Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live

ZIARA YA IGP SIRRO YAENDELEA WILAYA YA SERENGETI MKOANI MARA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akipokea zawadi ya Mbuzi iliyotolewa na Askari wa kike wa Wilaya ya Serengeti baada ya kuzungumza na Maofisa, Wakaguzi na Askari wa Wilaya hiyo wakati wa Ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kubaini changamoto za kihalifu na kuzipatia ufumbuzi. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara ACP Juma Ndaki .
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akifurahia ngoma na kikundi cha utamaduni cha Kijiji cha Rubanda Wilayani Serengeti wakati alipofika kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho wakati wa Ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kubaini changamoto za kihalifu na kuzipatia ufumbuzi. (Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Rubanda Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wakati wa Ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kubaini changamoto za kihalifu na kuzipatia ufumbuzi. (Picha na Jeshi la Polisi) 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima wakati alipofika ofisini kwake na kukutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo wakati wa Ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kubaini changamoto za kihalifu na kuzipatia ufumbuzi. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mhe. Nurdin Babu wakati alipofika ofisini kwake na kukutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo wakati wa Ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kubaini changamoto za kihalifu na kuzipatia ufumbuzi.

OLENASHA:IFIKAPO 2019 VIJIJI 35 VITAPATA UMEME WA REA NGORONGORO

$
0
0
Na.Vero Ignatus ,Ngorongoro.

Naibu Waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia ambaye pia ni mbunge wa Ngorongoro Mhe. Wiliam Olenasha amesema hadi kufikia mwaka 2019 vijiji 35 vitakuwa vimepata umeme wa REA awamu ya tatu na baadae wataendelea na maeneo mengine.

Ameyasema hayo tar 8 August 2018 katika kijiji cha Sakala alipofanya mkutano wa hadhara wa wananchi na kusema kuwa kila nyumba lazima itawaka umeme kinachotakiwa ni wananchi kuwa tayari kuupokea umeme huo.

Olenasha amesema tayari nguzo za umeme zinaendelea kupita katika maeneo mbalimbali lengo ni kuhakikisha ngorongoro inabadilika kuanzia miundombinu iliyopo mpaka mazingira yenyewe ya maisha ya watu na kuwa ngorongoro mpya.
“Wote ni mashahidi hili hatuzungumzi tena siyo hadithi nguzo tayari zinasambaa katika vijiji tunategemea ifikapo mwaka 2019 vijiji 35 vitakua vinawaka umeme”Alisema Olenasha

Wakati wanaendelea kusubiria kupata wa umeme Olenasha amewataka wananchi kuendelea kujenga nyumba zenye ubora zaidi ili mazingira yabadilike kwa kuwa Ngorongoro iliyokuwa inajulikana mwanzo kwa migogoro sasa inajulikana kwa maendeleo chanya.Wakitoa maoni yao baadhi ya wananchi wamesema kuwa kuwepo kwa umeme utawarahisishia wao kufanyashughuli za maendeleo ikiwemo kukuza kipato kwa wafanyabiashara ambao wanategemea umeme tofauti na ilivyo hivi sasa wanapata changamoto ya huduma ya matumizi ya vitu vinavyohitaji umeme.

Katika ziara Mbunge huyo ya kuwatembelea wananchi , wadau wa maendeleo pamoja na wananchi wamempongeza kwa kuendelea kutekeleza ahadi zake alizoahidi kipindi alipoomba kura ya kuchaguliwa kuliongoza jimbo hilo.Jimbo la Ngorongoro lina kata 28 Olenasha amezitembelea zote na kuzungumza na wananchi hii ikiwa ni mara yake ya nne kufanya hivyo .


Naibu waziri wa Elimu ambaye pia ni mbunge wa Ngorongoro akizungumza na wananchi.


JAFO AWAPONGEZA WILAYA YA MANYONI KWA UJENZI MZURI

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewapongeza viongozi wa wilaya ya Manyoni kwa kusimamia vyema fedha za serikali zilizowezesha kujenga vizuri sana kituo cha afya Kitinku. 

 Waziri Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayo tekelezwa chini ya ofisi ya Rais TAMISEMI.

 Jafo ameridhishwa na ujenzi wa kituo cha afya Kitimku ambacho serikali ilipeleka shilingi milioni 500 ili kufanya uboreshaji na kujenga majengo mbalimbali ikiwemo jengo la huduma za upasuaji.  Amesema kituo hicho kimekuwa mfano wa kuigwa. 

 Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amemshukuru Mbunge wa Jimbo hilo Mhe . Daniel Mtuka pamoja na Kaimu mkuu wa wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuiunganisha timu ya watendaji na wanajamii wa Manyoni.
       Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Manyoni katika wodi mpya ya akinamama kwenye Kituo cha Afya Kintinku.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akikagua jengo la upasuaji Kituo cha Afya Kintinku.
Baadhi ya majengo ya kituo cha Afya Kintinku.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akikagua chumba cha kuhifadhia maiti katika Kituo cha Afya Kintinku.
 

MARUFUKU BUTURA NA BIASHARA YA MAGENDO KATIKA KAHAWA-DKT TIZEBA

$
0
0
Na Mathias Canal-WK, Kagera

Biashara ya kuuza Kahawa nje ya nchi pasina kufuata utaratibu wa kisheria (magendo) imepigwa marufuku hivyo atakayebainika kuendelea na biashara hiyo atachukuliwa hatua Kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

Agizo hilo limehusisha pia zuio la wananchi kuuza kahawa mbichi ingali bado shambani haijakomaa (Butula) kwani kufanya hivyo ni kudhoofisha na kuzorotesha juhudi za muda mrefu alizotumia mkulima wa kahawa na kumkosesha mapato stahiki.

Marufuku hiyo imetolewa na Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba Leo 10 Julai 2018 wakati akizungumza na wadau wa zao la kahawa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isingiro Wilayani Kyerwa.

Waziri Tizeba alisema kuwa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 ambayo ndio mkataba wa wananchi na serikali yao inatoa maelekezo ya kuwezesha upatikanaji wa Masoko ya Mazao ya Kilimo kwa kuviimarisha na kuviwezesha vyama vya ushirika kuwa na uwezo wa kutafuta masoko ya mazao ya wakulima ya ndani na nje kwa kuweka mfumo madhubuti wa ukusanyaji, uchambuzi na uenezaji wa taarifa za Masoko na kutoa elimu juu ya uongezaji thamani na biashara.

Alisema serikali itajitahidi kutafuta bei nzuri ya zao la kahawa ndani na nje ya Afrika Mashariki ili wananchi wapate faida na tija ya Kilimo huku akieleza kuwa wakulima wa kahawa kote nchini hawawezi kuona mafanikio ya Kilimo hicho kwa kuendeleza biashara ya magendo sambamba na biashara ya kahawa mbichi ikiwa shambani (Butura).

Alisema kumekuwa na malalamiko mengi kwa wananchi hususani baadhi ya wakulima wa kahawa kuuza zao hilo nje ya nchi kinyume na sheria kwa hoja ya kwamba wanauza bei kubwa kuliko ndani ya nchi hivyo ili kutambua gharama zilivyo Kesho 11 Julai 2018 watakutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ushirika kutoka Uganda anayeshughulikia mambo ya ushirika ili kujua kama kweli Uganda kuna wanunuzi wenye uwezo wa kutoa kiasi kikubwa cha fedha kuliko wanunuzi wa Tanzania ili wapewe utaratibu bora wa namna ya kuja Tanzania kununua kahawa.

