Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1630 | 1631 | (Page 1632) | 1633 | 1634 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Na Bashir Yakub. 

  Kawaida safu hii huandika na kufafanua masuala mbalimbali ya kisheria na mahakama. Mara nyingi huandika kuhusu ndoa, mirathi, makampuni, jinai, ardhi, na madai mengine kwa ujumla. Leo itakuwa tofauti kidogo japo ni ndani ya tasnia ya sheria humohumo. 

  Nianze tu kwa kusema kuwa wakati taifa zima likifanya kazi kufikia uchumi wa kati ambao ndio dira ya mihimili yote mahakama,bunge na serikali, kuna jambo moja ambalo hatuwezi kulisahau. 

  Jambo hili ni utumishi uliotukuka. Hakuna ubishi, injini ya uchumi wa kati ni watumishi. Lakini ni aina gani ya watumishi ambao ni injini ndilo litakuwa swali. Aina ya watumishi ambao wanaweza kutufikisha huko ni wale wenye moyo wa kazi, ari, uvumilivu, waelewa,na wale ambao utumishi kwao sio kazi tu ya kusubiri mshahara mwisho wa mwezi, bali pia huduma nzuri kwa watu. 

  Kote duniani ambako si tu wamefikia uchumi wa kati tunaoulilia, bali pia wana uchumi wa juu kama china, amerika, na nchi za ulaya wamefikishwa hapo na watumishi bora . Waliowahi kufika huko wanajua ni namna gani watumishi wa huko wanavyotoa huduma. Unaweza kudhani unahudunmiwa na ndugu yako wa tumbo moja. 

  Niseme tu kuwa watumishi wa mahakama kuu ya Dar es salaam kitengo cha mawakili wameonesha mfano wa aina hii. Ni aina ya watumishi ambao ukibahatika kuhudumiwa nao unahisi kweli umepewa huduma. Hawatachoka kukupatia maelezo, hawatachoka kukuelekeza, na hata ukitaka namba zao binafsi hukupatia, na endapo utapiga muda wowote kutaka ufafanuzi utapewa bila kukaripiwa kama ambavyo imekuwa pahala pengine pa utumishi. 


  0 0


  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao chake na Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Uongozi wa Kampuni ya Iris Corporation Berhard. Viongozi wa kampuni hiyo wamepewa wiki mbili ili walete majibu kuwa wataleta mtambo wa kutengeneza kadi ghafi au shilingi bilioni 32 walizopewa na NIDA. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Massawe alipokua akijadili jambo katika kikao alichokiitisha Waziri huyo kwa ajili kufanya mahojiano na Wamiliki wa Kampuni ya Iris Corporation Berhard. Wapili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Shaiful Subhan, na Choong ambaye pia ni kiongozi mkuu wa Kampuni hiyo. 
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Iris Corporation Berhard, Shaiful Subhan alipokua anafafanua jambo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa wizara hiyo, jijini Dodoma leo. Viongozi wa kampuni hiyo wamepewa wiki mbili walete majibu kuwa wataleta mtambo wa kutengeneza kadi ghafi au shilingi bilioni 32 walizopewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Watatu kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA, Andrew Massawe. 
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao chake na Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Uongozi wa Kampuni ya Iris Corporation Berhard. Viongozi wa kampuni hiyo wamepewa wiki mbili ili walete majibu kuwa wataleta mtambo wa kutengeneza kadi ghafi au shilingi bilioni 32 walizopewa na NIDA. Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA, Andrew Massawe, na wapili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Shaiful Subhan. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   Na Felix Mwagara, MOHA 

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameipa wiki mbili Kampuni ya Kimataifa ya Iris Corporation Berhard impe majibu ya kuwa italeta mtambo wa kutengeneza kadi ghafi au Dola za Marekani Milioni 14 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 32 za Tanzania. 

  Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma leo, mara baada ya kumaliza kikao na Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na viongozi wa Kampuni hiyo, Waziri Lugola alisema kampuni hiyo haiwezi ikacheza na fedha za Watanzania ambao ni za walipa kodi. 

  Lugola aliongeza kua lazima fedha hizo au mtambo huo upatikane kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano haitakubaliana na mchezo mchafu wa aina yoyote, na pia yeye kama Waziri wa Wizara hiyo anaendelea kutekeleza maagizo ya Rais Dkt John Magufuli. 

  “Tumezungumza nao na tumekubaliana nao kwamba tuwape wiki mbili ili bodi ya kampuni hiyo ikakae ifanye maamuzi ya aidha waturudishie fedha zetu au walete mtambo, lakini sisi kama nchi huu mtambo muhimu sana, bado tuna uhitaji, sisi tungependa baada ya hiyo wiki mbili wafanye maamuzi ya kutuletea mtambo,” alisema Lugola. 

  Aidha, Waziri Lugola amewataka wamiliki wa kampuni zilizolipwa kifisadi fedha za Mradi wa mtambo wa NIDA kujisalimisha jijini Dodoma Agosti 3 mwaka huu wakiwa na mtambo huo vinginevyo warejeshe fedha zilizotumika. 

  Pia Lugola ametoa agizo kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu na Mfanyabiashara Jack Gotham kufika ofisini kwake Agosti 3 saa 3:00 asubuhi ili kutoa maelezo yanayojitosheleza yatakayomsaidia kutoa maamuzi sahihi kuhusiana na ufisadi wa fedha zaidi ya bilioni 32 za mtambo huo ambao hadi sasa haujafika nchini. 

  Lugola aliyataja kampuni hayo kuwa Gotham International ambayo imelipwa kifisadi shilingi 2,848,878,659.75, Iris Corporation Berhard ambayo imelipwa kifisadi 22,919,414,169,84, Gwiholoto Impex inayodaiwa shilingi 946,406,989,00, Sykes Travel Agent 5,979,600,00, Dk Shija Paul Rimoy 27,000,000,00, Aste Insurance 1,206,619.93, na Kampuni ya BMTL 569,192,090,00. 

