Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU MAJALIWA AMPOKEA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA KOREA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Mheshimiwa Lee Nak-Yon wakati mgeni huyo alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kamabarage Nyerere jijini Dar es salaam kwa ziara ya kikazi ya siku tatu chini Julai 21, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Mheshimiwa Lee Nak- Yon baada ya mgeni huyo kuwasili kwenye  uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam kwa Ziara ya siku tatu nchini, Julai 21, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais wa Jamhuri ya Korea ,Le Nak Yon wakifurahia ngoma kwenye uwanja wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Juilai 21, 2018. (Picha na ofisi a Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempokea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak-yon ambaye amewasili nchini leo saa 12:30 jioni (Jumamosi, Julai 21, 2018) kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Kwenye uwanja wa ndege, Waziri Mkuu huyo wa Jamhuri ya Korea alipokelewa pia na Waziri wa Mambo ya Nje, Dk. Augustine Mahiga, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Isack Kamwele, Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Eng. Stella Manyanya na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Lee Nak-yon anatembelea Tanzania ikiwa ni hatua ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili. Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa ngazi ya juu wa nchi hiyo kufanya ziara ya kiserikali tangu nchi hizo zianzishe mahusiano ya kidiplomasia mwaka 1992.

Pia ameambatana na ujumbe wa maafisa wa Serikali, wabunge na wafanyabiashara wakubwa ambao watashiriki Kongamano la Kibiashara baina ya Korea na Tanzania (Korea-Tanzania Business Forum) lililopangwa kufanyika kesho kutwa (Jumatatu, Julai 23, 2018) kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

Kesho (Jumapili, Julai 22, 2018), Waziri Mkuu Lee Nak Yon atakuwa na mazungumzo rasmi ya kiserikali na mwenyeji wake pamoja na viongozi kadhaa wa Serikali na pia kwa pamoja watashuhudia uwekaji saini mkataba wa kuondoa hitaji la viza kwa watu wenye hati za kusafiria za kidiplomasia na za utumishi (diplomatic and service passports).

Pia ataenda Ikulu kumsalimia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, atatembelea Makumbusho ya Taifa, Hospitali ya Mnazi Mmoja na kituo cha utunzaji taarifa cha NIDA kilichopo Kibaha. 

Anatarajiwa kuondoka nchini Jumatatu jioni, Julai 23, 2018. 


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, JULAI 21, 2018.

NEWS ALERT: RAIS DKT. MAGUFULI AMTEUA ELIUD SANGA KUWA MKURUGENZI MKUU WA PSSSF

WAGOMBEA UDIWANI KATA 30 WAPITA BILA KUPINGWA

$
0
0



Wagombea 30 wa Udiwani katika uchaguzi Mdogo wa kata 77 utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu, wamepita bila kupingwa.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athumani Kihamia amesema kuwa wagombea hao wamepita bila kupingwa baada ya Tume kukutana, kujadili na kuyatolea maamuzi mapingamizi mbalimbali yaliyoweka na wagombea wa udiwani.

Amesema Madiwani wote waliopita bila kupingwa wanatoka Chama cha Mapindizi (CCM) na kuongeza kuwa rufaa zilipokelewa na kujadiliwa kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 44(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, kikisomwa pamoja na Kanuni ya 28(1)(2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015.

“Tume, ilipokea, ilijadili na kufanya maamuzi ya Rufaa 25 ambapo jumla ya wagombea kumi (10) walifanikiwa na hivyo kuendelea na uchaguzi na wagombea 15 rufaa zao hazikufanikiwa na hivyo kutoendelea kuwa wagombea,” amesema Dkt. Kihamia.

Ameongeza kuwa katika kata sabini na saba (77) wanachama 254 kutoka vyama kumi na moja (11) vya siasa walichukua fomu za uteuzi na kwamba jumla ya wanachama 186 sawa na asilimia 73.2 ya waliochukua fomu za uteuzi walizirejesha na kuteuliwa kuwa wagombea ambapo kati yao wagombea 179 sawa na asilimia 96.2 ni wanaume na wagombea 7 sawa na asilimia 3.8 ni wanawake.

“Hadi muda wa mwisho wa uteuzi ulipofika (saa 10.00 jioni siku ya uteuzi) wanachama 68 sawa na asilimia 26.8 ya waliochukua fomu hawakuteuliwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kutorudisha fomu, kurudisha fomu nje ya muda unaokubalika kisheria na fomu kutojazwa ipasavyo,” amesema.

Dkt. Kihamia amefafanua kuwa katika uchaguzi huu mdogo wa madiwani utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu jumla ya vyama kumi na moja (11) vimesimamisha wagombea.

Amewataja Wagombea hao katika Kata kwa kila Chama kuwa ni ACT-Wazalendo Wagombea 17 (sawa na asilimia 22), ADC Wagombea 3 (sawa na asilimia 3.9), CCM Wagombea 77 (sawa na asilimia 100) CHADEMA Wagombea 54 (sawa na asilimia 70), CHAUMMA Wagombea 2 (sawa na asilimia 2.6), CUF Wagombea 17 (sawa na asilimia 22), Demokrasia Makini Wagombea 4 (sawa na asilimia 5.2), NCCR-MAGEUZI Wagombea 6 (sawa na asilimia 8), NRA Wagombea 3 (sawa na asilimia 3.9), SAU Mgombea 1 (sawa na asilimia 1) na UPDP Wagombea 2 (sawa na asilimia 2.6).

Wakati huohuo, Dkt. Kihamia amesema kwamba katika jimbo la Buyungu jumla ya wanachama kumi (10) kutoka vyama kumi (10) vya siasa vya AAFP, ACT-Wazalendo, CCM, CHADEMA, CUF, DP, Demokrasia Makini, NRA, UMD na UPDP walichukua fomu za uteuzi.

“Wanachama wote kutoka vyama hivyo walirejesha fomu na kuteuliwa kuwa wagombea wa Ubunge katika Jimbo hilo, kati yao wanaume ni tisa (9) na mwanamke mmoja (1),” amesema Dkt. Kihamia.

Amevitaka vyama vya siasa na wagombea wao kuzingatia maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2015, wakati wote wa kampeni na siku ya uchaguzi.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KITUO CHA AFYA CHA NANYALA WILAYANI MBOZI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amefungua kituo cha Afya cha Nanyala kilichopo kata ya Nanyala wilayani Mbozi kitakachotoa huduma kwa wakazi zaidi ya elfu kumi ikiwa siku ya pili ya ziara yake ya siku 5 katika mkoa wa Songwe. Pichani kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mh.Chiku Galawa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Muonekano wa jengo la  kituo cha Afya cha Nanyala kilichopo kata ya Nanyala wilayani Mbozi kitakachotoa huduma kwa wakazi zaidi ya elfu kumi
 Jiwe la Msingi lililowekwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (hayupo pichani) alipokuwa akiwahutubia mapema leo mara baada ya kufungua kituo cha Afya cha Nanyala kilichopo kata ya Nanyala wilayani Mbozi kitakachotoa huduma kwa wakazi zaidi ya elfu kumi ikiwa siku ya pili ya ziara yake ya siku 5 katika mkoa wa Songwe.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wananchi  mapema leo mara baada ya kufungua kituo cha Afya cha Nanyala kilichopo kata ya Nanyala wilayani Mbozi kitakachotoa huduma kwa wakazi zaidi ya elfu kumi ikiwa siku ya pili ya ziara yake ya siku 5 katika mkoa wa Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

WAZIRI KIGWANGALLA AAGIZA UJENZI WA VIWANDA VIDOGO VYA ASALI KWA WILAYA ZOTE ZA MIKOA YA TABORA NA KATAVI

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Skonge, Peres Magiri kukagua eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani humo jana. Ameigiza Halmashauri ya wilaya hiyo kukamilisha taratibu za Tathmini ya Athari za Kimazingira (EIA) ili Serikali ifanye uamuzi wa kuendelea au kusitisha mradi huo. Wengine kwenye msafara huo ni Naibu Waziri wa TAMISEMI na Mbunge wa Skonge, Joseph Kakunda (wa nne pichani ).

Na Hamza Temba - Tabora
.............................................................

