Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

WAZIRI JENISTA MHAGAMA AIPONGEZA WCF KWA KUINGIA KWENYE MFUMO WA TEHAMA KATIKA KUTOA HUDUMA KWA NJIA YA KIELEKTRONIK

$
0
0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, (wapili kushoto), Naibu Waziri wa Viwanda, Bishara na Uwekezaji, Mhe. Eng. Stella Manyanya, (wakwanza kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba wakipatiwa maelezo na wataalamu wa Mfumo wa Kielektroniki wa Mfuko huo, Bw.Uforo Henry, (wapili kulia) na Abdi Kalilo wakati Mhe. Waziri na Naibu Waziri walipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya 42 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Julai 6, 2018.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Jenista Mhagama, amefurahishwa na mwitikio wa waajiri kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) baada ya kuanza kushuhudia jinsi wafanyakazi wao wanavyonufaika na malipo ya Mafao ya Fidia.

Mhe. Waziri ameyasema hayo leo Julai 6, 2018 baada ya kutembelea banda la WCF kwenye maonesho ya 42 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere (Maarufu kama Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

“Nichukue fursa hii kuwashukuru waajiri wote nchini ambao wameitikia wito wa Serikali wa kujisajili na Mfuko kwa mujibu wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi. Nimetaarifiwa kuwa mpaka sasa jumla ya waajiri 14,855 wamesajiliwa na Mfuko. Na kinachonifurahisha zaidi ni kwamba sasa waajiri wameanza kuona manufaa ya kuanzishwa kwa Mfuko baada ya kushuhudia jinsi wafanyakazi wao wanavyonufaika na mafao yanayolipwa na Mfuko” Alisema Mhe. Waziri.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, kwa mwaka wa fedha uliomalizika (2017/2018), tayari Mfuko ulikwishalipa mafao ya jumla ya shilingi bilioni 2.3 kwa wanufaika 812.” Alisema Bw. Mshomba.

Halikadhalika Bw. Mshomba alisema Mfuko umekuwa na faida sio tu kwa wafanyakazi na waajiri lakini pia hata kwa serikali kupitia kodi, ambapo alisema Mfuko umelipa kodi serikalini kiasi cha shilingi bilioni 3.2 kama kodi kwa mwaka wa 2016/2017 na mwaka huu ulioisha Juni 2018 tunatarajia kulipa zaidi ya shilingi bilioni 5 kama kodi ya serikali.

Aidha, Mhe. Waziri Jenista Mhagama aliupongeze Mfuko na waajiri kwa kushirikiana pamoja katika kutekeleza sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, kwani mafanikio haya ni matokeo ya kufanya kazi kwa kushirikiana.

“Kama ambavyo nimekuwa nikisisitiza siku zote, nia ya serikali ni kuona majukumu yote yanayohusu fidia kwa wafanyakazi yanafanywa na Mfuko huu na hivyo kuwawezesha waajiri kubakia na jukumu la kubuni mbinu za kuongeza uzalishaji na kukuza biashara zao.  Hivyo, nitoe wito kwa waajiri ambao bado hawajajisajili na ambao hawalipi michango watekeleze wajibu wao kwa hiari bila kuchelewa.” Alisema Mhe. Waziri.

Aidha, Mhe. Waziri aliuagiza Mfuko uendelee kuchukua hatua mbalimbali za kisheria kwa waajiri ambao wataendelea kutokutekeleza wajibu wao wa kujisajili na kuchangia kwa mujibu wa sheria.

Waziri Muhagama pia aliupongeza Mfuko kwa kupanua mfumo wa utoaji huduma kwa kuanzisha matumizi ya Tehama kwa kutumia Mfumo wa kielektroniki. “Niupongeze Mfuko kwa kuwekeza katika mfumo wa kielektoniki ambayo inasaidia sana utoaji wa huduma kwa njia ya mtandao. Nimeoneshwa namna ambavyo mwajiri anaweza kujisajili, kupata hati ya usajili, kulipa michango ya kila mwezi na kupata stakabadhi kwa njia  kielektroniki. Mwajiri anaweza kupata huduma zote akiwa ofisini kwake. Haya ni mafanikio makubwa sana yaliyofikiwa na Mfuko katika kipindi kifupi cha miaka miwili ya utaoaji wa huduma. Nitoe wito kwa waajiri, kutumia mifumo hii ambayo ni rahisi kutumia na ni rafiki kwa watumiaji.” Alisema Mhe. Waziri.

Mheshimiwa Waziri aliwahimiza waajiri kuwa na taarifa sahihi za wafanyakazi wao “ili Mfuko uweze kulipa fidia bila kuchelewa, ni lazima mshirikiane katika kuhakikisha nyaraka muhimu zinazohitajika katika ulipaji wa fidia zinaufikia Mfuko kwa wakati. Nitoe rai kwa waajiri kuhakikisha wanawasilisha taarifa ya matukio ya majanga yanayotokana na kazi mapema pamoja na nyaraka muhimu zinazohitajika katika ulipaji wa fidia.

Waziri Mhagama akimsikilzia  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha Mshomba, wakati akifafanua baadhi ya mambo kwa waandishi wa habari.
 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, (kulia), akimuongoza Mhe. Waziri wakati akitembeela banda la Mfuko huo leo Julai 6, 2018.
 Waziri Jenista Mhagama, akimsikilzia Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Anselim Peter, wakati akifafanua kuhusu mfumo mpya wa Kielektroniki ambao WCF umeanza kuutumia katika kusajili na kupokea michango ya wananchama
 Maafisa wa WCF wakiwa wamesimama kwenye lango la kuingilia kwenye banda hilo tayari kupokea wananchi.

 Bw. Mshomba, (kulia), Bw. Anselim Peter (Kushoto), wakibadilishana mawazo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika, nje ya banda la WCF.
Mhe. Waziri akipokelewa wakati akiwasili kwenye banda la WCF.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge (kulia) na mwenzake wa SSRA, Bi. Sara Kibonde Msika, wakibadilishana mawazo kwenye banda la WCF.

 Abdi Kililo (kulia) kutoka kitengo cha Tehama cha WCF, akitoa maelezo kwa wananchi hawa waliotembeela banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi. Wakwanza kulia ni Afisa anayeshughulikia masuala ya Sheria wa Mfuko huo, Bi.Fransisca Kweka.
 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akiwa na Dkt.Damian Elias kutoka kitengo cha Huduma za Tiba na Tathmini Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
 Afisa Uhusoano Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Sebera Fulgence, (kushoto), akiwa na Justin Mwandumbya wa kitengo cha fedha
Maafisa wa WCF, Glady Madembwe, kutoka kitengo cha madai (Claims) (kushoto) na Afisa wa Afya na Usalama mahala pa kazi kutoka WCF, Bw. Robert Duguza (wapili kushoto), wakiwahudumia wananchi hawa waliotembelea banda la WCF.