  Hata hivyo, Waziri Lugola aliwataka Watanzania kutowahusisha viongozi wa sasa wa NIDA na ufisadi huo kwa kuwa hawahusiki hata kidogo, matukio yote ya ufisadi yamefanywa na watangulizi wao na viongozi waliopo sasa wameletwa kuiongoza Mamlaka hiyo kwa ajili ya kuboresha utendaji wa NIDA. Mwisho/-

  0 0

  Kamati ya Bunge ya Miundombinu imelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kujenga mazingira rafiki ya uwepo wa choo na kibanda cha mlinzi kwenye minara ya simu iliyojengwa na Shirika hilo maeneo mbali mbali nchini kote

  Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa Mchafu wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye kijiji cha Mbatamila kilichopo kwenye kata ya Nampungu wilayani Tunduru mkoani Ruvuma

  Mhe. Mchafu amesema kuwa tumeshuhudia kuwa Shirika letu la kizalendo la TTCL pekee ndilo ambalo limejenga miundombinu rafiki ya choo na kibanda kwenye minara yao yote waliyojenga kwenye maeneo mbali mbali nchi nzima kwa ajili ya mlinzi anayelinda minara ya mawasiliano tofauti na kampuni nyingine za mawasiliano ambapo zote kwa pamoja zimepatiwa ruzuku na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ya kujenga minara hiyo kwenye maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara

  “Hongereni mmepata mawasiliano ya mnara wa TTCL ambapo wamejenga miundombinu rafiki ya choo na kibanda cha mlinzi cha kupumzikia hivyo mnara utalindwa muda wote, kutakuwa hamna maambukizi ya magonjwa kwa kukosa choo”, amesema Mhe. Mchafu. Ameipongeza TTCL kwa kuwa wamejenga mnara ambao unatoa mawasiliano muda wote kwa kuwa kuna nishati ya jenereta kubwa ya kisasa.

  Naye Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameipongeza TTCL kwa kujenga minara ya mawasiliano yenye mazingira rafiki kwenye minara yao yote iliyopo maeneo mbali mbali nchi nzima. Nditiye ameongeza kuwa Tunduru ni Wilaya pekee ambapo TTCL ina jumla ya minara 14 na kupitia UCSAF itaongeza minara mingine mitatu kwenye vijiji ambavyo vina mawasiliano hafifu kwa kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanawasiliana. Ameongeza kuwa Serikali inajenga meli na reli ya kisasa hivyo wahakikishe kuwa muda wote wananchi wanawasiliana wakiwa safarini.

  Pia, ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhakikisha kuwa kampuni za simu zinatoa huduma ya mawasiliano kwa wananchi ya kupiga simu, vifurushi na ujumbe kuendana na gharama ya vocha iliyowekwa ambapo ni tofauti na TTCL ambao hawana ujaja ujanja wa kuwaibia wananchi.

  Akithibitisha kuhusu upatikanaji wa mawasiliano mbele ya Kamati hiyo, mwananchi wa kijiji cha Mabatamila kilichopo kwenye kata ya Nampungu iliyopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma Bwana Kassim Zuberi amesema kuwa wanaipongeza TTCL kwa kutoa mawasiliano kwa gharama nafuu zaidi ukilinganisha na kampuni nyingine za mawasiliano. “Tunaiomba TTCL watufungulie huduma za 4G ili tuweze kupata mawasiliano ya intaneti”, amesema Zuberi.

  Mwendeshaji wa UCSAF Mhandisi Albert Richard amesema kuwa UCSAF imetoa shilingi milioni 460 kwa TTCL ili iweze kujenga mnara huo ambapo wananchi wanapata mawasiliano. Pia, ameongeza kuwa tayari UCSAF kupitia ruzuku inayotoa tayari minara 14 imejengwa kwenye Wilaya hiyo na kwenye zabuni ijayo itaongeza minara mitatu ili wananchi waweze kuwasiliana muda wote.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme akizungumza na wajumbe wa Kamati hiyo walipofika ofisini kwake wakati wa ziara yao ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano mkoani humo, Mhe. Mndeme ameishukuru Serikali kwa kujenga minara 14 kwenye Wilaya ya Tunduru.
   
   Amesema kuwa mawasiliano ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi kwa kuwa wanapokea watalii wengi ambao wanachangia pato la taifa. “Niwaombe watoa huduma watoe huduma ya intaneti kwa kuwa ni kikwazo kwa wawekezaji mkoani kwetu ambapo wanataka wapate mawasiliano wakati wote,”amesema Mndeme. Ameongeza kuwa mawasiliano yatasaidia miamala ya kifedha ambapo inakuwa rahisi kwa wananchi kuwasiliana.

  Pia, amefafanua kuwa watoa huduma za mawasiliano wanaojenga minara waangalie jiografia ya mkoa wa Ruvuma kwa kuwa una milima, misitu ni mingi sana, hifadhi, mabonde, ziwa Nyasa na iko mpakani mwa nchi ambapo maeneo hayo yanakuwa na changamoto za mawasiliano na baadhi ya maeneo ya Chiwindi na Chimati wananchi hawapati mawasiliano. Amesema kuwa mawasiliano yanahitajika wakati wote hasa maeneo ya mipakani kwa kuwa mawasiliano ni muhimu katika kuimarisha ulinzi na usalama wa wananchi na taifa kwa ujumla

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano 

  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu (hawapo pichani) wakiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme (aliyekaa mbele) wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye mkoa huo 
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa Mchafu akisikiliza kwa makini maelezo kutoka Mhandisi wa TTCL mkoa wa Ruvuma Abrahamu Msangi kuhusu mtambo wa mawasiliano ya mnara huo wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati hiyo (hawapo pichani) ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye kijiji cha Mbatamila kilichopo wilayani Tunduru kwenye mkoani huo
  Mkuu wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Mhandisi Albert Richard (wa pili kushoto) akitoa maelezo kuhusu miundombinu rafiki ya mnara wa TTCL kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa Mchafu (wa tatu kushoto) wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye kijiji cha Mbatamila kilichopo Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye 
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa Mchafu (wa kwanza kushoto) akiongea na wananchi (hawapo pichani) wa kijiji cha Mbatamila kilichopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma kuhusu umuhimu wa kulinda miundombinu ya mawasiliano wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano mkoani humo. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye
  Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhandisi Ramo Makani na Mbunge wa jimbo la Tunduru Kaskazini akifafanua jambo kwa wananchi wa kijiji cha Mbatimila (wanaomsikiliza) kilichopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati hiyo (hawapo pichani) ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye mkoa huo .  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amehitimisha ziara ya siku tano Mkoani Songwe mapema leo na kusisitiza ushirikiano baina ya uongozi ili kuharakisha maendeleo.

