Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1641 | 1642 | (Page 1643) | 1644 | 1645 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Matokeo mazuri ya kila jambo yanahitaji maandalizi timamu na ndivyo tunavyofanya kuelekea msimu mpya wa ligi daraja la kwanza.

  Wakati maandalizi yakiwa yamenoga jana tumetangaza tarehe rasmi ya utambulisho wa timu kwa wakazi wa Temeke na mkoa wa Dar es salaam kwa ujumla.

  Mtendaji mkuu wa klabu Abubakar Jafo amewaambia wanahabari kwamba kuanzia leo ni wiki ya REHA FC ambapo kilele chake itakua siku ya jumapili kwenye uwanja wa Bandari Tandika. 

  "Wiki ya Reha itahusisha shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kufungua matawi yetu na kuhitimishwa kwa michezo maalum itakayohusisha timu nne  ambazo ni Mtibwa, KMC na Transit Camp  na wenyeji Reha fc" amesema Jafo.

  Jafo amesema michezo hiyo itaanza jumamosi kwa mchezo wa mapema saa 8 mchana kati ya Reha dhidi ya Transit Camp na saa 10 jioni Mtibwa itacheza na KMC kisha washindi watacheza fainal siku ya jumapili jioni huku waliofungwa wakicheza mchana. "Siku hiyo tutaitumia kuwatambulisha wachezaji wetu pamoja na benchi la ufundi".

  Mtendaji Mkuu wa timu ya Reha Fc Abubakar Jafo

  0 0


  0 0

   WAZIRI KALEMANI AWASIMAMISHA KAZI WATENDAJI TANESCO KWA KUSHINDWA KUWASHA UMEME VIJIJINI

  Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

  WAZIRI wa Nishati Dkt.Medard Kalemani amefanya ziara katika Wilaya ya Mkuranga katika kukagua utekelezaji wa utoaji wa huduma ya umeme kwa wananchi na hakuridhishwa na utendaji wa baadhi ya wahusika katika idara hizo na kuamua kuwaweka kando ili wenye kasi watekeleze jukumu hilo.

  Katika Ziara hiyo Kalemani  amemuagiza meneja Tanesco  mkoa wa Pwani kumsimamisha kazi  Mhandisi wa Mkoa na  pia amemuagiza meneja wa wilaya ya Mkuranga Mhandisi, Regina Mvungi kumsimamisha mhandisi mwenye dhamana hiyo katika wilaya ya Mkuranga kwa kushindwa kufanya kazi ya kuwasha umeme kwenye vijiji vilivyo kwenye mradi kata ya Vikundi.

  Aidha Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ametoa siku 14 Wilayani Mkuranga katika  kuhakikisha umeme unawaka katika vijiji vyote vilivyokatika mpango huo.Waziri hiyo aliyasema hayo Leo hii wakati wa ziara ya kutembelea wilayani Mkuranga ili kuona namna ya upatikanaji wa huduma ya Nishati ya Umeme katika Kata ya Kisiju,Vikindu na Tambani.

  Kalemani amesema kuwa mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya pili haikufanya vizuri katika Tarafa ya Kisiju hivyo natoa siku 14 kuanzia kesho kuhakikisha umeme unawaka, aidha Kalemani ametoa  maagizo  kwa viongozi wa Tanesco katika ngazi ya Mkoa na Wilaya kuhakikisha umeme huo unawaka kwa wakati.

  Naye Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh Abdallah Ulega amesema  wananchi katika vijiji ambavyo vilitakiwa kupata umeme walikata minazi na miembe yao ili kupisha miundo mbinu ya umeme lakini ni zaidi ya miaka mitano tangu miundombinu ya umeme iwekwe na hakuna umeme.

  Aidha Ulega amemshukuru Waziri Kalemani kwa ziara yake jimboni hapo kwani anaamini italeta mabadiliko na amewataka watendaji waliopewa maagizo na Waziri wayafanyie kazi mara moja.
  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (alienyosha mkono) akizungumza na wanachi wa kata ya Kisiju wilaya ya Mkuranga  ambapo amewaagiza  watendaji wa Tanesco siku  14  wahakikishe umeme umewaka (Picha Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
  Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na Mbunge wa jimbo la mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa  kijiji cha Kisiju ambapo amemshukuru Waziri Kalemani kwa ziara yake jimboni.
   Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani(katikati)kwa kushiriki na viogizo mbalimbali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa umeme katika kijiji cha Mkokozi Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
   Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Mkuranga Mhadisi, Mshamu Munde (kushoto) akisalimiana na wanachi Mkuranga mkoa wa Pwani.
   Wananchi wa Wilaya ya Mkuranga  wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani.  0 0

  WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kulia akimkabidhi madawati 40 Diwani wa Kata ya Chumbageni (CC) Saida Gadafi kwa ajili ya shule ya Sekondari Chumbageni ili kuweza kukabiliana na upungufu uliopo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chumbageni Gabriel Habash 
  AWAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kulia akiwa amekaa kwenye mmoja ya madawati 40 aliyoyakabidhi leo kwa shule ya Sekondari Chumbageni kushoto ni Diwani wa Kata ya Chumbageni (CC) Saida Gadafi ambaye alimuomba Waziri huyo madawati hayoi kwa ajili ya shule ya Sekondari Chumbageni ili kuweza kukabiliana na upungufu uliopo 
  WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya Sekondari Chumbageni mara baada ya kuwakabidhi madawati hayo 
  WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chumbageni Gabriel Habash na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa 
  Diwani wa Kata ya Chumbageni (CC) Saida Gadafi akizungumza katika halfa hiyo ambapo alimshukuru Waziri Ummy kwa kuwapa msaada huo 
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chumbageni Gabriel Habash akizungumza katika halfa hiyo ambapo alimshukuru Waziri Ummy kwa kuisaidia shule hiyo 
  Mwalimu Mkuu wa wa shule ya Sekondari Chumbageni Kavumo Juma Mziray akitoa hotuba yake 
  WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) katika akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chumbageni Gabriel Habash wakiimba wimbo wa Taifa
   WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akisalimiana na walimu wa shule ya Sekondari Chumbageni mara baada ya kuwasili shuleni hapo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chumbageni Gabriel Habash 
   Sehemu ya wanafunzi wa shule hiyo wakifutiliana makabidhiano hayo
   Sehemu ya madawati na viti ambayo yamekabidhiwa leo na Waziri Ummy kwa shule ya Sekondari Chumbageni
  WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na waalimu wa shule ya Sekondari Chumbageni mara baada ya kukabidhi madawati hayo leo
  WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) leo amekabidhia madawati 40 na viti katika shule ya sekondari ya Chumbageni Jijini Tanga ikiwa ni mpango wake wa kuhakikisha changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu zinapatiwa ufumbuzi. 