Aidha, waziri Tizeba ameagiza Wakulima waliouza kiasi kidogo cha kahawa wasilipwe kwa utaratibu wa benki ili kuepusha usumbufu badala yake kwa wale wakulima waliolima hekari nyingi na malipo yao yatahusisha kiasi kikubwa cha fedha walipwe kwa utaratibu wa njia ya Benki.

Aliongeza kuwa mafanikio ya Kilimo nchini hususani zao la kahawa ni lazima kuuza kupitia Vyama vya msingi vya ushirika ambapo ilani ya Chama Cha Mapinduzi sura ya pili kipengele cha 21 (n) inaeleza jinsi sheria ilivyofanyiwa marekebisho na kuanzisha sheria mpya ambayo imeanzisha tume huru ya ushirika ili kuwa na tija kwa wakulima kwa ajili ya kuwapatia faida kubwa ya kuuza kupitia ushirika.

Sambamba na hayo pia Waziri wa Kilimo Mhe Tizeba amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Ndg Shadrack Mhagama kukamilisha haraka iwezekanavyo kiwanda cha kukoboa kahawa cha Omkagando kilichozinduliwa na Mwenge wa Uhuru tangu mwaka 2016 kwa gharama za serikali lakini mpaka sasa kimeshindwa kuendekezwa.

Katika ziara hiyo Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage wametembelea na kuzungumza na viongozi wa Chama Cha Msingi cha Karukwanzi.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akieleza maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi wakati akizungumza na wadau wa zao la kahawa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isingiro Wilayani Kyerwa, Leo 10 Julai 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Wadau wa zao la kahawa wakifatilia kwa makini mkutano uliowakutanisha wadau wa zao hilo uliofanyika katika ukumbi wa Isingiro Wilayani Kyerwa, Leo 10 Julai 2018.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa zao la kahawa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isingiro Wilayani Kyerwa, Leo 10 Julai 2018. Wengine pichani kulia ni waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Mhe Salum Kijuu.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wadau wa zao la kahawa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isingiro Wilayani Kyerwa, Leo 10 Julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Tizeba wakikagua na kuzungumza na viongozi wa Chama Cha Msingi cha Karukwanzi Wilayani Kyerwa, Leo 10 Julai 2018.

DC TARIME AUNDA KIKOSI KAZI KUCHUNGUZA WALIOTAFUNA BIL 5/- ZA WANANCHI WA VIJIJI VITANO

$
0
0
Na Frankius Cleophace, Tarime 

MKUU wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara Glorious Luoga ameunda kikosi kazi kwa ajili ya kuchunguza na kukamatwa kwa watu ambao wamehusika kutafuna fedha Sh.bilioni tano ambazo ni za wananchi wa vijiji vitano.

Amevitaja vijiji hivyo ni Kewanja, Genkuru, Kerende, Nyangoto na Nyamwaga. 

Akizungumzia fedha hizo Mkuu wa Wilaya amesema zilipaswa kuingia kwenye akaunti za vijiji kutokana na mikataba iliyokuwepo baina ya vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Uchimbaji wa Dhahabu Nyamongo wilayani Tarime mkoani Mara.

Amesema lakini watu wachache wakafanya hujuma ya kujipatia fedha hizo kinyume cha sheria.Hivyo ametoa siku 14 kwa kikosi hicho kuhakikisha wote watakaotuhumiwa kutokana na sakata hilo kukamatwa mara moja huku mali zao zinazohamishika na zisizohamishika kukamatwa.

"Na wahusika wote kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu na fedha hizo lazima zirudishwe kwa ajili ya kufanya maendeleo ya wananchi."Hizi ni fedha nyingi ambazo zingeleta maendeleo ya wananchi.Nikipita wananitupia lawama kumbe fedha zipo zinaliwa na watu wachache.Siwezi kufumbia macho suala hili," Luoga.

Luoga amesema kampuni hiyo imeanza kujipatiwa fedha hizo baada ya kufoji mikataba na kusababisha kufuta mikataba ya Vijiji hivyo ya mwaka 1995 kufutwana kisha fedha hizo kuanza kulipwa na Mtu binafsi bila wananchi kunufaika .

Aidha ametoa mwito kwa jamii kuishi kwa kufuata sheria na kudaia kuwa fedha hizo zimekuwa zikitumika kuvuruga Serikali.
 Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorios Luoga akiongea na Vyomba vya habari katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.
 Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga akionyesha baadhi ya Mikataba ilikuwa ikisainiwa na kampuni ya  Keng’anyi Enterprises Limited pamoja na Mikataba ya Vijiji Vitano ukiwemo Mkataba wa Mwaka 1995.
Baadhi ya Watumishi wa serikali wakiwemo watendaji wa kata wakiwa katika kikao hicho cha Mkuu wa wilaya ya Tarime

WAZIRI LUGOLA AKABIDHIWA RASMI OFISI NA MWIGULU, ASEMA KIJITI ALICHOKABHIWA HATAANGALIA NYUMA

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema kijiti cha kuiongoza Wizara yake alichokabidhiwa na aliyekua Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Mwigulu Nchemba, atakikimbiza kwa kasi kwa kuwa yeye aliwahi kuwa mwanariadha. 
Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya makabidhiano yaliyofanyika ofisini kwake, jijini Dodoma leo, Lugola alisema amekabidhiwa kijiti cha majukumu hayo mapya atahakikisha anasonga mbele kwa kutekeleza majukumu aliyopewa na Rais John Magufuli. 

“Leo nimekabidhiwa ofisi, nimekabidhiwa dhana alizokua anatumia Daktari wa Falsafa Mwigulu, pamoja na shughuli alizokua anazifanya mpaka hapa alipofikia, pia mimi niliwahi kuwa mwanariadha, na nilikua nashiriki mbio za kupokezana kijiti, na  unapokabidhiwa kijiti, hautazami nyuma, ni kuendelea na safari,” alisema Lugola. 

Pia Waziri Lugola alisema anapenda kuwaaambia Watanzania kuwa, atafanya kazi kwa kujiamini na yale mambo ambayo alielekezwa na Mheshimiwa Rais Magufuli kuyafanyia kazi, anaahidi atayashughulikia pamoja na majukumu mengine ya kiutendaji. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Mwigulu Nchemba kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma leo. Hata hivyo, Waziri Lugola alisema aliwahi kuwa mwanariadha, hivyo atahakikisha anasonga mbele kuendelea na safari, hata angalia nyuma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akipongeza na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Mwigulu Nchemba mara baada ya kupokea taarifa ya makabidhiano kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsikiliza Katibu wa Waziri Nelson Kaminyoge, alipokua anataka kumkabidhi taarifa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Mwigulu Nchemba ilia aweze kukabidhiwa taarifa hizo. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisi ya Waziri huyo, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimuaga aliyekua Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Mwigulu Nchemba, mara baada ya kukabidhiwa taarifa kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma leo.

