Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1657 | 1658 | (Page 1659) | 1660 | 1661 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Na Frankius Cleophace Rorya.

  Mkurugenzi wa Halmashgauri ya Wilaya ya Rorya Mkoani Mara Charles Chacha ametupia lawana wazazi na walezi wilayani humo kwa kumaliza suala la kesi zinazohusu mimba kienyeji huku wakishawishi watoto wao kusema uongo jambo ambalo linakwamisha ushaidi ili kuwatia hatiani watuhumiwa kwa lengo la kumaliza changamoto hiyo.

  Akijibu hoja ya diwani viti maalum kata ya Robour Diana Charles kuhusu suala la waischana kupata mimba na kukatisha masomo yao, Mkurugenzi amesema kuwa kesi zipo lakini chagamoto kubwa ni wazazi na walezi kumaliza kesi zao na watumiwa kienyeji jambo ambalo linapoteza ushaidi ili polisi waweze kuendelea na kesi hiyo kwa lengo la kuwatia hatiani watuhumiwa hao.

  “Binti akiletwa polisi kuhojiwa anaambiwa na mzazi kuwa aseme alikutana na mwanaume sokoni akampa mimba kweli kwa kawaida mtu ukutane nae siku ya soko apo apo uwe na mahusiano akupatie ujauzito siyo kweli hivyo sasa wazazi na madiwani tushilikiane vyema kutokomeza suala hilo pia wazazi waondokane na suala la kumaliza kesi wenyewe jambo hilo linapoteza ushaidi na watoto wetu wanazii kuangamia ” alisema Charles.

  Akichangia hoja diwani wa viti maalum kata ya Rabour Diana Charles amesema kuwa Mikakati ambayo iliwekwa kipindi cha Nyuma takwimu za watoto kupata mimba zilishuka lakini kwa awamu hii ya robo ya tatu takwimu zimepanda tena ambapo watoto 18 wa shule za msingi na sekondari wilayani humo wamesitisha masomo kwa kupatiwa Ujauzito hivyo amesema kuwa kuna haja kubwa ya kuendeleza mikakati ya awali ili kupunguza takwimu hizo.

  Naye diwani wa kata ya Nyamagaro Ezra Masana amependekeza kuwa maofisa elimu sekondari na msingi ngazi ya kata wachukue jukumu la kufuatilia masuala ya mimbo kwa watoto wa shule na siyo jukumu hilo kuwaachia maofisa watendaji wa kata.

  “Ili jukumu la kufuatilia watuhumiwa wanaowapa watoto wetu mimba sasa maofisa elimu msingi na sekondari waweke mkazo na siyo kuwaachia jukumu hili watendaji wa kata kila mara wako mahakamani na kushindwa kufanya shughuli za utendaji” alisema Masana.

  Akichangia katika Sekta ya Elimu Diwani wa kata ya Koryo Peter Sarungi anabainisha kuwa suala la wanafunzi wa Shule za Msingi kutokujua kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) bado ni changamoto katika baadhi ya shule za msingi wilayani humo hivyo Madiwani wamesisitizwa kuleta taarifa hizo kwenye baraza la madiwani ili ziwezekufanyiwa kazi.

  “Kuna baadhi ya kata wamelta taarifa hizo zimo kwenye vitabu lakini wengine hawajaleta na mimi nilifanya ziara na kamati ya Elimu Afya na Maji lakini kuna baadhi ya shule wanafuzi zaidi ya Miambili darasa la kwanza mpaka la tatu hawajui KKK” alisema Peter.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Charles Chacha akisistiza suala watoto kupatiwa ujauzito amabapo anazidi kulaumu wazazi na walezi wilayani humo kumaliza kesi kienyeji na kusababisha kupotea kwa ushaidi ili kuwatia hatiani watuhumiwa.

  0 0

  Timu za mpira wa miguu za Wanawake ya Tanzania (waliovalia jezi nyeupe) na Burundi wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa mechi ya marudiano iliyofanyika katika uwanja wa Gitega, Burundi. Katika mpambano huo wa Tamasha la Michezo la Afrika Mashariki linaloendelea nchini humo Tanzania imeibuka na ushindi wa goli 5-0 dhidi ya Burundi katika

  Aidha, Tamasha la Michezo la Afrika Mashariki katika kipengele cha mpira wa miguu limekamilisha ratiba kwa mpambano kati ya Tanzania na Burundi, ambapo Tanzania imejishindia medali ya dhahabu kufuatia ushidi ilioupata. Burundi imejitwalia medali ya fedha kwa kushika nafasi ya pili katika mchezo huo.

  Katika mchezo wa awali Tanzania iliibuka na ushindi wa goli 8-1 dhidi ya Burundi.
  Timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Tanzania ikishangilia ushindi wa medali za dhahabu kufuatia ushindi wa goli 5-0 ilioupata dhidi ya Burudi katika Tamasha la Michezo la Afrika Mashariki 
  Sehemu ya mashabiki wakishangilia mchezo uliokuwa ukiendelea kati ya Tanzania na Burundi 
  Mmoja wa wachezaji wa timu ya Tanzania akipongezwa na Bw. Addo Komba Afisa kutoka Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo mara baada ya kuvishwa medali ya dhahabu 

  Picha na Matukio ya Mpira pete
  Timu ya mpira wa pete ya Tanzania ikiwa tayari kwa mchuano dhidi ya Uganda kwenye Tamasha la Michezo la Afrika Mashariki. Katika mchuano huo Uganda iliibuka na ushindi wa goli 53-33 dhidi ya Tanzania.Katika mchezo wa awali Tanzania iliibuka na ushindi mnono wa goli 79-14 dhidi ya wenyeji wa mashindano Burundi.
  Wachezaji wa timu ya Tanzania (walivalia jezi rangi ya waridi) wakijaribu kuzuia moja ya shambulio lililofanywa na timu pinzani ya Uganda 
  Mchezo wa mpira wa pete kati ya Tanzania na Uganda ukiendelea 
  Mshambuliaji wa timu ya Tanzania akilekeza mashambulizi kwa timu pinzani ya Uganda kwenye moja ya pambano la Tamasha la Michezo la Afrika Mashariki.

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva akiwasili kwenye uwanja lilipofanyika gwaride la wanafunzi. (kulia) ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Jitegemee, Robert Kessy.
  Kamanda mkuu wa gwaride, Stanrey Emmanuel akikabidhiwa zawadi na Mkuu wa Wiyala ya Temeke, Felix Lyaviva kwa kuliongoza vizuri gwaride hilo.
  Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
  Wazazi na walezi wa wanafunzi hao wakifuatilia gwaride hilo.
  Kikosi cha nne kikitoa heshima kwa mgeni rasmi kilipokuwa kikitembea kwa mwendo wa haraka.
  Gwaride la ukakamavu likipita mbele ya mgeni rasmi.
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva akimkabidhi zawadi Julieth Peter aliyekuwa kamanda wa kikosi namba tatu kwa kuongoza vizuri kikosi chake.
  Mkuu wa shule ya Sekondari ya Jitegemee, Robert Kessy akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva aliyekuwa mgeni rasmi.
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva, akihutubia.
  Gwaride likiendelea.