  Halfa hiyo ya makabidhiano ilifanyika leo shuleni hapo na kuhudhuriwa na walimu, wanafunzi na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ,Diwani wa Kata ya Chumbageni Saida Gadafi wakiwemo viongozi wengine. Hatua ya kukabidhiwa madawati hayo shule ya Sekondari ya Chumnageni ilitokana na ombi la Diwani wa Kata ya Chumbageni Saida Gadafi ambaye alimueleza waziri Ummy uwepo wa uhaba wa madawati kwenye shule hiyo. 

  Akizungumza namna alivyoweza kuipatia ufumbuzi changamoto hiyo, Waziri Ummy alisema baada ya ombi hilo aliwapata wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao walilikubali na kumpatia kiasi cha sh, milioni 5.4 ambazo wameweza kununua madawati 40 na viti “Mh Saida umetenda wajibu wako ipasavyo maana taarifa ya mkuu wa shule inasema kuna uhaba wa viti 163ubawa wa meza 100 hivyo kupatina kwa hivyo vilivyokabidhiwa leo kumepunguza nusu lakini nitaendelea kushirikiana nanyi “Alisema 

  “Kazi nzuri inafanywa kwenye shule ya sekondari Chumbageni na nimeambiwa kiwango cha ufaulu kinaongezeka mwaka hadi mwaka asilimia 51 hadi asilimia 77 lakini pia nitoe pongeze kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga kutatua changamoto ya elimu sio watu kusubiri mpaka serikali kuu kwani wamekuwa wakijiongeza na diwani Saida kutatua changamoto ya elimu kwenye kata yake “Alisema. 

  Hata hivyo alisema ataendelea kushirikiana na madiwani kuhangaika ili aweze kupata fedha za ujenzi wa ofisi ya walimu kwen ye shule hiyo lakini pia wanafunzi nitawaletea vitabu huku akitoa wito kwa wananchi kushirikiana kuona namna ya kutatua changamoto ya elimu sio kusubiri serikali pekee bali ni watu wote. 

  “Nimshukuru Rais kuanzisha sera ya elimu bure ambayo imewasaidia, watu wengi ...watu walikuwa wanaponda shule za kata wakati mimi nilipokuwa nasoma shule zikuwa chache kutokana na kukosekana nafasi lakini leo hii zipo za kutosha hivyo kuwasaidia watoto wa kike kuepushwa na ndoa za utotoni na wavulana kuvuta bangi. 

  Alisema leo hii Serikali chini ya Rais Dkt John Magufuli imekuwa ilileta milioni 161 kila mwezi kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa ajili ya elimu bure hii imesaidia sana lakini wengine walikuwa wanakosa kwa sababu ya ada lakini tatizo la ada limetatuliwa . 

  Alisema ndio maana kabla ya Serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani wanafunzi waliokuwa wanaanza kidato cha kwanza Jiji la Tanga walikuwa 4120 lakini leo watoto 6300 kwa sababu ya elimu bure wameweza kupatiwa elimu hivyo hao watoto wangekuwa nyumbani, elimu ndio nyenzo ya kuwaletea maendeleo

  Naye kwa upande wake Diwani wa kata ya Chumbageni Saida Gadafi alimshukuru Waziri Ummy kwa kuwasaidia msaada huo wa madawati ambao ulikuwa ni changamoto kubwa kwa wananchi kwenye shule hiyo na nimuhaidi tutayasimamia vizuri ili yaweze kutumika kwenye malengo yaliyokusudiwa kwa matumizi ya wanafunzi 

  "Nikushukuru sana Mh Waziri kwa kunisaidia suala hili ambalo ni muhimu sana niwaombe ndugu zangu wanafunzi tumuombee mungu waziri amjalie kilalaheri na mafanikio kwenye shughuli zake za kila siku "Alisema

  Awali aklizungumza kwenye halfa hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chumbageni Gabriel Habash alimshukuru sana waziri huku akieleza namna wakazi wa mji huo wanavyohitaji kushirikiana naye kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.

  "Nikushukuru sana Mh Waziri kwatatulia changamoto ya elimu kwenye shule yetu kwani msaad huu ni mkubwa na ninahaidi kushirikiana nawe katika kila jambo sisi tupo tayari "Alisema

  0 0


  0 0


  0 0

   Meneja Mahusiano wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Bi. Noves Moses  akimkabidhi msaada wa magodoro na mashuka Mbunge wa Jimbo la Ileje Mkoani Songwe Janeth Mbene (wapili kushoto) wenye thamani ya shilingi milioni 3.3 kwa  ajili ya Shule ya Sekondari Mlale kama sehemu ya kupunguza changamoto zinazoikabili shule hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo Bi. Furaha Mhagama.
  Meneja Mahusiano wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Bi. Noves Moses  akimkabidhi msaada wa magodoro na mashuka Mbunge wa Jimbo la Ileje Mkoani Songwe Janeth Mbene (wapili kushoto) wenye thamani ya shilingi milioni 3.3 kwa  ajili ya Shule ya Sekondari Mlale kama sehemu ya kupunguza changamoto zinazoikabili shule hiyo. Kushoto ni mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo aliyeshuhudia mmsaada huo kwao.
   Mbunge wa Jimbo la Ileje Mkoani Songwe Janeth Mbene akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) na wanafunzi  ya Sekondari ya Mlale mara baada ya kupokea msaada wa magodoro na mashuka yenye thamani ya Milioni 3.3 kutoka benki ya TPB.

