Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1623 | 1624 | (Page 1625) | 1626 | 1627 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa ametembelea Mkoa wa Shinyanga pamoja na Wilaya ya Kahama na vituo vya afya kwa nia ya kuangalia shughuli zinazofanywa na wauguzi na wakunga wa kada mbalimbali pia kuzungumza nao.

  Msajili alikutana na baadhi ya wauguzi katika vituo vyao vya kazi na kuwasisitizia kuzingatia maadili wanapowahudumia wagonjwa. Pia, alifanya mkutano Mjini Kahama katika Hospitali ya wilaya na aliwakumbusha wauguzi na wakunga juu ya majukumu ya Baraza la Uuguzi na Ukunga pamoja na Misingi ya utoaji huduma ya Uuguzi na Ukunga yaani (Professional code of conduct, the guiding principles).

  Katika hatua nyingine, aliwataka wauguzi na wakunga kuwa na leseni inayowaruhusu kutoa huduma, lakini pia alikemea vikali watu wanaoghushi vyeti na leseni za uuguzi na ukunga.Msajili alipata nafasi ya kujibu maswali mbalimbali ya kiutendaji pamoja na sheria inayoongoza taaluma ya uuguzi na ukunga.

  Pia, alitembelea pia Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga na kuonana na wauguzi na wakunga katika maeneo yao ya kutolea huduma na kujibu maswali mbalimbali yanayohusu taaluma ya uuguzi na ukunga, sheria inayoongoza taalama ya uuguzi na ukunga nchini.
  Msajili Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa akiwa ziarani mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuzungumza na wauguzi pamoja na wakunga kuhusu utoaji wa huduma bora.
  Wauguzi na wakunga wa Wilaya ya Kahama wakijiandaa kumsikiliza Msajili Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agness Mtawa.

  0 0

  *Ni kwa upotevu wa dola za Marekani 21,000
  *Wakimbia mkutano baada ya wananchi kuzomea

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule awakamate viongozi wa Chama cha Msingi cha Mkombozi kwa upotevu wa dola za marekani 21,000 za chama hicho.

  "Wabebe hawa watu, wahoji waseme hiyo fedha iko wapi na jambo la kwanza wailete hiyo fedha ya wakulima. Wakishindwa kurejesha fedha, wawekwe ndani," amesema.

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Julai 16, 2018) wakati akizungumza na mamia ya wananchi wa kijiji cha Kangeme, kata ya Ulowa katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama ambao alienda kuzindua mpango wa Ushirika Afya na NHIF.

  Waziri Mkuu amefikia uamuzi huo baada ya kuwaita viongozi wa chama cha Mkombozi watoke hadharani na kubaini kuwa hakuwepo hata mmoja. Inadaiwa kwamba walitoroka baada ya wananchi kuanza kuzomea. 

  Kamanda Haule amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Mwenyekiti, Bw. Shilinde Abdallah na mhasibu wa AMCOS hiyo, Bw. Kulwa Shinzi pamoja na wajumbe saba wa bodi ya chama hicho.

  Akiwa katika tukio hilo, Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Kahama (KACU), Bw. Emmanuel Cherehani alisoma taarifa ya Chama na alipotaja bei ya tumbaku kuwa ni nzuri, wananchi walimzomea kupinga kile alichokisema. Bw. Cherehani alikuwa akitoa mafanikio ya chama hicho, na kusema kuwa bei ya tumbaku ni nzuri.

  Akitoa ufafanuzi kuhusu kadhia hiyo, Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba alisema kuna tatizo katika uteuzi (grading) wa tumbaku kwani wakulima wanalima tumbaku nzuri lakini katika upangaji bei, wanalipwa bei ndogo. “Kuna wakulima wanakidai chama cha Mkombozi kiasi cha dola za Marekani ambayo ni madai ya tumbaku waliyoiuza tangu mwaka 2014.” 

  Akizungumza na wananchi hao, Waziri Mkuu alisema Serikali imeamua kufufua ushirika kwa sababu ndiyo mkombozi wa wakulima. "Tumeamua kurudisha ushirika aminifu kwa wakulima, na nirudie kutoa onyo kwa viongozi waliopata dhamana ya kuongoza ushirika wasidhani kule wameenda kupata ulaji.”

  “Tunataka ushirika unaosimamiwa na viongozi waaminifu. Kwenye ushirika kuna fedha na kuna mali za chama, kwa hiyo ni lazima tupate viongozi ambao ni waaminifu,” amesema. 

  “Kwa mfano, hapa Ulowa wakulima wamekuwa wakilalamikia kupewa bei ya chini wakati wakati wao viongozi wanabeba kile cha juu na kuwaumiza wakulima. Kiongozi wa KACU kasoma taarifa hapa mkaanza kuzomea, hiyo ni dalili tosha kwamba kuna tatizo la msingi,” amesema.

  Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaasa wakulima waachane na tabia ya kukopa pembejeo na kufunga mikataba na makampuni ya ununuzi wa tumbaku na badala yake wajiwekee akiba ili msimu wa kilimo ukianza wasirudie tena kukopa.

  “Gharama za kulima ekari moja, kuweka dawa, palizi na kuchoma haizidi sh. 150,000. Wewe amua unataka kulima ekari ngapi, weka fedha zako kwenye akaunti usubiri msimu ujao. Kwenye hii biashara ya tumbaku, ukitafuta mikopo utabakia kuwa maskini kwa sababu huna nguvu ya kubishania bei. Wenzenu wanaolima korosho, wameacha kukopa na bei mnazisikia kila mwaka zinapanda,” amesema.

  “Ukiwa na mazao yako utaweza kubishana na mnunuzi. Tanzania bei ya tumbaku iko chini sababu wakulima mmetufikisha hapo kwa kupitia mikopo na mikataba na makampuni ya ununuzi. Kuanzia sasa badilikeni, ili muweze kuinua bei ya zao hili muhimu, alisema.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATATU, JULAI 16, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Kangeme katika Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga wakati alipowasili kijijini hapo kuhututibia Mkutano wa hadhara na kuzindua Fao la Ushirika Afya ambalo litawazesha wanaushirika kunufaika na huduma za Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya, Julai 16, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba. (kushoto) wakati alipokagua uuzaji wa tumbaku katika Chama cha Ushirika cha Msingi cha Kangeme katika Halmashauri ya Ushetu, Julai 16, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Maendeloeo ya Ushirika Nchini, Dkt. Titus Kamani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kangeme kwenye Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga, Julai 16, 2018. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kangeme kwenye Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga, Julai 16, 2018. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Fao la Ushirika Afya ambalo litawawezesha wanaushirika kunufaika na huduma zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, kwenye kijiji cha Kangeme katika Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga Julai 16, 2018. Kushoto kwake ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba, watatu kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bernard Konga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi baada ya kukagua ujenzi wa zahanati ya Ukune katika Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga, Julai 16, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasha gari alilolizindua ambalo limenunuliwa na Halmashauri ya Ushetu kwa ajili ya Idara ya Kilimo ya Halmashauri hiyo , kwenye kijiji cha Kangeme Julai 16, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  Na Pamela Mollel,Arusha

  Serikali imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kuanza kuwekeza kwa watoto hasa wanaoishi katika mazingira Magumu ili kuepusha dhana ya kuwa na taifa lenye watoto ombaomba.

