Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1631 | 1632 | (Page 1633) | 1634 | 1635 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Na Zainab Nyamka,Globu ya jamii

  KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes wametangaza kuonesha mechi za maandalizi ya Msimu mpya kwa ligi kubwa za barani Ulaya ambapo zitawashirika timu 18 bora kutoka ligi kubwa tano duniani.

  Mechi hizo ambazo huchezwa chini ya mashindano yanayofahamika kama Kombe la Mabingwa wa Kimataifa( ICC) yatari zimeanza kutimua vumbi wikiendi iliyopita.Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Meneja Masoko wa Startimes David Malisa amesema kuwa kama ulikuwa unajiuliza nini kinafuata baada ya Kombe la Dunia basi majibu ni hayo.

  "Katika kuonyesha kwamba sisi ni wafalme wa Burudani, kutakuwa na mechi kali za ICC, maarufu kama Pre-Season yaani mechi za kujiandaa na msimu mpya."Ambapo utawaona wachezaji wakubwa kama Ronaldo akiwa na klabu yake mpya ya Juventus, Mahrez akiwa na Man City, Mo Salah, Mane, Messi na wennane wengi,"amefafanua .

  Amesema kuwa mechi hizo za ICC ama Pre-Season zinapatikana kwenye king’amuzi cha StarTimes pekee hakuna king’amuzi kingine kinachoonesha.
   " Mechi zote zitaonekana kwenye chaneli ya World Football na Sports Premium ambazo zipo katika kifurushi cha MAMBO kwa watumaji wa Antenna Tsh 13,000 tu kwa mwezi na kifurushi cha SMART kwa wateja wa Dish kwa Tsh 19,000 kwa mwezi,"amesema.

  Zamaradi Nzowa, Meneja wa kitengo cha Maudhui, StarTimes.“Katika kujali mahitaji ya wateja wetu pendwa kabisa, tumeongeza chaneli 5 mpya zaidi ambazo zitaanza kuonekana katika king’amuzi chetu kuanzia tarehe moja mwezi wa nane, chaneli hizo ni EBONY LIFE ya Nigeria, EWTN, Discovery Family ambayo ina vipindi vingi vya kifamilia, na DW kwa ajili ya Habari, pia tumeirudisha chaneli ya TV Imaan. Mbali na chaneli mpya tumeihamisha chaneli ya Fox Sports kutoka kifurushi cha UHURU kwenda kifurushi cha MAMBO

  Miongoni mwa timu hizo ni Bayern Munich, Borussia Dortmund (Bundesliga), Manchester City, Manchester United, Liverpool, Arsenal (Premier League), PSG (League 1), Barcelona, Real Madrid (La Liga), AC Milan, Inter Milan na Juventus (Serie A). Katika mechi zilizopigwa wikiendi iliyopita Borussia Dortmund wameonyesha kiwango kizuri baada ya kuwafunga Manchester City 1-0 na kuwachapa Liverpool 3-1.

  Wapenzi wa Soka nchini watapata nafasi ya kuishuhudia michuano hii kupitia chaneli ya World Football na Sports Premium katika king’amuzi cha StarTimes ambao wana haki za kipekee za kuonyesha michuano hiyo.
  Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuonyesha michuano ya ICC inayoendelea katika mabara matati tofauti ikizihusisha timu 18 bora kutoka ligi tano bora duniani. Kulia ni Meneja Maudhui wa Startimes Zamaradi Nzowa.
  Meneja Masoko wa kampuni ya Startimes David Malisa akiwa pamoja na Meneja maudhui Zamaradi Nzowa

  0 0


  0 0

  *Ni anayetuhumiwa kumiliki mali isiyolingana na kipato chake

  Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea barua ya kufutwa kazi kwa aliyekuwa Mhasibu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), Godfrey Gugai kama kielelelezo namba sita katika kesi ya utakatishaji na kumiliki mali isiyolingana na kipato chake inayomka bili Gugai na wenzake watatu

  Uamuzi huo umetolewa leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kutokana na pingamizi la upande wa utetezi waliokuwa wanapinga shahidi wa kwanza wa upande wa Jamuhuri kutoa kielelezo hicho wakidai kuwa siyo mtu husika.

  Katika pingamizi lao Wakili wa utetezi Alex Mgongolwa alidai mahakamani hapo kuwa, shahidi Huyo hapaswi kutoa kielelezo hicho kwa kuwa siyo mtu aliyeandika barua hiyo na wala haielewi vile vile hakikuwa mikononi mwake.

  Akitoa uamuzi wa kupokea kielelezo hicho, Hakimu Simba amesema, kifungu cha 34(b)(1) walichotumia upande wa utetezi kuwasilisha pingamizi hilo hakiusiani kabisa na mazingira ya kesi hiyo,"Shahidi Huyo Ayoub Akida katika ushahidi wake alidai yeye ni afisa Utumishi Mkuu wa Takukuru, ambaye ndie anahusika katika kutunza mafaili ya wafanyakazi ikiwemo barua hiyo ya kufutwa kazi.

  Amesema sababu zilizowasilishwa katika pingamizi la upande wa uetezi za kutaka barua hiyo isipokelewe mahakamani kama kielelezo hazina msingi hivyo zimekataliwa na barua imepokelewa kama kielelezo Namba 6. Amesema shahidi ndiyo mtu sahihi anayepaswa kuwasilisha kielelezo hiki mahakamani kwani yeye ndie anayetunza mafaili yote ya wafanyakazi wa Takukuru na kwamba alihusika katika suala la kujadiliwa nidhamu ya mshtakiwa Gugai.

  Mbali na Gugai, washtakiwa wengine, ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.Washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali.Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo alitenda kosa hilo kati ya January 2005 na Decemba 2015.

  Inadaiwa akiwa jijini Dar es Salaam kama mwajiriwa wa TAKUKURU alikuwa akimiliki mali za zaidi ya Sh 3.6 bilioni ambazo hazilingani na kipato chake cha awali na cha sasa cha zaidi ya Tsh.milioni 800,huku akishindwa kuzitolea maelezo.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga akipozi kwa picha na Mzewe Malkiadi Bura kutoka kata ya Masqaroda ambaye ni mlemavu wa miguu baada ya kumkabidhi baiskeli maalum kwa ajili ya kutumia katika shughuli zake wananchi walemavun wengine waliokabidhi wa baiskeli hizo ni kutoka kata za Tumati, Maghang, na Dinamu Wilayani Mbulu Mkoani Manyara.


  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga ametoa msaada wa baiskeli sita kwa ajili ya walemavu ili kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku. Kamoga amewashukuru marafiki zake waliochangia katika kuboresha maisha na kuwasaidia wananchi wanyonge.

  Kamoga amesema “Serikali hii inawajali wanyonge na sisi kama viongozi lazima pia tufikiri zaidi ya ukomo wa kazi zetu za kila siku katika kuwahudumia wananchi wa hali ya chini. Nafasi hii niliyopewa na Mungu kupitia kwa Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli ni kwa ajili ya kuwatumikia na kuwasaidia watanzania hasa wanyonge,nafasi hii ni kwa ajili ya watu ninaotakiwa kuwatumikia na si kwa ajili yangu binafsi,ndio maana ya utumishi”alisema Kamoga.

