Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1621 | 1622 | (Page 1623) | 1624 | 1625 | .... | 1897 | newer

  0 0  0 0


  0 0

  Ofisi Ndogo ya Makao Makuu, Lumumba, Dar es Salaam
  13 Julai 2018

  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuujulisha umma wa watanzania kuwa tarehe 17-18 Julai 2018 kutafanyika Mkutano wa Kidunia wa Vyama vya Siasa, Kikao Maalum cha Afrika, Jijini Dar es Salaam. Mkutano huu utaleta zaidi ya vyama vya siasa 38 kutoka Afrika na zaidi ya washiriki 130 kutoka nje ya Afrika. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepata heshima kubwa kuwa mwenyeji wa Mkutano huu wa kidunia.

  Mkutano huu umeandaliwa kwa ushirikiano wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Mkutano huu ni sehemu ya matokeo mazuri ya utendaji kazi wa uongozi wa awamu ya tano ya Chama na Serikali chini ya Ndg. John Pombe Joseph Magufuli, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Mkutano huu wa kihistoria na wa kwanza kufanyika Barani Afrika ni wapili kufanyika baada ya Mkutano kama huu wa kidunia kufanyika Jijini Beijing, China Mwezi Disemba mwaka 2017. Mkutano wa mwezi Disemba 2017 uliandaliwa na Chama Cha Kikomunisti Cha watu China (CPC) na Kiongozi Mwenyeji wa Mkutano huu alikuwa ni Kamaradi Xi Jinping Katibu Mkuu wa CPC na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China.

  Mkutano huu wa utahudhuriwa pamoja na wajumbe wengine wa mkutano ni Kamaradi Song Tao Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Watu wa China, Kamaradi Xu Luping Makamu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China na Kiongozi Mwenyeji wa Mkutano huu wa Kidunia wa Vyama vya Siasa ni Kamaradi John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Wazo la Mkutano huu wa kidunia linatokana na fikra za Kamaradi Xi Jinping Katibu Mkuu wa CPC na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China ambaye anapendekeza fikra ya mwelekeo mpya wa namna tunaenenda kidunia kwamba, “tushirikiane kujenga jamii ambayo ina matarajio ya pamoja ya baadaye na kufanya kazi pamoja ili kujenga Dunia bora”. Fikra hizi za Kamaradi Xi ndio zilizopelekea majadiliano ya kidunia kati ya CPC na Vyama vya Siasa vya Kidunia.

  Mwaka huu Nchi ya China inatimiza miaka 40 ya kufanya Mageuzi na Kuchangamana Kimataifa na Mkutano huu wa Dar es Salaam utakuwa hatua kuelekea katika Kongamano kubwa la ushirikiano wa China na Afrika (Forum on China-Africa Cooperation – FOCAC) litakalofanyika jijini Beijing, China. Kwa hiyo ni dhahiri kwamba Tanzania, Afrika na China katika Mkutano huu watajikita katika mjadala mpana na wa kina wa kuziangazia changamoto na fursa lukuki zitokanazo na kujengeka zaidi kwa mahusiano na mashirikiano ya Afrika na China.

  Jambo moja ambalo lina mfanano mkubwa kati ya China na Tanzania na CCM na CPC ni itikadi ambayo inatoa mwelekeo wa Sera za China na Tanzania. Mataifa haya mawili na vyama viwili ambayo ndio vinatoa uongozi katika nchi hizi mbili zinaamini katika Itikadi ya Ujamaa. China imeongozwa kwa mafanikio kwa zaidi ya miaka 40 sasa na Siasa na Itikadi ya Ujamaa wa Kisayansi ambao unashajihishwa na tabia ya Taifa la China “Socialism with Chinese characteristics”. Itikadi hii ya Ujamaa ndio imewezesha mafanikio ya Mageuzi na Mapinduzi makubwa ya kimfumo, kiutendaji, kiuongozi, kiuchumi na kisiasa ambayo Taifa la China limeyatenda katika kipindi hiki za miaka 40.

  Wakati huu China imeanza awamu mpya ya Mageuzi na Mtangamano wa Kimataifa na inaweka jitihada kubwa kufikia lengo la kujenga Taifa la kijamaa la kisasa na imara ifikapo mwaka 2050. Wakati China inaweka malengo haya makubwa ifahamike kwamba Bara la Afrika likiwa mojawapo ya mabara yanayokua haraka kiuchumi, kwa idadi ya watu, kwa utangamano na uwezekano mkubwa wa uchumi wake kukua kwa faida na tija duniani; Afrika pia imejitoa kuhakikisha inafikia Mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kujitengenezea njia yake ya kukua kulingana na mazingira ya Afrika “exploring independent path of modernisation”.

  Katika njia hii ya pamoja kuelekea katika lengo la pamoja na kwa lugha rahisi “kushughulika na shida za watu wetu”, CPC iko tayari kuimarisha utaratibu wa kubadilishana taarifa, maarifa na watu pamoja na vyama vya siasa vya Afrika ili kujenga jamii ya pamoja ya Afrika na China na yenye lengo la pamoja kuhusu maisha bora ya sasa na ya baadaye kwa watu wetu.

  Mada kuu ya Mkutano huu wa kidunia itakuwa ni Juhudi (vitendo) na Nadharia za Vyama vya Afrika na Chama Cha Kikomunisti cha China katika kufanya uchaguzi wa njia sahihi za kujiletea maendeleo na zinazoendana na mazingira ya nchi zetu za Afrika.

  Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama Cha Kikomunisti Cha China na vyama vyote vitakavyoshiriki katika Mkutano huu wa kidunia vitakuwa na majadiliano ya kina na ya kweli na kubadilisha taarifa na maarifa mbalimbali. Baadhi ya mada ndogo zitakazojadiliwa ni pamoja na “Majukumu ya kimaendeleo na machaguo ya njia za kujiletea maendeleo kwa China na Afrika”, “Fursa zilizopo na Changamoto za Mashirikiano ya Afrika na China” na “Wajibu wa vyama vya siasa katika ujenzi wa maendeleo ya kitaifa na mashirikiano baina ya China na Afrika”.

  Mada zote hizi zinalenga kutupa hamasa katika jitihada zetu Afrika na China katika kuchagua njia sahihi za kukua, kujiletea maendeleo, kupendekeza programu ya vyama vya siasa kwa Kongamano la Ushirikiano wa China na Afrika litakalofanyika Jijini Beijing na kujenga uelewa wa pamoja na kuweka mchango wa hoja katika Ubia wa Kimkakati kati ya Afrika na China na hasa katika kipindi hiki kipya.

  Mkutano huu utakuwa fursa kubwa kwa Tanzania kukumbusha na kusisitiza msimamo wake katika diplomasia ya kisiasa na kiuchumi na hasa katika zama hizi za uongozi wa awamu ya tano ambayo imejikita katika kutimiza wajibu wa kizazi cha sasa wa kulikomboa bara la Afrika na Tanzania Kiuchumi ili kuleta maendeleo ya haraka kwa watu wake wa Tanzania na Afrika.

  Ifahamike kwamba tangu uongozi wa awamu ya tano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali umejikita katika kushughulika na shida za watu kwa kuimarisha nyanja zote za kiuchumi na kijamii. Hii imekwenda sambamba na kuimarisha nidhamu ya viongozi na watumishi wa umma, kuweka nidhamu katika makusanyo na matumizi ya fedha za umma, kuongeza uaminifu, uadilifu, uchapa kazi, kuongeza mapambano dhidi ya rushwa na vitendo vya ubadhirifu wa mali za umma na uhujumu uchumi.

  Chama cha CPC na Serikali ya China imevutiwa sana na mwelekeo huu wa Tanzania chini ya Kamaradi John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni Imani yetu yetu kwamba Tanzania itanufaika kwa muda mfupi wakati wa mkutano huu kwa kutoa huduma mbalimbali kwa wageni hawa lakini pia itanufaika maradufu kwa matokea ya Mkutano huu na mwendelezo wake.
   

  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
   
  Imetolewa na,
   
  HUMPHREY POLEPOLE
  KATIBU WA NEC – ITIKADI NA UENEZI

  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.

