Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1634 | 1635 | (Page 1636) | 1637 | 1638 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Na Emmanuel Massaka, Blogu ya jamii

  NAIBU Waziri wa Nishati Subira Mgalu ameendelea na ziara yake Mkoani Mtwara kukagua miradi na kuangalia utekelezaji  wa huduma ya umeme kwa wananchi mkoani huo.

  Katika ziara yake Mgalu ameeleza kuwa kwa mwaka huu wananchi wa kata ya Chipuputa wataunganishiwa huduma ya umeme kwa bei ya shilingi elfu  99 ,gharama ambayo Tanesco iliwatangazia Wananchi tangu hapo awali.

  Aidha Waziri Mgalu ameagiza kuwa bei hiyo ya elfu 99 walizoahidiwa na shirika hilo kipindi cha nyuma, ndizo zitakazotumika kuwaunganishia huduma ya umeme kwa wananchi wa kata ya Chipuputa kijiji cha Kagera.

  "Takribani bilioni 1 zimetumika kwenye mradi huo, hivyo wananchi watakaokosa nafasi mwaka huu,waondoe hofu kwani  kuna nafasi zitaongezwa ambazo zitawafikia wakazi wa Mtwara'',alisema Waziri Mgalu na kuongeza kuwa amemwagiza Meneja wa Tanesco kuandaa orodha ya wananchi waliojiandikisha kupata huduma hiyo ili wapatiwe  huduma ya kwa wakati kama ilivyopangwa.

  Mgalu amesema kuwa kwa mwaka huu wananchi wa kata ya Chipuputa wajiandae kupokea umeme ,kwani ujio wa huduma hiyo itawasaidia katika shughuli za kukuza uchumi wao.Aidha wakazi wa Chipuputa wameshukuru kwa ujio wa Naibu Waziri na kueleza kuwa changamoto iliyodumu kwa muda mrefu sasa imetatuliwa.

  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kata ya Chipuputa kijiji cha Kagera mkoa wa Mtwara , ambapo alimuagiza Meneja wa Tanesco kuhakikisha wananchi wanaunganishwa umeme kwa bei ya zamani ya shilingi 99,000.

  Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mtwara wakikagua maendeleo ya mradi wa mashine mbili mpya za kuzalisha umeme katika Halmashauri ya Mtwara.

  Muonekano wa mashine mbili mpya za kuzalisha umeme zinazoendelea kufungwa katika Halmashauri ya Mtwara.
  Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akimsikiliza msimamzi wa mradi wa ujenzi wa mashine mbili mpya za kuzalisha umeme, Mhadisi Mkulugwa Chinumba namna mradi huo unavyofanya kazi.

  0 0

  WAFANYABIASHARA wa Soko la Mabibo, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam wamemuomba Rais John Magufuli kuingilia kati na kuzuia mpango wa manispaa kuwaondoa wafanyabiashara hao na kuwahamishia Soko la Simu 2,000.

  Akizungumza na waandishi wa habari Mmoja wa Wafanyabiashara George Mligo alisema, viongozi wa Manispaa ya Ubungo wamewataka wahame katika soko hilo ambalo linauza mazao na matunda mbalimbali.

  Mligo alisema wanamuomba Rais Magufuli aingilie kati sakata hilo ili kupata ufumbuzi. Mligo alisema, awali waliambiwa watapelekwa soko la Makuburi lakini baadae walipewa taarifa kuwa eneo hilo lipo karibu na mto hivyo wanapaswa kuhamishiwa Soko la Simu 2,000 ambalo ni dogo.

  Alisema katika soko la Mabibo kuna zaidi ya wafanyabiashara 4,000 ambao wanauza viazi, ndizi, nyanya, vitunguu, matunda na mbogamboga.“Kilio kikubwa tulichonacho wafanyabiashara wa soko la Mabibo, Serikali imeshindwa kututafutia soko lenye hadhi ya Kimataifa kama walivyoahidi na kinyume chake wanataka kutupeleka soko la Simu 2000 ambalo haliwezi kupokea zaidi ya watu 1,500 huku sisi hapa tupo zaidi ya 4,000,” alisema.

  Mligo alisema, mchango wa soko hilo kwa mwezi ni zaidi ya Sh. Milioni 120 hivyo kitendo cha manispaa kuwaondoa katika eneo hilo kitapoteza fedha nyingi.Akizungumzia kadhia hiyo Mfanyabiashara Swadaka Magesa alisema, hawapo tayari kuhama katika soko hilo kwani hoja za Serikali hazina mashiko kwa sasa hasa kwa kukosa eneo ambalo linaweza kuwatosha.

  Magesa alisema iwapo watapatiwa eneo lenye sifa ya kupokea wafanyabiashara zaidi ya 4,000 na magari 130 kwa wakati mmoja watahama kwani wanaamini watafanya biashara kwa uhuru.“Kusema kweli Simu 2,000 sio sehemu sahihi ya sisi kuhamia kwani hata vitengo viwili haviwezi kuingia kwani eneo ni dogo hadi tunawaita tumeandika barua hadi kwa Rais Magufuli kumuomba aje kuona hali hii ili atusaidie,” alisema.

  Akizungumzia sakata hilo Meya wa Manispaa hiyo Boniface Jacob, alisema, sio kwamba wanawahamisha ila ni mwenye eneo ambaye ni Kiwanda cha Urafiki kuhitaji eneo lake.“Sio kwamba tunawahamisha, Urafiki wanataka eneo lao ambalo wanalimiliki kisheria sasa sisi tufanyeje.

  “Eneo ambalo tunaweza kuwahamishia ni Simu 2,000 kwani manispaa haina maeneo, lakini naomba umtafute Mkurugenzi ataeleza kila kitu,” alisema.Mkurugenzi wa Ubungo, John Kayombo simu yake iliita bila kupokelewa na baadae alituma ujumbe kuwa hawezi kuzungumza.
  Mmoja wa Wafanyabiashara wa Soko la Mabibo George Mligo akieleza kwa hisia juu ya kuchukizwa na zoezi la wao kutolewa katika soko hilo 

  0 0

  Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya PETROBENA EAST AFRICA LIMITED Peter Kumalilwa mipango ya kampuni hiyo katika kumkwamua mkulima wa Tanzania.  Kampuni ya usambazaji ya Pembejeo ya PETROBENA EAST AFRICA LTD imeanza kuunga mkono kwa vitendo Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungwano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli kwa kuhakikisha wanafikisha pembejeo za kilimo kwa wakati kwa wakulima nchini.

