Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1655 | 1656 | (Page 1657) | 1658 | 1659 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2018, Charles Kabeho akizindua mradi wa vyumba vitatu vya madarasa Shule ya msingi Wishiteleja wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Taraba.
  Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Charles Kabeho akiwa ndani ya chumba cha darasa cha Shule ya sekondari Maganzo ambao ni mradi wenye thamani ya sh. miloni 141 uliogharamiwa na fedha kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). 
  Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Charles Kabeho akikagua moja ya vyumba vya madarasa Shule ya msingi Wishiteleja wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo
  Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa katika maeneo mbalimbali wilayani Kishapu ambako ulikagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani sh. bilioni 2.2.
  Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Charles Kabeho akipata maelezo kuhusu uandaaji wa chakula cha kulisha ng’ombe alipofika katika mradi wa unenepeshaji wa mifugo hiyo eneo la Ukenyenge ambao unamilikiwa na mjasiliamali Eliud Urasa ukiwa na thamani ya sh. milioni 285.
  Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Taraba (kulia) akimuongoza Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Charles Kabeho (kulia kwake) kwenda kukagua mradi wa utengenezaji wa madawati unaondelea katika ofisi za Halmashauri ya wilaya hiyo wenye thamani ya sh. milioni 289.3.
  Mhandisi wa Maji Wilaya ya Kishapu, Lucas Said (kushoto) akitoa maelezo kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Charles Kabeho kuhusu mradi wa maji kijiji cha Unyanyembe wakati Mwenge wa Uhuru ulipofika na kuweka jiwe la msingi ambapo una thamani ya sh. milioni 453.
  Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Charles Kabeho akikagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Songwa wenye thamani ya sh. milioni 400. Wengine pichani kushoto ni diwani wa Kata ya Songwa, Mhe. Abdul Ngolomole na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kishapu. Dkt. Josephat Shani.
  Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Charles Kabeho akizungumza na wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa nyumba za walimu shule ya sekondari Maganzo wenye thamani y ash. milioni 141. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Taraba.
  Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Taraba (kushoto) na mwenzake wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Hyasinta Mboneko wakikabidhiana Mwenge wa Uhuru katika eneo la Wame mara baada ya kumaliza mbio zake wilayani Kishapu.


  ………………….


  Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi

  Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2018, Charles Kabeho ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa kutekeleza miradi ya maendeleo yenye ubora na kwa gharama nafuu.

  Pia ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutoa fedha kwa ajili ya uimarishaji wa vituo mbalimbali vya afya pamoja na sekta ya elimu.Kabeho ametoa pongezi hizo jana kwa nyakati tofauti wakati akikagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya mendeleo wilayani humo ambako Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa.

  Sanjari na hilo Kiongozi huyo alipongeza wilaya hiyo kwa kuishirikisha jamii katika kutekeleza miradi hiyo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya elimu na afya jambo ambalo linachangia uboreshaji wa sekta hizo.“Kishapu mna kitu cha pekee tofauti na huko kwengine nilikopita, hapa ninyi katika miradi yenu mlipopewa fedha ndani ya gharama mmebakiza chenji na mnaongeza miradi mingine kwa fedha hizo hizo hivyo mnafanya kitu cha kuigwa,” alisema.

  Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge aliongeza kuwa kwa kuishirikisha jamii katika utekelezaji wa miradi hali inayoifanya nayo ifanye uwekezaji wa maendeleo katika senkta mbalimbali.Mwenge wa Uhuru wenye ujumbe “Elimu ni Ufunguo wa Maisha, Wekeza Sasa kwa maendeleo ya Taifa letu” ulikabibidhiwa mkoani Shinyanga wilayani Kishapu ukitokea wilayani Maswa mkoani Shinyanga umepitia miradi ya sh.bilioni 2.2.

  0 0  Na Benny Mwaipaja, WFM, Mtwara

  WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameuahidi uongozi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Naliendele kwamba Serikali itakiwezesha Kituo hicho na vituo vingine vya utafiti nchini ili viendeleze kazi ya utafiti wa mazao ya kilimo ambacho kinategemewa na watanzania wengi katika kujikwamua kiuchumi.

  Dkt. Mpango ametoa ahadi hiyo alipotembelea Kituo cha Utafiti Naliendele, mkoani Mtwara, ambacho uongozi wake ulielezea wasiwasi wake wa kupata rasilimali fedha za kuendeleza utafiti wa mazao likiwemo zao la korosho pamoja na watumishi baada ya kuondolewa kwa fedha za ushuru wa korosho inayouzwa nje, zilizokuwa zikitumika kuendeleza utafiti huo.

  Alisema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa shughuli za utafiti katika kuendeleza uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla na kwamba atajitahidi kama Waziri wa Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Waziri mwenzake anayeshughulikia kilimo ili taasisi hiyo isikwame kufanya shughuli zake.

  "Niwahakikishie kabisa kwamba Serikali haitakubali utafiti wa mazao yote unaofanyika hapa likiwemo zao la korosho udhurike, litakuwa ni janga kubwa, kwahiyo upatikanaji wa fedha za Kituo hiki litakuwa ni moja ya vipaumbele vyangu" alisisitiza Dkt. Mpango

  Alisema kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa Taifa na kwamba hakutakuwa na mapinduzi ya viwanda bila kilimo kwa sababu viwanda vinavyojengwa vinatarajiwa kuongeza thamani ya mazo ya kilimo pamoja na mazao ya mifugo na uvuvi.

  Awali, Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Naliendele, Dkt. Omari Mponda, alieleza kuwa Kituo chake kinahitaji zaidi ya shilingi bilioni 7 kwa mwaka ili kiweze kuendeleza shughuli za utafiti hasa baadaya Serikali kuamua kupanua shughuli za utafiti wa zao la korosho kwenye mikoa mingine nchini.

  Alisema kuwa hivi sasa Kituo kimeelekeza nguvu zake katika utafiti wa ugonjwa mpya unaoathiri kwa kiwango kikubwa zao la korosho ujulikanao kama mnyauko fusari (Fusarium wilt) , ulioathiri zao hilo katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mkuranga, Masasi, Tandahimba, Mtwara na Liwale, lakini changamoto kubwa inayowakumba ni ukosefu wa fedha za kuendeleza utafiti huo.

  "Mheshimiwa Waziri, Kituo hiki pia kina zaidi ya asilimia 50 ya watumishi ambao wameajiriwa kwa njia ya mikataba na wanahitaji kulipwa vizuri ili wabaki Kituoni hapa kuendeleza shughuli za utafiti ndio maana nasema tuna mahitaji makubwa ya fedha na tunaiomba Serikali iliangalie jambo hili" Alisema Dkt. Mponda.

  Kituo cha Utafiti Naliendele kilichoko mkoani Mtwara kinatajwa kuwa ni kitovu cha utaalamu wa zao la korosho katika Bara la Afrika na kwamba tafiti nyingi, ikiwemo aina 54 za mbegu za zao la korosho kunakifanya kituo hicho kuwa tegemeo kwa masuala ya utafiti katika nchi nyingi za afrika ambazo hutumia Taasisi hiyo kupata teknolojia ya uzalishaji wa mbegu bora za mazao mbalimbali hususan korosho.


  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akipata maelezo kuhusiana na zao la Korosho,alipotembelea Kituo cha Utafiti Naliendele, mkoani Mtwara
  Mmoja wa Wataalamu pichani juu na chini kutoka kituo cha Utafiti Naliendele akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipotembelea Kituo cha Utafiti Naliendele, mkoani Mtwara

  0 0

  Na Andrew Chale, Dar

  Tamasha kubwa na la aina yake la muziki wa Kiafrika maalum kumuenzi gwiji wa muziki Hayati Dk. Remmy Ongala lililopewa jina la ONGALA MUSIC FESTIVAL, linatarajiwa kulindima kwa mara ya kwanza kuanzia hapo kesho katika fukwe mwanana za Malaika Beach Club, Kigamboni, Agosti 23-25.

  Akizungumza Mratibu wa tamasha hilo Bi. Aziza Ongola anaesimamia mfuko wa Ongala (Ongala Foundation), amesema tayari maandalizi yote yameenda vizuri na watu wakae mkao wa kulishuhudia tamsha hilo ambalo ni la urithi wa muziki kutoka kwa gwigi Dk. Remmy.