  0 0

  *Awaambia zama zimebadilika …hii ni Awamu ya Tano

  MWENYEKITI wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini John Shibuda amewashauri viongozi wa vyama vya siasa kuwa makini na matumizi ya lugha wanayotumia pindi wanapotaka kumshauri Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano Dk.John Magufuli.

  Wakati huo huo amewahakikishia kuwa Rais Magufuli hawezi kuufuta mfumo wa vyama vingi bali kilichopo anaviimarisha na kwamba ipo siku atazungumzia hilo kwa kina.Shibuda ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati viongozi wa vyama vya siasa nchini vilipokutana kwa lengo la kujadili mabadiliko ya kikatiba na kisheria kuhusu uchaguzi kabla ya Uchaguzi kuu wa mwaka 2020.

  Katika mkutano huo ambao umeandaliwa na Jukwa la Katiba Tanzania (Jukata),Shibuda amesema ni vema wanasiasa wakawa makini katika matumizi ya lugha hasa kwa kuzingatia zama zimebadilika.Amesema lugha ambazo walikuwa wanazitumia katika awamu zilizopita lazima wanasiasa wajue zama hizi hazina nafasi na hivyo kushauri wachague lugha ya kusema wanapotaka kushauri au kuzingumza jambo kwa Rais.

  “Kikubwa lazima tutambue kila kabila na utamaduni wake.Lugha ambazo unaweza kuzitumia kumwambia Mzaramo au Mkwere anaweza kucheka lakini lugha hiyo hiyo ukiitumia kwa Mkurya atakukata panga.“Lugha ambazo unataka kumwambia Rais wa Serikali ya Awamu Tano lazima ziwe na staha kwani kinyume na hapo anaweza kukupa jibu ambalo litakukwaza.Tukubali kuwa mila na desturi zinatofautina sana,”amesema Shibuda.

  Akifafanua katika hilo Shibuda ametoa mifano kuwa hata unapotaka kwenda kuoa ukienda kutoa posa Bukoba watakwambia nenda na mkungu wa ndizi, ukienda Tanga watakwambia nenda na kuku wa kitoweo na ukienda Usukumani utaambiwa uswage Ng’ombe.“Vivyo hivyo hata unapotaka kumshauri Rais lazima uzingatie mila na desturi.Nimeona hili niwaambie kwani kuna changamoto ya matumizi ya lugha miongoni mwetu,”amesema Shibuda.

  Kuhusu hofu ya kufutwa vyama vingi ambayo wanasiasa wengi wameionesha kwenye mkutano huo,Shibuda amewahakikishia kuwa Rais hawezi kuvifuta wala kudhoofisha demokrasia bali ataimarisha.Amesema kuna mambo mengi yanayoendelea ndani ya vyama vya siasa na kwamba wanaendelea na mazungumzo na mwisho watakapomaliza wataeleza umma kupitia vyombo vya habari.

  Wakati huo huo wanasiasa wa vyama vya siasa nchini wameonesha kukerwa na tabia ya wanasiasa wanaohama vyama kila kukicha na kusababisha gharama kubwa za kurudia uchaguzi.Wanasiasa hao wamejadili eneo hilo kwa kina na kufikia muafaka iko haja ya kuwa na mjadala wa kitaifa kujadili masuala mbalimbali yanayohusu vyama vya siasa pamoja na chaguzi mbalimbali.

  Awali Katibu Mkuu wa Jukwaa la Katiba Tanzania(Jukata) Deus Kibamba amesema alitoa pendekezo linalosema iwe ruksa kuhama chama cha siasa bila kupoteza nafasi ya kuchaguliwa na bila kuhitajika uchaguzi mpya.

  Kibamba amesema kutokana na wimbi la wabunge na madiwani kuhama vyama kwasababu mbalimbali na malalamiko ya Watanzania kuhusu gharama kubwa zinatumika katika chaguzi ndogo kutokana na wanasiasa kuhama vyama.

  “Na kwa kuwa Taifa linaingia katika kipindi cha uchaguzi muda si mrefu ujao.Jukata tumetafakari na kuona ipo haja ya kuruhusu mfumo wa wanasiasa kuhama vyama pasipo kupoteza nafasi zao za kuchaguliwa.Hii italiokolea taifa fedha nyingi kiasi cha kuendeleza nchi yetu kiuchumi na maendeleo,”amesema Kibamba.
  Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini John Shibuda akizungumza katika mkutano wa ulioandaliwa na Jukwaa la katiba Tanzania (JUKATA) kwa lengo la kujadili mabadiliko ya kikatiba na kisheria kuhusu uchaguzi kabla ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ,mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es salaam
  Mjumbe wa Kamati kuu ya CHADEMA Profesa Mwesiga Baregu akitoa mchango wake katika mkutano uliolenga kujadili mabadiliko ya kikatiba na kisheria kuhusu uchaguzi kabla ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

  Katibu Mkuu wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw. Deus Kibamba akifafanua jambo katika mkutano huo.
  Mwenyekiti wa Chama cha CCK Bw. Renatus Mhabi akichangia hoja katika majadiliano hayo.
  Bw. Msafiri Mtemelwa kutoka Chama cha ACT Wazalendo akizungumza kwa uchungu wakati akichangia hoja.
  John Mnyika Naibu Katibu Mkuu Bara chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA akichangia hoja katika mkutano huo.
  Mjumbe wa kamati Kuu Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Profesa Mwesiga Baregu pamoja na wajumbe wangine wa mkutano huo wakifuatilia majadiliano hayo.

  0 0


  NA. GSENGOtV

  Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku, Kushindwa kuzuia mkojo, yaani ukichelewa kidogo unaweza kukutoka bila breki, Maumivu wakati wa kukojoa, Kuishiwa nguvu za kiume, Kupungua kwa uwingi wa mbegu (low sperm count), Maumivu wakati unafika kileleni, Damu kutokea kwenye mkojo au kwenye mbegu za kiume, Maumivu nyuma ya mgongo au hata nyonga nk basi uonapo dalili hizo unaweza kuanza kuhisi una saratani ya tezi dume.

