Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI MHE. JAPHET HASUNGA AWAITA WAWEKEZAJI KWENYE HIFADHI TANO ZILIZOPANDISHWA HADHI

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) akioneshwa ramani inayoonesha Ziwa Ngozi ambalo ni miongoni mwa vivutio vya utalii katika Pori la Akiba la Kimisi na aliyekuwa Meneja wa Pori hilo Bigilamungu Kagoma wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana pori hilo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika pori hilo lililopandishwa hadhi kuwa miongoni mwa hifadhi za Taifa.




Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ngala pamoja na baadhji ya watumishi wa TAWA na TANAPA wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana pori hilo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika hilo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( katikati) akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wakati alipowasili katika ofisi za wilaya ya Karagwe kabla ya kutembelea jana pori la akiba Kimisi katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika pori hilo lililopandishwa hadhi kuwa miongoni mwa hifadhi za Taifa, Wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Karagwe, Godfrey Luheluka
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga akisaini kitabu cha wageni mara alipowasili katika ofisi za wilaya ya Karagwe kabla ya kutembelea jana pori la akiba Kimisi katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika pori hilo lililopandishwa hadhi kuwa miongoni mwa hifadhi za Taifa.
(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-WMU)



NA LUSUNGU HELELA-KAGERA

Baada ya kuyapandisha hadhi mapori matano ya akiba, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amewataka wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wachangamkie fursa ya kuwekeza katika Mapori hayo.

Aidha, Amesema Serikali imefuta kodi ya kuingiza magari ya watalii nchini ili kuwawezesha wananchi walio wengi kuingia katika biashara hiyo ikiwa lengo ni kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya Utalii. Ametaja aina ya uwekezaji unaohitajika kuwa ni ujenzi wa hoteli zenye hadhi ya nyota moja hadi zenye nyota tano, nyumba za kulala wageni, uanzishwaji wa makampuni ya utalii pamoja na kutoa huduma za vyakula kwa ajili ya watalii.

Ametoa rai hiyo leo wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Karagwe mkoani Kagera kabla ya kutembelea ziwa Ngoma ambalo ni miongoni mwa vivutio vya utalii vilivyopo katika Pori la Akiba la Kimisi ambalo ni miongoni mwa mapori yaliyo katika mchakato wa kuwa hifadhi za taifa.

Naibu waziri huyo anatembelea mapori ya mkoa wa Kagera kufuatilia hatua iliyofikiwa na Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA)katika kuyaendeleza. Amesema Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika ni hazina na fursa kwa mikoa ya Kaskazini Magharibi mwa Tanzania kufunguka kiutalii kwa wananchi wa maeneo hayo na taifa kwa ujumla.

TAZAMA LIVE KUAPISHWA KWA RAIS WA ZIMBABWE MJINI HARARE HIVI SASA

TEMESA KUSIMIKA TAA ZA BARABARANI VISIWANI ZANZIBAR

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Bw. Mustafa Aboud Jumbe kulia na kaimu Meneja wa Kikosi cha Umeme kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Pongeza Semakuwa wakitia saini mkataba wa mradi wa kusanifu, kujenga na kusimika taa za kuongozea magari barabarani zitakazotumia umeme jua na umeme wa kawaida, tukio hilo lilifanyika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo barabara ya Fumba Kisauni kisiwani Unguja, huo ni mradi wa kwanza kufanywa na TEMESA katika visiwa hivyo na utatekelezwa katika makutano ya Muzamili, Mjini kati, Mtoni na Kwa Pweza mjini Unguja na Mtemani na PBZ Chake Visiwani Pemba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Bw. Mustafa Aboud Jumbe kulia akifurahia jambo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu kushoto mara baada ya kumaliza kutiliana saini mkataba wa mradi wa kusanifu, kujenga na kusimika taa za kuongozea magari barabarani zitakazotumia umeme jua na umeme wa kawaida, tukio lililofanyika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo barabara ya Fumba Kisauni kisiwani Unguja, mradi huo ni wa kwanza kufanywa na TEMESA katika visiwa hivyo na utatekelezwa katika makutano ya Muzamili, Mjini kati, Mtoni na Kwa Pweza mjini Unguja na Mtemani na PBZ Chake Visiwani Pemba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Bw. Mustafa Aboud Jumbe kushoto akijadiliana na uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mara baada kumaliza kutiliana saini mkataba wa mradi wa kusanifu, kujenga na kusimika taa za kuongozea magari barabarani zitakazotumia umeme jua na umeme wa kawaida, tukio lililofanyika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo barabara ya Fumba Kisauni kisiwani Unguja, mradi huo ni wa kwanza kufanywa na TEMESA katika visiwa hivyo na utatekelezwa katika makutano ya Muzamili, Mjini kati, Mtoni na Kwa Pweza mjini Unguja na Mtemani na PBZ Chake Visiwani Pemba. Kutoka kulia ni Kaimu Meneja Kikosi cha Umeme TEMESA Mhandisi Pongeza Semakuwa, Mtendaji Mkuu Dkt. Mussa Mgwatu, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Shomari Shomari na mwanasheria wa TEMESA Bi. Joyce Senkondo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Bw. Mustafa Aboud Jumbe (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mara baada ya kumaliza kutiliana saini mkataba wa mradi wa kusanifu, kujenga na kusimika taa za kuongozea magari barabarani zitakazotumia umeme jua na umeme wa kawaida, tukio lililofanyika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo barabara ya Fumba Kisauni kisiwani Unguja. Kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt Mussa Mgwatu, Mhandisi Pongeza Semakuwa, Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara hiyo Ndg. Hatibu M. Hatibu na kushoto ni Mwanasheria Bi. Joyce Senkondo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg. Shomari Shomari. PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA ZANZIBAR)

Mkurugenzi Mkuu NSSF amtaka Mkandarasi kumaliza barabara Kigamboni kwa wakati.

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF William Erio ametembelea daraja la Kigamboni kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara ya lami yenye urefu wa Kilomita mbili inayo unganisha daraja la Nyerere na barabara ya Feri - Kibada iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Akikagua barabara hiyo mwishoni mwa wiki, William Erio amemtaka Mkandarasi CRJE kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa haraka na kuhakikisha gharama ya ujenzi hazizidi kiasi cha gharama kilicho kubaliwa kwenye mkataba wa ujenzi kati ya NSSF na Mkandarasi huyo.

Kwa upande wa Mkandarasi amepokea maelezo ya Mkurugenzi Mkuu na kuahidi kutekeleza ujenzi huo. Pamoja na kuahidi utekelezaji, Mkandarasi ameomba nyongeza ya muda kutokakana na changamoto za kupatikana kwa malighafi ya udongo hasa ile ya G15.

Gharama ya mradi huu ni Tsh 21.3 billioni ambao unahusisha ujenzi wa barabara yenye njia sita, tatu kila upande zenye urefu wa kilomita mbili kutoka mwisho wa daraja hadi kwenye makutano ya barabara ya Fery - Kibada.

