Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

SERIKALI YA MAGUFULI SIO YA 'WALIMILA DOLE'

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Kibaha vijijini Hamood Jumaa katika kituo cha afya Mlandizi mkoani Pwani.


Viongozi wakiwa Katika zoezi la ukaguzi wa miradi ya maendeleo ndani ya halmashauri ya kibaha vijijini.
Mbunge wa Kibaha Vijijini Hamood Abuu Jumaa akimkaribisha Waziri wa Nchi, Tamisemi Selemani Jafo kijijini Magindu ili aongee na wananchi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa halmashauri ya Kibaha kukagua ukarabati wa sekondari ya Ruvu.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Ruvu.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo leo ametembelea halmashauri ya wilaya ya Kibaha kufanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo. 

Katika Ziara hiyo, Waziri Jafo amefanikiwa kutembelea kituo cha afya Mlandizi, ukarabati wa sekondari ya wasichana ya Ruvu, pamoja na uboreshaji wa Kituo cha afya cha Magindu ambapo zaidi ya sh. bilioni 1.9 zimeshatolewa na serikali kufanikisha miradi hiyo. 

Akizungumza na wananchi wa Magindu waziri Jafo amewaambia wananchi hao kwamba serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli ni serikali ya vitendo sio ya kuahidi bila kutekeleza na kwamba kwa kizaramo "Sio ya walimila Dole". 

Jafo alitumia neno hilo la Lugha ya kizaramo kwa wakazi hao wa magindu ambao wengi wao ni wazaramo ili kuleta msisitizo.Waziri Jafo amempongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini Hamood Abuu Jumaa kwa kazi kubwa anayoifanya ya kiwaletea wananchi wa kibaha vijijini maendeleo ya kweli. 

Aidha, waziri Jafo amewapongeza viongozi wa Kibaha vijijini kwa usimamizi mzuri wa ukarabati wa shule ya Ruvu kwani kwasasa imekuwa shule ya kuvutia kutokana na usimamizi mzuri wa fedha za serikali. Hata hivyo katika ziara hiyo, Jafo ametoa mwezi mmoja agizo la kuwekwa majokofu jengo la kuhifadhia maiti katika kituo cha afya mlandizi lililojengwa tangu mwaka 2015 ili wananchi waweze kupata huduma hiyo.

Nao, wananchi wa Magindu wamemshukuru mbunge wao kwa kuwapigania mpaka wamepatiwa fedha hizo za maendeleo.

PICHA MBALIMBALI ZA ZIARA YA WAZIRI KANGI LUGOLA JIJINI ARUSHA

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kushoto), akiongozana na Naibu Waziri  Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (kulia) na  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (wapili kulia), kutembelea eneo la Kaloleni zilipo nyumba za polisi, jijini Arusha.Kushoto ni mmoja wa wadau waliojitolea kujenga nyumba hizo,Hans Pol.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Waziri  wa Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi,  Kangi Lugola (wapili kushoto),  akimsikiliza Kamanda wa  Polisi  Mkoa  wa  Arusha, Ramadhani  Ng’anzi (kulia) baada ya kutoka kutembelea Kituo cha Polisi Utalii.Wapili  kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

 Waziri  wa Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi,  Kangi Lugola (wapili kushoto),  akimsikiliza Kamanda wa  Polisi  Mkoa  wa  Arusha, Ramadhani  Ng’anzi (kulia) baada ya kutoka kutembelea Kituo cha Polisi Utalii.Wapili  kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na mdau wa maendeleo mjini Arusha,Hans Pol.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo.Waziri Lugola yupo mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, Naibu Waziri  Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (kushoto)  na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kulia),wakisikiliza taarifa ya Kituo cha Polisi Utalii baada ya viongozi hao kutembelea kituo hicho.

MAHAKAMA YAWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WAKE KUHUSU MASUALA YA HABARI

$
0
0
Na Lydia Churi-Dodoma

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Mohamed Awadh leo amefungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari wa Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama Kuu na Mahakama za Mikoa na kuwataka washiriki hao kujifunza namna ya kutoa taarifa za Mahakama zilizo sahihi ili kuboresha suala zima la utoaji wa haki kwa wananchi.

Akifungua mafunzo hayo mjini Dodoma, Jaji Awadh amesema Mahakama ya Tanzania kupitia Mpango Mkakati wake wa miaka mitano (2015/16-2019/20) inalenga kujenga imani ya wananchi kwa Mahakama na kuimarisha ushirikishwaji wa wadau katika shughuli zake ambapo kwa kuwapatia mafunzo wawakilishi wa habari ni moja ya mikakati ya kufanikisha jambo hilo.

Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari wa Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama Kuu na Mahakama za Mikoa yanawahusisha Watumishi wa Mahakama wakiwemo Maafisa Habari, Maafisa Utumishi, Maafisa Tawala, Maafisa Tehama pamoja na Wasaidizi wa Kumbukumbu.

Aidha mafunzo hayo pia yanawahusisha Maafisa Habari wa Taasisi ambazo ni wadau wa Mahakama ya Tanzania zikiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume ya Kurekebisha Sheria, Wizara ya katiba na Sheria na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.

Alisema mafunzo hayo yatasaidia kuimarisha utoaji wa habari za mahakama kwa wananchi kwa kuwa Maafisa hao watajengewa uwezo utakaowawezesha kuandika taarifa za mahakama zitakazoongeza uelewa kwa wananchi juu ya maboresho yanayoendelea kufanyika na hatimaye kurejesha imani ya wananchi kwa Mhimili huo.

Jaji Awadh aliyataja madhumuni mengine ya mafunzo hayo kuwa ni pamoja na kuwapatia ujuzi washiriki hao hasa katika ukusanyaji, uandaaji na utoaji wa taarifa zinazohusu mahakama ya Tanzania pamoja na kuwajengea uwezo Maafisa hao kuhusu matumizi ya Teknolojia katika utoaji wa habari za Mahakama.

Mafunzo ya siku tano kwa watumishi hao wa Mahakama yameandaliwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.

 Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma Mhe. Mohamed Awadh akifungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari za Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama kuu ya Tanzania na kwenye Mahakama za Mikoa yaliyoanza leo mjini Dodoma. Kushoto ni Mshauri Mwelekezi wa Mawasiliano kutoka kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama (Judiciary Delivery Unit- JDU) Dkt. Cosmas Mwaisobwa na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mahakama ya Tanzania Bw. Nurdin Ndimbe.
Maafisa Habari, Maafisa Tawala, Maafisa Utumishi, Maafisa

Tehama na Wasaidizi wa Kumbukumbu wanahudhuria mafunzo hayo. Mafunzo hayo pia yanahudhuriwa na Maafisa habari kutoka baadhi ya Taasisi ambazo ni wadau wa Mahakama zikiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume na Tume ya Kurekebisha Sheria. 
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma Mhe. Mohamed Awadh akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washirikiwa Mafunzo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari za Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama kuu ya Tanzania na kwenye Mahakama za Mikoa yaliyoanza leo mjini Dodoma. Mafunzo hayo pia yanahudhuriwa na Maafisa habari kutoka baadhi ya Taasisi ambazo ni wadau wa Mahakama zikiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume na Tume ya Kurekebisha Sheria. 
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma Mhe. Mohamed Awadh akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washirikiwa Mafunzo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari za Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama kuu ya Tanzania na kwenye Mahakama za Mikoa yaliyoanza leo mjini Dodoma. Mafunzo hayo pia yanahudhuriwa na Maafisa habari kutoka baadhi ya Taasisi ambazo ni wadau wa Mahakama zikiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume na Tume ya Kurekebisha Sheria.

