Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU KUKUTANA NA TAASISI SEKTA BINAFSI, WADAU WAKE KUJADILI MAADILI NA RUSHWA

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa  atarajia kukutana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) na Wadau wake kujadiliana Maadali pamoja na masuala ya Rushwa ndani ya Sekta hiyo.

Katika Mkutano wake Mkuu wa Mwaka utakaofanyika August 28, 2018 jijini Dar es Salaam, TPSF itajadili pia Changamoto zinazowakumba katika kufanya Biashara nchini.

Mjadala huo wa Maadili na Sakata la Rushwa utakaofunguliwa na Waziri Mkuu unafanyika ikiwa ni baada ya Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kufanya mazungumzo na Wafanyabiashara Desemba 3, 2015 na kugusia suala hilo kwa Wafanyabiashara hao.Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye amesema kuwa wanakutana kama Sekta Binafsi kujadili suala hilo, kutokana na kuwepo kwa tuhuma za vitendo ambavyo havina maadili katika Sekta hiyo mchini.

Simbeye amesema kusipokuwa na ushirikiano na kuaminiana kati ya Sekta ya Umma na TPSF hakutakuwa na maendeleo ya haraka.Katika hatua nyingine, Simbeye ameahidi Sekta hiyo kusimamia ipasavyo Kanuni za maadili sambamba nakuacha kufanya vitendo vya rushwa vinavyotuhumiwa katika Sekta hiyo. 

Pia Mkitano huo wa Wanachama wa Sekta Binafsi utatumia nafasi hiyo kumtafuta Mwenyekiti mpya wa TPSF baada ya Mwenyekiti wake aliyehudumu kwa kipindi cha miaka minne, Dkt Reginald Mengi kumaliza muda wake.Kabla ya Mkutano huo, August 27, 2018 Kongano 14 zilizo katika Sekta hiyo zitapiga kura kumchagua Mjumbe mmoja atakayeingia kwenye Bodi ya TPSF ili kuwakilisha mawazo katika maendeleo ya Sekta Binafsi. 

Bodi hiyo itazinduliwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage ambapo watu 14 wanaowakilisha Kongano hizo atachaguliwa mmoja atakayekuwa Mwenyekiti wa TPSF. 
Mkurungenzi Mtendaji wa Taasisi Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Mkutano Mkuu wa Sekta hiyo utakaofanyika jijini Dar es Salaam August 28, Mkutano utakaojadili zaidi masuala ya Maadili na tuhuma za Rushwa katika Sekta hiyo.

ANZISHENI KAMATI ZA MAZINGIRA KATIKA NGAZI ZOTE - MAKAMBA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na mamia ya wakazi wa Mkoa wa Tabora (hawapo pichani) waliojitokeza katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kumsikiliza. Waziri Makamba amezindua Kamati ya Mazingira na kuwataka wananchi hao kuwa mstari wa mbele kusimamia masuala ya mazingira katika maeneo yao
 
Wakazi wa Kijiji cha Igambilo Kata ya Misha Mkoani Tabora waishio pembezoni mwa Bwala la Igombe wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (hayupo pichani) mara baada ya kutembelea Kijiji chao na kuzungumza nao umuhimu wa kuendelea kutunza Bwawa la Igombe. Waziri Makamba ameahidi kutoa mifuko 100 ya Saruji kuchangia ujenzi wa Zahanani Kijijii hapo.
Bwala la Igombe ambalo ni chanzo kikubwa cha maji kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora, shughuli zisizoendelelevu za kibinadamu zinapelekea kupungua kwa kina cha bwana hilo kila siku. Waziri mwenye dhamana ya Mazingira Mhe. January Makamba ametembelea eneo hilo na kuagiza wananchi wanaozuia maji kwa kutumia mabanio kuondolewa mara moja.



Jamii imetakiwa kufahamu kuwa Kamati za Mazingira katika ngazi zote zipo kwa mujibu wa Sheria, Sheria ya Mazingira kifungu Na. 38 (1-2) na Kamati hizo zina wajibu wa kusimamia mazingira kikamilifu yanayohusu maeneo yao.

Akizungumza na Watendaji wa Mkoa wa Tabora katika hafla ya kuzindua Kamati ya Usimamizi wa mazingira Mkoani hapo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameahidi kujenga uwezo kwa watendaji hao kwa kuwapatia mafunzo.

Aidha, Waziri Makamba amesisitiza unaziswaji kwa Kamati za Mazingira katika ngazi za vitongoji, vijiji na kata nchi nzima na kuahidi kutuma wataalamu kutoa mafunzo kwa kamati hizo ili ziweze kujua majumu yao ipasavyo na kusema kuwa shughuli za hifadhi za mazingira hazitafanikiwa kama Kamati za mazingira hazitatimiza majukumu yake katika ngazi hizo.

Waziri Makamba amesema kuwa dunia tunayoishi sasa tumeiazima kwa kizazi kinachokuja hivyo hatuna budi kuitunza. “Ukiazima kitu kwa mtu yeyote huna budi kukitunza na kukulinda ila kukirudisha kwa mwenyewe kikiwa katika hali nzuri.” Makamba alibainisha.

Katika wakati mwingine Waziri Makamba ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Tabora kuteua ama kuajiri Maafisa wa mazingira wa kutosha ili kusimamia kikamilifu uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira, pamoja na kuandaa mpango tekelezi wa mazingira katika ngazi ya Mkoa.

Kuhusu usimamizi wa taka, Waziri Makamba ametoa wito kwa uongozi wa Mkoa wa Tabora na Halmashauri zote kuwa na takwimu sahihi ya kiwango cha taka kinachozalishwa kwa siku ili taka hizo ziweze kutumia katika uzalishaji wa nishati. “Naagiza kila Halmashauri kufahamu kiwango cha uzalishaji wa taka, hii itasaidia kuja na miradi ya kuzalisha nishati mbadala pale fursa zitakapopatikana.” Makamba alisisitiza.

Katika hatua nyingine Waziri Makamba amesisitiza matumizi ya nishati mmbada kwa taasisi za Serikalini ili kupunguza kiwango cha ukataji wa miti na matumizi ya mkaa, pia amewataka wadau na wakulima wa tumbaku kubuni namna bora ya kuchoma tumbaku ili iweze kupata soko zaidi duniani. “Sote tunafahamu kuwa miti ni gharama, haiwezekani mkulima kuteketeza kiasi cha miti yenye thamani ya Shilingi laki mbili kuzalisha tumbaku ya elfu themanini, hii haikubaliki ni lazima tubadilishe uchomaji wake”. Waziri Makamba amebainisha.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri amemueleza Waziri Makamba jinsi Mkoa wake unavyotekeleza kikamilifu kampeni ya upandaji miti kwa kuwa na kauli mbiu ya ‘Tabora ya Kijani’ na amemshukuru Waziri Makamba kwa kufanya ziara katika Mkoa wake na kuahidi kutekeleza agizo la kuteua maafisa wenye sifa ya kuwa wakaguzi wa Mazingira.

