imechukua takribani miaka mitano kuandaa filamu hii wakishirikiana na Takukuru mpaka kuweza kuanza kurekodi na wakatumia wiki sita kukamilika na wameifanyia mkoani Arusha.

Louise amesema kuwa hii ni filamu yake ya tatu kuifanya nchini na wameweza kupata waigizaji hao kupitia filamu alizofanya hapo awali ikiwemo Catherine 'Hidaya' ambaye ni muigizaji bora wa filamu tizo aliyoipata kupitia Zanzibar International Film Festival (ZIFF) 2018

Filamu ya BAHASHA ni filamu inayozungumzia namna wananchi wanavyoathirika kwa ajili ya rushwa, tukimuona mwenyekiti wa mtaa wa Mtakuja, Kitasa akichukua fedha kwa ajili ya kuwashawishi kamati yake watie saini na kuruhusu eneo la wazi kujengwa eneo ambalo watoto wamekuwa wanalitumia kwa ajili ya michezo, likiwa karibu na shule ambapo katika jengo hilo walilojenga liliweza kuleta madhara ya uharibufu ya miundo mbinu ya maji, kubakwa kwa mtoto wake wa kike Hidaya na changamoto zingine mbalimbali.

Waigizaji wa filamu hiyo, mhusika mkuu Ayoub Bombwe 'kitasa' amesema kuwa kuanzia sasa yeye ni balozi namba moja wa kupinga rushwa kwani ameona ni namna gani rushwa inaleta madhara katika jamii, pia Catherine 'Hidaya' amesema kuwa filamu hii imelenga zaidi katika jamii iliyotuzunguka na filamu ya bahasha imeonyesha rushwa katika kila sekta ikiwa hospitali mtaani pia watu wameipokea kwa mapokezi makubwa sana tofauti na walivyodhania.

Filamu hii imetengenezwa na kampuni ya MFDi ikiongozwa na muandaaji Jordan Riber wakiwa tayari wameshafanya filamu ya Fatuma, tamthilia ya Siri ya Mtungi.
 
 Waalikwa mbalimbali wakifuatilia kwa makini filamu ya BAHASHA iliyozunduliwa jana usiku na Ubalozi wa Uswisi kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi na Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Valentino Mlolowa akizungumza na wageni waalikwa waliofika katika uzinduzi wa filamu ya BAHASHA uliofanyika jana usiku Jijini Dar es Salaam.
 Muandaaji wa Filamu hiyo Louise Kamin akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa filamu ya BAHASHA uliofanyika jana, filamu hiyo inayohusu Rushwa imewezwa kuandaliwa baina ya ubalozi wa Uswisi na Uholanzi pamoja Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU).



NEC YAENDELEA KUTOA DARASA KWA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MDOGO YAENDELEA JIJINI DODOMA

$
0
0



Afisa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Stephen Elisante akimtazama mmoja wa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi aliyekua akifunga kituturi cha kupigia Kura leo jijini Dodoma wakati wa mafunzo kwa vitendo ya Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16, 2018.
Mafunzo kwa Vitendo yanayoendeshwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi yakiendelea jijini Dodoma kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16, 2018 katika jimbo la Ukonga na Monduli na kwenye Kata 13 za Tanzania Bara.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo ya Usimamizi wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16, 2018 katika jimbo la Ukonga na Monduli na kwenye Kata 13 za Tanzania Bara.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo ya Usimamizi wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16, 2018 katika jimbo la Ukonga na Monduli na kwenye Kata 13 za Tanzania Bara.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo ya Usimamizi wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16, 2018 katika jimbo la Ukonga na Monduli na kwenye Kata 13 za Tanzania Bara.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi akichangia na kuuliza maswali wakati wa wa mafunzo ya Usimamizi wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16, 2018 katika jimbo la Ukonga na Monduli na kwenye Kata 13 za Tanzania Bara.

Wanakijiji Arumeru wafurahia kupata Mawasiliano ya uhakika kutoka Halotel.

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda (katikati), akiwaelekeza wakazi wa Kijiji cha Timbolo namna ya kutumia huduma za mtandao wa Halotel wakati wa ziara ya waandishi wa habari kutembelea miundombinu ya kampuni hiyo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Timbolo Halmashauri ya Wilaya ya Arusha DC, Samwel Kivuyo, akifafanua jambo wakati kwa waandishi wa habari waliotembelea kijiji hicho kuangalia miundombinu ya mawasiliano iliyowekwa na Kampuni ya Halotel. Kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Josephine Mhina.