  RAIS Dk.John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kitaifa wa tamasha la maalum la Mwezi wa Urithi kuenzi utamaduni wa Mtanzania ambalo litafanyika nchini nzima kwa kuaza na Mkoa wa Dodoma.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Kigwangala amesema Serikali kupitia wizara hiyo wameaandaa tamasha hilo ambalo linalenga kuenzi utamaduni na urithi wa Mtanzania na kwamba tamasha hilo linaitwa Urithi Festival ambalo litakuwa likifanyika kila fikapo Septemba ya kila mwaka kuanzia mwaka huu.

  "Dhumuni la tamasha ni kuenzi na kunadi kiutalii hazina kubwa ya utamaduni ,mila na desturi za makabila yote nchini ambayo ni zaidi ya 128.Hatua hii inaenda sambasamba na juhudi za Serikali za kuongeza wigo wa mazao ya utalii nchini hususan kukuza matumizi endelevu ya malikale,kutangaza utamaduni , vyakula vya asili , michezo ya jadi na kazi za sanaa mbalimbali.

  "Tamasha litaisaida pia kukuza utalii wa ndani na kuongeza wastani wa watalii wa kimataifa kukaa nchini , hatua itakayoleta matokeo chanya kwenye mapato yatokanayo na sekta ya utalii na malikale.Wadau wa mwezi wa Urithi wa Tanzania ni Watanzania wote chini na waliopo ughaibuni .

  "Aidha tamasha linawalenga raia wa mataifa mengine wanaoishi Tanzania na watalii wa kimataifa na kwamba tamasha litawashirikisha wadau wote wa utalii,"amesema Dk.Kigwangala.

  Kuhusu namna ya kushiriki Dk.Kingwangala amesema Urithi Festival itasheherekewa Septemba yote na kwamba tamasha litafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri ambapo patakuwepo na matukio mbalimbali yakiwamo maonesho ya ubunifu wa sanaa na tamaduni , kazi za wajasiriamali na wadau wa utalii.

  Ameongeza ambapo pia kutakuwa na maonesho ya vyakula na vinywaji pamoja a burudani za ngoma kutoka katika makabila ya mkoa wa Dodoma na mikoa jirani , muziki wa dansi na kizazi kipya.Pia watatemdelea michoro ya Miambani ya urithi wa dunia ya Kondoa .

  "Septemba 8 mwaka huu patakuwa na uzinduzi wa kitaifa wa Urithi Festival katika uwanja wa Nyerere Square Dodoma.Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Dk.Magufuli.Wiki ya kilele inatarajiwa kufanyika mkoani Arusha kuanzia Septemba 24 mpaka 29 mwaka huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo nako kutakuwa na matukio mbalimbali.Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,"amesema.

  Ameongeza pamoja na kufanyika Dodoma na Arusha pia tamasha la Urithi Festival litafanyika nchi nzima kwa mwaka huu ambapo Wizara itaanza na Majiji ya Dar es Salaam ,Mwanza na Mji Mkongwe-Zanzibar(Septemba 10 mpaka Septemba 16) na Mwanza (Septemba 17 mpaka 23).Dk.Kigwangala ametumia nafasi hiyo kuelezea kuwa kuna kila sababu ya Watanzania kushiriki kwenye tamasha hilo na kwa walio nje ya nchi ni vema nao wakaja kuona namna ambavyo shughuli za kiutamaduni na malikale zinavyoenziwa.

  Ametoa rai kwa Watanzania pia kujenda utamaduni wa kutemebela vivuto vya utalii na hifadhi mbalimbali zilizopo nchini na kufafanua gharama ziko chini , hivyo kila mtu anaweza kwenda.

  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kunatarajia kufanyika mkutano wa kidunia wa vyama vya siasa pamoja na kikao maalum cha Afrika ambapo zaidi ya washiriki 130 wanatarajia kushiriki mkutano huo utakaofanyika jiini Dar es Salaam.

  Akizungumzia mkutano huo katika Ofisi Ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema CCM imepata heshima kubwa ya mwenyeji wa mkutano huo wa kidunia.

  Tunapenda kuujulisha umma wa watanzania kuwa tarehe 17-18 Julai 2018 kutafanyika Mkutano wa Kidunia wa Vyama vya Siasa, Kikao Maalum cha Afrika, Jijini Dar es Salaam. Mkutano huu utaleta zaidi ya vyama vya siasa 38 kutoka Afrika na zaidi ya washiriki 130 kutoka nje ya Afrika,"amesema.

  Amefafanua mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kwamba mkutano huo ni sehemu ya matokeo mazuri ya utendaji kazi wa uongozi wa awamu ya tano ya Chama na Serikali chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais Dk.John Magufuli.

  Pia amesema mkutano huo wa kihistoria na wa kwanza kufanyika Barani Afrika ni wapili kufanyika baada ya mkutano kama huo wa kidunia kufanyika Jijini Beijing, China Desemba mwaka 2017. Mkutano huo wa Desemba mwaka 2017 uliandaliwa na Chama Cha Kikomunisti Cha watu China (CPC) na Kiongozi Mwenyeji wa Mkutano huu alikuwa ni Kamaradi Xi Jinping Katibu Mkuu wa CPC na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China.

  Polepole amesema kuwa mkutano huo utahudhuriwa pamoja na wajumbe wengine wa mkutano ni Kamaradi Song Tao Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Watu wa China, Xu Luping Makamu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China na Kiongozi Mwenyeji wa Mkutano huu wa Kidunia wa Vyama vya Siasa ni Kamaradi John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Amesema wazo la mkutano huo linatokana na fikra za Katibu Mkuu wa CPC na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping ambaye anapendekeza fikra ya mwelekeo mpya wa namna ya kuendana na dunia.Polepole anasema Rais Xi Jinping anasema “tushirikiane kujenga jamii ambayo ina matarajio ya pamoja ya baadaye na kufanya kazi pamoja ili kujenga Dunia bora”. 

  Hivyo fikra hizo za Jinping ndio zilizosababisha majadiliano ya kidunia kati ya CPC na Vyama vya Siasa vya Kidunia."Mwaka huu nchi ya China inatimiza miaka 40 ya kufanya Mageuzi na kuchangamana Kimataifa na Mkutano huu wa Dar es Salaam utakuwa hatua kuelekea katika Kongamano kubwa la ushirikiano wa China na Afrika litakalofanyika jijini Beijing, China. 

  "Kwa hiyo ni dhahiri kwamba Tanzania, Afrika na China katika mkutano huu watajikita katika mjadala mpana na wa kina wa kuziangazia changamoto na fursa lukuki zitokanazo na kujengeka zaidi kwa mahusiano na mashirikiano ya Afrika na China.

  "Jambo moja ambalo lina mfanano mkubwa kati ya China na Tanzania na CCM na CPC ni itikadi ambayo inatoa mwelekeo wa Sera za China na Tanzania. Mataifa haya mawili na vyama viwili ambayo ndio vinatoa uongozi katika nchi hizi mbili zinaamini katika Itikadi ya Ujamaa,"amesema Polepole.

  Ameongeza kuwa China imeongozwa kwa mafanikio kwa zaidi ya miaka 40 sasa na Siasa na Itikadi ya Ujamaa wa Kisayansi ambao unashajihishwa na tabia ya Taifa la China “Socialism with Chinese characteristics”. 

  Amesema Itikadi hiyo iya Ujamaa ndio imewezesha mafanikio ya Mageuzi na Mapinduzi makubwa ya kimfumo, kiutendaji, kiuongozi, kiuchumi na kisiasa ambayo Taifa la China limeyatenda katika kipindi hiki za miaka 40.

  Wakati huu China imeanza awamu mpya ya Mageuzi na Mtangamano wa Kimataifa na inaweka jitihada kubwa kufikia lengo la kujenga Taifa la kijamaa la kisasa na imara ifikapo mwaka 2050. Wakati China inaweka malengo haya makubwa ifahamike kwamba Bara la Afrika likiwa mojawapo ya mabara yanayokua haraka kiuchumi, kwa idadi ya watu, kwa utangamano na uwezekano mkubwa wa uchumi wake kukua kwa faida na tija duniani; Afrika pia imejitoa kuhakikisha inafikia Mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kujitengenezea njia yake ya kukua kulingana na mazingira ya Afrika “exploring independent path of modernisation”.

