Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1633 | 1634 | (Page 1635) | 1636 | 1637 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Miraji Mtaturu mara baada ya kuwasili wilayani hapo kwa ajili ya zoezi la kukabidhi Hati 661 za Hakimiliki ya Kimila kwa wananchi wa vijiji vya Kimbwi na Nkununkhana kata ya Puma wilayani Ikungi jana. Hati hizo zimetolewa ikiwa ni muendelezo wa zoezi la urasimishaji wa mashamba katika maeneo hayo lililoanza mwaka 2011 na kufanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza zilitolewa hati 405. Katikati Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bibi. Rustika Turuka.Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Bibi. Seraphia Mgembe akijadiliana na jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu (katikati) mara baada ya kuwasili wilayani hapo kwa ajili ya zoezi la kukabidhi Hati 661 za Hakimiliki ya Kimila kwa wananchi wa vijiji vya Kimbwi na Nkununkhana kata ya Puma wilayani Ikungi jana. Hati hizo zimetolewa ikiwa ni muendelezo wa zoezi la urasimishaji wa mashamba katika maeneo hayo lililoanza mwaka 2011 na kufanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza zilitolewa hati 405. Kulia ni Mtaalam wa Mawasiliano wa MKURABITA, Bibi. Gloria Mbilimonywa na Mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA, Bw. Emmanuel Mayeji (wapili kushoto).
  Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay akisisitiza jambo wakati wa haflka ya kukabidhi Hati 661 za Hakimiliki ya Kimila kwa wananchi wa vijiji vya Kimbwi na Nkununkhana kata ya Puma wilayani Ikungi jana. Hati hizo zimetolewa ikiwa ni muendelezo wa zoezi la urasimishaji wa mashamba katika maeneo hayo lililoanza mwaka 2011 na kufanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza zilitolewa hati 405. Kutoka kushoto ni Mratibu wa MKURABITA, Bibi. Seraphia Mgembe na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu.Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay akisisitiza jambo wakati wa haflka ya kukabidhi Hati 661 za Hakimiliki ya Kimila kwa wananchi wa vijiji vya Kimbwi na Nkununkhana kata ya Puma wilayani Ikungi jana. Hati hizo zimetolewa ikiwa ni muendelezo wa zoezi la urasimishaji wa mashamba katika maeneo hayo lililoanza mwaka 2011 na kufanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza zilitolewa hati 405. Kutoka kushoto ni Mratibu wa MKURABITA, Bibi. Seraphia Mgembe na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), NBalozi Daniel Ole Njolay akikabidhi a Hati za Hakimiliki za Kimila wakati wa hafla ya kukabidhi Hati 661 za Hakimiliki ya Kimila kwa wananchi wa vijiji vya Kimbwi na Nkununkhana kata ya Puma wilayani Ikungi jana. Hati hizo zimetolewa ikiwa ni muendelezo wa zoezi la urasimishaji wa mashamba katika maeneo hayo lililoanza mwaka 2011 na kufanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza zilitolewa hati 405. Kutoka kushoto ni Mratibu wa MKURABITA, Bibi. Seraphia Mgembe na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu.Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Bibi. Seraphia Mgembe akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi Hati 661 za Hakimiliki ya Kimila kwa wananchi wa vijiji vya Kimbwi na Nkununkhana kata ya Puma wilayani Ikungi jana. Hati hizo zimetolewa ikiwa ni muendelezo wa zoezi la urasimishaji wa mashamba katika maeneo hayo lililoanza mwaka 2011 na kufanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza zilitolewa hati 405. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Kapteni Mstaafu John Chiligati, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA, Balozi Daniel Ole Njolay na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu.Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi aliyemaliza muda wake Kapteni Mstaafu John Chiligati akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Hati 661 za Hakimiliki ya Kimila kwa wananchi wa vijiji vya Kimbwi na Nkununkhana kata ya Puma wilayani Ikungi jana. Hati hizo zimetolewa ikiwa ni muendelezo wa zoezi la urasimishaji wa mashamba katika maeneo hayo lililoanza mwaka 2011 na kufanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza zilitolewa hati 405.
  Baadhi ya wananchi waliopatiwa Hati za Hakimiliki ya Kimila wakisoma hati zao wakati wa hafla ya kukabidhi Hati 661 za Hakimiliki ya Kimila kwa wananchi wa vijiji vya Kimbwi na Nkununkhana kata ya Puma wilayani Ikungi jana. Hati hizo zimetolewa ikiwa ni muendelezo wa zoezi la urasimishaji wa mashamba katika maeneo hayo lililoanza mwaka 2011 na kufanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza zilitolewa hati 405.Mkurugenzi wa Urasimishaji Ardhi toka MKURABITA, William Werema akiwapongeza baadhi ya wananchi waliokabidhiwa Hati zao za Hakimiliki ya Kimila wakati wa hafla ya kukabidhi Hati 661 za Hakimiliki ya Kimila kwa wananchi wa vijiji vya Kimbwi na Nkununkhana kata ya Puma wilayani Ikungi jana. Hati hizo zimetolewa ikiwa ni muendelezo wa zoezi la urasimishaji wa mashamba katika maeneo hayo lililoanza mwaka 2011 na kufanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza zilitolewa hati 405.Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay (aliyejifunika shuka) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi waliokabidhiwa Hati za Hakimiliki za Kimila wakati wa hafla ya kukabidhi Hati 661 za Hakimiliki ya Kimila kwa wananchi wa vijiji vya Kimbwi na Nkununkhana kata ya Puma wilayani Ikungi jana. Hati hizo zimetolewa ikiwa ni muendelezo wa zoezi la urasimishaji wa mashamba katika maeneo hayo lililoanza mwaka 2011 na kufanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza zilitolewa hati 405. (Picha zote na: Frank Shija, MAELEZO, Ikungi, Singida)

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amesema hatakubali kuona maamuzi mabovu yanatolewa kwenye mkoa wake ikiwemo kufungia kiwanda bila sababu ya msingi.

  Mnyeti ameyasema hayo mjini Babati kwenye kiwanda cha pombe cha Mati Super Brands Ltd ambacho kilifungiwa hivi karibuni na mkemia wa serikali na yeye akaagiza kifunguliwe.Alisema viongozi wa serikali wanapaswa kuwa wasaidizi kwa kuwaelewesha kitaalamu wawekezaji ili warekebishe mapungufu pindi yakiwepo na siyo kufungia viwanda.

  Alisema hivi sasa serikali ipo kwenye mchakato wa ujenzi wa viwanda vipya hivyo wataalamu wanatakiwa kutumia elimu yao kuwaelimisha wawekezaji na siyo kuwakandamiza.“Hizo mbwembwe kafanyie sehemu nyingine siyo Manyara, haiwezekani mtu eti anajiita mtaalamu wa serikali anafungia kiwanda sababu ya ukosefu wa komeo la mlango au kuwa na eneo dogo la kuhifadhi bidhaa,” alisema Mnyeti.

  Alisema kabla ya kukifungulia kiwanda hicho kilichofungiwa na mkemia alifuatilia na kupeleleza ili kujiridhisha sababu ya kukifungulia akabaini hazina mantiki.Mkurugenzi wa kiwanda cha Mati Super Brands Ltd, David Mlokozi alisema ili kuunga mkono kauli ya Tanzania ya viwanda wapo mbioni kuanzisha viwanda vingine mkoani Manyara.