*Ahamasisha kilimo cha Korosho kama zao mbadala la kuinua uchumi na uhifadhi wa mazingira

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla ameuagiza Mfuko wa Ruzuku wa Misitu Tanzania (TAFF) kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuanzisha mradi wa viwanda vidogo vya kusindika na kufungasha asali katika mikoa ya Tabora na Katavi ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kujenga uchumi wa viwanda.

Ametoa agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mtakuja wilaya ya Skonge mkoani humo ikiwa ni muendelezo wa ziara zake mikoani kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake.

Alisema kwa kiwango kikubwa wananchi wa mikoa hiyo wamekuwa wategemezi kwenye zao moja tu la tumbaku ambalo sio rafiki kwa mazingira kwakuwa miti mingi hukatwa kwa ajili ya kukausha zao hilo jambo ambalo ni muhimu sasa kuwekeza zaidi kwenye mazao mengine ikiwemo viwanda vya kusindika na kufungasha asali ili kuongeza uzalishaji, ubora na hatimaye kuongeza kipato na faida zaidi.

"Mwaka huu ule mfuko wa misitu, kwa kiasi kikubwa tuamue tuwekeze ukanda huu wa magharibi  ambapo kuna zaidi ya asilimia 60 ya misitu yote hapa nchini, na tuanze kwa kujenga kiwanda kimoja katika kila wilaya, ikiwemo Nzega, Skonge, Uyui, Tanganyika, Mlele, Mpanda na Kaliua.

"Tuwawezeshe wananchi wajiunge katika vikundi, tuwagawie mizinga ya kisasa, wafuge nyuki kisasa, warine asali kisasa, wakisharina wapeleke kwenye viwanda, ifungashwe kisasa, ipate bei kubwa, na mwisho wa siku wataona faida ya kuwa na misitu.

"Hapo tutakuwa tumewasaidia, watapa kipato mbadala lakini watakua wakali sana kwa watu wanaoharibu misitu na tutatengeneza jeshi kubwa la wananchi la ulinzi wa misitu yetu, hivyo nataka mradi huu uanze mara moja bila kusuasua ili na sisi tuchangie jitihada za Serikali ya awamu ya tano katika ujenzi wa uchumi wa viwanda. " alisema Dk. Kigwangalla.

Wakati huo huo, Waziri Kigwangalla amewashauri wananchi wa mikoa hiyo kuanzisha kilimo cha korosho kama zao jingine mbadala la kuongeza kipato na kunusuru misitu badala ya kujikita kwenye zao moja la tumbaku ambalo ni chanzo kikubwa cha uharibifu wa misitu ya mikoa hiyo.

Amesema ni muhimu walau kwa kila kaya moja kuanza kwa kupanda ekari moja ya mikorosho ili kuongeza zao jingine mbadala la biashara ambalo lina tija zaidi kiuchumi na kiuhifadhi wa mazingira. 

"Kilimo cha tumbaku sio rafiki kwa mazingira tumejaribu kuleta mabani banifu yanayotumia kuni chache,  tumejaribu kuwashawishi wananchi wapande miti lakini tumechemsha, miti mingi imeendelea kukatwa misitu nayo inateketea siku hadi siku, ni lazima tutafute mbinu mbadala ya kukabiliana na changamoto hii, na hii ni kupitia zao hili la korosho" alisema Dk. Kigwangalla.

Amesema tafiti zinaonyesha kuwa zao la korosho katika mikoa hiyo lina uwezo wa kustawi zaidi na kuzalisha mara mbili kuliko mikoa ya kusini ambayo inasifika zaidi kwa uzalishaji huo hapa nchini.

Aidha ameziagiza halmashauri zote za mikoa hiyo kufanya utaratibu wa kupata mbegu na miche ya zao hilo mapema iwezekanavyo kwa ajili ya kuwagawia wananchi kabla ya msimu wa mvua kuanza na wataalamu wa kilimo wawaelimishe wananchi njia bora ya kupanda na kutunza miche hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Skonge, Peres Magiri alisema kiwango cha mvua kwa mwaka katika wilaya hiyo kimeshuka na kufikia 600mm kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu wa mazingira. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Skonge, Peres Magiri kukagua eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani humo jana. Ameigiza Halmashauri ya wilaya hiyo kukamilisha taratibu za Tathmini ya Athari za Kimazingira (EIA) ili Serikali ifanye uamuzi wa kuendelea au kusitisha mradi huo. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa TAMISEMI na Mbunge wa Skonge, Joseph Kakunda (wa nne).
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akipiga jaramba alipokuwa akikagua  eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani Skonge jana. Anayefuata ni Naibu Waziri TAMISEMI na Mbunge wa Skonge, Joseph Kakunda, Mkuu wa Wilaya ya Skonge, Peres Magiri na viongozi wengine wa wilaya hiyo. Ameiagiza Halmashauri ya wilaya hiyo kukamilisha taratibu za Tathmini ya Athari za Kimazingira ili Serikali ifanye uamuzi wa kuendelea au kusitisha mradi huo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akipiga jaramba alipokuwa akikagua  eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani Skonge jana. Kulia ni Naibu Waziri TAMISEMI na Mbunge wa Skonge, Joseph Kakunda. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akiongoza kupiga jaramba alipokuwa akikagua  eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani Skonge jana. Wengine pichani ni Naibu Waziri TAMISEMI na Mbunge wa Skonge, Joseph Kakunda (Nyuma Katikati). Ameiagiza Halmashauri ya wilaya hiyo kukamilisha taratibu za Tathmini ya Athari za Kimazingira ili Serikali ifanye uamuzi wa kuendelea au kusitisha mradi huo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani humo jana. Kulia kwake Mkuu wa Wilaya ya Skonge, Peres Magiri na Naibu Waziri TAMISEMI na Mbunge wa Skonge, Joseph Kakunda (wa pili kulia). Ameigiza Halmashauri ya wilaya hiyo kukamilisha taratibu za Tathmini ya Athari za Kimazingira ili Serikali ifanye uamuzi wa kuendelea au kusitisha mradi huo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani humo jana. Anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Skonge, Peres Magiri, Kaimu Mkurugenzi Mkuu TAWA, Mabula Misungwi, Naibu Waziri TAMISEMI na Mbunge wa Skonge, Joseph Kakunda na viongozi wengine wa wilaya hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani humo jana. Anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Skonge, Peres Magiri, Kaimu Mkurugenzi Mkuu TAWA, Mabula Misungwi, Naibu Waziri TAMISEMI na Mbunge wa Skonge, Joseph Kakunda na viongozi wengine wa wilaya hiyo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akizungumza na uongozi wa wilaya ya Skonge wakati wa ziara yake wilayani humo jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mtakuja katika wilaya ya Skonge mkoani Tabora baada ya kukagua eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani humo jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mtakuja katika wilaya ya Skonge mkoani Tabora baada ya kukagua eneo la mradi wa umwagiliaji wa Ulua ambao ulijengwa kimakosa ndani ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ipembampazi wakati wa ziara yake wilayani humo jana.

DKT MWIGULU NCHEMBA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA JIMBONI KWAKE,ACHANGIA BATI 200

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi mkoa wa Singida Dkt Mwigulu Nchemba akikagua ujenzi wa kituo cha Afya cha kata ya kinampanda kinachojengwa kwa nguvu za wananchi wakishirikiana na Mbunge pamoja na serikali kuu, kituo hicho ni cha kwanza tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika. 
Mbunge wa jimbo la Iramba magharibi mkoa wa Singida Dkt Mwigulu Nchemba akikabidhi Bati 200 kwa wananchi kwa ajili ya kuezekea majengo ya kituo cha afya cha kinampanda .
Mbunge wa jimbo la Iramba magharibi mkoa wa Singida Dkt Mwigulu Nchemba akiwahutubia Wananchi wa kata ya Kinampanda kutoa taarifa ya ulipofikia ujenzi wa kituo cha afya ambacho kilikua ni moja ya ahadi zake akiomba ridhaa ya kuongoza jimbo hilo.