  Brass Band ya JKT ikiongoza Gwaride hilo.  Na Dotto Mwaibale

  MKUU wa Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, Felix Lyaviva amewashauri wanafunzi waliopo shuleni kujiandaa kujiajiri na siyo kuajiriwa baada ya kuhitimu masomo yao.

  Lyaviva ametoa rai hiyo leo alipokuwa akifunga mafunzo ya ukakamavu ya wanafunzi wa Kidato cha Tano 2018 wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee ya jijini Dar es Salaam.Akiwahutubia wanafunzi hao mbele ya wazazi, walimu, maafisa wa jeshi wakiwemo wastaafu na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo, Lyaviva alisema;

  "Nawapongeza sana kwa mafunzo ya ukakamavu mliyopewa, mmeonesha ni jinsi gani mlivyoiva lakini niwaombe muwe na ndoto za kujiajiri siyo kuajiriwa mara mtakapotoka hapa."Mkuu huyo wa wilaya, amewaasa wanafunzi kutojihusisha na vitendo vya mapenzi, uvutaji wa madawa ya kulevya na sigara ambavyo vinaathari kubwa katika maisha.

  "Nyie wanafunzi wa kike, nawaasa msikubali kurubuniwa na wenzetu wa kiume kwani athari zake ni kupewa mimba ambazo zitawaharibia maisha yenu huku wao wakiendelea na masomo," alisema Lyaviva.Aliongeza kuwa, ni vyema wanapotongozwa wakatoa taarifa kwa walimu wa nidhamu ili vijana wenye tabia hiyo washughulikiwe na siyo kuwachekea.

  Kuhusu suala la kujiajiri, aliwashauri wanafunzi wawaeleze wazazi wao nini wanapenda kufanya maishani mwao ili wazazi wawaunge mkono kwa kuwaandalia mazingira ya kutimiza ndoto zao hizo."Kama unapenda kumiliki shule ya awali, wape wazo lako wazazi wako ambao wanaweza kukuunga mkono kwa kukujengea darasa moja halafu hapo baadaye ukaendelea mwenyewe, msiwaze kabisa suala la kuajiriwa," alisema.

  Aliongeza kuwa, hawawezi kutimiza ndoto zao kama hawatakuwa na hofu ya Mungu na kuzifuata amri zake kumi ambazo zipo kwenye vitabu vyote vitakatifu."Mkisoma kwa bidii huku mkiwa na hofu ya Mungu na kutimiza amri zake kumi, mtafanikiwa maishani mwenu, lakini mkienda kinyume mtakwama," alisema mkuu huyo wa wilaya.

  Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Kanali Robert Kessy akimkaribisha Lyaviva aliyekuwa mgeni rasmi, alimshukuru kwa kukubali kufika kufunga mafunzo hayo.Kessy alimfahamisha mkuu huyo dhumuni la mafunzo hayo kwa wanafunzi kwamba ni kuwaweka katika hali ya ukakamu, kuwa na nidhamu, afya nzuri na kuwa wazalendo kwa nchi yao."Mafunzo haya yalianza rasmi mwaka 1985 yalikuwa ya wiki mbili na yaliongozwa na makamanda wetu, lakini ilipofika mwaka 2003 ndipo wanafunzi walipoanza kujiongoza wenyewe kama unavyoona," alisema Kessy.

  Gwaride hilo lililowahusisha wanafunzi wa kiume na wakike lilikuwa na vikosi nane pamoja na kikosi maalum cha ukakamavu 'komandoo' liliongozwa na Stanrey Emmanuel.

  0 0


  0 0

  Idara ya Habari-NEC

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo wa Jimbo la Liwale Mkoa wa Lindi, kufutia kujiuzulu kwa alieyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Ndugu. Zuberi Mohamed Kuchauka.

  Kujiuzulu kwa Mbunge huyo ambaye alijiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kunamfanya apoteze sifa ya kuwa mbunge na hivyo kulifanya jimbo hilo kuwa wazi.

  Akitangaza uchaguzi huo Jijini Dar es Salaam leo (Agosti 25, 2018), Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage amesema tangazo la uchaguzi linakuja baada ya Tume kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  “Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, ameitaarifu Tume kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Liwale Mkoa wa Lindi, kuanzia tarehe 13 Agosti, 2018, kufuatia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Ndugu Zuberi Mohamed kujiuzulu uanachama wa Chama cha Wananchi – CUF, na hivyo kupoteza sifa ya kuwa Mbunge,” amesema.

  Jaji Kaijage aliongeza kuwa “…kwa mujibu wa vifungu vya 37 (1) (b),(5) na 46 (2) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Tume inatoa taarifa kwa Umma kuwa Jimbo la Liwale lipo wazi..”

  Akizungumza juu ya ratiba ya uchaguzi huo mdogo, Mwenyekiti huyo wa Tume alisema, kutoa fomu za uteuzi itakuwa kati ya tarehe 07 hadi 13 Septemba mwaka huu, uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 13 Septemba mwaka huu, kampeni za uchaguzi zitaanza tarehe 14 Septemba na kumalizika tarehe 12 Oktoba mwaka huu na siku ya uchaguzi itakuwa tarehe 13 Oktoba mwaka huu.
  “Tume inavikumbusha vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi, miongozo, na maelekezo yote wakati wa kipindi cha uchaguzi huo mdogo,” Jaji Kaijage amesema.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Ngukumo, Kata ya Nkiniziwa Wilayani Nzega, Mkoani Tabora kuhusu changamoto kubwa inayokabili Kijiji hicho ya ukataji ovyo wa rasilimali za misitu. Waziri Makamba ametoa wito wa wananchi hao kuweka ulinzi madhubuti.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Mazingira ya Kijiji cha Ngukumo na kuwakumbusha wajibu wao katika kusimamia mazingira. Waziri Makamba amewataka kutumia kutumia Sheria ndogo ndogo za Kijiji kunusuru mazingira yao

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akipanda mti kuunga mkono jitihada za upandaji miti kwa wakazi wa Kijiji cha Nkiniziwa. Mti huo pia ameukabidhi kwa mtoto Masoud Maganga ili aweze kuutunza kama kielelezo cha kutunza mazingira.
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwambaha, Wilayani Nzega wakijibu maswali mbalimbali ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba mara baada ya kutembelea Shule hiyo kupanda miti na kuimarisha Club ya Mazingira Shuleni hapo kwa kuiwezesha kuanzisha kitalu cha miche ipatayo Elfu tano.

