Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

VIJIJI 56 MANONGA KUPATA UMEME MWAKA WA FEDHA 2018/2019

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MBUNGE wa Manonga Seif Gulamali ameeleza mkakati wake katika kusimamia miradi ya maendeleo kwa bajeti ya mwaka 2018/2019 ambapo amesema kuwa huduma kama afya, elimu na miundombinu ni muhimu na lazima jimboni humo.

Akizungumza na Michuzi blog Gulamali emeeleza kuwa vijiji vyote vya jimbo la Manonga vitapata umeme mwaka huu wa fedha 2018/2019. 

Kuhusu huduma za afya Manonga amesema kuwa wamefanikiwa kujenga kituo cha afya kilichogharimu Sh. milioni 400 na hiyo ni katika kuwasaidia wananchi kutotembea umbali mrefu kufuata huduma za afya na kituo hicho kina jengo la upasuaji, jengo la kuhifadhia maiti, jengo la mama na mtoto, maabara ya kisasa, jengo la kufulia na nyumba ya mganga katika kituo cha afya Simbo.

Aidha ameeleza wanaelekea kupata shule ya kwanza jimbo la Manonga na shule 3 Wilaya ya Igunga kuwa na kidato cha 5 na 6 kwani hadi sasa mabweni 4 na madarasa 2 kwa ajili ya kidato cha tano na sita yamekamilika katika shule ya Sekondari Ziba.

Kuhusu ujenzi wa daraja la Manonga kutoka Choma kwenda Shinyanga ambalo limekuwa ni kilio kwa miaka 50 Gulamali ameeleza kuwa wamepata zaidi ya shilingi Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo.Aidha ameeleza kiwanda cha pamba cha Manonga kilichokufa kwa miaka 20 kimefufuliwa na kinatoa ajira zaidi ya 500 kwa vijana wa Igunga, Tabora na nchini kwa ujumla na hii ina inatoa fursa kwa wajasiriamali hasa mama ntilie kwa kupata kipato kutokana na huduma wanazozitoa.

Kuhusu mradi mkubwa wa maji kutoka Mwanza hadi Igunga Gulamali ameiambia blogu ya jamii kuwa zaidi ya dola milioni 265 za kimarekani zimetengwa kwa ajili kutekeleza mradi huo na vijijji na kata zitapata maji kupitia mradi huo pia vijiji vya Mwisi, Mwamala na Sungwizi vitapata maji kutoka fedha kiasi ya Milioni 600 iliyotengwa kwa ajili ya mradi wa maji.

Gulamali ametoa rai kwa wananchi kutumia fursa zinazotolewa hasa katika elimu kwa kuwasihi wanafunzi kusoma kwa bidii kwani kama serikali wamewekeza sana katika elimu na watahakikisha wanatengeneza mazingira bora katika upatikanaji wa elimu bora.

TRA YATANGAZA MSAMAHA WA MADENI YA RIBA NA ADHABU KODI ZA NYUMA

$
0
0
Na Rachel Mkundai

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imetangaza msamaha wa riba na adhabu za madeni ya nyuma ya Kodi hadi asilimia mia moja ili kutoa unafuu kwa walipakodi wenye malimbikizo kulipa kodi ya msingi tu yaani “Principal Tax”

Akitangaza msamaha huo, Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa msamaha huo ni matokea ya utekelezaji  Maelekezo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Baraza la Wafanyabiashara (TNBC) uliofanyika Ikulu tarehe 20/03/2018 ambapo wafanyabiashara walilalamikia kuwepo kwa malimbikizo makubwa ya madeni ya kodi za nyuma yakijumuisha riba na adhabu,

Kichere amesema kuwa, ili kukamilisha hilo, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limefanya marekebisho kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2018 na sehemu ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015. 

“Katika marekebisho hayo Waziri mwenye dhamana ya Fedha na Mipango amepewa mamlaka ya kutoa utaratibu maalum wa kuwezesha Kamishna Mkuu kutoa msamaha riba na adhabu wa hadi asmilia mia moja riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodikwa asilimia mia moja tofauti na asilimia 50 ya hapo awali”, amesema.

Aidha, amebainisha kuwa lengo kuu la msamaha huu ni kutoa unafuu kwa walipakodi wenye malimbikizo ya madeni ya riba na adhabu kwa kuwapa fursa ya kulipa malimbikizo ya madeni ya msingi ya kodi “Principal Tax” kwa awamu ndani ya mwaka wa fedha 2018/19 ili kuwapa motisha ya kulipa kodi kwa hiyari na kwa Wakati.

Amesema kuwa msamaha wa riba na adhabu utahusu kodi zotezinazotozwa kwa mujibu wa Sheria zinazosimamiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania, isipokuwa: Ushuru wa Forodha unaosimamiwa chini ya Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004; na malipo  mengine yasiyo ya kodi ambayo TRA imepewa jukumu la kisheria la kuyakusanya. Mapato hayo ni kama vile: Kodi za Majengo na Ada za Matangazo.

Hata hivyo, Kamishna Mkuu wa TRA amesema kuwa watakaonufaika na utaratibu huu watatakiwa kuwa na sifa zifuatazo: Wawe wamewasilisha ritani za kodi lakini bado wanadaiwa kodi yote au sehemu ya kodi zitokanazo na ritani hizo; Hawajawasilisha ritani za kodi na wana madeni ya kodi; Ambao walikuwa wanafanyabiashara bila kusjiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN), namba ya usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VRN) au usajili mwingine wa kodi kwa mujibu wa sheria zinazosimamiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania;

Sifa nyingine ni wawe wamewasilisha pingamizi za kodi kwa Kamishna Mkuu na ambao pingamizi zao bado zinashughulikiwa katika ofisi za Mamlaka ya Mapato na sio kwenye mahakama za kikodi;  Ambao wamewasilisha pingamizi katika mahakama za kikodi na mashauri yao bado hayajatolewa maamuzi na wale ambao  wana madeni ya nyuma ya kodi ambayo hayatokani na kesi za jinai za kodi, utakatishaji Fedha, Usafirishaji wa binadamu au shughuli nyingine haramu.