Wakazi wa kijiji cha Timbolo,Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, wamepongeza jitihada za mtandao wa simu wa Halotel kwa kufikisha mawasiliano kijijini hapo baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kupata huduma za Mawasiliano ya uhakika jambo ambalo limechangia kwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa kijiji hicho hususani huduma jumuishi za fedha(financial inclusion).

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa kijiji hicho, Bw. Samwel Kivuyo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali walipokwenda kutembelea katika kijiji hicho ili kuona na kujifunza shughuli mbalimbali za kimaendeleo ambazo zimechangiwa na mtandao huo kuwekeza katika maeneo ambayo awali hayakuwa na huduma za mawasiliano ya uhakika.

‘’Halotel wamesaidia sana kufikisha huduma jumuishi za kifedha kwa wananchi masikini wa kijiji hiki ambao awali walikuwa wanataabika na kupitwa na huduma hizo hivyo kulazimika kutembea kilometa nyingi kufuata huduma za kifedha,kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji hicho, Bw. Samwel Kivuyo.

Baadhi ya wanakijiji wa kijiji hicho katika kata ya Sambasha,wameelezea kufurahishwa na huduma ya Halopesa,ambapo wamesema,imekuwa rafiki kulinganisha na huduma kama hizo zinazotolewa na kampuni nyingine,kufutia Halotel kutotoza makato pindi mtumiaji wa huduma hiyo akituma pesa kwenda mtandao huo.

“ Kwakweli ukiwa na huduma za Haloteli,unafurahia kupata muda wa maongezi wa kutosha,data ndiyo siwezi kuelezea,yaani ni huduma rafiki sana kwa sisi hasa wa huku kijijini ambao kipato chetu ni cha chini. Alisema,Rehema Joshua,mkazi kijiji cha Timbolo,kata ya Sambasha,Wilaya ya Arumeru,mkoa wa Arusha.

“Sisi kama wananchi wa Timbolo tunashukuru kwanza kabisa jitihada za serikali kwa kuiwezesha kampuni ya Halotel kuweza kuweka minara ya mawasiliano katika kijiji chetu ili wananchi waweze kupata huduma za mawasiliano katika maeneo yao na kusaidia wananchi kutumia huduma za mawasiliano katika kujiendeleza kiuchumi kwani hapo awali hatukuwa na huduma ya mawasiliano ya uhakika.,”

Mpaka sasa hali ya mawasiliano katika kijiji chetu ni nzuri, watu wamepata ajira kufuatia kuanzisha biashara za huduma za kifedha kwa njia ya simu pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao ya mboga mboga ambayo ni kazi kuu ya wanakijiji wetu, kwani mara ya kwanza mawasiliano na wafanyabiashara wengine yalikuwa ni magumu ila sasa tuna uhakika wa wateja kwa sababu tunawasiliana nao moja kwa moja na hata upokeaji wa malipo umekuwa ni rahisi. Alisema Kivuyo na kuongeza.

“Tunafurahi sana kuwa na mradi wa mawasiliano katika kijijj chetu kwa sababu miundo mbinu ya mawasiliano iliyojengwa na Halotel .Katika kijiji chetu imesaidia wananchi kuimarisha usalama katika maeneo mbalimbali ya kijiji chetu kwani imekuwa rahisi kupeana taarifa mbalimbali katika kijiji chetu. Alisema

Aidha Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa hadi sasa changamoto inayowakabili kijijini hapo ni Ukosefu wa umeme katika kijii hicho jambo ambalo linatatiza shughuli za maendeleo kwa baadhi ya wananchi.

“Tunaomba Wakala wa umeme vijijini(REA) watusaidie kupata umeme hasa katika kitongoji cha Meduti na Murerian ili wananchi waweze kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo na kijamii,ikiwemo kilimo, uchomeleaji wa vyuma, shuleni, vituo vya afya ili wananchi waweze kuboresha maisha yao na kujiongezea kipato katika kijiji hicho kilichoanzishwa mwaka 1972 chenye wakazi 4638 na jumla ya kivitongoji vinne ambavyo ni Oltingidi, Madukani, Meduti na Muterian”,alisema mwenyekiti huyo.