TFDA ATOA NENO KWA WAJASIRIAMALI NCHINI, YAWAKUMBUSHA KUJISAJILI

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Agnes Kijo akizungumza na wajasiriamali wa bidha za Chakula katika Banda la Mfuko wa Fursa kwa Wote katika Maonesho ya 42 ya Biashara Kimataifa katika Viwanja vya Mwalim Julius Nyerere kijiji Dar es Salaam.
SAMSUNG CAMERA PICTURES
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Agnes Kijo akingalia moja ya bidhaa katika banda la Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote wakati alipotembelea maonesho ya Sabasaba.
SAMSUNG CAMERA PICTURES
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Agnes Kijo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Mamlaka hiyo .
..........................................................
MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) imewahimiza wajasiriamali kuhakikisha katika mamlaka hiyo kwa lengo la kutambulika na hatimaye kuwa na uhakika wa kuuz bidhaa zao mahali popote.
Pia imewashauri wajasiriamali nchini kutafuta maalumu ambalo litatumika kwa ajili ya kuuza bidhaa zao na hiyo itawafanya wanaohitaji kununua bidhaa kutambua mahali walipo na kufika kwa urahisi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Agnes Kijo baada ya kutembelea mabanda mbalimbali yaliyopo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Amesema ujumbe wake mkubwa kwa wajasiriamali wa ndani ambao amewatembelea kwenye mabanda yao ni kuwataka kujisajili TFDA na kufafanunua gharama ya kujisajili ni Sh.50,000.Pia amesema amewahimiza wajasiriamali hao kuangalia namna ya kuwa na eneo moja ambalo watapanga bidhaa zao mbalimbali kwani kufanya hivyo kutasaidia kutambulika waliko na hatimaye kufanyabiashara.

“Tunahimiza wajasiriamali kujisali maana bidhaa inapokuwa inatambulika na TFDA na TBS inasaidia kumfanya anayehitaji kuinunua kuwa na uhakika na ubora na usalama wa bidhaa,”amesema.Ameongeza kikubwa ambacho kimemfurahia ni namna ambavyo wajasiriamali wamekuwa na muamko mkubwa kuhusu TFDA na majukumu yake na wengi zaidi wamejisajiri tayari.

Pia amewashauri Watanzania kupenda na kuthamini bidhaa za ndani kwani hiyo itawasaidia kuwainua kiuchumi wa wajasiriamali nchini.Amefafanua kuwa kwa sasa wananchi walio wengi wameanza kuthamini vya ndani na kutoa mifano mbalimbali lakini akashauri kuthamini huko sasa kuende na kwenye bidhaa.
Pia amewahimiza wajasiriamali nchini ambao wanataka kusajili bidhaa zao kufika kwenye ofisi za TFDA ambazo zipo katika kanda saba na kwamba wakifika katika ofisi hizo watahudumiwa vizuri kwani jukumu lao ni kuwahumia Watanzania.

NSSF WASHAURIWA KUWEKA DIRISHA LA KUHAMASISHA WANAUME KUPIMA UKIMWI NSSF WASHAURIWA KUWEKA DIRISHA LA KUHAMASISHA WANAUME KUPIMA UKIMWI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama akizungmza na Bw. Charles Lyimo mwanachama wa Shirika la Taifa la Hafadhi ya Jamii (NSSF) huku akiwa amembeba Mtoto Martin Lyimbo aliyemkuta katika banda la hilo wakati alipotembelea kwenye maonesho ya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam na kukagua shughuli mbalimbali za (NSSF) leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa (NSSF) Godius Kahyarara wakati alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo, Kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Injinia Stella Manyanya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama na Mkurugenzi Mkuu wa (NSSF) Godius Kahyarara wakimsikiliza Kaimu Meneja wa Uhusiano na Masoko Shirika la Hifadi ya Jamii (NSSF) Bw. Salim Khalfan wakati akitoa maelezo kwa waziri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama na Mkurugenzi Mkuu wa (NSSF) Godius Kahyarara wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa vitengo (NSSF).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Injinia Stella Manyanya na Mkurugenzi Mkuu wa (NSSF) Godius Kahyarara wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa (NSSF).



SHIRIKA la Taifa la Hafadhi ya Jamii (NSSF) wameshauriwa kutumia Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaa kuhamasisha wanaume wanaofika katika maonesho hayo kupima Virusi vya Ugonjwa wa UKIMWI (VVU).

Ushauri huo umetolewa leo na Waziri wa Sera, Kazi, Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama, wakati anazungumza na uongozi pamoja na wafanyakazi wa NSSF baada ya kutembelea banda la shirika hilo ili kujionea shughuli ambazo zinatekelezwa na shirika hilo.Waziri Mhagama pamoja na kutoa pongezi kwa NSSF kutokana na juhudi ambazo wanazifanya katika kuwahudumia Watanzania pamoja na kuunga mkono juhudi za ujenzi wa viwanda nchini kwa kujenga kiwanda cha sukari kilichopo Mbigili mkoani Morogoro ni vema wakaweka dirisha kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kupima Vrusi vya UKIMWI.

“Niwapongeza NSSF kwa kazi nzuri ambayo mnaifanya nchini. Hata hivyo nitoe rai kwenu ni vema mkaweka na dirisha kwa ajili ya kuhamasisha wanaume kupima Virusi vya UKIMWI..Hivi karibuni Wazir Mkuu wetu Kassim Majaliwa amezindua kampeni ya kuhamasisha wananchi na hasa wanaume kupima Ukimwi. Hivyo niwaombe hata wanaume ambao wanakuja katika maoneshao nao wapime VVU.

“NSSF wekeni dirisha ambalo litatoa huduma hiyo na niwaombe wanaume ambao watakuja wapime na Ukimwi (VVU) .Tunataka watu kujitambua,”amesisitiza.Amefafanua kumekuwa na tabia ya wanaume wengi kuwaachia wanawake wapime na kisha wao wanachokifanya wanauliza tu kuhusu majibu ya vipimo.

“Lazima wanaume nao wapime Virusi vya UKIMWI badala ya kuacha mwanamke apime peke yake,”amesema Wazir Mhagama na kuongeza kuwa pamoja na kutoa ushauri huo kwa NSSF kuwa na dirisha la kupima Ukimwi anatambua juhudi zao katika kuwatumia Watanzania.Ametumia nafasi hiyo kufafanua kuwa NSSF kutokana na namna ambavyo wmaejipanga vema wamefanikiwa kujiimarisha na ni shirika ambalo linaweza kujiendesha kwa miaka 70.

“NSSF limeamua kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo na kwa mazingira ya aina hiyo lazima nitoe pongezi nyingi kwenu.NSSF mmethibitisha kwa vitendo namna ambavyo mnatekeleza kauli mbiu ya ujenzi wa viwanda nchini kwa vitendo,”amesema Waziri Mhagama.Kwa upande wa Mkurugenzi wa NSSF Profesa Godius Kahyarara amesema kuanzia kesho wataweka dirisha ili kuhamasisha upimaji Ukimwi na yeye atakuwa wa kwanza kupima.

MIFUGO ITAKAYOKAMATWA KWENYE MAENEO YA HIFADHI ITATAIFISHWA BILA YA HURUMA - DK. KIGWANGALLA

$
0
0

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Mhe. Said Mtanda (kushoto) alipowasili wilayani hapo jana kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja  ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Rukwa. Kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa, Albinus Mugonya.

Na Hamza Temba, Nkasi Rukwa
...............................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametangaza zoezi rasmi la kuanza kutaifishwa mifugo itakayokutwa kwenye maeneo ya hifadhi nchini kinyume cha sheria ili kukomesha vitendo hivyo.

Dk. Kigwangalla ametoa tamko hilo jana alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kizi kinachopakana na Pori la Akiba Lwafi lililopo wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani humo .

Amesema Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009, Kifungu cha 111 kinaruhusu kutaifisha mifugo na mali itakayokamatwa hifadhini. 

Amesema kwa kipindi cha miezi tisa tangu ateuliwe kuiongoza wizara hiyo amekuwa akitoa msamaha kwa wnanchi wanaakamatwa na mifugo hifadhini jambo ambalo kwa sasa hatofanya tena kwakuwa elimu imeshatolewa vya kutosha.