  Mhe Samia Suluhu Hassan amesema akiwa ziarani katika wilaya za Momba, Mbozi na Ileje amebaini kuwa Mkoa wa Songwe umebarikiwa kuwa na rasilimali na utajiri mkubwa kinachotakiwa ni viongozi kushirikiana katika kuwatumikia wananchi.“Nimefurahishwa na kaulimbiu yenu ya maendeleo yataletwa na sisi wenyewe kwa ushindani na ushirikiano, bila ushirikiano hakuna maendeleo, kauli mbiu hii sasa ionekane kwa vitendo”, amesisitiza.

  Ameongeza kwa kuwataka watendaji na viongozi wote wapende kuwatembelea wananchi kuanzia ngazi za vijiji ili waweze kuwahudumia vizuri na sio kukaa ofisini.Mhe Samia Suluhu Hassan ameongeza kwa kuzitaka halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya kuwakopesha wanawake na vijana na kubuni miradi mikubwa itayaowaunganisha wajasiriamali wanawake na vijana kutengeneza viwanda ili kuondokana na umasikini.

  Amesema mpango wa mkoa wa kuanzisha vituo vya maendeleo vya kata utawezekana na kuwanufaisha wananchi endapo watendapo watajitoa kwa dhati kuufanikisha na mpango huu utaiwezesha Songwe kupaa kiuchumi.

  Aidha Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Mkoa wa Songwe kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti na wale walioko mipakani kuendelea kutunza amani.Naye Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa ameshukuru Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kufanya ziara mkoani Songwe kuahidi kuwa maelekezo na maagizo aliyoyatoa atayasimamia yatekelezwe.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan mapema leo akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Songwe (walioko mstari wa nyuma) kabla hajaondoka kuelekea Mkoa wa Mbeya.

  0 0

  Na Rhoda Ezekiel Kigoma

  MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga ameyataka mashirika pamoja na vikundi vya wakimbizi vinavyo washawishi wakimbizi kuacha kujiandisha kurudi kwao kwa hiyari kuacha tabia hiyo.

  Mkuu huyo aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wakimbizi katika kambi ya Ndita wilayani Kibondo ambapo amesema mashirika na vikundi hivyo wanavijua endapo wataendelea na tabia hiyo watachukuliwa hatua za kisheria.

  "Mashirika yanayo chochea wakimbizi na kuunga mkono upinzani nchini Burundi yataondolewa na hayata ruhusiwa kutoa huduma tena," amesema.Ameongeza kwa sasa hali ya amani na usalama kwa nchi ya Burundi ni salama na mali walizoziacha kwao bado zipo,hivyo wakimbizi warejee nyumbani kwao kwani hakuna utaratibu wa mkimbizi wa Burundi kwenda nchi ya tatu utaratibu huo ni kwa Wakongomani pekee.

  AmesemakKambi ya wakimbizi sio mahali pa kudumu ni mahali pa kuhifadhi raia ambao nchini mwao kuna utishio wa kiusalama.Kwa sasa Burundi usalama upo hivyo wananchi wana wanatakiwa kurejea nchini kwao kwa hiyari na kusitokee vitisho wala ushawishi wowote.

  "Utaratibu wa kuwapeleka raia wa Burundi nchi ya tatu ni ya haupo na Serikali ya Tanzania haitoi uraia kwa wakimbizi wa Burundi kama njia zote zimefungwa njia iliyopo ni moja tu mrejee kwenu kwa hiyari na UNHCR na IOM itahakikisha mnasafiri na mnafika kwenu mnaishi vizuri," amesema Brigedia Jenerali Maganga.

  "Yapo mashirika shirika yana kwamisha mchakato huu tunawajua, niwaombe kitu kimoja kama mna maslahi yenu binafsi muyaweke pembeni hatuta wavumilia, ukiona shirika lako limeitwa ofisini kwangu jiandae kuondoka na tukifukuza hapo hakuna sehemu tena kstika Tanania hii utafanya kazi," alielezea Maganga.

  Pamoja na hayo baadhi ya wakimbizi akiwemo Nkruliyabanzi Andrew amesema wao kama wakimbizi wanapenda kurejea nchini mwao lakini bado wanauoga kuwa wanaweza kurudi nchini mwao wakaanza kunynyaswa kwakuwa walikimbia.Waliomba Serikali ya Tanzania kuzungumza na Serikali ya Burundi kuingia kambini kuzungumza na wakimbizi na kuwahahikishia endapo watarudi wataishi salama wao wako tayari kurejea nchini mwao wakihakikushiwa hayo.

  Uamuzi wa kuwarejesha wakimbizi walioingia nchini Tanzania 2015 ulifikiwa Mwishoni mwa mwaka 2017 ambapo pande tatu za shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR na nchi za Burundi na Tanzania kujiridhisha hali ya usalama Burundi imerejea na kuwaomba Wakimbizi warudi kwao ambapo mpaka sasa baadhi ya wakimbizi wamerejea nchini mwao kwa hiyari.
   Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga akizungumza na wakimbizi katika kambi ya Nduta wilayani Kibondo Mkoani Kigoma akiwataka kurejea Nchini kwao kwa hiyari, pembeni ni watumishi wa idara ya mambo ya ndani na Baadhi ya mashirika ya kuhudumia wakimbizI.
  Baadhi ya Wananchi  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga alipokuwa akizungumza na wakimbizi katika kambi ya Nduta wilayani Kibondo Mkoani Kigoma akiwataka kurejea Nchini kwao kwa hiyari.
   Burudani ya ngoma ilikuwepo