VODACOM YAPATA LESENI YA MASAFA

$
0
0
VODACOM YAPATA LESENI YA MASAFA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Vodacom imepata leseni ya mafasa ya mawasiliano katika bendi ya 700MHZ baada ya kuibuka mshindi katika mnada wa masafa hayo.

Vodacom ilishinda masafa hayo kwa jumla ya bei dola za Kimarekani 1,0005,000 ambapo masafa hayo yatalipiwa kodi kila mwaka dola za Kimarekani 40,000.

Akizungumza baada ya Vodacom kupata leseni Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzu Mhandisi Isaac Kamwelwe amesema kuwa TCRA imekuwa ikifanya kazi nzuri ambapo imetoa gawio la sh.bilioni 81.

Amesema kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) kuhakikisha Vodacom inatekeleza masharti ya leseni yanatekelezwa kama ilivyokusudiwa katika utoaji wa huduma ya mawasiliano.

Kamwelwe ameiataka TCRA kuendelea na utaratibu wa kugawa masafa kwa njia ya mnada kutokana na faida ya kiuchumi kwa fedha inayopatikana kuendeleza miundombinu ya huduma za simu za mikononi na data zenye kasi kubwa , ubora , kupunguza gharama za uwekezaji.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhadisi James Kilaba amesema kuwa kuna njia mbalimbali za ugawaji wa masafa ikiwemo kutoa masafa kwa anayewahi kuomba pamoja na njia ya mnada.

Amesema masafa ya simu za mkononi ya faida katika kuendeleza huduma za simu za mkononi na data zenye ubora ,kupunguza gharama za matumizi ya huduma za mawasiliano kwa mtoa huduma ya masafa hayo.

Kilaba amesema faida nyingine ni kukuza na kuchochea ubunifu wa huduma mpya na matumizi ya teknolojia za habari na mawasiliano pamoja na serikali kupata mapato kutokana na mauzo ya masafa hayo.
 01.Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzu Mhandisi Isaac Kamwelwe akizungumza na waandishi habari mara baada ya kampuni ya Vodacom kupata leseni ya masafa kutoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa TCRA jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini TCRA, Mhadisi James Kilaba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na utoaji wa leseni ya masafa kwa kampuni Vodacom katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa TCRA jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini TCRA, Mhadisi James Kilaba akimkabidhi leseni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom(T) Plc katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa TCRA jijini Dar es Salaam

KATIBU MKUU IKULU DKT . KUSILUKA AKUTANA NA UONGOZI WA TASAF

$
0
0
Na Estom Sanga-TASAF 


Katibu Mkuu mpya wa Ofisi ya Rais Dr Moses Kusiluka ametembelea ofisi za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF jijini Dar es salaam hii ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu ateuliwa na Rais John Magufuli kushika wadhifa huo mwezi uliopita. 

Akizungumza na Menejimenti ya TASAF ,Dr. Kusiluka amesema ziara hiyo imelenga kupata maelezo ya shughuli za Mfuko huo ambao uko chini ya Ofisi ya Rais. Aidha Katibu Mkuu huyo wa Ofisi ya Rais ameitaka menejimenti ya TASAF kuendelea kutoa huduma zake kwa umma kwa kuzingatia misingi ya uadilifu kama ambavyo serikali ya Awamu ya Tano inavyosisitiza. 

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TASAF,Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo Bw. Ladislaus Mwamanga amesema tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo mwaka 1999/2000 umefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hususani katika sekta za elimu, afya,miundombinu na uzalishaji mali katika maeneo mbalimbali nchini. “tumeshirikiana na wananchi katika kutatua kero na changamoto kwenye maeneo yao kwa mafanikio makubwa” amesema Bw. Mwamanga. 

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF pia amemweleza Katibu Mkuu huyo wa Ofisi ya Rais hatua mbalimbali zilizofikiwa na Mfuko katika kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao mkazo wake ni kuwawezesha walengwa kufanya kazi na kujipatia kipato kitakachowawezesha kuondokana na umaskini. 

Bw. Mwamanga amesema tathimini ya awali inaonyesha kuwa mafanikio makubwa yamepatikana kwa Walengwa kuanza kuboresha maisha yao ikiwemo kujenga nyumba bora,kuboresha lishe ,elimu,kuwekeza katika miradi midogo midogo ikiwemo ufugaji wa kuku,mbuzi,nguruwe na hata ng’ombe na hivyo kujiongezea kipato chao. 

Kuhusu huduma za kijamii Mkurugenzi mtendaji huyo wa TASAF amesema taasisi hiyo imeendelea kutoa mchango wa ujenzi wa visima vya maji katika maeneo mbalimbali nchini kwa kuwashirikisha wananchi kwenye maeneo yao. Dr. Moses Kusiluka ameteuliwa na Rais John Magufuli kushika wadhifa wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na kabla ya hapo alikuwa Katika Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Mkazi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Dr. Moses Kusiluka (kulia ) akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga (kushoto) katika maeneo ya Ofisi za TASAF jijini Dar es Salaam.
Dkt.r. Kusiluka akiwa katika jengo la mikutano la TASAF akiangalia ofisi zinazotumiwa na baadhi ya watumishi wa taasisi hiyo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Dr. Moses Kusiluka akizungumza na menejimenti ya TASAF alipotembelea taasisi hiyo kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe na Rais John Magufuli kushika wadhifa huo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Moses Kusiluka (walioketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya TASAF baada ya kuzungumza nayo.

AWESO AMURU KUWEKWA NDANI WAKANDARASI WA MRADI WA MAJI HANDENI KWA KUSHINDWA KUWEPO ENEO LA MRADI

$
0
0
 NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa Kata ya Mkata wilayani Handeni wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya Maji inayotekelezwa
 Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini (CCM) Mboni Mhita akuzungumza katika ziaa hiyo 
 MKUU wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe katika akimueleza jambo Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia wakati wa ziara hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa wilaya ya Handeni William Makufwe
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe mara baada ya kutembelea mradi wa Maji eneo la Mkata katikati ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa wilaya ya Handeni William Makufwe
 NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akimsikiliza kwa umakini Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini (CCM) Mboni Mhita wakati wa ziara hiyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe.
 Wakandarasi ambao Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso aliotaka wawekwe ndani wakiwa chini ya ulinzi 
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso wa pili kutoka kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Handeni kulia wakati wakitembelea miradi ya maji wilayani humo wakati wa ziara yake kulia ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa wilaya ya Handeni William Makufwe kushoto ni Diwani wa Kata ya Mkata
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akiwa amepanda juu kwenye tenki eneo la mkata kulikagua wakati wa ziara yake
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akiwa amepanda juu kwenye tenki eneo la mkata kulikagua wakati wa ziara yake
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akilakiwa na Mkurugenzi wa Mtendaji wa wilaya ya Handeni William Makufwe mara baada ya kuwasili mjini Handeni
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akiwa na Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe wakati wa ziara hiyo
Mkurugenzi wa Mtendaji wa wilaya ya Handeni William Makufwe akimueleza jambo Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso mara baada ya kutembelea miradi ya maji kwenye eneo la Mkata katikati ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akifuatilia kwa umakini
Sehemu ya bwawa la maji lililopo eneo la Mkata wilayani Handeni 


NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ameamuru kuwekwa ndani wakandarasi wanaotekelezwa mradi wa maji yenye thamani ya zaidi ya bilioni tatu eneo la mkata wilayani Handeni baada ya kushindwa kuwepo kwenye eneo la mradi licha ya kupewa taarifa za uwepo wa ziara yake. 

