Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

WAZIRI LUGOLA ATOA MILION 40 UJENZI SEKONDARI JIMBONI MWIBARA, AMWAGA ZAWADI WASHINDI WA KANGI BONANZA LA MICHEZO BUTIMBA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Bulimba katika Kiwanja cha Mpira cha Victoria, Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda, kabla ya Waziri huyo kugawa zawadi ya mshindi wa Bonanza la Kangi la mpira wa miguu ambapo timu ya mpira wa miguu ya Muungano pamoja na Miseni zote zinatoka Kata ya Butimba zilicheza. Lugola alitoa shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari Bulimba. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia) akimuangalia Kapteni wa timu ya mpira wa miguu ya Muungano, Bwire Metwisele wakati alipokua anashangilia mara baada ya Waziri huyo kumkabidhi zawadi ya mshindi wa kwanza wa Bonanza la Kangi, kwa kuifunga timu ya Miseni magoli mawili bila. Timu zote zinatoka Kata ya Butimba wilayani Bunda, Mkoa wa Mara. Pia Lugola alitoa shilingi milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari Bulimba.
Mchezaji wa Timu ya Muungano ya Kata ya Butimba wilayani Bunda, Bwire Metwisele (kulia), akimdhibiti mchezaji wa timu ya Miseni, Jovin Andrew, katika mashindano ya Bonanza la Kangi lililofanyika katika kiwanja cha Victoria, Kijiji cha Bulimba. Timu ya Muungano iliifunga Miseni magoli mawili kwa bila.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia) akimsalimia mzee wa Kijiji cha Bulimba, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara wilayani Bunda, wakati alipokua katika ziara ya kukagua mikradi ya maendeleo ndani ya Jimbo lake. Lugola pia alishiriki mashindano ya mpira wa miguu ya Bonanza la Kangi, iliyokutanisha timu mbili za Muungano na Miseni za Kata hiyo, Timu ya Muungano iliifunga Miseni magoli mawili bila. Pia katika hotuba yake, Mbunge huyo alitoa shilingi milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari Bulimba.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (aliyeonyesha alama ya vidole) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu za mpira wa miguu ya Muungano pamoja na Miseni pamoja na maafisa wa Wilaya ya Bunda, kabla ya kuanza kucheza katika kiwanja cha Victoria kijijini Bulimba, Jimboni humo. Lugola alitoa zawadi ya mshindi wa mashindano hayo na pia alitoa shilingi milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari Bulimba. Watatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili. 

MBUNGE WA KISHAPU SULEIMAN NCHAMBI MBARONI KWA TUHUMA YA RUSHWA

$
0
0

Kulia ni Mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi akiwa na rais John Pombe Magufuli - Picha kutoka maktaba

Mbunge wa Kishapu (CCM), Suleiman Nchambi na viongozi watatu wa mgodi wa Stamigold ulioko Tulawaka wilayani Biharamulo mkoani Kagera, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Biharamulo, Hassan Mosi amesema mbunge huyo na wenzake walikamatwa na kuwekwa rumande katika gereza la wilaya hiyo Jumamosi Agosti 4, 2018.

Amesema leo Jumatatu Agosti 6, 2018 watafikishwa mahakama ya wilaya ya Biharamulo kwa kosa la kufanya miamala ya kupokea rushwa.
Mosi amesema kitendo hicho ni kinyume na kifungu cha15 cha sheria namba 11 ya mwaka 2007 ya kupambana na kuzuia rushwa.

"Wakifikishwa mahakamani watasomewa mashtaka yanayowakabili. Wanaweza kukiri au kukanusha na sheria itachukua mkondo wake,” amesema.

Ndugu, jamaa na marafiki leo wamejitokeza kwa wingi katika mahakama hiyo, huku wengi wakionekana kuwa na shauku ya kujua hatima ya viongozi hao.

SOMA ZAIDI <>
Na Shaaban Ndyamukama, Mwananchi

JAFO AAGIZA WEZI WA VIFAA VYA UJENZI KITUO CHA AFYA NDAGO WAKAMATWE

$
0
0

Mganga mkuu wa wilaya ya Iramba akisoma taarifa ya ujenzi wa kituo cha Afya Ndago.
Baadhi ya makaravati yaliyojengwa kwa mawe ili kuwezesha barabara hiyo iweze kupitika wakati wote.
Meneja wa TARURA wilaya ya Iramba akitoa maelezo ya ujenzi wa barabara mpya.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ndago.
Baadhi ya vifaa vikiwemo Nondo na mifuko ya saruji ambavyo tayari zimekamatwa wakati wa ujio wa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida kupitia vyombo vya dola kuwasaka wezi wote waliiba vifaa vya ujenzi wa kituo cha afya Ndago wilayani huo na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Jafo ametoa agizo hilo leo baada ya kufanya ziara katika Kituo cha afya Ndago ambacho ni miongoni mwa vituo vya afya vilivyopokea Sh.Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa majengo mbalimbali lakini ujenzi wake haujakamilika hadi sasa kutokana na baadhi ya vifaa kuibwa na wananchi wasio waaminifu.

Katika ziara hiyo, Waziri Jafo ameonyesha kukerwa na uzembe wa usimamizi uliojitokeza katika ujenzi wa kituo hicho cha afya.

Hata hivyo, pamoja na kuagiza kusakwa kwa wezi wa vifaa, Waziri Jafo ameiagiza Ofisi ya mkoa wa Singida kufanya uchunguzi ndani ya wiki moja ili kubaini kama kuna watumishi waliohusika katika sakata hilo nao wachukuliwe hatua kali za kinidhamu.

Waziri Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iramba kukamilisha ujenzi wa majengo hayo kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Agosti ili wananchi wa Ndago waweze kupata huduma bora ya afya kama ilivyokusudiwa na serikali.

Aidha katika ziara hiyo waziri Jafo ametembelea na kukagua pia ujenzi wa barabara mpya ya kilometa 10 inayotoka Kiengege kwenda kata ya Ndago ambapo amepongeza Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini(TARURA) kwa kazi nzuri waliyoifanya katika ujenzi wa barabara hiyo.