Pia, ujenzi unajumuisha mzunguko wenye mita za mraba 5,762, mifereji ya maji taka na yale ya mvua, kingo za katikati ya barabara "new jersey barriers", kalavati nne za umbo la boksi na moja ya ya umbo la bomba.
Sehemu ya kipande cha barabara unganishi kutoka mwisho wa daraja upande wa Kigamboni kuelekea barabara ya Fery - Kibada.Kaimu Meneja wa Miradi NSSF Abdon Mhando (wa pili kushoto), akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF William Erio (wa kwanza kushoto), wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi wa NSSF Bw. Gabriel Silayo

TANZIA : MAMA MZAZI WA MBUNGE JOSEPH MBILINYI 'SUGU' AFARIKI DUNIA

$
0
0
*Sugu asema msiba upo nyumbani kwake Salasala Dar, mwili kusafirishwa Mbeya baada ya taratibu zitakapokamilika

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MAMA mzazi wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' kupitia Chadema, amefariki dunia leo akiwa  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).Mama wa Sugu alikuwa amelazwa katika hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha amethibitisha kutokea kwa msiba huo.

Kwa upande wake Sugu ameiambia Michuzi Blog kwa njia ya simu kwamba msiba wa mama yake npendwa upo nyumbani kwake Salasala jijini Dar es Salaam."Kama ambavyo mmesikia mama amefariki leo tena mchana huu, hivyo nachoweza kusema mama hatunaye na msiba upo nyumbani Salasala.

" Hata hivyo tutasafirisha msiba kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya kuupumzisha mwili wa mama.Tutatoa ratiba rasmi hapo baadae ila itoshe kusema msiba upo Salasala wakati tunaendelea na taratibu nyingine,"amesema Sugu.

Michuzi Media Group(MMG) inaungana na Watanzania wengine kutoa pole kwa familia ya Sugu,ndugu,jamaa na marafiki.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN

=====  =======  ========  ========

Mama mzazi wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu (Chadema), amefariki dunia leo Jumapili Agosti 26, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), alikokuwa akipatiwa matibabu. Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha, amethibitisha.Mungu ailaze roho ya Marehemu Mama yetu mpendwa mahali pema peponi-AMEN
Mbunge wa Mbeya mjini,Mh Joseph Mbilinyi almaarufu SUGU akiwa na Mama yake MzazI enzi za uhai wake.

HAKUNA SEKTA YOYOTE ISIYOHITAJI HIFADHI YA MAZINGIRA – MAKAMBA

$
0
0
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nyamirembe juu ya utayari wao wa kuhifadhi mazingira ya Kisiwa hicho ili kuwa miongoni mwa maeneo yanayopendekezwa kulindwa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akikagua maeneo ya Kisiwa cha Magafu, takribani mwendo wa dakika thelathini kutoka mwalo wa Nyamirembe. Waziri Makamba aheahidi kutuma wataalamu ili kujiridhisha zaidi kabla ya kutanga katika gazeti la Serikali.

…………………..

Siku ya Sita ya ziara ya Waziri Makamba imemfikisha Mkoani Geita, Wilayani Chato katika Kijiji cha Nyamirembe ambapo pamoja na mambo mengine Mhe. Makamba ametembelea Kisiwa cha Magafu na kuahidi kutuma timu ya wataalamu kwa ajili ya kufanya tathmini ya namna ya kulinda kisiwa hicho kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004, ikiwa ni eneo tengefu kwa mazalia ya samaki.

Akiongea na Uongozi wa Mkoa wa Geita Waziri Makamba amesema kuwa jitihada za Serikali ni pamoja na kuhakikisha ulinzi madhubuti kwa kisiwa hicho ili kiwe kielelezo cha mandhari tulivu kwa mazalia ya samaki na bioanuai.

Waziri Makamba amesema kuwa hakuna sekta yoyote muhimu kwa uchumi wa nchi isiyohitaji Hifadhi ya Mazingira hivyo Sheria ya Mazingira kifungu namba 51 inatoa mamlaka na nafasi ya kulinda maeneo nyeti na kuainisha kuwa kuna dhana potofu kuwa uhifadhi wa mazingira ni kinyume na maendeleo.

Dhana ya uhifadhi inaendana na utashi, uwezo, utayari na ushirikishwaji wa wananchi wenyewe. “Tunapoongelea uhifadhi tunaamanisha, kuweka utaratibu wa kutumia maeneo yaliyopendekezwa kuhifadhiwa kwa taratibu zitakazopendekezwa, mfano kama tunahifadhi kisiwa, tutaweka utaratibu maalumu wa uvuaji wa samaki katika eneo hilo” Makamba alisisitiza.

Pamoja na mambo mengine Waziri Makamba amesema Ofisi yake iko tayari kuteua wakaguzi wa mazingira kadri iwezekanavyo na kutoa mafunzo kwao pindi majina yatakapowasilishwa kwake na Sekretarieti ya Mkoa.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi amesema kuwa Mkoa wake kwa asilimi 35 umezungukwa na madini na kupelekea uharibifu wa Mazingira kutokana na shughuli za uchimbaji hata hivyo Ofisi yake imekuwa ikifanya ukaguzi wa mara kwa mara katika shughuli za uchenjuaji kwa kuhakikisha usalama wa afya za watu na mazingira.

Akielezea jitihada za Mkoa wake katika suala la kuhifadhi mazingira Mhandisi Gabriel amesema wamekuwa na mwendelezo wa kampeni ya upandaji miti kwa kila Halmashauri zote na kutunza miti ya asili, ikiwa ni pamoja kuondoa wavamizi haramu katika misitu, operesheni ambayo ni endelevu. “Huwezi kutenganisha mazingira na uhai wa watu” Mhandisi Gabriel alisisitiza.

Waziri Makamba yuko katika ziara ya kikazi katika Mikoa tisa (8) nchini yenye lengo la kukagua, kutathmini na kuzungumza na viongozi kuhusu maeneo yanayopendekezwa kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira kifungu namba 51.

Waziri Mkuu Majaliwa amjulia hali Dkt. Kigwangalla MOI

$
0
0

Na Andrew Chale,DAR .

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa leo Agosti 26,2018 amemtembelea na kumjulia hali Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla aliyelazwa katika wodi maalum kitengo cha Taasisi ya mifupa MOI, hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Hii inakuwa ni kwa mara ya pili kwa Waziri Mkuu Majaliwa kumtembelea kumjulia hali ambapo awali alimtembelea Jumapili ya Agosti 5, 2018), wakati Dkt. Kigwangalla akipatiwa matibabu ya awali katika Wodi ya Mwaisela. Akiwa wodini hapo, Waziri Mkuu Majaliwa amemtakia kila lakheri katika kuuguza mkono wake ambapo pia amepata kuzungumza nae juu ya maendeleo ya afya yake.

