Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1635 | 1636 | (Page 1637) | 1638 | 1639 | .... | 1896 | newer

  0 0


  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

  Serikali imesema kuwa wakati ukoloni kulikuwa na utumwa ukaisha lakini sasa baadhi ya watu wanawafanya wenzao kuwa watumwa kwa kuwalaghai kigezo cha ajira.

  Hayo ameyasema Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola wakati uzinduzi mpango mkakati wa Kitaifa wa Kupinga Usafirishaji wa binadam wa mwaka 2018/2019 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

  Kangi amesema baada ya kuzindua ameitaka kamati hiyo kufatilia wafanyakazi katika mashamba na pamoja na majumbani kuhoji ajira zao na mazingira ya kufika hapo.Amesema kuwa kuna watu wanakwenda kufanya kazi nje ya nchi na baada ya kufika kazi anayoifanya sio ile ambayo alikuwa katika taarifa zake.

  Waziri huyo amemtaka Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji kabla ya kutoa hati ya kusafiria kwa mtu anaekwenda kufanya kazi ajiridhishe na kisha kutoa hati hiyo."Serikali ya awamu ya Tano ya uchumi wa Viwanda haiwezi kuacha watu wengine kuwa watumwa kwa masilahi ya watu wa wachache"amesema Lugola.Aidha amesema kuwa kamati hiyo lazima umshauri vitu katika kukomesha ushafirishaji wa binadamu.

  Nae Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Abeatus Magere amesema kuwa magari mawili yalitaifishwa ambayo yalikuwa yakitumika katika usafirishaji wa Binadam.
  Amesema mpango huo kuzinduliwa wanajipanga katika kufikia malengo yaliyokusudiwa.

  Mwakilishi wa Legal services Facilities Fund (SLF) Fortunata Kitokesya amesema kuwa wanaendelea kutoa elimu juu usafirishaji wa binadam.


  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza katika uzinduzi wa mpango Mkakati wa Kitaifa wa Kupinga Usafirishaji wa Binadamu wa Mwaka 2018/2019 katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
  Waziri wa Nchi wa Ofisi ya Makam wa Rais Zanzibar, Mohamed Abood akizungumza kuhusiana na upingaji usafirishaji wa binadam.
  Mwakilishi wa SLF, Fortunata Kitokesya akizungumza katika Uzinduzi wa mpango wa kitaifa wa kupinga usafirishaji wa binadamu.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akikata utepe kuashilia uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kupinga Ushafirishaji wa binadam wa mwaka 2018/2021

  0 0

  NAIBU Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BOT), Yamungu Kagandabila (47), ameieleza mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) ilisaini mkataba wa kukodisha ndege kabla haijapata kibali cha dhamana ya serikali.

  Pia imeelezwa, kamati ya wataalam ya Uchunguzi ya Deni la Taifa (TDMC), ilibaini ATCL iliwasilisha maombi ya dhamana kwa Waziri wa Fedha (kwa sasa Wizara ya Fedha na Mipango) kwa kukiuka taratibu za sheria za manunuzi.

  Kagandabila ambaye ni shahidi wa upande wa jamuhuri katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya bilioni 71, inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL David Mattaka na wenzake wawili amedai hayo leo Julai 30.2018 wakati akitoa ushahidi wake dhidi ya washtakiwa hao.

  Kabla ya kuanza usikilizwaji wa kesi hiyo, Mattaka na washtakiwa wenzie, vigogo kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Ofisa Mtendaji Mkuu mstaafu, Dk. Ramadhan Mlinga na Mwanasheria Bertha Soka. Walisomewa Maelezo ya awali.

  Akiongozwa na wakili wa Serikali, Vitalis Peter kutoka Takukuru mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwinzile shahidi huyo alidai ATCL iliwasilisha ombi la kutaka kupata dhamana ikiwa imeisha kiuka sheria yenyewe ya mikopo, dhamana na misaada.Amedai Januari 2008 akiwa Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera na deni la Taifa, ATCL iliwasilisha maombi ya dhamana Wizara ya Fedha kupitia Wizara ya Miundombinu.

  Alidai kuwa Januari 11, 2008 walikaa kikao cha TDMC na kubaini kwamba ATCL ilishasaini mkataba wa kukodi ndege bila dhamana ya serikali na kukiuka sheria mbali mbali ikiwemo hawakufuata sheria ya manunuzi ya umma.Pia amedai, maombi ya TTCL hayakuwa yameambatanishwa na maamuzi ya bodi ya ATCL na pia hayakuwa yameambatanishwa na business planing kuweza kusapoti ombi lao hilo.

  Amedai kuwa baada ya kubaini hayo, waliwaagiza ATCL kurekebisha kasoro na kuwataka kuonyesha idhini ya bodi kama ilikubakubaliana na ukodishwaji wa ndege hiyo na pia ATCL walitakiwa kuwasiliana na PPRA ili waweze kuonyesha njia waliyotumia kupata ndege hiyo.Hata hivyo, pamoja na yote hayo Waziri wa fedha aliidhinisha kutolewa kwa dhamana hiyo kwa ATCL pamoja na kwamba walikiuka utaratibu kwa kuingia mkataba huo.

  Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa mkataba ulisainiwa Oktoba 9, 2007 na Mattaka alisaini kwa niaba ya ATCL na Andrew Wettern kwa niaba ya Wallis Trading Inc na kuisababishia Serikali hasara.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa Chunya kwenye uwanja wa Sabasaba ikiwa ni siku ya kuhitimisha ziara yake mkoani Mbeya.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mary Mwanjwelwa mara baada ya kumalizika kwa kikao cha majumuisho ya ziara yake katika Ukumbi wa Mkapa mkoani Mbeya.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mhe. Haroon Pirmohamed katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe muda Mfupi kabla Makamu wa Rais ajarejea Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiteta jambo na Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki wakati wa mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Sabasaba wilaya ya Chunya ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara ya Makamu wa Rais mkoani Mbeya. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0


  0 0

  WAZIRI wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, ameendelea na ziara yake vijijini y kukagua miradi ya umeme REA III inayoendelea huku akilazimika kuzindua umeme usiku.