  Baiskeli hizo zimetolewa na marafiki wa mkurugenzi huyo wanaotambua mchango wake katika kulitumikia taifa na kuwajali watu wanaoishi kwenye mazingira magumu, Wadau hao wameahidi kutoa vifaa vingine kila watakapokuwa na uwezo wa kifedha ili kusaidia jamii inayoishi kwenye mazingira magumu Wilayani Mbulu.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga akipiga picha ya pamoja na dada Rose Boay kutoka Haydom baada ya kumkabidhi baiskeli yake leo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga akipiga picha ya pamoja na mama Maria Chacha kutoka kata ya Haydom baada ya kumkabidhi baiskeli yake leo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga akiwa na wananchi wa Mbulu wenye ulemavu wa miguu aliowakabidhi baiskeli maalum kwa ajili ya matumizi katika shughuli zao za kila siku
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga akijadiliana jambo na baadhi ya viongozi huku mama Maria Chacha kutoka kata ya Haydom kushoto na dada Rose Boay kutoka Haydom wakiwasikiliza.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na walemavu aliowapatia baiskeli.

  0 0

  * Madaktari Bingwa nchini waungana na wezao kutoka India kuwahudumia wananchi,waombwa kujitokeza kwa wingi

  Na Said Mwishehe, Glob ya Jamii

  HEAMEDA Medical Clinic iliyopo Bunju B njia ya kuelekea Mabwepande imetangaza kambi ya uchunguzi wa afya ya magonjwa yasiyoambukiza kwa wananchi wote na kwamba hakutakuwa na gharama.

  Akizungumza na Michuzi blog leo jijini Dar es Salaam Dk. Hery Mwandolela amesema wameaza kambi hiyo ya uchunguzi leo jijini Dar es Salaam kwa kupima wananchi mbalimbali waliojitokeza na kusisitiza upimaji huo ambao umeanza leo Julai 26 utaendelea hadi Julai 28 mwaka huu.

  Amesema upimaji huo unafanywa na Madaktari bingwa wa hapa nchini kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka nchini India na lengo kuu ni kuwawezesha wananchi kutambua afya zao mapema na iwapo watabainika kuwa na tatizo la kiafya waaze tiba mapema.

  Amefafanua huduma zinazotolewa katika kambi hiyo ya uchunguzi ni pamoja na kupima magonjwa yasiyoambukizwa yakiwemo ya Moyo ,sukari,shinikizo la damu,Tenzi Dume, lehemu(cholestrol) nakiwango cha mafuta mwilini."Madaktari bingwa wa Heameda Medical Clinic kwa kushirikiana na madaktari bingwa wengine nchini pamoja na madaktari bingwa kutoka India tutatoa huduma hizo kwa kiwango cha hali ya juu.

  Nakuongeza kuwa " hivyo tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi nakwamba huduma hii inafanyika kwa siku tatu ambapo tumeaza leo na tunaendelea kesho na keshokutwa na hakuna gharama yeyote ."amesema Dkt Mwandolela.Amesisitiza kwakutambua umuhimu wa afya yako wameamua kufanya kampeni hiyo ya kupima magonjwa hayo wakiamini ni fursa ya kila mwananchi kujitambua kiafya mapema..

  Katika kampeni hiyo kwa siku ya leo ambayo ni ya kwaza idadi kubwa ya wananchi wamejitokeza lakini Dkt.Mwandolela anafafanua kwa idadi ya madaktari bingwa waliopo nivema wananchi wakaendelea kujitokeza kwani wote watahudumiwa kwakupata vipimo vya afya zao.
  Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo nchini Dk.Hery Mwandolewa akiwa ofisini kwake Heameda Medical Clinc Bunju B jijini Dar es Salaam.
  Muonekano wa sehemu ya mapokezi ndani ya Clinic hiyo
  Muonekano wa moja ya chumba chenye vifaa mbalimbali kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa/matibabu
  Muoneakano wa Clinic hiyo kwa nje

  0 0  0 0

  Na Mwandishi wetu
  NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Elimu ya Ufundi, Avemaria Semakafu ametaka kuvunjwa kwa vikwazo vya lugha vinavyosababisha mkanganyiko wa utoaji elimu barani Afrika kwa kutumia Kiswahili.

  Alisema mataifa ya Afrika yamekuwa yakibabaika katika matumizi ya lugha za kikoloni ambazo zimesababisha pia kuwa na ulingafu dhaifu wa utoaji elimu kwa bara hili.

  Alisema hayo kwenye kongamano la Mataifa zaidi ya 16 yaliyo Kusini mwa Jangwa la Sahara ambayo yamekuwa yakikutana kuanzia Jumatano kujadiliana namna bora ya kutengeneza mitaala na vifaa vya kufundishia ili kuboresha mbinu za kufundisha na kujifunza.

  Alisema ipo haja ya kuondokana na mifumo ya mapokeo ambayo imejaa taratibu za kikoloni zinazompima mtu kwa mitihani na akifeli kuonekana hana uwezo, wakati waliofeli ndio wanafanya vyema katika maisha ya kawaida ya kila siku.

  Akizungumza na wawakilishi hao ambao wanashiriki katika kongamano la siku tatu katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Kinondoni Dar Es Salaam, Naibu Katibu Mkuu huyo alisema ipo haja ya kuangalia mfumo mzima na kupata vigezo halali vya kutathmini mafanikio ya elimu kwa kuangalia elimu yenyewe mitaala na namna ya uwekaji wa ulinganifu wa matokeo.

  Alitaka mataifa ya Afrika kutumia lugha moja ya Kiswahili katika ufundishaji ili kuondokana na kikwazo cha lugha ambacho alisema ni moja ya kifaa cha utamaduni wa utoaji elimu.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Elimu ya Ufundi, Dk . Avemaria Semakafu akifungua kongamano la kikanda kuhusu ulinganifu wa mafunzo, mitaala, mafunzo kwa walimu na vifaa vya kufundishia mataifa zaidi ya 16 yaliyo Kusini mwa Jangwa la Sahara ili kubadilishana uzoefu wa namna ya kushirikiana na kufanyakazi kimtandao ili kuboresha mazingira ya kujifunza kwa mamilioni ya wanafunzi kwenye nchi hizo liliofanyika jijini Dar es Salaam. Kongamano hili limeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni-UNESCO na linaendeshwa na mtandao wa TALENT.
  Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki na Afisa Mwakilishi wa Unesco nchini, Ann Therese Ndong- Jatta akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo wakati wa kongamano la kikanda kuhusu ulinganifu wa mafunzo, mitaala, mafunzo kwa walimu na vifaa vya kufundishia lililokutanisha nchi 16 ili kutekeleza moja ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs, lengo la nne lililofanyika Jijini Dar es Salaam. Kongamano hili limeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na linaendeshwa na mtandao wa TALENT.
  Mratibu wa mtandao wa watoa elimu na mafunzo kwa mabadiliko (TALENT) kutoka UNESCO Dakar, Valérie Djioze-Gallet akizungumzia madhumuni kuratibu kongamano hilo la kikanda linalojadili kuhusu ulinganifu wa mafunzo, mitaala, mafunzo kwa walimu na vifaa vya kufundishia ili kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya elimu hasa kwenye nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SSA) ili kufikia lengo la nne la maendeleo endelevu (SDGs) katika elimu. Kongamano hili limeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na linaendeshwa na mtandao wa TALENT.
  Baadhi ya wadau kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia mada kwenye kongamano la kikanda linalohusu ulinganifu wa mafunzo, mitaala, mafunzo kwa walimu na vifaa vya kufundishia ili kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya elimu hasa kwenye nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SSA).
  Baadhi ya wanakamati ya maandalizi ya kongamano hilo kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
  Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Elimu ya Ufundi, Dk . Avemaria Semakafu katika picha ya pamoja ya washiriki wa kongamano la kikanda kuhusu ulinganifu wa mafunzo, mitaala, mafunzo kwa walimu na vifaa vya kufundishia mataifa zaidi ya 16 yaliyo Kusini mwa Jangwa la Sahara ili kubadilishana uzoefu wa namna ya kushirikiana na kufanyakazi kimtandao ili kuboresha mazingira ya kujifunza kwa mamilioni ya wanafunzi kwenye nchi hizo liliofanyika jijini Dar es Salaam. Kongamano hili limeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni-UNESCO na linaendeshwa na mtandao wa TALENT.