WAZIRI WA UVUVI NA MIFUGO LUHAGA MPINA ATEMBELEA BANDA LA TAASISI YA PASS KATIKA MAONESHO YA NANE NANE MKOANI SIMIYU

$
0
0
Muonekano wa Viwanja vya Nyakabindi ambako kunafanyika maonesho ya nane nane kitaifa mkoani Simiyu.
Waziri wa Uvuvi na Mifugo,Luhaga Mpina akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi Binafsi ya kusaidia Sekta ya Kilimo nchini (PASS) Nicomed Bohay wakati alipotembelea Banda la taaasisi hiyo lilipo katika viwanja vya nane nanemkoani Simiyu.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kusaidia Sekta Binafsi zinazojihusisha na masuala ya Kilimo,Uvuvi na Ufugaji ,(PASS) Nicomed Bohay akimuonesha Waziri wa Uvuvi na Mifugo,Luhaga Mpina mfano wa Bwawa linalotumika kufugia samaki ,Mabwawa ambayo Taasisi ya PASS imekuwa ikisadia katika upatikanaji wa mikopo kwa Wafugaji wa Samaki ili waweze kufuga kisasa.
Mmoja wa wanufaika wa  huduma zinazotolewa na Taasisi binafsi ya kusaidia sekta ya Kilimo nchini (PASS) ikiwemo ya unenepeshaji wa Ngombe  Michael Tegeshi akitoa maelezo kwa Waziri wa Uvuvi na Mifugo,Luhaga Mpina alipotembelea banda la taasisi hiyo katika maonesho ya nane nane yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi mkoni Simiyu.
Waziri wa Uvuvi na Mifugo,Luhaga Mpina akitizama Mchele uliowekwa vizuri katika mifuko kwa ajili ya kuongeza thamani ,Mchele huo unaandaliwa na vikundi ambavyo vimepata msaada kutoa katika taassi hiyo.
Meneja wa  PASS Trust  tawi la Mtwara ,Isaac Kileo akitoa maelezo kwa Waziri wa Uvuvi na Mifugo Luhaga Mpina alipotembelea banda la taasisi hiyo katika maonesho ya nane nane yanayofanyika kitaifa katika mkoa wa Simiyu
Waziri wa Uvuvi na Mifugo,Luhaga Mpina akimsikiliza Mkurugenzi wa Biashara PASS,Kilo Rusewa alipotembelea katika Banda la taasisi hiyo katika viwanja vya nane nane mkoani Simyu.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Prof Elisante Ole Gabriel akimuelekeza jambo Waziri wa Uvuvi na Mifugo ,Luhaga Mpina wakati akitembelea banda la Taasisi ya PASS katika maonesho ya nane nane mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akitizama Ng'ombe aliyenenepeshwa alipotembelea Banda la Taasisi ya PASS katika maonesho ya nane nane mkoani Simyu.
Baadhi ya Wananchi wakitizama Ng'ombe aliyenenepeshwa waliopo katika Banda la taasisi ya PASS katika maonesho ya nane nane mkoani Simiyu.
Meneja wa Biashara wa taasisi ya PASS ,Hamis Mmoni akizungumza na baadhi ya wananchi waliotembelea banda la taasisi hiyo katika maonesho ya nane nane yanayofanyika kitaifa mkoani Simiyu.
Baadhi ya wananchi wakitizama samaki katika moja ya bwawa la mfano lililopo katika banda la nane nane la taasisi ya PASS.

Sehemu ya mifugo iliyopo katika banda la maonesho ya nane nane la taasisi ya PASS  mkaoni Simiyu,

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyeko Simiyu.

Magazetini leo Jumanne August 07 2018

TCRA:HAKIKISHENI TAARIFA MNAZOZITOA WAKATI WA KUSAJILI KADI ZENU ZA SIMU NI SAHIHI, VINGINEVYO SHERIA ITAFUATA MKONDO WAKE

$
0
0
Na. Vero Ignatus Arusha. 

Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA imewataka wananchi kufahamu wajibu na haki zao wanazostahili  kupata kutoka kwenye mitandao inayotoa  huduma za mawasiliano sambamba na kutambua wajibu walionao kama watumiaji wa huduma za mawasiliano

Kaimu mkuu wa Kanda ya kaskazini Francis  Msungu amesema kuwa mamlaka inatoa elimu kwa wananchi kuzijua haki zao kutokana na mabadiliko yanayotokea ni mengi ya sayansi na teknolojia pamoja na maendeleo ya matumizi ya vifaa vya mawasiliano katika mitandao ya simu.

Amesema kwa sasa kumezuka wimbi la utapeli kupitia simu za mikononi,  hivyo wananchi  wametakiwa kuwa na tahadhari kubwa, wasikubali kurubuniwa katika vitu ambavyowanafahamuhawajashiriki Usitekeleze maagizo yeyote yahusuyo fedha kwa ujumbe wa maandishi,

"Mfano unatumiwa ujumbe kuwa umeshinda bahati na sibu katika
Mashindano ambayo hujashiriki, ukipokea ujumbe umetumiwa pesa na mtu usiyemfahamu usizitoe fedha hizo, hadi  uthibitishe ya kwamba zimetumwa kwa nia nzuri" 

Amewataka wananchi mara waonapo fedha imetumwa kwenye mitandao yao  na aliyezituma bado hajafahamika, ni vyema wakawa na subira hadi watakapo hakikisha zimetumwa kwa nia njema ili wasiingie kwenye matatizo."watu huwa wanakosea pia yamkini zilitumwa kwa bahati mbaya, ukiwahi kuzitoa nawe unahesabika unaiba. alisema"

Amewataka watumiaji wa simu za mkononi kufahamu kuwa zipo tahadhari za kuchukuliwa ikiwepo kusajili namba kwa majina kamili  ya muhusika kwani ni takwa la kisheria, bila kusahau kwamba kila taarifa zinazoyolewa wakati wa usajili ziwe za sahihi.Taarifa zako zikiwa za uongo hilo nikosa kisheria utapata adhabu ya kifungo au kulipa shilingi milioni 3 au vyote kwa pamoja. 

Ameshauri kwamba yeyote akipoteza simu au kadi atoe taarifa kwa jeshi la polisi na kwa mtoa huduma, samba na kuchukua tahadhari mara uokotapo simu au kadi ya simu utoe taarifa kwa usalama wako zaidi.Wananchi wote wanaotembelea maonyesho  25 ya kilimo na sherehe za nanenane kanda ya kaskazini mwaka 2018 wanashauriwa kutembelea banda la TCRA ili waweze kupata elimu zaidi ya mawasiliano.
Wa kwanza kulia ni Kaimu mkuu Kanda ya kaskazini Francis Msungu, akifuatiwa na Mhandisi Jan Kaaya wakiendelea kutoa elimu kwa baadhi ya wageni waliotembelea banda hilo katika maonesho ya 25 ya nanenane  viwanja vya TASO mkoani Arusha. 
Wananchi wakiendelea kupatiwa elimu juu ya nyenzo za mawasiliano. 

NEC YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATIKA KATA 21

$
0
0
Hussein Makame, NEC 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika kata 21 za mikoa 10 ya Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 16 Septemba mwaka huu. 

Akitoa taarifa ya uchaguzi huo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia, alisema fomu za uteuzi wa wagombea wa uchaguzi huo zitatolewa kati ya tarehe 17 hadi 23 Agosti mwaka huu. Aliongeza kuwa uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 23 Agosti wakati kampeni za Uchaguzi zitafanyika kati ya tarehe 24 Agosti hadi tarehe 15 Septemba mwaka huu. 

