Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel Catalog



Channel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1636 | 1637 | (Page 1638) | 1639 | 1640 | .... | 1897 | newer

  0 0


  PICHA A
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika banda la maonesho la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), lililopo Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
  PICHA B
  Meneja Masoko na Huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Hilipoti Lello  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika banda la maonesho la Mfuko huo, lililopo Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
  PICHA C
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwaonesha baadhi ya waandishi wa habari jengo la maonesho la mkoa huo, lililojenhgwa katika Uwanja wa Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi leo, ambalo lipo katika hatua za ukamilishaji.
  WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KUPIMA BURE MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA KATIKA MAONESHO YA NANENANE SIMIYU
  Na Stella Kalinga, Simiyu
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kujitokeza kupata huduma ya upimaji wa magonjwa yasiyaombukiza katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwenye Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nanenane  yatakayofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani humo, katika Uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
  Mhe. Mtaka ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la Maonesho la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) lililopo Uwanja wa Nananenane kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
  Amesema NHIF itatoa huduma ya upimaji wa magonjwa ya saratani ya mlango wa kizazi, saratani ya matiti, kisukari na magonjwa mengine yasiyoambukiza bure , hivyo hii ni fursa wananchi wa mkoa huo kwa kuwa itawapunguzia gharama waitumie vizuri.
  Wakati huo huoMtaka ametoa wito kwa wananchi mmoja mmoja na vikundi vikiwemo vyama vya ushirika zaidi ya 390 mkoani humo kujiunga nakuwa na kadi za Bima ya Afya,  ili waweze kuwa na uhakika wa kupata huduma wakati wowote na kupunguza gharama za matibabu.
  “Mini naamini ugonjwa hauna hodi hivyo nitoe wito kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa bima ya afya na sisi kwetu bima ya afya ni kipaumbele kwa kuwa tunahitaji mapinduzi ya kuchumi na kielimu tunayofanya ndani ya mkoa yaende sambamba na watu kupata kadi za bima ya afya, ili waone thamani ya Serikali kuwekeza katika sekta ya Afya” alisema.
  “Katika sherehe za nanenane za mwaka 2018 niwaombe wananchi popote walipo watumie fursa hii ya kufikiwa na wenzetu wa Bima ya Afya,ili wawezeka kupata huduma za upimaji magonjwa yasiyoambukiza bure na kujiunga na bima ya afya “ alisisitiza.
  Naye Meneja Masoko na Huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Hilipoti Lello  amesema pamoja na kutoa huduma za upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza bure, huduma za usajili kwa ajili ya kupata kadi za bima ya afya  ya mtu mmoja , familia na vikundi zitatolewa ambazo zitalipiwa kulingana na aina ya kadi itakayotolewa .
  “Tutatoa huduma za usajili na kutoa kadi za bima ya afya katika banda hili na mtu akishasajiliwa hapa kadi zitatolewa hapa hapa, tutakuwa na kadi za watoto toto afya kadi, tutakuwa na huduma za ktoa kadi kwa vikundi na kwa wakulima ni kwa wale walio kwenye vyama vya ushirika(AMCOS); mtu yeyote atakayepata kadi hii atapata matibabu Tanzania nzima kuanzia Zahanati hadi hospitali ya Rufaa” alifafanua.
  Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa, Bw. Shabani Kiduta ametoa wito kwa Wananchi wa mkoa wa Simiyu kujitokeza kwa wingi kupata huduma ya upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza kujua afya zao na kupata tiba, ili Mapinduzi makubwa ya kiuchumi yanayofanywa mkoani humo yaweze kuwafikiwa wakiwa na afya njema.

  0 0



  Kampuni ya SBC Tanzania Limited, watengenezaji na wasambazaji wa vinywaji baridi aina ya Pepsi, Mirinda, 7up, Mountain Dew na Evervess, Mkoani Mwanza wanayo furaha kuwaletea Shindano kabambe litakalojulikana kwa jina la“Jishindie Mamilioni ” Shindano hili litahusu soda aina ya Pepsi, Mirinda Orange, Mirinda Fruity, Mirinda Lemon, 7Up za ujazo wa mililita 350, na Mountain Dew (300ml).

  Shindano hili litatangazwa Katika Radio, Magazeti, Mabango na Vipeperushi mbalimbali. Madhumuni ya kuwaletea shindano hili niKuboresha hali ya maisha ya wateja wetu wa kanda ya Ziwa kwa kuwapatia zawadi za fedha taslimu ili kuwawezesha kujikomboa kiuchumi.Shindano hili litaendeshwa Kwa muda wa wiki sita kuanzia tarehe 01/08/18 hadi 16/09/18 katika mikoa ifuatayo: Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Tabora, Geita, Kigoma na Kagera. 
  Meneja Mafunzo na Uwezeshaji SBC Tanzania Limited Rashid Chenja akionesha moja ya mabango ya kutambulisha shindano la Jishindie Mamilioni.
  Kutoka kushoto ni Phocas lusato Meneja Rasilimali watu SBC, akifuatia Meneja Mafunzo na Uwezeshaji SBC Tanzania Limited Rashid Chenja na Hussein Mkwawa ambaye ni Meneja mauzo Kanda ya Ziwa wakisikiliza vyema maswali ya waandishi wa habari (hawako pichani) katika utambulisho rasmi wa shindano la Jishindie Mamilioni, uliofanyika ukumbi wa mikutano SBC Nyakato jijini Mwanza.

  "Safiiiiii.....!!"


  Balozi wa PEPSI Albert G. Sengo (kulia) akitoa maelezo kwa wawezeshaji SBC, anayemsikiliza mbele yake ni Meneja Mauzo kanda ya Ziwa Hussein Mkwawa, Meneja Mafunzo na Uwezeshaji SBC Tanzania Limited Rashid Chenja na Meneja Rasilimali Watu Phocas Lusato katika utambulisho wa shindano la Jishindie Mamilioni, uliofanyika ukumbi wa mikutano SBC Nyakato jijini Mwanza.
  "Hizi ndizo zawadi"
  Nikama wakisemezana "Hebu tuone umepata nini ndani ya kizibo chako...." Balozi wa PEPSI Albert G. Sengo (kushoto) Sara Onesmo kutoka Clouds Tv na Johari Shani wa Mwananchi Communication.
  Shindano hili la“Jishindie Mamilioni” litakuana vizibo vya rangi ya Silva. Shindano hili litakua na zawadi nyingi za pesa taslimu kuanzia shilingi za Kitanzania 1,000,000/-, 500,000/-, 10,000/-, 5000/-, 1000/= na SODA YA BURE.

  Ili Mteja ajishindie zawadi anatakiwa kununua soda za Jamii ya Pepsi kisha abandue ganda Ndani ya Kizibo akikuta maandishi aidha ya shilingi 1,000,000/-, 500,000/-, 10,000/-, 5,000/- 1000/- au Free Pepsi (SODA YA BURE), atakua amejishindia zawadi hiyo papo hapo. 