  Aziza amesema kuwa, Wasanii mbalimbali kutoka Nchi tofauti za Afrika na bendi zao watatoa burudani kwa muda wa siku tatu yaani kuanzia Agosti 23-25,2018 katika fukwe hizo za Malaika, Kigamboni.

  “Tutamuenzi Baba kupitia nyimbo zake nyingi ambazo zimekuwa na umaarufu ndani na nje ya Afrika. Hivyo tamasha ili ni kuamsha hali ya Muziki aliouacha na pia kuendelea kumkumbuka kupitia mashairi yake” alieleza Aziza.Aziza ameongeza kuwa, tamasha hilo pia litasaidia kuimarisha kumbukumbu na kazi za gwiji huyo aliyefariki Desemba 2010, Nchini.

  Kwenye tamasha hilo vikundi 22 kutoka nchi mbalimbali za Afrika vitatumbuiza kwa siku hizo tatu.Miongoni mwa wasanii hao ni msafiri Zawose, Ally Swahi, Siti and the Bend, Hokororo, King kiki na Sikinde. Pia atakuwepo Ashimba, Carola Ongala Music Festival kulindima kesho Agosti 23-25,Kigamboni

  Tamasha kubwa na la aina yake la muziki wa Kiafrika ambalo ni maalum kumuenzi gwiji wa muziki Hayati Dk. Remmy Ongola lililopewa jina la ONGALA MUSIC FESTIVAL, linatarajia kulindima kwa mara ya kwanza kuanzia hapo kesho katika fukwe mwanana za Malaika Beach Club, Kigamboni.

  Akizungumza Mratibu wa tamasha hilo Bi. Aziza Ongola anaesimamia mfuko wa Ongala (Ongala Foundation), amesema tayari maandalizi yote yameenda vizuri na watu wakae mkao wa kulishuhudia tamsha hilo ambalo ni la urithi wa muziki kutoka kwa gwigi Dk. Remmy.

  Aziza amesema kuwa, Wasanii mbalimbali kutoka Nchi tofauti za Afrika na bendi zao watatoa burudani kwa muda wa siku tatu yaani kuanzia Agosti 23-25,2018 katika fukwe hizo za Malaika, Kigamboni.

  “Tutamuenzi Baba kupitia nyimbo zake nyingi ambazo zimekuwa na umaarufu ndani na nje ya Afrika. Hivyo tamasha ili ni kuamsha hali ya Muziki aliouacha na pia kuendelea kumkumbuka kupitia mashairi yake” alieleza Aziza.

  Aziza ameongeza kuwa, tamasha hilo pia litasaidia kuimarisha kumbukumbu na kazi za gwiji huyo aliyefariki Desemba 2010, Nchini.Kwenye tamasha hilo vikundi 22 kutoka nchi mbalimbali za Afrika vitatumbuiza kwa siku hizo tatu.
  Miongoni mwa wasanii hao ni msafiri Zawose, Ally Swahi, Siti and the Bend, Hokororo, King kiki na Sikinde. Pia atakuwepo Ashimba, Carola Kinasha na wengine wengi Pamaoja na buradani hizo zitakazoanza muda wa jioni, pia milango itafunguliwa kuanzia asubuhi kwa Semina na Warsha kwa wasanii, Biashara mbalimbali na micheze ya Watoto.

  Kiingilio kwenye tamasha hilo ni Tsh. 10,000/ kwa mtu Mmoja huku gharama hiyo ya kiingilio ikitarajiwa kupungua kwa kuanzia watu watano gharama zitapungua.Mwisho. wa na la aina yake la muziki wa Kiafrika maalum kumuenzi gwiji wa muziki Hayati Dk. Remmy Ongala lililopewa jina la ONGALA MUSIC FESTIVAL, linatarajiwa kulindima kwa mara ya kwanza kuanzia hapo kesho katika fukwe mwanana za Malaika Beach Club, Kigamboni, Agosti 23-25.

  Akizungumza Mratibu wa tamasha hilo Bi. Aziza Ongola anaesimamia mfuko wa Ongala (Ongala Foundation), amesema tayari maandalizi yote yameenda vizuri na watu wakae mkao wa kulishuhudia tamsha hilo ambalo ni la urithi wa muziki kutoka kwa gwigi Dk. Remmy.Aziza amesema kuwa, Wasanii mbalimbali kutoka Nchi tofauti za Afrika na bendi zao watatoa burudani kwa muda wa siku tatu yaani kuanzia Agosti 23-25,2018 katika fukwe hizo za Malaika, Kigamboni.

  “Tutamuenzi Baba kupitia nyimbo zake nyingi ambazo zimekuwa na umaarufu ndani na nje ya Afrika. Hivyo tamasha ili ni kuamsha hali ya Muziki aliouacha na pia kuendelea kumkumbuka kupitia mashairi yake” alieleza Aziza.Aziza ameongeza kuwa, tamasha hilo pia litasaidia kuimarisha kumbukumbu na kazi za gwiji huyo aliyefariki Desemba 2010, Nchini.

  Kwenye tamasha hilo vikundi 22 kutoka nchi mbalimbali za Afrika vitatumbuiza kwa siku hizo tatu.Miongoni mwa wasanii hao ni msafiri Zawose, Ally Swahi, Siti and the Bend, Hokororo, King kiki na Sikinde. Pia atakuwepo Ashimba, Carola Ongala Music Festival kulindima kesho Agosti 23-25,Kigamboni

  Tamasha kubwa na la aina yake la muziki wa Kiafrika ambalo ni maalum kumuenzi gwiji wa muziki Hayati Dk. Remmy Ongola lililopewa jina la ONGALA MUSIC FESTIVAL, linatarajia kulindima kwa mara ya kwanza kuanzia hapo kesho katika fukwe mwanana za Malaika Beach Club, Kigamboni.

  Akizungumza Mratibu wa tamasha hilo Bi. Aziza Ongola anaesimamia mfuko wa Ongala (Ongala Foundation), amesema tayari maandalizi yote yameenda vizuri na watu wakae mkao wa kulishuhudia tamsha hilo ambalo ni la urithi wa muziki kutoka kwa gwigi Dk. Remmy.

  Aziza amesema kuwa, Wasanii mbalimbali kutoka Nchi tofauti za Afrika na bendi zao watatoa burudani kwa muda wa siku tatu yaani kuanzia Agosti 23-25,2018 katika fukwe hizo za Malaika, Kigamboni.

  “Tutamuenzi Baba kupitia nyimbo zake nyingi ambazo zimekuwa na umaarufu ndani na nje ya Afrika. Hivyo tamasha ili ni kuamsha hali ya Muziki aliouacha na pia kuendelea kumkumbuka kupitia mashairi yake” alieleza Aziza.Aziza ameongeza kuwa, tamasha hilo pia litasaidia kuimarisha kumbukumbu na kazi za gwiji huyo aliyefariki Desemba 2010, Nchini.Kwenye tamasha hilo vikundi 22 kutoka nchi mbalimbali za Afrika vitatumbuiza kwa siku hizo tatu.

  Miongoni mwa wasanii hao ni msafiri Zawose, Ally Swahi, Siti and the Bend, Hokororo, King kiki na Sikinde. Pia atakuwepo Ashimba, Carola Kinasha na wengine wengi Pamaoja na buradani hizo zitakazoanza muda wa jioni, pia milango itafunguliwa kuanzia asubuhi kwa Semina na Warsha kwa wasanii, Biashara mbalimbali na micheze ya Watoto.