ZEE MKAPA, DKT. BILAL, JAJI RAMADHAN WATOA POLE KWA RAIS MSTAAFU DKT KIKWETE KWA KUFIWA NA BABA MKWE WAKE, MAREHEMU MZEE RASHID MKWACHU

$
0
0
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamini Mkapa alipowasili nyumbani kwake Msasani, jijini Dar es salaam leo kuhani msiba wa Baba Mzazi wa Mama Salma Kikwete, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimaiana na Mke wa Mh. Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa walipowasili nyumbani kwake Msasani, jijini Dar es salaam leo kuhani msiba wa Baba Mzazi wa Mama Salma Kikwete, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu.
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamini Mkapa akisalimiana na Mke wa Mh. Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete wakati alipofika kuhani Msiba wa Baba yake, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu uliotokea hivi karibuni. Mh. Mkapa aliambatana na Mkewe Mama Anna Mkapa. Kulia ni Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
 Mama Anna Mkapa akimfariji Mama Salma Kikwete.  
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwaeleza jambo Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamini Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa, wakati walipofika nyumbani kwake, Msasani jijini Dar es salaam leo kuhani msiba wa Baba Mzazi wa Mama Salma Kikwete, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu.
 Rais Mstaafu Mh. Benjamini Mkapa pamoja na Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakifurahi jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Kangi Lugola wakati walipokutana nyumbani kwa Mh. Kikwete, Msasani jijini Dar es salaam leo kuhani msiba wa  Baba Mzazi wa Mama Salma Kikwete, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Kangi Lugola akitoa pole ya msiba kwa Mama Salma Kikwete, aliyefiwa na Baba yake Marehemu Mzee Rashid Mkwachu. 
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Makamu Wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohamed Gharib Bilal alipowasili nyumbani kwake Msasani, jijini Dar es salaam leo kuhani msiba wa Baba Mzazi wa Mama Salma Kikwete, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu.
 Makamu Wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akimpa pole Mama Salma Kikwete, kwa kufiwa na Baba yake Marehemu Mzee Rashid Mkwachu. Dkt. Bilal aliambatana na Wake zake, Mama Zakhia na Mama Asha Bilal.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimueleza jambo Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal na Wake zake, Mama Zakhia na Mama Asha Bilal, walipofika nyumbani kwake, Msasani jijini Dar es salaam leo kuhani msiba wa Baba Mzazi wa Mama Salma Kikwete, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu.
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal na Wake zake, Mama Zakhia na Mama Asha Bilal pamoja na baadhi ya watoto wao. 

Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha nyumbani kwake, Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhan wakati alipofika kuhani msiba wa  Baba Mzazi wa Mama Salma Kikwete, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu.

Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhan akimpa pole Mama Salma Kikwete, kwa kufiwa na Baba yake Marehemu Mzee Rashid Mkwachu. 
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimueleza jambo Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhan akimpa pole Mama Salma Kikwete, kwa kufiwa na Baba yake Marehemu Mzee Rashid Mkwachu.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kushoto) akimkabidhi Mke wa Rais Mstaafu, Mama Salma Kikwete Rambirambi iliyotolewa na Wabunge kufuatia kufiwa na Baba yake, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu. kushoto ni Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia. Naibu Waziri Mgalu aliambatana na Mh. Hawa Ghasia


Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiutambulisha ujumbe wa Africa-America Institute (AAI)  ukiongozwa na Mwenyekiti wake wa Bodi, Stephen Pfeifer pamoja na Mariam Sow uliofika nyumbani kwake kumpa pole kwa kufiwa na Baba Mzazi wa Mke wake, Mama Salma Kikwte, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu.

Tanzania inayo fursa kubwa kunufaika na utalii wa ndani na Afrika

$
0
0
Na Jumia Travel Tanzania

Msimu wa majira ya joto au ‘Summer Season’ kama unavyojulikana kwa nchi za Ulaya na Marekani huwa ni kipindi cha mapumziko miongoni mwa watu wengi. Mapumziko haya si hufanywa tu na watu wa kawaida kutokea nchi hizo bali pia watu mashuhuri kama vile wacheza soka, wanamuziki, wafanyabiashara na wanasiasa. 

Sababu kubwa zinazopelekea watu wa mataifa hayo kuchukua muda wa likizo ni kutokana na kipindi hiki kuwa na hali ya hewa nzuri. Kipindi kirefu cha mwaka kwenye maeneo yao hutawaliwa na baridi kali pamoja na barafu katika maeneo mengi.

Matokeo ya hali hii ni nchi tofauti zenye vivutio vya kitalii kunufaika kwa kiasi kikubwa kwani hupokea maelfu ya watalii. Miongoni mwa sehemu zinazotembelewa kwa kiasi kikubwa ni pamoja na Afrika, Tanzania ikiwemo. 
Kwa mfano hivi karibuni tumeshuhudia watu mashuhuri kama vile Rais aliyepita wa Marekani, Barack Obama na familia yake wakitembelea Hifadhi  ya Mbuga ya Serengeti kwa muda wa takribani wiki nzima. Naye, Rais wa sasa wa nchi ya Uswizi, Mh. Alain Berset aliyeingia Tanzania na kutarajiwa kutumia siku 15 kutalii vivutio kadhaa kama vile Serengeti, Tarangire, Manyara, Ngorongoro na Zanzibar. 

Pia tumeshuhudia mchezaji wa timu ya Taifa ya Hispania na klabu ya Atletico Madrid, Koke akiwa amekuja kupumzika na familia yake katika mbuga ya Serengeti mara baada ya timu yake kuondolewa katika michuano ya Kombe la Dunia.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zinazohusu masuala ya utalii, visiwa vya Zanzibar, Mlima Kilimanjaro, mbuga ya Serengeti na hifadhi ya bonde la Ngorongoro ni miongoni mwa vivutio vilivyopo kwenye orodha ya watalii wengi duniani.
Akizungumzia juu ya sababu zinazopelekea kukua kwa utalii wa ndani ya nchi pamoja na bara la Afrika, Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Travel Tanzania, Bw. Kijanga Geofrey amebainisha kuwa kujitangaza ndani na kimataifa, gharama nafuu za malazi na usafiri pamoja na uboreshwaji wa miundo mbinu ya usafiri ni vichocheo vikubwa.

“Tumeshuhudia taasisi zilizopewa mamlaka na serikali zikishiriki maonyesho ya kimataifa ya utalii ndani na nje ya nchi. Hii hutoa fursa kwa watalii na wadau wa sekta kujua vivutio vilivyopo na taratibu za kuvitembelea. Lakini maboresho katika sekta za usafiri hususani wa anga ambao ndio hutumiwa na asilimia kubwa ya watalii duniani umeleta chachu nchini,” alisema Bw. Geofrey.

Tanzania imekuwa ni kitovu cha utalii wa ndani ya Afrika ambapo hupokea watalii wengi kutokea nchi za Afrika ya Kusini, Nigeria na Kenya. Nchi hizi ambazo zina idadi kubwa ya watu barani Afrika na uchumi mzuri ni fursa kubwa ya kimasoko endapo zitatumiwa vizuri kutangaza vivutio vilivyopo.

Ukiachana na nchi hizo, China ni taifa lingine ambalo ni muhimu katika ukuaji wa sekta ya utalii Afrika. Takwimu zinaonyesha kuwa 10% ya wachina wanaosafiri duniani huja kutalii barani Afrika na miongoni mwa nchi tano ambazo hutembelewa zaidi ni Afrika ya Kusini, Morocco, Misri, Tanzania na Kenya. 

“Jumia Travel inajitahidi kuhakikisha kuwa inakuza shughuli za kitalii. Kwa kutumia teknolojia iliyonayo hurahisisha huduma za malazi, usafiri pamoja na kuyatangaza vema maeneo mbalimbali. Katika shughuli za kitalii gharama za malazi huwa changamoto ukilinganisha na usafiri,” aliongezea Meneja Uhusiano wa Jumia Travel nchini na kumalizia, “hivyo basi tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kuwa na huduma nafuu za malazi ambazo kila mtu anaweza kuzimudu. Lakini pia kuvitangaza sambamba vivutio vinavyopatikana katika maeneo hayo huku tukiwawezesha watalii kuzifikia huduma zetu mahali popote na muda wowote.” 

Ukuaji wa teknolojia katika sekta ya utalii na kuongezeka kwa mawakala wa  kitalii navyo vina mchango mkubwa kwa ujumla. Teknolojia imerahisisha watalii kuweza kufahamu vivutio mbalimbali vilivyopo nchini pamoja na namna ya kuvifikia. Kwa mfano, kupitia mtandao kama Jumia Travel, mtalii anaweza kufanya huduma ya malazi katika eneo analotaka kutalii na usafiri wa ndege akiwa mahali popote duniani. 
Hata hivyo, mawakala wa usafiri na utalii nao wamesaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha huduma za usafiri pamoja na kutangaza vivutio vya nchini. Hoteli nyingi za kitalii zipo kwenye maeneo ambayo watalii ni vigumu kuzifikia. Kwa kupitia mawakala wa utalii na usafiri usafiri huwa ni rahisi.