Dkt. Kihamia alisema kuwa Tume imetangaza uchaguzi huo baada ya kupokea taarifa ya uwepo nafasi wazi za udiwani katika kata hizo 21 zilizopo katika Halmashauri 15 kutoka kwa Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa. “Nafasi wazi za udiwani katika Kata hizo zimetokana na sababu mbalimbali zikiwepo kifo, kujiuzulu, kutohudhuria vikao na kufutwa uanachama” alisema Dkt. Kihamia na kuongeza kuwa; 

“Baada ya kupokea taarifa hiyo na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa; Tume ina utaarifu Umma kuhusu kuwepo kwa Uchaguzi mdogo katika Kata hizo 21.” Kufuatia taarifa hiyo, Dkt. Kihamia alitoa mwaliko wa Tume kwa vyama vya siasa, wadau wote wa Uchaguzi na wananchi kwa ujumla kushiriki katika Uchaguzi huo. 

“Tume inachukua fursa hii kuviasa vyama vya siasa na wadau wote wa Uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka 2015” alisema Dkt. Kihamia. Aidha alivitaka vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi kuzingatia Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 pamoja na maelekezo yote yaliyotolewa au yatakayotolewa na Tume wakati wote wa Uchaguzi mdogo. 

Uchaguzi huu mdogo wa udiwani katika kata 21 unatarajiwa kufanyika sanjari na uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo ya Korogwe Vijijini, Ukonga na Monduli na kata za Tindabuligi na Kisesa katika Halmashauri ya Wilayani Meatu, uliotangazwa juzi ambao utakaofanyika siku ya Jumapili tarehe 16 Septemba mwaka huu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia.

AWESO AMLILIA RAIS MAGUFULI BARABARA YA TANGA,PANGANI SAADANI

$
0
0
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika sokoni mjini Pangani ambako pamoja na mambo mengine aliweza kusikiliza kero zao zinazowakabili NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika sokoni mjini Pangani ambako pamoja na mambo mengine aliweza kusikiliza kero zao zinazowakabili Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani akizungumza katika mkutano huo
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akiwa amebebwa juu na wananchi mara baada ya kumaliza kuwahutubia
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)kulia akiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa Abdallah wakifuatilia hoja za wananchi kwenye mkutano huo MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa Abdallah akimtunza msaanii Dkt Nyau
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) kushoto akimtunza mmoja wa wananchi

sehemu ya wananchi wa mji wa Pangani wakimfuatilia NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)
Wananchi wakimfuatilia NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)
SERIKALI ya awamu ya tano imeombwa kuangalia namna ya kuanza ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani, Saadan hadi Bagamoyo ili kuweza kumaliza kilio cha wananchi wa wilaya ya Pangani cha muda mrefu ikiwemo kufungua fursa za kiuchumi na maendeleo kwa mkoa .

Ombi hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso wakati akizungumza kwenye mkutano wake wa hadhara wilayani humo ambapo alisema pamoja na kuwepo kwa miradi mingi inayotekelezwa huko lakini kilio kikubwa cha wananchi wake ni ukosefu wa barabara nzuri.

Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) alisema wakati Rais Magufuli akiomba kura kwa wananchi hao mwaka 2015 aliwaahidi wananchi ujenzi wa barabara hiyo na walikubali kumpa kura nyingi na imani kubwa kwake kwa mategemeo ya kumpata mkombozi atakae weza kumaliza kero hiyo ambayo imedumu katika awamu zote nne zilizopita bila ya mafanikio.

“Kwenye mkutano wangu wa leo hii nipo hapa nyumbani kama Mbunge wenu kawaida na sikuja kama Naibu Waziri na jukumu la Mbunge ni kuwasemea wananchi wake Mh Rais wananchi wangu kiukweli wanalia na suala la barabara hii na hawajui hatma yake lini mradi huu utaanza”Alisema Aweso.

Hata hivyo alisema kuzorota kwa uchumi na maisha magumu kwa wananchi wa wilaya hiyo unachangiwa kwa kiasi kikubwa na tatizo la kutokujengwa barabara ambayo ingesaidia kufungua wilaya hiyo ambayo inaonekana kama imesahaulika katika nyanja zote.

Hata hivyo akionyesha kuunga mkono ujenzi wa barabara hiyo Mkuu wa Mkoa Tanga Martin Shigella alimueleza Waziri wa Fedha na Mipango Phillip Mpango juu ya umuhimu wa barabara ya Tanga, Pangani hadi Saadan wakati wa uzinduzi wa Tawi jipya la Benki ya Kiislam ya Amana

“Mh kilio kikubwa ni tatizo la barabara ya Tanga –Pangani Saadani tunaomba mtusaidie suala hilo kwani hakuna ukombozi unatarajiwa na wananchi wengi mkoani Tanga zaidi ya ujenzi wake”Alisema.

Shigella alimueleza hadharani Waziri huyo wa fedha kuwa Serikali inapaswa kufanya kila njia kuhakikisha inatenga fedha za kutosha ili kukamilisha mradi huo ambao bado hatma yake haijulikani utaanza lini.

Alisema Tanga ni Mkoa ambao unafunguka kiuchumi hasa katika swala zima la viwanda na matarajio ya barabara hiyo inaweza kurahisisha shughuli mbalimbali za kibiashara, usafirishaji wa mazao na utalii katika Mbuga ya Saadan hivyo ni jukumu la Serikali kuhakikisha barabara hiyo
inajengwa.

“Waziri wa fedha tunaomba mchako wa fedha kwa ajili ya barabara hiyo ufanyike kwa wakati ili kuwakomboa wananchi wa maeneo hayo na kukuza pato la Mkoa,Wilaya na hata mtu mmoja mmoja”Alisema Shigella.

Awali akizungumzia suala la ujenzi wa barabara hiyo Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philp Mpango alisema wamiliki wa viwanda,wafanyabiashara wakubwa na wadogowadogo wajitahidi kulipa kodi ili fedha hizo ziweze kujenga miundombinu ndani ya Nchi.

Alisema Serikali kupitia ukusanyaji wa kodi zake inahakikisha inatenga fedha kwa ajili ya ujenzi na ukatabati wa miundombinu ili kuondoa kerokwa wananchi katika maeneo husika.

RC MAKONDA ATEMBELEWA NA RAIS WA TFF, WAWEKA MIKAKATI THABITI YA KUIMARISHA MICHEZO.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelewa ofisini kwake na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Wallace Karia na Mwenyekiti wa Michezo Mkoa wa Dar es Salaam ambapo wamefanya mazungumzo ya kuimarisha sekta ya Michezo.

Miongoni mwa mambo waliyozungumzia ni Suala la heshima iliyopata Tanzania kuwa mwenyeji wa Michuano ya Mashindano makubwa ya michezo kwa Jeshi la Polisi katika nchi za mashariki na Kati zikihusisha Nchi Saba ambapo tayari michuano hiyo imefunguliwa rasmi siku ya Jana na Waziri mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.