  Zawadi za shilingi 10,000/=, 5000/=,1000/=na Soda ya bure zitapatikana hapo hapo kwa aliyekuuzia soda, Gari ya Mauzo au Muuzaji wa Jumla. Vizibo vya zawadi vimeandikwa kwa rangi ya dhahabu, Zawadi za shilingi 1,000,000/-, 500,000/- zitatolewa kiwandani Mwanza tu, Barabara ya Musoma, Nyakato, Kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 9 jioni siku za Jumatatu hadi Ijumaa (isipokua siku za sikukuu). 
  Hii ndio fursa nzuri kwa wanywaji wa soda zetu kujishindia Mamilioni kila siku kwa kunywa Soda zetu, Kuna zawadi nyingi sana, kunywa sasa unaweza kuwa wewe ndio mshindi, ili uboreshe maisha yako.Tarehe ya mwisho ya kutoa zawadi ni Tarehe 30 Septemba 2018.Tuna imani utashirikiana nasi kufanikisha shindano hili na kuboresha maisha yako.
  “Jishindie Mamilioni ”

  0 0

  Washiriki wa Mafunzo ya Uongezaji Thamani Viazi Lishe kutoka mikoa mbalimbali nchini,wakionesha mikate na mandazi waliyotengeneza  kwa kutumia urojo wa viazi hivyo pamoja na unga wa ngano wakati wa mafunzo yaliyofanyika hivi karibuni katika Ushirika wa Wahitimu wa  Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (Sugeco). Washiriki hao walifundishwa mambo mbalimbali ikiwemo uandaaji wa shamba, kupanda, uangalizi, mavuno, biashara pamoja na faida ya viazi hivyo vyenye  wingi wa vitamini A. Kushoto ni Mkurugenzi wa Sugeco, Revocatus Kimario.

  Kuanzia leo naahidi kuwaletea yaliyojiri wakati wa mafunzo hayo yaliyoendeshwa na walimu makini na wenye weledi mkubwa  kuhusu zao hilo.MWANDAAJI RICHARD MWAIKENDA
  Washiriki wakiosha viazi lishe ikiwa ni maandalizi ya awali

  Wakimenya viazi lishe

  wakiweka kwenye mashine ya kukata kata silesi tayari kwa kuanikwa kwenye mitambo ya kukausha inayotumia nishati ya jua.

  Mshiriki Richard Mwaikenda ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari aliyeshiriki kwenye mafunzo hayo akisambaaza viazi vilivyokatwakatwa wakati wa kuvianika tayari kukaushwa kwenye mitambo inayotumia nishati ya jua.
  Washiriki wakisambaza silesi za viazi lishe
  Washiriki wakipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Viazi Lishe wa Sugeco, Jolenta Joseph
  Washiriki wakipata maelezo kuhusu mfano wa kilimo cha umwagiliaji kinachotumi matone katika eneo la Segeco, Sua Morogoro.
  Wakitembelea Dryer inayotumia Nishati ya jua
  Richard Mwaikenda akiangalia aina ya mbegu ya viazi lishe  ya mataya katika bustani iliyopo Sugeco. Kushoto ni  Mtaalamu wa Viazi Lishe, Jolanta Joseph
  Wakinywa Juisi iliyotengenezwa kwa kutumia viazi lishe. Kushoto ni Mkurugenzi wa Sugeco, Kimario na Mkufunzi wa Mafunzo ya Viazi Lishe, Massimba. Kulia ni wshiriki wa mafunzo hayo kutoka Dar. Doroth na Neema Ngowi.

  Wakiwa kwenye mafunzo hayo
  Viazi Lishe vilivyochemshwa kwa kutumia mvuke tayari kuwekwa kwenye mashine inayotengeza rojorojo inayotumika kutengenezea bidhaa mbalimbali
  Washiriki wakijiandaa kuweka Viazi Lishe kwenye mashine ya rojorojo


  Mashine ikitengeneza rojorojo inayotumika kwenye mandazi, mikate na bidhaa zinginezo
  Mjasiriamali Nasra kutoka Dar es Salaam akipanga vizuri mikate baada ya kushiriki kuitengeneza
  Mwalimu wa mafunzo hayo, Jolanta akitoa maelezo ya kuzingaatia wakati wa kutengez juisi
  Washiriki wakikanda mchanganyiko wa unga wa ngano na viazi lishe tayari kutengeneza maandazi

  0 0


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akitoa pole kwa shule ya sekondari ya Kimbiji katika maombolezo ya vifo vya wanafunzi wanne.

  Wanafunzi wa sekondari ya Kimbiji wakiwa katika huzuni kubwa ya kifo cha wenzao wanne
  Wanafunzi wa sekondari ya Kimbiji wakiwa katika huzuni kubwa ya kifo cha wenzao wanne
  Watumishi wa Kigamboni pamoja na wazazi walipoungana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo kwenye maombolezo ya vifo vya wanafunzi wanne.



  SERIKALI imesikitishwa na vifo vya wanafunzi wanne ambao ni wasichana wa kidato cha nne kutoka shule ya sekondari Kimbiji iliyopo Kigamboni jijini Dar es salaam waliofariki kwa ajali ya maji walipokuwa wakiogelea katika bahari ya Hindi.

  Vifo vya wanafunzi hao vilitokana na sherehe iliyoratibiwa na shule husika ili kuwapongeza wanafunzi hao wa kidato cha nne baada ya kufanya vyema mitihani yao ya kujipimAkizungumza kwa majonzi shuleni hapo,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amesema serikali imepokea kwa masikitiko vifo hivyo na kutoa pole kwa wanafunzi, wazazi, na walimu wa shule hiyo kwa msiba huo mzito.

  Waziri Jafo amewataka walimu wote nchini kujiepusha na ufanyaji wa sherehe za wanafunzi katika mazingira hatarishi. Aidha, Waziri Jafo aliwasilisha rambirambi kwa familia nne za wafiwa.Wanafunzi waliofariki dunia ni Secilia Ernest Paulo, Selestina Vitus Malipesa, Agnetha Philipo Mlaki na Queen Leonard Mandala

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsindikiza Waziri wa Uhamiaji, Wakimbizi na Uraia wa nchini Canada, Ahmed Hussein, mara baada ya kumaliza kikao chao kilichojadilia masuala mbalimbali ya Wakimbizi pamoja na kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na Canada. Katika kikao hicho kilifanyika katika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. 
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimsikiliza Waziri wa Uhamiaji, Wakimbizi na Uraia wa nchini Canada, Ahmed Hussein (wapili kushoto) alipokua akimfafanulia jambo katika kikao kilichofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo, viongozi hao walijadili masuala ya mbalimbali ya Wakimbizi pamoja na kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na Canada. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke. Watatu kushoto ni Balozi wa Canada nchini, Ian Myles, na kushoto ni Kansela wa Masuala ya Uhamiaji wa Balozi huo hapa nchini, Erin Brouse. 
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Uhamiaji, Wakimbizi na Uraia wa nchini Canada, Ahmed Hussein (wapili kushoto). Katika kikao hicho kilichofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo, viongozi hao walijadili masuala ya mbalimbali ya Wakimbizi pamoja na kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na Canada. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke. Watatu kushoto ni Balozi wa Canada nchini, Ian Myles. Na kushoto ni Kansela wa Masuala ya Uhamiaji wa Balozi huo hapa nchini, Erin Brouse. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (katikati) pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia pia akiwakilisha Tanzania Nchini Indonesia Mhe.Dkt Ramadhani Kitwana Dau (kulia) na Viongozi wengine wakipewa maelekezo na Afisa Maalum mara baada ya mapokezi walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta, Jakarta Indonesia leo wakiungana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika ziara ya siku saba Nchini humo kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla , [Picha na Ikulu.]31/07/2018. 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Kiongozi wa Ngazi ya Juu Nchini Indonesia Daniel T.S.Simanjuntak (kushoto) mara alipowasili katika Ukumbi wa Watu Mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta, Jakarta leo, akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Viongozi mbali mbali,katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla ,[Picha na Ikulu.]31/07/2018.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia pia akiwakilisha Tanzania Nchini Indonesia Mhe.Dkt Ramadhani Kitwana Dau (kulia) mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta, Jakarta Indonesia leo, akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Viongozi mbali mbali,katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla,[Picha na Ikulu.]31/07/2018.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (katikati) pamoja na Viongozi aliofuatana nao akiwa katika mazungumzo na Kiongozi wa Ngazi ya Juu Nchini Indonesia Daniel T.S.Simanjuntak (wa pili kulia) katika Ukumbi wa Watu Mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta,Jakarta leo katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchini Indonesia Mhe.Mohammed Jusuf Kalla, [Picha na Ikulu.]31/07/2018.