PASS NA TALIRI WAJIPANGA KUONGEZA BIDHAA YA NYAMA KATIKA JIJI LA DODOMA

$
0
0
Meneja wa Kituo cha Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Kongwa Dodoma,Wilfredy Munisi akizungumza wakati wa utamburisho wa wagei waliofika katika kituo hicho kwa ajili ya hafla fupi ya utiaji saini katika makubaliano kati ya TALIRI na Taasisi Binafsi ya kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ( PASS) ya kusaidia Wajasiliamali Vijana katika sekta ya Mifugo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ,Nocomed Bohay (katikati) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini kati ya Taasisi hiyo na TALIRI ya kusaidia Wajasiliamali vijana.Kulia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Ubunifu katika Kilimo Biashara ,Tamim Amijee na kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Dkt Jonas Kizima.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ,Nocomed Bohay pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Dkt Jonas Kizima wasaini Makubaliano kati ya Taasisi hizo mbili kusaidia Wajasiliamali vijana katika sekta ya Mifugo .Kulia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Ubunifu katika Kilimo Biashara ,Tamim Amijee na kushoto ni Meneja wa Kituo cha Utafiti wa Mifugo Kongwa,Wilfredy Munisi.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ,Nocomed Bohay pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Dkt Jonas Kizima wasaini Makubaliano kati ya Taasisi hizo mbili kusaidia Wajasiliamali vijana katika sekta ya Mifugo .
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ,Nocomed Bohay wakibadilishana faili na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Dkt Jonas Kizima zenye Makubaliano kati ya Taasisi hizo mbili kusaidia Wajasiliamali vijana katika sekta ya Mifugo .
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ,Nocomed Bohay pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Dkt Jonas Kizima wakionesha kwa wanahabari(hawako pichani) Makubaliano kati ya Taasisi hizo mbili kusaidia Wajasiliamali vijana katika sekta ya Mifugo .
Sehemu ya Mifugo (Mbuzi) inayofugwa katika kituo cha Utafiti wa Mifugo Kongwa.
PASS imejipanga kusaidia katika uwekezaji wa miundombinu ya ufugaji wa Mbuzi yakiwemo Mabanda ya Kisasa.
Mbuzi wakitoka katika Mabanda yao.
Ng'ombe wakiwa katika kituo cha utafiti wa Mifugo -Kongwa.
Mmoja wa watumshi katika kituo cha Utafiti wa Mifugo Kongwa akimlambisha Ndama vidole vyake .
Sehemu ya Mabanda ya mbuzi yaliyopo katika kituo hicho.



Na Dixon Busagaga ,Dodoma.

TAASISI ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) imetumia fursa ya mkoa wa Dodoma kuwa makao makuu ya nchi kuingia mashirikiano na Taasisi Binafsi ya kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ( PASS) ya kuwekeza katika sekta ya Mifugo kwa kuwaandaa Wajasiliamali vijana.

Hatua hiyo inatajwa kuondoa moja ya changamoto ya upatikanaji wa bidhaa ya Nyama katika jiji la Dodoma ambalo kwa sasa idadi ya watu imeanza kuongezeka baada ya ofisi na taasisi mbaimbali za serikali na umma kuhamia Dodoma.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini makubalinao hayo iliyofanyika katika kituo cha Kongwa Dodoma ,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Binafsi ya kusaidia Sekta ya Kilimo Nchini(PASS) ,Nicomed Bohay alisema PASS kupitia kituo cha ubnifu wa Biasharaza Kilimo wameamua kuanzisha Vituo atamizi vya Mifugo katika kituo cha TALIRI Kongwa .

“Tumelenga kuanza na mifugo aina ya Mbuzi katika kituo hiki ,zipo sababu zilizotupelekea tuweze kuchagua eneo hili la Kongwa moja wapo ni uwep wa soko la karibu ,… PASS tutawekeza kwenye Miundo mbinu ya ufugaji wa Mbuzi ,pamoja na gharama za kuendesha mradi na malisho hadi mbuzi watakapo weza kuuzwa sokoni .”alisema Bohay .

Alisema kazi hiyo itafanyika kwa kutumia wajasiliamali Vijana wa Kitanzania na kwamba utaratibu wa kuwapata vijana wenye sifa utatangazwa baadae na watakao pata nafasi hiyo watapata nafasi ya kuunganishwa na taasisi za kifedha kwa ajili ya kupata mitaji.

“Kwa kuanza tumelenga kuanza na Unit 10 za mbuzi 100 ,kifupi tumepanga kuanza na Mbuzi 1000 kwa mwaka huu ,nia yetu ni kwamba kutakuwa na Wajasiliamali vijana kama 20,ambao kila mmoja atakuwa na Mbuzi kama 50,na tutaongeza mbuzi 1000 kila mwaka hadi kufikia Mbuzi 5000 ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo.”alisema Bohay.

Bohay alisema kwa kuanzia PASS imetenga kiasi cha sh Mil 500,katika uwekezaji huo wa mwanzo kwa mifugo ya Mbuzi kutokana na uwepo wa gharama kubwa katika ujenzi wa miundombinu yakiwemo Mabanda ya kisasa.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo,Dkt Jonas Kizima alisema ujio wa PASS ni fursa muhimu kwa TALIRI kutumia utaalmau wa tafiti ili uweze kutumika na Wajasiliamali katika sekta ya Mifugo nchini.

“Kituo cha utafiti wa Mifugo ( TARIRI) kimesaini mkataba wa maelewano kwa ajili ya kuandaa wajasiliamali katika sekta ya mifugo ,kwetu sisi ni furaha inaipa nafasi sasa TALIRI ule ujuzi iliyonao ,zile Product ilizonazo ziweze kwenda sasa kwa wadau wengine kibiashara .”alisema Dkt Kizima.

Dkt Kizima aliyataja maeneo hayo kuwa sasa Taasisi hiyo ya serikali ambayo imejikita kwenye sekta ya mifugo itakuwa ni shamba darasa la kuwaandaa wajasiliamali ambao sasa watapata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali yanayotolewa na TALIRI.

Alisema jambo jingine TALIRI itatoa Mbegu kwa ajili ya Malisho ya Mifugo na kwamba ujuzi utakaotolewa kwa wajasiliamali hao kwa kushirikiana na Taasisi ya PASS utasaidia upatikanaji wa Wajasiliamali Wasomi katika sekta ya Mifugo.

“Kitu kingine taasisi ya utafiti wa mifugo (TALIRI) itapata nafasi ya kuzitumia hizi takwimu za wajasiliamli kusambaza kwa wajasiliamli wengine nchini ili wazitumie waone wanaweza kufuga kibiashara kukuza uchumi wa nchi yetu,”alisema Dkt Kizima.

Taasisi ya utafiti wa Mifugo (TALIRI)ina vituo saba vilivyotengwa kikanda ambavyo ni TALIRI Kongwa-Dodoma ,TALIRI West Kilimanjaro,TALIRI Tanga ,TALIRI Naliendere Mtwara ,TALIRI Uyole-Mbeya,TARILI Mpwapwa na TALIRI Mabuki ,Mwanza .

WANANCHI WA BUZA WAISHUKURU SERIKALI

$
0
0
Wananchi wa eneo la Buza katika Manispaa ya Temeke Jijini Dar es salaam wameishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa ujenzi wa kituo cha afya Buza. 

Shukrani hizo wamezitoa leo wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo alipofanya ziara ya kushtukiza kituoni akiwa safarini kuelekea wilayani Kibaha kukagua miradi ya maendeleo. 

Alipofika kituoni hapo, Waziri huyo alikutana na umati wa kinamama na watoto wakisubiri kupata huduma katika Majengo yenye changamoto kubwa. Akizungumza na wananchi na wagonjwa waliokuwepo Kituoni hapo, Waziri Jafo amesema ameamua kufanya ziara hiyo ili kujionea hali halisi ya wananchi hao wanavyopata huduma ya afya. 