  0 0

  *Biashara zake nchini kuendeshwa kwa jina la Howden Puri Insurance Brokers Limited

  Kampuni ya kimataifa ya Howden, chini ya kampuni mama ya Hyperion Insurance Group imeingia katika ushirikiano wa kimkakati wa kukuza biashara na kampuni kongwe ya masuala ya bima nchini ya B.R. Puri & Company Limited, ambapo chini ya ushirikiano huo imeanzishwa kampuni itakayoendesha biashara zake nchini inayojulikana kwa jina la Howden Puri Insurance Brokers Limited. David Howden, Afisa Mtendaji Mkuu wa Hyperion and Howden amesema (Pichani) “Hii ni hatua nzuri kwetu kwa kampuni ya Howden kuwa na mshirika wa kibiashara barani Africa na tunayo furaha kushirikiana kibiashara na kampuni ya B.R. Puri, ikiwa ni moja ya kampuni kubwa inayoongoza katika soko la Tanzania. 

   Mikakati yake mikubwa ya kibiashara inaenda sambamba na mikakati ya Howden na tuna imani kwa kuunganisha mikakati yetu ya kibiashara kupitia kampuni mpya ya Howden Puri tutaweza kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wa ndani na jumuiya za kimataifa nchini Tanzania, Afrika Mashariki na zaidi ya hapo. Kupitia ushirikiano huu tunaona zipo fursa nyingi zinazotuwezesha kukua zaidi kibiashara” 

  Akiongelea ushirikiano huu wa kibiashara, Arun Puri, Mwenyekiti wa Howden Puri alisema “Kampuni ya BR Puri & Company, ilianzishwa na baba yangu kwenye miaka ya 1950, ikiwa ni moja ya kampuni ya kwanza nchini Tanzania kujishughulisha na biashara za uwakala wa bima. Naamini kwa kuunganisha ujuzi wetu na uzoefu mkubwa tulionao na utaalamu wa Howden wa kutoa huduma katika nchi nyingi duniani kutanufaisha wateja wetu tulio nao na watakaojiunga nasi. 

   Umesh Puri, Afisa Mtendaji Mkuu wa Howden Puri, aliongeza kusema “Tukiwa kampuni ya uwakala wa bima inayoangalia mbele hapa nchini Tanzania, lengo letu ni kubuni huduma mpya za bima zinazoendana na hali ya soko la Tanzania. Howden imechagua kushirikiana na kampuni ya Tanzania kibiashara ikiwa ni ya kwanza barani Afrika kutokana na jitihada nzuri zinazofanywa na wasimamiaji wa sekta ya bima kuiboresha zaidi sambamba na mazingira mazuri ya kufanyia biashara yaliyopo nchini kwa ujumla”.

  0 0

  NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akifuatilia kwa umakini mkataba wa Maji wa Shume kuangalia mapungufu yaliyopo jana kabla ya kupelekwa Wizarani katikati ni Katibu wa Naibu Waziri huyo Karim Lichela kushoto ni Mhandisi wa Mipango na Ujenzi wa Tang Uwasa Rashidi Selemani .
  NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akifuatilia kwa umakini mkataba wa Maji wa Shume kuangalia mapungufu yaliyopo jana kabla ya kupelekwa Wizarani katikati ni Katibu wa Naibu Waziri huyo Karim Lichela kushoto ni Mhandisi wa Mipango na Ujenzi wa Tang Uwasa Rashidi Selemani wa mwisho kushoto ni Mhandisi wa Maji Mkoa wa Tanga Ladislaus Modestus 
  NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso wa tatu kutoka kushoto akimsikiliza Katibu Tawala wa wilaya ya Lushoto wakati alipotembelea chanzo cha maji cha Ngulu kata ya Magamba wilayanu lushoto wakati wa ziara yake 
  NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akikagua tenki la Maji la Kata ya Kwamashai wilayani Lushoto wakati wa ziara yake.

  NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ameagiza aliyekuwa Mhandisi wa Maji wilaya ya Lushoto ambaye amehamishiwa Maswa mkoani Shinyanga afike wilayani humo kuchukua mikataba ya mradi wa maji Shume ndani ya wiki moja aupeleke wizarani.

  Mradi huo wa ujenzi wa miundombinu ya maji Shume Manola hadi Madala unatakelezwa na mkandarasi MS Organes Contractors Co.Limited wa wilayani Lushoto ambapo unagharimu kiasi cha Bilioni 2,493,272,852.

  Aweso alitoa agizo hilo jana wakati akihitimisha ziara yake wilayani Lushoto ambapo aligundua kuwepo kwa mkanganyika kwa ulipwaji wa fedha za mradi wa Maji shume ambazo zimepelekwa na serikali kwa kulipwa mkandarasi kwa kiwango tofauti kwenye mkataba mmoja.

  Fedha ambazo alibaini kulipwa mkandarasi huyo kwa certificate ya kwanza mkandarasi alipaswa kulipwa kiasi cha bilioni 2.4,ya pili mkatandas alilipwa bilioni 2.4 na tatu inaonyesha alilipwa kiasi cha bilioni 2.9 jambo ambalo liliibua sintofahamu wakati wa kikao hicho baada ya kushindwa kupata maelezo halisi.

  “Ndugu zangu haiwezekani mradi mmoja unakua gharama tatu tofauti ambazo zina tofautiana na ndio sababu nimelazimika kuagiza mikataba yote irudi wizara kwenda kuhakikiwa kwa lengo la kuweza kubaini gharama halisi ya mradi “Alisema.Naibu Waziri huyo alisema kutokana na kuwepo kwa dalili za ubadhirifu ndani ya mradi huo wizara haitaweza kutoa fedha katika mradi huo hadi pale wataalamu kutoka wizarani kuufanyia uchunguzi mradi huo .

  Hata hivyo Naibu Waziri huyo alisema wizara itaunda tume ili kuchunguza miradi hiyo ya maji nchi nzima huku akiwataka wahandisi wa maji kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupata maji safi na salama kwenye maeneo yao.

