Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1632 | 1633 | (Page 1634) | 1635 | 1636 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Serikali imefanya mapitio ya mpango kabambe wa Taifa wa umwagiliaji wa mwaka 2002 kupitia Tume ya Taifa ya umwagiliaji ikiwa na lengo la kuongeza uzalishaji kwa hekta zaidi ya milioni moja nchini kufikia mwaka 2025 kupitia kilimo cha umwagiliaji ili kuweza kukuza uchumi, kuongeza chakula na malighafi za viwandani. 

  Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Mipango, Usanifu na Sekta Binafsi kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Muyenjwa Maugo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. 

  Bw. Maugo Alisema kuwa, Mpango huo kabambe unabanisha kuwa kupitia kilimo cha umwagiliaji chenye kutumia maji ya uhakika na kwa wakati mkulima anaweza kuzalisha awamu mbili au tatu kwa mwaka, na kuwa na uhakika wa chakula kwa kuzalisha tani nane (6) mpaka kumi (10) kwa Hekta tofauti na kilimo cha kutegemea mvua za msimu ambapo mkulima anaweza kupata tani mbili (2) za mazao kwa mwaka kwa hekta, hivyo kwa kuimarisha kilimo cha umwagiliaji malighafi za viwandani zinaweza kupatikana kwa wakati na kufikia hazima ya serikali ya kuijenga Tanzania ya viwanda. 

  “Mpaka sasa eneo la hekta laki 475 ndilo linalotumika kwa kilimo cha umwagiliaji nchini ambayo ni sawa na 1.6% kati ya hekta milioni 29.4, na kuchangia asilimia 24 (24%) ya uzalishaji wa chakula nchini, tuna uwezo wa kuongeza na kufikia asilimia 50 (50%) na tuna lengo la kufikia Hekta milioni moja” Alisisitiza Maugo. Aliendelea kusema kuwa Mpaka sasa kuna skimu 2947 za kilimo cha umwagiliaji nchini ambapo skimu zinazofanya kazi ni 1976, na mpango kabambe upo na malengo ya kuzifufua skimu zisizofanya kazi ili ziweze kufanya kazi. 

  Awali Mhandisi Maugo alisema kuwa mapitio ya Mpango huo kabambe wa kilimo cha umwagilaji unafanyika kwa ushirikiano wa Shirika la Maendeleo la Japan JICA. 
  Kulia Mhandisi Muyenjwa Maugo, Kaimu Mkurugenzi wa Mipango Sanifu na Sekta Binafsi kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akiongea na Muhariri wa kituo cha Televison cha StarTv, Dar es Salaam Leo Bw. Bernad James katika majadiliano maalum kuhusu, kilimo cha umwagiliaji na Tanzania ya viwanda.( Picha na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji).

  0 0


  Mke wa Waziri Mkuu Mhe. Mama Mary Majaliwa akiwakabidhi hundi ya shilingi milioni nne wazazi wa watoto Anjela Francis (4) na Sabina Mnyango (4) fedha ambazo zimetolewa na kikundi cha wake wa viongozi cha New Millenium Group kwaajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto hao ambao wanatibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Mhe. Mama Majaliwa pamoja na wake wa viongozi walipotembelea kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Chain of Hope ya nchini Uingereza.
  Mke wa Waziri Mkuu Mhe. Mama Mary Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wake wa viongozi, wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na wazazi wa watoto ambao kikundi cha wake wa viongozi cha New Millenium Group kimewachangia shilingi milioni nne kwa ajili ya gharama za upasuaji wa moyo. Mhe. Mama Majaliwa pamoja na wake wa viongozi walipotembelea kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Chain of Hope ya nchini Uingereza.
  Mke wa Waziri Mkuu Mhe. Mama Mary Majaliwa akimjulia hali mtoto aliyelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) aliyefanyiwa upasuaji wa kuziba matundu ya moyo katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Chain of Hope la nchini Uingereza. Mhe. Mama Majaliwa pamoja na wake wa viongozi wa kikundi cha Millennium Group walitembelea kambi hiyo leo na kuchangia shilingi milioni nne kwa ajili ya gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto wawili.
  Mke wa Waziri Mkuu Mhe. Mama Mary Majaliwa akimsikiliza Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani akimuelezea aina za upasuaji wa moyo kwa watoto zinazofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati alipotembelea kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Chain of Hope ya nchini Uingereza.

  MKE wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa amewaongoza wake wa viongozi kuchangia sh. milioni nne kwa ajili ya watoto wawili wanaohitaji kufanyiwa upasuaji wa moyo.

  “Kwa umoja wetu, na kwa kuguswa na uhitaji wa watoto wenye matatizo ya moyo, tuliamua tuchange fedha na zimefikia shilingi milioni nne ili tuweze kusaidia kuchangia gharama za matibabu kwa ajili ya watoto wawili,” amesema.

  Ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Julai 27, 2018) wakati akizungumza na baadhi ya wazazi na watumishi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuwatembelea watoto wengine waliofanyiwa upasuaji wiki hii.

  Mama Majaliwa ambaye aliongozana na wake wengine wa viongozi wakiongozwa na Mwenyekiti wa New Millenium Group, Mama Mbonimpaye Mpango, alikabidhi hundi kwa wazazi wa watoto wawili ambao ni Angela Francis (2) na Sabina Mnyango (4).

  Watoto hao ni miongoni mwa watoto tisa wenye umri wa miezi mitatu hadi miaka 17 ambao walipangiwa kufanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na madaktari bingwa wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Chain of Hope la Uingereza. Matibabu hayo yalianza Julai 23, mwaka huu na yanatarajiwa kukamilishwa leo.

  Mama Majaliwa aliwashukuru madaktari na wauguzi wa JKCI kwa uamuzi wao wa kuwafanyia matibabu watoto hao hapa nchini kwani kwa kufanya hivyo wameokoa fedha za Serikali ambazo zingetumika kumtibu kila mtoto kama wangeamua kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu.

  Pia alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Serikali ya awamu ya tano kwa jinsi wanavyoendelea kuimarisha utoaji wa huduma kwenye sekta ya afya hasa kwa mama na mtoto.

  Amesema gharama ya matibabu ya mgonjwa mmoja anapopelekwa nje ya nchi kwa siku 14, inakaribia wastani wa sh. milioni 30. “Kwa kuamua kufanya upasuaji huu hapa nchini, mmeongeza faraja kwa watoto wetu; mmewawezesha ndugu na wanafamilia kuwa karibu zaidi na mgonjwa wao tofauti na hali ambavyo ingekuwa kama upasuaji huo ungefanyika nje ya nchi,” amesema.

  Mama Majaliwa amesema inakuwa vigumu kwa mzazi kutambua mtoto yupi amezaliwa na tatizo la kwenye moyo pindi tu anapozaliwa. “Takwimu zilizopo zinaonyesha kwamba katika kila watoto 100 wanaozaliwa, mtoto mmoja huwa anazaliwa akiwa na tatizo kwenye moyo wake,” amesema.

  Mapema, akitoa taarifa fupi kuhusu taasisi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi alisema wagonjwa wote waliofanyiwa upasuaji wanaendelea vizuri na watoto sita wameruhusiwa kutoka katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) na kupelekwa wodini kuendelea na matibabu.

  Hii ni mara ya tatu kwa matibabu ya moyo kwa watoto kufanyika tangu Januari mwaka huu. Mara ya kwanza madaktari wa JKCI walishirikiana na wenzao kutoka Uingereza; mara ya pili ulifanyika upasuaji wa moyo bila kufungua kifua ambapo wa Save a Child’s Heart(SACH) kutoka Israel na Berlin Heart Centre ya Ujerumani walishiriki na mara ya tatu walishirikiana na taasisi ya Open Heart International(OHI) ya Australia.

  Akitoa shukrani kwa niaba ya wazazi wa watoto hao, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto, Dk. Nice Majani aliwashukuru akinamama hao kwa uamuzi wao wa kuwasaidia watoto wasio na uwezo wa kuchangia matibabu hayo.

  “Tunawashukuru sana kwa msaada wenu kwa sababu kuna wazazi wengine wanashindwa kupata kama hizi kwa sababu ya gharama kubwa za matibabu. Wako Wazazi wanakabiliwa na changamoto za kulea watoto wenye matatizo ya moyo, hawawezi kufanya kazi kama watu wengine kwa sababu ya uhitaji mkubwa wa huduma kwa watoto wao,” alisema.

