Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

Waziri Mahiga atembelea maonesho ya 42 ya biashara ya kimataifa (Sabasaba)

$
0
0
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisaini kitabu cha wageni, alipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonesho ya 42 ya biashara ya kimataifa yanayoendea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam. 
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Bi. Mindi Kasiga Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alipotembelea banda la Wizara. 
Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akiwa katika mahojiano na wanahabari kwenye maonesho ya biashara kimataifa maarufa sabasaba yanayofanyika jijini Dar  es Salaam 

Mhe.Waziri akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara alipotembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba 
Mhe. Mahiga akisikiliza maelezo kutoka kwa watumishi wa Wizara kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa 
Mhe. Mahiga akiwa kwenye banda la kituo cha kumbi za mikutano cha kimataifa (AICC) kwenye maonesho ya biashara ya sabasaba. Mbele yake ni baadhi ya watumishi wa kituo hicho. 
Mhe. Mahiga akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa Africafe alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya sabasaba 
Mhe. Mhiga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wafanyakazi wa AccessBank alipotembelea banda la benki hiyo kwenye maonesho ya sabasaba 
Mhe. Mahiga akimsikiliza mmoja wa wawezeshaji katika banda la UN kwenye maonesho ya sabasaba 
Mhe. Mahiga akikabidhiwa zawadi ya mchoro na Bibi Hoyce Temu kutoka Kitengo cha Mawasiliano cha Umoja wa Mataifa (UN). Waziri Mahiga alitembelea banda la UN kwenye maonesho ya sabasaba na kupata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini. 
Mhe. Waziri Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa UN alipotembelea banda la taasisi hiyo kwenye maonesho ya sabasaba 
Mhe. Waziri Mahiga akipata maelezo kuhusu bidhaa kutoka kwa mjasiriamali anayeshiriki maonesho ya sabasaba 
Mhe. Mahiga akiangalia bidhaa za wajariamali 
Mhe. Mahiga akiangalia bidhaa za wajariamali 
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kupata elimu katika banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba

WARATIBU ELIMU WAISHUKURU SERIKALI

$
0
0
Waratibu elimu Kata wameishukuru serikali kwa kuwapatia pikipiki ambazo zitawawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa. 

Pikipiki hizo walizopatiwa waratibu hao ni miongoni mwa pikipiki zilizotolewa na serikali kwa waratibu elimu wa Kata zote hapa nchini zenye lengo la kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa waratibu hao.

Waratibu hao wametoa pongezi zao mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo alipokuwa akikabidhi pikipiki 17 kwa waratibu elimu wote wa wilaya hiyo ya kisarawe. Waratibu hao wamemuahidi waziri huyo kwamba watafanya makubwa katika elimu kwa kuwa pikipiki hizo zitawasaidia zoezi la uratibu wa elimu katika kata zao. 

Kwa upande wake, Waziri Jafo amewaasa waratibu hao kuzitumia pikipiki hizo kwa lengo la kupandisha taaluma katika maeneo yao. "Ikumbukwe kwamba serikali imekuwa na utaratibu wa kutoa posho ya madaraka kwa waratibu elimu kata pamoja na wakuu wa shule za msingi na serikali hapa nchini,"amesema.Amebainisha kuwa kupatikana kwa pikipiki hizo kutawezesha kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hapa nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo akizungumza na waratibu wa elimu kata ya Kisarawe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo akikabidhi pikipiki kwa waratibu kata ya Kisarawe.
Baadhi ya pikipiki za waratibu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo akikabidhi pikipiki kwa waratibu wa elimu.

CUF WATANGAZA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO KATIKA KATA 79,MAJIMBO MAWILI

$
0
0

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema hakitashiriki Uchaguzi mdogo wa marudio katika Kata 79 na majimbo mawili ambao umetengazwa kufanyika Agosti 12 mwaka huu.

Taarifa ya Naibu Mkurugenzi wa habari, Uenezi na Uhusiano na Umma Mbarala Maharagande ametoa taarifa ya kutoshiriki kwenye uchaguzi kwa vyombo vya habari na kufafanua uamuzi huo umetokana na Kamati ya Utendaji baada ya kufanya uchambuzi na tathimini ya kina kuhusu tangazo la kufanyika uchaguzi huo.

Maragande ambaye yeye anatoka CUF ya upande wa Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Ahmad amesema sababu za msingi za kutoshiriki katika uchaguzi huo ni nyingi moja wapo ikiwa ni mgawanyiko wa uongozi Katika uchaguzi huo uliojitokeza kutokana na mgogoro aliodai umepandakizwa na Profesa Ibrahim Lipumba na Washiriki wake

Hivyo amesema CUF unaona ni ishara kwa sasa kuelekeza nguvu na rasilimali zake chache zilizopo katika kushughulika na kupata ufumbuzi wa mgogoro uliopo.
Ameongeza kuwa CUF inatoa mwito kwa vyama rafiki vyote katika UKAWA kukaa pamoja kufikia muafaka na maridhiano na kusimamisha wagombea bora, imara, na madhubuti kugombea nafasi hizo zote.

"CUF inatoa mwito kwa viongozi na wanachama wake wote katika maeneo yote ya marejeo ya uchaguzi kwa Tanzania Bara kushirikiana bega kwa bega na kuunganisha nguvu za pamoja na vyama rafiki vya UKAWA katika uchaguzi huu ili kuishinda CCM,"amesema.

Maharagande amesema katikankata 79 zilizotangazwa, CUF imepoteza Kata 4 ilizokuwa inaziongoza kwa madiwani wake ambao waliamua kwenda CCM. Kata mbili zipo manispaa ya Jiji la Tanga Mjini na Kata moja Mtwara Vijijini na Diwani mmoja Kufariki (Wilaya ya Kwimba).

Kutokana na vigezo vya kitaalamu na kitakwimu na ramani ya maeneo utakapofanyika uchaguzi huo wa marudio CUF ingeweza kushiriki kikamilifu katika Kata za mkakati 11 pekee.

Na kwamba Kata zingine CUF ingelazimika kuunganisha nguvu na vyama vingine katika UKAWA."Huu ndio msimamo wa CUF unaozingatia maslahi mapema ya chama unaopaswa kuheshimiwa na kila mwanaCUF wa ukweli,"amesema.

Kuhusu uchaguzi Jimbo la Jang'ombe visiwani zanzibar unatarajia kufanyika Oktoba 17 Maharagande amesema CUF ilishaweka msimamo wake hakitashiriki uchaguzi huo ambapo ametoa sababu mbalimbali ambazo wanaamini ndio msimamo wao.

Time ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)imetangaza kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika Jimbo la Buyungu, mkoani Kigoma ambalo lilikuwa linaongozwa na Mbunge wa Chadema aliyefariki dunia hivi karibuni na kwenye Kata 79 za Tanzania Bara.

Hivyo uchaguzi huo mdogo utafanyika ndani ya halmashauri 43 zilizopo kwenye mikoa 24 ya Tanzania Bara.Mikoa hiyo ni pamoja na, Kigoma, Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Lindi, Manyara, Mara, Mbeya, Mtwara, Morogoro, Mwanza, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Simiyu, Singida, Songwe, Tabora na Tanga.

Kwa upande wa Halmashauri zitakazokuwa na Uchaguzi ni Moshi, Ruangwa, Mbulu, Hanang, Babati, Serengeti, Tarime, Kyela, Mtwara, Newala, Kilombero, Kilosa, Kwimba, Makete, Wanging’ombe na Kalambo.

Pia Songea, Msalala, Meatu, Singida, Songwe, Tunduma, Tabora, Nzega, Urambo, Tanga, Karatu, Longido, Arusha, Ngorongoro, Monduli, Meru, Ubungo, Kondoa, Mpwapwa, Chamwino, Iringa, Kyerwa, Misenyi, Muleba, Nsimbo, Kasulu na Same.

Wilaya ya Siha yapiga hatua kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele

$
0
0
 Afisa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika Mpango wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Hope Rusibamayila akishirikiana na wanafunzi kutoka Shule ya Msingi ya Kilari iliyo katika Wilaya ya Siha katika Mkoa wa Kilimanjaro kutoa maelekezo kwa wawakilishi kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund namna ya Kibuyu Chirizi kikifanya kazi ya kuosha mikono kwa sabuni baada yakutoka Chooni.
 Wawakilishi kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund wakiendelea na ziara yao yakukagua baadhi ya miundombinu waliyoisaidia katika Shule ya Msingi ya Kilari iliyo katika Wilaya ya Siha katika Mkoa wa Kilimanjaro. 
 Picha ya Pamoja ya Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Kilari wakionesha kalamu zao juu kuonesha furaha zao baada ya kupokea kutoka katika Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund
 Mwanafunzi Kutoka Shule ya Msingi ya Kilari Vaileth Wilfred akimkabidhi ujumbe Afisa Elimu Wilaya ya Siha Rose Sandi baada ya kumaliza Shairi lao, kulia kwake ni  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Siha Dkt. Endrew Method na wa mwisho ni Afisa Mipango wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutoka Wizara ya Afya Bw. Oscar Kaitaba.