"Maeneo ya hifadhi sio shamba la bibi lisilokuwa na mwenyewe, ni lazima watu waheshimu sheria za uhifadhi, nawahakikishia tukiwakuta kwenye maeneo ya hifadhi, tutawakamata na kutaifisha mifugo yenu, hakutakuwa na huruma wala msalia mtume" alisisitiza Dk. Kigwangalla.

Wakati huo huo Dk. Kigwangalla ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kuwasilisha ahadi iliyotolewa na Waziri aliyemtangulia ya shilingi milioni 3 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Kizi. Pia ameiagiza mamlaka hiyo kuchangia mabati kwa ajili ya darasa moja katika kijiji hicho ili wananchi wanufaike na faida inayopatikana kwenye uhifadhi. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Mhe. Said Mtanda (kushoto) alipowasili wilayani hapo jana kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja  ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Rukwa.

Dk. Kigwangalla akizungumza katika mkutano huo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda (wa tatu kulia) wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani Nkui alipotembelea msitu wa Mfiri ambao ni chanzo cha maji yanayonyesha mji wa Namanyere wilayani Nkasi wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja  kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Rukwa.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kizi wilayani Nkasi wakati wa ziara yake ya siku moja kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Rukwa.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa TAWA, Imani Nkuwi (wa pili kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Pori la Akiba Lwafi alipotembelea maporomoko ya Ntembwa (pichani nyuma) ambayo ni kivutio cha utalii katika pori hilo wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya Nkasi mkoani Rukwa jana. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kushoto waliosomama) na Kaimu Mkurugenzi wa TAWA, Imani Nkuwi (wa pili kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Pori la Akiba Lwafi alipotembelea maporomoko ya Ntembwa (pichani nyuma) ambayo ni kivutio cha utalii katika pori hilo wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya Nkasi mkoani Rukwa jana. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia mandhari ya Pori la Akiba Lwafi alipotembelea maporomoko ya Ntembwa (pichani nyuma) ambayo ni kivutio cha utalii katika pori hilo wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi wilayani Nkasi mkoani Rukwa jana.

Rais Magufuli afanya uteuzi wa Mkuu wa Chuo na wenyeviti watatu

JAFO AWAAGIZA WATAALAM BAGAMOYO KUTUNZA VIFAA TIBA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo amewaagiza wataalam wa sekta ya afya wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kutunza vifaa tiba vilivyotolewa kwa msaada kutoka Taasisi ya Dhi Nurein Foundation.

Taasisi hiyo imesaidia ujenzi wa jengo la dharula, wodi ya wazazi, pamoja na vifaa mbalimbali vya afya ambapo Mradi huo umegharimu zaidi ya Sh.Milioni 900. Hatua hiyo ya taasisi hiyo ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa wilaya ya Bagamoyo na maeneo mengine hapa nchini. 

Akizungumza katika uzinduzi wa Mradi huo kwa niaba ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Jafo amesema taasisi hiyo inaungana na taasisi zingine hapa nchini zinazosaidia miradi mbalimbali na kuagiza vifaa hivyo kulindwa na kutunzwa bila kupoteza. 

Jafo amesema kuna baadhi ya watu wachache hapa nchini wasio waadilifu wamekuwa na tabia ya kuchukua vifaa vizuri vya hospitali na kuvihamishia katika hospitali zao binafsi. Wakati huo huo, Waziri Jafo amewapongeza sana Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, pamoja na Mbunge wa Bagamoyo Shukuru Kawambwa kwa kufanikisha upatikanaji wa mradi huo.

Pia Jafo amewaomba wananchi wajiunge katika mifuko mbalimbali ya bima ya afya ikiwemu CHF iliyo boreshwa ili waweze kupata huduma bora ya matibabu wao na familia zao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiongea na wananchi wa Bagamoyo
Dkt. Saleh kutoka nchini Saudia kutoka taasisi iliyofadhili mradi huo akitoa maelezo ya mradi kwa Waziri wa Tamisemi Mhe. Selemani Jafo.
Wananchi wa Bagamoyo wakiwa katika mkutano wa uzinduzi wa Mradi wa afya ya mama na mtoto katika hospitali ya wilaya ya Bagamoyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja mjini Bagamoyo.

GRACE PRODUCTS ATAJA SABABU ZA KUTWAA TUZO YA THE INTERNATIONAL QUALITY SUMMIT AWARDS

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MSHINDI wa tuzo ya The International Quality Summit Award amewataka watanzania kupenda vitu vya nyumbani kwa sababu ni bidhaa zinazotengenezwa kwa malighafi asili na kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ya Tanzania kwenda uchumi wa Viwanda.

Mwishoni mwa Mwezi wa June,Dr Elizabeth Kilili aliweza kunyakua tuzo ya International Quality Summit Awards iliyofanyika nchini Marekani akiwapiku nchi 116 kutoka duniani kote.

Akizungumza na Globu ya Jamii katika maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Sabasaba, Mkurugenzi Mtendaji Dr Elizabeth amesema kuwa ameweza kufanikiwa kupata tuzo hiyo kwa sababu alibuni na kuthubutu kutengeneza vipodozi akiwa hajanakili au kukopi kutoka kwa mtu yoyote na zaidi amekuwa anatumia vitu vya kiasili kuvitengengeza.

Dr Elizabeth amesema kupitia kampuni yake ya Grace Natural Products ametengenza vipodozi bora na vimewasaidia watu wengi sana hususani wale waliotumia bidhaa za kemikali (sumu) na watakapoanza kutumia bidhaa zake huwasaidia kwa asilimia kubwa.

Amesema, moja ya sababu iliyoweza kumpatia tuzo hiyo ni namna alivyoweza kutengeneza vipodozi vya kiasili kwa ajili ya walemavu wa ngozi (albinism) na vimekuwa msaada mkubwa sana kwa matumizi yao ya ngozi kwakuwa na vimekuwa vikiuzwa kwa bei nafuu zaidi huku zikipata mjini na vijijini.

Dr Elizabeth ameeleza kuwa vipodozi vyake anatengeneza kwa kutumia mazao ya nyuki, matunda na mafuta ya asili ambayo hayana madhara kwa ngozi ya mtu yoyote bali itamfanya mtumiaji kuwa na ngozi nzuri na kuvutia.

Akizungumzia muitikio wa wananchi kwenye maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba kwa mwaka huu yamekuwa sio mkubwa sana tofauti na miaka mingine ila ameweza kupokea pongezi mbalimbali kutoka kwa watanzania waliofika kwenye banda lake.

Grace Product iliyoanza kazi miaka 10 iliyopita imeweza kuleta ushindani mkubwa katika soko la vipodozi na kufanikiwa kuwavutia watu wengi katika matumizi akiwa anatengeneza mafuta ya watoto, mafuta ya nywele, sabuni za kuogea, dawa za kusafishia choo pamoja na Shampoo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Grace Natural Products Dr Elizabeth Kalili akionesha tuzo yake ya The International Quality Summit Awards katika banda lake kwenye maonyelakeya 42 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Grace Natural Products Dr Elizabeth Kalili akiwaonyesha bidhaa kwa wateja waliojitokeza katika banda lake lililopo ndani ya Jengo la Sabasaba Hall kwenye maonyelakeya 42 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba.