  ……………….

  Changamoto kubwa inayoikabili Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora ni uharibifu mkubwa wa mazingira utokanao na uvunaji holela wa rasilimali za misitu na shughuli za kilimo.

  Hayo yamesemwa hii leo na Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bw. Godfrey Ngukuwa wakati akiwasilisha taarifa ya Wilaya yake kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba katika Kijiji cha Ngukumo na Mwambaha, Wilayani Nzega.

  “Wilaya yetu imekuwa na ongezeko kubwa la wavamizi kutoka Mikoa jirani wanaojihusisha na shughuli za ukataji miti kwa ajili ya kuchoma mkaa na kilimo kisichoendelevu, kwa kiasi kikubwa wanachangia uharibufu wa Mazingira, kwa kuwa hivi sasa Nzega imekuwa soko la Mkaa kwa Shinyanga na Mwanza” alisisitiza Bw. Ngukuwa

  Akielezea jitihada zilizofanywa na Ofisi yake Bw. Ngukuwa amesema kuwa doria za mara kwa mara zianaendelea Kijiji hapo kwa kushirikiana na wananchi wenyewe kubaini wavamizi hao.

  Nae Waziri mwenye dhamana ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Nchini Mhe. January Makamba amewataka wakazi wa vijiji hivyo kuwa wakali kwa rasilimali zao na kuhakikisha mazingira kwa ujumla wake yanatunzwa kwa sheria kali zaidi.

  Pia, ameagiza kufanyika kwa operesheni kali na kuwachukulia hatua wale wote wanaojihusisha na uharibifu huo. “Ndugu zangu sina budi kuwakumbusha kuwa siku hizi kuna wakimbizi wa Mazingira, watu wanaharibu mazingira katika maeneo yao na kuhamia maeneo mengine, jitihada za maendeleo zote hazitakuwa na maana kama hatutatunza mazingira” Makamba alibainisha.

  Waziri Makamba amewaeleza wakazi wa Vijiji vya Ngukumo na Mwambaha kuwa na uhifadhi wenye tija ni ule ambao wananchi wako tayari kushiriki kwa nguvu zote. Katika kuunga mkono shughuli za maendeleo, Waziri Makamba amechangia kiasi cha Shilingi Milioni Moja kwa ajili ya Ujenzi wa Zahanati na matundu ya Choo katika Shule ya Msingi Mwambaha.

  Waziri Makmaba amehitimisha ziara yake Mkoani Tabora na amewasili Mkoani Geita ambapo atatembelea Kisiwa cha Magafu.

  0 0

  Na Frankius Cleophace Tarime.

  Mabinti 40 ambao wako nje ya mfumo rasmi wa shule kutoka kata tano wilayani Tarime Mkoani Mara wamepatiwa mafunzo ya ujasiramali kwa lengo la kuongeza mbinu, sifa na dhana bora katika kufanya shughuli zao za baishara ili kujikwamua kiuchumi kwa lengo la kuondokana na utegemezi.

  Mabinti hao baadhi yao hawakubahatika kwenda shule na wengine wao wamekatisha masomo kwa kupatiwa ujauzito wakiwa shuleni ,wengine kuolewa katika umri mdogo kutokana na mila na desturi ukiwemo ukeketaji kwa mtoto wa kike, huku wengine wakiwa kwenye ndoa japo wameolewa katika umri mdogo, na baadhi wameshindwa kumudu ndoa hizo na kuachika hapa kilio chao kikubwa ni kuomba Serikali kwa kushirikiana na shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Tarime kuwapatia Mitaji pamoja na Malighafi baada ya kupatiwa ujuzi.

  Magreth Kichele kutoka kata ya Komaswa ameiomba serikali kwa kushirikiana na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto kuwapatia malighafi pamoja na vifaa ili waweze kujitegemea na kuendeleza biashara zao huku wakionyesha tofauti baada ya kupatiwa elimu hiyo ya siku tatu na kuhaidi kwenda kufanyia kazi elimu hiyo waliyopewa.

  “Sisi tunaishi vijijini tunamaisha magumu sasa kama tumepatiwa elimu changamoto kubwa ni mitaji wengine wanavyereani hawana pesa za kununu malighafi hivyo sasa shirikal na serikali wakishirikiana wakatusaidia tutashukuru sana” alisema Magreth.

  Kambibi kamugisha kutoka Shirika la jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Tarime anasema kuwa kwa kushirikiana na shirika la Plan Internationa Tanzania chini ya ufadhili wa Shirika la umoja wa ulaya pamoja na Shirika la maendeleo ya Sweden (Sida) wamelenga kuwakomboa mabinti haoa ambao wako njee ya mfumo wa shule kupitia klabu ambazo zimeundwa na shirika hilo.

  Kambibi amesema kuwa wao kama shirika kupitia mradi huo wanafanya katika kata tano ikiwemo kata ya Binagi , Regicheri,Pemba,Komaswa, na Mbogi ambapo pia kupitia kata hizo wameunda klabu mbalimbali ambazo utumika kutoa elimu ya kupiga vita ukatili wa kijinsia ukiwemo ukeketaji kwa mtoto wa kike.

  Kamugisha ameongeza kuwa lengo kubwa la kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali mabinti hao na kisha kuwasaidia katika kuongeza sifa, Dhana na mbinu bora katika suala zima la ujasiriamali ili kuendeleza biashara zoa kwani baadhi yao ni wajasiriamali wadogowadogo. “Pia sisi kama shirikal tumekuwa tukisaidia mabinti hawa vifaa mbalimbali kama ni mafundi vyereani tunawapatia, wanaofanya shughuli za mighahawa tunawapatia vifaa, tunasaidi vikundi kulingana na kazi wanazozifanya” alisema Kamugisha.

  Aidha kambimbi ameongeza kuwa licha ya kupatia Elimu ya ujasirimali tayari mabinti hao wamepatia elimu ya kupinga suala la Ndoa za Utotoni,mimba za utotoni, kwani kupitia klabu hizo mabinti hao wamekuwa mabalozi wazuri kuendelea kutoa elimu hiyo kupitia Mikutano, Mashuleni,na Makanisani lengo ni kumaliza Ukatili wa kijinsia ukiwemo ukeketaji ambao ni chanzo kikubwa kukwamisha ndoto za mabinti hao.

  “Mabinti hawa baadhi yao wameshindwa kutimiza ndoto zao za kupata elimu kwa sababu mbalimbali mfano changamoto za kifamilia, Umaskini, Ndoa za Utotoni na Mimba za utotoni vimekuwa chanzo kikubwa cha kuzidi kufifisha ndoto za watoto wa kike hapa nchini japo jitiada za Mashirika likiwemo shirika la CDF Tarime na Maeneo mengine tukakofanya kazi tunaendelea kusaidia mabinti hawa” alisema Kambibi.


