Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

TAMUFO YAZIONYA KAMPUNI ZA KUUZA MUZIKI ZA NCHINI KENYA

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

UMOJA wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) umeyataka makampuni ya Kenya yanayouza nyimbo za wanamuziki wa Tanzania bila kufuata utaratibu kuacha kufanya hivyo mara moja.

Ombi hilo limetolewa na Rais wa TAMUFO Dk.Donald Kisanga mjini Arusha juzi wakati viongozi wa TAMUFO walipofanya mkutano na Vikundi mbalimbali vya Kwaya ili kuwajengea uelewa na kuhakikisha wanafaidika na kazi zao za muziki na kuwaunganisha na fursa za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa gharama nafuu kupitia umoja huo.

"Natoa onyo kali kwa makampuni ya Kenya yanayouza nyimbo zilizoimbwa na watanzania na kurekodiwa na Tanzania kuuzwa kenya Kinyume cha Taratibu na kuwakosesha wanamuziki wa Tanzania Kufaidika na kazi zao na serikali kukosa mapato kupitia kodi" alisema Kisanga

Alisema katika mkutano huo Kampuni ya Kenya ya Africha ilikiri kosa na Kuahidi kuwalipa Wanamuziki Wa Tanzania Pesa zao bila masharti yoyote baada ya kiziuza bila ya kufuata taratibu na kuwa TAMUFO na kampuni hiyo watatiliana saini za makubaliano kwenye mkutano huo. 

Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stellah Joel alivitaja Vikundi vilivyohudhuria mkutano huo kuwa ni Kwaya Kuu Habari Njema na Kwaya ya UinjilistI za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mjini kati Arusha, Kwaya kongwe za Ulyankulu Mapigano na Ulyankulu Barabara ya 13 zote za Tabora.
Wadau wa muziki kutoka Tanzania na Kenya wakiwa katika mkutano na viongozi wa Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO), ulioshirikisha vikundi mbalimbali vya Kwaya ili kuwajengea uelewa na kuhakikisha wanafaidika na kazi zao za muziki unaoendelea jijini Arusha. Kushoto mbele mwenye tai ni Rais wa TAMUFO Dk. Donald Kisanga.
Majadiliano yakiendelea.

WAZIRI MPINA ARUHUSU UINGIZAJI WA NYAVU ZA KUVULIA SAMAKI NA DAGAA KUTOKA NJE YA NCHI.

$
0
0
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameruhusu uingizaji wa vyavu za kuvulia samaki na dagaa kutoka nje ya nchi baada ya kubaini kuwa viwanda vya kuzalisha nyavu hizo vilivyopo nchini kushindwa kuhimili mahitaji ya soko la ndani na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wavuvi.

Akizungumza katika kikao cha tathmini ya operesheni Sangara 2018 jijini Dodoma, Waziri Mpina amemuagiza Katibu Mkuu- Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Rashid Tamatama kuhakikisha kuwa katika kipindi cha siku 14 awe amekamilisha kupitia maombi na kuruhusu uingizaji wa nyavu hizo kutoka nje ya nchi. Pia kuweka utaratibu ambao hautaathiri soko la viwanda vya ndani.

Mbali na hilo Waziri Mpina ameigiza wizara yake kuandaa mkakati wa kudhibiti upotevu wa mapato, usimamizi na udhibiti wa rasilimali za uvuvi nchini ili kuondoa mianya yote ya upotevu wa mapato ya Serikali na kuweka ulinzi thabiti wa rasilimali za uvuvi.

Pia ametaka Wizara hiyo kufanya mapitio ya mkakati wa ufugaji wa samaki kwenye maji, kufufua vituo vya kuzalisha vifaranga na kufanya tathmini ya uwekezaji wa sekta binafsi na kuainisha mahitaji ya sasa ili kuongeza uzalishaji utakaochangia kupunguza nguvu ya uvuvi kwenye maziwa na hivyo kutokomeza uvuvi haramu, kuongeza ajira na upatikanaji wa malighafi za viwanda nchini.

Akizungumzia matokeo ya operesheni Sangara 2018, Waziri Mpina alisema jumla ya watuhumiwa 3,998 walikamatwa kwa makosa mbalimbali na kutozwa faini na wengine kufikishwa Mahakamani,

nyavu haramu 575,152, makokoro 11,144 na kamba za kokoro zenye urefu wa mita 859,304 zilikamatwa na kuteketezwa kwa moto.Pia ndoano 1,910, 135 zisizoruhusiwa kisheria ziliharibiwa.

Pia kilo 359,869 za samaki wasioruhusiwa zilikamatwa na kutaifishwa na Serikali ambapo kilo 176,780 za samaki wachanga na wazazi ziligawiwa bure kwenye taasisi mbalimbali zikiwemo shule,magereza,hospitali na watu wenye mahitaji maalum huku kilo 183,059 za samaki wakavu (kayabo) pamoja na kilo 5,889 za mabondoziliuzwa kwa njia ya mnada.

Alizungumzia mafanikio ya operesheni hiyo, Waziri Mpina alisema miezi 6 (Julai-Disemba 2017) kabla ya operesheni Sangara 2018 jumla ya sh. Bilioni 8.5 zilikusanywa ikilinganisha na jumla ya sh. Bilioni 17.7zilizokusanywa miezi 6 (Januari- Juni 2018) kipindi cha operesheni.

Akitolea mfano Soko la Samaki la Kirumba jijini Mwanza, Waziri Mpina alisema mapato yake yameongezeka kutoka sh milioni 206.3 katika kipindi cha Julai-Dis 2017 kabla ya kuanza operesheni na kufikia sh milioni 848.3 katika kipindi cha Januari hadi Juni 2018 baada ya kuanza operesheni hii inaonesha kuwa kwa kipindi cha miezi sita mapato katika soko hilo yameongezeka mara nne.

Alisema jumla ya makusanyo ya sh.bilioni 26.3 yalikusanywa katika mwaka wa fedha 2017/2018 ukilinganisha na makusanyo ya jumla ya shilingi bilioni 18.5 yaliyokusanywa katika mwaka wa fedha 2016/2017. Aidha katika kutekeleza operesheni hiyo jumla ya sh. Bilioni 9.3 zilikusanywa na Serikali kutokana na tozo,faini na mauzo ya mazao ya uvuvi yaliyotaifishwa na Serikali.

Pia mauzo ya sangara nje ya nchi yameongezeka kutoka tani 26,000 mwaka 2016/2017 na kufikia tani 26,700 katika mwaka 2017/2018,urahisi wa upatikanaji wa samaki wenye ukubwa unaokubalika kisheria, kuongezeka kwa ukubwa wa samaki wanaochakatwa viwandani huku mahitaji ya vyavu halali yameongezeka na wananchi kujitokeza kwa wingi kuunga mkono vita ya uvuvi haramu kwa kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo vya uvuvi haramu.