  Amesema amelazimika kufanya uzinduzi huo usiku ili kutoa maana halisi ya uwepo wa mwanga wa umeme kwa wananchi ili nao waone hali halisi kuliko ya jinsi raha ya umeme ilivyo.

  Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ihanga Wilayani Chato, alisema kuwa Serikali pamoja na watalaamu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa kushirikiana na REA wamekuwa wakifanyakazi usiku na mchana ili kuhakikisha kazi ya uunganishaji umeme inafanyika kwa maslahi ya wananchi na kuvutia wawekezaji hasa wa viwanda.

  “Ninawashukuru sana wananchi kwani watu wengi wana shauku ya umeme na kila unapokwenda ukiwaambia leo ninakuja kuwaunganishia umeme wako tayar kusubiri mpaka usiku, niwapongeze wananchi kwa kweli walikuwa na shauku kubwa na leo wamepata furaha.

  “Na mimi kama mbunge wao bahati nzuri ni Waziri wa Nishati ilikuwa ni lazima kuwatembelea hata kama ingekuwa usiku. Lakini pia huu ni mwanga ili udhibitishe kama ni mwanga ni vizuri ukawasha usiku ikaonekana kuwa kweli hii ni taa. Nadhani walitaka wajiridhishe na wameshuhudia kwa sababu tumewasha usiku na kwangu nitatembea usiku na mchana kuwatumikia Watanzania ili mradi nitahakikisha wanapata maendeleo,” alisea Dk. Kalemani

  Akizungumzia suala la nguzo za umeme, Dk. Kalemani, alisema kuwa kwa sasa nchi ina nguzo nyingi kwani kwa mwezi huingizwa zaidi ya nguzo 118,000 na si 2000 kama ilivyokuwa nyuma.

  Alisema kuna kampuni 21 za zinatosambaza nguzo nchini.

  “Zamani tulikuwa na wasambazaji nguzo watano lakini kwa sasa tuna kampni 21 hiyo imetokana na kusitisha uagizaji wa nguzo kutoka nje ya nchi ambazo zilikuwa na gharama kubwa sana kwa Shirika letu la umeme Tanesco lakini hata wakandarasi. Sasa hivi nguzo wazalishaji wa nguzo ni wengi kwani hata gharama zimeshuka na pia suala la transfoma si changamoto.

  “Mradi unapoanza wanaleta nguzo kutokana na mahitaji kutokana na eneo husika leo wameanza na nguzo chache lakini kadri ya wananchi wanavyojiandisha magari huleta nguzo nyingi zaidi ili kuweza kutoa huduma ya kuunganisha umeme. Na wiki ijayo wataleta nguzo nyingine 200 ombi langu wananchi wajiandikisha na kulipia ili nguzo ziendele kuwa nyingi.

  “Watanzania wana shauku ya kulipia umeme sasa Serikali imekuja na mpango wezeshi badala ya wananchi kwenda Tanesco sasa litaanzishwa dawati dogo katika maeneo ya vijiji ili kuwapunguzia gharama za kutembea umbali mrefu.

  “Pia wananchi wanaweza kulipia kidogo kidogo na pindi wanapofikisha Shilingi 27,000 ataunganishiwa huduma ya umeme,” alisema Dk. Kalemani


  Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ihanga Wilayani Chato usiku wa jana baada ya kuzindua umeme
  Wananchi wa Kijiji cha Ihanga Wilayani Chato, wakimsikiliza kwa Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani
  Diwani wa Viti Maalumu, Grace Kubilima (CCM), ambaye pia ni mkazi wa Kijiji cha Ihanga, akimshukuru Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, baada ya kuzindua umeme jana usiku katika kijiji hicho.

  0 0

  Mfanyabiashara Said Lugumi akiongozwa na Ofisa wa Polisi kuelekea ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwenda kuonana na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Lugola baada ya kutoka Makao Makao Makuu ya Polisi Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai.(Picha na Jeshi la Polisi)

  0 0

  Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) inatarajia kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi katika vijiji 120 vinavyozunguka misitu ya Hifadhi ya Serikali Kuu.

  Akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya NLUPC and TFS kilichofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NLUPC Dkt. Stephen Nindi ameahidi kuwa taasisi yake itatoa ushirikiano wa kitaalamu kwa ajili ya kunusuru rasilimali za nchi wakati wowote kwa faida ya nchi na watanzania wote.

  Naye Mtendaji Mkuu wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo amesema kuwa mipango hiyo ya matumizi ya ardhi inalenga kumaliza changamoto zote ya kuhifadhi misitu nchini kwenye vijiji vinavyozunguka hifadhi hizo pamoja na kuwasaidia wanavijiji kuwa na matumizi rafiki ya ardhi yatakayosaidia kutunza misitu hiyo.“Mpaka sasa zaidi 60% ya misitu iliyopo nchini haijahifadhiwa na lengo letu ni kuhakikisha misitu hiyo inahifadhiwa. Hivyo nawataka wataalamu wa Tume pamoja na Wakala kuhakikisha lengo hili linafikiwa kwa kuweka mikakati ya kitaaaluma kwa kuzingatia wakati uliopo,” alisema Professa Silayo.

  Professa Silayo anasema hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali yanayoelekeza kutatua migogoro ya mipaka kati ya wananchi na maeneo ya jirani na hifadhi kwa kushirikisha wadau katika kuhakiki mipaka ya maeneo ya hifadhi kwa kuweka alama za kudumu; kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi; na kuzingatia utawala wa Sheria katika kusimamia rasilimali za maliasili.Mtendaji huyo anaongeza kuwa uharibifu wa misitu nchini ni mkubwa katika maeneo ambayo vijiji vimeanzishwa ndani ya misitu bila kufuata sheria na TFS imeendelea kuzuia upanuzi zaidi wa vijiji hivyo, na hadi sasa kuna vijiji 228 vinavyofahamika na miji kadhaa.