  Kiingilio kwenye tamasha hilo ni Tsh. 10,000/ kwa mtu Mmoja huku gharama hiyo ya kiingilio ikitarajiwa kupungua kwa kuanzia watu watano gharama zitapungua.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Hassan Khatib Hassan wakati alipowasili katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja leo kabla ya Swala ya Eid el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa katika Mkoa wa Kusini Unguja ambapo waislamu mbali mbali walihudhuria
     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na Mashekhe wakati alipowasili katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja kabla ya Swala ya Eid el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa katika Mkoa wa Kusini Unguja ambapo waislamu mbali mbali katika Mkoa huo walihudhuria
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa nne kulia) akijumuika na Viongozi na Waislamu mbali mbali na Mashekhe wa Mkoa wa Kusini Unguja katika swala ya Eid el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa leo katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja,ambapo Swala hiyo imeongozwa na Sheikh Suleiman Haji Ibrahim
  Waislamu mbali mbali wa Mkoa wa Kusini Unguja wakiwa katika swala ya Eid el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa leo katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini,ambapo Sheikh Suleiman Haji Ibrahim(hayupo pichani) aliongoza Swala hiyo,iliyohudhuriwa na Viongozi wa Kitaifa akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
  Baadhi ya akinamama waliojumuika katika swala ya Eid el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa leo katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini,Mkoa wa Kusini Unguja
  Sheikh Abdalla Issa Makame (kulia) kutoka Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini Unguja akisoma Khutba mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Viongozi wengine pamoja na Waislamu wa Mkoa wa Kusini Unguja leo baada ya Swala ya Eid el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa katika uwanja wa Jamhuri Makunduchi
  Waislamu wakimsikiliza Sheikh Abdalla Issa Makame (hayupo pichani) kutoka Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini akisoma Khutba ya Swala ya Eid el Hajj, mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Viongozi wengine pamoja na Waislamu wa Mkoa wa Kusini Unguja leo baada ya Swala hiyo iliyoswaliwa katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi
  Baadhi ya Viongozi na Wananchi waliohudhuria katika Swala ya Eid el Hajj wakisikiliza Khutba iliyosomwa na Sheikh Abdalla Issa Makame (hayupo pichani) kutoka Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini,ambapo Viongozi wa Kitaifa walihudhuria katika Swala hiyo iliyoswaliwa Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri Makunduzi Mkoa wa Kusini Unguja
  ais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) pamoja na Viongozi wengine na Waislamu mbali mbali waliohudhuria katika Swala ya Eid el Hajj wakiitikia dua iliyoombwa na Sheikh Abubakar Ali Mohamed (wa pili kuilia) baada ya Swala hiyo iliyoswaliwa Kitaifa katika Mkoa wa Kusini Unguja leo katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi, Wilaya ya Kusini.Picha na Ikulu

  0 0


  20 FINALISTS
  1 WINNER
  1 CROWN
  1CAR (Grand Prize)
  1 ' MISS TANZANIA 2018' TITLE HOLDER
  1 MISS WORLD 2018 REPRESENTATIVE .
  Who among these beautiful contestant will be the luckiest?? . On 8th September 2018 at Julius Nyerere International Convention Centre. This is definately something not to miss. A night of entertainment , performance from our beautiful contestants , glamour, fashion and style, intelligence and so much more...@cloudsfmtz

  Ticket za Miss Tanzania zinapatikana
  1. Theonetz Dar free market - ROOM F50
  2. Eaters Point -Masaki
  3. M'S Boutique - Mlimani City
  4. Dicksound - Magomeni
  5. Flying zone travel and tours- Shamo towers Mbezi Beach
  6. Aymans Boutique Salon & Spa-Kunduchi
  7.Jadore store- Mikocheni kwa Nyerere ABLA complex shop no 3
  Unaweza pia kununua kupitia application ya OTAPP.  Ambayo unaingia play store na ku download app ya OTAPP.  Kwa maelezo zaidi unaweza piga number 0719460871

  0 0

  Frank Mvungi- MAELEZO, Morogoro
  Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro Mhe. Adam Mgoyi  amewataka wananchi kutumia fursa zinazotokana na urasimishaji ardhi uliowezesha kutolewa kwa hati zaidi ya 300 za kimila za kumiliki ardhi kwa wakazi wa Kata ya Magubike Wilayani humo jana.
  Akizungumza na mamia ya wananchi  wa Kijiji hicho waliojitokeza katika hafla ya kutolewa kwa hati hizo amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano  ni kuleta ukombozi wa kiuchumi kwa wananchi wake kupitia mpango wa matumizi bora ya adhi uliotekelezwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara  za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) na Halmashuri ya Wilaya hiyo.
  “Tumieni hati hizi kutatua changamoto za kiuchumi kwani zinawawezesha kupata mitaji kutoka  katika taasisi za fedha zilizopo ambazo zimeonesha nia yakuwawezesha wananchi na nyingine zimeanza kutoa mikopo kwa wananchi wetu wenye hati za kimila” Alisisitiza Mgoyi.
  Akifafanua amesema kuwa hati  hizo zitasaidia kuondoa migogoro ya ardhi, kuongeza thamani ya ardhi na kuwapa wananchi uwezo wa kujiendeleza kiuchumi ambapo tangu MKURABITA ianze zoezi la urasimishaji ardhi Wilayani humo wananchi wengi wamenufaika na mikopo iliyowawezesha kuwa na kilimo chenya tija.
  Aliongeza kuwa Vijiji 37 vimenufaika na mpango wa matumizi bora ya ardhi katika Wilaya ya Kilosa ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kuwawezesha wananchi kiuchumi.
  “ Halmashuri ya Wilaya inao wajibu wa kutenga sehemu ya mapato yake ya ndani kuwawezesha wananchi katika upimaji wa ardhi na kuleta mpango bora wa matumizi ya Ardhi” Alisisitiza Mgoyi.
  Pia kwa kuzingatia umuhimu wa kurasimisha ardhi Mgoya alibainisha kuwa mpango huo  unasaidia kubainisha maeneo ya ufugaji na yale ya kilimo katika Wilaya hiyo.
   Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw. Adam Mgoyi akisisitiza kuhusu wananchi kutumia hati  za kimila za kumiliki ardhi kujiletea maendeleo ikiwemo kupata mikopo kutoka katika taasisi za fedha wakati wa hafla ya kuwakabidhi wananchi wa Kijiji cha Magubike Wilayani Kilosa hati hizo zilizotolewa baada ya maeneo yao kurasimishwa kwa kupimwa
   Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha  Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania ( MKURABITA) Bi. Serapia Mgembe akisisitiza umuhimu wa hati za kimila za kumiliki ardhi katika kuchochea ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi wakati wa hafla ya kutolewa kwa hati hizo kwa wananchi wa Kijiji cha Magubike Wilayani kilosa ambapo Mpango huo kwa kushirikiana na Halmashuri ya Wilaya hiyo wamefanikisha upimaji wa ardhi katika Vijiji 37.

   Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw. Adam Mgoyi akimkabidhi mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Magubike hati kimila ya kumiliki ardhi.
  C:\Users\CHIMESELA\Desktop\Magubike\2b.JPG
  Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Magubike wakipatiwa Hati Miliki za Kimila na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Adam Mgoyi. Pichani ni Bw. Jackson Mgoma, akiwa katika furaha baada ya kuipata Hati hiyo.  0 0

  *Pia agusia tamasha litakalofanyika Septemba 8 Ubungo Plaza Dar 

  Na Ripota Wetu,Nyasa

  SEPTEMBA   8 mwaka huu katika ukumbi wa Ubungo Plaza wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam kutafanyika tamasha kubwa la harambee ya kuchangia elimu kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi hasa  wakike kwa ajili ya Wilaya ya Nyasa.

  Tamasha hilo ambalo mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri wa TAMISEMI Seleman Jafo lengo likiwa kupata fedha kwa ajili ya ujenzi huo wa mabweni.Akizungumza leo wilayani nyasa Mkuu wa wilaya hiyo Esabela Chilumba amesema anawakumbusha wadau wote wa elimu kuendelea kuchangia.

  Amesema siku zinazidi kusogea hivyo wote waliopewa bahasha maalum za kuchangia anawakumbusha kuendelea kuchangia kwa njia mbalimbali ambazo zimewekwa wazi kwa ajili ya kukusanya fedha hizo." Binafsi niwaombe wadau mbalimbali waendelee kutoa michango yao lengo nikufanikisha harambee hiii ambayo lengo hasa nikukusanya Sh. bilioni moja ambazo zitatumika kujenga mabweni hayo,"amesema Esabela

  Ameongeza  kupitia kamati na akaunti mbalimbali zilizowekwa wazi wadau waendelee kuchangia kwani watoto wakike wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya mimba za utoto." Ndugu mwandishi kama nilivyosema awali kutokana na watoto wengi kuishi mazingira ya mbali na shule inapelekea waliowengi kukatisha masomo kwasababu ya kupata mimba za utoto,"amesema

  Amesema mbali na mimba wengine wanashindwa kumaliza shule kwa sababu ya utoro unaotokana na kuishi mbali naazingira ya shule hivyo nivema wakajitokeza kwa wingi kuchangia.Wilaya ya Nyasa ni miongoni mwa wilaya ambayo ipo pembezoni mwa Ziwa Nyasa ambapo shughuli zake kubwa ni uvuvi na kilimo hivyo  kujengwa kwa mabweni kutasaidia wanafunzi wa  kike kukaa shule na mwisho wa siku kufanya vizuri katika masomo yao.