MKUU WA WILAYA ARUSHA AIPONGEZA SHIRIKA LA FOUNDATION FOR TOMORROW KWA KUHAMASISHA ELIMU

$
0
0

Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro aipongeza Taasisi ya Foundation For Tomorrow kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuhamasisha maswala ya elimu katika Mkoa wa Arusha awataka wadau wengine kujitokeza kuiga mfano huo' aliyasema hayo juzi katika Juma la Elimu katika shule ya msingi Levolosi jijini hapa, ambapo Taasisi hiyo iliandaa Tuzo maalumu kwa mwalimu bora(Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
Meneja wa programu ya mafunzo kwa walimu Noah Kayanda kutoka shirika la Foundation for Tomorrow akizungumza katika hafla hiyo ,iliyofanyika hivi karibuni katika shule ya Levolosi jijini hapa,ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa wameaanda Tuzo hiyo kwa shule za msingi jiji la Arusha na Meru kwa walimu 20
Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya sombetini,Caroline Kiyoja cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow
Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Sinoni,Dorice Mhina cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow
Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Levolosi,Elizabeth Minja cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow

Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Uhuru,Jane Mkomwa cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow

Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Lucky Vicent Julius Saunyi cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow
Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Daraja mbili Leah Mshana cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow
Waalimu kutoka shule za msingi jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya cheti pamoja na kiasi cha shilingi laki moja na nusu kila mmoja Tuzo hiyo maalumu iliandaliwa na shirika la Foundation For Tomorrow kwaajili ya waalimu waliobainika kufanya kazi zao kwa umahiri mkubwa


Na Pamela Mollel,Arusha

Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro ameipongeza Taasisi ya Foundation For Tomorrow kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuhamasisha maswala ya elimu katika Mkoa wa Arusha .

Aliyasema hayo juzi katika Juma la Elimu katika shule ya msingi Levolosi jijini hapa ambapo alisema shirika hilo limekuwa bega kwa bega katika kuhamasisha maswala mbalimbali ya Elimu na kuwataka wadau wengine kujitokeza kuiga mfano huo

“Foundation for Tomorrow wamekuwa mstari wa mbele sana katika maswala ya elimu mfano mzuri leo wameanda Tuzo maalumu kwa mwalimu bora ambaye amekuwa akifanya kazi zake kwa umahiri mkubwa”alisema Daqarro

Kwa upande wake Meneja wa programu ya mafunzo kwa walimu Noah Kayanda kutoka shirika la Foundation for Tomorrow akizungumza katika hafla hiyo alisema kuwa lengo la Tuzo hiyo ni kutia hamasa miongoni mwa walimu waliobainika kufanya kazi zao kwa bidii na umahiri mkubwa

Alisema kuwa katika zoezi hilo la kumsaka mwalimu bora limezingatia vigezo vyote ikiwemo uwezo wa kuhamasisha ufikiri wa kina miongoni mwa wanafunzi,uwezo wa kutengeneza mazingira ya kushiriki na mazingira rafiki ya kujifunza,uvumbuzi na ubunifu katika swala zima la ufundishaji na utekelezaji wa mtaala.ayanda aliongeza kuwa vigezo vingine ni pamoja na kujikita katika kusaidia watoto wenye changamoto za kujifunza pamoja na uzoefu wa kujifunza

Alisema kuwa katika Tuzo hiyo ya mwalimu bora kila mwalimu atapewa zawadi ya cheti pamoja na kiasi cha shilingi laki moja na nusu kila mmoja

MWENYEKITI WA CCM RAIS MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
  Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongoza Kikao cha Kamati Kuu (CC) ya CCM kilichofanyika katika Ofisi ndogo za chama  hicho Lumumba Jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli  akipiga makofi  pamoja na wajumbe wengine wa Kamati Kuu (CC) ya CCM mara baada ya kuwasili  ukumbini kwa ajili ya kuongoza Kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ndogo za chama  hicho Lumumba Jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU

JUMLA YA WAHAMIAJI HARAMU 1470 KUTOKA MATAIFA MBALIMBALI WAKAMATWA MKOANI KAGERA

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera.

JUMLA ya wahamiaji haramu 1470 kutoka mataifa mbalimbali wamekamatwa Mkoani Kagera kwa kuingia nchini kinyume cha sheria.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Ofisa uhamiaji Mkoa wa Kagera Abdallah Towo alisema kuwa kwa kipindi cha January hadi June 30 mwaka jumla ya wahamiaji haramu walikamatwa katika maeneo mbalimbali ya mipaka iliyopo Mkoani humo.

Towo alisema kuwa kati yao Warundi 994,Waganda 223,Warwanda 193,Wathiopia 19,wacongo 39 na wakenya 2 jumla yao ni 1470.

Alisema jumla ya raia 5,787 wa Burundi kutoka kambi za mtendeli,Nduta na Nyarugusu zilizopo Mkoani Kigoma pia kambi ya rumasi Ngara wamerejea nchini kwao kwa hiyari.Alisema jumla ya raia 90 kutoka Mataifa mbalimbali wamemaliza vifungo vyao katika Magereza yaliyopo mkoani Kagera na wote wamerejeshwa makwao.

"Kwa mwaka huu toka january hadi June hakuna mkimbizi yoyote aliyeingia nchini kwasababu kule kwao kwasasa kumetulia"alisema.

Ofisa Uhamiaji u huyo alisema kuwa zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya utaifa linaenda vizuri Mkoani Kagera na mpaka sasa jumla wananchi 491513 ili kupata vitambulisho vya utaifa lengo ni kuandikisha wananchi 1,200,000.

Alisema pia zoezi la uzinduzi wa hati za kusafiria za kielectronic kwa mkoa wa Kagera ulifanyika tarehe 8 mwezi wa 6 mwaka huu linaenda vizuri kwani mpaka sasa wameshapokea jumla ya maombi 72 na hati 64 zimeshatolewa na kukabidhiwa kwa wahusika.
 Ofisa wa Uhamiaji Mkoa wa Kagera Abdallah Towo akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)juu y utendaji kazi wa uhamiaji Mkoa wa Kagera
Baadhi ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Kagera wakimsikiliza Ofisa wa uhamiaji Mkoa wa Kagera Abdallah Towo ofisini kwake

OPERESHENI ENDELEVU YA UKAGUZI WA MGARI USIKU NA MCHANA ARUSHA YAPAMBA MOTO

$
0
0
Na.Vero Ignatus,Arusha.

Ni operesheni endelevu yakukagua magari na pikipiki yenye makosa mbalimbali ya usalama barabarani mkoani Arusha ambapo jumla ya magari 1719 yalikaguliwa pikipiki 182,madereva 189 walipimwa ulevi na dereva mmoja wa basi alikutwa na kilevi anashikiliwa na jeshi la polisi.

Kamanda wa polisi mkoani Arusha Ramadhani Ng'anzi amesema jumla ya makosa mbalimbali ya usalama barabarani yaliyokamatwa kuanzia tarehe 07.07 hadi 09.07.2018 ni 1901 na jumla ya tozo na notification zilizokusanywa kwa kipindi hicho ni shilingi milioni hamsini na saba na thelatini elfu.(57,030,000)

Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Joseph Bukombe amesema mabasi ya abiria 102 yalikaguliwa kati ya hayo 7 yalikutwa mabovu ambapo yalizuiliwa yasiendelee na safari sambamba na malori 129 kati ya hayo 16 yamng'olewa namba kwa ubovu ili wamiliki wa magari hayo wakayatengeneze.

Kwasababu mtu anaweza kwenda shimoni huko akarudi jionihiyo siyo issue,kari ni zima?inakiwango?dereva anayeendesha anasifa ya kuendesha!ndiyo kitu amabacho tunakitaka"alisisitiza RTO.mesema wameamua kufanya oparesheni hiyo usiku na mchana kwani madereva hao wanapaki magari mchana usiku wanayaweka barabarani kuendekea na shughuli kama kawaida.