  Akiongea leo mkoani Morogoro katika mafunzo ya matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo kwa maafisa kilimo na wasambazaji wa pembejeo,Mkurugenzi wa Kampuni ya PETROBENA Peter Kumalilwa amesema wameamua kuweka Ghala kubwa mkoani Morogoro ili kuhakikisha wakulima wa mkoa huo na mikoa jirani wanapata pembejeo kwa haraka kupitia wauzaji wadogo na wakubwa.

  Kumalilwa amesema PETROBENA ikiwa wakala mkuu wa kampuni ya Mbolea ya YARA watahakikisha mbolea inapatikana katika katika kipindi chote na siyo kama ilivyo sasa katika maeneo mengi ambapo mbolea inaanza kupelekwa wakati wa msimu hali inayosababisha kuchelewa kutokana na ubovu wa miundo mbinu pamoja na umbali wa walipo wahitaji.

  Ameongeza kuwa katika mkoa wa Morogoro wanatarajia kuwa na wauzaji wa pembejeo wapatao 700 katika wilaya zote sita ambao watapewa mafunzo ya matumizi bora ya pembejeo itakayowasaidia kuwapa elimu wakulima wa mazao mbali mbali mkoani humo wakiwemo wa Miwa,Mpunga,Mahindi,Mboga mboga na mazao mengine.

  Naye Afisa Biashara wa kampuni ya YARA nyanda za juu kusini John Meshak amesema wameamua kuzindua ghala la mbolea Morogoro kwa kuwa kuna wakulima wengi wanaolima mazao mengi ila hawapati nafasi ya kupata mbolea bora na kwa wakati hali inayopunguza kasi ya uzalishaji wa mazao yao.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wakulima wa Miwa wilaya ya Kilombero Bakari Mkangamo akiongea kwa niaba ya wakulima wenzake ameipongeza kampuni ya PETROBENA ambao ni wakala mkuu wa YARA kwa kuwafikishia pembeo kwa wakati,na kuongeza kuwa kuanzia msimu ujao uzalishaji utaongezeka kwa kuwa wakulima wamelima na kuwekea mbolea kwa wakati tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

  Mwishoni mwa mwaka jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alitoa wito kuhakikisha kwamba Mbolea na pembejeo zingine zinapatikana muda wote zinapohitajika tena na kwa gharama nafuu ambapo Kampuni ya PETROBENA EAST AFRICA LTD ambao ni wakala wakuu wa Kampuni ya Mbolea ya YARA wameanza kutekeleza agizo hilo kwa mikoa ya Dar es salaam,Tabora,Morogoro,Njombe na Arusha.

  Na William Bundala.

  Mtaalamu wa kilimo kutoka kampuni ya YARA Maulid Mkima akitoa darasa la kwa maafisa kilimo na maafisa wa pembejeo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi mpya ya PETROBENA mkoani Morogoro.Picha zote na William Bundala.
  Afisa biashara wa kampuni ya YARA Nyanda za Juu Kusini John Meshack akiongea na Maafisa Milimo pamoja na Wauzaji wa Pembejeo 
  Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya PETROBENA EAST AFRICA LIMITED Peter Kumalilwa akisikiliza kwa makini darasa lililokuwa likitolewa na Mtaalamu wa Kilimo kutoka kampuni ya YARA bwana Maulid Mtima.
  Maafisa Kilimo na Wauzaji wa Pembejeo kutoka wilaya za mkoa wa Morogoro wakiwa makini katika mafunzo ya matumizi bora ya pembejeo na umuhimu wa kutumia mbolea.
  Mkurugenzi wa Utawala na Fedha kutoka Kampuni ya PETROBENA Sabena Kubini aliyesimama kulia amevaa t-shirt nyeupe pamoja na maafisa wengine wa PETROBENA na YARA wakisikiliza elimu ya matumizi bora ya mbolea kutoka kwa mtaalamu wa kilimo wa kampuni ya YARA hayupo pichani.
  Maafisa kilimo na wauzaji wa pembejeo wakiwa makini kusikiliza mafunzo kuhusu umuhimu wa matumizi bora ya mbolea na madhara ya kutumia mbolea tofauti na maelekezo ya wataalamu.
  Maafisa kilimo,wauzaji wa pembejeo na wafanyakazi wa kampuni ya PETROBENA wakiwa darasani wakiendelea kupata mafunzo ya matumizi bora ya mbolea katika ukumbi wa mikutano wa ofisi mpya za PETROBENA zilizopo Nane nane mkoani Morogoro.
  Mafunzo yakiendelea

  0 0  0 0

  Muheza – Tanga

  Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania - TFS imeendelea kuhakikisha kwamba Sekta ya Utalii katika Hifadhi za Misitu Asilia nchini inaimarishwa na kuendelezwa kwa kuwa ni moja ya sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika Pato la Taifa na ajira kwa wananchi pamoja na uhifadhi wa misitu hiyo. 

  Mtendaji Mkuu wa TFS, Profesa Dos Santos Silayo amesema hayo jana alipotembelea Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asili Amani wilayani hapa na kujionea changamoto mbalimbali ikiwamo idadi ndogo ya vitanda kwa ajili ya malazi.“TFS inasimamia utekelezaji wa mikakati ya kukuza utalii nchini kwa kuongeza msukumo katika utalii wa ikologiakwa kuboresha miundombinu kwenye maeneo ya Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilina kuyatangaza maeneo hayo.

  “Kuhamasisha wananchi kutembelea vivutio vya utalii wa ndani, mfano mwaka huu tulitoa ofa katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba)kutembelea Msitu huu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Amani na watu wengi walijitokeza kujionea vivutio vingi wakiwamo vinyonga wenye pembe tatu.Profesa Silayo anaongeza kuwa kutokana na Msitu wa HIfadhi ya Mazingira Asilia Amani kuwa na vivutio vingi, wameweka mazingira yatakayowezesha wawekezaji wa ndani kuendeleza biashara za utalii pamoja na kuwajengea uwezo waongoza watalii.

  Mtendaji huyo anasema tayari wameshatangaza tenda kwa wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye malazi na shughuli mbalimbali za utalii kwenye hifadhi ya Amani na sasa wako kwenye hatua za mwisho za kumpata mzabuni.Mhifadhi wa Hifadhi ya Hifadhi ya Mazingira ya Amani, Mwanaidi Kijazi anasema pamoja na mambo mengine, mkakati huo umefunguafursa za utalii mkoani Tanga na kujenga mazingira bora kwa wawekezaji binafsi kuweza kujenga hoteli za kisasa za kulala wageni ikiwamo usafiri wa kufikisha wageni katika maeneo hayo.