Aidha, Mlipakodi atastahili kupata msamaha wa riba na adhabu endapo yeye binafsi au mwakilishi wake aliyeidhinishwa kisheria atawasilisha maombi ya msamaha kwa kujaza Fomu maalumu .

Na.ITX207.01.Einayopatikana katika tovuti ya TRA ikiambatana na; Maelezo ya kuonyesha kiasi anachodaiwa pamoja nakukubali kwa hiyari kulipa deni lake la msingi “Principal Tax”  Kukubali kwa maandishi kulipa kiasi chote cha kodi bila riba na adhabu ndani ya mwaka wa fedha 2018/2019 ikiwa na maana kabla au ifikapo tarehe 30 Juni 2019; na Kwa madeni yaliyo katika pingamizi; kukubali deni la kodi alilokadiriwa na kuwa tayari kutoendelea na pingamizi au shauri husika la kodi lililowasilishwa kwa Kamishna Mkuu, Bodi ya Rufani za Kodi au Mahakama ya Rufaa.

Hata hivyo, msamaha utatolewa kwa maombi yatakayokidhi masharti na kukubaliwa na Mamlaka ya Mapato ambapo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Mlipakodi husika watasaini mkataba wa makubaliano utakaoanisha deni lote la kodi; riba na adhabu inayosamehewa, pamoja na kodi isiyo na riba wala adhabu itakayopaswa kulipwa kabla ya tarehe 30 Juni, 2019.

TRA inawahimiza walipakodi wote nchini kutumia fursa hii adhimu kwa kushiriki kikamilifu katika zoezi hili maalum la utoaji wa msamaha wa riba na adhabu na kwamba utoaji  wa taarifa sizizo sahihi ni kosa kisheria, endapo itabainika hivyo itapelekea muombajikupoteza sifa ya kufaidika na msamaha huu

DC MONDULI AZINDUA KIWANDA KIDOGO CHA KUCHAKATA NGOZI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Monduli,Idd Hassan Kimanta jana Julai,11/2018 amezindua kiwanda kidogo cha kuchakata Ngozi na kutengeneza bidhaa za ngozi kiwanda hicho kipo katika kijiji cha Mswakini na kutoa vyeti kwa wanakikundi waliofuzu mafunzo.

kiwanda hicho ni matokeo ya kikundi cha akinamama 22 ambao mwezi Agosti 2017 walijiunga pamoja na kupata ufadhili kutoka shirikikala OIKOS kwa lengo kujijenga kiuchumi kupitia Ngozi na kuunga mkono Juhudi za Serikaliya kuelekea Tanzania ya Viwanda.

Katika hafla hiyo,Mkuu wa Wilaya amewapongeza akinamama hao kwa uamuzi wao huo na kuwaahidi kuwa ,kupitia Halmashauri ya Wilaya Monduli atahakikisha wanapata Mkopo ili kuongeza mtaji.

Pia amelishukuru Shirika la Misaada la Marekani-USAID kwa kulipatia fedha shirika la OIKOS ambalo ndilo lililosimamia mchakato wote kupitia Mradi wa Ikolojia Hatarini Kaskazini mwa Tanzania. 
 Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Idd Hassan Kimanta  (pichani kati) akitazama baadhi ya bidhaa za ngozi zinazotengenezwa na kiwanda kidogo cha kuchakata Ngozi kilichopo katika kijiji cha Mswakini,wilayani humo.
 Mkuu wa Wilaya ya Monduli,Idd Hassan Kimanta akitoa vyeti kwa baadhi ya Wanakikundi waliofuzu mafunzo.
 Baadhi ya Bidhaa za ngozi zikiwa tayari kwa kuuzwa

TAARIFA YA KUHAMA KWA MAKAO MAKUU YA OFISI ZA PPRA

MTENDAJI WA KIJIJI KURUYA APEWA SIKU 19 KUREJESHA FEDHA ALIZOTAFUNA

$
0
0
Na Frankius Cleophace, Rorya

SERIKALI imemsimamisha kazi Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kuruya katika Kata ya Komuge wilayani Rorya mkoani Mara Mwita Mangondi kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha Sh.1,960,387 ikiwa ni pamoja na kushindwa kusomea wananchi mapato na matumizi huku akipewa siku 19 kurejesha mara moja fedha hizo.

Ofisa Mtendaji huyo amesimamishwa kazi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kuruya baada ya wananchi kutoa kilio chao cha muda mrefu kuhusu kutosomewa mapato na matumizi tangu Mwaka 2012 mpaka sasa.

Ambapo wamezidi kutupia lawama viongozi waliopo kuanzia ngazi za Vijiji hadi kata.Ofisa Utumishi Wilaya ya Rorya Peter Masanja akiwa katika mkutano huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Charles Chacha amesema asimamisha kazi mtendaji huyo nakumpa siku 19 kurudisha fedha hizo. Pia anatakiwa kuripoti kila siku ofisi ya Mtendaji wa kata

Amesema kuwa kitendo cha Mtendaji huyo kufanya ubadhirifu wa fedha hizo kutokana na sheria za utumishi hawawezi kulifumbia macho hivyo amewataka wananchi kuwa wavumilivu kuhusu kumwondoa madarakani mwenyekiti wa Kijiji hicho kutokana na tuhuma walizozisema wananchi katika mkutano huo.

“Mimi Mamlaka niliyonayo ni ya kuondoa Mtendaji wa kijiji lakini sina mamlaka ya kuondoa Mwenyekiti nyie ndo wenye mamlaka mkifuata taratibu lakini kwa sasa mkimwondoa Halmashauri hautuafanya uchaguzi mpaka mwakani sasa baadhi ya maendeleo yatazidi kukwama niwasihi kuwa wavumilivu,” amesema.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Komuge William Nestory amesema kuwa endapo fedha hizo hazitarudishwa ataungana na wananchi kutoa taarifa eneo husika.

Huku akiomba Ofisa utumishi kutilia mkazo kufanyika kwa mikutano ya kisheria ili wananchi wasomewe mapato na matumizi kwani suala hilo limekuwa changamoto kubwa katika vijiji vinavyounda kata yake.