Waziri Makamba amehitimisha ziara yake Mkoani Tabora kwa kutembelea Bwawa la Igombe na Kazima ili kuona utashi na utayari wa wananchi katika kuhifadhi maeneo hayo kabla ya kutangazwa katika gazeti la Serikali kama eneo lindwa. Akiwa Kijijini Igambilo Mheshimiwa Makamba ameahidi kutoa mifuko 100 ya Saruji kuchangia ujenzi wa Zahanati kijijini hapo.

TANAPA YATENGA BILIONI 3.9 KUENDELEZA HIFADHI TANO ZILIZOPANDISHWA HADHI NA KUWA HIFADHI ZA TAIFA

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) akioneshwa mpaka kati ya Pori la Akiba la Burigi na eneo la wananchi katika eneo la Nyungwe na Ofisa mwenye wadhifa wa Mkuu wa Hifadhi aliyeteuliwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kusimamia Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi kuwa Hifadhi za Taifa, Damian Saru ( wa kwanza kulia) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo, Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bihalamulo, Sada Malunde.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) akioneshwa mpaka kati ya Pori la Akiba la Burigi na eneo la wananchi katika eneo la Nyungwe na Meneja wa Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi kuwa Hifadhi za Taifa , Bigilamungu Kagoma ( wa kwanza kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo, Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bihalamulo, Sada Malunde.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga akizungumza na baadhi ya Watumishi wa Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi na kuwa Hifadhi za Taifa wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana kwenye mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Bihalamulo pamoja na baadhji ya watumishi wa TAWA na TANAPA wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo, Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bihalamulo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) akioneshwa eneo la Ziwa Burigi katika eneo la Nkonje na Meneja wa Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi kuwa Hifadhi za Taifa , Bigilamungu Kagoma ( wa kwanza kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga akisaini kitabu cha wageni i katika eneo la Nyungwe wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo, Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bihalamulo, Sada Malunde.

Baadhi ya mafuvu ya wanayamapori katika Pori la A kiba la Burigi katika eneo la Nyungwe. (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-WMU)

 
NA LUSUNGU HELELA-KAGERA .

Bodi ya Wadhamini ya Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA) imeidhinisha na kuruhusu matumizi ya bajeti ya mpito ya kiasi cha shilingi 3.9 bilioni zitumike kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi, uendelezaji utalii pamoja na ujenzi wa miundombinu katika Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi na kuwa Hifadhi za Taifa. 

Hatua hiyo imekuja kufuatia tangazo la Serikali la kuyapandisha hadhi Mapori ya Akiba ya Bihalamulo,Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika kuwa Hifadhi za Taifa kupitia kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamisi Kigwangalla wakati alipokuwa akihitimisha bajeti ya Wizara mwezi Mei mwaka huu Bungeni mjini Dodoma. 

Ofisa Mwenye Wadhifa wa Mkuu wa Hifadhi, Damian Saru amesema hayo jana mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga wakati alipotembelea mapori ya Biharamulo, Burigi na Kimisi ( BBK) ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo. 

Alitaja fedha hizo kuwa zimeshaanza kutumika katika kuimarisha ulinzi, kujenga miundo mbinu ya utalii na Utawala, kuainisha mipaka , kusimamia mchakato wa kupandisha hadhi mapori  Damian Saru, Ofisa mwenye wadhifa wa Mkuu wa Hifadhi aliyeteuliwa na TANAPA, aliwasilisha taarifa hiyo pamoja na kumweleleza Naibu Waziri huyo hatua za utekelezaji zilizofikiwa katika mapori hayo. 

Alimweleza kuwa askari 58 wameshafika kwenye mapori hayo matano kwa ajili ya kuongeza nguvu. Mashine ya kutengeneza barabara ‘ Motor Grader moja imeletwa kwa sjiki ya kutengeneza barabara. Pia, Alimweleza Naibu Waziri huyo ikiwemo vitendea kazi ikiwemo ndege moja magari manne, mahema silaha, GPS vimeletwa katika mapori hayo kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi
Kufuatia utekelezaji huo, Mkuu mwenye hadhi ya Mkuu wa Hifadhi alitaja mafanikio yaliyopatikana katika kIpindi kifupi cha utekelezaji maagizo hayo kuwa katika kipindi cha wiki mbili pamoja na ng’ombe 41 kukamatwa na kufunguliwa mashtaka. 

Pia , Alitaja idadi ya watuhumiwa 12 wa ujangili wamekatwa.
Aidha, Saru alitaja aina za vifaa vilivyokatwa kuwa ni mitumbwi mitatu, mkaa gunia mbili pamoja na baiskeli zopatazo 10. Kwa upande wake, Naibu Waziri , Mhe.Hasunga ameridhishwa na hatua ya TANAPA kwa ushirikiano na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) kwa nzuri waliyoifanya.

RC Hapi aahidi kuboresha sekta ya Utalii Nyanda za juu Kusini

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bw. Ally Hapi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Capital Plus International wakiongozwa na Mratibu wa Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018 Bw Clement Mshana (kulia kwake) alipotembelea ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bw. Ally Hapi (katikati) akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Capital Plus Internantional kuhusiana na maandalizi ya Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018 alipotembelea ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kampuni ya Capital Plus International inashirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kuandaa maonesho hayo yanayotarajiwa kufanyika Septemba 26 hadi 30 mwaka huu kwenye Viwanja vya Kihesa Kilolo mkoani Iringa yakihusisha mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bw Iringa Bw. Ally Hapi (katikati) akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho. Kulia ni Mratibu wa Maonesho hayo kutoka kampuni ya Capital Plus Internantional Bw Clement Mshana.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bw. Ally Hapi (kulia)akipokea zawadi ya kikombe maalumu chenye nembo ya Capital Plus Internantional kutoka kwa mfanyakazi wa kampuni hiyo Bi Farida Adam ikiwa ni ishara ya kumkaribisha kwenye ofisi hizo. Capital Plus Internantional inashirikiana na Ofisi ya Mkoa wa Iringa kuandaa maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018.


Mratibu wa Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018 kutoka kampuni ya Capital Plus Internantional Bw Clement Mshana akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bw. Ally Hapi kuhusu maandalizi ya Maonesho hayo wakati wa kikao hicho.
Mratibu Msaidizi wa Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018 kutoka kampuni ya Capital Plus Internantional Bw Malela Kassim (katikati) akifafanua jambo kuhusu maandalizi ya Maonesho hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bw. Ally Hapi (hayupo pichani)wakati wa kikao hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bw. Ally Hapi (kulia)akipokea zawadi ya kikombe maalumu chenye nembo ya Utalii Karibu Kusini kutoka kwa mfanyakazi wa Kampuni ya Capital Plus Internantional (CPI) Irene Lymo ikiwa ni ishara ya kumkaribisha rasmi Mkuu huyo kwenye mkakati wa kutangaza Utalii Nyanda za Juu Kusini sambamba na maandalizi ya Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018.
Nataka mambo yawe hivi! Ndivyo anavyo maanisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bw. Ally Hapi wakati akizungumza kwenye kikao hicho.