  Kupitia dalili hizo ni wazi kwamba afya ya mgonjwa itakuwa matatani kwenye mataabiko.Wahenga walironga mficha maradhi kifo humuumbua. Kila kiungo cha mwanadamu kikipata tatizo ni jukumu la matabibu kufanya uchunguzi na kutoa huduma kwa eneo lililodhurika, Haiingii akilini kwamba uendelee kuteseka ile hali tiba ipo. Nao wataalamu wanasema uchunguzi wa kutumia kidole hauhitaji gharama kubwa kama ilivyo njia nyingine za kutumia vifaa maalum vya uchunguzi.

  Ni tamaduni tu za watu wenye mawazo machafu ndizo zinazo wafanya wengi kudhani kipimo cha kidole ni udhalilishaji, lakini madaktari waliosomea fani hiyo wanasema kuwa ni njia ya kawaida sana.Kwa kuliona hilo Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza imezindua hudumu za kliniki za muda wa jioni kwa siku za wikiendi na sikukuu, lengo likiwa ni kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za Afya kwa wananchi wote ambao watahitaji huduma za kibingwa muda wote.

  Hasa wale ambao hawawezi kufika hospitali kutokana na kubanwa na kazi. Fuatilia kile kilichojiri katika uzinduzi ikiwa ni pamoja na mashuhuda wanaume wa Tezi dume.
  Huduma za uchukuaji vipimo zikiendelea katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza 
  Licha ya kuwa na idadi kubwa ya wahitaji wa kupima afya, idadi ya madaktari wahudumu wa afya iliendana na kasi. 
  Huduma rafiki. 
  Hakuna jambo lililojema kama kuijua afya yako. 
  Meza na meza vitengo kwa vitengo katika Uzinduzi wa Huduma za Kliniki za Jioni za Bure Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza. 
  Bibi akipata vipimo. 
  Jeh urefu wako unalingana na uzito wa mwili wako? 
  Jeh urefu wako uanalingana na uzito wa mwili wako? 
  Afya muhimu. 

  0 0

    Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Anselim Peter, (kulia), akimkabidhi kifunika tairi ya spea (wheel cover), Bibi Lilian Kinyemu, kutoka kampuni ya ABC Limited ya Wilayani Maswa, baada ya kutembelea banda la Mfuko na kupatiwa maelezo huhusu shughuli za Mfuko kwenye kilele cha Wiki ya Nanenane kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu Agosti 7, 2018. Maonesho hayo yanatarajiwa kufungwa leo Agosti 8, 2018 na Rais Mstaafu, Mhe. Benjamin Mkapa kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

  NA MWANDISHI WETU, SIMIYU
  MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeendelea kuwafikia wadau wake wengi katika mikoa mbalimbali Tanzania Bara, hii ni baada ya kushiriki katika maonesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) yanayofikia tamati leo terehe 08.08.2018.
  Maonessho hayo yalianza tarehe 01 katika viwanja vya Nyakabindi Vilivyopo Wilaya ya Bariada Mkoani Simiyu. Maonesho haya kwa mwaka huu yameratibiwa na Serikali ya Mkoa wa Simiyu chini ya usimamizi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Antony Mtaka akishirikiana na Mikoa Jirani ya Shinyanga na Mara.
  Pamoja na mambo mengine wadau wote pamoja na wageni waliotembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wamepata elimu kuhusu;
  1.   Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi
  2.   Majukumu ya Mfuko
  3.   Mafao yanayotolewa na Mfuko
  4.   Usajili wa Waajiri
  5.   Uwasilishaji wa Michango kwa Njia ya Kielektroniki
  6.   Taratibu za Uwasilishaji wa Madai
  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Sebera Fulgence amewasisitiza waajiri wote wakiwemo waliotemeblea banda la Mfuko kutembelea Tovuti ya Mfuko (www.wcf.go.tz) na kufungua Online Service au (Huduma za Kimtandao) ili waweze kujionea huduma mbalimbali wanazoweza kupata bila ya wao kutembelea ofisi za Mfuko. Miongoni mwa huduma hizo ni kujisajili, kuwasilisha michango ambapo wanapata stakabadhi moja kwa moja, waajiri kuona michango wa wafanyakazi wake na kadhalika.
  Maonesho hayo yanahitimishwa leo tarehe 08.08.2018. Aidha wawakirishi wa Mfuko wataendelea kuwepo maeneo ya viwanja vya Nyakabindi mpaka tarehe 12 ili wale ambao hawakupata firsa ya kufika toka tarehe moja waweze nao kufika ili wapate elimu kuhusu Mfuko huu.
   Bw. Anselim Peter, (wapili kulia), ambaye ni Mkurugenzi wa Uendeshaji, WCF, Bw. Sebera Fulgence (wapili kushoto), ambaye ni Afisa mwandamizi wa Uhusiano na Mawasilkiano wa Mfuko huo, wakiwa katika picha ya pamoja na wananchi hawa waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya Wakulima Nanenane viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu Agosti 7, 2018.
   Afisa Mwandamizi wa Uhusiano na Mawasilkiano wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi WCF, Bw. Sebera Fulfence, (kulia), akimkabidhi vipeperushi vyenye taarifa mbalimbali za Mfuko, kwa mama huyu aliyetembelea banda la WCF 
   Mwananchi akisaini kitabu cha waliotembelea banda la WCF
  Wananchi wakihudumiwa kwenye banda la WCF.

  0 0

  Na Editha Karlo,Kagera

  MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Kagera umewahamasisha wakulima kupitia vyama vya ushirika na masoko kujiunga na mpango wa ushirika afya (AMCOS)katika maonesho ya nane nane Mkoani humu yalifonyika katika viwanja vya Kakyailabwa (AMCOS)Kujiunga na mpango wa ushirika afya viwanja Kyakailabwa.

  Akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Maico Gaguti Meneja wa Mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo alisema kuwa ushirika afya ni mpango maalum wa Bima ya afya kwa wakulima ambapo mpango huo utawawezesha wakulima kuchangia mara moja gharama za matibabu na kuwa na uhakika wa matibabu kwa mwaka mzima pale wanapougua.

  Odhiambo alisema watakaojiunga na mpango huu watapata matibabu kwenye vituo vya tiba vilivyosajiliwa na mfuko nchi nzima ikiwa ni pamoja na huduma za kibingwa na vipimo.