  NLUPC na TFS wameunda kikosi kazi kitakachoandaa mikakati ya namna bora ya kufanya kazi hiyo ambapo wameanza kwa kupitia orodha ya misitu ya hifadhi yenye migogoro kwa kanda zote saba za TFS. Kanda hizo ni za Mashariki, Kaskazini, Kati, Kusini, Nyanda za juu Kusini, Ziwa na Magharibi. 
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo (aliyesimama) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt. Stephen Nindi wakiongoza kikao cha pamoja kati ya NLUPC na TFS juu ya maandalizi ya upangaji wa mipango ya matumizi ya ardhi katika vijiji vinavyozunguka hifadhi za Misitu inayosimamamiwa na Serikali Kuu. 
  Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu, Sera na Mawasiliano (DLCCP) wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, Bibi Albina Burra (kulia) pamoja na Watalamu wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) wakifuatilia kwa maokini mazungumzo kati ya taasisi zao.

  0 0

  Na Ripota wetu, Manyara

  Jumla ya timu 20, zinatarajiwa kushiriki ligi ya Chem Chem CUP, wilayani Babati mkoa wa Manyara ambapo zawadi zenye thamani ya sh 4.5 milioni zitatolewa.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mratibu wa ligi hiyo, ambayo hufanyika kila mwaka,katika uwanja wa Mdori, Charles Godluck alisema, lengo lake ni kupiga vita ujangili na kuhamamisha jamii uhifadhi za mazingira.Godluck alisema, ligi ya chem chem CUP,mwaka huu inatarajwa kufunguliwa na Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, Agosti 19 na itatanguliwa na mkutano wa kutolewa jezi wa timu zote agosti 10 mwaka huu.

  "hivi sasa tumezitaka timu zote ifikapo Agosti 4 ziwe zimethibitisha lakini pia kujitokeza kwenye kikao cha kupanga ratiba Agosti 10"alisema.Alisema mwaka huu bingwa wa soka, atapewa zawadi ya fedha taslimu 1.7 milioni na kombe,mshindi wa pili fedha 1.1 milioni, wa tatu 600.000 na wa nne 300,000.
  "pia kutakuwa na zawadi wa kocha, bora, timu bora na mchezaji bora"alisema.
  Alisema katika michuano hiyo, pia kutakuwa na michezo kwa wasichana ambapo, bingwa atazawadiwa 400,000 na pia kutakuwa na ngoma za kitamaduni na michezo mingine.Meneja wa taasisi ya Chemchem Foundation, Recardo Tossi, ambao wamewekeza ujenzi wa hoteli katika eneo la Mdori, alisema ligi hiyo, imekuwa ikishirikisha zaidi ya wanamichezi 400 na kuwa na ufanisi mkubwa.

  "tunataka jamii ambayo inazunguka kijiji cha Mdori na tarafa nzima ya Mbugwe na wilaya ya babati, kuwa wahifadhi wazuri na kupiga vita ujangili"alisema.Na hapa chini ni baadhi ya matukio katika picha ya michuano iliyofanyika mwaka jana ambapo timu ya mdori fc ilijinyakulia kombe la michuano hiyo.

  0 0

  Na Pamela Mollel,Arusha.

  Kampuni ya Uzalishaji wa Mbegu ya Monsanto imezindua mbegu mpya aina ya DK 777 ambayo ina uwezo mkubwa wa kustahimili ugonjwa wa Mnyauko wa Mahindi uliowasumbua wakulima wengi hususan katika kanda ya Kaskazini na kusababisha wakulima kukosa mazao .

  Mtafiti wa Mbegu hizo kutoka kampuni ya Monsanto ,Honest Temu amesema kuwa ugonjwa wa Mnyauko umeawaathiri wakulima wengi suala lililowasukuma kufanya utafiti ambao ulikamilika hivi karibuni na mbegu hizo zilisajiliwa na serikali kwa ajili ya kutumika na wakulima .

  Meneja Kiongozi wa Kampuni hiyo Frank Wenga amesema kuwa mbegu hizo zitakua mkombozi kwa wakulima na kuleta mavuno ya kutosha kwa ajili ya chakula na ziada kwa ajili ya biashara ili kukuza pato la mkulima na kuinua uchumi wa taifa kupitia kilimo. 

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Mbegu nchini Bob Shuma akizindua mbegu hizo amesema kuwa sekta ya mbegu ni sekta muhimu katika kukuza kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa taifa hivyo wadau wa mbegu hawana budi kufanya tafiti zitakazosaidia kukuza kilimo na kuinua ustawi wa mkulima kupitia uzalishaji wa mbegu bora.

  Kwa upande wake Mkulima Nko amesema kuwa mbegu hizo zitawasadia wakulima kupata uhakika wa kupata mazao ya kutosha kutosheleza mahitaji ya nyumbani na mahitaji ya soko hivyo kusaidia upatikanaji wa chakula na kukuza pato la mkulima.
  Meneja Kiongozi wa Kampuni ya Monsanto Frank Wenga Akizungumza katika uzinduzi wa mbegu mpya aina ya DK 777 ,ulifanyika katika viwanja vya Kituo cha utafiti wa kilimo Selian jana Mkoani Arusha.Picha na Pamela Mollel Arusha.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Mbegu nchini Bob Shuma akizungumza katika uzinduzi wa mbegu mpya aina ya DK 777 jana Mkoani Arusha na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa kilimo
  Viongozi wa kampuni ya Monsanto na wadau wa kilimo wakiwa katika shamba darasa.

  0 0


  HATIMAYE Mashindano ya golf ya Utalii Karibu Kusini Mufindi Golf Challenge 2018 yamehitimishwa kwa mafanikio makubwa huku serikali ikiahidi kushirikiana na wadau wa mchezo huo kuhakikisha unachezwa maeneo yote nchini ili utumike kutangaza sekta ya utalii zaidi.

  Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha mashindano hayo mwishoni mwa wiki kwenye Viwanja vya Golf vya Unilever wilayani Mufindi mkoani Iringa, Naibu Waziri wa Tamisemi, Bw Joseph Kakunda alisema mashindano hayo yameonesha wazi kuwa endapo mchezo huo utasambaa zaidi katika maeneo yote hapa nchini yatavutia zaidi washiriki kutoka mataifa mbalimbali ambao pia watakuja kama watalii.

  “Ni kupitia mashindano haya ndio nimeweza kugundua nguvu ya mchezo wa golf katika kutangaza utalii kwa sababu umeweza kuwavutia washiriki kutoka maeneo mbalimbali ya nchi ni bahati mbaya tu kwamba kwasasa mchezo huu unachezwa kwenye mikoa michache sana hapa nchini tena ukitafsiriwa kuhusisha tabaka flani jambo ambalo si kweli,’’ alisema.

  Aliongeza kuwa mkakati uliopo ni kuhakikisha kwamba mashindano ya golf ya Utalii Karibu Kusini Mufindi Golf Challenge yanakuwa ya kimataifa ili yavutie zaidi washiriki kutoka mataifa ya nje.

  Mashindano hayo ya siku tatu yaliandaliwa na serikali kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii na yalihusisha washiriki zaidi ya 80 wakiwemo wachezaji wa kulipwa yaani ‘Professionals’ na washiriki wa kawaida yaani ‘Amateurs’ ambapo mchezaji Aidani Nziku kutoka klabu ya Golf ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam akiibuka mshindi wa jumla.

  Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamhuri William alisema wilaya yake imejipanga kuhakikisha mashindano hayo yanakuwa ya kimataifa zaidi ili yavutie washiriki wengi ndani na nje ya nchi kwa kuwa uwepo wao katika kipindi chote cha mashindano utaleta tija zaidi kiutalii,kiuchumi na kimichezo kama ambavyo imeanza kuonekana kupitia mashindano hayo yaliyofanyika kwa mara ya kwanza baada ya miongo mingi.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Iringa mjini, Bw Richard Kasesela aliwahakikishia wenyeji wa mashindano hayo ambao ni klabu ya golf ya Mufindi kuwa mashindano hayo yataendelea kufanyika kila mwaka lengo likiendelea kuwa ni kuvutia watalii kutoka ndani na nje ya nchini ili waweze kutembelea vivutio vya utalii katika mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini.

  “Tunaamini kwamba kupitia ustawi wa mashindano haya mbali na kuvutia watalii tutafanikiwa pia kuvutia wawekezaji wa kiuchumi katika ukanda wetu huu wa Nyanda za Juu Kusini ambayo ni pamoja na Iringa, Mbeya, Njombe, Songwe, Ruvuma, Rukwa na Katavi.,’’ alitaja.

  Mratibu wa mashindano hayo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI) Clement Mshana alitoa wito kwa serikali kushirikiana na sekta binafsi kuhakikisha inaboresha zaidi miundombinu ya kiutalii ikiwemo barabara na sehemu za malazi ili kuwavutia zaidi si tu washiriki wa mchezo huo bali pia watalii waweze kufika kwa wingi kwenye vivutio hivyo vya kimichezo. Ombi hilo lilipokelewa na Naibu Waziri Kakunda ambapo aliagiza Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha wanaboresha barabara zinazoelekea kwenye vivutio vya utalii hapa nchini ili kurahisisha safari za kiutalii kuelekea kwenye vivutio hivyo.
  Naibu Waziri wa Tamisemi, Bw Joseph Kakunda (alieva jaketi la kaki) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa mashindano ya ya golf ya Utalii Karibu Kusini Mufindi Golf Challenge 2018 , mara baada ya kuwakabidhi zawadi zao wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha mashindano hayo mwishoni mwa wiki kwenye Viwanja vya Golf vya Unilever wilayani Mufindi mkoani Iringa. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamhuri William pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa mjini, Bw Richard Kasesela 
  Naibu Waziri wa Tamisemi, Bw Joseph Kakunda akionyesha ufundi wake kwenye mchezo huo.
  Mkuu wa Wilaya ya Iringa mjini, Bw Richard Kasesela nae akionyesha utaalamu wake kwenye mchezo huo.
  Nami nimo! Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamhuri William akionyesha utaalamu wake kwenye mchezo huo.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma (mteule) Prof Riziki Shemdoe nae akionyesha ufundi wake.
  Kapteni wa klabu ya Golf ya Mufindi Bw Glyn akionyesha umahili wake kwenye mchezo huo mbele ya wageni waalikwa.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Unilever Tea Tanzania Ltd Bw Ashton Eastman akizungumza kwenye hafla hiyo. Kampuni hiyo ni moja ya wadhamini wa mashindano hayo na ndiyo inayomiliki Uwanja huo wa golf ikiwa ni pamoja klabu ya golf ya Mufindi.
  Mkuu wa Wilaya ya Iringa mjini, Bw Richard Kasesela nae akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo aliwahakikishia wenyeji wa mashindano hayo ambao ni klabu ya golf ya Mufindi kuwa mashindano hayo yataendelea kufanyika kila mwaka lengo likiendelea kuwa ni kuvutia watalii kutoka ndani na nje ya nchini ili waweze kutembelea vivutio vya utalii katika mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini.
  Naibu Waziri wa Tamisemi, Bw Joseph Kakunda (Kulia)akifurahi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamhuri William baada ya kukabidhiwa zawadi ya mpira wa golf pamoja na kitabu cha muongozo kuhusu mchezo huo ikiwa ni ishara kumkaribisha rasmi kuwa mdau wa maendeleo ya mchezo huo hapa nchini.
  Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa Bw Fikiri Kissimba akizungumza kwenye hafla hiyo.
  Afisa Ushirikiano wa Jamii kutoka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Bw Moronda Moronda akizungumza kwenye hafla hiyo.
  Mratibu wa mashindano hayo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI) Clement Mshana akitoa nasaha zake kwenye hafla hiyo.