  Mlokozi alisema hivi karibuni watamuomba mkuu huyo wa mkoa afungue kiwanda kingine cha vinjwaji vikali ili kukuza uchumi wa nchi na kutoa ajira kwa wananchi wa eneo hilo.Alisema kwenye kiwanda hicho wakati huu wa uzalishaji hulipa sh60 milioni kama kodi ya mapato serikalini kupitia mamlaka ya mapato nchini (TRA).
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akikagua kinywaji kinachotengenezwa na kampuni ya Mati Super Brands Ltd ya Mjini Babati, kushoto ni katibu muktasi wa kampuni hiyo Melania Daniel na katikati ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Babati mjini Elizabeth Marley.
  Mkurugenzi wa kiwanda cha Mati Super Brands Ltd cha mjini Babati David Mlokozi akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, kushoto na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Babati mhandisi Raymond Mushi.
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha kampuni ya Mati Super Brands Ltd cha mjini Babati.

  0 0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa mkoa wa Mbeya pamoja na Wafanyakazi na Wataalam kutoka kampuni ya Songoro Marine wanaoshiriki katika kuunda meli ya MV. Mbeya II itakayobeba abiria 200 pamoja na tani 200 za mizigo katika bandari ya Itungi wilayani Kyela mkoani Mbeya. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua maendeleo ya ujenzi wa meli ya MV. Mbeya II itakayobeba abiria 200 pamoja na tani 200 za mizigo katika bandari ya Itungi wilayani Kyela mkoani Mbeya.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua meli mbili mpya za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 1000 kila moja ambazo ni Mv. Njombe na Mv. Ruvuma katika bandari ya Kiwira wilayani Kyela mkoani Mbeya. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0


   Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora,Mh.Gift Isaya Msuya
  0 0

  Na Magreth Kinabo 

  Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe .Profesa Ibrahim Juma amewataka mahakimu wapya wasiwe chanzo cha ucheleweshaji wa mashauri.

  Aidha kuacha kulalamika bali pale linapotokea matatizo, bali wawe chachu ya kuyatafutia ufumbuzi katika utendaji wao wa kazi wa kutoa huduma za haki kwa wananchi.Kauli hiyo imetolewa leo na Jaji Mkuu huyo wakati akiwaapisha Mahakimu wapya kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.

  “ Kiapo mlichoapa ni uzito muda wote mtakaofanya kazi ya kuwatumikia wananchi, wananchi wanataka kutatuliwa kwa malalamiko yao kwa haraka,” Aliongeza kwamba mfumo wa sasa sio wa kukaa na kulalamika, kama kuna tatizo litafutiwe ufumbuzi na kuepuka kuwa chanzo cha ulalamishi.

  Alisema mahakimu hao wanapaswa kuwa weledi wanapotoa huduma za utoaji haki ili waweze kutoa hukumu zinazoeleweka kwa kujibu wa sheria na kanuni. Hivyo wanapaswa kushirikiana na wadau wengine wa mahakama ili kuahakikisha hukumu zinatoka kwa haraka.Alisisitiza mahakimu hao kwamba kufanya kazi kwa kuepuka rushwa na kwa nidhamu.

  Jaji Mkuu huyo alifafanua kuwa changamoto za majengo chakavu na umbali , visikwamishe utendaji kazi wao, hivyo mahakama iko katika Mpango Mkakati wa Miaka Mitano ambao unalenga kutoa huduma za haki kwa wote na wakati, ikiwemo kuboresha miundombinu.

  Aliwataka mahakimu hao kuielewa taasisi inayofanyakazi na mpango mkakati huo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa nyumba 14 za watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Busekelo zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa Bw. Felix Manyama Maagi. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipitia kitabu kinachoelezea utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika jimbo la Busekelo alichokabidhiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Mhe. Atupele Mwakibete wakati wa ufunguzi wa nyumba 14 za watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Busekelo zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mzee Mark Mwandosya,alipowasili kuweka jiwe la msingi la ufunguzi wa nyumba 14 za watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Busekelo zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa Bw. Felix Manyama Maagi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

  Tanga: Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS), imejiwekea malengo zaidi ya kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 122 katika mwaka huu mpya wa fedha 2018/19 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali katika usimamizi endelevu wa rasilimali za misitu na nyuki ili waweze kuchangia mfuko mkuu wa fedha za serikali.

  Akifunga mafunzo ya siku nne ya kuhusu taratibu za kukusanya maduhuli ya serikali iliyofanyika katika ukumbi wa VETA mjini hapa, Mtendaji Mkuu wa TFS Professa Dos Santos Silayo, amesema lengo hilo litatilia mkazo uibuaji vyanzo vipya vya mapato.

  “Nawashukuru watumishi wote wa TFS kila mmoja kwa nafasi yake, uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya Mhe Waziri Dkt. Hamisi Kigwangala, Bodi ya Ushauri iliyomaliza muda wake chini ya mama Ester Mkwizu na wajumbe wote kwa uchapakazi na uongozi thabiti uliowezesha TFS kukusanya na hatimaye kuwasilisha sehemu ya mapato yake kwa serikali. 

  “Kwa kweli ni fahari kwetu kama taasisi kuweza kuwasilisha bilioni 22.41 katika mfuko huo wa serikali kiasi kwamba tumeshika nafasi ya tano katika utoaji wa gawiwo hilo,” amesema Profesa Silayo.

  Akizungumzia mikakati ya TFS katika mwaka huu wa fedha, Profesa Silayo amewataka watendaji wake kuhakikisha wanabuni vyanzo vipya vya mapato visivyokuwa na madhara katika shughuli za uhifadhi ili kuondoa dhana iliyojengeka kwamba vya taasisi hiyo kazi yao ni kuuza mbao na mkaa.

  Awali akizungumza katika mafunzo hayo Mhasibu Mkuu wa TFS Peter Mwakosya alisema miongoni mwa changamoto walizonazo ni migongano baina ya wahasibu na maofisa misitu inayosababisha migogoro inayohitaji ufumbuzi wa haraka ili taasisi hiyo iweze kuendelea kukua katika kipindi cha miaka minane tangu kuanzishwa kuwa wakala wa serikali.

  “TFS ni taasisi kubwa na ili kuweza kufikia malengo yake ni lazima migongano iliyopo iweze kutafutiwa ufumbuzi mapema kwa kuleta mashirikano baina ya idara zilizomo ndani ya taasisi, vingievyo inaweza kuzorotesha ufanisi na kasi iliyojiwekea taasisi katika kuhakikisha kuwa na usimamizi endelevu wa rasilimali za kitaifa za misitu na nyuki ili kuchangia mahitaji ya kijamii, kiuchumi, ki-ikolojia na kiutamaduni kwa kizazi cha sasa na kijacho,” amesema.

  Wakala wa Huduma za Misitu umeundwa miaka nane iliyopita kwa madhumuni ya kuhakikisha uwepo wa usimamizi madhubuti na wenye ufanisi na tija wa rasilimali za misitu na nyuki, kuongeza ubora na thamani ya kifedha katika kutoa huduma kwa umma, na kuendelea kukuza na kuboresha uwezo wa kutoa huduma kwa umma. Huku masuala ya uendelezaji sera na sheria, pamoja na kanuni na taratibu zake yanashughuliwa na Idara ya Misitu na Nyuki katika Wizara ya Maliasili na Utalii.
  Baadhi ya wahasibu wakifuatilia mkutano uliokuwa unaendelea
  Baadhi ya wahasibu wakifuatilia mkutano uliokuwa unaendelea
  Picha ya Pamoja Mtendaji Mkuu wa TFS akiwa na wahasibu wa TFS Tanzania nzima mara baada ya kufunga mafunzo yao katika Ukumbi wa Veta jijini Tanga Ijumaa jioni.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo wakati yeye na mkewe Mama Janeth Magufuli walipofika msibani Mikocheni B jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018 kutoa pole kwa Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo ambaye amefiwa na mama yake Mzazi Bi Asteria Kahabi Kapela  

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo wakati yeye na mkewe Mama Janeth Magufuli walipofika msibani Mikocheni B jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018 kutoa pole kwa Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo ambaye amefiwa na mama yake Mzazi Bi Asteria Kahabi Kapela

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa heshima za mwisho wakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo ambaye amefiwa na mama yake Mzazi Bi Asteria Kahabi Kapela walipofika kuwafariji msibani Mikocheni B jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa mwanafamilia Bi Leah James wakati yeye na mkewe Mama Janeth Magufuli walipofika msibani Mikocheni B jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018 kutoa pole kwa Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo ambaye amefiwa na mama yake Mzazi Bi Asteria Kahabi Kapela

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa Mama Veneranda Shigongo, mke wa Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo ambaye amefiwa na mama yake Mzazi Bi Asteria Kahabi Kapela wakati yeye na mkewe Mama Janeth Magufuli walipofika msibani Mikocheni B jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018 kutoa pole.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa Mama Veneranda Shigongo, mke wa Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo ambaye amefiwa na mama yake Mzazi Bi Asteria Kahabi Kapela wakati yeye na mkewe Mama Janeth Magufuli walipofika msibani Mikocheni B jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018 kutoa pole.