Aidha Waziri Mpina alisema katika operesheni hiyo walibainika baadhi ya watendaji wa Serikali,Madiwani,Wenyeviti wa Halmshauri,Wabunge wakihusika kufadhili uvuvi haramu na kwamba tayari majina ya viongozi hao yameshawasilishwa kwenye vyombo vya dola kwa hatua zaidi huku kwa upande wa watumishi wa wizara hiyo 12 wakisimamishwa kazi. 

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais(TAMISEMI), Suleiman Jafo aliwaagiza Wakuu wa Mikoa kuwabainisha kwa majina watumishi wote wa Serikali ngazi ya Serikali za Mitaa waliohusika kushiriki ama kufadhili uvuvi haramu na kuyafikisha ofisini kwake ili aweze kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria.Waziri Jafo alisema suala la ulinzi wa rasilimali za Taifa ni watanzania wote hivyo kama kuna baadhi ya watumishi wanashiriki hujuma katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya tano hawatapata nafasi kwani uvuvi ni miongoni mwa sekta inayotegemewa hasa katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

‘Kama Taifa tuna kila sababu ya kuungana katika mapambano ya uvuvi haramu hasa katika kipindi hiki cha uchumi wa viwanda,ofisi yangu haitasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu kwa watumishi wote watakaobainika kutajwa kushiriki uvuvi haramu”alisema Jafo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge,Kilimo, Mifugo na Maji, Mahmoud Mgimwa alimtaka Waziri Jafo kusimamia kikamilifu agizo lake kwani baadhi ya watendaji walioko chini ya wizara yake ndio wafadhili wakubwa wa mtandao wa uvuvi haramu na kukwamisha juhudi za Serikali za kumaliza tatizo hilo.

Mgimwa alisema mapato mengi ya uvuvi yalikuwa yanaishia mifukoni mwa watu wachache lakini kwa juhudi na ubunifu mpya uliofanywa na Waziri Mpina na wizara yake umewezesha kukusanya sh. bilioni 9.3 katika kipindi cha miezi sita na fedha hizo zimeingia mfuko mkuu wa Taifa na kwenda kusaidia kwenye ununuzi wa ndege,ujenzi wa reli, umeme,maji,elimu bure na uboreshaji wa sekta ya afya.

Kamanda Mkuu wa Operesheni Sangara 2018, Emanuel Bulai alisema operesheni hiyo imebaini kuwepo uvunjifu mkubwa wa sheria ikiwemo matumizi ya zana haramu za uvuvi, utoroshaji mkubwa wa mazao ya uvuvi na raia wa kigeni kuingia nchini na kufanya biashara ya samaki na mazao na yake bila kufuata Sheria za nchi.

WAKULIMA WAIOMBA SERIKALI KUWAONGEZEA MAENEO YA KILIMO

$
0
0
Wakulima katika eneo la Dakawa Wilayani Mvomero, wameiomba Serikali kuwaongezea eneo ambalo halitumiki kwa shughuli yoyote ile waweze kulitumia kwa kilimo cha mpunga.

Maombi hayo yametolewa baada ya kukamilika kwa ukarabati wa eneo lenye ukubwa wa hekta (2000), ambapo wananchi wamepata hamasa ya kulima baada ya kuona mafaniko ya tokanayo na kilimo cha umwagiliaji.

Akizunguma na waandishi wa habari katika skimu ya Dakawa, Mhandisi wa kanda ya Mororgoro kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Senzia Maeda, amesema Serikali kupitia Tume hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Misaada la Marekani USAID pamoja na kampuni ya SDM Smith ambayo imesanifu ukarabati wa eneo la awali imeshafanya upembuzi yakinifu kwa Hekta (500) katika hizo hekta (1000) na amesema kuwa makablasha ya zabuni yapo tayari.

“Hatua inayoendelea kwa sasa ni kwa Serikali kuu kupitia Tume kutafuta mfadhili kwa ajili ya kuendeleza hilo eneo.” Alisisitiza Maeda. Na aliongeza kwa kusema kuwa Serikali ilifikia uamuzi wa kuendeleza eneo la Dakawa baada ya kuridhishwa na ukulima wa kisasa

Awali, Akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero, Bw. Florent Kyombo amesema pamoja na eneo hilo kuwa katika hatua nzuri ya uendelezwaji, Idara ya kilimo kupitia serikali ya wilaya na wataalam wa kilimo imeweza kuthibiti panya waharibifu wa mazao pamoja na ndege aina ya kwelea kwelea kwa kuharibu mazalio yao yote pamoja na suala zima la kuwasadia wakulima kupata mikopo katika baadhi ya mabenki nchini.

Bw. Arcado Ruhengiza ni mmoja wa wakilima katika skimu ya Dakawa ambapo yeye alisema kuwa endapo serikali itaongeza eneo kwa ajili ya kilimo cha mpunga, itawawezesha wakulima wengi zaidi kulima kisasa na kukuza sekta ya kilimo nchini kutokana na mafanikio waliyoyapata kupitia shamba hilo.

Mhandisi wa kanda ya Mororgoro kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Senzia Maeda, akiongea kuhusu upanuzi wa eneo lenye ukubwa wa Hekta (1000) kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji katika skimu ya Dakawa, wilayani Mvomero.
Ghala la kuhifadhia mazao lililojengwa na serikali katika skimu ya Dakawa wilayani Mvomero, ili kuweza kuwasaidia wakulima kuuza mazao yako kwa bei nzuri.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Bw. Florent Kyombo akiongea na waandishi wa Habari Ofisini kwake kuhusu mpango mzuri wa Serikali kwa wakulima wa kilimo cha mpunga kinachofanyika katika skimu ya Dakawa.
Katika Picha, Mkulima Bw. Arcado Ruhengisa akitoa Ombi la Upanuzi wa eneo lenye ukubwa wa Hekta (1000) kwa Serikali kupitia baadhi ya vyombo vya habari, ili wakulima waweze kongeza pato la Taifa, ajira kwa vijana na chakula kupitia kilimo cha umwagiliaji.




KANGI LUGOLA ATEMBELEA KITUO CHA UCHAPAJI NYARAKA ZA UHAMIAJI,KILICHOPO MTONI KIJICHI,JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola(wapili kutoka kushoto), akimsikiliza Mchapaji wa nyaraka mbalimbali zinazotumiwa na Idara ya Uhamiaji,Enos Lwinga, wakati alipotembela kiwanda cha uchapaji nyaraka hizo kilichopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam.Wakwanza kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dk. Anna Makakala .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola(wapili kutoka kushoto), akimsikiliza Mchapaji wa nyaraka mbalimbali zinazotumiwa na Idara ya Uhamiaji,Enos Lwinga, wakati alipotembela kiwanda cha uchapaji nyaraka hizo kilichopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam.Wakwanza kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dk. Anna Makakala .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akikagua  nyaraka mbalimbali zinazotumiwa na Idara ya Uhamiaji,  alipotembela kiwanda cha uchapaji nyaraka hizo kilichopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam.Kulia  ni  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dk. Anna Makakala
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dk. Anna Makakala, akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola(kushoto), wakati waziri alipotembela kiwanda cha uchapaji nyaraka hizo kilichopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mtumishi wa Idara ya Uhamiaji ,Eva Kikoti  akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), wakati waziri alipotembela kiwanda cha uchapaji nyaraka hizo kilichopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam . Kulia  ni  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dk. Anna Makakala.

