Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1659 | 1660 | (Page 1661) | 1662 | 1663 | .... | 1898 | newer

  0 0

   
  Mhe. Mwanasha Tumbo(wakatikati) akishuhudia tukio la kusaini mkataba wa makabidhiano ya kituo cha polisi kati ya Mwenyekiti wa bodi la bonde la mto Pangani Ndugu Segule Segule na Kaimu Kamanda Mkuu wa Polisi Tanga Ndugu Lissu Jingi

  Picha ya pamoja.

  Bodi ya maji mto pangani yajenga kituo cha polisi katika kitongoji cha Kwelusanga kijiji cha Sakale kata ya Mbomole baada ya changamoto za uchimbaji madini kukithiri katika chanzo cha maji cha mto Zigi na katika hifadhi za mazingira.

  Akisoma taarifa ya Ujenzi wa kituo cha polisi Agosti 21, 2018 Bi Arafa Magidi kaimu Afisa bonde la Pangani, amesema bodi ya maji bonde la mto Pangani limejenga kituo hicho kupitia mkandarasi Kumba Quality Contractors kwa gharama ya Tsh. 76,088,000/= (Milioni sabini na sita na elfu themanini na nane tu.) ambazo ni mchango wa pamoja wa Serikali ya Tanzania na wadau wa maendeleo.

  Ameongeza kuwa kituo hiki kina vyumba viwili vya mahabusu, mahabusu ya wanaume na mahabusu ya wanawake, ofisi ya polisi, maliwato mbili (vyoo), na sehemu ya kupokelea malalamiko.

  Akikabidhiwa kituo hicho Mkuu wa Wilaya muheza Mhe. Mhandisi Mwanasha Tumbo amesema, Kituo hiki kitawasaidia wananchi wa Sakale kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kwa raia na mali zao, pia kuwasogezea huduma wananchi karibu kwani kituo cha awali kipo mbali sana na kijiji chao.

  Pia aliwahasa wananchi wa Sakale kuendelea kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji kwa kuhakikisha hakuna uchimbaji wa madini utakao endelea katika kijiji hicho. “Kila mmoja awe mlinzi wa mwenzie, tuendelee kuwaondoa watu wanaoharibu mazingira” Alisema Tumbo.

  Nae Kaimu Kamanda Mkuu wa Polisi Ndugu Lissu Jingi aliwashukuru wananchi na Serikali kwa ujumla kwa kujenga kituo cha polisi kwani anaamini ulinzi na usalama utaimarika sanjari na hayo aliomba kituo hicho kijengewe ghala (Amari ya kuhifadhia silaha), nyumba za kulala watumishi na huduma za kijamii ili ziweze kuwavutia watumishi watakaoletwa katika kituo hicho. Alisisitiza kuwa kazi ya ulinzi na usalama si kazi ya jeshi la polisi tu bali ni kazi ya kila mtu katika jamii kulingana na katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

  “Jukumu la ulinzi na usalama ni jukumu letu sote kulingana na katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania” Alisema Lissu 

  0 0

  *Wamo wakuu wa wilaya,mikoa na mawaziri,awataka waheshimu mamlaka nyingine
  *Aahidi kuandika barua kwa Kamishna wa TRA,aeleze namna wanavyowatafuta wawekezaji

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  MGURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Geoffrey Mwambe amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwamo baadhi ya wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa na mawaziri kuacha kutoa matamko na maagizo kwa wawekezaji nchini.

  Amesema ni vema kila mamlaka ikatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kufafanua iwapo kuna tatizo lolote likiwemo la kodi,vibali au bora wa bidhaa kwa muwekezaji yoyote kuna haja ya kufuata taratibu wa kutafuta ufumbuzi kupitia mamlaka husika badala ya kutolewa maagizo ambayo hazingatii sheria.

  Mwambe amesema hayo leo jijini Dar es Saalam wakati anazungumzia ziara ambayo TIC pamoja na wadau wanaohusika na sekta ya uzalishaji dawa na vifaa tiba nchini ambayo waliifanya Korea Kusini na China, ushiriki wao katika Maonesho ya Nanenane pamoja na kueleza majukumu yao ya kuelimisha umma na  kuhamasisha uwekezaji.

  Hivyo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa  kuna wimbi la viongozi  kutoa maagizo na matamko na hasa yanayohusiana na masuala ya kikodi,vibali na mambo mengine.Amesema kwamba TIC  wanafanya kazi kubwa na ngumu ya kuhamasisha wawekezaji na mitaji kuja nchini na wanatumia gharama katika kufanikisha

  "Kama kuna muwekezaji yoyote ana tatizo lolote wa kufahamishwa ni kituo cha wawekezaji.Ni jambo la kushangaza Mkuu wa Wilaya anatoa makadirio ya kodi, anatoa siku mbili kodi ilipwe wakati sheria haiko hivyo.

  " Unapozungumzia suala la kodi kuna utaratibu wake na sheria zake,hivyo iwapo kuna tatizo la kikodi kwa muwekezaji kiongozi wasiliana na mamlaka husika watatafuta ufumbuzi wake."Kama ni suala la vibali wapo wanaohusika na vibali kwa ajili ya wawekezaji,hivyo fuata utaratibu badala ya kutoa maagizo wakati huna mamlaka ya kufanya hivyo," amesema.

  Ameongeza kwamba viongozi wote jukumu lao ni kutoa taarifa kwa mamlaka husika na si kutoa maagizo na miongozo bila kufuata taratibu.Ametoa mwito kwa viongozi wote kushirikiana na TIC katika kuhakikisha wanaendelea kuweka uaminifu kwa wawekezaji ili kifikia uchumi wakati.Pia ameomba ngazi zote za kimamlaka kila mmoja kusimama katika mipaka yake kwani kila mmoja yupo kisheria na sababu za kueleza hayo ni kukumbusha wajibu wa kila taasisi kutekeleza majukumu yake bila kuingia mipaka ya mwingine.

  Mwambe ameeleza pia atamuandikia barua Kamisha wa TRA kumueleza umuhimu wa maofisa wake wa kodi kukusanya kodi kwa wawekezaji badala ya kumuacha muwekezaji anakaa miaka saba bila kulipa kodi."Kuna taarifa ya hivi karibuni muwekezaji amekaa miaka saba hakudaiwa kodi,anakuja mwingine mpya ndio anadaiwa na ile kodi ya miaka ya nyuma.Huu ni uzembe.

  "Kwanini  miaka yote ofisa wa TRA hawezi kwenda kukusanya kodi?Huo ni uzembe, nitahakikisha nasimamia hili kwa kuzungumza na Kamishna wa kodi," amefafanua.Mwambe na kusisitiza lazima TRA wakusanye kodi.

  Kuhusu ziara ya Korea Kusini na China,amesema Agosti 10 had I 18 mwaka huu aliongoza ujumbe wa wadau wanaohusika na dawa na vifaa tiba wakiwamo Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA)pamoja na Chama cha wenye viwanda vya dawa za binadamu na vifaa tiba.Mwambe amesema Agosti 13 wakiwa Korea Kusini walifanya kongamano ambalo lilihusisha zaidi ya kampuni 100 wanaohusika kwenye eneo na pia wanafanya kongamano China.

  Amesema matokeo ya ziara hiyo kuna kampuni tano ambazo zinahusika na uzalishaji dawa na vifaa tiba watakuja nchini Septemba mwaka huu kwa ajili ya mazungumzo kwani wanataka kuwekeza hapa nchini.Akizungumzia ushiriki wa maonesho ya Nane nane amesema wanazokanda saba na zote zimeshiriki kikamilifu katika maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kwa watanzania.Amesema wamefanikiwa kushika nafasi ya pili katika ubora wa utoaji huduma na hasa katika kuwafikia wananchi na katika maonesho hayo waliwatembelea wajasiriamali waliokuwa kwenye mabanda mbalimbali kutoa elimu.

  Kuhusu utendaji kazi wa pamoja ambapo TIC kuna kitengo maalum ambacho kinahusisha taasisi mbalimbali kwa lengo la kurahisisha utoaji huduma kwa wawekezaji kwa haraka.Amesema kutokana na uwepo wa kitengo hicho wamekubaliana na NIDA nao wawepo ndani ya kituo hicho na tayari maofisa wawili wa NIDA wamewasili hapo.