  “Lakini niseme kwamba kama kuna certificate inayotakiwa kulipwa sasa hivi nitawasiliana na katibu mkuu ili malipo hayo yasitishwe hadi uhakiki utakapo kamilika hasa kwa kipindi hiki kifupi ambacho wizara na wataalamu wake wanauhakiki mradi huo”Alisema

  Naye kwa upande wake,Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia alisema anaishukuru serikali kwa kutekeleza miradi kwenye Jimbo lake kutokana na kwamba changamoto ya maji imekuwa kikwazo kikubwa sana kwa wananchi wake.

  Aidha alimuomba Naibu Waziri huyo kuiangalia Jimbo hilo kwa ukaribu zaidi ili kuweza kuwasaidia wananchi waweze kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma ya maji jambo ambalo linawarudisha nyuma kimaendeleo.

  0 0


  Rais wa Uswisi Mhe. Alain Berset akipkelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Jumatano usiku wakati akijiandaa kuondoka kurudi nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake binafsi ambapo alitembelea hifadhi za Taifa na Zanzibar kwa muda wa wiki mbili akiwa pamoja na familia yake.
  Rais wa Uswisi Mhe. Alain Berset akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Jumatano usiku wakati akijiandaa kuondoka kurudi nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake binafsi ambapo alitembelea hifadhi za Taifa na Zanzibar kwa muda wa wiki mbili akiwa pamoja na familia yake. PICHA NA IKULU

  0 0
  Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akimkabidhi tuzo ya kushika nafasi ya kwanza katika utendaji kazi bora wa kutoa huduma kwa wagonjwa kwa Kurugenzi ya Tiba Shirikishi Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Delila Kimambo wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza washindi iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Prof. Mohamed Janabi.
  Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akimkabidhi tuzo ya kushika nafasi ya kwanza katika kuwezesha utendaji kazi bora wa kutoa huduma kwa wagonjwa kwa Kurugenzi ya Uuguzi Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo Robert Mallya wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza washindi iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Prof. Mohamed Janabi.

  Baadhi ya Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) akielezea kuhusu kazi zilizofanywa na Taasisi hiyo kwa mwaka 2018 katika kikao cha wafanyakazi na viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo uliopo Jijini Dar es Salaam. Picha na Brighton James -JKCI

  0 0

  MREMBO atakayeibuka mshindi wa shindano la urembo la Miss Dar  Zone2018 anatarajiwa kupewa zawadi ya kiwanja imeelezwa.

  Akizungumza na waandishi wa habari  mapema leo jijini Dar, Mratibu wa shindano hilo, Khalid Ngulume, alisema kuwa wamekuja kivingine msimu wa shindano la Miss Tanzania 2018 ,kutokana na ujio mpya wa shindano hilo na wao kama kanda wameamua kuweka zawadi ya tofauti.

  "Zawadi hii ya kiwanja tutatoa kwa mshindi wa kwanza na wa pili, lakini kwa mshindi wa kwanza atapata zawadi nyingine tofauti," alisema Ngulume.Aidha, alisema kuwa kwa kufuata taratibu zilizopo, leo mchana wamepeleka  nyaraka za zawadi hizo kwa Barazaa la Sanaa Taifa (Basata) kama kanuni inavyotaka.

  Aidha, alisema katika shindano hilo litakalofanyika Agosti 3 kwenye ukumbi wa Next Door Arena, wasanii Papi Kocha na Nandi wanatarajiwa kutoa burudani."Bado tupo kwenye mazungumzo na wasanii wengine kuona wanatoa burudani, lakini pia kwenye zawadi tutatoa zawadi kwa washiriki wote kama asante kwa kushiriki," alisema Ngulume.

  Alisema warembo wote 27 wanaoshiriki shindano hilo Julai 29 wataingia kambini kujiandaa na shindano hilo.

  Shindano hilo linadhaminiwa na  Manukato ya marcelina.

  Washindi watatu wa shindano hilo watakata tiketi ya kushiriki shindano la taifa la Miss Tanzania.
  Washiriki wa shindano la  urembo la Miss Dar  Zone 2018 ,wapatao 27 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na kilele cha shindano hilo hapo Agosti 3, 2018 jijini Dar
  Pichani kati ni  Mratibu wa shindano hilo, Khalid Ngulume, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar, kuhusu maandalizi ya shindano la Miss Dar zone 2018  linalotarajia kufanyika Agosti 3,katika ukumbi wa Next Door Arena,ambapo wasanii Papi Kocha na Nandi wanatarajiwa kutumbuiza,kulia ni Mmoja wa Wadhamini wa shindano hilo Matilda Marlon kupitia Manukato ya marcelina na kushoto ni Tahia Yusuph. 
  Walimbwenda hao wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0

  NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, atakuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Kwanza la Siku ya Urembo wa Nywele na Ngozi za Asili litakalofanyika Jumamosi wiki hii viwanja vya Makumbusho ya Taifa, Posta, Dar es Salaam.

  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Eagle Business Consultants ya Dar es Salaam, Antu Mandoza, ilieleza kuwa tamasha hilo lina lengo la kuwahamasisha wanawake wa Kiafrika kuthamini urembo wao wa asili na kuachana na tabia ya kuutukuza utamaduni wa kimapokezi wa kubadilisha mwonekano wao.

  Alisema tamasha hilo litakuwa likifanyika kila mwaka na kwamba Julai 28 itakuwa Siku ya Urembo wa Asili kwa kuanzia na Tanzania na baadaye Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

  “Onesho hili linalenga kutoa elimu kwa jamii nzima kuhusu madhara ya kiafya ya kutumia kemikali za aina mbalimbali za urembo wa nywele na uchubuaji ngozi, ili kurejesha ujasiri wa zamani wa mwanawake wa Afrika wa kujiamini na kupenda asili yake,” alisema Mandoza.Alisema alianza kampeni ya urembo wa asili kwa kupitia mitandao ya kijamii kuanzia Machi mwaka huu na amekuwa akitumia utambulisho au hashtag yanaturalhairsioushamba.