Wakandarasi ambao walilazimika kuwekwa ndani ni Mkandarasi wa Kampuni ya Tansino Logistick Limited ya Dar Abdul Ismail na Charles Stephano ambaye ni mkandarasi wa ujenzi huku Chales Tarimbo mshauri Mkandarasi naye akikumbana na kadhia hiyo. 

Agizo hilo alilitoa leo wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maji inayotekelezwa kwenye kata ya Mkata wilayani Handeni ambapo miradi hiyo mitatu ilikuwa ikigharimu zaidi ya sh.bilioni tatu. 

Akiwa kwenye eneo hilo Naibu Waziri huyo alisema haiwezekani wabunge wanaomba miradi ya maji na serikali inatenga lakini watu wachache wanatumia fedha hizo kwenye matumizi kwa maslahi yao binafasi na kuwafanya wananchi kuendelea kuteseka na tatizo la maji. 

Alisema kutokana na kuwepo kwa tabia hiyo ambayo imekuwa ikirudisha nyuma juhudi kubwa zinazofanywa serikali hawatavumiliwa badala yake watahakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria ili kuweza kukomesha vitendo vya namna hiyo kwenye jamii. 

“Ndugu zangu wakati Rais akiniteua aliniagiza nihakikisha wananchi wanapata 1maji vinginevyo nitatumbuliwaa nami sipo tayari kwa hilo hivyo nitahakikisha tunawachukulia hatua kali wakandarasi wanaoshindwa kuendena na kasi na hivyo kuikwamisha kwa maslahi yao binafasi huku wananchi wakiendelea kuteseka”Alisema. Naye kwa upande wake,Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini (CCM) Mboni Mhita alimuelezwa Naibu Waziri huyo kuwa mradi huo umejengwa chini ya kiwango na kusababisha wananchi kuendelea kuteseka na adha ya maji. 

“Mh Naibu Waziri wilaya ya Handeni ni miongoni mwa wilaya ambazo zinachangamoto kubwa ya tatizo la maji lakini sisi kama wabunge tumekuwa tukiiomba fedha za mradi ya maji lakini wakandarasi wamekuwa wakitukwamisha”alisema. Alisema kinachofanywa na wakandasi hao juu ya utekelezaji wa miradi hii ni ubadhirifu wa wazi kabisa hivyo ili kuondokana na tatizo hilo serikali inapaswa kuwachukulia hatua wakandarasi wa namna hiyo ili iwe fundisho wa wengine wenye tabia za namna hiyo. 

Naye kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe alisema miradi hiyo ambayo Rais aliagiza imalizike leo (jana)Julai 23 huku jambo la kushangaza hakuna dalili ya umalizikaji wa miradi hiyo. Miradi hiyo ambayo ilitakiwa kutelezwa Wilayani hapo ni pamoja na bwawa la mkata,bwawa la manga na miundombinu ya mambomba toka katika bwawa la mkata hadi mkata mjini jambo ambalo halijafanyika hadi mwisho wa agizo

SPIKA NDUGAI AFIKA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE KUMJULIA HALI MUME WA MHE. RUTH MOLLEL

$
0
0
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) akisalimiana na Ndg. David Mollel mume wa Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA) Mhe. Ruth Mollel alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Kushoto ni Mhe. Ruth Mollel.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai ( wa pili kushoto) akimsikiliza Ndg. David Mollel (wa kwanza kulia) mume wa Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA) Mhe. Ruth Mollel alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) . Wengine katika picha ni Katibu wa Bunge Ndg Stephen Kagaigai (wa pili kulia) na Mhe Ruth Mollel (wa kwanza kushoto).
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof Mohamed Janabi alipokutana naye hospitali hapo. Kulia ni Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof Mohamed Janabi alipokutana naye hospitali hapo.PICHA NA BUNGE

DC HAPI AANZA ZIARA YA KATA KWA KATA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI NA KUZITAFUTIA UFUMBUZI

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi akiwa ameambatana na wakuu wa idara mbalimbali kutoka ofisini kwake  mapema jana ameanza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ya Wananchi na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili Wananchi wa Wilaya hiyo.

Katika ziara hiyo iliyoanza jana kata ya Tandale Mkuu huyo wa Wilaya ameweza kusikiliza kero za wananchi waishio maeneo hayo,katika utangulizi wake alisema ni jukumu lake kuwasikiliza na kuzitatua kwani ndiyo jukumu ambalo Rais kamuagiza kulifanya.

"Nimejipanga na timu yangu kuanza ziara yangu na nitazunguka kata hadi kata kuwatembelea wananchi na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi wangu, hiyo ndo kazi nimepewa kama mkuu wenu wa wilaya.

Serikali ya awamu ya tano inafanya mambo mengi sana na kwa sababu serikali ni kubwa inawezekana sisi tukikaa juu tusijue yanayoendelea huku chini vizuri, wapo wananchi wanaoteseka kwa kukosa haki zao, wananchi ambao wananyanyasika, wananchi wenye kero mbalimbali zinazohusu maji, afya, elimu, ardhi, jeshi la polisi na n.k. Kwasababu mimi sio mtu wa kukaa ofisini nimeamua kuanzaisha huu mchamchaka kata hadi kata kuwasikiliza Wananchi" DC Hapi

Katika ziara hiyo wananchi waliibua kero zao mbalimbali zikiwemo huduma mbovu katika Zahanati ya Tandale, ukosekanaji wa dawa katika Zahanati hiyo, migogoro ya ardhi, tatizo la maji, wazee kutopata fedha zao stahiki na kupewa watu wanaojiweza, migogoro ya mirathi, shutuma za polisi jamii kuwapiga wananchi kinyume na sheria, ujenzi wa barabara, ujenzi wa shule ya sekondari katika kata hiyo na kadhalika.

Aidha DC Ally Hapi ametoa maagizo kwa wakuu wa idara husika kushughulikia kero hizo za wananchi za kuhakikisha zimepatiwa ufumbuzi wa kina ili wananchi wa kata hiyo wasiendelee kuteseka na kujivunia nchi yao.Katika hali nyingine Wananchi wa maeneo hayo walionekana kufurahishwa na ziara ya mkuu huyo wa wilaya kwani walikua wanatamani sana kukutana nae ili waeleze kero zao mbele yake lakini ikawa inawapa ugumu hivyo wamemshukuru.