“Serikali inatambua changamoto zinazowakabili lakini nimeleta habari njema kwenu kuwa serikali itakiboresha kituo hicho ili kuondoa kero zinazowakabili,”amesema.Ameeleza kuwa kituo hicho kitajengewa jengo la upasuaji, wodi, maabara, jengo la wagonjwa wa nje ikijumuisha vyumba vya madaktari pamoja na jengo la X-Ray na mradi unaotarajiwa kugharimu zaidi ya sh.Bilioni moja.

Kufuatia hali hiyo, Wananchi hao wameishukuru serikali kwa kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili na kwamba uboreshaji huo utawawezesha waweze kupata huduma bora za afya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akizungumza na wananchi alipokuwa akikagua utoaji wa huduma katika zahanati ya Buza.
Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo(hayupo pichani) alipofanya ziara ya kukagua utoaji wa huduma katika zahanati ya Buza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akizungumza na wananchi alipokuwa akikagua utoaji wa huduma katika zahanati ya Buza.
Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo(hayupo pichani).
Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo(hayupo pichani) alipofanya ziara ya kukagua utoaji wa huduma katika zahanati ya Buza.
Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo(hayupo pichani) alipofanya ziara ya kukagua utoaji wa huduma katika zahanati ya Buza.

MWENGE WA UHURU WAINGIA GAIRO NA KUZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA MILIONI MIASABA NA ZAIDII

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Mchembe akipokea Mwenge kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Morogoro Regina Chonjo mara ulipofika katika eneo la Makabidhiano mpakani kati ya Morogoro na Gairo ambapo mwenge huo umekimbizwa kwa Kilometa 72 katika Wilaya ya Gairo.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018 Charles Kabeho akiweka udongo wenye Saruji pembeni ya tofali wakati aliposhiriki ujenzi wa shule mpya ya sekondari iliyopo Wilayani Gairo kama Sehemu ya Miradi iliyotembelewa na Mwenge.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018 Charles na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Sirile Mchembe wakipiga makofi mara bada ya kuweka jiwe la kwenye Majengo Matano Mapya yanayojengwa katika Hospitali ya Gairo.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018 Charles Kabeho akizungumza na Wakazi w Gairo mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Majengo Matano ya Hospitali ya Gairo.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018 Charles Kabeho akimshikisha Mwenge Mmoja ya Wazee waliofika Kushuhudia Mwenge ukikimbizwa Wilayanai Gairo
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018 Charles Kabeho akikagua moja ya Bidhaa zilizotengezwa kwenye Viwanda Vidogo vya Wajasiliamali wa Wilaya ya Gairo.
 Mkuu wa Polisi Wilaya ya Gairo Akiwa ameshika Mwenge mara baada ya kuupokea kwa mkimbiza Mwenge Msaidizi Issa Mohamed
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018 Charles Kabeho akipokea Risala ya Utii kwa Rais kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Mchembe mara baada ya kumalizwa kuosomwa na katibu Tawala wa Wilaya.

PROGRAMU YA 'UNI LIFE CAMPUS' YAFANIKISHA NDOTO ZA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU TANZANIA

$
0
0
  Mwanzilishi wa programu ya 'Uni Life Campus' Mbunge wa Viti Maalum Mheshimiwa Esther Mmasi ambaye anawakilisha Vyuo Vikuu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na wanafunzi wa vyuo mbali mbali vya Tanzania wakati wa semina elekezi juu ya kuzitunza fursa wanazozipata katika maisha yao ikiwa ni pamoja na kupatiwa nafasi za kufanya mafunzo kwa vitendo (field) katika taasisi mbali mbali za serikali na mashirika binafsi mwishoni mwa wiki iliyopita katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dar es Salaam. Picha zote na Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.   Mkurugenzi DM Saikolojia Limited Bw. Dosi Said Dosi akitoa neno kwa wanafunzi wanaotarajia kuanza mafunzo yao kwa vitendo (field) wakati wa semina elekezi juu ya kuzitunza fursa wanazozipata katika maisha yao katika taasisi mbali mbali za serikali na mashirika binafsi mwishoni mwa wiki iliyopita katika Chuo cha CBE jijini Dar es Salaam..  Meza kuu wakifuatilia kwa makini. 


Mmoja ya maofisa katika Programu ya 'Uni Life Campus' Gladness akitoa maelezo machache kwa wanafunzi.


Rais wa Wanafunzi, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Said Hamisi Suba akitoa shukrani zake. 


Mratibu wa Programu ya 'Uni Life Campus' Elibariki Abel akitoa muongozo wa masuala mbali mbali kwa wanafunzi. 


Mwanafunzi Agustino wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) akiuliza swali...  Mwanafunzi Abdulatif wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dar es Salaam akiuliza swali. 


Mhe. Esther Mmasi (katikati mwenye miwani) akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa vyuo mbali mbali waliohudhuria katika semina elekezi mara baada ya kupatiwa nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo (field) katika taasisi mbali mbali za serikali na mashirika binafsi mwishoni mwa wiki iliyopita Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dar es Salaam.



Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

Wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania waaswa kuzilinda na kuzitunza fursa wanazozipata ili ziweze kuwaletea maendeleo endelevu katika maisha yao. Hayo yamesemwa na Mwanzilishi wa programu ya 'Uni Life Campus' Mbunge wa Viti Maalum Mheshimiwa Esther Mmasi ambaye anawakilisha Vyuo Vikuu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita katika semina elekezi ya kuwaasa wanafunzi waliopata nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo (field) katika tasisi mbali mbali za serikali na mashirika binafsi.

"Nawaomba sana wanavyuo wenzangu huko mnapokwenda mkawe mabalozi wema, mzingatie kuwa watiifu na muwe na moyo wa kujifunza huku mkifanya kazi kwa bidii hapo mnaweza kupata maarifa mapya," amesema Mhe. Esther Mmasi. Amesema kuwa tatizo la vijana wengi kwa sasa wamekuwa ni wakaidi na wanaoendeleza uvivu huku simu ikiwa ni kikwazo kikubwa pindi wanapofanya kazi. 

"Mkienda kwenye mafunzo kwa vitendo (field) mzingatie kufanya kazi na si kushinda unachezea simu maana wengi wenu kutwa kucha ni kuchat tu unasahau hata kilichowapeleka katika ofisi za watu, nangoja ripoti njema zitakazowajenga mbeleni" Amesema. 

Aidha amesema kuwa mpka sasa Programu ya 'Uni Life Campus' imewatafutia nafasi za mafunzo kwa vitendo (field) wanafunzi wapatao 100 waliokuwa wameomba kutoka vyuo mbali mbali Tanzania na watakwenda Shirika la Taifa la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Benki ya NMB na Benki ya Posta Tanzania (TPB). 

"Tunamshukuru Mungu tumeweza kuwatolea changamoto wanafunzi hasa waliokuwa wakiomba mafunzo kwa vitendo, tulipotangaza mwaka jana mwishoni zaidi ya vijana 1,900 waliweza kuomba ila tumeweza wapatia nafasi 100 ambao tulizipata licha ya kuendelea kuongea na taasisi mbali mbali za serikali ambazo zimetuahidi kutupatia nafasi zaidi ya 600," amesema. 

Kwa upande wake Mkurugenzi DM Saikolojia Limited Bw. Dosi Said Dosi aliwaasa wanafunzi hao kufuata kile kitakachokuwa kimewapeleka na kuacha kujirahisisha na kujikuta wakitumika. "Unajua unaweza kwenda kwenye maofisi lakini kama hautakuwa na msimamo utaishia kuwa mpira wa kona ambao kila mtu anaweza kupiga na kufunga goli, niwaombe sana mkawe mabalozi wema wa programu ya 'Uni Life Campus' ili mrudi na matokeo chanya yatakayowaweshesha mbeleni kupata kazi kwa urahisi. Kumbukeni huko mnaenda kufungua milango yenu ya mafanikio," amesema Bw. Dosi.

Nae mwanafunzi Agustino wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) aliyepatiwa nafasi ya kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo alimshukuru Mhe. Esther Mmasi kwa kuweza kupata maono ya kuanzisha programu ya 'Uni Life Campus' ambayo imekuwa chachu ya kuwafungulia milango ya kupata mafunzo kwa vitendo bila ya kupiga hoi mlango kwa mlango katika makampuni. 