Aidha, Waziri Majaliwa amewashukuru Madaktari wa MOI pamoja na uongozi wake kwa pamoja kutoa huduma bora kwa watanzania na raia wa Nchi za nje ambao wamekuwa kimbilio kuja nchini kupata tiba.

“Nakutakia kila lakheri Kigwangalla. Nimekuja baada ya kusikia umefanyiwa operesheni ya pili. Pia nawashukuru Uongozi na Madaktari wetu wa hapa MOI kwa kutoa tiba nzuri tiba zenu kwa sasa zimezifanya nchi zingine wananchi wake kukimbilia hapa. Viongozi wakuu pia Hospitali hii ndio kimbilio letu kwa sasa na tunawashukuru kwa huduma bora inayofanya Nchi kuwa na heshima kuwbwa,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Kwa upande wake Dkt. Kigwangalla amemwakikishia Waziri Mkuu kuwa kwa sasa anaendelea vizuri kwani ameweza kufanya mazoezi ya ikiwemo kutembea umbali wa kilometa nne pamoja na mazoezi mepesi kila siku majira ya asubuhi na jioni.

“Kwa sasa naendelea vizuri sehemu kubwa ni mkono ndio nauguza. Ila kwa hali ya maendeleo kwa sasa naendelea vizuri pamoja na mazoezi kidogo kidogo naendelea. Alisema Kigwangalla. Aidha, mbali na Waziri Mkuu Majaliwa, jana jioni Agosti 25,2018, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliweza kumtembelea tena na kumjulia hali. 

Dkt. Kigwangalla alipata ajali asubuhi ya Jumamosi, Agosti 4, 2018) katikati ya vijiji vya Mdolii na Minjingu wilaya ya Babati mkoani Manyara baada ya gari lake kupinduka na kusababisha kifo cha Afisa Habari wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Hamza Temba na wengine watano akiwemo Dkt. Kigwangalla kujeruhiwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimjulia haliWaziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, leo Agosti 26/2018 .akiwa anaendelea kupatiwa matibabu katika Wodi aliyo lazwa ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Muhimbili (MOI), PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mwakyembe Atoa Miezi 3 kwa Maafisa Utamaduni kukamilisha Ukusanyaji Wa Maoni Ya Sera

$
0
0

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe(katikati) akitoa maagizo kwa Maafisa Utamaduni Mkoa na Wilaya nchini kukamilisha ukusanyaji wa maoni ya wadau wa Sekta ya Utamaduni kwa ajili ya kuboresha Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1997 katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Umoja wa Machifu uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro,Kushoto ni Mlezi wa Umoja wa Machifu Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bi.Lilian Beleko kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania Chifu Frank Marrialle (kushoto) akitoa ahadi ya umoja huo kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya kuboresha Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1997 kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe(hayupo pichani) katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Umoja wa Machifu Tanzania uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro,kulia kwake ni Mlezi wa Umoja wa Machifu Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia) akikabidhi nakala 21 za Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1997 kwa Mlezi wa Umoja wa Machifu Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela (kushoto) katika Ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Umoja wa Machifu Tanzania,uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kugawa kwa Machifu waliyoshiriki Mkutano huo ili waweze kutoa maoni yao kutokana na mapungufu ya sera hiyo inayofanyiwa marekebisho.
Chifu Nshoma Hawa wa Ukamba Kahama akieleza changamoto zinazomkumba katika ikulu yake ambapo ardhi ya himaya yake iliyozikiwa machifu wenzake kuporwa na kugawiwa kwa wananchi kwa ajili ya kilimo kinyume na utaratibu wa uhifadhi wa ardhi za makazi ya machifu kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) katika Mkutano wa Saba wa Umoja wa Machifu Tanzania uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro.
Chifu Emmanuel Zulu Gama kutoka kwa Wangoni Songea akimwomba Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe(hayupo pichani) ofisi yake kushiriki katika Tamasha la Mashujaa waliyopigana Vita ya Majimaji linalofanyika kila Mwaka Mwezi Februari mkoani Songea,katika ufunguzi Mkutano wa Saba wa Umoja wa Machifu Tanzania uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe aliyeketi (watano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Machifu wa Tanzania mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Umoja wa Machifu Tanzania uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro,wanne kulia ni Mlezi wa Umoja wa Machifu Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela,na wanne kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania Chifu Frank Marrialle.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) akiwasisitiza Machifu wa Tanzania(hawapo pichani) kuhakikisha wanawasilisha maoni yao kwa ajili ya kuboresha Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1997 katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Umoja wa Machifu Tanzania uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro,kushoto kwake ni Mlezi wa Umoja wa Machifu Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela,na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bi.Lilian Beleko kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.

…………………

Na Anitha Jonas – WHUSM- Marangu Kilimanjaro – Moshi

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe amewataka Maafisa Utamaduni Mkoa na Wilaya kuwahimiza wadau wa Sekta ya Utamaduni kuwasilisha maoni yao ndani ya miezi mitatu.

Mheshimiwa Mwakyembe ametoa kauli hiyo leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Saba wa Umoja wa Machifu nchini wenye lengo la kujadili namna ya kuhakikisha umoja huo unasajiliwa kisheria pamoja na kuzungumzia nini kifanyike kutokana na kuwepo na mmomonyoko wa maadili katika jamii kwa kiasi kikubwa.

“Serikali iko katika mchakato wa kufanya maboresho ya Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997 ambayo imeonekana kuwa na mapungufu kulingana na hali ilivyosasa,hivyo basi nitoe rai kwenu Machifu kama wadau wakuu wa Sekta ya Utamaduni kutoa maoni yenu kwa haraka kwani yatasaidia kwa asilimia kubwa kuongeza ubora katika sera hii tunayoboresha na hivyo basi hakikisheni mnawasilisha maoni yenu kwa Maafisa Utamaduni ndani ya miezi hiyo,”alisema Mhe.Dkt.Mwakyembe.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania Chifu Frank Marrialle alieleza kuwa umoja huo ulianza tangu mwaka 2014 na mpaka sasa unajumla ya wanachama 105 na kupitia umoja huo umekuwa ukisisitiza wajumbe wake kusimamia utunzaji mazingira pamoja usimamazi wa maadili katika jamii kwani machifu ndiyo mhimili wa kulinda utamaduni wa taifa.

“Mbali na Machifu hawa kujitahidi kupigania usimamizi wa maadili katika jamii zao wamekuwa wakikumbwa na changamoto nyingi kwani kwa baadhi ya maeneo wamekuwa wakitolewa maneno ya dharau na kejeli kwa kuwaelezwa kuwa utawala wao umepitwa na hauna maana kwa sasa ombi letu kwa serikali ni kuhakikisha kupitia maoni yetu tutakayowasilisha kwa ajili Sera hii ya Utamaduni inayofanyiwa marekebisho yatiliwe mkazo ili kuonyesha wa nguvu ya machifu kwa jamii,”alisema Marrialle.