  Amesema katika njia hiyo ya pamoja kuelekea katika lengo la pamoja na kwa lugha rahisi “kushughulika na shida za watu wetu”, CPC iko tayari kuimarisha utaratibu wa kubadilishana taarifa, maarifa na watu pamoja na vyama vya siasa vya Afrika ili kujenga jamii ya pamoja ya Afrika na China na yenye lengo la pamoja kuhusu maisha bora ya sasa na ya baadaye kwa watu wetu.

  Kuhusu mada kuu ya mkutano huo wa kidunia itakuwa ni Juhudi (vitendo) na Nadharia za Vyama vya Afrika na Chama Cha Kikomunisti cha China katika kufanya uchaguzi wa njia sahihi za kujiletea maendeleo na zinazoendana na mazingira ya nchi zetu za Afrika.

  "Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama Cha Kikomunisti Cha China na vyama vyote vitakavyoshiriki katika Mkutano huu wa kidunia vitakuwa na majadiliano ya kina na ya kweli na kubadilisha taarifa na maarifa mbalimbali. Baadhi ya mada ndogo zitakazojadiliwa ni pamoja na “Majukumu ya kimaendeleo na machaguo ya njia za kujiletea maendeleo kwa China na Afrika”, “Fursa zilizopo na Changamoto za Mashirikiano ya Afrika na China” na “Wajibu wa vyama vya siasa katika ujenzi wa maendeleo ya kitaifa na mashirikiano baina ya China na Afrika”.

  "Mada zote hizi zinalenga kutupa hamasa katika jitihada zetu Afrika na China katika kuchagua njia sahihi za kukua, kujiletea maendeleo, kupendekeza programu ya vyama vya siasa kwa Kongamano la Ushirikiano wa China na Afrika litakalofanyika Jijini Beijing na kujenga uelewa wa pamoja na kuweka mchango wa hoja katika Ubia wa Kimkakati kati ya Afrika na China na hasa katika kipindi hiki kipya,"amesema Polepole.

  Pia amesema mkutano huo utakuwa fursa kubwa kwa Tanzania kukumbusha na kusisitiza msimamo wake katika diplomasia ya kisiasa na kiuchumi na hasa katika zama hizi za uongozi wa awamu ya tano ambayo imejikita katika kutimiza wajibu wa kizazi cha sasa wa kulikomboa bara la Afrika na Tanzania Kiuchumi ili kuleta maendeleo ya haraka kwa watu wake wa Tanzania na Afrika.

  "Ifahamike tangu uongozi wa awamu ya tano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali umejikita katika kushughulika na shida za watu kwa kuimarisha nyanja zote za kiuchumi na kijamii. Hii imekwenda sambamba na kuimarisha nidhamu ya viongozi na watumishi wa umma, kuweka nidhamu katika makusanyo na matumizi ya fedha za umma, kuongeza uaminifu, uadilifu, uchapa kazi, kuongeza mapambano dhidi ya rushwa na vitendo vya ubadhirifu wa mali za umma na uhujumu uchumi,"amesisitiza.

  Ameogeza Chama cha CPC na Serikali ya China imevutiwa sana na mwelekeo huu wa Tanzania chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Magufuli. 

  "Ni Imani yetu yetu Tanzania itanufaika kwa muda mfupi wakati wa mkutano huu kwa kutoa huduma mbalimbali kwa wageni hawa lakini pia itanufaika maradufu kwa matokea ya Mkutano huu na mwendelezo wake,"amesema Polepole.

  0 0

  Shirika la Taifa la Hifadji ya Jamii(NSSF) limejipanga kutoa pensheni ya Uzeeni kwa watanzania wote walio katika sekta rasmi na sekta isiyo rasmi 

  Hayo yalisemwa katika mkutano baina ya NSSF na viongozi wa vikundi vya uzalishaji mali Mkoani Morogoro jana. Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Stephen Kebwe uliofanyika katika ukumbi wa NSSF Mafao Haouse 

  Akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa mkoa wa Morogoro aliwaasa wale wote walio katika sekta isiyo rasmi kama vile Mama Lishe, bodaboda, wafugaji, wakulima n.k kubadili mtazamo wa maisha ili kuepukana na changamoto za uzeeni kwa Kujiunga na NSSF kwani watapata pensheni ya uzeeni kama wale walio katika sekta rasmi 

  Nae Mweneykiti wa Kamati ya kuratibisha Hifadhi ya Jamii kwa sekta isiyo rasmi Bi Mariam Muhaji alisema, pensheni ya uzeeni ni haki ya kila Mtanzania hivyo ni wakati sasa kwa wale wote walio katika sekta isiyo rasmi kujiunga na NSSF ili kufaidika na Mafao mbalimbali yatolewayo ikiwemo pensheni ya uzeeni. 
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Stephen Kebwe akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Viongozi wa Vikundi vya uzalishaji mali Mkoani Morogoro.
  Meneja wa NSSF Shinyanga Ndugu Omary Mziya akizungumzia kuhusu umuhimu wa Hifadhi ya Jamii wakati wa Mkutano na Viongozi wa Vikundi mbalimbali vya uzalishaji mali Mkoani Morogoro
  Viongozi mbalimbali wa Vikundi wakiwa katika mkutano ulioratibiwa na NSSF kwa ajili ya elimu kuhusu Hifdahi ya Jamii kwa sekta isiyo rasmi

  0 0

  Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

  RAIS wa Kenya Uhuru Kenyata amemwapisha  Fatuma Ahmed kuwa Meja Jenerali nchini humo na kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo.

  Jenerali Ahmed anakuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo kwa kuwa msaidizi mkuu wa majeshi nafasi ambayo haikuwa kushikwa na mwanamke katika masuala ya ulinzi na usalama nchini humo.

  Katika hafla hiyo Kenyata alieleza kuwa amemchagua ili awe kioo kwa wanawake nchini humo na kuthibitisha kuwa hakuna kinachoshindikana.

  Aidha alieleza kufurahishwa na namna jeshi la Kenya linavyofanya kazi hasa katika kulihudumia taifa bila kujali dini, itikadi wala rangi, wamekuwa waaminifu katika kuhudumia taifa hilo lenye watu 42 milioni.

  Naye Jenerali mteule amemshukuru Rais Kenyata kwa uteuzi huo na kueleza kuwa: "Ninafuraha sana kwa nafasi mpya niliyochaguliwa na inaonesha namna Rais anavyothamini mchango wa wanawake katika maendeleo ya taifa letu" alieleza Jenerali Fatuma.

  Jenerali Fatma Ahmed alianza kushika kasi mwaka 2015  baada ya kuchaguliwa kuwa  brigedia wa jeshi nafasi ambayo haikuwahi kushikwa na mwanamke nchini humo.

  Jenerali Fatuma ametumikia jeshi la ulinzi la Kenya kwa zaidi ya miaka 30 kuanzia miaka ya 1983.
   RAIS wa Kenya Uhuru Kenyata amemwapisha  Fatuma Ahmed kuwa Meja Jenerali nchini humo na kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo.
   RAIS wa Kenya Uhuru Kenyata amemwapisha  Fatuma Ahmed kuwa Meja Jenerali nchini humo na kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo.