  Wanafamilia ya Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo ambaye amefiwa na mama yake Mzazi Bi Asteria Kahabi Kapela wakiwa msibani Mikocheni B jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa pole kwa wanafamilia ya Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo ambaye amefiwa na mama yake Mzazi Bi Asteria Kahabi Kapela walipofika kuwafariji msibani Mikocheni B jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Bw. Daudi Machumu, ndugu wa Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo ambaye amefiwa na mama yake Mzazi Bi Asteria Kahabi Kapela walipofika kuwafariji msibani Mikocheni B jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo ambaye amefiwa na mama yake Mzazi Bi Asteria Kahabi Kapela walipofika kuwafariji msibani Mikocheni B jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018. Kushoto ni mwanafamilia Bw. Daudi Machumu.PICHA NA IKULU

  0 0

  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akionyeshwa na wananchi wa Kijiji cha Manolo Kata ya Manolo wilayani Lushoto maji wanayotumia kutoikana na kukabiliana na uhaba wa maji wakati wa ziara yake juzi iliyokuwa na lengo la kukagua miradi ya maji na kuzungumza na wananchi
   Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mgwashi Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto wakati wa ziara yake
   Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akikagua vyanzo vya maji kwenye Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto wakati wa ziara yake
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akikagua vyanzo vya maji kwenye Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto wakati wa ziara yake
   Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akipata maelekezo wakati wa ziara yake ya akikagua vyanzo vya maji kwenye Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto wakati wa ziara yake katikati ni mhandisi wa maji Halamshauri hiyo Samadu Makau
   aibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akiwa amebeba ndoo ya maji kwenye kijiji cha Mgwashi wilayani Lushoto wakati wa ziara yake
  AIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amewaonya wahandisi wa maji nchini wanaoshindwa kusimamia miradi ya maji kwenye maeneo yao na kupelekeea fedha zinazotolewa na serikali kushindwa kutumika kama iliyokusudiwa badala yake wanazitumia kulipana posho. 
  Kauli ya Naibu Waziri huyo aliitoa juzi wakati wa ziara yake ya kutembelea Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto alipokuwa akikagua miradi ya maji huku akilazimika tena kumsimamisha kazi Mhandisi wa Maji Samadu Makau kutokana na kushindwa kusimamia vema mradi wa Maji Mgwashi wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 1.5 na kupelekea wananchi kukosa maji. 

  Naibu Waziri ambaye alianza ziara yake mkoani Tanga kwenye wilaya ya Handeni,Korogwe,Lushoto na Halamshauri zote ndani ya wilaya hizo ambapo alibaini kuwepo kwa ubadhirifu mkubwa wa fedha za serikali katika miradi ya maji tokea mwaka 2012 kutokana na kutokuwepo kwa usimamizi makini wa watendaji wa serikali. 

  Alisema ubadhirifu na upotevu wa fedha za Serikali inatokana na wahandisi wa maji wa mikoa na wilaya waliopewa jukumu la kusimamia miradi hiyo na kushauri kushindwa kuwajibika ipasavyo hivyo kupelekea kuingiza hasara na kupelekea wananchi kukosa maji hivyo Wizara kuanza kutilia mashaka taaluma zao. 

  Naibu Waziri huyo alisema haiwezekani serikali inapeleka fedha nyingi kwenye miradi ili kuweza kutatua tatizo la uhaba wa maji kwa wananchi huku wahandisi hao wa maji wakishindwa kusimamia kwa waledi miradi hiyo huku Serikali ikiwalipa fedha za mishahara kwa ajili ya kuisadia majukumu hayo. 

  “Haiwezekani Serikali inatumia fedha nyingi sana kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama kwa lengo la kuondokana na adha hiyo huku wahandisi waliopo kwa niaba ya Serikali wakishindwa kuisimamia badala yake unapewa taarifa ya ubabaishaji kila maeneo ya miradi unapotembelea”Alisema. 

  “Kutokana na mradi huu kutumia muda mrefu bila kuwepo kwa mafanikio yoyote ni dhahiri Mhandisi utakuwa umeshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo hivyo niagize asimame kazi hii kwani haweze kutusaidia kwenye masuala ya maji hivyo ukae pembeni utipishe maana hauna msaada kwetu “Alisema. 

  Kabla ya kuchukua maamuzi hayo Naibu Waziri Aweso alisema eneo la Mgwashi kumekuwa na changamoto kubwa kutokana na serikali kupeleka fedha nyingi lakini maji wananchi hawajaweza kupata huduma ya maji ili kuweza kuendana na azma ya Rais Dkt John Magufuli ya kumsaidia kumtua ndoo kichwani mwanamama ikiwemo kutokutembea umbali usiozidi mita 400. 

  “Lakini hata mbunge wenu hapa January Makamba ameniambia kuhusu mradi huu wa Mgwashi umekuwa kama una magumashi umetumia fedha nyingi lakini maji hayaonekani hata yanayopatikana umbali mrefu na kupelekea shida kwa wananchi kutembea umbali mrefu hii sio sawa kabisa” 

  Naye kwa upande wake,Mhandisi wa Maji Halamshauri ya Bumbuli,Makau alimueleza Naibu Waziri huyo kuwa mradi huo ulioanza mwaka 2009 na ulitakiwa uwe na tanki mmoja la ujazo wa lita 225,000 na matenki mawili ya ukarabati huku moja ya tanki hilo likiwa na lita 225000 lilopo katika kijiji cha Kihitu huku tenki lengine 90 elfu tisini. Alisema mradi huo una vituo 54 vya kuchotea maji kutokana na aina iliyofanyika hivyo mateki ya huku mawili ililoukatabati 225,000 na elfu 90 linatakiwa kuhudumia vituo 45 wakati la huku linatakiwa kuhudumia vituo vyengine vilivyobakia ili kukamilisha idadi husika.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe wakishiriki katika ibada ya Jumapili katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe akipokea Sakramenti Takatifu wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018

  0 0

  Na Bashir Nkoromo.

  Wakili wa Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwesiga Zaidi na Mbunge wa Mbinga Vijijini Martin Msuha wamewahimiza Vijana kuchangamkia fursa ya mikopo kwa kuunda vikundi vya ujasiriamali na kuvirasimisha kisheria ili waweze kukopesheka ili kuinua hali zao za kimaisha

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi hao wamesema, vijana wengi kwa sasa hawakopesheki kwa sababu hawana vikundi na wengi walionavyo havijarasmishwa kiseria hivyo kuwa vigumu kukopesheka na hivyo kubaki wakilalamika tu kwamba serikali ya CCM haiwajali.

  Katika semina na Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Kata ya Msigani, Mbezi jijini Dar es Salaam, Mbunge Msuha ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Msingwa katika kata hiyo na pia Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM , alisema ni lazima vijana kuwa na vipango mizuri ya miradi na kisha kuunda vikundi ili kupata mikopo kwa ajili ya kuendesha miradi hiyo wanayobuni.