Aidha,akiendelea kuzungumza Chifu Marialle alipongeza uongozi wa serikali ya awamu ya tano kwa kusimamia utunzaji wa rasilimali za nchi kwa kuhakikisha hakuna utoroshwaji unaofanyika kwa lengo la taifa kupata faida itakayosaidia kuleta maendeleo nchini.

Pamoja na hayo nae Chifu Nshoma Hawa wa Ukamba – Kahama alitoa ombi lake kwa serikali la kuomba kusaidiwa kutokana na ikulu yake kuvamiwa na wanasiasa na kugaiwa kwa wananchi kwa matumizi ya kilimo kinyume na utaratibu wa himaya hiyo kwani eneo hilo ndipo walipozikwa machifu wote wa ukoo huo.

Halikadhalika nae Mlezi Mteule wa Umoja wa Machifu Tanzania Mheshimiwa Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela alieleza kufurahishwa na uteuzi huo na kuahidi kushirikia na Machifu hao katika kuhakikisha Machifu hao wanafanikiwa kuleta maendeleo kwa taifa pamoja na kusimamia hali ya kupambana na mmomonyoko wa maadili uliyopo sasa kutokana na hali ya utandawazi.

JK AMUWAKILISHA JPM KWENYE SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS MPYA WA ZIMBABWE LEO

$
0
0
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa baada ya kuapishwa kwake jijini Harare, Zimbabwe leo. Dkt. Kikwete amehudhulia sherehe hiyo akiwa amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo aliambayana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Phillip Mangula pamoja na Mwenyekiti wa UDP, John Momose Cheyo.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mtendaji Mkuu wa SADC, Dkt. Stergomena L. Tax walipokutana kwenye sherehe za kuapishwa Rais mpya wa Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa zilizofanyika leo mjini Harare, Zimbabwe. Dkt. Kikwete amehudhulia sherehe hiyo akiwa amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo aliambayana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Phillip Mangula pamoja na Mwenyekiti wa UDP, John Momose Cheyo.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe, mjini Harare Zimbabwe, alikokwendwa kwa kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kwenye sherehe za kuapishwa Rais mpya wa Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa zilizofanyika leo mjini Harare, Zimbabwe.

Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) chajizatiti kukabiliana na Ebola

$
0
0
KITENGO cha Afya katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kimeweka udhibiti madhubuti wa kujikinga na usambazaji wa magonjwa ambukizi ukiwemo ugonjwa wa Ebola. Ugonjwa wa Ebola unaosambazwa kwa virusi vya Ebola, husababisha homa kali inayoweza kuambatana na kutokwa damu mdomoni, puani, masikioni, machoni na sehemu nyingine za wazi na unaenea kwa haraka. 

Hivi karibuni umetangazwa kutokea nchini Kongo na kusababisha vifo. Akizungumzia kuhusiana na mikakati hiyo ya kupambana na magonjwa ambukizi ukiwemo wa Ebola, Afisa Afya Mfawidhi wa JNIA, Dk. George Ndaki amesema wanatoa mafunzo kwa watumishi na wahusika wote wanaotumia kiwanja hicho katika kujikinga na magonjwa hayo. 

 “Sisi tumejiandaa vizuri na tumeshafanya jitihada zote tumeshatoa maelekezo, mafunzo na kamati mbalimbali za kiwanja zimejipanga kudhibiti magonjwa yote ya kuambukiza, ikiwemo sisi wenyewe kujikinga na kuwakinga na abiria wote wanaotoka katika nchi hatarishi”, amesema Dkt. Ndaki. 

 Aidha akizungumzia kuhusiana na utaratibu ambao Kiwanja kimeweka ili kuhakikisha abiria wenye maambukizi wanapokelewa kwa tahadhari, ambapo wanapowasili na ndege zinazotoka nje ya nchi zinazopakia abiria wanaosafiri kutoka katika nchi zinazoshirikiana na Kongo hutakiwa kusafisha mikono kwa dawa maalum mara waingiapo katika eneo la kuwasili. 

 Pia abiria hao wanapoingia katika lango la kuwasili la abiria kutoka nje ya nchi, kumekuwa na mashine maalum inaangalia joto la mwili na likizidi nyuzi joto 38 wanamtaka kutoa maelezo Zaidi ya afya yake.

 “Abiria wote wanapowasili hupita katika eneo maalum ambalo wote hutakiwa kuosha mikono, lakini pia kuna mashine ambazo zimewekwa ili kuweza kuwatambua abiria ambao wanawasili wakiwa na hali ya joto isiyokuwa ya kawaida mfano kuwa na joto la juu sana kuanzia 38oC, ukiachana na hilo kuna fomu maalum ambazo abiria wanapowasili hujaza na pia taarifa kutoka kwa rubani wa ndege kama kuna abiria ana maambukizi kwenye ndege. 

Baada ya kumtambua mgonjwa basi atapitishwa katika njia ya tofauti na abiria wengine na kupakiwa katika gari la wagonjwa na kupelekwa Temeke Hospital,” amesema Dk. Ndaki.  Naye Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha akitoa ufafanuzi juu taarifa za uwepo wa ugonjwa wa Ebola, ameeleza kuwa tayari JNIA wanazo taarifa za mlipuko wa ugonjwa huo na taratibu zote zimeshachukuliwa kwa kuwakagua abiria wanaotoka nje ya nchi. 

 “Kwanza kabisa kwa abiria wote ambao wanatokea katika nchi ambazo zinasadikika kuwa na maambukizi wanapowasili wanakuwa sanitized (wanaosha mikono na dawa maalum) ili wasiweze kuleta maambukizi ndani, lakini pia tuna thermo scanners (mashine ambazo zinaangalia hali ya joto la mtu) anapowasili ambapo tunapogundua mgonjwa anamatatizo tunapeleka isolation (Chumba cha wagonjwa wa kipekee) na baada ya hapo anapelekwa katika vyumba vya waonjwa waliotengwa katika hospitali ya Temeke” alibainisha Bw. Rwegasha. 

 Katika hatua nyingine Dk. Ndaki amesema mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote ambaye amebainika kuwa na ugonjwa wa Ebola kupitia JNIA. Dk Ndaki ametaja namna ya kujikinga na ugonjwa wa Ebola ni pamoja na kuepuka kugusa damu, machozi, jasho, matapishi, kamasi, mkojo au kinyesi cha mtu mwenye dalili za ugonjwa; pia mtu hatakiwi kugusa, kuosha au kuzika maiti ya aliyekufa kwa Ebola; pia usiguse au kula wanyama kama popo, sokwe au swala wa msituni. 

 Dalili za Ebola ni pamoja na homa kali, maumivu ya kichwa na misuli, mwili kulegea, kutapika, kuharisha, vipele ma kutokwa damu 
 “Natoa wito tu kwa wananchi kuhakikisha wanafuata taratibu zote tulizoziweka ili kuhakikisha kwamba hatupati mgonjwa yeyote katika nchi yetu. 