“LAMBALAMBA MARUFUKU MKOANI SONGWE”-CHIKU GALLAWA

$
0
0
Waganga wote wa jadi wanaopiga ramli chonganishi maarufu kama Lambalamba wamepigwa marufuku kufanya shughuli hizo mkoani Songwe huku wenyeviti wa vijiji ambavyo lambalamba watabainika kuendelea na shughuli hizo, hatua kali dhidi yao zitachukuliwa.

Marufuku hiyo imetolewa mapema leo na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa katika kikao cha wadau wa Afya mkoani hapa ambapo ameeleza kuwa changamoto mojawapo ya sekta ya afya ni uwepo wa waganga wa jadi ambao huwapotosha wananchi kwa imani zisizo za kweli.

Gallawa amesema, “Hatutaki kuona wala kusikia hivi vikundi vya vya lambalamba, kazi yao kubwa ni ulaghai na kuwaibia fedha wananchi, na ninaagiza, mwenyekiti yeyote wa kijiji atakayebainika kuwaendekeza hawa watu tunaanza naye kumchukulia hatua kali za kisheria”.

Ameongeza kwa kuwaagiza wakuu wa wilaya zote mkoani hapa wasimamie kuhakikisha wananchi hawatapeliwi na lambalamba hususani wilaya za Mbozi na Ileje ambako lambalamba wameonekana mara kwa mara.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Waganga wa Jadi na Machifu Mkoa wa Songwe Mwenenzunda Mteleshwa amesema kuwa yeye hawatambui lambalamba hivyo serikali iwachukulie hatua za kisheria kwakuwa wanaenda kinyume na taratibu za utoaji wa huduma za jadi.

Wakati huo huo Gallawa amezitaja changamoto nyingine katika sekta ya afya mkoani hapa ni uwepo wa ugonjwa wa ebola nchi jirani ya Congo, upungufu wa vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na uwepo wa magonjwa yanayosababishwa na uchafu kama vile kipindupindu.

Gallawa amefafanua kuwa serikali imeweka mikakati ya kuboresha sekta ya Afya Mkoa wa Songwe kwa kutoa shilingi bilioni 2.7 kwa ajili ya uboreshaji wa vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na Kuimarisha huduma za kitabibu kwa kuipandisha hadhi Hospitali ya Wilaya ya Mbozi ili itumike kama Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe.

Ameongeza kuwa mkoa unatarajia kuzindua mkakati wa usafi na mazingira ukiwa na kauli mbiu ya “Kataa uchafu Songwe” lengo likiwa ni kupambana na magonjwa yanayosababishwa na uchafu na kutunza mazingira.
Mkuu wa Mkoa wa Chiku Gallawa akizungumza katika kikao cha wadua wa Afya kilichofanyika katika chuo cha Uuguzi Mwambani Mkwajuni-Songwe, Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samwel Jeremia na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje Joseph Mkude.

MKURUGENZI TARIME MJI ATAGANZA MGOMBEA UDIWANI KATA YA TURWA KUWA MSHINDI, APITA BILA KUPINGWA.

$
0
0
Na Frankius cleophace Tarime.

Mkurugenzi wa Halamshauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa ameamua kumutangaza aliyekuwa Mgombea udiwani kata ya Turwa kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi Bw Chacha Mwita Ghati kwa madai kuwa amepita bila kupingwa huku akieleza kuwa wagombea Wenzake kutoka vyama vya upinzani wamekosea kujaza fomu jambo ambalo lilisababisha msimamizi Msaidizi wa wa uchaguzi ambaye ni Afisa Mtendaji wa kata kutowateua kuwa wagombea katika Uchaguzi huo mdogo.

Elias amesema kuwa Uteuzi umefanyika na Mgombea wa CCM akawa ameteuliwa pekee yake na baada wagombea wengine kutoka CHAHADEMA, ACT Wazalendo pamoja na NCCR Mageuzi kukosa sifa za kuteuliwa ili waweze kugombea ameweza kupitia mapingamizi yaliyoletwa na wagombea hao baada ya kijiridhisha akiwa na wataalamu wenzake akaamua kutangaza Mgombea huyo Mmoja kuwa amepitwa bila kupangwa.

“Hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 45 kifungu kidogo cha pili cha sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa No4 ya Mwaka 1979 sura ya 292 kinasema endapo mgombea aliyeteuliwa ni mmoja baada ya pingamizi kukamilishwa msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mimi anapaswa kutalifu mgombea kwa barua kuwa amepita bila kupingwa na pia nitafaamisha tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu suala hilo, hivyo mimi kama Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Tarime Mjii natangaza rasmi kuwa Mgombea wa CCM Chacha Mwita Ghati amepita bila kupingwa” alisema Elias.

Pia Mkurugenzi huyo amemutaka Chacha kusubiri mpaka pale atakapoapishwa na kukabidhiwa cheti kutokana na tarehe za uchaguzi zilizotangangazwa na Tume ya Taifa ya Uchgaguzi.“Pamoja na kwamba amepita bila kupingwa asianze kazi ya udiwani kwa sababu tarehe za Uchaguzi hazijafika mpaka Agosti 12 Mwaka huu na sisi ndo tutaapisha diwani huyo na kuanza kazi ya udiwani lakini kama kuna mtu upande wa pili hajakubaliana na maamuzi yangu sheria iko wazi atakata rufaa” alisema Ntiruhungwa.

Lukas Ngoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Tarime akitaja sababu za mgombea wao kushindwa kuteuliwa amesema kuwa sababu hizo ukisoma kwenye kanuni za Usimamizi wa Uchaguzi hazipo.

Likas amesema kuwa wao kama Chama watakuwa bega kwa bega na mgombea wao na watakata rufaa katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi na wanaamini watarudi kwenye Kinyanganganyilo ili wananchi wafanye maamuzi wenyewe.Kwa upande wake Chacha Mwita Ghati ambaye ametangazwa kuwa amepita bila kupingwa amedai kuwa sasa anaenda kuwatumikia wananchi wa kata ya Turwa

Aidha Charles Daniel ambaye ni Mgombea Udiwani kata ya Turwa kupitia CHADEMA Amesema kuwa maamuzi aliyoyafanya Mkurugenzi ambaye ni msimamizi wa uchaguzi hakubaliani nayo bali watakata rufaa ili haki iweze kutendeka huku akiwataka Wananchi waendelee kuwa wavumilivu.