  "sisi tuliowatangulia tunao uzoefu mkubwa katika masuala ya miradi, ikiwa mnashindwa kubuni wenyewe miradi tufuateni tuwape ushauri nasi tupo tayari wakati wote kwa kuwa maendeleo yenu ndiyo maendeleo ya taifa letu", alisema Msuha katika Semina na Baraza hilo ambalo lilifanyika jana
  katika kata hiyo Mgeni rasmi akiwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala.

  Akihimiza suala hilo katika Baraza hilo na Baraza la Vijana wa CCM tawi la CCM Msumi Centre, Mbezi Mwanasheria huyo wa CCM ambaye pia ni mwanasheria wa Kujitegemea Mwesigwa Zaidi alisema kimsingi CCM haigawi fedha kwa mwananchi yeyote isipokuwa ilichofanya ni kutengeneza fursa ambazo mwananchi yeyote akizitumia vizuri atapata fedha.

  "kwa kutambua kuwa ipo haja ya Vijana na Kina mama kusaidiwa katika kuinua vipato vyao imeweka katika katika Katiba yake maelekezo kwa Halmashauri zote nchini kutenga fedha kutoka katika mapato yake kwa ajili ya kuwakopesha, lakini lazima mjue mikopo hiyo si zawadi, inatolewa kupitia benki na lazima kurejeshwa', alisema Wakili huyo.

  Alisema, wakati kinamama wameonekana kunufaika zaidi na fursa hiyo ya mikopo ya serikali ya CCM ambayo kwa sasa inasimamiwa na Rais Dk. John Magufuli, vijana wengi bado hawajanufaika tatizo kubwa likiwa ni kukosa utayari wa kubuni miradi na kuunda vikundi kisha kuvisajili kisheria ili
  wakopesheke.

  Wakili Mwesingwa alisema yupo tayari kuwasaidia vijana wa tawi hilo la Msumi Centre katika kusajili vikundi watakavyoanzisha ikiwa ni pamoja na kuwapigia mihuri yake ya uwakili bila malipo.

  Mapema katika risala vijana wa Msumi Centre walisema wanao mradi wa kutengeneza chakula cha Kuku wenye gharama ya sh. 444,000 lakini hadi sasa wanazo kibindoni sh. 46,000 tu ambapo katika kujibu risala mwanasheria huyo aliahidi kuwachangia sh. 200,000 ambazo alisema atawapa wiki ijayo.

  Wakili huyo pia aliwaasa vijana kuepuka watu wanaotafuta uongozi kwa rushwa badala yake wazingatie maadili ya CCM katika kupata viongozi na pia akahimiza wananchi kusomesha watoto wao ili kuwa chachu iliyo bora zaidi katika kulijenga taifa.

  Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam Mussa Kilakala akizungumza katika Semina na Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Kata ya Msigani, Mbezi jijini Dar es Salaam, lililofanyika jana katika Kata hiyo. Mwenyekiti wa Mtaa wa Msingwa katika kata hiyo na pia Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Martin MsuhaKatibu wa UVCCM Kata ya Msigani Reihard Chikanda akizungumza wakati wa Semina na Baraza hilo

  Katibu wa UVCCM kata ya Msigani Reinhard Chikanda akisoma Risala katika Semina na Baraza hilo

  Wajumbe waakiwaa kwenye semina na Baraza hilo

  Wakili wa Makao Makuu ya CCM ambaye pia n Wakili wa Kujitegemea Mwesiga Zaidi (katikati) akisubiri kutoa mada kwenye Semina na Baraza hilo

  Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mambo kutoka katika makabrasha waliyopewa kwenye Semina na Baraza hilo

  Mwenyekiti wa Mtaa wa Msingwa katika kata hiyo na pia Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Martin Msuha akizungumza katika Semina na Baraza hilo  MSUMI CENTRE⇩
  Wakili wa Makao Makuu ya CCM ambaye pia n Wakili wa Kujitegemea Mwesiga Zaidi (kulia) akipokewa na viongozi wa CCM tawi la Msumi Centre baada ya kuwasili ili kuwa mgeni rasmi katika Baraza kuu ya UVCCM la tawi hilo jana

  Wakili wa Makao Makuu ya CCM ambaye pia n Wakili wa Kujitegemea Mwesiga Zaidi (wapili kushoto) baada ya kuwasili meza kuu katika kikao hicho. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM tawi la Msumi Centre Omari Mohammed na Wapili kulia ni Mzee wa Baraza la CCM tawi hilo.

  Wakili wa Makao Makuu ya CCM ambaye pia n Wakili wa Kujitegemea Mwesiga Zaidi akimtuza mtoto Hamisa Mrisho baada ya kufurahishwa na uhodari wa mtoto huyo katika kucheza sarakasi wakati wa Kikao cha baraza hilo.

  Kijana wa kikundi cha Vijana wa Msumi Centre akionyesha uhodari wa kuchezea motoKatibu wa UVCCM tawi la Msumi Centre Justine Najumwe naye akijaribu kuchezea motoMwenyekiti wa UVCCM tawi la Msumi Chetre Omari Mohammed akifungua kikao cha Baraza hilo.

  Katibu wa UVCCM tawi la Msumi Justine Najumwe akisoma risalaKatibu wa UVCCM tawi la Msumi Cere Justine Najumwe akimkabidhi risala mgen rasmi Wakili wa Makao Makuu ya CCM ambaye pia n Wakili wa Kujitegemea Mwesiga Zaidi

  Wakili wa Makao Makuu ya CCM ambaye pia n Wakili wa Kujitegemea Mwesiga Zaidi akizungumza wakati wa kikao cha Baraza Kuu la umoja wa Vijana wa CCM tawi la Msumi Centre, Mbezi jijini Dar es Salaam, jana.

  0 0


  WAKATI mashindano ya golf ya Utalii Karibu Kusini Mufindi Golf Challenge 2018 yakihitimishwa leo kwenye Viwanja vya Golf vya Unilever wilayani Mufindi, Mkoani Iringa serikali imeahidi kuendelea kuyaboresha mashindano hayo ili yatumike kwa ufanisi zaidi kutangaza vivutio vya Utalii katika kanda za Nyanda za Juu Kusini.

  Akizungumza kwenye viwanja hivyo, Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Utalii Wizara ya Mali Asili na Utalii, Bw Deogratius Mdamu alisema uamuzi wa Serikali kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa kutumia mashindano hayo kutangaza Utalii wa Nyanda za Juu Kusini umeonesha mafanikio licha ya kuwa mashindano hayo yanafanyika mara ya kwanza baada ya kupita miongo kadhaa.

  “Lengo hasa nikuona ndani ya muda mfupi ujao mashindano haya yanakuwa makubwa si tu hapa nchini bali pia nje ya nchi ili tuweze kuvutia washiriki wengi hasa kutoka nje ya nchi tukiamini ujio wao hapa Mufindi utakuwa na tija si kimichezo bali pia kiutalii na kiuchumi,’’ alisema Mdamu.

  Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mashindano hayo wamesema uwepo wa mashindano hayo utatumika kikamilifu kutangaza fursa na vivutio vya Utalii vinavyopatikana katika ukanda huo. Bw Yeckonia Chaula ambaye ni mchezaji mwandamizi wa golf kutoka klabu ya Golf ya Mufindi alisema:

  “Naipongeza sana serikali kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa kuamua kutumia mchezo huu kutangaza vivutio vya Utalii katika Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini na kwa kweli dalili za mafanikio zimeanza kuonekana mapema kwa sababu licha ya mashindano haya kufanyika mara ya kwanza baada ya miaka mingi sana lakini yamevutia washiriki kutoka klabu zote za mchezo huu hapa nchini ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro, Arusha na Mufindi,’’

  Naye Mratibu wa Mashindano hayo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI) Bw Clement Mshana aliwashukuru sana washiriki hao kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mashindano hayo huku akiahidi kutumia maoni ya washiriki katika kuboresha zaidi mashindano hayo mwakani.