DC Hapi atafanya ziara ya kuzunguka na kusikiliza kero za wananchi kwenye kata zote 20 Za Wilaya ya Kinondoni na Kwa Siku Ya Kesho Jumanne Atakua Kata Ya Kinondoni Uwanja Wa Ufipa Kipande.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi akiwa ameambatana na wakuu wa Idara mbalimbali kutoka ofisini kwake mapema jana wakati akiendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Wananchi na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili Wananchi wa Wilaya hiyo. 
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi akiwa akiwahutubbia wakazi wa Tandale mapema jana wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Wananchi na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili Wananchi wa Wilaya hiyo.

KIMBUNGA CHAWASHUKIA 'WAPIGA DILI' WA MAJI JIJINI DAR

$
0
0
 Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasco), limeendelea na zoezi maalum yakuibua wezi wa Maji katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam nakuwachukulia hatua kali za kisheria pamoja na kutaifisha vifaa vyote vinavyotumika wizi huo. 

 Hayo yamebainshwa na Meneja wa Dawasco Mkoa wa Kawe Mhandisi Boniface Philemon wakati wa zoezi maalum linaloendeshwa na shirika hilo la kubaini kaya zilizojiunganishia huduma ya Maji kinyume na utaratibu katika eneo la Mbezi Goigi na kufanikiwa kubaini wizi mkubwa wa Maji unaofanywa na baadhi wakazi katika kaya hizo. 

 “Tupo katika zoezi maalum la kubaini wizi wa Maji katika eneo hili la Mbezi Goigi na leo tumeweza kubaini wizi wa Maji katika kaya hizi mbili zilizofanya mchezo wakuharibu mita kwa kuondoa seal katika mita nakufanya mita hizo kutokuwa na uwezo wakufanya kazi kwa ufanisi”, alisema Mhandisi Boniface. 

 Hata hivyo Mhandisi Boniface ameendelea kueleza kuwa katika kaya hizo mbili wameweza pia kubaini visima vikubwa viwili vya Maji vyenye ujazo wa zaidi ya lita elfu 30,000 pamoja na Pampu kubwa sita zinazotumika kuvuta Maji na kuuzia wafanyabiashara wa magari ya Maji maarufu kama maboza wakati wa asubuhi na jioni ambapo ni kinyume na utaratibu wa Dawasco. 

 Kwa upande wa mjumbe wa eneo la Mbezi Juu Bi. Happiness Tarimo amekiri kuwa amekuwa akiona magari ya Maji yakiingia katika nyumba hizo na kutoka bila kuelewa kinachoendelea hivyo amewataka wakazi wa eneo hilo kutojihusisha kabisa na wizi wa Maji kwani ni kosa kisheria na atakaye bainika atachukuliwa hatua mara moja. 

 “Nimekuwa nikiona Magari ya Maji yakiingia na kutoka katika nyumba hizi mbili mara kwa mara bila kuelewa kama kuna jambo lolote linaloendelea ila nitoe wito kwa wananchi wangu tuepukane kabisa na wizi wa Maji maana ni sawa naku hujumu uchumi ukibainika tutakuchukulia hatua za kisheria” alisema Bi. Tarimo. 

 Dawasco baada yakubainisha wizi huo wamechukua ya hatua kutaifisha pampu, mota zilizokuwa zinatumika kuchepushia Maji hayo pamoja na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria mmoja wa miliki wa nyumba hizo ambaye alikutwa katika eneo hilo wakati wa zoezi hilo maalum.
Zoezi maalum la kubaini kaya zilizojiunganishia huduma ya Maji kinyume na utaratibu katika eneo la Mbezi Goigi na kufanikiwa kubaini wizi mkubwa wa Maji unaofanywa na baadhi wakazi katika kaya hizo.
Upekuzi ukiendelea ambao uliweza kubaini mashine zinazotumika kuiba maji.
Moja ya magari ambayo yalikuwa wakiuziwa maji.
Usalama ukiwa unasimamiwa kwa kiwango cha juu.

TIPER yakabidhi gawio la bilioni 6 kwa wanahisa wake

$
0
0
Bodi ya Wakurugenzi ya kampuni ya Kuifadhi Mafuta ya Tanzania (TIPER) imekabidhi kwa Rais John Pombe Magufuli gawio la sh bilioni 3 ikiwa ni sehemu ya gawio la sh bilioni 6 kwa mwaka 2017 ambalo kampuni hiyo imetoa kwa wanahisa wake ambao ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Kampuni ya ADDAX-ORYX GROUP ya nchini Uswiss. 

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni hiyo Prof Abdulkarim Mruma alisema kiasi hicho ni ongezeko kutoka kiwango cha sh bilioni 1 kwenye miaka ya mwisho ya 2000 na wastani wa karibu sh bilioni 2 katika kipindi cha kati ya 2010-2013. “Uongozi wa Kampuni unaona fahari kubwa kuweza kusimamia uendeshaji na kuweza kukuza gawio kwa wanahisa wake.’’ Alisema. 

Akizungumzia mpango wa upokeaji wa Mafuta kwenye ghala moja ambapo kampuni hiyo inatarajia kuwa kituo pekee cha upokeaji wa mafuta yote yanayoingia nchini kupitia bandari ya Dar Es Salaam, Prof Mruma alisema manufaa yanayoyotarajiwa kupatikana kutokana na mpango huo yameshajadiliwana kupokelewa vyema na wadau wote. 

“ Faida za mpango huu zipo wazi ambazo ni pamoja na udhibiti bora wa kiwango cha mafuta kinachoingia nchini, kupunguza upotevu na wizi wa mafuta, kuzifanya gharama za ucheleweshaji wa meli zinazolipwa sasa kwa wamiliki wa nje wa meIi kuwa mapato ya serikali.’’ alitaja 

Alisema IIi kufanikisha mradi huu, Bodi ya Wakurugenzi ya TIPER imepitisha mpango mahususi wa uwekezaji wa zaidi ya Dolla za Marekani milioni ishirini na mbili (USD 22m) ndani ya kipindi cha 2018 mpaka 2019. 

“Tumeazimia kuongeza uwezo wa kuhifadhi mafuta kwa asilimia hamsini (50%) kutoka mita za ujazo laki mbili na kumi na tatu (213,000 cum) mpaka meter za ujazo laki tatu na kumi na tisa (319,000 cum) kwa kujenga matanki mawili mapya yenye ujazo wa mita za ujazo elifu thelathini kila moja na kukarabati tanki moja lililokuwa la mafuta ghafi lenye ujazo wa mita za ujazo arobaini na sita elfu.’’ Alifafanua. 

Alitaja azimio lingine kuwa ni Kutandika bomba la pili la mafuta ya Petroli kati ya Kurasini na Kigamboni Kuongeza uwezo wa kusukuma mafuta kwa zaidi ya asilimia hamsini (50%) kwa kujenga kituo kipya cha kusukumia mafuta ambacho kitakua na mashine sita (6) mpya pamoja na kukarabati mfumo wa kuzima mote iii kuweza kuongeza kiwango na kufikia viwango vinavyokuballiwa kimataifa iii kuhakikisha mafuta yako salama ndani ya ghala la TIPER. 