  “Kampeni hii iliungwa mkono na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Ummy Mwalimu.“Mwitikio mzuri wa kampeni ya mtandaoni ndio uliofanya kuzaliwa kwa wazo la kuandaa onesho hili maalumu linalotarajiwa liwe mkombozi wa kizazi kijacho cha Afrika kwa baraka za serikali kupitia kwa Naibu Waziri, Shonza.
  “Onesho hili litahudhuriwa na wasanii, wanamitindo na wataalamu mbalimbali akiwemo Dk. Andrew Foi ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya ngozi atakayetoa mada kuelezea madhara ya kutumia kemikali katika urembo na kutoa siri za kuboresha nywele na ngozi kwa kutumia vitu vya asili,” alisema.

  Kwa mujibu wa muandaaji huyo hakutakuwa na kiingilio chochote na wananchi wote wanakaribishwa na kuongeza kuwa kampuni yake pia inamiliki redio ya mtandaoni iitwayo radio7 www.radio7.co.tz ambayo huelimisha pamoja na kuiburudisha jamii.

  0 0


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Paulo Sango alipolitembelea banda la Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano kwenye kabla ya ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi kwenye ukumbi wa Royal Tughimbe mkoani Mbeya leo tarehe 26, Julai 2018.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya Huduma za TTCL kutoka kwa Afisa Huduma kwa Wateja Bi. Niva Frankie Mkwe kabla ya ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi kwenye ukumbi wa Royal Tughimbe mkoani Mbeya leo tarehe 26, Julai 2018. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi kwenye ukumbi wa Royal Tughimbe mkoani Mbeya leo tarehe 26, Julai 2018. (Picha na Ofisi ya Makamu wa  Rais)


  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makala akihutubia wakati wa kuwakaribisha wageni kwenye ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi kwenye ukumbi wa Royal Tughimbe mkoani Mbeya leo tarehe 26, Julai 2018.

   Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makala akizungumza na Waziri wa Viwanda Biashara na Utalii wa Malawi Mhe. Hon Henry Mussa (MB) wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi kwenye ukumbi wa Royal Tughimbe mkoani Mbeya leo tarehe 26, Julai 2018. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makala wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi kwenye ukumbi wa Royal Tughimbe mkoani Mbeya leo tarehe 26, Julai 2018. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati),Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makala (kushoto) pamoja na Waziri wa Viwanda Biashara na Utalii wa Malawi Mhe. Hon Henry Mussa (MB) wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi kwenye ukumbi wa Royal Tughimbe mkoani Mbeya leo tarehe 26, Julai 2018. (Picha na Ofisi ya  Makamu wa Rais)

  0 0

     
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani World Food Programme (WFP) David Beasley zawadi ya Picha moja ya mbuga za wanyama zilizopo nchini pamoja na kinyago cha mpingo mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Michael Dunford mara baada ya mazungumzo na ujumbe huo wa Shirika hilo la kimataifa Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi wa kanda wa (WFP)  Bi. Lola Castro mara baada ya mazungumzo na ujumbe huo wa Shirika hilo la kimatifa Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Michael Dunford pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Agustine Mahiga wakishuhudia. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani World Food Programme (WFP) David Beasley pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Agustine Mahiga mara baada mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani World Food Programme (WFP) David Beasley wanne kutoka (kushoto) Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Agustine Mahiga watatu kutoka kulia, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Omary Mgumba wapili kutoka kulia, Balozi Zuhura Bundala wakwanza kushoto akifatiwa na na Mkurugenzi wa kanda wa (WFP) Bi. Lola Castro pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Michael Dunford watatu kutoka kushoto. PICHA NA IKULU .

  0 0

  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa tatu kushoto) akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Voluntary Services Overseas (VSO), Dkt. Philip Goodwin (wa tano kulia) pale ugeni kutoka Shirika hilo ulipomtembelea leo tarehe 26 Julai 2018 Ofisini kwake Jijini Dodoma
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Voluntary Services Overseas (VSO), Dkt. Philip Goodwin alipomtembelea leo tarehe 26 Julai 2018 Ofisini kwake Jijini Dodoma. 
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Voluntary Services Overseas (VSO), Dkt. Philip Goodwin alipomtembelea leo tarehe 26 Julai 2018 Ofisini kwake Jijini Dodoma. 
  Spika wa Bunge (katikati) na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakimsikiliza Mkuu wa masuala ya Usimamizi wa tafiti na Tathmini kutoka Shirika la Kimataifa ya Voluntary Services Overseas (VSO), Ndg. Innocent Augustino (kushoto) wakati wa kikao kilichokuwa kinaeleza Shughuli Mbali mbali zinazofanywa na Shirika hilo, tukio lililofanyika leo tarehe 26 Julai 2018 Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma.
  Spika wa Bunge (katikati) na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu kutoka Shirika la Kimataifa la Voluntary Services Overseas (VSO), Dkt. Philip Goodwin (kushoto) wakati wa kikao kilichoelezea Shughuli Mbali mbali zinazofanywa na Shirika hilo, tukio lililofanyika leo tarehe 26 Julai 2018 Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma.(PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE) .

  0 0

  Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Shirika la Chain of Hope la nchini Uingereza wakimfanyia upasuaji wa kuziba matundu na kurekebisha mishipa ya moyo ambayo imekaa vibaya mtoto mwenye umri wa miezi mitatu katika kambi maalum ya upasuaji ya siku tano inayoendelea katika Taasisi hiyo. Jumla ya watoto saba wameshafanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri. 
  Kazi ya kumfanyia upasuaji wa kuziba matundu na kurekebisha mishipa ya moyo ambayo imekaa vibaya mtoto mwenye umri wa miezi mitatu ikiendelea.Picha na Brighton James - JKCI

  0 0

  Na Woinde Shizza, Arusha 

  MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru mkoani Arusha Christopher Kazeri amewapongeza walimu wa Shule ya Sekondari Kisimiri kwa kufanikisha kushika nafasi ya pili kitaifa matokeo ya mtihani wa kidato cha sita.