Baada ya kuzungumza na mwenyekiti huyo wa kijiji cha Timbolo,kuhusiana na kadhia hiyo ya umeme,waandishi walimtafuta mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro,kutaka kufahamu namna serikali inavyoweza kuwasadia wananchi hao,ambao tayari wameshafanya jitihada za kufungiwa mfumo wa umeme majumbani mwao.

“Kwakweli nawapongeza wananchi hao wa kijiji cha Timbolo,kwa jitihada zao na serikali inafurahishwa mno na ana ya wanachi wanaopenda kujiletea wenyewe maendeleo,na nimemtaka mwenyekiti wa kijji cha Timbolo, Samwel Kivuyo,aje wakati wowote ofisni kwangu akiwa na wawakilishi watatu wa wanakijiji waje tuzungumze na kumaliza mara moja kadhia hiyo ya umeme”,alisema,mkuu wa Wiayaya Arumeru, Jerry Muro.

Wakati huo huo mkuu wa Idara ya Mawasilianno,Kampuni ya Halotel Tanzania, Mhina Simwenda alisema kuwa kampuni ya Halotel Tanzania ipo mkoani Arusha kwa ajili ya kuongea na wateja,kusikiliza maoni kutoka kwao, kujua wanahitaji nini, kujua changamoto walizonazo ili waweze kuboresha huduma zao kwa wateja.

“Ukiangalia kijiji cha Timbolo ndiyo chenye mafanikio mazuri katika suala la mawasiliano na sisi kama Halotel Tanzania tunaishukuru serikali ya kijiji cha Timbolo kwa kuunga mkono juhudi za kampuni yetu ili tuweze kuleta huduma za mawasiliano hapa kijijini,” alisema, Semwenda.

Waziri Mwakyembe akutana na Wamiliki wa Televisheni nchini

$
0
0


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza na wawakilishi wa wamiliki wa televisheni nchini (hawapo pichani) wakati alipokutana nao mapema hii leo jijini Dar es Salaam ili kusikiliza matatizo ya visimbuzi, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi.
TCRA Wadau 3
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi (kushoto) akizungumza na wawakilishi wa wamiliki wa televisheni nchini (hawapo pichani) wakati Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) alipokutana nao mapema hii leo jijini Dar es Salaam ili kusikiliza matatizo ya visimbuzi, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba.
TCRA Wadau 1
Baadhi ya wawakilishi wa wamiliki wa televisheni nchini wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati alipokutana nao mapema hii leo jijini Dar es Salaam ili kusikiliza matatizo ya visimbuzi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS JOHN MAGUFULI KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA 18 WA TPSF

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. kwa niaba ya Rais John Magufuli akifungua Mkutano Mkuu wa 18 wa Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF). umefanyika leo Agosti 28/2018 Jijini Dar es salaam

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Akiwa katika Picha ya pamoja na Washriki wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF). leo Agosti 28/2018 Jijini Dar es salaam.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Akiwa katika Picha ya pamoja na Washriki wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF). leo Agosti 28/2018 Jijini Dar es salaam

WAKUTUBI WAPATIWA MAFUNZO YA KUHIFADHI TAFITI KWA NJIA YA TEHAMA

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa tume ya Sayansi na Teknolojia , Dkt .Amos Nungu akizungumza na watalaamu wa Maktaba wakati akifungua mafunzo ya Tehama kwa wakutubi  kutoka taasisi mbalimbali nchini
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Biashara cha CBE , Profesa  Frolence  Luoga, akizungumza wakati wa Mkutano wa wakutubi juu ya masuala ya Tehama katika kuhifadhi tafiti zinazofanywa hapa nchini na nje ya nchi kwa ajili ya kusoma.
 Sehemu ya Wakutubi walioshiriki  mafunzo ya kuhifadhi tafiti kwa njia ya Tehama wakisikiliza somo kwa makini
Mkurugenzi Mkuu wa tume ya Sayansi na Teknolojia , Dr .Amos Nungu akiwa katika picha ya Pamoja na wakutubi walioshiriki mafunzo ya Tehama kwa ajili ya kutunza tafiti katika Maktaba

Wapelelezi wa Kodi Afrika Mashariki Kushirikiana Kupambana na Uhalifu

$
0
0
Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Salim Kessi akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano wa Kamati ya wapelelezi wa Kodi Afrika Mashariki.
Wajumbe wa Kamati ya wapelelezi wa kodi wakifuatilia kwa makini hotuba ya Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi TRA Salim Kessi (hayupo katika picha) wakati akifungua rasmi mkutano.
Wajumbe wa Mkutano wa Kamati ya Wapelelezi wa Kodi Afrika Mashariki katika picha ya Pamoja na Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi TRA Salim Kessi (katikati walioketi) mara baada ya ufunguzi wa mkutano katika ukumbi wa Benki Kuu Zanzibar.