  “Pamoja na kuwashukuru washiriki hususani Klabu ya Golf ya Lugalo ambao wameshiriki kwa wingi kwenye mashindano haya kipekee niwashukuru kampuni ya Chai ya Unilever kwa mapokezi mazuri pamoja na maandalizi ya uwanja,’’ alisema.

  Mashindano hayo ya siku tatu yameandaliwa na serikali kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii na yamehusisha washiriki zaidi ya 80 wakiwemo wachezaji wa kulipwa yaani ‘Professionals’ na washiriki wa kawaida yaani ‘Amateurs’ na yanatarajiwa kuhitimishwa leo ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Tamisemi, Bw Joseph Kakunda.

  Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Utalii Wizara ya Mali Asili na Utalii, Bw Deogratius Mdamu (katikati) akikagua Uwanja wa Golf wa Unilever uliopo wilayani Mufindi mkoani Iringa ambapo mashindano hayo yanaendelea. Wengine ni pamoja na Afisa Utalii Mkoa wa Iringa Bi Hawa Mwachaga (kushoto) pamoja na Mratibu wa mashindano hayo kutoka kampuni ya Capital Plus International, Bw Clement Mshana.
  Washiriki kutoka vilabu mbalimbali vya gofu nchini wakiendelea kushindana kwenye mashindano hayo.

  Washiriki kutoka vilabu mbalimbali vya gofu nchini wakiendelea kushindana kwenye mashindano hayo.
  Waandaaji wa mashindano hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja.

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akikagua mazingira ya Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi alipotembelea pori hilo juzi katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo amegiza itolewe ilani ya siku 7 kwa kampuni ya Tanzam 2000 iliyokuwa ikifanya utafiti wa madini ya dhahabu ndani ya pori hilo iondoe mali zake zote na endapo itakaidi zitaifishwe kuwa mali ya Serikali. Kushoto kwake ni Meneja wa Pori hilo, Benjamin Kijika na Kaimu Mkurugenzi Mkuu TAWA, Mabula Misungwi.


  Na Hamza Temba-Geita
  ..........................................................
  Kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzam 2000 iliyokuwa ikifanya utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo la Luahika ndani ya Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi imetakiwa kuondoa vifaa na mitambo yake katika eneo la hilo ndani ya siku saba kwa amri ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla.

  Dk. Kigwangalla ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kutoa ilani ya siku saba kwa kampuni hiyo iondoe vifaa na mitambo yake katika eneo hilo na endapo muda huo utapita bila kufanya hivyo mali hizo zitataifishwa na kuwa mali ya Serikali kwa kuwa wao ni wavamizi kwa mujibu wa sheria.

  Waziri Kigwangalla ametoa agizo hilo juzi alipotembelea pori hilo katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo alihitimisha ziara yake ya siku 25 aliyoipa jina la Pori Kwa Pori kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi nchini na kutatua changomoto zake.

  Alisema uwepo wa vifaa na mitambo ya muwekezaji huyo ndani ya hifadhi hiyo imekuwa kishawishi kikubwa kwa wachimbaji wadogo wa madini kuvamia maeneo hayo wakiamini kuwa eneo hilo lina dhahabu na kwamba bado linaruhusiwa kwa shughuli za uchimbaji.

  Awali Meneja wa Pori hilo, Benjamin Kijika alisema kampuni hiyo ilipewa kibali na Wizara ya Malisili na Utalii kwa ajili ya kufanya utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo hilo kwa mwaka 2005 hadi 2010 na kuongezewa muda hadi 2012.Alisema wakati kibali hicho kinatolewa Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 ambayo inazuia tafiti kama hizo na shughuli nyingine za kibinaadamu kwenye maeneo ya hifadhi ilikua bado haijatoka.

  Alisema baada ya hapo wizara haikutoa tena kibali kwa kampuni hiyo licha ya wizara ya madini kuipa kibali cha kuchimba dhahabu katika eneo hilo mwaka 2013. Aliongeza kuwa kwa nyakati tofauti Wizara ya Maliasili imeitaka kampuni hiyo iondoe mali zake zote ndani ya eneo hilo, agizo ambalo bado halijatekelezwa mpaka sasa.

  Kwa upande wake aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Josephat Paulo Maganga alisema atasimamia utekelezaji agizo hilo la Waziri Kigwangalla ili eneo hilo liendelee kuhifadhiwa kwa mujibu wa sheria.Alisema hifadhi hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya uvamizi wa mara kwa mara wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu hususan katika eneo la Kigosi Kaskazini na hivyo kupelekea uharibu mkubwa wa mazingira katika hifadhi hiyo.

  Alisema ili kukabiliana na changamoto hiyo pori hilo limeanzisha kambi mbili za ulinzi katika eneo hilo kwa ajili ya kudhibiti uharibifu huo ambapo mpaka sasa kesi 24 zenye wachimbaji haramu 52 zimeshafikishwa mahakamani huku kukiwa na vielelezo kadhaa ambavyo ni pamoja na baiskeli 102, viroba vya mchanga unaosadikika kuwa na madini ya dhahabu na vifaa vya uchimbaji.

  Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi ni muunganiko wa mapori mawili yenye ukubwa wa kilometa za mraba 21,060. Pori la Moyowosi lipo katika wilaya za Kibondo na Kakonko (Kigoma) na Pori la Kigosi katika wilaya ya Biharamulo (Kagera), Bukombe na Mbogwe (Geita), Kahama (Shinyanga) na Kaliua (Tabora).

  Pori hili lina umuhimu mkubwa kiikolojia na kiuchumi kwakuwa pia ni ardhi oevu ambayo ni chanzo kikubwa cha maji ya ziwa Nyamagoma na Sagara ambayo huingiza maji mto Malagarasi na hatimaye ziwa Tanganyika, maji hayo hutumika kwa matumizi mbalimbali ya majumbani na kilimo. Pia hifadhi hiyo ni makazi muhimu ya wanyamapori adimu kama Nzohe ambao huliingizia Taifa fedha za kigeni.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akimuagiza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Mabula Misungwi (Kulia) kutoa ilani ya siku 7 kwa kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzam 2000 ili itoe mali zake zote katika eneo la Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi alipotembelea pori hilo juzi katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita na endapo muda huo utapita zitaifishwe kuwa mali na Serikali.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akikagua vifaa na mitambo ya kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzam 2000 katika eneo la Luahika ndani ya Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi alipotembelea pori hilo juzi katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo amegiza itolewe ilani ya siku 7 kwa kampuni hiyo iondoe mali zake zote na endapo itakaidi zitaifishwe kuwa mali ya Serikali, Nyuma yake ni Meneja wa Pori hilo, Benjamin Kijika.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akikagua vifaa na mitambo ya kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzam 2000 katika eneo la Luahika ndani ya Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi alipotembelea pori hilo juzi katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo amegiza itolewe ilani ya siku 7 kwa kampuni hiyo iondoe mali zake zote na endapo itakaidi zitaifishwe kuwa mali ya Serikali, Kulia ni Meneja wa Pori hilo, Benjamin Kijika.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akioneshwa vielelezo (mchanga wa madini ya dhahabu na baiskeli) walivyokamatwa navyo wachimbaji wadogo wa madini katika eneo Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi na Meneja wa Sekta ya Kigosi Kaskazini, Salum Kulunge alipotembelea pori hilo juzi katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo amegiza itolewe ilani ya siku 7 kwa kampuni ya Tanzam 2000 iliyokuwa ikifanya utafiti wa madini ya dhahabu ndani ya pori hilo iondoe mali zake zote na endapo itakaidi zitaifishwe kuwa mali ya Serikali.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amemshukia vikali mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Pauline Gekul (Chadema) kutodandia maendeleo yanayofanywa na Serikali ikiwemo ujenzi wa barabara na kuwadanganya wananchi kuwa yamesababishwa na Chadema.