   Hivyo amesema wawekezaji wote wanaohitaji vibali vya NIDA watavipata TIC.Pia ameelezea umuhimu wa kuwawezesha wajasiriamali waliopp nchini kwani ndio muhimili wa maendeleo ya nchi.Amesema nchi nyingi ambazo zimefanikiwa ni kwasababu ya wajasiriamali na kwamba TIC wanataka kuona  wajasiriamali wanashiriki katika shughuli mbalimbali baada ya wawekezaji kuingia.

  Amefafanua kwa mtazamo wake haoni sababu ya Dangote kuingiza magari 600 kwa ajili ya kubeba saruji, kwani hilo lilipaswa kufanywa na watanzania.Ameongeza haiwezekani Dangote ahangaike kuzalisha saruji na wakati huo huo anahangaika na kusafirisha saruji.Amesema jukumu  muwekezaji baada ya kuzalisha kazi inayofuata ni watanzania kuchangia fursa hizo.

  "Malengo ya Rais ni kuona Watanzania wanafanikiwa na ndicho ambacho hata TIC nasi tunakisimamia," amesema.


  Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw.
  Geoffrey Mwambe akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar es salaam leo wakati alipozungumzia kuhusu Viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo wakuu wa wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa mikoa na Mawaziri wanaotoa matamko kuhusu wawekezaji hapa nchini.
  Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw.
  Geoffrey Mwambe akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar es salaam leo. Alipozungumzia kuhusu Viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa mikoa na Mawaziri wanaotoa matamko kuhusu wawekezaji hapa nchini.

  Waandishi wa habari na wakuu wa vitengo mbalimbali kutoka kituo cha Uwekezaji TIC wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kituo cha hicho Bw.
  Geoffrey Mwambe akizungumza leo

  0 0  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

  MKUU wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Mfaume ametoa ombi kwa wawekezaji kuwekeza kwa kujenga kiwanda ambacho kitaisaidia kuongeza thamani ya zao la Soya ambalo linalimwa kwa wingi wilayani hapo.

  Mfaume ametoa ombi hilo leo wakati anazungumzia jitihada zinazofanywa na wakulima wa Wilaya ya Namtumbo na hasa katika zao la Soya.

  Amesema ombi kubwa ni kupata kiwanda cha Soya ndani ya Wilaya ya Namtumbo kwani kitakapojengwa kitasaidia kuongeza thamani ya zao la Soya."Tunaomba muwekezaji iwe anatoka Marekani au Taifa lolote aje awekeze kwa kujenga kiwanda cha kuchakata Soya kwa lengo la kuongeza thamani ya zao hili.

  " Kwa mwaka huu wakulima wamepata tani 50,000 za Soya na kukiwa na kiwanda ambacho kitasaidia kuongeza thamani wanaweza kuzalisha zaidi ya tani za mwaka huu,"amesema.

  Mfaume amesema kuwa mbali ya kuomba kiwanda kwa ajili ya kuongeza thamani ya zao la Soya ,pia ombi lao lingine ni kiwanda cha mbolea.Amefafanua changamoto waliyonayo wakulima ni mbolea na hivyo kukiwa na kiwanda katika wilaya hiyo watakuwa na uhakika wa mbolea na hivyo kuongeza uzalishaji.

  Awali wakati anazungumzia zao la Soya amesema wakulima wengi wanalitumia zao hilo kwa chakula na chakuka cha wanyama.Amefafanua kuwa Soya inaweza kuzalisha maziwa,Soseji na nyama lakini hiyo ili ifanyike kunahitajika kiwanda cha kuchakata Soya.

  0 0

  Na Veronica Kazimoto-Tabora

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataja walengwa wanaostahili kuomba msamaha maalum wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi kwa asilimia 100 ambapo mwisho wa kutuma maombi ya msamaha huo ni tarehe 30 Novemba, 2018. 

  Akizungumza wakati wa mkutano wa washauri wa walipakodi (Tax consultants) mkoani Tabora, Afisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo Rose Mahendeka amesema Walengwa wa msamaha huu ni makampuni, taasisi na watu binafsi ambao wamewasilisha ritani za kodi lakini bado wanadaiwa kodi yote au sehemu ya kodi zitokanazo na ritani hizo.

  "Walengwa wengine ni wale wote ambao hawajawasilisha ritani za kodi, hawajasajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) au Namba ya Usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na wale walio wasilisha pingamizi au rufaa za kodi ambazo bado zinashughulikiwa katika ofisi za TRA, Bodi ya Rufaa na Mahakama ya Rufani za kodi", alisema Mahendeka.

  Aidha, amewataja wasiohusika na msamaha huu kuwa ni pamoja na wale ambao wangestahili kupata msamaha lakini tayari wameshalipa madeni yao, ambao masuala yao ya kikodi yapo katika hatua ya ukaguzi au uchunguzi, wana madeni ya nyuma ya kodi ambayo yanatokana na kesi za jinai za kodi, utakatishaji fedha, usafirishaji wa binadamu au shughuli nyingine haramu kama ilivyothibitika kisheria.

  "Wengine ambao hawahusiki na msamaha huu ni taasisi, makampuni na watu binafsi ambao wana madeni ya nyuma ya kodi yanayotokana na adhabu zilizoamuliwa tayari au adhabu za makosa yatokanayo na uzembe wa kukusudia uliobainika kisheria pamoja na wenye riba au faini zilizotokana na kutoa au kutumia risiti za kielektroniki za kughushi," alibainisha Mahendeka.

  Kwa upande wake Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA Chama Siriwa ametoa wito kwa washauri wa walipakodi mkoani hapa kuendelea kuwaelimisha wafanyabiashara na wale wote wenye taasisi na makampuni mbalimbali yenye malimbikizo ya madeni ya kodi kuwahi kutuma maombi ya msamaha huo kabla muda uliopangwa haujamalizika.

  "Mimi napenda tu kusisistiza kuwa mwisho wa kutuma maombi ya msamaha huu ni tarehe 30 Novemba, 2018. Hivyo, natoa wito kwenu washauri wa walipakodi muendelee kuwaelimisha wafanyabiashara na wote wenye taasisi na makampuni kutuma maombi mapema ili waweze kunufaika na msamaha huu," alieleza Siriwa.

  Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania ilitangaza msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi mwezi Julai, 2018 kwa lengo la kutoa unafuu kwa walipakodi wenye malimbikizo ya madeni ya riba na adhabu kwa kusamehe madeni yao na kuwapa fursa ya kulipa malimbikizo ya madeni ya msingi ya kodi - principal tax mara moja au kwa awamu ndani ya mwaka wa fedha wa 2018/19.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii

  MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu imedai kwamba  Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando anayekabiliwa na mashtaka ta matumizi mabaya ya madaraka ana kesi ya kujibu.

  Uamuzi huo umetolewa leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi baada ya upande wa mashtaka kufunga kesi yao kwa kuleta mashahidi watano.

  Hakimu Shaidi amesema amepitia ushahidi wote wa mashahidi watano ulioletwa na upande wa mashtaka na kuona mshtakiwa ana kesi ya kujibu.Katika kesi hiyo Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh.milioni 887.1.

  Kabla ya kutolewa kwa uamuzi huo, leo shahidi wa tano wa upande wa mashtaka, Dominic Mahundi alitoa ushahidi wake.Miongoni mwa  mashahidi  wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi ni ofisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya;  mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana.

  Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa Juni 16, mwaka 2008 akiwa  Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido  aliyekuwa Mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.

  Tido  ambaye anatetewa na Wakili Ramadhani Maleta na yupo nje kwa dhamana ataanza kujitetea Septemba 20 mwaka 2018,Katika kesi hiyo Tido anakabiriwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni.

  Kabla ya kutolewa kwa uamuzi huo, leo shahidi wa tano wa upande wa mashtaka, Dominic Mahundi alitoa ushahidi wake.Miongoni mwa  mashahidi  wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi ni, ofisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya;  mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana.

  Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa Juni 16, 2008,  akiwa  Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido ambaye alikuwa mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.

  0 0

  TSN Oil imeshinda tuzo ya Africa Leadership Oil and Gas Retail of the Year.
  TSN Oil imeshinda tuzo hiyo ya ‘Oil and Gas Retail of the Year’ ya Africa Leadership Awards 2018, katika hafla iliyofanyika jana (tarehe 26 Agosti 2018) katika ukumbi wa hoteli ya Sandton Sun, Johannesburg Afrika ya kusini.