  Kambibi Kamugisha kutoka shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Tarime akitoa ufafanuzi jinsi mafunzo hayo yalivyotolewa kupitia Shirikal hilo kwa kushirikiana na Shirika la Plan Internation Tanzania chini ya Ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Sweden (Sida) pamoja na Shirika la Umoja wa Ulaya.
  Washiriki wa Mafunzo hayo ambao ni mabinti 40 kutoka kata tano Halmashauri ya Tarime Vijijini wakiendelea kupatiwa elimu ya ujasiraimali.

  Picha ya pamojana washiriki wa mafunzo hayo baada ya kupatiwa elimu ya ujasiriamali.Kambibi Kamugisha kutoka shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Tarime akitoa ufafanuzi wa jambo katika Mafunzo hayo ya siku tatu katika ukumbi wa MCN Mjini Tarime Mkoani Mara.

  0 0


  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Marko Mbata, akizungumza na waandishi wa habari mjini Bukoba mkoani Kagera jana, kuhusu kuhimarika kwa upatikanaji wa dawa mkoani humo ambapo alisema anatamani Rais Magufuli aendelee kuongoza nchi milele.
  Mfamasia wa mkoa huo, Pyuza Daniel akizungumza kwenye mkutano huo.
  Na Dotto Mwaibale, Kagera

  MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Marko Mbata ameishukuru Serikali kwa kutenga bajeti kubwa ya dawa nchini ambayo imewezesha upatikanaji wa dawa kuimarika nchini ambapo kwa sasa upatikanaji wa dawa mkoani Kagera umefikia asilimia tisini na nane.

  Mbata alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na ambao wapo ziarani mkoani Kagera kuangalia taratibu za usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenye vituo vua kutolea huduma za afya mkoani Kagera.

  "Kwa kazi kubwa ya kuongeza bajeti ya dawa tangu alipoingia madarakani, natamani Rais Magufuli angeendelea kuongoza milele bila kufikia ukomo, kwani hii imeboresha kwa kiasi kikubwa sana hali ya upatikanaji wa dawa nchi nzima" alisema Mbata.

  Amesema kwa wao kama wataalamu, walikuwa wakikwazika sana miaka ya nyuma pale mwananchi alipokuwa anakuja kupata matibabu na kukosa dawa, hivyo kwa hali ya sasa wanawahudumia wananchi vizuri na malalamiko ya wananchi yamepungua.Ameipongeza MSD kwa kuweza kununua dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji na kubadilisha vifungashio vya dawa kutoka kwenye makopo na kuziweka kwenye blister.

  Katika hatua nyingine Dkt. Mbata aliishukuru MSD kwa kujenga kituo cha mauzo wilayani Muleba kwani imewarahisishia watoa huduma wa afya kuwa karibu zaidi na MSD tofauti na ilivyokuwa awali walipokuwa wanapata huduma kutoka Mwanza.

  Kwa upande wake mfamasia wa mkoa huo, Pyuza Daniel alisema licha ya maeneo ya vituo vya afya na zahanati yanapatikana visiwani,lakini kwa kushirikiana na MSD, wananchi na halmashauri dawa zimekuwa zikiwafikia walengwa kwa wakati.

  "Kwa kweli lazima niwapongeze MSD kwa kazi kubwa wanayoifanya kwani sasa hivi wameboresha huduma, kikubwa waongeze idadi ya dawa ambazo zinakosekana kwenye orodha ya dawa ya sasa ili mgonjwa akifika kutibiwa kwenye aweze kuzikuta" alisema Daniel.

  0 0

  Na Shani Amanzi,Chemba

  MKUU wa Wilaya ya Chemba Saimon Odunga amewataka wananchi wa kitongoji cha Lalalami katika Kijiji cha Itolwa waache mara moja mgogoro wa kung’ang’ania kuwa wapo eneo la Wilaya ya Kiteto.

  Badala yake amewataka wajue kabisa bado wapo wilayani Chemba kwani Serikali inafata ramani ambayo inatambulika.

  Odunga amesema wanatambua kabisa kitongoji cha Lalalami kipo mpakani kati ya Wilaya ya Chemba na wilaya ya Kiteto ambapo mgogoro ulianza kuanzia mwaka 2012 na mwaka 2016 kupitia Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia vifungu vyake vya sheria ya ardhi waliamua Kitongoji cha Lalalami kuwa wilayani Chemba."Lakini bado wananchi wakakataa maamuzi hayo na ukweli ndiyo huo. Leo hii ni mara ya tatu mwaka 2018 Serikali imeamua kukaa chini na wananchi tena kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Magesa ,Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Chemba na Kiteto .

  "Wataalam wa Halmashauri za Wilaya zote na kufanya maamuzi ya pamoja ya kuzuia kabisa mgogoro huo wa mara kwa mara wa wananchi kukataa kuwa eneo la Serikali ya Wilaya ya Chemba na atayekwenda kinyume hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa sababu serikali haiwezi kupoteza muda na fedha kusuluhisha mgogoro ambao ukweli unajulikana,” amesisitiza Odunga.

  Aidha Odunga amesema “tunajua sababu kubwa ni shughuli za kiuchumi ambapo jamii iliopo inafanya shughuli za ufugaji na mnataka kujumuika na jamii yenzenu ya Kiteto ya Ufugaji lakini wilaya ya Chemba wengi wao ni wakulima." Lakini mkumbuke jamii zote hizi mbili za wakulima na wafugaji zipo wilayani Chemba na huwa wanafata kanuni na taratibu za ufugaji na kilimo ili kuzuia migogoro ya ardhi,wakulima na wafugaji ambapo ni janga la nchi nzima,"amesema.

  Odunga alifanya ziara ya siku moja kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Magesa ambayo ilikuwa Agosti 21 mwaka huu ambapo walikuwa wanasuluhisha mgogoro kati ya wilaya na wilaya kati ya Chemba na Kiteto.
  MKUU wa Wilaya ya Chemba Saimon Odunga akizungumza na Wanachi wa kitongoji cha Lalalami katika Kijiji cha Itolwa,kuhusua kuacha mara moja mgogoro wa kung’ang’ania kuwa wapo eneo la Wilaya ya Kiteto,na badala yake amewataka wajue kabisa bado wapo wilayani Chemba kwani Serikali inafata ramani ambayo inatambulika.Katika mkutano huo DC wa Chemba aliambatana na DC wa Kiteto pamoja na maofisa mbalimbali wa wakiwemo wa Ulinzi na usalama,kuhakikisha mgogoro huo unatatuliwa.  Baadhi ya wananchi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa kitongoji cha Lalalami katika Kijiji cha Itolw,wilayani Chemba

  0 0


  0 0

  WAZAZI kote nchini wametakiwa kuacha kulalamikia wadau wa elimu na badala yake wameshauriwa kushirikiana na walimu kukagua madaftari ya watoto wao kwa lengo la kuongeza ufaulu ili kupunguza mimba za utotoni zinazosababisha ndoto zao kushindwa kufikiwa. 

  Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati halfa ya kukabidhiano ya madawati na viti vyake 40 aliyoyatoa kwenye shule ya Sekondari Toledo ya Jijini Tanga. 

  Ummy ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama cha Mapinduzi {CCM) mkoa wa Tanga alisema kimsingi wazazi wanapaswa kutambua kufanya hivyo kutawasaidia kuwawezesha vijana wao kuongeza ufaulu na hivyo kufanikiwa kuepukana na vishawishi ambavyo wanakabiliana navyo wakati wakiwa shuleni. 

  “Ndugu zangu wazazi na walezi lazima tutambue jukumu letu la kufuatilia maendeleo ya watoto wetu kwani hii ndio njia pekee inayoweza kuwasaidia kwa kushirikiana na walimu wao kwa lengo la kuwezesha kufikia ndoto zao”Alisema. Naye ka upande wake Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa aliwataka wanafunzi kutumia fursa hiyo kuongeza jitihada kwenye kusoma ili azma ya serikali ya kuongeza ufaulu kwa shule zake iweze kufikiwa. 

  “Ndugu zangu wanafunzi mmepata madawati haya yatumieni vizuri kwenye matumizi yaliyokusudiwa kwa lengo la kuwawezesha kufikia malengo yenu kwa kuongeza ufaulu “Alisema. Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Sekondari Toledo Daudi Nchia alimshukuru Waziri Ummy kwa msaada huo na kuongeza kuwa bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa matundu ya vyoo vya wasichana . 

  Alisema kutokana na uhaba huo umesababisha wasichana na wavulana kushiriki katika huduma hiyo.
   WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga{CCM) kulia akimkabidhi madawati 40 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Toledo ya Jijini Tanga Daudi Nchia ikiwa ni mkakati wake wa kukabiliana na uhaba uliopo
   WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga{CCM) kushoto akiwa amekaa kwenye moja ya madawati 40 aliyokabidhi kwa shule ya Sekondari Toledo Jijini Tanga 
   WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga{CCM) katika akiwa na Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Toledo Daudi Nchia mara baada ya kuwakabidhi madawati 40
   WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga{CCM) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Toledo mara baada ya kuwakabidhi madawati 40

  0 0

  Na Grace Semfuko-MAELEZO

  Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amewataka Maafisa Habari Nchini kufanya kazi zao kwa kufuata sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 ambayo inawapa fursa Waandishi wa Habari kupata,kuhariri na kurusha habari kwa wananchi ili waweze kuelewa maendeleo ya nchi yao.

  Ameyasema hayo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti Jijini Dar Es Salaam Ijumaa Agosti 24, 2018 alipotembelea Kampuni ya Magazeti ya New Habari na Shirika la Habari linalounganisha Redio zenye Maudhui ya kijamii la TADIO ambao walimweleza Msemaji Mkuu wa Serikali kuhusiana na changamoto za kupata habari wanazofanyiwa na baadhi ya Maafisa Habari wa Taasisi mbalimbali za Serikali Nchini.

  “Ni kweli wapo baadhi ya Maafisa Habari ambao wanakwamisha juhudi za waandishi kupata Habari,Idara ya Habari MAELEZO tumeliona hilo na tulishaanza mkakati wa kuhakikisha kila taasisi inatoa habari ili wananchi waelewe maendeleo ya maeneo yao na taasisi hizo, tumekaa na Maafisa Habari mara kadhaa na tumewapa mafunzo na sasa changamoto hiyo imepungua kwa kiasi kikubwa” alisema Dkt Abbasi.

  Sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge Novemba 5 Mwaka 2016 na Kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Novemba 16 mwaka huo huo wa 2016, pamoja na mambo mengine, inalenga kulinda maslahi ya waandishi wa habari,kulinda kazi zao pamoja na kuboresha Taaluma hiyo ili iweze kuheshimika kama taaluma ilivyo kwa zingine.

  Aidha Dkt. Abbasi amezungumzia mkakati wa kuanzishwa kwa mfuko wa taaluma ya habari ili kuwawezesha waandishi kumudu kufanya kazi za utafiti wa habari na vipindi mbalimbali vya kijamii badala ya kutegemea ruzuku za mashirika ambazo pia huja kwa masharti ambayo mengi yanaweza kuwaingiza hatiani.

  Aidha Dkt. Abbasi pia amewakumbusha Waandishi wa Habari nchini kujiunga na vyuo mbalimbali ili kujiendeleza kitaaluma na hatimaye waweze kuendana na kanuni ya kuwa na diploma itakayoanza kutumika mwishoni mwa mwaka 2021.

  “Kanuni ya kumtaka mwanahabari awe na diploma kwenda juu katika fani ya habari itaanza kutumika mwaka 2021, tumetoa muda wa kutosha kabisa kwa waandishi kujiendeleza,kama hukufanya hivyo sheria haitakuruhusu kupata ithibati ya kuendelea na majukumu ya kazi za Habari,” alisisitiza Dkt. Abbasi.

  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari-MAELEZO ambaye pia anashughulikia Usajili wa Magazeti Bw. Patrick Kipangula amesema Sheria mpya ya Habari inalenga kuimarisha kazi za Waandishi ili waweze kuheshimika na sio adhabu kama wengi wanavyoitafsiri na kuongeza kuwa Sheria hiyo imeweka bayana namna ambavyo Waandishi wa Habari watakavyonufaika nayo.

  Amesema lengo ni kuwafanya waandishi wa Habari kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa na kuhoji kuwa ni “kwa nini taaluma zingine ikiwemo ya Sheria,Udaktari na nyinginezo ziheshimike na sio kwa taaluma ya Habari? Ni lazima tuifanye taaluma hii iheshimike” Alisema Kipangula.

  Kwa upande wake Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari Absalom Kibanda ameipongeza MAELEZO kwa mageuzi makubwa katika kuisemea Serikali na kuongeza kuwa Sheria ya Huduma za Habari imekuwa ni chachu kubwa ya Waandishi wengi wa Habari kuamua kwenda kuongeza elimu na kwamba wanaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuimarisha taaluma hiyo nchini kwa kuwaruhusu Wafanyakazi wao kujiendeleza kimasomo.

  Kibanda pamoja na mambo mengine alizungumzia changamoto ya upatikanaji wa matangazo ya Serikali ambayo kwa kiasi kikubwa alidai yamewaathiri kiuchumi ambapo Dkt Abbas alitumia ziara hiyo kufafanua kuwa unaandaliwa utaratibu mpya wa kuhakikisha matangazo ya taasisi za Serikali yanatolewa kwa ufanisi.