"Tumeamua kufanya oparesheni hii mchana hayaonekani wanapaki kwahiyo usiku ndiyo tunafanya ili tuwapate " alisema Bukombe.Jumla ya pikipiki 161 zilikamatwa kwa makosa mbalimbali ya usalama barabarani na kuandikiwa faini ,leseni 365 zilikaguliwa kati ya hizo 104 zimekwisha muda wake.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Ramadhani Ng'anzi akizungumza na waandishi wa habari leo katika kituo kikuu cha polisi Arusha,aliyepo kulia kwake ni Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Arusha Joseph Bukombe.Picha na Vero Ignatus.
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Arusha Joseph Bukombe akionyesha moja ya makosa waliyoyabaini baada ya kufanya ukaguzi kwenye moja ya Lori la kubebea mizigo.Picha na Vero Ignatus.
Baadhi ya pikipiki zilizokamatwa zikiwa katika kituo kikuu cha polisi mkoani Arusha.


Haya ni baadhi ya magari ya kubebea mizigo yaliyokamatwa na makosa tofauti tofauti.Pichq na Vero Ignatus.

Mkaguzi wa Magari kutoka kikosi cha usalama barabarani akionesha jinsi ambavyo gari kwa nje linaonekana jipya lakini kwa ndani lina ubovu,kama inavyoonekana katika picha chuma kikiwa kimevungwa na mfuko wa kiroba .


Basi la Abiria kampuni ya Chakito amabalo linashikiliwa kituoni hapo kwa ubovu,taa zote haziwaki,kioo cha kuangalia usalama sitemirrow kimefungwa kwa manati pamoja na makosa mengine mengi.


RTO Arusha Joseph Bukombe akionyesha moja ya lori la mchanga ambalo halina reflector na mara nyingi yanafanya kazi usiku.Picha na Vero Ignatus.

Wakaguzi wa magari (vehicle inspectors) wakiwa katika picha ya pamoja na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Joseph Bukombe na baadhi ya waandishi wa habari.Picha na Vero Ignatus.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI, SUBIRA MGALU AZINDUA MRADI WA UMEME VIJIJINI REAIII WILAYANI KILOSA, VIJIJI 180 MKOANI MOROGORO KUNUFAIKA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, na viongozi wengine wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini REA Awamu ya Tatu (REAIII), kwenye kijiji cha Mandera Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro Julai 9, 2018. Mhe. Naibu Waziri pia alitumia fursa hiyo kusikilzia kero za wnanchi kuhusu upatikanaji umeme kwenye vijiji vyao.


NA K-VIS BLOG, MOROGORO

NAIBU Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, amezindua mradi wa usambazaji umeme vijini REA awamu ya tatu (REAIII), ambapo jumla ya vijiji 180 vya Mkoa wa Morogoro vitanufaika.
Naibu Waziri alifanya uzinduzi huo kwenye kijiji cha Mandera Wilayani Kilosa Mkoani humo Jumatatu Julai 9, 2018 kwa kukata utepe na kuwasha swichi ya umeme na hivyo kuibua shangwe, nderemo na vifijo kutoka kwa wananchi waliojawa na furaha.
Akizungumza baada ya uzinduzi huo Mhe. Naibu Waziri Subira Mgalu, alisema, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli inayo dhamira ya kweli ya kuhakikisha ahadi zote ilizotoa kuhusu upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi wote wa Tanzania mijini na vijijini inatekelezwa kwa kasi.
“Tayari umeme umefika sasa utumieni kika milifu kujiletea maendeleo yenu na taifa kwa ujumla.” Alisema Mhe. Naibu Waziri.
Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni nafuu sana kiasi cha shilinbgi Elfu Ishoirini na Saba tu (27,000) 
 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mafulu kata ya Kitete wilaya ya Kilosa wakati wa ziara yake kusikiliza kero na kuzipatia ufumbuzi kuhusiana na mradi wa umeme vijijini (REA) REA Awamu ya Tatu (REAIII) mzunguko wa tatu mkoa wa Morogoro.
 Wananchi wakimsikilzia Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, wakayti akihutubia
 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mafulu kata ya Kitete wilaya ya Kilosa
 Diwani wa kata ya Kimamba A, Upendo Mpoto akizungumza jambo mbele ya Naibu waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu wakati akisikiliza kero zinazohusiana na mradi wa umeme vijijijini.
Diwani wa Kata ya Kimamba akizungumza kwenye mkutano huo.
  Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu (Mwenye Kilemba chekundu kichwani) akimsikiliza Diwani wa kata ya Kitete wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, Bw. Stephen Lukobe wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Maful. Wakwanza kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mussa Maganga.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu kulia akizungumza jambo na Diwani wa kata ya Kitete wilaya ya Kilosa, Stephen Lukobe katika ofisi ya kijiji cha Madudu wakati wa ziara ya naibu waziri huyo ya kutembelea vijiji vitavyonufaika na mradi wa umeme wa REA Awamu ya tatu (REAIII), mzunguko wa tatu mkoa wa Morogoro Julai 9, 2018
Makzi wa kijiji cha Mandera, Wilayani Kilosa, akizungumza mbele ya Naibu Waziri

WAFANYABIASHARA WA OMAN WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUNUNUA DREAMLINER

$
0
0

*Washauri inunuliwe na ndege ya mizigo ili kusafirisha bidhaa za Tanzania


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAFANYABIASHARA wa nchini Oman wamesema wamefurahishwa na hatua ya Rais Dk.John Magufuli kununua ndege ya Dreamliner huku wakishauri inunuliwe na ndege ya mizigo itakayotumika kusafirisha bidhaa za Tanzania na nchi yao.

Mwenyekiti wa Baraza la Biashara kati ya Tanzania na Oman Seikh Saud Al Rawadhi amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa baraza ambapo wafanyabiashara wa nchi hizo mbili wamekutana kujadii fursa za kibiashara kati ya nchi hizo.

Sheikh Al Rawadhi ametumia nafasi hiyo kueleza wameona Dreamliner imetua nchini Tanzania na kwamba wafanyabiashara wa Oman wanampongeza Rais Magufuli kwa ununuzi wa ndege hiyo.

“Tunampongeza Rais Magufuli kwa kununuzi Dreamliner .Ni hatua nzuri katika kuimarisha sekta ya anga nchini.Wafanyabishara wa Oman tunaomba ipatikane na ndege ya mizigo itakayotumika kusafirisha bidhaa za Tanzania kwenda Oman,”amesema Sheikh Al Rawahi.

Kwa upande wa mgeni rasmi katika ufunguzi huo wa baraza la kibiashara Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Mwinyi amewataka wafanyabiashara nchini Tanzania kuchangamkia fursa ya kibiashara kwa kuuza bidhaa zao nchini Oman.

“Wafanyabiashara changamkieni fursa ya soko lililopo Oman wanahitaji bidhaa za aina mbalimbali kutoka kwetu.Wenzetu wana fedha lakini hawana aridhi, na huku kwetu tuna kila kitu hivyo tutumie nafasi hii kupeleka bidhaa huko.“Takwimu zinaonesha kuwa Oman wanauza bidhaa nyingi kwetu kuliko ambavyo sisi tunauza katika nchi yao.Hivyo ni wakati sasa wa kuhakikisha tunauza zaidi bidhaa zetu kwao kuliko ambavy wao watauza kwetu kwani tuna kila kitu,,”amesema Balozi Mwinyi.

Ameongeza jukumu la Serikali ni kuandaa mazingira mazuri ya kibiashara ambayo yatatoa nafasi kwa kupatikana kwa soko la kuuza bidhaa za Tanzania katika nchi mbalimbali ikiwamo ya Oman na kwamba kumekuwa na mazungumzo ambayo yamekuwa yakifanyika kwa ajili ya kuimarisha sekta ya biashara.