  0 0

   Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia (kushoto) akisaini taarifa ya makabidhiano ya ofisini na mtangulizi wake Bw. Kailima Ramadhani ambaye sasa ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
   Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia (kushoto) akikadhiwa sehemu ya makabrasha ya ofisini na mtangulizi wake Bw. Kailima Ramadhani ambaye sasa ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
  Baadhi ya Wakuu wa Idara za Tume ya Taifa ya Uchaguzi  wakishuhudia utiaji saini wa taarifa ya makabidhiano ya ofisini kati ya Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia (kulia) na mtangulizi wake Bw. Kailima Ramadhani ambaye sasa ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0


   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimuuliza swali, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho, Alphonce Malibiche (kushoto), wakati wa ziara ya kutembelea Kituo Kikuu cha Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa, kilichopo Kibaha, Mkoani Pwani.Wapili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Andrew Masawe.
   Mkurugenzi  Mkuu wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho, Alphonce  Malibiche, akifafanua jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kulia), kutembelea Kituo Kikuu cha Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa, kilichopo Kibaha, Mkoani Pwani.Wakwanza  kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida),Andrew Masawe
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Andrew Masawe  wakati wa ziara yake ya kikazi  kutembelea Kituo Kikuu cha Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa, kilichopo Kibaha, Mkoani Pwani
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akisalimiana na watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(Nida), baada ya kuwasili  Kituo Kikuu cha Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa, kilichopo Kibaha, mkoani Pwani.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (watatu kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(Nida), baada ya kutembelea Kituo Kikuu cha Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa,kilichopo Kibaha,Mkoani Pwani.Wapili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Andrew Masawe Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  0 0

  ZAIDI ya Sh.milioni 46 kutoka Mfuko wa Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto, Mkoani Tanga zimegawiwa kwenye kata 18 za jimbo hilo ili kuweza kuchangia kasi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Bumbuli ni Jimbo linaloongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulia Mazingira na Muungano January Makamba. 

  Kwa mujibu wa Katibu wa Mbunge wa Jimbo hilo,Hozza Mandia alitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na miradi ya huduma ya maji, ujenzi wa madarasa, zahanati na matengenezo ya barabara. Mandia alitaja mchanganuo wa pesa hizo zilizotolewa kuwa kata ya Kisiwani imepata jumla ya sh. Milioni 4 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa mradi wa huduma ya maji, wakati ambapo kata ya Tamota itapatiwa Sh. Million 3 kwa ajili ya ujenzi wa zahanatati katika kijiji cha Ngwelo. 

  Miradi mingine ni mradi wa zahanati katika kijiji cha Tekwa ambao mfuko umechangia Sh. Milioni 1.44, mradi wa zahanati kwemsambia aruji yenye thamani ya Sh 675,000, saruji ye thamani kama hiyo kwa mradi wa ujenzi wa darasa shule ya msingiya kivilu na saruji nyingine yenye thamani sh. 700,000 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi ya kata ya Kwemkomole. 

  Kata ya Dule B itapata mchango wa jumla ya Sh. Milioni 3.42 milioni kwa ajili ya miradi mbalimbali, , wakati ambapo kata ya Mamba imepata jumla ya Sh. Milioni 3.4, Bumbuli (Sh. 2.99 milioni), Vuga (Sh. 2.97 milioni) na Mponde (Sh. 2.25 million). 

  Diwani wa Kata ya Vuga Jumaa Dhahabu alisema kuwa fedha hizo zitawasaidia kuweka lenta kwenye jengo la zahanati pamoja na kuweka sakafu kwenye chumba cha darasa kinacho tumika kwaajili ya maabara ya sayansi na kuweka miundombi katika darasa mabara hiyo ameongeza kwa kusema anamshukuru Mbunge wa Jimbo hilo kwanamna anavyoendelea kuwasaidia katiaka kata ya vuga Hata hivyo alisema kuwa serikali iliwapatia sh. Million 10 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya kata ya kwemkomole , hivyo fedha hizo zitawasaidia kusafisha jengo hilo nakwamba kama viongozi wa kata hiyo tayari wamepokea mifuko 200 ya saruji kutoka kwa Mbunge wa jimbo hilo January Makamba ambayo itapelekwa kwenye madarasa naa zahanati .

  0 0

  Na.Vero Ignatus .Dodoma. 

  Taasisi ya RSA kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kimefanya ukaguzi wa magari yanayoingia na kutoka stendi kuu ya mabasi mkoani Dodoma nanenane.

  Ukaguzi huo umeenda sambaba pamoja na kutoa elimu kwa abiria namna ya kufunga mikanda awapo ndani ya gari,kuzifahamu haki zao za msingi pamoja na kupaza sauti kutokaa kimya pale anapomuona dereva anakiuka sheria na taratibu za usalama barabarani

  John Seka ni mwenyekiti wa RSA nchini amesema Imekuwa ni tabia ya Taasisi hiyo kufanya hivyo mara kwa mara ili kuwakumbusha madereva wajibu wao,kufuata taratibu na kanuni za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazosababishwa madereva wazembe .

  "Tumejaribu kupenyeza elimu kuhusu maswala ya usalama barabarani na tumefanya hivyo kwasababu ajali zimekuwa zikiongezeka kila siku,hivyo tumeona na sisi kama RSA kuna umuhimu wa kupaza sauti kwaajili ya usalama barabarani"

  Askari wa kikosi cha usalama barabarani wankituoncha mabasi mkoani Dodoma Koplo Athuman amewataka RSA kuendelea kushirikiana na Jeshi la polisi katika kutoa taarifa, pale wanapoona mwenendo mbaya wa madereva wawapo barabarani kwani itasaidia kupunguza ajali.Sisi askari hatupo mahali pote ila nyie RSA mkitupa taarifa tutazitendea kazi,endeleeni kutoa elimu kwa abiria na kwa madereva hii itasaidia kupunguza ajali.Alisema Athumani.

  Katika ukaguzi huo uliofanyika katika stendi hiyo ya mabasi makosa mbalimbali yamegundulika likiwemo la baadhi ya mabasi kuwaongezea abiria nauli,magari kukosa mikanda,pamoja na baadhi ya magari kuktwa na ubovu mbalimbali.
  Baadhi ya mabalozi wa Usalama barabarani wakiwa katika stendi kuu ya mabasi mkoani Dodoma.
  Meneja wa TIRA Kanda ya Kati Stella Rutaguzaal akizungumza na mabalozi wa usalama barabarani leo Mkoani Dodoma
  Mmoja wa askari wa kikosi cha usalama barabarani akimsaidia mmiliki wa mabasi ya Kamwana Nassoro Khlfani
  Mratibu wa Elimu kutoka RSA Augustus Fungo akiwa anazungumza na baadhi ya madereva,makondakta na abiria katika stendi kuu ya mabasi mkoani Dodoma leo.
  Ukaguzi ukiendelea katika stendi kuu ya mabasi mkoani Dodoma.
  Askari wa Usalama barabarani wakikagua moja ya ratiba ya basi katika stendi kuu ya mabasi Dodoma .
  Baadhi ya askari wa Kikosi cha usalama barabarani wakiwa katika picha ya pamoja na RSA leo katika stendi kuu ya mabasi Mkoani Dodoma.

  0 0   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Phaustine Martin Kasike kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvalisha cheo Phaustine Martin Kasike kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania Phaustine Martin Kasike akipiga saluti mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Joseph Edward Sokoine kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Balozi Joseph Edward Sokoine akila kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania Phaustine Martin Kasike akizungumza mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapishwa viongozi hao wawili Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania Phaustine Martin Kasike ( watatu kutoka kulia),Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Balozi Joseph Edward Sokoine(watatu kutoka kushoto) Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wapili kutoka kulia, viongozi wengine wa Serikali pamoja na Maafisa mbalimbali kutoka Jeshi la Magereza nchini.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania Phaustine Martin Kasike ( watatu kutoka kulia),Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Balozi Joseph Edward Sokoine(watatu kutoka kushoto) Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wapili kutoka kulia, viongozi wengine wa Serikali pamoja na Maafisa mbalimbali kutoka Jeshi la Magereza nchini.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizugumza jambo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania Phaustine Martin Kasike pamoja na Kamishna Mstaafu wa Jeshi hilo la Magereza Dkt. Juma Ali Malewa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania Phaustine Martin Kasike mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Bodi ya Utalii Nchini (TTB) kwa kutambua umuhimu wa vivutio vingi zaidi nchini mbali na wanyama pori wamekeza msisitizo zaidi katika utalii wa fukwe na majiji hususani Dar es Salaam. TTB wameanza na wadau wa mahoteli ya kitalii Jijini Dar es Salaam kwa kufanya usafi kwa pamoja kwenye fukwe ilyopo Hotel ya Ramada na fukwe za jirani. Kwa pamoja TTB na wadau wengine watakutana katika kikao kitakachofanyika Julai 19 mwaka huu kitalenga zaidi kutafuta njia mbadala ya kuzuia takataka zisiingie baharini.