  Mnyeti aliyasema hayo jana mjini Babati kwenye mkutano wa hadhara baada ya Gekul kujinasibu kuwa maendeleo yanayoonekana Babati yanafanywa na Chadema.Mkuu huyo wa mkoa aliwaeleza wananchi kuwa fedha za bajeti ya mkoa wa Manyara alienda mwenyewe bungeni jijini Dodoma kuzitetea lakini Gekul na wapinzani walipinga ila wabunge wa CCM walitetea.

  "Acheni kudandia maendeleo ya watu, diwani au mbunge atapata wapi fedha za kukamilisha miradi ya maendeleo kwenye halmashauri ambayo haina vyanzo vya mapato vya uhakika kama serikali kuu isipotoa fedha zake na kukamilisha hayo," alisema Mnyeti.Alimtaka mbunge huyo kuungana na wapenda maendeleo wa kweli na kuachana na siasa za kudanganya wananchi ili hali bungeni wanapinga maendeleo kwa kukataa bajeti.

  Alisema baada ya serikali kujenga kilomita 4.5 za barabara za lami ndani ya mji wa Babati hivi sasa kutaongezwa kilomita nyingine 10 za lami ili kufanikisha miundominu bora ya eneo hilo ambalo ni makao makuu ya mkoa huo."Hizo barabara zilizotengenezwa mjini Babati na zinazoendelea kujengwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais John Magufuli alizoahidi wakati wa kampeni na siyo vinginevyo wapinzani msidandie maendeleo," alisema Mnyeti.

  Alisema kila kiongozi anapaswa kubeba mzigo wake mwenyewe kwa kufanya mikutano mwenyewe na siyo kusubiri kudandia ziara ya mkuu wa mkoa na kuongopea wananchi waliojitokeza kwa wingi.Awali, Gekul ambaye alikuwa kwenye msafara wa Mnyeti alipopewa nafasi ya kuwasalimia wananchi alisema Chadema imefanikisha maendeleo mengi Babati tangu wachaguliwe mwaka 2015.

  "Tangu wananchi walipotuchagua na kutupa nafasi ya kuongoza halmashauri ya mji wa Babati tumefanikisha miradi mbalimbali ikiwemo sekta ya afya, elimu, maji na barabara na tutaendelea kuwatumikia," alisema Gekul.

  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Mati Super Brands Ltd, David Mulokozi (kushoto) wakati akikagua vinjwaji vinavyotengenezwa na kampuni hiyo, katikati ni mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Pauline Gekul na Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji huo Mohamed Kibiki.
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Pastory Mnyeti (watatu kulia) akiongoza ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo mjini Babati, kulia ni mbunge wa viti maalum wa mkoa huo Ester Mahawe.
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti, akizungumza na wananchi wa mjini Babati ambapo alisikiliza kero zao na kuwapa majawabu, kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati Mohamed Kibiki na mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Pauline Gekul.

  0 0

  WAZIRI wa Nishati, Medard Kalemani, amezindua umeme wa gridi ya Taifa Wilaya ya Muleba, ambapo alisema kuwa hatua hiyo sasa inakwenda kuifanya wilaya hiyo kuwa na umeme wa uhakika. 

  Akizungumza leo kwenye uzinduzi wa umeme huyo wa gridi ya Taifa ulifanyika katika Kijiji cha Nyamagojo Wilayani Muleba, Dk. Kalemani, amesema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kila Mtanzania hasa wa maeneo ya vijijini wanapata umeme kwenye nyumba zao. 

  Amesema katika utekelezaji wa mradi huo wa ujenzi wa KV 33 wa umeme wa gridi ya Taifa kutoka Wilayani Chato, Rais Dk. John Magufuli, aliridhia na kutoa Sh milioni 778 ili kuweza kukamilisha kazi hiyo. 

  Kutokana na hali hiyo Waziri Dk. Kalemani, amesema kuwa mkakati wa Serikali kuunganisha Mkoa wa Kagera kwenye umeme wa gridi ya Taifa ambao ni wa uhakika katika kufanikisha uchumi wa viwanda kwa kjuwa na nishati ya uhakika na yenye usalama. 

  “Kuzinduliwa kwa umeme huu wa gridi ya Taifa sasa kuzifanya Wilaya za Muleba, Biharamulo na Ngara sasa kuwa na umeme wa uhakika wa hapa nchini kwetu. Tena umeme huu ni salama zaidi maana awali tulikuwa tunategemea umeme kutoka kwa wenzetu nchi ya Uganda jambo ambalo hata wakizima kule hatuna la namna ya kuuliza. 

  “Na ninafuraha kubwa kuwaambia kwamba mkataba wa kazi hii ya ulikuwa ni wa miezi miwili ambapo Juni 2, mwaka huu ulisaini na kuwekeana malengo kwamba hadi kufikia Agosti 2, mwaka huu kazi hii iwe imekamilika. Lakini leo (jana) ninafuraha kuona kazi hii imekamilika wiki moja kabla ya muda wa mkataba,” amesema Dk. Kalemani 

  Kutokana na hali hiyo, aliwataka wananchi wa Kijiji cha Nyamagojo, kuhakikisha wanatumia muda ambao wakandarasi wa wanaotekeleza REA III, kuunganisha umeme kwa gharama nafuu kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma ya umeme hata ikiwa kwa lazima. 

  “Kati ya vijiji zaidi ya 600 vya Kagera ninafuraha kuwambia hadi sasa vijiji zaidi ya 400 vina umeme lakini kuna vijiji zaidi ya 100 navyo wakandarasi wapo site wanaendelea na kazi. Hivyo ni vema wananchi wakati muda huu wakandarasi wakiendelea na kazi ya kuunganisha vijiji umeme lipieni Shilingi 27,000 ili muweze kuunganishiwa huduma ya umeme ndani ya siku saba. 

  “…pia unaweza kulia hata kidogo kuanzia Shilingi 10,000 na kuendelea kulipa hadi utakapokamilisha Shilingi 27,000 unaunganishiwa umeme. 

  “Ninawataka maneja wa Tanesco nchi nzima kuhakikisha mnatafanyakazi hii ikiwamo kwenda kukagua miradi na yule ambaye hawezi kwenda na kasi hii tutamuondoa ili aweze kupisha waliokuwa tayari kufanyakazi,” amesema Dk. Kalemani 

  Awali kwa kiwasilisha taarifa kwa Waziri kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Richard Muyango, amesema hatua ya kuunganisha mkoa huo kwenye gridi ya Taifa, sasa kutaufanya mkoa huo kuwa na umeme wa uhakika. 

  “Tunawakaribisha wawekezaji waje kujenga viwanda vidogo na vikubwa hapa Muleba, sasa nasi tuna umeme wa uhakika ambao ndio suluhisho ya uhakika kwa uchumi wa kati na wa viwanda katika nchi yetu. 

  “Tunamshukuru sana Rais Dk. John Magufuli kwa kweli amefanyakazi kubwa kwetu wana Kagera kwa kuhakikisha wanapata maendeleo ya uhakika katika mkoa wetu, asante sana Rais Magufuli na tunaomba Mheshimiwa Waziri (Kalemani) utufikishie salamu zetu,” amesema DC Muyango. 