Wakati huo huo Balozi wa Tanzania nchini Oman Abdalah Kilima amesema kuna fursa nyingi kwa wafanyabiashara wa Tanzania kuuza bidhaa zao Oman na kufafanua asilimia zaidi ya 90 wanategemea bidhaa kutoka nje ya nchi yao.Pia ametoa mfano kuwa kilo mbili za unga nchini Oman zinauzwa Sh.17,000 na hivyo wafanyabiashara wanaweza kuona namna ya mahitaji ya unga yanayohitajia.

“Watanzania wanaweza kuuza bidhaa za aina mbalimbali Oman.Kutoka Uholanzi mpaka Oman kwa usafiri wa ndege ni saa 11 na kutoka Tanzania mpaka Oman ni saa tano hivyo unaweza kuona kwamba sisi tunaweza kufika kwa haraka Zaidi kuliko nchi zilizo mbali,”amesema Balozi Kilima.
Naibu Katibu MKuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Afrika Mashariki,Balozi Ramadhani Mwinyi akizungumza mapema jana jijini Dar kwenye mkutano wa pamoja kati ya ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Nchini Oman na Wafanyabiashara wa Tanzania , wakijumuika kwa pamoja kwenye kongamano la biashara, kwa madhumuni ya kupeana fursa za bishara zilizomo ndani ya nchi hizo mbili.

Balozi Mwinyi alisema kongamano hilo ni muhimu kwa Wafanyabiashara hasa kutoka Tanzania ambao hadi sasa hawajalitumia vyema soko lililopo nchini oman, kuuza bidhaa zao kutokana na nchi hiyo kuhitaji bidhaa nyingi kutoka nje kunakosababishwa na hali yake ya uzalishaji nchini OMAN.
Mwenyekiti wa baraza la wafanyabiashara nchini Oman,Saud Al Rawadhi akizungumza mapema jana jijini Dar kwenye mkutano wa pamoja kati ya ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Nchini Oman na Wafanyabiashara wa Tanzania , wakijumuika kwa pamoja kwenye kongamano la biashara, kwa madhumuni ya kupeana fursa za bishara zilizomo ndani ya nchi hizo mbili.

Mwenyekiti huyo amewataka Watanzania amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kufanyabiashara OMAN huku akisisitiza kuwa baraza lake litatowa msaada wa kila aina ili kuhakikisha kuwa Watanzania wanafanya biashara na Oman bila vikwazo vyovyote. 
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika Mashariki na Kati-Wizara ya Mambo ya Nje Mhe. Suleiman Saleh akizungumza mbele ya wageni waalikwa wa Kongamano la Kibiashara kati ya Tanzania na Oman,liliofayika mapema jana jijini Dar Es Salaam.Ambapo kongamano hilo lilikuwa na madhumuni ya kupeana fursa za bishara zilizomo ndani ya nchi hizo mbili.
Sehemu ya Meza Kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo wakati wa majadiliano ya Kibiashara Baina ya Tanzania na Oman kwenye kongamano la pamoja lililofanyika jana jijini Dar
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Oman wakipeana ushauri na kubadilishana ujuzi wa kibiashara 
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Oman wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya Wawakilishi kuhusiana na fursa zilizopo katika nchi zao. 
Baadhi ya Wafanyabiashara wakifuatilia mada mbalimbali za fursa zilizokuwa zikiwakilishwa ukumbini humo
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Oman wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya Wawakilishi kuhusiana na fursa zilizopo katika nchi zao. 
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Oman wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya Wawakilishi kuhusiana na fursa zilizopo katika nchi zao. 
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Oman wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya Wawakilishi kuhusiana na fursa zilizopo katika nchi zao. 
Piicha ya Pamoja mara baada ya mkutano kuhitimishwa

WAZIRI WA NISHATI AAGIZA TANESCO, REA KUANZISHA VITUO VYA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma, 

WAZIRI wa Nishati Medadi Kalemani amewagiza wasimamizi wa mradi wa umeme Vijijini (REA) pamoja na TANESCO kuanzisha madawati ya kutoa huduma na vituo vidogo kwa kila kata nchini kwa lengo l kutatua kero za wananchi na kuhakikisha ifikapo Juni 2021 kila kijiji na kila mwananchi anapata umeme.

Maagizo hayo aliyatoa jana katika Kijiji cha Rusesa wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wakati wa uzinduzi wa REA awamu ya tatu katika Vijiji 149 vya Wilaya nne za Mkoa wa Kigoma ambazo zilichelewa kupata mradi huo.

Ambapo aliwataka wasimamizi wa TANESCO na mawakala wa Umeme vijijini REA kumsimamia Mkandarasi aliekabidhiwa mradi huo mchana na usiku kuhakikisha wananchi wanapata umeme kwa wakati.

Amesema TANESCO wanatakiwa kuanzisha ofisi ndogo katika kila kata na dawati la kusikiliza kero za wananchi ,ili kuhakikisha wananchi wanaunganishiwa umeme kwa gharama ya Serikali ya Sh.27,000 bila kuibiwa na wananchi wapate eneo la kupeleka kero zao ilikuepusha kero na kuhakikisha umeme katika kata unawekwa kwenye vijiji vyote na vitongoji vyote vilivyo kusudiwa kama Serikali ya awamu ya tano ilivyo kusudia kwa kila kijiji kupata umeme .

" Fananisheni umeme huu na treni ambayo mmezoea kuipanda na kila mwananchi ataipanda treni hii ya umeme, mmechelewa kuipanda lakini mtakuwa wa kwanza kufika, nimekuja kufanya kazi kumtambhlisha kwenu mkandarasi na kutoa majukumu yake ya kazi.

" Tulikuwa hatujaanza kutekeleza mradi huu tulianza kwa sehemu ndogo katika Wilaya ya Kibondo na Kakonko leo tumekuja kupiga hodi katika Wilaya nne zilizo kuwa zimebaki,"amesema Waziri huyo. 

Amewaomba wananchi wsuitunze miundombinu hiyo itakayowekwa, kwani Serikali imetumia gharama kubwa kuwekeza katika miundombinu hiyo na ametoa mwito kwa wakandarasi kuwatumia vijana wa mkoa wa kigoma katika utekelezaji wa mradi huo kwani Rais ametoa sh. bilioni 54 kwaajili ya mradi huo kutekeleza ahadi yake aliyo ahidi wakati wa uchaguzi.

Aidha ameahidi kuuunganisha Mkoa wa Kigoma na gridi ya Taifa kutokana na maombi yaliyotolewa na wabunge wa Mkoa huo na kuwataka wasimamizi wa mradi huo kuweka umeme katika maeneo yote ya taasisi za umma pamoja na maeneo yote yaliyotengwa kwaajili ya viwanda na uwekezaji ilikuweza kuinua uchumi wa wananchi wa Mkoa wa Kigoma.

Akizungumzia Mradi huo Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa nishati Vijijini REA,Amosi Maganga amesema mradi unao zinduliwa ni mradi wa awamu ya tatu mzunguko wa kwanza, ni muendelezo wa miradi iliyo tangulia.Amesema kuwa Kigoma mradi wa Rea awamu ya tatu ulianza kwa Wilaya za Kakonko na Kibondo miezi miwili iliyopita.