“Mpango huu wa upanuzi wa ghala unafanikishwa kwa fedha inayotokana na mapato ya ndani pamoja na mkopo wa Dolla milioni kumi na tano (USD 15m) toka benki.’’ alitaja 

Alisema mafanikio ya mradi huo yatakuwa ni chanzo cha kushughulikia miradi mingine kama Ghala maalumu la Forodha ambalo litavutia mafuta mengi kuingia nchini iii koboresha nguvu ya ushindani na kuifanya Bandari ya Dar Es Salaam kuwa Bandari mkakati itakayovutia uingizaji wa kiwango kikubwa cha mafuta kwa ajili ya Biashara ya nchi jirani katika ukanda huu. 

“Niwashukuru wadau wote upande wa Serikali na Sekta binafsi ambao walituwezesha kufikia matokeo mazuri ya pato halisi la Shilingi bilioni tisa nukta tisa (9.9 bn) kwa mwaka 2017 kutoka pato la shilling bilioni sita nukta tano tisa (6.5 bn) mwaka 2016, na kufanikiwa kuongeza gawio kwa kiwango hicho.’’ alisema.
Rais John Pombe Magufuli (katikati) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh bilioni tatu kutoka kwa Mwenyeki wa Bodi ya kampuni ya Kuifadhi Mafuta ya Tanzania (TIPER) Prof Abdulkarim Mruma ikiwa ni sehemu ya gawio la sh bilioni 6 ambalo kampuni hiyo imetoa kwa wanahisa wake ambao ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na pamoja na Kampuni ya ADDAX-ORYX GROUP ya nchini Uswiss. Wengine ni pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dr Phillip Mpango (kushoto kwake).

Airtel Money yaungana na serikali kurahisisha malipo kupitia mfumo wa GePG

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kwa utoaji wa huduma bora za Smartphone Airtel Tanzania leo imetangaza kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango kupitia kitengo chake cha (Government Electronic Payment Gateway) katika kutoa suluhisho la malipo rahisi ya papo kwa hapo kupitia huduma ya Airtel Money. Kupitia mfumo huo, wateja wa Airtel Money sasa wataweza kulipia malipo ya huduma mbali mbali pamoja na tozo za serikali mahali popote kutoka kwenye simu zao kama vile ushuru, karo na malipo mengine yoyote.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati akitangaza ushirikiano huo, Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda alisema kuwa “idadi ya wateja wa Airtel Money imekuwa ikikua siku hadi siku na hivyo kupelekea kufanikisha moja kati ya malengo ya serikali yetu ya kuhakikisha kuwa inafanikisha upatikanaji wa huduma za kifedha kila mahali yaani mjini na vijijini. Pia mafanikio haya leo hii yanapelekea kuwezesha ukusanyaji wa kodi na mapato mbalimbali  ya serikali, Airtel tunawahimiza na kuwapa taarifa wateja wa Airtel Money kuwa tumeunganishwa sasa na GePG hivyo waendelee kutumia mfumo huu rahisi kulipia malipo mbalimbali kupia simu zao wakiwa popote”

Mfumo wa GePG ni kwa ajili ya kila mtanzania. “Nachukua fursa hii kuwaomba watanzania kutumia mfumo huu kwani ni salama, rahisi na nafuu”, alisema Nchunda huku akiongeza kuwa Airtel Tanzania imedhamiria kuendelea kuhudumia wateja kwa ubora wa hali ya juu kwa kuongeza idadi ya mawakala wa Airtel Money ambao kwa sasa wanafikia zaidi ya elfu 55.”Vile vile, tunaendelea kuongeza mawakala kupitia usambazaji wa vioski vya Airtel Money na kuongeza uekezaji katika maduka ya Airtel Money Branch ambayo sasa tayari yanatoa huduma kama wakala wa kawaida  na pia kama wakala mkubwa ambapo hadi sasa hivi tumeshafungua matawi (Airtel Money Branch) zaidi ya 300 yanayotoa wigo mkubwa zaidi wa mawakala nchini.

“Wateja wa Airtel Money wanachotakiwa kufanya ili  kulipa kodi au tozo mbalimbali za serikali piga *150*60# kuchangua namba 5 halafu 3 kisha weka kiwango cha malipo ikifuatiwa na namba ya kumbukumbu ya malipo kisha kulipia huduma yoyote papo kwa papo kama vile TRA, faini mbali mbali, LUKU, DAWASCO, pasi ya kusafiria, kodi ya majengo pamoja na malipo mengine”, alisema Nchunda.
 Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda akiongea wakati wa  kutangaza kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango kupitia kitengo chake cha (Government Electronic Payment Gateway) katika kutoa suluhisho la malipo rahisi ya papo kwa hapo kupitia huduma ya Airtel Money. Kupitia mfumo huo, wateja wa Airtel Money sasa wataweza kulipia malipo ya huduma mbali mbali pamoja na tozo za serikali mahali popote kutoka kwenye simu zao kama vile ushuru, karo na malipo mengine yoyote. Kushoto ni Ofisa mwakilishi wa GePG kutoka wizara ya Fedha na Mipango Bw, Basil S. Baligumya na Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando.
Ofisa mwakilishi wa GePG kutoka wizara ya Fedha na Mipango Bw, Basil S. Baligumya akiongea wakati wa  kutangaza kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango kupitia kitengo chake cha (Government Electronic Payment Gateway) katika kutoa suluhisho la malipo rahisi ya papo kwa hapo kupitia huduma ya Airtel Money. Kupitia mfumo huo, wateja wa Airtel Money sasa wataweza kulipia malipo ya huduma mbali mbali pamoja na tozo za serikali mahali popote kutoka kwenye simu zao kama vile ushuru, karo na malipo mengine yoyote. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Jackson Mmbando.




Rais Magufuli atuma salamu za pongezi kwa Rais Nyusi wa Msumbiji

MPINA AUNDA KANDA MPYA YA ULINZI NA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UVUVI ZIWA VICTORIA

$
0
0
Picha ya pamoja ya Maafisa (waliosimama) walioteuliwa kusimamia rasilimali za uvuvi katika kanda maalumu kwenye Ziwa Victoria na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina mwenye koti jeupe kushoto kwake ni Mahamoud Mgimwa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji kulia ni Katibu Mkuu Uvuvi Rashid Tamatama na Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Magesa Bulayi.



NA JOHN MAPEPELE,DODOMA

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameunda Kanda mpya ya Ulinzi na Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Ziwa Victoria na kuteua maafisa wapya wataokuwa na jukumu la kudhibiti na kutokomeza uvuvi haramu na biashara haramu ya mazao ya uvuvi katika Ziwa Victoria ifikapo Desemba 2018.