  0 0

  Na Beatrice Lyimo-Maelezo, Dodoma
  Serikali imetangaza rasmi kuanza kutumika kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumsihi wa Umma (PSSSF) kuanzia Agosti 1, mwaka huu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ametangazaa leo jijini Dodoma.
  Mhe. Mhagama amesema kuwa Serikali imekamikisha maandalizi yote muhimu ya utekelezaji wa Sheria ya PSSSF na imeridhika kwamba Mfuko huo unaweza kuanza kutekeleza majukumu yake, na kwamba kutokana na hatua hiyo wafanyakazi wote watakaoajiriwa katika sekta ya umma watasajiliwa katika Mfuko wa PSSSF na wale watakaoajiriwa katika sekta binafsi watasajiliwa katika Mfuko wa NSSF.
  "Napenda kutangaza rasmi kwamba, kwa mamlaka niliyonayo chini ya kifungu cha 1(1) cha Sheria ya PSSSF nimeteua tarehe 1 Agosti, 2018 kuwa ndiyo tarehe rasmi ya kuanza kutumika kwa Sheria ya PSSSF", alisisitiza mhe. Mhagama
  Waziri Mhagama kaongeza kuwa Wanachama wote ikiwa ni pamoja na wastaafu na warithi waliopo katika mifuko inayounganishwa watahamishiwa katika mfuko wa PSSSF na haki na stahili zao zitaendelea kutolewa na mfuko huo bila kuathiriwa kwa namna yeyote ile.
  Akizungumzia rasilimali, vitega uchumi, madeni, mifuko ya hiari na mikataba iliyokuwa chini ya mifuko inayounganishwa  Waziri Mhagama amesema itahamishiwa katika Mfuko mpya wa PSSSF. Pia Waziri Mhagama amewatoa hofu ya kupoteza ajira watumishi wote wa mifuko iliyounganishwa  kwa kuwa watahamishiwa katika mfuko mpya ambako uongozi wa mfuko huo utawapangia majukumu yao kwa kuzingatia muundo wa taasisi.
  Amesema ili kuondoa sintofahamu Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi ya Mifuko ya Hifadhi za Jamii (SSRA) imeandaa mkakati maalumu wa kutoa elimu kwa umma kuhusu sheria na kanuni za PSSSF ili kuhakikisha kwamba wanachama na wadau wote wa sekta ya hifadhi ya jamii wanakuwa na uelewa sahihi wa sheria hizo na mabadiliko yaliyofanyika.
  Mbali na hayo, Waziri Jenista ameteua wajumbe wa Bodi ya Mfuko huo ambao ni Bi. Leah Ulaya, Bw. Rashidi Mtima, Dkt. Aggrey Mlimuka, Bi. Stella Katende, Bw. Thomas Manjati, Bw. Henry Katabwa, Bi. Suzan Kabogo pamoja na Bw. Jacob Mwinula.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akitangaza rasmi leo Jijini Dodoma tarehe ya kuanza  kufanya kazi kwa mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF) ambapo mfuko huo unaanza kazi Agosti Mosi mwaka huu.Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera na Uratibu Prof. Faustine Kamuzora.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera  Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF)  unaanza kutekleza majukumu yake bila kuathiri huduma kwa wanachama wa mifuko iliyounganishwa.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma  (PSSSF) Bw. Eliud Sanga (katikati) akisisitiza kuhusu hatua watakazochukua kuhakikisha kuwa mfuko huo mpya unatatua changamoto zilizokuwepo awali katika mifuko iliyounganishwa kuunda mfuko huo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera  Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kutangaza tarehe ya kuanza rasmi kufanya kazi kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa  Watumishi wa Umma(PSSSF) leo Jijini Dodoma.Kulia ni Mkurugenzi mkuu wa SSRA Dkt. Irene Isaka. Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO

  0 0

  Na Dixon Busagaga wa Globu 
  ya Jamii, Kanda ya Kaskazini
  MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira leo amemuapisha Mkuu mpya wa wilaya ya Hai Mhe. Lengai Ole Sabaya katika hafla fupi ya kuapishwa kwa mteule huyo wa Rais Magufuli katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro,Wakurugenzi,Makatibu tawala wa wilaya, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na ndugu na marafiki wa mkuu huyo mpya wa wilaya ya Hai.
  Mkuu mpya wa wilaya ya Hai, Mhe. Lengai Ole Sabaya akila kiapo mbele ya mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira (hayupo pichani) ,Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
  Mkuu Mpya wa wilaya ya Hai Mhe. Lengai Ole Sabaya akitia saini katika karatasi ya Kiapo mara baada ya kuapa kushika nafasi ya Ukuu wa wilaya ya Hai.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira (kushoto) akitia saini katika karatasi ya kiapo,mbele yake ni Mkuu Mpya wa wilaya ya Hai Mhe. Lengai Ole Sabaya akishuhudia.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akimkabidhi Mkuu Mpya wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya katiba ya Jamhuri ya Muungano muda mfupi baada ya kuapishwa.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akimkabidhi Mkuu Mpya wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya Ilani ya Chama cha Mapinduzi muda mfupi baada ya kuapishwa.

  0 0


  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mha. Kapuulya Musomba (mwenye overall ya bluu) akijadiliana jambo na Ndg. Ildefons Mnimbo ambaye ni mtaalamu kutoka kampuni ya Plasco anaesimamia zoezi la kuunganisha mabomba, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kuunganisha bomba kubwa la gesi kutoka Mtwara na lile la kutoka Ubungo kuelekea Mikocheni. 
  Sehemu ya eneo la barabara ya Ubungo Maziwa inayochimbwa kitaalamu bila kuvunja barabara ili kuruhusu bomba la gesi kuvuka barabara hiyo. 
  Bomba lenye kipenyo cha 315mm likiwa limelazwa katika mtaro tayari kufukiwa, hii ni sehemu ya bomba linalochukua gesi asilia kutoka kwenye bomba kuu linalotoka Mtwara hadi Dar es Salaam na kuunganisha na bomba linalotoka Ubungo kuelekea Mikocheni. 