Inadaiwa kuwa Mgombea Udiwani kupitia CHADEMA alikosa sifa baada ya fomu zake kuwa na Makosa mawili ambapo kosa la kwanza picha yake iligongwa Mhuri wa maakama huku wazamini wake wawili wakiandika majina badala ya kuweka saini zao.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tarime Mkoani Mara Elias Ntiruhungwa akitanganza rasmi mgombea Udiwani kata ya Turwa Chacha Mwita Ghati CCM baada ya kupita bila kupingwa.
Wananchi wakiwa katika ofisi ya Kata ya Turwa kwa ajili ya kusikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime akitangaza rasmi Mgombea udiwani kata ya Turwa.
Baadhi ya wanachama wa CCM Wakiwa na mgombea udiwani kata ya Turwa Chacha Mwita Ghati wa pili kutoka kushoto aliyevaa sare ya chama hicho.
Chacha Mwita Ghati akiongea na Vyombo vya habari baada ya kutangazwa rasmi kuwa amepita bila kuoingwa na anasubiri tarehe za uchaguzi zifike ili aweze kuapishwa kwa lengo la kuwa diwani wa kata hiyo.
Mwenyekiti wa CHADEMA Lukas Ngoto akisoma baadhi ya Vifungu vilivyidaiwa kukiukwa na wasimamizi wa Uchaguzi huo ambapo ameoa kauli ya chama kuwa hakubaliani na maamuzi hayo bali wanaenda kukata rufaa.
Charles Daniel ambaye alikuwa mgombea udiwani kata ya Turwa kupitia CHADEMA akiongea na Vyombo vya habari ambapo amesema kuwa alipeleka pingamizi juu ya Mgombea aliyetangazwa lakini hazikufanyiwa kazi hivyo atakata rufaaTume ya taifa ya Uchaguzi.

JAFO AWAPONGEZA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewapongeza wanafunzi na walimu wa Shule ya sekondari Kibaha kwa kushika nafasi ya kwanza Kitaifa kwenye matokeo ya kidato sita mwaka huu yaliyotangazwa mwishoni mwa wiki. 

Jafo ametoa pongezi hizo leo katika shule hiyo ambayo ni miongoni mwa shule alizozitembelea Januari mwaka huu na kuweka mikakati ya kuhamasisha shule hizo zifanye vyema kwenye mitihani ya Kitaifa.

Waziri Jafo amesisitiza kwamba matokeo haya mazuri yanayoanza kujitokeza kwa shule za serikali yametokana na juhudi kubwa ya Rais John Magufuli katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ambapo shule kongwe zote zipo katika hatua mbalimbali ya ukarabati sambamba na maboresho mengine katika sekta ya elimu. 

Jafo amemshukuru Rais Magufuli kwa moyo wake wa kuipambania jamii ya watanzania hadi kufikia mafanikio hayo makubwa yanayoanza kujitokeza hapa nchini. 

Aidha Jafo ameanza mkakati wa kuzifanya shule za serikali hapa nchini kushika nafasi zaidi ya sita katika ya kumi bora kwa matokeo ya kidato cha sita mwakani. Katika kufanikisha mkakati huo, Waziri Jafo ameitisha kikao cha kazi kwa wakuu wa shule pamoja na walimu wa taaluma wa shule za sekondari za vipaji maalum na shule za serikali zilizoingia katika nafasi ya 30 bora katika matokeo ya kidato cha sita ya mwaka huu ambapo kikao hicho kinatarajiwa kufanyika jijini Dodoma Agosti 2 mwaka huu.

Awali, kabla ya pongezi hizo,Walimu na wanafunzi wa Kibaha wamekiri wazi kwamba hamasa aliyotoa Waziri Jafo iliwafanya kuwa na uchungu na nguvu ya mapambano katika elimu hadi kufikia mafaniko hayo makubwa waliyoyapata.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akizungumza na walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibaha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akipokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akipokelewa katika shule ya sekondari Kibaha.
Wanafunzi wa Shule ya sekondari Kibaha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akikagua ukarabati wa miundombinu katika shule ya sekondari Kibaha.

WAZIRI MKUU: MUWAFUATE WANANCHI VIJIJINI

$
0
0
*Ataka watenge siku tatu hadi nne waende waliko wananchi
*Asema Serikali hii haitaki mambo ya urasimu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wote wa Serikali za Mitaa nchini watenge theluthi mbili ya muda wao wa kazi kwa kuwasikiliza wananchi na kuwahudumia.

Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Julai 15, 2018) wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa Halmashauri za Wilaya za Ushetu, Msalala na Kahama Mji, wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

“Jukumu la watumishi ni kuwatumikia wananchi, Serikali hii hatutaki urasimu na wala hatutarajii kuwa mtatoa huduma kwa urasimu. Lugha ya ‘njoo kesho, njoo kesho’ siyo ya kwa awamu hii.”

Amesema Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya wana jukumu la kusimamia agizo hilo kwa kuhakikisha kuwa wanatoa usafiri kwa watumishi hao ili waweze kufika vijijini kwa haraka. “Wakurugenzi wa Halmashauri simamieni zoezi hilo kwa kupanga ratiba na kutoa gari ili maafisa wanne au watano watumie gari hilo kwenda vijijini wakawahudumie wananchi.”

Amesema wananchi wengi hawana uwezo wa kusafiri kutoka vijijini hadi mijini ili kuleta matatizo yao, kwa hiyo wakifanya hivyo, watumishi watakuwa wamewapunguzia matatizo wananchi.Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye ziara ya siku tano ya kikazi mkoani humo, amewataka watumishi wa idara ya ardhi wapime ardhi kwa wingi na watoe hati mapema ili wananchi wazitumie kuongeza mitaji.

“Pimeni ardhi na kutoa hati ili wananchi wazitumie kukopa na kupata mitaji ya kujiendeleza kiuchumi. Pia muweke mipango mizuri ya ardhi ili kuepusha migogoro baina ya wananchi.Waziri Mkuu leo anaendelea na ziara yake wilayani Kahama kwa kukagua shughuli za maendeleo na kuzungumza na wananchi.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JULAI 15, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea eneo la Viwanda la Bukondamoyo katika Kata ya Zongomela kwenye Halmashauri ya wilaya ya Kahama Julai 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

KOMREDI SONG TAO WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA (CPC) AWASILI NCHINI TANZANIA

$
0
0
Komredi Song Tao Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti Cha China (CPC) amewasili nchini Tanzania na kupokelewa na mamia ya wanachama wa CCM wakiongozwa na Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

Komredi Song Tao amefanya mazungumzo na Viongozi wa Sekretariati ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba, ambapo ameendelea kusisitiza kuwa CPC itaendeleza ushirikiano na urafiki mzuri na CCM uliosisiwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mao Zedong miaka zaidi ya 50 iliyopita.

Naye Ndg. Bashiru ally Katibu Mkuu wa CCM akimkaribisha Ndg. Tao nchini Tanzania amesema, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinathamini sana uhusiano kati ya CCM na CPC na Uhusiano mzuri sana uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya China na kwa niaba ya CCM amemhakikishia Ndg. Song kwamba ushirikiano zaidi katika Nyanja mbalimbali kwa manufaa ya vyama vyetu na wananchi wa mataifa yetu.

