Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1639 | 1640 | (Page 1641) | 1642 | 1643 | .... | 1897 | newer

  0 0
 • 08/06/18--00:10: MAGAZETINI LEO

 • 0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro jana ameungana na Waumini wa Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Meru kuwasilisha Salamu za Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkoa wa Arusha na Wilaya ya Arumeru kwa Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Meru Askofu Elias Kitoi Nasari katika Hafla ya Harambee ya Uchangiaji wa Fedha kwa ajili ya Ununuzi wa Vyombo vya Kwaya pamoja na Gari kwa ajili ya huduma za Kanisa.
  Mhe Muro Amelipongeza Kanisa kwa kuendelea Kushirikiana na Serikali katika Utoaji wa Huduma za Kijamii katika Sekta Ya Afya, Elimu na Maji pamoja na Shughuli za maendeleo ya Kijamii. 

  Mhe Muro amesema Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli itaendelea Kudumisha na kuimarisha Ushirikiano kati ya Serikali na kanisani katika kuendelea kuwahudumia Wananchi wa Arumeru na Tanzania ambapo amesisitiza kila Mdau kuendelea kusimama na kutimiza wajibu wake katika eneo lake.

  Akipokea Salamu hizo, Baba askofu Elias Kitoi Nasari wa Jimbo la Meru Amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuendelea kupambana na Ufisadi pamoja na Maendeleo ambayo yameanza kuonekana katika Taifa la Tanzania.

  Askofu Nasari pia Amemshukuru Mhe Rais Magufuli kwa Kumteua Mhe Jerry Muro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru kutokana na Wilaya hiyo kukosa Mkuu wa Wilaya kwa Kipindi kirefu na Kusisitiza kuwa Kanisani litaendeea Kuungana mkono jitihada za Serikali katika Kuendelea kuwahudumia wananchi.

  Katika Hafla Hiyo Mhe Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro amejibu baadhi ya Hoja zilizowasilisha na Baba Askofu Nasari ikiwemo ya Changamoto ya Soko la Karoti na Lumbesa ambapo Mhe Muro amefafanua tayari ameshatoa Maagizo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote Mbili kupitia Maafisa kilimo na biashara kuzungumza na Wafanyabiashara na madalali wanakwenda kununua bidhaa hizo nje ya nchi kwa kuwataka kwanza kununua Bidhaa zinazolimwa na Wananchi wa Arumeru ambazo ubora wake unakidhi Viwango vya kimataifa na endapo Msimu utamalizika zikiwa zimeisha watatoa fursa ya kuagiza katika maeneo mengine ya nchini Tanzania na Sio nje ya nchi.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Ujumbe wake wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Mwani cha PT Aga Swallow Hendrico Soewardjono wakati alipotembelea leo akimalizia ziara yake ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Dkt.Mohamed Jusuf Kalla
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiangalia mwani uliosarifiwa ambao unaendelea na unaendelea kutengenezwa bidhaa mbali mbali ulioshikwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Mwani cha PT Aga Swallow Hendrico Soewardjono wakati alipotembelea leo akimalizia ziara yake ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Dkt.Mohamed Jusuf Kalla

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiangalia mwani uliosarifiwa ambao unaendelea na unaendelea kutengenezwa bidhaa mbali mbali ulioshikwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Mwani cha PT Aga Swallow Hendrico Soewardjono wakati alipotembelea leo akimalizia ziara yake ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Dkt.Mohamed Jusuf Kalla
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) na ujumbe wake wakiangalia unga wa mwani uliosarifiwa baada ya maandalizi ambao tayari kwa kuuzwa kwa matumizi ya mabo mbali mbali katika Nchi nyingi Duniani Rais alijionea wakati akimalizia ziara yake ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Dkt.Mohamed Jusuf Kalla,(wa pilikushoto)Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Mwani cha PT Aga Swallow Hendrico Soewardjono,
  Baadhi ya mashine katika kiwanda cha mwani ambazo hupelekea kuusarifu mwani katika mambo mbali mbali ambayo huwapatia mapato wenyekiwanda hicho kiliopo nje ya Mji wa Jakarta Indonesia ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo alitembelea na ujumbe wake akimalizia ziara yake ya mualiko wa Makamo wa Rais wa nchini hiyo Dkt.Mohamed Jusuf Kalla

  Marobota ya Mwani yakiwa katika kiwanda cha mwani cha PT Aga Swallow ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe wake walitembelea sehemu hii akimalizia ziara yake ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Dkt.Mohamed Jusuf Kalla

  Baadhi ya mashine katika kiwanda cha mwani ambazo hupelekea kuusarifu mwani katika mambo mbali mbali ambayo huwapatia mapato wenyekiwanda hicho kiliopo nje ya Mji wa Jakarta Indonesia ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo alitembelea na ujumbe wake akimalizia ziara yake ya mualiko wa Makamo wa Rais wa nchini hiyo Dkt.Mohamed Jusuf Kalla,[Picha nma Ikulu.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Mwani Hendrico Soewardjono alipowasili katika kiwanda cha kampuni hiyo leo na Ujumbe wake akimalizia ziara yake ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Dkt.Mohamed Jusuf Kalla
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na Mshauri Mkuu wa Bodi ya Kampuni ya Mwani ya Pt.Aga Swallow Dr.Agung Laksono alipowasili katika kiwanda cha kampuni hiyo leo na Ujumbe wake akimalizia ziara yake ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Dkt.Mohamed Jusuf Kalla,(kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Mwani Hendrico Soewardjono
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Mwani Hendrico Soewardjono alipowasili katika kiwanda cha kampuni hiyo leo na Ujumbe wake akimalizia ziara yake ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Dkt.Mohamed Jusuf Kalla
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) na Ujumbe wake akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya Mwani ya Pt Aga Swallo unaoongozwana Mkurugenzi Mkuu Hendrico Soewardjono (wa tatu kulia) alipowasili katika kiwanda cha kampuni hiyo leo na Ujumbe wake akimalizia ziara yake ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Dkt.Mohamed Jusuf Kalla,

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  TIMU ya Flying Dribblers imefanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kufanikiwa kushinda michezo yake miwili dhidi ya wapinzani wake Team Kiza huku Bingwa Mtetezi Mchenga BBall Stars wakibanwa mbavu na Portland katika mchezo uliofanyika mwishoni mwa wiki.

  Flying Dribblers ambao waliishia hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya mwaka uliopita, wameshinda mechi mbili kwenye 'best of three' za nusu fainali hivyo kukata tiketi ya fainali moja kwa moja.

  Kwenye game 1 Flying Dribblers walifanikiwa kushinda pointi 84 kwa 75 za Team Kiza. Katika mechi ya leo nyota wa Flying Dribblers Baraka Mopele amefunga pointi 21 rebound 3 na Assist 1 hivyo kuipa tiketi ya fainali timu yake.

  Kwa upande wa Team Kiza mchezaji Abdul Chingwengwe amefunga pointi 23, rebound 5 na Assist 2. Flying Dribblers sasa wanasubiri mshindi wa game 3 kati ya Portland dhidi ya Mchenga Bball Stars ili kujua wanakwenda kuchuana na nani kwenye fainali.

  Timu ya Portland imefanikiwa kushinda game 2 ya nusu fainali ya michuano ya Sprite Bball Kings dhidi ya Mchenga Bball Stars hivyo kulazimisha kucheza game 3 ili kupata mshindi atakayekwenda fainali.