 Picha yapamoja ya Watumishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Wageni kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund baada ya kumaliza shughuli ya kutembelea na kukagua miundombinu katika Shule ya Msingi Kilari wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro.

GAVANA PROFESA LUOGA ATEMBELEA BANDA LA (BOT) MAONESHO YA SABASABA

$
0
0


Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Frolens Luoga akisaini kitabu cha wageni jana wakati alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania viwanja vya maonesho ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Kulia ni Beatrce Ollotu Afisa Uhusiano BOT.????????????????????????????????????
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Frolens Luoga akisikiliza maelezo kutoka kwa Naibu Gavana wa Benki Kuu Usimamizili Sekta ya Fedha Dk. Yohana Kibese wakati alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya Sabasaba jana jjini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Frolens Luoga akieleza jambo wakati akitembelea banda hilo huku Naibu Gavana wa Benki Kuu Usimamizili Sekta ya Fedha Dk. Yohana Kibese akifurahia.
????????????????????????????????????
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Frolens Luoga akiangalia na kulinganisha noti halisi ya shilingi elfu kumi na noti bandia wakati akitembelea katika banda hilo na kupata maelezo namna wanavyotambua noti bandia kushoto ni Naibu Gavana wa Benki Kuu Usimamizili Sekta ya Fedha Dk. Yohana Kibese akifurahia na kulia ni Patrick Fata Ofisa wa Benki.
????????????????????????????????????
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Frolens Luoga akiongozana na Naibu Gavana wa Benki Kuu Usimamizili Sekta ya Fedha Dk. Yohana Kibese wa pili kutoka kulia na Dk. Yamungu Kayandabila Naibu Gavana Sera ya Fedha na Uchumi wakimsikiliza Afisa Uhusiano Mkuu kutoka Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki kulia ni Lusajo Mwankemwa Mchumi wa BOT.
????????????????????????????????????
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Frolens Luoga akipata maelezo kutoka kwa Boniventura Mlamka Mchumi wa BOT wakati akitembelea banda hilo.
????????????????????????????????????
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Frolens Luoga akiangalia moja ya kijarida kinachoelezea shughuli za Benki Kuu wakati akipata maelezo kutoka kwa Revelian Felix Meneja Masoko ya Ndani BOT, Katikati ni Dk. Yamungu Kayandabila Naibu Gavana Sera ya Fedha na Uchumi.
????????????????????????????????????
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Frolens Luoga akitoa maagizo kwa James Masoy Meneja Usimamizi na Sera BOT.
????????????????????????????????????
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Frolens Luoga akizungumza jambo na Kenedy Nyoni Mkurugenzi Usimamizi wa Mabenki wa pili kulia ni Mecky Katyale Meneja Msaidizi.
????????????????????????????????????
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Frolens Luoga , Naibu Gavana wa Benki Kuu Usimamizili Sekta ya Fedha Dk. Yohana Kibesena Dk. Yamungu Kayandabila Naibu Gavana Sera ya Fedha na Uchumi wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa BOT wanaoshiriki katika maonesho ya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelea banda la benki hiyo.

KAMPUNI YA KUFANYA MATENGENEZO YA UMEME BILA KUUKATA YATUA DODOMA

$
0
0

NA Said Mwishehe Blogu ya Jamii

UAMUZI wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya utawala madhubuti wa Rais Dk.John Magufuli umesababisha Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Afrique Live Power Line Maintenance T&D Ltd Donald Mwakamele kuamua kuirudisha kampuni yake iliyokuwa nchini Botswana na kuihamishia makao makuu ya nchini Dodoma.

Mwakamele ni mtaalam wa kimataifa wa kufanya matengenezo ya umeme bila kuuzima kupitia teknolojia hiyo imemfanya awe maarufu katika nchini mbalimbali barani Afrika lakini sasa anasema uongozi wa Rais Dk.Magufuli umemfanya arudi nchini na lengo lake kubwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kuelekea uchumi wa kati na ujenzi wa Tanzania ya viwanda.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalumu na Michuzi Blog Mwakemele amesema kilichosababisha arudishe mitambo yake ya kufanya matengenezo ya kuunganisha umeme bila kuuzima umetokana na namna ambavyo Rais Magufuli ameonesha dhamira ya dhati ya kuwainua Watanzania kiuchumi.

Amesema Rais Magufuli ameonesha namna ambavyo anataka kuona nchi yetu inapiga hatua na hivyo ameamua kuja na kauli mbiu ya viwanda , hivyo kwa kutumia taaluma yake ameamua kurudi nchini ili kuhakikisha wawekezaji hawapati nafasi ya kushuhudia umeme ukikatika kwani anao utaalam ambao ukitumika hakuna siku ambayo umeme utakatika.

“Nimekuwa nchini Botswana kwa miaka sita sasa na nikiwa huko nilikuwa nafanya kazi na Shirika la Umeme la nchi hiyo ambalo linafahamika kama BPC.

“Kazi yangu kubwa ilikuwa kufanya matengenezo ya umeme bila kuukata.Pia nilipewa jukumu la kuwasomesha wataalam wao kutumia teknolojia hii ambayo inafahamika kama Live Power Maintenance,”amesema.Amesema akiwa nchini huko amepata nafasi ya kusikiliza hotuba za Rais Magufuli na kuibaini dhamira njema aliyonayo katika kuleta maendeleo ya Taifa letu.Hivyo ameamua kuirejesha mitambo na kampuni yake nchini ili ashiriki kikamilifu kuunga mkono jitihada za Rais.

“Tunapozungumzia ujenzi wa viwanda maana yake ni moja tu lazima kuwepo na umeme wa uhakika.Rais Magufuli amekuwa akizungumzia namna ambavyo Serikali yake ilivyo na nia thabiti ya kutatua changamoto ya kukatika kwa umeme na anataka uwepo wa uhakika.

“Hivyo unapozungumzia suala la umeme hilo ndilo eneo langu na ninao utaalam wa hata umeme ukileta hitilafu katika eneo fulani basi nitatengeneza bila kuzima umeme.Teknolojia ambayo inatumiwa na wengi kukiwa na matengenezo ya umeme basi unakatwa umeme kwanza halafu ndio yanafanyika matengenezo na wakati huo kunakuwa hakuna umeme.

“Kwa maana hiyo ni vema utaalam huu sasa nikauleta nyumbani ili kuondoa changamoto hiyo. Natambua kazi nzuri inayofanywa na Tanesco kwa kuhakikisha umeme unapatikana wakati wote hivyo kurudi kwangu nyumbani nategemea zaidi ushirikiano wao katika katimiza kile ambacho nimekipanga kama sehemu ya kutoa mchango wangu kwa Taifa letu,”amesema .

Ameongeza sehemu ya mitambo hiyo tayari ameanza kuileta mkoani Dodoma na kwamba gari linalobeba mtambo wa kisasa limeshapiga kambi mkoani humo.Gari hilo mbali ya kuwa na mitambo pia kuna eneo maalum linalotumika kama darasa la kufundishia teknolojia hiyo.

“Kampuni ya Afrique Live Power Line T& D Ltd itakuwa Dodoma ambako ndiko Makao makuu ya nchini yetu.Jukumu langu kubwa litakuwa ni kuhakikisha umeme haukatiki na kwa kuwa tunalo shirika la umeme madhubuti basi kila kitu kitakwenda sawa.

“Pia nimeamua kuweka kampuni Dodoma kutokana na kutambua umuhimu wa mkoa huo ambao ndiko shughuli za Serikali zimehamia huko.Hivyo kwa kutumia utaalam wangu wa kufanya matengenezo ya umeme bila kuukata iwe sehemu ya kufanikisha mkoa huo umeme kutokatika hata sekunde wakati wa matengenezo ya umeme aidha nguzo imekatika au vinginevyo’amesema.

Amefafanua Rais Magufuli anapozungumzia kukuza uchumi na kujenga viwanda maana yake anazungumzia watu kufanya kazi na hivyo naye ameamua kurejea nchini kushiriki kwenye ujenzi wa uchumi na bila umeme wa uhakika maendeleo nayo yanaweza kuchelewa.