Aidha wamezungumzia maandalizi ya mashindano makubwa ya SECAFA Cuf kwaajili ya michuano ya AFCON yakihusisha vijana wenye umri chini ya miaka 17 yanayotaraji kufanyika August 11 Mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa yakijumuisha mataifa 10 Afrika.

RC Makonda amesema michuano yote hiyo itafanyika Jijini Dar es salaam na kwakuwa inahusisha ugeni kutoka mataifa mbalimbali itatoa fursa kwa wananchi wa Dar es salaam hususani wenye hotel, vyakula, usafiri na wafanyabiashara kupata kipato kupitia mashinano hayo.

Kwa upande wake Rais wa TFF Wallance Karia amempongeza RC Makonda kwa jitiada za kuinua sekta ya michezo kupitia ujenzi wa uwanja wa Bandari ambapo amesema wameamua kumuomba ushirikiano kwakuwa wanaamini uwezo ukubwa alionao kwenye kusimamia jambo na kufanikisha.
 Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Wallace Karia akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhusiana na michuano ya Vijana ya AFCON itakayofanyika mwakani hapa nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari baada ya ujio wa Rais wa TFF Wallace Karia ofisini kwake

DKT TIZEBA AAGIZA VIUATILIFU VYOTE VINAVYO ONYESHWA BILA KUFUATA UTARATIBU KUONDOLEWA KWENYE MAONESHO YA NANENANE

$
0
0
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza jambo mara baada ya kutembelea Kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro Leo 6 Agosti 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akikagua mashine ya mbalimbali za kilimo mara baada ya kutembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro Leo 6 Agosti 2018. 
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akijionea michoro mbalimbali ya ramani za nyumba mara baada ya kutembelea banda la VETA, Kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro Leo 6 Agosti 2018.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akimsikiliza Mhandisi wa Kanda ya Umwagiliaji Morogoro Mhandisi Senzia Maeda mara baada ya kutembelea banda la Tume ya Umwagiliaji, Kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro Leo 6 Agosti 2018.

Na Mathias Canal, WK-Morogoro


Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba Leo 6 Agosti 2018 amewaagiza waratibu wa maonesho ya nanenane kuhakikisha Viuatilifu vinavyoonyeshwa kwenye maonesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane pasina kufuata utaratibu wa kisheria vinaondolewa haraka.


Waziri Tizeba ameyasema hayo wakati akizungumza na wauzaji wa viuatilifu Kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro mara baada ya kutembelea banda la Tan Vaterinary ambalo linauza viuatilifu vya aina mbalimbali zikiwemo dawa za virutubisho kwa ajili ya Nguruwe na kuku.


Alisema katika agizo hilo kuwa viuatilifu vyote vinavyouzwa pasina nembo ya Mamlaka ya viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) na kampuni ya kutoa barcode za bidhaa zilizofungashwa (GS 1) hazipaswi kuwepo kwenye maonesho ya Nanenane kote nchini kwani kuruhusu viendelee kuuzwa ni hatari kwa wanyama sambamba na binadamu.


Alisema kuwa katika maeneo mengi nchini udhibiti wa viuatilifu ni mdogo hivyo wakaguzi wa viuatilifu wanapaswa kutilia mkazo ukaguzi ili kuzuia viuatilifu vinavyoingia nchini kinyume cha sheria na taratibu za nchi.


Kuhusu elimu kwa wananchi juu ya njia bora za kuhifadhi mahindi Waziri huyo anayeshughulikia sekta ya kilimo nchini aliagiza elimu kutolewa kwa kina kwa wananchi ili wawe na uelewa mkubwa pindi wanapomaliza kuvuna.


Alisema kuwa kumekuwa na biashara ya vihenge jambo ambalo ni zuri lakini changamoto kubwa wananchi bado hawajapatiwa elimu ya namna bora ya kuvitumia vihenge hivyo.


Aidha, amewataka washiriki mbalimbali kutuma wawakilishi kwenye weledi kuhusu bidhaa wanazoonyesha kwani kumekuwa na wawakilishi wengi ambao sio msaada kwa wakulima ambao wengi wao wanatembelea katika maonesho hayo kwa mtazamo wa kujifunza.


Katika hatua nyingine akiwa katika banda la maonesho ya Mifugo, Waziri Tizeba amewataka wataalamu hao wa Mifugo kubadili mtazamo wa kifikra kwa kuonyesha bidhaa bora, "Kila mwaka mnaleta Ng'ombe wa kisasa kwenye maonesho ya Nanenane wakati wanaokuja kujionea maonesho wengi ni wafugaji wa Ng'ombe wa kienyeji, hivyo badilikeni leteni Ng'ombe wa kienyeji" Alikaririwa Dkt Charles Tizeba

MKUU MPYA WA MKOA WA SONGWE BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AWASILI KITUONI , AAHIDI KUENDELEZA MAZURI YA GALLAWA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Elias Mwangela amewasili katika ofisi yake mapema leo asubuhi kufuatia kuteuliwa kwake kuuongoza Mkoa wa Songwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Magufuli Julai 28, 2018.

Brigedia Jenerali Mwangela amepokelewa na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya nne za Mkoa wa Songwe, wakurugenzi wa halmashauri tano za Mkoa huu, wakuu wa idara pamoja na watumishi wote wa ofisi yake.

Mara baada ya mapokezi hayo Brigedia Jenerali Mwangela amepokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Gallawa katika kikao cha pamoja na wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wakuu wa idara na wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama.

Gallawa amesema kuwa anayo furaha kumkaribisha Brigedia Jenerali Mwangela na anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Magufuli kwa kumteua Brigedia Jenerali Mwangela, na kuwa wale waliokuwa wakifurahia kuondoka kwake wakijua sasa wataanza kufanya kazi ndivyo sivyo wajue wamepata kiongozi ambaye ni makini zaidi”.

Ameongeza kwa kuwataka watendaji na wanasiasa waendelee kuchapa kazi kwa bidii wakiwa na lengo la kumkomboa mwananchi wa Songwe kutoka katika umasikini na kuongeza pato la mkoa na taifa.Naye Brigedia Jenerali Mwangela amemshukuru Gallawa kwa kuweka misingi mizuri ambayo imelenga kuuinua Mkoa wa Songwe kiuchumi na kuahidi kuwa atahakikisha mazuri yote atayaendeleza hasa pale alipoishia.

Ameongeza kwa kuwasihi watendaji kufanya kazi kwa kufuata sheria, taratibu na maadili ya utumishi wa umma na kwa kushirikiana kwa kuwa anaamini katika ushirikiano kazi zinafanyika kwa ufanisi."Tufanye kazi tuwatumikie wananchi wa Songwe, milango ya ofisi yangu itakuwa wazi kwenu kwakuwa napenda kufanya kazi kwa ushirikiano, nami pia ninaomba ushirikiano wenu kama mliokuwa mnapa Gallawa ikiwezekana hata Zaidi,” amesema Brigedia Jenerali Mwongela.