  Akizungumza baada ya kumaliza usafi, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Ernest Mwamwaja amesema lengo kuu la kufanya usafi huu ni katika kuhakikisha wanaboresha fukwe zote na majiji ili kuweza kuwa kivutio kwa watalii nchini. Mwamwaja amesema kuwa, ukiachilia mbuga za wanyama ambazo zipo nchini, fukwe za bahari kwa upande mwingine zinatakiwa ziwe safi ili kuvutia zaidi watalii pindi wanapokuja nchini.

  Amesema kuwa, kama watalii watakuwa wanavutiwa na mazingira ya Fukwe ifikapo mwaka 2020 tunaweza kufikia wastani wa watalii Milioni 2 kwa mwaka pamoja na pato la taifa kuongezeka kutoka Dola Bilion 2.1 hadi 4.2 kwa mwaka.

   Kaimu Meneja wa Utalii Bodi ya Utalii Nchini Joseph Sendwa amesema kuwa kikao na wadau kitakachofanyika mwezi huu kitaleta maboresho makubwa sana katika sekta ya utalii kwakuwa kwa pamoja watatoka na azimio la kuhakikisha wanafanya usafi katika fukwe zote ikiwemo kwenda maeneo ya makazi ya watu yanayopita mkondo wa bahari ambapo kumekuwa na changamoto kubwa ya wananchi kutupa taka ovyo.

  Mbali na hilo, Sendwa amesema wameanzia katika fukwe ya Ramada ila wataenda sehemu zote za Dar es Salaam ikiwemo pia kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na utunzaji wa mazingira.
   Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Nchini(TTB) Ernest Mwamwaja akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa Ramada Resort Dar es Salaam Barath Swarup wakifanya usafi kwa pamoja katioa fukwe ya Hotel hiyo uliofanyika kwa ushirikiano wa pamoja leo Jijini Dar es Salaam.
  Usafi ukiendelea ndani ya fukwe Ramada Resort Dar es Salaam  wakiwa pamoja na Raia wa Ufaransa anayeishi katika Visiwa vya Reunion JeanMart Francois akishirikiana na Wafanyakazi wa TTB na Ramada kufanya usafi.
   Wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) pamoja na wafanyakazi wa Ramada Resort Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa usafi uliofanyika kwenye fukwe ikiwa na lengo la kuzitumia kama vivutio kwa watalii.

  0 0


  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe (MB), ametembelea na kuona miradi mbalimbali inayotekelezwa Mkoani Geita akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Mhandisi Robert Gabriel, Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Shaaban Ntarambe, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Mhandisi Deusdedith Kakoko, pamoja na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Geita Mhandisi Harun Senkuku. 

  Miradi aliyoitembelea ni pamoja na Bandari ya Nyamirembe iliyoko kijiji na Kata ya Nyamirembe Wilayani Chato ambayo ilikua ikitumika tangu enzi ya Mkoloni ambayo kwa sasa haifanyi kazi. Waziri amewaeleza wananchi wajiandae kufurahi kwani muda si mrefu bandari hiyo itafufuliwa na kuanza kazi; ni baada ya kujitokeza kumlaki kwa fuaraha baada ya kumuona akitembea kwenye bandari hiyo. 

  Amesema “mwezi wa nane mwaka huu tunasaini mkataba, tunairudisha Bandari ya Nyamirembe. Na sasa tunajenga meli kubwa, itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria elfu moja mia mbili (1,200), mizigo tani mia nne (400) ambayo itapita hapa kwenda Bukoba ndiyo maana kituo hiki lazima tukijenge na mkandarasi anaingia hapa mwezi wa nane. 

  Hivyo ni ushindwe mwenyewe mwananchi kwa sababu sasa meli itakuwepo, barabara ya lami ipo, kiwanja cha ndege kinaendelea kujengwa unataka nini tena?” alimaliza kwa kushangiliwa na wananchi. 

  Kisha,  Waziri ametembelea na kujionea maendeleo ya hatua ya ujenzi wa barabara ya Bwanga – Biharamulo yenye urefu wa kilomita sitini na saba (Km.67) inayojengwa kwa kiwango cha lami na kufurahishwa na hatua iliyofikiwa baada ya kupewa taarifa kuwa, barabara hiyo imeshajengwa hadi kilomita hamsini na saba (Km.57) hivyo bado kilometa kumi (Km.10) ili iweze kukamilika. 

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Mhandisi Gabriel amemshukuru Mhe. Waziri kwa ujio wake lakini pia kwa kuteuliwa kuwa msimamizi wa wizara hiyo na kupendekeza maombi ya kutanuliwa barabara za kuingia Geita mjini ili ziwe mbili wakati wa kuingia na mbili wakati wa kutoka, lengo ikiwa ni kupunguza ajali na kuokoa maisha ya watumia barabara waendesha baiskeli  na watembea kwa miguu ambao hupata ajali kutokana na msongamano barabarani. 

  Mkuu wa Mkoa pia ametumia nafasi hiyo kuomba Daraja la Wavuka kwa Miguu (Pedestrian Bridge) karibu na soko jipya la kisasa Mjini Geita litakalokuwa na duka lenye bidhaa zinazotengenezwa Tanzania pekee katika kutafuta soko la bidhaa za ndani , jambo lililopelekea Mhe. Waziri kusema amelipokea ombi hilo na kuahidi kulishughulikia kwa kumuagiza Meneja TANROADS Mkoa kuandaa maombi hayo na kumwasilishia ili aweze kusaidia utekelezaji wake. 

  Kisha alimshukuru Mhe. Waziri kwaniaba ya wananchi wa Geita kuendelea kufungua milango ya fursa na kutoa wito kuhusiana na jukwaa la fursa za biashara litakalofanyika mkoani Geita kuanzia tarehe 15 hadi 16.08.2018 na kwamba endapo bandari hiyo itakamilika, uwanja wa ndege ukakamilika, basi wageni wengi watakuja kwani kuna vivutio vya utalii lakini pia biashara ya dhahabu. 

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Shaaban Ntarambe alimhakikishia Mhe. Waziri kuwa, wananchi wapo tayari kupokea maendeleo na ameshukuru kwa namna ambavyo mkandarasi anayejenga barabara hiyo ana mahusiano mazuri na wananchi wa Chato jambo linalosaidia utekelezaji mzuri wa mradi usiwe na migogoro.
   kibao cha bandari ya nyamirembe
   Mkuu wa mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akiwa(mweye kofia nyeusi-kulia) , Mkurugenzi wa mamlaka ya bandari,Mhandisi Deusdedith Kakoko, (kushoto) wakitembea bandarini
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe (koti la mistari, wapili mbele kushoto) na alioambatana nao wakitafakari jambo
  Barabara ya bwanga-biharamulo
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe (kulia) akipeana mkono wa kwaheri na Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel

  0 0

  Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

  WAZIRI wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe amemuagiza mkandarasi wa mradi wa barabara ya Nyakanazi Kabingo Nyanza road work  kuhakikisha ifikapo Agosti 30 mwaka huu kilometa 23 kati ya kilometa 50 za lami ziwe zimekamilika kwa kiwango cha lami.

  Ametoa maagizo hayo jana wilayani Kakonko mkoani Kigoma wakati alipoanza ziara yake akitokea mkoani Geita ambapo alianza kwa kutembelea barabara hiyo inayounganisha mkoa wa Kigoma na mikoa mingine.

  Mhandisi Kamwelwe amesema wananchi wa Mkoa wa Kigoma hawajawahi  kuona lami, hivyo wanashauku kubwa ya kuona barabara hiyo ya lami inakamilika na Rais amewaletea mradi huo lazima na wao wafaidi ndani ya utawala wa awamu ya tano na wao wapate barabara.

