Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

WATUMISHI TAKUKURU TOENI ELIMU KUHUSU MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA- MLOWOLA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Valentino Mlowola akisalimiana na mmoja wa watumishi wa taasisi hiyo alipotembelea leo kuona namna shughuli za kutoa elimu kwa wananchi wanaofika bandani hapo.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Valentino Mlowola na Naibu Mkurugenzi wa taasisi hiyo Brigenia Jenerali John Mbungo kulia wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa taasisi hiyo wakati walipotembelea na kuona shughuli za kurelimisha wananchi navyoendelea.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika banda hilo ili kupata elimu juu ya mapambano ya Rushwa.



MKURUGENZI wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa(Takukuru) Valentino Mlowola amewataka watumishi wa taasisi hiyo waliopo kwenye maonesho ya Biashara ya kimataifa yanayoendelea Sabasaba kutoa elimu kwa wananachi kuhusu mapambano dhidi ya rushwa nchini.

Mlowola ametoa kauli hiyo leo wakati anazungumza na watumishi wa Takukuru walioko katika banda la taasisi hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amewakumbusha umuhimu wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali.

“Ni vema mkatumia nafasi hii kuzungumza na wananchi kuhusu majukumu ambayo Takukuru inayafanya.Wakija wasikilizeni na muwape elimu kuhusu taasisi na majukumu yake,”amesema Mlowola.

Mlowola alifika kwenye banda hilo akiwa ameongozana na Naibu Mkurugunzi wa Takukuru Brigedia Jeneral John Mbungo ambapo walipata nafasi ya kuelezewa na watumishi walioko kwenye banda hilo majukumu ambayo wanaendelea kuyafanya katika kuwahudmia wananchi.

Akiwa kwenye banda hilo Mratibu wa Maonesho ya Takukuru Sabasaba Asseri Mandari ametumia nafasi hiyo kumulezea Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo kuwa wanapokea wananchi mbalimbali na kasha kuwasilikiza.

Ameongeza wapo baadhi ya wananchi ambao wamewasikilizwa matatizo yao katika banda lao na wale ambao wanaonekana wanahitaji msaada zaidi wanakitengo kingine ambacho kinawasikiliza.

“Tunao wananchi saba ambao wamekuja kwenye banda letu na baada ya kuwasikiliza tukawapeleka katika banda letu lingine ili wasikilizwe.Hata hivyo hatujapata mrejesho, hivyo tunasubiri,”amesema Mandari wakati anamueleza Mlowola.

RC SHINYANGA AFUNGA MAFUNZO YA WAKUNGA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amefunga mafunzo ya wakunga mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga mkoani Shinyanga yaliyoandaliwa na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA),Cuso Internation na Chama Cha Wakunga wa Canada (CAM).
Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Mkunga Okoa Maisha ‘Midwives Save Lives’ unaotekelezwa katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu na yalilenga kuwajengea uwezo wakunga wanaotoa huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya zahanati na vituo vya afya. 
Akizungumza jana Julai 4,2018 akifunga mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa wiki tano na kukutanisha wakunga 100 katika ukumbi wa Submarine Hotel mjini Kahama,Telack aliwashukuru watekelezaji wa mradi wa Mkunga Okoa Maisha kuchagua mkoa wa Shinyanga kuwa katika mradi ili kuinua kiwango cha utoaji huduma za afya ya mama na mtoto. 
Telack alisema wakunga ni kati ya kundi kubwa la wafanyakazi wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto katika kutoa huduma kwa wanawake wakati wa ujauzito,kujifungua na baada ya kujifungua hivyo ni muhimu kwa kila mkunga kuwa na stadi muhimu za ukunga za kuweza kuokoa maisha ya akina mama na watoto na kuepusha vifo vinavyoweza kuzuilika. 
“Takwimu zinaonesha kuwa mkoa wetu kwa mwaka 2017 akina mama 73 walipoteza maisha kutokana na matatizo yanayotokana na uzazi,kuanzia mwezi Januari hadi Juni mwaka 2018 akina mama 20 wamefariki",
“Hivi sasa kuna mabadiliko kidogo ukilinganisha na mwaka 2017 kwa kipindi hicho kwani Januari hadi Juni 2017 akina mama 26 walifariki,hali hii bado hairidhishi hivyo sisi sote tunatakiwa kuongeza juhudi za kutokomeza kabisa vifo hivi”alieleza Telack. 
Alizitaja sababu zilizochangia kutokea kwa vifo hivyo mwaka 2017 kuwa ni kutoka damu nyingi kabla na baada ya kujifungua vifo 25,kifafa cha mimba vifo 10,maambukizi vifo 10,kupasuka kizazi vifo 7,upungufu wa damu vifo 5 na sababu zingine vifo 16. 
Alisema vifo vya akina mama na watoto vitazuilika kwa kiasi kikubwa kama wakunga wakiwezeshwa  vizuri katika kutoa huduma kwani takwimu zinaonesha kuwa wakunga wakifundishwa vizuri na kufikia kiwango cha kimataifa wanaweza kutoa huduma kwa asilimia 87 ya huduma zote anazohitaji mama mjamzito na mtoto mchanga. 
“Wakunga tumieni pia uzoefu wenu kuhudumia akina mama na watoto,naomba mjue kuwa taaluma mliyonayo mko wachache,itendeeni haki,tunataka kila mama anayebeba mimba azae mtoto aliye hai na hatuna sababu ya kupoteza nguvu kazi ya taifa kwa uzembe wa mkunga",aliongeza Telack.
Aidha aliishukuru serikali ya Canada kupitia Global Affairs Canada kwa kufadhili mradi wa Mkunga Okoa Maisha na kuwataka wakunga kutekeleza majukumu yao kwa weledi,umakini ,uzalendo na upendo katika kuwahudumia akina mama na watoto.
Awali akizungumza, Mratibu wa  mradi wa Mkunga Okoa Maisha nchini Tanzania, Martha Rimoy alisema mafunzo hayo ya wiki tano yalilenga kuwapa stadi muhimu za kuokoa maisha ya akina mama na watoto wachanga mara inapotokea dharura.
"Katika wiki hizi tano za mafunzo,tumekutana na wakunga 100 hivyo kufanya idadi ya wakunga waliopatiwa mafunzo kuwa 220 baada ya kuwapa mafunzo wakunga 120 mwaka 2017",alisema.Naye Katibu wa Chama cha Wakunga nchini, Dkt. Sebalda Leshabari alisema Mradi wa Mkunga Okoa Maisha unatekelezwa katika nchi nne ambazo ni Ethiopia,Benin,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Tanzania,na kwamba kwa Tanzania mradi unatekelezwa katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu. 
Aidha aliiomba serikali kuongeza ajira za wakunga kwani ni wachache ukilinganisha na mahitaji yanayotakiwa lakini pia kuhakikisha wakunga wanajengewa nyumba karibu na vituo vya kutolea huduma.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Chama Cha Wakunga wa Canada (CAM,Deborah Bonser alisema chama hicho kitaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali nchini Tanzania ikiwemo TAMA katika kuhakikisha kuwa wakunga wanafanya kazi katika mazingira bora. 
Hata hivyo, Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, (TNMC) Agnes Mtawa aliwataka wakunga kuzingatia maadili ya kazi na kusisitiza kuwa baraza hilo halitasita kumnyang’anya leseni mkunga atakayekwenda kinyume na maadili ya kazi.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga katika ukumbi wa Submarine Hotel Mjini Kahama - Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akifunga mafunzo ya Wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga. Pichani ni wakunga 20,waliowakilisha wakunga 100 waliopatiwa mafunzo hayo kwa kipindi cha wiki tano  
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwasisitiza wakunga kufanya kazi kwa weledi,umakini na upendo kwa akina mama na watoto
Wakunga wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dkt. Rashid Mfaume akizungumza wakati  mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akifunga  mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga. Kushoto ni Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Kahama Said Yasin,kulia ni Katibu wa Chama cha Wakunga nchini, Dkt. Sebalda Leshabari.
Mratibu wa  mradi wa Mkunga Okoa Maisha nchini Tanzania, Martha Rimoy akielezea malengo ya mafunzo kwa wakunga 100 waliyoyatoa kwa muda wa wiki 5.
 Mwakilishi wa Chama Cha Wakunga wa Canada (CAM, Deborah Bonser akizungumza wakati mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akifunga  mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga.
 Mwakilishi wa Chama Cha Wakunga wa Canada (CAM, Deborah Bonser akiiomba serikali kuendelea kushirikiana na wakunga ili kumaliza changamoto ya vifo na mtoto.
Wakunga wakiwa ukumbini
Meza kuu
 Mkunga kutoka Chama Cha Wakunga wa Canada (CAM, Patrice Latka akizungumza wakati  mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akifunga  mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga.
Mkunga kutoka Chama Cha Wakunga wa Canada (CAM, Jasmin Tecson akizungumza wakati  mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akifunga  mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga.
 Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, (TNMC) Agnes Mtawa akiwataka wakunga kuzingatia maadili ya kazi yao.
Mkurugenzi wa Shirika la Cuso International Romanus Mtung'e akizungumza wakati  mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akifunga  mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga.
Zoezi la kufunga mafunzo likiendelea
Katibu wa Chama cha Wakunga nchini, Dkt. Sebalda Leshabari akizungumza wakati  mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akifunga  mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga.
Katibu wa Chama cha Wakunga nchini, Dkt. Sebalda Leshabari akiiomba serikali kuendelea kushirikiana na chama hicho katika kuhakikisha vifo vya mama na mtoto vinamalizika mkoani Shinyanga.
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Kahama Said Yasin akizungumza wakati  mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akifunga  mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akizungumza wakati  mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akifunga  mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga.
Mkunga Innocent Rwiza akisoma risala ya washiriki  wa mafunzo hayo
Wakunga wakifuatilia matukio ukumbini
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akimkabidhi mkunga cheti cha ushiriki wa mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga yaliyofanyika katika ukumbi wa Submarine Hotel Mjini Kahama 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akimkabidhi mkunga cheti cha ushiriki wa mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga
Zoezi la kukabidhi vyeti likiendelea
Mkunga akishikana mkono na Katibu wa Chama cha Wakunga nchini, Dkt. Sebalda Leshabari
Picha ya pamoja mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na washiriki  wa mafunzo hayo
Picha ya pamoja mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na washiriki  wa mafunzo hayo.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