Mwakamele ambaye amekuwa na kampuni hiyo kwa muda mrefu nchini aliamua kuihamishia nchini Botswana kutokana na makubaliano aliyokuwa ameingia na shirika la umeme la nchini hiyo lakini haoni sababu ya kuendelea kubaki huko wakati anaona sasa ni wakati sahihi wa teknolojia yake kutumika kwa maslahi ya Watanzania.
 Mataifa Mengi yaliyoendelea katika masuala ya viwanda yanaitumia sana teknolojia hiyo kama wanavyoonekana katika picha hii.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Afrique Live Power Line Maintenance T&D Ltd Donald Mwakamele kulia akiwapa maelezo  wataalam kutoka nchini Kenya ambao walijifunza teknolojia hiyo kwake Morogoro  na sasa wanaitumia nchini mwao.
 Gari Maalum la Mitambo ya kurekebisha umeme bila kuzima ambalo limewasili mkoani Dodoma tayari kwa kazi hiyo.
Gari hili pia ina eneo maalum linalotumika kama darasa kwa wananfunzi lilikwa na vifaa mbalimbali vya kufanyika kazi hiyo.

Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete atembelea banda la Nssf maonesho ya saba saba

$
0
0

Rais wa awamu ya nne Mh Dkt Jakaya Kikwete akipata maelezo kuhusiana na huduma mbali mbali zinazofanywa na Shirika la Taifa ya Hifadhi ya jamii NSSF kutoka kwa Kaimu Meneja uhusiano na masoko Bwana Salim Khalfan ,pembeni yake ni Mkurugenzi wa mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania Tan Trade, Edwin Rutegaruka mara baada ya kutembelea katika banda la NSSF kwenye maonesho ya 42 Biashara ya Kimataifa kwenye viwanja vya sabasaba,jijini Dar

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji atoa wito kwa taasisi za umma kuunganishwa kwenye mfumo wa ununuzi wa umma

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amewahamasisha wanyabiashara na wazabuni kutembelea banda la Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma – PPRA lililopo ndani ya banda la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye viwanja vya Sabsaba ili kuelimishwa kuhusu Mfumo mpya wa ununuzi wa Umma kwa njia ya Mtandao (Tanzania National e-Procurement System – TANePS) pamoja na kujisajili kwenye mfumo huo. 

Dkt. Kijaji alitoa wito wakati alipotembelea banda la PPRA na kupatiwa maelezo kuhusu mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na namna mfumo huo unavyofanya kazi. Amesema dhamira ya Serikali ni kuondoa malalamiko kwenye manunuzi ya Umma kwa upande wa wazabuni na Umma kwa ujumla kwa kuhakikisha michakato yake inafanyika kwa uwazi na ushindani ili mwisho wa siku ipate thamani halisi ya fedha inayotumika kwenye manunuzi. 

Pia ametoa wito kwa PPRA kuhakikisha taasisi zote za Umma zinaunganishwa kwenye mfumo huo mapema iwezekanavyo.Kwa upande wake Mtaalamu wa Mifumo ya Habari wa PPRA Bi. Giftness David alisema, kwa kuanza, mfumo wa TANePS umeanza kutumiwa na taasisi za Umma mia moja kwa ajili ya manunuzi ya dawa, vifaa tiba, bidhaa na huduma mtambuka. Ameongeza kwamba, kwa wakati huu, PPRA imetoa kipao mbele katika kutoa mafunzo kwa watoa huduma (wazabuni) na taasisi nunuzi kuhusu matumizi ya mfumo huo. 

TANePS ni mfumo ulioandaliwa na PPRA ili kukidhi matakwa ya sheria ya ununuzi wa Umma, na unawezesha mchakato mzima wa ununuzi wa bidhaa, vifaa, huduma na kazi za ujenzi kufanyika kwa njia ya mtandao (kielektroniki).
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la PPRA
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akipata maelezo kuhusu shughuli zinazotekelezwa na PPRA kutoka kwa Mtaalam wa Mifumo ya Habari wa Mamlaka hiyo Bi. Giftnes David
Mmoja wa wafanyabiashara walojitokeza kusajiliwa kwenye mfumo wa TANePS akielekezwa namna ya kujisajili na Mtaalam wa Mifumo wa PPRA Bi. Giftnes David
Baadhi ya watumishi wa PPRA wakifurahia matunda ya kazi wanazofanya kwenye banda la Mamlaka hiyo katika viwanja vya Sabasaba

WAZIRI MKUU AKEMEA MAAFISA USHIRIKA WENYE VISINGIZIO

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekemea tabia ya kutowajibika miongoni mwa watumishi kwa kisingizio cha mgawanyo wa madaraka.

Ametoa onyo hilo jana (Jumamosi, Julai 7, 2018) wakati akizungumza na wanaushirika na mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha, jijini humo.


Amesema kuna maafisa ushirika ambao hawataki kuwajibika kwa sababu wameajiriwa TAMISEMI na wengine wako chini ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika."Afisa Ushirika wa Wilaya yuko mkoani ambako ni chini ya TAMISEMI, Mrajis Msaidizi wa Mkoa yuko Wizarani. Serikali ni moja, kwa hiyo wote bado mnawajibika kwa Mrajis Msaidizi wa Mkoa," alisema.

Aliwataka Wakurugenzi wa Halmashauri (DED) wasiwapangie kazi nyingine zilizo nje na taaluma yao maafisa ushirika wa wilaya na wahakikishe wanatoa taarifa kwenye vikao vya Halmashauri zao.

"Msimpe kazi ya kufundisha Afisa Ushirika kwa sababu hakuna mtu mwingine. Afisa Ushirika aachwe afanye kazi ya ushirika na atoe taarifa kwenye vikao vyenu. Madiwani mnapokutana kwenye Baraza, mpeni nafasi Afisa Ushirika aeleze maendeleo ya ushirika yakoje katika wilaya yenu."

Alisema changamoto nyingine zinazoikabili sekta ya ushirika ni wizi na ubadhirifu miongoni mwa watendaji wa vyama vya ushirika waliopewa dhamana ya kuvisimamia na kuviendesha vyama hivyo.Alisema changamoto nyingine ni ukosefu wa elimu ya kutosha ya ushirika miongoni mwa wanachama, viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika; kuporomoka kwa imani ya ushirika miongoni mwa jamii na kwa baadhi ya wanachama kutokana na vyama vya ushirika kushindwa kukidhi mahitaji ya wanachama wake.

Nyingine ni uwepo wa madeni makubwa katika baadhi ya vyama vya ushirika nchini na baadhi ya viongozi wa kisiasa na wafanyabiashara kuwa na mtazamo hasi kwenye ushirika kwa malengo ya upotoshaji kwa maslahi yao binafsi. Ili kukabiliana na changamoto hizo, Waziri Mkuu aliitaka Tume ya Maendeleo ya Ushirika ihakikishe kwamba usimamizi, udhibiti, uhamasishaji wa vyama vya ushirika unafanyika kikamilifu na kwa wakati kwa kuzingatia Sheria ya Ushirika namba 6 ya mwaka 2013 na kanuni zake za mwaka 2015.

Pia aliiagiza Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika iwasaidie wanaushirika katika mchakato wa urasimishaji wa mali zao na utoaji wa hati miliki za kimila za kumiliki ardhi kwa wakulima wadogo wadogo vijijini ili waweze kuzitumia kama dhamana ya kukopa mikopo katika taasisi za kifedha kwa ajili ya kilimo na shughuli nyingine za kiuchumi. 

Aidha alizitaka mamlaka zote zinazohusika na maendeleo ya sekta ya ushirika nchini zijiwekee malengo yanayotekelezeka ya kusukuma gurudumu la maendeleo ya ushirika na kujipima kila inapohitajika.

Siku ya Ushirika Duniani huadhimishwa Jumamosi ya kwanza ya Julai kila mwaka. Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni: “Ushirika kwa ulaji wa uzalishaji endelevu wa bidhaa na huduma.” 


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JULAI 8, 2018.