  Katika viwanja vya kyakailabwa kwenye maonyesho ya sikukuu ya nane nane banda la NHIF lilisheheni huduma mbali mbali ikiwa ni pamoja na upimaji afya bila malipo kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza, usajili wa Ushirika Afya,Toto Afya na Bima kwa wajasiliamali ambapo muitikio wa wananchi kujitokeza kupima afya zao ni mkubwa

  Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Generali Marco Gaguti alitembelea banda la NHIF na kushiriki katika upimaji wa Afya pia alihaidi kuhamasisha wakulima kujiunga na mpango huo kwaninutawasaidia wakulima kuwa na uhakika wa matibabu pale wanapougua wao na familia zao.
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Maico Gaguti akipima afya kwenye banda la mfuko wa bima ya afya(NHIF)kwenye viwanja vya Kyakailabwa wakati wa sherehe za nane nane.
  Meneja wa Bima ya afya Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Maico Gaguti juu ya mpango wa ushirika afya kwa wakulima
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Maico Gaguti akipata maelezo kutoka kwa mtumishi wa mfuko wa bima ya afya katika banda la NHIF baada ya kutembelea kwenye nane nane viwanja vya Kyakailabwa


  0 0

  Na Woinde Shizza Globu ya jamii ,Arusha

  Wataalamu wa manunuzi ya Umma nchini wametakiwa kuzingatia weredi katika utendaji wao wa kazi na kuepukana na vitendo vya ubadhirifu ,rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma, jambo litakalosaidia kudhibiti matumizi mabaya ya fedha na kusaidia fedha hizo kutumika katika maendeleo mapana zaidi ya Taifa.

  Akizungumza kwa niaba ya Rais Dkt John Magufuli,wakati alipokuwa akifungua mkutano wa siku tatu wa wataalamu na wabobezi wa manunuzi ya umma(IPPC) kutoka nchi 46 Duniani unaofanyika jijini Arusha,nchini Tanzania,Waziri wa fedha na mipango Dkt Mpango amesema mkutano huo unalenga kujadiliana namna ya kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma kupitia taknolojia mpya ya manunuzi .

  ‘’Ununuzi wa umma ndio sehemu kubwa ambapo fedha za bajeti zinapita, hivyo ukifanyika vibaya maana yake serikali inapata hasara ndio maana tunasisitiza weredi wa wataalamu wa manunuzi kwa sababu kuna mamunuzi hewa na miradi hewa ’amesema dkt Mpango

  Aidha amesema asilimia 70 ya fedha za matumizi ya kawaida zinapitia ununuzi wa umma na asilimia 100 ya bajeti ya fedha zote za maendeleo zinapitia manunuzi ya umma ,hivyo bajeti zote katika maeneo hayo mawili zikitumika vibaya lazima serikali iumie.

  Amesema wataalamu wa manunuzi ya Umma wakitumia vizuri taaluma yao itasaidia maeneo mengine ya sera katika kukuza viwanda na kuinua sekta binafsi hivyo ununuzi utumike vizuri ili kusaidia kuinua nchi za afrika ikiwemo Tanzania kuendana na teknolojia iliyopo.

  Awali Mwenyekiti wa bodi ya manunuzi ya umma nchini,dkt Hellen Bandiho amesema taasisi yao imeanza kuchukua hatua kwa wataalamu wake wasiozingatia weredi na maadili katika kazi zao na kuwataka waajiri kuhakikisha wanachukua wataalamu wa manunuzi ya umma wenye usajiri wa bodi yao.

  ‘’Wataalamu wa manunuzi ya umma wasio na usajiri ambalo wameajiriwa ama kufanya kazi zao bila usajiri ni makosa kwao na kwa mwajiri aliyewaajiri na hatua kali zitachukuliwa’’Amesema dkt Bandiho

  Alivitaka vyombo vya dola kama polisi,takukuru na mahakama kushirikiana katika kuwaibuka na kuwachukulia hatua watu hao ambao wamekuwa wakiipaka matope bodi hiyo kwa kuendesha shughuli zako kinyume cha sheria.

  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango akisalimiana na mwenyekiti wa bodi ya manunuzi Dkt. Hellen Bandiho wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wabobezi na wanunuzi wa umma jana ,uliofanyika katika ukumbi wa simba uliopo ndani ya jengo la mikutano la AICC .


  Dkt Mpango akifungua mkutano wa siku tatu unaohusu bodi ya manunuzi, jana jijini Arusha 
  Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ndani ya mkutao huo   waziri Dkt Mpangao akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa taasisi zilizopo chini ya taasisi ya wizara ya fedha na mipango(picha zote na Woinde Shizza,Glob ya jamii Arusha

  0 0

  Na.Vero Ignatus Arusha. 

  Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu) Jenista Mhagama amewataka Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya kaskazini kuhakikisha wanatatua migogoro ya ardhi ya wakulima na wafugaji ili waondokane na tatizo hilo na kujikita kwenye maendeleo. 

  Waziri Mhagama ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya 25 ya maonyesho ya kilimo na mifugo nane nane kanda ya kaskazini jijini Arusha.
  Amewataka viongozi hao kutatua migogoro hiyo ili kukuza sekta hizo kwani lengo la serikali ni kuhakikisha matumizi bora ya ardhi yanafanikishwa ili kuongeza tija za kiuchumi. 

  Mhe. Jenista amesema kuwa migogoro ya ardhi ya wakulima na wafugaji inachangia kuzorotesha ustawi wa jamii kutokana na migogoro hiyo hivyo viongozi hao wahakikishe wanakomesha tatizo hilo. "Sekta hizo zinatakiwa kuungwa mkono na kuachana na migogoro hiyo ya muda mrefu ambayo haina tija kwa jamii zaidi ya kusababisha mtafaruku na uvunjifu wa amani," alisema. 

  Alisema pamoja na kuyafunga maonyesho hayo rasmi yenye kauli mbiu ya wekeza katika kilimo, mifugo na uvuvi kwa maendeleo ya viwanda, lakini yataendelea kwa siku mbili zaidi Agosti .Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kilimo na mifugo ndiyo sekta zinazoshikilia uchumi wa wananchi wengi kanda ya kaskazini hivyo wataendelea kuwaunga mkono wanaojishughulisha na sekta hizo. 