  Katika mchezo huo uliweza kumalizika kwa Portland kushinda pointi 71 dhidi ya 64 za Mchenga Bball Stars ambao ndio mabingwa watetezi.

  Nyota wa Portland Denis Babu ameweza kuifungia timu yake pointi 42, na kuchukua rebound 7 na Assist 2 na kuwaokoa kutoaga mashindano kwenye game 2.

  Katika mchezo huo Portland waliweza kucheza wachezaji watano kwa dakika zote 40 bila kuwa na mchezaji wa akiba na kufanikiwa kushinda mechi hiyo.

  Kwa upande wa Mchenga Bball Stars wao waliwaeza kuongozwa na nyota Baraka Isack ambaye amefunga pointi 22, rebound 3 na Assist 2, japo zimeshindwa kuisadia timu yake kwenda fainali bila kucheza game 3.

  Katika game 1 Mchenga Bball Stars walishinda kwa pointi 70 kwa 54. Portland sasa zitacheza game 3 ili kumpata mshindi atakayekwenda fainali kuwania milioni 10 akiwa bingwa au milioni 3 akiwa wa pili pamoja na milioni 2 kwa atakayekuwa MVP. 
  Mchezaji wa timu ya Portland (Jezi ya Kijani) Denis Babu akijaribu kuwatoka wachezaji wa Mchenga BBall Stars (jezi nyeupe) Cornelius na Chriss wakati wa mchezo wa nusu fainali ya pili ya Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 uliofanyika mwishoni mwa wiki hii na Portland kufanikiwa kushinda kwa pointi 71 dhidi ya 64 za Mchenga BBall Stars.
  Mchezaji wa timu ya Mchenga BBall Stars(jezi nyeupe) Baraka Isack akiambaa ambaa na mpira pembeni ya mchezaji wa Portland wakati wa mchezo wa nusu fainali ya pili ya michuano ya Sprite BBall Kings 2018 uliofanyika mwishoni mwa wiki hii na Portland kufanikiwa kushinda kwa pointi 71 dhidi ya 64 za Mchenga
  Mashabiki wakiwa wanafuatilia michuano ya Sprite BBall Kings 2018

  0 0

  Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza Dodoma katika kikao kazi alichofanya na watumishi wa shirika hilo wakiwemo wajumbe wa Bodi ya Tanesco, viongozi wa menejimenti ya TANESCO, Bodi ya EWURA na watendaji wa REA. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgallu.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini Dkt Titto Mwinuka (Kulia) akifuatilia kwa Makini Mkutano wa Kikao Kazi Ulioitishwa Mjini Dodoma na Waziri wa Nishati Dkt Kalemani na Kuhudhuriwa na watumishi wa shirika hilo wakiwemo wajumbe wa Bodi ya Tanesco, viongozi wa menejimenti ya TANESCO, Bodi ya EWURA na watendaji wa REA.
  Wajumbe wa Bodi ya Tanesco, Viongozi wa Menejimenti ya Tanesco, Bodi ya EWURA na Watendaji wa REA Wakiwa Kwenye Kikao Kazi Kilichoitishwa na Waziri wa Nishati Dkt MEDARD KALEMANI Mjini Dodoma.

  0 0

  Wakwanza kulia ni Mtoa huduma wa kutuo cha tiba ya Kinywa na Meno cha Elite Dental Clinic Bi Baby Luck akiwa na Muuguzi wa Kituo hicho Bi Rosemary Kwilasa wakitoa ushauri wa tiba ya meno kwa wafanyakazi wa Airtel kutoka vitengo mbalimbali pamoja na wadau wao. Airtel imefanya Gulio maalum la kuwakutanisha wadau na watoa huduma mbalimbali pamoja na wafanyakazi wake kupata huduma hizo BURE. Gulio hilo Gulio lililofanyika makao makuu ya Airtel.

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imeungana na wadau wengine kutoa tiba na uchunguzi wa afya ya kinywa na meno bure ikiwa ni juhudi zake za kutambua umuhimu wa Afya ya Kinywa na Macho. Uchunguzi huo  imefanyika  kwenye makao makuu ya Airtel  na kuwafaidisha wafanyakazi kutoka vitengo mbali mbali pamoja na wadau wengine waliofika kwenye ofisi za kampuni hiyo.

  Akiongea wakati wa tukio hilo Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu Airtel Bi Stella Kibacha alisema “Airtel Tanzania tunatambua watu walio kwenye ajira mbalimbali hubanwa sana na kazi na wakati mwingine kukosa muda wa kuchunguza mwenendo wa Afya zao, hii ndio imetufanya Airtel kuwaleta wadau wetu hapa ili wafanyakazi wetu pamoja na  wadau wanaotembelea jengo la Airtel kupata huduma hizi”

  Kibacha aliendelea kueleza kuwa kuwa “wote tunatambua Wizara ya Afya kupitia waziri Ummy Mwalimu imekuwa mstari wa mbele kusisitiza sana swala la kulinda Afya zetu, sisi Airtel tumeona umuhimu wake pia ndio maana watoa huduma wa Afya ya kinywa Elite  wapo, Macho wapo wadau wetu International Eye Hospital na Mazoezi tumewaita Club9 Wellness Servicess kuja hapa na  wataalam wao ili kutoa ushauri wao kwa jamii hapa ofisini kwetu kwa siku nzima wafanyakazi na wadau wakaribu wapate muda wa kufanyiwa uchunguzi wa awali na kupanga muda  wao kwenda baadae kwenye vituo vya huduma hizi na kujipatia huduma kwa ufasaha zaidi”

  kwa upande wake Dokta Latha Sujit wa Elite Dental Clinic alitoa wito kwa watanzania wote kuona umuhimu na kuwa na utaratibu wa kutembelea vituo vya afya na kufanya uchunguzi wa kinywa mara kwa mara.

  “Sisi Elite Dental Clinic tunatoa huduma ya kuchunguza na kutibu meno, lakini wito wangu  kama daktari kwa watanzania kuhusu Afya ya Kinga ya meno msisubirie mpaka usikie maumivu au tatizo litokee, nashauri familia na jamii kwa ujumla tuwe tunatenga muda na utaratibu wakwenda kwenye vituo vya Afya popote pale kwa uchunguzi na ushauri ni muhimu sana kwa Afya zetu” alieleza Dr Latha