IGP AFUNGA MAFUNZO YA POLISI WANAMAJI

$
0
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akifuatilia kwa kutumia darubini mazoezi kwa vitendo katika Ziwa Viktoria Mwanza yaliyokuwa yakioneshwa na askari waliohitimu mafunzo katika Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza.Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bi. Mary Tesha.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na wanafunzi waliohitimu mafunzo katika Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza baada ya kuangalia Onesho lao la utayari katika ukanda wa Ziwa Viktoria Mwanza. (Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bi. Mary Tesha wakati wa ufungaji wa mafunzo ya Polisi Wanamaji yaliyokuwa yakiendeshwa katika Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza (Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akifanya mazoezi mafupi na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Mwanza baada ya Askari hao kuonyesha zoezi lao la utayari wakati wa Ziara ya IGP mkoani humo (Picha na Jeshi la Polisi).
Askari Polisi wakionesha umahiri wao wa kupambana na wahalifu kupitia kwa vitendo katika Ziwa Viktoria Mwanza wakati wa kufunga mafunzo yao katika Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza.

JITIHADA ZA UFUFUAJI NA UENDELEZAJI VIWANDA ZA ZAA MATUNDA MBEYA, WAKULIMA, WAWEKEZAJI WAPONGEZA

Rais Magufuli amteua Jenerali Mstaafu Mwamunyange kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA

SERIKALI KUPAMBANA NA WABADHIRIFU KWENYE VYAMA VYA USHIRIKA - DKT TIZEBA

$
0
0

Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Tanzania linalofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Leo 6 Julai 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Baadhi ya wananchi pichani wakimsikiliza Mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Tanzania linalofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Leo 6 Julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Tanzania linalofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Leo 6 Julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisikiliza maelezo ya utunzaji fedha mara baada ya kutembelea banda la Mfuko wa kuendeleza sekta ya fedha Tanzania wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Tanzania linalofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Leo 6 Julai 2018.

Na Mathias Canal-WK, Mwanza


Serikali imetangaza Kiama kwa viongozi na baadhi ya watendaji wa vyama vya ushirika waofanya ubadhilifu wa Mali za ushirika kwa manufaa yao pekee pasina kuwanufaisha wanachama wote.


Imeelezwa kuwa ubadhilifu wa rasilimali za ushirika unaofanywa na baadhi ya viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika umekuwa ni tatizo sugu na hata kuwakatisha tamaa baadhi ya wananchi kujiunga na vyama hivyo.


Kalipio kwa wabadhilifu hao limetolewa na Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba Leo 6 Julai 2018 wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Tanzania linalofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.


Kongamano hilo la Siku mbili litaambatana na maonesho ya bidhaa na shughuli zinazofanywa na vyama hivyo vya ushirika kote nchini ambapo wanachama watapata fursa ya kubadilishana uzoefu, na kujadili mafanikio na changamoto wanazokabiliana nazo katika uendeshaji wa sekta ya ushirika nchini.


Dkt Tizeba aliwasisitiza washiriki wa kongamano hilo kutumia vizuri siku hizo mbili za kongamano hilo kwa ajili ya ustawi wa Maendeleo ya vyama vya ushirika na kujadili kwa kina namna bora ya uendeshaji na usimamizi wa vyama hivyo.


Alisema kuwa kauli mbiu ya siku ya ushirika Duniani kwa mwaka 2018 isemayo "Ushirika kwa ulaji na uzalishaji endelevu wa bidhaa na huduma" inakumbusha kwamba vyama vya ushirika sharti vihakikishe vinajitangaza na kutafuta Masoko ya bidhaa na huduma zake kwa jamii nzima.


Mhe Waziri wa Kilimo Dkt Charles Tizeba aliongeza kuwa serikali inatambua kuwa ushirika ni nyenzo muhimu ya kuwasaidia wananchi katika upatikanaji wa mtaji na kuwawezesha kuunganisha nguvu zao za kiuchumi katika kujiendeleza kiuchumi.


Alisema kuwa zipo juhudi kubwa zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanahamasishwa na hatimae kujiunga kwenye vyama vya ushirika kulingana na shughuli zao za kiuchumi ili kuondoa dhana kuwa vyama vya ushirika ni kwa ajili ya Kilimo cha Mazao ya biashara ya nchi za nje.


Sambamba na hayo Mhe Tizeba ameitaka Tume ya Maendeleo ya ushirika na shirikisho la vyama vya ushirika kuendelea kuwahamasisha wananchi kuendelea kutambua umuhimu wa kujiunga katika vyama vya ushirika kulingana na shughuli za wananchi mfano ushirika wa Viwanda, Madini, Ufugaji, Usafirishaji, Uvuvi na Kilimo.


Aliongeza kuwa serikali inatambua na kuthamini mchango wa ushirika wa Taifa katika kuyafikia malengo ya milenia na malengo mbalimbali ya nchi kama uimarishwaji wa sekta ya viwanda, Kilimo, uvuvi na biashara na kuchangia katika ongezeko la kipato kwa wananchi na hatimaye kuchangia katika ukuaji wa pato la Taifa

GAVANA WA BENKI KUU AIPONGEZA TRA KWA KUKUSANYA KODI YA MAJENGO KIELEKTRONIKI

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Prof. Florens Luoga ameipongeza TRA kwa kukusanya kodi ya majengo kwa kutumia Mfumo wa Kielektroniki.

Akizungumza wakati alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba, Prof. Luoga amesema kuwa, mfumo huo umesaidia kupunguza adha kwa wananchi ambao sasa wengi wao wanatumia simu za mkononi kulipia Kodi ya Majengo badala ya kwenda kupanga foleni benki.

"Nimefurahishwa sana na uboreshaji wa mifumo ya malipo hususani katika kulipia Kodi ya Majengo ambapo watu wengi wanatumia simu zao za mkononi kulipia kodi hiyo badala ya kwenda benki kukaa kwenye foleni. Hii ni moja ya maboresho makubwa yaliyofanywa na TRA hivyo nawapongeza sana," alisema Gavana.

Gavana Luoga ameongeza kuwa, mifumo ya malipo inapoboreshwa husaidia walipakodi kulipa kodi zao kwa urahisi na kwa wakati na hivyo kuongeza mapato ya Serikali kwa manufaa ya wananchi wote kwa ujumla.Aidha, Prof. Luoga ametoa wito kwa walipakodi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kulipa kodi kwa wakati kwa sababu maendeleo yaliyopo nchini yanatokana na kodi mbalimbali zinazolipwa na wananchi hao.

"Wito wangu kwa walipakodi na wananchi wote ni kuwasihi kuendelea kulipa kodi kwa wakati kwani faida zote wanazozipata kutokana na mfumo wa utawala waelewe kwamba umetokana na kodi mbalimbali wanazozilipa. Wanachi wanatakiwa kuelewa kwamba, upatikanaji wa elimu, maji, barabara, umeme na mambo mengine kama hayo yote yametokana na kodi," alieleza Prof. Luoga.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inashiriki maonyesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam ambapo inatoa huduma mbalimbali kama vile kusajili walipakodi, kuelimisha wananchi umuhimu wa kulipa kodi, kutoa bili na kulipa Kodi ya Majengo.