  Kauli hiyo aliitoa Mkuu Wa Nchi wa Shirika la Compassion Nchini, Agnes's Hotay alipokuwa kwenye Mahafali ya Nne ya kuondoka kwenye ufadhili Wa shirika hilo kwa watoto waliokuwa wakilelewa kwenye Klasta ya USA River, wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha baada ya kufikisha umri Wa Miaka 22 .

  Hotay amesema kuwa ipo haja kwa serikali kuunga mkono jitihada zinazoonyeshwa na Mashirika , taasisi mbalimbali katika kuwahudumia watoto waliopo katika mazingira magumu kwa kuwapatia elimu na ujuzi ili waweze kujiajiri ,jambo litakalosaidia kupunguza namba ya vijana wasio na ajira .

  Amesema shirika hilo hapa nchini limeifikia mikoa 17 na linafanya kazi na makanisa wenza zaidi ya 400 na linahudumia watoto zaidi ya 93,000 ikiwa lengo ni kuwaondoa watoto kwenye umasikini na kuwajengea uwezo Wa kujitegemea,kujikinga na maradhi na kuwajenga kiuchumi.

  Alitoa rai kwa wahitimu kuhakikisha wanakuwa waadilifu kwa kuzingatia yale mema yote waliofundishwa na walimu wao.Awali katika risala ya wahitimu hao wapatao 78 walilishukuru shirika la Compassion kwa ufadhili huo ambao umewasaidia kuwajenga kiroho,kuwapatia Elimu ya ujasiliamali na kutaka makanisa mengine kuinga mfano huo utakao saidia kupunguza changamito za vijana.

  Naye Mwenyekiti wa Klasta ya USA River ,Saluni Kisangas amesema Shirika hilo kwa kushirikiana na Makanisa wenza limekuwa likiwahudumia watoto tangia wakiwa na umri mdogo wa kuingia chekechea na punde wanapofikisha umri wa miaka 22 wanaamini umri huo wanastahili kujitegemea.

  Aidha amesema katika Klasta ya USA River inayohudumia kata 4 ,tangia kuanzishwa kwa Klasta hiyo mwaka 1999 ambapo wahitimu wengi wamenufaika na Mpango huo kwa kupata ajira serikalini na baadhi yao kuchukuliwa na mashirika Mbalimbali.
  Mkuu Wa Nchi wa Shirika la Compassion Nchini, Agnes's Hotay akizungumza katika Mahafali ya Nne ya kuondoka kwenye ufadhili Wa shirika hilo kwa watoto waliokuwa wakilelewa kwenye Klasta ya USA River, wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha .
  Wahitimu

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Matumizi Bora ya Ardhi Dkt. Stephen Nindi (aliyekaa) akimsikiliza kwa makini Mtendaji Mkuu wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo alipokuwa akiwasisitiza wajumbe wa kikao kazi kwa ajili ya kuhakikisha kunakuwepo na mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa vijiji 120 vinavyozunguka misitu ya Hifadhi ya Serikali Kuu mapema jana.

  wajumbe wa kikao kazi

  0 0

  Balozi Mteule wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu akiwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.). Mara baada ya kuwasilisha nakala hizo Mhe. Mahiga na Balozi Kazungu walipata fursa ya kuzungumza kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya hususan kwenye sekta za biashara, uchumi na elimu. Tukio hilo lilifanyika kwenye Ofisi Ndogo ya Wizara iliyopo Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Julai, 2018. 
  Dkt. Mahiga akiendelea na mazungumzo na Balozi Mteule wa Kenya hapa nchini 
  Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo kati ya Dkt. Mahiga na Balozi Mteule wa Kenya nchini. Kushoto ni Bibi Judica Nagunwa na Bw. Magabilo Murobi 
  Balozi Kazungu akimweleza jambo Dkt. Mahiga .
  Mazungumzo yakiendelea kati ya Dkt. Mahiga na Balozi Kazungu 
  Picha ya pamoja. 
  Dkt. Mahiga akiagana na Balozi Mteule wa Kenya nchini Tanzania.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya, akizungumza katika Mkutano ulioandaliwa na Bohari ya Dawa (MSD), uliowakutanisha  na wazalishaji wa dawa na vifaa tiba kutoka ndani na nje ya nchi uliofanyika leo Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam ambapo wazalishaji zaidi ya 
  130 kutoka nchi 25 walihudhuria.
  Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Rugambwa Bwanakunu akizungumza.
  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Elisante ole Gabriel, akizungumza katika mkutano huo.
  Viongozi mbalimbali wa MSD wakifuatilia  mkutano huo.
  Wafanyakazi wa MSD wakiwa katika mkutano huo.
  Wazalishaji dawa na vifaa tiba wakiwa kwenye mkutano.
  Wafanyakazi wa MSD, wakiwa kwenye mkutano huo.
  Mkutano ukiendelea.
  Mwakilishi wa Wazalishaji wa ndani, kutoka Kiwanda cha Prince Phermaceutical,Hetal Vitalan, akizungumza.
  Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Abdul Mwanja akizungumza.
   Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa MSD, Sako Mwakalobo, akizungumza.
   Mkurugenzi wa Dawa na Bidhaa Nyongeza  wa  Mamlaka ya  Chakula na Dawa (TFDA), Adonis Bitegeko, akizungumza.
  Wazalishaji dawa  wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.


  Na Dotto Mwaibale

  KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt.Mpoki Ulisubisya, amesema uwezo wa Bohari ya Dawa (MSD), umeongeza na kupanua wigo wa uwekazaji na uzalishaji wa dawa nchini.

  Akizungumza kwenye Mkutano wa pili wa mwaka wa MSD na wazalishaji na washitiri wa dawa na vifaa tiba zaidi ya 130 kutoka nchi 25, Dkt. Mpoki amesisitiza kuwa, MSD niya kiwango cha kimataifa hivyo milango iko wazi kwa wawekezaji wa dawa na vifaa tiba kuja kuwekeza nchini.