NHIF YATOA MIFUKO 245 YA SARUJI KUSAIDIA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA

$
0
0
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akimkabidhi mifuko ya saruji 245 Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza ambayo ilitolewa na mfuko huu kuunga mkono juhudi hizo kushoto ni Mhasibu wa NHIF Tanga Hellena Manyanda na katikati aliyevaa kilemba ni Afisa Matekelezo wa Mfuko huo mkoani Tanga Sophia Kaku
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akimkabidhi mifuko ya saruji 245 Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza Julius Mgeni kushoto wanaoshuhudia ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu katikati kushoto ni Mhasibu wa NHIF Tanga Hellena Manyanga na kulia ni Afisa Matekelezo wa Mfuko huo Sophia Kaku.
 Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akiteta jambo na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Tanga Ally Mwakababu katikati 
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Tanga Ally Mwakababu katika akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia 
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Tanga Ally Mwakababu kulia akifurahia jambo na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo mara baada ya mazungumzo
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Tanga Ally Mwakababu kushoto akiwa na Afisa Matekelezo wa Mfuko huo Sophia Kaku katikati na Mhasibu wa Mfuko huo kulia Hellena Manyanda wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo 
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga Ally Mwakababu kulia akiagana na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo mara baada ya kumaliza mazungumzo na makabidhiano ya Saruji hiyo 



MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF)umekabidhi mifuko 245 ya saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza inayojengwa eneo la Lusanga ambayo itaondoa changamoto ambazo walikuwa wakikumbana nazo wananchi.

Makabidhiano hayo yalifanyika juzi wilayani Muheza na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga Ally Mwakababu kwa Mkuu wa wilaya hiyo Mhandisi Mwanasha Tumbo ambapo mifuko hiyo itasaidia ujenzi huo

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo wa saruji,Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha aliushukuru mfuko huo kwa kuona umuhimu kusaidia juhudi walizoanzishwa za ujenzi wa hospitali hiyo ili kuwapunguzia adha wananchi ikiwemo kuunga mkono jitihada za harambee iliyoendshwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu.

Alisema msaada huo umefika wakati muafaka wakiwa kwenye harakati za kuendelea na ujenzi wa hospitali hiyo ambao ni muhimu kwa ustawi wa wakazi wa wilaya hiyo katika kuhakikisha wanakuwa nayo ili iweze
kuwahudumia.

Mkuu huyo wa wilaya alisema ujenzi wa hospitali hiyo ambao utagharimu bilioni 11 mpaka itakapo kamilika lakini hatua iliyopo kwa harambee walioifanya Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu waliweze kupata bilioni 1.7.

Alisema na michango mingine tayari walikwisha kukusanya milioni 100 zinawawezesha kuendelea na ujenzi ambapo fedha hizo zilizokusanywa sambamba na vifaa pamoja na ahadi zitakawawezesha kukamilisha majengo mawili ya ikiwamo wodi za wazazi na watoto ambao tayari wameanza ujenzi wake unaendelea.

“Lakini wapo ambao walitoa vifaa mbalimbali ikiwemo Milango,Saruji,Matofali na Mabati jambo ambalo limetupa nguvu kubwa kuendelea na shughuli za ujenzi kwa lengo la kuhakikisha hospitali hiyo inakamilika na kuweza kuwahudumia wananchi “Alisema DC Mwanasha.

Aidha alisema wanaishukuuru pia serikali kwakutupangia bajeti ya mwaka huu ya fedha kiasi cha sh.bilioni 1.5 hivyo tuna uhakika wa kujenga majengo maengine na kuwawezesha ujenzi wake kwenda kasi na ubora
unaotakiwa.

Hata hivyo alisema katika harambee hiyo ambayo iliongozwa na Makamu wa Rais wapo wadau ambao walihudhuria wamesaidi kusaini nao mkataba wa sh.milioni 100 na wanategemea kuchimba kisima na ujenzi wake utaanza baada ya mvua kupungua.

Naye kwa upande wake Meneja wa Mfuko huo mkoani Tanga Ally Mwakababu akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo alisema wameamua kuchangia ujenzi huo ikiwa ni kama sehemu ya kuunga mkono jitihada zilizoanzishwa.

Alisema wao kama taasisi wapo tayari kuona juhudi zilizoanzishwa kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto mbalimbali kwenye huduma za afya ili waweze kutekeleza vema majukumu yao ya kila siku ya
kujiletee maendeleo.

WAZIRI JAFO AKABIDHI PIKIPIKI 17 KWA WARATIBU WA ELIMU KATA HALMASHAURI WILAYA YA KISARAWE MKOA WA PWANI

$
0
0

VICTOR MASANGU, KISARAWE

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Raisi Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh. Seleman Jafo amewataka waratibu wa elimu kata kuachana kabisa na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na uzembe na badala yake watimize majukumu yao ipasasavyo bila ya kutegeana kwa lengo la kuweza kuongeza kasi ya kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo wakati wa halfa ya kukabidhi pikipiki 17 kwa waratibu wa elimu kata katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa lengo la kuweza kuwawezesha vizuri usafiri kwa ajili ya kuweza kusimamia na kuboresha sekta ya elimu katika maeneo mbali mbali hususn vijijini.

Pia Jafo amewaagiza maafisa elimu wote kuhakikisha wanaweka mipango endelevu ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi, ambapo pia ametoa onyo kali kwa waratibu hao ambao watazitumia pikipiki hizo kwa kufanyia shughuli nyingine kwa maslahi yao binasfi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Kisarawe Hamisi Dikupatile amemshukuru Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kuamua kutoa pikipiki hizo 17 ambazo zitaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa waratibu wa elimu kata ambao hapo awali walikuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kuwepo kwa changamoto ya kusafiri umbari mrefu kwenda katika vituo vyao vya kazi.

Naye Afisa elimu wa Wilaya ya Kisarawe Shomari Bane aliahidi kulisimamia kwa hali na mali suala la usimamizi kwa waratbu wote wa kata kwa ajili ya kuweza kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu kwa kuweza kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule ya msingi pamoja na sekondari na kuondokana na changamoto ya kushuka kwa elimu.

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe iliyopo Mkoa wa Pwani kwa kipindi cha muda mrefu imekuwa ikibabiliwa na changamoto kubwa ya kufanya vibaya katika sekta ya elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na kupekekea kuzindua kampeni maalumu kwa ajili kuweza kutokomeza divisheni ziro.
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Raisi Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh. Seleman Jafo akiwasha moja ya pikipiki kati ya 17 ambazo zimetolewa na serikali ya awamu ya tano kwa ajili ya kuwapatia waratibu elimu wa kata katika halmashauri ya Kisarawe,Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuweza kuongeza ufanisi katika sekta ya elimu na kuongeza ufaulu.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Raisi Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh. Seleman Jafo akiendesha moja ya pikipiki kati ya 17 ambazo zimetolewa na serikali ya awamu ya tano kwa ajili ya kuwapatia waratibu elimu wa kata katika halmashauri ya Kisarawe,Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuweza kuongeza ufanisi katika sekta ya elimu na kuongeza ufaulu.
Waziri wan chi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Seleman Jafo akimkabidhi funguo mmoja wa waratibu wa elimu kata wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, ambao wamepatiwa pikipiki 17 kwa ajili ya kusimamia sekta ya elimu.(NA VICTOR MASANGU)

WAZIRI KIGWANGALLA AWASIMAMISHA KAZI MAOFISA NA ASKARI WOTE 27 WA TAWA KATIKA PORI LA AKIBA UWANDA

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, akimsikiliza mkazi wa kijiji cha Kilyamatundu, Shija Imeli (kulia) alipokuwa akiwasilisha malalamiko yake kuhusu tuhumu za kuwapa rushwa ya shilingi milioni 5.8 Askari watano wa Wanyamapori wa Pori la Akiaba Uwanda (pichani) ili alishe mifugo yake kwa kipindi cha miezi mitano ndani ya pori hilo.


Na Hamza Temba, Rukwa
.......................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewasimamisha kazi Maofisa na Askari Wanyamapori wote 27 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA katika Pori la Akiba Uwanda akiwemo Kaimu Meneja, Lackson Mwamezi kwa kushindwa kusimamia vizuri pori hilo na kutuhumiwa kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku tatu tangu amsimamishe kazi meneja wa Pori hilo, Mark Chuwa kwa tuhuma kama hizo pamoja na tuhuma nyingine ikiwemo kushindwa kuondoa ngo'mbe zaidi ya 12,000 ambao wamedaiwa kuwepo ndani ya pori hilo.

Pori la Akiba Uwanda lipo katika bonde la ziwa Rukwa katika wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa na linasimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).

Dk. Kigwangalla amefanya uamuzi huo jana alipotembelea pori hilo sambamba na kufanya mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kilyamatundu ambapo alipokea taarifa ya malalamiko kuhusu askari hao kupokea rushwa kutoka kwa watu wenye uwezo na kuwaruhusu kuchunga hifadhini huku wakiwanyanyasa masikini kwa kukamata mifugo yao.