Amewataka wananchi kuendelea kujitoa katika suala la kuchangia maendeleo ikiwemo ujenzi wa maboma katika sekta ya elimu na afya ili Serikali iweze kumalizia.“Nikiwa katika Halmashauri fedha zinakuja naulizwa kama kuna maboma ili fedha zije kumalizia hakuna wananchi hawaji kwenye maendeleo viongozi wa vijiji ni mizigo sasa tumechoka kila sehemu napita lawama za fedha za wananachi,” amesema.

Kwa upande wa Kaimu Mkuu wa Takukuru wilayani Aloyce Marenge amesema fedha za Serikali kukaa mikononi mwa mtu na kuwekwa katika akaunti ya mtu binafsi na siyo akaunti ya Serikali ya kijiji ni kosa kisheria.

Pia akihaidi kafuatilia fedha hizo zinalipwa mara moja na kuchukua hatua kali dhidi ya kiongozi huyo.“Sisi Takukuru tutaendelea kufanya kazi yetu ikiwa ni pamoja na Kuhakikisha mtendaji huyo anarejesha pesa zote kama alivyoewa mwisho wa Mwezi na hatua nyingine zitaendelea kuchukuliwa,” amesema Aloyce.

Awali katika mkutano wa wananchi uliofanyika katika kijiji cha Kuruya kata ya Komuge Wilayani Rorya mkoani Mara wananchi wanatupia lawama viongozi wa Serikali za Vijiji akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji hicho Benard Wambura kuwa wamekuwa wakitunza fedha za Serikali mifukoni mwao na kushindwa kusoma mapato na matumizi na wakati mwingine kujikopesha wenyewe fedha hizo suala ambalo limewachosha wananchi.

Ili kikao kiweze kuendelea vizuri Mwenyekiti wa kijiji hicho Benard Wambura na Mtendaji aliyesimamishwa walipisha kiti Mpaka mkutano huo unamalizika kutokana na wananchi hao kuwatuhumu na kudai wakiendelea kuongoza kikao kuna baadhi ya wananchi wataminywa kuongea ukweli unaowahusu.
Afisa utumishi Wilaya ya Rorya Mkoani Mara Peter Masanja akiongea na Wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kuruya kata ya Komuge Wilayani Rorya Mkoani Mara.
Wananchi wa kijiji cha Kuruya wakiwa katika Mkutano wa hadhara.
Wananchi wa kijiji cha Kuruya wakiwa katika Mkutano wa hadhara.
Mtendaji wa kijiji cha Kuruya Mwita Mangondi aliyesimamishwa Kazi katika Mkutano huo akijibu baadhi ya hoja za Wananchi zikiwemo tuhuma zake za ubadhilifu wa fedha.
Diwani wa kata ya Komuge William Nestory akiongea na Wananchi katika Mkutano huo ambapoameomba Afisa Utumishi kutilia Mkazo kufanyika kwa Vikao vya Kisheria ili wanaanchi wasomewe Mapato na Matumizi.
Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Wilayni Rorya Aloyce Marenge akitoa somo kwa wananchi hao ambapo amesema kuwa kutunza fedha za serikali katika akaunti ya binafsi ni kosa kisheria huku akihaidi wananchi hao kufuatilia suala la upotevu wa fedha zilizosababisha Mtendaji wa kijiji kusimamishwa kazi zinapatikana na kuchukuliwa hatua kali.
Kutoka kushoto ni Mtendaji wa Kijiji cha Kuruya Mwita Mangondi ambaye amesimamishwa kazi akiwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bernard Wambura ambaye pia wananchi wamemutupia lawama kuwa kiti chake kinapwaya naye amekuwa akikumbwa na tuhuma mbalimbali za ubadhilifu wa fedha za serikali japokuwa mpaka saas ameisha rejesha fedha hizo.

RAIS DK MAGUFULI AMTEUA CASMIR SUMBA KYUKI KUWA MWENYEKITI WA BODI YA UTT AMIS

"HAKUNA BEI NZURI YA KAHAWA-UGANDA" DKT TIZEBA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akikisitiza jambo wakati akizungumza na wadau wa biashara ya Kahawa katika ukumbi wa Happiness Hoteli uliopo katika eneo la Mtukula Wilayani Misenyi, Leo 11 Julai 2018. (Picha zote Na Mathias Canal-WK)
Wadau wa biashara ya Kahawa wakifatilia mkutano wa Waziri wa Kilimo Mhe. dkt Charles Tizeba katika ukumbi wa Happiness Hoteli uliopo katika eneo la Mtukula Wilayani Misenyi, Leo 11 Julai 2018.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage akisalimiana na Waziri wa biashara na ushirika nchini Uganda Mhe Fredric Ngobi Gume muda mchache kabla ya kuanza kwa mkutano wa mawaziri wa nchi hizo mbili, mkutano uliohudhuriwa pia na Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba, Leo 11 julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisalimiana na Waziri wa biashara na ushirika nchini Uganda Mhe Fredric Ngobi Gume muda mchache kabla ya kuanza kwa mkutano wa mawaziri wa nchi hizo mbili, mkutano uliohudhuriwa pia Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage, Leo 11 Julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati wa mkutano na Waziri wa biashara na ushirika nchini Uganda Mhe Fredric Ngobi Gume (Kushoto), Mwingine ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage (Katikati).

Na Mathias Canal-WK, Mtukula-Kagera

Imebainika kuwa bei ya uuzaji wa Kahawa nchini Uganda haina tofauti kubwa na bei ambayo ingepatikana nchini Tanzania endapo wakulima wangeuza Kahawa zao kwenye soko la awali jambo ambalo linawatoa wasiwasi wakulima wa Kahawa nchini waliokuwa wakidanganywa kuwa bei ya Uganda ni kubwa na yenye tija kwa wakulima kuliko hapa nchini.

