Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

MPINA AAMURU KUUNDWA KWA IDARA YA ULINZI WA MIFUGO NA MAZAO YAKE

$
0
0
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina akitoa maelekezo ya serikali katika kikao hicho kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Abdallah Ulega 
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji Mh Mahamoud Mgimwa na wajumbe wa kamati hiyo akisikiliza mawasilisho ya Taarifa za Operesheni Nzagamba kutoka kwa wawasilishaji leo 
 WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akiwa kwenye picha ya pamoja na kikosi kazi alichokiunda cha Operesheni Nzagamba 2018 na viongozi wakuu wa wizara na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji Mh Mahmoud Mgimwa 



Na John Mapepele,Dodoma

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameamuru kuundwa Kitengo kipya cha Usimamizi na Udhibiti wa Rasilimali za Mifugo katika Idara ya Uzalishaji na Masoko cha wizara hiyo ili kutoa ulinzi wa kutosha wa mifugo na mazao yake baada ya kubainika kuwepo mianya mikubwa ya utoroshaji rasilimali hizo nje ya nchi na uingizaji holela wa mazao hayo nchini.

Pia ameagiza kuandaliwa mkakati wa kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato yatokanayo na sekta ya mifugo baada ya kubainika kuwepo kwa mianya mingi na mbinu haramu zinazotumiwa kukwepa kulipa mapato ya Serikali hatua inayosababisha sekta ya mifugo kutoa mchango mdogo katika Pato la Taifa.

Sambamba na hilo pia Waziri Mpina ameagiza kupitiwa upya kwa mfumo wa uagizaji, ununuzi na usambazaji wa dawa za mifugo ambapo wafugaji wengi wamelalamikia mfumo wa sasa hasa katika upatikanaji wa dawa, bei kubwa, kuuziwa dawa zilizokwisha muda wa matumizi na dawa nyingi kutokuwa na viwango vya ubora unaotakiwa.

Akizungumza jijini Dodoma jana wakati wa tathmini ya operesheni ‘Nzagamba’, iliyodumu kwa muda wa miezi mitatu katika mikoa yote ya Tanzania Bara, Waziri Mpina alisema makusanyo ya maduhuli kutokana na operesheni hiyo jumla ya Tsh bilioni 7.1 zilikusanywa kutokana na tozo, kodi na faini mbalimbali ambapo kumepelekea makusanyo ya maduhuli ya wizara kwa mwaka wa fedha 2017/18 kufikia sh bilioni 19.5 ikilinganishwa na Tsh bilioni 12 zilizokusanywa katika mwaka wa fedha 2016/17.

Waziri Mpina alisisitiza kuwa awali Serikali ilikuwa inakusanya mapato yatokanayo na sekta ya mifugo yaliyokuwa kati ya Bilioni 10 hadi 12 kwa mwaka licha ya idadi kubwa ya mifugo iliyoko nchini hatua ambayo iliisukuma wizara hiyo kufanya operesheni ‘Nzagamba’ ili kubaini mianya ya upotevu wa mapato yatokanayo na sekta hiyo.

“Katika kipindi cha miezi mitatu ya operesheni hiyo jumla ya Ng’ombe 37,262, Mbuzi na kondoo 125,015, Punda 2,156 zilikamatwa zikisafirishwa bila vibali wala kulipiwa tozo husika kwenda nchi jirani za Kenya, Zambia, Comoro na Burundi huku tani 10,600 za vyakula vya mifugo na uingizaji wa mazao ya mifugo bila vibali kilo 1,619 nazo zikikamatwa katika operesheni hiyo”alisema.

Waziri Mpina alisema operesheni hiyo imebaini ukwepaji wa sh bilioni 1.27 kwa kampuni 15 zinazoingiza bidhaa za nyama na maziwa nchini.Aidha Serikali inapoteza vyote yaani mapato, ajira, malighafi za viwanda na kuigeuza Tanzania kuwa soko la bidhaa na machungio ya mifugo ya nchi jirani jambo ambalo Serikali ya awamu ya tano haitaliruhusu liendelee.

Kuhusu suala la usafirishaji mifugo ndani ya nchi bila kuwa vibali, Waziri Mpina alisema kosa hilo lilihusisha jumla ya ng’ombe 28,712, mbuzi/kondoo 11,251, nguruwe 801 na tani 480 za vyakula vya mifugo pia operesheni hiyo ilibaini uwepo dawa zilizokwisha muda wake kilo 805.

Mkuu wa Operesheni Nzagamba 2018, Dk. Lovince Assimwe alisema vikosi vya operesheni hiyo viligawanyika katika makundi matatu ya minadani,viwandani na ukaguzi wa hesabu ambapo imebainika kuwepo ukiukukwaji mkubwa wa Sheria, Kanuni na taratibu za uzalishaji,biashara ya mifugo,pembejeo na mazao ya mifugo katika maeneo ya usafirishaji mifugo nje ya nchi bila kuwa na vibali wala leseni.

Pia usafirishaji wa mifugo ndani ya nchi bila ya vibali, ukiukwaji wa haki za wanyama,uingizaji wa mazao ya mifugo nchini bila kuwa na vibali pamoja na uwepo wa dawa zilizokwisha muda wa matumizi,maeneo ya uzalishaji kutokuwa na wataalamu wa fani husika.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji, Mahmoud Mgimwa alisema kazi inayofanywa na wizara hiyo ya kudhibiti rasilimali za Taifa ni kuliunga mkono Bunge kwa kuzisimamia sheria ilizozitunga kusimamia sekta hiyo.

“Mnatuunga mkono kwa kusimamia sheria ambazo tumezitunga wabunge na  kwa usimamizi huu wa sheria sisi wabunge tutaendelea kuunga mkono juhudi zako Mhe Waziri na wizara kwa ujumla tumeridhika sana na hii operesheni ina manufaa makubwa kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa letu”alisema Mgimwa. 

Mgimwa alisema Wizara ya Mifugo ni kubwa ina umuhimu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda na kuiagiza Wizara kuhakikisha operesheni hiyo inakuwa endelevu kwani imeonesha ongezeko kubwa la mapato ya Serikali.Pia Mgimwa alizitaka Wizara nyingine zinahusika na operesheni Nzagamba kutoa ushirikiano wa kutosha bila kukwamishana kwani kazi hiyo sio ya Wizara ya Mifugo peke yake bali ni suala la Taifa zima.

Nao baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo walipongeza juhudi zilizofanywa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika kuokoa rasilimali za Taifa na kutaka Serikali kutengeneza mfumo rasmi wa kuhakikisha ulinzi wa rasilimali hizo za mifugo unakuwa endelevu.