Na Oliver Njunwa

Wapelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki wametakiwa kuharakisha mchakato wa kuandaa mtaala wa kuwajengea uwezo wapelelezi wa kodi pamoja na mfumo wa kisheria ili kuweza kushirikiana katika kupambana na uhalifu katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Wito huo umetolewa na Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Salim Kessi wakati akifungua Mkutano wa Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Makamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki unaofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Zanzibar.

“Tunataka mchakato huu umalizike mapema ili tuweze kupambana na uhalifu katika ukusanyaji wa kodi kwani kadri tunavyochelewa ndivyo na wahalifu wanaendelea kusababisha upotevu wa kodi kwa mamlaka zetu za mapato”, alisema Bw. Kessi.

Aliongeza kwamba kwa siku nne ambazo watakuwa Zanzibar wanatakiwa kukamilisha hiyo kazi ili iweze kuwasilishwa katika kikao cha Makamishna wa Upelelezi wa Kodi Afrika Mashariki ambao walikubaliana kushirikiana kufanya upelelezi wa kodi kwa pamoja kupampana na kudhibiti uhalifu katika masuala ya kodi.

Aidha aliwapongeza wajumbe wa kamati hiyo ya ufundi kwa jitihada zao ambazo zimewezesha kuundwa kwa chombo cha uendeshaji ambacho kitasaidia ubadilishanaji wa taarifa na upepelelezi wa pamoja katika ukanda wa Afrika Mashariki.

“Ni kutokana na jitihada hizo sasa tayari tuna rasimu ya mkataba wa huduma ambayo itatoa uhalali wa operesheni katika kubadilishana taarifa na upepelezi wa pamoja”, alisisitiza Bw. Kessi na kuongeza kwamba pia kuwepo kwa mwongozo wa upelelezi wa pamoja na kanuni za maadili ni jambo la kujivunia.

Mkutano huo unahudhuriwa na wapelezi wa kodi kutoka Mamlaka za Mapato za Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi na Tanzania ambao ni wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Makamishna wa Upelelezi wa Mamlaka za Mapato Kodi Afrika Mashariki.

Kaimu Naibu Kamishna huyo wa Upelelzi wa Kodi aliwaambia wajumbe hao kwamba ishara ya kwamba mwelekeo wa kushirikiana katika upelelzi ni mzuri inaonekana hata kama chombo cha kisheria hakijakamilika kwani tayari wamebadilishana taarifa za Himaya ya Pamoja ya Forodha na kufanya usuluhishi katika jumuiya.

Naye Meneja wa Upelelezi wa Mamlaka ya Mapato Kenya (KRA) Jonah Ogalo amesema kwamba mkutano huo ni muhimu kwa nchi za Afrika Mashariki katika kuweka mikakati ya pamoja kukabiliana na uhalifu katika ukusanyaji wa kodi na kuongeza kwamba kukamilika kwa mtaala wa mafunzo kwa wapelelezi wa kodi kutawasaidia kushirikiana na kubadilishana taarifa za kiintelijensia na hivyo kuokoa mapato ya serikali.

Kamati ya Ufundi ya wapelelezi wa kodi inatarajiwa kutoa mtaala wa pamoja wa mafunzo ya kuwaongezea ujuzi wapelelezi wa Kodi pamoja na kuunda mfumo wa pamoja wa kisheria utakao wawezesha kufanya upelelezi kwa pamoja kutokana na kila nchi kuwa na sheria zake isipokuwa katika masuala ya Forodha ambapo nchi za Afrika Mashiriki zinatekeleza sheria moja ya Usimamizi wa Forodha.

WALENGWA WA TASAF MKOANI KILIMANJARO WAIANGUKIA SERIKALI.

$
0
0
Na Estom Sanga-Kilimanjaro.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Mkuchika yuko katika ziara ya kikazi mkoani Kilimanjaro kukutana na wananchi wanaonufaika na huduma za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF kupitia Mpango wake wa Kunusuru Kaya Maskini- PSSN.