Komredi Song Tao yupo nchini kwa ajili ya Mkutano wa Kidunia wa vyama vya siasa utakaofanyika siku ya tarehe 17 na 18 Julai 2018, pia atashiriki katika uwekaji wa jiwe la msingi wa Chuo cha Uongozi cha Chama Cha Mapinduzi kitakachojulika kwa jina la Chuo cha Uongozi Cha Mwalimu Julius Nyerere.

Aidha, Komredi Song Tao atatembelea Chuo kikuu cha Dar es Salaam na Stesheni ya Tazara.


Ndg Song Tao Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama cha Kikomunisti cha Watu wa China akivalishwa Skafu na Vijana wa Chipukizi wa Chama cha Mapinduzi mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl Nyerere jijini Dar es salaam, Kulia kwake ni Ndg Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi.
Ndg Song Tao (Kushoto) Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama cha Kikomunisti cha Watu wa China na mwenyeji wake Ndg Bashiru Ally Kakulwa (Kulia) Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi wakikagua Gwaride maalum la vijana wa Chipukizi wa Chama cha Mapinduzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Ndg Bashiru Ally Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Kakulwa akifanya mazungumzo na Mgeni wake Ndg Song Tao Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama cha Kikomunisti cha Watu wa China mara baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Ndg Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi akiwa na Mgeni wake Ndg Song Tao Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama cha Kikomunisti cha Watu wa China Uwanja wa Ndege wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

UKAGUZI WA MAGARI, LESENI NA OPARESHENI YA KUKAMATA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI JIJINI MBEYA.

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu na ajali za barabarani ili kuhakikisha kuwa wageni na wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao. Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa usalama hali inayopelekea kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu pamoja na ajali za barabarani. 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea na Oparesheni ya kukagua magari pamoja na kukamata makosa mbalimbali ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani. Katika Oparesheni iliyofanyika mnamo tarehe 14.07.2018 kuanzia majira ya saa 05:00 alfajiri katika Stendi Kuu ya Mabasi jumla ya Mabasi 43 yaendayo Mikoa mbalimbali yamekaguliwa kati ya hayo 38 yaliruhusiwa kuendelea na safari wakati Mabasi 05 yaligundulika kuwa na hitilafu hivyo hayakuruhusiwa kuendelea na safari hadi yatakapo tengenezwa. 

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanya Oparesheni ya kushtukiza katika maeneo ya Kabwe, Mwanjelwa, Isanga, Soweto, Uyole na Iyunga na kufanikiwa kukamata magari 45 kati ya hayo 29 yamekutwa na makosa mbalimbali yakiwemo ya ubovu, kuvuja mafuta, kuisha kwa matairi na baadhi ya gari za abiria @ daladala kuchakaa kwa viti vya kukalia abiria.

Kufuatia Oparesheni hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ULRICH MATEI amewataka madereva kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuepuka ajali za mara kwa mara. 

Aidha Kamanda MATEI amewataka wamiliki wa vyombo vya moto hasa magari kujenga utaratibu wa kuyafanyia matengenezo ya mara kwa mara magari yao ili yaweze kutumika kikamilifu katika kazi ya kubeba na kusafirisha abiria vinginevyo Jeshi la Polisi litawachukulia hatua za kisheria wamiliki wote ambao magari yao yatabainika kuwa mabovu hali inayoweza kupelekea ajali.

Imesainiwa na: 
[ULRICH O. MATEI - SACP] 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

WAZIRI MKUU AKEMEA MAHUSIANO MABAYA YA WATUMISHI KAHAMA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekemea mahusiano mabaya baina ya watumishi wa wilaya ya Kahama na kusema wanapaswa kubadilika mara moja.

Ametoa onyo hilo leo (Jumapili, Julai 15, 2018) wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa Halmashauri za Wilaya za Ushetu, Msalala na Kahama Mji, wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

“Hali ya mahusiano hapa Kahama ni mbaya kuliko Kishapu na Shinyanga. Mnachapa kazi vizuri lakini tatizo kubwa kila mmoja anaenda kivyake, hakuna anayemsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri wala Mkuu wake wa idara,” amesema.Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye ziara ya siku tano ya kikazi mkoani humo, amewaeleza watumishi na viongozi hao kwamba Serikali haitavumilia kuona watumishi wa aina hiyo wanaendelea kufanya kazi.

“Serikali haitavumilia kuona watumishi wakifanya mambo ya hovyo. Kahama ni wilaya yenye majaribu na Shinyanga nayo ni wilaya yenye majaribu makubwa. Kwa hiyo watumishi inabidi muwe makini, kuweni waangalifu msije mkaingia kichwakichwa kwenye majaribu haya.”

“Migogoro niliyoisikia ambayo iko hapa ni kwa sababu ninyi mmeingia kwenye biashara na kutake sides. Hapa Kahama, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Wilaya hamuelewani, Mkurugenzi na wakuu wa idara hamuelewani, wakuu wa idara na wasaidizi wao nao pia hawaelewani,” alisema.“Napenda kusisitiza kwamba ninyio ni viongozi wa umma, kwa hiyo ni lazima mzingatie itifaki za kiuongozi, mzingatie mahusiano mema mahali pa kazi. Hatupendi viongozi muwe chanzo cha matatizo hapa Kahama,” aliwaasa.

Alisema Kahama ina fursa kubwa na nzuri kwenye kilimo, madini, mifugo na biashara na akawataka viongozi wanaoletwa kwenye wilaya hiyo wawe makini. “Kiongozi ukiletwa hapa inabidi uwe na kichwa kilichotulia. Inabidi uwe mwaminifu sana ili uweze kudumu kwenye wilaya kama hii,” alisisitiza.

“Kama kiongozi ulizoea kwenda disco inabidi uache, kama ulizoea kwenda baa inabidi ununue kreti uweke ndani kwako. Kama ulizoea kushabikia mpira kwa kujichora chaki, sasa basi. Kaa sebuleni kwako, angalia mpira kwenye luninga yako, ndiyo dhamana ya uongozi hiyo,” alisema.

Aliwataka watumishi wa umma wawasaidie wananchi kuboresha utendaji wao kwenye kilimo, uvuvi na ufugaji ili kila kuleta tija kwenye kila sekta.
Waziri Mkuu leo anaendelea na ziara yake wilayani Kahama kwa kukagua shughuli za maendeleo na kuzungumza na wananchi.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JULAI 15, 2018.

KANISA lagawa Pikipiki kwa wachungaji,Polisi

$
0
0
KANISA la Pentecostal Assemblies of God (PAG), limegawa Pikipiki kwa wachungaji wake ikiwamo Kituo cha Polisi cha wilaya ya Hanang mkoani Manyara. 