  0 0

  Watendaji na Watumishi wa Serikali katika jiji la Arusha wametakiwa kushirikiana,kupendana na kufanya kazi kwa bidii ili kulinda mafanikio ya kimaendeleo yaliyofikiwa na jiji hilo. 


  Kauli hiyo imetolewa leo jijini Arusha na aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athumani Kihamia wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Ofisi jijini hapo. 

  Akizungumza na Watumishi na Watendaji wa jiji hilo Dkt. Kihamia amewataka wafanye kazi kwa bidii na kuepuka vitendo vinavyoweza kuleta mgawanyiko miongoni mwao. Amesema katika kipindi cha uongozi wake akiwa Mkurugenzi wa jiji hilo aliwaunganisha watumishi wote akiweka msisitizo katika bidii, nidhamu ya kazi na matumizi mazuri ya rasilimali na fedha Serikali hali iliyolifanya jiji hilo kupata Hati Safi ya Matumizi ya fedha za Serikali. 

  “Watumishi Wenzangu mimi nimekaa katika jiji hili kwa muda wa miaka 2, nafurahi kuwa nawaacha mkiwa na morali ya kufanya kazi na muendelee kufanya kazi kwa bidii, mzidi kupendana ili kazi mnazozifanya zifanikiwe kwa manufaa ya jiji ” Amesisitiza Dkt. Kihamia. Ameongeza kuwa ili jiji hilo liendelee kupiga hatua zaidi za Kimaendeleo, watendaji na wakuu wa Idara wana wajibu wa kufanya kazi kwa pamoja, kuaminiana na kuepuka kufanya vitendo vya dhuruma na uonevu wa aina yoyote kwa watumishi wa kada mbalimbali walio chini yao. 

  Amesema maendeleo yaliyofikiwa katika jiji hilo yasingekuwepo kama watumishi waliopo wasingekuwa waaminifu na wanaoshauri vizuri na kuwataka wakuu wa Idara, watendaji na watumishi wanaotoa maamuzi kuepuka vitendo vinavyoweza kushusha chini morali ya kazi ya watumishi. “Watendaji mlio na mamlaka msifanye mabadiliko yoyote kwa kumwonea mtu, mafanikio haya tusingeweza kuyapata kama kusingekuwa na watumishi wanaofanya kazi zao kwa bidii na uaminifu wapo watumishi walio na utendaji mzuri na wanaoshauri vizuri hawa tuendelee kuwalinda na kuwaheshimu” Amesisitiza Dkt.Kihamia. 

  Katika hatua nyingi Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia amesema kuwa maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu yanaendelea na vizuri katika maeneo mbalimbali yenye uchaguzi huo. 

  Amesema kuwa mpaka sasa hakuna changamoto zozote kubwa za kiutendaji zinazoweza kukwamisha uchaguzi huo. “ Mchakato wa uchaguzi unaenda vizuri, mpaka sasa hakuna kasoro zozote na zoezi la Kampeni linakwenda vizuri hakuna vurugu wala vitendo vya uvunjifu wa amani vilivyoripotiwa mpaka sasa kutokana na kampeni hizo” Amesema Dkt. Kihamia. 

  Kwa upande wake Mstahiki Meya wa jiji hilo Mhe. Karisti Lazaro akizungumza na Watendaji na watumishi wa jiji hilo waliohudhuria kwenye hafla hiyo amempongeza Dkt. Athumani Kihamia kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) 

  Ameeleza kuwa uteuzi wake umezingatia viwango vyake vya utendaji kazi uliotukuka katika jiji hilo la Arusha uliolenga kuleta maendeleo kwa wananchi. “ Nichukukue fursa hii kumpongeza sana kwa namna ambavyo Mhe. Rais amemuona katikati ya majiji yote kwa kuona anafaa kumsaidia katika majukumu makubwa ya kitaifa” 

  Amewaeleza watumishi hao kwamba wana kila sababu ya kujifunza kutoka kwa Dkt. Kihamia kwa kuwa yeye alitimiza wajibu wake kwa uaminifu mkubwa na kuongeza kuwa kuwa kutokana na utendaji wake jiji la Arusha liko katika hali nzuri ya mapato kwa kuwa na asilimia zaidi ya 103, uanzishaji wa miradi mikubwa ya Afya, Elimu, Maji na Usafirishaji ambayo yote inalenda kuinua uchumi wa jiji la Arusha. 

  “Hili ni fundisho kwetu, Mkurugenzi unayeondoka umetuachia jiji letu likiwa salama, tuko kwenye mazingira mazuri sana, leo unaiacha Halmashauri ikiwa na mapato kwa zaidi ya asilimia 103 ikiwa na Hati safi na hoja chache sana maana ulipoingia ulikuta hoja 400 za CAG leo unaondoka ikiwa na hoja 23 ambazo zote zinajibika, hii yote inatokana na udhibiti wake” Amesisitiza Mhe. Lazaro. 

  Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa jiji hilo Afisa Mtendaji wa Kata ya Ngarenaro Bw. Braison Nassari ameeleza kuwa wao kama watumishi wa jiji hilo wanamwelezea Dkt. Athumani Kihamia kama Mkurugenzi aliyekuwa akiwatunza watumishi wa Serikali katika jiji hilo. 

  Amesema kwa kipindi chote alichokuwa Mkurugenzi Dkt. Kihamia hakukubali kuyumbishwa na mtu yeyote wakiwemo wanasiasa waliopingana naye katika hatua zake alizozichukua katika kusimamia taratibu za Serikali na utumishi wa umma. 

  “ Napenda kuweka wazi kwamba sisi kama watumishi wa jiji la Arusha tunakupongeza sana, kwa kipindi chote ulichokuwepo hapa tuliona kwamba hata watu walipokuwa wakileta maneno ya hila wewe ulichukua hatua ya kuchunguza mambo hayo, na hata baadhi ya watu waliotaka kukutengenezea mambo mengi ya kukuchafua hawakuweza kufanikiwa ulisimamia katika kulinda haki, ukweli na taratibu za utumishi “ Amesisitiza. 

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo akimkabidhi vifaa vya michezo Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Gongoni Mwl. Mohamed Kikwayu.
  Baadhi ya walimu wakuu wa sekondari wilayani Kisarawe pamoja na wanafunzi wa Minaki wakiwa katika zoezi la kupokea vifaa vya michezo kutoka kampuni ya Coca-Cola.
  Walimu wa shule ya Msingi Kazimzumbwi wakiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo .
  Wanafunzi wa Kazimzumbwi wakiwa katika picha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo 


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo amewataka wanafunzi kujenga upendo na kuacha ubinafsi katika kuipambania elimu.

  Jafo ameyasema hayo leo katika ziara yake alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Minaki pamoja na walimu wakuu wote wa shule za sekondari zilizopo wilayani Kisarawe Mkoani Pwani. 