"Binafsi nilikuwa siamini programu ya 'Uni Life Campus' kama inaweza kufanikisha hiki ilichokifanya leo maana jambo ambalo limekuwa ni msalaba kwa wanafunzi wengi ni suala la uataji wa nafasi za kufanya kazi kwa vitendo (field), ila kwa sasa limefanikishwa kilahisi sana, niwashukuru sana kwa moyo wao huo maana tumeweza kupata bila hata ya kutoa hela yeyote," amesema Mwanafunzi Agustino. 

Programu ya 'Uni Life Campus' imeanzishwa ili kuweza kuwaongezea wanafunzi wa Vyuo Vikuu kiwango cha kujitambua kwa wanafunzi ili kupunguza changamoto wanazokabiliana nazo wakiwa vyuoni.

WAZIRI MKUU KUANZA ZIARA YA SIKU NNE MKOANI KIGOMA

$
0
0
Na Editha Karlo,Kigoma

WAZIRI Mkuu Kasimu  Majaliwa anatarajia kuanza ziara yake ya kikazi siku nne Mkoani Kigoma ambapo atatembelea Wilaya nne.

Akizungumza na Waandishi wa habari jana (leo) ofisini kwake  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia mstaafu Emanuel  Maganga juu ya ziara hiyo, alisema  ugeni wa Waziri Mkuu ambae ataambatana na Waziri wa Kilimo, Naibu waziri wa madini na Naibu Waziri wa Tamisemi watawasili Mkoani humo Julai 28,2018 saa nne asubuhi. 

Alisema ziara hiyo  imelenga Kuamsha hali na Muendelezo wa zao la mchikichi Kwa wakulima na wawekezaji wa zao hilo Mkoani Kigoma kwakuwa  mafuta yanachukua nafasi ya pili katika Kuingiza fedha za kigeni  na hivyo wakulima wakiongeza tija ya uzalishaji zao hilo litawainua.

"Waziri Mkuu  atawasili Mkoani Kwetu siku ya Jumamosi,na atatembelea Wilaya nne za Kigoma , Kasulu , Uvinza na Buhigwe katika ziara hiyo  itahusisha Kikao cha ndani na Viongozi wa Mkoa kufanya mkutano wa wadau wa zao la michikichi na  atatembelea wakulima wa Michikichi na kahawa ambapo atasikiliza kero za wakulima na kubadilishana nao mawazo", alisema Brigedia Jenerali Maganga .

Alieleza kuwa serikali imejipanga kuinua zao la mchikichi na kuwataka wamiliki wote wa mashamba ya michikichi ambayo hayatumiki  wayarudishe iliwaweze kupatiwa watu ambao wanaweza kuwekeza na kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Aidha Maganga aliwaomba Wananchi kujitokeza kwa Wingi katika mikutano  atakayo ifanya na kutoa kero zao kwa kufuata utaratibu na kuwasilisha mambo yote ambayo yameshindwa kutatuliwa na Viongozi wa  wilaya na Mkoa  waziwasilishe kwa Waziri Mkuu ziweze kutatuliwa kwa wakati.

Puma Energy Tanzania yakabidhi gawio la bilioni 18 kwa wanahisa wake

$
0
0
Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Puma Energy Tanzania leo imekabidhi kwa Rais John Pombe Magufuli gawio la sh bilioni 9 kwa Rais John Pombe Magufuli ikiwa ni sehemu ya gawio la sh bilioni 18 kwa mwaka 2017 ambalo kampuni hiyo imetoa kwa wanahisa wake ambao ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Puma Investments Limited. 

Kampuni hiyo inamilikiwa kwa pamoja na serikali ya Jamhuri ya Muungano (Kupitia Msajili wa Hazina, Wizara ya Fedha) pamoja na Puma Investments Limited, kila moja ikiwa na umiliki wa hisa kwa asilimia 50 na hivyo kupitia gawio hilo kila mwanahisa amepata shilingi bilioni tisa (9).

Akizungumza,kwa niaba Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Limited Philippe Corsaletti, Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania Bw Lameck Hiliyai alisema kutokana na utendaji mzuri wa kampuni ya Puma Energy, gawio limekua kwa asilimia 100% ikilinganishwa na gawio la mwaka 2015 na kwa asilimia 29% ikilinganishwa na gawio na mwaka 2016.

Kwa mujibu wa Hiliyai, kufikia mwisho wa mwaka jana kampuni ilitengeneza faida kabla ya kodi ya jumla ya Shilingi 31 bilioni huku ikiwekeza takribani shilingi 9 bilioni kununua na kuendeleza miundombinu ikiwemo kununua vituo viwili vya mafuta kwenye jiji la Dodoma ikiwa ni juhudi za kuiunga serekali mkono katika kuhamia Dodoma.

“Ukuaji huu unaendana sambamba na mikakati ya kampuni ya kuhakiksha kampuni inaendelea kukua, kutengeneza faida, kukuza ajira nchini, kuchangia pato la taifa kupitia kodi, na kuendelea kuiunga serekali mkono katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo,’’ alisema.

Alisema ufanisi wa kibiashara wa Puma Energy Tanzania kwa mwaka 2017 ulikua mzuri kwa pande zote za mauzo pamoja na mapato. “Ufanisi wetu mkubwa unatokana zaidi na biashara ya mafuta ya ndege ambako kwa sasa sisi ndio tunaongoza katika soko.’’

Kwa mujibu wa taaarifa za masoko zilizochapishwa na Mamlaka ya udhibiti (EWURA) inaonesha kuwa uwepo wa Puma Energy kwenye soko la mafuta umeongezeka kutoka asilimia 12% mwaka 2015 hadi asilimia 14% kwa mwaka 2017.

Bw Hiliyai amepongeza juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais Dkt John Pombe Magufuli kwa mikakati yake ya kukusanya kodi na kutoa fursa kwa wawekezaji wa nje na ndani kama ilivyooneshwa kwenye bajeti ya 2017/2018.

“Mikakati hii imeweza kutengeneza mazingira rafiki kwa wawekezaji na kufanya makampuni mengi ikiwemo Puma kutengeneza faida zaidi. Mazingira haya mazuri ya biashara yameiwezesha kampuni ya Puma kukua zaidi kutoa gawio mara mbili zaidi ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita.,’’ alisema

Aliahidi kuwa kampuni hiyo itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na Serikali ya Awamu ya tano, na kuendelea kuchangia katika maendeleo ya taifa.Kampuni ya Puma ni ya mkondo wa kati kimataifa katika masula ya mafuta na pia kampuni ya mafuta inayojihusisha na uhifadhi mkubwa na usambazaji.

Majukumu makuu ya kampuni ni masoko na usambazaji wa bidhaa za petroli ndani ya Tanzania. Kampuni inauwezo wa kuhifadhi jumla ya lita za mafuta 94 milion, vituo 52 vya mafuta maeneo mbalimbali nchini na inahudumia viwanja vinane vya ndege. 
 Rais John Pombe Magufuli  (katikati) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh bilioni tisa ikiwa ni sehemu ya gawio la sh bilioni 18 ambalo kampuni hiyo imetoa kwa wanahisa wake ambao ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  pamoja na Puma Investments Limited wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dr Phillip Mpango  (kushoto kwake), Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo Bw Prof Joseph Buchweshaija (kushoto) na Meneja Uendeshaji wa  Kampuni ya Puma Energy Tanzania Bw Lameck  Hiliyai (kulia)
 Meneja Uendeshaji wa  Kampuni ya Puma Energy Tanzania Bw Lameck  Hiliyai (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh bilioni tisa kwa Rais John Pombe Magufuli  (katikati) ikiwa ni sehemu ya gawio la sh bilioni 18 ambalo kampuni hiyo imetoa kwa wanahisa wake ambao ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  pamoja na Puma Investments Limited. Hafla hiyo fupi imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dr Phillip Mpango  (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo Bw Prof Joseph Buchweshaija.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuniya Puma Energy Tanzania Bw Prof Joseph Buchweshaija (kushoto) akipokea mkono wa pongezi kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Phillip Mpango wakati wa hafla ya makabidhiano hayo.

PUMA ENERGY TANZANIA LIMITED YATANGAZA GAWIO LA BILIONI 18 KWA MWAKA 2017 KWA WANAHISA WAKE

$
0
0
*Wakabidhi gawio lao kwa Rais Dk.Magufuli leo Dar 

KAMPUNI ya mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited imetangaza gawio la Sh.bilioni 18 kwa mwaka wa fedha wa 2017 kwa wanahisa wake.