  Alisema hapa Tanzania kuna watoto wapatao 750 ambao wako nje wakisubiri kupatiwa matibabu kama hayo lakini hawawezi kulazwa wote kwa sababu hakuna nafasi ya kutosha. “Tunatamani kujua ni wapi tutapata mtu wa kutusadia kujenga hilo jengo ili tuweze kuwahudumia watoto wengi zaidi,” alisema.

  (mwisho)

  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU,

  IJUMAA, JULAI 27, 2018.

  0 0


  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis uma (katikati) na Majaji wastaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Benard Luanda (wa tatu kulia) na Mhe. Sauda Mjasiri wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
  Majaji Wastaafu wa Mahakama ya Rufani wakiwa katika nyuso za furaha mara baada ya kuagwa rasmi kitaaluma baada ya kustaafu kwa mujibu wa sheria, kushoto ni Mhe. Benard Luanda na kulia ni Mhe. Sauda Mjasiri, na katikati ni mke wa Mhe. Jaji Luanda.
  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (aliyeketi upande wa juu kulia) akiongoza hafla ya kuwaaga kitaaluma Majaji wastaafu wawili wa Mahakama ya Rufani waliomaliza muda wao kwa mujibu wa sheria, wa kwanza kulia ni Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Benard Luanda, na aliyeketi kushoto ni Jaji Mstaafu, Mhe. Sauda Mjasiri, walioketi mbele ya Wahe. Majaji kushoto ni Msajili, Mahakama ya Rufani, Mhe. John Kahyoza na kulia ni Mhe. Mpepo, Naibu Msajili Mahakama ya Rufani.
  Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (aliyeketi mbele wa kwanza kushoto) pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Watendaji na Watumishi wa Mahakama wakiwa katika sherehe ya kuwaaga Kitaaluma Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani waliostaafu kwa mujibu wa sheria.
  Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga (kulia) pamoja na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati na baadhi ya Watendaji wengine wa Mahakama wakiwa katika hafla hiyo.

  MAJAJI na Mahakimu wameshauriwa kuzingatia sheria katika utoaji haki na wafuate miiko ya kazi zao na kuhakikisha hawafanyi wanayoyataka wao.

  Ushauri huo ulitolewa mapema Julai 27, jijini Dar es Salaam na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Bernard Luanda katika hafla ya kuagwa kitaaluma yeye na Jaji mstaafu wa mahakama hiyo, Sauda Mjasiri iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.

  Hafla hiyo ambayo iliongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma na kuhudhuriwa watu mbalimbali wakiwemo Majaji wa mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu, Majaji wastaafu wa mahakama ya Rufani.

  “Kazi ya kutoa haki ni ngumu, wanapokuja watu mahakamani kila mtu anavutia upande wake, hivyo lazima utumie busara zako na sheria inasemaje,”alisema Jaji Mstaafu, Mhe.Luanda.

  “Majaji na Mahakimu wazingatie sheria, katika mahakama kila hatua ni sheria, lakini siyo sheria tu imani ya wananchi kwa mahakama ni nguzo ya mahakama,” alisema na kuongeza wananchi ni muhimu kwa na imani na mahakama.

  Alisema wananchi wasipokuwa na imani na Mahakama ni hatari kwa kuwa wanaweza kujichukulia sheria mkononi.

  Jaji mstaafu Luanda alisema Majaji na Mahakimu wanapaswa kufanya kazi zao kwa kufuata miiko na wasijaribu kufanya wanavyotaka wao na wasifanye vitu vya ajabu ajabu.

  Mbali na hayo, Jaji huyo Mstaafu ambaye ametumikia Mahakama kwa miaka 38, aliwaeleza Mahakimu na majaji kuzingatia miiko 10 ya kazi zao ikiwemo ya kutojaribu kukwepa majukumu yao katika kutoa uamuzi wa haki, kutojaribu kumtoa hatiani mtu kwa kufahamu mwenendo wake mbaya, isipokuwa uwe umejiridhisha ametenda kosa aliloshitakiwa nalo.

  Pia, wasisite kumwachia mtu ambaye ushahidi wake haujakamilika hata kama katika uelewa wako inaonesha ametenda kosa, wasisite kumtoa hatiani mtu na kumwadhibu ipasavyo kama ushahidi unaonesha ana hatia, bila kujali nafasi yake.

  Jaji Mstaafu Luanda amewaasa Majaji na Mahakimu kutokwenda nje ya ushahidi wa kesi na kutotoa uamuzi kwa kufuata maoni ya ofisa wa mahakama, kutojadili kesi kabla haijakufikia na usiruhusu kujadiliwa ikiwa ipo tayari kwenye mikono na vizuri kujadili kesi ambayo imekuwa historia.

  Jaji mstaafu Luanda ambaye amestaafu akiwa ametumikia mahakama ya Rufani kwa miaka 10 aliwashukuru majaji wenzake, mahakimu, wasajili, manaibu wasajili na wafanyakazi wengine kwa ushirikiano waliompatia katika utendaji wake wa kazi.

  Naye Jaji mstaafu Mjasiri alisema ametumikia mahakama ya Rufani kwa miaka 15 ambapo kabla ya hapo amefanya kazi katika sehemu mbalimbali.

  Jaji mstaafu Mjasiri alisema kuna umuhimu mkubwa kwa wadaawa ambao hawana uwakilishi mahakamani kwenye mashauri mbalimbali katika Mahakama ya Rufani kuwa na uwakilishi wa mawakili kwa kuwa hiyo ndiyo mahakama kubwa hapa nchini.

  Alisema kwa kuwa huyo ndiyo mahakama kubwa, wadaawa wa kesi wanaofika mahakamani wanatakiwa wawakilishwe Ili kuhakikisha wanafuatilia kile kinachoendelea na kipo sawa kwa ajili ya haki
  .
  “Kwa kuwa mahakama ya Rufani ndiyo mahakama ya mwisho, ni muhimu wadaawa kuwakilishwa na mawakili anajua kuna hatua zinachukuliwa kufikia hatua hiyo, lakini zinahitajika za haraka.

  Alisema kwa kuwa kuna wengine wakati wa usikilizwaji wa rufani wadaawa huamua kuachia kila kitu kwenye mikono ya mahakama, kutokana na kutokuwa na uelewe wa kile kinachoendea.

  “Hivyo Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kinatakiwa kuangalia hilo kwa namna mawakili wake watawawakilisha wadaawa ambao hawana uwakilishi,” alisema.

  Kwa upande wake, Jaji Mkuu Profesa Juma alisema kwa kawaida baada ya majaji kustaafu wanaagana kitaaluma ambapo Jaji Luanda ametumikia kwa miaka 37 huku Jaji Mjasiri akiwa ametumikia sehemu mbalimbali na kutumikia mahakama kwa miaka 15.

  Jaji Mkuu Profesa Juma alisema hafla ya kuagwa kitaaluma, mbali ya kutoa ushauri inatoa nafasi kwa majaji wengine wastaafu kukutana.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ujio wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Bw. David Beasley hapa nchini ni fursa itakayowawezesha Watanzania kunufaika kwa kiwango kikubwa katika kilimo, uhifadhi na uuzaji wa mazao ya chakula yanayolimwa hapa nchini. 

  Akizungumza baada ya kukutana na Bw. Beasley jijini Dar es Salaam leo mchana (Ijumaa, Julai 27, 2018), Waziri Mkuu amesema Tanzania inatarajiwa kuwa na ziada ya chakula msimu wa mavuno utakapokamilika mwaka huu hivyo itahitaji sana kupata soko nje ya nchi ili iweze kuuza ziada hiyo.

  Taarifa za Wizara ya Kilimo zinaonesha kuwa mavuno ya mazao ya chakula kama mahindi, maharage na mbaazi yatafikia tani milioni 16 wakati mahitaji ya chakula kwa Watanzania kwa mwaka ni tani milioni 13, hivyo tutakuwa na ziada ya tani milioni tatu,” amesema.