Alifafanua tuhuma hizo kuwa ni pamoja na kudaiwa kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa wavuvi wanaovua samaki Ziwa Rukwa kwa kuwatozwa kila mmoja Sh. 100,000/- kwa mwezi na kuruhusu mifugo kuchungwa hifadhini kwa kipindi cha miezi mitatu ambapo kila mfugaji hutozwa kati ya Shilingi milioni sita hadi saba.

Dk. Kigwangalla pia ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru kuchunguza mali na tuhuma za rushwa walizopewa askari wote wa pori hilo wakiwemo watano waliotuhumiwa kwenye mkutano wa hadhara kwa kuomba rushwa ya shilingi milioni 6 kwa ndugu Shija Imeli ili wamruhusu kulisha mifugo yake hifadhini kwa muda wa miezi mitano.

Shija alisema mnamo tarehe 05 Januari mwaka huu akiwa nyumbani kwake na Ndugu Shemen Kuzenza, askari watano wa pori hilo walifika nyumbani kwake na kumtishia kuwa endapo atalisha mifugo hifadhini wangemkamata huku wakijua hana sehemu nyingine ya malisho hivyo wakamtaka kutoa rushwa ya shilingi milioni 6 ili aruhusiwe kulisha mifugo yake hifadhini kwa muda wa miezi mitano.

Alisema walifanikiwa kuwapa askari hao jumla ya shilingi mil. 5.8 kwa nyakati tofauti na kwamba walivyoshindwa kumalizia laki 2 zilizobakia askari hao walikamata mifugo yao nje ya eneo la hifadhi.

Kufuatia malalamiko na tuhuma hizo, Dk. Kigwangalla aliitisha gwaride la utambuzi lililohusisha askari wa Jeshi la Wananachi wa Tanzania (JWTZ), askari wa usalama barabarani na maofisa na askari wanyamapori wa TAWA waliokuwepo katika mkutano huo wa hadhara.

Shija na mwenzake Kusenza waliweza kuwatambua askari watano wa TAWA waliowatuhumu kuwaomba rushwa na hapo hapo Waziri Kigwangalla akawaamuru kukabidhi silaha zao na kumuagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kipolisi ya Laela, Aloyce Nyatola kuwakamata mara moja na TAKUKURU ianze uchunguzi wa tuhuma hizo ili sheria ichukue mkondo wake na iwe fundisho kwa wengine. 

Hata hivyo, baada ya mkutano wa hadhara, Dk. Kigwangalla aliamua kukagua baadhi ya maeneo ndani ya pori hilo na kubaini uharibifu mkubwa uliofanywa na mifugo huku dalili zikiwa ni kinyesi cha ng'ombe kilichokuwa kimezagaa kila mahali. 

Hapo hapo alimuagiza Mkurugenzi Mkuu TAWA, Dk. James Wakaibara ambaye aliwakilishwa na Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Utalii wa mamlaka hiyo, Imani Nkuwi kuwasimamisha kazi wafanyakazi wote wa pori hilo na kuleta wengine wapya wasimamie pori hilo ili kupisha uchunguzi.

"Hawa wote wasimamishwe kazi na uchunguzi ufanyike kitu gani kilikua kinaendelea hapa, kwanza ifanyike parade kuhusu suala la kumuomba rushwa yule mfugaji, wabainike moja kwa moja wafunguliwe mashtaka, na hawa wote nataka wachungunguzwe na mali walizonazo kama ambavyo imeelezwa kuwa hawa wametumia hili pori kama kitega uchumi chao binafsi, huu ni uhujumu uchumi" aliagiza Dk. Kigwangalla.

Wakati huo huo, Dk. Kigwangalla ametoa siku 30 kwa wananchi wote wenye mifugo ndani ya pori hilo kuitoa kwa hiari yao wenyewe kabla ya operesheni maalum itakayowaondoa kwa nguvu. Alisema kama walijua pori hilo ni shamba la bibi sasa wasahau na wajipange namna ya kutafuta malisho au kupunguza idadi ya mifugo yao na kuanzisha miradi mingine ya maendeleo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, akiamuru askari watano wa Pori la Akiba Uwanda wanyang'anywe silaha zao na wawekwe chini ya ulinzi kwa ajili ya uchunguzi baada ya kutambuliwa kwenye gwaride kwa tuhuma kupokea rushwa ya shilingi milioni 5.8 kutoka kwa mfugaji, Shija Imeli (Kulia) kwa makubaliano ya kulisha ng'ombe wake ndani ya pori hilo kwa muda wa miezi mitano.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa mkoa wa Rukwa, wakikagua mazingira ya Pori la Akiba Uwanda baada kuwasimamisha kazi maafisa na askari wote 27 wa pori hilo kupisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa zinazowakabili. Watumishi hao wananalalamikiwa kupewa rushwa ili kuruhusu wananchi wachunge mifug hifadhini na kwa wale ambao hawatoi rushwa huishia kukamtwa mifugo yao. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa mkoa wa Rukwa, wakikagua mazingira ya Pori la Akiba Uwanda baada kuwasimamisha kazi maafisa na askari wote 27 wa pori hilo kupisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa zinazowakabili. Watumishi hao wananalalamikiwa kupewa rushwa ili kuruhusu wananchi wachunge mifug hifadhini na kwa wale ambao hawatoi rushwa huishia kukamtwa mifugo yao.

WAZIRI MBARAWA AWATAKA WATAALAM WA DAWASA, DAWASCO KUTOA MAJIBU YA UPOTEVU WA MAJI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

SERIKALI imewaagiza wataalamu kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) na Shirika la Majisafi na Majitaka (DAWASCO) kutoa majibu kuhusu upotevu wa maji unaosababisha hasara kubwa kwa Serikali.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Process Makame Mbarawa ameagiza hayo leo wakati wa ziara yake ya kukagua miundombinu ya maji iliyopo chini ya Dawasa ya Ruvu Juu na Ruvu chini.

Profesa Mbarawa ameeleza  licha ya juhudi zinazofanywa na Serikali ya kumaliza tatizo la maji, Dar es Salaam na Pwani, asilimia 44 ya maji kati ya lita milioni 504 zinazozalishwa kila siku katika vyanzo mbali mbali hupotea kabla ya kufika kwa mtumiaji wa mwisho.

 Kwa mujibu wa Waziri Mbarawa, takribani bilioni nne hupotea kila mwezi kutokana na upotevu wa maji hayo, upotevu ambao ni mkubwa wakati wananchi wakiwa hawana maji. 

"Serikali inapoteza fedha nyingi kutokana na upotevu wa maji njiani kabla ua kufika kwa mtumiaji wa mwisho, ni wakati umefika sasa kwa wataalumu wetu kumaliza tatizo na kutoa majibu yanayoeleweka, lazima Tuingie kwa undani tuangalie maji haya yanapotelea wapi" amesema Profesa Mbarawa

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, akikagua mtambo wa Ruvu Chini, wakati wa ziara yake ya kikazi, Ruvu, mkoani Pwani.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamalaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Dk. Suphian Masasi, kuhusu mtambo wa mpya wa Ruvu Juu wa kudhalisha maji, mkoani Pwani.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kukagua kituo cha kusukuma maji ghafi katika mtambo wa Ruvu Juu, Mkoa wa Pwani.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamalaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Dk. Suphian Masasi, kuhusu kituo cha kusukuma maji ghafi katika mtambo wa Ruvu Juu, Mkoa wa Pwani.
Mkazi wa Kiluvya wilayani Ubungo akitoa malalamiko yake kuhusu mfumo wa kulipia maji unaotumiwa na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), unavyowasumbua wananchi kupata huduma ya majisafi.


TIMU NANE ZATINGA ROBO FAINALI SPRITE BBALL KINGS

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


MICHEZO minne ya hatua ya 16 bora ya Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 imefanyika katika viwili tofauti na timu nane kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali.


Mechi hizo zimepigwa Jumamosi na Jumapili huku michezo minne ya awali ikipigwa katika Viwanja vya Airwing huku mingine ikipigwa Viwanja vya Bandari Kurasini Jijini Dar ed Salaam.

Katika mchezo wa kwanza, timu ya DMI ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapu 113 dhidi ya 64 vya Fast Heat na Mechi ya pili ilikua ni kati ya Flying Dribbellrs dhidi ya Ukonga Hitmen ambapo Flying Dribbllers walifanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapun 87 dhidi ya 63.

Mchezo wa tatu ulikua baina ya Airwing na St Joseph ambapo Ushindi wa vikapu 98 vya St Joseph dhidi ya 78 vya Airwing uliwapeleka hatua ya robo fainali.Mchezo wa nne ulikua ni baina ya Portland wakichuana na Mbezi Beach KKKT, na Portland kuondoka na ushindi mkubwa wa Vikapu 126 dhidi ya 54.