Puma Energy Tanzania ni kampuni inayomilikiwa kwa pamoja na Serikali(kupitia Msajili wa Hazina, Wizara ya Fedha) pamoja na Puma Investments Limited, kila moja ikiwa na umiliki wa hisa kwa asilimia 50 imetanza gawio hilo leo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti, ni kwamba ni kampuni ya mkondo wa kati kimataifa katika masula ya mafuta na pia kampuni ya mafuta inayojihusisha na uhifadhi mkubwa na usambazaji. 

Amesema majukumu ya makuu ya kampuni ni masoko na usambazaji wa bidhaa za petroli ndani ya Tanzania. "Kampuni inauwezo wa kuhifadhi jumla ya lita za mafuta 94 milion, vituo 52 vya mafuta maeneo mbalimbali nchini na inahudumia viwanja vinane vya ndege. "Kufikia mwisho wa mwaka ulioishia 31 Desemba 31 2017 kampuni ilitengeneza faida kabla ya kodi ya jumla ya Sh. bilioni 31,"amesema.

Amefafanua kampuni iliwekeza takribani Sh.bilioni 9 bilioni kwa mwaka 2017 kununua na kuendeleza miundombinu ikiwemo kununua vituo viwili vya mafuta kwenye Jiji la Dodoma ikiwa ni juhudi za kuiunga Serekali mkono katika kuhamia Dodoma.Ameongeza wakurugenzi wa kampuni hiyo wamependekeza gawio la Sh.bilioni 18 kwa mwaka ulioishia Disemba 2017.

Ameongeza kila mwanahisa atapata Sh.bilioni 9 na kwamba mwaka 2016 Gawio lilikua Sh.bilioni 14 na 2015 gawio lilikua Sh.bilioni 9 .) "Kutokana na utendaji mzuri wa kampuni ya Puma Energy, gawio limekua kwa asilimia 100 ikilinganishwa na gawio la mwaka 2015 na kwa asilimia 29 ikilinganishwa na gawio na mwaka 2016. 

"Ukuaji huu unaendana sambamba na mikakati ya kampuni ya kuhakiksha kampuni inaendelea kukua, kutengeneza faida, kukuza ajira nchini, kuchangia pato la taifa kupitia kodi, na kuendelea kuiunga serekali mkono katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo,"amesema Corsaletti.

Amesisitiza kuwa “Ufanisi wa kibiashara wa Puma Energy Tanzania kwa mwaka 2017 ulikua mzuri kwa pande zote za mauzo pamoja na mapato.
"Ufanisi wetu mkubwa unatokana zaidi na biashara ya mafuta ya ndege ambako kwa sasa sisi ndio tunaongoza katika soko,"amesema.

Meneja Mkuu huyo pia ameongeza kwa kueleza taaarifa za masoko zilizochapishwa na Mamlaka ya udhibiti (EWURA) inaonesha kuwa uwepo wa Puma Energy kwenye soko la mafuta umeongezeka kutoka asilimia 12 mwaka 2015 hadi asilimia 14 kwa mwaka 2017

Kwa kuongezea Corsaletti pia amepongeza juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli na Serikali yake katika mikakati yake ya kukusanya kodi na kutoa fursa kwa wawekezaji wa nje na ndani kama ilivyooneshwa kwenye bajeti ya 2017/2018. 

"Mikakati hii imeweza kutengeneza mazingira rafiki kwa wawekezaji na kufanya makampuni mengi ikiwemo Puma kutengeneza faida zaidi,"amesema. Amefafanua mazingira hayo mazuri ya biashara yameiwezesha kampuni ya Puma kukua zaidi kutoa gawio mara mbili zaidi ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita. 

Pia Puma itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na Serikali ya Awamu ya tano, na kuendelea kuchangia katika maendeleo ya taifa, hivyo uongozi wa Puma Energy utaendelea kutoa ushrikiano kama ambavyo wamekua wakishirikiana siku zote.Hivyo Puma imekabidhi gawio hilo leo kwa Rais Dk.John Magufuli ambapo pia kulikuwa na kampuni na mashirika mbalimbali yamekabidhi gawio kwa Serikali.
 Rais John Pombe Magufuli  (katikati) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh bilioni tisa ikiwa ni sehemu ya gawio la sh bilioni 18 ambalo kampuni hiyo imetoa kwa wanahisa wake ambao ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  pamoja na Puma Investments Limited wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dr Phillip Mpango  (kushoto kwake), Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo Bw Prof Joseph Buchweshaija (kushoto) na Meneja Uendeshaji wa  Kampuni ya Puma Energy Tanzania Bw Lameck  Hiliyai (kulia)
 Meneja Uendeshaji wa  Kampuni ya Puma Energy Tanzania Bw Lameck  Hiliyai (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh bilioni tisa kwa Rais John Pombe Magufuli  (katikati) ikiwa ni sehemu ya gawio la sh bilioni 18 ambalo kampuni hiyo imetoa kwa wanahisa wake ambao ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  pamoja na Puma Investments Limited. Hafla hiyo fupi imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dr Phillip Mpango  (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo Bw Prof Joseph Buchweshaija.

RAIS MAGUFULI NA WAZIRI MKUU WA KOREA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MKATABA WA UJENZI WA DARAJA JIPYA LA SELANDER IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Lee Nak-yeon mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Lee Nak-yeon wakati wakielekea katika ukumbi wa Jakaya Kikwete uliopo Ikulu kwa ajili ya kushuhudia tukio la Utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Daraja jipya la Selander litakalopita baharini kuanzia katika Hospitali ya Agha Khan mpaka Coco beach jijini Dar es Salaam.
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Lee Nak-yeon wakishuhudia tukio la utiaji saini Mkataba wa mradi wa ujenzi wa Ujenzi wa Daraja jipya la Selander litakalopita baharini kuanzia katika Hospitali ya Agha Khan hadi maeneo ya  Coco beach jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali  mara baada ya tukio la utiaji saini wa mradi wa ujenzi wa Ujenzi wa Daraja jipya la Selander litakalopita baharini kuanzia katika Hospitali ya Agha Khan mpaka Coco beach jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Lee Nak-yeon mara baada ya tukio la utiaji saini wa mradi wa ujenzi wa Ujenzi wa Daraja jipya la Selander litakalopita baharini kuanzia katika Hospitali ya Agha Khan mpaka Coco beach jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Lee Nak-yeon watatu kutoka (kushoto)pamoja na viongozi wengine wa Jamhuri ya Korea, Serikali ya Tanzania, Wabunge, Wakuu wa Wilaya pamoja na viongozi wa Mkoa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya Picha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Lee Nak-Yeon mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

WATANO WAHUKUMIWA KUNYONGWA BAADA YA MAHAKAMA KUWATIA HATIANI KWA MAUAJI YA BILIONEA MSUYA.

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,kanda ya Kaskazi.

MAHAKAMA kuu ya Tanzania ,Kanda ya Moshi imewahukumu washtakiwa watano kunyongwa hadi kufa ,huku ikimuachia huru mshtakiwa wa pili ambao kwa pamoja walikuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya kukusudia ya mfanyabiashara wa Madini ya Tanzanite,Bilionea, Erasto Msuya.

Waliohukumia adhabu ya kifo ni mshtakiwa wa kwanza Sharif Athuman ,mshitakiwa wa tatu,Musa Mangu,Mshitakiwa wa tano,Karim Kihundwa,mshitakiwa wa sita ,Sadiq Jabir na mshtakiwa wa saba,Alli Majeshi.

Akisoma hukumu hiyo jana ,Jaji Salma Maghimbi wa Arusha alisema mahakama hiyo imejiridhisha pasipo shaka kwamba washtakiwa watano ndio waliohusika kutekeleza mauaji ya kukusudia ya mfanyabiashara huyo lakini imeshindwa kumtia hatiani mshitakiwa wa pili ,Shaibu Said maarufu Mredii kutokana na ushahidi kushindwa kumuunganisha katika tukio la mauaji.

Awali akisoma maelezo ya kila Mshtakiwa kabla ya kutoa hukumu ,Jaji Maghimbi alisema katika shauri hilo namba 12 la mwaka 2014 upande wa Jamhuri uliwasilisha Mashahidi 27 na vielelezo 26 ambapo vielelezo 21 kati ya hivyo ni vya maandishi na vitano ni ushahidi wa vitu.