  0 0

  Na Ramadhani Ali – Maelezo

  Ujumbe wa watu nane wa Wataalamu wa afya kutoka Serikali ya Brazil upo Zanzibar kutekeleza ombi la Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhamed Shein kuitaka nchi hiyo kuzidisha ushirikiano katika sekta ya Elimu, Afya na Utalii.

  Ujumbe huo ukiongozwa na Mratibu Mkuu wa Kanda ya Afrika, Asia, nchi za Oceanic na Mashariki ya mbali Fabio Webber umefanya mazungumzo na Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed kujifunza changamoto zinazowakabili mama wajawazito na watoto wachanga.

  Webber alisema Rais wa Zanzibar alipofanya mazungumzo na Balozi wa Brazil aliomba nchi hiyo kufungua ubalozi mdogo Zanzibar, kusaidia kuimarisha masuala ya afya na kuwajengea uwezo wafanyakazi wa sekta hiyo.Balozi wa Heshma wa Brazil hapa Zanzibar Abdulsamad Abdulrahim alisema baada ya Serikali ya Brazil kufungua Ubalozi mdogo Zanzibar, wanaelekeza nguvu zao juu ya afya ya mama mzazi na mtoto pamoja na kuwajengea uwezo wafanyakazi wa kitengo hicho.

  Alisema ujumbe huo utafanya ziara katika vituo mbali mbali vya afya Unguja na Pemba kuangalia changamoto zinazowakabili mama wajawazito wakati wa kujifungua na watoto wachanga na hatiamae kuzitafutia ufumbuzi.Waziri wa Afya aliueleza ujumbe huo kuwa Serikali inaendelea kuimarisha huduma za afya ya msingi vijijini ili vituo vya afya vya huko viwe na uwezo na vifaa vya kutosha na wananchi waviamini na wavitumia.

  Alisema hivi sasa kumekuwa na msongamano mkubwa wa wazazi katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja huku vituo vya afya vijijini vyenye uwezo wa kutoa huduma za kuzalisha vinakosa wazazi kutokana na dhana kuwa huduma ni ndogo.Alisema kuimarika kwa vituo vya afya vya vijijini vinavyotoa huduma ya mama na mtoto kutaipunguzia hospitali hiyo msongomano wa wazazi na kumudu kutoa huduma zilizo bora zaidi.

  Ujumbe huo umeanza kazi ya kutembelea vituo vya afya vinavyotoa huduma ya kuzalisha kuona hali halisi na kujua changamoto zinazovikabili vituo hivyo na baadae kufanya uchambuzi wa kujua masuala yanayopaswa kutekelezwa kuongeza mashirikiano .
  BALOZI wa Heshima wa Brazil hapa Zanzibar, Abdulsamad Abdulrahim (suti buluu) akiwa na Ujumbe wa wataalamu wa Afya kutoka Brazil wakitembelea Kituo cha Afya Fuoni.
  WAZIRI wa Afya Zanzibar Hamad Rashoid Mohamed akizungumza na Ujumbe wa Wataalam wa Afya kutoka Nchi ya Brazil Afisini kwake Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
  UJUMBE wa wataalamu wa Afya kutoka Brazil wakiangalia takwimu za mama wajawazito wanaofika kupata huduma ya kujifungua Kituoni hapo

  0 0


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya Kigamboni katika eneo la ujenzi wa majengo ya Ofisi ya Mkuu wa wilaya na Halmashauri ya Kigamboni.
  Kazi ya ujenzi inavyoendelea kigamboni.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akiendelea na zoezi la ukaguzi wa jengo la Manispaa ya Kigamboni.
  Ukaguzi wa maendeleo ya jengo la Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kigamboni.

  .

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo amewapongeza wilaya na Manispaa ya Kigamboni kwa kuanza ujenzi wa Ofisi za Kisasa.

  Waziri Jafo ametoa pongezi hizo alipotembelea kukagua ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na ujenzi wa Ofisi mpya za Manispaa ya Kigamboni. Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amefurahishwa na ujenzi unaoendelea wilayani humo unaojengwa na Wakala wa Majengo(TBA) chini ya mkandarasi Mshauri kutoa Chuo cha Ardhi.

  Jafo amewataka wakandarasi kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda ili watumishi wa Manispaa ya Kigamboni wapate maeneo mazuri ya kufanyia kazi. Naye, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Rahel Mhando amemuhakikishia Waziri Jafo kwamba viongozi wote wa Kigamboni wamejipanga vyema ili ujenzi huo ukamilike ndani ya muda uliopangwa.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema jana amepokea Msaada wa jengo la Choo cha kisasa chenye matundu 10 kilichojengwa katika Shule ya Msingi Kivule na kampuni ya Mafuta ya Total.

  Akipokea msaada Kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Total nchini, Tarik Moufaddal, Dc Mjema amesema kuwa Msaada huo utasaidia kwa sehemu kubwa ya wasichana ambao walikuwa wanapata tabu ya vyoo katika shule hiyo.

  Amesema kuwa shule hiyo yenye wanafunzi 3000 kwa sasa wanaweza kukabiliana na changamoto ya vyoo kwa watoto wa kike kutokana na kuongezeka kwa matundu hayo 10 ,ambayo yameelekezwa maalumu kwa ajili ya watoto wa kike.