  Amesema ni vyema wanapoipambania elimu wakawa na upendo na kuachana na ubinafsi. Katika ziara hiyo, waziri Jafo amefanikiwa kupokea vifaa vya michezo kutoka kampuni ya vinywaji ya Coca-Cola na kuwapatia wakuu wote 22 wa shule za sekondari zilizopo wilayani Kisarawe. 

  Pamoja na shughuli ya ugawaji wa vifaa vya michezo, Jafo ameungana na wananchi wa Kazimzumbwi katika zoezi la Kuboresha madarasa ya shule msingi ya kijiji hicho kwa kuchangia mifuko yote ya saruji ambayo itawezesha uwekaji wa sakafu katika madarasa yote na ofisi ya walimu ambayo hayajawekwa sakafu.

  Zoezi hilo la uwekaji wa sakafu linatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi ili wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Kazimzumbwi wapate mazingira mazuri ya kusomea na kufundishia.

  0 0


  Katika kuendelea kusogeza huduma zake kwa wananchi zaidi na kutoa masuluhisho ya kifedha, Benki ya Azania leo imezindua huduma mbili mpya maalumu kwa ajili ya wastaafu kutoka katika mashirika mbalimbali ya kiserikali na hata ya binafsi. Huduma hizi ni Akaunti maalumu ya wastaafu (Wastaafu Akaunti) ambayo pamoja na faida nyingine za kibenki akaunti hii haitakuwa na makato yoyote na watapata ATM kadi bure huduma nyingine ambayo  Azania Bank imeiletea  kwa wastaafu ni fursa ya kupata mikopo kuweza kujikimu na kuboresha maisha yao. 
  Akizungumza na vyombo vya habari katika uzinduzi wa huduma hizi Mkurugenzi wa Bank ya Azania Bw. Charles Itembe alisema Azania Bank inaendea kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha inaendelea kukuza maisha ya watanzania wote kupitia huduma mbalimbali za kifedha inazozitoa. Leo Azania Bank inazindua rasmi Mikopo ya Wastaafu na pia uzinduzi wa kampeni yetu tuliyoibatiza jina la Bega kwa Bega.Mikopo hii ya wastaafu inalenga wastaafu wote wanaopata pensheni kupitia mifuko ya jamii ambapo kupitia mikopo ya wataafu mteja ataweza kufanya marejesho kwa miezi 72 yaani miaka 6.  Alielezea Zaidi Bw. Charles Itembe
  Mzee Haron L Kigondo ni mmoja wa wanufaika wa huduma hii mpya ya mikopo kwa wastaafu ambapo pamoja na kushuhudia yeye kuupata mkopo wake ndani ya wiki chache tu, alisema “Mikopo hii kweli inakwenda kutupa nafasi sisi Wastaafu kuweza kuendesha maisha yetu na hata kuendesha biashara wakati tukiwa bado tunaendelea kusubiri mafao yetu, Ninaishukuru sana Azania Bank kwa wazo hili kwani litakwenda kusaidia wastaafu wengi sana kuweza kuboresha maisha pamoja na biashara zao”

  Azania Bank kwa sasa ina matawi 17 ambapo ndani ya wiki 3 zijazo inategemea kuwa na matawi 19 baada ya kufungua matawi mapya Dodoma na Morogoro, pamoja na matawi haya Azania Bank inatoa huduma kupitia ATM zaidi ya 270 za Umoja Switch na hii kutoa fursa kwa mtu yoyote popote Tanzania kuweza kupata huduma za kibenki.
  0 0

  Mkurugenzi wa Kilimo na Mifugo katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Luteni Kanali Peter Lushika akitoa maelezo kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka, kuhusu Mabanda ya miifugo yaliyojengwa na jeshi hilo kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika Kitaifa, 2018 Uwanja wa Nyakabindi katika Halmashauri ya mji Bariadi .
  Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu kabla ya viongozi hao kutembelea eneo la jeshi hilo lililoandaliwa kwa ajili ya maonesho ya Nanenane lililopo katika Uwanja wa Nanenane uliopo Nyakabindi Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa na viongozi wa Mkoa huo kabla ya kutembelea eneo la jeshi hilo lililoandaliwa kwa ajili ya maonesho ya Nanenane lililopo katika Uwanja wa Nanenane uliopo Nyakabindi Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
  Mkurugenzi wa Kilimo na Mifugo katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Luteni Kanali Peter Lushika akitoa maelezo juu ya vipando vilivyoandaliwa na jeshi hilo kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka walipotembelea eneo hilo lililopo Uwanja wa Nyakabindi katika Halmashauri ya mji Bariadi.
  Viongozi wa JKT na mkoa wa Simiyu wakiangalia moja ya mabwawa ya samaki yaliyoandaliwa na Jeshi la kujenga Taifa(JKT) kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Nanenane wa kanda ya ziwa mashariki, uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
  Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu akisaini vitabu vya wageni vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, kabla ya kuanza kutembelea eneo la jeshi hilo lililoandaliwa kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika kitaifa mkoani humo Agosti 2018, lililopo katika Uwanja wa Nanenane uliopo Nyakabindi Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akisisitiza jambo katika kikao kati ya viongozi wa Mkoa huo na viongozi wa JKT wakati wa ziara ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu katika eneo la jeshi hilo lililoandaliwa kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika kitaifa mkoani humo Agosti 2018, lililopo katika Uwanja wa Nanenane wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
  Mkurugenzi wa Kilimo na Mifugo katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Luteni Kanali Peter Lushika akizungumza na viongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa na viongozi wa Mkoa wa Simiyu kabla ya kutembelea eneo la jeshi hilo lililoandaliwa kwa ajili ya maonesho ya Nanenane lililopo katika Uwanja wa Nanenane uliopo Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu ameahidi kuwa Jeshi hilo litajenga Majengo ya kudumu katika Uwanja wa Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki wa Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu, ili kuendelea kutoa elimu ya teknolojia mbalimbali za kilimo na ufugaji kwa wakulima, wafugaji na wavuvi.

  Meja Jenerali Busungu ameyasema hayo wakati alipotembelea eneo la JKT lililopo Uwanja wa Nanenane Nyakabindi kwa lengo la kujionea maandalizi hayo yanayofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa.Busungu amesema baada ya Nanenane wataanza ujenzi wa majengo ya kudumu ili wakulima, wafugaji na wavuvi wanufaike na teknolojia ya kilimo kwa muda wote.

  “Mkuu wa mkoa ametupa mkakati wao kuwa kila baada ya miezi mitatu kutakuwa na maonesho katika uwanja huu, tunaahidi kujenga majengo ya kudumu hapa na maonesho yajayo miezi mitatu inayofuata wananchi watarajie kupata vitu vizuri kutoka JKT, maana JKT ni kisima cha kila kitu” alisema Meja Jenerali Busungu.

  “ Katika maonesho haya watarajie kuona teknolojia mbalimbali za kilimo, ufugaji, uvuvi pia watarajie kuona bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na JKT zikiwemo bidhaa za kilimo, viwanda na kwa ndugu zangu Wanyantuzu wataona mbuzi na kondoo wa maziwa na wataona kuwa si ng’ombe tu wanaotoa maziwa” alisisitiza Meja Jenerali Busungu.

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru JKT kwa kazi kubwa ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane waliyoifanya, huku akibainisha kuwa uwepo wa JKT utasaidia kuwabaadilisha vijana wa Simiyu kwa kuwa watapata fursa ya kujifunza teknolojia mbalimbali.