Kama kila mtu atatekeleza wajibu wake kwa abiria kufuata taratibu, wanaosimamia masuala ya afya wakitimiza wajibu wao, na Kiwanja kikitimiza wajibu wake basi hakika magonjwa ya mlipuko hayataweza kufika katika nchi yetu” alieleza Dkt. Ndaki.
 Mlango wa kuingilia abiria kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wanaotoka nje ya nchi ambao baadhi ya ndege zimelengwa kutokana na abiria wake aidha kupita au kuanzia safari kwenye nchi ya Kongo iliyotangazwa kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola.
 Eneo maalum la ukaguzi wa afya kwa abiria mara baada ya kuingia kwenye sehemu ya wanaowasili kutoka nje ya nchi, ambapo kumefungwa mashine maalum zenye kuonesha joto la mwili na likizidi 38 abiria huyo hufanyiwa mahojiano ya afya yake, kwa kuwa moja ya dalili za ugonjwa wa Ebola ni kuwa na joto kali.

 Mmoja wa abiria aliyewasili na ndege ya Rwanda Air kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akinawa mikono kwa dawa maalum inayoua vijidudu vya maradhi mbalimbali yanayoambukiza, ukiwemo Ebola uliotangazwa hivi karibuni umeibuka nchini Kongo.
 Afisa Afya Mfawidhi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Dkt. George Ndaki akionesha mashine maalum inayompima abiria (thermo scanners) mara anapopita eneo la ukaguzi wa afya, ambapo linakuwa likisomwa na Afisa Afya kwenye komputa iliyopo (kulia). JNIA wamejidhatiti na makonjwa ya milipuko ukiwemo wa ebola uliotangazwa kuwepo nchini Kongo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha (kulia) akizungumza na waandishi wa habari juu ya udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kwenye kiwanja hicho. Hivi karibuni ugonjwa wa Ebola umetangazwa kutokea nchini Kongo.
Bango linalotoa maelezo yanayohusiana na ugonjwa hatari wa Ebola likiwa eneo la wasafiri wanaowasili kutoka nje ya nchi kweney Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

MKOA WA MOROGORO WAJIPANGA KUONGEZA UZALISHAJI WA ZAO LA KOROSHO

$
0
0

KATIBU Tawala Msaidizi anayesimamia sekta ya uchumi na uzalishaji ofisi ya mkuu wa mkoa mkoa wa Morogoro Ernest Mkondo akizungumza kuhusiana na mpango wao wa kuongeza uzalishaji wa zao la Korosho wakati wa ziara ya viongozi wa bodi Korosho nchini ilipokutana na wakulima wa korosho wa wilaya za Morogoro, Ulanga, Malinyi, Kilosa, Mvomero, Gairo mkoani Morogoro na kutoa elimu namna bora ya wakulima wanaweza kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia kilimo bora
Afisa Kilimo wa Bodi ya Korosho Tanzania Frank Mfutakamba kulia akimsikiliza mmoja wa wakulima wa zao la Korosho mkoani Morogoro mara baada ya kuwatembelea wakulima na kutoa elimu namna bora ya wakulima wanaweza kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia kilimo bora

KATIBU Tawala Msaidizi anayesimamia sekta ya uchumi na uzalishaji ofisi ya mkuu wa mkoa mkoa wa Morogoro Ernest Mkondo kushoto akiagana na Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Tanzania Bryson Mshana mara baada ya kufanya mazungumzo naye

Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Tanzania Bryson Mshana kulia akisalimiana na wakulima wa zao la Korosho mkoani Morogoro mara baada ya kuwatembelea na kutoa elimu namna bora ya wakulima wanaweza kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia kilimo bora



NA MWANDISHI WETU, MOROGORO.

KATIBU Tawala Msaidizi anayesimamia sekta ya uchumi na uzalishaji ofisi ya mkuu wa mkoa mkoa wa Morogoro Ernest Mkondo amesema mkoa huo umejipanga kufanya uhamasishaji na ufuatiliaji wa zao la Korosho ili kuhakikisha uzalishaji unaongezeka kuliko iliyokuwa miaka iliyopita

Mkondo aliyasema hayo wakati wa bodi Korosho nchini ilipokutana na wakulima wa korosho wa wilaya za Morogoro, Ulanga, Malinyi, Kilosa, Mvomero, Gairo mkoani Morogoro na kutoa elimu namna bora ya wakulima wanaweza kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia kilimo bora

Ambapo alisema uhamasishaji huo utashirikishi wakuu wa wilaya na viongozi wengine wa ngazi za chini kwa lengo la kuhakakikisha kilimo hicho kinalimwa kwa tija kubwa ili kuweza kuwasaidia kuwainua wakulima kiuchumi..

Alisema licha ya kwamba wana wataalamu wana upungufu mkubwa wa wataalamu wa kilimo kwenye maeneo ya vijijini wakati wanawasubiri wanachofanya wamewagawa wa maeneo ya kata na Vijiji ili kuwasaidia kuongeza nguvu kutoa ushauri wa ugani kwa wakulima “Anasema

Aidha alisema hivi sasa wanawahimiza wataalamu waliopo ngazi za kata wafike kwenye maeneo ya vijiji kutoa ushauri hasa mashamba darasa hilo litasaidia kutoa elimu inayohusika kwenye mazao mbalimbali ikiwemo zao la korosho.

Mkondo alisema wanalifanya hilo kwa kushirikiana na bodi ya Korosho na maafisa ugani ambao hawajapata elimu juu ya uzalishaji huo wanaitwa na kupewa elimu juu ya zao husika ili waweze kujua namna ya kuwaelimisha wakulima.

Akizungumzia suala la malipo yanayofanywa na bodi ya korosho alisema licha ya kuwepo kwa changamoto lakini wamehaidi kuanza kuyashughulikia kwa kuanza kufanya uhakiki ili waweze kujua vikundi vipi vimezalisha na baadae waweze kulipwa malipo halali.

“Lakini kama uhakiki umekwisha kufanyika bodi ya korosho na umekamilika malipo yafanyike kwa wakati ili vikundi viweze kulipwa kwa haraka huku akisisitiza kwamba pembejeo zinasambazwa na serikali kupitia bodi ya Korosho hivyo wakulima wafuatwe taratibu zilizopo waweze kupata pembejeo hizo”Anasema

Aliongeza kuwa mwaka jana mkoa huo uliweza kustawisha vitalu 36 vya korosho ambavyo walipata miche 702,000 ilioteshwa na vikundi mbalimbali vilivyopata msaada kutoka bodi ya Korosho lakini waliweza kupata mbegu za kupanda kilo 4154.

Alisema baada ya kupata mbegu hizo waliweza kusambazwa na kupandwa na wakulima kutokana na uhamasishaji katika mkoa kuwa mkubwa zaidi kama kutokana na wananchi kuitikia mwitikio mzuri wa kuweza kulima zao hilo.