  Ni miezi mitatu sasa tangu Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alipozindua rasmi mradi wa kuunganisha bomba kubwa la gesi asilia linalotoka Mtwara hadi Dar es Salaam na bomba la kipenyo kidogo linalotoka Ubungo kuelekea Mikocheni. 


  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mha. Kapuulya Musomba alifafanua kwamba utekelezaji wa mradi huo unalenga kuongeza matumizi ya gesi asilia kwa jiji la Dar es Salaam kwa kuwaunganisha wateja zaidi wa matumizi ya majumbani na viwandani. 

  Mradi huu unahusisha ujenzi wa msingi kwa ajili ya kusimika mtambo wa kupunguza mgandamizo, uunganishaji wa vipande vya mabomba, kuthibitisha njia ya bomba, uchimbaji na ulazaji wa bomba litakalochukua gesi kutoka bomba kubwa, uwekaji wa viainisho vya bomba linapopita na ujenzi wa daraja la waenda kwa miguu kuvuka mto Ubungo. 

  Akizungumza juu ya hatua za utekelezaji, Meneja Mradi Ndg. Denice Byarushengo alisema “mradi umepiga hatua kubwa na muhimu ambapo hadi sasa ujenzi wa msingi kwa ajili ya kusimika mtambo wa kupunguza mgandamizo umekamilika kwa asilimia 97%, uthibitisho wa njia ya bomba na zoezi la kuchimba mitaro kwa ajili ya mabomba umekalimilika kwa asilimia 76.8%, uunganishaji wa mabomba umekamilika kwa asilimia 88.6%, ulazaji na ufukiaji wa mabomba umekamilika kwa asilimia 56.9%, viainisho sita (6) vya bomba linapopita vimeshawekwa na ujenzi wa dara la waenda kwa miguu umekamilika kwa asilimia 90%”.

  Aidha, Meneja Mradi aliongeza kwamba utekelezaji wa mradi huu unahusisha kuvuka mto Ubungo pamoja na barabara ya Ubungo Maziwa na ya Mandela ambapo hadi sasa kazi ya kuvuka mto Ubungo imekamilika kwa asilimia 100% na ile ya kuvuka barabara ya Ubungo Maziwa imekamilika kwa asilimia 50% wakati ya kuvuka barabara ya Mandela ikiwa mbioni kuanza. 

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mha. Kapuulya Musomba ambaye alifanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo hapo jana alionyesha kuridhishwa na kazi na ubora wa utekelezaji wa mradi, Mha. Kapuulya alisema “pamoja na changamoto zilizopo, ninayo furaha kwamba kazi zinafanyika kwa kasi na ubora wa hali ya juu na ni matumaini yangu baada ya kuongea na mkandarasi pamoja na msimamizi wa mradi kwamba mradi utamalizika ndani ya wakati”.

  Mradi wa kuunganisha bomba kubwa la gesi asilia na lile la Ubungo kuelekea Mikocheni lenye urefu wa kilomita 7.8 na uwezo wa kusafirisha gesi kiasi cha futi za ujazo milioni 7.5 kwa siku unalenga kuunganisha kiwanda cha Coca Cola Kwanza Ltd na BIDCO pamoja na wateja takribani 1000 wa majumbani ambao wataunganishwa kwa awamu. 

  Mradi huu utawezesha upatikanaji wa gesi asilia ya kutosha katika bomba litokalo Ubungo kuelekea Mikocheni kupitia barabara ya Sam Nujoma kusambaza gesi kwa wateja wa majumbani katika maeneo ya Ubungo, Shekilango, Mlalakuwa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sinza na Mikocheni. Mkandarasi wa mradi huu ni kampuni ya SINOMA kutoka Jamhuri ya Watu wa China na mradi unagharimu shilingi za kitanzania bilioni 4.2 ambazo ni fedha za ndani kutoka TPDC. 

  Vile vile mradi huu unatoa fursa kwa kampuni za wazawa kutoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuuza bidhaa za ujenzi kama vile mabomba ambapo kwa sasa kampuni ya Plasco ndio mshindi zabuni hiyo. Mkandarasi wa mradi pia ana fursa ya kutoa kazi kwa mkandarasi mwingine (sub-contracting) lengo likiwa ni kuchochea ushirikishwaji wa wazawa katika sekta ya mafuta na gesi hapa nchini.

  0 0  0 0

   Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage, akizungumza wakati wa kikao na Uongozi wa Benki ya CRDB, walipotembelea Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Dar es Salaam. (Wa kwanza kushoto) ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei.
   Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (wa kwanza kushoto) akizungumza na Kamishna wa Operesheni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage (wa kwanza kulia) pamoja na maafisa wa Jeshi hilo, mikakati ya kudumisha uhusiano baina ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Benki ya CRDB, wakati wa kikao na Uongozi wa Benki ya CRDB, walipotembelea Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Dar es Salaam.
   Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Peter Mabusi, akifafanua jambo kwa Uongozi wa Benki ya CRDB, wakati wa kikao walipotembelea Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Dar es Salaam. (Wa kwanza kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei na (wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Operesheni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage.
  Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage (watano kulia),  akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (mwenyesuti nyeusi), Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji waliombatana na Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo na Viongozi Waandamizi wa Benki ya CRDB, jijini Dar es Salaam.
  habari na Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

  0 0

  NA WAMJW-DAR ES SALAAM.
  SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imewaagiza waajili wote wa Serikali na Sekta binafsi kutenga chumba maalum kwa ajili ya waajiliwa wao wanaonyonyesha.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akitoa Tamko kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani leo jijini Dar es salaam.“Ninazitaka Halmashauri zote nchini kupitia maafisa kazi kuhakikisha wanawake waajiriwa waliojifungua wanapata haki yao ya likizo ya uzazi na muda wa kunyonyesha kwa ukamilifu” alisema Waziri Ummy.