  “Matangazo ya taasisi za Serikali yalikuwa yakitolewa kiholela tu na yalikuwa yakiisababishia Serikali madeni makubwa,ukiangalia mfumo wa utoaji wa matangazo yenyewe utashangaa,mtu anakutana na kiongozi barabarani anamwambia atoe tangazo na analitoa, hii ilikuwa changamoto kubwa kwa sababu baadhi ya matangazo hayo hayakuwa kwenye Bajeti na hivyo kutengeneza madeni yasiyolipika,” alisema Dkt. Abbasi.

  Ziara ya Dkt. Abbasi kwenye taasisi hizo za Habari ilikuwa ni ya kujifunza na kutoa mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano wa kushirikiana na vyombo vya Habari katika kusimamia taaluma na kutangaza maendeleo ya nchi.

  0 0


  0 0  Afisa Madini Mkazi wa Mirerani, Mhandisi David Ntalimwa, akieleza jambo wakati akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ushauri na Uchambuzi wa Kazi kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Nolasco Kipanda, akiwasilisha mada kuhusu Muundo na Majukumu ya Wizara ya Madini na Tume ya Madini.
  Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa, akieleza jambo wakati akiwasilisha mada kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
  Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini pamoja na Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Madini wakifuatilia uwasilishaji wa mada mbalimbali zilizotolewa kwa kamati ya Bunge.
  Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini pamoja na Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Madini wakifuatilia uwasilishaji wa mada mbalimbali zilizotolewa kwa kamati ya Bunge.

  Na Asteria Muhozya, Dodoma

  Serikali imesema inafanya utaratibu wa kuwa na Hati ya Utambulisho wa Kimataifa wa Madini ya Tanzanite, ambayo yanapatikana katika nchi ya Tanzania pekee katika vilima vya Mirerani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara.

  Hayo yamebainishwa leo tarehe 25 Agosti na Waziri wa Madini Angellah Kairuki wakati wa Semina ya mafunzo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo imefanyika Makao Makuu ya Wizara, jijini Dodoma.

  Waziri Kairuki amesema kuwa, serikali inataka kuona kuwa dunia inafahamu kuwa, madini hayo yanapatikana Tanzania pekee na kuhakikisha kwamba yanajulikana zaidi.

  Semina ya wabunge imefanyika kufuatia maelekezo ya Kamati hiyo ambayo ilitaka kufahamu kuhusu mwenendo mzima wa Madini ya tanzanite, biashara na udhibiti wa madini hayo baada ya kujengwa kwa Ukuta wa Mirerani unaozunguka migodi ya madini ya tanzanite, Muundo wa Wizara ya Madini, Tume ya Madini na majukumu yao.

  Waziri Kairuki amesema kuwa, Wizara imepata fursa ya kuwasilisha kwa Kamati hiyo taarifa za utekelezaji wa majukumu mbalimbali ikiwemo mikakati ya serikali katika kudhibiti utoroshaji wa madini hayo na mipango madhubuti ambayo serikali inakusudia kuifanya ili kuhakikisha kwamba rasilimali madini inalinufaisha taifa na hatimaye sekta ya madini iweze kufikia asilimia 10 ya machango wake katika pato la taifa ifikapo mwaka 2025.

  Ameongeza ni kikao ambacho kimekuwa na manufaa kwa upande wa Serikali kwa kuwa imetoa elimu kwa Kamati hiyo kuhusu yale ambayo serikali imefanya na inayokusudia kufanya kuhusuiana na madini ya tanzanite lakini pia serikali imepata wasaa wa kupokea maoni, mapendekezo na maelekezo kutoka kwa wabunge ambayo yatawezesha kupeleka mbele sekta ya Madini.

  Mbali ya tanzanite, Waziri Kairuki amewaeleza wabunge hao kuhusu mkakati wa serikali kuanzisha Mineral Exchange ambapo amesema tayari wizara imeshaandaa timu ya wataalam ili kwenda kujifunza na kufanya utafiti katika nchi nyingine ili suala hilo liweze kufanyika kwa ubora .

  Pia, ameeleza kuwa, Wabunge wa Kamati hiyo, wamepata fursa ya kufahamu majukumu ya Wizara baada ya kuundwa kwa Tume ya Madini, majukumu ya tume ya madini na mahusiano ya kiutendaji kati ya Tume na Wizara.

  Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mariam Ditopile, amesema kuwa, kamati imebaini kuwa, Serikali imechukua hatua nyingi za kulinda na kudhibiti madini ya tanzanite ikiwemo kudhibiti utoroshaji wa madini hayo. “Kama kamati tumeona mnyororo mzima wa thamani ya madini ya tanzanite, awali tulikuwa hatunufaiki kama taifa,” amesema Ditopile.

  Awali, akiwasilisha mada kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kudhibiti utoroshaji wa madini ya tanzanite na usimamizi wa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini ndani ya ukuta, Afisa Madini Mkazi wa Mirerani Mhandisi David Ntalimwa, amezungumzia sababu za kushuka kwa mapato na kueleza kuwa, kunategemea kiwango cha ubora na sifa za madini husika.

  Ameongeza kuwa, kutokana na mazingira hayo, kiwango cha thamani ya madini na tozo ya mrabaha kitakuwa tofauti kutegemea na mwezi na uzalishaji uliopo.

  Akizungumzia sababu za utoroshaji wa madini ya tanzanite, Mhandisi Ntalimwa amesema kuwa, zinatokana na uwezo mdogo wa kusanifu na kuongeza thamani na kunga’risha madini ya vito na hivyo watu kutamani kuuza tanzanite ghafi.

  Pia, amesema utoroshaji wa madini unatokana na kukwepa kulipa kodi na tozo mbalimbali zinazotozwa na serikali ili kujipatia faida kubwa, kuwepo kwa raia wa kigeni nchini wanaofanya biashara ya madini kinyume na sheria kwa kushirikiana na wazawa na kukosekana kwa masoko ya uhakika ya kuuzia madini yanayozalishwa.

  Akizungumzia hatua zilizochukuliwa na serikali katika kudhibiti utoroshaji wa madini baada ya kujengwa ukuta amesema kuwa, serikali imeimarisha ulinzi na ukaguzi getini kwa kutumia vikosi vya ulinzi na usalama, kuzuia magari kuingia na kutoka ndani ya ukuta, watu kuingia ndani ya ukuta kwa vitambulisho maalum.

  “ Sasa watu wanaingia kwa utaratibu maalum tofauti na walivyozoea awali. Ukuta umeleta utaratibu mzuri na si kero, kama baadhi ya watu wanavyodhani,” amesisitiza Ntalimwa.