VIFUNGASHIO VYA KISASA VYA BLISTA VYARAHISISHA KAZI UGAWAJI DAWA KWA WAGONJWA

$
0
0

Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kata ya Nyakabonga katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Fausta Rugalinda, akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu upatikanaji wa dawa katika zahanati hiyo pamoja na vifungashio vya dawa.
Mkazi wa Kata ya Nyakabonga, Agnes Mganga, akiishukuru Serikali kwa kuwapelekea dawa katika zahanati hiyo.
Wananchi wa Kata ya Nyakabonga wakiwa wamesimama jirani ya kibao cha zahanati
Ofisa Mauzo wa MSD Kanda ya Mwanza, Conoria Godfrey (kulia), akimuelekeza jambo Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo,Fausta Rugalinda wakati alipokuwa akikagua dawa zilizohifadhiwa kwenye stoo ya zahanati hiyo.











Na Dotto Mwaibale, Muleba

WATENDAJI wa Vituo vya kutolea huduma za afya wilayani Muleba mkoani Kagera wamesema vifungashio vya dawa za serikali viliboreshwa kutoka kwenye makopo kwenda kwenye Blister pack vina uhakika wa kubakiza dawa katika ubora unaohitajika pamoja na kurahisisha kugawa dawa kwa wagonjwa.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti mkoani Kagera, watendaji hao wamesema hata kwa upande wa watumiaji ambao ni wagonjwa vifungashio vya blister hata wakiangusha ama bahati mbaya zikamwagikiwa na maji hazitaathiriwa wala kupoteza ubora wake.

"Kupima dawa kwa kijiko kwa ajili ya kuziweka kwenye bahasha wakati wa kuwahudumia wagonjwa kulituchukulia muda sana na mara nyingine unakuta kopo linakaa wazi hadi msururu mzima unaohitaji aina hiyo ya dawa uishe"

Kwa upande mwingine wananchi wa Kata ya Nyakabango wilayani Muleba mkoani Kagera wameipongeza serikali kwa kufanikisha kuwapelekea dawa kwa wakati kupitia Bohari ya Dawa (MSD).
Julius Kamuhaba alisema hivi sasa hali ya upatikanaji wa dawa katika zahanati hiyo ni nzuri na hakuna mtu atakayekwenda kupata matibabu akatoa malalamiko ya kukosa dawa.

"Naipongeza serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa jitihada inayoifanya ya kuhakikisha wananchi wake tunapatiwa dawa kwa wakati kupitia MSD" alisema Agnes Mganga mkazi wa kata hiyo.

Alisema kila anapokwenda kupata matibabu katika Zahanati ya Nyakabango amekuwa akipata dawa tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo walikuwa wakiandikiwa kwenda kuzinunua.

Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Fausta Rugalinda alisema kuwepo kwa mawasiliano mazuri na ushirikiano baina ya MSD na watendaji wa sekta ya afya wilayani humo ni moja ya sababu kubwa ya kupatikana kwa dawa kwa wakati katika vituo vya afya na zahanati.

"Tunaomba dawa kila baada ya miezi mitatu na dawa zinapokuwa zimepungua katika stoo yetu tunapopeleka maombi ya dharula wahusika wamekuwa wakiwasiliana na dawa kuletewa kwa wakati na MSD" alisema Rugalinda.

Rugalinda aliongeza kuwa mara ya mwisho kupata dawa walizoomba MSD katika mwaka huu wa fedha 2017/2018 ilikuwa ni Julai 24 na kwamba maombi mengine wanatarajia kuyafanya mwezi ujao na kuwa bado wana dawa za kutosha.

HATUTARUDIA MAKOSA SIMBA MJIANDAE-MBEYA CITY

$
0
0
Na Agness Francis,blogu ya Jamii.

Kikosi cha Mbeya city chatamba kufanya vizuri katika mchezo wao dhidi ya mnyama Simba sc hapo kesho katika muendelezo wa michuano ya Ligi kuu Tanzania bara.

Mpambano huo utakao tifulia katika dimba la Uwanja wa Taifa huku Mbeya city wakiwa wageni wa mchezo huo.Mechi ya kwanza Mbeya city ilipata kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa wana lamba lamba Azam fc katika dimba la Azam complex Chamazi,ambapo simba alishinda 1-0 dhidi ya Prisons.

Lakini katika kuelekea mtanange huo dhidi ya mabingwa watetezi Simba,kikosi cha Mbeya city imejihakikishia kutorudia makosa waliyoyafanya katika mchezo uliopita 

"Kambi ipo salama vijana wanajituma kwa kuwa tunajua tumekosea wapi tunafanyia kazi makosa tunarekebisha pale tulipokosea ili tuweze kufanya vizuri gemu inakuja dhidi ya Simba,hatuturudia tena makosa tuliyoyafanya"amesema kocha msaidizi Josiah Steven. 

Meneja wa Mbeya city Deo Julias amesema vijana wanamorali ya kufanya vizuri kuhakikisha wanapata ushindi na kurudi nyumbani wakiwa na pointi 3.
Kikosi cha Mbeya City.

MCHENGA BBALL STARS WAUNYAKUA TENA UBINGWA WA SPRITE BBALL KINGS 2018

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mchenga Bball Stars imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa Sprite Bball Kings kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanikiwa kuwafunga wapinzani wake Flying Dribbllers kwa pointi 87 dhidi ya 76 kwenye mchezo wa game 3 ya 'best of five' za fainali uliochezwa mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa ndani wa taifa.

Mechi hiyo iliyoanza kwa kasi kwa pande zote, Mchenga alifanikiwa kushinda katika quarter zote nne na kuzidi kuonesha ubabe kwa timu zingine kwenye michuano ya Sprite BBall Kings.

Mchenga wamefanikiwa kuchukua ubingwa huo kwa kushinda game zote tatu mfululizo yaani (Swipe) kati ya tano za fainali hivyo kuwanyima furaha wapinzani wao Flying Dribbllers kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuwafunga kwa aina hii hii kwenye nusu fainali ya michuano hiyo mwaka 2017.

Katika game 1 Mchenga walishinda kwa pointi 103 dhidi ya 73 za Flying Dribblers, kabla ya kushinda kwa pointi 85 kwa 65 kwenye game 2 na leo kumalizia kazi kwa ushindi wa pointi 87 kwa 76.Katika ushindi huo wa Mchenga Bball Stars mchezaji Baraka Sadick amekuwa na msaada mkubwa hali ambayo imepelekea kuibuka kama 'Most Valuable Player' wa mashindano kwa mwaka 2018.

Baraka amefunga pointi 239 katika michezo 8 aliyocheza. Katika michezo hiyo amekuwa na wastani wa kufunga pointi 30 katika kila mchezo. Katika mchezo wa leo Baraka amefunga pointi 33 kati ya 87 za timu yake.ainali hiyo ya aina yake iliweza kushuhudiwa na Rais wa Shirikisho la Kikapu (TBF) Phares Magesa akiwa na viongozi wengine na kujionea michuano hiyo ilivyokuwa na ushawishi mkubwa kwa vijana wa kitanzania.