  Nafasi ya kwanza katika matokeo ya mtihani imeshikwa na Shule ya Sekondari Kibaha kati ya shule 543 zilizofanya mtihani huo.Akizungumza leo wakati akitoa pongezi hizo Kazeri amesema walimu wa Shule ya Sekondari Kisimiri kwa jitihada zao wamefanikisha shule hiyo kushika nafasi ya pili kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka huu 2018.

  Pia amewataka walimu hao kuongeza bidii katika ufundishaji ili kupata matokeo mazuri zaidi kwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya mitihani ijayo.Akiwa shuleni hapo pamoja na kutoa pongezi kwa walimu, wazazi na wanafunzi amepata nafasi ya kusikiliza na kutatuo changamoto zinazowakabili walimu kwa lengo la kuleta tija zaidi kwenye taaluma ya Shule hiyo.

  Kwa upande wa Makamu Mkuu wa shule ya Sekondari Kisimiri Mwalimu John Awe amesema kuwa mojawapo ya mbinu zilizotumika kuhakikisha shule hiyo inapata matokeo mazuri illikuwa kutoa mafunzo ya ziada kwa wanafunzi waliokuwa na uwezo mdogo.

  "Hivyo walimu walitenga muda wa ziada kuwafundisha wanafunzi hao ambao wengi wao walifanya vibaya kwenye mtihani wa utamirifu (MOCK) kwa kupata alama sifuri,"amesema.
  Pia amesema walimu wa shule hiyo wana moyo wa kufundisha na kufafanua kwenda darasani ni suala moja na kufundisha kama inavyotakiwa na wanafunzi kuelewa ni jambo jingine .

  Wakati walimu nao walimu wametoa changamoto zinazoikabili shule hiyo ikiwamo ya uhaba wa viti vya walimu 50 na madawati ya wanafunzi 300.Pi walimu hao wamehitaji ufafanuzi wa maslai yao kama watumishi ikiwemo kupanda daraja.Akitoa ufafanuzi wa masuala ya watumishi Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu Grace Mbilinyi amesema kutokana na mchakato wa kuwabaini watumishi hewa na wenye vyeti vya kugushi Serikali ilisitasha upandaji madara kwa watumishi wa umma.

  "Ila kwa sasa maelekezo mbalimbali yanatolewa.Kuhusu malipo ya likizo ni vema walimu mkaweka viambatanisho vyote muhimu vikiwemo vyeti vya watoto vya kuzaliwa na vyeti vya ndoa,"amesema.Aidha katika matokeo haya ya shule ya Sekondari Kisimiri imeonesha kuweka rekodi nzuri ya kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani hiyo ya kidato cha sita.

  "Kwani kwa miaka 3 mfululizo imekuwa kwenye kundi la shule tatu bora kitaifa.Mwaka 2016 ilishika nafasi ya kwanza, mwaka 2017 ikashika nafasi ya tatu na kwa mwaka huu 2018 imeshika nafasi ya pili kitaifa."Kwa watahiniwa wetu 67 kupata daraja la kwanza na la pili ikiwa 51 kati yao wamepata daraja la kwanza na 16 kupata daraja la pili,"amefafanua.

  Imeelezwa matokeo ya Sekondari ya Kisimiri imezidi kuutangaza mkoa wa Arusha wenye shule 31 zenye watahiniwa zaidi ya 30 za Serikali na binafsi.

  0 0

  Na Woinde Shizza,Arusha 

  OFISA Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwalimu Sara Kibwana amesema halmashauri hiyo imeibuka mshindi wa kwanza na wa jumla ngazi ya Mkoa kwenye mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) yaliyofanyika Juni 6 mwaka huu.

  Akizungumza leo wilayani hapa amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Meru imezawadiwa vikombe vitano kutokana na kuwa mshindi wa kwanza kwenye mpira wa miguu wavulana na mpira wa wavu wasichana.Ameongeza pia mpira wa mikono wasichana na mpira wa kengele  pia ilikuwa mshindi wa pili kwenye mchezo wa mpira wa wavu wavulana.

  Kibwana amesema siri ya ushindi huo ni pamoja na maandalizi mazuri yaliyofanyika kwani halmashauri hiyo ilitoa maelekezo zaidi ya miezi 9 iliyopita kwa walimu wakuu wa shule za msingi.Ambapo yalilenga kuhakikisha kila wiki wanafunzi wanakua na siku za kufanya michezo.Pia maandalizi yalikuwa mazuri wakati wa michezo kwani wachezaji walijiandaa kikamilifu kwa kukaa siku tano kambini.

  Wakati huo huo Ofisa Utamaduni wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Senyaeli Pallangyo amesema uchaguzi wa wachezaji umefanyika kwa kuzingatia viwango vilivyofanyika kuanzia ngazi ya chini hadi Wilaya."Ushindi huo mkubwa ikiwa ni pamoja na uwezo wa makocha sambamba na wachezaji kuwa na nidhamu ya hali ya juu na kufuata taratibu za michezo,"amesema .

  Jumla ya wachezaji 25 kutoka timu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Meru na makocha wanne wamechaguliwa kuunda timu ya Mkoa wa Arusha .Imeelezwa kuwa ikumbukwe Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa mwaka huu imekuwa mshindi wa kwanza na wa jumla kwa ngazi ya Mkoa wa Arusha wenye Halmashauri 7.
  Picha ni vikombe ambavyo halmashauri ya meru imevishinda (picha na Woinde Shizza,Arusha0.

  0 0

  Leo, mahakama ya rufaa ya Tanzania, imetoa uamuzi dhidi ya Kampuni ya Yusuf Manji ya ughaibuni ya Golden Globe International Services Ltd na kampuni yake ya hapa nchini ya Quality Group Ltd, katika mgogoro juu ya madai ya Bw. Manji ya kupata hisa katika kampuni ya simu za mkononi ya MIC Tanzania Limited, ambayo inatambulika kibiashara kama Tigo Tanzania. Madai makuu ya Bw. Manji yaliyotokana na amri ya siri ya Mahakama ya kuuza hisa kwa mnada pamoja na taratibu husika za utekelezaji. 