  Pia Chilumba amewataka wananchi wa wilaya hiyo ya Nyasa kuendelea kushikamana na kudumisha usalama ukizingatia ni wilaya ambauyo ipo mpakani  na pia waendelea kuchapa kazi kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao huku wakiunga mkono kwa vitendo kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi akisoma hotuba ya ufunguzi ya Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Uganda kwa ngazi ya Makatibu Wakuu. Katika hotuba hiyo, Balozi Mwinyi alieleza kuwa tokea JPC kati ya Tanzania na Uganda ilipoanzishwa mafanikio makubwa yamepatikana. Mafanikio hayo ni pamoja na kusainiwa kwa mikataba ya makubaliano mbalimbali ikiwemo mkataba wa kushirikiana katika ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Kikagati/Murongo na makataba wa kushirikiana katika usafiri wa anga ambapo Tanzania inakusudia kuanza safari za moja kwa moja kutoka Dar Es Salaam kwenda Kampala hivi karibuni. 
  Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia kwa makini hotuba ya Balozi Mwinyi 
  Ujumbe wa Uganda ukifuatilia hotuba za ufunguzi zilizokuwa zinasomwa na Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje za Tanzania na Uganda. 
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi akiongea na mwenyeji wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda, Balozi Patrick Mugoya kabla ya viongozi hao hawajafungua rasmi mkutano wa JPC kwa ngazi ya Makatibu Wakuu. 
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salvator Mbilinyi akibadilishana mawazo na Balozi wa Uganda nchini Uingereza, Mhe. Leonard Mugerwa nje ya ukumbi wa mikutano.

  0 0

  Mwenyekiti wa Taasisi ya Pondeza Foundeshen akiwa pia ni Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza akishiriki pamoja na Wananchi wa Jimbo hilo kusoma dua ya kuwaombea wazee waliotangulia mbele ya haki katika Chakula cha mchana kilichotayarishwa na Taasisi hiyo kwa Watoto yatima na wenyemazingira magumu katika Hoteli ya Maruhubi Beach Villa Zanzibar.
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Pondeza Foundeshen akiwa pia ni Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza akijumuika na Watoto Mayatima na wenye mazingira magumu katika Chakula cha mchana kilichotayarishwa na Taasisi hiyo kwa Watoto yatima na wenyemazingira magumu katika Hoteli ya Maruhubi Beach Villa Zanzibar.
  Muakulishi wa Jimbo la Chumbuni Miraji Khamis Mussa akijumuika na Watoto Mayatima na wenye mazingira magumu katika Chakula cha mchana kilichotayarishwa na Taasisi Pondeza Foundeshen katika Hoteli ya Maruhubi Beach Villa Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

  Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akimsikiliza kwa makini mwezeshaji katika semina ya uzazi na malezi bora iliyoandaliwa na Chama cha UMATI kwaajili ya wabunge iliyofanyika  jana jijini Dodoma. 
  Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akifungua semina ya uzazi na malezi bora iliyoandaliwa na Chama cha UMATI kwaajili ya wabunge iliyofanyika jana jijini Dodoma. 
  Wabunge wakimsikiliza kwa makini Spika katika semina ya uzazi na malezi bora iliyoandaliwa na Chama cha UMATI kwaajili ya wabunge iliyofanyika leo jijini Dodoma. 
  Waheshimiwa wabunge wakipata picha ya pamoja na Spika Mhe Job Ndugai ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika semina iliyoandaliwa na UMATI

  0 0

  Mwananchi ambae jina lake halikupatikana mara moja amejikita katika suala la hifadhi ya vichaka vya Itigi, ambavyo humsaidia kuongeza kipato kwa kuvuna asali.
  Sehemu ya vichaka adimu duniani vinavyopatikana Itigi, “Itigi thickets” katika bara la Afrika vichaka kama hivyo vinapatikana Tanzania na Zambia pekee, viko hatarini kutoweka kutoweka kutokana na shughuli za kibinadamu.


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akisalimiana na Bw. Khatib Ally mmoja wa wananchi waliojitokeza kumpokea katika Kijiji cha Aghondi Wilayani Manyoni, Mkoani Singida. Waziri Makamba ametembelea eneo hilo ambalo lina vichaka vya aina yake na vyakipekee barani Afrika. Wananchi wa eneo hilo wamewasilisha ombi kwa Waziri Makamba la kuweka ulinzi wa kutosha na namna bora ya kuhifadhi eneo hilo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akisalimiana na Bw. Khatib Ally mmoja wa wananchi waliojitokeza kumpokea katika Kijiji cha Aghondi Wilayani Manyoni, Mkoani Singida. 
  Waziri Makamba ametembelea eneo hilo ambalo lina vichaka vya aina yake na vyakipekee barani Afrika. Wananchi wa eneo hilo wamewasilisha ombi kwa Waziri Makamba la kuweka ulinzi wa kutosha na namna bora ya kuhifadhi eneo hilo. 
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba hii leo amehitimisha ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Singida na kuwasili katika Mkoa wa Tabora, ikiwa ni mwendelezo wa kukagua, kutathmini, kuzungumza na viongozi, na wananchi kuhusu maeneo yanayopendekezwa kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira, sambamba na uanzishwaji na ufuatiliaji utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi Mazingira ya mwaka 2004 katika ngazi za Serikali za Mitaa.

  Katika siku ya tatu ya ziara yake Mhe. Makamba ametembelea vichaka vya Itigi ‘Itigi thicket” na kupata fursa ya kuzungumza na viongozi wa wilaya ya Manyoni juu ya namna bora ya kuhifadhi eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 410,000 na kuahidi kutuma wataalamu kuandaa andiko la Mradi utakaonufaisha wakazi wa eneo hilo katika sekta uvunaji wa asali kwa njia ya kisasa zaidi.

  “Ndani ya muda mfupi nitatuma wataalamu wangu kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, waje wakae na wataalamu wenu na kuandaa Mradi utaonufaisha wakazi wa wanaozunguka eneo lote la msitu ili kutunza na kuhifadhi rasilimali za asili zilizopo katika eneo hili” Makamba alisisitiza.

  Katika hatua nyingine Waziri Makamba amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Bi. Rahabu Jackson kuwasilisha kwake majina wa watalaamu wa Mazingira ambao wana sifa za kuwa Wakaguzi wa Mazingira ili waweze kuteuliwa kwa mujibu wa Sheria.

  Pia, ametoa wito wa Halmashauri kuingia makubaliano na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ili kukasimu mamlaka kisheria ya kukagua na kusimamia masuala ya mazingira kwa msukumo zaidi.

  Vichaka vya Itigi huwa na urefu wa mita 2-5 na katika Bara la Afrika vinapatikana Tanzania na Zambia pekee vinawakilisha bioanuani ya kipekee duniani yenye umuhimu kitaifa na kimataifa na uoto wake ni muhimu kwa mustakabali wa maisha ya binadamu na wanyamapori.

  Imebainika kuwa vichaka vya Itigi viko hatarini kutoweka kutokana na shughuli za kibinadamu kama vile kilimo cha kuhamahama, uchungaji wa mifugo, uchomaji wa mkaa, uvunaji wa mazao ya misitu na uchimbaji wa madini. Hivyo kuna haja ya kuchukua hatua za haraka kuhakikisha uhifadhi endelevu wa vichaka vya Itigi.

  0 0


  Yatoa Riba  ya Robo ya pili ya Mwaka Kutoka Kwenye Akaunti Za Wateja wa Tigo Pesa.

   Wateja wa mtandao unaongoza kwa maisha ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania ambao wamejisajili  na huduma ya kifedha ya Tigo pesa wamepokea TSH 2.35 billioni kama gawio la riba ya robo ya mwaka kutoka kwa akaunti za wateja wa Tigo Pesa.