  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwila alisema wakulima na wafugaji wakitumia elimu waliyoipata kwenye maonyesho hayo watanufaika kiuchumi. Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti alimpongeza Waziri Mhagama kwa hotuba yake na alimuahidi kwa niaba ya Wakuu wenzake wa mikoa kufanyia kazi ushauri uliotolewa. 

  "Pamoja na hayo tunakupongeza mno kwani huku kwetu masaini wakishasema mama anachapa kazi hatuna la zaidi la kuongoza zaidi ya kukubalina na hilo hongera sana kwa kuchapa kazi," alisema Mnyeti .Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu mkoani Manyara, Hudson Kamoga ambaye mkulima wa eneo lake alishika nafasi ya tatu kwenye maonyesho hayo alisema wataendelea kuwaunga mkono wafugaji na wakulima kwa lengo la kukuza sekta hizo. 

  Mkurugenzi wa Bajuta International Ltd, Gesso Bajuta ambaye kampuni yake ilipata ushindi kwenye maonyesho hayo alisema wamejipanga kuendelea kutoa huduma ya dawa za mifugo pembejeo za kilimo kwa wananchi wote.
  Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu) Jenista Mhagama, akizungumza na wananchi waliohidhuria katika maonyesho ya wakulima na sikukuu ya nanenane katika viwanja vya TASO Njiro mkoani Arusha. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu mkoani Manyara, Hudson Kamoga akipokea kwa niaba zawadi ya mkulima kutoka Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu) Jenista Mhagama, katika halmashauri hiyo aliyeshika nafasi ya tatu, kushoto kwake ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akifiatiwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo pamoja na mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti


  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimshuhudia aliyekua Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mwita Waitara, akinadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi, katika Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa, Waziri Mkuu yupo kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Wilayani hapo, Agosti 8.2018
  Aliyekua Mwenyekiti wa Kata ya Nandagala Jafari Omari (katikati), akikabidhi kadi yake ya CHADEMA kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye mkutano wa hadhara uliyofanyika katika Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa, Agosti 8.2018 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Nandagala Wilayani Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Wilayani hapo, Agosti 8.2018

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua mradi wa ujenzi wa zahanati ya Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Wilayani humo, Agosti 8.2018
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasalimia wananchi wa kata ya Nandagala wakati akiwasili katika uwanja wa zahanati ya kijiji cha Nandagala kwa jailli ya kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara, Agosti 8.2018.Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu

  ………………………..


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wabadilike na watafakari namna bora ya kuboresha maisha yao na wafanye kazi kwa bidii badala ya kukaa vijiweni na kulalamika.

  Amesema kama kuna changamoto zinawakabili katika utekelezaji wa shughuli zao, basi watumie njia sahihi ikiwemo kuwasilina na viongozi husika waliopo kwenye maeneo yao.

  Aliyasema hayo jana jioni (Jumatano, Agosti 8, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Nandagala, wilayani Ruangwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye zahanati ya kijiji cha Nandagala.Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mary Majaliwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Ruangwa, alisema vijana wanatakiwa kujitambua na kuiunga mkono Serikali kwa kufanyakazi kwa bidii.

  Kadhalika, Waziri Mkuu aliwataka vijana washirikiane kwa pamoja katika kubuni shughuli mbalimbali zitakazowaingizia kipato, jambo ambalo litawakwamua kiuchumi na kuwawezesha kujitegemea.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi hao mikakati mbalimbali inayofanywa na Serikali katika kuboresha maendeleo ya wilaya hiyo ikiwemo upatikanaji wa huduma za afya pamoja na maji safi na salama.

  PiaWaziri Mkuu aliwataka wananchi hao waendelee kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

  0 0

  Image may contain: 1 person, smiling
  Na Emmanuel J. Shilatu
  Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za Msiba wa Msanii nguli na Bingwa wa tasnia ya Sanaa za uigizaji na vichekesho, Amir Athuman almaarufu "King Majuto" kilichotokea usiku wa Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
  ...
  Kifo hiki kimenikumbuka miaka ile ya zamani alipoanza kuwika na msemo wa hamsini, hamsini mia akiwa na muigizaji mwenzake mkongwe Marehemu Mzee Small.
  Kwa wasiomjua vyema King Majuto alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini mkoani Tanga. Alianza kuigiza mwaka 1958 akiwa na umri wa miaka 9 akiigiza katika majukwaa.
  Mzee Majuto maarufu kama King Majuto ni mtunzi, muigizaji, mwandishi wa mswada. Pia Mzee Majuto ni muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC).
  Kwa sasa King Majuto ni mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki.
  King Majuto ni kipaji halisia cha kuzaliwa cha uchekeshaji kuwahi kutokea hapa nchini. Wenzake walikuwa kina Mzee Jongo, Hamis Kitambi, Fundi Said (Mzee Kipara) na Mama Haambiliki.Msiba huu ni majonzi makubwa sana kwa familia, Wasanii, Tasnia ya Filamu nchini, Wapenzi wa kazi zake za sanaa na Taifa kwa ujumla.
  Daima tutakukumbuka kwa ufundi, ustadi wa uigizaji wako, vituko vyako, tabasamu lako, upendo wako kwa kila Mtu.
  Pumzika kwa amani Mfalme na Bingwa wa vichekesho wa kipindi chote hapa nchini Mzee "King Majuto".
  Inna lillaahi wainna ilaihi raajiuun.
  *Shilatu E.J*
  0767488622

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko ametembelea mikoa ya Lindi na Mtwara kwa lengo la kufanya tathimini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa shughuli za UKIMWI zinavyotekelezwa katika mikoa hiyo.

  Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Dkt. Mboko alisema kuwa kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa matokeo ya UKIMWI ya mwaka 2016/17 unaonesha maambukizi kwa mkoa wa Lindi yapo kwa asilimia 0.3 wakati kiwango cha kitaifa ni asilimia 4.7 kwa Tanzania bara.