  Amesema barabara hiyo imepitiliza muda kwani ilitakiwa iwe imekamilika na kwa sasa wataenda na mkandarasi huyo kwa kupeana muda wa kukamilisha kazi kidogo.Pia amewatala Kampuni ya Nyanza road work kumsimamia mtu waliomuajiri kufanya kazi usiku na mchana ilimradi ukamilike kwa wakati."Nimeanza kumkagua Nyanza road work sijaridhishwa na mradi  unavyoendelea.Mradi huu umeanza mwaka 2014  na ulitakiwa uwe umekamilika.

  Aidha amesema tayari wametanganza zabuni ya mradi mwingine wa Kabingo hadi Nduta kilomita 89 baada ya mienzi miwili watasainiana mkataba na mkandarasi mwingine aanzie hapo.Amefafanua malengo ni  miaka miwili maeneo yote yaliyobaki mkoani Kigoma yatakuwa na wakandarasi  ili mkoa wa Kigoma ufunguke kwa kiwango cha lami.

  Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amesema wananchi wanataka barabara iwepo na lami wamechoka vumbi kila siku, na  kuwataka wakandarasi kasi walioionyesha leo baada ya kusikia Waziri anakuja waendeleze kasi hiyo.

  Waziri huyo amewasili jana mkoani Kigoma ambapo atakuwa katika ziara ya siku nne,ambapo akiwa mkoani hapo atatembelea barabara ya Nyakanazi Kabingo na Kasulu Kidahwe zenye wakandarasi pamoja na kutembelea bandari ya Kigoma na Uwanja wa ndege.
  Waziri wa Ujenzi uchukuzi na mawasiliano Muhandisi Isack Kamwelwe (pichani kati) akitoa malekezo kwa Meneja mradi wa barabara ya Nyakanazi-Kabingo kutoka kampuni ya Nyanza Road Work Massimo Cartula kuhusiana na ujenzi wa barabara hiyo,kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala
   Ujenzi wa bara bara Nyakanazi-Kabingo ukiendelea kwa kusua sua,ambapo Waziri Ujenzi amutolea maagizo mazito kuhakikisha mradi huo
  ifikapo Agosti 30 mwaka huu kilometa 23 kati ya kilometa 50 za lami ziwe zimekamilika kwa kiwango cha lami.

  0 0

  Na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii

  MWENGE wa Uhuru unatarajiwa kuzindua miradi mbalimbali katika Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani yenye zaidi ya Sh. bilioni 2.9.

  Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filibeto Sanga wakati alipokuwa akisoma taarifa ya Wilaya hiyo ya miradi ya Maendeleo wakati wa Mwenge huo ukiwa wilayani hapo.

  "Miradi itazinduliwa katika mwenge huu na imetekelezwa kwa nguvu za wananchi. Katika kuchangia nguvu zao,Serikali kuu kutuwezesha fedha ikiwamo na wadau wa maendeleo," amesema.Aliongeza kuwa miradi hiyo ya maendeleo itasimamiwa vizuri ili kuwawezesha wananchi kunufaika nayo.Pia amesema miradi yote ipo katika ubora na imesimamiwa kikamilifu kutokana na fedha zilizotolewa kwa ajili ya miradi hiyo.

  Akizungumza kuhusu elimu amesema kuwa,Wilaya imejikita katika kusimamia suala la elimu ambapo idadi ya wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza na chekechea inaongezeka kila mwaka.Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Everist Ndikilo amesema kuwa Mkoa huo una wilaya saba ambapo miradi ya maendeleo yenye zaidi ya thamani ya shilingi bilioni 162 itazinduliwa katika mbio hizo za mwenge.

  Ndikilo aliyasema hayo wakati akikabidhiwa mwenge na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda.Ndikilo alikabidhiwa Mwenge na Makonda,katika kijiji cha Kipara Mpakani kilichopo Mkuranga.Ndikilo amesema atahakikisha wakimbiza mwenge wote sita wanakaa kwa usalama katika Mkoa huo.Akizungumzia hadi ya elimu katika mkoa wa Pwani,amesema wamejipanga kuboresha elimu ambapo wamefanikiwa kila mwaka idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa inaongezeka na wanaojiunga kidato cha kwanza idadi iinaogezeka.

  Amesema kutokana na Tanzania kuwa ya viwanda,wamekuwa wakiwajengea uwezo wanafunzi kusoma masomo ya sayansi.Amesema Mkoa wa Pwani unafanywa vizuri katika utekelezaji wa viwanda,ambapo asilimia 20 viwandani wameajiliwa wakazi wanaoishi Pwani.

  Wakati huo huo Mbunge wa Jimbo Mkuranga ambaye ni Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ullega amesema kuwa anaunga mkono utendaji wa Rais John Magufuli,kwa kusimamia Ilani ya CCM na kuleta maendeleo makubwa.Amesema anampongeza Rais kwa kuwakumbuka wakazi wa Mkuranga kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa madaraja na barabara ya kutoka Mkuranga mjini na kuelekea maeneo ya hospital ya Wilaya Mkuranga,Zahanati mablimbali zinazojengwa katika wilayani hiyo.

  Mkimbiza mwenge kitaifa Charles Francis Kabeho amewataka watumishi wafanye kazi kwa weledi kwa manufaa ya taifa.Amesema si busara mtumishi akashindwa kufanya kazi iliyomuweka hapo na kushindwa kuwaletea wananchi maendeleo.
   Mku wa Mkoa wa Pwani Muhandisi,Everist Ndikilo  akimkabidhi mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga.(picha na Emmanuel Massaka MMG)
   Kiongozi wa  mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018,Ndugu  Charles Kabeho akiweka jiwe la msingi katika kituo cha Afya Mkamba kilichopo kijiji cha Kizapala  Mkuranga  mkoa wa Pwani,kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mh.Abdallah Ulega .
   Kiongozi wa  mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018,Ndugu  Charles Kabeho akifungua vyumba sita vya vya madarasa ya shule ya msingi Kipara mpakani Mkuranga  mkoa wa Pwani.(picha na Emmanuel Massaka,MMG)
  Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega  akizungumza na wananchi wa waliojotokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru.
   

  0 0

  Mkuu wa Wilaya mteule wa Kahama mkoani Shinyanga,Ndugu Anamringi Macha


  0 0


  Rais Mstaafu wa Marekani Mhe. Barack Obama akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa ya Kilimanjaro (KIA) akitokea hifadhi ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara alikotalii yeye na familia yake kwa muda wa siku nane, kabla ya kuelekea Afrika Kusini kwenye maadhimisho ya miaka 100 yaNelson Mandela
  Rais Mstaafu wa Marekani Mhe. Barack Obama akipewa zawadi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa ya Kilimanjaro (KIA) akitokea hifadhi ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara alikotalii yeye na familia yake kwa muda wa siku nane, kabla ya kuelekea Afrika Kusini kwenye maadhimisho ya miaka 100 yaNelson Mandela
  Rais Mstaafu wa Marekani Mhe. Barack Obama akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Mghwira mara baada ya kulakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga (pichani kushoto), alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa ya Kilimanjaro (KIA) akitokea hifadhi ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara alikotalii yeye na familia yake kwa muda wa siku nane, kabla ya kuelekea Afrika Kusini kwenye maadhimisho ya miaka 100 yaNelson Mandela
  Rais Mstaafu wa Marekani Mhe. Barack Obama akisalimiana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP,Hamisi Issa mara baada ya kulakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga (pichani kushoto), alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa ya Kilimanjaro (KIA) akitokea hifadhi ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara alikotalii yeye na familia yake kwa muda wa siku nane, kabla ya kuelekea Afrika Kusini kwenye maadhimisho ya miaka 100 yaNelson Mandela

  0 0

  Na Said Mwishehe, Globu ya jamii


  NAOMBA kutumia nafasi hii kwanza kabisa kutoa salamu kwa Watanzania wote.

  Pili naomba nitoe salamu zangu za unyenyekevu kwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano Dk. John Magufuli.

  Baada ya salamu hizo pia naomba nitumie nafasi hii kupongeza jitihada za Rais Magufuli katika kuwatumikia Watanzania wote na kubwa zaidi harakati zake za kuhakikisha tunapiga hatua.