Kilogramu moja ya Kahawa ya maganda nchini Uganda inanunuliwa kwa shilingi 2000 ya Uganda sawa na Shilingi 1400 za Kitanzania (exchange rate 1.7) ilihali hapa nchini Tanzania bei ya Kahawa kwa kilo moja ya maganda ni Shilingi 1460 ya bei elekezi hivyo kuwa na tofauti ya Shilingi 60. 

Hata hivyo, wakulima wa Tanzania watapata zaidi kwa kuuza mnadani moja kwa moja na kuachana na bei ya shambani kwa kutumia ushirika wao ambapo bei ya chini inayopatikana ni wastani wa Shilingi 1950 kabla ya gharama za uendeshaji. Kwa kuuza mnadani mkulima anapata bei kutokana na Ubora wa Kahawa yake na ikiwa kwenye madaraja na hivyo kutoa motisha kwa wakulima kuzalisha Kahawa bora kuliko kuuza ikiwa ghafi.

Hayo yamebainishwa leo 11 Julai 2018 na Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba wakati akizungumza na wadau wa biashara ya Kahawa katika ukumbi wa Happiness Hoteli uliopo katika eneo la Mtukula Wilayani Misenyi.

Dkt Tizeba amezungumza hayo ikiwa ni muda mchache tangu alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Biashara na Ushirika nchini Uganda Mhe Fredrick Ngobi Gume katika mkutano uliohudhuriwa pia na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage.

Mkutano huo ni muendelezo wa utekelezaji wa maagizo ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliyoyatoa wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 2 Julai 2018 na kuitaka Wizara ya Kilimo kufuatilia kwanini wakulima wa zao la Kahawa wanacheleweshewa malipo yao sambamba na kujua kwanini wakulima wanauza Kahawa yao nchini Uganda.

"Ndugu zangu kuna jambo hamlifahamu wale wanaosema Uganda bei ya Kahawa ni nzuri kuliko Tanzania wanawadanganya hakuna bei nzuri Kule kinachofanya watu kupeleka Kahawa Uganda ni kutokana na mikopo wanayokopeshana isiyo rasmi (Butura) hivyo makubaliano ya kurejesha mkopo yanakuwa na masharti magumu yanayowataka wakulima wa Kahawa nchini kulipa madeni kwa kupeleka Kahawa sio fedha" Alisisitiza Dkt Tizeba wakati akizungumza na wadau wa Kahawa eneo la Mtukula Wilayani Misenyi

Waziri wa biashara na ushirika nchini Uganda Mhe Fredric Ngobi Gume amemuhakikishia mwenyeji wake kuwa biashara ya Kahawa nchini humo ina changamoto sawa katika nchi zote mbili kwa kuwa swala la mikopo isiyo rasmi inayowanyonya wakulima (Butura) nchini Uganda ipo kwa kiwango cha juu kiasi kwamba ameomba kuja kuja nchini kwa miadi maalumu kwa minajili ya kujifunza kuhusu namna bora kuendesha ushirika na kuanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani.

Aidha, Gume alisema kuwa serikali ya Uganda inayoongozwa na Rais wa nchi hiyo Mhe Yoweri Kaguta Museveni itaendeleza ushirikiano na serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli hivyo panapohitajika ushirikishwaji katika biashara hususani kwenye sekta ya Kilimo watakuwa na msimamo wa pamoja.

Katika hatua nyingine pande zote mbili kutoka Tanzania na Uganda wameeleza changamoto mbalimbali zinazoikabili mipaka ya nchi hizo ikiwemo biashara ya magendo inayofanyika huku wakiahidi kutokomeza kadhia hiyo.

MZEE MANGULA ATEMBELEA BANDA LA NSS MAONESHO YA SABA SABA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Kaimu meneja wa Uhusiano na Masoko,Salim Khalfan akitoa ufafanuzi wa huduma zinazopatikana ndani ya NSSF kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara, Philip Mangula alipotembelea banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF leo asubuhi kwenye maonesho ya biashara ya 42 ya kimataifa yanayoendelea jijini Dar es salam,Ndugu Mangula pia alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zitolewazo na Shirika hilo,Pichani kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Professa Godius Kahyarara

HESLB YASOGEZA MBELE MAOMBI YA MKOPO KWA MTANDAO HADI JULAI 31

WAZIRI MKUU AHUTUBIA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CCT JIJINI DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Makamu wa Kwanza wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dkt. Fredrick Shoo wakati alipowasili kwenye ukumbi wa CCM jijini Dodoma kuhutubia Mkutano wa Halmashairi Kuu ya CCT Julai 12, 2018. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dkt. Anilikisa Cheyo  na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Jukuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)  jijini Dodoma, Julai 12, 2018. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dkt. Anilikisa Cheyo, na wapili kushoto ni Makamu wa Pili wa Mwenyekiti wa CCT, Askofu, Dkt. Jacob Chimeledya.
 Baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania  (CCT) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCT jijini Dodoma Julai 12, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana  na  Makamu wa Kwanza wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo  Tanzania (CCT), Askofu Dkt. Fredrick Shoo baada ya kuhutubia Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCT jijini Dodoma Julai 12, 2018. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dkt. Anilikisa Cheyo na wapili kulia ni  Makamu wa Pili wa Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dkt. Jacob Chimeledya. (Picha na  Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI LUGOLA ATEMBELEA IDARA YA UHAMIAJI MAKAO MAKUU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, akizungumza na Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, aliyefika Idara ya Uhamiaji,jijini Dar es Salaam,wakati wa ziara ya kikazi.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dk. Anna Makakala akimkaribisha  Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola aliyefika Idara ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ndani.
 Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiangalia pasipoti ya kielektroniki inayotolewa na Idara ya Uhamiaji, alipotembelea Makao Makuu ya idara hiyo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Msimamizi wa chumba cha Uchapaji, Mrakibu Msaidizi, Samuel Gambadu.
 Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akiongea na wananchi waliofika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na idara hiyo.jijini Dar es Salaam. 
 Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimuuliza swali mwananchi aliyefika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji kupata huduma.Waziri Lugola yupo katika ziara ya kikazi.