Amewataka watumishi kuzingatia muda katika kila jambo wanalotekeleza wasiopoteze muda huku akiwasisitiza kufanya kazi kama timu moja.

“Nawapa mfano wa silaha ya mzinga ambao ili iweze kufanya kazi vizuri wanahitajika watu sita ambao kila mmoja ana jukumu lake la kufanya ili mzinga huo ufanye kazi kwa ufanisi, hii ni timu na akikosekana mmoja mzinga hautaweza kufanya kazi sawasawa, nasisi tuige ushirikiano kama huu kila mmoja atekeleze jukumu lake ili tufikie lengo moja”, amefafanua Brigedia Jenerali Mwangela
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Elias Mwangela akipokelewa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Gallawa mapema leo asubuhi alipowasili ofisini kwake.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Elias Mwangela akisalimiana na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila mapema leo asubuhi alipowasili ofisini kwake.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Elias Mwangela akisaini kitabu ofisini kwake mapema leo mara baada ya kuwasili na kupokelewa na watumishi na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Songwe.

MBUNGE GULAMALI AELEZWA NAMNA CHUO CHA NIT KILIVYOJIPANGA KUWAPOKEA WATALAAM WA BOEING ILI KUWANOA ATCL

$
0
0
Na Francis Daudi, Glogu ya jamii

MBUNGE wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali amtembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ambacho kimejidhatiti kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya Usafirishaji nchini Tanzania kwa kuzalisha wataalamu wengi zaidi ikiwa ni sehemu ya mkakati wao wa kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya tano katika kujenga Tanzania ya Viwanda. 

Akizungumza leo chuoni hapo baada ya kupokelewa na Mkuu wa chuo hicho Profesa Zacharia Mginilwa, Gulamali amesema amefurahishwa na utendaji kazi sambamba na mikakati iliyopangwa katika kuhakikisha sekta ya usafirishaji inakua zaidi.Amesema kuwa amefurahi kuona chuo alichosoma kinaendelea kuzalisha wataalamu zaidi katika sekta ya usafirishaji ambayo inachangia uchumi wa Taifa kwa asilimia kubwa.

Pia chuo hichokinaonesha jitihada za kuunga mkono juhudi za Rais Dkt John Magufuli na amehaidi kutoa ushirikiano wa hali na mali pindi itakapohitajika.

Akiwa Chuoni hapo Gulamali alipata fursa ya kutembelea Shule ya usafiri wa anga (School of Aviation) yenye madarasa ya waendesha ndege, karakana maalumu za kutengeneza injini za ndege na baadaye alitembelea idara ya ukaguzi wa magari na kueleza kufurahishwa na utendaji kazi unaofanywa kwa kutumia teknolojia ya juu.

Akieleza historia ya Chuo hicho, Mkuu wa Chuo Profesa Zacharia Mganilwa amesema kilianzishwa mwaka 1975 na ni miongoni mwa vyuo vya mwanzo kabisa kuanzishwa na Rais wa Awamu ya Kwanza Mwalim Julius Nyererere kwa lengo la kuhakikisha vinakuza sekta ya usafirishaji nchini.

Profesa Mginilwa amesema mipango ya Chuo hicho na hatua walizofikia ni kuhakikisha kinakuwa Chuo Kikuu cha Usafirishaji nchini Tanzania na Afrika.Ameongeza kuwa chuo hicho kimepata fedha karibu Sh.bilioni 140 toka Serikali ya China ili kujenga majengo na kuimarisha miundo mbinu katika chuo hicho na Kuwa Chuo Kikuu cha Usafirishaji.

Profesa Mganilwa amefafanua wamejikita pia katika kuzalisha wataalamu bora zaidi ili kwenda na kasi ya Serikali katika kujenga miundombinu bora ya usafiri nchini.Pamoja na mambo mengine pia chuo hicho kimeanzisha kozi zinazoendana na uhitaji wa soko la ajira kama vile Shahada ya Marekebisho ya Ndege na Shahada ya Elimu katika Hisabati na Teknolojia ya Mawasiliano.

Ameongeza kuwa fani hizo ni sehemu ya fani nyingi zilizopo chuoni hapo ambazo hazipatikani katika Chuo chochote hapa nchini na kuongeza wamepeleka wataalamu katika nchi za China, Korea na Japan ili kuongeza ujuzi katika Uzamili na Uzamivu ili kuimarisha idara mbalimbali ndani ya Chuo cha NIT.

Chuo cha NIT kimepokea takribani Sh.milioni 400 kutoka Benki ya Dunia na Mashirika ya ndege duniani ili kusaidia kuzalisha zaidi wataalamu bora katika sekta ya usafirishaji hasa wa usafiri wa anga na kinatarajia kupokea wataalamu kutoka Shirika la Boeing ambao watatoa mafunzo kwa wataalamu na wafanyakazi wa Shirika la Ndege(ATCL).

Na hiyo inatokana na chuo hicho kuwa miundo mbinu na vifaa bora vya kufundishia masuala mbalimbali katika usafiri wa anga.Mkuu wa Chuo hicho amemshukuru na kumpongeza Gulamali kwa kuwa kijana mchapakazi na anayehamasisha maendeleo na kwamba amekuwa chachu kubwa kwa wanafunzi wa chuo hicho ambacho alisoma miaka 8 iliyopita.

Amemuomba asichoke kutembelea na kutoa mawazo yake katika kujenga na kuimarisha sekta ya usafirishaji nchini.
 Mbunge wa Manonga Seif Gulamali ( kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chuo cha usafirishaji nchini (NIT) mara baada ya kumaliza ziara yake chuoni hapo.
 Mbunge wa Manonga Seif Gulamali akikagua baadhi ya vifaa katika karakana chuoni hapo kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Zacharia Mginilwa.
Mbunge wa Manonga Seif Gulamali akiwa katika chumba cha uongozaji wa ndege katika chuo cha usafirishaji (NIT) mara baada ya kufanya ziara  Chuoni hapo.