  Aliongeza kuwa mkutano huo ni fursa ya kubadilishana uzoefu na kujadili namna yakufanya manunuzi,utekelezaji wamikataba na uimarishaji wa uwekezaji katika sekta ya afya.

  “Tunaitikia wito wa serikali wa kuhakikisha wawekezaji wa ndani wanapewa kipaumbele, hivyo mkutano huu wakiutendaji,utaijengea uwezo MSD na kuongeza ushirikiano kati yake na wawekezaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba kwa kujua mahitaji aliyopo na kuwashauri soko tulilonalo ndani na njeya nchi ilikupanua wigo wautendaji,”alisema.

  Aidha alisisitiza  kuwa  uwezo wa MSD katika usambazaji wa dawa na vifaa tiba umekua na  ndio sababu ya kukidhi viwango vya kimataifa, huku  mwaka wa fedha uliopita wakiwa wameweza  kutumia dola milioni 700 kwa ajili ya kufanya manunuzi.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Elisante Ole Gabriel, alisema utendaji wa MSD meboresha huduma za afya nchini na uhusiano wa karibu kati ya wizara yake na sekta ya afya nikichocheo muhimu cha uchumi nchini.

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Rugambwa Bwanakunu, alisema hatua ya bohari kununua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, imewawezesha kupanua wigo wa huduma na  kuwa karibu na wafanyabiashara na wawekezaji 160 alioingia nao mikataba, hivyo mkutano huo utawajengea uwezo na kuongeza ushindani kwa wazalishajihao.

  Aidha, kwa upande wake mwakilishi wa wazalishaji wa ndani, kutoka kiwanda cha Prince Phermaceutical,HetalVitalan, lisema uimarishaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba  hapa nchini,umesaidia fedha inayotengwa na serikali katika bajeti ya dawa  kuweza kukuza uchumi wa ndani,kuongeza ajira kwa watanzania  na kupanua wigo waukusanyaji wa kodi kwa viwanda vya ndani.


  0 0


  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akijibu kero mbalimbali za wananchi katika kijiji cha Mariwanda kata ya Hunyari wilaya ya Bunda mkoani Mara wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Lydia Bupilipili na Mbunge wa Bunda Vijijini, Bonafasi Mwita Getere (kulia). 

  Na Hamza Temba-Bunda, Mara
  .........................................................................

  Kilio cha muda mrefu cha wananchi wa wilaya ya Bunda hususan katika ukanda unaopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kuhusu wanyamapori waharibifu jamii ya Tembo kuvamia makazi yao na  mashamba kinaelekea kupata ufumbuzi wa kudumu.
  Hatua hiyo inakuja kufuatia agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuanzisha mradi wa ufugaji nyuki kwa vijiji kumi vinavyopakana na hifadhi hiyo ili watumike kama uzio wa kudhibiti wanyamapori hao.
  Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mariwanda, kata ya Hunyari wilaya ya Bunda mkoani Mara wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani humo. 
  "TANAPA wakishirikiana na TFS waje waanzishe mradi wa ufugaji nyuki wa kisasa katika vijiji vyote 10 vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa Serengeti, waje wahamasishe uundwaji wa vikundi, wafundishe namna ya kuweka mizinga ya kisasa na namna ya kufuga nyuki na kuvuna, na mwisho wa siku wananchi wapate faida ya kuzuia wanyamapori kuvamia mashamba na makazi yao pamoja na kuvuna asali itakayowatengenezea kipato mbadala" ameagiza Dk. Kigwangalla. 
  Akielezea mbinu hiyo mpya inavyofanya kazi Dk. Kigwangalla amesema, wataalamu ndani ya wizara yake wameeleza kuwa mbinu hiyo ya kuweka mizinga ya nyuki kuzunguka maeneo ya mashamba na makazi ya wananchi itasaidia kudhibiti Tembo  kwakuwa huogopa sana nyuki na endapo wakisikia tu harufu yake huwa vigumu kusogelea maeneo hayo.
  Awali akiwasilisha malalamiko kwa niaba ya wananchi wa vijiji hivyo, Mbunge wa Bunda Vijijini, Bonifasi Mwita Getere alisema kwa muda mrefu sasa wananchi hao wamekuwa wakipata madhara ya kuvamiwa na Tembo ambao hula mazao yao mashambani na hata majumbani, kuwajeruhi wananchi na wengine kupoteza kabisa maisha.
  Baraka Abdul ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mariwanda wilayni humo alisema, mbinu zinazotumika kufukuza Tembo hivi sasa ikiwemo kupiga makelele na madebe na kutumia tochi za mwanga mkali zimekua hazisaidii, hivyo ameiomba Serikali kuongeza idadi ya askari na vituo katika maeneo yanayoathirika zaidi na matukio hayo.
  Wakati huo huo, Waziri Kigwangalla ametoa onyo kali kwa wananchi wanaofanya vitendo vya ujangili na uingizaji mifugo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuwataka kuacha mara moja kwakuwa wakikamatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kutaifishwa mifugo yao kwa mijibu wa kifungu cha 111 Na. 5 cha Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori ya mwaka 2009.
  Katika hatua nyingine, ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kupitia eneo la mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (Bufer Zone) kuanzia Ghuba ya Speke hadi kwenye mpaka na nchi ya Kenya, wabaini mipaka halisi na ramani na kuainisha mahitaji ya wananchi na changamoto zilizopo na hatimaye kuwasilisha kwake mapendekezo ya kuondoa changamoto zilizopo.Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na uongozi wa wilaya ya Bunda alipowasili wilayani hapo jana kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja.Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza uongozi wa wilaya ya Bunda ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Lydia Bupilipili (kulia kwake) wakati wa ziara yake ya siku moja kwa ajili ya kutatua changamoto za uhifadhi wilayani humo jana. 
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kata Nyatwali wakati wa ziara yake ya siku moja kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali za uhifadhi katika wilaya ya Bunda mkoani Mara jana. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TANAPA, Martin Loibooki na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili (wa pili kulia). 
  Mwananchi wa kata Nyantwali akitoa maoni yake kwa Waziri Kigwangalla.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bukore wakati wa ziara yake ya siku moja kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali za uhifadhi katika wilaya ya Bunda mkoani Mara jana.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini, Bonifasi Mwita Getere muda mfupi baada ya kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Bukore wakati wa ziara yake ya siku moja kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali za uhifadhi katika wilaya ya Bunda mkoani Mara jana.
  Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mariwanda  wakati ziara ya Waziri Kigwangalla wilayani humo.
  Baraka Abdul, mkazi wa kijiji cha Mariwanda akiwasilisha maoni yake kwa waziri Kigwangalla katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.
  Dk. Kigwangalla akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mariwanda.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akijibu akifafanua jambo katika mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Mariwanda kata ya Hunyari wilaya ya Bunda mkoani Mara wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo jana.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Dk. James Wakibara akifafanua jambo kwenye mkutano huo.
  Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mariwanda wakimasikiliza Waziri Kigwangalla (hayuko pichani) wakati wa mkutano wa hadhara kijijini hapo.