  “kwetu sisi huu ni msaada mkubwa sana kutoka Total kwani choo hichi kimegharimu Zaidi ya Shilingi Milioni 33 za kitanzania na kampuni hii imeweza kutenga Zaidi ya Milioni 700 kwa ajili ya kusaidia sehemu mbalimbali Tanzania kwanii tayari wamejenga choo kama hiki katika shule ya msingi Yombo Dovya hivyyo sisi watu wa ilala tunaomba wasiache kutukimbia kwani bado tutaitaji msaada Zaidi ya huu”amesema Dc Mjema.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Total nchini Tarik Moufaddal amesema kuwa kampuni yake inaona fahari kuwa karibu na jamii kwa kuona inatoa msaada kwa watoto ili waweze kuwa katika mazingira mazuri na afya bora.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na Wanfunzi wa Shule ya Msingi Kivule mara baada ya kupokea Msaada wa Choo Cha Matundu 10 chenye thamani ya Milioni 33
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Total nchini, Tarik Moufaddal akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya Msingi Kivule
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kivule , Dede Lupembe akitoa neno la shukrani mara baada y kupokea choo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akiwa na Mkurungenzi Mkuu wa Total Tanzania Tarik Moufaddal wakati wa kuzindua jiwe la Msingi wa choo hicho
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akiwa na Mkurungenzi Mkuu wa Total Tanzania Tarik Moufaddal wakikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa kuanza kutumika kwa choo hicho
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akiwa na Mkurungenzi Mkuu wa Total Tanzania Tarik Moufaddal wakikagua majengo ya choo hicho kwa ndani
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akiwa na Mkurungenzi Mkuu wa Total Tanzania Tarik Moufaddal akiwa katika picha ya Pamoja na Wafanyakazi wa Total Tanzania.

  0 0

   Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiwaonyesha Mkakati wa kudhibiti upotevu wa mapato yatokanayo na biashara ya mifugo na mazao yake baada ya kuuzindua katiika ukumbi wa VETA Dodoma. Picha na John Mapepele
  Kikosi kazi kilichoandaa mkakati wa kudhibiti magonjwa ya mifugo nchini kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ( aliyekaa katikati)kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Bi Selina Lyimo, kushoto Kaimu Katibu Mkuu Uvuvi Bwana Julius Mairi.Picha na John Mapepele .


  Na John Mapepele

  WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amezindua mikakati 15 itakayotumika kama nyenzo ya kusimamia utekelezaji wa majukumu ya wizara hiyo na kuleta mageuzi makubwa na ya muda mfupi kwenye sekta za mifugo na uvuvi kabla ya kumalizika awamu ya kwanza ya utawala wa Serikali ya awamu ya tano mwaka 2020.

  Mikakati hiyo ni pamoja nakudhibiti magonjwa ya mifugo chanjo na viatilifu, mpango kazi wa kudhibiti upotevu wa mapato yatokanayo na biashara ya mifugo na mazao yake, mkakati wa usimamizi na udhibiti wa rasilimali za uvuvi nchini, mkakati wa upatikanaji wa uhakika wa malisho na maji kwa ajili ya mifugo pamoja na mkakati wa kuboresha na kuzalisha kwa wingi ng’ombe wa nyama na maziwa kwa njia ya uhimilishaji.

  Mwingine ni mkakati wa kudhibiti na kuondoa migogoro baina ya wakulima, wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi, mkakati wa kuboresha uzalishaji wa kuku,mkakati wa kuanzisha na kuwezesha ushirika wa wafugaji, mkakati wa kuendeleza ukuzaji wa viumbe kwenye maji pamoja mkakati wa kufufua Shirika la Uvuvi nchini TAFICO

  Akizungumza jijini Dodoma mara baada ya kuzindua mikakati hiyo, Waziri Mpina ameiagiza wizara hiyo kuunda kikosi kazi kitakachosimamia utekelezaji wake na kwamba kila baada ya miezi mitatu kufanyike tathmini na kwa watumishi wataoshindwa au kukwamisha utekelezaji wa mikakati hiyo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria,Kanuni na taratibu. 

  Alisema mikakati hiyo ikikamilika Serikali itaweza kukusanya zaidi ya sh bilioni 100 kwa mwaka zitokanazo na sekta za mifugo na uvuvi tofauti na sh bilioni 30 zilizokusanywa katika kipindi cha mwaka 2016/2017 ambapo kwa mwaka 2017/2018 Serikali imeweza kukusanya sh bilioni 46 baada kufanyika Operesheni Sangara na Nzagamba.

  Hivyo Waziri Mpina alisisitiza kuwa utoroshaji wa mazao ya mifugo nje ya nchi, uvuvi haramu,mifugo kufa kwa kukosa tiba sahihi za magonjwa kwa wakati havitapata tena nafasi chini ya uongozi wake huku ulinzi wa rasilimali za mifugo na uvuvi ukiimarishwa kwa kuweka vizuizi katika njia zote zilizobainika kuhusika na utoroshwaji huo.

  Alisema udhibiti wa magonjwa ya mifugo utawezesha kuongeza uzalishaji kuanzia ndege wafugwao, mbuzi, kondoo,ng’ombe na kuchochea uwekezaji katika viwanda vya kuchakata mazao ya mifugo hapa nchini na kuwezesha upatikanaji wa ajira,kodi na upatikanaji wa bidhaa za mifugo kwa gharama nafuu.

  Waziri Mpina alisema ni aibu kwa Taifa ambalo asilimia 37 ya nchi yake ni maji na yenye uoto wa asili mzuri lakini tunashuhudia mifugo ikidhoofika na mingine hata kufa kwa kukosa maji na malisho hivyo mkakati huo utatoa majawabu ya changamoto hiyo.

  Pia alishangazwa na kitendo cha baadhi ya watu wakihodhi mashamba ya mifugo ya Serikali waliobinafsishiwa na kubadilishiwa matumizi na kwamba kwa miaka mingi wameshindwa kuendeleza mashamba hayo hivyo Serikali itayataifisha yote na kurejeshwa serikalini ili yatumike kulishia mifugo.

  Pia mikakati hiyo itamaliza kabisa tatizo la wafugaji kukosa haki ya kupata malisho kutokana na migogoro ya ardhi huku akitolea mfano mnada wa Pugu wenye ukubwa wa ekari 1,900 lakini sasa zimebaki ekari 108 tu baada ya wananchi wengi kuvamia eneo la mnada na kugeuza makazi.

  Waziri Mpina alisema mikakati hiyo ndio itakuwa mwarobaini wa matatizo yote yaliyokuwa yanakabili sekta ya mifugo na uvuvi , na kuziagiza halmashauri zote nchini nazo zishiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mikakati ili kuiwezesha sekta ya mifugo na uvuvi kutoa mchango unaostahili katika pato la taifa.

  Hivyo Wizara itaandaa mafunzo kwa maofisa Mifugo na Uvuvi kutoka katika halmashauri zote nchini mwezi Agosti ili kuwawezesha kuufahamu mkakati huo na kuutekeleza kwa umakini na kwa wakati.

  Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu-Mifugo, Celina Lyimo alisema kuandaliwa kwa mikakati hiyo ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mpina alilolitoa Julai 6 mwaka huu la kutaka kuandaliwa mikakati ya kuwezesha kuwepo mageuzi katika sekta hizo na kuwataka watumishi wa wizara hiyo kuifanyia kazi kwa wakati weledi na uadilifu ili kupata matokeo chanya katika kipindi kifupi.

  Naye Kaimu Katibu Mkuu-Uvuvi, Julius Mairi alisema mikakati hiyo itawezesha sekta za mifugo na uvuvi kuwezesha kuongeza pato la Taifa na mtu mmoja mmoja na kumshukuru Waziri Mpina kwa uongozi wake thabiti uliolenga kuona kunakuwepo mageuzi ya haraka kwenye sekta hizo.