  “ Tunawashukuru sana JKT kwa kutuamini na tunajua kuwepo JKT kutasadia kuwabadilisha vijana wa hapa kwa kuwa kuna vijana wanamaliza darasa la saba au kidato cha nne hawana pa kushika na sisi tuna vikundi vingi vya vijana , tuko tayari kuleta vikundi vyetu vya vijana kuja kujifunza hapa” alisisitiza Mtaka.

  Naye Mbunge wa Itilima amesema maonesho ya nanenane na uwepo wa JKT kutakuwa msaada kwa wananchi kwa kuwa watapata elimu itakayowawezesha kufanya uzalishaji wenye tija ikiwemo ufugaji wa kisasa na kilimo bora.

  0 0


  Na Rhoda Ezekiel Kigoma

  KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa Bashiru Ally amewaapisha wanachama wapya 269 kutoka vyama vya upinzani akiwemo aliekuwa Mbunge wa jimbo la Kasulu Vijijini Agripina Buyogera na Mwenyekiti wa Chama cha NSSR Mkoa na Wilaya ya Kasulu Hitra Joseph Gelvasi Bahenga katika amkutano wa kampeni za uchaguzi Wilayani Kakonko mkoani Kigoma.

  Tukio hilo lilifanya jana Katika mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu wilayani humo wakati akimnadi mgombea wa Chama hicho ambapo wananchi hao walioamua kujiunga na CCM na kuwaomba wananchi kuendelea kukiamini na kumpa kura mgombea wao.

  Amesema wanachama hao hawajawanunua ila wamevutiwa na utekelezwaji wa Ilani ya Chama na amewaahidi wananchi kabla ya uchaguzi huo kuisha watapokea vigogo wengi na watawapokea hawata wabagua wote watakaotaka kujiunga na CCM na wote wanahaki ya kujiunga.

  " Milango ya wanachama wapya iko wazi na tuna wakaribisha sana na hawa ndio wamefungua mlango tunawakaribisha wote CCM haina mwenyewe wote tuna sifa ya kuwa wanachama.Sasa tunapokea wote na hatuko tayari kununua Watu kutoka vyama vingine wataona mambo wenyewe watakuja," alieleza Bashiru.

  Akimkaribisha mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni hizo Ally alisema CCM ni chama cha wanyonge kipo kwaajili ya kuwatetea katika kuleta maendeleo hivyo amewaomba Wanakakoko kumchagua Chiza ili akafanye kazi na Chama cha Mapinduzi.Alisema anatambua mchango wa Chiza kwa wanakakonko na yapo mengi ambayo ameyafanya kwa Jimbo la Buyungu suala la kuwashawishi wananchi wasimchague kwa kigezo kwamba ni mzee hii sio kweli wamuamini wampe kura aweze kuwaletea maendeleo zaidi.

  "Tunae mgombea ambae tunamnadi kwa sifa zake angalia elimu yake busara zake mchango wake katika jamii kupitia mkutano huu wana CCM wote watakao hisika na kampeni muwe na moyo wa kuvumilia mkitupiwa matusi msirudishe matusi hayo CCM ni chama cha wastaarabu muwe wavumilivu" alisema Katibu Mkuu.

  Alisema Serikali imefanya mambo mengi ya maendeleo na anasimamia na utekelezaji wa Ilani ya CCM kinachofanya kazi ya uongozi katika kusimamia mapambano ya kupunguza umasikini vijijini, ili uweze kuondoa umasikini lazima uwekeze katika elimu ambayo ni sekta mama na Serikali imefanya vizuri.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mkoa wa Kigoma James Bahingai alisema ameridhishwa na utendaji wa Rais Dk.John Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanaya na kutamka kuanzia leo amejiunga CCM.

  Aliseme Watanzania waangalie mambo muhimu wasikalie ushabiki kwenye mambo ya maendeleo ya nchi waendelee kuunga mkono Serikali alisema Dk. Magufuli amefuta ada katika shule , kuboresha huduma za afya, miundombinu inaendelea kujengwa kila siku."Leo Mkoa wa Kigoma ni sehemu ya Serikali na Serikal imewaamini wananchi wa kigoma kwa kutoa mawaziri watatu," amesema.

  Ameongeza "Rais ameikubali Kigoma kwa kuwapa mawaziri ni heshima kubwa na nimeahidi kukaa katika jimbo la Buyungu ili kuhakikisha mgombea wa anapita.Tunataka kiongozi atakaeenda kuzungumza na Rais mambo yanayofaa," alisema Bahingai.

  Wakati huo huo aliekuwa mbunge wa jimbo la Kasulu vijijini Agripina Buyogera aliahidi kuendelea kuruka kama ndege na anatua kama ninja huku akifafanua kwa dhamira yake ameamua mwenyewe kurudi CCM na kuhakikisha maendeleo yanapatikana wamapitishe Chiza kwani ndie mbunge pekee atakaeweza kuleta maendeleo.
  Mwanasiasa Mkongwe na aliyewahi kuwa Katibu MKuu wa chama cha CCM,Ndugu Yusuf Makamba akimtambulisha na kumnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Buyungu Mh.Christopher Chiza wakati wa uzinduzi wa Kampeni za ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo wilayani Kakonko mkoani Kigoma 
  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi akiwa ameambatana na mgombea Ubunge wa jimbo la Buyungu Mh.Christopher Chiza wakati wa uzinduzi wa Kampeni za ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo wilayani Kakonko mkoani Kigoma.
  Mwanasiasa Mkongwe na aliyewahi kuwa Katibu MKuu wa chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu Yusuf Makamba  akiwa katika picha ya pamoja na baaadhi ya Wabunge wa chama hicho mapema jana wakati wa uzinduzi wa Kampeni za ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma,Pichani kulia ni Mh Bashe,Peter Serukamba na mwisho kabisa kushoto ni Mh Nape.
  Baadhi ya viongozi na Wabunge wa CCM wakifurahia shuughuli za uzinduzi wa kampeni za Ubunge ndani ya jimo hilo la Buyungu wilani Kakonko mkoani Kigoma 
  Baadhi ya Wanachama na Wafuasi wa chama cha Mapinduzi (CCM),wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Kampeni za ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu wilayani humo .

  0 0
 • 07/27/18--01:13: HALI YANGU KWA SASA-WAKONTA

 • 0 0

   
  Kaimu Meneja Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS), ambaye ni Ofisa Kujenga Uwezo wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Simon Lugazo akizungumza na madiwani wa Halmashauri ya Kilosa kuhusu mradi wa TTCS kufikia mwisho 2019. (Picha na Suleiman Msuya).

   
  NA SULEIMAN MSUYA, KILOSA

  HALMASHAURI ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro imetenga Sh. milioni 46 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ajili ya Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamii (CBFM) katika vijiji vitatu.

  Hayo yamesemwa Mkuu wa Idara ya Maliasili, Ardhi na Misitu wilaya ya Kilosa, Ibrahim Ndembo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana wilayani hapo .Ndembo alisema halmashauri imekubali kutenga fedha hizo ili kuweza kuendeleza jitihada ambazo zimefanywa na Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS) katika vijiji 20 vya wilayani hapo.

  Alisema halmashauri katika kutekeleza dhana ya CBFM iliyoanza kutekelezwa na Mradi wa TTCS wataanz katika vijiji vitatu ambavyo ni New Mamboya, Inyunywe na Nyangala kata ya Mamboya."Zipo taarifa kuwa hawa ndugu zetu wa TTCS ambao wanatekeleza dhana ya CBFM katika vijiji 20 wanatarajia kuondoka Novemba mwaka hivyo ili kuendeleza lengo lao halmashauri imetenga Sh.Mil 46 ambayo itatumika kwenye vijiji vitatu vya maeneo ya Kaskazini mwa Kilosa," alisema.