  Akitangaza gawio hilo la riba ya robo ya pili ya mwaka jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema, “Gawio hili ni uthibitisho zaidi kuwa Tigo Pesa ni Zaidi ya Pesa. Kila robo ya mwaka tunatoa gawio la riba kwa wateja wetu kwa kuzingatia kiwango cha fedha kilichopo katika akaunti ya Tigo Pesa ya mteja husika.

  Tigo inajivunia mtandao unaokua kwa kasi zaidi nchini wa wateja waliosajiliwa 12 milioni, zaidi ya watumiaji milioni 7 wa huduma yake ya kifedha ya Tigo Pesa, pamoja na mtandao mpana wa wafanyabiashara zaidi ya 40,000 na mawakala 85,000 waliosambaa kote nchini.

  Tigo ilikuwa kampuni ya kwanza ya simu duniani kutoa gawio la riba itokanayo na akaunti yake maalum ya huduma za kifedha. Kuanzia mwaka 2014, kampuni hiyo imetoa gawio la jumla ya TSH 81.8 billioni kwa wateja wake wanaopokea malipo kwa kuzingatia thamani waliyo nayo katika akaunti zao za Tigo Pesa kwa kuzingatia kanuni za Benki Kuu,’ Simon alisema. 

  Alibainisha kuwa ongezeko kubwa la wateja ambao wanaotumia huduma za kifedha kwa njia simu limetokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Tigo katika kupanua huduma zake, kufanya ubunifu unaozingatia matakwa ya wateja, teknologia ya kisasa ya pamoja na utoaji wa huduma za mahususi zinazoongeza thamani kwa wateja wake.

  Tigo Pesa imedhamiria kuunga mkono juhudi za Serikali ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania za kupanua wigo wa upatikaji wa huduma za kifedha nchini. Tigo pia inafungua ukurasa mpya wa uchumi na maisha yasiyotegemea pesa taslim kwa kupanua na kuboresha huduma zake na kubuni njia mpya na bora zaidi za wateja wake kufurahia huduma za haraka, salama, uhakika, za fedha kwa njia ya simu za mkononi popote walipo.

  Ili kuwapa wateja wake uwezo zaidi juu ya miamala yao, Tigo ndio kampuni ya kwanza ya simu nchini kuanzisha huduma ya Jihudumie inayowezesha wateja kuzuia kwa haraka miamala iliyokosewa ya kutuma fedha kwa wateja wengine wa Tigo, bila kuhitaji msaada wa moja kwa moja wa kitengo cha huduma kwa wateja.

  Pia, Tigo ndio mtandao wa kwanza nchini kuleta huduma ya Masterpass QR inayowezesha wateja kulipia huduma na bidhaa kwa urahisi na usalama kwa kuscani nembo ya Masterpass Quick Response (QR) inayopatikana katika maelfu ya maduka nchini.

  Tigo Pesa imeunganishwa na mfumo wa Serikali wa malipo ya mtandao (GePG) kupitia namba za USSD, App ya Tigo Pesa na kwa kuscan nembo ya QR, ili kuwezesha wateja kufanya malipo ya haraka kwa mashirika ya kiserikali zaidi ya 150 nchini.

  Katika kupanua wigo wa mfumo wake wa malipo, Tigo imeingia katika makubaliano ya kimkakati na kampuni ya kiteknologia ya Uber ili kuwezesha wateja wake kutumia app ya  Uber bure pasipo gharama za intaneti. Vile vile, kila wanapofanya miamala ya Tigo Pesa, wateja wa Tigo Pesa wanafurahia huduma za usafiri wa Uber kwa punguzo la bei.  

   Kwa kipindi cha miaka mingi sasa, Tigo imeongoza katika mageuzi ya soko la huduma za mawasliano. Mwaka 2014, Tigo ilikuwa kampuni ya kwanza ya mawasiliano Africa kuzindua huduma ya kifedha iliyoruhusu wateja wa mitandao tofauti kufanya miamala baina ya mitandao yao. Mwaka huo huo, Tigo ilizindua huduma ya kwanza ya kifedha Afrika Mashariki iliyowezesha utumaji wa fedha kutoka nchi moja hadi nyingine kwa kuzingatia thamani ya sarafu ya nchi husika, hivyo kurahisisha na kuongeza uhamishaji wa fedha kuvuka mipaka ya nchi. 

  Mifano hii inathibitisha kuwa Tigo inazidi kufanya ubunifu unaozingatia mahitaji maalum ya wateja na kutoa huduma bora na rahisi zaidi zinazoboresha maisha nchini kote.

  0 0

  Familia ya Marehemu Bw & Bibi Julius Vicent Kibaja wa Makongo Juu Dar es Salaam tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Ndugu, Jamaa na marafiki, Wauguzi na Madaktari kwa ushirikiano wenu mkubwa mlioutoa kwetu tangu kutokea kwa kifo cha MAMA YETU MPENDWA Bi. JOYCE CLARA KIBAJA tarehe 5-07-2018 katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) na mpaka tulipompumzisha kwenye nyumba yake ya milele katika Kijiji cha Kwemhosi- Kigunga-Muheza –Tanga .

  Ibada ya shukrani itafanyika tarehe 25-08-2018 katika Kanisa la Mt. Jacob lililopo Kijiji cha Kwemhosi - Muheza ikitanguliwa na mkesha tar 24-08-2018.

  Aidha, siku ya Ijumaa tarehe 31-08-2018 kutakuwa pia na ibada ya shukrani itakayofanyika katika kanisa la Anglikan la Mt. .Nikolaus - Ilala Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni, Wote mnakaribishwa. 

  “Bwana alinitokea zamani akisema, Naam nimekupenda kwa Upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu” YEREMIA 31:3 

  “ JOYCE CLARA KIBAJA YOU ARE THE BEST DEVOTED MUM FOREVER IN OUR HEART” 

  R.I.P 

  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Wazohuru Blog

  Mwandishi na mchambuzi wa Habari nchini Tanzania ambaye ni Afisa Habari Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA)-Wizara ya kilimo ameingia kwenye historia ya vijana wachache waliofanya maamuzi ya busara na tija katika mustakabali wa maisha mema katika jamii kwa kufunga ndoa Takatifu.
  Ibada ya ndoa Takatifu ilifanyika siku ya jumamosi tarehe 18 Agosti 2018 kuanzia majira ya saa sita na nusu (6:30) mchana mpaka saa nane na nusu (8:30) mchana katika kanisa la Kiinjili La Kilutheli Tanzania-Usharika wa Mabibo Farasi Jijini Dar as salaam.

  Mathias Canal amefunga ndoa na Binti mstaarabu, wenye nidhamu na busara huku akiwa mcha Mungu Bi Elizabeth Chagamba mzaliwa wa Tanga ambaye kihistoria tangu kufahamiana urafiki wao umedumu kwa takribani miaka sita mpaka kufikia maamuzi ya kufunga ndoa Takatifu.

  Ibada hiyo ya ndoa Takatifu iliendeshwa na Mchungaji Remmya Chuma kutoka kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Dayosisi ya Mashariki ya Pwani Usharika wa Kawe Jijini Dar es salaam ambapo aliwataka Bwana Harusi Mathias Canal na Bi Elizabeth Chagamba kuishi kwa kuzingatia misingi ya ndoa na agano Takatifu baina yao na Mungu kwani ndoa yao imeshuhudiwa na watu duniani lakini shahidi pekee mwenye maono zaidi ya ndoa hiyo ni Mungu mwenyewe.

  Mchungaji Chuma aliwakumbusha waumini wengine katika ibada hiyo kumshukuru Mungu kwa kila hatua wanazopita huku akiwasihi waumini hususani vijana ambao hawajafunga ndoa Takatifu kuingia katika tendo hilo muhimu machoni pa wanadamu na Mungu wa Mbinguni. Na kuongeza kwa kunukuu Kitabu cha Mathayo 19:5 kisemacho, "Kwa sababu hiyo mtu atamwacha Baba na Mama yake ataambatana na Mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja".

  Mara baada ya Ndoa Takatifu kati ya Afisa Habari NFRA Ndg Mathias Canal na Bi Elizabeth Chagamba kukamilika kanisani ilihudhuriwa na tafrija fupi iliyofanyika katika eneo la Urafiki Social Hall katika ukumbi wa Nyangumi ambapo hafla hiyo ilihudhuriwa na mamia ya wananchi huku viongozi mbalimbali wa Chama na serikali wakihudhuria.