  Mahakama ya Rufaa imetupilia mbali madai hayo kwa sababu ya makosa makubwa yaliyofanyika. Millicom inayofuraha kuwa jaribio hili la kutwaa hisa zake limevunjwa na kwamba uamuzi wa Mahakama ya Rufaa umedhibitisha kuwa MIC Tanzania Limited (Tigo) inabaki kumilikiwa na kuwa chini ya mamlaka ya Millicom Group. 

  Naye msemaji wa Tigo Tanzania alisema: "Tumepokea na kuridhika na uamuzi huu wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania. Mahakama imesema kuwa jaribio la Golden Globe International Services Ltd la kutaka kujipatia hisa za MIC Tanzania Ltd (Tigo) kwa mnada usio halali na bila taarifa yeyote kwa Millicom (Tanzania) NV limeshindikana. 

  Tumejitahidi kupambana na makosa ya wazi na majaribio ya Bw. Manji ya kudhalilisha mfumo wa Mahakama ya Tanzania. Tunakubaliana na uamuzi wa Mahakama, amabayo inasisitiza mchakato wa ufuatiliaji wa sheria nchini Tanzania. 

  Tigo Tanzania ni kati ya watoa huduma wakubwa wa huduma za mawasiliano ya simu Tanzania na tunatarajia kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wetu wengi."

  0 0


  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifuatilia Sokwe Mtu kwenye mapito yao ndani ya Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma.


  Na Hamza Temba-Kigoma

  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla ameagiza wavamizi wote waliopo ndani ya Pori la Akiba Kigosi/Moyowosi na Hifadhi ya Msitu wa Makere mkoani Kigoma waondoke mara moja kupisha maeneo hayo yaendelee kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria.

  Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na uongozi wa mkoa wa Kigoma, ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

  Alisema taarifa za kiitelijensia zinaonyesha kuwa wengi wa wavamizi hao ambao wameanzisha makazi, kilimo na ufugaji ni raia kutoka nchi jirani ambao pia wamekuwa wakijihusisha na uharibifu wa mazingira na vitendo vya ujangili.

  "Haivumiliki kwa kiongozi yeyote mzalendo kwa nchi yake ambaye anajua kabisa maeneo yetu yamewekwa akiba kwa ajili ya uhifadhi na tunawazuia hata wananchi raia kuyatumia alafu wanakuja raia wa nchi nyingine wanaachiwa wafanye wanavyotaka, hapana hili halikubaliki" alisisitiza Dk. Kigwangalla huku akiutaka uongozi wa Mkoa huo usaidie kusimamia Sheria na wavamizi hao waondoke mara moja.

  Aidha, ametoa kipindi cha miezi mitatu kwa watu wote waliovamia maeneo ya kinga za hifadhi (bafa) ambayo ni mita 500 kutoka mpaka wa hifadhi na vijiji waondoke kwa hiari yao wenyewe kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

  Katika hatua nyingine, Waziri Kigwangalla ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Kigoma na Halmashauri husika pamoja na Wakala wa Huduma za Barabara TANROADS katika ujenzi wa barabara inayounganisha Hifadhi ya Taifa ya Gombe na Mkoa huo na maeneo mengine.

  Alisema, Serikali ya awamu ya tano imepanga kufungua Sakiti mpya za utalii ikiwemo ya Kanda ya Magharibi ambayo inaujumuisha mkoa wa Kigoma, hivyo ni lazima miundombinu ya barabara ijengwe na kuimarishwa ipitike muda wote ili hifadhi hizo zitumike zaidi kibiashara na ziweze kuchangia ipasavyo kwenye pato la Taifa kuliko ilivyo hivi sasa.

  Ameuagiza pia uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu TFS kupima maeneo ya misitu ya vijiji jirani na Hifadhi ya Taifa ya Gombe ili kuona uwezekano wa kuyahifadhi kwa kutumia sheria za misitu na hivyo kutengeneza mapito muhimu ya Sokwe Mtu yatakayounganisha Hifadhi ya Taifa ya Gombe na Mahale na hifadhi za Misitu ya Tongwe East, Tongwe West, Masito East na Masito West.

  Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Donatus Bayona alisema changamoto kubwa iliyopo katika hifadhi hiyo ni miundombinu ya barabara ya kuunganisha hifadhi hiyo na maeneo mengine ikiwemo mji wa Kigoma ambapo amesema kwa sasa hifadhi hiyo inafikika kiurahisi kwa kutumia usafiri wa boti.

  Akiwa katika hifadhi hiyo, Waziri Kigwangalla alizindua tukio la kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwa Hifadhi hiyo na kuzindua rasmi kituo cha utafiti wa Sokwe Mtu ambacho kimefadhiliwa na Taasisi ya Jane Goodal, pia alitembelea Maporomoko ya Maji ya Kakombe ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii ndani ya hifadhi hiyo.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa, Muongoza Watalii wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe, Iddi Kaluse kuhusu Maporomoko ya Maji ya Kakombe ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma.

  Baadhi ya Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipanda mlima kwa ajili ya kuwaona Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma.

  Msafara wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ukielekea Hifadhi ya Taifa Gombe kwa kutumia usafiri wa boti.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishuka kwenye boti alipotembelea Hifadhi ya Taifa Gombe wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma jana.

  Mandari ya Hifadhi ya Taifa ya Gombe.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akicheza ngoma na kikundi cha Mwamgongo alipotembelea Hifadhi ya Taifa Gombe wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma jana.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akizindua rasmi kituo cha utafiti wa Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe ambacho kimefadhiliwa na Taasisi ya Jane Goodal, alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake mkoani Kigoma.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akikata keki kama ishara ya kuzindua hafla fupi ya kuadhimisha miaka 50 toka kuanzishwa kwa Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake mkoani Kigoma. Anaeshudia kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu, TANAPA, Nyamakumbati Mafuru na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Donatus Bayona.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa Gombe katika Maporomoko ya Maji ya Kakombe alipotembelea hifadhi hiyo janawakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma jana.

older | 1 | .... | 1630 | 1631 | (Page 1632) | 1633 | 1634 | .... | 1897 | newer