  Alisema CBFM kuanzishwa katika vijiji hivyo vya New Mamboya, Inyunywe na Nyangala itasaidia kuokoa misitu ambayo inaharibiwa kwa wingi.Mkuu huyo wa idara alisema lengo lao lilikuwa ni kutekeleza dhana ya CBFM katika vijiji vitano kila mwaka wa fedha ila kutokana na uhaba wa fedha wataanza na vijiji hivyo vitatu.

  Ndembo alisema matarajio yao ni kupitia Baraza la Madiwani katika mwaka wa fedha 2019/2020 watatenga fedha nyingine kwa ajili vijiji vingine vya Kaskazini hasa Dumila ili kufikia vijiji 20 mwaka 2021.Mkuu huyo wa idara alisema Kilosa ina vijiji 139 na vijiji ambavyo vinatekeleza CBFM ni 20 na vyote vipo Kusini.

  Alisema watatumia wana vijiji kutoka Kusini kutoa elimu ya CBFM na mkaa endelevu katika vijiji vipya vya mradi.Alisema wanachofanya ni kusimamia Sheria na Sera ya Misitu ambayo inahitaji kuwepo kwa CBFM."Mwananchi hawezi kuambiwa misitu inatoa hewa pekee anatakiwa aone faida inayoshikika ndio ataitunza na hili limeonekana huko Kilosa Kusini hivyo an aye pings ni kwamba anapingana na Sheria,"alisema.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilosa Hassan Mkopi alisema madiwani wote wameridhia utengaji fedha kwa ajili ya CBFM hivyo kuwataka watendaji kutekeleza kwa ufanisi.Mkopi alisema mradi wa TTCS umekuwa mkombozi mkubwa katika utunzaji mazingira na uchumi wa wana vijiji wao hivyo ni lazima uwe endelevu.Kaimu Meneja wa Mradi wa TTCS, Simon Luganzo alisema mradi huo unatarajia kufikia mwisho hivyo wamelazimika kuwaita wadau wa Serikali na madiwani ili kujua wamejipangaje kuendeleza.

  Alisema mradi huo unaotekelezwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (Mjumita) na Shirika la Kuendeleza Nishati Asilia Tanzania (TaTEDO) kupitia Ufadhili wa Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswis (SDC), umefanikiwa kuokoa uharibifu wa misitu kwa zaidi ya asilimia moja kwa miaka michache ya uwepo wake.

  "Tunataka tukiondoka dhana ya CBFM iwe endelevu na ili kujihakikishia ni lazima ujue unaowaachia wamejipangaje na hapa Kilosa wameonesha mfano mzuri," alisema.Luganzo alisema mradi wa TTCS umesaidia usimamizi misitu shirikishi, utawala bora na sheria huku pia zaidi Sh.milioni 800 zikikusamywa

  0 0

  Na Jumbe Ismailly- ITIGI

  MWENEYEKITI wa Halmashauri ya Itigi,Wilayani Manyoni,Mkoani Singida,Ally Minja amewaagiza wakuu wa idara za Kilimo na Ushirika kuanzisha ushirika wa wakulima wa zao la dengu katika Halmashauri hiyo,ili kuwapunguzia wakulima wa zao hilo unyanyasaji wanaoupata wakati wanapotaka kuuza dengu kwa wafanyabiashara wa zao hilo.

  Mwenyekiti huyo alitoa agizo hilo kwenye mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za Kijiji cha Songambele,katika Mji mdogo wa Itigi,wilayani Manyoni.

  Aidha Minja alisisitiza kwamba wakati umefika kwa Halmashauri hiyo kuwanasua wakulima wa dengu katika manyanyaso wanayopata kutoka kwa wanunuzi wa zao hilo waliojenga utamaduni wa kuwadhulumu haki zao kwa kutaka kuuziwa zao hilo likiwa bado lipo shambani.

  “Tumechoka wakulima wa dengu kuendelea kunyanyaswa na kudhulumiwa,dengu kuendelea kununuliwa zikiwa bado shambani haitapendeza sana tunataka tuanzishe ushirika wa dengu”alisisitiza Mwenyekiti huyo.

  Kwa mujibu wa Minja itapendeza sana iwapo wakulima wa dengu watapata bei inayostahili na bei ambayo mnunuzi ameipanga kabisa kununua zao hilo,ili aweze kuipata mkulima wa zao hilo moja kwa moja.

  Akitoa maelezo mafupi ya shughuli za maendeleo kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Halmashauri kufungua mkutano huo wa Baraza,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Itigi,Pius Luhende alisema pamoja na kwamba mvua ilizidi kunyesha kwa mwezi wa pili na kuathiri kilimo cha dengu,lakini bado dengu iliyopo ni nyingi sana.

  “Na wadudu wengi Red boloes waliokuwa wametuvamia,lakini Halmashauri yako Mh.Mwenyekiti tuliaamua maamuzi magumu tukaamua kununua dawa kwa fedha za serikali tukawanunulia wananchi wasio na uwezo kwamba wamwagilie wadudu wale ili wakivuna mazao yao waweze kulipa”aliweka bayana Luhende.

  Hata hivyo katika kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo,kwa Mkurugenzi Mtendaji yaliyoulizwa,diwani wa viti maalumu,Jane Ismaili Chungwa alitaka kufahamu serikali ina mpango gani juu ya kuwasaidia wakulima wa zao la dengu kutokana na umuhimu wa mazao hayo.

  Akijibu swali hilo,Luhende alisema kwa sasa wana mkakati wa kufuatilia soko zuri la mauzo ya zao la dengu ili wananchi waweze kunufaika na kuongeza kwamba wanajipanga kwenda Dar-ES- Salaam kwenda kujadiliana na wadau wanaohitaji zao hilo ili waende wakanunue kwenye vyama vya ushirika.
  Ni baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Itigi wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Kijiji cha Songambele,mjini Itigi wakiomba dua ya kuliombea baraza hilo kufanya maamuzi yenye hekma na busara.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi,Ally Minja(wa pili kutoka kulia) akiwaongoza madiwani wa Halmashauri hiyo katika dua ya kuliombea baraza hilo kufanya maamuzi yenye hekma na busara sambamba na kudumisha amani iliyopo nchini.
  Makarani wa mikutano ya madiwani wakiwa katika ukumbi wa mikutano wakinukuu maazimio yanayopitishwa na wajumbe wa mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Kijiji cha Songambele.mjini Itigi.
  Magunia ya zao la dengu yakiwa yamehifadhiwa kwenye ghala moja la mfanyabiashara wa mjini Itigi,yakisubiri kusafirishwa kwenda kwenye soka la zao hilo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).