  0 0

  Mbunge wa Singida Magharibi, Mheshimiwa, Elibariki Kingu, akihutubia katika hafla ya kuwapokea viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri kutoka Marekani waliotembelea Zahanati ya Kanisa hilo ya Kijiji cha Msungue iliyopo Kata ya Sepuka mkoani Singida jana. Zahanati hiyo inasimamiwa na kanisa hilo Dayosisi ya Kati. Dotto Mwaibale
  Mkurugenzi anayesimamia Hospitali na Zahanati za Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kati, Mchungaji Manase Msengi, akimuonesha picha ya vitanda vya Hospitali vinavyo sambazwa na Bohari ya Dawa (MSD), Mkurugenzi wa Uhusiano Kati ya Sinodi ya Kusini Mashariki ya Minessota na makanisa ya nje ya Marekani, Callemia Chatelaine. Kushoto ni Mganga wa zahanati hiyo.
  Mganga wa zahanati hiyo akiwaelekeza jambo wageni hao walipotembelea chumba cha maabara cha zahanati hiyo.
  Mkurugenzi anayesimamia Hospitali na Zahanati za Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kati, Mchungaji Manase Msengi, akiwaelekeza jambo wageni hao eneo ilipofungwa mfumo wa maji katika zahanati hiyo.
  Muonekano wa meza kuu katika hafla hiyo.
  Wananchi wa Kijiji cha Sengue wakiwa kwenye hafla hiyo.
  Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa Kata ya Sepuka, Juma Mghenyi akizungumza kwenye hafla hiyo.
  Wageni hao wakifurahi ngoma ya utamaduni iliyokuwa ikipigwa na wasanii kutoka kikundi cha umoja cha Kijiji cha Sengue.
  Mbunge Elibariki Kingu, akicheza sanjari na wasanii wa kikundi cha umoja cha Kijiji cha Sengue.
  Askofu Steve Delzar kutoka Sinodi ya Kusini Mashariki (Minessota) ya Makanisa ya nje ya Marekani, akicheza pamoja na wasanii wa kikundi cha Umoja cha Kijiji cha Sengue Kata ya Sepuka.
  Wasanii wa kikundi cha Umoja wakitoa burudani.
  Viongozi wa chama, Kanisa la KKKT na Serikali wakiwa kwenye hafla hiyo.

  0 0

  Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kuahidi kuwasaidia watoto wenye saratani ambao wanatibiwa katika hospitali hiyo.

  Katika ziara hiyo balozi huyo alimtaka Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tumaini la Maisha (TLM) katika hospitali hiyo, Dkt. Trish Scanlan kumwandikia mahitaji ambayo watoto hao wanapaswa kupatiwa ili aweze kushiriki katika kuwapatia tiba pamoja na mambo mengine. 

  Balozi huyo aliongozana na Naibu Mwenyekiti wa Red Crescent kutoka Kuwait, Anwar Alhasawi, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Suleiman Salehe pamoja na pamoja na viongozi mbalimbali wa Lions Club ambayo imekuwa ikiwasadia watoto hao mahitaji mbalimbali.

  Pia, balozi huyo alitembelea watoto wenye saratani katika jengo la watoto pamoja na kuwapatia zawaidi mbalimbali ikiwamo vifaa vya kuchezea.
  Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa mwezi imekuwa ikipokea wastani wa watoto 30 hadi 40 wenye saratani ya aina mbalimbali. Wengi wa watoto wanaopokelewa wamekuwa wakisumbuliwa na saratani ya damu, jicho, figo na saratani ya matezi.
   Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem akimkabidhi zawadi mmoja wa kina mama, Martha John Zakaria anayemuuguza mtoto wake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kushoto ni Naibu Mwenyekiti wa Red Crescent kutoka Kuwait, Anwar Alhasawi na mwakilishi wa Jumuiya ya Red Crescent, Mayouf Alenezi.
   Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem akizungumza na wazazi wa watoto ambao wanatibiwa saratani katika hospitali hiyo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Suleiman Saleh na Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Red Crescent kutoka Kuwait, Anwar Alhasawi.
   Wazazi na watoto wakimsikiliza balozi huyo katika jengo la watoto.
   Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem akizungumza na Ofisa Mtendaji wa Tumaini la Maisha (TLM), Dkt. Trish Scanlan  baada ya ofisa huyo kumweleza mahitaji wanahitaji watoto wanaotibiwa saratani katika hospitali hiyo.  Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Suleiman Saleh, kulia ni Naibu Mwenyekiti wa Red Crescent kutoka Kuwait, Anwar Alhasawi (mwenye koti) na wengine ni wawakilishi wa Jumuiya ya Red Crescent.
  Balozi huyo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto baada ya kupewa zawadi mbalimbali.

  0 0

   Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akisalimiana na Mkuu wa Kiwanda cha Viatu Gereza Kuu Karanga, Moshi, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Hezron Nganoga alipotembelea kiwanda hicho kukagua maboresho ya ufungaji wa mashine mpya za kutengenezea viatu vya aina mbalimbali ikiwemo buti zinazotumiwa na Majeshi ya Ulinzi na Usalama hapa nchini leo Agosti 1, 2018.  Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiangalia mtambo maalum wa kukata ngozi zinazotumika kutengenezea viatu. Mtambo huu ni mpya na ni sehemu ya maboresho katika kiwanda hicho.
   Mtaalam kutoka nchini Italia akijaribisha mashine mpya ambazo zimefungwa katika Kiwanda hiki cha uzalishaji wa viatu cha Gereza Kuu Karanga(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike.
   Maofisa Wataalam wa Jeshi la Magereza wakiendelea na majaribio ya mashine mpya katika mradi wa ubia uliokuwa mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF na Jeshi la Magereza. 
   Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiangalia buti la jeshi ambalo limetengenezwa kiwandani hapo. Wengine wakiangalia viatu hivyo ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa uliokuwa mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF, Hosea Kashimba(wa pili kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Onesmo Buswelu.
  Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Hassan Mkwiche (wa pili kulia) akionesha eneo la uwekezaji wa kiwanda kipya katika awamu ya pili ya mradi wa kiwanda cha viatu chini ya Kampuni ya Kiwanda cha viatu Karanga (wa pili kushoto) ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Viwanda vya ngozi – Gereza Kuu Karanga, Bw. Masoud Omary (wa tatu kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Makao Makuu ya  Jeshi la Magereza).

  0 0


  0 0

  Na. Vero Ignatus  Ngorongoro

  OXFAM kwa kushirikiana na Shirika la PALISEP wameendesha mafunzo ya teknolojia ya kidigitali kwa wananchi wilaya ya  Ngorongoro mkoani Arusha ili kuleta  maendeleo katika jamii husika. 

  Maratibu wa Teknolojia kwa maendeleo shirika la Oxfam Bill Marwa amesema  wametoa mafunzo kwa wananchi zaidi ya (90)yakiwa na lengo la wao kutambua namna ya kuitumia mitandao hiyo pamoja  nyenzo mbalimbali za kidigital kwa kutuma ujumbe mfupi, kutoa taarifa kwa viongozi wao wa kijiji,kujibuwa changamoto wanazokutana nazo kwaajili ya kujiletea maendeleo.