  0 0

  Na .WAMJW-Tabora

  Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto inatarajia kupeleka shilingi milioni 300 kwenye hospitali ya rufaa ya Mkoa ya Kitete kwa ajili ya kupanua wodi ya wazazi pamoja na ununuzi wa vifaa vya upasuaji kwa kumtoa mtoto tumboni Mkoani humo

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipotembelea hospitali hiyo ziara ya kikazi mkoani hapa.

  "tutaleta fedha hizi kabla ya desemba mwaka huu ili kuhakikisha kila mwanamke mjamzito anajifungua salama na mtoto wake anakua salama pia"alisema Waziri Ummy.Aidha,aliwaagiza hospitali hiyo kununua vifaa vyote muhimu vinavyowezekana kuliko kusubiri wizara iwaletee'lazima mjiongeze na kuwa wabunifu muwe na vitu muhimu ili msonge mbele'alisisitiza

  Hata hivyo aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na miiko ya utumishi wa umma ili kuondoka malalamiko kwa wananchi wanaofika kupata huduma katika hospitali hiyo.
   Picha jengo la upasuaji lililopo katika hospitali hiyo
   Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt.Gunini Kamba akimueleza Waziri wa Afya vifaa vilivyofungwa kwenye chumba cha upasuaji vilivyofungwa kwenye jengo la Upasuaji lililojengwa hospitalini hapo
   Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akimbeba mtoto mchanga aliyezaliwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kitete Mkoani Tabora.

  0 0

  Na Rachel Mkundai, Arusha

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha kwamba pato la Serikali na kodi stahiki inapatikana kupitia sekta ya utalii nchini.

  Akizungumza Jijini Arusha, Kamishna wa Kodi za Ndani, Bwana ELIJAH MWANDUMBYAamesema kwamba, sekta ya utalii ni moja ya sekta inayoiingizia Serikali fedha nyingi za kigeni na hivyo inahitaji mkakati madhubuti ili kuongeza pato kwa Serikali

  “Sekta ya utalii inaingizia serikali fedha nyingi za kigeni, TRA tumekuja na mkakati maalum ili kuhakikisha kuwa sekta hii inachangia pato la taifa kupitia kodi stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi”, amesema Kamishna wa kodi za ndani.

  Mwandumbya ameongeza kuwa kwa muda mrefu sekta ya utalii imekuwa ikifanya vizuri lakini bado inahitaji mkakati wa kuhakikisha kwamba kila pato linaloingia kupitia sekta hii linaongeza tija kwenye mapato ya nchi kupitia kodi mbalimbali kama zilivyoainishwa na sheria za kodi.

  Aidha, Kamishna Mwandumbya amefafanua kuwa moja ya mikakati hiyo ni kushirikiana na taasisi zingine za serikali zilizopo kwenye sekta ya utalii zikiwemo Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Chama cha wafanyabiashara wa Utalii (TATO) pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii na wadau wengine wanaojihusisha na utalii.

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Bwana Allan Kijazi amesema TANAPA ipo tayari kushirikiana na TRA pamoja na taasisi zingine za serikali kwa kuwa lengo ni kukusanya mapato ya serikali na hivyo kuhakikisha kuwa mapato yanayopatikana kupitia utalii yatanufaisha nchi kwa kuleta tija katika mapato.

  “Sisi sote ni taasisi za serikali , tunajenga nyumba moja, tutashirikiana nanyi ili serikali yetu Isimame imara na kupata kodi stahiki”, amesema Bw Kijazi.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bwana Wilberd Chambulo amewataka Wafanyabiashara wanaojihusisha na masuala ya utalii kujenga utamaduni wa kulipa kodi kwa manufaa ya nchi ambapo pia ameunga mkono ujio wa mkakati huo maalum wa TRA wa kuongeza mapato kupitia sekta ya utalii.

  Sekta ya utalii inatajwa kuwa moja ya sekta inayoiingizia Serikali fedha za kigeni hata hivyo takwimu zinaonesha kuwa kuna wafanyabiashara 2,200 wanaotambulika katika utalii nchini na kati ya hao 1,403 wanafanya shughuli zao katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga 

  Hivyo, utekelezwaji wa mkakati huo utaipelekea Serikali kuongeza makusanyo ya mapato yake na kukuza maendeleo kwa wananchi katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii.

  Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.
  Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Arusha, Bw. Faustine Mdesa (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara ya kikazi ya Kamishna wa Kodi za Ndani Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.
  Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kulia) akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo (kushoto) akimwelezea jambo Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya pamoja na watendaji wengine wa TRA aliofuatana nao kuhusu namna sekta ya utalii nchini inavyochangia pato kubwa kwa Serikali wakati wa ziara ya kikazi ya Kamishna huyo Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini. (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA)

  0 0

  Watalii kutoka nchini Uswisi Daniel Gehring na Andre Luethi wakitalii Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli kwa muda wa siku saba na kufanikiwa kufika kilele cha juu kabisa cha Uhuru. 

  0 0

  Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

  WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezindua fao la Ushirika Afya ambalo linawalenga wananchi wanaojishughulisha na kilimo kupitia ushirika.

  Amezindua fao hilo jana (Jumatatu, Julai 16, 2018) kwenye mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ulowa katika kijiji cha Kangeme, kata ya Ulowa, Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama, Shinyanga.

  Waziri Mkuu alikabidhi kadi 20 kwa niaba ya wanachama 259 ambao wamejiunga na mpango huo. Wanachama hao wanatoka katika vyama mbalimbali vya ushirika kwenye Halmashauri ya Ushetu, wilayani Kahama.

  Amesema katika kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanapata huduma za afya katika hospitali yoyote ile nchini, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, wameamua kuzindua mpango wa Ushirika Afya, ambao unahusisha wakulima walio katika vyama vya ushirika.

  “Gharama ya kujiunga na fao hili kwa mwaka ni sh. 76,000 kwa mtu mmoja na sh. 50,400 kwa mtoto mmoja lakini unakuwa na uhakika wa kutibiwa katika hospitali yoyote ile hapa nchini,” amesema.