  Tuzo hizo za Africa Leadership zinalenga kutunuku Washikadau mbalimbali na viongozi waliochangia mafanikio makubwa katika kukuza uchumi na uongozi bora. Tuzo hiyo kwa TSN Oil inatambulisha Mchango wake katika sekta ya Mafuta Nchini na pia jitihada zake katika kupeperusha bendera wa ukuwaji wa sekta hiyo hapa Tanzania. Tuzo ya TSN Oil ilikabidhiwa na Senator wa Marekani jimbo la Georgia, Michaael Rhett, na kupokelewa na Mkurugenzi wa TSN Group , Bwana Farough Ahmed Baghozah mwenyewe.

  Mr Farough ametambuliwa kama Mchangiaji Mkubwa katika ukuaji wa sekta na biashara ya Mafuta Nchini kutokana na Mchango wake, Muda wake wa thamani katika kupigania sekta hiyo na kwa nafasi ambayo TSN Oil imecheza hapa nchini.Mkurugenzi wa TSN Oil kampuni dada ya TSN Group yenye zaidi ya Miaka 10 kwenye sekta ya Mafuta, Farough Ahmed Baghozah akipokea tuzo hiyo amesema “Ushindi huu unamaana kubwa kwetu kama kampuni na kama Nchi kwa ujumla, unatambulisha kukua kwa sekta hii katika uchochezi wa ukuwaji wa sekta ya viwanda hapa nchini, Unaelezea safari yetu kama kampuni kwa kusimamia ubora na mhimili wa kauli mbiu yetu, Tanzania Sisi Nyumbani. “
  “Tunashukuru na kuendela kuwashukuru wateja wetu kama wadau wakuu kwenye utambulisho huu, Tanzania hii ni ya kwenu.”


  Kampuni ya TSN Oil yenye makazi yake makuu Dar es salaam na depo ya mafuta iliyopo Kisosora Tanga inamiliki vituo vya mafuta zaidi ya 28 na kushika asilimia 5% ya soko la Mafuta nchini Tanzania, kwa zaidi ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 14th November, 2006.

  Mafanikio ya TSN Oil ambayo ilitokana na Chemoil yanaonekana kwa kuzalisha pia kampuni nyingine dada kama.

  2009 - TSN Supermarket Ltd
  2010 - TSN Logistics Ltd
  2012 - TSN Distribution Ltd / TSN (UK) Ltd / TSN General Traders FZE UAE
  2015 – Prime Brands Distribution Co. Ltd / TSN Media / TSN Foundation

  0 0

  Nchi ya MAREKANI kupitia ubalozi wake nchini Tanzania na kuwakilishwa na kaimu balozi INMI PATTERSONI umegawa magari matano kwa tume ya kudhibiti UKIMWI nchi TACAIDS katika mikoa ya nyanda za juu kusini ikiwemo RUVUMA,MBEYA,KATAVI,RUKWA NA SONGWE kwa ajili ya kwenda kudhibiti maambukizi wa ugonjwa wa UKIMWI katika mikoa hiyo ambapo ugawaji wa magari hayo umefanyika mkoani Ruvuma na kukabidhiwa kwa waziri ofisi ya waziri mkuu sera ,bunge ,ajira,na watu wenye ulemavu mh JENISTER MHAGAMA

  0 0

  Mgeni rasmi Afisa Ushirika Jiji la Arusha Huruma Kibendwa akimkabidhi cheti mmoja wa kundi la Kanono, aliyepo kushotonkwake ni Mwenyekiti wa Kundi la Kanono Wilbald Ngambeki, na wakwanza kulia ni Davis Kalegea mtendaji wa kundi hilo.
  Wakina mama pamoja na wanaume kutoka kabila la Wanyambo waishio mkoani Arusha wakifanya maandalizi ya kutengeneza vyakula vya asili katika tamasha hilo. Picha na Vero Ignatus
  Maandalizi ya chakula cha asili yakiendelea kama inavyoonekana pichani.

  Tayari unga wa muhogo umeshapatikana kwaajili ya kupika maandazi ya asili ya watu
  Maandalizi ya juice ya asili ikiendelea.
  Juice ya asil iliyoandaliwa na wakina mama wa kabila la Kinyambo katika tamasha hilo
  Ngoma ya asili ya Kabila la Wanyambo wakitumbuiza katika tamasha hilo. Picha na Vero Ignatus.


  Na. Vero Ignatus. ARUSHA


  Watanzania wameshauriwa kuenzi mila na desturi nzuri ili kuzirithisha kwa vizazi vijavyo na kuwa na Taifa lenye utamaduni madhubuti.

  Rai hiyo imetolewa katika tamasha linalokutanisha familia 172 zenye jumla ya watu 323 kutoka katika kabila la wanyambo kutoka wilaya za Karagwe na Kerwa waishiao mkoani Arusha. Akizungumzia lengo la tamasha hilo mwenyekiti kikundi cha Kanono Wilbard Ngambeki amesema lengo kubwa ni kuimarisha umoja na kuzifanya familia zilizozaliwa kufahamu tamaduni zile nzuri za wazazi wao.

  '' Katika tamasha hili michezo imekuwa ni kivutio kikubwa, wazazi wanawaleta watoto wao ila sisi tunapitisha mila zetu na desturi zetu njema kwao ili wakue wakitambua wazazi wao ndipo tulipotoka hata watakapokuwa kwenye miji mingine ya watu mbali na wazazi wao.''

  Ngambeki amesema umoja huo wa Kundi la Kanono tayari walishaanzisha Saccos ambayo inawanachama 105 waliojiunga na tayari wameshakopeshana zaidi ya milioni 800 kwa riba nafuu. Afisa Ushirika Jiji la Arusha Huruma Kibendwa aliyekuwa mgeni rasmi katika tamashaa hilo amepongeza umoja kwa kuwa na saccos ambayo inawasaidia kukopeshana wao kwawao na kujikwamua kiuchumi na kimaendeleo

  '' Kwani mara nyingi tunawashauri wanamchi wajiunge kwenye vikundi ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kukopeshana wao kwa wao mkopo wenye riba nafuu uzuri kikundi hiki kimesajiliwa na mna saccos inayofanya vizuri '' Alisema Kibendwa.

  David Igola ni mmoja wa wa wanakanono amesema kuwa zipo faida kubwa ambazo amezipata katika kundi hilo ikiwemo kuenzi mila na desturi nzuri za kabila hilo, ikiwemo kusaidiana katika nyanja mbalimbali kama vile elimu, matibabu, shughuli za kijamii na nyinginezo nyingi.

  '' Sanasana ukiangalia vile vitu vya asili tunavyokuanavyo, watoto wetu ambao wengi wamezaliwa mjini wengi hawavuelewi unakuta tunapokwenda nao vijijini wengi wanavushangaa, ila kwenye tamasha kama hili vinatengenezwa wazi na wanajifunza''Alisema Igola. Tamasha hilo limeambatana na michezo mbalimbali iliwemo ya ngoma za asili, mapishi ya asili, kuvuta kamba kukimbiza kuku, ngonjera pamoja na ushairi.

  Kundi hilo la Kanono lilianzishwa rasmi 1996 na kupata usajili 27August 2012 ambapo Jina Kanono ni heshima kutoka kwa kiongozi wao Omkama.

  0 0


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Sylvain Ore muda mfupi kabla ya kuapishwa kwa Majaji wapya watatu wa mahakama hiyo mjini Arusha. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya kuapishwa kwa majaji wapya watatu wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu mjini Arusha.
    Majaji watatu wapya wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu wakiwa wameketi pamoja muda mfupi kabla ya kuapishwa, kutoka kushoto ni Mhe.Jaji Blaise Tchikaye (Congo), Mhe. Jaji Stella Isibhakhonem Anukam (Nigeria) na Mhe. Jaji Imani Aboud (Tanzania). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi kutoka kwa  Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Sylvain Ore mara baada ya kuapishwa kwa Majaji wapya watatu wa mahakama hiyo mjini Arusha.
   
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha mpya na Majaji wateule wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ambao wameapishwa leo mjini Arusha  kushoto ni Mhe.Jaji Blaise Tchikaye (Congo), Mhe. Jaji Imani Aboud (Tanzania) na kulia ni Mhe. Jaji Stella Isibhakhonem Anukam (Nigeria)  . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  SERIKALI imesema kuwa wenye viwanda vya saruji wazalishe saruji ya kutosheleza mahitaji ya ndani pamoja na kusimamia bei ya bidhaa hiyo mpaka kwa mlaji wa mwisho.