Katibu Mkuu Mifugo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Mary Mashingo alisema Serikali ya awamu ya tano imetilia mkazo suala la usimamizi wa sheria katika sekta ya Mifugo na kuwa uchochea muhimu katika uchumi wa viwanda

RAIS MAGUFULI ALIVYOWAONGOZA WATANZANIA KUPOKEA NDEGE MPYA YA BOEING 787-8 DREAMLINER

JUMUIYA YA ISTIKAMA ZANZIBAR YAKABIDHI MSAADA WA FEDHA KWA WANANCHI WALIOPATWA NA MAAFA YA UPEPO KISIWA CHA TUMBATU

$
0
0
MWENYEKITI wa kitengo cha Maafa Jumuiya ya Istikama Zanzibar Said Hemed Alshaybar akimkabidhi Msaada wa Fedha Bi. Dawa Jabiri Haji mkaazi wa Tumbatu Uvivini ambae Nyumba yake iliharibiwa na upepo. 
MKURUGENZI Mtendaji Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Makame Khatibu Makame akimkabidhi Msaada wa fedha Makame Mdungi Makame mkaazi wa Shehiya ya Bomani.
MWENYEKITI wa Kitengo cha Maafa katika Jumuiya ya Istikama Zanzibar Said Hemed Alshaybar akizungumza na Wananchi wa Tumbatu baada ya kukabidhi Msaada wa fedha kwa waliopatwa na Maafa ya upepo. 
SHEHA wa Shehiya ya Uvivini Hassan Muhidini akitoa shukurani kwa niaba ya Masheha wa Shehiya wenzake wa shehia tatu za Tumbatu, kwa Jumuiya ya Istikama, baada ya kukabidhiwa msaada wa fedha kwaajili ya kununulia vifaa vya ujenzi. Picha na Abdalla Omar Maelezo – Zanzibar.
WAFANYAKAZI wa Jumuiya ya Istikama Zanzibar wakiwa kwenye Boti wakielekea katika Kisiwa cha Tumbatu kwaajili ya kukabidhi Msaada wa fedha kwa Wananchi waliopatwa na Maafa ya Upepo hivi karibuni. 

Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar 

Jumuiya ya Istiqama Zanzibar kwa kushirikiana na Radio Adhana imekabidhi msaada wa shilingi 13,600,000/ kwa wananchi wa Shehia tatu za Tumbatu waliopata maafa ya upepo uliotokea tarehe 30 mwezi uliopita. 

Mwenyekiti wa Kitengo cha Maafa Jumuiya ya Istika Zanzibar Said Hemed Al shaybar alikabidhi msaada huo katika hafla iliyofanyika Shehia yaTumbatu Uvivini na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Makame Khatib Makame.A 

Al shaybar alisema Jumuiya ya Istiqama imepokea kwa masikitiko makubwa athari zilizosababishwa na upepo huo ambapo watu sita walijeruhiwa kwa kuangukiwa na bati na matufali na kuharibu nyumba 136 za wananchi na nyumba za Ibada na vyuo vya Qur ani. 

Mwenyekiti huyo alitoa mkono wa pole kwa wananchi wote wa Tumbatu Maafa ya upepo huo na kuwaomba wawe wastahamilivu katika kipindi hiki kigumu kwani hiyo ni Rehma za Mwenye-ez-Mungu. 

Aliahidi kuwa Jumuiya ya Istiqama itaendelea kushirikiana na wananchi wote wa Zanzibar watakaofikwa na Maafa ya aina hiyo kwa kuwapatia msaada wa hali na mali utakaoweza kuwasaidia kuwapunguzia matatizo. 

Hata hivyo aliwataka wananchi waliopata msaada huo kuutumia katika malengo yaliyokusudiwa ya kununua vifaa vya ujenzi ili waweze kurejea katika hali ya maisha ya kawaida. 

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji Kamisheni ya Kukabaliana na Maafa Zanzibar Makame Khatibu Makame alisema uwamuzi wa Jumuiya ya Istikama ya kutoa msaada huo ni kusaidia juhudi za Serikali za kuwafariji wananchi wanaopatwa na maafa ya aina hiyo. 

Alisema Serikali kwa upande wake ilianza kutoa msaada kwa wananchi waliopata maafa hayo katika shehia tatu za uvivini, Bomani na Mtakuja mara tu baada ya kutokea na hatua ya Jumuiya Istikama ni muendelezo wa kuwasaidia wananchi hao. 

Aliwashauri wananchi wa Zanzibar kuendelea kuungana na kushirikiana hasa panapotokezea matatizo ya kiminaadamu bila kujali tofauti zao kwani kufanya hivyo ni kuendeleza umoja na udugu uliopo.

UN YATUNUKU UBUNIFU KATIKA MAENDELEO ENDELEVU

$
0
0
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu (kushoto) akimkabidhi Latifa Mohammed Ngea kutoka Zanzibar (kulia) mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni tatu mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa tuzo za Umoja wa Mataifa za ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.

Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu (kushoto) akimkabidhi Gracious Fanuel kutoka Kilimanjaro (kulia) mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni mbili mara baada ya kuibuka mshindi wa pili wa tuzo za Umoja wa Mataifa za ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu (kushoto) akimkabidhi Amos Mtambala kutoka Dar es Salaam (kulia) mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja mara baada ya kuibuka mshindi wa tatu wa tuzo za Umoja wa Mataifa za ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tuzo za Umoja wa Mataifa za ubunifu kwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.
Mshindi wa kwanza Latifa Mohammed Ngea kutoka Zanzibar aliyebuni mfumo unaojiendesha wenyewe wa umwagiliaji katika kilimo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea tuzo ya Umoja wa Mataifa ya ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.
Mshindi wa pili Gracious Fanuel kutoka Kilimanjaro aliyebuni roboti kwa kutumia vifaa vinavyopatikana majumbani akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea tuzo ya Umoja wa Mataifa ya ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.

Mshindi wa tatu Amos Mtambala kutoka Dar es Salaam, ambaye anatumia kipaji chake cha sanaa kwa shughuli za kijasiriamali akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea tuzo ya Umoja wa Mataifa ya ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.
Mshindi wa tatu Amos Mtambala kutoka Dar es Salaam, ambaye anatumia kipaji chake cha sanaa kwa shughuli za kijasiriamali akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea tuzo ya Umoja wa Mataifa ya ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa kwanza Latifa Mohammed Ngea kutoka Zanzibar (katikati), mshindi wa pili Gracious Fanuel kutoka Kilimanjaro (kushoto) pamoja na mshindi wa tatu Amos Mtambala kutoka Dar es Salaam (kulia) huku wakiwa wameshikilia hundi zao.




LATIFA Mohammed Ngea kutoka Zanzibar ameibuka kidedea katika tuzo za Umoja wa Mataifa za ubunifu na kupata hundi ya shilingi milioni 3.

Latifa ni miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.Latifa alipata tuzo hiyo kwa kubuni mfumo unaojiendesha wenyewe wa umwagiliaji katika kilimo.

Mfumo huo unaojiendesha wa umwagiliaji maji unaweza kutumia king’amuzi ili kubaini wapi pana unyevu na wapi pakavu ili maji yaweze kupelekwa.Tangu kuanza kwa maonesho hayo takribani wiki sasa, wageni mbalimbali wamepata nafasi ya kuona ubunifu wa vijana hao katika roboti, sanaa na kilimo.Aidha walionesha ubunifu wao unavyofanyakazi sanjari na kauli mbiu ya sabasaba mwaka huu inayosema “Kukuza biashara kwa maendeleo ya viwanda”.