Jaji Maghimbi mesema upande wa utetezi uliwasilisha Mashahidi nane pamoja na vielelezo vinne vya maandishi huku akitaja baadhi ya vielelezo vilivyo wasilishwa na upande wa jamhuri kuwa ni pamoja na Pikipiki mbili moja aina ya King Lion namba T751 CKB na Toyo namba T316 CLG zinazotajwa kutumika kutumiwana washtakiwa.

Vielelezo vingine vilivyowasilishwa mahakamani hapo ni pamoja na maelezo ya Onyo ,yaliyotolewa na washtakiwa wa kwanza ,Sharif Athuman, wa tatu ,Musa Mangu na wa saba,Alli Majeshi huku maelezo ya ungamo yakitolewa na Karim Kuhundwa.

Aidha Jaji Maghimbi ameeleza kuwa awali shauri hilo lilikuwa na washitakiwa saba ambapo mmoja kati yao, mshtakiwa wa wanne Jalila Zuberi, Mahakama ilimuachia huru Mei 29,2018 kutokana na kutokupatika na kutotajwa mahala popote wakati wa uwasilishwaji wa ushahidi wa upande wa Jamhuri.

Katika maelezo yake Jaji Maghimbi amesema baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashitaka ,kwa mshtakiwa wa kwanza, Sharif Athuman,ushahidi umeonyesha bayana kuwa ndiye mhusika katika kupanga mauaji ya mfanyabishara huyo kwa kuwatumia washtakiwa wengine.

Kuhusu mshitakiwa wa tatu, Musa Mangu, Jaji Maghimbi alisema pamoja na kujua nia ovu ya mauaji dhidi ya Marehemu,mshtakiwa aliendelea kushiriki na hakuonyesha nia ya kujitoa na kwamba katika maelezo yake alijaribu kuonyesha kuwa yeye hakuusika katika mauaji bali watuhumiwa wenzake ikiwemo aliyekuwa bosi wake Sharifu Athuman.

Maelezo kuhusu Mshtakiwa wa tano ,Karim Kihundwa na wa sita Sadiki Jabir ,Jaji Maghimbi alisema mshtakiwa wa tano alikiri kosa la kufyatua risasi na kumuua Msuya na kwamba kwa mujibu wa ushahidi ulitolewa unaonyesha jinsi walivyotoa ushirikino wa kupatikana kwa bunduki walioitumia katika mauaji.

Mshitakiwa wa Sita Sadiki Jabir, hakuonyesha uwoga wowote wakati akitoa maelezo ya ungamo kwa mlinzi wa Amani na kwamba mahakama imeridhika na ushahidi ulitolewa dhidi yao wa kushiiki kufanya mauaji hayo kwa makusudi.

Jaji Maghimbi amesema mshitakiwa wa saba, Ally Majeshi, kulingana na ushahidi ulitolewa ndiye alikuwa mtu wa kwanza kumvuta eneo la mauaji marehemu Msuya na kwamba ndiye aliyetaja fedha walizoahidiwa kulipwa baada ya kutekeleza mauaji hao.

Awali kabla akizungumza kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo Wakili wa serikali, Ignasi Mwinuka, aliiomba Mahakama hiyo itoe adhabu stahiki kwa washtakiwa hao kama sheria inavyoelekeza.

Akiwakilisha Jopo la Mawakili wa upande wa utetezi, Wakil Majura Magafu, alisema kulingana na umri mdogo wa shitakiwa hao Mahakama ione umuhimu wa kuwawaweka katika orodha ya watu wanaostahili msamaha wa Rais haswa ikizingatiwa wamekwisha kaa mahabusu kwa muda wa miaka mitano.

Jopo la mawakili wa upande wa utetezi katika shauri hilo uliongozwa na Wakili Hudson Ndusyepo, Majura Magafu,Emanuel Safari na John Lundu huku upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Abdala Chavula,Omary Kibwana,Kassim Nasir,Neema Mwenda,Wiliam Maugo,Lilian Kyusa,Ignasi Mwinuka,Verediana Mlenza.

MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI KITUO CHA AFYA CHA TUNDUMA NA KUHUTUBIA WANANCHI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Utawala Bora ni moja ya ahadi waliyoitoa kwa wananchi wakati wa kampeni.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Tunduma ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake katika mkoa wa Songwe. “Lazima tunapofanya kazi zetu sheria zifuatwe, unapoacha kufuata sheria kwa sababu ya Matakwa binafsi, kwa sababu ya kunufaika wewe binafsi hili ni Tatizo hapa hapana utawala bora” 
alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais alisema Utawala bora usisukumwe tu upande wa Serikali unapaswa kupimwa kwenye ngazi zote mpaka za chini zikiwemo ngazi za Udiwani.Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Utawala bora ni pamoja na maendeleo ya Serikali yanapatikana.

Makamu wa Rais amesema Serikali itajenga pamoja na kuboresha vituo vya Afya 9 katika mkoa wa Songwe ambapo wilaya ya Momba kutakuwa na vituo vitatu.
Mapema leo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefungua kituo cha Afya cha Tunduma kilichofanyiwa maboresho na kugharimu zaidi ya shilingi milioni 500 na ambacho kitahudumia wakazi zaidi ya elfu 80.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la  Kituo cha Afya cha Tunduma ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Songwe.  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi waTunduma  kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Tunduma ikiwa siku ya tatu ya ziara yake mkoani Songwe. 
 Sehemu ya Umati wa wakazi wa Tunduma waliojitokeza kumsikiliza Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wauguzi wa Kituo cha Afya cha Tunduma mara baada ya kukifungua  ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Songwe. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Esther Luila mwenye umri wa miaka 7 mara baada ya kukifungua  kituo cha Afya Tunduma  ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia viatu vya ngozi vilivyotengenezwa na Wajasiriamali wa Wilaya ya Momba muda mfupi kabla hajahurubia kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Tunduma ikiwa siku ya tatu ya ziara yake mkoani Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

RAIS MAGUFULI APOKEA MAGAWIO TOKA KATIKA TAASISI, MASHIRIKA NA MAKAMPUNI YA UMMA

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya TIPER Profesa Abdulkarim Mruma  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Bw. Edwin Rutageruka.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mfuko wa Misitu Tanzania akiwa na Katibu Dkt. Tuli Salum Msuya  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na (EWURA) Maji Profesa Jamidu Kamika akiwa na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa  EWURA Bw. Nzinyangwa Mchani  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekliti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Profesa Rutasitara akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Balozi Ben Moses akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa TFDA Bi. Agnes Kijo   katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Shirika la Viwango (TBS)  Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko akiwa na  Mkuruigenzi wa TBS Profesa Egird Mubofu  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari  Profesa Ignas Rubaratuka aliye pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi Deusdedit Kakoko  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu wakipata picha ta pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumua ya Bunge ya Uwekezaji wa Mtaji wa Umma baada ya kupokea magawio kutoka katika taasisi, mashirika na Makampuni ya Umma katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018. Picha na IKULU

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Wafanyakazi wa JKCI wamuaga Afisa Muuguzi Mwandamizi Mama Hadija Mradi aliyestaafu utumishi wa Umma

$
0
0
 Afisa Muuguzi Mwandamizi Mstaafu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mama  Hadija Mradi (kulia) akikata keki wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Taasisi hiyo ilizopo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi  Robert Mallya
 Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akimlisha keki Afisa Muuguzi Mwandamizi Mstaafu Mama  Hadija Mradi wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo katika  ukumbi wa mikutano wa  Taasisi hiyo uliopo jijini Dar es Salaam . Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi (kushoto) akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wake katika utumishi wa umma kwa kufanya kazi kwa miaka 41 Afisa Muuguzi Mwandamizi Mstaafu Mama  Hadija Mradi katika  hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi Robert Mallya.
 Afisa Muuguzi Mwandamizi Mstaafu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mama  Hadija Mradi (kulia) akifuatilia yaliyokua yakiendelea wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Delila Kimambo.
Baadhi ya wafanyakazi  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa hafla fupi ya kumuaga Afisa Muuguzi Mwandamizi Mstaafu Hadija Mradi (hayupo pichani) iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo uliopo jijini Dar es Salaam. Picha na JKCI
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images