Mechi zingine nne zimechezwa kwenye Viwanja vya Bandari Kurasini jana zikiwakutanisha Mchenga BBall Stars dhidi ya Oysterbay, Mchenga kufanikiwa kuingia robo kwa vikapu 117 dhidi ya vikapu 56. Mchezo wa pili kati ya Stylers alikua anapambana na Temeke Heroes, na Temeke kufanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapu 76 dhidi ya vikapu 58 vya stylers.

Mechi nyingine ya tatu iliwapeleka Team Kiza robo fainali kwa vikapu 66 dhidi ya 56 vya Ukonga Warriors huku mchezo wa mwisho ulikua ni baina ya Raptors akichuana na Water Institute na Vikapu 77 vikawapa ushindi Water Institute dhidi ya 68.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) Manase Zabron amesema kuwa timu zimejiandaa sana na aliyejiandaa vizuri ndio ataondoka na ubingwa wa 2018. Amesema kwa mwaka huu kutakua na ushindani mkubwa sana.

Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 yanayodhamiwa na kinywaji cha Sprite yameanza mwishoni mwa wiki kwa hatua ya mchujo kufanyika, timu 8 kufanikiwa kuvuka kuingia robo fainali na zinaenda kukutana siku ya Jumamosi baada ya droo kuchezeshwa kesho mubashara kupitia kituo cha EATV na EA Radio.

Mshindi wa kwanza atafanikiwa kuondoka na kitita cha Milioni 10 pamoja na Kombe, Mshindi wa pili milioni 3 na mchezaji bora wa mashindano akitwaa milioni 2

RPC ARUSHA:MADEREVA AMBAO HAWATAZINGATIA SHERIA NA TARATIBU ZA USALAMA BARABARNI KUCHUKULIWA HATUA

$
0
0
Na Vero Ignatus Arusha.

Ukaguzi wa magari ya abiria na mizigo umefanyika leo mkoani Arusha ukiongozwa na Kamanda wa polisi Ramadhani Ngazi ,ambapo yamebainika makosa mbalimbali yakiwemo baadhi ya madereva hawana leseni ,magari mabovu,mifumo ya breki na mifumo ya usukani ni mibovu.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo RPC amesema lengo kuu la ukaguzi huo ni kuhakikisha abiria wanaposafiri wanakuwa salama pamoja na chombo husika .Aidha amewataka madereva kufahamu kuwa lazima wazingatie kanuni za sheria za usalama barabarani kwani atakaekiuka sheria itafuata mkondo wake.

Akisisitiza umuhimu wa kufunga mikanda Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Joseph Bukombe amesema kuwa utafiti unaonyesha kuwa asilimia 40%ya kufunga mkanda unaokoa maisha pale ajali inapotokea.

"Watafiti wanasema kuwa asilimia 40%ya kufunga mkanda hivyo ni vizuri elimu hii mkaitoa hata kwenye familia zenu umuhimu wa kufunga mkanda uwapo ndani ya chombo cha usafiri" alisema Bukombe.Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Joseph Bukombe amewaomba wamiliki wa vyombo vya usafiri kutengeneza na kurekebisha mifumo ya ndani ya magari yao,badala ya kuweka urembo wa kupaka rangi

Baadhi ya madereva wamepongeza jitihada hizo za jeshi la polisi ,Kwa upande wao madereva,akiwemo Salum Said ambao wamewashauri wenzao waache tabia za kutumia vilevi.Pia wamelipongeza jeshi la polisi kwanjitihada wanazozifanya zanihakikikisha kila dereva anapata elimu ya kutosha ili kuhakikisha wanajitahidinkuzuia ajali zinazosababishwa na kizembe.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Ramadhani Ng'azi akizungumza na waandishi juu ya zoezi la ukaguzi wa magari katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoaninna nchi jirani aliyepo kushoto kwake ni RTO mkoani hapo Joseph Bukombe.Picha na Vero Ignatus
Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Ramadhani Ng'aziakikagua matairi kwenye moja ya gari .Picha na Vero Ignatus.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Ramadhani Ng'azi akiendelea na ukaguzi wamagari kama inavyoonekana pichani.Picha na Vero Ignatus.

DKT TIZEBA NA DKT MABULA WAMALIZA MGOGORO WA ARDHI WA CHAMA CHA USHIRIKA ULIODUMU KWA MIAKA 17

$
0
0

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza jambo kwa msisitizo wakati wa mkutano wa utatuzi wa mgogoro baina ya Chama Cha Ushirika Nyamatongo dhidi ya Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamatongo Ndg Itembwe Mnana uliodumu kwa miaka 17, Kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula, Leo 8 Julai 2018. (Picha zote Na Mathias Canal-WK)
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza na wazee kijijini Nyamatongo wakati wa mkutano wa utatuzi wa mgogoro baina ya Chama Cha Ushirika Nyamatongo dhidi ya Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamatongo Ndg Itembwe Mnana uliodumu kwa miaka 17, Leo 8 julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba, Naibu waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa kijiji cha Nyamatongo mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa utatuzi wa mgogoro baina ya Chama Cha Ushirika Nyamatongo dhidi ya Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamatongo Ndg Itembwe Mnana uliodumu kwa miaka 17, Leo 8 Julai 2018.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza jambo wakati wa mkutano wa utatuzi wa mgogoro baada ya Chama Cha Ushirika Nyamatongo dhidi ya Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamatongo Ndg Itembwe Mnana uliodumu kwa miaka 17, Leo 8 Julai 2018.
Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamatongo Ndg Itembwe Mnana (Kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha ushirika Nyamatongo Ndg Willium Elikana mara baada ya kuridhia mgogoro kumalizika.




Na Mathias Canal, Sengerema-Mwanza

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula wametatua mgogoro baina ya Chama Cha Ushirika Nyamatongo dhidi ya Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamatongo Ndg Itembwe Mnana uliodumu kwa miaka 17.

Mgogoro huo umemalizika kwa maelewano ya pande zote mbili kuwa na kauli moja ambapo Mwenyekiti wa kijiji hicho amekubali kuketi meza moja na Uongozi wa chama hicho cha ushirika ili kukubaliana namna bora ya kuchochea Maendeleo katika kijiji na Taifa kwa ujumla badala ya kuendeleza mgogoro usiokuwa na maslahi kwa pande zote.

Alisisitiza umuhimu wa ushirika nchini ambapo aliwaeleza wananchi hao kutoendeleza vita ya kutokuwa na maelewano kwani kufanya hivyo kunarudisha nyuma shughuli za Maendeleo ya kijiji na Taifa kwa ujumla wake.

Pia, Dkt Tizeba ametangaza Kiama kwa maafisa ugani wanaokaa maofisini badala ya kuwasaidia wakulima kwenye hatua muhimu za uandaaji wa shamba na hatimaye wakati wa Kilimo.Katika mkutano huo Naibu Waziri wa Ardhi, nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe Dkt Angelina Mabula aliwataka wananchi hao kuwa na utamaduni wa kuketi pamoja na kujadili changamoto zinazowakabili ili kuzitatua kwa manufaa yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Alisisitiza kuwa migogoro kama hiyo haihitaji sintofahamu ya mashitaka ya muda mrefu kwani kufanya hivyo ni kutengeneza uhasama usio kuwa na sababu ilihali wote ni watanzania.Dkt Mabula aliongeza kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imekusudia kutatua changamoto zote zinazohusisha wananchi katika migogoro ya ardhi pamoja na kadhia zingine zote.

Mgogoro huo ambao ulianza tangu mwaka 2001 umekuwa na hatua za kushitakiana baina ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyamatongo dhidi ya Chama cha ushirika Nyamatongo katika maeneo mbalimbali tangu mwaka 2001 ambapo awali ulitolewa maamuzi katika ngazi ya baraza la kijiji baadae baraza la kata na hatimaye Baraza la Ardhi la Wilaya ya Sengerema ambalo ndilo liliamua kuvunja maamuzi yote ya baraza la kijiji na Kata ili kuanza upya usikilizwaji wa kesi hiyo.

Mara baada ya kumalizika kwa mgogoro huo wananchi kijijini hapo wamempongeza Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe Dkt Angelina Mabula kwa kuzuru kijijini hapo hatimaye kutatua mgogoro huo ambao umekuwa sugu kwa miaka 17.

Aidha, katika mkutano huo wananchi wamepata nafasi ya kueleza kero mbalimbali zinazowakabili kijijini hapo ikiwemo ukosekanaji wa maji safi na salama, huku wengine wakieleza kusikitishwa na maafisa ugani kuketi maofisini pasina kuzuru kwa wakulima ili kuwafundisha mbinu bora za Kilimo.