WASHINDI WA AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY DROO YA TATU WAPATIKANA

$
0
0
Mkazi wa Morogoro, Frank Kisayo ameshinda zawadi ya televisheni ya kisasa aina ya Samsung yenye ukubwa wa inchi 32 kupitia promosheni ya Amsha Amsha Ushinde na Airtel Money ambayo inaendeshwa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.

Kisayo ambaye ni mkulima, alishinda televisheni hiyo kwenye droo ya tatu iliyofanyika kwenye Ofisi Makao Makuu ya Ofisi za kampuni ya simu ya Airtel jijini.

Akizungumza kwa njia ya simu mara baada kushinda droo hiyo, Kisayo alisema kuwa amefurahi sana kushinda zawadi hiyo yenye thamani si chini ya Sh750,000.

“Siamini kama nimeshinda, nasubiri kwa hamu zawadi yangu, naamini sasa suala la kununua televisheni kwangu limeisha baada ya kushinda zawadi hii nono ya droo ya Amsha Amsha,” alisema Kisayo.

Mbali ya Kisayo, pia Masoud Saleh wa Kisarawe  na Shadrack Sanga wa Manyara kila mmoja alishinda simu ya mkononi aina ya Samsung Galaxy yenye thamani Sh500,000.

Pia Eric  Samwel ambaye ni mkazi wa Tanga alijishindia jezi na tiketi ya msimu ya kuona mechi ya Yanga na Simba za msimu ujao.

Maneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema kuwa mpaka sasa washindi watatu wa televisheni, simu 25 na jezi 25 wamepatikana katika droo hiyo.
Meneja Matukio wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Dangio Kaniki, akiongea na moja ya washindi wa AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY kwa kushirikiana na Sportpesa, Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Uhusiano Sabrina Msuya Kushiriki, mteja atatakiwa kupiga *150*60# kisha kutuma pesa kwenye akaunti ya SportPesa namba 150888 kisha kuweka kubashiri.
Meneja Uhusiano SportPesa Sabrina Msuya, akiongea na moja ya washindi wa AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY kwa kushirikiana na Sportpesa, Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Matukio Airtel Tanzania. Mteja atatakiwa kupiga *150*60# kisha kutuma pesa kwenye akaunti ya SportPesa namba 150888 kisha kuweka kubashiri.


Tigo Yazindua Kampeni mpya ya ‘Tigo Pesa ni Zaidi ya Pesa’

$
0
0
Kampuni ya Tigo Tanzania, leo imezindua kampeni ya ‘Tigo Pesa ni Zaidi ya Pesa’, kama uthibitisho kuwa huduma hiyo sasa ina hadhi ya huduma kamili ya kifedha ambayo inawapa wateja huduma za kipekee, bora na  nyingi zaidi kupitia mtandao wa simu. 

‘Tigo Pesa ni Zaidi ya Pesa’ inazingatia sifa ya Tigo kuwa mtandao pekee unaobuni huduma na bidhaa kulingana na mahitaji ya wateja ili kuboresha na kurahisisha maisha yao. 

‘Tigo Pesa imepanua wigo wa bidhaa na huduma zake na kuibua njia bora zaidi kwa wateja kufurahia huduma za haraka, uhakika na salama za kifedha popote walipo nchini Tanzania,’ Hussein Sayed, Afisa Mkuu wa  Huduma za Kifedha wa Tigo aliwaambia waandishi wa habari. 

Kama sehemu ya kampeni hii, Tigo Pesa inajivunia kuwa mtandao pekee na wa kwanza wa simu unaotoa huduma inayowezesha wateja wa Tigo kurudisha miamala ya fedha zilizotumwa kimakosa kwenda kwa wateja wenzao wa Tigo.  Huduma hiyo inayopatikana kupitia menu ya Tigo Pesa  *150*01# inawapa wateja wa Tigo uwezo wa kurudisha kwa haraka miamala yoyote ya kutuma hela ikiwa watagundua kuwa wamekosea miamala hiyo, bila ya kuhitaji msaada wa moja kwa moja kutoka kitengo cha huduma kwa wateja. 

‘Huduma hii ya kipekee ya kurudisha miamala iliyokosewa kwa haraka inajibu mahitaji ya wateja wengi ambao kwa sababu moja au nyingine wanafanya makosa pindi wanapotuma pesa. Ni huduma ya aina yake ambayo inawapa wateja uwezo zaidi juu ya miamala wanayofanya na imeundwa kwa kuzingatia vigezo vya hali ya juu vitakavyozuia matumizi mabaya ya huduma hii,’ Hussein alifafanua
Afisa Mkuu wa  Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Tigo Pesa ni Zaidi ya Pesa.’ Tigo Pesa pia imezindua huduma mpya ya Jihudumie itakayowasaidia wateja wa Tigo kurudisha miamala ya kutuma fedha waliyokosea, bila kuhitaji msaada kutoka kitengo cha huduma kwa wateja. Kulia ni Mkuu wa Udhibiti Ubora wa Tigo Pesa, Angelica Pesha.


WAZIRI WA BIASHARA NA USHIRIKA-UGANDA AVUTIWA NA UENDESHAJI USHIRIKA NCHINI TANZANIA AOMBA RIDHAA KUJA KUJIFUNZA NCHINI TANZANIA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisalimiana na Waziri wa biashara na ushirika nchini Uganda Mhe Fredric Ngobi Gume muda mchache kabla ya kuanza kwa mkutano wa mawaziri wa nchi hizo mbili, mkutano uliohudhuriwa pia Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage, Jana 11 Julai 2018. (Picha zote Na Mathias Canal, WK)

Kikao kikiendelea eneo la Mtukula Wilayani Misenyi. Jana 11 Julai 2018
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage akisalimiana na Waziri wa biashara na ushirika nchini Uganda Mhe Fredric Ngobi Gume muda mchache kabla ya kuanza kwa mkutano wa mawaziri wa nchi hizo mbili, mkutano uliohudhuriwa pia na Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba, Jana 11 julai 2018.


Mathias Canal-WK, Mtukula-Kagera


Serikali ya Uganda imeeleza kuvutiwa na uendeshaji wa ushirika nchini Tanzania hivyo imeomba kupata ridhaa ya kuzuru nchini Tanzania ili kujifunza namna bora ya uendeshaji wa ushirika.