MKUU wa mkoa wa Iringa Bw. Ally Hapi ameahidi kushirikiana kikamilifu na wakuu wenzake wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kutangaza fursa na vivutio vya kiutalii vinavyopatikana katika ukanda huo, ikiwa ni mwendelezo wa harakati za kuunga mkono adhma ya Rais John Pombe Magufuli ya kufungua na kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana katika ukanda wa Nyanda za Juu Kusini.

Katika kuthibitisha hilo kwa vitendo, Bw Hapi ameahidi kuunga mkono jitihada zilizoanzishwa na mtangulizi wake aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Bi. Amina Masenza za kuyaboresha zaidi Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018 yanayoenda sambamba na Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani ambayo Kitaifa yatafanyika mkoani Iringa Septemba 26 hadi 30 mwaka huu.

Bw Hapi ametaja mkakati wake huo, mapema wiki hii jijini Dar es Salaam alipotembelea Ofisi za Kampuni ya Capital Plus International (CPI) inayoshirikiana na ofisi ya Mkuu wa Iringa pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kuratibu maonesho hayo yanayofanyika mjini Iringa kwa mwaka wa tatu mfululizo.

“Tungependa watu kutoka maeneo mengine ya Tanzania na hata nje ya nchi waje katika maonesho hayo ili waone na kutembelea vivutio vya utalii, kihistoria na kufahamu fursa za uwekezaji tulizo nazo”, alisisitiza kiongozi huyo wa Iringa.

‘’Mikoa ya nyanda za juu Kusini inasifika kuwa na hifadhi zenye sifa za kipekee ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Ruaha yenye makundi makubwa ya tembo na wanyama wengine. Aidha, hifadhi ya Kitulo yenye aina mbali mbali za maua ambayo hayapatikani mahali pengine Duniani na Udzungwa yenye wanyama na viumbe adimu duniani kama vyura wa Kihansi,’’ alitaja

Alisema mkoa wa Iringa ambao unaratibu maonesho hayo kwa kushirikiana na mikoa jirani ya Mbeya, Njombe, Songwe, Ruvuma, Rukwa na Katavi, umejipanga kushirikiana na sekta ya utalii, sekta binafsi pamoja jamii ya kimataifa ili kuyaboresha.

“Kwa mfano mkoa wetu wa Iringa mbali na vivutio vya hifadhi tuna vivutio vya kihistoria. Inafahamika kuwa mkoa huu kupitia Chifu Mkwawa ulikuwa mstari wa mbele kwenye harakati za kupinga ukoloni hasa wa Kijerumani.’’

“Naamini tukishirikiana vizuri na wenzetu wa Ujerumani tunaweza kupokea watalii wengi zaidi kutoka huko watakaokuja kujifunza mengi ya kihistoria ikiwemo kumjua huyu Mkwawa alikuwa ni mtu wa aina gani,aliyeweza kutumia silaha za jadi akawashinda wajerumani waliokuwa na bunduki na risasi za moto’’, alitaja.

Alitoa wito kwa wadau wa Utalii na maendeleo nchini kumuunga mkono kwa kushiriki kikamilifu kwenye maonesho hayo yatakayoambatana na matukio kadhaa ya kimichezo, kitaaluma na kiutamaduni ili kuongeza tija zaidi katika kufikia malengo ya kuongeza mazao ya utalii katika kanda hiyo.

Akizungumzia maandalizi ya maonesho hayo, Mratibu kutoka kampuni ya Capital Plus International Bw Clement Mshana alisema yanaendelea vizuri na kwa sasa kinachoendelea ni kutafuta ushiriki zaidi wa wadau mbalimbali kutoka mashirika na taasisi za kiserikali, sekta binafsi pamoja na mashirika ya kimataifa ili kufanikisha maonesho hayo kwa ubora uliokusudiwa.

“Mbali na maonesho yenyewe kutakuwa na Kongamano la kujadili masuala ya Utalii na Uchumi litakalofanyika tarehe 27 Septemba, 2018 likihusisha washiriki zaidi ya 300. Vile vile kutakuwa na matukio ya kimichezo yakiwemo mashindano ya mbio za baiskeli, ngoma za asili, huku kilele cha maonesho hayo kikitarajiwa kupambwa na mashindano ya mbio za nyika (marathon) zitakazifanyika Septemba 30 mkoani Iringa,’’ alisema.

Bw Mshana alisema katika kipindi chote cha maonesho hayo umeandaliwa utaratibu wa usafiri kwa washiriki, wageni pamoja na wenyeji wa Mkoa wa Iringa ili waweze kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo katika ukanda huo.“Nawaomba sana wananchi wote wajipange kushiriki katika maonesho haya makubwa. Pia niwaombe sana wadau wetu wa maendeleo, ikiwemo sekta binafsi, wajitokeze kwa wingi kuunga mkono maonesho haya.’’ Alisema

Matumizi bora ya Mtandao-Maadili na Kizazi Kipya-MAKIKI

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James M. Kilaba akisisitiza kutumia vizuri Mfumo wa Mawasiliano kwa ajili ya Maendeleo yetu na kwa Faida ya Umoja na Mshikamano wa Taifa Letu.

WASANII ASLEY, SHILOLE WASAINI MKATABA TTCL KUNOGESHA KAMPENI YA RUDI NYUMBANI KUMENOGA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba (kulia) akibadilishana hati ya mkataba na msanii Zuena Mohamed maarufu kama Shilole ‘Shishi Baby’ (kushoto), mara baada ya kusaini mkataba huo. Mkataba huo ambao pia msanii Asley Isihaka maarufu kama Dogo Asley amesaini na kampuni hiyo, wasanii hao wameingia makubaliano kushiriki katika Kampeni kubwa ya Rudi Nyumbani Kumenoga itakayoshirikisha Mikoa yote ya Tanzania. 
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba (kulia) akisaini mkataba na msanii Zuena Mohamed maarufu kama Shilole ‘Shishi Baby’ (kushoto), mkataba huo ambaao pia Asley Isihaka maarufu kama Dogo Asley amesaaini na kampuni hiyo ili waasanii hao kushiriki katika Kampeni kubwa ya Rudi Nyumbani Kumenoga itakayoshirikisha Mikoa yote ya Tanzania. 



SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania, TTCL leo limetiliana saini na wasanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva) Zuena Mohamed maarufu kama Shilole ‘Shishi Baby’ na Asley Isihaka maarufu kama Dogo Asley watakaoshiriki katika Kampeni kubwa ya Rudi Nyumbani Kumenoga itakayoshirikisha Mikoa yote ya Tanzania.

Akizungumza na Waandhishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba amesema Kampeni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilino Mhandisi Isaack Kamwelwe Agosti 31 mwaka huu Mkoani Katavi.

Amesema lengo la Kampeni hiyo ni kuwafikishia taarifa wananchi kuhusu TTCL mpya ambayo kwa sasa imefanya mabadiliko makubwa katika biashara ya Huduma za Mawasiliano hapa Nchini.

Asema Tamasha hilo ambalo halitakuwa na kiingilio litakuwa la aina yake ambapo wasanii wamejipanga kutoa burudani kabambe huku wananchi wakipata fursa ya kuelimishwa kuhusu Shirika la TTCL, Huduma zake na majukumu yake ya msingi pamoja na kujipatia Sim Kadi na kujisajili bure na kuuziwa bidhaa mbalimbali za TTCL kwa bei nafuu.