  Kwa upande wa Chama cha Mapinduzi ndoa hiyo ilihudhuriwa na Timu ya uenezi kutoka Chama Cha Mapinduzi Taifa, Mohammed Alliyan Kaimu Katibu wa Idara ya oganaizesheni na uhusiano wa kimataifa Umoja wa Vijana (UVCCM) Makao makuu pamoja na wasaidizi wa Mwenyekiti na Katibu Mkuu UVCCM Taifa.

  Kwa upande wa serikali hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (Mb) ambaye katika salamu alizozitoa kwa niaba ya Wizara yake alisema kuwa Ndoa ni muunganiko wa kiagano wa kudumu kati ya mwanaume mmoja na mwanamke mmoja wenye kuishi na kuwa mume na mke. Neno agano ni neno muhimu sana kwa sababu agano ni patano la milele ambaye shahidi yake ni Mungu mwenyewe wala si mwanadamu hivyo kuwataka sana ndoa hao kuwa waaminifu milele.

  Aidha, alitaja umahiri katika utendaji unaofanywa na wasaidizi wake akiwemo Mathias Canal pamoja na mwenzake Innocent Masaka kuwa ni wadogo sana kwake kiumri lakini wamekuwa msaada mkubwa katika kutekeleza majukumu ya serikali yakiwemo na yale ya Chama cha Mapinduzi.

  Katika hafla hiyo Mhe Dkt Tizeba alisema kuwa Fungate ni jambo muhimu baada ya ndoa Takatifu hivyo akatoa ofa maalumu kwa maharusi hao kwenda mapumzikoni Mjini Unguja-Zanzibar huku akisema kuwa gharama zote za siku tano atagharamia yeye. Pia Dkt Tizeba ametoa ofa ya mapumziko ya siku tano kwa Ndg Mathias Canal ambaye muda wake wa mapumziko ulikuwa umemalizika hivyo kuendelea na mapumziko ya siku tano.

  Tayari Mathias Canal na Mkewe Bi Elizabeth Chagamba wamewasili Mjini Unguja-Zanzibar ambapo katika mapumziko hayo wamesafiri na wapambe 10 waliohudumu katika sherehe yao (Maids) ili kufurahi kwa pamoja katika mapumziko hayo.
  Mwandishi Mathias Canal akionyesha cheti cha ndoa aliyoifunga Jumamosi tarehe 18 Agosti 2018 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Mabibo Farasi Jijini Dar es salaam na mkewe Bi Elizabeth Chagamba.
  Mwandishi Mathias Canal na mkewe Bi Elizabeth Chagamba (walioketi) pamoja na watumishi wa Wizara ya Kilimo wakiongozwa na waziri wa wizara hiyo Mhe Dkt Charles Tizeba, Watumishi kutoka Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wakati wa hafla ya jioni baada ya ibada ya ndoa Takatifu tarehe 18 Agosti 2018 katika eneo la Urafiki Social Hall Ukumbi wa Nyangumi Jijini Dar es salaam.
  Mwandishi Mathias Canal akivishwa Pete na mkewe Bi Elizabeth Chagamba wakati wa ibada ya ndoa Takatifu iliyofanyika katika kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Mabibo Farasi jijini Dar es salaam tarehe 18 Agosti 2018.
  Mwandishi Mathias Canal akimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji J. Mtaturu wakati wa tafrija iliyofanyika eneo la Urafiki Social Hall ukumbi wa Nyangumi baada ya ibada ya ndoa Takatifu iliyofanyika katika kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Mabibo Farasi jijini Dar es salaam tarehe 18 Agosti 2018.
  Bwana harusi Mathias Canal na Bi harusi Elizabeth Chagamba wakicheza wimbo maalumu ulioimbwa na msanii wa midondoko ya (RnB) Elias Barnabas maarufu Barnaba Boy Classic wakati wa tafrija iliyofanyika eneo la Urafiki Social Hall ukumbi wa Nyangumi baada ya ibada ya ndoa Takatifu iliyofanyika katika kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Mabibo Farasi jijini Dar es salaam tarehe 18 Agosti 2018.

  0 0
  MKUU wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella leo Agosti 23, 2018 ameungana waombolezaji mbalimbali kushiriki mazishi ya Bi. Anna Makwega Manasse (81) ambaye ni bibi wa Mhe.Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa Dar es salaam.

  Mazishi ya Bi. Manasse ambaye alifariki dunia juzi Agosti 21, 2018 akiwa katika hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu, yamefanyika katika makaburi ya nyumbani yaliyopo Kahangala wilayani Magu.

  Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa serikali mkoani Mwanza, Mhe. Mongella amewaombea uvumilivu ndugu, jamaa na marafiki kutokana na msiba huo na kuwahimiza kumuombea kwa Mola ili apumzike kwa Amani. 
   Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella aliye kaa katikati waombolezaji mbalimbali kushiriki mazishi Bi. Anna Makwega Manasse (81) ambaye ni bibi wa Mhe.Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa Dar es salaam.
   Mhe.Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa Dar es salaam akiwa kwenye makaburi kwaajili ya kumzika bibi yake.
  Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella  akiweka shahada kwenye kaburi la Bi. Anna Makwega Manasse (81) ambaye ni bibi wa Mhe.Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa Dar es salaam.

  0 0

  Afisa Kilimo Bodi ya Korosho Tanzania Frank Mfutakamba kulia akisisitiza jambo kwa wakulima hao kuhusu magonjwa hatari yanayolishambulia zao hilo wakati wa uzalishaji wake na namna ya kukabiliana nalo MKUU wa wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro Ngolo Malinya katika akiwa na Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana kulia kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Ulanga (DAS) Abraham Mwaikwila akifuatiwa na Afisa Kilimo Bodi ya Korosho Tanzania Frank MfutakambaAfisa Habari wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana kulia akionyeshwa kitu na mmoja wa wakulima wa zao la Korosho wa kikundi cha Igombiro wilayani Ulanga mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kuhamasisha umuhimu wa kulimo hicho
  Afisa Habari wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana akisistiza jambo kqwa Mkuu wa wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro Ngolo Malinya wakati wa ziara yao ya kuhamasisha wakulima umuhimu wa kuongeza tija ya kilimo hicho Afisa Habari wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana akisaini kitabu cha wageni ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ulanga mara baada ya kuwasili kulia kwake ni Mkuu wa wilaya hiyo Ngolo Malinya Mkuu wa wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro Ngolo Malinya akisistiza jambo Katibu Tawala wa wilaya ya Ulanga (DAS) Abraham Mwaikwila akizungumza kuhusu namna walivyojipanga kuhimiza kilimo cha zao la Korosho wilayani humo Katibu Tawala wa wilaya ya Ulanga (DAS) Abraham Mwaikwila kulia akisisitiza jambo kwa Afisa Kilimo Bodi ya Korosho Tanzania Frank Mfutakamba mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake Afisa Habari wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana kushoto akiagana na Katibu Tawala wa wilaya ya Ulanga (DAS) Abraham Mwaikwila mara baada ya kumaliza mazungumzo nae Afisa Habari wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana kulia akisistiza jambo wakati akitoa elimu kwa wakulima wa zao hilo kwenye kikundi cha Igombiro wilayani Ulanga mkoani Morogoro


  NA MWANDISHI WETU, ULANGA.

  SERIKALI wilayani Ulanga mkoani Morogoro imesifu jitihada kubwa zinazo fanywa na bodi ya Korosho Tanzania kwa kuwatembelea wakulima ili kuwahamasisha umuhimu wa kulima kilimo chenye tija ili kuongeza uzalishaji ikiwa ni mpango wa kuliendeleza zao hilo.

  Hayo yalibainishwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Ulanga (DAS) Abraham Mwaikwila wakati wakati wa ziara ya viongozi wa Bodi ya Korosho iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kilimo hicho kwa wakulima wilayani Ulanga ikiwemo upuliziaji wa dawa ili kuongeza uzalishaji.