  Gulio la Airtel mbali na kuwepo na tiba hiyo ya Kinywa  toka kwa Elite Dental Clinic na huduma za uchunguzi wa macho toka kwa International Eye Centre pia lilihudhuriwa na watoa huduma nyingine za  kijamii wakiwemo Seifi Group wanaotoa huduma za vifaa vya elimu, 1st House (kwa huduma za mikopo ya nyumba), Superdoll (kwa huduma za matairi pamoja vipuli vya vifaa vya moto), Club9 (huduma ya mazoezi na mazoezi tiba) GT Bank, pamoja na  Asas Milk.
  Dokta Latha Sujit (kushoto) wa Elite Dental Clinic akiwa na Muuguzi wa Kituo hicho wakitoa ushauri wa tiba ya meno kwa mfanyakazi wa Airtel Bw James Moilo kutoka vitengo mauzo wakati Airtel ilipofanya Gulio maalum la kuwakutanisha wadau na watoa huduma mbalimbali pamoja na wafanyakazi wake kupata huduma mbalimbali BURE. Gulio hilo lililofanyika makao makuu ya Airtel.
  Meneja Mauzo na Masoko wa Seifi Group Bi Zarina Riyas (mwenye baibui) akiwa na watoa huduma wengine wa kampuni hiyo wakitoa huduma kwa mfanyakazi wa Airtel wakati Airtel wa ilipofanya Gulio maalum la kuwakutanisha watoa huduma mbalimbali pamoja na wafanyakazi wake kupata huduma hizo BURE. Gulio hilo lililofanyika makao makuu ya Airtel.
  Dokta Latha Sujit (kushoto) wa Elite Dental Clinic akiwa na Muuguzi wa Kituo hicho wakitoa ushauri na tiba ya meno kwa mdau wa habari mtandaoni wa Michuzi media Group Bw Ahmad Michuzi wakati Airtel ilipofanya Gulio maalum la wadau na wafanyakazi wake kukutana na watoa huduma mbalimbali nakupata huduma mbalimbali BURE. Gulio hilo lilifanyika makao makuu ya Airtel.
  Meneja Masoko wa Club9 inayojiusisha na huduma ya Mazoezi tiba Bi Janeth John akiwa na watoa huduma wengine wa kampuni hiyo wakitoa huduma kwa mmoja ya mdau wa Airtel kwenye Gulio maalum la watoa huduma mbalimbali BURE. Gulio hilo lilifanyika makao makuu ya Airtel.

  0 0

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuonya mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko kwa kushindwa kuwasiliana na mdhamini wake na kutoa sababu za msingi mahakamani.

  Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ametoa onyo hilo leo Agosti 6,2018 wakati kesi ya kufanya maandamano yasiyo halali inayowakabili viongozi 9 wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe ilipokuja kwa ajili ya washtakiwa hao kusomewa maelezi ya awali.

  Kabla ya kutolewa onyo hilo, wakili wa serikali Mkuu, Faraja Nchimbi ameeleza kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya washtakiwa kusomewa PH lakini mawakili wa utetezi hawakufika mahakamani.Wakikli Hekima Masipo alidai mahakamani hapo kuwa Wakili wa washtakiwa Peter Kibatala yupo Mahakama kuu huku Jeremiah Mtobesya akiwa katika kesi nyingine Mtwara.

  Hata hivyo, mahakama ilimtaka mshtakiwa wa 5, Esther Matiko ambaye hakufika mahakamani hapo tarehe iliyopita na shahidi wake akaeleza kuwa alipatwa n dharura, basi aelezee hiyo dharula yake.Matiko amedai kuwa alipigiwa simu ya dharura kwenda shuleni anaposoma mwanaye Agosti 1, 2018 na akaondoka saa 4 usiku. Ambapo baada ya kufika shule aliambiwa mtoto wake ni mgonjwa na alipompeleka hospital alikutwa na Tetekuwanga na akaambiwa apumzike kwa siku 4.

  Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mashauri alimuhoji Matiko kuwa mbona mdhamini wake alishindwa kuieleza mahakama kwamba amekwenda Kenya kufanya nini."Nakupa warning mara nyingine uwe muwazi, hii iwe mara ya mwisho, siku nyingine unapaswa kumueleza mdhamini wako ni dharura gani imekupata," Hakimu Mashauri.

  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 13.2018 kwa ajili ya washtakiwa kuja kusomewa PH.

  Mbali na Mbowe, washitakiwa wengine ni Katibu mkuu wa CHADEMA, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Iringa Mjini Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya.

  Miongoni mwa mashitaka yanayomkabili washitakiwa hao ni kula njama kwa nia ya kutenda kosa, kufanya mkusanyiko usio halali, kufanya mkusanyiko wenye ghasia na kukiuka tamko la kutawanyika na kuendeleza mkusanyiko wenye ghasia.Washitakiwa hao wanadaiwa kati ya Februari mosi na 16, mwaka huu, Dar es Salaam kwa pamoja na ujumla wao walikula njama ya kutenda makosa ya kufanya mkusanyiko usihalali, mkusanyiko wenye ghasia na kukiuka tamko la kutawanyika.

  Mbowe na wenzake pia wanadaiwa Februari 16, mwaka huu, katika viwanja vya Buibui na barabara ya Mwananyamala na Kawawa, Kinondoni, wakiwa wamekusanyika kwa nia ya kutekeleza azma ya pamoja ya kuandamana hivyo kuwatia hofu wananchi kwamba kutakuwa na uvunjifu wa amani. 

  Pia wanadaiwa wakiwa na wenzao 12 ambao hawapo mahakamani siku hiyo waliandamana isivyo halali wakiwa na lengo la kuvamia ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni na kutokana na mkusanyiko huo wa ghasia walisababisha kifo cha Akwilina Akwiline na majeraha kwa askari H. 7856PC Fikiri na E6976 CPL Rahim Msangi.
  Baadhi ya viongozi wa CHADEMA wakiwa kwenye moja ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo kusikiliza kesi  yao


  0 0

   WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee wa Watoto Ummy Mwalimu katika akitata utepe kuashiria uzinduzi na makabidhiano ya majengo ya chuo cha Uuguzi Tanga yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella na Mkuu wa Chuo hicho Leah Makala
   WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee wa Watoto Ummy Mwalimu katika akitata utepe kuashiria uzinduzi na makabidhiano ya majengo ya chuo cha Uuguzi Tanga yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella na Mkuu wa Chuo hicho Leah Makala
   WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee wa Watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa uzinduzi na makabidhiano ya majengo ya chuo cha Uuguzi Tanga yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) 
   KAIMU Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt Otilia Gowelle akizungumza katika uzinduzi huo kulia ni Mkuu wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga Tanga Leah Makala 
  Mwakilishi wa Mfuko wa Dunia ambaye ni Mratibu wa Mfuko wa Dunia,Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt Hiltruda Temba akizungumza katika uzinduzi huo.
   MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza katika uzinduzi huo.
   Mkuu wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga Tanga Leah Makala akizungumza katika uzinduzi huo
   WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee wa Watoto Ummy Mwalimu akilakiwa na KAIMU Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt Otilia Gowelle mara baada ya kuwasilia chuoni hapo 
  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee wa Watoto Ummy Mwalimu kushoto akiteta jambo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt Otilia Gowelle mara baada ya uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella anayefuatia mwenye miwani ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi
   WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee wa Watoto Ummy Mwalimu katikati akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Chuo hicho kulia 
   Mkuu wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga Tanga Leah Makala akimueleza jambo Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia
   Katikati ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiangalia namna wanafunzi wanavyojifunza kwa vitendo kumfanyia mazoezi mtoto ambaye amezaliwa akiwa hapumui vizuri 
  Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi huo


  WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema wizara yake itaendelea kukarabati na kupanua vyuo vya mafunzo ya afya kada ya kati nchini ili kuweza kuongeza udahili kwa wanafunzi wanaofaulu kwenye masomo ya sekondari wenye vigezo vya kuingia kwenye vyuo hivyo. 

  Aliyasemma hayo leo wakati halfa ya uzinduzi na makabidhiano ya Majengo ya chuo cha Uuguzi Tanga yaliyojengwa kupitia ufadhili wa mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) alisema kwani ukarabati huo utasaidia kuongeza idadi kubwa ya wanafunzi watakaokuwa wakipata fursa ya kusoma kwenye vyuo hivyo. 