Baada ya wananchi kuwasikiliza wabunifu wote watatu, wageni walipata fursa ya kupiga kura nani waliamini alionyesha ubunifu bora zaidi, ndipo Latifa alipoibuka mshindi.Mbunifu mwingine alikuwa ni Gracious Fanuel anayetoka mkoani Kilimanjaro alipata ushindi wa pili. Huyu yeye alitengeneza roboti kwa kutumia vifaa vinavyopatikana majumbani.Roboti aliyotengeneza ni mfano wa Mkono ambao unaweza kuendeshwa kwa simu ya mkononi na anatarajia kukuza ubunifu wake ili ufikie hatua ya kuwa na mkanda wa uzalishaji bidhaa na pia kusaidia watu wenye ulemavu.

Mbunifu mwingine ni Amos Mtambala, kutoka Dar es Salaam, ambaye anatumia kipaji chake cha sanaa kwa shughuli za kijasiriamali yeye alishika nafasi ya tatu. Amos alipata mafunzo kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) na tangu hapo amekuwa akipanua mtandao wake na kuwachukua zaidi ya vijana 100 ambao hutengeneza kazi za sanaa na kuuza nchini na pia kimataifa.

Zaidi ya watu 500 katika Viwanja vya Sabasaba na kupitia mitandao ya kijamii walipiga kura kwa kijana yule wanayeamini aliandaa ubunifu bora zaidi.Mshindi wa kwanza alipata shilingi milioni 3 huku mshindi wa pili akipata shilingi milioni 2 na wa tatu shilingi milioni 1.Wabunifu hao watatu walikuwa miongoni mwa vijana 100 kutoka nchi nzima walioshinda ili kuonyesha ubunifu wao katika banda la UN. Hawa walichaguliwa kwa umakini ili kuendana na ujumbe wa mwaka huu wa Sabasaba, ambao ni Kukuza Biashara kwa Maendeleo ya Viwanda.

Akizungumza katika banda la maonyesho la Umoja wa Mataifa wakati wa kutangaza washindi, Mtaalamu wa Mawasiliano wa UN, Bi. Hoyce Temu, aliwapongeza vijana ambao kwa kuwa na ndoto ya serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha kwamba azma ya maendeleo ya viwanda inatimia.Banda la maonyesho la UN ambalo Jumatano lilitangazwa kushika nafasi ya kwanza katika eneo la Utoaji Taarifa, Machapisho, Habari na Mawasiliano kwa jamii ni moja ya mabanda yaliyokuwa na pilika nyingi.

Kupatikana kwa Tuzo hiyo iliyokabidhiwa na Waziri Mkuu, Mh. Kassim Majaliwa, wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam kumetokana na mkazo wa banda hilo mwaka huu la kutoa taarifa za matokeo na ushaiishaji wa UN katika Ubunifu kwa ajili ya Maendeleo Endelevu.

Umoja wa Mataifa Tanzania umeshinda nafasi ya kwanza katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam mara kadhaa tangu UN ilipoanza kushiriki, kwani imeshiriki mara 8 mfululizo. Umoja wa Mataifa una nia ya kuendelea kushiriki ili kuwafikia watu wengi zaidi walio nje ya mfumo rasmi katika muktadha wa Sabasaba na Nanenane.

Kikosi Kazi cha Mawasiliano cha Umoja wa Mataifa (UNCG), ambacho ni kundi linalojumuisha maofisa wote wa Mawasiliano kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi nchini Tanzania, lina wajibu wa kubuni na kusimamia maandalizi ya banda la maonyesho.

Rais Magufuli aongoza mapokezi ya ndege Boeing 787-8 Dreamliner

$
0
0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ndege hiyo mpya na yakisasa aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali ikiwasili katika uwanja wa ndege wa wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali.

Ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ikiwasili katika ardhi ya Tanzania wakati ikitokea nchini Marekani.
Ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ikiwasili katika ardhi ya Tanzania wakati ikitokea nchini Marekani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na furaha pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Dkt. Inmi Patterson wapili kutoka (kulia) pamoja na viongozi wengine wa Kidini na Serikali wakati ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ilipo tua katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Muonekano wa Ndege Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akitia sahihi pamoja na Katibu Mkuu (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leonard Chamuriho kwa ajili ya makubaliano ambayo Serikali imeikodisha Ndege yake mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner kwa Shirika la Ndege la ATCL kwa ajili ya kufanyia biashara ya usafiri wa anga.
Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner akijiandaa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


MAGUFULI: WASIOPENDA UJIO WA NDEGE MPYA WATAPA TAABU SANA

$
0
0
*Asema anaamini Watanzania wengi wanatambua umuhimu wa ndege hiyo
*Asisitiza ujio wa ndege hizo zimenunuliwa kutokakana na kuziba mianya ya rushwa.

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli amesema ujio wa ndege mpya unafurahiwa na kila Mtanzania na kwamba yule ambaye haifurahii ajue atapa taabu sana huku akiwashukuru Watanzania wote kwa kufanikisha ujio wa ndege hizo.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati anazungumza kabla ya ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner ambapo amefafanua kuwa ujio wa ndege hizo unatokana na kutekeleza ahadi ya kufufua shirika la ndege nchini. Amesema katika juhudi hizo Serikali imeamua kununua ndege saba kwa fedha za Serikali na kwamba tayari ndege tatu zilishawasili nchini na leo ni ndege ya nne kuwasili nchini. 
“Mafanikio haya ni makubwa sana na niseme hajajileta yenyewe bali ni ya Watanzania wote.Nitumie nafasi hii kuwashukuru Watanzania wote na kubwa zaidi anawashukuru kwa kulipa kodi kwani ndio imesababisha kununuliwa kwa ndege hizo saba. “Hivyo niwashukuru wote ambao wameshiriki katika ujio wa ndege hizi.Ukweli Watanzania tukiamua tunaweza na niishukuru Kamati ya Miundombinu kwa kukubali kununuliwa kwa ndege hizi na kuunga mkono juhudi zinazoendelea,”amesema Rais Magufuli.

Ameongeza Serikali ya CCM iliamua kufufua shirika la ndege kuna sababu tatu , mowapo ni kurudhisha heshima ya Taifa kwani ilikuwa ni aibu kuwa nchi ambayo ina kila kitu halafu hakuna hata ndege ilikuwa ni aibu. “Tuliona tuanze kuitoa aibu hii ambayo tulikuwa tunaipata Watanzania.Kuna nchi ndogo lakini zina ndege lakini sisi hatukuwa nazo.Hivyo tuliona lazima tuiondoe aibu huu kwa kuwa na ndege.

“Watanzania wanahitaji usafiri wa ndege kwani mchango wake ni mkubwa na unahihitajika sana.Zipo sababu za watu kutopanda ndege ikiwamo ya kutokuwepo na miundombinu. “Sababu nyingine ya waanchi wengi kutopanda ndege ilikuwa ni gharama.Kwa watu wa Kagera wanafahamu kwenda Bukoba na kurudi ilikuwa ni Sh.milioni moja lakini sasa kupitia ndege za ATCL ni Sh.400,000,”amefafanua Rais.