Ombi hilo limetolewa jana 11 Julai 2018 na Waziri wa Biashara na Ushirika nchini Uganda Mhe Fredrick Ngobi Gume wakati akizungumza kwenye mkutano uliohudhuriwa pia na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage uliofanyika katika eneo la Mtukula Wilayani Misenyi.


Katika mkutano huo Waziri huyo  anayeshughulikia Ushirika nchini Uganda alimpongeza Waziri wa Kilimo nchini Mhe Dkt Charles Tizeba kwa Nazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha muda mfupi kurejesha imani kubwa na ushirika kwa wakulima ambapo alimpongeza pia kwa tuzo ya heshima aliyokabidhiwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe Kassim M. Majaliwa kwa niaba ya wana ushirika wakati wa sherehe za kilele cha siku ya ushirika Duniani kwenye viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza.


Waziri wa biashara na ushirika nchini Uganda Mhe Gume alimuhakikishia mwenyeji wake kuwa biashara ya Kahawa nchini humo ina changamoto sawa katika nchi zote mbili kwa kuwa swala la mikopo isiyo rasmi inayowanyonya wakulima (Butura) nchini Uganda ipo kwa kiwango cha juu.


Alisema kuwa serikali ya Uganda inayoongozwa na Rais wa nchi hiyo Mhe Yoweri Kaguta Museveni itaendeleza ushirikiano na serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli hivyo panapohitajika ushirikishwaji katika biashara hususani kwenye sekta ya Kilimo watakuwa na msimamo wa pamoja.


Alisema miongoni kwa mambo mengine ya kujifunza nchini Tanzania itakuwa ni pamoja na kujifunza kuhusu namna bora  ya kuendesha ushirika na kuanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani.


Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba alimueleza Waziri Gume kuwa njia mojawapo ya kusimamia ushirika ni pamoja na mkakati wa usimamizi madhubuti ikiwa ni pamoja na kuwaweka kizuizini wabadhilifu wote katika ushirika.


Mkutano huo ni muendelezo wa utekelezaji wa maagizo ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliyoyatoa wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 2 Julai 2018 na kuitaka Wizara ya Kilimo kufuatilia kwanini wakulima wa zao la Kahawa wanacheleweshewa malipo yao sambamba na kujua kwanini wakulima wanauza Kahawa yao nchini Uganda.


Naye Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage aliongeza kuwa wakulima wa Tanzania na Uganda wanapaswa kuweka msisitizo katika Kilimo kwani kufanya hivyo kutaongeza uimara na uanzishwaji wa viwanda vitakavyoongeza chachu ya ajira kwa wananchi.

RC MAKONDA AKABIDHI MWENGE WA UHURU MKOA WA PWANI.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Julai 12 amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo baada ya Mwenge huo kukamilisha shughuli ya uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 32.

RC Makonda amesema kuwa ndani ya siku tano ambazo mwenge ulikuwa jijini Dar es salaam umefanikiwa kutembelea, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi 36 ya maendeleo kwenye wilaya zote tano. 

Aidha RC Makonda amewashukuru wananchi wa Dar es salaam kwa ushirikiano mkubwa walioonesha tangu siku mwenge ulipoingia hadi leo alipoukabidhi kwa mkoa wa Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo mapema leo baada ya Mwenge huo kukamilisha shughuli ya uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 32 Mkoani Dar Es Salaam.

“GHARAMA ZA UENDESHAJI WA VYAMA VIKUU VYA USHIRIKA KUDHIBITIWA”-DKT TIZEBA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akitoa ufafanuzi kuhusu sintofahamu ya biashara ya kahawa wakati akizungumza kwenye mualiko maalumu na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera kwenye Hoteli ya Bukoba Coop, Leo 12 Julai 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wakisikiliza ufafanuzi wa Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kuhusu sintofahamu ya biashara ya kahawa wakati akizungumza kwenye mualiko maalumu na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa kwenye Hoteli ya Bukoba Coop, Leo 12 Julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akitoa ufafanuzi kuhusu sintofahamu ya biashara ya kahawa wakati akizungumza kwenye mualiko maalumu na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera kwenye Hoteli ya Bukoba Coop, Leo 12 Julai 2018.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera Bi Costansia Buhiye akitoa neno kwa niaba wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoani humo mbele ya Waziri Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kutokana na ufafanuzi alioutoa kuhusu sintofahamu ya biashara ya kahawa wakati akizungumza kwenye mualiko maalumu na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera kwenye Hoteli ya Bukoba Coop, Leo 12 Julai 2018.
Waziri Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akijadili jambo na Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Kagera Mhe Oliver Semuguruka mara baada ya kutoa ufafanuzi kuhusu sintofahamu ya biashara ya kahawa wakati akizungumza kwenye mualiko maalumu na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera kwenye Hoteli ya Bukoba Coop, Leo 12 Julai 2018.





Na Mathias Canal-WK, Bukoba-Kagera

Malalamiko ya muda mrefu ya wakulima yaliyokuwepo kwamba ushirika unatoa bei ndogo, sasa yamepatiwa muarobaini baada ya serikali kupitia kwa kina gharama za uendeshaji na uongezaji thamani kwa zao la kahawa kwa Vyama vikuu vya ushirika Mkoani Kagera.

Serikali imepiga marufuku kwa vyama hivyo vya ushirika kutoza zaidi ya shilingi 490 kwa kilo moja ya Kahawa ya maganda kama gharama za uendeshaji na uongezaji thamani, Awali maainisho ya gharama hizo yalikuwa ni makubwa ambapo kiasi cha shilingi 1350 kwa kilo moja ya Kahawa ya maganda ilianishwa kama gharama za uendeshaji.

Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba ameeleza agizo hilo Leo 12 Julai 2018 wakati akizungumza na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera kwenye Hoteli ya Bukoba Coop ambapo miongoni mwa ajenda ya kikao hicho ilikuwa ni kujadili kuhusu soko la Kahawa na uendeshaji wa ushirika.