  Alisema kutokana na ukarabati huo kwenye chuo cha Uuguzi mkoani Tanga idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa kwenye chuo hicho imeongezeka kutoka wanafunzi kutoka 190 hadi 260 ambao wameweza kupata fursa mafunzo kwenye chuo hicho ambao watasaidia kwenye kada hiyo muhimu kwa ustawi wa maendeleo. 

  “Kutokana na ukarabati wa majengo haya nimeambiwa na Mkuu wa Chuo kwamba udahili wa wanafunzi kutoka 190 hadi 260 wameweza kutoa fursa kwa vijana wao kuweza kupata nafasi ya kupata mafunzo ya afya kada ya kati huwa naambiwa kwamba na dkt Guwele ambaye ni mkuu wa idara ya mafunzo na afya kada ya kati anasema wanafunzi wengi wanafaulu lakini hawapati mahali pa kuwapeleka sababu kubwa zikiwa ni miundombinu na uchakavu wa majengo na inaumiza vijana wamefaulu vizuri sana lakini hakuna nafasi“Alisema. 

  “Lakini tunawashukuru Global Fund kwa ujenzi wa majengo hayo yameweza kusaidia kuongeza udahili hivyo niagize msije mkaacha wanafunzi kwa kusema hakuna nafasi..Wanafunzi waliofaulu kwenye masomo ya sekondari wenye vigezo vya kuingia kwenye vyuo vya mafunzo wachukuliwe wote wasiachwe majumbani “Alisema. 

  wanafunzi wengi wanafaulu lakini hawana mahali pa kuwapeleka kutokana na miundombinu na uchakavu wa majengo na miundombinu na inaumizsa unakuta vijana wamefaulu vizuri sana lakini hakuna nafasi tunawashukuru global fund wameweza kuongeza udahili,msije mkaacha wanafunzi kwa kusema hakuna nafasi,wanafunzi waliofaulu kwenye masomo ya sekondari wanaovigezo vya kuingia kwenye vyuo vya mafunzo wachjukuliwe wote wasiachwe nyumbani. 

  Hata hivyo alimuagiza Mkurugenzi ashiriane na Baraza la Mitihani nchini (Nacte) ili wanafunzi wote waliofaulu kwenye masomo yao ya sekondari wenye vigezo vya kuingia kwenye vyuo vya mafunzo wachukuliwe wasiachwe nyumbani maana watu wamepambana sana wamesoma sana. 

  Naye kwa upande wake,Mwakilishi wa Mfuko wa Dunia ambaye ni Mratibu wa Mfuko wa Dunia,Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt Hiltruda Temba alisema kwa ushirikianao kati ya mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI,Kifua Kikuu na Malaria kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulianza mwaka 2003. 

  Alisema hadi kufikia June 2018 mfuko huo umeipatia serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia serikali kuu na Asasi zisizo za kiserikali zaidi ya dola za kimarekani Bilioni 1.9 ambazo ni sawaa na wastani wa fedha za kitanzania sh.trilioni 3.8 na Tanzania ni miongoni mwa nchi tano za kwanza zinazopokea kiasi kikubwa cha fedha katika kusaidia kupambana na magonjwa ya ukimwi,kifua kikuu na malaria pamoja na kuboresha mifumo ya utoaji wa huduma za afya kutoka katika miradi inayofadhiliwa na mfuko wa dunia.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na balozi wa Canada nchini aliyemaliza muda wake Mhe. Ian Myles walipokutana Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na balozi wa Ubelgiji nchini aliyemaliza muda wake Mhe. Paul Cartier walipokutana Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa China Mhe. Wang Ke walipokutana kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Balozi wa Burundi nchini Mhe. Gervais Abayeho aliyemsindikiza Mjumbe maalumu wa Rais wa Burundi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Ezechiel Nibigira Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na mjumbe maalumu wa Rais wa Burundi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Ezechiel Nibigira Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2018.


  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Makungu katika mkutano wa hadhara uliohusu miradi ya maendeleo ukiwemo wa ujenzi wa kituo cha afya kitakacho gharimu sh.milioni 500 zilizotolewa na serikali uliofanyika wilayani Ikungi mkoani Singida jana.
   Wananchi wakifuatilia mkutano huo.
   Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Iyumbu, Mohamed Itambu Athumani, akizungumza katika mkutano huo.
   Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi, Mheshimiwa Tweve, akizungumza kwenye mkutano huo.
   Ofisa Mtendaji wa Kata ya Iyumbu, Tatu Bolosi, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Makungu.
   Diwani wa Kata ya Iyumbu, Peter Gwiligwa, akizungumza.
   Wananchi wa Kijiji cha Makungu, wakishoona mikono kukubali kushiriki shughuli za miradi ya maendeleo.
   Hapa ni furaha tupu wakati wakimsikiliza mbunge wao katika mkutano huo.
   Nyimbo za hamasa zikiimbwa kwenye mkutano huo.
   Mkutano ukiendelea.
   Mhandisi wa Maji, akizungumza na wananchi wa kijiji hicho kuhusu kupatikana kwa maji katika eneo hilo.
   Msanii Omari Kiherehere kutoka Mjini Singida akitoa burudani ya ushairi.
  Baadhi ya viongozi wa Kijiji cha Makungu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano huo.

  Na Dotto Mwaibale, Singida

  SERIKALI imetoa sh.milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya chenye hadhi ya kimataifa kitakachojengwa Kijiji cha  Makungu Kata ya Iyumbu Wilayani Ikungi Mkoa wa Singida.

  Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu, wakati akiwahutubia wananchi wa kata hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana.

  "Ndugu zangu licha ya wiki iliyopita kunipokea kwa mabango yaliyokuwa yakielezea changamoto mbalimbali mlizonazo leo nimewaletea habari njema kwani kupitia jitihada zangu binafsi Serikali imeweza kusikia kilio chenu ambapo imetoa sh.milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya katika Kijiji chenu cha  Makungu" alisema Kingu huku wananchi wakilipuka kwa shangwe.

  Kingu aliwaambia wananchi wa kata hiyo kuwa amerudi kwa mara ya pili katika kijiji hicho ili kuzungumzia utatuzi wa changamoto kadhaa walizozitoa wananchi hao kupitia mabango yao ambazo zilikuwa ni shule, maji, barabara, umeme pamoja na kuwekewa mnara wa simu ambapo tayari alikuwa ameenda na majibu yake.

  "Nimekuja na majibu ya changamoto zetu kwani mungu amesikia kilio chenu kuhusu changamoto ya maji leo hapa nimekuja na Mhandisi wa maji ambaye atawaelezeni nini kifanyike ili mpate maji, na kuhusu shule licha ya kutoa saruji ambayo mmeifungia .ndani bila kuifanyia kazi tangu mwaka 2016 nitawapa mifuko mingine 100 ili muendelee na ujenzi wakati Usambaji wa Umeme Vijiji wa REA awamu ya tatu ukisubiriwa baada ya kuhakikishiwa na wahusika ambapo utawekwa katika kata mbili ikiwemo hii ya kwenu katika mwaka huu wa fedha wa 2018/2019" alisema Kingu.