  0 0


   Meneja wa DAWASCO wa Magomeni Mhandisi Damson Mponjoli akizungumza na waandishi wa habari wakati wa operesheni maalumu ya kufichua wezi wa maji iliyofanyika katika maeneo ya Magomeni Manzese, Manzese Midizini, Manzese Kilimahewa ampapo operesheni hiyo inaendelea maeneo mengine. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
  Moja ya maungio yaliyokuwa yakitumika kuiba maji na kuyaweka kwenye matanki kwa ajili ya kuyauza. 
  Mashine za kuvuta maji zilizokuwa zikitumika kuiba maji na kuyaweka kwenye matanki kwa ajili ya kuyauza. 
  Mtaa wa Magomeni Manzese zilipokamatwa mashine hizo.
  Moja ya eneo zilipokuwa zimefungwa mashine. 
  Wananchi wakichota maji katika tanki la maji lililokuwa likijazwa na kuuziwa wananchi kwa shilingi 100/- kwa ndoo. 
  Wananhi wakitoa kero zao. 
  Maungo na tanki lililokuwa linajanzwa maji na kuuzia wananchi. 
  Meneja wa DAWASCO wa Magomeni Mhandisi Damson Mponjoli akitoa elimu kwa wananchi. Na 


  Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

  Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) imekamata mashine za maji (pump) zilizokuwa zimeunganishwa kwenye mabomba ya shirika hilo na kuwauzia wananchi kinyume cha sheria. Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa operesheni maalumu ya kufichua wezi wa maji Meneja wa DAWASCO wa Magomeni Mhandisi Damson Mponjoli amesema kuwa shirika halitaacha watu wanaohujumu shirika na kuathiri wananchi wengine wasipate maji. 

  Amesema kuwa licha waliojiunganishia maji kenyemela kukimbia lakini kidhibiti chao hakiwezi kukimbia hivyo hatua za kisheria zitafuata kwanza ni kujisarimisha kwenye mamlaka. Mhandisi Mponjoli amewaomba wajumbe wa serikali za mtaa kupeleka orodha ya watu 50 ili kuwawekea vizimba vya maji ili kuondoa adha ya upatikanaji wa maji katika maoeneo yao. 

  Amesema kuwa miundombinu yote iliyokuwa imeunganishwa lazima ifumuliwe kutokana na watu hao kuunganisha mabomba hayo na kupitisha katika katika vyoo na mitaro ya maji machafu. Mponjoli amesema kuwa yao walijiungia maji kiholela suala ambalo linahatarisha usalama wa afya za wananchi pamoja na shirika kukosa mapato ya kuendeshea huduma ya maji katika maeneo yao.

  Katika operesheni hiyo wamekamata Mashine za Kuvuta Maji kutoka katika Mabomba makubwa ya dawasco, matanki Nane(8) ya Lita 10000,5000 na lita 2000. Operesheni imefanyika katika maeneo ya Magomeni Manzese, Manzese Midizini, Manzese Kilimahewa ampapo operesheni hiyo inaendelea maeneo mengine.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameutaka Uongozi wa mkoa wa Mbeya kuweka mpango wa kuyatumia maji ambayo yamechakatwa kutoka kiwanda cha soda cha pepsi cha SBC Mbeya.

  Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Kiwanda Kipya cha Soda za Chupa za Plastiki cha Pepsi, SBC Mbeya. Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Mbeya, ameupongeza Uongozi wa SBC Mbeya kwa kuajiri Watanzania zaidi ya asilimia 90%.

  “ Niliyoayaona yamenipa moyo na nimepata mafunzo pia nitakapokwenda kwenye viwanda vingine nini niwaelekeze cha kufanya” alisema Makamu wa Rais. Makamu wa Rais amepongeza kiwanda hicho kwa kuwa walipaji wazuri wa kodi na kwa wakati. Makamu wa Rais pia alipongeza mchango kwa jamii na michango mingine katika ngazi ya Kitaifa.

  Mapema, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya SBC Tanzania Bw. Foti Nyirenda alimueleza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznia Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa Kiwanda kipya cha soda za chupa za plastiki ktazalisha kreti 24,000 na pia Kiwanda cha Kuchakata maji taka ambapo kiwanda hicho kinatumia zaidi ya dola laki sita kwa ajili ya shughuli za kutunza na kuboresha mazingira.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kiwanda kipya cha soda za chupa za plastiki katika kiwanda cha soda za Pepsi SBC Mbeya, wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBC Tanzania Bw. Ziad El Khalil (kulia), Mkurugenzi Mkuu Bw. Avinash Jhah , Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Naibu Waziri Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Amos Makala na Meneja wa Kiwanda cha SBC Mbeya Mr. Sanam Mahambrey . (Picha na ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la uzinduzi wa kiwanda kipya cha soda za chupa za plastiki katika kiwanda cha soda za Pepsi SBC Mbeya, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBC Tanzania Bw. Ziad El Khalil . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya chupa ya plastiki wakati wa uzinduzi wa kiwanda kipya cha soda za chupa za plastiki katika kiwanda cha soda za Pepsi SBC Mbeya, kulia ni Mhandisi Mkuu wa Pepsi Tanzania Bw. Prabir Bhowmick na Msimamizi wa Mitambo Bw. Odestus Kabelenga. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikitoa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SBC Tanzania Bw. Ziad El Khalil mara baada ya kuweka jiwe la msingi la Ufunguzi wa kiwanda cha kuchakata maji taka SBC Mbeya.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea maua kutoka kwa mtoto mwenye mahitaji maalum Amina Hawa kutoka Child Support Tanzania kama ishara ya kumkaribisha alipotembelea kiwanda cha Soda za Pepsi, SBC Mbeya. 
  Mtoto Maurine Chalanga mwenye umri wa miaka 5 akipiga ngoma na kuwaongoza wenzake kuimba wimbo wa Taifa wakati wa mapokezi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kiwanda cha soda za Pepsi SBC Mbeya. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa SBC Tanzania Bw. Ziad El Khalil wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda kipya cha soda za chupa za plastiki katika kiwanda cha soda za Pepsi SBC Mbeya.(picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


  0 0

  Katibu wa HKT Siasa na uhusiano wa kimataifa Cde Ngemela Lubinga ameanza ziara yake ya kampeni katika Kata ya Nyamichige wilaya ya Ruangwa na jimbo LA Ruangwa.

  Katika mkutano huo cde Ngemela Lubinga aliwasisitiza wananchi wa kata ya Nyamichige wamchague diwani Ndg Mikidadi Ibadi Matauna almaarufu Mbute ambaye alihama Chama cha Chadema na kujiunga na CCM kutokana na Chama hivyo kushindwa kumpa ushirikiano wa kutosha kama diwani na kumtenga mara kwa mara anapozisifia jitihada za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Cde Lubinga amewaomba wananchi hao wamchague diwani huyo ili kuweza kukamilisha safu ya uongozi katika jimbo hilo kwani kwa kufanya hivyo hawataipa heshima CCM peke yake kama Chama kilichowaletea maendeleo katika wilaya ya Ruangwa lakini pia itakuwa ni heshima kubwa kwa mbunge wa jimbo hilo ambaye Rais Dr John Pombe Magufuli alimpa heshima ya kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya tano.

  Aidha cde Lubinga aliendelea kusisitiza kuwa maendeleo yanayoendelea kupatikana katika jimbo la Ruangwa ni juhudi kubwa za mbunge wa jimbo hilo Mhe Majaliwa Kasim Majaliwa,Waziri Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Cde Lubinga amewasisitiza wananchi katika kata ya Nyamichige kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kujituma pamoja na kuhakikisha vijana wao wanawapeleka shuleni na pia kuhakikisha wanatokomeza mimba za mapema kwa watoto wa kike ili waweze kuwa viongozi wa kesho.

  Mwisho cde Lubinga alichukua wasaa wake kumpongeza mbunge wa jimbo la Ruangwa Mhe Majaliwa Kasim Majaliwa kwa kuwa anaweza kuwa ni Waziri Mkuu wa kwanza kuweza kufanya ziara katika kata zote 22 za jimbo la Ruangwa na pia vijiji 88 kati ya vijiji 90 vilivyopo katika jimbo la Ruangwa kwani kwa kufanya hivyo ameonyesha mfano kama kiongozi wa kitaifa.