  Mhifadhi huyo anasema wanashirikiana kuhifadhi msitu huo kwa kuishirikisha jamii kutumia mazingira asilia ya msitu huo kama chanzo cha kujipatia kipato kwa kutoa elimu ya ujasiriamali, kutenga maeneo ya biashara, kuishirikisha sekta binafsi na kutoa elimu ya uhifadhi kwa umma. 

  Aidha, Kijazi amesema katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 wamefanikiwa kuingiza shilingi milioni 59.2 kutokana na wageni 782 waliotembelea hifadhi hiyo.Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2015 inaielekeza Serikali kuongeza idadi ya watalii wanaoingia nchini kutoka 1,102,026 mwaka 2015 hadi 2,000,000 mwaka 2020 kwa kuwezesha Sekta Binafsi kuwekeza katika huduma za miundombinu ya utalii pamoja na kuendeleza Mkakati wa Kimataifa wa Utangazaji wa Utalii ili kuwavutia watalii wengi zaidi.
  Watalii wa ndani wakifurahia Mazingira mazuri ya HIfadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia Amani 
  Watalii wakiwa wanafurahia safari yao ya kutalii katika hifadhi ya mazingira asilia ya amani
  Mtendaji MKuu wa Wakala wa Huduma za MIsitu Tanzania Prof Dos Santos Silayo (wa kwanza kulia anayeshika maji) akifurahia maji yanayotiririka kwenye maporomoko ya maji yaliopo ndani ya Hifadhi za Mazingira Asilia-1

  0 0

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

  ASKOFU Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini , Baba Askofu Dkt Martin Shao amezindua Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Vunjo itayoshughulika na kutatua kero katika Sekta ya Miundombinu ya barabara ,Elimu ,Afya na Maji.

  Kwa kuanza taasisi hiyo imepanga kuanza matengenezo ya barabara katika vijiji vyote Vilivyoko katika Jimbo la Vunjo ,barabara ambazo zinakadiliwa kuwa na urefu wa Km 272.8 ambazo zitagharimu kiasi cha Sh Bil 7 na Mil 290.Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo uliofanyika katika kata ya Mshiri ,Marangu wilaya ya Moshi ,Katibu wa Bodi ya taasisi hiyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Vunjo James Mbatia amesema Vunjo litakuwa jimbo la kwanza kufanya tukio hilo.

  “Mzigo huu tulionao utakuwa mwepesi tukiw ana raha kwenye nafsi zetu ,na tunataka tuongoze kama wana vunjo hili liwe jimbo la kwanza Tanzania kwa watu wake kuwa na raha bila ya kuwa na bughdha za aina yoyote”alisema Mbatia.Alisema tukio la kuleta viongozi wa Dini pamoja ,viongozi wa vyama vya siasa pamoja na ananchi pamoja kufanya na kukubaliana kwa maendeleo yao na kwamba litakuwa ni jimbo la mfano kwa majimbo mengine kwa kuanzisha utaratibu huo.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi hiyo,Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Dkt Martin Shao alisema taasisi hiyo bado ni changa lakini hata hivyo tayari imeweza kuanza kazi kwa upande wa miundombinu ya barabara.

  “Hii taasisi yetu ni change kweli ,maana tarehe 23 mwezi Julai ndio katiba yetu tumeiweka wazi mbele ya watu wote na ikapata Baraka za Mkuu wetu wa mkoa wa Kilimanjaro,lakini leo mtoto huyu ambaye ana siku chache tu ameanza kutembea na ameanza kufanya kazi”alisema Dkt Shao.

  Kero za Muda mrefu sasa kwa wananchi katika jimbo la Vunjo zikiwemo za Miundombinu ya barabara,Elimu,Afya na Maji sasa zitafika kikomo huku suluhisho likitajwa kuwa ni kuanzishwa kwa taasisi hii ya Maendeleo Endelevu katika jimbo la Vunjo.
  Mbunge wa Jimbo la Vunjo,James Mbatia akisalimiana na Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Dkt Martin Shao alipowasili katika kata ya Mshiri-Marangu kwa ajili ya uzinduzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Vunjo.(katikati) ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawira .
  Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Dkt Martin Shao na viongozi wengine wa Dini wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa shughuli ya uzinduzi wa Taasisi ya Maendeleo katika Jimbo la Vunjo. 
  Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Dkt Martin Shao akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Vunjo wakati a uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo.
  Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Dkt Martin Shao akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Maendeleo ya jimbo la Vunjo,uzinduzi uliofanyika katika kata ya Mshiri-Marangu.
  Baadhi ya Wananchi waliohudhuria uzinduzi huo.
  Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akizungumza katika uzinduzi huo.
  Baadhi ya Wananchi waliohudhuria mkutano wa uzinduzi uliofanyika katika kata ya Mshiri -Marangu .
  Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Baba Askofu Dkt Martin Shao akizungumza jambo na viongozi wenzake wa Dini waliohudhuria mktano wa uzinduzi wa taasisi hiyo.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawira akizungumza wakati wa mkutano huo .
  Mmoja wa Viongozi wa Dini ya Kiislamu Sheakh ,Abdalah Mwacha akizungumza wakati wamkutano wa uzinduzi wa taasisi ya Maendeleo katika jimbo la Vunjo.
  Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba za viongozi zilizotolewa wakati wa Uzinduzi huo.
  Diwani wa kata ya Mshiri,Exaud Mamuya akizungumza katika mkutano huo.
  Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Baba Askofu Dkt Martin Shao akiwa ameongozana na Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia na Viongozi wengine kuelekea eneo ambalo uzinduzi wa Mitambo ya kukarabati barabara za jimbo la Vunjo ulifanyika.
  Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Baba Askofu Dkt Martin Shao akikata utepe katika mtambo unaotumika kukarabati barabara ikiwa ni ishara ya kuanza kazi kwa Taasisi ya Maendeleo katika jimbo la Vunjo ambayo moja ya kazi zake ni kutengeneza barabara katika jimbo la Vunjo.
  Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Baba Askofu Dkt Martin Shao akibariki moja ya Mitambo itakayotumika katika kufanya matengenezo ya barabara katika jimbo la Vunjo.
  Mtambo wa kukwangua barabara ukianza kazi muda mfupi baada ya kuzinduliw kwa Taasisi ya Maendeleo ya Vunjo ambayo moja ya kazi zake ni kutengeneza miundo mbinu ya barabara.

  0 0


  SHIRIKA la Utangazaji Nchini (TBC) limezindua studio kubwa ya Kumbukumbu ya ukombozi wa Afrika ya Mwalimu Nyerere katika majengo yake yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam.