Akiwa katika ziara hiyo, Mhe. Mkuchika amejionea namna Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, walivyoboresha maisha yao kwa kutumia huduma za TASAF kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini zinazoambatana na ruzuku ya fedha, elimu ya ujasiliamali na utekelezaji wa masharti ya Elimu na Afya huku mkazo ukiwekwa katika kuwajengea mazingira ya kukuza kipato cha Walengwa hao.

Akizungumza na Walengwa katika wilaya za Same, Mwanga,Siha na Hai kwa nyakati tofauti ,Mhe. Mkuchika amesema shughuli za TASAF ni mwendelezo wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2015 ambayo imeielekeza serikali kutumia mbinu mbalimbali za kutatua kero ya umaskini miongoni mwa wananchi kwa lengo la kuboresha maisha yao.

Amesema kutokana na dhamira thabiti ya serikali katika mapambano dhidi ya Umaskini , wananchi kwa ujumla wao hususani wale waliojumuishwa kwenye Mpango wa TASAF wanapaswa kujituma zaidi katika kuanzisha na kutekeleza miradi ya uzalishaji mali ili waweze kujiongezea kipato na hatimaye kuondokana na adha ya umaskini.

Waziri huyo wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora amesema kwa kiwango kikubwa amevutiwa na jitihada zilizoonyeshwa na sehemu kubwa ya Walengwa wa TASAF kwa kutumia vizuri huduma za Mfuko huo ambazo amesema zimeanza kuboresha maisha yao na kuamusha ari ya kujiletea maendeleo kwa kufanya kazi kwa bidi zaidi.

Amesema uboreshaji wa makazi ,ufugaji wa mbuzi,kuku,bata na hata ng’ombe unaofanywa na Walengwa hao wa TASAF ni kieleleza tosha cha namna wananchi hususani waliokuwa wakiishi katika umaskini, walivyo na ari kubwa ya kujiondoa kwenye umaskini wa kipato jambo ambalo amesema serikali itaendelea kuwaunga mkono kwa kuwawekea mazingira wezeshi ya kufanikisha azma yao hiyo.

Aidha amesema hivi sasa mipango ya kujumuisha vijiji ambavyo havikupata fursa ya Mpango huo wa TASAFiko mbioni na kuwa wananchi ambao katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini hawakujumuishwa , watapata fursa hiyo katika awamu ijao ya utekelezaji wake baada ya wananchi wengi kuendelea kuomba huduma hizo za TASAF.

Kwa upande wao baadhi ya Walengwa licha ya kuipongeza Serikali kupitia TASAF ,wameomba huduma za Mfuko huo ziendelee kuwasaidia wao na Wananchi wengine ambao kwa sasa wanaishi katika umaskini mkubwa lakini hawakupata fursa ya kutambuliwa na kuandikishwa kwa utaratibu wa Mfuko huo.

“Baadhi ya wenzetu kwenye vijiji vyetu hawanufaiki na utaratibu huu mzuri wa serikali kupitia TASAF lakini nao pia wanakabiliwa na umaskini ,tungeliomba serikali kupitia TASAF iwafikirie pia” amesema bi. Upendo Issa mkazi wa kijiji cha Kileo,wilaya ya Same.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Mkuchika (aliyevaa kofia) akikagua nyumba inayojengwa na mmoja wa Walengwa wa TASAF (wa kwanza kulia ) katika kijiji cha Kileo,wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.
Waziri wan chi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Mkuchika (katikati waliosimama) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walengwa wa TASAF katika wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro baada ya kuzungumza nao juu ya manufaa wanayoyapata kutokana na huduma za mfuko huo.

Mhe. George Mkuchika Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (aliyevaa koti nyeusi ) akihesabu fedha kabla ya kumkabidhi mmoja wa Walengwa wa TASAF mkoani Kilimanjaro baadhi ya kuridhishwa na jitihada za mlengwa huyo katika kupambana na umaskini kwa kutumia ruzuku ya TASAF.
Waziri Mkuchika akiangalia moja ya mazizi ya mbuzi za Walengwa wa TASAF katika wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro ikiwa ni mojawapo ya njia za kujiongezea kipato kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Mhe. Kippi Warioba(wa pli kulia )akieleza jambo baada ya Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mhe. George Mkuchika kutembelea mojawapo ya makazi ya Mlengwa wa TASAF (mwenye kilemba) wilayani Siha