  Pia, ahsante Rais Magufuli kwa jitihada zako ambazo umekuwa ukizifanya katika kuhakikisha tunakuwa nchi ya kujitegemea kupitia rasilimali ambazo Mwenyezi Mungu ametujaalia katika nchi yetu.

  Ila Rais nikunong'oneze kuwa ujio wa Dreamliner umenikosha sana kama si kunifurahisha. Ni juzi tu macho ya Watanzania yameshuhudia ujio wa ndege hiyo kubwa na ya kisasa.Inahitaji uwe na akili za wendawazimu ili uweze kukosoa ujio wa ndege hiyo. Pia, inahitaji kujitoa ufahamu ili upate nafasi ya kuupotosha umma kuwa ujio wa Dreamliner haustahili.

  Kwa mwenye akili timamu na anayejua nini maana ya maendeleo ataungana  na watanzania wote kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa uamuzi wa kununua ndege kwa lengo la kuliboresha Shirika la Ndege la ATCL. Ahsante Rais.Baada ya utangulizi huo nielezee hivi leo hii nimeamua kujikita katika kuzungumzia urafiki kati ya nchi za Tanzania na China. 

  Nazungumzia urafiki huo nikitambua kuwa Julai 17 mpaka Julai 18 mwaka huu Tanzania inapokea ugeni mkubwa ambao utahudhuria mkutano wa kidunia ambao unahusisha vyama vya kisiasa ambavyo vilikuwa mstari wa mbele kupigania ukombozi kwa nchi za Kusini mwa Bara la Afrika.

  Mkutano huo utafanyika jijini Dar es Saalam. Ni mkutano ambao umeandaliwa na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC). Ni mkutano  mkubwa haswaa. Yaani mkubwa naomba unielewe. Kwa msisitizo niandike kwa herufi kubwa kwamba NI MKUTANO MKUBWA SANA.

  Hivyo kabla ya kuzungumzia mkutano huo niombe nizungumzie alau kwa uchache urafiki wa miaka mingi kati ya Tanzania na China. Kwa kukumbusha tu uhusiano kati ya Tanzania na China umeleta faida kubwa za kimaendeleo.

  Kupitia urafiki huo kuna mambo mengi Watanzania tumenufaika nayo na wao China yapo mambo mengi ambayo wamenufaika nayo kutoka na urafiki wao na sisi.Uhusiano wa China na Tanzania umekuwa na mafanikio makubwa ya kuziunganisha nchi hizo katika kusaidiana katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.

  Kila mmoja anaweza kuelezea namna anavyoona inafaa kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili lakini jambo la msingi na la kuzingatiwa Tanzania na China wamekuwa na urafiki wa muda mrefu uliofanikisha mambo mengi kufanyika.

  Kumbukumbu zinaonesha baada tu ya uhuru wa Tanganyika na Zanzibar, wataalam wa kilimo, ujenzi na madini walifika kusaidia wenzao wa Tanzania katika fani zao.

  Baadae, mamia kwa maelfu ya wafanyakazi wa reli walifika kujenga kilomita 1,860 za Reli ya Tanzania hadi Zambia, ambayo inajulikana zaidi kama TAZARA.

  Unaweza kuona urafiki wa nchi hizo mbili ulivyo na pengine unaweza usifananishwe na nchi yoyote ile ingawa nikiri Tanzania inao uhusiano mzuri na nchi mbalimbali duniani.


  Wakati kukiwa na uhusiano mzuri kati ya China na Tanzania pia umenogeshwa zaidi na uhusiano ulitokuka kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).

  Vyama hivyo vimekuwa na urafiki wa muda mrefu na urafiki wao umesababisha mambo mengi kuonekana kuingilia hasa katika mfumo wa utendaji wake.

  Ni vyama ambavyo vimekuwa na misimamo hasa linapokuja suala la usawa na haki kwa wote. Ni vyama ambavyo kila kimoja kwa nafasi yake kinapambana kujenga hali bora za watu wake. 

  Itoshe kusema kuna uhusiano mkubwa kati ya CCM na CPC katika kutekeleza majukumu yao. 

  Ni jambo la kawaida viongozi wa CPC kutembelea ofisi za CCM na hivyo hivyo kwa viongozi wa CCM kutembelea ofisi za CPC nchini China tena kwa raha zao. Hakika ni urafiki ambao unaakisi udugu ndani yake.

  Nimegusia kidogo kuhusu mkutano wa vyama vilivyoshiriki kukomboa nchi za Kusini mwa Bara la Afrika. Iko hivi China imeamua kuichagua tena Tanzania kwa ajili ya kufanyika mkutano huo mkubwa wa kidunia ambao utahusisha vyama vyote ambavyo vilikuwa mstari wa mbele katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Bara la Afrika.

  Kama nilivyotangulia kueleza awali mkutano huo unatarajiwa kufanyika Julai 17 mpaka Julai 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

  Hivyo vyama vyote ambavyo vilishiriki katika kukomboa nchi za ukanda huo watakuwa jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umeandaliwa na Chama cha CPC cha nchini China kwa kushirikiana na CCM.

  Na hivyo kutakuwa na ugeni mkubwa wa viongozi wa kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika. Wageni zaidi 130 kutoka nje ya Afrika watahuhlshuria mkutano

  Mwenyeji wa mkutano huo ni  Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli.

  Kwa lugha ya mjini ni kwamba Julai 17 mpaka Julai 18 dunia itaelekeza macho yake nchini Tanzania. 

  Kikubwa itataka kujua nini kimejadiliwa na hasa ukizingatia China ni moja ya Taifa ambalo lipo juu kiuchumi.

  Binafsi kuna mambo kadhaa nayatarajia kuona yakitokea kwenye mkutano huo wa vyama vya ukombozi wakiongozwa na CCM.

  Naamini mbali ya kujadili kwa kina masuala ya vyama hivyo na mchango wao pia itakuwa nafasi nzuri ya kujadili namna ya kuendeleza nchi za Afrika ikiwamo Tanzania.

  Ndio ukweli huo maana vyama hivyo vinamchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya nchi zao.

  Nani anabisha kuhusu mchango wa CCM katika ustawi wa maendeleo ya nchi. Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Magufuli imeendeleea kutekeleza Ilani ya CCM. 
  P
  Rais Magufuli anaendelea na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.Utendaji wake ndani ya CCM huenda nayo umekuwa chachu kwa China kuamua mkutano huo ufanyike katika aridhi ya Tanzania.

  Kasi yake katika kuleta maendeleo ni kubwa na inaleta matumaini kuwa Tanzania tunakwenda kuwa Taifa kubwa katika medani za kimaendeleo.

  Kupitia rasilimali zilizopo Rais Magufuli anafanya mambo makubwa na wakati mwingine unajiuliza anawezaje? Lakini anaongozwa na dhamira ya kweli ya kuona Taifa lake linapiga hatua na hatimaye tunashuhudia mambo makubwa yanafanyika.

  Achilia mbali suala la elimu bure ambalo Serikali ya CCM inatekeleza pia kupitia Rais Magufuli kuna miradi mikubwa ya ujenzi inaendelea kila kona ya nchi yetu.

  Unapomuangalia Rais Magufuli unamuona namna ambavyo anaona kabisa Tanzania kuwa na maendeleo ni jambo ambalo linawezekana. Ukimtazama usoni unamuona namna ambavyo anafikiria zaidi nchi yake katika kuelekea uchumi wa viwanda ili kufikia uchumi wa kati. Kwa namna ambavyo anakwenda kikubwa ni kumuombea kwa Mungu.

  Unajua kwa nini nimeweka kando kidogo kuzungumzia mkutano wa vyama hivyo ni kwa sababu naona kabisa viongozi wa vyama hivyo ambavyo vitakuwepo nchini kwenye mkutano huo watatumia nafasi hiyo kumpkongeza Rais Magufuli kwa kazi ambayo anaifanya tangu ameingia madarakani.

  Kwa ujinga wangu au ufinyu wa akili nilionao kuna mambo ambayo nayaona kabisa Rais Magufuli anayafanya kwa ajili ya nchi yeke kumbe kuna mataifa mengine makubwa yanaiga.