Pia amesema sababu ya kufufua ATCL ni kukuza utalii kwani Tanzania inashika nafasi ya pili duniani huku akifafanua pamoja na kuwa na vivutio vya utalii idadi ya watalii ni ndogo. Amesema hiyo inatokana na kukosekana kwa ndege kwani kote ambako wanapokea idadi kubwa ya watalii inatokana na uwepo na ndege za uhakika katika nchi zao. Mnapokuwa na ndege watalii wengi wanakwenda kuangalia utalii wanatumia ndege , hivyo hata uamuzi wa ndege hii ni kutaka kubeba watalii wengi.

“Na ninaamini ndege hii itakapoanza kufanya kazi na ile nyingine itakapokuja itaongeza watalii,”amesema Rais Magufuli. Amesema amesikiliza maoni ya wananchi mbalimbali kutokana na ujio wa ndege hiyo ambapo wengi wameizungumzia vema na hivyo anwashukuru kwa ushirikiano wao. Pamoja na kuimarisha shirika la ndege ,Rais Magufuli amesema pia Serikali ya CCM inaendelea kuboresha usafiri wa majini , ujenzi wa miundombinu ya barabara yakiwamo madaraja na kwamba daraja linalojengwa Tazara litaitwa Mfugale. ia Rais Magufuli amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu ya nishati ya umeme, miundombinu ya afya na elimu na kufafanua anaamini ifikapo mwaka 2025 Watanzania watakuwa katika uchumi wa kati.

Rais Magufuli amesema maendeleo yanayopatikana sasa yanatokana na kuzima mianya ya rushwa na upotevu wa fedha kwani hivi sasa amebana upotevu wa fedha na matokeo yake fedha zinatumika katika kufanya maendeleo ya nchi.

WAZIRI LUGOLA, JENISTA MHAGAMA WAFANYA KIKAO KUJADILI MFUMO WA PAMOJA WA KUTOA VIBALI VYA KAZI NA UKAAZI, JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza katika kikao chake na Maafisa Waandamizi wa Idara ya Uhamiaji kuhusu utaratibu wa kuunganisha mifumo ya vibali vya kazi na ukaazi. Kulia ni Kaimu Kamishna wa Vibali vya Ukaazi, Idara ya Uhamiaji, Mary Palmer, kushoto ni Afisa wa Kitengo cha Vibali vya Ukaazi, Isaac Fota, pamoja na Afisa Mahafudhi Nassoro. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma leo, kabla ya kikao chake na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama.  
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto meza kuu), akimsikiliza Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama alipokua akifafanua jambo kuhusiana na mfumo unaoziunganisha Wizara hizo mbili, wa utoaji wa vibali vya kazi na ukaazi. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, jijini Dodoma leo.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza katika kikao cha kujadili mfumo wa pamoja wa utoaji wa vibali vya kazi na ukaazi. Kulia meza kuu ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama. Mfumo huo unaoziunganisha wizara hizo mbili. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, jijini Dodoma leo.  
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiwa ofisini kwake jijini Dodoma mara baada ya kuwasili jijini humo leo. Waziri Lugola alifanya kikao na Maafisa Uhamiaji kutoka Kitengo cha Vibali vya Ukaazi, na baadaye alifanya kikao na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama jijini humo, wakijadili mfumo wa pamoja wa utoaji wa vibali vya kazi na ukaazi ambao unaziunganisha Wizara hizo mbili.  
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akikaribishwa na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama, ofisini kwake jijini Dodoma, kabla ya Mawaziri hao kuanza kikao cha kujadili mfumo wa pamoja wa utoaji wa vibali vya kazi na ukaazi ambao unaunganisha wizara hizo mbili. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, jijini humo leo.

NSSF KUTOA MAFAO SITA KWA WOTE SEKTA ISIYO RASMI

$
0
0
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limedhamiria kutoa mafao yote sita yatolewayo ili kuisaidia sekta isiyo rasmi kujikinga na majanga mbalimbali na kujikwamua Kiuchumi

Akizungumza katika semina kwa viongozi wa vikundi vya ujasiriamali mkoani pwani, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng.Evaristi Ndikilo.

Alisema sekta isiyo rasmi ina kundi kubwa sana ambalo halijafikiwa na Hifadhi ya jamii hivyo ni fursa na muhimu kwa wale wote walio katika sekta hiyo wakiwemo mamalishe, bodaboda, wakulima, wavuvi, walio katika vikundi kama SACCOS na Vikoba kujiunga na NSSF ili waweze kujikinga na majanga mbalimbali.

Pia Mkuu wa mkoa ameongezea kuhimiza wajasiriamali wote wa Mkoa wa Pwani kujiunga na Mfuko wa hifadhi ya Jamii ili koungeza pato la Mkoa wa pwani na pia aliwahimiza viongozi mbalimbali wa serikali kuunga mkono mpango huu kwani utaisaidia serikali ya awamu ya tano katika mikakati ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii.

Pia mkuu huyo wa mkoa amesema wajasiriamali wengi wanavilio vikubwa kwa kukosa mikopo na pia riba kubwa pindi warejeshapo mikopo hiyo..,Lakini amelipongeza sana shirika la Taifa la hifadhi ya jamii kuliona hilo na kukaa chini pamoja na Benki ya Azania kutoa mikopo kwa wajasiriamali wote na kwa riba nafuu kupitia vikundi vyao.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evaristi Ndikilo akizungumza na Viongozi wa Vikundi vya uzalishaji mali wakati wa semina iliyoandaliwa na NSSF inayohusu Hifadhi ya Jamii kwa sekta isiyo rasmi.
Viongozi wa Vikundi vya uzalishaji mali wakiwa katika semina iliyoandaliwa na NSSF kwa ajili ya kuratibisha Hifadhi ya Jamii kwa sekta isiyo rasmi.

JUMIA YARAHISISHA MANUNUZI SABA SABA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Jumia Tanzania

Wateja wanaoshiriki katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Kibiashara ya Sabasaba mwaka 2018 wamerahisishiwa kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao na kupelekewa bidhaa zao mpaka wanapoishi.

Imezoeleka kwa kawaida wateja wanapokwenda kufanya manunuzi Sabasaba huwalazimu kubeba bidhaa zao. Jambo ambalo si tu huwasababishia usumbufu wa kubeba mizigo mingi, bali pia huwagharimu pesa kwa kulipia usafiri pamoja na kuhatarisha usalama wa bidhaa zao.

Safari hii mambo yamekuwa tofauti kwani Jumia imetambulisha utaratibu mpya wa kufanya manunuzi kwa wateja ambao ni salama na rahisi zaidi kuutumia.

Utaratibu wa siku zote uliozoeleka ni kwa wateja kutembelea kwenye mabanda ya wafanyabiashara na makampuni tofauti ili kufanya manunuzi kwa bidhaa wanazoziona. Hii ni kwa sababu utamaduni wa Watanzania wengi wanapofanya manunuzi mbalimbali lazima waione bidhaa yenyewe ikiwezekana kuishika, kuikagua na wengine huenda mbele zaidi hata kwa kuijaribisha ili kujiridhisha zaidi.