RICHARD TANGANYIKA AKABIDHIWA PIKIPIKI YA ‘TUSUA MAISHA NA GLOBAL’

$
0
0
Mshindi wa pikipiki katika shindano la Tusua Maisha na Global, Richard Tanganyik, akiongea na wanahabari baada ya kukabidhiwa funguo za pikipiki yake leo katika ofisi za Global Group zilizooo Sinza-Mori jijini Dar es SalaamOfisa Usambazaji, Keffa Massaga (kushoto) akimkabidhi funguo za pikipiki, Richard Tanganyika.[/caption] [caption id="attachment_226424" align="alignnone" width="1024"]Tanganyika akiwa na zawadi yake. Washindi wakiwa na zawadi zaoWashindi na wafanyakazi wa Global Group. MSHINDI wa pikipiki katika Shindano la Tusua Maisha na Global, Richard Tanganyika, amekabidhiwa zawadi yake pamoja na washindi wengine katika ofisi za Global Group, zilizoko Sinza-Mori jijini Dar es Salaam. Washindi wengine waliokabidhiwa zawadi zao ni Shaaban Kamoye aliyejishindia dinner set, Nasoro Juma aliyejishindia headphones za kisasa, za Beats by Dre na Novart Magere aliyejishindia jezi, ambaye amewakilishwa na ndugu yake, Hassan Mathias.
(PICHA: RICHARD BUKOS | GPL)

UKAGUZI WA MAGARI KILIMANJARO WABAINI ,MADEREVA KUTUMIA LESENI ZA NDUGU ZAO

$
0
0
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP,Hamis Issah akitembelea kikuu cha Mabasi mjinib Moshi kwa ajili ya ukaguzi wa Magari ya Abiria.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP.Hamis Issah akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Operesheni wa kikosi cha Usalama Barabarani,Mkaguzi ,Peter Mizambwa wakati wa ukaguzi huo uliofanyika katika kituo kikuu cha Mabasi mjini Moshi.
Mkuu wa Operesheni wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro,Inp Peter Mizambwa  akimuonesha kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP,Hamis Issah moja ya karatasi ambazo zinatumiwa na madereva kama Leseni.
Mkuu wa Operesheni wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro,Inp Peter Mizambwa  akimuonesha kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP,Hamis Issah alama za leseni ambayo ni halisi .
Kamanda Issah akitoa maelekezo kwa askari wake.
Mmoja wa Madereva waliokaguliwa akionesha vipande vya karatasi ambavyo alidai kuwa ni leseni .
Mkaguzi wa Magari akikagua  moja ya mabasi yaliyokuwa yafanye safari ya kuelekea Dar es Salaam .
Kamanda wa Polisi akimuuliza mmoja wa madereva  waliokamatwa ,matumizi ya silaha ya Kisu kilichokutwa katika gari lake.
Mmoja wa Madereva akipelekwa kituo cha Polisi mara baada ay kubainika kutumia leseni ya ndugu yake kuendesha gari.

Na Dixon Busagaga  wa Globu ya Jamii KAnda ya Kaskazini.

UKAGUZI wa Magari ya Abiria pamoja na Leseni unaofanywa na Jeshi la Polisi mkoa  wa Kilimanjaro umebaini udanganyifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya Madereva wa Magari ya abiria ukiwemo kuendesha bila  Leseni ,Umri  wa kuendesha gari kupitiliza , wengine wakitumia Leseni za Ndugu zao.

Katika kituo Kikuu cha Mabasi ya abiria yaendayo mikoani na yale yanayofanya safari zake ndani ya mkoa wa Kilimanjaro,Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamisi Issah akiwa ameongozana na Mkuu  Operesheni kikosi cha usalama Barabarani ,Peter Mizambwa na maofisa wengine wa Polisi wamefanya ukaguzi.

Katika ukaguzi huo magari zaidi ya 800 yamekaguliwa na yaliyobainika kuwa mabovu yalizuiliwa kuendelea na safari huku  baadhi ya Madereva wakikutwa  na silaha katika magari yao vikiwemo Visu,kamanda Issah akatoa onyo kwa madereva kutembea na silaha pamoja na kujaza abiria hali inayochangia abiria kukaa katika mikao isiyo rafiki .

Mkuu wa operesheni wa kikosi cha usalama barabarani ,Mkaguzi wa Polisi Peter Mizambwa akazungumzia Operesheni Nyakua iliyoanza kwa lengo la kupunguza ajali  huku baadhi ya Madereva na wananchi wakipongeza utaratibu huo.