Lengo la kutolewa kwa vyombo hivyo vya usafiri ni kuwawezesha Wachungaji hao kuwafikia watu wengi hususani wanaoishi pembezoni pamoja na kuunga mkono juhudi za jeshi la polisi katika kupambana na uhalifu. 

Akizungumza wakati wa Ibada fupi ya kuzindua pikipiki pamoja na kumuombea Rais Dk.n Magufuli iliyofanyia Kanisa la PAG Hanang’ Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Daniel Awet, aliwataka kutumia pikipiki hizo kuhubiri Injili ya Yesu ili jamii inayowazunguka iache matendo ya maovu. 

“Tumieni Pikipiki hizi kama nyenzo ili Injili ifike kwa kasi kwa waamini hasa maeneo ambayo mlikuwa hamuwezi kufika lakini sasa mmepata nyenzo za kuwafikisha,” alisema Askofu Awet. Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya ya Hanang’, Sutibert Tryphone, alisema pikipiki waliyopewa itawasaidia kuhudumia wananchi mpaka kwenye maeneo ambayo magari hayafika. 

“Maeneo mengi ambayo hayapitiki kwa usafiri wa magari, sasa tutakuwa tunatumia pikipiki, tunaomba wadau wengine nao wajitokeze kutuunga mkono,” alisema OCD Tryphone. Naye Mchungaji Alex Mapanga wa PAG, ambaye kampuni yake iliwezesha kuagiza pikipiki hizo toka kiwandani kwa fedha zilichangwa na waamini wa kanisa hilo, alisema ataendelea kushirikiana na waamini katika kukfanikisha upatikanaji wa usafiri kwa wachungaji. 

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Hanang’ Mary Nagu, aliliomba kanisa hilo kuendelea kuliombea amani taifa na Rais John Magufuli. “Amani na utulivu ziwafanye mchape kazi ndani ya kanisa, serikalini na kwa jamii,” alisema na kuongeza, kanisa hilo limefanya jambo jema kuwawezesha wachungaji wake kupata vyombo vya usafiri.


Askofu Mkuu wa Kanisa la Pentecostal Assembilies of God (PAG), Daniel Awet akikata utepe kuzindua rassmi ugawaji wa Pipikipi 200 kwa Wachungaji wilayani Hanang' mkoani Manyara.
Sehemu ya Pikipiki 200 zilizogawiwa kwa Wachungaji wa Kanisa la Pentecostal Assemblies of God (PAG), wilayani Hanang' mkoani Manyara kwa ajili ya kazi ya kuhubiri Injili.
Mkurugenzi wa Kampuni ya MCB Investiment Mchungaji Alex Mapanga katikati akimuonyesha namba za moja ya Pikipiki zilizogawiwa kwa Wachungaji wilayani Hanang' mkoani Manyara Askofu Mkuu wa Kanisa la Pentecostal Assembilies of God (PAG), Daniel Awet. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya MCB Investiment Mchungaji Alex Mapanga akifafanua jambo kuhusu Pikipiki hizo mbele ya viongozi wa dini wakati wa zoezi la ugawaji Pikipiki hizo kwa Wachungaji. 
Mkuu wa Polisi wilaya ya Hanang' mkoani Manyara (OCD), Sweetbert Tryphone akimshukuru Askofu Mkuu wa Kanisa la Pentecostal Assemblies of God (PAG), Daniel Awet mara baada ya kumkabidhi Pikipiki moja kwa ajili ya jeshi la polisi. 

RPC ARUSHA ATAJA VIPAUMBELE VITANO KUELEKEA KUUSHINDA UHALIFU

$
0
0
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Jeshi la Polisi mkoani hapa kupitia Kamanda wake wa mkoa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi, limetaja mambo matano ambayo yakifanyika basi kutakuwa na mafanikio zaidi katika kuushinda uhalifu.

Akizungumza katika mahojiano yaliyofanywa na Redio Sunrise ya Jijini hapa kupitia kipindi chake cha “Kwa ajili ya Nchi yako” kinachorushwa hewani kila siku ya Ijumaa kuanzia saa 9:00 Alasiri hadi saa 10:00, Kamanda Ng’anzi alisema, kwanza kabisa kila mwananchi anatakiwa ajue ana wajibu wa kutoa taarifa za matukio ya Uhalifu na Wahalifu zinatokea katika eneo lake.

Pili alisema ni lazima askari wa Jeshi hilo watoe huduma bora na kwa kiwango cha juu kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza pindi wanapoeleza shida zao lakini pia kwenda haraka katika maeneo yaliyoripotiwa kutokea uhalifu.

Tatu alisema lazima kila askari adumishe na kuongeza kiwango cha nidhamu hali ambayo itasaidia baadhi ya wanaokwenda kinyume kutofanya kazi kwa mazoea na hivyo watafanya kazi kwa kufuata taratibu zilizopo.

Nne alisema askari watatakiwa kufanya kazi kwa kuheshimu Utu pamoja na kufuata Maadili ya kazi yao na tano kufanya kazi kwa Uweledi na Usasa ambapo askari atafanya kwa namna alivyofunzwa lakini pia kuendana na kasi ya ukuaji wa Teknolojia na mwisho wa siku waone kwa jinsi gani wananchi mkoani hapa wanaridhishwa na utendaji wa Jeshi hilo.

Mbali na kutaja vipaumbele hivyo Kamanda Ng’anzi alisema Jeshi hilo litaendelea kutunza siri za watoa taarifa kwani ni sehemu ya miongoni mwa viapo vya kazi yao lakini pia aliwaeleza wananchi wenye mashaka juu ya kuvujishwa kwa siri zao wanaweza kuzitoa moja kwa moja kwa viongozi wa ngazi za juu.

“Kwa wenye mashaka juu ya taarifa zenu toeni kwangu au viongozi wa juu wa ngazi ya mkoa mfano RCO “Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa “, RTO “Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani mkoa” na viongozi wengine wa ngazi ya juu wa Polisi mkoa na kwa ngazi ya wilaya toeni taarifa kwa OCD “Mkuu wa Polisi wilaya au OC-CID “Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa wilaya”. Alisema Kamanda Ng’anzi.

Aidha Kamanda Ng’anzi alisema kwamba Jeshi hilo lina mkakati wa kutekeleza Progamu ya MUONGORIKA kwa kushirikiana na wadau ili waweze kuanzisha mashindano mbalimbali ya Michezo na Sanaa kwa vijana wanaoshinda vijiweni bila ajira hali ambayo itasaidia kuibua vipaji vyao vitakavyowawesha kujiendeleza na pengine kujikwamua kiuchumi huku wakiondokana na fikra za kujiingiza kwenye uhalifu.