MWAKILISHI WA JIMBO LA TUNGUU ZANZIBAR MHE. SIMAI MOHAMMED SAID AKABIDHI CHETI CHA SHUKRANI KWA UONGOZI WA SHIRIKA LA BIMA ZANZIBAR

$
0
0


Mkurugenzi Muendeshaji wa Shirika la Bima Zanzibar Ndg. Abdulnasir Ahmed Abdurahaman akiwa na mgeni wake Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said wakielekea chumba cha mkutano wakati wa mkutano wake wa kutowa shukrani na kukabidhi Cheti cha shukrani kwa kuthamini mchango wao kusaidia Wananchi wa Jimbo la Tunguu Wilaya ya Kati Unguja kuimarisha Miradi ya Maji Safi na Salama.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza na kutowa shukrani za Wananchi wa Jimbo lake kwa msaada wao katika kufanikisha Mradi wa usambazaji wa mabomba ya maji katika Jimbo hilo, kulia Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Bima Zanzibar Ndg. Jumbe Said Ibrahim na kushoto Mkurugenzi Muendeshaji wa Shirika la Bima Zanzibar Ndg. Abdulnasir Ahmed Abdulrahaman. wakiwa katika ukumbi wa Ofisi hizo.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza kabla ya kukabidhi Cheti cha shukrani kwa Shirika la Bima Zanzibar kwa msaada wao kusaidia Mradi wa usambazaji wa mipira ya kusambaza maji katika Jimbo hilo katikati Mkurugenzi Muendeshaji wa Shirika la Bima Zanzibar Ndg. Abdulnasir Ahmed Abdulraham na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Bima Zanzibar Ndg Jumbe Said Ibrahim.wakifuatilia maelezo hayo.

MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Wilaya ya Kati Unguja Mhe. Simai Mohammed Said akimkabidhi Cheti cha shukrani Mkurugenzi Muendeshaji wa Shirika la Bima Zanzibar Ndg.Abdulnasir Ahmed Abdurahaman , kwa
ushirikiano wa kuchangia maendeleo ya Wananchi wa Jimbo la Tunguu, katika sekta ya maji, akishuhudia Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bima Zanzibar.Ndg. Jumbe Said Ibrahim.hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Bima Mpitani Zanzibar

MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Wilaya yaKati Unguja Mhe. Simai Mohammed Said akimkabidhi Cheti cha shukrani Mkurugenzi Muendeshaji wa Shirika la Bima Zanzibar Ndg.Abdulnasir Ahmed Abdurahaman , kwa
ushirikiano wa kuchangia maendeleo ya Wananchi wa Jimbo la Tunguu, katika sekta ya maji, akishuhudia Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bima Zanzibar.Ndg. Jumbe Said Ibrahim.hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Bima Mpitani Zanzibar

Mkurugenzi Muendeshaji wa Shirika la Bima Zanzibar Ndg. Adbulnasir Ahmed Abdulrahamn akifurahia wakati akikabidhiwa Cheti cha Shukrani na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, kushoto, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Bima Mpirani Zanzibar.


Mkurugenzi Muendeshaji wa Shiriki la Bima Zanzibar, Ndg. Abdulnasir Ahmed Abdulrahaman kulia akitowa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa Cheti cha shukrani na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu kwa kuthamini mchango wao kwa Wananchi wa Jimbo lake.kushoto Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Bima Zanzibar Ndg. Jumbe Said Ibrahim.



Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akipata maelezo kutoka kwa Wafanyakazi wa Shirika la Bima wakati alipopata fursa ya kutembelea Ofisi za Bima Mpirani kujionea utendaji na ufanisi wa Kazi zao kuhudumia wateja wao.katikati Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Ndg. Jumbe Said Ibrahim na Mkurugenzi Muendeshaji wa Shirika la Bima Zanzibar Ndg. Abdulnasir Ahmed Abdurahaman.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akipata maelezo kutoka kwa Wafanyakazi wa Shirika la Bima wakati alipopata fursa ya kutembelea Ofisi za Bima Mpirani kujionea utendaji na ufanisi wa Kazi zao kuhudumia wateja wao.katikati Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Ndg. Jumbe Said Ibrahim na Mkurugenzi Muendeshaji wa Shirika la Bima Zanzibar Ndg. Abdulnasir Ahmed Abdurahaman.

Mkurugenzi Muendeshaji wa Shirika la Bima Zanzibar Ndg. Abdulnasir Ahmed Abdulrahaman mwenye tai nyekundu akitowa maelezo kwa Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar alipokuwa akitembelea Ofisi za Bima Mpirani Zanzibar wakati wa hafla ya kukabidhi Cheti cha Shukrani.

ALICHOZUNGUMZA DC WA NAMTUMBO MARA TU BAADA YA KUAPISHWA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo

MWENYEKITI WA CCM TARIME ACHANGIA VIFAA VYA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 2.4.

$
0
0
Na Frankius Cleophace Tarime.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Tarime Marwa Daud Ngicho amechagia Vifaa mbalimbali katika shule ya Msingi Mturu iliyopo Kata ya Turwa Mjini Tarime Mkoani Mara kwa ajili ya kuanzisha Stationery ya shuke hiyo kwa lengo la kuondokana na adha ambayo wamekuwa wakipata katika kipindi cha Mtihani.

Mwenyekiti huyo ametoa Vifaa mbalimbali ikiwemo Mashine ya kutolea kopi Mitiani huku wazazi na walezi pamoja na wadau wa Elimu wakiunga Mkono harambee hiyo kwa kuchangia zaidi ya shilingi 70,000.Ngicho amesema kuwa ameamua kutoa vifaa hivyo kwa lengo la kuunga jitiada za serikali ya awamu ya tano katika kutoa elimu bure ili kila mtoto wakiwemo watoto wa maskini wanaenda shule.

“Nilipokea barua yenu ya mahitaji hayo yote sasa nimenunua vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi Millioni mbili na Laki Nne wajibu wenu ni kuvitunza ili kizazi na kizazi kiweze kunufaika” alisema Ngicho.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Mturu Jumanne Obogo amesema kuwa gharama za kuandaa mitiani kipindi cha Mwaka mzima zilikuwa kubwa ambapo shule hiyo utumia kiasi cha shilingi Mill3.5 jambo ambalo ni changamoto kubwa , hivyo upatikanaji wa vifaa hivyo vitasaida changamoto hiyo hukua wakitoa shukrani zao. 

Pia Mwalimu huyo amesema kuwa licha ya shule hiyo kupatiwa vifaa hivyo bado inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa Matundu ya vyoo na kuomba Mgeni rasmi kuwasaidia kutatua changamoto hiyo ambapo baadhi ya wadau na wazazi katika harambee hiyo wameweza kutoa Mifuko ya Saruji pamoja na ahadi mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa Vyoo hivyo.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Tarime Daud Marwa Ngicho akikabidhi moja ya kifaa kati ya Vifaa vilivyotolewa katika Shule ya Msingi Mturu kwa ajili ya kuanzisha Stationery Vyenye thamini ya Mill2.4 ikiwemo Mashine ya Kutolea Kopi Mitihani.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Tarime Daud Marwa Ngicho akionyesha wazazi baadhi ya vifaa alivyotoa.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Tarime Daud Marwa Ngicho akisisitiza suala la ushirikiano baina ya wazazi na walimu hao ili kuongeza ufaulu pamoja na mahudhurio ya wanafunzi.