  Akitoa ufafanuzi, Waziri Mkuu amesema hadi kufikia Julai 2018 ambapo msimu wa mavuno bado unaoendelea, tayari nchi ina ziada ya tani milioni moja kwani taarifa za Wizara ya Kilimo zinaonyesha kuwa tayari zimekwishavunwa tani milioni 14.

  Amesema hatua ya WFP kukubali kununua chakula cha ziada kitakachozalishwa hapa nchini imewahakikishia Watanzania kuwa mazao yao hayatakosa soko kwani utaratibu wa uuzaji na ununuzi wa nafaka hasa mahindi unafanywa na Wizara ya Kilimo ikishirikiana na WFP.

  Ili kuhakikisha usalama wa chakula kinachozalishwa nchini, Serikali inajenga maghala ya kuhifadhi nafaka kwenye mikoa minane yenye uwezo wa kuhifadhi chakula cha kutosha kwa viwango vinavyokubalika na vinavyolinda afya za walaji.

  Waziri Mkuu amesema Mkurugenzi huyo, Bw. Beasley ambaye ametembelea vijiji kadhaa katika Halmashauri za Songea, Namtumbo na Madaba mkoani Ruvuma alijionea jinsi wananchi walivyopata mavuno mazuri hasa mahindi. “Amesema Serikali inahitaji kuweka mkazo mkubwa katika kujenga maghala ya kisasa ya kuhifahia nafaka ili kuepuka uharibifu wa mazao unaoweza kusababishwa uhifadhi duni wa mazao.”

  Amesema akiwa mkoani Ruvuma, Bw. Beasley alitembelea maghala kadhaa ya kuhifadhia mahindi na kugundua kuwa ipo changamoto inayohitaji kutatuliwa haraka iwezekanavyo katika eneo hilo kuanzia ngazi ya wilaya.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  IJUMAA, JULAI 27, 2018.


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, David Beasley, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Julai 27, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, David Beasley, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Julai 27, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimikana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, David Beasley kabla ya mazungumzo yao kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Julai 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Mbunge wa Chato, Dk. Medard Kalemani, ambaye pia ni Waziri wa Nishati, akimtambulisha kwa kina mama walioepeka watoto wao Kliniki leo, katika Hospitali Wilaya ya Chato, ambapo alitumia fursa hiyo kumtambulisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile. 
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, akizungumza na mmoja wa watoto katika Hoaspitali ya Wilaya ya Chato. Kulia ni Mbunge wa Chato ambaye pia Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani. 
  Mbunge wa Chato, Dk. Medard Kalemani, ambaye pia ni Waziri wa Nishati, akizungumza wakati wa kumkaribisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, ambaye leo amewasili Wilayani Chato kwa ziara ya kikazi.   MBUNGE wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani (CCM), aliishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vipya vya afya wilayani Chato. 

  Hospitali hiyo kubwa ya kisasa inajengwa na serikali kwa gharama ya Sh bilioni 9.1 ambapo hadi sasa zimetolewa Sh bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi huo. 

  Amesema ujenzi wa hospitali kubwa ya rufaa ya kisasa inakuwa msaada kwa wananchi wa mikoa ya Geita na Kagera ambao walikuwa wakisafiri umbali mrefu kutafuta huduma za afya kwa madaktari bingwa. 

  Akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu yake ya kibunge kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, leo Mjini Chato, alisema kuwa anaishukuru Serikali wakati wote kwa kusaidia maendeleo ya jimbo lake hasa kwenye sekta ya afya. 

  “Ninaishukuru Serikali pamoja na nawe Mheshimiwa Naibu Waziri ambaye muda wote umekuwa msaada kwetu wananchi wa Chato, kwa miaka mitatu mfululizo ninapoleta maombi yangu ya ujenzi wa vituo vya afya muda wote wizara yako imekuwa ikitupa fedha. 

  “Na kukamilika kwa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Chato, itakuwa mkombozi kwani itaweza kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi wa Chato, Geita, Muleba na Biharamulo. 

  “Hata hivyo bado ninaishukuru sana Serikali kwa mwaka wa tatu mfululizo niliomba pesa kwa ajili ya zaidi ya Shilingi milioni 400 ujenzi wa kituo cha afya Bwanga nilipewa. Na bado hata Chato tuliletewa magari mawili ya kubebea wagonjwa (Ambulance) ambayo ni mazima na yanatoa huduma nzuri,” alisema Dk. Kalemani 

  Licha ya hali hiyo alisema anafuatilia ujenzi wa hospitali hiyo kila mwezi na pale kwenye changamoto hulazimika kufikisha kilio chake kwa Wizara ya Afya kwa ajili ya kupata ufumbuzi. 

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, alisema Serikali imesema itahakikisha inatoa fedha zote kwa wakati ili hospitali hiyo iweze kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi wa Mkoa wa Geita pamoja na Wilaya za Biharamulo na Muleba za Mkoa wa Kagera. 

  Akizungumza jana mjini Chato Mkoani Geita, baada ya kukagua pamoja na mikoa ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta huduma bingwa za afya katika Hospitali ya Bugando Jijini Mwanza. 

  Amesema hatua ya kukamilika kwa hospitali hiyo itakuwa msaada kwa wananchi wa maeneo hayo ambayo walikuwa wakisafari umbali mrefu kutafuta huduma za afya za kibigwa. 

  Kutokana na ujenzi huo, Dk. Ndugulile, aliitaka Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), kuhakikisha wanakalimisha ujnzi huo kwa wakati kwa mujibu wa mkataba ili huduma za afya zianze kutolewa kwa wagonjwa. 

  “TBA ninaomba sana mkamilishe kwa haraka ujenzi wa hospitali hii kubwa ya kisasa ili wananchi waanza kupata huduma za afya za kibingwa. Pamoja na kazi hii nzuri ni nawaagiza wataalamu wa afya mtembelee mara kwa mara kwa lengo la kutoa ushauri wa aina ya majengo ya afya,” amesema Dk. Ndugulile 

  Awali akitoa taarifa ya ujenzi huo, Kaimu Meneja wa TBA, Mhandisi Gladys Jeffa, amesema hadi kukamilika kwa mradi huo kutagharamu Sh bilioni 9.1 ambapo tayari Serikali imeshatoa Sh bilioni 2 katika robo ya kwanza ya ujenzi huo ambapo ujenzi huo unatarajiwa kukamilika Machi, 2019.

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu, akishirikiana na wananchi wa Kata ya Sepuka mkoani humo juzi, kuandaa eneo kitakapo jengwa Kituo cha Afya cha kisasa ambacho kitagharimu shilingingi milioni 400.
  Wananchi wa Kata ya Sepuka wakiandaa eneo hilo.
  Mbunge Elibariki Kingu akiwa kazini sanjari na wananchi wa Kata ya Sepuka.
  Mbunge Elibariki Kingu akibadilishana mawazo na wazee wa Kata ya Sepuka.
  Wananchi wa Kata ya Sepuka wakizungumza na Mbunge wao, Mheshimiwa Elibariki Kingu.
  Wananchi waking'oa visiki katika eneo kitakapo jengwa kituo cha Afya cha kisasa.
  Wanawake wa Kata ya Sepuka wakiandaa kitoweo kilichonunuliwa na Mbunge huyo ili kiliwe na wananchi baada ya kazi ya kuandaa eneo kitakapo jengwa kituo hicho cha afya.
  Kazi ya kuandaa eneo hilo ikiendelea.
  Mbunge Elibariki Kingu akishirikiana na wanawake wa Kata ya Sepuka kukata nyama ya kitoweo.
  Ng'ombe akichinjwa kwa ajili ya kitoweo. 
  Mbunge Elibariki Kingu, akiwahutubia wananchi wa Kata ya Sepuka baada ya kuandaa eneo kitakapo jengwa kituo cha afya, ambapo aliwaeleza miradi mbalimbali iliyofanywa na inayoendelea kufanywa katika jimbo hilo la uchaguzi la Singida Magharibi.
  Wananchi wa Kata ya Sepuka wakimsikiliza Mbunge wao.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa Mbeya mjini kwenye viwanja vya Ruandanzovwe, Makamu wa Rais yupo mkoani Mbeya kwenye ziara ya kuhamasisha maendeleo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia waliokuwa madiwani wa Chadema ambao wametangaza rasmi kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Ruandanzovwe Mbeya mjini. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Mhe. Joseph Mbilinyi (Chadema) mara baada ya kumaliza kuhutubia wakazi wa Mbeya mjini kwenye viwanja vya Ruandanzovwe, Makamu wa Rais yupo mkoani Mbeya kwenye ziara ya kuhamasisha maendeleo.
  Sehemu ya Wakazi wa Mbeya mjini waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya Ruandanzovwe. 
  Sehemu ya Wakazi wa Mbeya mjini waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya Ruandanzovwe. 
  Sehemu ya Wakazi wa Mbeya mjini waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya Ruandanzovwe.