  Viongozi wa bodi ya Korosho ambao walikuwa kwenye ziara hiyo ya uhama sishaji huo ni Afisa Habari wa Bodi ya Korosho Tanzania Bryson Mshana na Afisa Kilimo Bodi ya Korosho Tanzania Frank Mfutakamba ambao walikutana na wakulima wanaolima korosho wa kikundi cha Igombiro

  Alisema kwamba wilaya hiyo tokea miaka ya nyuma walikuwa wanalima korosho lakini baadae waliliacha kutokana na kutokuwa na soko la uhakika lakini kwa sasa ili kuhakikisha zao hilo linalimwa kwa tija mwaka jana walipewa ruzuku ya uzalishaji wa miche ya korosho laki tatu ambayo waliigawa kwa wakulima.

  “Sio hilo mikorosho ya zamani iliyokuwepo tulikuwa na Mkurugenzi aliyekuwa akiitwa Isabela Chiluba aliyetoka Tandahimba kwani baada ya kufika aliweza kuja na mwamko mzuri wa kufufua mikorosho ya zamani kwa mfano mwaka jana walipata pembejo na kupulizia mikorosho ya zamani jambo ambalo limefungua ukurasa mpya kwetu “Alisema.

  Alisema kutokana na hilo mwaka huu wanatarajia kuzalisha miche kwa wingi hivyo anaamini bodi ya korosho itakuwa na uhamasishaji mzuri na miche laki tatu iliyotolewa kwa hiyo mwaka huu itakuwa chachu ya wananchi kuhitaji miche utakuwa mkubwa sana.

  Hata hivyo aliiomba bodi ya Korosho kuweka utaratibu wa kuwapa miche ya korosho kutokana na kwamba asilimia kubwa ya mapato kwenye Halamshauri ya Ulanga yanatokana na mazao hivyo anaamini Mkurugezi na timu yake ya idara ya kilimo watajipanga kuhakikisha wanaenda kununua mbegu kwenye vituo vya naindelee ili waweze kupata miche iliyobora na kuwawezesha kuongeza uzalishaji wenye tija.

  Naye kwa upande wake, Mratibu wa zao la Korosho wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro Samweli Masaro alisema kutokana na kuwepo kwa uhamaishaji huo umewawezesha kuongeza uzalishaji kufikia tani 80.

  Ambapo awali ulikuwa kwa kiwango cha chini hali iliyowa ikiwalazimu kutilia mkazo uzalishaji wa zao hilo kwa kuhamasishaji wakulima kulima ikiwemo kutunza miti yao na kupiga dawa jambo ambalo kwa asilimia kubwa limesaidia kuweza kuwawezesha kupata tani hizo ambazo pia wanatarajia huenda zikaongezeka

  0 0


  Baadhi ya Vituo vya Usajili vinavyokamilishwa kila kila wilaya ya Unguja na Pemba 
  Mifumo mipya iliyofungwa ili kuhifadhi kumbukumbu kisasa (kidigitali).
  Baadhi ya Vifaa vilivyoko ndani ya vituo vipya.
  Baadhi ya Vifaa vilivyoko ndani ya vituo vipya .
  Jengo jipya ambapo Ofisi kuu ya Wakala wa usajili wa matukio ya Kijamii Zanzibar 
  Mambo Msiige jengo la mwanzo lililotunza kumbukumbu za Wazanzibar za maswala ya matukio ya kijamii 
  Zaharan Nassor Mhifadhi Mkuu wa Nyaraka wa wakala wa usajili wa matukio ya kijamii Zanzibar akionyesha Nyaraka Kongwe zaidi yenye majina ya Uzazi kuanzia mwaka 1909 hadi 1911 
  Mhifadhi akichambua Taarifa katika Ghala la Nyaraka Ofisi kuu ya Mamlaka ya Usajili matukio ya kijamii Zanzibar. 
  Dr Hussein Khamis Shaaban, Mkurugenzi mtendandaji wa wakala wa usajili wa matukio ya kijamii akikagua Nyaraka za Kale za vizazi na vifo ambazo zinachakatwa kuwekwa katika mfumo wa Kidigitali
  Nyaraka zenye kumbu kumbu za wazanzibari za Uzazi, Vifo, Talaka, Ndoa na na utambulisho tangu 1909
  Msajili wa vizazi na vifo Wilaya ya Kati Mkoa wa kusini Unguja akichambua Taarifa za mwananchi ili kujaza vyeti mbali mbali vya Wazanzibar 

  *Ni baada ya kuimarishwa kwa mifumo ya kuhifadhi taarifa kieletroniki. 


  MWENDO ni wa kidigitali! Hivyo ndivyo unaweza kuelezea baada ya Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar kuamua kuingia kwenye mfumo wa kieletroniki katika kusajili wakaazi wa Zanzibar (E-ID CARD). 

   Hivyo Wakala hiyo imeamua kuingia katika mfumo wa kisasa zaidi katikka kuhifadhi kumbukumbu za wakaazi wa Zanzibar na kwamba hivi sasa taarifa zao muhimu zitatuzwa kwenye mfumo wa kidigitali. Hayo yameleezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii, Dk. Hussein Khamis Shaaban wakati anazungumzia mikakati yao katika kuboresha na kuhifadhi taarifa za wakaazi wa Zanzibar ambapo ametumia nafasi hiyo kuwahamisisha kujitokeza katika kuboresha taarifa zao kupitia mfumo wa kidigitali. 

   "Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar imeamua kuanzisha vituo maalumu ambavyo vitatumika kuwasajili wananchi katika mfumo huo wa kieletroniki ambao maarufu zaidi kama mfumo wa kidigitali,"amefafanua Dk.Shaaban. Pia amesema pamoja na kuhakikisha taarifa hizo zinakuwa katika mfumo wa kisasa wa kutunza kumbukumbu za wananchi wa Zanzibar bado wanaamini utasaidia katika kulinda usalama wa nchi sambamba na kuwatambua kwa kina Wazanzibari wenye makazi ya kudumu visiwani humo na kwamba mfumo huo unaifanya nchi hiyo kupiga hatua zaidi katika matumizi ya kieletroniki katika kutunza kutunza na kutambua watu wake. 

   Mfumo huu mpya utasaidia katika kutoa huduma kwa haraka kwani taarifa zitakazoifadhiwa katika mfumo huo zitatumika na mamlaka nyingine kama Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZRB), Idara ya Uhamiaji, National Internet Data Center (NIDC), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Msajili wa Makampuni, mfumo wa hosptali (e-health) na mfumo wa utalii. Hata hivyo baada ya kukamilisha mifumo hiyo ya kieletroniki jukumu linaloendelea sasa ni kuhamasisha wananchi kuanza kujitokeza kwa ajili ya kuboresha kumbukumbu zao na siku za karibuni watatangaziwa siku ya kuanza kwa mchakato huo . 

  Aidha tayari kila wilaya kumejengwa kituo cha kidigitali ambapo vituo vyote katika wilaya 11 Unguja na Pemba vinaunganishwa na mkongo wa Taifa na Wananchi watajisajili huko huko wilayani na kuboresha taarifa zao, kwa sasa utaratibu wa kuchakata data za kale tangu daftari la mwanzo la mwaka 1909 zina hitahifadhiwa kidigitali katika kanzi data ya Taifa. Kwa kukumbusha tu majukumu ya wakala hiyo ni kusajili matukio ya vizazi, vifo , ndoa , talaka na vitambulisho na kusisitizwa usajili huo unatakiwa ufanyike kwa njia ya kieletroniki na kubwa zaidi wakala imemua kuimarisha taarifa katika mfumo wake.

   "Hivyo wakala inawatangazia Wazinzibar wakaazi wote kuwa itaendesha mchakato wa kuimarishaji taarifa kwa wote wenye vitambulisho vya Mzanzibar mkaazi pamoja na waombaji wapya katika mikoa yote ya unguja na pemba. "Ratiba ya mchakato huu utatangazwa hivi karibuni na tunasisitiza kuwa uimarishaji wa taarifa za kila mmoja wetu ni wajibu wa kisheria na atakayeshindwa kuimarisha taarifa zake hataweza kukitumia kitambulisho chake katika huduma mbalimbali za kiserikali na za kijamii,"amesema Dk.Shaaban. 