Akizungumza jijini Dodoma mwishoni mwa wiki, Waziri Mpina amemteua Didas Mtambalike kuwa Mkuu mpya wa Kanda mpya ya Ulinzi na Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Ziwa Victoria huku akiunda kanda mbili za kiulinzi za Sengerema na Ukerewe .Pia Serikali imeanzisha Kituo cha Ukaguzi wa Mazao ya Uvuvi mkoani Singida na kuweka vizuizi katika maeneo yote yaliyoripotiwa kuwepo matukio ya utoroshaji wa rasilimali za uvuvi hapa nchini.

Maafisa wengine walioteuliwa na Waziri Mpina kuongoza kanda zingine ni pamoja na West Mbembati ambaye ataongoza Kanda ya Kagera, Vicenti Masui Munda Kanda ya Mwanza, Jairos Mahenge Kanda ya Mkoa wa Mara.Wengine ni Judith Mgaya atakayeongoza Kanda ya Kiulinzi Ukerewe na Roman Mkenda Kanda ya Mkoa wa Geita, Wencleslaus Luhasile aliyekuwa Afisa Uvuvi wa Wilaya ya Magu sasa ataongoza Kanda ya Kiulinzi ya Sengerema na Samson Mboje kutoka Kituo cha Usimamizi na Ulinzi wa Rasilimali Kanda ya Mwanza, sasa ameteuliwa kuongoza Kanda ya Simiyu/Magu.

Aidha Waziri Mpina alisisitiza kuwa katika operesheni inayoendelea Serikali inaandaa utaratibu wa kwenda na mahakama inayotembea ili watuhumiwa na wahalifu wahukumiwe pale pale wakiwa na mashahidi wao.Kuhusu maendeleo ya wavuvi wadogo, Waziri Mpina amesema Wizara yake kwa kushirikiana na Benki ya NMB inawafuatilia wavuvi na kuwafungulia akaunti ambapo hadi sasa zaidi ya wavuvi 20,000 wamefikiwa.

Amesema utafiti umebaini kuwa asilimia 98 ya wavuvi ni vibarua wa matajiri ambapo mapato yanayotokana na uvuvi kila wanapotoka kuvua hugawanywa nusu na tajiri wao ambaye ndiye mmliki wa chombo na nusu iliyobaki kugawana kila mvuvi aliyekuwa katika chombo hicho hali iliyowafanya wavuvi kote nchini kuendelea kuwa masikini na kuwanufaisha matajiri wachache.

Vile vile, Waziri Mpina amesema kuwa Operesheni Sangara awamu ya tatu itaendelea na kwa maji baridi yote ikiwemo Ziwa Tanganyika, Nyasa, Rukwa, Nyumba ya Mungu na Mtera na mito ili kuhakikisha rasilimali hiyo inalindwa na kunufaisha taifa.Mbali na hatua hiyo Waziri Mpina ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi nchini (TAFIRI) kufanya utafiti ili kujua kiasi cha samaki waliopo katika Ziwa Victoria baada ya kuendesha Operesheni Sangara kwa miezi sita sasa.Kuhusu viongozi waadilifu na wanaosimamia kikamilifu ulinzi wa rasilimali uvuvi Waziri Mpina amesema Wizara yake itaendelea kuwatambua na kuwapongeza wananchi na viongozi wanaofanya vizuri kwenye usimamizi wa raslimali za uvuvi nchini.

Alisema katika kipindi hiki Wizara yake inatambua mchango wa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Kipole na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara, Dkt. Vicenty Anney pamoja na Afisa Mtendaji wa Kata ya Kagya Wilaya ya Bukoba, Beatrice Lugemalila.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Kilimo, Mifugo na Maji, Dk. Christine Ishengoma alisema mawaziri waliopita katika wizara hiyo walifanya kazi nzuri lakini ubunifu wa kipekee uliofanywa na Waziri Mpina umeiwezesha sekta ya uvuvi kuongeza mapato kutoka sh bilioni 18.5 katika mwaka wa fedha 2016/2017 hadi kufikia sh bilioni 26.3 mwaka wa fedha 2017/2018 fedha ambazo zitasaidia uboreshaji wa huduma za kijamii katika maeneo yote nchini.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji, Katani Ahmad Katani alipongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya kulinda rasilamili za Taifa na kutaka juhudi hizo kuwa endelevu kwani pamoja na kuwa na eneo kubwa la maji bado uvuvi haujaweza kunufaisha Taifa.Katani ambaye pia ni Mbunge wa Tandahimba mkoani Mtwara aliishauri Serikali kuangalia uwezekano wa kufungua maduka yake ya zana za uvuvi ili kuwarahishia wavuvi kupata zana hizo kwa wakati na zenye ubora unaotakiwa kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Uvuvi-Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Rashid Tamatama alisema suala la ulinzi wa rasilimali za uvuvi litakuwa ni moja ya majukumu ya kila siku ya watumishi wa wizara hiyo ili kuhakikisha Taifa linanufaika vya kutosha na rasilimali hizo.

MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA YAJA KIVINGINE

MZEE WA MIAKA 71 AKUTWA NA NYARAKA BANDIA ZA SERIKALI .

$
0
0
. ALIKUWA NI MTUMISHI WA SERIKALI OFISI YA MKUU WA WILAYA -MOSHI
. AKUTWA NA VYETI 240 NA MIHURI 159.
. RPC KILIMANJARO ATAKA WALIOCHONGEWA VYETI NA MZEE HUYO KUJISALIMISHA.

Na Dixon Busagaga ,Moshi

JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mzee wa miaka 71 na watu wengine watatu baada ya kukutwa na Nyaraka  bandia za serikali  240 ambazo wamekua wakiziandaa kwa njia ya udanganyifu pamoja na Mihuri 159 na kuuzwa kwa bei ya Sh 20,000.

Nyaraka zilizo kamatwa ni pamoja na Vyeti vya kuzaliwa ,vyeti vya ndoa ,vyeti vya ubatizo,vyeti vya Kliniki na matamko ya vizazi na vifo pamoja na mihuri mbalimbali miongoni mwao ikionyesha ni ile inayotumika wakati wa usajili vizazi na vifo katika manispaa ya Moshi na Kitete mkoani Tabora.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishana Msaidizi wa Polisi,Hamisi Issa alisema vifaa vingine vilivyo kamatwa ni pamoja na Mashine moja ya kuandikia (Type Writer) na kifaa cha kuwekea namba huku akiwataja watuhumiwa kuwa ni pamoja na Athuman Selemani (71) anayetajwa kuwa aliwahi kuwa mtumishi wa serikali katika ofisi ya mkuu wa wilaya .