Huduma nyingine ni pamoja na kuelezea haki na wajibu wa Mlipakodi kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Huduma na Mlipakodi, kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya Mashine za Kielektroniki za kutolea Risti (EFDs), kuelezea mwenendo wa makusanyo ya mapato ya Serikali, na kupokea maoni, malalamiko, mrejesho pamoja na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wananchi.
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Prof. Florens Luoga (katikati) akisaini kitabu cha wageni  wakati alipotembelea Banda la TRA katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Prof. Florens Luoga (kulia) akimsikiliza Afisa Mwandamizi Mchambuzi Mifumo ya Biashara wa TRA, Bw. Mathias Chanila wakati akielezea shughuli zinazofanywa na Kitengo cha Utafiti na Sera mara alipotembelea Banda la TRA katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Prof. Florens Luoga (kulia) akiwaeleza jambo Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Pugu ambao pia ni Wanachama wa Klabu ya Kodi (TRA Tax Club) ya TRA mara alipotembelea Banda la TRA katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Prof. Florens Luoga (kulia) akiagana na Msimamizi wa banda la TRA Bw. Julius Caesar mara baada ya kumaliza kutembelea banda hilo katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA)

MAAFISA WA BUNGE WAENDELEA KUTOA ELIMU KWENYE MAONYESHO YA SABASABA

$
0
0
Afisa Habari wa Ofisi ya Bunge Ndg. Deonisius Simba akitoa Elimu kwa Wageni mbalimbali waliotembelea banda la Bunge la Tanzania katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam
Naibu Mpambe wa Bunge (DSA) Ndg Peter Magati akitoa Elimu kwa Wageni mbalimbali waliotembelea banda la Bunge la Tanzania katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam 

Afisa Utumishi wa Ofisi ya Bunge Ndg. Twaha Said pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Kamati za Bunge Ndg. Athuman Hussein wakitoa Elimu kwa Wageni mbalimbali waliotembelea banda la Bunge la Tanzania katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam
Mshauri wa mambo ya Sheria kutoka Ofisi ya Bunge Ndg. Mariam Mbaruku pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Habari Ofisi ya Bunge Ndg. Zuhura Mtatifikolo wakitoa Elimu kwa Wageni mbalimbali waliotembelea banda la Bunge la Tanzania katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam
Afisa Tehama Mwandamizi wa Ofisi ya Bunge Ndg. Aziz Mussa akitoa Elimu kwa Wageni mbalimbali waliotembelea banda la Bunge la Tanzania katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam
Sehemu ya Wageni mbalimbali waliotembelea banda la Bunge la Tanzania ili kujifunza kuhusu Bunge katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam .


Afisa Elimu wa Ofisi ya Bunge Mwl. Omary Machunda akitoa Elimu kwa Wageni mbalimbali waliotembelea banda la Bunge la Tanzania katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam
Afisa Habari wa Ofisi ya Bunge Ndg. Zanele Chiza akitoa Elimu kwa Wageni mbalimbali waliotembelea banda la Bunge la Tanzania katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam 
PICHA NA OMARY MACHUNDA – BUNGE

Washiriki wa Urembo Zingatieni Maadili na Utamaduni wa Kitanzania- Mhe. Shonza

$
0
0


Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza katika mashindano ya kumtafuta mrembo wa Jiji la Arusha, shughuli iliyoandaliwa na The Fuction House chini ya Mkurugenzi Bw. Tilly Chizenga jana Jijini hapo.
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (Katikati) akifuatilia matukio mabalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa na washiriki wa urembo waliokuwa wanawania taji la Miss Arusha, jana katika ukumbi wa Lake Nyasa AICC, kushoto ni Meya wa Jiji la Arusha Bw. Kalisti Lazaro na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa The Fuction House Mrs. Chizenga.
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (mwenye gauni la bluu) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa taji la Miss Arusha baada ya kumalizika kwa mashindano hayo jana Jijini hapo . Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha


Na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ametoa wito kwa washiriki wa mashindano ya urembo nchini kuzingatia maadili na tamaduni za kitanzania kwa kuwa kielelezo bora kwa jamii .

Hayo ameyasema jana Jijini Arusha wakati wa shindano la kumtafuta mrembwende wa Jiji hilo , yaliyoandaliwa na The Function House chini ya uongozi wa Mkurugenzi Bw. Tilly Chizenga yaliyoshirikisha warembo 19.

“ Ninyi ni kioo cha jamii, mnaangaliwa na jamii nzima hivyo msibweteke mnapopata umaarufu bali muwe kielelezo bora cha utamaduni na maadili ya Kitanzania ” amesema Mhe. Juliana Shonza . Anazidi kufafanua kuwa sanaa ya urembo ni ajira kama zilivyo ajira nyingine,na kuwaomba wazazi na jamii kutoa ushirikiano wa karibu katika kuhakikisha mabinti wanatimiza ndoto zao katika sanaa hiyo.

Aidha ameeleza kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua wale wote watakaojihusisha na vitendo vya unyanyasaji na uzalilishaji kwa washiriki wa mashindano hayo. Vilevile alieleza kuwa tasnia hiyo iliingia doa ambapo kwa kipindi cha takribani mwaka mmoja , Serikali ilisimamisha shughuli hizo kutokana na ubabaishaji na kukiukwa kwa taratibu na sheria za kuendesha mashindano hayo.

“Serikali ilichukua uamuzi wa kumfutia leseni muendeshaji wa awali, ila kwa sasa yamefunguliwa tena na jukumu hili linasimamiwa na Bi. Basila Mwanukuzi naamini tutaona mabadiliko mazuri katika tasnia hii” amesema Mhe. Shonza. Naye Muandaaji wa Mashindano hayo Mkurugenzi wa The Fuction House Bw. Tilly Chizenga amesema kuwa maandalizi yalikuwa mazuri , ingawa kulikuwa na changamoto za hapa na pale .

Mashindano ya kumtafuta mrembo wa kuwakilisha Mkoa wa Arusha, yalishirikisha jumla ya warembo 19, ambapo Bi. Rukia Mhona aliibuka mshindi, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Bi. Teddy Mkenda na nafasi ya tatu imechukuliwa na Bi. Belinda Matemu washindi hao wote na wengine watatu wataungana na wenzao katika Kambi ya Miss Tanzania iliyopo Hoteli ya Serena Duluti Jijini hapo ili kumpata muwakilisha atakayewakilisha kanda ya Kaskazini katika mashindano ya Miss Tanzania.

RC MAKONDA APOKEA MWENGE WA UHURU, WAANZA KUZINDUA MIRADI WILAYA YA ILALA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo July 07 amepokea Mwenge wa Uhuru uliowasili Asubuhi ya leo uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere ukitokea Mkoa wa Kusini Pemba na kuukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sophia Mjema kwaajili ya kuanza shughuli ya uzinduzi wa miradi ya maendeleo.

Makonda ameeleza kuwa Mwenge wa Uhuru utakuwa Jijini Dar es salaam kwa Muda wa siku tano ambapo utazindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi 38 yenye thamani ya Shillingi Billion 33.4.

Aidha Makonda amesema katika miradi itakayozinduliwa kupitia mbio za mwenge, miradi 16 itazinduliwa, Miradi 14 itawekewa mawe ya msingi na Miradi 8 itatembelewa.Mwenge wa Uhuru umeanza kwa kukimbizwa Wilaya ya Ilala na baada ya hapo utaenda Wilaya za Kigamboni, Kinondoni, Ubungo na kumalizia na Wilaya ya Temeke.

Akikabidhi mwenge huo kwa kwa mkuu wa wa Dar es salaam Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Seleman Abdallah ameshukuru uongozi wa Mkoa kwa kuwa nao pamoja katika shughuli nzima ya mapokezi ya mwenge na amewatakia kila la heri kati mbio hizo.Naye msimamizi na mkimbiza mwenge taifa Charles Fransis Kabeho amewashukuru wakazi waliojitokeza na amehaidi kufikisha ujumbe wa mwenge katika jiji la Dar es salaam.