  Dkt. Maboko aliongeza kuwa hali hii haimaanishi kuwa kiwango cha maambikizi hakiwezi kuongezeka kwani ni wazi kabisa kuwa kuna fursa za kiuchumi ambazo zinaongezeka na kuongeza mwingiliano wa watu. 

  Alishauri kuwa kinachotakiwa ni kuongeza jitihada katika kutoa Elimu ya kujikinga na maambukizi ya VVU pamoja na elimu ya mabadiliko ya Tabia.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi alisema kuwa Mkoa wa Lindi bado unaendelea kutoa elimu kwa wananchi kwani uwezekano wa kuongezeka kwa kiwango cha maambukizi haupingiki.
  Pichani kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dr Leonard Maboko

  0 0

  Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akipongeza juhudi zilizofanywa na serikali na wadau wa kilimo katiika kufanikisha maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika kanda ya Ziwa Mashariki katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu, Jana Tarehe 8 Agosti 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
  Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika kanda ya Ziwa Mashariki katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu wakati akitoa taarifa ya maonesho ya Nanenane mbele ya Mgeni rasmi ambaye ni Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Benjamin Mkapa, Jana Tarehe 8 Agosti 2018.
  Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (Kulia) akifurahi jambo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt Bashiru Ally wakati wa kilele cha maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika kanda ya Ziwa Mashariki katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu, Jana Tarehe 8 Agosti 2018.Baadhi ya mamia ya wananchi kutoka mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga wakifatilia akwa makinbi maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika kanda ya Ziwa Mashariki katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu, Jana Tarehe 8 Agosti 2018. 

  Na Mathias Canal, WK-Simiyu


  Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba ametangaza kuwa maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima NanenaneKitaifa yatafanyika Mkoani Simiyu kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2018 mpaka 2020 ili kuongeza tija ya elimu kuhusu sekta ya kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa wananchi wa kanda ya Ziwa Mashariki.


  Waziri wa kilimo Mhe Tizeba ametanga neema hiyo kwa wananchi wa kanda ya ziwa Mashariki jana tarehe 8 Agosti 2018 kwa wakazi wa mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara ambayo inaunda kanda ya ziwa Mashariki ambao watanufaika na elimu kuhusu kilimo, mifugo na uvuvi.


  Alisema kuwa kumekuwa na utaratibu wa kufanyika mfululizo maonesho hayo kwenuye mikoa inayoandaa huku akieleza kuwa utashi uliopo katika kanda hiyo ni mkubwa ukilinganisha na maonesho ya Nanenane yaliyofanyika kwa miaka minne mfululizo katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.


  Alisema kuwa kufanyika mfululizo kwa miaka mitatu mkoani Simiyu kutawafanya wananchi kuwa na uhakika wa bidhaa za uwekezaji watakazoziweka. “Mkoa wa Simiyu na kanda yenu hii ya Magharibi ingetosha kuonyesha hata kwa miaka miwili tu lakini nimeamua kutumia utaratibu mzuri zaidi ili ifanyike kwa miaka mitatu naamini hamtaniangusha” Alikaririwa Mhe Dkt Tizeba


  Aliwataka wakuu wa mikoa ya Shinyanga Mhe Zainab Telack, Mkoa wa Mara Mhe Adam Malima na Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka kuyafanya maonesho ya Nyakabindi katika miaka miwili ijayo kuifanya sherehe hiyo ya Nanenane kuwa ya kimataifa ili kuwe na washiriki kutoka katika nchi zote nane zinazoizunguka Tanzania.


  Alisema kuwa ingependeza zaidi kuwa na washiriki wa maonesho ya teknolojia na mambo mbalimbali ya kilimo kutoka katika nchi hizo za jirani ili kubadilishana uzoefu katika kuinua sekta ya kilimo, Mifugo na Uvuvi.


  Waziri Tizeba alisema kuwa nchi ya Tanzania ndiyo kinara katikja kilimo katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati hivyo maonesho ya kilimo yanapaswa kuwa katika mpango madhubuti wa kufikia maonesho ya kimataifa.


  “Naomba niwaahidi hapa kuwa sisi kama wizara tutatoa ushirikiano mzuri ili kuhakikisha kuwa maonesho yajayo yanakuwa katika sura ya kimataifa kwani kufanya hivyo tutakuwa tumeongeza ufanisi na elimu pana kwa wakulima wetu  wa chini” Alisisitiza Mhe Dkt Tizeba


  Sambamba na hayo pia Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba alimshukuru Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Benjamin Mkapa kwa kukubali kuwa mgeni reasmi katika kilele cha maonesho ya Nanenane Kitaifa kwani amekuwa chachu na hamasa katika kuongeza ufanisi na tija kwenye sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.


  Dkt Tizeba alieleza kuwa kanda hiyo ya Ziwa Magharibi ya Nanenane ilianzishwa kwa wazo la Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka ambaye alitaka kutoa fursa ya urahisi wa hudua ya mafunzo kwa wananchi kufahamu mbinu mbalimbali za kilimo, Ufugaji na Uvuvi.

  0 0

  Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akizungumza na wananchi katika Kilele cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa Simiyu mwaka 2018, katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
  Vijana wa Skauti wakimvisha Skafu Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa mara baada ya kuwasili Bariadi katika Uwanja wa Nyakabindi kuhitimisha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018.
  Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka katika Kilele cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa ,katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
  Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akiwapungia mkono wananchi (hawapo pichani), katika Kilele cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa mwaka 2018 , katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
  Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akikagua Banda la Jeshi la Magereza wakati alipotembelea baadhi ya mabanda katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi., katika Kilele cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa mwaka 2018 Simiyu, katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
  Mtaalam wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Kilimo akitoa maelezo kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa kuhusu Teknolojia ya Ufugaji wa Samaki kupitia Vizimba.
  Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizaba akizungumza na wananchi katika Kilele cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa mwaka 2018 Simiyu ,katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
  Mkulima kutoka Wilaya ya Maswa akipokea zawadi yake ya fedha taslimu katika Kilele cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa ,katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi, kwa kuwa mkulima bora kutoka Wilayani Maswa.  ………………………


  Na Stella Kalinga, Simiyu


  Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa amesema Serikali imeondoa zuio la kuuza Mazao ya Chakula nje ya nchi ikiwa ni njia nyingine ya kuongeza soko la mazao ya wakulima hapa nchini.