Picha4 Richard Tiboche ambaye ni Mjumbe wa kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Tarime akiongea na wazazi na walezi katika Shule ya Msingi Mturu Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara.
Wazazi na walezi wakiwa katika harambee ya kuchagia Vifaa vya Stationery katika Shule ya Msingi Mturu ambapo wazazi hao pamoja na walimu na wadau wa elimu wamechangia zaidi ya 70,000.
Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Mturu Jumanne Obogo akibainisha changamoto mbele ya mgeni rasmi ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime Daud Marwa Ngicho.
Baadhi ya Vifaa vilivyotolewa na Mgeni rasmi Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime Daud Marwa Ngicho vyenye thamani ya shilingi Mill 2.4.

WATANZANIA WASHAURIWA KUTUMIA MCHICHA NAFAKA

$
0
0
WATANZANIA hususani watoto na akina mama wajawazito wametakiwa kutumia zaidi mchicha nafaka kama chakula kitakachowaongezea viini lishe muhimu kwa afya ya miili yao. 

Wito huo umetolewa mjini Arusha wakati wa Kongamano la linalojadili Afya na na Lishe bora liliwakutanisha wataalamu wa masuala ya lishe kutoka ndani na nje ya nchi wakiwamo wanajamii. 

Kongamano hilo lililoanza Agosti 6 na kukamilika Agosti 9, Mwaka huu linafanyika hapa ambapo wataalamu wanabadilishana uzoefu kuhusu masuala ya afya na lishe bora limeandaliwa na Shirika la World Vission Tanzania (WVT), wakishirikiana na Taasisi ya Amaranth ya Marekani na ECHO. 

Akizungumza kwenye kongamano hilo Mkurugenzi wa Uendeshaji Miradi ya Shirika la World Vission Tanzania, Dk. Yosh Kaslima alisema kupitia shughuli wanazofanya kwenye mikoa 13 na wilaya 36 wamebaini kuwapo tatizo la lishe bora kwa watoto na mama wajawazito. 

“Wananchi hawajui wawalishe nini watoto na akina mama wajawazito, kwa hiyo tunatarajia kupitia kongamano hili washiriki watatoa na kupokea elimu mimea gani ina virutubisho vitakavyowawezesha kuboresha afya za watoto wakiwa wadogo,” alisema Kaslima. 

Kwa upande wake mgeni rasmi katika Kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema, ujumbe wa kongamano hilo unaohamasisha lishe ni muhimu kwani umekuja kwa wakati sahihi. “Hii inakwenda sambamba na Sera ya Taifa ya Chakula na Lishe ya mwaka (2007) inayohamasisha uhusiano wa chakula na lishe katika sekta mbalimbali na utokomezaji wa utapiamlo hasa kwa watoto na kina mama,”

“Kumuelimisha kila mwananchi, aelewe kuwa ana wajibika moja kwa moja kutunza afya yake na ile ya familia yake. Kujenga ushirikiano kati ya sekta ya umma, sekta binafsi, mashirika ya dini, asasi za kijamii na jamii katika kutoa huduma za lishe na afya,” alisema Gmbo kupitia kwa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega.
 Wataalamu wa masuala ya afya na lishe kwa mama na mtoto wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye kongamano la Kimataifa kuhusu Lishe katika maeneo kame nchii lililofanyika mjini Arusha 
Wataalamu wa masuala ya afya na lishe kwa mama na mtoto wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye kongamano la Kimataifa kuhusu Lishe katika maeneo kame nchii lililofanyika mjini Arusha katika picha ya pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega

UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA UHAKIKA WAIVA

DC ARUMERU AWAFARIJI WANANCHI WA KATA YA MBUGUNI ILIYOKUMBWA NA MAFURIKO

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh Jerry Muro amefanya ziara kata ya Mbuguni,iliyokumbwa na changamoto ya mafuriko Aprili Mwaka huu, ambapo amewatembelea wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo na kuwafariji kwa kutoka misaada mbalimbali ikiwemo magodoro,mablanketi, vifaa vya kuhifadhia maji dawa za kutibu maji na vyandarua pamoja na vifaa vya chakula kwa kila Kaya 60 zilizoathirika.

DC Muro pia ametoa msaada wa vifaa vya usafi kwa wanafunzi wa Shule ya mbuguni,ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Mh.Rais John pombe Magufuli katika kuhakikisha mtoto wa kike anapata Elimu bora huku akiwa katika mazingira bora ya kusoma.

Wananchi wamemshukuru Mh Rais kwa kumteua Jerry Muro kuwa Mkuu wa Wilaya ambaye tayari ameanza kuwahudumia kwa kuwaletea misaada. 

Pia wananchi wamempongeza Rais Magufuli kwa kuendelea kutafuta wadau mbalimbali wa Maendeleo ambao wameanza kuunga mkono jitihada za serikali hususani katika upande wa kukabiliana na majanga kupitia kazi nzuri inayofanywa na Shirika la msalaba mwekundu Tanzania ( Tanzania RedCross )

Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru 

 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh Jerry Muro akigawa msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo mablanketi kwa mmoja wa waathiriwa na mafuriko kutoka kijiji cha Mbuguni,ambao walikumbwa na adha ya mafuriko Aprili mwaka huu.
 DC Muro akikabidhi msaada wa vifaa vya usafi kwa  mmoja wa Wanafunzi wa Shule ya mbuguni
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh Jerry Muro akizungumza na Wakazi wa Mbuguni mara baada ya kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa waathiriwa wa mafuriko waishio katika kijiji hicho
Baadhi ya vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh Jerry Muro,ikiwa ni sehemu ya msaada wa vifaa mbalimbali kama vile mablanketi,vifaa vya kufanyia usafi kwa wanafunzi wa shule,Magodoro na vinginevyo kwa waathiriwa na mafuriko kutoka kijiji cha Mbuguni  waliokumbwa na adha hiyo Aprili mwaka huu.

MTIBWA, KMC KUITAMBULISHA REHA FC.

$
0
0
Matokeo mazuri ya kila jambo yanahitaji maandalizi timamu na ndivyo tunavyofanya kuelekea msimu mpya wa ligi daraja la kwanza.

Wakati maandalizi yakiwa yamenoga jana tumetangaza tarehe rasmi ya utambulisho wa timu kwa wakazi wa Temeke na mkoa wa Dar es salaam kwa ujumla.

Mtendaji mkuu wa klabu Abubakar Jafo amewaambia wanahabari kwamba kuanzia leo ni wiki ya REHA FC ambapo kilele chake itakua siku ya jumapili kwenye uwanja wa Bandari Tandika. 

"Wiki ya Reha itahusisha shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kufungua matawi yetu na kuhitimishwa kwa michezo maalum itakayohusisha timu nne ambazo ni Mtibwa, KMC na Transit Camp  na wenyeji Reha fc" amesema Jafo.