  Amesema takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa Tanzania kuna vyama vya ushirika 10,522 vyenye wanachama 2,234,000 ambapo asilimia 35 ya wanaushirika huwa wanapata magonjwa ya dharura na wanakuwa hawana namna ya kupata fedha kwa haraka.

  “Tunatambua wote kuwa fedha ya mkulima ni ya msimu, lakini mkulima ukiwa na kadi ya bima ya afya, utapata matibabu kokote kule hata kama huna fedha taslimu,” amesema.Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumpongeza kijana aliyebuni mpango huo ambaye anatoka Taasisi ya Ukuzaji wa Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), Mwombeki Baregu. 

  “Huyu kijana si mwajiriwa wa NHIF, wala siyo mtumishi Serikalini, lakini kwa sababu ya uzalendo, alikuja na huu mfumo akauelezea na kuonesha manufaa yake kwa wananchi wa kawaida, na kwa sababu Serikali yenu ni sikivu, tukaufanyia kazi na leo ninauzindua,” amesema.

  Mapema, akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga amesema kuna vyama vya ushirika takribani 10,000 ambavyo vina wanachama zaidi ya milioni 2.5 wanaojishughulisha na kilimo cha mazao mbalimbali ikiwemo pamba, korosho, tumbaku, chai na kahawa."Lengo letu ni kuwafikia wanachama hawa pamoja na familia zao ili kuwawezesha wapate huduma katika kipindi cha mwaka mmoja tangu siku alipochangia. 

  "Kupitia utaratibu huu, mwanachama atapata huduma za uchunguzi na matibabu katika vituo zaidi ya 6,000 vilivyosajiliwa na mfuko wetu nchi nzima," amesema.

  Ameongeza “Kupitia mpango huu wa ushirika afya, mwanachama atapata huduma za vipimo na matibabu mpaka ngazi ya Taifa kulingana na ushauri wa wataalam. Mfuko kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, itaendelea kutoa elimu kwa wanachama wa ushirika kwa lengo la kuongeza uelewa wa mpango huu kwa walengwa.” 

  Amesema NHIF imeufanyia maboresho mpango huo ambapo kwa sasa wameanzisha vifurushi mbalimbali ambapo mwanachama ataweza kuchagua kulingana na uwezo wake na ukubwa na hali ya familia yake.

  “Vifurushi hivyo vinaanzia kwa mwanachama aliye peke yake, aliye na mwenza, aliye na mwenza na mtoto mmoja, wawili mpaka wanne. Kwa mwanachama asiye na mwenza lakini ana familia, mpango huu umeweka utaratibu wake,” amefafanua.

  Akitoa shukrani kwa Waziri Mkuu, Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF, Mama Anne Makinda amesema uzinduzi uliofanyika jana umewakilisha kuzinduliwa kwa fao hilo kwenye mikoa yote nchini. 

  Amesema wana mpango wa kwenda kwenye mikoa yote inayozalisha mazao makuu matano ya kimkakatii ambayo ni chai, kahawa, pamba, tumbaku na korosho ili waweze kuwafikia wananchi wengi kwa urahisi.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi kadi ya bima ya afya mmoja wa wakulima waliopo kwenye Ushirika huo ambapo wanachama 120 wamepatiwa kadi hizo na wanachama 200 wameshajaza fomu za kijiunga
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe mfano wa kadi ya bima ya afya kwa matibabu kwa vyama vya Ushirika wilayani Ushetu
   Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa akimkabidhi kadi ya bima ya afya ya Ushirika Waziri Ummy Mwalimu
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bernad Konga akizungumzia Fao hilo ambalo litawanufaisha wakulima wa mazao waliopo kwenye vyama vya msingi.
   Wananchi wa kata ya Ulowa wakifuatilia uzinduzi huo.

  0 0


  Na Khadija Seif , Globu ya jamii  .
   
  CHAMA cha Wanawake Waandishi wa Habari Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ya kutoka nchini Canada na mataifa ya Ulaya wamefanya uzinduzi wa filamu inayohusu maisha ya binti wa kike inayojulikana kama  In the name of your daughter.

  Uzinduzi wa filamu hiyo umefanyika jana katika ukumbi wa Alliance Francie's jijini dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi wa  ndani na nje ya nchi.

  Filamu hiyo inazungumzia maisha ya watoto wa familia zenye utamaduni wa ukeketaji hasa mkoani Mara wakiwa bado wanaendelea na mila hiyo potofu inayowakandamiza  watoto wa Kike kwakuwa  hawajapata elimu ya kutosha kuhusu athari zake.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mwakilishi kutoka Serikalini   Grace Mwangwa  amesema jamii bado zinahitaji elimu ya kutosha ili kupiga vita dhidi ya ukeketaji na kwamba Serikali inaunga mkono jitihada zinazofanywa na mashirika ili kumkwamua mtoto wa kike kufikia malengo yake.

  Mwangwa amesema baadhi ya jamii  wameichukulia  desturi hiyo kama  sheria kwao na watoto wengi hunyanyasika pindi wanapokataa kufanyiwa kitendo hicho na hata kutengwa na jamii kabisa .

  Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA  Edda Sanga  amesema  chama chao kimefanya juhudi na jitihada na kuona kwa namna moja au nyingine kushirikiana na vyombo vya habari kutokomeza vita hiyo ya ukatili wa kijinsia.

  "Kwani kwa kiwango kikubwa mpaka sasa ndoa za utotoni zimepungua kutokana na elimu kufika sehemu mbalimbali pamoja na madhara yake kubainishwa  na kuwepo kwa Sheria kali kwa wanaojihusisha na uhalifu huo wa kumnyima haki za msingi mtoto wa kike,"amesema.

  Pia ameeleza kuwa  vituo vya kuhifadhi wahanga hao hasa watoto wa kike vilijengwa kwa ajili yao kutokana na kutengwa na familia zao na kubaki wakizurura maporini ambapo yanahatarisha maisha yao endapo watakutana na wanyama wakali au hata kujiingiza kwenye ulawiti au kubakwa .

  Wakati huo huo Mratibu wa Save House Robi Samweli amesema anashirikiana pia  na  dawati la jinsia ,mwenyekiti wa mtaa ,Ofisa ustawi na Jeshi la polisi kukamata wahalifu wanaojihusisha na ukatili huo.