Takwimu zinaonyesha kiwango cha matukio ya uhalifu yaliyoripotiwa mkoani hapa kwa kipindi cha miezi sita mwaka huu zinaonekana kupata mafanikio makubwa ambapo matukio yalikuwa 654 tofauti na mwaka 2017 kipindi cha Januari hadi Juni ambapo kulikuwa na matukio 996 hivyo yalishuka kwa asilimia 20.7.
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng'anzi

TRA YAKUSANYA TRILIONI 15.5 KWA MWAKA WA FEDHA 2017/18

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Makusanyo ya kodi kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 yameongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 15.5 kutoka shilingi trilioni 14.4 kwa Mwaka wa Fedha 2016/17 sawa na ongezekeo la asilimia 7.5.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya makusanyo ya kodi ya mwaka wa fedha 2017/18, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo amesema kuwa katika mwezi Juni, 2018 pekee, TRA imekusanya jumla ya shilingi trilioni 1.5 ikilinganishwa na shilingi trilioni 1.4 kwa mwezi Juni, 2017 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 8.0.

“TRA inapenda kuwapongeza na kuwashukuru walipakodi wote ambao mchango wao umeiwezesha Serikali kupata mapato haya tunayotangaza leo kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo na za jamii zikiwemo ujenzi wa miundombinu ya reli na barabara, ununuzi wa ndege, upatikanaji wa elimu, afya na mambo mengine kwa manufaa ya watanzania wote,” alisema Kayombo.

Kayombo amezitaja sababu zilizosababisha kuongezeka kwa makusanyo hayo kuwa ni pamoja na elimu ya kodi kuzidi kueleweka kwa walipakodi na wananchi kwa ujumla, kuongeza ukaribu na walipakodi kwa kuwasikiliza na kutatua changamoto zao za kikodi, kuongezeka kwa walipakodi wapya kupitia kampeni ya kuwasajili kwa kuwafuata waliko na kurahisisha ulipaji wa kodi kwa njia ya kielektroniki.

Aidha, Mkurugenzi huyo alisema kuwa, katika Mwaka huu wa Fedha 2018/19, TRA imedhamiria kutekeleza kwa vitendo kampeni kabambe ya msamaha wa riba na adhabu kwa malimbikizo ya madeni ya nyuma na inategemea kuongeza urahisi wa kulipa madeni ambayo yalikuwa kikwazo kwa wafanya biashara wengi kulipa na hata kuendelea na biashara.

“Vilevile, mamlaka imedhamiria kuongeza kasi ya usajili wa walipakodi wapya. Hivyo, tunaendelea na kasi ya utambuzi na usajili wa wafanyabiashara wadogo ili kila mtu anayestahili kulipa kodi asajiliwe na kuchangia kikamilifu maendeleo ya Taifa,” alieleza Kayombo.

Mkurugenzi Kayombo ametoa wito kwa walipakodi na wananchi wote kuendelea kulipa kodi kwa hiari na kujenga utamaduni wa kudai Risiti za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) kila mfanyabiashara anapofanya mauzo na mnunuzi anatakiwa kudai risiti kila anaponunua bidhaa na huduma mbalimbali.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya makusanyo ya kodi ya Mwaka wa Fedha 2017/18 ambayo yameongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 15.5 kutoka shilingi trilioni 14.4 kwa Mwaka wa Fedha 2016/17 sawa na ongezekeo la asilimia 7.5.
Mmoja wa waandishi wa habari akiuliza swali wakati wa Mkutano wa waandishi hao ulioandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambapo Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Richard Kayombo (hayupo pichani) leo ametoa taarifa ya makusanyo ya kodi ya Mwaka wa Fedha 2017/18 ambayo yameongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 15.5 kutoka shilingi trilioni 14.4 kwa Mwaka wa Fedha 2016/17 sawa na ongezekeo la asilimia 7.5. (PICHA NA TRA).

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI CHUO CHA UONGOZI CHA MWALIMU JULIUS NYERERE KINACHOJENGWA KIBAHA KWA MFIPA MKOANI PWANI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao wanne kutoka kushoto pamoja na Makatibu wa vyama vya, CCM, ANC, SWAPO, ZANU-PF, MPLA, FRELIMO, wakiweka mchanga kama ishara ya uwekaji wa Jiwe la msingi Ujenzi wa Chuo cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao wanne kutoka kushoto pamoja na Makatibu wa vyama vya, CCM, ANC, SWAPO, ZANU-PF, MPLA, FRELIMO, wakiweka mchanga kama ishara ya uwekaji wa Jiwe la msingi Ujenzi wa Chuo cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na mgeni wake Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao wanne kutoka kushoto waliokaa, viongozi wa vyama vya ANC, SWAPO,ZANU-PF, MPLA, FRELIMO pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani. Chuo hicho kinajengwa na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwa gharama ya Shilingi Bilioni mia moja(100). 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao kabla ya tukio la uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma pamoja Sophia Shaningwa Katibu wa Chama cha SWAPO kutoka nchini Namibia huku Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao akipiga makofi mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma na Katibu wa Chama cha SWAPO kutoka Namibia Sophia Shaningwa pamoja na Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma na Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi kabla ya ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mfano wa moja ya majengo ya chuo hicho kitakapo kamilika kujengwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kwa wananchi(hawaonekani pichani) wakati akiwasili katika eneo kitakapojengwa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani. PICHA NA IKULU

BENKI YA CREDIT SUISSE KUIPATIA TANZANIA MKOPO WA DOLA MILIONI 200

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea picha ya alama ya ushirikiano ya kiasi cha Dola 500 kutoka kwa Afisa mwandamizi wa Benki ya Suisse ya Uingereza Bi. Elizabeth Muchemi, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Mchumi Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Omary Khama (kulia), anayeshughulika na maswala ya uchambuzi wa madeni akimwelezea Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia) kuhusu miradi mbalimbali itakayotekelezwa kutokana na pesa iliyopatikana, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Benki ya CREDIT SUISSE.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (kulia) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wea Benki ya Suisse Bw. Lawrence B. Fletcher kwa mikopo mbalimbali ambayo Benki hiyo imetoa kwa Serikali ya Tanzania katika Sekta mbalimbali, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.




Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Benki ya Credit Suisse ya nchini Uingereza imeonesha nia ya kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa zaidi ya Dola milioni 200 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo miradi mikubwa ya Nishati ya Umeme na miundombinu ya Reli.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam katika Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Ujumbe wa Benki ya Credit Suisse ya Uingereza ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo Bw. Lawrence B. Fletcher, kuhusu ushirikiano katika miradi ya maendeleo.

Dkt. Mpango alisema kuwa tayari zipo hatua mbalimbalimbali zimefikiwa katika kufanikisha upatikanaji wa Mkopo kutoka Benki ya Suisse hivyo kuwa na tumaini la kupata kiasi cha Dola milioni 200 katika mwaka wa fedha wa 2018/19 .

“Miradi ya Kipaumbele ambayo Serikali inaitekeleza ni pamoja na Ujenzi wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (SGR), kufufua Shirika la Ndege Tanzania kwa kununua Ndege mpya na miradi ya umeme ambayo itachochea maendeleo ya watu na Taifa kwa ujumla”, alieleza Dkt. Mpango.