KASI YA UJENZI WA JENGO LA TRA PWANI HAIRIDHISHI -RC NDIKILO

$
0
0


Jengo la mamlaka ya mapato mkoani Pwani ambalo linasuasua katika ujenzi wake ambao ulitakiwa kukamilika tangu june 2016 .(picha na Mwamvua Mwinyi).
Mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo alipotembelea jengo la idara ya uhamiaji mkoani Pwani ambalo limekamilika kwa gharama ya bilioni 1.6(picha na Mwamvua Mwinyi) .
Mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo(kulia) alipotembelea ujenzi wa jengo la CRDB mkoani Pwani ambalo limekamilika kwa gharama ya milioni 900 , mbele kulia meneja CRDB Pwani Rosemary Nchimbi. (picha na Mwamvua Mwinyi


NA MWAMVUA MWINYI,PWANI .

MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa jengo la mamlaka ya mapato Tanzania, (TRA) mkoani humo ,ujenzi ambao unasuasua kwa miaka miwili sasa na kubaki gofu.
Aidha amesema jengo hilo hadi lilipofikia halilingani na thamani ya sh.bilioni 1.653.267 .510 ambayo ni awamu ya kwanza iliyofikia asilimia 61 hadi sasa.
Kufuatia hali hiyo ,Ndikilo amemuelekeza meneja wa mamlaka hiyo mkoa ,kumfikishia salamu kamishna wa mamlaka ya mapato makao makuu kufuatilia mradi wa ujenzi huo . 

Mkuu huyo wa mkoa alieleza masikitiko hayo ,wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea maeneo ya ujenzi wa viwanja ya taasisi binafsi na serikali katika halmashauri ya Mji wa Kibaha,ikiwemo Uhamiaji,TRA na CRDB.
Alisema ,lengo la kupewa viwanja hivyo ni kujenga maeneo hayo na sio kukumbatia viwanja bila sababu za msingi.

“Serikali ya mkoa na waziri mkuu Kassim Majaliwa ilishatoa agizo tangu mwaka juzi kuwa maeneo hayo yote yahakikishwe yanajengwa na kama haiwezekani wanyanganywe wahusika na kupewa wengine wenye uwezo” alisisitiza Ndikilo.
Ndikilo alishangazwa na kupewa taarifa pia kuwa ujenzi huo bado unahitaji zaidi ya milioni 200 wakati hatua ya kwanza haiendani na maelekezo ya serikali na mkoa. “Gharama imesemwa itakuwa bilioni 2.693.402.120 ,ambapo mkandarasi Humphrey Construction Ltd, bado anahitaji fedha zaidi ambayo itafikia bilioni 2.8 jambo ambalo haliniingii akilini'” .

“Kwanza mmeshaezeka mabati Leo hii mnaniambia mtaendelea na hatua nyingine ya ujenzi kwa ghorofa tatu ambapo mtaondoa mabati ambayo yameshagharamiwa halafu muongeze majengo tena , haiwezekani nitaagiza vyombo vyangu vya ulinzi na usalama vichunguze zaidi, ” alifafanua Ndikilo .
Awali meneja wa TRA Pwani, Euvensia Lwiwa alisema ,jengo hilo lilitakiwa likamilike 23,June 2016 ,na ilipofika 2017 mkandarasi aliongezewa muda hadi Juni 2017 . 

Alisema ,walisimamisha kazi ili kutafuta fedha za kuendeleza mradi kwa kipindi cha miezi mitatu July -September 2017 suala ambalo limekwama kutokana na kukosa fedha . Euvensia alielezea kuwa ,kumekuwepo na mazungumzo kati ya mkandarasi, mshauri wa mradi na TRA kuhusu maelewano ya gharama za kumaliza mradi ambao bado upo chini ya mkandarasi. 

Nae mshauri elekezi kutoka Alpha Architects Ltd ambae pia ni meneja mradi ,Fulgence Kibiki alisema, wamekwama kutokana na TRA kukosa fedha kwa wakati hali inayosababisha jengo kukosa ubora . 

Akiwa kwenye ziara hiyo kwenye jengo la CRDB ,meneja wa taasisi hiyo ya kifedha Rosemary Nchimbi alisema ,jengo hilo ni la ghorofa moja na ujenzi unatarajiwa kugharimu sh. milioni 900.Kwa upande wake ,naibu kamishna wa uhamiaji ambae pia ni Ofisa wa idara ya uhamiaji Mkoani Pwani, Plasid Mazengo alisema jengo la uhamiaji limegharimu bilioni 1.6 na limeshaanza kutumika.