  Studio hiyo yenye kuhifadhi historia ya kumbukumbu ya ukombozi barani Afrika zilizopo katika kanda za sauti na video imetengenezwa kwa ushirikiano kati ya TBC na Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na wadau wengine wa maendeleo.

  Kuwapo kwa studio hiyo kumelenga kuongeza uwajibikaji, uwezo wa kupata taarifa za zamani na kuongeza uratibu wa menejimenti ya hifadhi ya mambo muhimu ambayo ni ya urithi wa Tanzania.

  Studio hiyo ambayo ni sehemu ya mradi mkubwa wa hifadhi ya mambo ya urithi (TAHAP) wenye lengo la kuhamasisha hifadhi na utunzaji wa urithi wa Tanzania na kumbukumbu za mapambano ya ukombozi katika bara la Afrika, pia itaongeza uelewa wa watanzania juu ya urithi wao ambao umekuwa ukiongezeka jinsi miaka inavyozidi kusonga mbele.

  Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mkurugenzi wa Idara ya Maelezo na Msemaji Mkuu wa serikali Dk. Hassan Abbas alisema kwamba serikali itaendelea kuhakikisha kwamba urithi wa nchi hii unahifadhiwa kwa manufaa ya kizazi kijacho.

  "Kwa sasa tunaondoka katika mfumo wa maandiko, sauti na video.  Sisi kama serikali tunafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba matukio yetu ya kihistoria yanarekodiwa na kuhifadhiwa vyema. Hatua hiyo itasaidia kuongeza uelewa wa historia kwa watu wetu na serikali kwa ujumla," alisema Dk Abbas .
   Mkurugenzi wa Idara ya Habari  na Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali ,Dkt. Hassan Abbas (katikati)  akikata utepe wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mwakilishi  mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO Ms.Anna Therese Ndong-Jatta(kulia) wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba, Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bw. Charlie Stuart  na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),Bw. Alvaro Rodriguez.

   Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na  Msemaji wa Serikali  Dkt. Hassan Abbas (wapili kulia) akishuhudia Mkurugenzi Mwakilishi mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO Bi. Anna Therese Ndong-Jatta (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba moja ya  Kamera pamoja na  vifaa  mbalilmbali vya utangazaji vilivyotolewa msaada na  UNESCO kwa kushirikiana na wadua na Washirika wa Umoja wa Ulaya (EU) wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo  umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya nchini. Kushoto ni Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bi. Charlie Stuart.
    Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali  Dkt.  Hassan Abbas (wa pili kulia) akishuhudia Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bi. Charlie Stuart akimkabidhi moja ya kifaa cha kurekodia  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba  kati ya vifaa mbalimbali vilivyotolewa msaada na UNESCO kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo  umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) nchini.
   Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na  Msemaji wa Serikali  Dkt. Hassan Abbas (katikati) akishuhudia Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),Bw. Alvaro Rodriguez akimkabidhi moja ya kifaa cha kuhifadhia kumbukumbu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba kati ya vifaa mbalimbali vilivyotolewa msaada na UNESCO kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) nchini.
   Kutoka Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),  Bw. Alvaro Rodriguez, Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bw.Charlie Stuart, Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO Bi.Anna Therese Ndong-Jatta, ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali  Dkt. Hassan Abbas, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya utangazaji vilivyotolewa msaada na UNESCO Kwa kushirikiana na wadau wa mradi wa Umoja wa Ulaya.(EU)
  Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO Bi. Anna Therese Ndong-Jatta, (wa tatu kulia) Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bw. Charlie Stuart (kushoto), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),Bw. Alvaro Rodriguez ( wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba, wakimsikilza kwa makini mmoja wa wafanyakazi wa TBC akiwaonyesha moja ya mitambo iliyotumika kurekodia enzi kupigania ukombozi wa Afrika.


  0 0

  Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
  Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Wanawake “Kilimanjaro Queens” imerejea nchini ikitokea Rwanda ilipokuwa ikishiriki mashindano ya Afrika Mashariki na Kati maarufu kama CECAFA ambapo imefanikiwa kutwaa Kombe la michuano hiyo.
  Timu hiyo imepokelewa leo Jijini Dodoma  na Katibu Mkuu  wa Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo  Bibi Suzan Mlawi ambaye mbali tu na kuipongeza timu hiyo lakini pia ameishukuru kwa kuipeperusha vyema Bendera ya nchi.
  “Mmeiwakilisha vizuri nchi yetu mmeonyesha nidhamu na kubwa zaidi mmeshinda na kufanikiwa kutetea kombe lenu   nawapongeza sana na nawaahidi Serikali itaendelea kushirikiana na nyie ili mlete mafanikio zaidi kwa nchi yetu”Alisema Bibi Suzan.
  Aidha Bibi Suzan amelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF ) kutafuta mikakati mizuri itakayosaidia timu hiyo kupata wadhamini kama zilivyo timu nyingine lakini pia kuandaa tuzo kwa wachezaji wanaofanya vizuri ili kutoa hamasa kwa wadau wengi kutoa ushirikiano wa kuendeleza mpira wa miguu kwa wanawake.
  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Bw. Kidao Wilfred ameeleza kuwa mafanikio waliyopata Kilimanjaro Queens yametokana na ushirikiano mkubwa baina ya Serikali Jeshi la Kujenga Taifa, Benchi la ufundi pamoja na Taasisi yake kwa kuwa karibu, kuijenga na kuiandaa timu hiyo vizuri.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Suzan Mlawi (Katikati) akizungumza na timu ya Kilimanjaro Queens (haipo pichani) baada ya kurejea nchini ikitokea Rwanda kwenye mashindano ya ligi ya Wanawake ya mpira wa miguu Afrika Mashariki na Kati ambapo imefanikiwa kutetea ubingwa wa michuano hiyo.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa Wizara hiyo Bw.Orest Mushi na kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF Bw.Kidao Wilfred.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Suzan Mlawi (Katikati) akipokea Kombe kutoka kwa Nahodha wa Timu ya Kilimanjaro Queens Bi Asha Rashid baada ya kurejea nchini ikitokea Rwanda kwenye mashindano ya ligi ya Wanawake ya mpira wa miguu Afrika Mashariki na Kati ambapo imefanikiwa kutetea ubingwa wa michuano hiyo.
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya  Michezo  wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo akizungumza na Timu ya Kilimanjaro Queens (hawapo katika picha) baada ya kurejea nchini ikitokea Rwanda kwenye mashindano  ya ligi ya wanawake ya mpira wa miguu Afrika Mashariki na Kati ambapo imefanikiwa kutetea ubingwa wa michuano hiyo.
  Nahodha wa timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu “Kilimanjaro Queens”Bi Asha Rashid akizungumza wakati timu hiyo ilipopokelewa leo Jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Suzan Mlawi ikitokea Rwanda kwenye mashindano ya ligi ya wanawake ya mpira wa miguu Afrika Mashariki na Kati ambapo imefanikiwa kutetea ubingwa  wa michuano hiyo.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Suzan Mlawi (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na timu ya mpira wa Miguu ya wanawake “Kilimanjaro Queens” na viongozi wengine baada ya kuipokea timu hiyo iliyotokea nchini Rwanda kwenye mashindano  ya ligi ya wanawake ya mpira wa miguu Afrika Mashariki na Kati ambapo imefanikiwa kutetea ubingwa  wa michuano hiyo.  0 0

  Collabo mpya ya Yvonne Chakachaka na msanii wa Tanzania.