  Pamoja na hali hiyo pia aliwasha umeme katika vijiji vya Nyamagojo katika Jimbo la Muleba Kusini na Nundu upande wa Muleba Kaskazini.
  Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyamagojo Wilayani Muleba Mkoani Kagera leo, wakati wa uzinduzi wa umeme wa gridi ya Taifa wa KV 33 ambapo sasa Wilaya ya Muleba, Biharamulo na Ngara zitakuwa zinatumia umeme huo.
  Waziri wa Niashati, Dk. Kalemani, akiwashukuru mafundi waliofanikisha ujenzi znjia za umeme wa gridi ya Taifa baada ya kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.
  Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akishangilia baada ya kuzindua umeme wa gridi ya Taifa katika Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera leo.
  Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa umeme wa gridi ya Taifa Wilayani Muleba Mkoani Kagera leo.

  0 0

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (kushoto) akizungumza jambo na Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Longido Bw. Jummaa Mohamed Mhina nje ya jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Longido. Dkt. Kihamia alifika katika Halmashauri ya wilaya ya Longido kufuatilia maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakaofanyika katika Kata 4 za wilaya hiyo Agosti 12 mwaka huu.
  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (katikati) akizungumza jambo na Msimamizi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Moshi Bw. Michael Mwandezi (kulia) mara baada ya kuwasili katika Manispaa hiyo kufuatilia maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakaofanyika katika Kata 1 . Kushoto ni Afisa kutoka NEC, Bw. Athuman Masesa.
  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (katikati) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Halmashauri ya wilaya ya Longido kufuatilia maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakaofanyika katika Kata 4 . Kushoto ni Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Longido Bw. Jummaa Mohamed Mhina na Kulia ni Afisa kutoka NEC, Bw. Athuman Masesa. 
  Msimamizi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Moshi Bw. Michael Mwandezi (kulia) akimweleza jambo Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (katikati) mara baada ya mkurugenzi huyo kuwasili katika Manispaa ya Moshi kufuatilia maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakaofanyika katika Kata 1 Agosti 12 mwaka huu . Kushoto ni Afisa kutoka NEC, Bw. Athuman Masesa. 
  kurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Msimamizi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Moshi Bw. Michael Mwandezi (wa pili kutoka kulia) na Maafisa wa Uchaguzi jana mjini Moshi. 
  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (kulia) akipokea taarifa ya maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakaofanyika katika Kata 4 za jimbo la Longido kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Longido Bw. Jummaa Mohamed Mhina. 
  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (katikati) akipokea taarifa ya maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakaofanyika katika Kata 4 za jimbo la Arusha kutoka kwa Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo Namyaki Wilfred Laitetei.PICHA ZOTE / NEC

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeliteua Gereza la Kwitanga lililopo wilayani Kigoma kuwa kituo kikuu cha uzalishaji wa zao la michikichi nchini.

  Hivyo ameuagiza uongozi wa gereza hilo waongeze nguvu katika uzalishaji wa michikichi kwa kupanua mashamba na kuongeza askari wenye ujuzi wa kilimo cha michikichi na kupanda miche mipya ya michikichi na kukata ya zamani.

  Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 29, 2018) wakati alipotembelea gereza hilo akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi yenye lengo la kufufua zao la michikichi mkoani Kigoma.

  Amesema Serikali imedhamiria kwa dhati kufufua kilimo cha zao la michikichi mkoani Kigoma, hivyo kila mwananchi lazima awe na shamba la michikichi.Katia hatua nyingine, Waziri Mkuu ameuagiza Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma Bw. Sabas Matolo kuhakikisha Gereza la Kwitanga linawezeshwa kwa kuwa na zana bora na za kisasa za kilimo yakiwemo matrekta na vifaa vya kuvunia ili waweze kuongeza uzalishaji wa mafuta.

  Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Bw. Matolo awahamishe askari ambao ni wataalamu wa kilimo wenye ujuzi wa zao la michikichi kutoka kwenye Magereza mengine mkoani Kigoma na kuwahamishia katika gereza la Kwitanga ili kuimarisha uzalishaji.

  Awali, Mkuu wa gereza hilo Bw. Majuto Masila alisema ili kilimo cha michikichi na uzalishaji wa mafuta uweze kuwa na tija, wanahitaji wafungwa wasiopungua 300 wawepo kila siku gerezani hapo ili kumudu shughuli za shamba hilo. Kwa sasa kuna wafungwa 112.

  "Uzalishaji wa mafuta kwa miaka mitatu mfululizo gerezani Kwitanga ni kama ifuatavyo mwaka 2015/2016 tulizalisha lita 16,094, mwaka 2016/2017 lita 12,674, na mwaka 2017/2018 tulizalisha lita 16,000," alisema.Alisema mafuta yanayozalishwa gerezani hapo yanatumika katika kulisha wafungwa wa gereza hilo la Kwitanga, Bangwe, Kasulu, na Kibondo. Ziada ya mafuta hutumika kulisha wafungwa magereza ya mikoa ya Kagera, Mwanza, Shinyanga, Singida, Dodoma, Morogoro na Tabora.

  Baada ya kutoka katika Gereza la Kwitanga, Waziri Mkuu alitembea shamba darasa na eneo la kuzalisha miche ya michikichi la Seed Change katika eneo la Mungonya na kuziagiza halmashauri zote zinazolima michikichi mkoani Kigoma kwenda kununua mbegu kwenye shamba hilo.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,JUMAPILI, JULAI 29, 2018.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mazao ya michikichi yaliyokuwa yakikamuliwa kuwa mafuta ya kula wakati alipotembelea Gereza la Kwitanga mkoani Kigoma kujionea kilimo cha michikichi na uzalishaji wa mafuta ya mawese katika gereza hilo Julai 29, 2018. Kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojiwa na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamadi Masauni na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kitalu cha kuzalisha miche ya Michikichi cha Asasi ya Seed Change katika kijiji cha Simbo kwenye jimbo la Kigoma Vijijini Julai 29, 2018. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi hiyo, Alex Chetkovic.
  Wananchi wa Kijiji cha Kazuramimba wilayani Uvinza wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati aliposimama kijijini hapa kuwasalimia Julai 29, 2018. Alikuwa njiani kwenda Uvinza kuendelea na ziara ya mkoa wa Kigoma. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba wilayani Uvinza alipokuwa safarini kwenda Uvinza akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Julai 29, 2018.
   

  0 0

  Kwanza napenda kutumia fursa hii kuwapongeza vijana walioteuliwa kushika nafasi mbalimbali, tambueni Rais amewaamini na amewapa nafasi hizo ili mkawe chachu ya maendeleo katika maeneo yenu ya kazi ili kutekeleza ilani ya CCM na kutatua kero za wananchi hasa wanyonge.

  Najua tangu taarifa ya uteuzi ilipotolewa mmepokea salamu nyingi za pongezi, nawasihi 'msilewe' kwani Rais Magufuli amekuwa akisema katika teuzi zake pongezi ni chache ila pole ndiyo nyingi.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli, mefanya uteuzi na mabadiliko ya viongozi wa wizara, mikoa na wilaya mbalimbali. Ni uteuzi makini kwani Rais amezingatia sifa na mahitaji ya kiutendaji katika kuwaletea wananchi maendeleo.
   
  Tangu uteuzi huu ufanyike kumekua na maneno mengi mitandaoni ya kubeza na kejeli kwa baadhi ya wateule hawa wa Rais na huo ndiyo msingi wa andiko langu.

  Wapo waliotumia maneno makali katika mitandao mbalimbali ya kijamii wakidai Rais Magufuli amewateua wapinzani waliokuwa wakimpinga wakati wa uchaguzi wa 2015 na kuwaacha vijana wa CCM waliohangaika usiku na mchana kuhakikisha kura zake zinatosha na CCM inashinda.Ukichunguza, ni watu hawahawa walipinga ununuzi wa ndege, wakawa wa kwanza kuipanda, wanapinga ujenzi wa reli ya kisasa, huku mataifa makubwa yakiona umuhimu wake, kiasi cha kumuahidi Rais wetu kumsaidia.