  Amezitaja hatua nyingine kuwa ni pamoja na kuzuia Mabroker kwenda migodini na badala yake kutakiwa kusubiria madini getini, uthaminishaji madini kufanyika ndani ya ukuta na serikali kujenga jengo lenye ofisi ya ukaguzi, uthaminishaji na ukumbi wa mabroker ndani ya ukuta.

  Aidha, pamoja na kushiriki semina hiyo, pia wabunge hao wamepata fursa ya kutembelea Makumbusho ya Taifa ya Jiolojia na Madini katika Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania, (GST).

  0 0

   Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kakunyu, Auston Martin (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari ambao wapo katika ziara ya kuangalia taratibu za usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenye vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Kagera jana. Kulia ni Mwanahabari Peter Saramba.
   Meneja wa MSD Kituo cha Muleba, Egidius Rwezaura, akikagua dawa katika stoo ya kuhifadhi dawa ya zahanati hiyo ya Kakunyu. Kushoto ni Muuguzi Msaidizi wa zahanati hiyo, Devotha Kamugisha.
  Majengo ya Zahanati ya Kata ya Kakunyu.


  Na Dotto Mwaibale, Kagera

  Kupatikana kwa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa wakati kwenye vituo vya afya nchini kunasaidia sana kupunguza malalamiko ya wananchi na kudhibiti magonjwa ambayo yanaweza kuzaa usugu kwa wagonjwa kutopata dawa kwa wakati. 

  Hayo yameelezwa na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kakunyu, Auston Martin, wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao wapo katika ziara ya kuangalia taratibu za usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenye vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Kagera.

  "Kupatikana kwa dawa muhimu kwa wakati katika zahanati yetu kumesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza magonjwa mawili makubwa ya malaria na yale ya zinaa yaliyokuwa yanasumbua eneo hili kwa muda mrefu" alisema Martin

  Dkt. Martin alisema kwamba hivi sasa dawa wanazozipata kutoka MSD zinapatikana kwa asilimia 94 ukilinganisha na awali, hivyo kuwa faraja kwa wananchi wanao pata huduma za matibabu katika zahanati hiyo.

  Alitaja magonjwa ya zinaa yanayosumbua katika eneo hilo kuwa ni kaswende na kisonono na hali hiyo inasababishwa na wananchi kuona aibu kwenda kuchukua mipira ya kiume (kondomu) na uelewa mdogo kuhusu matumizi ya mipira hiyo, hivyo wanaangalia utaratibu wa kuwawezesha wananchi kupata zana hiyo kwa njia itakayokuwa rahisi kwao kuzipata.

  Martin alitaja sababu nyingine kuwa ni muingiliano wa watu kutoka nchi jirani ya Uganda Wilaya ya Usingilo na wanaume wengi kutofanyiwa tohara ambapo tayari Mashirika ya nje ya nchi yanayojishughulisha na masuala ya kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi (MDH) yameanzisha  kampeni  ya utoaji wa tohara kuanzia watoto wenye umri wa miaka 10 hadi watu wazima.

  Dk. Martin alisema pamoja na kupungua kwa magonjwa hayo changamoto nyingine ni maambukizi ya virusi vya UKIMWI, HIV ambapo katika zahanati hiyo ina wananchi 21 wenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI na wanapatiwa huduma katika kliniki za kudhibiti makali ya virusi vya UKIMWI ya mama na mtoto.

  Alisema katika zahanati hiyo kwa mwezi wanahudumiwa wagonjwa 200 kutoka katika vitongoji vinne vya Kitoboka, Nsheshe, Kakunyu na Kalola.

  Meneja wa MSD Kituo cha Muleba,Egidius Rwezaura alisema wana mpango wa kuanzisha  utaratibu wa kupeleka dawa katika zahanati, vituo vya afya na hospitali kila baada ya miezi miwili badala ya miezi mitatu kutokana na kuwepo kwa mahitaji makubwa ya dawa na MSD tayari imeongeza idadi ya magari ya usambazaji pamoja na kuajiri madereva wa kutosha.


  0 0

   Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndugu Philip Mangula akiwa na Mwenyekiti wa United Democratic Party (UDP) Mhe. John  Momose Cheyo wakiwa ndani ya ndege ya Rais kabla ya kuondoka kuelekea mjini Harare, Zimbabwe, kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa nchi hiyo Mhe.  Emmerson Dambudzo Mnangagwa  zinazofanyika leo Jumapili Agosti 26, 2018. Katika safari hiyo viongozi hao wanafuatana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) ambaye atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipanda ndege ya Rais tayari kuelekea mjini Harare, Zimbabwe, kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulikwenye kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa nchi hiyo Mhe.  Emmerson Dambudzo Mnangagwa zinazofanyika leo Jumapili Agosti 26, 2018
  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya anaeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kwa kutekeleza vyema mpango mkakati wa kitaifa wa miaka mitano kuanzia 2017/22 wa kutokomeza Ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake.

  Nkima alitoa pongezi hizo Agosti 21, 2018 wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni maalum ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika Kata ya Idetemya Halmashauri ya Misungwi, inayotekelezwa na Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI.

  Alisema Misungwi imekuwa Halmashauri ya kwanza nchini kutafsiri kwa vitendo mpango huo na kulishukuru shirika la KIVULINI kwa kushirikiana na Halmashauri hiyo kupambana na vitendo vya ukatili hatua itakayosaidia kuelekea kwenye maendeleo endelevu bila ukatili wa kijinsia.
  Tazama makala maalum hapo chini

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya anaeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza ukatili kwa watoto na wanawake katika Kata ya Idetemywa wilayani Misungwi
  Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally akizungumza kwenye uzinduzi huo
  Tazama hapa chini BMG Online Tv

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Peter Mavunde amewataka wananchi wa Jimbo la Dodoma Mjini kushirikiana na serikali na Viongozi wao katika kujiletea maendeleo na kutoa wito kwa jamii kujitoa kwa dhati kuchangia maendeleo kama wanavyofanya kwenye shughuli mbalimbali za kijamii hasa katika sherehe mbalimbali zikiwemo harusi.

  Mavunde ameyasema hayo jana wakati akiongoza mamia ya wananchi wa kata ya kikuyu kusini katika ujenzi wa vyumba vya madarasa leo Jijini Dodoma ambapo Mbunge huyo amechangia matofali 1000 na mifuko ya Saruji 130,Computer 1,Jezi na mipira pamoja kuweka magoli ya Chuma katika uwanja wa michezo uliopo katika Shule ya Msingi Kikuyu B.

  Akimuunga mkono Mh Mavunde,Mbunge wa Jimbo la Bahi Mh Omary Badwell amewapongeza wananchi wa Kata ya Kikuyu Kusini kwa muitikio wao mkubwa kwenye shughuli za maendeleo na kuahidi kushirikia na Mh Mavunde kutatua changamoto za shule hiyo kwa kuchangia **mifuko 20 **ya Saruji iliyopo eneo ambalo na yeye ni mkazi wake na watoto wake pia wanasoma katika shule husika.