Amesema mzunguko wa kwanza wa Awamu hiyo ya tatu utaanza na vijiji 80 vya Wilaya ya Buhigwe, Kasulu ,Uvinza na Kigoma Vijijini na mradi huo utapita katika vijiji 149 na Vijiji hivyo vina kamilisha idadi ya Vijiji 195 vyenye umeme kati ya Vijiji 306 Vya Mkoa mzima na 111 vimeanza kusanifiwa ili na vyenyewe vianze kupata Umeme kuanza Julai mwaka 2019 .

Awali akimkaribisha Waziri kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe na Kasulu , Brigedia Jenerali Marco Gaguti alisema kila walipo kuwa wakipita katika maeneo ya utendaji wananchi walikuwa wakiuliza umeme utafika lini, anaamini uzinduzi wa leo uwe Chachu kwa Wananchi kuanzisha viwanda na kuanzisha miradi mbalimbali.

" Katika mpango wa Kigoma ni kwenda kwa spidi ya kukimbia kuhakikisha maendeleo yanakuja Kwa kasi kubwa, tumejipanga na tunaamini kwa umeme huu tulioupata Kigoma yetu haita kuwa nyuma tena nakuanza rasmi uwekezaji na uanzishwaji wa viwanda kuunga mkono kauri mbiu ya Rais wa awamu ya tano ya serikali ya Viwanda ",amesema Brigedia Jenerali Gaguti.

Nae Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vuma Holle amesema wanakasulu wanamshukuru Rais Kwa kukamilisha baadhi ya ahadi zake alizo ahidi wakati wa kampeni ikiwa ni pamoja na umeme, huduma za Afya na barabara, kilichobaki ni huduma za maji kitu kimoja ambacho wananchi wanakisubir kwa hamu ni Maji 

Amesema umeme huo ulichelewa kutokana na mkandarasi alieomba wakwanza aligushi Nyaraka na kulikuwa na kesi inaendelea Mahakamani ambapo Waziri husika amejitahidi kutafuta wanasheria Wa serikali wazuri waliosaidia Suala hilo kuisha Kwa wakati na kuomba mradi utakapo anza Wakandarasi kufanya haraka kutekeleza mradi huo na wananchi wa Kigoma wanufaike na Mradi huo. 
WAZIRI wa Nishati Medadi Kalemani pichani kati akizindua umeme wa REA awamu ya tatu katika Vijiji 149 vya Wilaya nne za Mkoa wa Kigoma ambazo zilichelewa kupata mradi huo.Katika uzinduzi huo Waziri Kalemani amewagiza wasimamizi wa mradi wa umeme Vijijini (REA) pamoja na TANESCO kuanzisha madawati ya kutoa huduma na vituo vidogo kwa kila kata nchini kwa lengo l kutatua kero za wananchi na kuhakikisha ifikapo Juni 2021 kila kijiji na kila mwananchi anapata umeme.

POLISI KILIMANJARO WAKAGUA LESENI YA MADEREVA 2000

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro limekagua Leseni za Madereva 2182 ,madereva 13 wakibainika kutumia Leseni za madaraja yasiyoruhusu kuendesha Magari ya Abiria huku Madereva watatu wakishikiliwa kwa kosa la kuendesha gari bila ya kuwa leseni.

Katika ukaguzi huo uliofanyika kwa muda wa wiki moja katika mkoa wa Kilimanjaro ,Jeshi la Polisi pi limebaini uwepo wa madereva waliovuka umri wa kuendesha gari kwa mujibu wa sheria ambao ni miaka 60 huku likiwataka kuacha mara moja kuendelea na kazi hiyo.

Kutokana na mapungufu mbalimbali yaliyobainika kwa Madereva wa Magari ya Abiria ,Jeshi la Polisimkoa wa Kilimanjaro likatangaza kuanza mafunzo kwa Madereva wa magari ya Abiria yanayofanya safari zake ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni pamoja na maelekezo ya alama mpya za barabarani.

Akizungumza kwa niaba ya Madereva,Dereva mzoefu wa magari makubwa ,Apolonary Malya amepongeza utaratibu huo wa jeshi la Polisi kutoa mafunzo ikiwa ni sehemu ya kuwakumbusha madereva baadhi ya sheria ya usalama barabarani.

Mafunzo kwa madereva hao yameanza kutolewa katika ukumbi mdogo uliopo ofisi za kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro chini ya Mkuu wa kikosi hicho Mrakibu msaidizi wa Polisi Zauda Mohamed na maofisa wengine wa Polisi .
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP ,Hamis Issah akizungumza na madereva katika kituo kikuu cha Mabasi mjini Moshi wakati akifungua rasmi mafunzo kwa madereva hao ikiwa ni njia mojawapo ya kuwakumbusha Sheria ya Barabarani pamoja na matumizi ya Alama mpya za barabarani.  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP,Hamis Issah akiwaonesha Madereva baadhi ya Alama mpya ambazo zimeanza kutumika katika maeneo mbalimbali ya barabara. 
 Madereva wa Magari ya Abiria yanayofanya safari zake ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Kamanda wa Polisi wakati akizngumza nao katika kituo Kikuu cha Mabasi mjini Moshi. 
 Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ,ASP,Zauda Mohamed akimuonesha jambo Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,ACP,Hamis Issah wakati alipokutana na madereva wa magari ya Abiria,Kulia ni Mkuu wa Operesheni wa jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,ACP,Costantine Maganga na kushoto ni Mkuu wa operesheni wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro,Ins,Peter Mizambwa. Dereva mstaafu wa Magari makubwa ,Apolonary Malya akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo .

WATENDAJI WAKUU WA MAKAMPUNI (CEORT) MBALIMBALI WAJADILI BAJETI SERIKALI ILIYOPITISHWA BUNGENI, WARIDHISHWA NA UTENDAJI WA SERIKALI

$
0
0

Mkurugenzi wa Huduma za Kodi wa PricewaterhouseCoopers Joseph Lyimo akitoa muhtasari kwa waandishi wa habari Dar es Salaam Julai 10 2018, kuhusu maswala ya bajeti ya serikali iliyopitishwa Bungeni jijini Dodoma hivi karibuni. Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Watendaji Wakuu wa makampuni (CEORT) Sanjay Rughani. (Imeandaliwa na Robert Okanda)
Sehemu ya washiriki wa Mkutano huo wakibadilishana mawazo katika mkutano huo.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano huo wakibadilishana mawazo katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Jukwaa la Watendaji Wakuu wa makampuni (CEORT) Santina Benson akiongea kuwakaribisha washiriki wa Mkutano huo
Sehemu ya washiriki wa Mkutano huo wakifuatillia mada kwa makini.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano huo wakifuatillia mada.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano huo wakifuatillia mada kwa makini.

Sehemu ya washiriki wa Mkutano huo wakifuatillia mada kwa makini.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Watendaji wakuu wa makampuni (CEORT) Sanjay Rughani akiongea machache wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwezi wa huu wa watendaji hao.

Sehemu ya washiriki wa Mkutano huo wakijuliana hali kabla ya kuanza kwa mkutano huo.