MBARAWA ATEMBELEA MRADI WA UBORESHAJI MIFUMO YA USAMBAZAJI MAJI INAYOSIMAMIWA NA DAWASA NA KUTOA MAAGIZO MAZITO

$
0
0
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (katikati), akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara yake aliyoifanya leo Julai 5, 2018 kutembelea mradi wa uboreshaji wa mfumo wa usambazaji maji Dar es Salaam na Pwani (kushoto) ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA), Dkt. Suphiani Masasi na kulia ni Mkandarasi wa mradi huo kutoka kampuni ya Jain Irrigation ya nchini India, Bw.Anil Vitankar.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, leo Julai 5, 2018 ametembelea mradi wa uboreshaji wa mfumo wa usambazaji maji Dar es Salaam na Pwani ambao umefikia asilimia 87.5 na kumuhimiza mkandarasi kumalizia asilimia iliyobaki kwa wakati vinginevyo atachukua hatua kali
Profesa Mbarawa alisema, mradi huo ambao unatekelezwa na Serikali kupitia Mamlaka ya Mai Safi na Maji Taka (DAWASA), unathamani ya shilingi bilioni 72.43 na ni mradi muhimu sana katika utoaji huduma kwa wananchi.
“Mkandarasi yuko kwenye site lakini kasi yake hairidhishi, hivyo sisi kama serikali tunajaribu kutatua kero hii ya maji kwa wananchi, lakini mkandarasi kidogo analeta shida, kama mjuavyo mradi ulianza mwaka 2016 mwezi Machi na ulitarajiwa kukamilika Novemba 2017 utaona tuko nyuma karibu miezi 18 tuko nyuma.” Alisema na kutoa maelekezo
“Kwanza tunataka uwepo kwenye site saa 24, na sio tunakuona tu lakini tuone unafanya kazi, pili ukishinbdwa kumaliza mradi huu kama tulivyokubaliana mwezi Septemba uelewe kwamba hii ndio itakuwa mara yako ya mwanzo na ya mwisho kupata kazi tena hapa Tanzania, na tatu tutakutoa kwenye usajili wa chama cha makandarasi yaani bodi ya makandarasi nah ii maana yake hutaweza kufanya kazi tena hapa Tanzania na mwisho tutachukua Pasipoti yako ya kusafiria ili kuhakikisha kwamba unafanya kazi na unamaliza.” Alisema.
Ziara hiyo ya Profesa Mbarawa imemuwezsha kujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo ulioanza Machi 2016 na unaohusisha ujenzi wa matenki matano (5) ya kuhifadhi na kusambaza maji yenye ukubwa wa kuhifadhi lita milioni 5.0 hadi 6.0.
Pia alitembelea ujenzi wa vituo vine (4) vya kusukuma maji vilivyo na matenki yenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 3.0 kila moja, ununuzi na ufungaji wa pampu kubwa 16 za kusukuma maji ununuzi wa transfoma na ufungaji wa njia za umeme wa msongo mkubwa, ununuzi na ulazaji wa mabomba makubwa ya ugawaji maji na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji mitaani yatakayokuwa na urefu wa jumla ya kilomita zipatazo 477.
Kwa mujibu wa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Dkt. Suphiani Masasi, mradi huo utanufaisha maeneo ya Salasala, Bunju, Wazo, Makongo, Changanyikeni, Bagamoyo, Mpiji, Zinga, Kiromo, Kitopeni, Ukuni, Kerege, Buma, Mataya na ukanda maalum wa WPZA ambayo ni maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu Chini.
Aidha mradi pia utanufaisha maeneo yaliyopo kati ya Mbezi Louis na Kiluvya ambayo ni Kiluvya yenyewe, Kibamba, Mbezi, Msakuzi, Makabe, Malamba- mawili na Msigani na maeneo haya yanapata maji kutoka Mtambo wa Ruvu Juu ambao ulizinduliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania Juni 2, 2017.
Mtendaji Mkuu huyo wa DAWASA alimueleza Mhe. Waziri kuwa lengo la mradi ni pamoja na kuhakikisha kuwa wananchi wa kawaida wenye viwanda na biashara katika eneo lote la mradi wanapata huduma bora za maji hasa baada ya maji kuongezeka kufuatia kukamilika kwa kazi za upanuzi wa mitambo ya maji Ruvu Juu na Ruvu Chini.

 Muonekano wa sasa wa tanki kubwa la kuhifadhia maji e neo la Changanyikeni jijini Dar es Salaam ambapo tayari tenki hilo limeshafunikwa.
 Muonekano wa kituo cha kusukuma maji cha Salasala 
 Huu ni muonekano wa Tanki la kuhifadhia maji la Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
 Profesa Mbarawa, akiongozana na Bi.Modester Mushi (kulia), ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa ufundi DAWASA, wakati Mhe. Waziri alipotembelea eneo la ujenzi wa kituo cha kusukuma maji cha Boko ambacho ujenzi wake umefikia hatua za mwisho.
 Profesa Mbarawa akitoa maagizo hayo.
 Bw. Anil Vitankar, wa kampuni iliyopewa kandarasi ya ujezni wa mradi huo ya Jain Irrigation, akisikiliza maagizo ya Mhe. Waziri.
Baadhi ya vifaa vya kukamilisha mradi huo vikiwa kwenye karakana huko Boko nje kidogo ya jiji

KANGI LUGOLA AREJEA JIJINI DAR ES SALAAM, AVUNJA KAMATI ZOTE ZA USALAMA BARABARANI

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (kushoto) baada ya kurejea kutoka jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam,walijadiliana  mambo mbalimbali yanayolihusu jeshi hilo. Akiwa mkoani Mbeya Mhe. Lugola amelivunja Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Kamati zote za Usalama barabarani za mikoa na wilaya zote, na kusema atayaunda upya ili kupambana na janga sugu la ajali za barabarani. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akipeana mikono na   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye(kulia), baada ya kurejea kutoka jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Video courtesy of MCL Digital

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu yatembelea TAA kuona utendaji wake

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi  mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania, Richard Mayongela akimpokea mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Suleimani Kakoso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Suleimani Kakoso akisalimiana na watendaji waandamizi wa Mamlaka wa Viwanja vya ndege Tanzania mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Watu Mashuhuri.
 Kaimu Mkurugenzi  mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania, Richard Mayongela  akiwasilisha taarifa ya Utendaji ya Mamlaka mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu uuwasili.
 Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakifuatilia taarifa ya utendaji ya Mamlaka ya Viwanja yya Ndege iliyokuwa ikiwasilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Richard Mayongela.
 Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha JNIA, Paul Rwegasha akitoa historia ya Jengo la kwanza la abiria wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu.
Moja ya gari jipya lililowasili kati ya sita ambayo Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania imeyanunua na kuyakabidhi kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kuweza kusaidia katika dharura za moto zinazoweza kutokea Kiwanjani.

JAFO AWAPONGEZA SIMIYU

$
0
0
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewapongeza viongozi wa mkoa wa Simiyu na halmashauri zake kwa kusimamia vyema ujenzi wa miradi ya afya mkoani humo. 

Jafo ametoa pongezi hizo wakati akipokea vituo vya afya 38, magari ya wagonjwa matatu, magari ya kuratibu shughuli za afya sita , pamoja na vifaa vilivyofadhiliwa na shirika la Kimataifa la UNFPA wakishirikiana na KOICA. Katika makabidhiano hayo,Waziri Jafo amefurahishwa na usimamizi mzuri wa ujenzi wa miundombinu hiyo kupitia utaratibu wa FORCE ACCOUNT. 

Jafo amempongeza mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka pamoja na wabunge wa mkoa huo kwa kuwashirikisha vyema wananchi ambao wameungana na serikali yao pamoja na wadau katika kufanikisha miradi hiyo ya afya. Katika shughuli hiyo waziri Jafo amesisitiza magari hayo tisa yatumike kwaajili ya sekta ya afya na si vinginevyo. 

Wakati huo huo, Waziri Jafo amefurahishwa na wananchi wa Malya wilayani Kwimba mkoa Mwanza kwa kujenga vizuri sana majengo yao ya kituo cha afya Malya baada ya serikali kuwapatia fedha milioni 400.

Naye mbunge wa Sumve Mhe. Ndasa aliishukuru serikali na ameiomba kuwasaidia mashine ya X-Ray kituoni hapo ili wananchi waondokane na usumbufu wa kwenda hospitali ya wilaya iliyopo Ngudu.Waziri Jafo amemaliza ziara yake ya mikoa miwili ya Simiyu na Mwanza na kuelekea wilayani Bagamoyo kwaajili ya uzinduzi wa jengo la wazazi katika hospitali ya wilaya ya Bagamoyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za  Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka na viongozi wengine katika uzinduzi wa vituuo vya Afya.

Wananchi waliohudhuria uzinduzi wa vituo vya afya
Wananchi waliohudhuria uzinduzi wa vituo vya afya
Viongozi mbalimbali waliokuwepo kwenye uzinduzi wa vituo vya Afya mkoa wa Simiyu.
Majengo yaliyojengwa kwa ufadhili wa shirika la UNFPA na KOICA.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akisikiliza maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Baadhi ya vifaa vilivyopo kwenye vituo vya afya vya mkoa huo vilivyozinduliwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Sumve Richard Ndassa katika uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Afya Malya wilayani Kwimba mkoa Mwanza.
Jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Afya Malya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akikagua ujenzi unaoendelea katika Kituo cha Afya Malya

WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUFICHUWA WATOTO WENYE ULEMAVU.