Sababu kubwa kwa wateja wengi nchini na Afrika kwa ujumla kufanya hivyo ni kutokana na mfumo huu kuwa mgeni, masuala ya kiusalama hususani utapeli wa mitandaoni pamoja na changamoto ya teknolojia ambapo ni maeneo machache wanayoweza kunufaika.

Inachokifanya Jumia ni sawasawa na kusema maonyesho ya Sabasaba yaliyo kwenye mfumo wa mtandaoni. Kama unavyoona mabanda ya wafanyabiashara na makampuni tofauti kwenye maonyesho, Jumia nayo imesheheni bidhaa halisi na bora kutoka kwa maelfu ya wafanyabiashara tofuati nchini. Kwa kuzisajili biashara zao kwenye mtandao wake, wateja wanaweza kupata taarifa zote za bidhaa wanazozihitaji.

Kupitia mtandao wao, wateja wanaweza kuperuzi bidhaa za wafanyabiashara mbalimbali kama wanavyotembelea mabanda ya Sabasaba. Wateja wanaweza kuona bidhaa, maelezo yake, bei na kununua papo hapo na kisha kupelekewa mpaka alipo. Faida kubwa wanayojipatia kupitia mfumo huu ni kwamba malipo ya manunuzi yote hufanyika pale bidhaa zinapowafikia.

Wateja waliotembelea na wanaoendelea kutembelea Sabasaba watakuwa wamepata kitu kipya kwamba kwa dunia tunayoishi sasa unaweza kufanya manunuzi na kisha usionekane ukiwa umebeba mzigo wowote.

Katika msimu huu ambao Jumia inasherehekea miaka 6 ya huduma zake barani Afrika, wametoa ofa kemkem ikiwemo huduma ya bure ya usafiri. Hii itakuwa ni kwa wateja watakaonunua bidhaa za kuanzia shilingi 100,000 na kuendelea.

TONY ELUMELU FOUNDATION HOSTS INTERACTIVE SESSION WITH MACRON AND 2000 YOUNG AFRICAN ENTREPRENEURS

$
0
0

President Macron at TEF Interactive Session 4: The President of the French Republic, Mr. Emmanuel Macron and Founder, Tony Elumelu Foundation and Chairman of UBA Group, Mr. Tony O. Elumelu listening to an entrepreneur at the interactive session with President Macron and young African entrepreneurs hosted by the Tony Elumelu Foundation, in Lagos on Wednesday.
President Macron at TEF Interactive Session 3: The President of the French Republic, Mr. Emmanuel Macron and the Founder, Tony Elumelu Foundation and Chairman, UBA Group, Mr. Tony O. Elumelu addressing young African Entrepreneurs at the interactive session hosted by the Tony Elumelu Foundation for President Macron and young African entrepreneurs in Lagos on Wednesday
President Macron at TEF Interactive Session 2: The President of the French Republic, Mr. Emmanuel Macron discussing with the Founder, Tony Elumelu Foundation and Chairman, UBA Group, Mr. Tony O. Elumelu during an interactive session hosted by the Tony Elumelu Foundation for President Macron and young African entrepreneurs in Lagos on Wednesday.
President Macron at TEF Interactive Session 1: The President of the French Republic, Mr. Emmanuel Macron and the Founder, Tony Elumelu Foundation and Chairman, UBA Group, Mr. Tony O. Elumelu at the interactive session hosted by the Tony Elumelu Foundation in Lagos on Wednesday.


LAGOS, NIGERIA, 4 July 2018 – French President Emmanuel Macron offered a bold and new vision of France’s relationship with Africa, speaking at an exclusive session hosted by the Tony Elumelu Foundation in Lagos today. He passionately advocated a new partnership, prioritizing the role of entrepreneurship in driving Africa’s renaissance, highlighting the importance of the private sector and most importantly saying Africa’s future was and should be in Africa’s hands.

Macron spoke at a vibrant, no-holds barred interactive session, in front of nearly 2,000 alumni of the Tony Elumelu Foundation, who sought advice from the youthful President on how to grow their businesses, reach European markets amidst rising nationalism and emerging trade wars and the secrets of his political success. Macron’s experience as an outsider, who transformed French politics and spoke directly to and not at the audience, electrified the room.

“To young African entrepreneurs: never listen to people who are telling you to wait,” Macron said. “If you believe in your projects: just do it. Our role is to help the new generation to seize opportunities and rise to the challenge. This is what underpins a new, balanced relationship.”

TEF Founder and Chairman of Heirs Holdings and United Bank for Africa (UBA), Tony O. Elumelu, CON moderated the event and opened by acknowledging the importance of the occasion for African entrepreneurship: "The French President recognises the critical importance of African entrepreneurs to sustainable economic development on the continent – he knows the African narrative is changing and will change. His voice is refreshing and welcome” he said. “We want France and the rest of the world to realise that Africa is a continent of opportunities.”

The two leaders stood side-by-side, surrounded by emerging and established business women and men from across Africa, during an exciting and at times charged session. Concluding the event, TEF signed an agreement with the Agence Française de Développement (AFD), the French development bank. Theagreement established a research partnership to examine the entrepreneurship ecosystem in West Africa, with a special focus on francophone countries, a risk-sharing guarantee framework and access to high-level mentors for TEF entrepreneurs.

Video of the session is available at http://www.tonyelumelufoundation.org/news/interactive-session-with-president-emmanuel-macron-and-tony-elumelu-entrepreneurs/

NEWZ ALERT: KIONGOZI MBIO ZA MWENGE AGOMA KUZINDUA JENGO LA ZAHANATI MSASANI

$
0
0
 
Kiongozi wa mbio za mwenge Charles Francis amegomea kuzindua jengo la Zahanati ya Mkoroshini (pichani) ilioyopo Msasani jijini Dar es Salaam kutokana na kutokidhi viwango vya ujenzi vya jengo hilo.

Vilevile limekuwa na gharama za juu kwenye ujenzi wa jengo hilo ambapo amewataka TAKUKURU kufuatilia suala hilo kwa undani ili kubaini yaliyomo ndani ya ujenzi huo na gharama kwa ujumla.

KATIBU MKUU WA CCM DKT BASHIRU ATEMBELEA BANDA LA NSSF SABASABA

$
0
0
Katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi CCM ,Dk Ally Bashiru akimsikiliza Afisa  Matekelezo wa NSSF  Kassim Mfunda aliyekuwa akitoa maelezo na taratibu namna ya wanachama wanavyoweza kujiunga na shirika hilo na kujipatia huduma mbalimbali zikiwemo za Mafao.
Afisa huduma kwa wateja  Riziki Kibwasali akimpatia zawadi Katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Ally Bashiru ,pembeni yake ni Afisa Uhusiano wa NSSF Angella Msangi.Kushoto ni Mkurugenzi  wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade) ,Edwin Rutegaruka akishuhudia tukio hilo
Afisa Uhusiano  wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF Angella Msangi akitoa maelezo ya huduma mbali mbali zinazofanywa na shirika hilo kwa katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dk Ally Bashiru alipotembelea kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa yanayoendelea  jijini Dar es salam,pembeni ni Afisa mkuu  matekelezo kitengo cha Hiari,Abas Cothema

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM ZANZIBAR

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameongoza kikao Cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar katika ukumbi wa mikutano Afisi Kuu CCM Zanzibar.