  Hayo ameyasema Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charle’s Mwijage wakati alipotembelea viwanda vya Saruji vya Camel na Twiga , amesema amekosa hivi usingizi kwa kuadimika kwa saruji nchini na kuwataka viwanda hivyo vizalishe saruji ya kukidhi mahitaji ya ndani kutokana na kuwepo miradi mbalimbali ya ujenzi.

  Mwijage amesema kuwa hivi karibuni kulikuwa kuadimika kwa saruji iliyotokana na baadhi ya viwanda kuwa katika matengenezo pamoja na makaa ya mawe kuzalishwa kwa kiwango kidogo.Amesema kuwa katika kusimamia wizara hiyo kwa mzalishaji ambaye hatakwenda na kasi ya uzalishaji wa saruji anatomlaka ya kuifuta leseni hivyo wenye viwanda lazima wakidhi mahitaji ya saruji.

  Aidha amesema kuwa kwa mwaka tani milioni 10.5 zinalishwa hivyo lazima kila kiwanda kiongeze uzalishaji na kuweza kuuza hata masoko ya nje ya nchi kwa kupata fedha za kigeni zinazotokana na saruji.Amesema kuwa kuna viwanda vitatu vya saruji vinajengwa nchini ambavyo vitaongeza uzalishaji wa wa saruji hiyo.

  Mwijage amesema kuwa viwanda vikizasha saruji na kuweza kuuza katika masoko ya nje kuna uwezekano wa bidhaa ya saruji ikwa inachangia uchumi wa nchi na kuongoza katika uchangiaji huo kwa pato la taifa.Meneja wa Masoko wa kiwanda cha Saruji cha Twiga , Danford Semwenda amesema kuwa kwa sasa wanazalisha tani 6000 kutoka tani 300O kwa siku 15 zilizopita iliyotokana na matengenezo ya mtambo.

  Waziri Mwijage leo Augusti 27,2018 ametembelea viwanda vya kutengeneza Saruji kuanzia cha Camel kilichopo Mbagala rangi Tatu na cha Twiga kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akitembelea kiwanda cha Camel kilichopo Mbagala jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuangalia utendaji kazi wa kiwanda hicho kutokana na kukosekana kwa saruji hapa nchini.
    Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akitembelea kiwanda cha Twiga kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam na kushoto ni Mkurugenzi Mkuuwa Kiwanda cha Twiga, Alphonso Velez.
   Mchanga wa kutengeneza Saruji katika kiwanda cha Saruji cha Twiga Tegeta jijini Dar es Salaam.

  Meneja wa Masoko wa kiwanda cha Saruji cha Twiga , Danford Semwenda akijibu swali kutoka kwa  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alipotembelea kiwanda cha Twiga kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi Mkuuwa kiwanda cha Twiga kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaa, Alfonso Velez.

  0 0

  Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

  WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika eneo la kuhifadhia makontena-Bandari Kavu Dar es Salaam (DICD), na kukagua makontena 20 yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania -TRA kuendelea na mnada wa makontena hayo ili kupata kodi ya Serikali inayokadiriwa kufikia shilingi bilioni 1.2.

  Dkt. Mpango amesema kuwa kodi hiyo inadaiwa kwa mujibu wa sheria za nchi baada ya mwenye mali kushindwa kulipa kodi na kwamba amesikitishwa na vitisho vinavyotolewa na Mkuu huyo wa Mkoa na vilivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini  akitumia vifungu vya Biblia kwamba yeyote atakaye nunua mzigo huo atalaaniwa.

  "Sheria za nchi hazichagua sura wala cheo cha mtu, na mimi ndicho nilicho apa, kutekeleza sheria za nchi, sheria za kodi, ndiyo dhamana niliyo pewa kwahiyo Kamishna, simamia sheria za kodi bila kuyumba" alisisitiza Dkt. Mpango akitoa maelekezo kwa Kamisha wa Forodha Bw. Ben Usaje.

  Alifafanua kuwa mzigo wa Samani ulioagizwa kutoka nje ya nchi hauna msamaha wa kodi na kwamba huyo aliye agiza (RC Paul Makonda) alipe kodi stahidi na asipo lipa kodi hiyo mchakato unaoendelea wa kuyapiga mnada makontena hayo uendelee.

  "Napenda niwaombe viongozi wenzangu Serikalini, ni muhimu tukachuja maneno! unasema mtu anayekuja kununua samani atapata laana, tena laana ya Mungu, kwa nini tunamhusisha Mungu kwenye vitu vya namna hii" alieleza kwa masikitiko Dkt. Mpango

  Dkt. Mpango alitoa wito kwa watanzania wanaotaka kununua bidhaa hizo ambazo nyingi ni vifaa vinavyoweza kutumika shuleni ama maofisini kama vile viti meza na makabati, kujitokeza bila hofu kununua mali hizo.

   Aliwaomba walimu na wanafunzi wasiwe na wasiwasi na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua na kuwekeza kwenye elimu kwa kutenga zaidi ya shilingi bilioni 20 kila mwezi kulipa ada ya wanafunzi ili wasome bila kulipa ada na ina mpango madhubuti wa kuboresha miundombinu ya elimu nchi nzima ikiwemo ujenzi wa madarasa na ofisi za walimu.

  "Tunawapenda na kuwathamini sana walimu wetu, asitokee mtu yeyote  akaanza kuwaambia hadithi kama vile Serikali hii inawapuuza! si kweli hata kidogo" Aliongeza Dkt. Mpango

  Kwa upande wake, Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Ben Usaje, alimweleza Dkt. Philip Mpango kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, aliwasilisha maombi ya kutaka kupewa msamaha wa kodi wa makontena 36 yenye samani kutoka Diapora nchini Marekani.

  Alisema kuwa kati ya makontena hayo, yaliyoingia nchini ni makontena 20 ambayo yanadaiwa kodi ya shilingi bilioni 1.2 na kwamba utaratibu kwa kumtaka Paul Makonda alipe kodi hiyo ili aruhusiwe kuyachukua makontena hayo ulifanyika kwa mujibu wa sheria na kwamba mpaka sasa hajayachukua ndio maana yanapigwa mnada.

  Naye aliwatahadharisha watu wanao tumia masuala ya siasa na uongozi Serikalini kutaka kukwepa kulipa kodi a kwamba suala la kodi za samani zinaonekana ziko juu kwa sababu Bunge lilitunga sheria hiyo ili kulinda soko la ndani la samani na kuweka sheria ya kutokuwepo kwa msamaha wowote wa kodi kwenye bidhaa kama hizo.
    Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwasili kukagua Kontena  ishirini za Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul makonda, zilizo na Samani vikiwemo viti na Meza katika Bandari ya Dar es Salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akifunguliwa Kontena Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, zenye Samani za Viti na Meza ili kushuhudia kilichopo kabla hajaagiza taratibu za mnada ziendelee ili kodi inayodaiwa ya thamani ya Sh. Bilioni 1.2 iweze kupatikana.
   Baadhi ya meza zilizopo katika moja ya Kontena  ambazo  zinadaiwa kodi ya Sh. Bilioni 1.2, wakati Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam na kuagiza Kamishna wa Forodha kuchukua hatua za kisheria ikiwemo kupigwa mnada kwa vifaa hivyo ili kodi ya Serikali ipatikane.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akitoa maagizo kwa Kamishna wa Forodha  wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Benny Usaje, ya kuendelea kupigwa mnada kwa Kontena ishirini za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, zinazodaiwa kodi ya Sh. Bilioni 1.2 ili Serikali iweze kupata kodi yake kama kodi kutoka kwa mmiliki wa Kontena hizo hatalipa kodi kwa wakati.
  Baadhi ya meza zilizopo katika moja ya Kontena  ambazo  zinadaiwa kodi ya Sh. Bilioni 1.2, wakati Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam na kuagiza Kamishna wa Forodha kuchukua hatua za kisheria ikiwemo kupigwa mnada kwa vifaa hivyo ili kodi ya Serikali ipatikane.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella (katikati) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Shinyanga Mhe. Zainab Telack kwenye mapokezi yaliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Izizimba A wilayani Kwimba.

  Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

  Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella jana Agosti 26, 2018 amepokea Mwenge wa Uhuru ukitokea mkoani Shinyanga.


  Akizungumza kwenye mapokezi hayo yaliyofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Izizimba A wilayani Kwimba, Mhe.Mongella alibainisha kwamba mwenge huo unatarajia kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 13.


  Naye kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa ndugu Charles Kabeho alimpongeza Mhe.Mongella kwa mapokezi makubwa na kuahidi kukagua miradi yote iliyokusudiwa hatua kwa hatua ili kujiridhisha ubora wa utekelezaji wake.


  Mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Mwanza zinatarajiwa kufikia tamati jumapili ijayo Septemba 02,2018 na kukabidhiwa mkoani Mara jumatatu Septemba 03, 2018.

  Mkuu wa Mkoa Mwanza akipokea mwenge wa Uhuru
  Tazama picha mbalimbali za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mkoani Mwanza
  Tazama BMG Online Tv hapa chini

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela akizungumza jambo katika haflla hiyo, wa pili kushoto ni Mhe. Jaji Imani Aboud na kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi Kanda ya Tanga, Mhe. E.J. Mkasimongwa.
  Viongozi mbalimbali wa Serikali waliohuhuria.
  Baadhi ya watumishi waastafu walioagwa kwenye hafla hiyo (kushoto ni Bi. Bi. Lydia Yohana Andrew na kulia ni Bi. Shehu Ally Muhsin )
  Bi. Shehu Ally Muhsin (Mstaafu) akipokea zawadi
  Mhe. Arnold Kileo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Handeni, akipokea cheti kwa kushika nafasi ya kwanza kwa Mahakimu wa Wilaya walisikiliza na kumaliza mashauri mengi.
  Bwn. Emmanuel Machimo, Afisa Tawala Mahakama ya Wilaya ya Korogwe akipokea cheti kwa kushika nafasi ya kwanza kwa kada ya Maafisa Tawala/Utumishi Kanda ya Tanga.
  Bi. Elizabeth Noah Mavoa, Mhasibu Msaidizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga, akipokea cheti kwa kushika nafasi ya pili ya Mhasibu bora Kanda ya Tanga.
  Bw. Seif Mkuya, Dereva bora wa mwaka 2017 akipokea cheti.

  ……………………..

  Na Amina Ahmad, Mahakama Kuu-Tanga

  Mahakama Kuu, Kanda ya Tanga imewapongeza baadhi ya Watumishi wake waliofanya vizuri kwa kuwapa vyeti maalum ikiwa ni ishara ya kutambua mchango pamoja juhudi zao katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

  Vyeti hivyo vilitolewa kwa Watumishi hao na Mgeni rasmi ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Bw. Martine Shigela, Agosti 24, 2018 katika hafla fupi ya kuwaaga Wahe. Majaji na Mahakimu waliohamishwa vituo pamoja na watumishi wa kada mbalimbali waliostaafu.

  Utaratibu huu umeanzishwa katika Kanda hii ili kuenzi jitidaha na ufanisi wa kazi waliokuwa nao kipindi cha utumishi wao.

  Miongoni mwa Watumishi waliopatiwa vyeti hivyo ni pamoja na Mahakimu wa Mahakama za Wilaya na Mahakama za Mwanzo, Maafisa Utumishi, Wasaidizi wa Kumbumbuku, Wahasibu, Makatibu Mahsusi, Madereva, Walinzi, Mahakama za Wilaya zilizofanya ukarabati mkubwa wa Mahakama za Mwanzo, Kituo kilichoongoza kwa watumishi wake kuvaa sare na kuonekana nadhifu pamoja na Mahakama za Wilaya na Mwanzo zilizosikiliza na kuamua mashauri kwa asilimia nyingi kuliko zingize.

  Watumishi waliostaafu ambao waliagwa katika hafla hiyo ni Bwana. Jumbe Athumani Kai, Msaidizi wa hesabu, Mahakama ya Wilaya Korogwe, Bi. Lydia Yohana Andrew (Msaidizi wa kumbukumbu, Mahakama ya mwanzo Mashewa Wilayani Korogwe) na Bi. Shehu Ally Muhsin (Msaidizi wa kumbukumbu, Mahakama ya Wilaya ya Tanga).

  Viongozi wengine waliohudhuria katika hafla hiyo ni pamoja na Mkuu wa chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto IJA, Mhe Jaji Faustine Kihwelo, Mkuu wa Wilaya wa Handeni, Mhe. Godwin Gondwe, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Mhe. Sauda Mtondoo), Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Thobias Mwilapwa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji – Korogwe (Mhe. Nicodemus John Bee, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Mhe. na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga (Benedict Wakulyamba).

  0 0

   
  Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Inmi patterson akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge,Sera ,Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama funguo za magari waliyoyatoa kwa ajili ya Waratibu wa Kudhibiti UKIMWI, hivi karibuni Wilayani Songea Mkoani Ruvuma

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge,Sera ,Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama akionesha funguo za magari waliyokabidhiwa na Marekani kwa ajili ya Waratibu wa Kudhibiti UKIMWI, katika hafla iliyofanyika hivi karibuni Wilayani Songea Mkoani Ruvuma, katikati ni Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Inmi patterson na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndema.


  Serikali imeongeza nguvu za uratibu wa udhibiti UKIMWI nchini kwa kutoa vitendea kazi kwa Waratibu wa Kudhibiti UKIMWI nchini katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

  Vitendea kazi vilivyotolewa ni pamoja na magari 5 na vifaa bongine vya ofisi zikwemo komputa katika Mikoa ya Mbeya,Katavi,Rukwa,Ruvuma na Songwe.

  Lengo la kuwezesha Mikoa hiyo ni kuhakikisha uratibu wa UKIMWI nchini unaratibiwa ipasavyo kuanzia ngazi ya Kijiji/Mtaa,Kata,Halmashauri,Mkoa hadi Taifa.
  Awali Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania ( TACAIDS) Dr Leonard Maboko akizungumza katika hafla hiyo alisema kuwa lengo la Serikali ni kudhibiti maambukizi mapya ya VVU na hii itawezekana endapo uratibu utaimarishwa kuanzia ngazi ya jamii.   Dr Maboko aliongeza kuwa anaamini kuwa baada ya kukabodhowa vitendea kazi hivi, Waratibu wa Kudhibiti UKIMWI wa TACAIDS katika Mikoa watakuwa hawana kipingamizi katika utendaji wa kazi na kuwafikia wananchi ,ikiwa ni pamoja na kuandaa na kuwasilisha taarifa kwa wakati.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge,Sera ,Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama akiwasha Moja ya Gari waliyokabidhiwa na Ubalozi wa Marekani hivi Karibuni, Wilayani Songea Mkoani Ruvuma.

  Dr Maboko amewaasa Waratibu hao kuakikisha wanatunza vifaa hivyo na kuvitumia kwa manufaa ya Serikali na sio manufaa binafsi.

  Naye waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge,Sera ,Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama alisema kuwa hali ya maambukizi ya vvu nchini inatutahadharisha kuwa ni lazima kuwa na mbinu mbadala za kukabiliana na maambukizi mapya.

  Kwa sababu hiyo Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Watu wa Marekani kupitia Idara yake ya Ulinzi (DOD)ilianzisha Mkakati wa Kikanda wenye kulenga mazingira na vichocheo vinavyofanana katika Mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya na Ruvuma ili kukabiliana na maambukizi ya VVU kwa kuunganisha nguvu na rasilimali.