$
0
0

Na Frankius Cleophace SERENGETI.

Wilayani Serengeti Mkoani Mara katika Kata ya Manchira Wameendelea kubaini watoto wenye Ulemavu wa aina yeyote ili wapelekwe Shule ili kupata haki zao kama Watoto Wengine hivyo wazazi na Walezi Wilayani humo wametakiwa kuendelea kufichua Watoto wenye Ulemabu ili kupata Elimu.

Hayo yamebainishwa na Afisa elimu kata ya Machira Fidel Sylivanus katika Tamasha lililoandaliwa na Shirika la RIGHT TO PLAY lengo ni Kutoa Elimu kwa Jamii ili kuondokana na Mila zenye Madhara ukiwemo Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.

Sylivanus amesema kuwa katika kata nzima tayari wamezunguka na kubaini watoto wenye ulemavu wa aina yeyote na kuwataka Wazazi na Walezi kufichua watoto hao ili kupatiwa Elimu kama Watoto wengine.

Pia Afisa Elimu amezi kuimiza Wazazi na Walezi kusisitiza Suala la Elimu kwa watoto wote bila Ubaguzi wa Jinsia huku watoto wakitaja Changamoto kubwa kuwa ni Wazazi kuwapatia kazi nyingi na kushindwa kufanya kazi zao ikiwemo Michezo pamoja na Kujisomea.

Leah Kimaro Kutoka Shirika la RIGHT TO PLAY amesema kuwa takribani Siku Nne amabazo shirika hilo limefanya Matamasha wamefikia wananchi takribani Elfu tano na kuweza kuwapatia ujumbe uliokusudiwa kupitia Michezo Mbalimbali Nyingo, Ngonjera, Maigizo, Mpira wa Miguu kwa Watoto wakike, Kukimbiza Kuku na kukimbia ndani ya Magumia lengo ni kukusanya Jamii ili kupatiwa Elimu hiyo.

Aidha Wananchi wamekuwa na Maoni tofautio kuhusu Matamasha hayo ambao yameandaliwa na Shirika la RIGHT TO PLAY kwa siku Nne na kutoa Elimu ilikusudiwa katika Jamii Wilayani Serengeti Mkoani Mara ambapo wameomba KuwaMatamasha hayo yawe endelevu katika Maeneo ya Vijijini na ukiaangalia Ukeketaji ufanyika Mwaka unagawabyika kwa Mbili hivyo Mwaka huu 2018 unagawanyika kwa mbili Jamii inaweza kukeketa licha ya kutolewa kwa Elimu hiyo hivyo serikali sasa inajukumu la kuwasaka na kuwatia Nguvuni wale wote watakao huska na Vitendo vya Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike Mkoani Mara.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Miseke na Wananchi wakata ya Manchira Wilayani Serengeti Mkoani Mara wakiwa katika Maandamano na Mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kupiga Vita Ukatili kwa watoto kwenye Tamasha la Michezo lililoandaliwa na Shirika la RIGHT TO PLAY lililopo Serengeti Mkoani Mara.
Afisa Elimu kata ya Manchira Fidelis Sylivanus akisalimiana na Timu ya Mpira wa Miguu Miseke Wakubwa FC na Miseke Wadogo FC.
Afisa Elimu kata ya Manchira Fidelis Sylivanus akisalimiana na Timu ya Mpira wa Miguu wa Wasichana baina ya Timu Miseke FC na Bwitenge FC katika Viwanja vya Shule ya Msingi Miseke.
Mgeni rasmi ambaye ni Afisa Elimu Kata ya Manchira Fidels Syilivanusi akikabidhi zawadi mbalimbali kwa Washiriki wa Michezo hiyo.

HATIFUNGANI YA SH.BILIONI 120 YA TMRC YAORODHESHWA DSE

$
0
0

*CMSA yahimiza kampuni kuingia katika DSE

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji amesema kuwa katika kuhakikisha mikopo ya nyumba inaanzishwa nchini, Serikali ikishirikiana na Benki ya Dunia ilianzisha mradi wa kuwezesha kuwepo kwa mfumo wa mikopo ya nyumba.

Dk.Kijaji ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kuorodhesha hatifungani yenye thamani ya Sh.bilioni 120 za Kampuni ya Mikopo ya Nyumba (TMRC) katika Soko la Hisa Dar es Salaam(DSE).

Amefafanua kuhusu mfumo wa mikopo ya nyumba amesema kuwa mradi huo uitwao mikopo ya nyummba ulilega kuanzisha mifumo wa mikopo ya nyumba kutokana na kufilisika kwa Benki ya Nyumba Tanzania mwaka 1995 ambayo ilikuwa inatoa mikopo ya muda mrefu kwa wateja kwa ajili ya ujenzi wa ununuzi wa nyumba za makazi.

“Mradi huu ulikuwa na maeneo makuu matatu ambayo ni uanzishwaji wa mfumo wa mikopo ya nyumba, uanzishwaji wa mfuko wa mikopo midogo midogo ya nyumba na kuendeleza mfumo wa ujenzi wa nyumba wa gharama nafuu kwa lengo la kupunguzia wananchi gharama za ujenzi na kuwa na nyumba za gharama nafuu,”amesema.

Amefafanua ili kutekeleza malengo hayo matatu Serikali ilikopa jumla ya Dola za Marekani milioni 100 mwaka 2010 kutoka benki ya dunia ili kuwezesha mradi wa mikopo ya nyumba kufikia malengo.

“TMRC ilianzishwa katika harakati za kutekeleza sehemu ya kwanza ya mradi wa mikopo ya nyumba ambayo ni kutoa mikopo ya nyumba ya muda mrefu.TMRC ilianzishwa kwa mtahi wa bilioni sita na benki nne mwaka 2010 kama mtaji wa kuanzisha kampuni chini ya sheria ya benki ya mwaka 2006 na kuanza kutoa mikopo kwa benki mwaka 2011,”amefafanua.

Ameongeza TMRC ilianzishwa ili kutatua changamoto ya uwiano mdogo wa mikopo ya nyumba ikilinganishwa na pato la Taifa ambalo ni chini ya asilimia moja. Amefafanua TMRC kwa sasa inajumla ya mtaji wa Sh.bilioni 19.3 kutoka kwa wanahisa 16.Tangu kuanzishwa kwake TMRC imetoa mikopo ya thamani ya Sh.bilioni 91 kwa benki 14 hapa nchini.

“Hadi sasa jumla ya Watanzania 937 wamenuifaka moja kwa moja na mikopo inayotolewa na TMRC kwa benki .Pia wananchi 4,209 wamenufaika na mikopo ya nyumba kutokana kutokana na mfumo wa mikopo ya nyumba unaowezeshwa na TMRC,”amesema.

Dk.Kijaji amesema hatifungani ya TMRC kwa siku ya leo ni ya muda wa miaka mitano ambayo kitaalam itaipatia kampuni hiyo fedha za kukopesha mabenki kwa ajili ya mikopo ya nyumba kwenye soko la fedha la ndani. “Hatua hii pia itachangia kukua kwa masoko ya mitaji hapa nchini.Kipekee nawapongeza kwa uamuzi mzuri wa kujirodhesha katika soko la hisa la Dar es Salaam kwa wakati muafaka kabisa.

“Hii ni ishara tosha kuwa sekta ya fedha ni imara na inakuwa na itaendelea kuchachua ukuaji wa uchumi wetu,”amesema. Wakati huo huo Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama ameipongeza TMRC kufanikisha uorodheshwaji wa hatifungani ya kampuni katika soko la hisa la Dar es Salaam.

Pia amehimiza kampuni zingine ziingie katika mfumo huo katika kuelekea uchumi wa viwanda.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji (katikati) akibonyeza kengele leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuorodhesha hatifungan za Kampuni ya Mikopo ya Nyumba(TMRC) yenye thamani ya Sh.bilioni 120 kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam(DSE).Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya DSE Jonathan Njau na kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Soko la Mitaji na Dhamana Nicodemas Mkama.
 .Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji (katikati) akifafanua jambo wakati  hafla ya kuorodhesha hatifungan za Kampuni ya Mikopo ya Nyumba(TMRC) yenye thamani ya Sh.bilioni 120 kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam(DSE).Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya DSE Jonathan Njau.
 