“Hii ni kampeni ya Mkoa kwa mkoa, ambayo pia itatumika kutatua changamoto na kero mbalimbali walizonazo wateja wetu juu ya huduma na bidhaa zetu” alisema Kindamba.Kwa upande wake Zuena Mohamedi kw aniaba ya msanii mwenzake amesema amejipanga kutoa burudani kabambe itakayotoa hamasa kwa wananchi kupenda vya kwao na hivyo kurudi nyumbani kwa kutumia Mtandao wa TTCL.

“Nawaomba Watanzania wenzangu tuwe wazalendo tutumie bidhaa za nyumbani, mfano mimi nina line ya TTCL ambayo intaneti yake ni ya kasi zaidi inaniwezesha kufanya kazi zangu kwa urahisi ikiwa ni pamoja na kuendesha Akaunti zangu katika mitandao mbalimbali ya kijamii” alesema Shilole.

TTCL imedhamiria kuwa Shirika kinara katika utoaji wa huduma za Mawasiliano Nchini, nafasi iliyokuwa nayo hapo awali. Kupitia maboresho makubwa inayoyafanya, TTCL imeweza kutoa gawo la Tsh Bilioni 1.5 mwaka huu wa fedha na kuahidi kuongeza kiasi cha gawio katika miaka inayofuata sambamba na kuongeza uwekezaji katika teknolojia za kisasa, ubora wa huduma na ushiriki wa TTCL katika kutoa ajira kwa Watanzania na kusaidia shughuli za kijamii.
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba (kulia) akibadilishana hati ya mkataba na msanii Zuena Mohamed maarufu kama Shilole ‘Shishi Baby’ (kushoto), mara baada ya kusaini mkataba huo. Mkataba huo ambao pia msanii Asley Isihaka maarufu kama Dogo Asley amesaini na kampuni hiyo, waasanii hao wameingia makubaliano kushiriki katika Kampeni kubwa ya Rudi Nyumbani Kumenoga itakayoshirikisha Mikoa yote ya Tanzania. 
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba (kulia) akizungumza katika hafla hiyo ya kusainishana mkataba. 
Msanii Zuena Mohamed maarufu kama Shilole ‘Shishi Baby’ (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo ya kusainishana mkataba.

UN WOMEN KUENDELEA KUTOA MSAADA KWA WANAWAKE TANZANIA

$
0
0



 Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Wanawake (UN Women), Phunzile Mlambo- Ngcuka, akisalimiana na wanawake wajasiriamali baada ya kuwasili viwanja vya Soko la Mchikichini, Ilala jijini Dar es Salaam juzi kwenye sherehe ya mafanikio ya mradi wa 'Mpe Riziki si Matusi' ambapo alikuwa ni mgeni rasmi. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita.
 Wanawake wajasiriamali wakiwa na Mkurugenzi huyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, akimpa Bi. Mlambo zawadi ya Khanga.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, akiteta jambo na Bi. Mlambo.
 Kundi la Sanaa la Nimujo, likitoa burudani.
 Wasanii wakundi hilo wakiigiza.
 Mwezeshaji wa kisheria masokoni, Consolatha Cleophas, akitoa ushuhuda mbele ya mgeni rasmi.
  Mwezeshaji wa kisheria Soko la Tabata Muslim, Aisha Juma, akitoa ushuhuda mbele ya mgeni rasmi.
 Mwenyekiti wa Soko la Temeke Stereo, Omary Mangilile, akizungumza katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, akihutubia kwenye sherehe hizo.
 Bi.Mlambo akihutubia.
 Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
 Picha ya pamoja.


 Sherehe ikiendelea.
 Mgeni rasmi akiserebuka sanjari na Mkurugenzi wa EfG, Jane Magigita.
 Hapa mgeni rasmi akisalimiana na wanawake wajasiriamali.



Wanawake wajasiriamali wakiwa na mabango yao.

Mgeni rasmi akiaga wakati akiondoka katika viwanja hivyo.

Na Dotto Mwaibale

MKURUGENZI Mtendaji wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Wanawake (UN Women), Phunzile Mlambo- Ngcuka, amesema umoja huo utaendelea kuwasaidia wanawake wa Tanzania.

Mlambo ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyasema hayo kwenye sherehe ya mafanikio ya mradi wa 'Mpe Riziki si Matusi' zilizofanyika viwanja vya Soko la Mchikichini, Ilala jijini Dar es Salaam ambao unasimamiwa na Shirika la Equality for Growth (EfG).

"Tutaendelea kuwasaidia wanawake wa Tanzania katika maeneo mbalimbali lakini pia napenda kuwapongeza kwa hatua mliyoifikia kupitia mradi huu na kuwa na moyo wa kupenda kuyapeleka mafanikio mliyopata kwa wanawake wenzenu jambo ili limenifurahisa sana" alisema Mlambo.

Katika hatua nyingine Mlambo aliwaomba wanaume kuendelea kuthamini mchango wa wanawake ili kuwatia nguvu badala ya kuwabeza kwani kazi wanayoifanya ni kubwa.

Mkurugenzi wa EfG, Jane Magigita alisema hivi sasa matukio ya ukatili wa kijinsia yamepungua kwa asilimia 81 hasa lugha za matusi na bughudha kwa wanawake.

Alisema utafiti uliofanywa na EfG Desemba 2017 umeonesha asilimia 92 ya wanawake wako huru kufanya biashara, 89 kupata haki za kiuchumi, 70 kugombea na kushika nafasi mbalimbali za uongozi, 83 kufanya maamuzi na 91 kupata huduma za msaada pindi wanapofanyiwa ukatili.

"Hivi sasa wanawake katika uongozi wa masoko wameongozeka kutoka asilimia 14 mpaka 26 na tuna mwenyekiti mwanamke katika Soko la Kiwalani na pia katika masoko mengine, uongozi wa soko ni asilimia 50/50," alisema Magigita. 

MKUU WA WILAYA YA CHEMBA ATATUA MGOGORO MATUMIZI YA ARDHI

$
0
0
 Na Shani Amanzi,Chemba.
 
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Saimon Odunga amewataka Wananchi wa Kwamtoro waache tabia ya kuchukua maeneo kiholela badala yake wafate kanuni na taratibu za kuwa na ardhi kwani Serikali inapoteza muda mwingi na pesa katika kuwataftia wananchi maeneo mengine na kuwalipa fidia.

Mhe.Saimon Odunga aliyazungumza hayo alipokuwa anafanya Mkutano wa Adhara ndani ya siku moja akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chemba,Wataalam wa Halmashauri ya Chemba pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama, Kwamtoro kwa ajili ya kutatua mgogoro wa ardhi , tarehe 20/8/2018.