Timu zote zimekabidhiwa zawadi zao na Rais wa TBF Phares Magesa akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa TBF Mike Mwita ambazo ni shilingi milioni 3 kwa mshindi wa pili Flying Dribbllers, milioni mbili na tuzo kwa 'MVP' ambaye ni Baraka Sadick na milioni 10 kwa mabingwa ambao ni Mchenga Bball Stars. Sprite Bball Kings inaandaliwa na East Afarica Television chini ya udhamini wa kinywaji baridi cha Sprite.

Michuano hiyo ilianza rasmi mwaka 2017 kukiwa na timu 54 na Mchenga Bball Stars kufanikiwa kuchukua ubingwa huo kwa mara ya kwanza , msimu wa pili ulioanza mwezi June uliweza kuzikutanisha timu 51 zilizoanzia hatua ya mtoano na fainali kufanikiwa kuingia kwa timu mbili na Mchenga kutetea ubingwa wake tena.


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) Phares Magesa akimkabiidhi kombe Nahodha wa timu ya Mchenga BBall Stars Mohamed Yusuph sambamba na hundi ya Milioni 10 baada ya kunyakua ubingwa wa pili mfululizo wa Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 yaliyofanyika katika Uwanja wa Ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam
Mchezaji Baraka Sadick (aliyebebwa) akishangilia pamoja na wenzake baada ya kutangazwa kuwa mchezaji bora wa michuano hiyo ya Sprite BBall Kings 2018 (MVP) na kujinyakulia kikombe pamoja na hundi ya Milioni 2.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini (TBF) Phares Magesa akimkabidhi Kikombe na hundi ya milioni 2 mchezaji bora wa mashindano ya Sprite BBall Kings 2018 (MVP) Baraka Sadick kutokea Mchenga BBall Stars katika fainali iliyofanyika Uwanja wa Ndani wa Taifa

DC MURO AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mh.Jerry Muro amefanya ziara ya kushtukiza katika baranara ya mchepuko Arusha Bypass katika eneo la muungano Makumira na kubaini uwepo wavitendo vinavyoashiria ukiukwaji wa taratibu za kazi na haswa katika kazi zinazofanywa na RAIA kutoka nje.

Mh Muro Pamoja nakuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo itakayosaidaia kupunguza msongamao wa magari kuelekea Jijini Arusha ameonyeshwa kukerwa na tabia ya baadhi ya wageni kufanya kazi zinazoweza kufanywa na watanzania jambo linaloendela kuminya fursa ya vijana wa kitanzaia kupata ajira.
Kutoka na sababu hiyo Dc Muro alilazimika kuchukua hatua ya kuwaagiza maofisa wa Uhamiaji kufuatilia suala hilo jambo lililopelekea kubainika uwepo wa RAIA Tisa ( 9 ) wa kigeni wanaofanya kazi hizo pasipo kuwepo na baadhi ya vibali husika vya kufanya kazi.

Katika ziara hiyo Dc Muro aliambatana na Naibu katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote ambao ni waratibu wa ujenzi wa Barabara hiyo.
Dc muro anaendelea na zoezi la ukaguzi wa miradi mbalimbali ya ujenzi katikaa wilaya ya Arumeru yenye kata 53 na Halmashauri mbili za Arusha Dc na Meru Dc

baadhi ya viongozi wa Chadema Mkoa wa Mbeya na wananchi waendelea kujitokeza Nyumbani kwa Mama yake mzazi mh Sugu

$
0
0
Kufuatia Msiba wa Mama wa Mbunge wa Mbeya mjini  Joseph Mbilinyi (Sugu) baadhi ya viongozi wa Chadema Mkoa wa Mbeya na wananchi wameendelea kujitokeza Nyumbani  Sae kwa Mbilinyi,Mama wa Mh Sugu kwa ajili kutoa Pole .

Bado Mpaka sasa taarifa kutoka kwa familia juu ya wapi Mama wa Mbunge atazikwa haijawekwa hadharani, kwani bado inaelezwa kuwa huenda Mama akasafirishwa Songea au Mbeya kwa ajili ya mazishi .

Mama mzazi wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu (Chadema), amefariki dunia leo Jumapili Agosti 26, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), alikokuwa akipatiwa matibabu.
 Baadhi ya viongozi wa Chadema Mkoa wa Mbeya na wananchi wameendelea kujitokeza Nyumbani  Sae, kwa Mbunge wa Mbeya mjini Mh Joseph Mbilinyi,kufuatia kifo cha Mama yake mzazi mbunge huyo kwa ajili ya kutoa pole na kufahamu ratiba za msiba huo.
 Baadhi ya viongozi wa Chadema Mkoa wa Mbeya na wananchi wengine wakijadaliana jambo Nyumbani  Sae,jijini Mbeya amapo ndio nyumbani  kwa Mama mzazi wa Mh Joseph Mbilinyi
 

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMATATU AGOSTI 27,2018

Jukumu la kuendeleza Sanaa Nchini ni la Serikali ,Wadau wa Sanaa na Wananchi

$
0
0
Na Lorietha Laurence-WHUSM,Shinyanga.

Jukumu la kuendeleza sekta ya sanaa nchini ni la Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sanaa na wanachi ambao wako mstari wa mbele kuhakikisha sekta hiyo inaleta manufaa ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Leah Kihimbi kwa niaba ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza katika halfa ya ufunguzi wa filamu ya Ruanda Mkoani Shinyanga.

Leah Kihimbi anaeleza kuwa Serikali kwa kuona umuhimu wa sekta ya sanaa nchini imeandaa Sera ya Maendeleo ya Sanaa itakayotoa muongozo kwa taifa kuhusu masuala yote ya sekta hiyo ikiwemo hakimiliki, urasimishaji wa kazi za sanaa na uendelezaji wa sekta hiyo nchini.

“Sera hii itakuwa dira na muongozo wa kazi zote za sanaa, hivyo kuwanufaisha wasanii pamoja na nchi” amesema Leah Kihimbi.

Aidha Leah Kihimbi amewapongeza wasanii kikundi cha Viwawada kwa kutoa filamu nzuri ya Ruanda ambayo inapinga na kukemea mimba na ndoa za utotoni, mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) na watu wenye umri mkubwa (Vikongwe).

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Leah Kihimbi akizungumza na wadau wa sanaa (hawapo katika picha) alipokuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Naibu Waziri wa Wizara hiyo katika halfa ya ufunguzi wa filamu ya Ruanda,jana Mkoani Shinyanga.