  Akizungumzia miradi hiyo itakayo jengwa kwenye kata hiyo Kingu alisema kituo cha afya kitakaho jengwa katika kata hiyo kitakuwa na wodi kwa ajili ya wajawazito, chumba cha upasuaji, maabara, jengo maalumu la kuchomea takataka pamoja na nyumba ya daktari ambapo kuhusu mnara wa simu tayari ameitwa  jijini Dodoma na waziri husika kuona namna atakavyosaidiwa kuweka mnara huo haraka iwezekanavyo.

  Kingu aliwataka wananchi hao kuunga mkono jitihada za serikali kwa kujitoa kimichango na nguvu kazi ili kukamilisha miradi hiyo ambapo wote kwa umoja wao walimuhakikishia ushiriki wao kwa kunyoosha mikono huku akimtaka Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, Tatu Bolosi kuanza kuandaa eneo kitakapo jengwa kituo hicho ili ujenzi huo uanze mara moja baada ya fedha hizo kuingizwa benki mapema mwezi ujao. 


  0 0

  Na.khadija seif ,Globu ya jamii.

  Katika kuunga mkono juhudi za Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John pombe Magufuli kukuza sekta ya viwanda Taasisi ya ki_uanachama ya African Forestry (AF) ikishirikiana na Taasisi ya Uendelezaji Misitu Tanzania (FDT) ya Mkoani Iringa wameanzisha jukwaa la kuwasaidia wawekezaji wa sekta ya kilimo cha miti nchini Tanzania,na kuwapatia taarifa na elimu ya kilimo cha miti kwa njia ya mtandao ili kuongeza chachu ya uwekezaji katika sekta ya misitu.

  Aidha akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya ki_uanachama ya African Forestry (AF) Francis Rwebegora amesema Misitu hiyo ina manufaa kwa jamii kwani misitu inafaida kwani baadhi ya mazao ya misitu ni pamoja na mbao zinazotumika katika sekta ya ujenzi ,viwanda vya kutengeneza samani,magogo yanayotumika katika viwanda vya karatasi ,nguzo za umeme na simu .

  Rwebegora amefafanua zaidi faida nyingine za misitu ni pamoja na udhibiti wa ongezeko la joto kwani miti hutumia hewa_ukaa,kusanisi chakula chake, utunzaji wa vyanzo vya maji ,na faida nyingine nyingi za ki_ikolojia.

  Mratibu wa biashara na masoko Taasisi ya Uendelezaji misitu nchini(FDT) Emmanuel sangalah amesema wakulima watapata mafunzo stahiki kuhusu kilimo cha miti kuanzia kuandaa shamba ,upatikanaji wa mbegu bora, utunzaji wa shamba,masoko,bei na ushauri wa kitaalam kea kuongeza pato la Taifa.

  Ameeleza hatua jinsi ya kujiunga na huduma hiyo kupitia simu ya kiganjani nakutembelea tovuti ya www.mitibiashara na hakuna malipo yoyote ya kujiunga na jukwaa hilo na kutoa wito kwa wakulima kujiunga ili waweze kunufaika na mazao bora.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya African Forestry (AF) Francis Rwebegora akizungumzaa na wanahabari jijini Dar es salaam leo katika ufunguzi wa   huduma ya Mitibiashara kimtandao kwa ajili ya wakulima kupata elimu jinsi ya kuandaa mashamba yao.

  0 0


  0 0


  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha watanzania kuwa kwa kushirikiana na wataalam kutoka nchini Marekani (Madaktari Afrika) “electro physiologist” (EP) tunatarajia kufanya kambi maalum ya magonjwa ya moyo yatokanayo na mfumo wa umeme wa moyo usiofanya kazi sawasawa. Matibabu yatakayotolewa katika kambi hiyo inatarajia kuanza tarehe 11 hadi 18 Agosti 2018 ni pamoja na kuwawekea wagonjwa Pacemakers, ICDs, CRT-Ds na CRT-Ps kutokana na ugonjwa utakaogundulika.

  Taasisi inawaomba madaktari wote wa Hospitali za Rufaa nchini kuwaleta wagonjwa wenye matatizo yafuatayo kwa ajili ya matibabu:

  Atrioventicular block

  Chronic bifascicular and tri fascicular block

  Sinus node dysfunction

  Complete Heart block

  Tachyarrhythmias

  Third degree block

  Heart Failure with severe LV dysfunction (LBBB) >130m/s

  Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Dkt. Peter Kisenge kwa namba 0713 236 502 na +255 22 2151379 ambaye atawaelekeza utaratibu wa kuwatuma wagonjwa hao.


  Imetolewa na:

  Kitengo cha Uhusiano
  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
  06/08/2018

  0 0

  MKURUGENZI mkuu wa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) William Erio amewataka watumishi wa shirika hilo kufanya kazi kwa bidii na kufikia lengo la kukusanya Shilingi Trilion 1.5 na kwamba hatovumilia wazembe.

  Erio aliyasema hayo jana katika mkutano wake na Wakurugenzi na Mameneja wa shirika hilo kwenye ukumbi wa NSSF Ilala Dar es Salaam.

  "Mwaka jana mlipaswa kukusanya shilingi Trillion 1 lakini mlikusanya shilingi billion 700 pekee hivyo hamkufikia lengo." Mwaka huu katika mpango kazi ulioidhinishwa na Waziri mnapaswa kukusanya shilingi Trilioni 1.5 target hii lazima hifikiwe."alisema Erio 

  Alisema fedha hizo zitapatikana kupitia uandikishwaji wa wanachama wapya, makusanya ya fealisema. wanachama wa zamani pamoja na fedha za pango za majengo ya shirika hilo."Hakuna haja ya kuwa na wanachama lukuki ambao hawalipi michango yao, ni lazima wafuatiliwe kwa karibu kuhakikisha michango inalipwa kwa wakati.

  " Najua pia tuna majengo yetu ambayo yapo wazi hayana wapangaji, nimeshaongea na SSRA wanampango wa kufungua ofisi mikoa yote 26 ya Tanzania bara, wapange kwenye majengo yetu." alisema.Hata hivyo, Erio alisema kuwa hatomvumilia mfanyakazi mzembe ambae hatofikia malengo waliyojiwekea."Mkuu wa idara ambae hatofikia performance tuliyojiwekea sitomvumilia, naomba target tuliyoiweka ifikiwe, isipofikiwa maana yake kazi zmewashinda na Mimi sitokuvumilia." alisisitiza.

  Erio alisema kuwa jukumu la kusajili wanachama wote ni la wafanyakazi wote na si idara moja pekee." Mwaka huu tunatakiwa kuandikisha wanachama wapya 417,000, NSSF inawafanyakazi 1,000 kila mfanyakazi akileta wanachama 10 kwa mwezi lazima watalipa michango na tutafikia lengo.

  Akisisitiza hilo alisema malengo ya shirika yalifikiwa kwenye vikao halali vya wafanyakazi na muktasari ya yatokanavyo kwenye vikao hivyo upo, hivyo ni jukumu la kila mfanyakazi kutekeleza jukumu lake ili kufikia lengo la shirika ambalo ni kujiimarisha na kukua zaidi.