Aidha katika ziara hiyo ya kukimbiza mwenge ukiongozwa na Kabeho umezindua miradi miradi sita ambayo ni daraja la kivule ambapo jiwe la msingi limewekwa na hadi mradi kukamilika itagharimu takribani shilingi 869, 887.20 za kitanzania, hosteli ya wasichana katika sekondari ya Mbondele mradi utakao gharimu takribani shilingi 286, 905, 743 hadi kukamilika kwake, ujenzi wa madarasa 3, jengo la utawala, ununuzi wa samani za ofisi na madawati mradi ambao una thamani ya shilingi 268, 919, 700 mradi uliojengwa katika kata ya Zingiziwa.

Aidha mwenge wa uhuru umezindua ujenzi wa hospitali ya Miracolo kata ya Segerea mradi wenye thamani ya shilingi 1, 250,000,000 pamoja na ukaguzi wa kituo cha DMDP wa ghorofa moja lililowekwa jiwe la msingi mwaka 2017.Mwenge wa uhuru utakabidhiwa Mkoa wa Pwani Julai 12 mwaka huu na kufungua na kukagua miradi Mkoani humo.

Uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru 2018 ulianzia mkoani Geita April 2 mwaka huu na kilele ni siku ya kumbukumbu ya mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Oktoba 10 mwaka huu huko Mkoani Tanga.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda,(kulia)akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba,Hemed Suleiman Abdallah leo katika uwanja wa ndege Mwalimu Nyerere jijini Dar as Salaam.(picha na Emmanuel Massaka wa MMG)
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimkabidhi mwenge wa Uhuru kwa mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema kwa ajili ya kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeo katika wilaya hiyo.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018,Ndugu Charles Kabeho akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la Kivule (picha na Emmanuel Massaka wa MMG)
Muonekano wa jengo la bweni la wasichana la shule ya Sekondari Mbondole lilipo Ilala jijini Dar as Salaam.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018,Ndugu Charles Kabeho akiweka jiwe la msingi ujenzi wa bweni la wasichana shule ya Sekondari Mbondole leo jijini Dar as Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa na mkuu wa wilaya ya Ubungo Kisare Makori wakijiandaa kupokea Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa ndege Mwalimu Nyerere jijini Dar as Salaam.
Burudani ikiendelea katika uwanja wa ndege Mwalimu Nyerere jijini Dar as Salaam.


Semu ya viongozi mbalimbali wakiwa katika uwaja wa ndege Mwalimu Nyerere kuupokea mwenge wa Uhuru ulikua ukitoka Pemba Zanzibar.

DKT TIZEBA AKABIDHIWA TUZO YA HESHIMA KWA KUIMARISHA SEKTA YA USHIRIKA NCHINI

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim M. Majaliwa (Mb) akimkabidhi tuzo ya heshima Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kwa kuimarisha sekta ya ushirika nchini wakati wa kilele cha siku ya ushirika Duniani kwenye dhifa iliyofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Leo 7 Julai 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akitoa salamu za Wizara ya Kilimo kwa Waziri Mkuu wakati wa kilele cha siku ya ushirika Duniani kwenye dhifa iliyofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Leo 7 Julai 2018.
Baadhi ya wananchi wakifatilia Mkutano wa kilele cha siku ya Ushirika Duniani
Wazori Mkuu Mhe Kassim M. majaliwa akisalimiana na Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege Mkoani Mwanza kwa ajili ya  kushiriki sherehe kilele cha siku ya ushirika Duniani kwenye dhifa iliyofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Leo 7 Julai 2018.

Na Mathias Canal-WK, Mwanza

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim M. Majaliwa (Mb) amemkabidhi tuzo ya heshima Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kwa kazi kubwa aliyoifanya na anayoendelea kuifanya katika kuimarisha sekta ya ushirika nchini katika kipindi cha muda mfupi tangu alipoteuliwa kuhudumu katika nafasi hiyo.

Tuzo hiyo imetolewa Leo 7 Julai 2018 wakati wa kilele cha siku ya ushirika Duniani na Mhe. Waziri Mkuu kwa niaba ya wanaushirika ambao ndio wameandaa Tuzo hizo ikiwa ni heshima na Utumishi mkubwa kwa Waziri Tizeba katika kipindi kifupi kwa kurudisha imani ya ushirika kwa wananchi waliokuwa wamepoteza matumaini kutokana na baadhi ya viongozi wabadhilifu kujinufaisha na Ushirika kinyume na utaratibu.

Tuzo hiyo kwa Dkt Tizeba inatolewa wakati ambapo ni siku moja pekee imepita tangu Waziri huyo wa kilimo kutangaza Kiama kwa viongozi na baadhi ya watendaji wa vyama vya ushirika wanaofanya ubadhilifu wa Mali za wanaushirika kwa manufaa yao pekee pasina kuwanufaisha wanachama wote.

Kwa msisitizo mkubwa hapo jana Julai 6, 2018 Mhe. Dkt Tizeba alieleza kwa ukali kuhusu ubadhilifu wa rasilimali za ushirika unaofanywa na baadhi ya viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika kwenye hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Tanzania linalofanyika kwa siku mbili katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.

Kongamano hilo liliambatana na maonesho ya bidhaa na shughuli zinazofanywa na vyama hivyo vya ushirika kote nchini ambapo wanachama wamepata fursa ya kubadilishana uzoefu, na kujadili mafanikio na changamoto wanazokabiliana nazo katika uendeshaji wa sekta ya ushirika nchini na kutoa maoni yao kwa serikali.

Dkt Tizeba amesisitiza kuwa serikali inafanya juhudi mahususi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanahamasishwa na hatimae kujiunga kwenye vyama vya ushirika kulingana na shughuli zao za kiuchumi ili kuondoa dhana kuwa vyama vya ushirika ni kwa ajili ya Kilimo cha Mazao ya biashara ya nchi za nje.

Pia, alisema kuwa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kupitia serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua na kuthamini mchango wa ushirika wa Taifa katika kuyafikia malengo ya milenia na malengo mbalimbali ya nchi kama uimarishwaji wa sekta ya viwanda, Kilimo, Mifugo, uvuvi na biashara na kuchangia katika ongezeko la kipato kwa wananchi na hatimaye kuchangia katika ukuaji wa pato la Taifa.

Tuzo hiyo ya kuimarisha sekta ya ushirika nchini pia imetolewa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli sambamba na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim M. Majaliwa (Mb).