Dkt Tizeba amewaeleza wajumbe hao kuwa amepiga marufuku hiyo kufuatia malalamiko ya wadau wa Kahawa Mkoani Kagera ambapo gharama hizo zilionekana kuwa kubwa ukilinganisha na gharama halisi.

"Ndugu zangu wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM inawezekanaje shilingi mia mbili inatozwa kama ushuru wa chama kikuu, na shilingi mia mbili tena inatozwa kama ushuru wa chama cha msingi, ni nani anaweza kukupa faida namna hii sasa rasmi ushuru huu tumeupunguza kama nilivyoeleza" Alikaririwa Mhe Tizeba

Aliongeza kuwa swala la ushirika ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo ni mkataba kati ya wananchi na serikali katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2015-2020 kwa imani kubwa kwamba ndicho chombo pekee kitakacho mkwamua mkulima na changamoto anazo kabiliana nazo kwenye Kilimo na masoko ikiwa ni pamoja na kujiondoa katika umasikini.

Aidha, Dkt Tizeba aliwaeleza wajumbe hao kuwa vyama vya ushirika havipaswi kuendeleza mazoea ya kujiwekea gharama bila kwanza kutazama kipato cha mkulima huku akieleza kuwa amewaelekeza wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ambapo Wilaya zao zinalima Kahawa kote nchini kufuatilia kwa karibu mwenendo wa masoko ya Kahawa kuanzia inavyokusanywa mpaka wakati inapouzwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera Bi Costansia Buhiye amempongeza Waziri huyo wa kilimo kwa kujibu kero namba 10 ya kikao cha Halmshauri kuu ya CCM kuhusu wasiwasi wa bei ya kahawa na namna na uendeshaji wa ushirika.

Buhiye alimpongeza Waziri huyo kwa kutatua kadhia mbalimbali za wakulima wa Kahawa katika ziara yake ya siku tatu Mkoani humo huku akieleza kuwa ana imani kubwa sasa kuwa wajumbe hao watatembea kifua mbele endapo wakulima wao watapatiwa bei nzuri.

BINGWA WA KAGAME CUP KUJULIKANA KESHO

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya Jamii. 

Michuano ya Kagame Cup 2018 yanafikia kilele chake siku ya kesho tarehe 12 julai kwa kuzikutanisha Azam na Simba katika dimba la Uwanja wa Taifa. 

Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Michezo Afrika Mashariki CECAFA Nicolaus Musonye amesema timu mbili kutoka Tanzania ambazo ni Simba na Azam zimefanikiwa kuingia fainali na zitakutana kesho ili kumfahamu Bingwa mpya wa michuano hiyo kwa mwaka 2018.

"timu zilizofanikiwa kutinga fainali ni Azam pamoja na Simba na mchezo huo utachezwa kuanzia majira ya saa 12 jioni katika Uwanja wa Taifa,"amesema Musonye.Mchuano huo utafanyika majira ya saa 12 jioni ,huku akiwapongeza wadau wote wa mpira Kwa kutoa michango yao kwa Hali na mali mpaka hapo walipofikia . 

Musonye ameeleza kuwa timu 12 zote zilizoshiriki Kagame Cup zimefanya vizuri kwenye mashindano hayo na wajitahidi, kwenye mashindano yajayo wasivunjike moyo Kwa wale wasiofanikiwa kuingia fainali. Sanjari na hilo, Musonye amesema amepokea maombi kutoka nchi zingine za jirani kujiunga kwenye michuano hiyo ikiwamo Zambia,malawi pamoja na Congo . 

Musonye amewaomba Wadau na mashabiki wa timu hizo wajitokeze Kwa wingi na viingilio vitakuwa vya bei ya kawaida ili watu wote waweze kumudu kuingia japo mpaka sasa havijatangazwa rasmi alisema Musonye.
Katibu Mkuu wa CECAFA Nicolaus Musonye.

Tutamfunga Simba kutetea ubingwa wetu-Azam fc

$
0
0
Na Agness Francis,globu ya jamii

Azam fc yatamba kumgaragaza mnyama simba katika fainali za kuwania kombe la kagame cup (CECAFA).

Timu hizo zote mbili za kutoka hapa nchini ambazo zimefanikiwa kutinga fainali, zitashuka dimbani kesho majira ya saa 12 jioni kuchoshana nguvu katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya jana Azam FC kumuondosha Gor Mahia ya Nchini Kenya katika michuano hiyo kwa kipigo cha mabao 2-0, sasa wanakutana na wekundu wa msimbazi katika kumjua nani ataibuka kidedea wa kombe hilo.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam msemaji wa Azam FC Jaffary maganga amesema kuwa kikosi chao kimejipanga vizuri kuhakikisha wanatetea ubingwa wao wa mwaka 2015 ambapo michuano hiyo ilifanyika kwa mara ya mwisho hapa nchini,Jaffary amesema maandalizi waliyofanya ni mazuri na ndio maana wamefanya vema na mpaka kufikia hatua hiyo.

"Tunaiheshimu Simba ni timu kongwe ya muda mrefu ilio na kikosi mahiri lakini sisi azam tunaliamini benchi letu la ufundi pamoja na mwalimu,tunaahidi kufanya vizuri kwa kumfunga simba"amesema jaffary.

Mtanange huo utakaokuwa wa ina yake wa kiburudani kwa mashabiki ,inaonyesha zahiri kuwa soka la Tanzania limezidi kuimarika katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati.
Msemaji wa Azam FC Jaffary maganga

WAZIRI KANGI LUGOLA AFANYA KIKAO NA MAAFISA NA ASKARI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI, JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza wakati wa Kikao na Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Katikati ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye na kushoto ni Kamishna wa Usalama dhidi ya moto, Jesuald Ikonko. Kikao hicho kimefanyika ofisi ndogo ya wizara jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza wakati wa Kikao na Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Katikati ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye na kushoto ni Kamishna wa Usalama dhidi ya moto, Jesuald Ikonko. Kikao hicho kimefanyika ofisi ndogo ya wizara jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Operesheni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage, akiwasilisha taarifa ya shughuli za jeshi hilo mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kulia), wakati wa ziara ya waziri alipotembelea makao makuu ya jeshi hilo, jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (hayupo pichani), wakati wa ziara ya waziri kutembelea jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

POLISI SHINYANGA YATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO

$
0
0
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limeendesha mafunzo kuhusu masuala ya usalama barabarani kwa wamiliki na madereva wa magari,pikipiki na bajaji ikiwa ni sehemu ya njia za kukabiliana na ajali zinazojitokeza na kusababisha vifo na majeruhi. 