  Miezi kadhaa iliyopita King wa Bongo Flava Ali Kiba alitangaza rasmi ujio wa ngoma yake na mwanamuziki mkongwe, maarufu na wa zamani kutoka Afrika ya Kusini Yvonne Chakachaka. 

  Hii ilikuwa ni hatua muhimu sana ya kimuziki kwa nguli huyo wa muziki kutoka Tanzania katika juhudi za kuutangaza muziki wa Tanzania nje ya mipaka, lakini pia kuuthibitisha umma juu ya uwezo wake kimuziki. 

  Lakini inaonekana kwamba Yvonne Chakachaka aliyetamba na nyimbo kama "Mama Afrika", "Thank you Mr. Dj" na "Umqombothi" miaka ya 80, amevutiwa sana na muziki wa Bongo na hivyo kuwa tayari kufanya kazi na wasanii wengine kutoka hapa nchini. 

  Hii inathibitika baada ya hivi karibuni, kupitia account yake ya instagram kuonesha kuwa yuko studio na moja ya wasanii wa Tanzania, Otuck William, wakirekodi wimbo. Legend huyo wa muziki wa Africa AKA "The Princess of Africa" aliandika, "Spending some time with my son @otuck_william in Kigali, doing some work for the youth. Day well spent, thank you @mrmingz". 

  Yvonne Chakachaka alikua jijini Kigali, nchini Rwanda kwa ajili ya onesho na kukutana na Otuck, ambaye pia alikua huko kwenye shughuli zake za kikazi na kimuziki, hivyo tutegemee kikubwa kutoka kwa hivi vichwa viwili. Otuck ni msanii mkongwe wa RnB nchini anayetambulika sana na ngoma zake kama Deja Vu, Roho Juu alitomshirikisha Heri Muziki na So Cold aliyoitoa hivi karibuni.

  0 0

  *Asema lengo ni kudhibiti uingizwaji wa silaha haramu nchini 
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamesema ukaguzi wa watu na mizigo unaofanywa kwenye kizuizi cha Uvinza mkoani Kigoma utaendelea kufanyika ili kudhibiti wimbi la uingizwaji wa silaha haramu nchini.

  “Lazima ukaguzi ufanyuke ili kujiridhisha kama watu wote wanaoingia nchini wamepita kihalali na kama hawapitishi silaha haramu na vitu vingine ambavyo haviruhusiwi kuingizwa nchini,”.

  Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 29, 2018) wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Uvinza akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma. 

  Ametoa ufafanuzi huo baada ya Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini, Bibi Hasna Mwilima kudai kuwa wananchi wengi wanapata usumbufu mkubwa kutokana na ukaguzi unaofanywa na Maafisa wa Uhamiaji katika kizuizi cha Uvinza.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Ilagala wilayani Uvinza baada ya kutembelea kiwanda kidogo cha kukamua mafuta ya mawese Julai 29, 2018. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipanda mchikichi baada ya kukagua shamba la zao hilo katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa ya Bulombora wilayani Uvinza, Julai 29, 2018.  Wapili kulia ni mkewe Mary.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama mchikichi wakati walipotembelea shamba la Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa ya Bulombora wilayani Uvinza, Julai 29, 2018.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama mikungu ya matunda ya  michikichi yanayosubiri kukamuliwa kuwa mafuta ya mawese katika kiwanda kidogo kilichopo kwenye kijiji cha Ilagala  wilayani Uvinza, Julai 29, 2018. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama matunda  ya michikichi yaliyokuwa yakichambuliwa kabla ya kukamuliwa kuwa mafuta ya mawese katika kiwanda kidogo kwenye kijiji cha Ilagala wilayani Uvinza, Julai 29, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama kazi ya kukamua mafuta ya mawese kwenye kiwanda kidogo  katika kijiji cha Ilagala wilayani Uvinza Julai 29, 2018. Kulia ni Mbunge wa Kigoma Kusini, Hasna Mwilima na watatu kushoto ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na Viongozi mbali mbali katika Uwanja wa Ndge wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume alipokuwa akiondoka Nchini leo  kuelekea Indonesia katika ziara ya Kikazi akifauatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Watendaji wengine wa Serikali
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud (kushoto) katika Uwanja wa Ndge wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume alipokuwa akiondoka Nchini leo kuelekea Indonesia katika ziara ya Kikazi akifauatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (kulia) pamoja na Watendaji wengine wa Serikali,
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na Makamu wa Pili wa Rais Mhe.Balozi Seif Ali Iddi (kulia) katika Uwanja wa Ndge wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume alipokuwa akiondoka Nchini leo kuelekea Indonesia katika ziara ya Kikazi akifauatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (hayupo pichani) pamoja na Watendaji wengine wa Serikali.
  Picha na Ikulu.

  0 0

  Na.khadija seif ,Globu ya Jamii

  SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania TFF limeingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Milioni 420 na Benki ya KCB kwa ajili ya udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

  Akizungumza wakati wa utiaji saini mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu Benki ya KCB nchini Cosmas Kimario ameeleza madhumuni ya Benki hiyo ni kushirikiana na TFF kwa ajili ya kukuza sekta ya Michezo, ambapo hapo awali walishirikiana kwenye msimu uliopita 2017/2018 kwa kuwa moja wa wadhamini wa ligi kuu nchini.

  Kimario amesema udhamini huo unalenga zaidi kuendeleza soka hilo nchini pamoja na kuwapatia ajira vijana na kuipeperusha bendera ya nchi ya Tanzania.

  Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) Wallace Karia ametoa shukrani za dhati kwa benki ya KCB kwa udhamini huo, kwani watanufaika na kusaidia kunyanyua michezo katika msimu wa 2018/19. Hata hivyo  Karia amesema Benki ya KCB imekuwa ikishirikiana na TFF kwenye michezo na hata msimu uliopita walishirikiana nao kudhamini michezo nchini na hii ikiwa ni mara ya pili.

  Kaimu mwenyekiti wa Bodi ya benki ya KCB Fatma Chiro ameeleza Benki hiyo imetoa ajira kwa watu wengi na rasmi,hivyo inaunga mkono kauli ya serikali katika kutoa ajira kwa vijana na wameamua kuanza na sekta ya michezo.

  Amefafanua zaidi kuwa benki hiyo haitaishia hapo kushirikiana na shirikisho la mpira wa miguu (TFF) katika kudhamini michezo hususani mpira wa miguu na kutazama uwezekano wa kusaidia timu ya mpira wa miguu ya wanawake Kilimanjaro Queens ambao wameshinda mechi waliocheza hivi karibuni dhidi ya Ethiopia na kurudi na kombe nchini Tanzania.
  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania Bw. Wallace Karia akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 420 kutoka kwa kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Bi. Fatma Chilo baada ya kusaini  mkataba wa udhamini kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania, Cosmas Kimario na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Bw. Boniface Wambura.

  0 0

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

  MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar amesema ushiriki wa Viongozi vijana wa Kiafrika Katika Kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Rais Mstaafu wa Marekani ,Barack Obama ,Obama Foundation ni chachu kwa viongozi walioko madarakani kuendelea kuwamini kwa kuwapa nafasi za ju za uongozi .

  Nassar ametoa kauli hiyo zikiwa zimepita siku chache tangu ashiriki Kongamano lililoandaliwa na taasisi ya Obama Foundation na kuwashikisha vijana 200 kutoka mataifa 44 barani Afrika wanaofanya kazi serikalini ,asasi za kiraia na sekta binafsi ambao walikutana kwa muda wa siku tan katika jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini.

  Amesema katika Kongamano hilo kama vijana wamejifunza mambo mengi ambayo kwa kiasi kikubwa yatachangia kujitokeza kwa vijana wengi zaidi katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi watakaosaidia kuleta mabadiloko chanya katika bara la Africa.Katika kongamano hilo lililoenda sambamba na sherehe za kilele cha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muasisi wa taifa la Afrika Kusini ,Nelson Mandela,vijana nane kutoka Tanzania walichaguliwa kuiwakilisha nchi ya Tanzania.

  Miongoni mwa Viongozi na watu Mashuhuri walioshiriki katika utoaji wa mada katika kongamano hilo ni pamoja na Rais Mstaafu wa Marekani ,Barack Obama,Rais Mstaafu wa Liberia,Ellen Johnson Sirleaf, Katibu Mkuu Mstaafu wa UN,Koffi Annan na Mmiliki wa Kampuni ya Celtel na Muasisi wa taasisi ya Mo Ibrahimu ,Bw Mo Ibrahim.

  Wengine ni Mke wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini,Mama Graca Machel,Mfanyabiashara Tajiri,Aliko Dangote, Waziri (mdogo) wa Viwanda ,Biashara na Uwekezaji Botswana ,Bogolo Kenewendo,Muandishi wa filamu maarufu zaidi Duniani ya Black Panther ,Ryan Coogler Lakhdar Brahimi ,Trevor Manuel na wengine wengi.
  Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassar akizungumzajambo na Rais Mstaafu wa Marekani ,Barack Obama walipokutana nchini Afrika Kusini akiwa ni miongoni mwa Viongozi vijana 200 kutoka mataifa 44 ya Afrika waliochaguliwa kushiriki Programu ya OBAMA AFRICA LEADERS PRORAM.
  Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassar kwa pamoja na Rais Mstaafu wa Marekani ,Barack Obama wakiwajibika kwa kufanya kazi za mikono katika kuboresha miundombinu ya shule ya Far North School iliyopo pembezoni mwa jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini.
  Rais Mstaafu wa Marekani ,Barack Obama akipeana mikono na washiriki wengine wa Programu ya Viongozi wa Afrika mara baada ya kumaliza kazi za mikono katika shule hiyo.
  Mbali na kushiriki kazi za mikono Rais Mstaafu wa Marekani,Barack Obama pia alipata nafasi ya kutoa mada katika kongamano lililowashirika viongozi vijana 200 kutoka mataifa 44 ya Africa.
  Wengine waliowasilisha mada katika Kongamano hilo ni pamoja na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa (UN) Koffi Annan ,Rais wa Kwanza Mwananmke Barani Afrika na Rais Mstaafu wa Liberia ,Ellen Johnson Sirleaf 
  Pia Mjane wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini ,Mama Graca Machel alikuwa ni miongoni mwa viongoz walioshiriki kutoa mada kwa washiriki wa kongamano hilo.
  Muanzilishi na Mmiliki wa Kampuni ya Celtel na muasisi wa Taasisi ya Mo Ibrahim Foundation inayoshiriki katika utoaji wa tuzo malumu kwa viongozi mbalimbali wa bara la Africa waliofanya vizuri,Mo Ibrahim pia alishiriki katika kutoa mada katka Kongamano hilo.
  Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar akiwa na vijana wengine wa Kitanzania wakishikilia Bendera ya Taifa wakati wa Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Obama Foundation.
  Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar akiwa na Waziri wa Viwanda ,Biashara na uwekezaji Botswana Bogolo Kenewendo .
  Mbunge wa Jimbo la Arumerua Mashariki ,Joshua Nassar akiwa na Waziri wa Ubunifu na Mafunzo ya Ufundi nchini Cape Verde ,Pedro Lopez.
  Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar akiwa na mmoja wa Familia ya Mmiliki wa Klabu ya Mancheter United ,Malcolm Glazer,walipokutana wakati wa Kongamano 

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na watumishi raia, askari na maafisa (hawapo pichani), wakati wa kikao cha ndani na watumishi hao wakati wa ziara ya kikazi, mkoani Shinyanga, leo.Ambapo amewataka askari kutojihusisha na matendo ya rushwa pamoja na kubambikia rushwa wananchi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Sajenti wa Jeshi la Magereza, Athumani Massawo, akizungumza wakati wa kikao cha ndani cha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati wa kikao cha ndani na watumishi hao wakati wa ziara ya kikazi, mkoani Shinyanga, leo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyaga,Mrakibu Mwandamizi Venance Mwamakula akizungumza wakati wa kikao cha ndani cha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati wa kikao cha ndani na watumishi hao, mkoani Shinyanga, leo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Askari wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hawapo pichani), wakati wa kikao cha ndani na watumishi hao wakati wa ziara ya kikazi, mkoani Shinyanga, leo.Ambapo amewataka askari kutojihusisha na matendo ya rushwa pamoja na kubambikia rushwa wananchi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0


  United Bank for Africa – Tanzania Limited donated literature books to Dar es Salaam Christian Seminary school as part of her corporate social responsibility through “Read Africa” Initiative to support education sector in Tanzania. Understanding given that Education is key UBA Tanzania donates literature books to some Secondary schools in Tanzania to encourage youths to read.