TAMASHA la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka 2018 lafunguliwa mjini Zanzibar

$
0
0
TAMASHA la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka 2018, limefunguliwa juzi usiku huku Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ikijipiga kifua kusaidia utatuzi wa changamoto zinazoikabili tasnia ya filamu nchini. 

Akizungumza kwenye ufunguzi wa tamasha hilo la 21 katika ukumbi wa Ngome Kongwe mjini Zanzibar, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi, alikiri kuwa pamoja na mafanikio yake, kuna maeneo ambayo halijafanya vizuri.

Alisema miongoni mwa upungufu huo, ni kutokufikiwa ufanisi wa asilimia 100 katika ulinzi wa haki za wabunifu na watengenezaji filamu, akisema iko haja ya kuuangalia upande huo kwa jicho la tatu ili wasanii hao wafaidi matunda ya jasho lao.Aliiambia hadhira iliyofurika ukumbini hapo wakiwemo watalii kutoka nchi mbalimbali, kuwa Serikali ya Zanzibar ilianzisha kwa nia njema Ofisi ya Msimamizi wa Haki za Ubunifu (COSOZA), mfumo unaoendeshwa kimataifa ili kulinda haki za wasanii.

Alifahamisha kuwa tasnia ya filamu ni miongoni mwa maeneo yanayoweza kusaidia kuyapatia ufumbuzi matatizo ya kijamii hasa uhaba wa ajira, kama ilivyo katika mataifa mengine yaliyopiga hatua kubwa kifilamu na matamasha yanayotambulika kimataifa.

“Kwa upande wa serikali, naamini taasisi na vyombo husika vitaendelea kusimamia upatikanaji wa haki kwa waliopoteza jasho lao katika tasnia hii ili nao wanufaike kwa malengo waliyojiwekea,” alisema.Waziri huyo alisema kuanzishwa kwa COSOZA ni sehemu ya msukumo wa serikali katika kutoa mchango ili kuwainua kimaisha wananchi waliojikita katika tasnia ya filamu.

“Na katika hili lazima tukiri liko eneo ambalo hatujafanya vizuri sana. Suala la uzalishaji wa filamu ni muhimu, lakini suala la miundombinu, ugawaji wake, upatikanaji wake, usimamizi, uuzaji na mgawanyiko wake bado hatujafanya vyema,” alisema Waziri huyo.Kwa hivyo alitaka serikali ijitoe katika kuhakikisha inasimamia vyema haki za wabunifu wa filamu, kwani inaonekana bado wasambazaji wananufaika zaidi kuliko wazalishaji wake.

Hata hivyo, alieleza kufurahishwa kwake, kuwa pamoja na changamoto hizo na uhaba wa udhamini, tamasha la ZIFF limeendelea kuishi na kujiongozea umaarufu, hali inayowavutia watalii wengi wanaokuja nchini wakati wa tamasha hilo.Mapema, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ZIFF Mahmoud Thabit Kombo, aliwashukuru wadhamini mbalimbali wanaoendelea kulibeba tamasha hilo, pamoja na wajumbe wa bodi kwa mshikamano wao kuhakakisha haliyumbi.

Alisema bila kuungwa mkono na wadhamini, Zanzibar inaweza kupoteza matamasha kama hayo na hivyo kupunguza nafasi za ajira na pato la taifa.
Akizungumzia ukuaji wa tasnia ya filamu Zanzibar, Kombo ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utalii na Mambao ya Kale, alisema wakati umefika Zanzibar iwe na tamasha kubwa kwa jina la Zollywood, akifananisha na Hollywood (USA), Bollywood (India) na Nollywood (Nigeria).

Uzinduzi wa tamasha hilo ulipambwa na filamu ya Kiswahili iitwayo ‘Bahasha’, iliyoongozwa na Jordan Riber, ambapo miongoni mwa washiriki wake ni Ayoub Bombwe, Godliver Gordian, Omary Mrisho na Catherine Crede.
 Baadhi ya vikundi mbalimbali pichani juu na chini vikiwasili kwenye uzinduzi wa tamasha hilo la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka 2018.

Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete atembelea banda la Nssf maonesho ya saba saba

$
0
0

Rais wa awamu ya nne Mh Dkt Jakaya Kikwete akipata maelezo kuhusiana na huduma mbali mbali zinazofanywa na Shirika la Taifa ya Hifadhi ya jamii  NSSF kutoka kwa Kaimu Meneja uhusiano na masoko Bwana Salim Khalfan ,pembeni yake ni Mkurugenzi wa mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania Tan Trade, Edwin Rutegaruka mara baada ya kutembelea katika banda la NSSF kwenye maonesho ya 42 Biashara ya Kimataifa kwenye viwanja vya sabasaba,jijini Dar
 Rais wa awamu ya nne Mh Dkt Jakaya Kikwete akikabidhiwa zawadi na mmoja wa Maofisa wa Shirika la Taifa ya Hifadhi ya jamii  (NSSF) ,Angella Msangi mara baada ya kupata maelezo kuhusiana na huduma mbali mbali zitolewazo na  Shirika hilo,alipotembelea mapema leo katika banda la NSSF kwenye maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  kwenye viwanja vya sabasaba,jijini Dar.
 Rais wa awamu ya nne Mh Dkt Jakaya Kikwete akiwasili kwenye banda la Shirika la Taifa ya Hifadhi ya jamii  (NSSF),mapema leo alipotembelea katika banda la shirika hilo kwenye maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  kwenye viwanja vya sabasaba,jijini Dar,Kushoto kwake akiwa ameambatana na Mmoja wa Maofisa wa Shirika hilo,Angella Msangi .

NAIBU KATIBU MKUU JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA KUTOKA ZANZIBAR AKABIDHI SH.MILIONI 1.5 KWA UONGOZI WA CHUO CHA KILIMO NA MIFUGO CHA KAOLE BAGAMOYO

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa kutoka Zanzibar,Najma Murtaza Giga (katikati) akimkabidhi cheti cha Stashahada cha Kuhitimu Mafunzo ya Kilimo na Ufugaji,Rais wa Chuo cha chuo cha Kilimo na ufugaji cha Kaole,Glorious Kalabamu (kushoto) katika Mahafali ya tatu ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani jana. Kulia ni Mjumbe wa Baraza la Wazazi la CCM Mkoa wa Pwani,Dk.Zainab Gama na Mkuu wa Chuo hicho,Sinami Simba. Picha zote na Elisa Shunda
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa kutoka Zanzibar,Najma Murtaza Giga (katikati) akimkabidhi cheti cha Stashahada cha Kuhitimu Mafunzo ya Kilimo na Ufugaji,Rais wa Chuo cha chuo cha Kilimo na ufugaji cha Kaole,Asnat Kasukuru (kushoto) katika Mahafali ya tatu ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani jana. Kulia ni Mjumbe wa Baraza la Wazazi la CCM Mkoa wa Pwani,Dk.Zainab Gama na Mkuu wa Chuo hicho,Sinami Simba (mwenye shati la bluu).


NA ELISA SHUNDA,BAGAMOYO 

UMOJA wa wazazi taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM, imeahidi kuendelea kusaidia kuboresha chuo cha Kilimo na ufugaji cha Kaole ili kiendane na adhi ya kuwa chuo bora kitakachotambulika kitaifa na kimataifa pamoja na kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya Tano wa kuelekea kwenye manufaa ya uchumi wa viwada nchini.

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam, na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa wa Wazazi Taifa kutokea Zanzibar, Najma Murtaza Giga alipokuwa mgeni rasmi katika mahafari ya tatu ya chuo hicho yaliyofanyika Chuoni kaole-Bagamoyo mkoani Pwani.

Giga ambaye pia ni mbunge na mwenyekiti wa kamati ya Bunge kwenye bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania, amewapongeza walimu na watumishi mbalimbali waosimamia chuo hicho kwa kufanya kazi kwenye werefi mkubwa wa kuongeza idadi ya wahitimu katika chuo hicho kwa mwaka huu kufikia 108 tofauti na mwaka jana ambao wahitimu walipungua kufikia 72.

‘’ki ukweli chuo chetu kinachosimiwa na umoja wa wazazi taifa ya chama cha mapinduzi CCM, kinapaswa kijitangaze na kipewe sapoti kubwa hasa kwa wazaz, walezi, wadau na serikali kwa ujumla ili kiwe na hadhi kama vyuo vingine na kiiendane na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya Dr. John Magufuli” alisema Giga.