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akisalimiana na Uongozi wa juu katika Gereza Kuu la Isanga jijini Dodoma. Ziara ya Naibu Waziri katika gereza hilo imelenga kuhimiza viongozi hao kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya ‘Dodoma ya Kijani’

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima (kushoto) akiteta jambo na Meneja wa Ranchi ya Kongwa mara baada ya kutembelea ranchi hiyo mapema leo. Pamoja na mambo mengine Naibu Waziri amemuagiza Meneja huyo kuwa na mpango kabambe wa upandaji miti katika eneo hilo.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima (kushoto) akiteta jambo na Meneja wa Ranchi ya Kongwa mara baada ya kutembelea ranchi hiyo mapema leo. Pamoja na mambo mengine Naibu Waziri amemuagiza Meneja huyo kuwa na mpango kabambe wa upandaji miti katika eneo hilo.
  Meneja wa Ranchi ya Kongwa Bw. Euzebius Mutayabarwa akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) wa namna ya shughuli za hifadhi ya mazingira zinavyotekelezwa katika eneo lake. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine na viongozi wa Wilaya ya Kongwa.
  Meneja wa Ranchi ya Kongwa Bw. Euzebius Mutayabarwa akifafanua jambo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) na ujumbe wake mara baada ya kutembelea ranchi hiyo leo iliyopo Wilayani Kongwa Jijini Dodoma.


  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima hii leo amefanya ziara ya kikazi katika Gereza Kuu la Isanga lililopo Jijini Dodoma na kuutaka uongozi wa Gereza hilo kuifanya Dodoma kuwa ya kijani kwa kupanda miti zaidi na kuacha matumizi yasiyoendelevu ya mkaa na kuni kama nishati ya kupikia.

  Akizungumza na Uongozi wa Gereza hilo Mhe. Sima amewataka kutumia majiko banifu ili kupunguza kasi ya ukataji miti kwa matumizi ya kupikia. “Natoa wito kwenu kuanza kutumia teknolojia mbadala ya kuni na mkaa kama nishati ya kupikia na kuwaagiza kuona namna bora ya kutumia gesi ili kunusuru misitu yetu”

  Pia, Waziri Sima ameagiza uongozi wa gereza hilo kutenga eneo maalumu kwa ajili ya kuotesha miti inayostahimili ukame kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa na shamba darasa kwa watu kujifunza kilimo hicho cha miti na kutoa ushauri wa kitaalamu.

  Akitoa taarifa ya Gereza hilo Naibu Kamishna wa Magereza Julius Mayenga Sang’udi amesema kuwa kwa siku gereza hilo hutumia wastani wa kuni mita za ujazo 8-10 kwa matumizi ya kupikia, kuni ambazo hutolewa katika kambi ya Mayamaya, Taasisi za Serikali na ujenzi binafsi.Kufuatia maelekezo ya Naibu Waziri, Kamishna Sang’udi amesema kuwa mpango uliopo sasa ni kugeuza changamoto kuwa fursa ikiwa ni pamoja na kuhuisha wazo la kujenga mfumo wa matumizi ya gesi na ‘biogas’ kama nishati ya kupikia.

  Katika hatua nyingine Waziri Sima ametembelea Ranchi ya Kongwa na kumuagiza Meneja wa Ranchi hiyo Bw. Euzebius Mutayabirwa kuandaa mpango maalumu wa uoteshaji wa miti katika eneo lao haraka iwezekanavyo, na kuwaomba Wakala wa Misitu Tanzania kupeleka miti katika eneo hilo yenye kuhimili ukame na rafiki kwa mazingira.

  “haiwezekani eneo kama hili lenye ufugaji mkubwa, eneo lenye ngo’mbe zaidi ya 9000 lakini hamuwezi kupanda miti wakati mnataka kutunza vyanzo vya maji, eleweni kuwa ufugaji ni sambamba na kutunza mazingira. Inawezakanaje kuwa na ufugaji kama huu halafu hakuna mpango wowote wa upandaji wa miti?” Waziri Sima alihoji.

  Sambamba na hilo Mhe. Sima amemwagiza Meneja wa Ranchi hiyo Bw. Mutayabirwa kuwa mfano kwa kuwa na shamba darasa la matumizi ya ‘Biogas’.Nae Meneja wa Ranchi hiyo Bw. Mutayabirwa amesema kuwa utekelezaji wa maagizo hayo unaanza mara moja ikiwa ni pamoja na upandaji wa miti kwa ajili ya vivuli vya mifugo na kuhifadhi vyanzo vya maji na kuwashirikisha wataalamu wa Carmatec kwa ajili ya kukamilisha andiko la mradi wa kuzalisha biogas.

  Naibu Waziri Sima amekamilisha ziara yake ya siku tatu kwa kutembelea Wilaya za Chemba, Bahi na Kongwa zote za Jijini Dodoma.

  0 0

  Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Chain of Hope la nchini Uingereza wamefanya upasuaji wa kufungua kifua kwa watoto tisa wenye umri wa miezi mitatu hadi miaka 17 kuanzia tarehe 23/07/2018 hadi leo tarehe 27/07/2018. 

  Watoto waliofanyiwa upasuaji ni wale wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambapo madaktari wanatengeneza valve na kuziba matundu, kurekebisha mishipa ya moyo ambayo imekaa vibaya, kurekebisha mfumo wa uzungukaji wa damu katika moyo na kuweka valvu za bandia kwa wale walio na valvu za moyo zilizoharibika. 
  Wagonjwa wote waliofanyiwa upasuaji hali zao zinaendelea vizuri na sita kati yao wameruhusiwa kutoka katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) na kupelekwa wodini kwa ajili ya kuendelea na matibabu. 

  Kambi hiyo inaenda sambamba na utoaji wa elimu pamoja na kubadilishana ujuzi wa kazi kwa wataalamu wetu. Katika kambi hii Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto ni mwanamke hii imeleta hamasa kwa madaktari wetu wa kike kusomea upasuaji wa moyo ambapo kwa Tanzania hatuna Daktari wa kike wa upasuaji wa moyo wote ni wanaume. 

  Hii ni kambi ya tatu ya matibabu ya moyo kwa watoto tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2018 na ni mara ya kwanza kwa Uingereza kuja hapa nchini. Kambi nyingine zilizofanyika ni za upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua ambayo tuliifanya na wenzetu kutoka Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel na Kituo cha Moyo cha Berlin (Berlin Heart Center) ya nchini Ujerumani katika kambi hii jumla ya watoto 17 walipata matibabu. Upasuaji wa kufungua kifua tulifanya na wenzetu wa Taasisi ya Open Heart Internartional (OHI)ya nchini Austarial na kufanya upasuaji kwa watoto 20. 

  Kwa upande wa wamama wajawazito ni muhimu wakafanya uchunguzi (Fetal Echocardiography) wa kuangalia kama mtoto aliyeko tumboni anamatatizo ya moyo au la. Hii itasaidia kama mtoto anamatatizo ya moyo kupata matibabu mapema pindi atakapozaliwa. 

  Kama mnavyofahamu matibabu ya moyo ni ya gharama hivyo basi tunaendelea kuwahimiza wananchi kujiunga na Mifuko ya Bima za Afya. 

  Imetolewa na: 
  Kitengo cha Uhusiano 
  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete 
  27/07/2018

older | 1 | .... | 1631 | 1632 | (Page 1633) | 1634 | 1635 | .... | 1898 | newer