  "Kushirikiana na mashirika mbalimbali tumeweza kujenga nyumba hizo kwa ajili ya kuwahifadhi ili kuwanusuru kwenye janga hilo,na watoto wameonyesha muamko kwani baadhi yao yameweza kuja pasipo kushawishiwa na mtu na wengine kubaki kuishi hapo kutokana na kutoamini tena familia zao," amesema.

  Anafafanua zaidi imani zilizojengeka na sababu zinazowasabisha watoto hao kufanyiwa hivyo ni pamoja na kujipatia utajiri pindi msichana husika anapoolewa kwani msichana aliyefanyiwa kitendo hiko anapewa ng'ombe 10 hadi 11. Wakati msichana ambae hajafanyiwa hupewa ng'ombe saba.

  Hata hivyo watoto wengi wanakosa amani mashuleni kwani wanaingia kwenye wakati mgumu wa kufikiria wakati wowote watafanyiwa kitendo hiko. Na baadhi ya familia wamekua wakiwatia hofu watoto hao na kuwatenga kuwa endapo hawatokeketwa hawataweza kuishi tena kwenye familia zao.
    Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA  Edda Sanga akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa filamu ya "In The Name of Your Daughter" inayohusu ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike katika Ukeketaji.
  Baadhi ya waalikwa wakifuatilia filamu hiyo

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam John Kayombo amemtangaza Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Pascal Manota kuwa mshindi katika uchaguzi mdogo ulioitishwa nchini katika Kata ya Kimara.

  Kayombo  amemtangaza Manota kuwa Diwani Mteule kutokana na madiwani wengine kutoka vyama upinzani kushindwa kujibu hoja za mapingamizi aliyowawekea kama mapungufu wakati wa ujazaji wa fomu.

  “Vyama vilivyoweza kuchukua fomu ya kugombea Udiwani katika Kata ya Kimara ni , ACT-Wazalendo, Chadema, CUF na CCM lakini kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika ujazaji wa fomu Pascal Manota namtangaza kama Diwani Mteule aliyepita bila ya kupingwa,”amesema Kayombo.

  Kwa Upande wake Manota ambaye ni Diwani Mteule katika Kata ya Kimara amewetaka wapinzani kuacha siasa za uongo za kuwasingizia watendaji kuwa ndio wanaharibu uchaguzi wakati wao ndio wa kwanza kuvunja taratibu za uchaguzi na sharia zilizowekwa.

  Amesema wagombea wote walichukua fomu na zikajazwa na kubandikwa katika mbao ya matangazo katika Kata, hivyo baada ya kuona mapungufu ya wagombea wake aliamua kuwawekea mapingamizi.Kutokana na mapingamizi hayo wagombea wote wametupwa nje.

  Amesema kuwa sasa anasubiri kuapishwa ili aendelee kuwatumikia wakazi wa Kimara na hatimaye wapate maendeleo ya kweli kupitia Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo , John Kayombo ambaye pia ndio Msimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri hiyo akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo kuwa Ndugu Pascal Manota kapita bila kupingwa.
  Diwani Mteule wa Chama Cha Mapinduzi Pascal Manota akisaini kitabu cha kupokea barua ya kuwa Diwani Mteule aliyepita bila kupingw akatika kata ya Kimara.
  Diwani Mteule wa Chama Cha Mapinduzi Pascal Manota akipokea barua ya kuwa Mshindi wa uchaguzi mdogo kwa kupita bila kupingwa mara baada ya kuwashinda wapinzani wake kwa mapingamizi
  Diwani Mteule wa Chama Cha Mapinduzi Pascal Manota akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya kutangazwa mshindi

  0 0

  *Ahimiza hivyo kujikita kujenga uchumi imara ili wananchi wapate huduma bora.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii
  UKOMBOZI wa sasa kwa vyama tawala katika nchi za Afrika  ni vema wakajikita katika katika kujenga uchumi katika sekta mbalimbali ili wananchi wapate huduma bora.

  Hayo ameyasema Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.John Magufuli wakati akifungua Mkutano wa Vyama vya siasa ambavyo vilivyopigania ukombozi kwa nchi za Kusini mwa Afrika ambapo vina uhusiano na Chama cha Kikomonisti cha China (CPC) uliofanyika leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

  Rais Dk.John Pombe Magufuli amesema kuwa chama cha CPC kimekuwa na uhusiano ya muda mrefu na kilisaidia ukombozi katika Afrika kwa kutoa silaha lakini sasa wamekuwa na maendeleo ambapo lazima kujifunza kutoka kwao.

  Amesema kuwa nchi za Afrika zitoke katika mnyororo wa unyonyaji na kuingia katika uchumi wa kujitegemea. Amesema kuwa nchi ya China imekuwa ikitoa msaada bila masharti na kwamba kinachofanyika maelewano na msaada unatoka.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia viongozi wa vyama vya Siasa kutoka nchi za mbalimbali za Afrika kabla ya kufungua mkutano kati ya viongozi wa vyama hivyo na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na  Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao akizungumza katika mkutano huo wa viongozi wa vyama vya Siasa kutoka nchi za mbalimbali za Afrika na Chama hicho cha CPC jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bashiru Ally akihutubia katika mkutano huo.
  Washiriki wa Mkutano huo wakifatilia kwa makini hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na  Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao mara baada ya kufungua mkutano huo jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
  0 0

  katika kuwafikia wananchi na kuwaelimisha kuhusu maswala ya haki za binadamu na msaada wa kisheria , taasisi ya Peoples Development Forum(PDF) chini ya ufadhili wa Legal Services Facility imeendesha Tamasha la burdani na kutoa elimu mbagala mkoani Dar es saalam

  katika tamasha hilo elimu juu ya haki katika ujasiriamali na maswala mbalimbali ya haki na sharia ilitolewa na vilevile watoa huduma za msaada wa kisheria (paralegal) kutoka Temeke walipata fursa ya kuongea na wananchi na kuandikisha matatizo yao yanayohitaji msaada wa kisheria

  LSF kwa kushirikiana na wadau wake nchi nzima imekuwa ikiwawezesha watanzania kwenye kila wilaya Tanzania bara na Zanzibar kupata msaada wa huduma za kisheria kupitia watoa huduma za msaada wa kisheria bila gharama yoyote

  kupitia mradi huu unaofadhiliwa na DANIDA na DFID , LSF imewawezesha wananchi kupata haki zao, utatuzi wa migogoro midogo midogo na msongamano mahakamani, imetoa elimu juu ya maswala mbalimbali ya kisheria na kuelimisha jamii umuhimu wa kulinda haki za binadamu, lakini pia imeshirikiana na serikali, kupitia wizara ya Katiba na Sheria, katika uandaaji na hatimaye kupitishwa kwa sheria mpya ya kutambua wasaidizi wa kisheria nchini (Legal Aid Act 2017).