Afisa Utamaduni Mkoa wa Shinyanga Bi. Mariam Ally akiongea katika hafla ya ufunguzi wa filamu ya Ruanda iliyoigizwa na wasanii wa Viwawada wa Mkoa huo yenye maudhui ya kukemea na kupinga mimba na ndoa za utotoni,  mauji ya watu wenye ulemevu wa ngozi (Albino) pamoja na watu wenye umri mkubwa (Vikongwe), jana Mkoani Shinyanga.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Leah Kihimbi (kushoto) akipokea risala kutoka kwa Bi. Elizabeth Vedastus (kulia) wakati ya halfa ya ufunguzi wa filamu ya Ruanda jana Mkoani Shinyanga.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Leah Kihimbi (kushoto) akisaidiana na Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Mariam Ally kufungua boski lilikuwa limewekwa CD ya filamu ya Ruanda ikiwa ni ishara ya kuizindua, jana Mkoani Shinyanga.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Leah Kihimbi akionyesha CD ya filamu ya Ruanda baada ya kuifungua rasmi wakati wa hafla hiyo jana Mkoani Shinyanga
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Leah Kihimbi (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na waigizaji wa filamu ya Ruanda mara baada ya kuifungua hapo jana Mkoani Shinyanga.(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Shinyanga)


WAZIRI LUGOLA AITAKA POLISI, MAGEREZA KUWAONDOA WANANCHI WALIOVAMIA MAENEO YA JESHI NCHINI

$
0
0

Na Felix Mwagara, MOHA-Lindi 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake kuwaondoa mara moja wananchi wote waliovamia katika maeneo ya majeshi nchini. 

Lugola alisema hayo baada ya kulikagua Gereza jipya la Wilaya ya Ruangwa linalojengwa ambalo lina ekari 100 lakini ekari 20 limevamiwa kwa kujengwa kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti, ufuta na korosho katika eneo hilo la Jeshi la Magereza. 

Akizungumza baada ya kulikagua Gereza hilo, mjini Ruangwa leo, Lugola alisema kuanzia sasa viongozi wa vyombo vyake wahakikishe hawaruhusu mwananchi yeyote kuingia katika maeneo ya jeshi na atakua mkali kulifuatilia suala hilo. 

Lugola ambaye pia aliikataa kuipokea taarifa ya ujenzi wa gereza hilo ambayo ilikua inasomwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi, Rajabu Nyange, alisema taarifa hiyo ina upungufu mkubwa na hawezi kuipokea licha ya kua imeeleza kuhusu ardhi ya jeshi hilo kuvamiwa. 

“Mimi huwa nashangaa sana inakuaje wananchi wanavamia ardhi ya jeshi tena bila woga, halafu jeshi linakaa kimya linabaki kunung’unika, hii haijakaa sawa kabisa na kamwe sikubaliani nalo,” alisema Lugola. 

Lugola aliongeza kua, “uvamizi wa ardhi mara nyingi unakua kwa jeshi la polisi na magereza, mbona Jeshi la Wananchi silisikii hili, kwanini nyie mnakaa kimya wananchi wakivamia ardhi yenu, sasa nawataka muhakikishe ardhi ya jeshi popote nchini iliyoporwa inarudishwa ndani ya jeshi, na wote waliovmia waondooeni haraka iwezekanavyo.” 

Kwa upande wake Mkuu wa Magereza mkoani humo, alisema licha ya ujenzi wa gereza hilo kuendelea kujengwa lakini ekari 20 ilichukuliwa kimakosa na kujengwa kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti na ufuta pamoja na kubangua korosho vinavyomilikiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa. 

“Jitihada za ufuatiliaji urejeshaji wa eneo hilo zimefanyika ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri hii ameonyesha nia ya kurejeshwa eneo hlo,” alisema Bakari. 

Aliongeza kuwa, ujenzi wa gereza hilo ambalo linatarajiwa kukamilika Septemba mwaka huu, unatarajiwa kumaliza msongamano wa wafungwa na mahabusu kwenye Gereza la Wilaya ya Nachingwea kutokana na mahabusu wengi kutoka Ruangwa. 

Waziri Lugola alifanya ziara ya dharura katika mikoa hiyo, pia aliambatana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu kwa kufanya ziara ya kutembelea Jengo lililokwama ujenzi la uhamiaji Mkoa wa Mtwara na Lindi na pia kulitembelea Gereza la mahabusu na wafungwa linalojengwa mjini Ruangwa, mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kubaini mapungufu ya ujenzi wa majengo hayo.

TBL YAANIKA MAFANIKIO YAKE KWENYE MKUTANO WA MWAKA WA WANAHISA

$
0
0
Mkutano wa mwaka wa 45 wa wanahisa wa kampuni ya TBL Group umefanyika jijini Dar es Salaam ambapo licha ya changamoto mbalimbali za kibiashara,kampuni imeweza kuendelea kufanya vizuri na inaendelea kufanikisha mikakati ya kuifanya biashara yake kuimarika zaidi,kuwa endelevu na kunufaisha jamii.

 Kutokana na mafanikio hayo kampuni imetoa gawio la hisa kiasi cha shilingi 770/-kwa kila hisa kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa kampuni uliomalizika ikiwa ni ongezeko la asilimia 28% kulinganisha na gawio la shilingi 600/-lililotolewa katika mwaka wa 2016. 

Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group,Roberto Jarrin, ambaye pia ni Rais wa kitengo cha Masoko cha kampuni mama ya ABInBev kanda ya Afrika Mashariki alisema mafanikio makubwa ya kampuni yametokana na mkakati wa kuimarisha masoko hususani kwa kuwekeza katika uzalishaji wa bidhaa ambazo wananchi wengi wanamudu kuzitumia. 

Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group , Roberto Jarrin (wa pili kushoto) akiongea wakati wa Mkutano Mkuu wa 45 wa Mwaka 2018 wa Wanahisa wa Tanzania Breweries Ltd (TBL Group) wa kujadili maswala mbalimbali ya Kampuni uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Convention Cetre Dar es Salaam, wengine kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa TBL Bruno Zambrano, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi , Cleopa Msuya, Katibu wa Kampuni Huruma Ntahena na Mjumbe wa Bodi hiyo Leonard Mususa. Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group , Roberto Jarrin (wa pili kushoto) akiongea wakati wa Mkutano Mkuu wa 45 wa Mwaka 2018 wa Wanahisa wa Tanzania Breweries Ltd (TBL Group) wa kujadili maswala mbalimbali ya Kampuni uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Convention Cetre Dar es Salaam, wengine kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa TBL Bruno Zambrano, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi , Cleopa Msuya, Katibu wa Kampuni Huruma Ntahena na Mjumbe wa Bodi hiyo Leonard Mususa.  Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Tanzania Breweries Ltd (TBL GROUP) Cleopa Msuya wa (katikati) akiongea wakati wa Mkutano Mkuu wa 45 wa Mwaka 2018 wa Wanahisa wa Kampuni hiyo .
Baadhi ya wanahisa waliohudhuria mkutano wakitoa michango yao ya mawazo Baadji ya wanahisa wa TBL waliohudhuria mkutano huo katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa kampuni.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images