  Ni hawa hawa walitangaza hatuwezi kujenga barabara za juu, lakini ndio watakuwa wakwanza kupita pale Tazara, wakienda kupanda Dreemliner pale Uwanja wa JK Nyerere.Watu hawa leo wameibuka kivingine wanajaribu kuuaminisha umma kwamba uteuzi uliofanywa na Rais unashaka ndani yake na hauna afya kwa wanaCCM. Hawa ni watu wa kupuuzwa. Nakupongeza Rais wangu Dk. John Magufuli kwa uamuzi wako wa kuwapotezea.

  Eti wanadiriki kuwataja wateule hawa eti ni wapinzani kana kwamba hawakustahili kupewa nafasi hizo Patrobas Katambi, David Kafulila na Moses Machali. Katika hoja zao mitandaoni wengine wamediriki kusema uteuzi huu umeleta makundi mawili ndani ya chama kwamba eti umeibua vita kati ya CCM asilia wanaobaki watazamaji na CCM wahamiaji wanaopewa nafasi. Kauli kama hizi zinapaswa kupuuzwa kwani zinapandikiza chuki na kuchochea mpasuko ndani ya chama (CCM).

  Kabla sijaendelea nitumie fursa hii kumkaribisha Patrobasi Katambi Dodoma, karibu mh DC tushirikiane kusukuma maendeleo katika jiji letu la Dodoma.Chama Cha Mapinduzi kimejengwa katika misingi ya umoja na ushirikiano unaohanikizwa na kaulimbiu ya Umoja Ni Ushindi. WanaCCM wamejengwa katika misingi hiyo na wanaamini hakuna kununa katika chama kwani kazi za kufanya zipo nyingi ndani na nje ya chama ni suala la muda tu! Hivyo hakuna sababu ya kununa.

  Kwa kuwa wapinzani wanajua silaha kubwa ya CCM ni umoja wanajaribu kupenyeza chuki na kutengeneza makundi ili kusambaratisha umoja huu iliodumu kwa muda mrefu, wanaCCM tusikubali kuingia kwenye mtego huo tukamchukia Mwenyekiti wetu taifa tukamwona anaubaguzi, tuwapuuze.

  Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) katika andiko lake linalozunguka mitandaoni anasema. " Kwa teuzi hizi tuseme vijana wa CCM ni useless? Kwamba Mwenyekiti wa CCM anawaamini sana vijana waliopo upinzani kuliko waliopo CCM? Patrobas Katambi alikuwa Mwenyekiti wa BAVICHA kahamia CCM Mwenyekiti wa CCM akamteua kuwa DC wa Dodoma. Nyota za upinzani zinang'ara CCM wanazitolea macho.

  Akasema maneno kama hayo kwa Machali kwamba alikua Mbunge wa NCCR-Mageuzi akahamia CCM kateuliwa DC wa Nanyumbu na Kafulila aliyekuwa Mbunge NCCR akajiunga Chadema baadae akahamia CCM ameteuliwa kuwa RAS wa Songwe.

  Nataka nimwambie kaka yangu Selasini kwamba, Chama Cha Mapinduzi kina katiba, taratibu na kanuni zake, wanachama wa CCM wote wanahaki sawa kwa mujibu wa katiba ya chama bila kujali idadi ya miezi au miaka yako ndani ya chama, katika chama hakuna mwenyeji na mgeni.

  Namshangaa kaka yangu Selasini anayeshangaa akina Kafulila waliokuwa upinzani na leo wamepewa nafasi baada ya kuhamia CCM, mbona hakushangaa wakati ule Edward Lowassa aliyekuwa CCM na baada ya kuhamia Chadema akateuliwa kuwa mgombea urais wa Chadema tena bila kuwapo mchakato wa kura za maoni?

  Je! Tuseme wanachadema wote akiwamo na yeye mwenyewe walikuwa useless? Frederick Sumaye baada ya kuhamia Chadema akitokea CCM leo ni Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Je! Hapakuwa na wanachadema vindakindaki wenye uwezo hadi nafasi hizo apewe Sumaye mhamiaji?

  Ifahamike kwamba, kila Mtanzania anauhuru wa kujiunga na chama chochote cha siasa. Hii ni kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Haki hii aliyoitumia Lowassa baada ya kuhamia Chadema akateuliwa kuwa mgombea urais, ndiyo haki hiyo hiyo waliyoitumia akina Kafulila baada ya kuhamia CCM wakateuliwa na Rais shida iko wapi?

  Ndiyo maana nasema uteuzi uliofanywa na mh Rais Dk. John Magufuli hauna shaka yoyote na ni uteuzi makini kwani mamlaka ya uteuzi imewaona wanasifa ikawateua kwa nafasi zao.

  Walioteuliwa ni Watanzania wenzetu, tuwaunge mkono na kuwapa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao mapya badala ya kuwabeza na kujaribu kupandikiza chuki kwa wanaCCM. Tanzania ni kubwa kuliko vyama vyetu, tujielekeza katika kumsaidia Rais wetu Dk. John Magufuli katika kuwaletea wananchi maendeleo na azma yake ya kujenga Tanzania Mpya, Tanzania ya Viwanda inafanikiwa.

  Ni muhimu sana kwetu kuhubiri umoja, upendo, amani na mshikamano itatusaidia kama taifa, kuliko kujenga makundi, mifarakano na chuki miongoni mwetu.


  Khamis S. Mkotya

  Mjumbe Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Dodoma

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasliano, Dkt. Leonard Chamuriho akishuka katika ndege mpya ya Serikali ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyoanza rasmi shughuli zake rasmi leo Jumapili Julai 29, 2018 kwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro. Anayemlaki ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira na baadhi ya Watendaji wengine wa Sekretarieti ya Mkoa huo.
   Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira akisalimiana na mmoja wa Marubani wa ndege mpya ya Serikali ya Boeing 787-8 Dreamliner wakati ndege hiyo ilipokuwa ikianza rasmi kazi zake leo jumapili Julai 29, 2018. Ndege hiyoitaanza kufanya  safari zake katika mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwelwe akizungumza na Watendaji, Watumishi na Wananchi mbalimbali waliohuduhuria katika hafla ya kuanza kazi kwa ndege mpya ya Serikali ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyoanza kazi zake leo Jumapili Julai 29, 2018. Kushoto ni Mkoa wa Mwanza John Mongella, na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Antony Diallo.
   . Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leonard Chamuriho akisalamiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira muda mfupi baada ya kushuka katika ndege ya Serikali ya Boeing 787-8 Dremaliner iliyoanza safari zake leo Jumapili Julai 29, 2018. Ndege hiyo itaanza kufanya safari zake katika Mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Mwanza na Kilimanjaro. 
  Mhudumu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), akitoa maelekezo kwa abiria waliopanda ndege mpya ya Serikali ya Boeing 787-8 Dremaliner muda mfupi kabla ya kuondoka Jijini Dar es Salaam kuanza safari zake nchini kwa kuanzia na Mikoa mitatu ya Kilimanjaro, Mwanza na Dar es Salaam.
  (PICHA NA MAELEZO)   

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na mgeni wake Balozi wa 
  Kuwait katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jasem Ibrahuim Al-Najem alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kumuaga Rais, baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na mgeni wake Balozi wa Kuwait katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jasem Ibrahuim Al-Najem alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kumuaga Rais, baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini,[Picha na Ikulu.] 29/07/2018.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na mgeni wake Balozi wa Kuwait katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jasem Ibrahuim Al-Najem alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kumuaga Rais, baada ya mazungumzo yao ambae amemaliza muda wake wa kazi Nchini

older | 1 | .... | 1633 | 1634 | (Page 1635) | 1636 | 1637 | .... | 1897 | newer