  Lengo kubwa la mradi huu ni kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa jamii maskini hususani wanawake na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa kuamasisha jamii kuheshimu haki za binadamu.


  Bi Stella Singano, mtoa huduma za msaada wa kisheria (Paralegal) kutoka Temeke, akitoa elimu juu ya haki za ujasiriamali kwa wakazi wa Mbagala wakati wa Tamasha la uhamasishaji lililoandaliwa na Peoples Development Forum(PDF) chini ya ufadhili wa LSF.
  Kikundi cha sanaa cha Machozi kikitumia sanaa kufundisha jamii kuhusu haki za binadamu na usaidizi wa kisheria katika tamasha lililofanyika Mbagala jijini Dar es Salaam.
   

  0 0

  Na Said Mwishehe, Globu ya jamii 

  KAMPUNI ya Phimona Ltd inayojihusisha na ushauri wa biashara na mawasiliano kwa kushirkiana na wadau waliobobea kuhamasisha uwekezaji imetangaza kufanyika kwa Maonesho ya kukuza uwekezaji Tanzania(TIPEC). 

  Uamuzi huo una lengo la kuitambua , kutengenezea andiko na kuitangaza miradi kwa ajili ya uwekezaji hasa kwa kutambua eneo hilo halijanyiwa kazi kikamilifu. 

  Wakati wa kutangaza maonesho hayo leo jijini Dar es Salaam mbali ya Phimona pia walikuwa wadau wengine wakiwamo TanTrade, TNBC, EPZA, TCCIA, NDC, TBC na TSN. Akizungumzi maonesho hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Phimona Rodgers Mbaga amesema kupitia maonesho hayo yanayofahamika kwa jina la TIPEC yatawaleta pamoja wenye miradi inayotafuta wawekezaji na wenye mitaji. 

  Ameongeza na kwa upande mwingine inawaleta wawekezaji na wenye mitaji kuja kukutana ana kwa ana na wenye miradi. Amesema lengo la maonesho hayo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kutangaza na kukuza uwekezaji wameamua kuaandaa maonesho ili kukuza miradi na kutafuta wawekezaji na wenye mitji. 

  "TIPEC 2018 itaitambua , kutengenezea andiko na kuitangaza miradi isiyopungua 300 .Ingawa sekta nyingine itatangazwa pia.Mkazo utakuwa kwa miradi ya viwanda na kilimo,"amesema. Mbaga amesema maonesho hayo yatafanyika kuanzia Novemba 14 hadi 16 mwaka huu kwenye hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam. 

  Ametumia nafasi hiyo kuelezea kuwa wanakaribisha maombi kwa wale ambao wana mawazo ya biashara na wanajitaji kuandikiwa andiko kwa ajili ya kupata mtaji na wale ambao wanahitaji kukutanishwa na wawekezaji. Kwa upande wa Meneja Ukaguzi Biashara wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade) Stephen Koberou amesema maonesho hayo ni muhimu hasa katika kipindi hiki cha ujenzi wa viwanda nchini. 

  Wakati Mkuu wa Kitengo cha Masoko-TSN Goodluck Chuwa amesema kwa upande wao wamebobea katika kutangaza fursa zilizopo nchini na wamekuwa wakiifanya kazi hiyo ndani na nje ya nchi kupitia majukwaa ya kibiashara wanayoyaandaa. 

  Kwa upande wa Meneja Huduma wa TCCIA Fatma Hamis amesema kwa kutumia mtandao wao uliosamba nchini kote watatoa hamasa ya maonesho hayo ambayo wanamini yafungua fursa kwa watanzania.
  Meneja Uwekezaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Said Tunda akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kufanyika kwa Maonesho makubwa ya kukuza Uwekezaji kuanzia Novemba 14-16, mwaka huu jijini kwa udhamini wa makampuni mbalimbali ikiwemo Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN Ltd). Kutoka kushoto kwake ni Mchambuzi wa Mazingira ya Biashara (TNBC), Kabenga Kaisi, Mkuu wa Kitengo cha Masoko TSN, Goodluck Chuwa, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Phimona Ltd, Rodgers Mmbaga, Meneja Ukuzaji Biashara wa TANTRADE, Stephen Koberou na Meneja Huduma na Uanachama wa TCCIA, Fatuma Hamis.

  0 0


   Wakili wa Kujitegemea kutoka Haki Advocates,  Aloyce Komba akitoa Mada ya utoaji wa Habari za Kimahakama kwa waandishi wa Habari za Mahakama wanaoshiriki katika mafunzo ya Uandishi wa Habari za Kimahakama katika Ukumbi wa Magadu mkoani Morogoro. 
  Naibu Msajili, Mahakama Kuu,  Augustino Rwizile akitoa mada ya ‘Hatua mbalimbali za Mashauri ya Jinai na Madai’, lengo ni kuwaelimisha zaidi Waandishi hao juu ya hatua/taratibu mbalimbali katika uendeshaji wa mashauri hayo. 
  Afisa Tehama kutoka Mahakama ya Rufani-Tanzania, Allan Machella akitoa mada ya ‘Njia kuelekea Mahakama Mtandao, Mipango na Mafanikio.’
  Mwandishi wa Nipashe, Hellen Mwango akichangia mada katika mafunzo hayo.
   Washiriki wakifuatilia mada kwa umakini.
  (Picha na Mary Gwera)

  0 0

  Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mwenzao kutoka nchini China wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa bila kufungua kifua kupitia tundu dogo lililotobolewa katika paja (Catheterization) wa kuzibua mshipa wa moyo ambao haupitishi damu vizuri kwa kutumia mtambo wa Cathlab. Kwa mwaka huu wa 2018 madaktari watatu wametolewa na Serikali ya China kwaajili ya kufanya kazi ya Matibabu ya Moyo katika Taasisi hiyo. 
  Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa bila kufungua kifua kupitia tundu dogo lililotobolewa katika paja (Catheterization) wa kuzibua mshipa wa moyo ambao haupitishi damu vizuri . 
  Madaktari bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na mwenzao kutoka nchini China wakimfanyia upasuaji wa moyo mtoto mwenye umri wa miaka 13 wa kuziba tundu la moyo na kufungua njia inayopeleka damu kwenye mapafu. Kwa mwaka huu wa 2018 madaktari watatu wametolewa na Serikali ya China kwaajili ya kufanya kazi ya Matibabu ya Moyo katika Taasisi hiyo. Picha na JKCI.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao wakati wa dhifa ya Kitaifa aliyowaandalia Viongozi wote wanaoshiriki Mkutano huo jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao wakati wa dhifa ya Kitaifa aliyowaandalia Viongozi wote wanaoshiriki Mkutano huo jijini Dar es Salaam.
  Viongozi wa vyama vya siasa kutoka nchi mbalimbali za Afrika pamoja na Chama cha Kikomunisti cha China cha CPC wakiwa katika Dhifa hio ya kitaifa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao wakiangalia burudani kutoka katika kikundi cha TOT katika Dhifa hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao akizungumza katika hafla hiyo ya chakula cha jioni. 
  Kikundi cha TOT kikitumbuiza katika Dhifa ya kitaifa Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao mara baada ya hafla hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya Dhifa ya Kitaifa Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  0 0


  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima mtego wa misumari uliotegwa na watu wasiojulikana kwa lengo la kuzuia msafara wake wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.