SERIKALI IMETENGA BILIONI 30 KUJENGA HOSPITALI ZA RUFAA ZA MIKOA

$
0
0

Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya uendeshaji wa hospitali za rufaa za mikoa mbele ya kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii jijini Dodoma.
Naibu waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwasilisha ripoti ya uendeshaji wa Hospitali za rufaa za mikoa mbele ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge huduma na maendeleo ya jamii jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii Mhe. Peter Selukamba akitoa neno wakati wa kuwasilisha kwa taarifa za uendeshaji wa hospitali za rufaa za mikoa kutoka wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto jijini Dodoma.
Wajumbe wakifuatilia mjadala uliokua unaendelea katika kikao cha mawasilisho ya taarifa za uendeshaji wa Hospitali za rufaa za mikoa kutoka wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto katika kamati ya kudumu ya Huduma na maendeleo ya jamii jijini Dodoma

Na.WAMJW-Dodoma


Serikali imetenga shilingi bilioni 30 kwa ajili ya kujenga na kukarabati miundombinu ya hospitali zaRufaa za Mikoa kila mkoa ili kuweza kuwawezesha wananchi kupata huduma za rufaa za kibingwa karibu na wanapoishi na hivyo kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati akiwasilisha taarifa za uendeshaji wa hospitali za rufaa za Mkoa kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Jijini Dodoma.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha hospitali za Rufaa za Mikoa ya Geita, Katavi, Simiyu, Njombe na Songwe ambapo zipo katika hatua za ujenzi wa hospitali hizo hivyo itafanya idadi ya hospitali hizo kuwa 28 pindi zitakapokamilika.

“Serikali ilifanya mabadiliko ya kuzihamishia hospitali za Rufaa za Mikoa Wizarani ili kuboresha huduma za kibingwa ikiwemo kutoa fursa nzuri ya udhibiti ,usimamizi na mgawanyo wenye tija zaidi wa rasilimali chache zilizopo”alisema Dkt.Ndugulile.

Alisema kuwa baada ya Wizara kukabidhiwa hospitali hizo ilifanya tathimini ya awali ya hali halisi na kubaini changamoto mbalimbali zilizoathiri utoaji wa huduma za afya katika maeneo yote ambayo ni nguzo ya msingi katika kuwezesha upatikanaji wa huduma bora. “Hospitali za Rufaa za Mikoa zinapaswa kutoa huduma za kibingwa ambazo hazitolewi katika hospitali ngazi ya Halmashauri,Huduma za kibingwa ambazo ni lazima kupatikana katika hospitali za Rufaa”.Alisema Naibu Waziri Dkt. Ndugulile

Alitaja huduma za kibingwa ambazo zinatakiwa kutolewa katika hospitali hizo za Rufaa za Mikoa ni pamoja na upasuaji wa jumla,magonjwa ya uzazi na yanayoathiri wanawake, magonjwa ya watoto,magonjwa ya ndani ,magonjwa ya kinywa na meno na Radilojia.

Kwa upande wa ubora wa huduma zinazotolewa Naibu Waziri huyo alisema Wizara ilifanya kaguzi za kuzitambua hali halisi ya ubora wa huduma za afya zinazotolewa katika hospitali hizo na jumla ya hospitali za rufaa ishirini na moja zilifanyiwa tathimini na kupewa nyota kutokana na vigezo vilivyowekwa na kupewa mpango kazi wa kuboresha huduma.

“Ni hospitali 9 zilipata nyota mbili, hospitali kumi na moja zilipata nyota moja na hospitali moja ilipata nyota sifuri,hivyo hakuna hospitali yeyote iliyopata nyota 3 hapa nchini.Alimalizia Dkt.Ndugulile

RAIS DKT SHEIN AKUTANA NA UJUMBE WA BoT

$
0
0

Rais wa Zanzibar na Mswenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akisalimiana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof Florens D.M Luoga alipofika Ikululu Mjini Zanzibar leo akifuatana na ujumbe wake,[Picha na Ikulu.] 28 Aug 2018.

Rais wa Zanzibar na Mswenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akifuatana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof Florens D.M Luoga baada ya mazungumzo alipofika Ikululu Mjini Zanzibar leo akifuatana na ujumbe wake,[Picha na Ikulu.] 28 Aug 2018.