Mafunzo hayo yaliyofunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro yamefanyika leo Alhamis Julai 12,2018 katika ukumbi wa Bwalo la Polisi mjini Shinyanga. 

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema suala la utii wa sheria za barabarani ni jukumu la watu wote hivyo kila mmoja lazima azingatie sheria za barabarani ili kuepuka ajali zisizo za lazima.

"Madereva ni wadau wakuu wa kuzuia ajali za barabarani, nalipongeza jeshi la polisi kwa kuona umuhimu na wadau hawa ili kuwapa elimu hii kwani madereva wakisikiliza na kufanyia kazi elimu hii hakika ajali hazitatokea mkoani Shinyanga",alieleza Matiro.

"Ili kutokomeza ajali,ni vyema jeshi la polisi likaendelea kufanya doria katika barabara kuu, kukagua leseni na kuhakikisha magari yote mabovu hayaiingii barabarani lakini pia kutoa elimu kwa wadau wote wakiwemo wanafunzi",aliongeza Matiro.

Aidha aliagiza mashimo yote katika barabara za mkoa wa Shinyanga yafukiwe huku akiwataka madereva kuacha kuwa wakimya wanapokutana na changamoto hivyo wawasiliane na viongozi wa jeshi la polisi na serikali kwa ujumla ili kutatua changamoto hizo.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule aliwataka watumiaji wa vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuepuka kuongea na simu barabarani,kuendesha kwa mwendo kasi,kutaka kupita magari bila tahadhari,kulewa na kuendesha magari mabovu.

"Tutaendelea kukamata magari yote mabovu,kukagua leseni,kufanya doria na kutoa elimu kuhusu usalama barabarani kwa makundi yote ili tutokomeze ajali mkoani Shinyanga",alisema Kamanda Haule.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua mafunzo kuhusu usalama barabarani kwa wamiliki na waendeshaji wa vyombo vya moto yaliyoandaliwa na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasisitiza waendeshaji wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za barabarani ili kutokomeza ajali mkoani Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua mafunzo hayo. Kushoto ni Afisa Mnadhimu wa polisi mkoa wa Shinyanga Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Lutufyo Mwakyusa, kulia ni Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule akieleza lengo la mafunzo ya usalama barabarani kwa madereva na wamiliki wa vyombo vya moto
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule akiwataka madereva kuacha uzembe barabarani ili kuepuka ajali barabarani
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule akisisitiza kuwa jeshi la polisi litaendelea kuwachukulia hatua za kisheria madereva watakaokiuka sheria za usalama barabarani.Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro . Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Shinyanga SSP Richard George Abwao
Madereva na wamiliki wa vyombo vya moto wakiapa kuzingatia sheria za barabarani ili kutokomeza ajali mkoani Shinyanga.
Kiapo kikiendelea....
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Anthony Gwandu akizungumza wakati wa mafunzo hayo ambapo alisema kila mmoja ana wajibu wa kutii sheria za usalama barabarani.
Wamiliki na Waendeshaji wa vyombo vya moto wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Kulia ni Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule akimuonesha Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ratiba ya mada zinazofundishwa kwa wamiliki na waendeshaji wa vyombo vya moto ikiwemo magari,pikipiki na bajaji.
Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Shinyanga SSP Richard George Abwaoakiteta jambo na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga ASP Anthony Gwandu.
Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wilaya ya Shinyanga Mkaguzi Msaidizi Emmanuel Pallangyo akitoa mada kuhusu sheria za barabarani
Madereva na wamiliki wa magari,pikipiki na bajaji wakifuatilia mada
Mafunzo yanaendelea
Dereva na mmiliki wa Tax na pikipiki, Omari Gindu akiomba askari wa usalama barabarani 'Trafiki' nao wapewe elimu ya usalama barabarani akidai baadhi yao hawajui sheria hivyo kukamata ovyo madereva na kuchangia kutokea kwa ajali
Mwendesha bodaboda Daudi Salamba akiliomba jeshi la polisi kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wadau ili kila mmoja azijue sheria za usalama barabarani
Dereva wa magari/bodaboda Jackson Masengeja akielezea kero yake juu ya baadhi ya askari polisi wanaoendesha bodaboda bila kuvaa kofia ngumu huku wao wakiwa mstari wa mbele kukamata waendesha bodaboda wasiovaa kofia ngumu. 
Mwenyekiti wa waendesha Hiace na Noah wilaya ya Shinyanga Ayub Majenga akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo
Mwenyekiti wa Kituo cha Mabasi mkoa wa Shinyanga John Mshandete akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Mwenyekiti wa waendesha bodaboda Manispaa ya Shinyanga Wenceslaus Modest akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Afisa Bima kutoka Shirika la Bima la Taifa Tanzania (NIC),Stella Paul akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya bima kwa vyombo vya usafiri. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wilaya ya Shinyanga Mkaguzi Msaidizi Emmanuel Pallangyo
Afisa Mwandamizi kutoka SUMATRA, Bahati Musiba akitoa ufafanuzi kuhusu hoja ya kuondoa baiskeli mjini Shinyanga. Alisema 'huwezi kuondoa baiskeli bila kuleta njia mbadala ni vyema magari yakianza kufanya safari mjini Shinyanga ndipo baiskeli zinaweza kutoka'
Eng. Venance Masanja kutoka TANROADS akitoa ufafanuzi kuhusu mashimo kwenye barabara kuu ya kutoka Mwanza - Shinyanga- Tabora na kueleza kuwa tayari zoezi la kuziba mashimo linaendelea.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images