  As part of its mission to improve the lives of the communities in which the United Bank for Africa operates, UBA Foundation continues to encourage African youths to adopt the culture of reading through its ‘Read Africa’ initiative by providing books to schools in Tanzania. Read Africa aims to rekindle the reading culture amongst young Africans. Designed and introduced in 2011 by the UBA Foundation, the initiative has donated hundreds of thousands of books to African schools since its inception, the same has been done by UBA Tanzania.

  With the aim to promoting a reading culture among school pupils in the country, the United Bank for Africa Tanzania, through their UBA Foundation Read Africa Initiative, Friday 27th July, 2018 donated literature books to Dar es Salaam Christian Seminary. The bank donated over 250 literature books to the school.
  The UBA Foundation Read Africa Initiative was launched in 2011 and the project is aimed at encouraging children to improve on their vocabulary and communication skills through reading.

  Through its Read Africa Initiative, the UBA Foundation is helping rekindle the dwindling reading culture among African youth as they pursue their education. Over hundred thousand books and educational materials have been donated to various schools across Africa as UBA Foundation continues to traverse the continent, contributing positively to the development of African youth.

  Speaking at the donation ceremony in the school grounds at Mbagala, 
  Kongowe Dar es Salaam, on behalf of the Managing Director and Chief Executive Officer of UBA Tanzania, Stella Shangali, said United Bank for Africa (UBA) Plc is one of Africa’s largest financial institutions with operations in 20 African countries and three global financial centres – New York, London and Paris.

  She said it was no longer a secret that pupils pay more attention to social media and avoid the culture of reading, adding that reading culture helps to improve the intelligence capacity of pupils. She said that through the Read Africa Project, they have donated lots of literature books to schools in African countries where they operate.

  She encouraged pupils to read voraciously as that would help them master the English language and be able to write and speak good English.
  Receiving the donation, the headmaster Mr Erick said the bank’s Read Africa project was a welcome, especially in Tanzania where pupils no longer have time and passion to read. He promised they would use the books judiciously and that he believed the books would help his pupils improve on their reading culture.

  He promised that they would do all in their powers to encourage pupils to prioritise reading and use it to empower themselves academically. He also said the new technology called social media has now taken over and that pupils no longer have interest in reading books.

  0 0

  Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

  JUMLA ya wahamiaji Wasio rasmi 1054 Wamekamatwa katika Wilaya ya Buhigwe na Kasulu mkoani kigoma, Kwa kipindi cha Mwaka mmoja katika oparesheni zilizofanywa na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya hizo.

  Akimkaribisha Waziri Mkuu katika Wilaya ya Buhigwe Mkuu wa Wilaya ya Kasulu na Buhigwe Brigedia Jenerali Marco Gaguti alisema wameendelea kuimalisha ulinzi na usalama katika Wilaya hizo kuhakikisha Wananchi wanafanya shughuli zao kwa amani na utulivu na kuendelea kupambana na vitendo vya uhalifu na uingizwaji wa silaha kiholela .

  Alisema kutokana na Muingiliano uliopo baina ya Wilaya hizo na Nchi jirani ya Burundi kumekuwa na Wahamiaji haramu wengi wanaoingia Nchini bila vibali na wengine wamekuwa wakishirikiana na Watanzania kufanya vitendo vya utekaji kwa kutumia silaha ambapo Wamejitahidi kuzuia vitendo hivyo kwa kuwakamata wote wanaoingia bila Vibari Nchini .

  "Kwa sasa hali ya ulinzi na usalama Imeendelea kuimarika na Wananchi wameendelea kuiunga mkono serikali kwa kutoa taarifa endapo wanamuhofia mtu anapoingia katika maeneo yao na tumefanikiwa katika hili na kwasasa hakuna malalamiko yoyote ya uvunjifu wa amani kutoka Kwa Wananchi", alisema Brigedia Jenerali Gaguti. 

  Nae Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa aliwataka Polisi kwa kushirikiana na Maafisa uhamiaji kudhibiti njia ambazo sio rasmi katika Wilaya ya Buhigwe kwaajili ya kuzuia silaha zinazoingizwa Nchini kiholela na watu wanaingia bila vibali.Alisema Serikali inampango wa kuifanya mji wa Manyovu kuwa mji wa biashara hovyo jeshi la polisi wanatakiwa kuwa macho kwaddhibiti vizuizi hivyo ilikuhakikisha wote wanaoingia Nchini wanakuwa na vibali na kudhibiti silaha zilizopo katika Nchi jirani kuingia Nchini.

  " Tunajua Wilaya hii inachangamoto ya muingiliano Mkubwa na ndugu zetu wa Nchi jirani, Leo hii Tanzania tunarekodi mbaya ya kumiliki silaha kinyume na taratibu zote hizi zinatoka Nchi za jirani na kufanya uharifu wa kutumia silaha", alieleza Waziri Mkuu."Lazima jeshi la polisi Muandae mipaka iliyo rasmi ilikudhibiti haya uwezo huo mnao hatutaki kuona uhalifu unaendelea kuingia Nchini jeshi la polisi kazi yenu ni kulinda amani na jukumu hili ninlakwenu", alisema.

  Alisema Serikali ya Tanzania inamahusiano mazuri na Nchi jirani hivyo mahusiano hayo yaendelee lazima utaratibu uwekwe na usalama uimalishwe.

  0 0

  JUMLA ya Wanafunzi 200 kutoka shule mbalimbali za sekondari nchini wanatarajiwa kuonesha kazi zao za teknolojia ya ugunduzi na sayansi kukabiliana na changamoto za maendeleo nchini.

  Kazi hizo ziko katika nyanja za sayansi kama kemia,fizikia ,hesabu, baiolojia, mazingira, sayansi ya jamii na teknolojia.Maonesho ya kazi hizo za wanafunzi yameandaluwa na Taasisi inasaidia wanasayansi Chipukizi ya YST ikiwahusisha pia walimu 100 wakiambatana na wanafunzi hao ili kuonesha kazi hizo walizoziandaa kwa kipindi cha mwaka mmoja.