Mhe.Saimon Odunga amesema “Wananchi wamekuwa na tabia ya kuvamia maeneo na hata wakipewa maeneo mengine wanatabia ya kuyauza kitendo ambacho siyo kizuru na kusababisha serikali kupoteza muda kuendelea kufatilia nini kifanyike na wengine wanajua kabisa maeneo wanayoyachukua au kukaa ni ya matumizi ya umma kama shuleni,sokoni pamoja na stand ya mabusi”

Aidha amewataka wakazi wa Kwamtoro waliojenga nje ya utaratibu maeneo ya soko,standi na shule watoke haraka sana ndani ya siku 90 na Viongozi wa siasa pamoja na wa Serikali wasipende kutoka nje ya taratibu na kusababisha uchochezi bali fateni taratibu za ardhi kwani Serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli inafata kanuni,taratibu na sharia za nchi hasa kwenye ardhi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba amesema Serikali haiwezi kuwaonea wananchi wake ni sawasawa na baba kumuonea mwanae ,badala yake wananchi wanatakiwa kuwa makini na watu wanaowauzia maeneo sa nyingine kwani huwa wanawapotosha kwa kuwauzia maeneo ya umma kitendo ambacho kipo kinyume na taratibu .

Mashimba aliongeza kwa kusema “kwa wale wenye tabia ya kujiegesha maeneo ambayo siyo na kutegemea fidia tabia hiyo waiache mara moja kwani mambo ya kupeleka kesi mahakamani wakati wanajua wapo kinyume na taratibu wanasababisha Serikali kutumia gharama kubwa kuendesha kesi mahakamani na kupoteza muda” .

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba

MKURABITA Yawezesha Wananchi Kupata Hati za Kimila Zaidi ya 300 Kilosa

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar awatahadharisha Wananchi matumizi ya umeme

$
0
0

Mabaki ya Nyumba ya Marehemu Maalim Rajab Mzee iliyopo Mtaa wa Rahaleo ambayo iliungua moto mapema asubuhi uliosababishwa na Hiter ya Umeme.
Wa kwanza na wa Pili kutoka Kulia ni miongoni mwa Watoto Tisa wa Familia ya Marehemu Maalim Jaba Mgeni wa Nyumba iliyoungoa Moto mapema asubuhi katika Mtaa wa Rahaleo wakimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mkasa uliowapata wa kuunguliwa Nyumba yao.
Balozi Seif akizungumza na vyombo vya Habari mara baada ya kutoa pole na kuisisitiza Jamii kuwa na tahadhari ya matumizi salama ya huduma za Umeme ili kuepuka maafa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud wakifika katika eneo la tukio kuifariji na kuipa pole Familia ya Watoto Tisa ya Marehemu Maalim Rajab Mzee kufuatia Nyumba yao kuungua Moto.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameinasihi Jamii Nchini kuwa na tahadhari kubwa wakati wa matumizi ya vifaa vya umeme ili kuwepuka madhara yanayoweza kuleta maafa makubwa hapo baadae.

Alisema Huduma ya umeme ni nzuri na muhimu katika matumizi ya mwanadamu kwenyea harakati zake na kimaisha za kila siku lakini inaweza kuwa janga iwapo mwanaadamu huyo ataamua kutumia huduma hivyo ovyo.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo muda mfupi tu alipopata taarifa ya kutokea kwa Janga la Moto katika Nyumba ya Familia ya Marehemu Maalim Rajab Mgeni iliyopo Rahaleo mbele ya Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Muembe Shauri.

Hata hivyo hakuna mtu aliyepata matatizo kutokana na mripuko wa moto huo uliosababishwa na kuungua kwa Hita iliyokuwemo kwenye Nyumba hiyo ambayo wakati inawaka alikuwemo Kijana Mmoja wa familia ya Marehemu Maalim Rajab Mgeni.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuzingatia umuhimu wa kulinda maisha na mali za Rais imeazimia kujenga Vituo vya Huduma za Zimamoto kila Wilaya kwa lengo la kuwa tayari wakati yanapojitokeza matukio ya majanga.

“ Umeme tunaupenda sana katika matumizi yetu ya kawaida ya kila siku lakini pia unahatari iwapo hatutakuwa makini katika matumizi yake ya ovyo”. Alisisitiza Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikipongeza Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar kwa umakini wake uliopelekea kuuzima moto huo kwa dakika chake na kuepusha maafa ya kuendelea kuathiri nyumba zilizo jirani na eneo hilo.

USHAURI WA JULIUS MTATIRO IWAPO ATAONANA NA RAIS DK. MAGUFULI HUU HAPA

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KADA mpya wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Julius Mtatiro amesema iwapo atapata nafasi ya kuonana na Mwenyekiti wa Chama hicho kuna jambo la msingi ambalo anataka kumshauri kwa maslahi ya Watanzania walio wengi.

Mtatiro ambaye kabla ya kujiunga na CCM alikuwa Chama cha Wananchi(CUF) ambapo akiwa huko alishika nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za juu na sasa anasema baada ya kujiunga CCM anaoana ni kama ameutua mzigo mzito uliokuwa kichwani.

Akizungumza na Michuzi Blog katika mahojiano maalum yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam Mtatiro amezungumzia mambo mbalimbali na kubwa ni kwamba viongozi wa ngazi zote za juu ndani ya CCM wamempokea na kumpa baraka na siku yoyote atachukua kadi.

Alipoulizwa iwapo atapata nafasi ya kuonana na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk.John Magufuli Mtatiro amejibu iwapo atakutana naye atamshauri umuhimu wa kuongeza juhudi katika kupambana na umaskini nchini.Amesema anapongeza juhudi zinazoendelea katika kuondoa umaskini lakini ukweli ni kwamba umaskini bado mkubwa na anaamini Rais akifanikiwa katika hilo atakuwa ameondoa changamoto inayowakabili Watanzania wengi.

Amesema sababu za yeye kuamua kuingia katika siasa ni kutokana na hali ya umasikini uliopo kwenye familia anayotoka na jamii inayomzunguka.Hivyo anasema aliamini akiwa katika siasa atashiriki kuhamasisha na kuweka mipango ya maendeleo na ndio maana siku zote amekuwa akishauri namna bora ya kuondoa umaskini nchini.

"Jambo kubwa ambalo nitamueleza Mwenyekiti wangu wa CCM ni kumshauri aongeze kasi katika kuondoa hali ya umaskini kwani watanzania wengi wamezungukwa na umaskini." Ndio maana pamoja na sababu nyingi ambazo nimetoa wakati naondoka CUF moja ilikuwa ni kujiunga na CCM ili kama kijana na Mtanzania mzalendo nishiriki katika kuzungumzia na kuhamasisha maendeleo badala ya kukaa upande wa kupinga kila kinachofanyika,"amesema Mtatiro.

Alipoulizwa anajisikiaje anavyoshambuliwa na kutukanwa na baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii,Mtatiro amejibu anaona na kusikia namna anavyotukanwa lakini haimuumizi kwani anaamini amefanya uamuzi sahihi.Amefafanua kabla kuondoka CUF amefanya utafiti wa kutosha kwa kuangalia aina ya siasa za upinzani, siasa za nchi na CCM na kuona sehemu sahihi ni huko alikokwenda sasa kwani yupo salama.