JUISI ZA AZAM YAJA KIVINGINE 'AFRICAN FRUTI'

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bakhresa Foods and Beverages Ltd wakionyesha juisi ya African Fruti iliyokuwa ikijulikana kama Azam juisi kwenye hafla ya uzinduzi wa juisi hiyo uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akionja utamu wa juisi ya African Fruti baada ya kuzindua rasmi juisi hiyo.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa juisi ya African Fruti.
Mkuu wa Uhusiano na Masuala ya ndani wa kampuni ya Bakhresa Group, Hussein Sufian akizungumza machache kwenye hafla ya uzinduzi wa juisi ya African Fruti.
Baadhi ya wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa juisi ya African Fruti.
Baadhi ya wafanyakazi na wageni waalikwa wakifurahia juisi ya African Fruti. Kampuni ya Bakhresa Food Products Ltd imetangaza kubadili chapa za bidhaa zake za juisi za Azam zinazotamba kwenye soko nchini, kuanzia sasa zitajulikana kama ‘African Fruti’. Mabadiliko haya yanaenda sambamba na kubadilika kwa muonekano wa nje wa bidhaa hizo, isipokuwa ladha na ubora wa bidhaa hizo utabaki palepale hivyo wateja wataendelea kufurahia juisi zenye viwango vya kimataifa zinazozalishwa na kampuni ya Bakhera Food Products Ltd, kampuni tanzu ya Bakhresa Group. 

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa juisi za African Fruti, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage aliipongeza kampuni ya Bakhresa kwa kutengeneza bidhaa bora na kufikia lengo la kusafirisha bidhaa hiyo nje ya nchi. “Kwa niaba ya serikali, napenda kuipongeza kampuni ya Bakhresa Group kwa uwekezaji na ubunifu mkubwa ambao imekuwa ikiufanya katika jitihada za kukuza sekta ya viwanda nchini kwa kuzalisha bidhaa za aina mbalimbali zenye viwango na serikali itaendelea kuunga mkono jitihada zenu,” alisema Mwijage. 

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bakhresa Foods, Salim Aziz alisema, “baada ya bidhaa za juisi kufanikiwa kwenye soko kutokana na ubora wake, kampuni ikaamua kuja na mkakati utakaofanya juisi hizi zitambulike kirahisi kama bidhaa halisi za Tanzania hivyo kuzipa jina la “African Fruti”. 

 Aliongeza “Licha ya kulenga masoko ya nchi za Afrika ambako tayari tumeanza kuuza juisi zetu, hivi sasa tuko kwenye mchakato wa kusambaza bidhaa hizi katika nchi za China na Nchi za Kiarabu,” alisema Bakhresa. Kwa upande wake Mkuu wa Uhusiano na Masuala ya ndani wa kampuni ya Bakhresa Group, Hussein Sufian alisema walifikia hatua ya kubadilisha muonekano wa juisi ili kuzipa hadhi ya kimataifa, ikiwa ni namna ya kuwashukuru wateja wake ambao wengi wao ni watanzania wa kawaida kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele kuzinunua.

 “Tumetaka tuwape wateja wetu fursa ya kutumia bidhaa halisi za kitanzania zenye muonekano na hadhi ya kimataifa, vivyo hivyo, hii inadhihirisha kuwa Bakhresa imefanikiwa kujiendeleza katika sekta ya viwanda hapa nchini na ndio maana tuko kwenye mkakati wa kuuza juisi zetu nje ya Tanzania na tunaamini zinaweza kushindana kwenye soko la kimataifa,” alisema Sufian. 

Aliongeza kuwa kuptia mkakati huu wa kusafirisha juisi za ‘African Fruti’ nchi za nje, wakulima wengi zaidi wa matunda nchini wataendelea kunufaika. “Tunawashukuru wateja wetu ambao siku zote wamekuwa wakituunga mkono nasi tunawahakikishia kuwa tutaendelea kuwaletea bidhaa bora zaidi zikiwa kwenye ujazo tofauti tofauti ili kukidhi mahitaji yao,” aliongeza.

UJENZI WA VISIMA VYA ASILI KUPUNGUZA TATIZO LA MAJI NAMTUMBO

$
0
0
NA YEREMIAS NGERANGERA,NAMTUMBO.

Kata ya Namtumbo wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma imepanga kupunguza tatizo la upatikanaji wa maji safi kwa kutumia milioni 6,500,000 za awali ,kuanza kujenga visima vya asili kusaidia kupunguza tatizo la upatikanaji wa maji katika kata hiyo kwa muda mrefu.

Wakizungumza kwenye kikao cha Maendeleo ya kata hiyo mwenyekiti wa mtaa wa ushirika B bwana Zuberi Kipeleka na Ally kalonga mwenyekiti wa Mtaa wa Lusenti B katika kata hiyo,  walimshukuru Diwani wa kata hiyo Halfani Hamis Kigwenembe kwa kuibua wazo la kujenga visima vya asili ili kupunguza tatizo la upatikanaji wa maji safi katika kata hiyo.

Mtendaji wa kata ya Namtumbo Zainabu Enock Maduhu alisema kuwa walipokea shilingi 6.500,000 kutoka kwa mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kama Rejesho la asilimia 20 ya makusanyo yaliyokusanywa katika kata hiyo na kupelekwa katika mfuko mkuu wa Halmashauri hiyo.

Maduhu alidai makusanyo yaliyopatikana katika mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo asilimia 20 ya mapato yaliyokusanywa katika kata yake ndiyo yaliyosababisha kurejeshewa shilingi 6,500,000 ikiwa ni asilimia 20 ya fedha aliyokusanya katika kata yake.

Adha maduhu alisema mpaka sasa wamejenga visima 3 vya asili vilivyogharimu 180,000 mpaka 204,000 kwa kisima kimoja na visima hivyo vimeonesha kuwa na uwezo wa kuwapatia wananchi maji safi mara baada ya kukamilisha ujenzi wake.

Hata hivyo Maduhu alisema wanaendelea kujenga visima hivyo vya asili ambapo Mtaalamu kutoka idara ya maji fani ya ujenzi ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Rainery Mtengeti anashirikiana na wananchi wa mtaa husika katika kutoa mwongozo wa namna ya kujenga visima hivyo alisema Maduhu.

Asha yusuph na Hawa mohamedi wakazi wa mtaa wa Ushirika B walimpongeza diwani wa kata hiyo Halfani Kigwenembe kwa jitihada zake za kuzitaka fedha hizo kuelekeza kupunguza tatizo la upatikanaji wa maji mjini Namtumbo na sio vinginevyo.

Rainery Mtengeti mtaalamu wa ujenzi wa visima hivyo vya asili aliwataka wananchi waliojengewa visima hivyo kuvitunza kwa kuwa walinzi kwa kuzuia uharibifu wa miundombinu ya visima hivyo pamoja na kupanda miti kuzunguka visima hivyo ili kuvifanya visima hivyo viendelee kutoa maji

Diwani wa kata ya Namtumbo Halfani Hamisi Kigwenembe kwa upande wake alidai tatizo la maji katika kata yake ni kubwa hivyo fedha hiyo kidogo itapunguza tatizo hilo la maji huku akiendelea kutafuta wadau ambao wanaguswa na tatizo hilo waweze kuchangia ili waweze kuongeza kujenga visima vingi vya asili na kupunguza tatizo la uhaba wa maji katika kata yake  ya Namtumbo.

Kata ya Namtumbo ni miongoni mwa kata 21 za Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ambayo kwayo imekubwa na uhaba wa maji kutokana na kata hiyo kuwa makao makuu ya wilaya ya Namtumbo na kusababisha ongezeko kubwa la watu wanaohitaji huduma ya maji huku miundombinu ya maji katika wilaya hiyo ilikuwa ya kijiji cha Namtumbo.