  Mhe Mhagama aliongeza kuwa hadi sasa kila Mkoa tayari umetengeneza Mpango Mkakati wa Mkoa wa Kudhibiti UKIMWI kulingana na vihatarishi vilivyotajwa kwenye utafiti wa viasharia vya VVU na UKIMWI vya mwaka 2016/2017 aliagiza viongozi wote kushiriki katika kutekeleza Mwitikio wa UKIMWI kwa kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa katika mpango mkakati ulioainishwa na Mkoa husika katika maeneo ya kinga ,matunzo na matibabu ili kupunguza athari zitokanazo na UKIMWI.
  Mkurugenzi Mtendaji TACAIDS Dkt. Leonard Maboko akionesha funguo baada ya kupokea magari kutoka Waziri Jenista Mhagama (kulia) aliyekabidhiwa na Ubalozi wa Marekani,

  Naye kaimu Balozi wa Marekeni alisema kuwa lengo la ushirikiano wa Marekeni ni kuwawezesha watanzania kufanya kazi ya kujenga nchi imara ,yenye afya na ustawi zaidi,”nami ninafurahi kuendeleza mtizamo huu kuhakikisha kwamba jamii ya Watanzania waliojitoa na kuwa na dhamira ya dhati,wanapata nyenzo zinazohitajika katika kujenga maisha bora ya baadae”
  Aidha Serikali ya Marekani inajivunia kuunga mkono jitihada nyingi za ushirikiano kwenye masuala ya Afya,ikishirikiana na Watanzania ili kuimarisha uwezo wa kushughulikia malaria,Afya ya mama na mtoto,uzazi wa mpango,Kifua kikuu,Lishe, VVU na UKIMWI.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge,Sera ,Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Inmi patterson (wapili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko (wa kwanza kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme (wa pili kulia)

  Aliongeza kuwa magari sita yaliyonunuliwa yatasaidia kuboresha uratibu na uwajibikaji kwenye programu za UKIMWI za Mikoa kuboresha usimamizi na uangalizi katika Mikoa na Makao Makuu ya TACAIDS katika kuboresha afya katika Nyanda zaJuu Kusini.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko( kulia) akimkabidhi funguo za gari Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Ruvuma Bw. Daniel Mwaiteleke Baada ya kupokea magari hayo kutoka Ubalozi wa Marekani, anayeshuhudia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama.

  Magari sita yaliyokabidhiwa kwa TACAIDS yameenda katika Mikoa mitano ya Mbeya,Rukwa,Katavi,Songwe na Ruvuma na moja limebaki TACAIDS kwa ajili ya usimamizi wa program.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mhe Christine Mndeme alishukuru kwa mikoa ya Nyanda za juu kusini kupatiwa msaada huo kwa kuwa mikoa hiyo ndio yenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU na UKIMWI,kwa kubuniwa mradi huo kutasaidia zaidi katika kuongeza ushirikishwaji wa jamii katika kupambana na maambukizi ya VVU.

  Kwa kufanya hivyo wanjamii wataelewa kuwa wanao wajibu mkubwa wa kufanya ili kukabiliana na maambukizi ya VVU badala ya kutegemea serikali na wadau wa maendeleo pekee.

  Mhe Mndeme aliongeza kuwa mradi huu umekusudia kushirikisha viongozi wakuuwa siasa kama wakuu wa Mikoa na Wilaya katika kusimamia Mwitikio wa UKIMWI ili kuongeza uwajibikaji

  0 0

  Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashantu Kijaji akizungumza katika mkutano wa 41 wa umoja wa kikanda wa makampuni ya Bima kutoka nchi 39 za Mashariki na Kusini mwa Afrika (OESAI)Picha na Vero Ignatus. 
  Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa BIMA nchini (TIRA) Dk, Baghayo Saqware akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus
  Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo,Khamis Suleiman akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Arusha. 
   Wapili kutoka kushoto ni Naibu waziri wa Fedha Dkt. Ashantu Kijaji, aliyepo kulia kwake ni Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa BIMA nchini (TIRA) Dk, Baghayo Saqware, akifuatiwa na Rukia Adam Mjumbe kutoka (TIRA) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka baadhi ya matataifa 39 Duniani. Picha na Vero Ignatus. 


  Na.Vero Ignatus.Arusha

  Mkutano wa 41 wa umoja wa kikanda wa makampuni ya Bima kutoka nchi 39 za Mashariki na Kusini mwa Afrika (OESAI) umefunguliwa leo rasmi mkoani Arusha.

   Mkutano huo umefunguliwa  na Naibu waziri wa fedha Dkt. Ashatu Kijaji ambapo ameyataka makampuni ya Bima kutoa huduma za Bima  kwa wakulima ili kufikia uchumi wa kati. 


  Dk, Kijaji amesema asilimia 75 ya Watanzania ni wakulima ambao bado hawana elimu kuhusu  bima ikiwemo kupata mikopo ya bei nafuu kwaajili ya kutatua changamoto za kilimo na kufikia katika uchumi wa kati. 

  Ameyataka makampuni ya bima nchini kuangalia kundi hilo la wakulima ili nao waweze kunufaika na bidhaa wanazozalisha kwakuwa kundi hilo ni kubwa na ni fursa kwa makampuni ya bima nchini kuongeza idadi ya watumiaji wa bima. 


  Amesema watanzania wanaotumia bima  hapa nchini ni chini ya asilimia moja idadi ambayo hairidhishi kabisa kwakuwa watanzania wapo zaidi ya milioni 45 kwa mujibu wa ofisi ya Takwimu za Taifa. 

  Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa BIMA nchini (TIRA) Dk, Baghayo Saqware amesema mkutano huo wa 41 unatoa fursa kwa kampuni za bima zilizopo hapa nchini kujifunza jinsi kampuni za nje za bima zinavyofanya kazi kwa ufanisi. 

  Aidha amesema kampuni hizo zitapata fursa ya kujifunza uboreshaji wa huduma kwa kutumia mfumo wa Tehama unaoleta mageuzi katika utoaji wa huduma bora zako bima,  rasilimali watu  na kuongeza wigo wa kutafuta watu mbalimbali kwaajili ya kulipia bima ya maisha. 

  Hata hivyo Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo,Khamis Suleiman amesema lengo la mkutano huo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 asilimia 50 ya watanzania wawe na aina yoyote  ya bima kwani kwa sasa Tanzania ipo kwenye nafasi ya pili  kwa nchi za Afrika Mashariki kwa kutoa huduma za bima.

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimuuliza maswali Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara mjini, Ibrahim Mhando (kushoto) baada ya kushindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne akiwemo Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Y&P Architects ambaye ni mshauri mkuu wa ujenzi wa Ofisi Kuu ya Uhamiaji Mkoani Mtwara. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Wapili kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Lucas Mkondya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akitoka Kituo cha Polisi cha Kati mjini Mtwara mara baada ya kumsweka ndani Mkuu wa Kituo cha Polisi hicho ambaye aliwaweka watuhumiwa chumba cha upelelezi badala ya mahabusu kituoni hapo. Nyuma ya Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Lucas Mkondya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimuangalia Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni ya Ujenzi ya Lucas, ambaye pia kandarasi aliyejenga Jengo la Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Theophilius Kessy, wakati alipokua anambana maswali ya kutaka kujua kwanini Jengo la Uhamiaji Mkoa wa Mtwara limejengwa chini ya kiwango. Aliyeshika kitabu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   
                                                                                                                           
  Na Mwandishi Wetu, Mtwara
  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemweka ndani Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kati mjini Mtwara (OCS), Ibrahim Mhando, kwa kushindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne akiwemo Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Y&P Architects ambaye alitoa taarifa ya uongo kwa Waziri huyo kuhusu ujenzi wa Makao Makuu ya Uhamiaji Mkoani humo.

  Tukio hilo lilitokea saa 12:46 asubuhi Agosti 27 leo Jumatatu, wakati Waziri Lugola na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Meja Jenerali, Jacob Kingu walipofika Kituo hicho kikuu cha mkoa kwa kushtukiza wakati alipokua anakwenda Uwanja wa Ndege kwa ajili ya kurudi jijini Dar es Salaam, ndipo Waziri huyo alitaka kuthibitisha kama mtuhumiwa ambaye alielekeza jana usiku akamatwe awekwe mahabusu endapo Polisi walitekeleza agizo lake.

  Hata hivyo, Waziri Lugola alimkuta mtuhumiwa huyo, Benjamin Kasiga akiwa chumba cha upelelezi badala ya kuwekwa mahabusu ya polisi hiyo, ndipo akamuuliza Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Lucas Mkondya, kwanini agizo lake halijatekelezwa.

  “Hivi ndivyo polisi mnafanya hivi, haya ndio madudu mnayoyafanya? Tabia hii siku zote tunaipinga ikichafua Jeshi la Polisi, na hii ndiyo tabia yenu, najua ndio mana nimekuja ghafla, mnafahamu maadili ya Jeshi? RPC hawa polisi wako wanafanya nini, OCS njoo hapa, kwanini umeweka hawa watuhumiwa chumba cha upepelezi badala ya mahabusu, nawe unaingia ndani kwa kushindwa kuwaweka ndani hawa watuhumiwa, RPC muweke ndani sasa hivi huyu,” alisema Lugola akiwa amekasirika. 

  Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo (RPC), Mkondya alimweleza Waziri Lugola kituoni hapo kuwa, Polisi wake walifanya makosa kwa kutowaweka mahabusu watuhumiwa hao.

  Kwa upande wake mkuu wa kituo huyo, Mhando kabla ya kuwekwa mahabusu pamoja na wale watuhumiwa ambao alishindwa kuwaweka mahabusu, alisema sababu kuu yakutowaweka mahabusu watuhumiwa hao ni kwasababu mahabusu ilijaa na wanafanya hivyo mara chache inapotokea mahabusu wamekuwa wengi kituoni hapo. 

  0 0

   Mkazi wa Kata ya Katunguru, Robert Lomwadi, akipakia moja ya boksi la dawa, katika Boti namba BKT 00098 MV BMU Mulumo tayari kupelekwa Zahanati ya Kisiwa cha Mazinga, wilayani Muleba mkoani Kagera leo hii.
   Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Dkt. Modest Burchard, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya afya na upokeaji wa dawa kutoka MSD.
   Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kisiwa cha Mazinga, Johanes Sweetbert (kulia), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jinsi wanavyopokea dawa kutoka MSD na changamoto zilizopo.
   Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD Kanda ya Mwanza, Cornelia Mwillawi (kushoto), akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Afya wa Kisiwa cha Mazinga wakati wa kukabidhi dawa.
   Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD Kanda ya Mwanza, Cornelia Mwillawi (kushoto), akiwakabidhi mifuko ya vifaa vya mama vya kujifungulia.
   Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kisiwa cha Mazinga, Johanes Sweetbert (wa pili kulia), akisaini fomu maalumu baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo. Wendine ni wajumbe wa kamati ya afya wa Kisiwa cha Mazinga.
   Mkazi wa Kata ya Katunguru, Robert Lomwadi, akibeba boksi la dawa kuzipeleka tayari kwenda kwenye boti kabla ya kuziingiza kwenye boti.
   Mjumbe wa Kamati ya Afya ya Kisiwa cha Mazinga, Winfrida Itaganisa, akizungumzia jinsi wanavyo pokea dawa kutoka MSD.
  Wananchi wa Kata ya Katunguru walioshuhudia makabidhiano ya dawa hizo.

  Na Dotto Mwaibale, Muleba Kagera.  

  MGANGA Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Dkt. Modest Burchard amesema licha ya changamoto za kusafirisha dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenda visiwani, Bohari ya Dawa (MSD) imekuwa ikitoa ushirikiano mkubwa kuhakikisha dawa zinafika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa wakati kwenye visiwa 26 vilivyopo katika wilaya hiyo.

  Dkt. Burchard ameyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao wapo ziarani mkoani Kagera kuangalia taratibu za usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara pamoja na kuzungumza na wateja wa MSD.

  "Tunaishukuru sana MSD kwa kazi kubwa ya kufikisha dawa katika maeneo yote ya visiwa licha ya kuwepo kwa changamoto ya usafiri majini, hasa vipindi vya hali mbaya ya hewa kwenye ziwa victoria".

  Alisema katika mkoa wa Kagera, wilaya ya Muleba ndiyo ina visiwa vingi lakini serikali kwa kushirikiana na MSD wamefanikiwa kufikisha dawa katika visiwa hivyo kwa ushirikiano mkubwa wa wananchi.

  Aliongeza kuwa Halmshauri ya Wilaya ya Muleba ina boti mbili kwa ajili ya kusafirisha wananchi kutoka mwaloni katika Kijiji cha Katunguru kwenda kisiwa cha Mazinga, ambapo pia ina mpango wa kununua boti jingine kwa ajili ya kuongeza nguvu ya usafirishaji.

  Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa dawa muhimu wilayani humo, alisema hivi sasa hali ni nzuri kwani upatikanaji wake ni kati ya asilimia 90 hadi 98  na kuwa hali hiyo imetokana na ushirikiano uliopo baina ya Serikali na MSD.

  "Kuhusu upatikanaji wa dawa kwa kweli hivi sasa hakuna mtu anayelalamika kwani serikali imeongeza fedha katika bajeti yake  karibia mara 10 kutoka sh.bilioni 30 mwaka 2015/16 hadi kufikia sh.bilioni 260 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo kwa wilaya yetu tunatumia zaidi ya milioni 600 kwa ununuzi wa dawa" alisema Burchard.

  Alisema wilaya hiyo ina kata 43, wakazi 750,000 wanaotoka kwenye visiwa ishirini na sita, huku ikiwa na vituo vya afya vitano, zahanati 27 na Hospitali teule moja ya Rubya.

  Naye Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kisiwa cha Mazinga, Johanes Sweetbert alisema licha ya usafiri wa majini kuwa na changamoto zake lakini dawa zote muhimu zimekuwa zikipatika na kuwa zahanati hiyo inahudumia vijiji viwili vya Iramba na Rubili ambavyo vina visiwa tisa ambavyo ni Rubili, Iramba, Mjunwa, Runenke, Magege, Garinzila, Kino, Mazinga na Buyonzi.

  Alisema mawasiliano mazuri kati ya MSD na serikali yamewezesha dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kufika kwa wakati ambapo hutumia boti kusafirisha dawa hizo pamoja na wagonjwa waliopewa rufaa kwenda hospitali ya wilaya.

  Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Afya wa Kisiwa cha Mazinga Winfrida Itaganisa amesema kamati ya afya imekuwa ikivuka kwenda Muleba kwa ajili ya kupokea dawa wanazokuwa wameomba na kufanya makabidhiano kabla ya kuvushwa.


  0 0

  Na WAMJW - KAGERA, NGARA

  Serikali kupitia Wizara ya Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yaendelea kuweka mikakati thabiti katika maeneo yote hatarishi ikiwemo mipakan na njia za panya ili kudhibiti ugonjwa wa Ebola kuingia nchini.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu leo wakati alipofanya ziara katika Mpaka wa Rusumo kati ya nchi ya Tanzania na Rwanda ili kuangalia ni jinsi gani Mkoa wa Kagera umejipanga katika kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kuingia nchini.

  Waziri Ummy amesema kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ambao umetokea eneo la Kivu katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo unaiweka Tanzania katika hatari zaidi ya kuweza kupata wagonjwa wa Ebola kutokana na muingiliano wa wananchi baina ya nchi hizo.

  "Mlipuko huo wa Ugonjwa wa Ebola ambao umetokea katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo sasa hivi inatuweka Tanzania katika hatari kubwa zaidi kupata wagonjwa kutokana na mlipuko huo kutokea eneo la Kivu Kaskazini ambalo ni karibu na Tanzania na muingiliano wa wananchi baina ya nchi hizi mbili ni mkubwa " Alisema Waziri Ummy Mwalimu.

  Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa Serikali inaendelea kutoa mafunzo kwa wahudumu wa Sekta ya Áfya ili kufahamu jinsi ya kuwahudumia wanaohisiwa kuwa na Virusi vya ugonjwa wa Ebola sambamba na hilo Serikali imeleta vifaa kinga watakavyovaa wakati wakitoa huduma kwa mgonjwa au mhisiwa wa ugonjwa wa Ebola.

  "Kama Serikali, kubwa ambalo tumelifanya ni kuhakikisha tunatoa mafunzo kwa watoa hudumu wa sekta ya Áfya nchini.kwa mujibu wa taarifa ya WHO nchini Kongo watoa huduma wa Áfya 9 wamepata ugonjwa wa Ebola huku mmoja amefariki" Alisema Waziri Ummy.

  Pia Waziri Ummy alimwagiza Mkuu wa mkoa wa Kagera kuhakikisha wanatenga Zahanati moja katika maeneo ya mipaka ambayo itakuwa inapokea wahisiwa au wagonjwa wa Ebola, vivyo hivyo kwa ngazi ya Wilaya kutenga hospitali kwa ajili ya wahisiwa pindi utapoingia nchini.

  Hata hivyo h Waziri Ummy amewataka wananchi wanaokaa katika vijiji vya mipakani ambavyo vinapokea watu kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na Burundi wamuonapo mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola wamwelekeze kufika kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya vilivyo jirani.