Mtatiro amesema anatambua wapo walioumia kwa kuondoka upinzani kwasababu mbalimbali kwani anaamini akiwa CUF wapo waliokuwa wakimfanya daraja ili kufanikisha mambo yao.Pia wapo walioumia kwasababu walikuwa wanafurahishwa na siasa ambazo alikuwa anazifanya na hasa kwa vijana ambao wapo waliotamani kuwa kama yeye.

Ameongeza wapo ambao wanafurahishwa na uamuzi wake wakiamini yupo sahihi,hivyo wanaomtukana na kumkejeli hawamuumizi kichwa na hana muda wa kushindana nao.Alipoulizwa iwapo amewasiliana na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba ,amejibu hana mawasiliano naye na hajawahi kuwasiliana naye.Amesema anafahamu Prof.Lipumba yupo CUF kwasababu ya kukimaliza Chama hicho upande wa Bara na baada ya hapo ataendelea na siasa kwenye majukwaa mengine ya kisiasa.

Alipoulizwa kuhusu kauli ya Prof.Lipumba kwamba Mtatiro walimuokota,amejibu hivyo ni vijembe vya kisiasa na havina madhara kwake."Hiyo kauli ya kwamba amenikota ni kijembe tu lakini ukweli nimefanya mambo makubwa ya mabadiliko ndani ya CUF.Uwepo wangu umetoa mchango mkubwa wa kuijenga CUF upande wa Bara.

" Pamoja na kwamba anasema waliniokota nashukuru nimetoa mchango mkubwa na hata idadi ya wabunge na madiwani iliongeza.Subiri uone kitakachotokea uchaguzi mkuu wa 2020.Muda ukifika ukweli utaeleweka,"amesema.Alipoulizwa mbona amekuwa kimya baada ya kujiunga CCM ,amesema tayari kunashughuli za kichama anazoendelea kuzifanya.

Alipoulizwa anaizungumziaje CUF ambayo Mwenyekiti wake ni Prof.Lipumba ,Mtatiro anasema haoni afya ya Chama hicho zaidi ya kukiua kabisa.Amesema anaweza asieleweke leo kuhusu hilo lakini Watanzania watathibitisha anachokieleza miaka miwili kuanzia sasa.

Alipoulizwa kuna tofauti gani kati ya Mtatiro wa CUF na huyu ambaye amejiunga CCM,amejibu jukumu lake la msingi la kujiunga CCM amelieleza kwa kina ila anachoahidi ni ushiriki wake katika harakati za siasa za maendeleo na zenye tija kwa Taifa."Mtatiro nitabaki yule yule wa kuchambua mambo kwa kina na kutoa ushauri kwa maslahi ya nchi yangu.

"Tofauti ambayo itajitokeza sitakuwa kwenye siasa za kupingana na maendeleo yanayofanyika bali nitatumia akili na maarifa yangu yote kuhakikisha tunapiga hatua za kimaendeleo," amesema Mtatiro.

KORTINI KWA TUHUMA ZA KUONGOZA MBINU ZA KIHALIFU,KUSAIDIA KUSAFIRISHA BINADAMU

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

WATU nane wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na tuhuma za kuongoza mbinu za kiuhalifu na kusaidia kusafirisha binadamu.

Hata hivyo, ni watuhumiwa wanne tu waliofanikiwa kusomewa mashtaka yao kwa kuwa watuhumiwa wengine wanne hawakuwa wakijua lugha ya Kiswahili wala Kingereza.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Faraji Nguka  amewataja washtakiwa wanne waliosomewa mashtaka yao kuwa ni, Abdallah Kassim Bashrahil, Idd Hussein Said, Muhidin Said Machelenga, Swed Twaibu Swed.

Mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde imedaiwa kuwa, katika siku na mahali tofauti tofauti, ndani ya Jiji la Dar es Salaam, na nchi ya Comorro washtakiwa hao waliongoza genge la uhalifu na kuweza kutekeleza tukio la kusafirisha binadamu kutoka Comorro kwenda Saudi Arabia kupitia Tanzania. 

Katika shtaka la pili imedaiwa kuwa, siku na mahali hapo hapo, washtakiwa hao, walisaidia kuwasafirisha Halima Mmadi, Tereha Mlahaili, Ali Miraaji na raia 162 huku wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Imedaiwa  walifanya hivyo kwa kuwapatia hati za kusafiria za Tanzania huku wakijua kuwa watu hao ni raia wa Commoro. 
Pia washtakiwa wanadaiwa kufanya hivyo ili kuwarahisishia kupata kibali cha makazi kutoka Idara ya Uhamiaji ya Tanzania kwa lengo la kuwasafirisha watu hao kwenda nchini Saudi Arabia.

Hata hivyo, washtakiwa hawakutakiwa kujibu kitu chohote mahakamani hapo kwani Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi hadi mahakama kuu au kwa kupata kibali kutoka kwa DPP.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 27 mwaka 2018 kwa ajili ya washtakiwa wengine wanne kusomewa mashtaka yao mkalimani atakapopatikana

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi bado haujakamilika.

 Watuhumiwa wanaotarajiwa kusomewa mashtaka yao Jumatatu ni Said Ally, Ahamada Mchangama, Hamada Ali Ben Ali na Suulaimana Abdallah.

UTARATIBU MPYA WA KUSAJILI KAMPUNI

$
0
0
Na Bashir Yakub.
TOKEA April mwaka huu 2018 utaratibu wa kusajili kampuni umebadilika. Ni tofauti kabisa na ambavyo tulizoea.Hata hivyo, yapo mambo ambayo yamebaki vile vile kama awali, kadhalika yapo mengi pia yaliyobadilika.
Tutapitia utaratibu wa awali kidogo na huu mpya.

UTARATIBU WA AWALI.
a ). Ulikuwa unatakiwa kuandika barua kuuliza jina unalotaka kutumia kama jina la kampuni iwapo lipo au hapana. Kama lipo ungetakiwa kuleta jingine, na kama halipo ulikuwa unapewa ruhusa ya kulitumia katika usajili.

b ).Ulikuwa unatakiwa kuandaa waraka na katiba ya kampuni(article and
memorandum of association). Zilikuwa zinatakiwa kwa uchache angalau nakala nne.

C ) Ulikuwa unatakiwa kupakua fomu namba 14(a) na 14( b ) kutoka kwenye
mtandao wa BRELA, au kuzifuata fomu hizo hapohapo BRELA ambapo ungetakiwa kuzijaza kisha kuzisaini.

d ) Kisha ulikuwa unatakiwa kubeba hizo nakala za waraka na katiba ya kampuni, pamoja na hizo fomu zilizojazwa na kuzipeleka BRELA mnazi mmoja jengo la ushirika kwa ajili ya usajili.

e ) Huko BRELA, baada ya kuzipitia na kuona hazihitaji masahihisho sasa
ungepewa ruhusa ya kulipia ambapo malipo yalikuwa yakifanyika kupitia benki ya CRDB.

f ) Baada ya hapo ungetakiwa kusubiri kipindi cha wiki moja au wiki na
sikukadhaa, au wiki mbili ili uweze kupatiwa cheti rasmi cha usajili wa
kampuni(certificate of incorporation).
KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com

NAIBU WAZIRI WA NISHATI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA YA MOU-KAMPALA- UGANDA

$
0
0

TANZANIA na Uganda zilitia saini Mikataba mbalimbali ya ushirikiano ikiwa pamoja na Mkataba wa Uendelezaji wa Bomba la Kusafirisha Gesi Asilia kutoka Tanzania kwenda Uganda na mwingine ni Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Kupeleka Umeme katika Vijiji vya Mpakani mwa Tanzania na Uganda.