  Hata hivyo kwa sasa anaendelea kusoma ripoti mbali mbali za utekelezaji alizokabidhiwa na mtangulizi wake pamoja na wakurugenzi wa kanda na kisha atafanya ziara ya kutembelea kila kitengo ili kubaini changamoto zilizopo miongoni mwa wafanyakazi na kuangalia namna ya kuziondoa.

  Erio ambae awali alikuwa mkurugenzi wa PPF aliteuliwa Julai 14 mwaka huu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF akichukua nafasi ya Godius Kahyarara.
  Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) William Erio akizungumza na  Wakurugenzi na Mameneja wa shirika hilo kwenye ukumbi wa NSSF Ilala  jijini Dar es Salaam jana huku akiwataka watumishi wa shirika hilo kufanya kazi kwa bidii na kufikia lengo la kukusanya Shilingi Trilion 1.5 
   Baadhi ya Wakurugenzi na Mameneja wa shirika la NSSF  wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) William Erio ,alipozungumza nao jana kwenye ukumbi wa NSSF Ilala  jijini Dar es Salaam kuhusiana mikakati mipya ya kuimarisha zaidi mfuko huo,ambapo Watumishi wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kufikia lengo la kukusanya Shilingi Trilion 1.5 . 
   Sehemu ya Viongozi wakuu wa NSSF wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu William Erio ,alipozungumza nao jana kwenye ukumbi wa NSSF Ilala  jijini Dar es Salaam kuhusiana mikakati mipya ya kuimarisha zaidi mfuko huo,ambapo Watumishi wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kufikia lengo la kukusanya Shilingi Trilion 1.5 . 

  0 0

  Na Editha Karlo,Blobu ya Jamii Kagera.

  MKUU wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewataka wanakagera kumpa ushirikiano katika majukumu yake mapya ya kikazi aliyoanza ili kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na watangulizi wake.

  Gaguti ameyasema hayo leo kwenye ukumbi wa halmashauri ya Bukoba baada ya kukabidhiwa ofisi na Mkuu wa Mkoa mstaafu Meja Jenerali Salum Kijuu na kumuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu.

  Alisema nafasi yake ni kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na watangulizi wake kwa wanakagera ili kuhakikisha Mkoa wa Kagera unasonga mbele."Ni wajibu wangu kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na watangulizi wangu na nina imani kubwa tutashirikiana na viongozi wenzangu na nitatoa ushirikiano wakati wowote nipo tayari"alisema Mkuu huyo wa Kagera

  Gaguti alisema Mkoa wa Kagera ni Mkoa ambao upo mpakani na unapakana na nchi karibia tatu hivyo aliwataka wananchi wa Mkoa huo kutumia fursa hiyo kuuza mazao ili kuufanya Mkoa kuwa wa viwanda na wenye neema.

  Mkuu wa Wilaya ya Kywerwa Rashid Mwaimu baada ya kuapishwa alisema kuwa atakwenda kusimamia mapato katika Wilaya yake na kuhakikisha yanaongezeka ili shuhuri za maendeleo ndani ya Wilaya hiyo zifanyike vizuri.

  "Najua nina majukumu makubwa na kazi yangu ni kutatua matatizo ya wananchi ili Wilaya yetu iweze kufanya vizuri katika sekta za miundombinu,afya na Elimu"alisema.
  Mkuu wa Mkoa mstaafu wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu akimkabidhi nyaraka za ofisi mkuu wa Mkoa mpya wa Kagera Brigedia Jenerali Maico Gaguti kwenye ofisi za halmashauri ya Bukoba

  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Maico Gaguti akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu katika ukumbi wa halmashauri ya Bukoba.

  Baadhi ya viongozi wa chama ,Serikali na kamati ya Ulinzi Mkoa wa Kagera wakishuhudia makabidhiano ya ofisi kwa Mkuu wa Mkoa na kuapishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu .

  0 0

  Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng'i  Issa katikati akisaini nyaraka ya makubaliano ya mkataba wa kufanya kazi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP pamoja na Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF),  kushoto ni Mkuu wa Idara ya maarifa na Ubunifu ESRF,Bi. Margareth Nzuki na kulia ni Mwakilishi  wa Mkuu wa Idara ya Uchumi UDSM Dkt. Kenneth Mdadila.
   Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi (NEEC),Beng'i  Issa,akibadilishana nyaraka na Mkuu wa Idara ya maarifa na Ubunifu Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Margareth Nzuki (kushoto) baada ya kusaini mkataba wa kufanya kazi kati ya baraza hilo pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).
  Katibu mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Beng'i  Issa,akibadilishana nyaraka  na Mwakilishi wa Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dkt. Kenneth Mdadila, (kulia) baada ya kusain Mkataba wa kufanya kazi za tafiti kati ya baraza hilo pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) pamoja na chuo hicho .(Picha na Mpiga Picha Wetu, Dar es Salaam).

  Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
  Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limeingia makubaliano na taasisi ya umoja wa mataifa la maendeleo UNDP pamoja na Chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM) na Taasisis ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii  (ESRF) kufanya tafiti mbalimbali zitakazo wezesha halmashauri za wilaya na mikoa kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwenye maeneo yao.

  Makubaliano hayo yamesainiwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Bi.Beng’i Issa pamoja na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu  ESRF, Bi. Margareth Nzuki na Mwakilishi wa Mkuu wa Idara ya Uchumi UDSM,Dkt. Kenneth Mdadila ambapo taasisi hizo kwa pamoja na UNDP watashirikiana kufanya tafiti hizo.

  Bi. Issa alisema tafiti hizo zitasaidia halmashauri kutambua vipaumbele vyao katika  uzalishaji, kuandaa mpango mkakati utakaowezesha kutafuta fedha kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo hususani kwa vijana.“ 

  Kwa pamoja tumeamua kufanya hivi ili kuleta matokeo chanya ya tafiti na kusaidia jamii hususani katika  halmashauri zetu,” kazi za tafiti ni za kitaalam na tunataka zisaidie na hiyo ni njia muhimu katika kuunga mkono serikali ya awamu ya tano inayojenga uchumi wa viwanda, alisema Bi. Issa.

  Pia alisema matokeo ya tafiti hizo pia yatasaidia baraza hilo kupata taarifa ambazo zitatumika kwenye utekelezaji wa mradi maalum wa miaka mitatu unaoratibiwa na baraza hilo kwa kushirikiana na umoja wa mataifa ambao utaanza mapema mwakani.

  Alisema kazi hizo zinatarajiwa kukamilika kabla ya Desemba 2018 kwa kuwa nia ya ushirikiano huo ni kupata taarifa zitakazo tumika kuandaa andiko kubwa la mradi unaotakiwa kutekelezwa kwa miaka mitatu ijayo kati ya UNDP na baraza kuanzia Januari 2019.

  Alisisistiza kuwa tafiti hizo zitatoa taarifa ambazo zitawezesha kushughulikia zaidi uwezeshaji wananchi kiuchumi kulingana na makundi yanayolegwa.

  Naye Mratibu wa mradi kutoka taasisi za kiuchumi na kijamii Magreth Nzuki, alisema utafiti huo utakapo kamilika  Utaleta mageuzi katika teknolojia ya kilimo kwa kuzalisha malighafi zitakazo hitajika kwenye viwanda.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack amemuapisha Jasinta Venant Mboneko kuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga leo Jumatatu Agosti 6,2018.