  Amesisitiza wananchi wote waimairishe taarifa zao ili waweze kuvitumia vyema vitambulisho vyao vya Mzanzibari Mkaazi na kwamba "Kupitia mfumo huo, Wakala inatarajia kutoa kitambulisho kipya cha Mzanzibari Mkaazi cha kielektroniki (e-ID Card) na vyeti vya kuzaliwa vipya. "Lengo kuu la mradi huu ni kuhakikisha tunaimarisha utoaji huduma za kijamii kwa Wazanzibari na wageni wakaazi wanaoingia na kuishi Zanzibar kwa madhumuni mbalimbali yakiwamo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii,” amesema Dk. Shaaban.

  0 0


  Tanzania na Uganda zimepata mafanikio makubwa kupitia Mikutano ya Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) iliyofanyika Arusha Aprili 2017 na sasa wa Kampala unaohitimishwa leo.

  Kauli hiyo ilitolewa kwa pamoja na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Mhe .Dkt. Augustine Mahiga (Mb) na mwenzake wa Uganda, Mhe. Sam Kutesa walipokuwa wanasoma hotuba za ufunguzi wa mkutano huo.

  Mafanikio yaliyoelezwa ni pamoja na kusainiwa kwa Mikataba ya Makubaliano tisa ikiwemo Mikataba ya kushirikiana katika uendelezaji wa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Dar Es Salaam hadi Uganda na ushirikiano katika masuala ya elimu na mafunzo iliyosainiwa leo katika mkutano wa Kampala.

  Mkutano huo ulijulishwa kuwa utekelezaji wa mikataba hiyo unaridhisha na inalenga kurahisisha ukuaji wa uchumi wa nchi hizo ili kutimiza azma ya viongozi wake, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mhe. Yoweri Museveni wa Uganda ya kukuza biashara kati ya nchi hizo.Mikataba iliyosainiwa inahusu uendelezaji wa miradi ya miundombinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na nishati ya Umeme, barabara hususan za mipakani, bandari, reli na usafiri wa anga. 

  Kufuatia mikataba hiyo miradi mbalimbali ipo katika hatua tofauti za utekelezaji ikiwemo mradi wa kuzalisha umeme wa Kikagati/ Murongo uliopangwa kukamilika mwaka 2020. Aidha, Shirika la Ndege la Tanzania litaanza safari za moja kwa moja kutoka Dar Es Salaam hadi Entebbe mwishoni mwa mwezi huu kufuatia kusainiwa kwa mkataba wa masuala ya anga katika mkutano wa Arusha mwezi Aprili 2018

  Miradi mingine ni ya ukarabati wa bandari za Bell na Bukasa na ukarabati wa meli za Kagawa na Pamba kwa upande wa Uganda ambayo italeta muunganiko mzuri katika usafirishaji hasa baada ya Reli ya Kisasa ya kiwango cha kimataifa inayojengwa na Tanzania itakapokamilika.Waheshimiwa Mawaziri walisisitiza umuhimu wa Serikali za Tanzania na Uganda kuwekeza ipasavyo katika ushoroba wa kati ili kuleta muunganiko kwa ajili ya kukuza biashara. Aidha. Walisisitiza umuhimu wa kuondoa vikwazo visivyo vya kibiashara na kushughulikia changamoto za mipakani kwa haraka kadri zinavyojitokeza

  Kutokana na umuhimu wa utekelezaji wa miradi inayoafikiwa katika mikutano hiyo, pande zote mbili ziliwakilishwa na viongozi wa ngazi ya juu wakiwemo Mawaziri na Makatibu Wakuu. 

  Kwa upande wa Tanzania, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwele, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu walishiriki mkutano huo.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  Kampala
  23 Agosti 2018
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kulia) na Waziri wa Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhe. Peter T. Lokeris wakiweka saini Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa kuendeleza ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Dar Es Salaam hadi Uganda. Aliyesimama kushoto kwa Mhe. Mahiga ni Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu. 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akibadilishana Mikataba na Waziri wa Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhe. Peter T. Lokeris baada ya kusainiwa. 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Elimu ya Juu wa Uganda, Mhe. J.C Muyingo wakiweka saini Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa kushirikiana katika masuala ya Elimu na Mafunzo. 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Elimu ya Juu wa Uganda, Mhe. J.C Muyingo wakibadilishna Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa kushirikiana katika masuala ya Elimu na Mafunzo. 
  Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Mhe. Sam Kutesa akimkabidhi Hati za Viwanja va Ubalozi wa Tanania nchini Uganda Mhe. Dkt. Augustine Mahiga. 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda, Balozi Patrick Mugoya (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi wakibadilishana taarifa ya masuala yote yaliyoafikiwa katika mkutano huo. 


  Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Mhe. Sam Kutesa akisoma hotuba katika Mkutano wa Pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika Kampala kwa siku tatu kuanzia tarehe 21 hadi 23 Agosti 2918. 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisoma hotuba katika Mkutano wa Pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika Kampala kwa siku tatu kuanzia tarehe 21 hadi 23 Agosti 2018. 
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akichangia jambo katika Mkutano wa Pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Uganda. 
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwele akichangia jambo katika Mkutano wa Pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Uganda. 
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akichangia jambo katika Mkutano wa Pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Uganda. 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji akichangia jambo katika mkutano wa pili wa JPC kati ya Tanzania na Uganda. 
  Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akichangia jambo katika Mkutano wa Pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC0 kati ya Tanzania na Uganda. 
  Sehemu ya Waheshimiwa Mawaziri kutoka Uganda wakiwa katika mkutano huo. 
  Kaimu Mkurugenzi wa Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salvator Mbilinyi akichangia jambo katika mkutano huo. 
  Wajumbe wa Tanzania na Uganda wakiendelea na mkutano.

  0 0
 • 08/23/18--23:39: SOKONI MABIBO LEO
 •  Wafanya biashara wa  nyanya katika soko la Mabibo lililopo wilaya ya Ubungo jijini Dar as Salaam wakisubili wateja kwa ajili ya kununua, ambapo kasha moja la nyanya hivi sasa linauzwa shilingi elfu 23,000 mpaka 25,000.(picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)

  Wafanya biashara wa ndizi wa soko la Mabibo jijini Dar as Salaam  wakijadiliana bei na mteja ambapo mkungu mmoja huuzwa shilingi 15,000.

  0 0

  Waumini wa Dini ya Kislamu Wilayani Hai wamemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ambae pia ni Mzaliwa wa Wilaya ya Hai Kwa Kitendo chake cha Kukubali kuufanyia Ukarabati Msikiti wa Lyamungo Sinde Kwa kuweka Mabati mapya yote ya Jengo la msikiti ,pamoja na kuweka Sealing Board ndani , na ukarabati Mwingine Mdogo

  Akizungumza Kwa Niaba ya Viongozi wa Bakwata Wilaya ya Hai,Ramadhani Matinga ambae ni Mwenyekiti wa ZAWIA ya Lyamungo Sinde,amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kujitolea kwake,katika kuhakikisha mambo ya kijamii yanakwenda sambamba na maendeleo.
   
   Mbali na Kumshukuru Mhe Muro Kwa kukubali Kubeba Jukumu la Kukarabati Msikiti huo,amebainisa kuwa hawajawai kumuona Kiongozi Mkuu wa Serikali Kuanzia ngazi ya Kijiji, kata, wilaya na Mkoa na Hata Mbunge Pamoja na Taifa ambae ameingia katika Msikiti huo Isipokuwa Dc Muro,aidha wamemhakikishia kumpa Ushirikiano pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe Lengai Ole Sabaya Kutokana na Jitihada walizoonesha katika Kuwatumikia wananchi pasipo ubaguzi

  Katika tukio Hilo Pia Mhe Muro alitoa Zawadi ya Mabox ya Tende Kwa Waumini wa Msikiti wa Lyamungo Sinde pamoja na kina mama wa Kware Wilaya ya Hai
  DC Muro pichani kati akiwakaribisha badhi ya Waumini wa Msikiti wa Lyamungo Sinde kupata chakula kwa pamoja
  DC Muro akikabidh zawadi ya Mabox ya Tende Kwa Waumini wa Msikiti wa Lyamungo Sinde pamoja na kina mama wa Kware Wilaya ya Hai.

  DC Muro akishiriki sala pamoja na Waumini wa Msikiti wa Lyamungo Sinde

older | 1 | .... | 1655 | 1656 | (Page 1657) | 1658 | 1659 | .... | 1898 | newer