  Mhe. Mkapa amesema hayo katika Kilele cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, Uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi ambapo alikuwa mgeni Rasmi akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

  “Ninachukua fursa hii kuwafahamisha kuwa Serikali imeondoa zuio la kuuza Mazao ya Chakula nje ya nchi ikiwa ni njia nyingine ya kuongeza soko la mazao ya wakulima hapa nchini, hata hivyo mazao hayo yatauzwa nje ya nchi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu”alisema.

  Aidha, amesema Serikali inawakumbusha wananchi wote kuhifadhi akiba ya kutosha ya chakula wakati wa kuuza mazao yao ili kujihakikishia usalama wa chakula katika kaya zao.Mkapa pia amesema Serikali ina mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la pamba kutoka tani 121,000 mwaka 2016/2018 hadi kufikia tani milioni moja mwaka 2020.

  Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba ametangaza rasmi kuwa Maonesho ya Nane nane Kitaifa kwa miaka mitatu mfululizo hadi mwaka 2020 yatafanyika kanda mpya Kanda ya Ziwa Mashariki katika Uwanja wa Nyakabindi Bariadi, huku akisisitiza kuwa maonesho hayo yafanyike Kimataifa kwa kushirikisha nchi jirani zinazoizunguka Tanzania.

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu utaendelea kulipa kiupaumbele zao la Pamba na mwaka ujao uzalishaji utaongezeka kutoka kilo milioni 70 hadi kufikia kilo 150.

  “Simiyu tunajivunia wananchi wachapa kazi wenye uthubutu na Simiyu inajengwa na Wanasimiyu, mwaka jana tumezalisha kilo milioni 70 za pamba, kwa mwaka huu sasa hivi msimu ukiwa umefikia katikati tuna kilo milioni 85, mwakani tunatarajia kuzalisha kilo zaidi ya 150” alisema

  Ameongeza kuwa wananchi wamelima chakula cha kuwatosheleza si watu wa kuomba chakula cha msaada huku akiupambanua Mkoa wa Simiyu kuwa ni mkoa pekee ambao watu wake wanafanya biashara saa 24.

  Maonesho ya Nanenane Mwaka 2018 yaliwashindanisha wakulima na wafugaji mmoja mmoja, Taasisi, Wakala, Mashirika ya Umma na Binafsi, Wizara pamoja na Halmashauri 21 za Mikoa ya Simiyu Mara na Shinyanga ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Maswa katika Mkoa wa Simiyu imekuwa ya tatu kati ya hizo 21.

  Kauli mbiu ya Maonesho ya Nanenane mwaka 2018 “ WEKEZA KATIKA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KWA MAENDELEO YA VIWANDA”

  0 0


  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

  Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Urafiki, Mrakibu wa Polisi (SP) Batseba Kasanga ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alimkamata Halima Mdee kwa tuhuma za kutoa lugha chafu ya matusi kwa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli akiwa nyumbani kwa wazazi wake.

  Ameeleza kuwa, walipofika nyumbani kwa wazazi wa Mdee Ubungo Kibangu, alipokelewa na mama mzazi yake zazi ambaye baada ya kujitambukisha na mahojiani mafupi aliwaeleza wamsubiri Halima anajiandaa kwa kuwa alikuwa amepumzika kidogo.

  Mrakibu Kasanga ambaye ni shahidi wa tatu wa upande wa mashtaka ameeleza hayo leo, Agosti 9,2018 wakati akitoa ushahidi dhidi ya kesi ya lugha ya matusi inayomkabili Mdee.Mdee anadaiwa, Julai 3,2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chadema,, alitamka maneno dhidi ya Rais John Magufuli kuwa “anaongea hovyohovyo , anatakiwa afungwe breki” na kwamba kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa Amani.

  Akiongozwa na wakili wa serikali Mwandamizi, Patrick Mwita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amedai Julai 4, mwaka Jana, akiwa katika kituo cha polisi cha urafiki akiendelea na majukumu yake ya kawaida alipokea oda kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kinondoni Mark Njela akimtaka kwenda nyumbani kwa wazazi wa Mdee Ubungo Kibangu kumkamata Halima Mdee kwa tuhuma za kutoa lugha ya matusi dhidi ya rais Magufuli.

  Amedai baada ya kupewa oda hiyo, walikwenda kama walivyoagiza na walipofika walipokelewa na kaka wa Halima ambaye aliwaelekeza kwa mama yao.Ameendelea kudai kuwa, mama Halima aliwapokea vizuri, akaenda kuongea na Halima na akaomba wamsubiri ajiandae kwa kuwa alikuwa amepumzika kwa kidogo.

  Shahidi Kasanga amedai, baada ya hapo Halima alitoka na wakamueleza kuwa wamekwenda kumkamata na kumpeleka Osterbay Polisi na kwamba wakati huo Halima alikuwa yupo vizuri na baadhi ya ndugu zake walitoka wakaongozana nao kwenda Osterbay polisi.

  Aidha shahidi huyo alidai kuwa yeye alikuwa hajawai kumuona Halima Mdee ana kwa ana alikuwa akimsikia katika vyombo vya habari ikiwamo TV na Magazeti.

  Aliendelea kudai kuwa, baada ya kumkamata, alimpeleka katika kituo cha polisi Osterbay, ambapo Njela hakuwepo hivyo alimpigia simu na akamuelekeza amkabidhi Mdee kwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Ilala(RCO), Davis Msangi.

  Mdee anatetewa na mawakili Peter Kibatala na Hekima Mwasipu.

  Hekima alimuuliza shahidi huyo kuwa tangu tarehe aliyomkamata Halima Mdee hadi sasa,ulishawahi kuyasikia Maneno yaliyotamkwa na Halima Mdee.

  Kasanga alijibu kuwa kwa kweli hakuwahi kuyafuatilia.

  Kesi imeahirishwa hadi Septemba 11.2018

  Mdee alifikishwa mahakamani hapo Julai 10, 2017.

  0 0


older | 1 | .... | 1641 | 1642 | (Page 1643) | 1644 | 1645 | .... | 1897 | newer