Rais wa Zanzibar na Mswenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akizungumza na Ujumbe wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ulipofika Ikululu Mjini Zanzibar leo ukiongozwa na Gavana Prof Florens D.M Luoga (wa pili kuli),[Picha na Ikulu.] 28 Aug 2018.

Waziri Mwakyembe atembelea Global Group

$
0
0







Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdalah Mrisho (kulia) akimkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe wakati Waziri alipotembelea ofisi za Global Group mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mhariri wa gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli (kushoto) akimuonesha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe wakati Waziri alipotembelea ofisi za gazeti hilo Global Publishers mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi (kushoto) akizungumza na wafanyakazi Global Group wakati Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) alipotembelea ofisi za Global Group mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdalah Mrisho.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Global Group wakati Waziri alipotembelea ofisi za Global Tv mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (mwenye shati la zambarau) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Global Group wakati Waziri alipotembelea ofisi hizo mapema hii leo jijini Dar es Salaam

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI KIJAZI AMJULIA HALI DKT.KIGWANGALLA MOI

$
0
0

Katibu Mkuu Kiongozi nchini, Balozi Mhandisi John Kijazi akitoa maelekezo kwa jopo la Madaktari Bingwa na Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Taasisi ya Mifupa ya MOI ambao wanamtibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (Aliyeketi) alipomtembelea mapema leo Agosti 28,2018, Wodi ya Kitengo cha Mifupa MOI.
Katibu Mkuu Kiongozi nchini, Balozi Mhandisi John Kijazi akishuhudia picha ya X ray inayoonesha eneo la mkono wa kushoto wa Waziri Dkt. Hamisi Kigwangalla anayepatiwa tiba MOI namna unavyoendelea. Aliyeshika Xray ni Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface, wengine ni Mkurugenzi mtendaji wa Muhimbili, Profesa Laurence Museru na Mkurugenzi wa Tiba MOI Dkt. Samuel Swai. Mapema leo Agosti 28,2018, Wakati alipomtembelea Wodi ya Kitengo cha Mifupa MOI.

…………………..

Katibu Mkuu Kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Mhandisi John Kijazi leo tarehe 28/08/2018 amemtembelea na kumjulia hali Dkt Hamisi Kigwangalla ambaye anapata matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI akiuguza majeraha ya mkono aliyopata katika ajali iliyotokea Agosti 4, mwaka huu Mkoani Manyara.

Balozi Kijazi amempa pole Mh Dkt. Kigwangalla na kumtakia heri na apone haraka ili aweze kurejea kwenye majukumu yake ya kila siku kwani Taifa linauhitaji mchango wake. “Pole sana. Mungu atajalia utapona na utarejea nyumbani mapema, na kwa kuwa wewe ni daktari ukiona hali si nzuri utawafahamisha wenzio mapema ili mjadiliane namna ya kuikabili hali itakayojitokeza” Alisema Balozi Kijazi wakati wa kumjulia pole Hospitalini hapo.

Aidha, Balozi Kijazi amemueleza Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface kwamba kwa sasa wananchi wanaridhishwa na huduma zinazotolewa na MOI na Muhimbili kwa ujumla na hii ni faraja kubwa kwa Serikali na hivyo kuelekeza ari hiyo iendelezwe. “Pamoja na Jitihada kubwa za Mh Rais Dkt John Pombe Magufuli za kuboresha huduma za Afya hapa nchini, nanyi pia kwa upande wenu mnajitahidi sana na wananchi wanaridhishwa na huduma mnazotoa. Nafahamu kuna changamoto chache lakini bado mmeendelea kufanya kazi nzuri” Alisema Balozi Kijazi.

Kwa upande wake, Dkt Hamis Kigwangalla amemshukuru Balozi Kijazi kwa kumtembelea na kumjulia hali na amemueleza kwamba afya yake imeendelea kuimarika na anaamini katika kipindi kifupi kijacho madaktari watakapojiridhisha wanaweza kumpa ruhusa ya kutoka hospitalini.

“Ninaendelea vizuri, afya yangu inaimarika siku hadi siku, na pia naendelea na mazoezi na kila siku najiona imara zaidi na hii ni ishara tosha kwamba ninaweza kuruhusiwa kurejea nyumbani” Alisema Dkt. Kigwangalla. Dkt. Kigwangalla alihamishiwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI tarehe 12/08/2018 baada ya kupata matibabu ya awali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kwa sasa bado anaendelea na tiba kuuguza mkono wake wa kushoto.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images