  Aidha Waziri Ummy amewataka Wanaume wanaopewa likizo za uzazi kuzitumia ipasavyo kwa kumsaidia mama kazi ili aweze kumnyonyesha mtoto mchanga aliyejifungua badala ya ktumia likizo hizyo kwenda kukaa baa.
  Waziri Ummy alisema kuwa vituo vyote vinavyotoa huduma ya afya vinatekeleza vidokezo kumi vya kufanikisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama na hivyo kuwa rafiki wa Mtoto.

  “Wazazi tunatakiwa kufuata taratibu za kunyonyesha ikiwemo kuanza kumnyonyesha mtoto ndani ya saa moja ya kwanza ya mama kujifungua, kunyonyesha mtoto mara kwa mara kadiri anavyohitaji, kuendelea kunyonyesha maziwa ya mama pekee bila kumpatia mtoto kitu kingine chochote hata maji katika miezi sita ya mwanzo na kuendelea kunyonyesha hadi anapofikisha umri wa miaka miwili au zaidi” alisema Waziri Ummy.

  Aidha Waziri Ummy amesema kuwa takwimu za utafiti wa hali ya kidemografia na afya uliofanyika mwaka 2015 zinaonesha kuwa asilimia 59 ya watoto wenye umri wa miezi 0 hadi miezi 6 wananyonyeshwa maziwa ya mama pekee.

  “kila Mwajiri anatakiwa kumruhusu mfanyakazi mwanamke aliyejifungua kumnyonyesha mtoto wakati wa saa za kazi kwa jumla ya mpaka masaa 2 kwa siku kwa kipindi kisichopungua miezi 6 tangu kumaliza likizo yake ya uzazi” alisisitiza Waziri Ummy.

  Kila ifikapo tarehe 1 – 7 Agosti ya kila mwaka Tanzania huungana na nchi nyingine ulimwenguni kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama na maadhimisho yam waka huu yamebeba kauli mbiu isemayo “UNYONYESHAJI WA MAZIWA YA MAMA NI MSINGI WA MAISHA.”


  Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbalimbali wa sekta ya afya hawapo pichani kuhusu umuhimu wa kunyonyesha watoto wachanga wakati akitoa Tamko kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani leo jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wa pilia kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa sekta ya afya mara baada ya tamko kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani leo jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya wadau wa sekta ya afya wakimsikiliza Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati akitoa Tamko kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani leo jijini Dar es salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)

  0 0

  Na Hamza Temba-WMU

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amesema Serikali itatumia fursa ya ujio wa Mcheza Golf mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus kutoka nchini Marekeni kubuni viwanja vya mchezo huo karibu na maeneo ya vivutio vya utalii nchini ili kuvutia watalii wengi wa kimataifa na hivyo kukuza pato la sekta hiyo.

  Dk. Kigwangalla amesema hayo jana mara baada ya kumuaga mchezaji huyo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam alipokuwa akirudi nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku kumi yeye na familia yake katika vivutio mbali mbali vya utalii hapa nchini.

  “Tutatumia utaalamu na uzoefu wake kwenye mchezo wa Golf kwa kumtaka aje na kampuni yake atusaidie kutengeneza plan (mpango) ya kujenga viwanja vya golf.

  “Amedesign viwanja zaidi ya 300 kwenye nchi zaidi ya 50 duniani na nchi hizo zimefaidika, amesema katika project zake zaidi ya asilimia 90 zinafanya vizuri pamoja na kwamba ni uwekezaji wa gharama kubwa bado imelipa kwa kiasi kikubwa na hakuna hata kiwanja kimoja kimepata hasara na vimekuwa vinasaidia kukuza utalii katika nchi hizo.

  “Lengo letu ni kutengeneza ukanda maalum wa viwanja vya golf ambao utakuwa na viwango vya kimataifa na utavutia wacheza Golf kutoka nchi mbalimbali duniani, kwahiyo hii ni aina nyingine ya utalii wa watu wenye uwezo ambao wataleta pesa nyingi kwa wakati mmoja.

  “Tutaendelea kuwa na mawasiliano nae na kampuni yake ili tuweze kuona anawezaje kutusaidia na sisi walau tuwe na hiyo plan (mpango) lakini pia tukapata wawekezaji wakaja kuwekeza kwenye viwanja vya golf vitakavyojengwa karibu na fukwe, karibu na mito au hifadhi za Taifa ambapo tutavutia sio tu watalii ambao wanaokuja kufanya utalii wa wanyamapori au beach lakini tutavutia watalii wanaokuja mahsusi kwa kwa ajili ya utalii wa golf” alisema Dk. Kigwangalla.

  Wakati huo huo Dk. Kigwangalla amesema Serikali itaendelea kuheshimu na kujali maslahi ya wageni mashuhuri wanaokuja nchini ikiwemo ya usiri wa safari zao na kwamba atakayetaka aje kimya kimya na aondoke kimya kimya atapata heshma hiyo na atakayekubali kuwa wazi naye pia atapata heshma hiyo.

  Kwa upande wake Jack Nicklaus alisema amefurahishwa sana na vivutio mbalimbali vya utalii alivyovishuhudia katika safari yake hapa nchini pamoja na ushirikiano na ukarimu mzuri kutoka kwa watanzania na ameahidi kuwa balozi wa utalii wa Tanzania huo aendako.

  Jack Nicklaus ndiye mchezaji mwenye tuzo nyingi kuliko wachezaji wengine wa mchezo huo hapa duniani kwa sasa, ameweka rekodi ya kushinda mashindano ya kulipwa 117 na mashindano makubwa 18 (major champions). 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi Mcheza Golf mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus wa nchini Marekeni zawadi ya kinyago cha Makonde walipoagana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku 10 ya kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na Mcheza Golf mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus wa nchini Marekeni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku 10 ya kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa na Mcheza Golf mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus wa nchini Marekeni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kuondoka kurudia kwao baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku 10 ya kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na Mcheza Golf mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus wa nchini Marekeni wakitumbuizwa na kikundi cha ngoma katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kuondoka kurudia kwao baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku 10 ya kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini.
  Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mcheza Golf mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus wa nchini Marekeni na familia yake na uongozi wa Bodi ya Utalii Tanzania ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Jaji Mst. Thomas Mihayo muda mfupi kabla ya ugeni huo kuondoka na kurudi kwao.