   "Kadri miaka inavyoenda kumekuwa na ongezeko la mitandao ya kijamii ulimwenguni hivyo Oxfam kama shirika limeona upo umuhimu wa maendeleo, kupata taarifa, kutoa matokeo"alisema Bill Marwa.Washiriki wa mafunzo hayo walifundishwa sheria za mtandao 2015 pamoja na makosa ya mtandaoni, jinsi ya kutumia vifaa hivyo katika namna ambayo havivunji sheria ya nchi. 

  Sambamba na hayo walifundishwa maswala Mbalimbali jinsi ya ukingi haswa kwa wanawake kulinda haki za mwanamke na kupinga ukatili wa kijinsia dhidi yao.Mafunzo hayo yaliyokuwa ya siku nne yaliyoshirikisha kata zaidi ya 10 katika wilaya ya Ngorongoro,ikiwa ni mradi wa  miaka miwili unaotekelezwa katika mikoa (4) Arusha, Geita,Kigoma,na Mtwara katika wilaya za Mtwara vijijini, Mbogwe Geita, Kibondo,na Ngorongoro. 

  Mradi huo unalengo la kuwawezesha wananchi kutumia nyenzo za digitali ili kujiletea maendeleo katika jamii husika,amabapo ulianzishwa rasmi mwaka 2016 desemba na unatarajiwa kumalizika novemba 2018 ,mradi huo upo chini ya ufadhili kutoka nchini Ubelijiji. 
   Baadhi ya wananchi wakifuatilia kwa makini kile kinachofundishwa kuhusiana na matumizi ya digitali sambamba na mitandao ya kijamii
  Meneja wa Program Shirika la Oxfam Kefar Mbogela akitoa Elimu namna ya kutumia mitandao na nyenzo mbalimbali za kidigitali bila kuleta madhara kwa jamii wala kuvunja sheria ya mitandao hiyo
  Rachel yeye anasema mwanzoni alikuwa akitumia simu ya hali ya chini ambayo alikuwa hapati mambo mengi ya faida ,ila kwa sasa mara baada ya kupewa simu na Oxfam imemsaidia sana kuweza kuwasiliana na na jamii ,amesema kwasasa anaweza kupaza sauti kwa kutumia simu yake,kutatua changamoto mbalimbali na viongozi wanapoona ujumbe wake wanatatua tatizo na majibu yanapatikana kwa wakati.
  Darasa la mafunzo ya kutumia nyenzo za mitandao ya kijamii na namna ya kutumia nyenzo za kidigitali yakiendelea.
  Ndugu Ezekiel Ndukumat kutoka Kijiji cha Pinyinyi tarafa ya Sale wilaya ya Ngorongoro amesema yeye anapata habari za kila sehemu kwa muda wowote ,pia jamii yake imenufaika kupitia , uragabishi wa kutumia njia ya digitali,ujumbe unakwenda kwa haraka na wanapata majibu kwa wakati.
  Norkitoi Lengela kutoka kijiji cha Piyaya kata ya Piyaya wilaya ya Ngorongoroanasema amepata faida kubwa sana kupata simu kwani ameelewa jinsi dunia inavyokwenda tofautina awali,pia amefahamu kuwa ipo faida ya kuisaidia jamii yake,pia ukaribu wake na viongozi wa kijiji,amesema tukio likitokea kijijini kwake anaitwa na kuambiwa alirushe ili waweze kupata msaada wa haraka.
  Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya KONCEPT inajihuisha na masuala la ya ushauri wa masoko,matangazo,mahusiano kwa umma na mitandao yakijamii  Krantz Mwantepele akitoa elimu lwa wananchi wa Ngorongoro namna ya kutumia simu zao kwa faida .

  Mafunzo yakiendele namna ya kutumia Digitali kwa kuleta maendeleo katika jamii husika na kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji na kutatua changamoto mbalimbali zilizopo.
  Wananchi wakifuatilia kwa makini kile kinachofundishwa kuusiana na matummizi ya mitandao ya kijamii na nyenzo mbalimbali za kidigitali
  Wananchi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupata mafunzo namna ya kutumia mitandao ya kijamii na nyenzo za kidigitali Loliondo(w)Ngorongoro  mkoani Arusha.
  Wananchi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupata mafunzo namna ya kutumia mitandao ya kijamii na nyenzo za kidigitali katika Hotel ya Flamingo Safari iliyopo (w)Karatu mkoani Arusha. Habari / Picha :VERO IGNATUS 


  0 0



  Na WAMJW - KAGERA

  Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile amepiga marufuku kwa hospitali na vituo vyote vya kutolea huduma za Afya nchini kuonesha miziki katika maeneo yote yakutolea huduma na kuwataka kuweka jumbe zinazohusu Elimu Afya kwa umma pindi wanapongoja kupata huduma.

  Ameyasema hayo mapema leo wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika ukumbi wa halmashauri ya Muleba katika Mkoa wa Kagera."Ni marufuku kwa hospital zote kuonesha miziki katika maeneo yote ya utoaji huduma za afya" alisema Dkt Ndugulile.

  Pia Dkt. Ndugulile amemwagiza Mganga mkuu wa Wilaya ya Ngara DKt. Revokatus Ndyekobora kuhamasisha wananchi Juu ya umuhimu wa kuudhuria kliniki kwa mama mjamzito walau mara nne ndani ya kipindi chá ujauzito wake na kuhakikisha wanajifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya.

  "Tuongeze kasi katika kuhamasisha wakina mama wajawazito kuhudhuria kliniki, na kwenda kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya" alisema Dkt Ndugulile. Pia alisema kuwa Serikali inaendelea kuboresha sekta ya Áfya nchini kwa kutoa pesa ya ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za Afya na kuhamasisha ushirikishwaji wa wananchi katika ujenzi wa vituo hivyo (Forced account)

  "miundombinu tunaendelea kuboresha, Mkoa mzima tumeleta shilingi Bilion 5.9 kwaajili ya kuboresha vituo vya Áfya, viwili vikiwa katika Wilaya ya Ngara "alisema Dkt Ndugulile .

  Kwa upande mwingine Dkt Ndugulile aliendelea kusema kuwa katika kuelekea kuboresha huduma za afya Serikali imeanzasha utaratibu wa kituo nyota kwa vituo vya Áfya, hospitali na Zahanati, na kutoa maagizo kwa Halmashauri zote nchini kuhakikisha Asilimia 80 ya vituo vyake vyote vya kutolea huduma za Afya havishuki chini ya nyota tatu (3)

  "Serikali imeanzisha utaratibu wa kutoa madaraja ya Ubora kwa vituo vyote vya kutolea huduma za Afya , tunaanzia nyota sifuri kwa maana Kwamba kiwango chako chá Ubora ni chá chini sana Mpaka nyota 5 ambacho kiwango chako ni chá juu sana, tunataka Asilimia 80 ya Vituo vyao vyote katika kila halmashauri visipungue nyota tatu" Alisema Dkt Ndugulile.

  Mbali na hayo Dkt Ndugulile amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Ngara. Luten.... Kuimarisha usimamizi katika ngazi zote za Wilaya ili kuweza kufikia Ubora wa huduma za afya kwa Asilimia 80 katika vituo vyake vyote.