  0 0


  Hyasinta Kissima- Afisa Habari Halmashauri ya Mji Njombe

  Halmashauri ya Mji Njombe imepokea jumla ya pikipiki 13 zenye thamani ya shilingi milioni 39 kwa waratibu elimu Kata 13 lengo ikiwa ni kufanya ufatiliaji na usimamizi wa elimu katika Kata.

  Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Salum Mkuya amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuboresha sekta ya elimu kwa kuhakikisha kuwa wasimamizi wa elimu wanawezeshwa upatikanaji wa vitendea kazi ili kufanya mazingira ya kazi kuwa rafiki.

  “Pikipiki hizi zikafanye kazi ya ufuatiliaji kwa kupandisha kiwango cha ufaulu, kuhakikisha wanafunzi wanajua kusoma na kuandika ikiwa ni sambamba na kuthibiti utoro mashuleni.”Alisema Mkuya

  Aidha, Mkuya ameiomba Halmashauri kuhakikisha kuwa pikipiki zote zilizokabidhiwa zinapatiwa bima kama serikali ilivyoagiza.

  Naye mwenyekiti wa Halmashauri Edwin Mwanzinga amesema kuwa anaishukuru serikali ya CCM kupitia kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa kutambua umuhimu wa pikipiki hizo kwa waratibu elimu kwani itarahisisha shughuli za usimamizi na ufuatiliaji elimu hususani katika Halmashauri ambazo maeneo mengi jiografia yake ni ngumu kufikika kutokana na ukubwa wa eneo halikadhalika changamoto za miundombinu.

  “Najua waratibu mlikua mnafanya kazi katika mazingira magumu niwaombe sasa tukafanye kazi bila visingizio na ni lazima tuwe wa kwanza kimkoa kwa sababu tumepata vitendea kazi. Lakini niwaombe sana mkazitunze pikipiki hizi ili tuweze kwenda nazo kwa muda mrefu. Kwa wale ambao hamjui kuzitumia tusitumie pikipiki hizi kujifunzia. Ni imani yangu mtaenda kujifunza mpate leseni na muweze kuzitumia vizuri na kwa tahadhari” Mwanzinga alisema

  Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya waratibu elimu Ester Mjuu Mratibu Elimu Kata ya Ramadhani Halmashauri ya Njombe alisema kuwa sasa wataweza kufika kila kona ya Kata zao katika kufuatilia usimamizi wa elimu.“Tunashukuru sana kwa vitendea kazi hivi,miongoni mwa changamoto iliyokuwa inatukabili imepata ufumbuzi tutaenda kufanya kazi kwa kadri mlivyotuelekeza ili kuhakikisha kuwa tunakuwa na Taifa la wasomi kwa kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa karibu kwenye sekta ya elimu.”Alisema
  Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Salum Mkuya akikabidhi Pikipiki kwa ajili ya waratibu elimu Kata 13 kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Edwin Mwanzinga.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Edwin Mwanzinga akitoa mkono wa pongezi kwa Mratibu Elimu Kata ya Ramadhan Ester Mjuu mara baada ya kumkabidhi pikipiki.
  Waratibu Elimu Kata kutoka Katika Kata 13 za Halmashauri ya Mji Njombe wakipongeza serikali kwa jitihada za kuwapatia Pikipiki ikiwa kama nyenzo muhimu katika utekelezaji wa majukumu yao.

  0 0

  Na Luteni Selemani Semunyu

  Wachezaji wa klabu Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo imewasili salama Mufindi Mkoani Iringa kwa ajili ya kushiriki mashindano ya wazi ya mufindi ya utalii karibu Kusini Mufindi gofu challenge yanayotarajiwa kuanza kesho(leo) kwa wachezaji wa ridhaa..

  Akizungumza mara baada ya kuwasili Afisa Utawala wa klabu ya Lugalo Kapteni Amanzi Mandengule alisema timu imewasili salama na hakuna majeruhi na siku ya leo wataitumia kwa ajili ya mazoezi ili kuufahamu uwanja.“ Tumefika salama na Timu yetu sote tukiwa salama na Wachezaji wetu wa Kulipwa wameingia uwanjani leo ikiwa ndio siku yao na tunaimani tutafanya vizuri pia kwa kundi hilo” Alisema Kapteni Mandengule.

  Kapteni Mandengule aliongeza kuwa licha ya kuwa wamefika salama lakini kuna changamoto ya hali ya hewa kwani Mufindi ni baridi ukilinganisha na Dar es Salaam ambapo hali nin ya Joto lakini watapambana kwa kuwa walilifahamu hilo.Kwa upande wa wachezaji wa kulipwa wachezaji 11 wameingia uwanjani kumenyana katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa iringa kwa kushirikiana na wizara ya maliasili na utalii yakilenga kutangaza fursa na vivutio vya utalii nyanda za juu kusini.

  Katika hatua ya mwanzo ya michuano hiyo Mchezaji George Leverian wa Lugalo ameibuka na ushindi kwa kupiga mpira mrefu na wameingia katika Raundi ya pili itakayoamua mshindi katika vipengele vingine na ushindi wa Jumla.Katika mashindano hayo ya siku tatu mbali na kushiriki katika mashindano hayo lakini watapata fursa ya kutembelea na kujifunza masuala mbalimbali kuhusu sekta ya utali hususani utalii wa nyanda za juu kusini.

  Mbali na wachezaji wa kutoka Klabu ya Lugalo pia Wachezaji kutoka Vilabu vya Morogoro Gymkhana, Dar es Salaam Gymkhana, Moshi Club ,TPC, Kili Golf Club ya Arusha na wenyeji klabu ya Mufindi ya Iringa watashiriki katika mashindano hayo.
  Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Golf ya Lugalo wakiwasili katika uwanja wa Gofu wa Mufindi mkoani Iringa yenye lengo la Kutangaza vivutio vya Utalii vya nyanda za juu kusini hususani Mufindi.
  Mchezaji gofu wa kulipwa kutoka Klabu ya Lugalo Geofrey Leverian aliyeibuka mshindi kwa kupiga mpira Mrefu akipiga Mpira wakati wa Mashindano ya wazi ya Mufindi yenye lengo la Kutangaza vivutio vya Utalii vya nyanda za juu kusini hususani Mufindi.

  0 0

  Frank Mvungi- MAELEZO, Tunduru

  Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari (MAELEZO) vimepongezwa kwa kubuni na kuweka utaratibu wa kufuatilia utendaji wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini hadi katika ngazi ya Halmashuri.

  Akizungumza na Ujumbe wa chama hicho uliofika Ofisini kwake mapema wiki , Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Bw. Chiza Marando amesema kuwa hili ni jambo la kihistoria ambapo ufuatiliaji wa utendaji wa Maafisa Habari unafanyika katika ngazi zote.

  “Tangu nimeanza kazi sijawahi kushuhudia ufuatiliaji wa namna hii na sisi tuko tayari wakati wote kutoa ushirikiano utakaosaidia Afisa Habari katika Halmashauri yetu atekeleze majukumu yake vizuri hasa katika kutangaza miradi ya maendeleo” Alisisitiza Marando

  Akifafanua Bw. Marando amesema kuwa Halmashuri yake inatambua umuhimu wa mawasiliano kati ya Serikali na Wananchi hivyo imeweka kipaumbele katika kuwezesha utoaji wa taarifa za maendeleo kwenda kwa wananchi ili waweze kushiriki katika kujiletea maendeleo.

  Kwa upande wake Kiongozi wa Msafara wa Viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari – MAELEZO Bi. Gaudensia Simwanza amesema kuwa maafisa habari wanalo jukumu kubwa katika Halmashauri na Mikoa katika kutangaza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yao.