Kikao hicho kilichobeba ajenda kuu mbili, ambazo ni Mapendekezo ya Kupiga Kura za maoni katika uchaguzi wa Jimbo la Jang’ombe na Mapendekezo ya Wanachama wa CCM wanao omba kuteuliwa kugombea nafasi ya Uwakilishi jimbo la Jang’ombe.

Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Dkt. Ali Mohammed Shein yupo safarini nje ya nchi hivyo wajumbe walimchagua Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa muda na kuongoza kikao hicho.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kwenye ukumbi wa Afisi Kuu Zanzibar, kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe.Balozi Seif Idd na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Sadalla. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisoma Ilani ya Uchaguzi ya CCM wakati kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kwenye ukumbi wa Afisi Kuu CCM Zanzibar, kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe.Balozi Seif Idd
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Sadalla akisoma ajenda zitakazojadiliwa kwenye Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar. 
 Wajumbe waliohudhuria Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Heads of State Owned Enterprises meet on Industrialisation Agenda

$
0
0
The Minister of Finance and Planning, Hon. Dr. Philip Mpango will officiate a National Roundtable Dialogue on “The Role of State Owned Enterprises (SOEs) in Implementing the Industrialisation Agenda” today. 

This one-day event is organised by UONGOZI Institute in collaboration with the Office of the Treasury Registrar in the Ministry of Finance and Planning. 

According to a statement released by UONGOZI Institute, the meeting aims to bring heads of State Owned Enterprises together to examine the role of SOEs and their contribution in the implementation of the industrialisation agenda. 

A keynote presentation by Dr. John Page, Senior Fellow in the Global Economy and Development Program at the Brookings Institution in Washington, D.C will be delivered at the event, with subsequent presentations and discussions focusing on lessons from other countries, how SOEs can take advantage of the opportunities emerging during the process of industrialization, and how SOEs can meet the challenges arising from the process of industrialization. 

Over 60 Board Chairpersons and Chief Executives of State Owned Enterprises are expected to participate in the dialogue.

VIGOGO WATANO WA KNCU LTD,TCCCO WAFIKISHWA MAHAKAMANI LEO KWA MASHTAKA YA UHUJUMU UCHUMI

$
0
0
Na Dixon Busagaga,Moshi

VIONGOZI watano wa Chama cha Ushirika mkoa wa Kilimanjaro(KNCU LTD) na Kiwanda cha Kukoboa Kahawa cha Tanganyika (TCCCO) leo wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ,Moshi na kusomewa Mashtaka tofauti yakiwemo ya uhujumu Uchumi.

Waliofikishwa Mahakamani na kupandishwa Kizimbani ni pamoja na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Kikuu cha Ushirika ,Kilimanjaro (KNCU) Aloisi Kitau (70) Makamu Mwenyekiti mstaafu wa KNCU,Hatibu Mwanga(70) na Meneeja Mkuu wa KNCU ,Honest Temba (38).

Wengine waliofikishwa mahamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi ,Pamela Mazengo ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Kukoboa Kahawa (TCCC0) Maynard Swai (57) na aliyekuwa Meneja Mkuu wa TCCCo ,Andrew Kleruu wanaotajwa kukiuka sheria wakati wa ununuzi wa mtambo wa kukoboa Kahawa.

Wakili wa serikali Jaqueline Nyantori aliieleza mahakamani kuwa Washitakiwa ,Maynard Swai na Andrew Kleruu wanakabiliwa na makosa mawili huku akiyataja kuwa ni Matumizi mabaya ya ofisi na kusababishia serikali hasara .

Upande wa Jamhuri katika Shauri hilo unawakilishwa na Wakili wa serikali Mandamizi ,Shadrack Martin,Wakili wa serikali Mwandamizi ,Abdalah Chavula na Wakili wa serijali Jacqueline Nyantori huku Wakili Julius Semali akimtetea Mshtakiwa Honest Temba na Wakili Captain Sawayaeli Shoo akimtetea Mshtakiwa Hatibu Mwanga.



Watuhumiwa hao wakishushwa Mahakamani mapema leo chini ya Ulinzi wa Jeshi la Polis,kusomewa mashtaka yao

MAMA SALMA AWANYOSHEA KIDOLE WAZAZI, WALEZI WANAOWAFUNGIA NDANI WATOTO WENYE ULEMAVU, ATAKA WAPEWE HAKI ZAO

$
0
0


Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAZAZI na Walezi nchini wameshauriwa kutowafungia ndani watoto wenye ulemavu wa aina yoyote ile na badala yake wahakikishe wanaacha watoke nje na kubwa zaidi wapatiwe haki zao za msingi ikiwamo ya elimu.

Amesema watoto wenye ulemavu wakiwezeshwa wanaweza kufanya mambo makubwa yakiwamo ya kutimiza ndoto zao, hivyo kuwafungia ndani ni kuwanyima haki zao za msingi, hivyo jamii yenye tabia hiyo ni vema wakaiacha.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Mke wa Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) wakati akizungumza na walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mchanganyiko Kariakoo jijini Dar es salaam.

Mama Salma alikuwa mgeni rasmi katika tukio la kukabidhi msaada wa vifaa vya kufundisha zikiwamo Laptop maalum kwa wanafunzi wenye ulemavu waliopo shuleni hapo. Msaada huo umetolewa na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasem Al-Najem.Hivyo Mama Salma ametumia nafasi hiyo kuwashauri wazazi na walezi ambao wana watoto wenye ulemavu wa aina yoyote ile kutowafungia ndani.

“Kitendo cha kumfungia mtoto ndani kwasababu ya ulemavu alionao si jambo nzuri na wala halimpendezi Mwenyezi Mungu kwani mtoto hakuomba kuwa alivyo.Pia kumfungia mtoto ndani unamfanya ashindwe kukua kutokana na kukosa miale ya jua na hasa ya nyakati za asubuhi.

“Nitoe rai watoto wenye ulemavu waachwe wawe huru na wapewe haki zao za msingi ikiwamo elimu ambayo ndio msingi wa maendeleo yake ambayo yatamfanya atimize ndoto yake.Tuwaendeleze watoto wenye ulemavu kufikia malengo yao,”amesema Mama Salma.

Kuhusu msaada ambao umetolewa na Balozi Al-Najem ,wenye jumla ya thamani ya zaidi ya Sh.milioni 80,Mama Salma amesema amefurahishwa na msaada huo ambao kimsingi unakwenda kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum.Amesema yeye aliona haja ya kuhakikisha wanafunzi hao wanasaidiwa hivyo kupitia Balozi wa Kuwait wakafanikiwa kuupata msaada huo wa vifaa.Hivyo amesema kutokana na msaada huo ametoa amri kwa wanafunzi hao kusoma kwa bidii.

Kwa upande wa Balozi Al-Najem amesema msaada huo kwao wanautafsiri ni zawadi ambayo imetolewa na wananchi wa Kuwait kwa wanafunzi hao kama sehemu ya kutambua kundi la wanafunzi wenye uhitaji maalumu nchini.“Zawadi hii imetokana na ushirikiano kati ya Kuwait na Wama ambayo Mwenyekiti wake ni Mama Salma Kikwete.Ni jambo la kushukuru kuona tunatoa zawadi kwa wanafunzi wa shule hii.Jumla ya thamani ya zawadi hii ni Sh.milioni 80,”amesema.