  Na Kadama Malunde – Malunde1 blog
  Hafla fupi ya kuapishwa kwa mkuu huyo mpya wa wilaya ya Shinyanga imefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali,vyama vya siasa,taasisi na wadau mbalimbali.
  Akizungumza baada kula kiapo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mheshimiwa Jasinta Venant Mboneko alisema amekuja wilayani humo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na kusimamia Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

  “Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuniamini kuwa na mimi kuwatumikia wananchi wa Shinyanga,nipo tayari kuwatumikia wananchi na nitaendelea kuisimamia ilani ya uchaguzi ya CCM na kuhakikisha tunaifanya wilaya ya Shinyanga kuwa salama”,alisema Mboneko.
  “Nimekuja Shinyanga kufanya kazina tumeelekezwa kuwatumikia wananchi,kazi hii sitaifanya peke yangu,wapo watu wataniwezesha ikiwemo kamati ya ulinzi na usalama lakini pia viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ,viongozi wa dini pamoja na wananchi,naomba mwenyezi Mungu anisaidie sana na aniwezeshe”,aliongeza.

  Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack alimtaka mkuu huyo wa wilaya na viongozi wengine kufanyia kazi malalamiko ya wananchi na kuepuka urafiki katika kazi.

  “Mwananchi akilalamika msikilize,hakikisha unafanyia kazi kila jambo linalokuja mbele yako,Shinyanga iko salama,naomba tushirikiane kufanya kazi”,alisema Telack.

  “Najua utapata watu wengi wa kukukaribisha,kuwa makini na watu wanaokukaribisha,hizi kazi zetu hazina urafiki,nikumbushe tu kwamba mishahara mnayopewa na serikali inatosha msikubali kupewa rushwa”,aliongeza.
  Kulia ni Jasinta Venant Mboneko akila kiapo kuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga leo Jumatatu Agosti 6,2018 - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Jasinta Venant Mboneko akila kiapo kuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akisaini hati ya kiapo
  Kushoto Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akishikana mkono na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Venant Mboneko baada ya kumkabidhi katiba ya nchi,ilani ya CCM na kanuni ya maadili ya utumishi wa umma.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Venant Mboneko akiwa na wazazi wake
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Venant Mboneko akizungumza baada ya kula kiapo
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Venant Mboneko akiomba ushirikiano kutoka kwa viongozi na wananchi wilayani Shinyanga
  Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Venant Mboneko 
  Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akizungumza ukumbini
  Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha,akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Venant Mboneko,Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba wakiwa ukumbini
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza baada kumuapisha Jasinta Mboneko kuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga
  Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga Bakari Mohamed Kasinyo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi (kushoto) wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea ukumbini
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza ukumbini
  Askofu David Mabushi akitoa neno ukumbini
  Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Charles Sangura akitoa neno
  Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha akizungumza ukumbini
  Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba akizungumza ukumbini
  Picha ya pamoja mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack,Katibu tawala mkoa,wakuu wa wilaya za Kahama,Shinyanga na Kishapu
  Picha ya pamoja mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack,Katibu tawala mkoa,wakuu wa wilaya na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Shinyanga
  Picha ya pamoja mkuu wa mkoa,katibu tawala mkoa,wakuu wa wilaya na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Shinyanga
  Picha ya pamoja mkuu wa mkoa,katibu tawala mkoa,wakuu wa wilaya na wazazi wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko
  Picha ya pamoja mkuu wa mkoa,katibu tawala mkoa,wakuu wa wilaya na kamati ya ulinzi na familia ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko
  Picha ya pamoja mkuu wa mkoa,katibu tawala mkoa,wakuu wa wilaya na kamati ya ulinzi na viongozi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini
  Picha ya pamoja mkuu wa mkoa, katibu tawala mkoa,wakuu wa wilaya na kamati ya ulinzi na viongozi wa dini
  Picha ya pamoja mkuu wa mkoa,katibu tawala mkoa,wakuu wa wilaya na sekretarieti ya mkoa wa Shinyanga
  Picha ya pamoja mkuu wa mkoa,katibu tawala mkoa,wakuu wa wilaya na viongozi wa taasisi mbalimbali
  Picha ya pamoja mkuu wa mkoa,katibu tawala mkoa,wakuu wa wilaya na viongozi wa taasisi mbalimbali
  Picha ya pamoja mkuu wa mkoa,katibu tawala mkoa,wakuu wa wilaya na waandishi wa habari
  Picha ya pamoja mkuu wa mkoa,katibu tawala mkoa,wakuu wa wilaya na waandishi wa habari
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Venant Mboneko akiteta jambo na ndugu yake

  ANGALIA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI UKUMBINI

  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

  Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani, (wapili kushoto), Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya, (kulia), na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kamel Group, wamiliki wa Kamel Industrial Estate, Bw.Gagan Gupta, wakitembelea eneo la EPZA la Kamel Industrial Estate huko Bagamoyo Mkoani Pwani Agosti 6, 2018.  WAZIRI wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, na mwekezaji wa Kampuni ya Kamel Group, Bw. Gagan Gupta, wamelipongeza Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), kwa kuharakisha uwekaji umeme mkubwa kwenye eneo la EPZA Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
  Pongezi hizo zimetolewa Agosti 6, 2018 wakati Mhe. Dkt. Kalemani alipofika kwenye eneo hilo la uwekezaji viwanda (Kamel Industrial Estate), lililoko kandokando ya Barabara ya Bagamoyo Wilayani humo.
  “Niipongeze TANESCO kwa sababu imechukua muda mfupi sana tangu ulipolalamika, takriban miezi miwili kazi ya kufikisha umeme hapa imekamilika, na ilikuwa ni kazi kubwa, umeme wa kiwanda hiki ulikuwa una –share na watumiaji wengine wengi, 33kV uki-share na watu wa Bagamoyo, watu wa Tegeta, kwa mtu wa kiwanda usingekutosha.” Alisema.
  Alisema TANESCO baada ya kupokea malalamiko hayo kazi ya kuongeza kiasi cha umeme kwenye kiwanda hicho ilianza kwa kufunga mitambo hapo hapo kiwandani, ambapo umeme ulivutwa kutoka unapoanzia Mkoa wa Pwani kuelekea Bagamoyo.
  “Tumeamua kukuwekea laini yako peke yako, kutoka pale Mkoa wa Pwani unapoanzia na kuleta umeme hapa, na kisha tumeuingiza kwenye transfoma yako, tumeingiza 33kV kwa ajili yako yenye uwezo wa kutumia Megawati 22, ingawa umetuambia mahitaji yako ni Megawati 20, sisi tumekuletea ziada ya Megawati 2 hivyo ni matumaini yetu sasa kero itapungua na uzalishaji utaongeza.”
  Alisema ni matumaini ya Serikali kuwa kiwanda kitazalisha zaidi ya Mitungu 500 iliyokuwa ikizalisha kwa siku kwani hivi sasa umeme upo wa kutosha.
  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Bw. Gagan Gupta alisema, amefurahi sana kupelekewa umeme wa kutosha moja kwa moja kwenye kiwanda chake na kwamba ameahidi kuwa uzalishaji mkubwa utafanyika ndani ya kipindi kifupi kijacho.
  “Kwangu mimi leo ni siku ya kihistoria, Mhe. Waziri uko hapa ninakuahidi katika nia hii ya serikali ya kuweka uchumi wa viwanda, ninachoweza kusema, ongezeko la Megawati 20 moja kwa moja hapa kiwandani, ndani ya mwaka mmoja utakuta mabadiliko makubwa hapa.” Alitoa hakikisho Bw. Gupta.  Mhe. Waziri akimsikiliza Bw. Gupta kuhusu mipango ya uwekezaji viwanda kwenye eneo hilo
  Mhe. Waziri akimsikiliza Bw. Gupta kuhusu mipango ya uwekezaji viwanda kwenye eneo hilo
  Mhandisi Mahende Mgaya, (Kulia), akimpatia maelezo Mhe. Dkt. Kalemani kwenye eneo ambalo TANESCO imetengeneza laini pekee ya kuelekea moja kwa moja eneo la EPZA la Kamel Industrial Estate.
  Dkt. Kalemani akizungumza na Bw. Gupta alipowasili kwenye eneo hilo.
  Mhe. Dkt. Kalemani, akimpongeza Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi Mahende Mgaya. Kulia ni Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Madulu