  Hata hivyo kuiga jambo jema si dhambi. Kwa mfano wakati Rais Magufuli moja ya mkakati wake ni kuhakikisha kunakuwa na miundombinu ya mawasiliano inayounganisha Tanzania na nchi nyingine iliyo imara na ya uhakika Rais wa China naye amekuja na mkakati wa kuiunganisha china na nchi nyingine duniani.

  Huwa nakaa na kisha natafakari namna ambavyo Rais Magufuli ambavyo anachukia rushwa .Namna ambavyo anataka nchi yake ipige hatua kwa kasi kubwa. 

  Namna ambavyo Rais Magufuli anasimamia uwajibikaji na utumishi wa umma wenye uadilifu.

  Naangalia namna ambavyo Rais Magufuli ameamua kuleta mageuzi ya kimaendeleo kwa nchi yake. 

  Ndivyo hivyo hvyo ambavyo pia namuona Rais wa China naye anapita njia ambayo Rais Magufuli ameamua kuipitia kwa ajili ya maendeleo.

  Nikiri China ni taifa ambalo ndani ya miaka 73 limefanikiwa kuwa taifa kubwa na lenye uchumi imara duniani. Ndivyo ambavyo namuona Rais Magufuli ambavyo anataka kutumia muda mfupi kuipeleka  Tanzania kuwa taifa lenye uchumi imara. Inawezakana kikubwa ni kumuombea afya njema.

  Tofauti iliyopo kati ya Rais Magufuli na Rais Xi Jinping ni kwamba China wamemua Rais wao akae madarakani hadi mwenyewe atakaposema basi.

  Lakini kwa Rais Magufuli kwa kuheshimu Katiba amekuwa akieleza mara kwa mara muda wake kwa mujibu wa Katiba ukimalizika basi atakwenda kupumzika.

  Ukiondoa tofauti hiyo huwa nakaa na kuona kama vile ndani ya kichwa cha Rais Magufuli kwa maana ya mipango aliyonayo kwa nchi yake haina tofauti kabisa na mipango ambayo Rais wa China anayo kwa watu wake. 

  Ni kama vile namuona Rais wa China katika kichwa cha Rais Magufuli.

  Nihitimishe kwa kuelezea msingi wa kueleza yooote hayo ni kwamba Julai 17 mpaka Julai 18 mwaka huu Tanzania inapokea ugeni mzito kwa ajili ya mkutano huo.

   Msemaji wa CCM Humphrey Polepole tayari ameulezea vema mkutano huo.Bado naamini Utendaji kazi wa Rais Magufuli umechangia kumfanya Katibu Mkuu wa CPC na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China kuamua mkutano huo kufanyika nchini Tanzania.

  Nikushukuru kwa kunisoma kuanzia mwanzo hadi hapa nilipoishia. Ahsante kwa uvumilivu wako maana ni maelezo ya kutosha lakini yenye nia njema na hasa katika hili la urafiki kati ya Tanzania na China.

  Pia ni kuhusu mkutano huo unaofanyika Julai 17 hadi Julai 18 mwaka huu. 

  Maoni 0713833822
  Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa katika mazungumzo na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong na ujumbe wake  walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam Machi 22, 2017 
  Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongozana na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong  walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam Machi 22, 2017.PICHA NA IKULU

  0 0

  Mwanasheria kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) Dkt. Philip Filikunjombe, akizungumza wakati wa kufunga kongamano la kujadili matumizi ya mtandao na utawala lililofanyika Chuo cha Usafirishaji (NIT) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
  Washiriki wakiwa kwenye kongamano hilo.
  Washiriki wakiwa kwenye kongamano hilo.
  Mratibu wa Jukwaa la Utawala wa Mtandao (TzIGF), Rebecca Ryakitimbo, akizungumza katika kongamano hilo kuhusu matumizi ya mtandao.
  Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Jabhera Matoghoro, akizungumzia matumizi ya mtandao. Kushoto ni Mratibu wa Jukwaa la Utawala wa Mtandao (TzIGF), Rebecca Ryakitimbo.
  Washiriki wakiwa kwenye kongamano hilo
  Mwakilishi kutoka Jamii Forums, Max Maxence, akizungumza.
  Mkuu wa Idara ya TEHAMA Chuo Kikuu cha Usafirisha (NIT), Edgar Telesphory, akizungumza.
  Mwakilishi kutoka Tanzania Youth Vission Association, Abdilah Lugome, akizungumza.
  Joy Wathagi kutoka nchini Kenya, akizungumza.
  Mshiriki Peter Mmbando, akizungumza  Na Dotto Mwaibale

  WATUMIAJI wa mitandao wametakiwa kujua haki na wajibu wanapotumia mtandao ili kuondoa mikanganyiko inayoweza kujitokeza kwa watumiaji dhidi ya serikali na makundi mengine.

  Hayo yalisemwa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mratibu wa Jukwaa la Utawala wa Mtandao (TzIGF), Rebecca Ryakitimbo wakati wa kufunga kongamano la kujadili matumizi ya mtandao na utawala.

  Alisema ni vizuri watumiaji wa mtandao wakajua haki na wajibu wakati wa matumizi ya mtandao.Ryakitimo alisema hapa nchini limeundwa jukwaa la utawala wa mtandao litakaloshughulikia kutoa elimu juu ya masuala ya mtandao ikijumuisha masuala ya kisheria, wajibu wa mtumiaji wa mtandao pamoja na kutoa mapendekezo ya watumiaji wa serikalini katika kutengeneza sera zenye tija kwa mamlaka na watumiaji.

  Alisema matumizi ya mtandao yamekuwa ni sehemu ya maisha ya binaadamu wa sasa ya kila siku ambapo watu wamekuwa wakitumia kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kujiajiri, kuwasiliana na hata kutoa na kupata elimu pia, kadri mawasiliano hayo ya mitandao yanavyozidi kukua, ndivyo mamlaka nazo zimeweza kuunda sera na sheria kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ya mitandao. 

  Aliongeza kuwa Umoja wa Mataifa nao uliunda jukwaa linaloshughulikia haki na wajibu wa watumiaji wa masuala ya mtandao, UNIGF. Hivyo hata nchi wananchama nao wameunda majukwaa kama hayo ili kuwa na kauli moja katika kutunga sera zinazokubalika kwa mamlaka na watumiaji ili kuleta usawa unaoleta uwajibikaji katika mitandao. 

  Mwanasheria kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) Dkt. Philip Filikunjombe alisema kuwa jukwaa hilo limekuja wakati muafaka ambapo watumiaji wa mtandao wanaongezeka kwa kasi huku wengi bado hawajui sheria na kanuni zinataka nini kwa mtumiaji.

  Baadhi ya watumiaji wa mtandao walisema kuwa ingawa jukwaa hilo lina mchanganyiko wa watu, hivyo wanantarajia uwakilishi mzuri serikalini siku za usoni, lakini jukwaa hilo limechelewa kwani serikali imekwishapitisha sheria walizozitaja kuwa ni kandamizi kwa watumiaji wa mitandao.

  Jukwaa la utawala wa mtandao lipo pia kwa mataifa mengine ya Afrika ya Mashariki, Joy Wathagi kutoka nchini Kenya, anasema kuwa jukwaa hilo kwa nchini kwao linanguvu kubwa na linatoa maoni yanayozingatiwa katika uundwaji wa sera, huku serikali nayo ikitoa ushirikiano mkubwa kwa jukwaa: 

  Jukwaa hilo liliandaa mjadala wa maoni na elimu, ambapo maoni mbalimbali ya wadau yalitolewa, fursa mbalimbali za kiuchumi na elimu kwa vijana kupitia mtandaoni yaliwekwa bayana.huku baadhi ya washiriki wakitoka mataifa mengine ya afrika ya mashariki ikiwemo kenya na wengine kutoka nchi zingine ikiwemo Afrika kusini na Nigeria walihudhuria.

older | 1 | .... | 1621 | 1622 | (Page 1623) | 1624 | 1625 | .... | 1897 | newer