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA OFISI ZA MAMLAKA YA HALI YA HEWA NCHINI

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), Dkt. Agnes Kijazi akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Seleman Kakoso, wakati kamati hiyo ilipotembelea mamlaka hiyo kukagua namna inavyofanya kazi, jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi, Aunyisa Meena (kushoto), kuhusu namna walivyojipanga kuimarisha miundombinu ya miradi ya hali ya hewa kwa mwaka mpya wa fedha 2018/2019, wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miudombinu ilipotembelea Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Seleman Kakoso, akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), Dkt. Agnes Kijazi (katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo Dkt. Buruhani Nyenzi (kushoto), wakati kamati hiyo ilipotembelea mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Seleman Kakoso (katikati), akifafanua jambo wakati kamati hiyo ikiwa katika ziara ya kujifunza namna  Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) inavyofanya kazi, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), Dkt. Agnes Kijazi (kulia), akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati Kamati hiyo ilipokuwa kwenye ziara ya kujifunza namna mamlaka hiyo ivyofanya kazi. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Seleman Kakoso na wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Seleman Kakoso (katikati), akiwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (kushoto), katika chumba cha kutangazia taarifa za hali hewa, wakati kamati hiyo ilipotembelea Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Bi. Hellen Msemo kutoka Mamlaka hiyo.

TIGO NA HMD GLOBAL WANAUNGANA KULETA SIMU ZA KISASA KWA GHARAMA NAFUU

$
0
0
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu aina ya Nokia 1 kwa mpiga picha Anthony Siame (kulia) aliyoshinda katika droo ndogo iliyofanyika wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe za simu kutoka Tigo na Nokia katika msimu huu wa Sabasaba. Katikati ni Meneja wa Biashara wa kampuni ya HMD Global inayosambaza simu hizo za Nokia, Gopher Ogembo.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu aina ya Nokia 1 kwa mwandishi wa habari, Ellen Manyangu (kulia) aliyoshinda katika droo ndogo iliyofanyika wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe za simu kutoka Tigo na Nokia katika msimu huu wa Sabasaba. Katikati ni Meneja wa Biashara wa kampuni ya HMD Global inayosambaza simu hizo za Nokia, Gopher Ogembo.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu aina ya Nokia 1 kwa mwandishi wa habari Vumilia Mwasha (kulia) aliyoshinda katika droo ndogo iliyofanyika wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe za simu kutoka Tigo na Nokia katika msimu huu wa Sabasaba. Katikati ni Meneja wa Biashara wa kampuni ya HMD Global inayosambaza simu hizo za Nokia, Gopher Ogembo.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) na Meneja wa Biashara wa kampuni ya HMD Global inayosambaza simu za Nokia, Gopher Ogemb (kulia) wakizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe za simu kutoka Tigo na Nokia katika msimu huu wa Sabasaba. Tigo na Nokia wanatoa simu za kisasa kwa bei nafuu zenye ofa ya bando ya intaneti bure kwa miezi sita.

Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati) akionesha simu wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe za simu kutoka Tigo na Nokia katika msimu huu wa Sabasaba. Tigo na Nokia wanatoa simu za kisasa kwa bei nafuu zenye ofa ya bando ya intaneti bure kwa miezi sita.


Tigo na HMD Global wanaungana kuleta simu za kisasa kwa gharama nafuu.

Ofa murwa kwa simu mpya za Nokia zenye intaneti bure kwa miezi sita toka Tigo
Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidigitali, Tigo Tanzania imeungana na HMD Global, wauzaji wa simu za Nokia kuwapa wateja fursa ya kumiliki kw abei nafuu, simu janja zenye uwezo wa 4G na intaneti bure kwa miezi sita kutoka Tigo.

Katika msimu huu wa Sabasaba, Tigo na HMD Global wanakuletea simu za Nokia 3310 kwa bei ya TSH 99,000, na Nokia 1 kwa bei pungufu ya TSH 174,999 pekee.

“Simu inayotumia laini mbili ya Nokia 3310 pamoja na simu janja ya Nokia 1 zote zinakuja na ofa ya GB 2 za intaneti kwa miezi sita kutoka Tigo,’ Woinde Shisael, Meneja Mawasiliano wa Tigo alisema katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika Maonyesho ya Dar es Salaam ya Kimataifa ya Biashara katika viwanja vya JK Nyerere jijini Dar es Salaam.

Shisael aliongeza kuwa,“Tigo wanaongoza mabadiliko ya maisha ya kidigitali. Tunalenga kuongeza matumizi ya simu janja nchini na kuhakikisha kuwa wateja wetu wote wanafurahia huduma bora zaidi ya kidigitali kupitia mtandao wetu mpana na wenye kasi ya juu zaidi wa Tigo.”

Akizungumzia ushirikiano huo, Gopher Ogembo, Meneja wa Biashara wa HMD Global, Ukanda wa Africa Mashariki alisema, “Simu zetu zinaweka viwango vipya vya ubora na raha ya matumizi. HMD Global inaamini kuwa kila mteja anahitaji kupata bidhaa yenye viwango vya juu vya ubora na umbo la kuvutia.

Ogembo aliongeza kuwa “Pamoja na kutengeneza bidhaa za kuvutia zinazolenga kuongeza raha ya matumizi kwa wateja, kila kifaa kinachotumika kutengeneza simu za Nokia kimetazamwa kwa undani zaidi ili kuboresha faida kwa maisha ya kila sikui ya mteja. Tunafurahia kufungua ukurasa mpya wa Nokia kwa wateja wetu wote nchini Tanzania. Simu mpya za Nokia zimetengenezwa kwa ajili ya kizazi kipya cha wateja kwa kuzingatia historia ndefu ya ubora, umathubuti na urahisi wa matumizi.”

Simu zote zinapatikana katika banda la Tigo lilipo katika Maonyesho ya Dar es Salaam ya Kimataifa ya Biashara pamoja na katika maduka yote ya Tigo nchi nzima.

Dk.shein Asafiri Safari Maalum Nchini Uingereza

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akiagana na Viongozi Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi Zanzibar katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akiondoka nchini kuelekea Uingereza kwa safari maalum ya wiki tatu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akiagana na Wazee wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akiondoka nchini kuelekea Uingereza kwa safari maalum ya wiki tatu
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (kushoto) alipokuwa akiagana na Wazee wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akiondoka nchini akiungana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuelekea Uingereza kwa safari maalum ya wiki tatu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akiagana na katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akiondoka nchini kuelekea Uingereza kwa safari maalum ya wiki tatu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akiondoka nchini kuelekea Uingereza kwa safari maalum ya wiki tatu
VIONGOZI mbali mbali wakimpungia mkono wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akiondoka nchini kuelekea Uingereza kwa safari maalum ya wiki tatu,[Picha na Ikulu

SIMIYU YAPOKEA VITABU 174, 188 VYA DARASA LA NNE

$
0
0

Na Stella Kalinga, Simiyu

Mkoa wa Simiyu umepokea jumla ya vitabu 174,188 awamu ya kwanza kwa masomo ya Kiingereza na Hisabati, vyenye thamani ya takribani shilingi milioni 348 kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la nne, ambavyo ni sawa na uwiano wa mwanafunzi mmoja kwa kitabu kimoja.

Akizungumza na viongozi , baadhi ya walimu na wanafunzi wa mkoa wa Simiyu kabla ya kukabidhi vitabu vitabu hivyo kwa Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka Julai 05 jioni mjini Bariadi, Mwakilishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Bw. Didas Hamsini, amesema Taasisi hiyo imejipanga kuhakikisha vifaa vyote vya kielimu ikiwemo vitabu, vifaa vya maabara na vifaa vingine vinavyohitajika vinapatikana.