Wengine ni Justine Mziray (55) anayetajwa kuwa ni mtaalamu wa kuchonga mihuri,Sporah Daud anayetajwa kushiriki katika uandaaji wa nyaraka hizo kwa kuchapa maandishi kwa kutumia mashine maalumu (Type writer) na Costa Lyatuu  anayetajw kuwa mtaalamu wa kughushi sahihi.
 Sehemu ya nyaraka  mbalimbali za bandia zilizokutwa kwa mtuhumiwa huyo
 JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mzee wa miaka 71 na watu wengine watatu baada ya kukutwa na Nyaraka  bandia za serikali  240 ambazo wamekua wakiziandaa kwa njia ya udanganyifu pamoja na Mihuri 159 na kuuzwa kwa bei ya Sh 20,000.
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishana Msaidizi wa Polisi,Hamisi Issa akionesha baadhi ya mihuri iliyokutwa kwa mtuhumiwa huyo
 Mihuri iliyokuwa ikitumika
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishana Msaidizi wa Polisi,Hamisi Issa akionesha baadhi ya mashine aliyokuwa akitumia mtuhumiwa huyo kutengenezea nyaraka bandia za serikali

MKURUGENZI WA ZAMANI NSSF AKABIDHI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA

$
0
0
Aliyekuwa Mkurugenzi mkuu wa Shirika  la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF ,Professa Godius Kahyarara akimkabidhi  baadhi ya nyaraka MKurugenzi mkuu mpya wa NSFF Ndugu William  Erio kwenye makabidhiano ya ofisi leo makao makuu ya Shirika hilo.
 Mkurugenzi mkuu wa Shirika  la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF ,Professa Godius Kahyarara akizungumza jambo na MKurugenzi mkuu mpya wa NSSF Ndugu William  Erio mara baada ya makabidhiano ya ofisi leo makao makuu ya Shirika hilo.

MATAYARISHO JENGO LA KIHISTORIA MJI MKONGWE YAANZA RASMI

$
0
0

Na Mwashungi Tahir Maelezo 

Matayarisho ya matengenezo ya Jengo la Kihistoria la Mji mkongwe la Beit el Ajaib yameanza rasmi kwa ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Oman

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mji Mkongwe Issa Makarani Sariboko alieleza hayo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya maandalizi yanavyoendelea katika jengo hilo Forodhani.

Alisema ujenzi wa jengo hilo mashuhuri katika Ukanda wa Afrika Mashariki lililoporomoka mwaka 2012 litagharimu zaidi ya Dola za Marekani milioni nne na nusu na matengenezo yake yatachukua miezi 18.

Aliwaeleza waandishi wa habari kwamba wataalamu wazalendo wamemaliza kufanya uchambuzi wa matengenezo hayo na kazi ya ujenzi wa jukwaa kuelekea sehemu ya juu unaendelea.

“Tayari wataalamu wetu wamemaliza kufanya ufafanuzi wa jumba lote kuanzia sehemu ya juu iliyoporomoka, sehemu za ndani na eneo la chini ya ardhi ya jengo hilo’’, alisema Mkurugenzi Makarani.

Alisema kutakuwa na mchanganyiko wa timu ya wataalamu kutoka nchi za nje na wataalamu wazalendo wa Zanzibar ili kupata ufanisi mzuri wa ujenzi huo.

Nae Mkurugenzi wa Makumbusho Salim Kitwana Sururu alisema Serikali ya Oman ilifikia makubaliano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya kulifanyia matengenezo jengo hilo la kihistoria lililohifadhi kumbukumbu muhimu za tawala zilizopita.

Muhandisi wa Mji Mkongwe Suhad Sultani Alawi alitoa wito kwa wananchi wanaotumia eneo hilo kuwa tahadhari kubwa wakati wa matengenezo ya jengo hilo kwa kulinda usalama wao.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

SHILOLE AAMUA KUSOMA KIINGEREZA KWA WATAALAMU WA LUGHA DUNIANI

$
0
0
Baada ya kuchekwa sana kwa kutojua kiingereza, msanii wa bongo flava Shilole aingia kwenye mkataba na shirika la uingereza British Council Tanzania ili kujifunza lugha hiyo. 

Mbali ya muziki, msaani huyo anajulikana sana kwa kuwa na hamasa ya kuongea kiingereza bila kujali makosa ambayo anayafanya. Wiki iliyopita tuliona video ikitrend ya mwanadada huyo akijaribu kusema “Subscribe” alivyokua anaongelea kuhusu mwimbo wake mpya.

Shirika la Uingereza British Council Tanzania, limefurahi Shilole ameamua kutaka kujiendeleza katika lugha ya kiingereza ambayo itamsaidia katika kazi yake kama msanii. 

Hususani kumpa fursa za kimataifa zaidi. Angela Hennelly, Country Director, amesema kuwa ni fursa nzuri kwa Shilole kujua lugha ya Kiingereza na amempongeza kwa hatua hiyo aliyoichukua. Ameendelea kusema kuwa hii itamfungulia milango mingi ya fursa kulingana na jinsi uchumi wa dunia unavyokua na changamoto wanazozipata haswa wasanii.

Angela ameendelea kusema kuwa anategemea hii fursa itawapa moyo vijana kufikiria pia kujiendeleza katika lugha ili waweze kufanya mawasiliano kwa urahisi katika shughuli zao za kila siku haswa kwa upande wa ajira.

“SHILOLE DECIDES TO LEARN ENGLISH WITH THE WORLD’S LEADING EXPERTS?

Tanzanian “Bongo Flava” artist Shilole has signed a contract with the British Council Tanzania to learn English. This comes after videos trending showing the star keen to speak English but experiencing some challenges. This has led to many people following her and being eager to hear her speak.
The British Council is the United Kingdom’s international organisation for cultural relations and educational opportunities. Angela Hennelly the Country Director, applauded Shilole for her determination in wanting to know the language, as it will open many doors and opportunities in this fast-paced global economy, especially as an artist. She hopes that this will be an encouragement especially to young people to try to improve their communication skills so as to be able to tap into employment and other opportunities.

JWTZ KUADHIMISHA SIKU YA MASHUJAA KWA KUPIMA AFYA ZA WANANCHI BURE

$
0
0
Na Khadija Seif,Globu ya jamii

JESHI la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) limesema litatoa huduma ya kupima afya za wananchi bure katika mikoa mbalimbali ukiwemo Mkoa wa Dar es Salaam.

Wakati Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo atatembelea wagonjwa katika Hospitali Kuu ya jeshi Lugalo.Akizungumza Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa jeshi hilo Kanali Ramadhani Dogoli amesema huduma hiyo itatolewa huduma hiyo Julai 25 mwaka huu.

Amesema Julai 25 ya kila mwaka huadhmishwa Siku ya Mashujaa wetu na hivyo watatumia siku hiyo kushiriki kwenye shughuli za kijamii.Amesema kuwa Makao Makuu ya JWTZ(Ngome) watakuwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Saalam.

"Wanachi wananchi watakaofika viwanjani hapo watapata fursa ya kupima shinikizo la damu ,kisukari ,uchunguzi wa kinywa na meno, uzito, kupima VVU kwa hiyari pamoja na kutoa ushauri nasaha.Upimaji huo utaanza saa moja asubuhi."Kila mwaka inapofika Julai 25 huwa inaadhiishwa siku ya mashujaa.Kwa JWTZ pamoja na mambo mengine huwa tunaadhmisha siku hiyo kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii,"amesema.

Pia JWTZ watafanya usafi katika maeneo mbalimbali na kwamba mbali ya Dar es Salam wanajeshi walioko mkoani Mbeya, Tabora na Pwani nao watashiriki kwenye shughuli za kijamii.Ameongeza kwa Dar es Salam JWTZ watafanya usafi katika katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke, hospitali ya Mbagala Zakhiem, hospitali ya Dar group na stendi ya mabasi ya Mbagala na Temeke.