  Aliongeza kuwa kutokana na jukumu hilo wanapaswa kutumia rasilimali zilizopo kutekeleza jukumu hilo kwa weledi.

  Ziara ya Viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini na Idara ya Habari MAELEZO inafanyika katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kufuatilia na kuona utendaji wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini katika ngazi zote ili kutoa msukumo na kuweka mikakati ya pamoja katika kuimarisha Mawasiliano ya Serikali kwa umma ili kuchochea maendeleo na ustawi wa wananchi.
  Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza Marando akisisitiza kuhusu namna Halmashuri hiyo ilivyojipanga katika kuimarisha mawasiliano ya kikakati hasa kutangaza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.
  Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza Marando akisisitiza jambo kwa ujumbe wa chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO wakati wa ziara ya ujumbe huo katika Halmashauri hiyo kukagua na kujionea jinsi maafisa Habari wanavyotekeleza jukumu la kuisemea Serikali katika Mikoa na Halmashuri zao.
  Kiongozi wa Ujumbe wa Viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Gaudensia Simwanza akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza Marando wakati wa ziara ya ujumbe huo katika Halmashuri hiyo uliolenga kukagua na kuweka mikakati ya pamoja katika kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma.
  Mwakilishi wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo akisisitiza umuhimu wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kuwajibika katika kuisemea Serikali hasa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mikoa na Halmashuri zao, hiyo ilikuwa katika ziara iliyoandaliwa na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na Idara ya Habari MAELEZO.

  0 0

  *Afurahishwa na idadi kubwa ya wananchi wanavyojitokeza kupima afya bure
  *Ataja kiini cha kuongezeka kwa kasi magonjwa yasiyo ya kuambukiza nchini

  Na Said Mwishehe, Glob ya Jamii.
   

  DAKTARI Bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Heameda Medical Clinic Dk.Hery Mwandolela amesema uamuzi wa kuweka kambi ya kupima afya za wananchi bure katika Clinic hiyo inalenga kuwahamasisha wananchi wanapata fursa ya kutambua afya zao mapema.

  Kwa sasa Heameda Medical Clinic ipo katika kampeni hiyo ya kupima afya za wananchi bure iliyoanza Julai 26 na inatarajia kumalizika Julai 27 mwaka huu.

  Akizungumza leo na Michuzi Blog wakati wa kamepeni hiyo Dk.Mwandolela amesema Heameda Medical Clinic iliyopo Bunju B jijini Dar es Salaam imeamua kutenga siku tatu ili kutoa huduma hiyo ya wananchi kuwapima afya zao bila gharama yoyote.

  "Tumeamua kutenga siku tatu hizi kwa ajili ya kuwahudumia wananchi na jambo la kubwa na la kujivunia ni namna ambavyo wamejitokeza kwa wingi kupima afya zao.Kwetu sisi kampeni hii ni sehemu ya shukrani kwao.

  "Kupima afya ni jambo la msingi katika maisha ya binadamu kwani husaidia kujitambua mapema na kama kuna tatizo inakuwa rahisi kupata ushauri kulingana na madaktari bingwa watakavyoshauri.

  "Tunajisikia fahari pale mtanzania anapojenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara.Heameda Medical Clinic tupo kwa ajili ya kuwahudumia na kipindi hiki cha kampeni tumeungana na madaktari bingwa wengine nchini pamoja na madaktari bingwa kutoka India.Lengo ni kuhakikisha afya ya mtanzania inakuwa salama wakati wote,"amefafanua.

  Kuhusu magonjwa ambayo wanapima kwenye kampeni hiyo amesema wanapima magojwa ambayo si ya kuambikiza ambayo kwa kipindi hiki yameshika kasi na kusababisha vifo vya wananchi walio wengi.

  Amesema kuwa magonjwa yatokanayo na moyo ndio yanayoongoza kwa kuua yakifuatiwa na magonjwa mengine yakiwamo ya kisukari na shinikiza la damu.
  "Kuna sababu nyingi zinazosababisha magonjwa yasiyoambukiza kushika kasi nchini kwetu na mojawapo ni mfumo wa maisha ambao umebadilika sana.

  "Watu wanakula vyakula ambavyo kwa sehemu kubwa vimejaa wanga, vyakula vyenye mafuta mengi, sigara na kutofanya mazoezi.Hivyo tunashauri jamii kuangalia mfumo wa maisha wanayoishi na kuwa makini na vyakula wanavyokula,"amesema Dk.Mwandolela.

  Alipoulizwa hatua gani inafuata baada ya kutoa huduma ya pima afya bure? Dk.Mwandolela amejibu wale watakaobainika kuwa na tatizo watapata ushauri wa kitaalamu na kama inahitaji kuanza tiba watashauriwa na si lazima iwe kwao.

  Kuhusu idadi ya wagonjwa ambao wamewahudumia kwa siku ya jana na leo amesema ni zaidi ya wananchi 250 na miongoni mwao wapo waliotoka mikoa mbalimbali baada ya kusikia kutakuwa na madaktari bingwa wa magonjwa wa moyo wakiwamo waliotoka India kuwa watatoa huduma bure.

  Akizungumzia malengo yao amesema wana mpango wa kuhakikisha wanakuwa na utaratibu wa kampeni ya aina hiyo ya mara kwa mara itakayofanikisha wananchi kupima afya zao na kwa kutumia madaktari bingwa wa Heameda Medical Clinic watashiriki kikamilifu katika kutoa mchango wao katika eneo afya kwa wananchi.

  Pia amasema katika Clinic hiyo ambayo madaktari wake wamebobea katika magonywa ya moyo ni kuhakikisha wote ambao wanabainika kuwa na ugonjwa wa moyo wanapata huduma hapa hapa nchini na hakutakuwa na sababu ya kwenda nje ya nchi.


  Mmoja wa madaktari wa Heameda Medical Clinic iliyopo Bunju B jijini Dar es Salaam wakiendelea kutoa huduma ya upimaji afya bura kwa mmoja wa wakazi wa eneo hilo.
  Baadhi wananchi mbalimbali wakiwa wamejitokeza Heameda Medical Clinic kupima afya zao.
  madaktari wa Heameda Medicla Clinic iliyopo Bunju B jijini Dar es Salaam wakiendelea kutoa huduma ya upimaji afya bura kwa wananchi

  0 0

  ais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na mgeni wake Balozi wa Jamhuri ya Malawi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bibi.Hawa Olga Ndilowe alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kumuaga Rais, akimaliza muda wake wa kazi Nchini
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na mgeni wake Balozi wa Jamhuri ya Malawi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bibi.Hawa Olga Ndilowe alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kumuaga Rais, kwa kumaliza muda wake wa kazi Nchini

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na mgeni wake Balozi wa Jamhuri ya Malawi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bibi.Hawa Olga Ndilowe baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kumuaga Rais,kwa kumaliza muda wake wa kazi Nchini,[Picha na Ikulu.] 27/07/2018.

  0 0

  SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), lipo mbioni kuiunganisha Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera na umeme wa gridi ya Taifa ili kuvutia wawekezaji hasa wa sekta ya viwanda nchini.

  Akizungumza leo wakati wa kazi ya kuunganishaji wa laini ya umeme wa grid ya Taifa inayofanyika katika vijiji ya Kitete Wilayani Chato Mkoani Geita, Meneja wa Tanesco Wilaya ya Muleba, Julius Bagasheki, amesema kazi ya uunganishaji wa umeme wa gridi ni utekezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya chama tawala CCM kwa kuhakikisha wanatekeleza sera ya Tanzania ya Viwanda.

  Amesema umeme huo wa gridi kwa Wilaya ya Muleba tayari wameanza na mradi wa uunganishaji 33KV ambao sasa unakwenda kuifanya Muleba kuwa na umeme wa uhakika.

  “Umeme wetu tunachukulia kutoka Uganda ila ila kwa mradi huu sasa unakwenda kuifanya Wilaya ya Muleba kuwa na umeme wa uhakika wa gridi wa Taifa ambao haukatiki ovyo.