  0 0

  Na Rhoda Ezekiel, Kigoma

  MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amewataka Vijana wilayani Kakonko wasitumiwe na watu wenye nia mbaya katika Kipindi hiki cha kampeni na wakati wa uchaguzi kuvuruga amani iliyopo.

  Kauli hiyo ameitoa leo wakati akizungumza na vijana wa Bodaboda katika Kata ya Kasanda wilayani humo ambapo aliwataka vijana hao kufanya shughuli za maendeleo zitakazo waondoa katika umasikini na kuachana na watu wachache wenye lengo la kuvunja amani katika Wilaya hiyo kwa kuchochea vurugu.

  Kanali Ndagala amesema vijana wengi wamekuwa wakitumika sana katika kipindi cha uchaguzi kufanya maandamano na vurugu mbalimbali wakitumiwa na baadhi ya wanasiasa wasio waaminifu, ambapo aliwaasa vijana hao kuwa wazalendo na kusikiliza wagombea wote ili waweze kuchagua mgombea atakaye wasaidia kuleta maendeleo.Mkuu huyo amesema Serikali haita mvumilia yeyote atakayejihusisha na uvunjifu wa amani katika Wilaya hiyo na atakayebainika anatumika vibaya hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

  Amesema lengo la Serikali ni kuona uchaguzi huo unaisha salama na kampeni zinazofanyika ni za kistaarabu kwa kuwa amani na utulivu ndio nguzo bora ya kuwafanya wananchi wafanye shughuli zao."Mpaka sasa hatujapata taarifa ya kuwepo na vurugu katika maeneo ambayo kampeni zinaendelea niwaombe vijana msikubali kutumika kuleta vurugu wakati huu fanyeni kazi ili muweze kujikwamua kiuchumi nguvu mnazo lazima mzitumie katika kuleta maendeleo," amesema Kanali Ndagala.

  Katika hatua nyingine Mkuu huyo amewataka vijana hao katika msimu mpya wa kilimo kila kijana kuwa na shamba ekari moja ya pamba ili kuweza kuinua uchumi wao kwa kuwa zao hilo ni moja kati ya mazao ya biashara katika Wilaya.Hata hivyo baadhi ya Vijana hao waliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo na kuomba serikali kuendelea kudumisha amani na usalama katika Wilaya hiyo.Thadeo Bitungwa ni moja kati ya vijana wajasiliamali amesema kwa sasa amani imeimalika tofauti na kipindi cha nyuma ambapo vijana wengi walikuwa wanatekwa na Kunyang'anywa bodaboda zao, kwa sasa vitendo hivyo havipo.Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akizungumza na Vijana wa Boda boda katika kata ya Kasanda mapema leo Wilayani Kakonko, kuhusu kukataa kutumiwa na watu wenye nia mbaya katika Kipindi hiki cha kampeni na wakati wa uchaguzi kuvuruga amani Wilayani humo.DC Ndagala amewataka vijana hao kujishughulisha na shughuli za maendeleo zitakazo waondoa katika umasikini na kuachana na watu wachache wenye lengo la kuvunja amani katika Wilaya hiyo kwa kuchochea vurugu.
  0 0

  Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akisalimiana na Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Hassan Mkwiche mara baada ya kuwasili Gereza la Wilaya Same kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia leo Julai 31, 2018, Mkoani Kilimanjaro kabla ya kuendelea na ukaguzi katika magereza ya mwanga na Gereza Rombo. Lengo la ziara hiyo ni kukagua utendaji kazi pamoja na kusikiliza changamoto mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi hilo.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati) akiongea na Maafisa na askari wa Gereza la Wilaya ya Same alipotembelea gereza hilo katika ziara yake ya kikazi leo Julai 31, 2018(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Hassan Mkwiche.
  Maafisa na askari wa Gereza Same wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Kamishna Jenerali wa Magereza(hayupo pichani) alipotembelea gerezani hapo katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua utendaji kazi pamoja na kusikiliza changamoto mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi hilo.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike (wa kwanza kushoto) akikagua nyumba ya askari inayojengwa kwa njia ya kujitolea katika Gereza la Wilaya ya Same. Nyumba hiyo itakuwa na uwezo wa kuhifadhi familia nne za askari hivyo kutatua uhaba wa nyumba katika gereza hilo.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa na askari wa Gereza la Wilaya ya Same alipotembelea gereza hilo kwa lengo la kukagua utendaji kazi pamoja na kusikiliza changamoto mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi hilo Mkoani Kilimanjaro leo Julai 31, 2018(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Makao Makuu ya Jeshi la Magereza).

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akimsikiliza Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, na Ajira, Mhe Antony Mavunde, alipokua akiwafafanulia jambo wadau wa usafiri na usafirishaji kuhusu jinsi ya kupambana na ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwa Waziri Lugola ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima.
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akifafanua jambo kwa wadau wa Usafiri na Usafirishaji jinsi ya kupambana na ajali za mara kwa mara nchi. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Waziri Kangi Lugola wa wizara hiyo akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw Kailima Ramadhani.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akimsikiliza Omari Mponda, Kaimu Rais Chama cha Wasafirishaji Tanzania akichangia jambo jinsi wadau hao wanavvyoweza kushirikiana na wizara hiyo katika kupambana na ajali za barabarani .. Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima. Kulia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, na Ajira, Antony Mavunde. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam.

older | 1 | .... | 1635 | 1636 | (Page 1637) | 1638 | 1639 | .... | 1896 | newer