Wakati huo huo Mwalim Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko Anna Mshana amesema wanashukuru kwa msaada huo na kutoa ombi kwa ubalozi huo na Mama Salma kuendelea kusaidia kwani bado wana uhaba wa vifaa vya kufundishia wanafunzi hao wenye ulemavu.

 Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al- Najem, akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa  mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi  walemavu  shule katika shule ya  Msingi Uhuru Mchanganyiko, vyenye thamani ya shilingi milioni 80.picha na Emmanuel Massaka (Globu ya jamii).
 Balozi wa Kuwait nchini,  Jasem Al- Najem na Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mama Salma Kikwete,wadau mbalimbali wa elimu wakikagua vifaa hivyo walivyo vikabidhi katika shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko vitakavyo wasaidia walemavu katika masomo yao,jana jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akizungumza  katika hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo.

WANANCHI WA MIKUMI WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI

$
0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Selemani Jafo akiongea viongozi wa wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
Waziri wa Nchi, Ofisi Rais, Tawala za Mikoa na Serikali Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Mikumi juu ya utekelezaji wa ahadi ya Rais Magufuli ya ujenzi wa Kituo cha Afya.
Ukaguzi wa jengo la zahanati inayotumika kwasasa eneo la Mikumi.
Wananchi wa Mikumi walipokuwa katika mkutano wa hadhara.



Wananchi wa Mikumi wamemwagia sifa Rais Dk.John Magufuli kwa kusikia kilio chao cha kukosa huduma za afya.

Wananchi hao wamemwaga sifa kwa Rais Magufuli wakati Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo alipombelea zahanati ya Mikumi na kuzungumza na wananchi wa mikumi.

Katika ziara hiyo,Waziri Jafo amewataarifu wananchi hao kwamba serikali inaanza ujenzi wa kituo cha afya Mikumi ambacho kiliahidiwa na Rais Magufuli alipokuwa katika ziara mkoani Morogoro.

Kituo hicho kimeshapokea shilingi milioni 400 ambapo ujenzi wa majengo muhimu unatarajiwa kuanza ndani ya wiki moja kuanzia sasa kwa kutumia utaratibu wa force account.

Kufuatia habari hiyo, Wananchi wa Mikumi wameishukuru Sana serikali ya awamu ya tano kwamba Rais Magufuli na serikali yake imejipambanua katika kuwahudumia wananchi wanyonge.

TUMEANZA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA WAZIRI MKUU KWA VITENDO-RC MASENZA

$
0
0
Na Francis Godwin Michuzi Blog, Iringa 

MKUU wa mkoa (RC) wa Iringa Amina Masenza amesema kuwa mkoa wake umeanza utekelezaji wa agizo la waziri mkuu Kasimu Majaliwa la kutaka wanaume kupimwa virusi vya UKIMWI ili kupunguza kasi ya maambukizi ya  VVU nchini.

Akizungumza leo katika ukumbi wa siasa ni kilimo mara baada ya kuwaongoza wadau wa maendeleo mkoani Iringa walioshiriki kikao cha mikakati ya utekelezaji wa agizo la waziri mkuu kupima VVU ,Masenza alisema kuwa zoezi la upimaji wa VVU kwa wanaume mkoani Iringa litasaidia kuwatambua wale ambao wameambukizwa na kuanzishiwa dawa za ARVs huku wale ambao hawajaathirika kujikinga na VVU.

Alisema kuwa michango ya wajumbe wa kikao hicho iliyotolewa ya kutaka wanaume kuhamasishwa kupima VVU kwa hiari majumbani kwao ni michango ambayo itasaidia kufikia malengo ya mapambano dhidi ya UKIMWI iwapo wanaume wote mkoani hapa wataonyesha ushirikiano katika zoezi hilo pindi litakapo anza .

Alisema kuwa taarifa za mganga mkuu wa mkoa wa Iringa zinaonyesha tatizo la UKIMWI bado kubwa ndani ya mkoa na kuwa pamoja na ukubwa wa tatizo ila bado kuna wadau wengi wa mapambano ya UKIMWI .

Kuwa kampeni ya kitaifa ya upimaji wa VVU na utoaji wa dawa za kupumbaza VVU iliyozinduliwa na Juni 19 mjini Dodoma na waziri mkuu imekwenda sanjari inajumuisha na usemi usemao Furaha yangu pima jitambue hivyo kampeni hiyo itanaza kwa wanaume na baadae makundi mengine katika jamii .

Kuwa makundi hayo ni pamoja na mabinti wa miaka kuanzia 15 hadi 21 ,wanawake wajawazito na wengine wote na kuwa njia pekee ya kufanikisha kampeni hiyo ni wananchi wote kujitokeza kupima VVU .

Alisema kuwa hali ya VVU ni mbaya nchini kwani kitaifa asilimia 52.2 ya watu wanaoishi na VVU hawajui kama wanaishi na VVU na kuwa hali hiyo inachangiwa na wanaume ambao kiwango chao cha upimaji ipo chini sana kwa kuwa na asiimia 45.3 ukilinganisha na asilimia 55.9 ya wanawake .

Hivyo alisema umefika wakati kwa kampeni za upimaji kuelekezwa kwa wanaume na vijana wote na kuwa hakuna sababu ya wanaume kuendekeza mfumo dume hata katika upimaji wa VVU .

Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wanawake kuwahamasisha waume zao kujitokeza kwa wingi katika kampeni ya upimaji wa VVU kwani wanaume ni kichwa cha familia lazima kuonyesha ushiriki mkubwa wa kwenda kupima VVU .

" Kwa heshima kubwa na unyenyekevu usio na kiwango nawaombeni sana wanaume wote vijana wote na akina mama nendeni mkapime VVU ili kuanzishiwa dawa kwa wale ambao watakutwa wameathirika furaha yako ipo kwenye kupima ukijitambua utaishi kwa raha lakini mtambue ninyi wakina baba ndio ambao mnatuchanganya hamuachi kuwa na nyumba ndogo "

Wanawake tunaomba mseme nao wanaume kwa upore na kuwashauri kuitikia wito wa kupima VVU kwa siri majumbani kwao ama kujitokeza katika vituo vya afya na katika hospitali zetu .

Alisema kuwa mkoa wa Iringa ni wa pili kwa maambukizi ya VVU ukiongozwa na mkoa wa Njombe ambao unaongoza kitaifa na kuwa si sifa nzuri kwa mkoa kuongoza kwa maambukizi ya VVU na hivyo kusudio la mkoa ni kuona wanashuka katika kasi hiyo na kufikia asilimia 0.03.

Hata hivyo alisema kuwa uzinduzi wa kitaifa wa kampeni ya Furaha yangu umemethibitisha kuwa serikali yetu ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli imelenga kuona wananchi wake wanakuwa na afya njema na kufanikisha azima yake ya kuelekea Tanzania ya uchumi wa viwanda na yenye watu wenye afya njema.