Aliitaja miradi mingine ambayo Serikali inampango wa kuitekeleza kuwa ni pamoja na Ujenzi wa Bwawa la Umeme la Rufiji (Rufiji Haydro Project) ambalo kukamilika kwake kutasaidia kuzalisha umeme wa Megawati 2100 ambao utatumika katika kuchochea uchumi wa viwanda unaohitaji umeme wakutosha.

Waziri Mpango amebainisha kuwa Serikali inatekeleza miradi ya kupanua Bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Kigoma pamoja na ujenzi wa miradi mbalimbali ya barabara ambazo zitahudumia nchi ya Tanzania na nchi jirani ya Rwanda na Burundi hivyo kuchochea maendeleo.

Ameishukuru Benki ya Suisse, kwa kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya Maji, barabara na Umeme na kuahidi kuendelea kukuza ushirikiano na Benki hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Credit Suisse ya nchini Uingereza, Bw. Lawrence B. Fletcher, amesema kuwa Benki yake inaangalia uwezekano wa kufadhili miradi ya kipaumbele ya Serikali ili kuweza kufanikisha nia yake ya kufikia uchumi wa kati unaotegemea viwanda.

Aidha amesema Benki yake itatoa mkopo wa Dola milioni 200 baada ya hatua za mkopo huo kukamilika katika mwaka huu wa fedha ili kuweza kufanikisha kutekeleza miradi mbalimbali lakini pia ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano kati ya Benki yake na Tanzania.

KANGI LUGOLA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA, UKONGA JIJINI DAR

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akithibitisha ubora wa silaha baada ya kutembelea Makao Makuu ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia kilichopo Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (watatu kutoka kushoto), akipata maelezo juu ya ubora wa silaha inayotumika katika kupambana na uhalifu baada ya kutembelea Makao Makuu ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia, kilichopo Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Marijani (kulia), akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, baada ya waziri kutembelea Makao Makuu ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia, kilichopo Ukonga, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mrakibu Mwandamizi, Paulo Sanga.
Sajenti wa Jeshi la Polisi, Kusekwa Machibya akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kutoka kushoto) baada ya waziri kutembelea Makao Makuu ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia, kilichopo Ukonga, jijini Dar es Salaam. Wengine ni Maofisa wa jeshi kutoka Makao Makuu ya Polisi, walioongozana na waziri katika ziara hiyo.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Marijani akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, baada ya waziri kutembelea Makao Makuu ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia, kilichopo Ukonga, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

AIRTEL MONEY NA SPORTPESA WAENDELEA KUTOA ZAWADI KWA WASHINDI

$
0
0
Mshindi wa promosheni ya AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY Fredy Mduma wa Kimara DSM akikabidhiwa zawadi yake ya simu aina ya smartphone na Meneja Uhusiano SportPesa Tanzania Sabrina Msuya wakati wa kuwazadia washindi wa promosheni hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kwenye promosheni hiyo, wateja wa Airtel wanajishindia zawadi mbali mbali kwa kuweka kisha kubashiri kwenye akaunti ya SportPesa 150888. Kushoto ni Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mbando.
Mshindi wa promosheni ya AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY Mazoea Rashidi wa Keko DSM akionyesha zawadi yake ya simu aina ya smartphone na Meneja Uhusiano SportPesa Tanzania Sabrina Msuya wakati wa kuwazadia washindi wa promosheni hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kwenye promosheni hiyo, wateja wa Airtel wanajishindia zawadi mbali mbali kwa kuweka kisha kubashiri kwenye akaunti ya SportPesa 150888. Kushoto ni Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mbando na kulia ni Meneja Uhusiano SportPesa Tanzania Sabrina Msuya.

ZFDA YATEKETEZA TANI 95 ZA CHAKULA NA TANI MOJA YA DAWA ZA BINADAMU ZILIZOMALIZA MUDA WA MATUMIZI

$
0
0
Na Ramadhani Ali, Maelezo Zanzibar
Mamlaka ya Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) imejidhatiti kuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingizwa nchini zinawafikia wananchi zikiwa salama kwa matumizi kwa lengo la kulinda afya zao.

Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Usalama wa chakula wa ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar alieleza hayo katika jaa la Kibele wakati wa kazi ya kuangamiza tani 95 za bidhaa za mchele, sembe na Unga wa ngano pamoja na tani moja ya dawa za binadamu.

Alisema bidhaa za chakula zilizoangamizwa za mfanyabiashara Mohamed Mattar ziliharibika baada ya kuhifadhiwa kwa muda mrefu katika maghala yasiyorasmi na yaliyokosa sifa za kutumika kwa kazi hiyo.

Dkt. Khamis alieleza kuwa kutokana na maghala hayo kukosa viwango vinavyokubalika na kutosajiliwa na ZFDA, mfanyabiashara Mattar alikuwa  akiweka bidhaa zake kwa siri wakati wa usiku.

Akitaja viwango vya bidhaa zilizoangamizwa, Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti na uhifadhi wa chakula wa ZFDA alisema mchele ulikua tani 52, unga wa ngano tani 37 na sembe ilikuwa tani sita.
  Fundi wa mageti akikata geti la Ghala lililokua likihifadhiwa bidhaa za Mchele, Unga wa ngano na sembe uliomaliza muda na haufai kwa matimizi ya binadamu katika mtaa wa Migombani Mjini Zanzibar.
 Sshemu ya bidhaa ya Mchele na Unga wa Ngano na Sembe zikiteremshwa katika magari kwa ajili ya Kuangamizwa katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Unguja.
 Dawa za binadamu za aina mbali mbali za kuondosha maumivu na Virutubisho zilizo angamizwa katika  Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
 Gari la Kijiko likiangamiza Dawa za kuondosha maumivu na Virutubisho zilizoangamizwa katika  Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkurungezi Idara ya Udhibiti na Usalama wa Vyakula wa ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar akizungamza na Waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuangamizaji Bidhaa zisizofa kwa Matumizi ya Binadamu lililofanyika katika  Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Picha na Abdalla Omar Maelezo  -  Zanzibar.


Rais Magufuli awaagiza viongozi wa mkoa wa Pwani na Dar es Salaam kutatua changamoto ya wafanyabiashara kando ya Morogoro road

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia ya wananchi wa Mbezi Mwisho waliosimama katikati barabara ya Morogoro kuhusu kero zao mbalimbali wakati akitokea Kibaha Kwa mfipa mkoani Pwani ambapo aliweka jiwe la Msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere. 
Wananchi mbalimbali wakikimbilia msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kusimama katika eneo la Mbezi Mwisho ambapo aliwahutubia wananchi hao.
Wanchi wa Mbezi Mwisho wakishangilia wakati msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ulipokuwa ukipita katika eneo la Mbezi mwisho jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kibaha maili moja wakati akitokea Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani ambapo aliweka jiwe la Msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere. PICHA NA IKULU 

Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images