SHIRIKA LA ICS LAKABIDHI MRADI WA KISASA WA MAJI WA MALIPO KABLA KATIKA MJI WA MAGANZO SHINYANGA

$
0
0
Shirika la Investing in Childrean and Societies (ICS) limeikabidhi serikali ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga mradi endelevu wa maji kwa malipo kabla (sustainable prepaid water meter system project) unaotekelezwa katika mji mdogo wa Maganzo na kijiji cha Masagala wilayani Kishapu.
Hafla fupi ya ICS kukabidhi shughuli zote za mradi huo endelevu wa maji kwa serikali imefanyika  Ijumaa Julai 6,2018 katika uwanja wa Maganzo ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa mradi ,Mwakilishi wa Meneja Mkazi wa shirika la ICS Tanzania, Peter Matyoko alisema mradi huo umeanzishwa na shirika la ICS mwishoni mwa mwaka 2015 kwa ufadhili wa shirika la UK Aid kupitia Human Development Innovation Fund (HDIF) kwa lengo la kutoa huduma ya maji kwa wakazi 17,072 wa Mji mdogo wa Maganzo na kijiji cha Masagala ifikapo mwaka 2025.
“Huu ni mradi wa mfano katika matumizi ya malipo kabla (Pre-paid) umegharimu kiasi cha Shilingi billion 1.1 zilizotolewa na wadau watatu ambao ni ICS, Susteq na HDIF na chanzo cha maji ya mradi huu ni maji ya Ziwa Victoria kupitia bomba kubwa la Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA)”,alieleza.
Matyoko alisema lengo la mradi ni kuwapunguzia wananchi adha ya kufuata maji umbali wa kutoka kilomita 5 hadi kufikia umbali wa usiozidi mita 400 kama ilivyo katika sera ya Maji ya Taifa ya Mwaka 2002 kwa wakazi.
“Tumekamilisha ujenzi kwa asilimia 100,tumemaliza ujenzi wa bomba la maji lenye kipenyo cha 6’’ na urefu wa 1.3 km kutoka katika bomba kuu la KASHWASA,ujenzi wa mfumo wa bomba za usambazaji maji kutoka kwenye tanki hadi kwenye vituo vya kuchotea maji (water kiosks) 11.7 km,ujenzi wa matanki mawili yenye ujazo wa lita 135,000 na 80,000”alieleza.
“Pia tumejenga vituo 25 vya kuchotea maji vyenye mfumo wa nishati ya jua ( solar power),ufungaji wa dira 25 za mfumo wa ulipaji wa kabla (prepaid water meters) katika kila kituo na ufungaji wa mfumo wa nishati ya jua kwa kila kituo cha kuchotea maji na vituo 11 vya mawakala wa kuuza vocha za maji pamoja na kuwapatia wananchi vifaa vya kuwawezesha kununua Maji kwa njia ya mtandao (tags)”,aliongeza Matyoko.
Aidha aliiomba Halmashauri ya wilaya ya Kishapu kuendeleza Teknolojia hiyo ya maji iliyowekezwa katika mradi huu kwa mujibu wa makubaliano na kwamba ICS itaendelea kushirikiana na halmashauri kwa mambo yanayohusu ushauri ili kutatua changamoto zitakazoibuka muda wowote.Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Mfuko wa HDIF, Joseph Manirakiza aliishukuru serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa kutoa miongozo mbalimbali juu ya utekelezaji wa mradi huo huku akiwasisitiza wananchi na serikali kutunza mradi huo.
Akipokea mradi huo, Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba alisema mradi huo wa kisasa utasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi kutumia maji safi na salama,kupunguza muda wa kutafuta maji, kupunguza gharama yamaji ya kunywa na matumizi mengine ya nyumbani ambapo kabla ya mradi ndoo moja ya lita 20 ilikuwa ikiuzwa Shilingi 500 hadi 700 na sasa itakuwa shilingi 35 kwa ndoo moja.
Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za vijiji kutunza mradi huo na kuwadhibiti na kuwachukulia hatua za kisheria watu watakaohujumu miundombinu ya mradi ili mradi huo uwe na manufaa kwa wananchi.
“Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga niwashukuru sana wadau wetu Shirika la ICS kwa kutekeleza mradi huu lakini pia shukrani za pekee ziende kwa shirika la Human Development Innovation Fund (HDIF) na UKaid kwa kukubali kuwa wafadhili wa mradi huu,niwaondoe hofu tu kuwa tutahakikisha tunautunza mradi huu”,aliongeza Talaba.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba akiangalia mradi endelevu wa maji kwa malipo kabla katika mji mdogo wa Maganzo wilayani Kishapu wakati shirika la ICS lenye makao yake makuu nchini Uholanzi linalotekeleza shughuli za ulinzi wa mtoto (Child protection) katika nchi za Kenya na Tanzania likikabidhi mradi wa maji kwa serikali Julai 6,2018. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Injinia wa mradi endelevu wa maji kwa malipo kabla unaotekelezwa katika mji mdogo wa Maganzo na kijiji cha Masagala wilayani Kishapu, Opita Tarcisius akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba kuhusu ujenzi wa mradi huo uliogharimu shilingi bilioni 1.1.
Kulia ni Injinia Opita Tarcisius akielezea namna wananchi wanavyotumia vifaa vya kuwawezesha kununua maji kwa njia ya mtandao (Tags) kwenye vituo vya kuchotea maji ambavyo vina mfumo wa nishati ya jua (solar power).
Injinia Opita Tarcisius akionesha kifaa cha kununulia maji kwa njia ya mtandao (tag) kwenye vituo vya kuchotea maji.
Wadau wa maji wakiwa katika mradi endelevu wa maji kwa malipo kabla katika mtaa wa Majimaji kata ya Maganzo wilayani Kishapu.
Mashine ambayo mtumiaji wa maji hugusisha kifaa chake cha kununulia maji 'tag' kisha maji huanza kutoka.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akiwashukuru wadau wa maji shirika la ICS, Susteq na HDIF kwa ufadhili wa shirika la UK aid kufanikisha ujenzi wa mradi endelevu wa maji kwa malipo kabla ambao utakuwa mkombozi kwa wananchi kwa kuwapunguzia gharama za maji na adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma ya maji.
Injinia wa Maji wilaya ya Kishapu, Lucas Said akielezea namna serikali ilivyoshirikiana na wadau katika kufanikisha ujenzi wa mradi endelevu wa maji kwa malipo kabla katika Mji wa Maganzo na kijiji cha Masagala wilayani Kishapu.
Kijana Jamal Juma akigusisha kifaa cha kununulia maji kwa njia ya mtandao (Tag) kwenye mashine iliyopo katika kituo cha kuchotea maji katika mtaa wa Majimaji kata ya Maganzo wilayani Kishapu
Mwakilishi wa Meneja Mkazi wa shirika la ICS Tanzania, Peter Matyoko akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi endelevu wa maji kwa malipo kabla (sustainable prepaid water meter system project) unaotekelezwa katika mji mdogo wa Maganzo na kijiji cha Masagala wilayani Kishapu.
Makamu Mkuu wa Mfuko wa HDIF, Joseph Manirakiza akizungumza wakati wa hafla ya zoezi la kuikabidhi serikali ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga mradi endelevu wa maji kwa malipo kabla unaotekelezwa na shirika la ICS katika mji mdogo wa Maganzo na kijiji cha Masagala wilayani Kishapu kwa ufadhili wa shirika la UK Aid kupitia Human Development Innovation Fund (HDIF).
Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akizungumza wakati wa kupokea mradi endelevu wa maji kwa malipo kabla unaotekelezwa na shirika la ICS katika mji mdogo wa Maganzo na kijiji cha Masagala wilayani Kishapu.
Kushoto ni Makamu Mkuu wa Mfuko wa HDIF, Joseph Manirakiza,katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Susteq na Injinia wa mradi endelevu wa maji kwa malipo kabla katika mji mdogo wa Maganzo na kijiji cha Masagala wilayani Kishapu, Opita Tarcisius wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba.
Kushoto ni Mwakilishi wa Meneja Mkazi wa shirika la ICS Tanzania, Peter Matyoko akimkabidhi Makamu Mkuu wa Mfuko wa HDIF, Joseph Manirakiza nyaraka za mradi endelevu wa maji kwa malipo kabla katika mji wa Maganzo na kijiji cha Masagala ikiwa ni ishara ya kukabidhi mradi huo. Makamu Mkuu wa Mfuko wa HDIF, Joseph Manirakiza ndiye aliyekabidhi mradi huo kwa Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Kulia ni Makamu Mkuu wa Mfuko wa HDIF, Joseph Manirakiza akikabidhi nyaraka za mradi endelevu wa maji kwa malipo kabla katika mji wa Maganzo na kijiji cha Masagala kwa Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba akikabiidhi nyaraka za mradi endelevu wa maji kwa malipo kabla katika mji wa Maganzo na kijiji cha Masagala kwa Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu,Injinia Lucas Said.
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu,Injinia Lucas Saidakikabiidhi nyaraka za mradi endelevu wa maji kwa malipo kabla katika mji wa Maganzo na kijiji cha Masagala kwa Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mji wa Maganzo (MAGAWASA), Rehema Abel.
Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mji wa Maganzo (MAGAWASA), Rehema Abel akizungumza baada ya kukabidhiwa mradi endelevu wa maji kwa malipo kabla katika mji wa Maganzo na kijiji cha Masagala.
Meneja rasilimali watu KASHWASA Denis Mlingwa akiwasisitiza wananchi kutunza miundo mbinu ya maji na kuwafichua watu wanaohujumu miundombinu hiyo.
Meza kuu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Diwani wa kata ya Maganzo Lwinzi Kidiga akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi endelevu wa maji kwa malipo kabla katika mji wa Maganzo na kijiji cha Masagala.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Boniface Butondo akiwataka wananchi kutunza miundombinu ya maji ili miradi hiyo idumu.
Mwenyekiti wa kijiji cha Maganzo Charles Manyenye akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi wa maji ambapo aliahidi kushirikiana na wananchi kutunza mradi huo kwa nguvu zote.
Wakazi wa Maganzo wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Wadau wa maji wakiwa katika eneo la tukio.
Wakazi wa Maganzo wafuatilia matukio yaliyokuwa yanajiri.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