Kwa upande wake washiriki wa kikao hicho waliunga mkono kampeni hizo na kuwa wapo tayari kushiriki kuelimisha jamii na kuwa mfano kwa kujitokeza kupima.Mbunge mstaafu wa viti maalum mkoa wa Iringa (CCM) Lediana Mng'ong'o alisema kuwa suala la maambukizi ya VVU mkoani Iringa ni kubwa na imekuwa ikichangiwa na madereva wa malori na wanawake wanaofanya kazi ya kujiuza mitaani .

Pia alisema wapo baadhi ya wanaume wamekuwa wakikwepa kwenda kupima VVU na wakiishia kuwatuma wake zao kupima wakijua kuwa akipima mwanamke na kuonekana salama na yeye atakuwa salama .

Huku mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliam alisema kuwa zipo dhana potofu kuwa wilaya ya Mufindi imekuwa na maambukizi makubwa ya VVU kutokana na kuwa na uchumi mkubwa jambo ambalo si kweli na kuwa ulaya ina uchumi mkubwa mbona kasi ya maambukizi ya VVU ipo chini.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiongoza kupima VVU katika kikao cha mikakatiya kuanzakampeni za kupima UKIMWI kwa wanaume 
Viongozi wa mkoa wa Iringa wakiwemo wakuu wa wilaya ya Mufindi na kilolo wakionyesha karatasi baada ya kupima VVU 
Washiriki wa kikao cha kuweka mikakati ya zoezi la upimaji UKIMWI wanaume wakiwa katika kikao hicho.

SERIKALI YATOA MILL 400/- KWA AJILI YA UJENZI KWA KITUO CHA AFYA KATA YA NKENDE

$
0
0
 Na Frankius Cleophace, Tarime

SERIKALI imetoa  Sh.Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo Cha Afya katika kata ya Nkende Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara kwa lengo la kusogeza huduma ya afya karibu na Wananchi.

Huku wananchi hao wakichangia kununua eneo lenye thamani ya Sh.milioni 8 kwa lengo la upanuzi wa eneo hilo ili kuweza kufanikisha mchakato huo. 
 Akizungumzia ujenzi huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tarime Elias Ntiruhungwa amesema kuwa tayari Serikali imeshapelekal kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya kata ya Nkende.

“Mpaka nazungumza kwa sasa hivi tayari fedha zipo kwenye akaunti na hivyo nataka kuona  wiki hii kila kitu kimekamilika na ujenzi kuanza mara moja leo nimeambatana na wataalamu wote ili kumaliza  mapema shughuli hii,” amesema Elias

Pia Elias amewapongeza wananchi kujitoa kununua eneo kwa ajili ya upanuzi wa ujenzi wa kituo cha Afya na kuahidi kuendelea kushirikiana nao vyema ili kumaliza mapema ujenzi huop.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nkende Daniel Komote amesema kuwa wananchi wamewiwa ujio wa  ujenzi wa kituo cha afya na ndo maana wamejitoa kwa nguvu zao ili maeneo ya kutosha yapatikane huku akishukuru Serikali kutoa Fedha hizo.

“Nimeweza kushawishi wananchi wangu kuchangia na mimi nikiwa wakwanza kuchangia ili tununue eneo la kutosha ata kama halitatosha bado kunaeneo lingine takribani heka tisa bado tutapendekeza  eneo hilo ili kujenga Kituo cha afya kwa lengo la kunusuru Wananchi ambao ulazimika kwenda katika hospitali ya Wilaya ya Tarime,” amesema Komote.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa akiongea na Wakazi wa kata ya Nkende katika mtaa wa Magena ambapo wanatarajia kujenga kituo cha Afya baada ya Serikali kutoa kiasi cha Shilingi Milioni 400.
Zahanati ya Mtaa wa Magena ambayo inahudumia wakazi wa kata ya Nkende Halmashauri ya Mji wa Tarime.
Diwani wa kata ya Nkende Daniel Komote akiongea na Wananchi katika eneo la mtaa wa Magena ambapo wanatarajia kujenga kituo cha Afya.
Jengo linalomilikiwa na Ccm tawi la Magena ambalo wametoa eneo hilo lenye thamini ya Millioni 10 ili kujenga Kituo cha Afya

DKT. KIGWANGALLA ATEMBELEA MAPOROMOKO YA KALAMBO, AMBAYO NI YA PILI KWA UREFU AFRIKA

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa mkoa wa Rukwa wakifurahia kufika karibu na kina cha Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo yapo katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, maporomoko haya ni ya pili kwa urefu barani Afrika. Eneo hilo la kivutio linaendelea kuboreshwa kwa kujengewa ngazi maalum zinazowawezesha watalii kufika hadi kwenye kina cha maporomoko hayo. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishuka kuelekea karibu na kina cha Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo yapo katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, maporomoko haya ni ya pili kwa urefu barani Afrika. Eneo hilo la kivutio linaendelea kuboreshwa kwa kujengewa ngazi maalum zinazowawezesha watalii kufika hadi kwenye kina cha maporomoko hayo. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipanda mlima baada ya kuona Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo yapo katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, maporomoko haya ni ya pili kwa urefu barani Afrika. Eneo hilo la kivutio linaendelea kuboreshwa kwa kujengewa ngazi maalum zinazowawezesha watalii kufika hadi kwenye kina cha maporomoko hayo. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa mkoa wa Rukwa wakishuka kwenda kuona Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo yapo katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla viongozi wengine wa mkoa wa Rukwa wakinawa mikono kwenye mto kalambo ambao unatengeneza Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika katika kijiji cha Kapozwa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kapozwa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa muda mfupi baada ya kutembelea Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika. Eneo hilo la kivutio linaendelea kuboreshwa kwa kujengewa ngazi maalum zinazowawezesha watalii kufika hadi kwenye kina cha maporomoko hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia mandhari ya Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika katika kijiji cha Kapozwa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa. Eneo hilo la kivutio linaendelea kuboreshwa kwa kujengewa ngazi maalum zinazowawezesha watalii kufika hadi kwenye kina cha maporomoko hayo. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika katika kijiji cha Kapozwa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa. Eneo hilo la kivutio linaendelea kuboreshwa kwa kujengewa ngazi maalum zinazowawezesha watalii kufika hadi kwenye kina cha maporomoko hayo. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa Serikali wakishuka kwenda kuona Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo yapo katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, maporomoko haya ni ya pili kwa urefu barani Afrika. Eneo hilo la kivutio linaendelea kuboreshwa kwa kujengewa ngazi maalum zinazowawezesha watalii kufika hadi kwenye kina cha maporomoko hayo. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa mkoa wa Rukwa wakipanda ngazi baada ya kuona Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo yapo katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, maporomoko haya ni ya pili kwa urefu barani Afrika. Eneo hilo la kivutio linaendelea kuboreshwa kwa kujengewa ngazi maalum zinazowawezesha watalii kufika hadi kwenye kina cha maporomoko hayo. 
Muonekano wa eneo la kuingilia kuelekea kwenye mporomoko ya mto Kalambo.
Muonekano mwanana wa Maporomoko ya Mto Kalambo.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>