  Nae Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ngara Dkt Revokatus Ndyekobora amesema kuwa lishe duni kwa watoto hasa walio chini ya Miaka 5 bado imekuwa tatizo na kusema kuwa wameweka mikakati thabiti yakuweza kupambana dhidi ya tatizo lá lishe duni. "Hali ya Lishe bado ni shida, ambapo tunaendelea kupambana nayo na tayari tumeweka mikakati thabiti yakuweza kupambana dhidi ya lishe duni " alisema

  DKt. Revokatus Ndyekobora aliendelea kusema kuwa Wilaya ya Ngara ináupungufu wa watumishi kwa Asilimia 59.2 jambo linaloleta changamoto katika utoaji wa huduma za afya.

  " Tuna upungufu wa watumishi kwa Asilimia 59.2 , Kwaiyo tunafanya kazi katika hali ya upungufu, tunamshukuru tumepata watumishi 36, lakini waliripoti 33, na juzi TAMISEMI waliondoa watumishi 2" alisema Dkt Revokatus Ndyekobora


  Naibu Waziri wa Áfya Dkt Faustine Ndugulile akikagua vifaa vya maabara katikati hospitali ya Wilaya ya Ngara mkoa wa Kagera
  Naibu Waziri wa Áfya Dkt Faustine Ndugulile akikagua cheti cha Mtoto pindi alipotembelea wodi ya Watoto katika hospitali ya Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera
  Naibu Waziri wa Áfya Dkt Faustine Ndugulile akiwaonesha nembo ya vifaa vya Serikali Kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Biharamuro Sada Malunde (wakushoto).

  0 0

  *Awaambia katika hilo hakuna 'Neutral', agusia uwajibikaji 
  *Akumbusha Kafulila alivyoitwa Tumbili kwenye sakata la IPTL

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  RAIS Dk.John Magufuli amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali nchini kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kikamilifu na kusimamia vema utekelezaji wa Ilani.

  Amesema kuna watendaji wa Serikali ambao wamekuwa wakidai hawawezi kufuata Ilani kwa madai ya kuwa wapo Neutral na kwamba katika hilo hakuna Neutral kwani lazina Ilani itekelezwe.

  Dk.Magufuli ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa tukio la kuwaapisha wakuu wa mikoa, Makatibu wakuu,manaibu makatibu wakuu pamoja na makatibu tawala ambao aliwateua mwishoni mwa wiki iliyopita..
  Hivyo baada ya kuwaapisha viongozi hao Rais Magufuli amehimiza utendaji kazi kwa viongozi wa ngazi mbalimbali ili kuwatumikia vema Watanzania.

  Amesema kuwa nchi yetu idadi ya watu ni milioni 55 hivyo waliopata nafasi imetokana na mipango ya Mungu na si kwa matakwa yao.Ameongeza kila aliyekuwa kwenye nafasi atambue yupo hapo kwasababu Mungu ameeamua na hata yeye kuwa Rais ni mpango wa Mungu.

  Hivyo amewataka viongozi wote kwa ngazi mbalimbali kuanzia juu mpaka chini kila mmoja kwa nafasi yake afahamu yupo hapo kwasababu Mungu ametaka iwe hivyo na lazima wafanye kazi.Wakati anahimiza utendaji kazi na ushirikiano ameeleza umuhimu wa watendaji wa Serikali kuisimamia na kuitekeleza Ilani ya uchaguzi mkuu.

  Amefafanua kuna watendaji wa Serikali ambapo wakienda kutekeleza majukumu yao wanasema wao ni watendaji wa Serikali na wapo Neutral.Amewataka wafahamu watendaji wa Serikali wanatakiwa kutekeleza Ilani ya CCM na katika hill lazima watambue hakuba bahari ya Neutral."Mimi ni Rais ninayetokana na CCM ,Makamu wa Rais ni wa CCM na Waziri Mkuu pia anatokana na CCM,"amesema na Rais Magufuli na kufafanua kila mmoja lazima ashiriki kuitekeleza Ilani hiyo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

  Wakati huo huo Rais Magufuli amesema wakati anafanya uteuzi wa majina kwa ajili ya nafasi hizo alikuwa katika wakati mgumu lakini amefanikisha kuwapata,hivyo ambao wamepata nafas hizo wakafanye kazi kwa maslahi ya Watanzania wote.Pia amehimiza watumishi kushirikiana ili kufikia lengo la kuleta maendeleo na kufafanua kuna baadhi ya maeneo kati ya kiongozi na kiongozi hawana ushirikiano jambo ambalo si nzuri.

  Amefafanua yeye pamoja na viongozi wenzake akiwemo Makamu wa Rais ni Waziri Mkuu wamekuwa na ushirikiano mkubwa na wanapeana taarifa ya kila jambo na ndio maana shughuli zao zinakwenda vizuri." Viongozi ambao nimewateua na kuwaapisha leo, nendeni mkafanye kazi kwa ushirikiano na viongozi ambao mtawakuta huko pamoja na wananchi wote,"amesema Rais Magufuli.

  Kuhusu kuchagua wapinzani amesema Tanzania haina mpinzani bali kuna watanzania ambao wapo kwa ajili ya kushiriki katika kuleta maendeleo.Ametoa mfano David Kafulila alikuwa mstari wa mbele katika kukemea suala la IPTL hadi akafananishwa na tumbili."Hakuna aliyekuwa anafurahishwa na IPTL.

  "Lakini Kafulila amebaki kuwa yule yule,hivyo unapomteua kumpa nafasi maana yake ni kuongeza nguvu katika kuleta maendeleo na suala la maendeleo halina chama." Pia unapokuwa vitani halafu mkafanikiwa kuchukua vifaru na mizinga kinachotakiwa ni kuitumia hivyo mizinga badala ya kuiweka mahali,"amesema Rais Magufuli.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

  Baadhi ya walimu wa shule za sekondari nchini ambao wameshiriki katika maonesho ya Young Scientists Tanzania yanayoendelea katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere, wamekubali kuwa wao ndio wamekuwa wazito kubadilika na mazingira ya teknolojia ya ufundishaji katika karne hii ya 21.

  Hayo yamesemwa na Mtalaamu wa Mawasiliano kutoka Dot Tanzania , Ndimbumi Mwisongole alipokuwa akitoa majumuisho kwa walimu hao ambao wameshiriki mafunzo maalumu yaliyaondaliwa na Mfuko wa Ufadhili na Kuendeleza Ubunifu na Maendeleo ya watu (HDIF).

  “tumeweza kuzungumza na walimu Zaidi ya 50 ambao wameshiriki warsha hii na wote wamekiri kuwa wao ndio wamekuwa wazito kubadilika kutokana na Teknolojia inavyokwenda katika sekta ya elimu.

  Mwisngole amesema kuwa umefika wakati wa Walimu kuanza kubadilika na kutumia mtandao kwa ajili ya kupata matirio ya kufundishia ambayo wameyapata popote wanaposafiri kwenda kufundisha” amesema Mwisongole.Mwisongole ametoa wito kwa walimu wote kote nchini kuanza kutumia mtandao kwa ajili kujipatia matio ya kufundushia nakuacha kufikiaria kutembea na mavitabu mengi wakati wanaweza kutimia mtandao kuhifadhi kazi zao.