  " Wananchi ambao wanakaa mipakani hasa katika vijiji ambavyo vinapokea watu kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na Burundi mnaowajibu wa kuhakikisha mnafuata taratibu za uhamiaji, lakini pale ambapo mtu ameingia na ana dalili za ugonjwa wa Ebola muelekezeni aende kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya" alisema Waziri Ummy

  Kwa upande mwingine Waziri Ummy alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Áfya imeajiri Watumishi wapya wa Sekta ya Áfya 33 ambao wamesambazwa kwenye maeneo ya mipakani ili kusaidia kudhibiti ugonjwa wa Ebola usiingie nchini."Zuli ambalo tumelifanya, tumeajiri watumishi wapya wa Áfya 33 kwa ajili ya kuwasambaza katika maeneo haya ya mipakani ili kudhibiti ugonjwa huu wa Ebola usiingie nchini kwetu" alisema Waziri Ummy.

  Mbali na hayo Waziri Ummy amekiagiza kitengo cha Elimu ya Áfya kwa umma kutoka Wizara ya Áfya kutoa Elimu juu ya ugonjwa wa Ebola kwenye Serikali za vijijini kupitia Redio, vipeperushi, video jambo litalosaidia kuweka msukumo kwa wananchi ili kujua athari za ugonjwa huo kwa maendeleo ya Taifa.

  Mwisho Waziri Ummy aliendelea kuwatoa hofu wananchi wa Tanzania kuwa ugonjwa wa Ebola bado haujaingia nchini.
  Waziri wa Áfya Mhe Ummy Mwalimu akisisitiza jambo juu ya mikakati ya kudhibiti ugonjwa wa Ebola usiingie nchini wakati alipofanya ziara katika Mpaka wa Lusumo Wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera
  Afisa Afya wa kituo cha uhamiaji Mpaka wa Lusumo Stanley S. Chipasula akipokea maelekezo kutoka kwa Waziri wa Áfya Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara ya kuangalia utayari wa Kagera kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini kupitia Mpaka wa Lusumo.
  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera Dkt Marco Mbata (aliyevaa suti ya bluu) akimwelekeza jambo Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (wakatikati) Leo wakati alipofanya ziara katika Mpaka wa Lusumo Wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera
  Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akimwelekeza jambo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera Dkt Marco Mbata mikakati ya kudhibiti ugonjwa wa Ebola usiingie nchini, wakati alipofanya ziara katika Mpaka wa Lusumo Wilaya ya Ngara.Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ngara Luten Kanali Michael M.

  0 0


  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wa pili kulia, akiagana na mgeni wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeiwakilisha Marekani Bw. J. Steven Dowd (wa pili kushoto) Nje ya jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa AfDB Dkt. Alex Mubiru na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulikia nchi nane za Afrika Dkt. Nyamajeje Weggoro.
  Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeiwakilisha Marekani Bw. J. Steven Dowd ukiendelea katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akijadiliana jambo na Mwakilishi Mkazi wa AfDB nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru (kushoto) na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulikia nchi nane za Afrika Dkt. Nyamajeje Weggoro.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akisalimiana na Mgeni wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeiwakilisha Marekani Bw. J. Steven Dowd alipowasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam katika Mkutano ulioangazia ushirikiano wa Maendeleo kati ya Tanzania naBenki hiyo.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeiwakilisha Marekani Bw. J. Steven Dowd (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) baada ya Mkutano na waandishi wa habari kuhusu Ushirikiano wa Maendeleo kati ya Tanzania na AfDB uliofanyika Jijijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeiwakilisha Marekani Bw. J. Steven Dowd akieleza nia yake ya kuzungumza na Bodi ya Benki hiyo ili kuangalia namna ya kusaidia kutekeleza miradi ya kipaumbele nchini Tanzania ikiwemo ya Umeme na Reli alipokutana na kuzungumza na waandishi wa habari (Hawapo Pichani) Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeiwakilisha Marekani Bw. J. Steven Dowd na mwanyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wakielekea ukumbini kwa ajili ya Mkutano na waandishi wa Habari kuhusu Miradi inayotekelezwa kwa msaada wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) yenye thamani ya Sh. Trilioni 4.4.
  Mkurugenzi Mtendaji wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeiwakilisha Marekani Bw. J. Steven Dowd akisalimiana na Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga alipowasili nchini kwa mazungumzo na Mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb). (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

  …………………..

  Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

  Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinapewa fedha nyingi kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika kutekeleza miradi ya maendeleo katika Sekta ya Nishati, Maji, Kilimo na Barabara ili kuchochea uchumi na kutimiza malengo ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo mwaka 2025 ambapo mpaka sasa Benki hiyo imewekeza nchini zaidi ya shilingi trilioni 4.4.

  Hayo yamebainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeiwakilisha Marekani Bw. J. Steven Dowd katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango, alieleza kuwa Tanzania inapata fedha nyingi za kutekeleza miradi kutoka Benki ya AfDB kutokana na vipaumbele vya Benki hiyo kuendana na vipaumbele vya Serikali ya Tanzania katika Awamu ya Tano ya Uongozi wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

  “Miradi inayotekelezwa kwa fedha za AfDB ni pamoja na mradi wa kusafirisha umeme kutoka Mbeya, Sumbawanga hadi Nyakanazi utakao gharimu shilingi dola za Marekani milioni 123, miradi mingine ni ile ya ushirikiano na Sekta Binafsi (Dola Milioni 57.6m), ujenzi wa barabara ya Nyakanazi mpaka Burundi kupitia Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma na pia mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Msalato Jijini Dodoma ambao AfDB imeahidi kutoa shilingi bilioni 200 kwa kuanzia”, alieleza Dkt. Mpango.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeiwakilisha Marekani Bw. J. Steven Dowd, alisema kuwa ameona dhamira ya dhati ya Tanzania katika kufikia malengo tarajiwa hivyo anaangalia uwezekano wa kukaa na bodi ya Benki ya AfDB ili kuendelea kuisaidia Tanzania katika miradi mikubwa ya Nishati ya Umeme na Ujenzi wa Reli ya Kisasa.

  Pia ameahidi kuwashawishi wawekezaji kutoka Marekani kuja kuwekeza Tanzania kwa kuwa kuna mazingira mazuri ya uwekezaji na kuishauri Serikali kuweka mazingira mazuri zaidi ya kimikataba kati yake na wawekezaji ili waweze kuwa na uhakikak wa usalama wa uwekezaji wao.

  Aliahidi kutumia ushawishi wake katika masuala ya biashara na uwekezaji ili wafanyabiashara wengi kutoka nchji hiyo waweze kuwekeza mitaji na teknolojia hapa nchini na kuisaidia Tanzania kufikia malengo yake ya kukuza uchumi wan chi na watu wake.

  Alisema kuwa Rais wa Marekani Donald Trump ni mtu wa vitendo kuliko maneno na kuihakikishia Tanzania kwamba itapata ushirikiano mkubwa kutoka Serikali ya nchi hiyo ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais FDkt. John Pombe Magufuli za kujenga uchumi wan chi.

  Akieleza kuhusu maombi ya Serikali ya kutaka Benki yake isaidie ujenzi wa MIradi mikubwa ya Maendeleo ikiwemo ujenzi wa Reli ya kiwango cha Kimataifa-SGR, Mradi mkubwa wa kufua umeme kutoka Mto Rufiji, na miundombinu mbalimbali, Bw. J. Steven Dowd alisema kuwa wataijadili miradi hiyo ili kuangalia namna ya kuifadhili.

  Akizungumza na vyombo vya habari baada ya Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango na mgeni wake kumalizika, Mkurugenzi wa AfDB Kanda ya Afrika, Dkt. Nyamajeje Weggoro, alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki yenye hisa nyingi katika Benki hiyo hivyo kunufaika katika fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya Maendeleo.

  “Tanzania inahisa takribani asilimia moja kati ya asilimia tano zinazomilikiwa na nchi nane ikiwemo Uganda, Rwanda, Ethiopia, Kenya na Sudani Kusini na pia inatekeleza miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika yenye thamani ya Sh.Trilioni 4.4”, a;lieleza Dkt. Weggoro.

  Waziri Mpango amemshukuru Bw. Dowd kwa kuitembelea Tanzania na kuonesha dhamira ya kusaidia miradi ya maendeleo na akaahidi kuendeleza ushirikiano na Benki ya AfDB na pia Marekani.

older | 1 | .... | 1659 | 1660 | (Page 1661) | 1662 | 1663 | .... | 1898 | newer