RAIS NA AMIRI JESHI MKUU DKT MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WANAFUNZI WA JWTZ IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitunuku  Kamisheni Maafisa Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  leo Jumamosi Julai 7, 2018

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la  Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) aliowatunuku kamisheni katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  leo Jumamosi Julai 7, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine akipatiwa muhtasali na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Luteni jenerali Paul Massao wakati wa hafla ya  hafla ya  kuwatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  leo Jumamosi Julai 7, 2018.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mafunzo wakati wa hafla ya kutunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  leo Jumamosi Julai 7, 2018
 Sehemu ya  Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) waliotunukiwa kamisheni na Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  leo Jumamosi Julai 7, 2018.
Kikosi cha gwaride la kimya kimya kikitumbuiza wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni kwa Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  leo Jumamosi Julai 7, 2018

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu  Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine katika picha ya pamoja na watunukiwa baada ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  leo Jumamosi Julai 7, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine akiondoka eneo la gwaride baada ya kutunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  leo Jumamosi Julai 7, 2018

IGP AFANYA ZIARA KATIKA VISIWA VYA ZIWA VIKTORIA

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Wakazi wa kata za Kagongo, Nyasungu na Kiriba zilizopo Visiwani Ziwa Victoria Mkoani Mara wakati wa Ziara yake ya kuhakikisha wahalifu wanaovamia wavuvi na vitendo vya wizi wa mifugo vinakomeshwa katika maeneo hayo. (Picha na Jeshi la Polisi)
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Diwani wa Kata ya Kiriba Msendo Nyamsora wakati wa ziara ya kikazi ya IGP katika Visiwa vilivyopo Mkoani Mara kwa lengo kuhakikisha wahalifu wanaovamia wavuvi na vitendo vya wizi wa mifugo vinakomeshwa katika maeneo hayo. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiagana na Wakazi wa kata za Kagongo, Nyasungu na Kiriba zilizopo Visiwani Ziwa Victoria Mkoani Mara baad ya kuzungumza  nao wakati wa Ziara yake ya kuhakikisha wahalifu wanaovamia wavuvi na vitendo vya wizi wa mifugo vinakomeshwa katika maeneo hayo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Wakazi wa kata za Kagongo, Nyasungu na Kiriba zilizopo Visiwani Ziwa Victoria Mkoani Mara baad ya kuzungumza  nao wakati wa Ziara yake ya kuhakikisha wahalifu wanaovamia wavuvi na vitendo vya wizi wa mifugo vinakomeshwa katika maeneo hayo. (Picha na Jeshi la Polisi)

OLENASHA:KINACHOTAKIWA KWA WANANCHI NI MAENDELEO NA SIYO SIASA CHAFU

$
0
0

Na.Vero Ignatus Ngorongoro

Mbunge wa jimbo la Ngorongoro ambaye pia ni naibu waziri wa elimu sayansi na Teknolojia William Olenasha ameanza ziara ya kutembelea wananchi wa jimbo lake kwa ajili ya kueleza kazi aliyofanya kwa muda wa miaka mitatu tangu achaguliwe na wananchi wake ikiwemo mradi wa barabara ya Lami kutoka Loliondo mpaka Mto wa Mbu.

Imekuwa ni desturi ya mara kwa mara kwa mbunge huyo kutembelea wananchi wake kila kata ambapo kila kata amepita mara nne tangu achaguliwe kuwa muwakilishi wa wananchi Bungeni.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Ngaresero pamoja na kata ya Pinyinyi zilizopo katika wilaya hiyo Olenasha amesema kuwa yeye ni mbunge ambaye amechaguliwa na wananchi wanyonge ambao wana changamoto hivyo lazima azitatue kwa kuwa ndiyo jambo alilotumwa na wananchi kuwawakilisha.Amesema kwasasa serikali inayoongozwa na Raisi John Magufuli imejitofautisha sana na kipindi cha nyuma kwakuwa hata maeneo ambayo yalisahaulika kwa muda mrefu kwa sasa yameshaanza kupatiwa vipau mbele ikiwemo pia miradi mikubwa ambayo imepelekwa katika jimbo hilo la Ngorongoro.

Olenasha amesema kuwa tayari kupitia yeye kama mbunge wananchi wameshaanza kuletewa mradi mkubwa wa barabara ya lami ambao ni wa kihistoria kutoka Loliondo mpaka mto wa Mmbu kilomita 213 mradi ambao wengi walizani ni ndoto tayari umeshaanza kujengwa.“Napenda kuwataarifu wananchi kuwa ujenzi wa barabara ya lami umeshaanza na shilingi Bilioni 87 zimeshatolewa tayari jambo ambalo wengi walidhani ni ndoto lakini imewezekana na mradi umeanza kwa ksi kubwa”Alisema Olenasha

Hata hivyo Olenasha amemshukuru Raisi Dokta Magufuli kwa kuwapa kipau mbele katika kuletea wananchi wake maendeleo ambapo nje na mradi huo wa Barabara upo mradi wa Umeme,Afya,maji na Elimu ambapo miradi hiyo imeshaidhinishiwa fedha kwa ajili ya kuanza mara moja.Kwa upande wa wananchi ambao wameshiriki mkutano huo wa Mbunge wamesema kuwa tangu kuanza kwa historia ya Uhuru hawajawahi kupata mawasiliano hata ya Simu wala kuona kituo cha afya lakini kupitia mbunge wao wameona mafanikio hayo.

Pamoja na hayo wamesema kuwa mbunge wao amekuwa mstari wa mbele katika suala la maendeleo kwasababu kila mara anatembea jimboni kwake licha ya kuwa na changamoto zilizopo lakini wanampa ushirikiano mzuri ili afanikishe kile ambacho ameshakianza kwa muda mrefu.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Olenasha,ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Ngorongoro William Olenasha akizungumza na wananchi wa jimbo hilo.
Wananchi wa kijiji cha Ngarasero wakimsikiliza mbunge wao Wiliam Olenasha katika ziara yake ya kutembelea wananchi
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images