Amesema utoaji wa vitabu 29,003 kwa kila somo kwa wanafunzi wa darasa la nne Mkoani Simiyu ni sehemu ya utekelezaji wa elimu bila malipo, huku akibainisha kuwa Taasisi ya Elimu inatarajia kuzalisha vitabu 681, 527 kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la nne nchi nzima.

Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl. Julius Nestory amesema wamepokea vitabu awamu ya kwanza kwa masomo ya kiingereza na hisabati kwa uwiano wa kitabu kimoja mwanafunzi mmoja, huku akibainisha kuwa vitabu vilivyobaki vinatarajiwa kuletwa tena wiki ya kuanzia tarehe 16 Julai, 2018 na akawataka walimu na wanafunzi kuvitumia vitabu hivyo kama ilivyokusudiwa.

“Naishukuru sana Serikali kwa kutoa vitabu hivi hadi sasa tuna wanafunzi 53, 187 darasa wa nne na vitabu tulivyopokea kwa awamu hii kwa masomo ya Hisabati na Kiingereza, kila mwanafunzi wa Mkoa wa Simiyu atapata kitabu cha kwake, kwa masomo manne yanayobaki tumeahidiwa kuwa baada ya majuma mawili vitakuwa vimefika” alisema Afisa Elimu Mkoa.

Kwa upande wao wanafunzi wa mkoa wa Simiyu wameishukuru Serikali kwa kuwaletea vitabu, hivyo ambavyo wanaamini vitawasaidia kujisomea na kuinua ufaulu hatimaye kuufikisha mkoa huo katika mikoa kumi bora inayofanya vizuri kitaaluma.“Tunaishukuru sana Serikali kwa kuwaleta hivi vitabu, tunaamini vitawasaidia wadogo zetu wa darasa la nne kujifunza na kuongeza ufaulu na siku moja mkoa wetu na sisi utakuwa kati ya mikoa bora inayofanya vizuri kitaaluma “ alisema Liku Malisha mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Somanda A.

Mbunge wa Itilima Mhe. Njalu Silanga ameishukuru Serikali kwa kutoa vitabu hivyo na akatoa wito kwa walimu na wanafunzi mkoani humo kuhakikisha kuwa vitabu hivyo vinawezesha kuongeza ufaulu kwa kuwa mkoa huo umeshajipanga kutokomeza ujinga na kuwa mkoa kiongozi kielimu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kutimiza ahadi yake na kujibu kilio cha muda mrefu cha wazazi, walimu na wanafunzi juu ya changamoto ya ukosefu wa vitabu wa darasa la nne.

Ameongeza kuwa vitabu hivyo vitausaidia mkoa wa Simiyu kufikia malengo yake katika kuongeza ufaulu na kuboresha Sekta ya Elimu, ambapo amebainisha kuwa kupata vitabu hivyo, kupata walimu, kukamilisha miundombinu na mwamko wa wazazi kuchangia chakula watoto wao shuleni kutaufanya mkoa huo kushindana kielimu katika miaka ya mbeleni.

Katika hatua nyingine Mhe. Mtaka amewataka walimu mkoani humo kuwafundisha kwa moyo, wanafunzi kuvitumia vema vitabu hivyo na wazazi kuwafuatilia watoto wao katika masomo ili wanafunzi waweze kufanya vizuri, kwa kuwa ufaulu wa mwanafunzi hutegemea ushirikiano kati ya walimu, wanafunzi na wazazi.
 Mwakilishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Bw. Didas Hamsini(kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwa na baadhi ya viongozi na wanafunzi wa Shule ya Msingi Somanda A vitabu vya Darasa la nne mkoani humo, makabidhiano hayo yalifanyika Julai 05, 2018 katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Somanda A, mara baada ya makabidhiano ya vitabu vya Darasa la nne mkoani humo na Mwakilishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Bw. Didas Hamsini,  yaliyofanyika Julai 05, 2018 katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi.

 Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl.Julius Nestory  akihojiwa na waandishi wa habari baada ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka Mtaka kukabidhiwa vitabu vya Darasa la nne na Mwakilishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Bw. Didas Hamsini,  katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi Julai 05, 2018. 
 Mbunge wa Itilima Mkoani Simiyu,  Mhe. Njalu Silanga akihojiwa  na waandishi wa habari baada ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka Mtaka kukabidhiwa vitabu vya Darasa la nne na Mwakilishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Bw. Didas Hamsini,  katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi Julai 05, 2018. 
 Abdallah Twalib Mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Somanda A, akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kukabidhiwa vitabu vya Darasa la nne mkoani humo na Mwakilishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Bw. Didas Hamsini,  katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi. 
 Liku Malisha mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Somanda A akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kukabidhiwa vitabu vya Darasa la nne mkoani humo na Mwakilishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Bw. Didas Hamsini,  katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi 
 Afisa Elimu Halmashauri ya Mji wa Bariadi,  Mwl.Juma Mnyeti   akihojiwa na waandishi wa habari baada ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka Mtaka kukabidhiwa vitabu vya Darasa la nne na Mwakilishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Bw. Didas Hamsini,  katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi Julai 05, 2018. 
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akihojiwa  na waandishi wa habari mara baada ya kupokea vitabu vya Darasa la nne kutoka kwa Mwakilishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Bw. Didas Hamsini,  katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi Julai 05, 2018.

DKT. MWAKYEMBE AKUBALI KUKUTANA NA WATOA HUDUMA ZA MAUDHUI MTANDAONI, KUJADILIANA MALIPO YA TCRA

$
0
0
 Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii.

 Waziri wa Habri, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (pichani) amekubali kukaa na kujadiliana na Wahusika wa utoaji huduma za Maudhui Mtandaoni kujadiliana nao kwa kina namna yakulipia huduma hizo katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). 

 Akizungumza na watoa huduma hao mapema leo jijini Dar es Salaam, Dkt. Mwakyembe amesema kuwa Kanuni za Huduma hizo Mtandaoni zimetungwa na yeye Waziri mwenye dhamana ya Habari na TCRA ni Watekelezaji wa Sheria hizo.  ‘Milango bado ipo wazi kuhusu kanuni lakini zinarekebishika kukibainika kuwa na utata mkubwa, na pia kanuni hizi ni za wote’, amesema Dkt. Mwakyembe.

 Waziri huyo ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari na mtaalamu bingwa wa mambo sheria za mitandao, amesema kuwa kanuni hizo ni mpya ambapo wamekaa Wanasheria wa Wizara na Wataalam wa Mitandao kutoka TCRA kutengeneza kanuni hizo, hata hivyo amedai kila nchi inakuja kuiga mfano kwa Tanzania. 

 ‘Kanuni hizi zimetungwa kuangalia Mazingira ya nchi kutokana na Mitandao kuwa chanzo kikubwa cha Habari’, ameeleza Dkt. Mwakyembe Amesema Serikali ya Tanzania itafurahia kusimamia Kanuni ambazo zinaeleweka pamoja na kufuatwa na kila mtu.
 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza mbele ya baadhi ya Waendesha mitandao ya kijamii mbalimbali (hawapo pichani), kuhusiana na changamoto wanazokumbana nazo kufuatia kuanza kwa utekelezaji wa kanuni za maudhui ya mtandaoni zilizoanza kutumika hivi karibuni,ambapo Waziri Mwakyembe amekubali kukutana na Wadau hao ili kuangalia maeneo ya kufanyiwa marekebisho kwa namna moja ama nyingine.