Jafo amesema michezo hiyo itaanza jumamosi kwa mchezo wa mapema saa 8 mchana kati ya Reha dhidi ya Transit Camp na saa 10 jioni Mtibwa itacheza na KMC kisha washindi watacheza fainal siku ya jumapili jioni huku waliofungwa wakicheza mchana. "Siku hiyo tutaitumia kuwatambulisha wachezaji wetu pamoja na benchi la ufundi".

Mtendaji Mkuu wa timu ya Reha Fc Abubakar Jafo

MBUNGE AWATAKA WANACCM NA WANANCHI MKOANI SINGIDA KUMPA HESHIMA RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI

$
0
0

Mbunge wa Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu (kulia), ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea udiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Unyambwa Wilaya ya Singida mjini, Abdulazizi Hamisi Labu, akihutubia wananchi na wana CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika  katika Viwanja vya Kitongoji cha Unyambwa Juu mkoani humo jana.
Mbunge wa Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu (kulia), akimnadi mgombea huyo, Abdulazizi Labu.
Naibu wa Waziri wa Mazingira na Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mheshimiwa Musa Ramadhan Sima, akihutubia kwenye mkutano huo.
Kampeni Meneja wa uchaguzi huo, Selemani Hamisi Mdulu, akizungumza kwenye mkutano huo.
Wakazi wa Kata ya Unyambwa Juu wakiwa kwenye mkutano huo.
Wazee wa kata hiyo wakifuatilia mkutano huo.

Muonekano wa meza kuu kwenye mkutano huo.
Naibu wa Waziri wa Mazingira na Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mheshimiwa Musa Ramadhan Sima (katikati), Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Mjini, Lusia Andrew.
Mkutano ukiendelea.
Mgombea udiwani wa Kata ya Unyambwa, Abdulazizi Labu (kulia), akiwa na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida mjini katika mkutano huo.
Madiwani wa Wilaya ya Singida Mjini wakiwa wamepiga magoti kumuombea kura mgombea huyo kwa wananchi.
Vijana wa CCM wakipiga pushapu kumuombea kura mgombea huyo.
Wanawake wa CCM wakiwa wamenyoosha mikono kumuombea kura mgombea huyo.
Mkuu wa Wilaya mstaafu wa Wilaya ya Nchemba, Francis  Mtinga, akizungumza katika mkutano huo wakati akimuombea kura mgombea huyo.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida, Diana Mkumbo Chilolo, akimuombea kura mgombea huyo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Singida Mjini, Chifu ya Aledi Sylvester akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa, akihutubia kwenye mkutano huo wakati akimuombea kura mgombea huyo.
Mhemiwa Musa Sima , akiserebuka na wanawake wa CCM wakati akienda kuhutubia.
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Jimson Mhagama, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Singida, Aisharose Matembe, akimuombea kura mgombea huyo.
Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Singida Mjini, Lusia Andrew akimuombea kura mgombea.
Naibu wa Waziri wa Mazingira na Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mheshimiwa Musa Ramadhan Sima, akiteta jambo na Salum Kingi, mwenye ulemavu wa miguu ambaye alikuwa akionesha kuomba msaada fulani kutoka kwa waziri huyo.

Mgeni rasmi katika mkutano huo, Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akiongoza kutoa kiapo kwa wananchi na wana CCM cha kumchagua diwani Abdulazizi Labu.
Wananchi na wana CCM wakila kiapo hicho.
Mgombea udiwani wa Kata hiyo, Abdulazizi Labu, akiomba kura kwa wananchi.
Watoto nao walikuwepo kwenye mkutano huo.
Wabunge wakifurahi jambo kwenye mkutano huo. Kulia ni  Mheshimiwa Aisharose Matembe na Mheshimiwa Elibariki Kingu.
Mheshimiwa Musa Sima na Elibariki Kingu, wakiserebuka na wanachama wenzao wa CCM na wananchi huku wakiwa wamejitwika vibuyu. 'Hakika ina pendeza sanaaaaa.'

Na Dotto Mwaibale, Singida

MBUNGE wa Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu amewataka wananchi na wana CCM wa Kata ya Unyambwa Wilaya ya Singida mjini kumpa heshima Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa kumchagua mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulazizi Hamisi Labu.

Kingu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea huyo wa udiwani uliofanyika kitongoji cha Unyambwa Juu jana alisema hakuna heshima kubwa ya kumpatia Rais Magufuli zaidi ya kumchagua Labu kuwa diwani wa eneo hilo.

"Ndugu zangu wanananchi na wanaccm wenzangu hakuna heshima kubwa ya kumpa Rais wetu Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama chetu Taifa kama si kumchagua Labu awe diwani wa kata hii kwani Magufuli ameonesha kutujali sana wananchi wa Singida" alisema Kingu huku akishangiliwa na wananchi ambao walisema watamchagua Labu.

Kingu alisema heshima kubwa ya kumpa Rais Dk.John Magufuli ni kuhakikisha wana mchagua Labu tena kwa kura zote ili aungane na Rais na mbunge wa jimbo hilo kwa ajili ya kuwaletea maendeleo na si kumchagua diwani kutoka chama kingine.

Alisema Rais Magufuli amekuwa na imani na wananchi wa Mkoa wa Singida kwani amekuwa akisaidia kupeleka miradi mikubwa kama ya maji na kuteua viongozi wa serikali hivyo hawana zawadi ya kumpa zaidi ya kumchagua Labu ili kuongeza kasi ya maendeleo katika kata hiyo.

"Msifikiri haya yote yanayofanywa na Rais yana kuja bure hapana ni imani aliyonayo kwetu wana Singida kutokana na kushika nafasi ya pili kitaifa ya kuwa na kura nyingi tulizompigia  katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2015" alisema Kingu.

Alisema Rais Magufuli anafanya kazi kubwa ya kuliletea taifa maendeleo kwanza ameanza kwa kuanzisha miradi mikubwa ikiwemo kununua ndege saba za kisasa mpaka wazungu wanamshangaa kwa utendaji wake, miji karibu yote sasa imewekwa taa, kubana matumizi kwani hapo zamani viongozi mbalimbali walikuwa wakipishana angani kwenda nje ya nchi ambapo walikuwa wakitumia fedha nyingi za umma lakini leo hii safari hizo hazipo tena na hata wao wabunge wanapata mshahara na posho za kuhudhuria bunge tu na si kama ilivyokuwa zamani.

Katika mkutano huo viongozi mbalimbali wa CCM mkoa wa Singida wakiwepo wabunge na madiwani walipata fursa ya kuzungumza na kumuombea kura mgombea huyo ambapo wote kwa umoja wao waliomba achaguliwe Labu ili aungane na Rais na mbunge ambao ni kutoka CCM katika kutekeleza ilani ya chama hicho kwa kuwapelekea miradi mbalimbali ya maendeleo badala ya kumchagua diwani wa upinzani.

Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images