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUAGANA NA MABALOZI WATATU WALIOMALIZA MUDA WAO HAPA NCHINI

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Sweden hapa nchini anayemaliza muda wake Katarina Rangnitt mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatambulisha Baadhi ya Viongozi (hawaonekani pichani ) kwa Balozi wa Sweden hapa nchini anayemaliza muda wake Katarina Rangnitt mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Sweden hapa nchini anayemaliza muda wake Katarina Rangnitt mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mchumi kutoka Ubalozi wa Sweden True Schedvin
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi Balozi wa Norway anayemaliza muda wake hapa nchini Hanne-Marie Kaarstad mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Norway anayemaliza muda wake hapa nchini Hanne-Marie Kaarstad mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Balozi wa Malawi anayemaliza muda wake hapa nchini Hawa Olga Ndilowe mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi Balozi wa Malawi anayemaliza muda wake hapa nchini Hawa Olga Ndilowe mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA ATOA MAFUNZO WA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MDOGO

$
0
0

Na Monica Laurent, Dar es salaam.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetoa mafunzo maalumu kwa watumishi wa ofisi yake ili kuwajegea uwezo wa kufanya uangalizi wa uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika tarehe 12 Agosti 2018 katika jimbo la Buyungu na kata 79.

Mafunzo hayo yamefanyika jana Julai 11, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambapo mada mbalimbali zimewasilishwa zikiwemo mada juu ya Elimu ya Maadili ya Vyama vya Siasa, Haki na wajibu wa Vyama vya Siasa, wajibu wa Msajili wa Vyama vya Siasa, matendo yanayokatazwa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi na Sheria ya Vyama vya Siasa, Umuhimu wa kujaza fomu za gharama za Uchaguzi.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi amewawataka watumishi hao kufanya kazi kwa ueledi na kwa kufuata sheria za nchi.

“ kila mmoja wetu atambue kuwa ofisi yetu imepewa dhamana kubwa ya kusimamia Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 na Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 ili kudumisha demokrasia ya vyama vingi nchini, ni wajibu wetu kufanya kazi kwa ueledi na kwa mujibu wa sheria” amesisitiza Jaji Mutungi

Naye Bi. Piencia C. Kiure mmoja wa wakufunzi katika mafunzo hayo ambaye ni Msajili Msaidizi anayeshughulika na masuala ya Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa Umma amesisitiza umuhimu wa wagombea na vyama vya Siasa kurejesha fomu za Gharama za uchaguzi zinazobainisha mapato na maksio ya kiwango cha matumizi wakati wa uteuzi,kampeni na uchaguzi ndani ya muda uliotengwa kisheria ili kuepuka ukiukwaji wa sheria ya Gharama za Uchaguzi.

Watumishi pia wamesisitizwa kuhakikisha wanavikumbusha vyama vya siasa na wagombeakunadi sera za vyama kwa kusimamia maadili ya vyama vya siasa ili kuendelea kudumisha amani ya nchi.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni taasisi yenye wajibu wa kisheria wa kufanya uangalizi wa mwenendo wa chaguzi zinazofanyika kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wagombea na vyama vya siasa vinatekeleza matakwa ya sheria kwa kuepuka vitendo ambavyo vimekatazwa na sheria hizi ili kuimarisha demokrasia ya vyama vingi.
Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis  Mutungi akionesha kitabu chenye kuelimisha uma juu ya makatazo yaliyomo katika Sheria ya Gharama za Uchaguzi wakati wa Mafunzo ya Watumishi yaliyofanyika jana Julai 11, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. Jaji Francis  Mutungi akifungua mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msajili Msaidizi anayeshughulikia Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa Umma Bi. Piencia Kiure,(Picha zote na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Msajili Msaidizi anayeshughulikia Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa ummaPiencia Kiure, akitoa mwongo zo juu ya jinsi ya fomu za gharama za uchaguzi ambazo hubainisha mapato na matumizi ya wagomea na vyama vya siasa wakati wa uchaguzi.
Mwanasheria Mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Bi. Monica Mwailolo akiwakilisha mada wakati wa mafunzo.

KIWANDA CHA SUKARI KAGERA CHAAGIZWA KUACHA URASIMU KATIKA KUUZA SUKARI WANAYOZALISHA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage wakijadili jambo wakati walipotembelea kiwanda cha Sukari Kagera wakiwa kwenye ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani humo iliyoanza Jana 10 Julai 2018, Jana 11 Julai 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK) 
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akikagua uzalishaji wa sukari wakati walipotembelea kiwanda cha Sukari Kagera wakiwa kwenye ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani humo iliyoanza Jana 10 Julai 2018, Jana 11 Julai 2018. 
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage wakikagua eneo linalo wakati walipotembelea kiwanda cha Sukari wakiwa kwenye ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani humo iliyoanza Jana 10 Julai 2018, Jana 11 Julai 2018. 


Na Mathias Canal-WK, Misenyi-Kagera

Uongozi wa kiwanda cha Sukari Kagera umeagizwa kuacha urasimu katika mfumo wa uuzaji wa Sukari wanayozalisha badala yake kuingiza mtaani kwa wingi Sukari kwa wananchi ili kuepuka kadhia ya upungufu wa huduma hiyo muhimu katika jamii.

Agizo hilo limetolewa na Mawaziri wa sekta ya Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba na waziri wa sekta ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage wakati wakizungumza na uongozi wa kiwanda hicho Jana 11 Julai 2018 walipotembela kiwanda cha Sukari wakiwa kwenye ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani humo iliyoanza Juzi 10 Julai 2018.

Mawaziri hao kwa kauli moja wametoa siku 14 kwa kiwanda hicho kuongeza kasi ya uzalishaji kutoka uzalishaji wa Sukari kwa Tani 350-360 kwa siku ili kufikia walau Tani 450 mpaka 500 kwa siku kwani kufanya hivyo wataimalisha uwezo wa Sukari kupatikana kwa wingi kwa wananchi hivyo kuondoa usumbufu wa gharama katika ununuzi wa bidhaa hiyo.

Aidha, Mawaziri hao wametoa kalipio Kali kwa uongozi wa kiwanda hicho kwa kuwa na mawakala wachache wa usambazaji wa sukari jambo ambalo linapelekea ushindani wa kibiashara kuwa mchache mbinu inayopelekea Sukari kuuzwa kwa gharama isiyokuwa rafiki kwa watumiaji.

Walisema kuwa ndani ya muda mfupi uongozi wa kiwanda hicho unapaswa kutathmini upya namna ya kuongeza Uwekezaji ili kurahisisha huduma za wananchi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 hatimaye kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ifikapo mwaka 2025.

Dkt Tizeba alisema kuwa kumekuwa na uingizaji wa Sukari kwa magendo kutoka nje ya nchi kwa sababu Viwanda vya Sukari ndani ya nchi vimefungia sukari kwenye magodaoni bila kuingiza sokoni kwa wingi kuwafikia watumiaji.

Pia, alisema kuwa wataalamu wa kiwanda cha Sukari wanapaswa kutoa elimu ya muwa kwa umma ili kuona umuhimu wa uzalishaji wa zao hilo sambamba na kushirikiana na wakulima wadogo zaidi ya 490 katika vijiji vya jirani na kiwanda hicho.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage alisema kuwa serikali inatazama namna bora zaidi ya kukuza takwimu za uzalishaji wa Sukari nchini hivyo Viwanda vya Sukari vinapaswa kuunga mkono juhudi hizo kwa kuchochea Uwekezaji ili kuongeza tija katika uzalishaji.

Pia alisisitiza kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli haitasita kuvifungia Viwanda vyote vitakavyobainika kukiuka taratibu, sheria na kanuni za nchi katika utekelezaji wa majukumu yake.
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live




Latest Images