Mkutano huo umefanyika mapema leo katika ofisi za Radio7  Msasani  jijini Dar es Salaam ambapo waziri Mwakyembe alikuwa amealikwa.Pichani kulia ni Mwakilishi kutoka TCRA,Ndugu Kibaja sambamba na Mmiliki  na Mkurugenzi wa Radio 7  Online Antu Mandoza na kushoto ni Kaimu MKurugenzi Idara ya Habari MAELEZO,Patric Kipangula.
  Waziri wa Habri, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa ufafanuzi kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo suala la kanuni za utoaji huduma za Maudhui Mtandaoni,alipokuwa akifanya mahojiano mafupi na kituo cha radio ya Mtandaoni Radio 7,Msasani Jijin Dar Es Salaam .  
 Mmoja wa Waendesha Mtandao wa DarMpya.Com John Marwa akiuliza moja ya swali kwa Waziri Mwakyembe kuhusiana  na kanuni/sheria za mtandao zilizoanza kutumika hivi karibuni,Mkutano huo umefanyika mapema leo katika ofisi za Radio7  Msasani  jijini Dar es Salaam ambapo waziri Mwakyembe alikuwa amealikwa.Pichani kulia ni Mwakilishi kutoka TCRA,Ndugu Kibaja sambamba na Mmiliki  na Mkurugenzi wa Radio 7  Online Antu Mandoza na kushoto ni Kaimu MKurugenzi Idara ya Habari MAELEZO,Patric Kipangulamapema leo 
 Sehemu ya Meza kuu ikichukua sehemu ya maoni yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya Wadau.

MADEREVA WA PIKIPIKI WAFURAHISHWA NA HUDUMA ZA TRA KATIKA MAONYESHO YA SABASABA

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Madereva wa Pikipiki ambao ni wanachama wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Wilaya ya Temeke (UWAPITE) wamefurahishwa na huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam.

Madereva hao wapatao 20 wametembelea banda la TRA kwa ajili ya kusajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kwa lengo la kukatia leseni mara baada ya kumaliza mafunzo ya udereza wa pikipiki yaliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke kwa kushirikiana na Umoja huo.

Akizungumza baada ya kusajiliwa madereva hao, Mwenyekiti wa Umoja huo Said Kagomba amesema kuwa, amefurahishwa na huduma nzuri waliyopatiwa na TRA ambapo wanachama wote wamesajiliwa na kupatiwa TIN kwa muda mfupi.

"Mimi kama Kiongozi wa Umoja huu nimefurahia sana huduma tuliyopata hapa TRA, kwanza tumepokelewa vizuri na kisha tumehudumiwa haraka na kila mwanachama amepatiwa cheti chake cha TIN na sasa tunaendelea na hatua nyingine ya kwenda kukata leseni," alisema Kagomba.

Naye mmoja wa Madereva hao Ramadhan Mwilombwa ametoa wito kwa vijana kujiunga katika vyama mbalimbali kwa kuwa kuna faida nyingi ikiwa ni pamoja na kupata mafunzo, TIN na leseni kwa urahisi kwa sababu viongozi wa vyama husika wanajua sheria na taratibu mbalimbali.

"Ninaomba vijana wenzangu wajiunge na vyama hivi kwa sababu palipo na wengi hakiharibiki kitu. Mimi binafsi mpaka sasa nimepata faida nyingi za kujiunga na Umoja huu, kwanza nimepata mafunzo ya udereva na kujua vizuri sheria za barabarani, pili nimefahamiana na vijana wenzangu ambao nilikuwa siwafahamu, tatu nimefanikiwa kusajiliwa na TRA na kupata TIN na mwisho kiongozi wetu ametuambia tunakwenda kukata leseni," alifafanua Mwilombwa.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inaendelea kutoa huduma mbalimbali katika Maonyesho ya Sabasaba. Miongoni mwa huduma hizo ni pamoja na kusajili walipakodi, kuelimisha wananchi umuhimu wa kulipa kodi, kutoa bili na kulipa Kodi ya Majengo.

Huduma nyingine ni kuelezea wananchi haki na wajibu wa Mlipakodi kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Huduma na Mlipakodi, kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risti (EFDs), kuelezea mwenendo wa makusanyo ya mapato ya Serikali, na kupokea maoni, malalamiko, mrejesho pamoja na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wananchi.
Wanachama wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Wilaya ya Temeke (UWAPITE) jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwa wameshika Namba za Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) wakati wa Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018.
Afisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Helly Shindano Akimhudumia Dereva wa Pikipiki katika banda la TRA wakati wa Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018.
Wanachama wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Wilaya ya Temeke (UWAPITE) jijini Dar es Salaam wakiwa katika banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakisubiri kupatiwa huduma ya usajili na kupewa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) wakati wa Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018.
Afisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Jackline Lutare akisikiliza kero za mteja katika banda la TRA wakati wa Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA)

TFDA iwe chachu ya Uchumi wa Viwanda nchini.

$
0
0
Na  WAMJW,Dar as Salaam

Mamlaka ya chakula na dawa TFDA imetakiwa kuwa chachu ya uchumi wa viwanda hususani katika kuzalisha dawa hapa nchini ili kupata matokeo chanya katika hatua ya kuinua uchumi wa viwanda.

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa kukabidhi vyeti vya ithibaki kwa kiwango cha kimataifa ISO 17025 kwa maabara ya chakula na maikrobailojia za TFDA.

"TFDA isiwe kikwazo kwa wawekezaji nchini hususan Viwanda vya kuzalisha dawa ili kuunga mkono juhudi za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli ya kuelekea uchumi wa viwanda"

Aidha,Waziri Ummy amesema TFDA wanawajibu wa kuwawezesha wafanyabiashara kutoa bidhaa zao wanazozileta nchini mapema zaidi Mara wanapokuwa wamejiridhisha na ubora unaokidhi afya za watanzania na kuwapa vibali mapema.Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA )Agnes's kijo amesema wanawajibu wa kuimarisha afya za watanzania na kuimarisha maabara zao kwa viwango vinavyokubalika kitaifa.

Kijo amesema vyeti hivyo vya kimataifa ni ishara kubwa inayoonyesha Kuwa TFDA inafanya kazi katika kudhibiti ubora wa bidhaa hususan vyakula na dawa ili kujenga afya za wananchi.TFDA imepokea vyeti vya uthibiti kwa kiwango cha kimataifa kwa maabara ya chakula na daea ambapo wamefanya vizuri katika upimaji wa vyakula na dawa vinavyoingia na kutoka nchini.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA na baadhi ya wadau wa afya hawapo pichani wakati wa upokeaji wa vyeti vya Ithibati kwa kiwango cha kimataifa iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Bi. Agness Kijo akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo na baadhi ya wadau wa afya hawapo pichani wakati wa upokeaji wa vyeti vya Ithibati kwa kiwango cha kimataifa iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa kushoto akikata utepe kuashiria kupokea rasmi vyeti vya Ithibati kwa kiwango cha kimataifa walivyopewa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA katika hafla ya kupokea vyeti hivyo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Maabara wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA wakati wa upokeaji wa vyeti vya Ithibati kwa kiwango cha kimataifa iliyofanyika leo jijini Dar es salaam, wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Bi. Agness Kijo.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Sehemu ya tendaji wa Mamlaka ya chakula na dawa

UBALOZI WA JAPAN WAMUUNGA MKONO WAZIRI UMMY MWALIMU KUJENGA MADARASA SITA YA SHULE YA MSINGI MWAKIDILA JIJINI TANGA

$
0
0
SHIRIKA la Maendeleo ya Wanawake mkoani Tanga (Tanga Women Development Initiative-TAWODE) chini ya Mwenyekiti wale Waziri Ummy Mwalimu (MB) leo wamewekeana saini ya ujenzi wa madarasa sita ya shule ya msingi kata ya Tanga sisi katika Jiji la Tanga. 

Msaada huo wenye thamani hya dola za kimarekani 84,000 (Takribani shilingi za kitanzania milioni 188) umetolewa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kufuatia maombi ya Mwenyekiti wa TAWODE Mh Ummy Mwalimu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari katika Jiji la Tanga. 

Akizungumza katika halfa hiyo Mh Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida alisema serikali ya Japan imetoa fedha hizo ili kuwasaidia maendeleo ya elimu kwa Jiji la Tanga ili kutatua tatizo la mrundikaano wa wanafunzi madarasani huku akiwataka Tawode kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kikamilifu na kukamilika kwa wakati. 

Naye mgeni rasmi katika uzinduzi huo,Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu aliushukuru ubalozi wa Japan kwa kukubali ombi lao la kufadhili ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Mwakidila ambayo ina wanafunzi zaidi ya 1400 kulinganisha na madarasa machache yaliyopo na hivyo kusababisha mrundikano mkubwa kwa wanafunzi. 