  Aidha Diwani wa kata ya Kikuyu Kusini Mh Kutika amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kusaidia kutatua kero hiyo ya ukosefu wa vyumba vya madarasa na hivyo ujenzi huo utasaidia kuboresha miundombinu ya shule hiyo na hivyo kuchukua wanafunzi wengi kwa wakati mmoja.
  Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Peter Mavunde akiongoza mamia ya wananchi wa kata ya kikuyu kusini katika ujenzi wa vyumba vya madarasa Jijini Dodoma, ambapo Mbunge huyo amechangia matofali 1000 na mifuko ya Saruji 130,Computer 1,Jezi na mipira pamoja kuweka magoli ya Chuma katika uwanja wa michezo uliopo katika Shule ya Msingi Kikuyu B.
  Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Peter Mavunde akishiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa Jijini Dodoma, ambapo Mbunge huyo amechangia matofali 1000 na mifuko ya Saruji 130,Computer 1,Jezi na mipira pamoja kuweka magoli ya Chuma katika uwanja wa michezo uliopo katika Shule ya Msingi Kikuyu B.

  0 0

  Afisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Rose Mahendeka akitoa elimu juu ya msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi wakati wa semina elekezi kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali iliyofanyika mkoani Kigoma kwa lengo la kutoa uelewa kuhusu msamaha huo.

  Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Chama Siriwa akiwasilisha mada kuhusu msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi wakati wa semina elekezi kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali iliyofanyika mkoani Kigoma kwa lengo la kutoa uelewa kuhusu msamaha huo.

  Baadhi ya wafanyabiashara na wadau mbalimbali waliohudhuria semina elekezi ya msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi iliyofanyika mkoani Kigoma kwa lengo la kutoa uelewa kuhusu msamaha huo.

  Baadhi ya wafanyabiashara na wadau mbalimbali waliohudhuria semina elekezi ya msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi iliyofanyika mkoani Kigoma kwa lengo la kutoa uelewa kuhusu msamaha huo.


  Na Veronica Kazimoto-Kigoma

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaendelea kutoa elimu juu ya namna ya kuomba msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali nchini.

  Akizungumza wakati wa semina elekezi kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali mkoani Kigoma, Afisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo Rose Mahendeka amewaambia wafanyabiashara hao kuwa lengo la kutoa msamaha huo ni kuwapunguzia mzigo ili waweze kulipa kodi ya msingi isiyokuwa na riba wala adhabu ambapo mwisho wa kulipa kodi hiyo ni tarehe 30 Juni, 2019.

  “Serikali imeamua kutoa msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi kwa asilimia 100 ili kuwasaidia wafanyabiashara kulipa kodi ya msingi tu ambayo mfanyabiashara anaweza kuilipa mara moja au kwa awamu ndani ya Mwaka wa Fedha 2018/19,” alisema Mahendeka.

  Mahendeka ameeleza kuwa, msamaha huu ni wa miezi 6 na ulianza mwezi Julai na utamalizika Desemba, 2018 na kuongeza kuwa huu ni muda muafaka wa wafanyabiashara hao kutuma maombi ya msamaha huo kabla muda uliopangwa haujamalizika.

  “Natumia fursa hii kuwasihi wafanyabiashara kutuma maombi TRA ya msamaha huu kabla ya mwezi Novemba, 2018 na msisite kuwasiliana na ofisi yetu ya hapa mkoani pindi mtakapohitaji ufafanuzi zaidi,” aliongeza Mahendeka.Aidha, Mahendeka alisisitiza kuwa TRA itatoa majibu ya maombi ya msamaha huo kwa maandishi ndani ya siku thelathini (30) tangu siku ya kupokea maombi.

  Naye Mfanyabiashara wa Vifaa vya Ujenzi ambaye pia ni Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani hapa Raymond Ndabhiyegetse ameishukuru TRA kwa kutoa elimu hiyo ya msamaha wa kodi na kuiomba mamlaka kuwashawishi watengeneza hesabu (wahasibu) kuwekeza mkoani Kigoma kwa kuweka wahasibu wengi ambao watawasaidia kutengeneza hesabu za biasahara zao.

  “Mimi napenda kuishukuru TRA kwa kutupatia uelewa huu wa namna ya kuomba msamaha wa riba na adhabu za kodi, kwakweli elimu mliyotupatia leo imetusaidia sana. Pia naomba TRA mtusadie kuwashawishi watengeneza hesabu waje Kigoma kwa sababu tuna changamoto kubwa ya watengeneza hesabu na kwa sasa tunao wawili tu, hivyo tunapata changamoto kubwa katika kutengeneza hesabu zetu,” alisema Ndabhiyegetse.

  Baada ya Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania kutoa msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi kwa asilimia 100, TRA imejiwekea mikakati ya kufikisha ujumbe huo kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukutana na wafanyabiashara kwa lengo la kutoa uelewa juu ya namna ya kuomba msamaha huo kabla muda uliopangwa haujamalizika.

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Timu ya taifa ya tennis ya walemavu (Table Tennis) imeshindwa kusafirisha wachezaji wake kuelekea nchini Malaysia kutokana na uhaba wa fedha pamoja na vifaa ikiwemo viti (wheel chairs)

  Kocha wa timu hiyo Riziki Salum amesema changamoto kubwa katika chama chao kumekuwa ni uhaba wa fedha unaopelekea kushindwa kuwasafirisha wachezaji wake kuelekea katika mashindano mbalimbali.

  Riziki amesema, katika safari ya Malaysia wamempeleka mchezaji mmoja tu kwa ajili ya mashindano yaliyopo huko, wakati wanatakiwa wapeleke wachezaji japo wanne ili waweze .Amesema, kuna safari zingine ikiwemo ya Afrika Kusini ya Septemba 28 itahitajika kwenda kwa wachezaji wannne na gharama ni dola 400 kwa kila mmoja itakayotumika kwa ajili ya nauli ya kwenda na kurudi pamoja na malazi.

  Ameongezea kuwa ndani ya mwaka huu kuna mashindano pia nchini Sweden, Ghana na Nigeria na gharama ya kusafirisha timu nzima inafikia dola 7000 ila watashindwa kuwasafirisha kutokana na ukata wa fedha.

  Riziki amewaomba wadau wa table tennis kujitokeza kwa ajili ya kuisaidia timu yao kifedha ambapo kwa sasa wapo katika maandalizi kwenye kipindi hiki ili waweze kusafirisha timu nzima kuelekea Afrika kusini, Sweden, Ghana na Nigeria.
  Timu ya Taifa ya tennis ya walemavu (Table Tennis)

older | 1 | .... | 1657 | 1658 | (Page 1659) | 1660 | 1661 | .... | 1897 | newer