  0 0


   MKUU wa wilaya ya Bahi Mwanahamisi Mkunda akitoa shukrani kwa  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mhandisi Charles Francis Kabeho kushoto mara baada ya uzinduzi wa Jengo la Tanesco wilaya ya Bahi
   MKUU wa wilaya ya Bahi Mwanahamisi Mkunda kulia akiwa na   KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mhandisi Charles Francis Kabeho kushoto mara baada ya uzinduzi wa Jengo la Tanesco wilaya ya Bahi

  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mhandisi Charles Francis Kabeho amefungua Jengo la Ofisi za Shirika la Umeme nchini (Tanesco) wilayani Bahi mkoani Dodoma ikiwa ni mpango wao wa kusogeza huduma karibu na wananchi waliopo maeneo mbalimbali hapa nchini.

  Akizungumza mara baada ya kufungua Jengo hilo Mhandisi Kabeho amepongeza juhudi zinazofanywa na shirika hilo katika kuhakikisha ofisi zao zipo kwenye mazingira mazuri ya wafanyakazi kuweza kuwahudumia wananchi kwa ufanisi wakati wanapokuwa wakifika kwenye maeneo yao kupata huduma

  Alisema hatua ya wao kupanua wigo mpana wa kuwafikia wananchi itawawezesha kuondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kuzifuata kwa umbali mrefu hivyo jambo hilo linahitaji kupongezwa kutokana na kuona umuhimu wa kuwafikia

  “Nimependezwa na jitihada za TANESCO katika kuhakikisha wateja wanafiki wa na huduma za Umeme kwa ukaribu zaidi, nakuhudumiwa katika mazingira mazuri, hivyo niwapongeze TANESCO kwa hili lakini pia nisistize kuwa ofisi hizi ziweze kuhudumia wateja hao kwa weledi”alisemaMhandisi Kabeho

  Naye Mkuuwa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Mkunda amemshukuru Mkuuwa Mbioza Mwenge kwa kuweza kufungua jingo hilo na kuwa hakikishia wananchi wa Bahi kuwa Huduma ya umeme sasa ipo karibu na kuwa wilaya ya Bahi sasa inauhakika wakupata hudumaza Umeme masaa 24,

  Kwa upande wake Meneja wa TANESCO wilaya ya Bahi, Mhandisi Bryceson Kitila amesema kuwaUjenzi wa jengo la Ofisi ya Bahi umetekelezwa naShirika la Umeme Tanzania kwa madhumuni ya kuongeza Ufanisi wakazi katika mji wa Bahi na vijiji vya Jirani,pia kuwezesha wananchi wa Bahi kupata Huduma Bora nayaUhakika kwa kuwa na kituo cha huduma kwa wateja(one stop shop center) hivyo mteja anaweza kupata huduma zote katika dawati moja ikiwemo na manunuzi ya umeme (LUKU).

  Mbio hizi za Mwenge wa Uhuru, zimehitimishwa katika mkoawa Dodoma ambapo zimehusishau funguaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo Jengo la TANESCO.

  0 0

  Na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii

  NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amefungua rasmi maonesho ya Nane Nane Kanda ya kati ambayo yanaenda sawa na mashindano ya Nane ya Mifugo kitaifa yanayofanyika jijini Dodoma.

  Ulega amefungua mashindano ya Mifugo ambayo yalianza mwaka 2011 na huwa yanafanyika Agosti 5  ya kila mwaka mkoani Dodoma na hujumuisha ng'ombe wa maziwa na nyama walioboreshwa pamoja na Mbuzi wa asili.Akizungumza jana Ulega amesema kuwa lengo kuu la mashindano hayo ni kutambua umuhimu na mchango wa rasmilimali za mifugo ya asili katika kuendeleza sekta ya mifugo nchini.

  Aidha amesema kuwa mchakato huo linalenga kutambua juhudi na maarifa wanayotumia wafugaji wa mifugo ili kufuga kwa tija na hatimaye kuvutia wafugaji wengi na kuiga na kuingia kwenye ufugaji wenye tija kwa taifa.Ulega amesisitaza kuwa sekta ya mifugo ni moja ya Sekta muhimu zinazochangia kupunguza umaskini wa wananchi na kukuza uchumi wa nchi kwani ni mhimili katika kuendeleza viwanda kama ilivyoainishwa katika mpango kabambe wa Mifugo Tanzania.

  Hata hivyo ametoa maagizo kwa wafugaji na wadau mbalimbali kuunda na kuimarisha vikundi na vyama vya ushiriki ili kuongeza kasi ya uwekezaji katika viwanda vya kusindika mazao ya mifugo na hatimaye kufikia malengo na kauli mbiu ya Nane Nane 2018 isomekayo ''WEKEZA''.Aidha Ulega ameagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha utekelezaji wa mfumo wa utoaji kinga mbalimbali za magonjwa ya mifugo uwe ni lazima kwa wafugaji wote nchi.

  Pia Ulega amesema wafugaji pamoja na wafanyabiasha  hawaruhusiwi kuhamisha au kusafirisha mifugo pamoja  mazao kutoka sehemu moja hadi nyingine bila kibali.Hivyo imesababisha maeneo ya mipakani mwa nchi yetu imeshamiri biashara haramu za mifugo na mazao yake zisizo rasmi na amewataka watendaji kusimamia sheria kwa kushirikiana na wadau ili kutatua changamoto ya utoroshaji wa rasilimali za mifugo yetu na mazao yake.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa mkoa wa mkoa Dodoma wakati wa kufungua rasmi maonesho Nane Nane kanda ya kati na mashindano ya nane ya Mifungo kitaifa yanayo fanyika katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia viatu katika banda la Magereza vinavyotegene na ngozi katika maonesho ya Nane Nane Nane katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

  Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa ameambatana na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge wakitembelea banda la wajasiria mali katika maonesho ya Nane Nane yanayo fanyika katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
  Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia samaki aina ya kamongo alikaushwa katika banda la wajasiria mali katika maonesho ya Nane Nane yanayo fanyika katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)


  Wafugaji mbalimbali wakionesha mifungo yao katika mashindano ya nane ya mifungo yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma

  Wafugaji mbalimbali wakionesha mifungo yao katika mashindano ya nane ya mifungo yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)

older | 1 | .... | 1639 | 1640 | (Page 1641) | 1642 | 1643 | .... | 1897 | newer