  Kwa upande wake Mtengenezajai wa Vikaragosi vya Ubongo Kids Nisha Ligon amesema kuwa programu yake imekuwa kivutio kikubwa sana kwa watoto na kusaidia kuongeza uelewa mashuileni .
  Kiongozi Mkuu wa Shirika la Ufadhili wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Binadamu(HDIF), David Mc. Ginty akizungumza na Walimu wanaoshiriki Maonesho ya Wanasayansi Chipukizi ambapo tasisi yake ya HDIF ilipata Wasaa wa kutoa Mhadhara juu ya Ubunifu kwa walimu wa Masomo ya Sayansi Jijini Dar es Salaam.
  Meneja Mawasilinao wa Taasisi Digital Opportunity Trust (Dot Tanzania), Ndimbumi Mwesongole akizungumza na Walimu kuhusu progarmu ya elimu kupitia mtandao kwa walimu kujipatia mtandao.
  Mwanzilishi na Muongozaji wa Programu ya Vikaragosi vya kufundishia vya Ubongo Kids , Nisha Ligon akizungumza kuhusu uzoefu wake wa kufundisha kwa kutumia Vikaragosi kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari .
  Mmoja wa Walimu walioshiriki katika Warsha hiyo iliyoandaliwa na HDIF akichangia mada wakati wa mafunzo.
  Sehemu ya Walimu walioshiriki katika Mafunzo hayo wakifatilia kwa makini mafunzo yanayotolewa na wataalamu.

  0 0

  NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO

  Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na taasisi ya WEPMO (Water and Environmental Sanitation Projects Maintanance Organisation) imewahimiza wananchi kujenga vyoo bora kwani inaonyesha kaya zenye vyoo vilivyoboreshwa vyenye kutumia maji na sakafu inayosafishika ni asilimia 50 pekee.

  Pande hizo zipo katika utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa afya na usafi wa mazingira kwa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo.Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Fatuma Latu akizungumza katika utambulisho wa mradi huo utakaotekelezwa kupitia kampeni ya “Usichukulie Poa nyumba ni Choo” alisema, halmashauri imekuwa ikifanya uhamasishaji huo kupitia maafisa afya wa kata kila mara.

  "Mradi huu unatekelezwa katika kata zote 11 za halmashauri ambapo wananchi wanahamasishwa kujenga vyoo bora kwa bei nafuu na kuelimishwa juu ya umuhimu wa kila nyumba kuwa na choo bora" alisema Fatuma.Fatuma aliiwashukuru taasisi ya WEPMO kwa kuja kuongeza nguvu katika uhamasishaji huu wa ujenzi wa vyoo bora.

  Alielezea “Ni lazima kila mmoja afanye wajibu wake, wataalam wawajengee wananchi uelewa juu ya ujenzi na utumiaji wa vyoo bora""Ni vyema wananchi wakaelewa kwanza kabla watendaji wa kata hawajatumia nguvu na sheria kwa watakaokaidi kujenga na kutumia vyoo bora katika kaya zao kwa kuwafungulia mashauri katika mabaraza ya kata”alisisitiza.

  Nae mratibu wa mradi huu wa uboreshaji wa afya na usafi wa mazingira katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Renatus Rweyemamu alisema katika utafiti wa awali uliofanywa na taasisi hiyo, hali ya afya na usafi wa mazingira inaonesha asilimia 84 pekee ndio wananchi wenye kaya zenye vyoo vya kawaida.

  Alisema , yaani aina yoyote ya choo kinachotenganisha kinyesi na mazingira hata vile visivyosafishika, ilihali, kaya zenye vyoo vilivyoboreshwa vyenye kutumia maji na vyenye sakafu inayosafishika ni 50% .Rweyemamu alielezea , vyoo vyenye vifaa vya kunawia mikono zikiwa ni asilimia 18 pekee. 

  Alifafanua ,lengo la mradi huo ni kuongeza ufahamu kwa wananchi kutambua athari za kujisaidia ovyo katika mazingira .
  Mratibu wa mradi wa Uboreshaji sekta ya Afya na usafi wa mazingira H/W Bagamoyo Renatus Rweyemamu akitoa maelezo ya mradi kwa wataalm wa halmashauri.( picha na Mwamvua Mwinyi)
  Afisa Afya Wilaya ya bagamoyo Bi. Joyce Nganzo akichangia mada wakati wa utambulisho wa mradi wa uboreshaji sekta ya Afya na Usafi wa mazingira Bagamoyo.
  1. Picha ya pamoja ya wataalamu wa Halmashauri, Watendaji wa kata za bagamoyo na wataalamu wa Taasisi ya WEPMO mara baada ya utambulisho wa mradi wa uboreshaji sekta ya Afya na usafi wa mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya bagamoyo.( picha na Mwamvua Mwinyi)

  0 0

  SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesisitiza kuwa huduma za uzazi kwa wajawazito zinatolewa bila ya malipo katima Hospitali na vituo vya afya vya Serikali. 

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa ziara yake ya kujua hali ya utoaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa Temeke, Amana na Mwananyamala leo jijini Dar es salaam. 

  "Nimesikia pale wajawazito wameniambia wamekuja na vifaa vya kujifungulia kutoka majumbani mwao sitaki kusikia mwanamke mjamzito analipishwa wala kuja vifaa vya kujifungulia kwani sera yetu inasema huduma za uzazi ni bure" alisema Dkt. Ndugulile. 

  Aidha Dkt. Ndugulile alisema kuwa wanawake wajawazito , watoto chini ya miaka 5 na wazee wasio na uwezo wanapata matibabu bure kulingana na sera ya Afya inavyosema. Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa kila mtoa huduma anapaswa kuandika taarifa ya mgonjwa kabla na baada ya kumpa huduma katika kituo chake cha kazi.Aidha Dkt. Ndugulile aliwataka watoa dawa katika hospitali na vituo vya afya kuandika majina asilia ya dawa na siyo yale ya kampuni pamoja na kufuata muongozo wa dawa uliyowekwa na Serikali. 

  "Marufuku watoa dawa kuwaandikia wagonjwa dawa na kwenda kununua nje ya kituo cha afya na badala yake dawa zote zitolewe katika hospitali au kituo cha afya kama zimeisha zinatakiwa kuagizwa kwa haraka na nauagiza uongozi wa Hospitali ya Amana kuwarudishia wagonjwa wa wodi ya watoto waliokwenda kununua dawa nje leo hii " alisema Dkt. Ndugulile. 

  Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Temeke Dkt. Amaan Malima amesema kuwa changamoto kubwa inayowakumba ni upungufu wa watumishi .

  Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Hospitali ya Rufaa ya Amana Dkt. Meshack Shimwela amesema kuwa anaomba radhi kwa tatizo hilo lililojitokeza kwani hakuna tabia kama hiyo hospitalini hapo na amehaidi kulifanyia kazi haraka iwezekanavyo.
  Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwajulia hali baadhi ya wagonjwa waliofika kupata huduma kwenye Hospitali ya Rufaa Temeke wakati wa ziara yake ya kujua hali ya utoaji huduma za afya Hospitalini hapo.
  Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua akiangalia dawa zinazopatikana katika Stoo ya dawa ya Hospitali ya Rufaa Amana wakati wa ziara yake katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam. 
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua taarifa za maabara katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke leo jijini Dar es salaam, katikati ni Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Amaan Malima.

older | 1 | .... | 1636 | 1637 | (Page 1638) | 1639 | 1640 | .... | 1897 | newer