  Tarime - Mara
  .......................................................
  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameliagiza Jeshi la Polisi wilaya ya Tarime mkoani Mara kumkamata na kumfungulia mashtaka Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wa Wilaya hiyo, Newton Mongi na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya wilaya hiyo, Richard Tiboche kwa tuhuma za kuikashifu Serikali na kuchochea mgogoro wa mpaka kati ya hifadhi ya Serengeti na vijiji jirani.

  Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana majira ya saa tatu usiku baada ya kuhitimisha ziara yake wilayani humo iliyolenga kutafuta suluhu ya mgogoro uliodumu kwa miongo kadhaa kuhusu mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani ikiwemo kijiji cha Kegonga.

  Akiwa njiani majira ya saa tatu za usiku kwenye gari la wazi baada ya kukagua eneo hilo la mpaka kwa zaidi ya masaa sita, Waziri Kigwangalla na msafara wake walikuta lundo la mawe yakiwa barabarani ndani ya eneo la hifadhi hiyo, hali iliyosababisha taharuki kubwa na msafara wake kushuka na kuanza kuondoa mawe hayo ili kupata njia ya kupita.

  Wakati zoezi hilo likiwa linaendelea, Kiongozi huyo wa UVCCM alisikika akiituhumu Serikali kwa kuweka mawe hayo na kwamba hayakuwekwa na wananchi wa eneo hilo, jambo lililozua mshangao mkubwa kwa viongozi wa Serikali waliokuwepo katika msafara huo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.

  Mkuu huyo wa mkoa alisema tukio hilo sio la mara ya kwanza na kwamba limewahi kuripotiwa mara nyingi na uongozi wa hifadhi hiyo kuwa wananchi wa vijiji jirani hujaza mawe barabarani kwa ajili ya kuzuia magari ya doria ili waweze kulisha mifugo yao ndani ya hifadhi hiyo. Alisema hata msafara wa tume ya Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda iliyoundwa na CCM hivi karibuni kufuatilia mgogoro katika eneo hilo nao ulizuiliwa kwa mawe barabarani.

  Imedaiwa pia kuwa kwa nyakati tofauti viongozi hao wamekuwa wakiwatolea viongozi wa Serikali maneno ya kejeli pamoja na kuwakwamisha kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi ipasavyo.Awali, kabla ya tukio hilo la mawe barabarani moja ya gari lililokuwa likiongoza msafara huo lilipata pancha baada ya kukanyaga misumari iliyokuwa imetengwa kwenye moja ya barabara zinazoingia na kutoka ndani ya Hifadhi ya hiyo ya Serengeti.

  Waziri Kigwangalla alisikitishwa na kitendo hicho ambacho alikielezea kuwa sio cha kiuungwana kwa kuwa kinalenga kudhoofisha juhudi za Serikali kumaliza mgogoro huo kwa faida ya pande zote.
  "Mimi ni Muislam, nimesikia kwa masikio yangu na wala sijaambiwa na mtu yeyote na siwezi kumsingizia mtu, nimeshangazwa sana na kiongozi tena mtendaji wa chama tawala anawezaje kuitukana Serikali, na hapa sisi tumekuja kuwahudumia wananchi" alisema Dk. Kigwangalla kwa masikitiko makubwa.

  Wakati huo huo, Waziri Kigwangalla ametoa miezi mitatu kwa wananchi wote waliovamia ndani ya Hifadhi ya Serengeti na eneo la wazi (buffer zone) ambao wanaendesha shughuli zao ikiwemo kilimo, ufugaji na makazi kuachia maeneo hayo kwa hiari yao wenyewe, na kwamba muda huo ukipita wataondolewa kwa nguvu na chochote kitakachokutwa ndani ya eneo hilo kitatekezwa kwa mujibu wa sheria.

  Akizungumzia kuhusu suluhu ya mgogoro huo wa mpaka amesema, Serikali itaunda timu ya wataalam kutoka wizarani kwake, wizara ya ardhi, uongozi wa mkoa wa Mara na wilaya ya Tarime ambao watashirikiana na watu wengine huru watakaochaguliwa na wananchi wa vjiji husika wakiongozwa na mbunge wao, John Heche ambao watakuwa na uelewa wa kusoma ramani na kutafsiri mipaka ili kushirikiana kuhakiki mipaka halisi ya eneo hilo na kufikia muafaka.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (kushoto) na viongozi wengine wa mkoa huo wakiangalia mawe yaliyowekwa njiani kuzuia msafara wake kutoka ndani hifadhi ya Serengeti na watu wasiojulikana wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya hifadhi hiyo na vijiji jirani jana usiku.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, viongozi wa mkoa wa Mara na wananchi wa vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakikagua eneo la mpaka lenye mgogoro kati ya vijiji na hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mbunge wa Tarime John Heche wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa eneo lenye mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani na Mbunge wa Jimbo la Tarime, John Heche wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro huo mkoani Mara jana. Katikati aliyeinama ni Mkuu wa Mkoa huo, Adam Malima.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, viongozi wa mkoa wa Mara na wananchi wa vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakikagua eneo la mpaka lenye mgogoro kati ya vijiji na hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, viongozi wa mkoa wa Mara na wananchi wa vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakikagua eneo la mpaka lenye mgogoro kati ya vijiji na hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisoma taarifa mbalimbali kuhusu mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani vya wilaya ya Tarime mkoa wa Mara wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya ya Tarime mkoani Mara kwa ajili ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya vijiji na hifadhi hiyo jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Mbunge wa Jimbo la Tarime, John Heche.

older | 1 | .... | 1623 | 1624 | (Page 1625) | 1626 | 1627 | .... | 1897 | newer