  “Sisi Tanesco Muleba na Mkoa wa Kagera kwa ujumla tumejipanga vema kuitekeleza kwa vitendo sera ya Tanzania ya viwanda. Hivyo tunawaalika wawekezaji mbalimbali hasa wa sekta ya viwanda sasa waje Muleba kujenga viwanda kwani muda si mrefu tunakwenda kuwa na umeme wa uhakika wa gridi ya Taifa ambao ni mkombozi wa uhakika,” amesema Bagasheki

  Baadhi ya wananchi ambao wameshafikiwa wa umeme wa REA III, katika Kijiji cha Kitete, wamesema kuwa hatua ya kupata huduma hiyo sasa wanakwenda kupata maendeleo ya kasi ya kuweza kujiletea maendeleo kwa kuwa na uhakika wa umeme.

  Mmoja wa wananchi hao Veronica John, ambaye ni mmiliki wa Duka la Dawa Muhimu (DLDM) ameishukuru serikali kwa kuwafikishia huduma ya umeme kwwenye kijiji chato.

  “Mwanzo tulikuwa tunanunua mafuta ya taa kwa gharama kubwa lakini baada ya serikali tuletea umeme nasi sasa tutapata maendeleo. Hivi karibuni nitatununua jikofu kwa ajili ya kuhifadhi dawa ili zisiweze kuharibika baada ya kupata umeme. Kwa kweli tuna furaha ya hali ya juu,” amesema Monica

  Naye Kinyozi Makoye Mwango, amesema kuwa hatua ya kupata umeme imemsadia kutoa huduma ya uhakika kwa wateja wao ambao hufika kunyoa nywele kwa uhakika.

  “Awali tulikuwa tunachaji betri kwa gharama kubwa na unanyoawateja wawili hadi watatu…kwa sasa baada ya umeme kuja kwa kweli ninaweza kunyoa watu wengi za zaidi na kipato changu kimeongezeka mara dufu, hongera serikali pamoja na Tanesco,”amesema Mwango 
   Meneja wa Tanesco, Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera, Julius Bagasheki, akieleza kuhusu kazi ya uungwanishaji wa umeme wa gridi ya Taifa ambayo itasaidia kupata umeme wa uhakika ili kuruhusu uwekezaji wa viwanda vya uhaka wilayani hapa
   Meneja wa Tanesco, Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera, Julius Bagasheki (mwenye fulana ya mistari) akiwaongoza mafundi wa Tanesco, kusimika nguzo mpya ili kuruhusu uunganishahi wa umeme wa gridi ya Taifa
   Mafundi wakiendelea na kazi ya kuunganisha nyaya ili kuweza kuinganisha Wilaya ya Muleba kwenye umeme wa uhakika wa gridi ya Taifa.
   

  0 0
  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa ametembelea mradi mkubwa maji wa bwawa katika Mto Rufiji utakaoweza kusaidia matumizi ya maji kwenye kambi ya ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge)

  Mradi huo unaotekelezwa Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia  Mamlaka ya Maji safi na Maji taka (DAWASA) na umeweza kugharimu kiasi cha Milioni 604.9 ukiwa ni muendelezo wa mradi mkubwa wa maji unaoendelea Kisarawe.

  Akizungumza baada ya kutembelea maporomoko ya Mto Rufiji Prof Mbarawa amesema kuwa mradi huo wa maji utakuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita 209,000( laki mbili na elfu tisa) kwa ajili ya matumizi ya kambi ya ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge).

  Amesema, mradi huo wa maji utawasaidia wakandarasi kusa na miundo mbinu wezeshi itakayowapatia maji muda wote wa matumizi yao ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanusi mkubwa.

  "Miundo mbinu wezeshi itawapa fursa wakandarasi wafabye kazi kwa ufanisi mkubwa sana kwa  sababu maji yatakuwa yanapatikana muda wote na kila siku na hili litasaidia katika kuhakikisha mradi wetu wa ujenzi wa bwawa la umeme kumalizika kwa muda ulipangwa,"amesema Prof Mbarawa.
   Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akifunga bomba la kisasa la kusafirishia maji  kwenye eneo la kambi lenye jumla ya Km 1463,kipenyo cha nchi 1.5 na nchi 3 kwenye eneo la ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge).
   Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akifunikia bomba la kusafirishia majighafi kwenye eneo la kambi lenye jumla ya Km 1463,kipenyo cha nchi 1.5 na nchi 3 kwenye eneo la ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge).
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dr Suphian Masasi wakiwa wanakagua  bwawa la kusafishia maji yanayotoka katika Mto Rufiji kwa ajili ya matumizi ya wakandarasi waujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge).
   Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makamd Mbarawa akirusha maji katika moja ya bwawa la kusafishia maji yanayotoka katika Mto Rufiji kwa ajili ya matumizi ya wakandarasi waujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge).
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akiwa anakagua mradi mkubwa wa maji katika Bwawa la Mto Rufiji utakaoweza kuwasaidia wakandarasi kupata maji ya uhakika kwenye ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge) akiambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka (DAWASA) Dr Suphian Masasi.

  0 0

  Yasema wasipojirekebisha italivunja baraza lao

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku 30 kwa Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kujirekebisha na kumaliza tofauti zao ndani ya siku 30 na iwapo wataendelea na vurugu Serikali haitosita kuvunja baraza la Madiwani.

  Amesema hatua hiyo inatokana na Madiwani hao kutumia muda mwingi wakigombana badala ya kuwahudumia wananchi, Serikali inataka kuona wananchi wakihudumiwa kwa kuboreshewa maendeleo katika maeneo yao na si kushuhudia viongozi wakigombana kwa maslahi binafsi. 

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Julai 28, 2018) wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Kigoma katika mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Kigoma Ujiji kwenye uwanja wa Kawawa, akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Kigoma.

  “Serikali hairidhishwi na utendaji wenu na nimewapa muda wa mwezi mmoja kumaliza tofauti zenu. Nataka muendelee kufanya kazi za kuwatumikia wananchi wa Manispaa hii ambao wamewachagua ili muwatatulie kero zao na si kuendeleza migogoro,” amesisiza.

  Amesema Madiwani hao wanatakiwa kufuatilia changamoto zinazowakabili wananchi wao ikiwemo ya upatikanaji wa dawa katika hospitali, zahanati na vituo vya afya, ambapo licha ya Serikali kutoa fedha nyingi kwa ajili ya ununuzi wa dawa lakini bado wananchi wanaendelea kukosa huduma hiyo.

  Waziri Mkuu amesema matatizo ya madiwani wa Manispaa hiyo anayafahamu na iwapo watashindwa kujirekebisha Serikali haitosita kulivunja baraza hilo kwa sababu Madiwani wake wanatumia muda mwingi kugombana badala ya kuwahudumia wananchi.

  Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amewahakikishia wananchi wa mkoa wa Kigoma kwamba Serikali itaboresha miundombinu ya mkoa huo ikiwemo ya reli, barabara, ujenzi wa bandari na uwanja wa ndege utakaokuwa na uwezo wa kutua ndege kubwa.

  Amesema lengo la maboresho hayo ni kuufanya mkoa huo kuwa kitovu cha biashara utakaounganisha nchi za Rwanda, Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Burundi kwa kuimarisha vivutio vya uwekezaji.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAMOSI, JULAI 28, 2018.
  Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa akizungumza wakati alipoongoza Mkutano wa Wadau wa Michikichi kwenye ukumbi wa NSSF mjini Kigoma Julai 28, 2018. Kulia ni mkewe Mary na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga. 
  Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa akizungumza wakati alipoongoza Mkutano wa Wadau wa Michikichi kwenye ukumbi wa NSSF mjini Kigoma Julai 28, 2018. Kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba.
  Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Michikichi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipoongoza mkutano huo kwenye ukumbi wa NSSF mjini Kigoma Julai 28, 2018.

  0 0

  Na Ahmed Mahmoud Arusha

  Chama cha mapinduzi kimesema kuwa kipo kwa ajili ya kuwatumikia na kusikiliza shida za wananchi na wamejipanga kuhakikisha wanaisimamia serikali ipasavyo ili ilani ya chama hicho inatekelezwa kwa asilimia zote na serikali inayoongozwa na chama hicho.

  Akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni ya ccm katika kata ya Kaloleni jijini Arusha Naibu Katibu mkuu wa ccm Bara Rodrick Mpogoro amesema kuwa wakazi wa jiji la Arusha wanategemea sekta ya utalii na jiji hilo ni kitovu cha utalii ndio maana ccm chini ya serikali inayoongozwa na chama hicho ikaona hilo na kuamua kufufua shirika la ndege ili watalii waje moja kwa moja na kusaidia mkoa huo kukua kiuchumi.

  Amesema kuwa mgombea wa chama cha mapinduzi kwenye kata hiyo atasaidia ukuaji wa maendeleo kwa wananchi na kuhakikisha kuwa malengo ya huduma bora yanawafikia wananchi kwa kasi badala ya hapo awali kwani chama hicho kimejipanga kuhakikisha wanashinda chaguzi mbali mbali kama hapo awali.

  “Najua Teyari wagombea 12 wa ccm wanasubiria kuapishwa kati ya wagombea 20 hivyo hawa 8 ninaimani kuwa nao watapigiwa kura na chama chetu kuendelea kupata ushindi katika uchaguzi huu”alisema Mpogoro

  Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya siasa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka alisema anayoimani na chama hicho kushinda uchaguzi kwani teyari dalili zinaonyesha kuwa chama hicho teyari kimeshinda kwa kishindo uchaguzi huo.

  Amesema kuwa wakati akimndai mgombea urais wa ccm 2015 kwenye uwanja wa sheikh Amri Abeid aliwaambia huyu ndio rais lakini wengi walimshangaa na kuona kinyume kwa mapenzi yao lakini sasa wanaona yale aliyowaeleza na wengi wanakubaliana na kauli hiyo.

  “Najua wengi mmesahau wakati ule wa kampeni ya urais leo nakuja tena hawa wanaorudi ccm sio bahati mbaya hata mgombea wa ukawa 2015 alishasema upinzani ukishindwa uchaguzi huo wasubiri miaka 50 sasa wenyewe mnaona hilo linajitokeza kwa sababu alitambua mgombea wa ccm ni mtu muadilifu na anafanyakazi kile anachoamini kwa maslahi ya wanyonge”alisema sendeka

  Nae Moja wa wananchi wa Kaloleni na Kada wa chama hicho John Mshana amesema kuwa anaamini wagombea waliotoka chadema wameaacha maslahi mapana na kuamua kuona wananchi waliowachagua ndio wenye maamuzi na wao kurudi ccm kwa maslahi mapana ya wananchi kuwatumikia kwa mapana badala ya huko walikokuwa awali.

  Amesema kuwa kulikuwa na mtu mmoja alikuwa mjanja sana akamshika kipepeo na kumuuliza mwenzake mjanja huyu kipepeo amekufa au yu hai basi Yule mwezake alijibu kuwa uhai wa kipepeo upo mikononi mwako ndio hawa wagombea wetu uhai na maendeleo ya wananchi yapo mikononi mwao kwa sasa.

  0 0

  *Lengo ni kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula nchini

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua kampeni ya kufufua zao la michikichi mkoani Kigoma na kuagiza kuanzishwa kwa kituo cha utafiti wa zao hilo katika chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Kihinga kilichopo mkoani Kigoma kwa kuwa ndiko zao la Michikichi linalimwa kwa wingi.

  Amesema Serikali imedhamiria kumaliza changamoto ya upatikanaji wa mafuta ya kula nchini kwa kuhamasisha kilimo cha zao la michikichiki kwa sababu kila mwaka Serikali hutumia zaidi ya sh. bilioni 600 kwa ajili ya kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.

  Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Julai 28, 2018) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Kigoma, wadau wa zao la michikichi na wabunge wa mkoa wa Kigoma baada ya kuwasili mkoani hapa kwa ziara ya kikazi ya siku nne inayolenga kuhamasisha maendeleo na kilimo cha zao la Michikichi.Amesema Serikali haiwezi ikaendelea kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza mafuta ya kula kutoka nje wakati uwezo wa kulima michikichi na kuzalisha mafuta ya mawese kwa wingi tunao, hivyo amewataka viongozi wa Serikali wabadilike na wawafuate wakulima kwenye maeneo ya vijijini na wakawasimamie na kuwashauri namna bora ya kulima zao hilo.

  Aidha, ameagiza Wizara ya Kilimo ianze taratibu za kisheria za kukihamisha chuo cha Kihinga kutoka Wizara ya Elimu Sayansi ya Teknolojia kwenda wizara ya Kilimo ili shughuli za tafiti za zao la michikichi lifanyike kwa ufanisi. Pia, ameiagiza Wizara ya Kilimo kuwahamishia mkoani Kigoma watumishi wa kituo cha utafiti wa michikichi cha Bagamoyo ifikapo mwezi Agosti, 2018 isipokuwa wale wanaohusika na utafiti wa zao la minazi tu.

  Kadhalika, amewataka viongozi wa mikoa yote inayolima michikichi waanzishe mashamba ya michikichiki ili waoneshe mfano kwa wananchi. “Serikali inataka kuona mabadiliko kwenye zao hili. Sioni umuhimu wa Taifa kuendelea kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi wakati uwezo wa kuzalisha ndani upo,”.

  Amesema Serikali inataka kuona mabadiliko ya zao hilo, hivyo amewaagiza maafisa ugani katika maeneo yote wanayolima zao hilo wakafualitie maendeleo ya zao hilo kwa ukaribu zaidi. Zao hili litasimamiwa kuanzia hatua za uandalizi wa mashamba, upatikanaji wa pembejeo na utafutaji wa masoko.

  Waziri Mkuu amewataka wananchi wote wa mkoa wa Kigoma pamoja na mikoa mingine inayolima michikichi, wahakikishe wanapanda michikichi kwa wingi kuanzia kwenye makazi yao na kwenye mashamba yote wanayolima mazao mengine ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

  “Serikali imefanya maamuzi ya kumaliza tatizo la mafuta ya kula nchini, kila mmoja lazima awajibike katika kuinua zao la michikichi ili tuweze kuzalisha mafuta ya kutosha,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema Serikali itafuatilia kwa umakini kuhakikisha zao la michikichi linalimwa kwa wingi na kuleta tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla. “Tutumie zao hili kama fursa ya kujikwamua na umasikini pamoja na maliza changamoto ya upatikanaji wa mafuta nchini,”.

  AwaliNaibu Waziri wa Kilimo, Bw. Omary Mgumba alisema zao la mchikichiki ni muhimu katika ukuzaji wa uchumi wa nchini, hivyo ufufuaji wa zao hilo ni kichocheo cha viwanda kwa kuwa kutakuwa na uhakika wa upatikanaji wa malighafi, hivyo kuvutia wawekezaji.  Amesema kiasi kikubwa cha zao hilo hutumika katika kuzalisha mafuta ya kula, sabuni, hivyo ameshauri kiwepo chuo cha utafiti wa zao la michikichi mkoani Kigoma ili kurahisisha shughuli za uzalishaji. Mafuta yatokanayo na zao la michikichi yana mahitaji makubwa kwa kuwa bei yake ni nafuu jambo linalowezesha watu wengi wakiwemo wa hali ya chini kuyatumia.  Kwa upande,wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga aliishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kufufua zao la michikichi kwa kuwa linalenga kuinua uchumi wa Taifa.  Kikao hicho kimehudhuriwa na Mke wa Waziri Mkuu Mary Majaliwa, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhadisi Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na Miundombinu, Mhandisi Atashasta Nditie, Naiubu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Naibu Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Jpsephat Kandege, Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba.

  0 0

  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inaendelea kupata mafanikio makubwa kutokana na kuboresha huduma za upasuaji wa watoto, huku ndani ya siku mbili watoto 24 wakiwa wamefanyiwa upasuaji.

  Wataalamu wa upasuaji wa watoto wa Muhimbili wamesema idadi ya watoto wanaofikishwa katika hospitali hiyo kutokana na matatizo mbalimbali, inaeendelea kuongezeka kutoka maeneo mbalimbali nchini.

  Watoto waliofanyiwa upasuaji ni wale wenye matatizo mbalimbali wakiwamo waliozaliwa bila kuwa na njia ya haja kubwa na wengine wenye matatizo kwenye mfumo wa chakula na hewa.Upasuaji wa watoto hao 24 umefanywa na wataalamu wa upasuaji wa watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa upasuaji wa watoto kutoka Chuo Kikuu cha Alexandria nchini Misri.