Pia soko la Mbagala ,Temeke,Tandika na kutakuwa na upandaji wa miti katika shule ya Wailes.Ameeleza kwa upande wa Kamandi ya jeshi la nchi kavu Msangani amesema watatoa huduma ya vipimo kuanzia saa mbili asubuhi katika Hospitali ya Galagaza na kutoa misaada katika kituo cha watoto yatima Mwanalugali kilichopo Msangani.

Amesema kwa upande wa Kamandi ya jeshi la Anga itafanya usafi katika Shule ya Msingi ya Changanyikeni na Jeshi la Kamandi ya jeshi la wanamaji watafanya usafi katika Hospitali ya Vijibweni, Hospitali ya Kigamboni na soko kuu la Kigamboni.

Dogoli amesema Brigedi ya Nyuki Zanzibar itafanya usafi soko la Mombasa ,Sebuleni Majumba ya Wazee na Soko la Mwanakwerekwe.Wakati Brigedi ya Faru Tabora itafanya usafi katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Manyara.

TRC WAENDELEA KUTOA ELIMU VIJIJINI KUHUSU MRADI WA UJENZI WA RELI YA KISASA-SGR PAMOJA NA MRADI WA UBORESHAJI WA RELI YA KATI DAR- ISAKA,

$
0
0
Uongozi wa shirika la reli Tanzania - TRC kwa kutumia timu ya mawasiliano wamedhamiria kuwashirikisha watanzania kwa kufanya kampeni ya uhamasishaji ili kufahamu hatua za miradi pamoja na kutoa elimu kuhusu miradi inayosimamiwa na kuratibiwa na shirika la reli Tanzania, miradi hiyo ni uboreshaji wa reli ya kati Dar- Isaka pamoja na mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa - SGR ili kuwapatia uelewa na kuwakumbusha wananchi kuwa miradi hiyo ni mali ya umma na kila mtanzania ana haki ya kuilinda na kuithamini, ili kuwezesha miradi kufanikiwa.
Lengo la uboreshaji wa reli ya kati pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa -SGR ni kutoa huduma ya usafiri wa kuaminika na kukuza upatikanaji wa huduma bora nchini. Ujenzi wa reli ya kisasa pamoja na maboresho ya reli ya kati yatasaidia kuinua uwezo wa kubeba mizigo kwa reli zote, kuongezeka kwa mwendo, kuokoa muda wa safari kwa kipindi kirefu na kupelekea kukua zaidi kiuchumi, kuanzia ngazi za familia mpaka maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Katika kufikia malengo, timu ya mawasiliano TRC mpaka sasa imefanya kampeni ya uhamasishaji kwa kutoa elimu mwezi Julai 2018 kwa kutembelea wilaya ya kilosa na vijiji vyake ambavyo ni Mkadage, Munisagara, Mzaganza , Kikundi ,Mwasa na Kidete. Kampeni ya uhamamsishaji juu ya miradi ya shirika la reli yaani mradi wa uboreshaji wa reli ya kati pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa-SGR itaendelea katika mikoa ya Dodoma,Singida,Tabora na Shinyanga.
Tangu kampeni ya uhamasishaji wa uelewa kuhusu miradi ianze wanananchi wamepata fursa ya kujua faida za miradi wakati wa ujenzi ambazo ni kuwepo kwa fursa za ajira, kukua kwa kipato cha wananchi maeneo ya miradi na kujengewa ujuzi kwa wote watakaoshiriki kwenye shughuli za ujenzi.

Pia wananchi wamepata fursa ya uelewa wa alama zitakazotumika katika miundo mbinu ya reli katika kipindi cha uboreshaji na ujenzi wa reli, Lengo kila mwananchi apate uelewa, atii sheria na achukue tahadhari mara baada kuona alama hizo na kuhamasishwa zaidi kuchukua tahadhari za kiafya na tabia zozote hatarishi ili kuepuka maambukizi ya magonjwa ya zinaa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa kuwa miradi imeletwa ili wananchi watanzania wanufaike na miradi na si kuleta maafa kwa wananchi. 

Vilevile kampeni hizi zimeweza kuwafikia wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari zilizopo karibu na maeneo ya reli.Wanafunzi wameweza kupata elimu kuhusiana na alama mbalimbali zitakazotumika wakati wa ujenzi, elimu kuhusiana na tabia hatarishi zinazoweza kutokea kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu wakati wa ujenzi na kusababisha athari mbalimbali kama vile mimba za utotoni na magonjwa kama vile UKIMWI, Kaswende ,Kisonono na magonjwa mengine ya zinaa.

Imetolewa na kitengo cha Uhusiano kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TRC 
 Mtaalamu wa masuala ya kijamii kutoka Shirika la Reli Tanzania -TRC Bi Catherine Mroso  akitoa elimu kuhusu faida, Changamoto na mambo ya kuzingatia kuhusu miradi inayoratibiwa na kusimamiwa na TRC kwa wanakijiji wa Kikundi katika wilaya ya Kilosa  mkoani Morogoro,mwezi Julia 2018.
 Mhandisi kutoka Shirika la reli Tanzania Bwana Christopher Mang'wela akitoa elimu kuhusu mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa - SGR,faida za mradi,Changamoto na mambo ya kuzingatia katika kijiji cha Kikundi wilaya ya kilosa mkoani Morogoro
 Mhandisi wa TRC Bwana Edwin Leonard akitoa elimu kuhusu Mradi wa Uboreshaji wa reli ya kati Daressalaam- Isaka  kwa wanakijiji wa Kidete wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro katika kampeni ya uhamasishaji na uelewa kuhusu Miradi inayosimamiwa na TRC
 Mtaalamu wa masuala ya kijamii Bi Grolia Mrengo kutoka upande wa mkandarasi wa Yap Markez wa ujenzi wa Reli ya kisasa akiambatana na timu ya mawasiliano TRC kutoa elimu na uelewa wa mambo yanayotakiwa kuzingatiwa kipindi cha ujenzi wa Reli ya kisasa kwa awamu ya pili Morogoro - Makutupola katika kijiji cha Mzaganza wilaya kilosa mkoani Morogoro.
 Mtalaamu wa masuala ya kijamii kutoka upande wa mkandarasi wa mradi wa uboreshaji reli ya kati Daresalaam- Isaka Bi Mary Frank akiambatana na timu ya mawasiliano TRC akitoa elimu ya matumizi ya alama za tahadhari katika njia ya Reli kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mwasa wilaya ya Kilosa,mkoani Morogoro.
 Mtaalamu wa masuala ya kijamii TRC Bi Catherine Mroso akitoa elimu kuhusu miradi inayosimamiwa na mambo ya kuzingatia kipindi cha mradi kwa wanafunzi wa Shule ya sekondari kidete wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
 Wanakijiji wa kidete wilaya ya kilosa mkoani Morogoro wakifuatilia kwa umakini  taarifa kuhusu  miradi zinazotolewa na timu ya mawasiliano kutoka TRC.

Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images