Uwekaji saini huo ulifanyika katika Mkutano wa Pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika Kampala Uganda kwa siku tatu kuanzia tarehe 21 Agosti 2018.

Miradi mingine iliyojadiliwa katika Mkutano huo ni pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Uganda kuja Tanzania (EACOP), Mradi wa Utafutaji wa Mafuta katika Kitalu cha Eyasi Wembere, Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Murongo Kikagati (14MW) na Mradi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Nsongezi (MW 35).

Mkutano huo pamoja na mambo mengine ulifanya tathmini ya utekelezaji wa masuala yaliyokubalika wakati wa mkutano wa kwanza wa JPC uliofanyika Arusha mwezi Aprili 2017 na kuweka mikakati ya utekelezaji kwa masuala ambayo hayajakamilika.

Aidha, ulijadili mikakati ya kuondoa vikwazo vya kibiashara kwa nchi hizo mbili.

Katika Mkutano huo ujumbe wa Wizara ya Nishati uliongozwa na Naibu Waziri,  Subira Mgalu, pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Wizarani, TANESCO na Shirika la Maendeleo ya Petroli ( TPDC)
Naibu Waziri wa Nishati, Subira  Mgalu akishuhudia utiaji saini wa Mikataba ya Makubaliano (MoU) inayohusu utekelezaji wa Miradi ya Umeme na Gesi asilia, kati ya Tanzania na Uganda. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga.
Watendaji mbalimbali wa Serikali za Uganda na Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza Mkutano wa Pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika Kampala Uganda kwa siku tatu kuanzia tarehe 21 Agosti 2018.

KATIBU MKUU WA SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI ATEMBELEA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

$
0
0
SHIRIKA la Hali ya Hewa Duniani (World Meteorological Organization (WMO)) ni taasisi mahsusi la Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya ushirikiano wa kimataifa yanayohusiana na ufuatiliaji wa mifumo ya hali ya hewa na namna mifumo hii inavyoathiri mazingira yetu. 

Shirika hufanya kazi zake kupitia taasisi za hali ya hewa za nchi wanachama (National Meteorolgical and Hydrological Services - NMHSs) ambapo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ni mwakilishi rasmi wa shirika hili hapa nchini. 

Katibu Mkuu wa WMO amefanya ziara katika ofisi za TMA ili kujionea shughuli za hali ya hewa na namna ambavyo WMO inaweza kusaidia katika maeneo mbalimbali yahusuyo hali ya hewa ikiwa pamoja na mafunzo na vifaa vya hali ya hewa. Aidha aliipongeza TMA katika juhudi zake za utekelezaji wa programu za WMO na kuzisaidia nchi zingine za Afrika. 

Aliongeza kwa kusema kuwa TMA ni taasisi ya mfano Afrika katika utoaji wa huduma bora za hali ya hewa 
IMETOLEWA NA KITENGO CHA UHUSIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA .
   Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akishuhudia na kushiriki mkutano wa kuandaa utabiri wa siku unaofuatilia hali mbaya ya hewa kwa nchi za Afrika mashariki zilizoko katika Bonde la Ziwa Victoria.
 Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas katika picha ya pamoja na menejimenti ya TMA.
 Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akichangia jambo baada ya kupata maelezo ya mfumo wa kisasa utoaji taarifa za hali ya hewa kwa usafiri wa anga wakati alipotemebelea ofisi za hali ya hewa zilizopo katika Uwanja wa ndege wa Kiamataifa wa Julius Nyerere. hewa.

Hospitali za Wilaya 67 Kujengwa Mwaka Huu wa Fedha

$
0
0
Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma.

SERIKALI ya Awamu ya Tano Kujenga Hospitali za Wilaya 67 katika mwaka huu wa  fedha ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuimarisha sekta ya Afya nchini.

Akizungumza Katika Kipindi cha TUNATEKELEZA Kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na kuratibiwa na Idara ya Habari MAELEZO, Waziri wa Nchi Ofisi  ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa Serikali itatumia shilingi bilioni 105 kutekeleza mradi huo.

 “Tangu tupate uhuru tulikuwa na hospitali za wilaya 77 lakini sasa Serikali ya Awamu ya Tano inaenda kuweka historia kwa mageuzi makubwa yanayofanyika katika sekta hii ya afya na tumejipanga kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata huduma bora za afya,” alisisitiza Mhe. Jafo.

Akifafanua Mhe. Jafo amesema kuwa Serikali  imeweka  historia, kwa kuwa tangu Taifa lipate uhuru kulikuwa na vituo vya afya vinavyofanya upasuaji 115 nchi nzima lakini katika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali imejenga vituo vya afya vyenye uwezo wa kufanya upasuaji 208 vinavyoenda sambamba na ujenzi wa hospitali za wilaya zinazoanza kujengwa  mwaka huu.

Aidha amesema, Bohari Kuu ya Dawa (MSD) imeshapatiwa fedha ili iweze kusambaza vifaa tiba katika vituo vya afya vilivyojengwa ili viweze kuanza kufanya kazi.Katika mwaka wa fedha 2017/2018 Mamlaka za Serikali za Mitaa zimapata mafanikio makubwa katika kuimarisha sekta za elimu,  afya na ujenzi wa miundo mbinu kama barabara, vyumba vya  madarasa na miundo mbinu mingine inayochochea  maendeleo ya wananchi.

Pia ameziagiza Halmashuri zote nchini kusimamia ukusanyaji wa mapato, lengo likiwa ni kuweka mfumo mzuri wa ufuatiliaji ili kuboresha makusanyo na  kusimamia matumizi ya fedha hizo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.“Nawataka wakurugenzi wote wawe wakali katika ukusanyaji mapato na tutatoa onyo maalum kwa halmashauri zote ambazo hazifanyi vizuri katika ukusanyaji mapato,” alisema Mhe. Jafo.

Kipindi cha TUNATEKELEZA kinaratibiwa na Idara ya HABARI MAELEZO na kurushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na awamu hii inawashirikisha Mawaziri wote ambapo wanapata fursa ya kueleza utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Sera na program mbalimbali  zinazotekelezwa na Serikali.
 Sehemu ya Vifaa vya Kisasa vya Upasuaji kama vinavyoonekana katika moja ya vituo vya afya vilivyojengwa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Wataalamu wa afya wakikagua sehemu ya vifaa tiba vipya  katika moja ya Kituo cha afya kilichojengwa na Serikali ya Awamu ya Tano.
(Picha zote na OR- TAMISEMI).