  Akizungumza leo katika mkutano na waandishi wa habari, Daktari Bingwa wa Watoto katika hospitali hiyo, Dkt. Mwajabu Rashid Mbaga amesema wataalamu wa muhimbili na wa Chuo Kikuu cha Alexandria nchini Misri wameshirikiana kufanya upasuaji mgumu (difficult cases) kwa watoto hao.

  Dkt. Mbaga amesema upasuaji huo umekuwa ukifanywa mara kwa mara na wataalamu wa Muhimbili kwa muda mrefu na kwamba katika siku mbili wamekuwa na wataalamu wa Chuo Kikuu cha Alexandria kwa ajili ya kubadilisha uzoefu.“Kuanzia Alhamisi hadi Ijumaa wiki hii tumekuwa na jopo la watalaamu wenzetu 10 wa upasuaji kutoka Chuo Kikuu cha Alexandra kilichopo Misri wakiongozwa na Prof. Saber Mohamed Waheeb mshauri mwelekezi katika upasuaji wa watoto na Dkt. Mohamed Abdelmalak Morsi bingwa wa upasuaji wa watoto,” amesema Dkt. Mbaga.

  Kufanyika kwa upasuaji huo kumetokana na juhudi za uongozi wa Muhimbili kuimarisha miundombinu ya vyumba maalumu(exclusive operating theaters) vya upasuaji wa watoto.Wakati huo huo, hospitali hiyo ilipokea watoto pacha walioungana ambao walizaliwa Julai 12, 2018 kwa njia ya kawaida wakati mama akiwa njiani kuelekea hospitalini huko Vigwaza Mkoani Pwani.

  Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto wa Muhimbili, Dkt. Petronilla Joseph Ngiloi amesema pacha hao wameungana sehemu ya tumbo na sehemu ya ndani na kwamba wanachangia INI tu huku viungo vingine kila mmoja akijitegemea. 

  “Watoto hawa walizaliwa na kilo mbili, lakini sasa wamefikisha kilo 4 na gramu 640. Tunategemea kuwafanyia upasuaji wa kuwatenganisha katika kipindi cha miezi mitatu hadi minne ijayo kuanzia sasa. Tumejiridhisha kwamba tutaweza kuwatenganisha sisi wenyewe hapahapa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,” amesema Dkt. Ngiloi.

  Naye Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Muhimbili, Dkt. Julieth Magandi alishukuru jopo la wataalamu kutoka Misri kwa kushirikiana na wataalam wa hospitali hiyo kwa kuwa wamebadilishana uzoefu.
  Madaktari na wataalamu wengine wakiendelea na upasuaji kwa mtoto mwenye tatizo kwenye mfumo wa chakula (Gastroeso Phageal Reflux disease).
  Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Mwajabu Rashid Mbaga akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya wataalamu wa upasuaji wa watoto wa Muhimbili na wale wa Chuo Kikuu cha Alexandria nchini Misri kufanya upasuaji kwa watoto 24 wenye matatizo mbalimbali. Watoto hao wanaendelea vizuri baada ya kupatiwa huduma hiyo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa MNH, Dkt. Julieth Magandi, Dkt. Petronilla Joseph Ngiloi wa MNH, Prof. Saber Mohamed Waheeb kutoka Misri, Dkt. Mohamed Abdelmalak kutoka Misri na Dkt. Ibrahimu Mkoma wa MNH.
  Madaktari bingwa wa upasuaji wa watoto kutoka Chuo Kikuu cha Alexandria nchini Misri wakifanya upasuaji kwa mmoja wa watoto ambaye ana tatizo kwenye mfumo wa chakula (Gastroeso Phageal Reflux) disease) kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kulia ni Prof. Saber Mohamed Waheeb kutoka Misri, Dkt. Mwajabu Rashid Mbaga wa Muhimbili na Dkt. Mohamed Abdelmalak kutoka Misri wakifanya upasuaji.
  Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Mwajabu Rashid Mbaga (kushoto), Daktari Bingwa wa Nusu Kaputi, Dkt. Kareman Ibrahim kutoka Chuo Kikuu cha Alexandria nchini Misri na Muuguzi msaidizi, Agness Charles wa Muhimbili (kulia) wakiendelea na upasuaji katika hospitali hiyo.
  Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Mwajabu Rashid Mbaga (kushoto), Prof. Saber Mohamed Waheeb kutoka Misri (kushoto), Dkt. Mohamed Abdelmalak kutoka Misri (kulia) na Muuguzi msaidizi, Agness Charles wa Muhimbili (kulia) wakiendelea na upasuaji leo.
  Dkt. Julieth Magandi wa Muhimbili akipokea zawadi kutoka kwa Prof. Saber Mohamed Waheeb wakati wa mkutano wa wataalamu hao na waandishi wa habari leo.

  0 0

  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike akikagua shamba la miwa la gereza Mbigiri, Morogoro lililopo chini ya mradi wa ubia kati ya Magereza na mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PPF na NSSF. Mradi huo ukikamilika unatarajiwa kuzalisha zaidi ya tani elfu 30 za sukari kwa mwaka.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike (wa kwanza kushoto) akikagua baadhi ya matrekta na mitambo inayotumika katika kuandaa mashamba ya miwa ya gereza Mbigiri kwenye mradi wa ubia kati ya Magereza na mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PPF na NSSF wa kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari. Jenerali Kasike ametembelea mradi huo leo Julai 27, 2018.
  Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akitoa hotuba wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa zahanati ya gereza la Mahabusu Morogoro iliyofanyika leo tarehe 27 Julai, 2018.Kamishna Kasike alitumia hafla hiyo kuwakubusha na kuwasihi wageni waalikwa kuitikia wito wa serikali wa kupima afya zao mara kwa mara ikiwa ni njia mojawapo ya kupambana na ukimwi.
  Mkuu wa Gereza la Mahabusu Morogoro Marakibu wa Magereza Zephania Neligwa akisoma risala kwa mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike katika hafla fupi ya uzinduzi wa zahanati ya gereza la Mahabusu Morogoro iliyofanyika leo tarehe 27 Julai, 2018. Mrakibu Neligwa amesema ujenzi wa zahanati hiyo pamoja na ununuzi wa vifaa vya tiba na dawa hadi inazinduliwa imegharimu zaidi ya shilingi 24.8 milioni.
  Baadhi ya maafisa na askari wa Kingolwira Complex inayojumuisha Chuo cha Ufundi KPF, Gereza Mtego wa Simba, Gereza Mkono wa Mara na Gereza Kuu la Wanawake wakifuatilia kwa makini maelekezo ya kiutendaji kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike (hayupo pichani) alipowatembelea kwa mara ya kwanza leo tarehe 27 Julai, 2018 mara baada ya kufanya uzinduzi wa Zahanati ya gereza la Mahabusu, Morogoro.  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike amehitimisha ziara yake fupi mkoani Morogoro kwa kuongea na baadhi ya maafisa, askari na watumishi raia wa Ofisi ya Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Morogoro na Gereza Kihonda.

  Jenerali Kasike ametumia ziara hiyo ya kwanza tangu ateuliwe kuwa mkuu wa Jeshi hilo Julai 13 mwaka huu kuwataka watendaji wote ndani ya Jeshi la Magereza kutambua alama za nyakati na kubadilika kabisa kimtazamo, kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kujisikia aibu kwa kuona Jeshi lao linatajwa kwa ubaya wa kushindwa kutimiza majukumu yake sawasawa.

  Amewataka maafisa na askari wote kujiandaa kupokea mpango kazi wa kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa ambao hivi sasa unaandaliwa katika ngazi ya makao makuu ya Jeshi hilo.

  Jenerali Kasike amewatolea wito viongozi wote ndani ya Jeshi la Magereza kuwa tayari kupokea maoni ya walio chini yao bila kujali vyeo vyao ili kuweza kufikia malengo tarajiwa.

  Aidha amesisitiza kuwa ni lazima watendaji wote kufuata maadaili kwakuwa suala la maadili ya kazi halihitaji raslimali ni mtu kubadilika tu.

older | 1 | .... | 1632 | 1633 | (Page 1634) | 1635 | 1636 | .... | 1897 | newer