  Akizungumzia maonesho hayo yatakayofanyika Agosti 1 na 2 jijini Dar es Salaam, Mwanzilishi Mwenza was YST ,Dr Gosbert Kamugisha alisema katika mashindano ya kazi hizo, wataonesha kazi za kigunduzi na wale watakaoshinda watapata udhamini wa kusoma masomo ya sayansi katika vyuo vya elimu ya juu.

  Alisema lengo la maonesho hayo yaliyoanza kuoneshwa nchini tangu mwaka 2012 ,yatasaidia kuinua ari ya wanafunzi kusoma masomo ya sayansi jambo litakalosaidia kupata wataalam wengi katika eneo sayansi na kufanya kazi katika viwanda.

  " wanasayansi hao ambao ni chipukizi watakaonesha ugunduzi mzuri wataawadiwa pesa taslimu,medali na vifaa vya maabara," alisema na kuongeza kuwa wanne watapewa ufadhili kusomeshwa elimu ya chuo kikuu ambao huyolewa na shirika la Karimjee,Jivanjee Foundation ili kuendelea kjimarisha vipaji vyao vya ugunduzi wa kisayansi.

  Amesema maonesho hayo kuhamasisha wanafunzi was sekondari kupenda sayansi na ugunduzi na kujenga utamafuni was kisayansinkwa vijana was kitanzania,in fursa nzuri kwa wanafunzi was sekkndari kuonesha njia madhubuti za kukabiliana na chanhamoto za kijamii na kiuchumi.
   Mwanzilishi Mwenza wa YST,Dk Gosbert  Kamugisha (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu wanafunzi 200 kutoka shule za sekondari nchini  wanaotarajiwa kuonesha kazi zao za teknolojia Agosti 1,2 mwaka huu  katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar as Salaam.
  Mwanzilishi Mwenza wa shirika la YST,Joseph Clowry (kulia) akizungumza na waandishi wa habari juu ya maonesho yatayofanyika Agosti 1,2  mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar as Salaam.Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Mabalozi wa nchi mbalimbali na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa baada ya kuwakabidhi bila malipo hati za viwanja vya kujengea mjini Dodoma kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2018.
  Balozi wa Rwanda nchini na Kiongozi wa Mabalozi  Mhe. Eugene Segore Kayihura akimshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa niaba ya mabalozi na wawkilishi wa mashirika ya kimataifa kwa kupatiwa bila malipo hati za viwanja vya kujengea mjini Dodoma kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2018
   Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Augustine Mahiga akimkaribisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuongea na mabalozi na wawkilishi wa mashirika ya kimataifa baada ya kuwapatia  bila malipo hati za viwanja vya kujengea mjini Dodoma kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Balozi wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania Mhe. Thamsangqa Dennis Mseleku hati hati ya kiwanja cha  kujengea mjini Dodoma kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2018
  Rais  wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke  hati ya kiwanja cha  kujengea mjini Dodoma kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Alvaro Rodriguez hati ya kiwanja cha  kujengea mjini Dodoma kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Balozi wa  China nchini Tanzania  Mhe. Wang Ke hati ya  kiwanja cha  kujengea mjini Dodoma kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Balozi wa  Kenya nchini Mhe. Dan Kazungu  hati ya kiwanja cha  kujengea mjini Dodoma kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2018
  Mabalozi wa nchi mbalimbali na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa baada ya kupatiwa bila malipo na Rais Dkt John Magufuli hati za viwanja vya kujengea mjini Dodoma kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa nchi mbalimbali baada ya kuwakabidhi bila malipo hati za viwanja vya kujengea mjini Dodoma kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi wa Mashirika Mbalimbali ya Kimataifa baada ya kuwakabidhi bila malipo hati za viwanja vya kujengea mjini Dodoma kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2018.


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Kenya hapa nchini Dan Kazungu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Julai 30, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo Balozi mteule wa Kenya hapa nchini Dan Kazungu  mara baada ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam leo Julai 30, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Picha kutoka kwa Balozi mteule wa Kenya hapa nchini Dan Kazungu. Zawadi hiyo ya picha imetoka kwa Mama mzazi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Mama Ngina Kenyatta na katika picha hiyo anaonekana Rais Dkt. Magufuli akiwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mama Ngina Kenya walipokuwa Nairobi nchini Kenya.


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Balozi wa  Kenya nchini Mhe. Dan Kazungu  hati ya kiwanja cha  kujengea mjini Dodoma kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2018
   Balozi wa  Kenya nchini Mhe. Dan Kazungu  akielekea kuketi baada ya kupatiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli hati ya kiwanja cha  kujengea mjini Dodoma kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2018. Hii ilikuwa kazi ya kwanza kwa balozi huyu ambaye alijiunga na wenzie baada ya kukabidhi hati za utambulisho kwa Rais muda mfupi uliopita.

  0 0

  Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

  WAZIRI mkuu Kasimu Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Hospitali ya Wilaya ya Kasulu mji ambao wanatuhumiwa kuiba dawa na kwenda kuuza katika maduka ya mjini.

  Aidha, Waziri Mkuu ameahidi kuyafunga maduka yote yanayo nunua dawa kwa Watumishi ambao wanaiba dawa katika hospitali za Wananchi na kwenda kuuza kwa ajili ya kujinufaisha wao.

  Waziri Mkuu alifikia uamuzi huo leo wakati alipotembelea Hospitali ya Wilaya ya Kasulu na kubaini tatizo la upotevu wa dawa na vifaa tiba katika hospitali hiyo na kumuagiza mganga Mkuu kuwasimamisha kazi watumishi hao wapishe uchunguzi na watakapo bainika wanahusika na tuhuma hizo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

  " watumishi wazembe , wezi na wala rushwa na wasio waadilifu hawatufai katika serikali yetu na kamwe hatutawavumilia hivyo tutawaondoa.Aliwataja watumishi wanao husika ni wanaohusika na tuhuma hiyo ni Michael Nindi ambae ni mfamasia wa Wilaya , Tilasi Mbombwe ambae ni mtu wa maabara na Venancea Batega muuguzi.
  PMO 0608 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Bibi Pendo Lilola kwa kujifungua salama mtoto wa kiume katika wodi ya wazazi kwenye Hospitali ya wilaya ya Kasulu Julai 29, 2018. Mheshimiwa Majaliwa aliitembelea Hospitali hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Julai 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

older | 1 | .... | 1634 | 1635 | (Page 1636) | 1637 | 1638 | .... | 1898 | newer