Akizungumzia kuhusiana na suala la ajira katika serikali ya awamu ya tano, Giga aliwataka watafunzi wanaosoma katika chuo hicho na wale waliohitimu kwamba wasiwe na wasiwasi kuhusiana na suala hilo kwani najira kwao itapatikana pia hakusita kuwatakawanafunzi hao kwamba wasikimbilie kuajiriwa peke yao bali wahakikishe wanakuwa na m binu mbadala wa kujiajiri na kutoa elimu hiyo kwa vijana wengine waliopo mitaani.

Hata hivyo Katibu mkuu huyo wa wazazi taifa kutokea Zanzibar, ametoa kiasi cha zaidi ya sh. Milioni 1.5 ni ahadi yake aliyoaidi hivi karibuni hivyo zitakwenda kununulia madawati katika chuo hicho.

Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho, Sinani Simba amesema chuo hicho kinatoa kozi mbalimbali ikiwemo kozi ya Kilimo na Miufugo ngazi ya Astashahada na Shahada (Cheti na Diproma).

Amezungumzia kuhusu kilimo, Simba amesema chuo cha Kaole cha Kilimo na Mifugo kinachomilikiwa na umoja wa wazazi Taifa , hamesema tangu chuo kicho kianzishwe Desemba 15 mwaka 2015 hakijawai kutambulika vizuri ndani ya jamii ingawa kuna azina tosha ya wataalu na walimu, hivyo chuo hicho kinampango wa kujitangaza zaidi kusudi kiweze kuwa chuo cha kimataifa.

Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake, Exavery Mwakilema amesema chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo suala la ukosefu wa ajira kwa wanafunzi wanaomaliza chuoni hapo, Upungufu wa vitambu katika maktaba, Mifugo hasa ng’ombe wa maziwa na vifaa vya michezo.

Jumla ya wahitimu 108 wa mwaka wa tatu wa ngazi Cheti na diploma katika fani ya Kilimo na Mifugo leo wamehitimu masomo yao katika chuo hicho na huku wakiahidi wanaporudi ulaiyani watakuwa mabalozi bora kwa kutoa elimu kwa vijana wenzao . 
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa kutoka Zanzibar,Najma Murtaza Giga (katikati) akiwaongoza wahitimu kuingia katika viunga vya chuo kuanza sherehe za mahafali hiyo.
Wahitimu wakicheza na kufurahi wakati wakiingia katika viunga vya chuo cha Kilimo na mifugo cha Kaole cha Umoja wa wazazi wilayani Bagamoyo tayari kuanza hafla hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa kutoka Zanzibar,Najma Murtaza Giga akizungumza katika sherehe za mahafali ya chuo hicho. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho,Sinani Simba na Mjumbe wa Baraza la Wazazi CCM Mkoa wa Pwani,Dk.Zainab Gama.
Baadhi ya wahitimu wa ngazi ya Astashahada na Stashahada wakimsikiliza kwa umakini Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa kutoka Zanzibar,Najma Murtaza Giga (hayupo pichani) wakati akizungumza katika mahafali hayo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani,Jackson Mtuka akizungumza katika mkutano huo.
Baadhi ya wahitimu wa ngazi ya Astashahada na Stashahada wakimsikiliza kwa umakini Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani,Jackson Mtuka (hayupo pichani) wakati akizungumza katika mahafali hayo.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Mkoa wa Pwani,Gama Juma Gama akizungumza katika mkutano huo.
Baadhi ya wananchi na ndugu waliohudhuria katika shughuli hiyo ya mahafali wakifuatilia kwa umakini matukio yote yanayofanyika katika viunga vya chuo hicho.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM wa Wilaya ya Bagamoyo,Abubakar Mlawa akizungumza katika mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu wa ngazi ya Astashahada na Stashahada wakifuatilia kwa umakini matukio yanayoendelea katika eneo hilo.
Mwanafunzi na Msoma Risala kutoka upande wa Wanachuo Wahitimu,Exavery Mwakilema akisoma changamoto zinazoikabili chuo hiko.
Wahitimu wa Masomo ya Mifugo wakila kiapo katika mahafali hayo.
Burudani zikiendelea chuoni hapo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Kibaha Mjini,Edwin shunda akimpongeza msanii aliyekuwa akiburudisha katika mahafali hayo.
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa kutoka Zanzibar,Najma Murtaza Giga akicheza muziki na wahitimu katika mahafali hayo.
Wahitimu wakicheza muziki aina ya kwaito katika mahafali hayo.

Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa kutoka Zanzibar,Najma Murtaza Giga akiwa kwenye picha ya pamoja na wakufunzi na wageni waalikwa baada ya kumalizika kwa shughuli hiyo ya mahafali ya tatu ya Chuo cha Kilimo na Ufugaji cha Kaole Bagamoyo.
Mkuu wa Chuo cha Kilimo na Ufugaji cha Kaole kilichopo Bagamoyo,Sinani simba,akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa kutoka Zanzibar,Najma Murtaza Giga na wageni waalikwa wengine kuhusu maendeleo ya chuo hicho na historia yake tangu kuanzishwa kwake na mazingira yake kwa ujumla.
mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa kutoka Zanzibar,Najma Murtaza Giga akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu na wageni waalikwa.
mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa kutoka Zanzibar,Najma Murtaza Giga akiwa katika picha ya pamoja na wananchi na ndugu mbalimbali wa wahitimu.
Mkuu wa Chuo cha Kilimo na Ufugaji cha Kaole kilichopo Bagamoyo,Sinani simba,akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa kutoka Zanzibar,Najma Murtaza Giga na wageni waalikwa wengine kuhusu wanachuo wanavyofanya mazoezi kwa vitendo katika shamba darasa lililopo chuoni hapo.

MKOA WA PWANI WAPIGA STOP KUHUSISHA WATOTO KWENYE VIGODORO NA NGOMA ZA USIKU

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE

SERIKALI Mkoani Pwani ,imekemea tabia inayofanywa na baadhi ya wazazi ya kuwahusisha watoto wao kwenda katika vigodoro, kudhurula nyakati za usiku na badala yake wawasimamie katika suala la elimu ili kuinua taaluma zao.

Aidha imewaonya wazazi wanaowakataza watoto wao kwenda shule na wengine kuwashawishi watoto hao kufanya vibaya kwenye mitihani yao ya kumaliza darasa la saba na kidato cha nne.

Akitoa rai hiyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Pwani ,katibu tawala wa mkoa huo ,Zuberi Samataba alisema ,wapo wazazi na walezi ambao ndio chanzo cha kudidimiza suala la elimu .

Alieleza ,endapo watambaini mzazi ama mlezi akimwachia mtoto kudhurula na kumhusisha kwenye vigidoro na ngoma za usiku atakiona."Serikali haiwezi kukubali mzazi akaachia mtoto kiholela ,watoto ni wa serikali ,mzazi atakaebainika kufanya hayo hatutamvumilia ,hii inasababisha kudumaza elimu mkoani kwetu"

Alizielekeza halmashauri kuwachukulia hatua wazazi wanaowaachia huru watoto wao kwani wanahatarisha maisha ya watoto hao hasa kusababisha mimba za utotoni.Samataba alikemea mimba za utotoni ,na amesisitiza kuchukuliwa hatua kali kwa wanaosababisha mimba hizo .

Alisema, zipo taarifa zilizokuwa zikidai wapo wazazi wanaojua watoto wao wanafanya vizuri darasani ambapo wanawakataza kufanya vizuri kwenye taaluma zao.Nae kaimu afisa elimu mkoa ,Hedegald Makundi alieleza uandikishaji katika elimu ya awali bado upo chini tofauti na wanaoandikishwa darasa la kwanza.

"Elimu ya awali lengo lilikuwa ni kuandikisha wanafunzi 35,418 walioandikishwa ni 26,997 sawa na asilimia 76 ambapo uandikishaji darasa la kwanza lengo ilikuwa 47,686 walioandikishwa ni 52,551 sawa na asilimia 110" alieleza Hedegald.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Pwani ,Ramadhani Maneno alisema ili kuhakikisha elimu inaboreshwa ni lazima kushirikiana wadau ,wazazi na walimu kutatua changamoto za kielimu bila kuiachia serikali pekee.
 Katibu tawala mkoani Pwani ,Zuberi Samataba akitembelea baadhi ya mabanda ya maonyesho ya kielimu yaliyoandaliwa na baadhi ya wanafunzi Chalinze Mkoani Pwani wakati wa maadhimisho ya Juma la elimu kimkoa yaliyofanyika Chalinze. 
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali Chalinze Mkoani Pwani wakionyesha mabango katika maadhimisho ya Juma la elimu kimkoa yaliyofanyika Chalinze .(picha na Mwamvua Mwinyi)
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images