WARAMI WAMVAA MBOWE WAMTAKA ASIIPANGIE KAZI MAHAKAMA

$
0
0

Mkurugenzi wa Tafiti wa Warami, Philipo Mwakibinga

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kuishukia mahakama kuwa haimtendei haki, Watetezi wa Rasilimali za taifa Wasio na Mipaka (WARAMI) wameibuka na kupinga vikali kitendo hicho kwa kusema Mahakama aingiliwi wala aipangiwi hivyo ni vyema wakaicha ifanyekazi kwa weledi .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo , Mkurugenzi wa Tafiti wa Warami, Philipo Mwakibinga, alisema kitendo kilichofanywa na Mbowe cha kulalamika kwa vyombo vya habari kuhusu kesi ambayo bado ipo mahakamani, ni fedheha na kuidhalilisha Mahakama.

Amesema Mbowe kupitia tamko lake alidai kuwa kuna viashiria ambavyo vinaonyesha kuwa mahakama inaingiliwa na dola huku akijua kwamba si kweli na kwamba mahakama ni mhimili unaotenda kazi zake kwa uhuru.

“Si mara ya kwanza kwa Mbowe kuingilia uhuru wa mahakama hasa pale anapoona kuwa kusa analoshtakiwa nalo linaweza kumtia hatiani kwa mujibu wa sheria,” alisema Mwakibinga na kuongeza Mbowe anafanya hivyo kwa nia ya kupata huruma ya watanzania.

“Jana (juzi) kupitia tamko lake alisema kuwa dola inaingilia mahakama ili kuishinikiza yeye ashindwe. Utagundua kwamba huku ni kuvunja sheria na taratibu ambazo tumejiwekea. Tunafahamu kwamba suala lililopo mahakamani halipaswi kuzungumzwa katika public (hadharani) likiwa bado linaendelea mahakamani,” amesema Mwakibinga.

amesema Mbowe kupitia vyombo vya habari alitoa kauli za uchochezi na kulitisha Taifa kwa kusema kuwa yatatokea yale yaliyotokea nchini Uganda.“Kwanini Mbowe anatumia vibaya uhuru wake wa kujieleza, je anahaki miliki ya nchi hii? Kwanini ameanza kuitilia shaka mahakama kwamba haitamtendea haki,”

Amesema pamoja na Mbowe kudai kuwa wameonewa kuhusu sakata la kifo cha Mwanafunzi Akwilina ambacho kilitokea wakati wa maandamano yao, watu wanajua kuwa kifo hicho kilisababishwa na wao kwa mazingira yeyote.

“Mbowe ndiye aliyehamasisha watu kwenda kufuata barua za mawakala kwa maandamano tena yasiyo na kibali, lakini pia Mbowe amenukuliwa akisema kwamba wapo tayari kubeba majeneza zaidi ya 200, sasa yawezekana hilo jeneza moja lilikua kati ya hayo aliyosema,” amesema.

Amesema endapo Mbowe na wafuasi wao wasingeenda kufuata barua kwa maandamano hakuna machafuko ambayo yangetokea na kwamba kifo cha Akwilina kisingetokea.

“Ukijaribu kuangalia mwenendo mzima wa tukio hilo Mbowe anaona kabisa anayo hatia na ndiyo maana anakimbia na kusema anaonewa huku akilalama suala la wakili wake kujitoa ambalo kimsingi ni kawaida endapo wakili anaona atafedheheka kutetea watu ambao wana hatia, alitaka wakili afanye nini?” amehoji.

“Hawa ndio ambao kwa miaka yote wamekuwa wakilalamika mahakama zetu zinachelewesha kesi, leo hii mahakama zimeongeza ufanisi na kujitahidi kusikiliza mashauri kwa haraka wao wanadai kesi inapelekwa haraka,” amesema .Aidha alitoa wito kwa vyombo vya usalama nchini kumchukulia Mbowe hatua za kisheria kutokana na kutoa matamko ya kichochezi licha ya kuwa ni mshtakiwa wa kesi ya uchochezi.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA BALOZI WA CHINA HAPA NCHINI LEO

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa China Nchini Tanzania Bibi Wang Ke kabla ya kuanza kufanya mazungumzo ya kikazi katika ofisi yake ndogo Jijini Dar es salaam leo Agosti 24/2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekutana na Balozi wa China Nchini Tanzania Bibi Wang Ke nakufanya naye mazungumzo ya kikazi katika ofisi yake ndogo Jijini Dar es salaam   leo    Agosti 24/2017

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Changamkieni hii fursa iliyotolewa na Ubalozi wa India- RC Mwanza

$
0
0
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella akifungua mkutano baina ya balozi wa India nchini Tanzania na wafanyabiashara mkoani Mwanza uliolenga kuangazia fursa za kibiashara kati ya Mwanza na India.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella amewataka wafanyabiashara kutumia vyema fursa za kibiashara zilizofunguliwa na Ubalozi wa India hapa nchini kwa kutanua wigo wa biashara zao.


Mhe. Mongella ametoa rai hiyo wakati akifungua mkutano baina ya Balozi wa India nchini Tanzania na wafanyabiashara mkoani Mwanza kupitia taasisi ya wafanyabiashara wa kilimo na viwanda TCCIA uliofanyika jana katika ukumbi wa Rock City Mall Jijini Mwanza.


Alisema Tanzania na India ni nchi ambazo zina uhusiano wa miaka mingi tangu enzi za Uhuru hivyo wawekezaji na wafanyabiashara mkoani Mwanza watumie fursa iliyotolewa na India ya kuwaunganisha na wafanyabiashara wa Tanzania na nchi hiyo hatua itakayoleta chachu ya mafanikio katika kuelekea Tanzania ya Viwanda.


Awali Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Sandeep Arya alisema nchi hiyo ni miongoni mwa wawekezaji wakubwa nchini Tanzania ikiwa na uwezo wa hali ya juu katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali hususani zana kilimo, viwanda, vyombo vya usafiri, afya pamoja na elimu hivyo mkutano huo umelenga kuongeza ushirikiano zaidi wa kibiashara baina ya India na Tanzania.


Akizungumza na wanahabari, Mwenyekiti wa TCCIA mkoani Mwanza, Dkt. Elibariki Mmari alieleza fursa mbalimbali zilizopo mkoani Mwanza ikiwemo uwekezaji wa viwanda vya nguo, bidhaa za ngozi, ujenzi wa makazi ya kisasa pamoja na ufugaji wa samaki na hivyo kuhimiza India kutumia vyema fursa hizo kuwekeza mkoani Mwanza huku watanzania nao wakitumia fursa ya ushirikiano uliopo na India kwenda kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo teknolojia kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Sandeep Arya akielezea fursa za kibiashara zilizopo India na namna India inashirikiana na Tanzania kibiashara
Katibu wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Hassan Karambi akizungumza jambo kwenye mkutano huo
Mshiriki akichangia mada
Mshiriki
Wanafunzi pia walialikwa kwenye mkutano huo ili kujifunza fursa za kibiashara baina ya Mwanza na India
Mshiriki akichangia mada
Mgeni rasmi, RC John Mongella akiwasili ukumbini
Mgeni rasmi akikagua mabanda ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa India
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella (kushoto), akiagana na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Sandeep Arya (kulia).
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images