Aidha Waziri Ummy alieleza kuwa ongezeko la wanafunzi limechangiwa na uamuzi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli wa kutoa elimu bure hivyo wakati serikali ikiweka jitihada kubwa za kuboresha miundombinu ya elimu katika Halmashauri mbalimbali kote nchini bado zipo changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa madarasa. 

Alisema kutokana na hilo wao kama sehemu ya wana jamii wa Jiji la Tanga waliona wana wajibu wa kutafauta vyanzo vingine vya fedha ili kuwezesha elimu ya msingi mpaka kidato cha nne kutolewa bure bila vikwazo vyoyote. 

Waziri Ummy alisema fedha zilizotolewa na ubalozi wa Japan ni za Jamii ya wana Tanga kwa maendeleo ya Tanga hivyo shirika la TAWODE kupitia Halmashauri ya Jiji la Tanga itahakikisha msaada huo unatumika kikamilifu na mradi kukamilika kwa wakati ili kupunguza changamoto ya mrundikano wa wanafunzi madarasani. 

Naye kwa upande wake,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Mhina Selebosi aliushuruku ubalozi wa Japan kwa kufadhili ujenzi wa madarasa hayo ikiwemo kumpongeza Waziri Ummy Mwalimu kwa kuwa mstari wa mbele katika kusukuma mbele maendeleo ya wananchi wa Jiji la Tanga hasa katika sekta ya Afya na Elimu. 

Hata hivyo pia Mstahiki Meya hiyo alimkaribisha Balozi wa Japan kutembelea Jiji la Tanga ikiwemo shule ya Sekondari ya Japani iliyojengwa kwa ufadhili wa serikali ya Japan. 
Mkurugenzi waShirika la Maendeleo ya Wanawake mkoani Tanga(Tanga Women Development Initiative-TAWODE) Tawode Fatuma Mganga kushoto akisaini na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida Msaada huo wenye thamani hya dola za kimarekani 84,000 (Takribani shilingi za kitanzania milioni 188) umetolewa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kufuatia maombi ya Mwenyekiti wa TAWODE Mh Ummy Mwalimu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari katika Jiji la Tanga. wanaoshuhudia ni Mstahiki meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Selebosi na kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
 Mkurugenzi waShirika la Maendeleo ya Wanawake mkoani Tanga(Tanga Women Development Initiative-TAWODE) Tawode Fatuma Mganga kushoto na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida wakionyesha hati za makubaliano ya msaada huo wenye thamani hya dola za kimarekani 84,000 (Takribani shilingi za kitanzania milioni 188) umetolewa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kufuatia maombi ya Mwenyekiti wa TAWODE Mh Ummy Mwalimu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari katika Jiji la Tanga.
 Mkurugenzi waShirika la Maendeleo ya Wanawake mkoani Tanga(Tanga Women Development Initiative-TAWODE) Tawode Fatuma Mganga kushoto wakibalishana hati za makubaliano na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida Msaada huo wenye thamani hya dola za kimarekani 84,000 (Takribani shilingi za kitanzania milioni 188) umetolewa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kufuatia maombi ya Mwenyekiti wa TAWODE Mh Ummy Mwalimu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari katika Jiji la Tanga.
 Mkurugenzi waShirika la Maendeleo ya Wanawake mkoani Tanga(Tanga Women Development Initiative-TAWODE) Tawode Fatuma Mganga kushoto akimshukuru Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida Msaada huo wenye thamani hya dola za kimarekani 84,000 (Takribani shilingi za kitanzania milioni 188) umetolewa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kufuatia maombi ya Mwenyekiti wa TAWODE Mh Ummy Mwalimu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari katika Jiji la Tanga.
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika akiwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida kulia Msaada huo wenye thamani hya dola za kimarekani 84,000 (Takribani shilingi za kitanzania milioni 188) umetolewa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kufuatia maombi ya Mwenyekiti wa TAWODE Mh Ummy Mwalimu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari katika Jiji la Tanga. kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Selebosi kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
Waziri Ummy akishukuru Ubalozi wa Japani kwa kusaidia juhudi za sekta ya elimu
 Mkurugenzi waShirika la Maendeleo ya Wanawake mkoani Tanga(Tanga Women Development Initiative-TAWODE) Tawode Fatuma Mganga kulia akiwa na Balozi wa Japan nchini katikati mara baada ya kumalizika makubaliano hayo
NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM.

BAADHI YA MAWAZIRI WATEMBELEA BANDA LA TRA KATIKA MAONYESHO YA SABASABA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenister Muhagama akimsikiliza kwa makini Afisa Mwandamizi Uchambuzi Mifumo ya Biashara Mathias Chanila wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati Waziri huyo alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018 yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (kushoto) akitoa maoni yake kwa Afisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Chama Siriwa (kulia) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018 yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenister Muhagama.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akionyeshwa bili ya majengo na Meneja wa Huduma kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Honester Ndunguru wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018 yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka Shule ya Sekondari St. Joseph Cathedral Tax Club iliyopo jijini Dar es Salaam Bertha Bureta akimuelezea Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji faida za kulipa kodi wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018 yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA)

TCAA YASHAURIWA KUWEKEZA KWENYE WATAALAMU WA NDANI

$
0
0
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga, Aristide Kanje, akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu kozi zinazotolewa, wakati kamati hiyo ilipotembelea chuo hicho, jijini Dar es Salaam. Wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Selemani Kakoso.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Hawa Mchafu, akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (kushoto), wakati kamati hiyo ilipotembelea Chuo cha Usafiri wa Anga, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga, Aristide Kanje akiwaonesha Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu eneo la Chuo hicho, wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara chuoni hapo, jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Selemani Kakoso
Muonekano wa jengo la rada katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambalo linaendelea kujengwa, jijini Dar es Salaam. Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwakani.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA), Hamza Johari, akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa rada ya kisasa inayosimikwa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani Kakoso, akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA), Hamza Johari (Kushoto), mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa rada katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Richard Mayongela, akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo, wakati Kamati hiyo ilipokuwa kwenye ziara ya mafunzo, jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa gari jipya la Zimamoto lililonunuliwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA). Gari hilo litatoa huduma katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.



Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeishauri Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA) kuwekeza kwenye rasilimali watu ili kuongeza tija kwa wataalam wa ndani mara baada mradi wa ujenzi wa rada nne kukamilika.

Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa rada katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mwl. Julius Nyerere (JNIA), Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Selemani Kakoso, amesema kuwawezesha wataalam wa ndani kutawajengea uwezo wa kwenda na kasi ya teknolojia kwenye uongozaji ndege.

“Mradi huu utatumia fedha nyingi hivyo ni vyema kuzingatia wataalam wa ndani kupata elimu ya rada hizi ili mradi ukikamilika wasimamie vyema na si watalaam kutoka nje ya nchi”, amesisitiza Mhe. Kakoso.Mhe. Kakoso, amesema kuwa Kamati imeridhishwa na kasi ya ujenzi wa rada unaoendelea na kuwataka mradi ukamilike kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa kwenye mkataba.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa, amesema uboreshaji wa Viwanja vya ndege mbalimbali nchini unafanywa kwa pamoja na ufufuaji wa Shirika la Ndege ambapo mpaka sasa Serikali imeshanunua ndege sita.Naye Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari ameihakikishia Kamati kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati na kwa viwango na kusema kuwa tayari kuna wataalam zaidi ya 20 ambao watapata mafunzo ili kuongoza rada hizo mara baada ya mradi kukamilika.

“Nawahakikishi Waheshimiwa Wabunge kuwa mradi huu utakamilika kwani hakuna changamoto yoyote kifedha na kiutalaam kwani fedha zipo na wataalam wapo, hivyo hatuna sababu za kuchelewesha mradi” amesema Johari.Katika hatua nyingine Kamati imetembelea Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kuipongeza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), kwa kununua gari jipya la Zimamoto ambalo litatumika katika kiwanja hicho na kukifanya kuendelea kuwa salama kwa kuzingatia viwango vya Kimataifa vya Usafiri wa Anga.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>