Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMKABIDHI DKT TIZEBA MATREKTA 500 YA URSUS

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim M. Majaliwa (Mb) akimkabidhi hati ya makabidhiano Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba ya matrekta 500 yaliyonunuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo nchini katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi matrekta 560 yaliyonunuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo nchini katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara ya Uwekezaji, Charles Mwijage, Wapili kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na kulia ni Naibu Waziri wake, Dkt, Mary Mwanjelwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba Kitabu cha Mwongozo wa Taratibu za Kujenga Kiwanda Nchini Tanzania baada ya kufungua Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba (Mwenye maiki) akizungumza kabla ya kukabidhiwa matrekta 500 yaliyonunuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo nchini katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe ikiwa ni ishra ya kukabidhi matrekta 560 yaliyonunuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo nchini katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara ya Uwekezaji, Charles Mwijage na kushoto ni Naibu Waziri wake, Mhandishi Stella Manyanya. Wapili kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na kulia ni Naibu Waziri wake, Dkt, Mary Mwanjelwa


Na Mathias Canal, Dar es salaam

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) leo 4 Julai 2018 amemkabidhi Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba jumla ya matrekta 500 yatakayopelekwa kwa vyama vya ushirika vya msingi ili wakulima kunufaika na tija katika kilimo hususani zao la Pamba.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 42 ya sabasaba katika viwanja vya Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam, Mhe. Dkt Tizeba alisema kuwa sekta ya kilimo nchini bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo tija ndogo inayosababishwa na matumizi madogo ya pembejeo, huduma duni za ugani na matumizi ya zana duni za kilimo ambapo wakulima wengi wanatumia majembe ya mkono au kutumia maksai wakati wa kulima.

“Katika kilimo cha Pamba msimu wa mwaka 2017/2018 ushahidi unaonyesha kwamba wakulima walichelewa kuanza kuandaa mashamba yao kwa sababu Maksai wakati wa kiangazi wanadhoofu sana, na mara mvua inaponyesha hawawezi kulima mpaka majani yawe mengi ndio wapate nguvu za kuanza kulima, hali hii inaondoa uwezekano wa wakulima kutumia teknolojia mpya katika kilimo kama vile kilimo hifadhi ambacho kimedhihirika kuongeza tija zaidi ya mara mbili” Alikaririwa Mhe Dkt. Tizeba

Aliitaja mikoa itakayoanza kunufaika na mpango huo katika awamu hii ya kwanza kuwa ni pamoja na Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Tabora na Geita, awamu ya pili ikijumuisha mikoa ya Singida, Kagera, na Kigoma huku awamu ya tatu ikitarajiwa kuhusisha mikoa ya Kanda ya Mashariki kwa kuzingatia ongezeko la uzalishaji wa pamba katika maeneo hayo.

Mhe Tizeba alisema mtazamo wa mpango huo ni kuunganisha nguvu za mkulima mmoja mmoja ili kuharakisha kuleta maendeleo yao ambapo utatekelezwa kwa kutumia sehemu ya fedha zinazolipwa AMCOS kama kamisheni ya kusimamia ununuzi wa pamba ambapo matarajio ni kukusanya Bilioni 6 kama uzalishaji wa pamba utafika kilo milioni 400 kwa mwaka.

Mhe. Dkt Tizeba alimuhakikishia Waziri Mkuu kuwa Wizara ya kilimo itatekeleza mpango huo kupitia kwa Mrajis na Bodi ya Pamba ambapo kutakuwa na vituo vinane (8) vya kusimamia Trekta hizo huku kituo kimoja kikiwa ni kwa kila mkoa na viwili kwa mikoa mikubwa inayozalisha pamba kwa wingi.

Aidha, alisema kuwa vituo vitatoa mafunzo kwa madereva na vitafuatilia matengenezo na ushauri wa kitaalamu kuhusu usimamizi wa zana hizo ambapo hadi sasa wizara ya kilimo imepeleka wahandisi wanne (4) na wengine wawili (2) watapelekwa hivi karibuni katika kituo cha kuunganisha matrekta kilichopo Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani ambapo lengo ni kuwapa uzoezfu na uelewa mpana wa kitaalamu wa usimamizi wa matrekta hayo.

Aliongeza kuwa ili kufanikisha azma hiyo ya kimapinduzi itafanya kazi kwa ufasaha na wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri ili utekelezaji uweze kupata mafanikio na kufanikisha mtazamo wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli katika hatua anazozichukua za kuboresha kilimo nchini ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika sherehe hizo Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa amemkabidhi waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba matrekta 500 ya Ursus kwa ajili ya wateja wa mwanzo katika awamu ya kwanza ya uunganishaji wa matrekta maalumu kwa ajili ya shughuli za kilimo vijijini huku Jeshi la Magereza likikabidhiwa matrekta 50 na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Matrekta 10.

NiDA NA RITA WAENDELEA KUTOA HUDUMA KWENYE MAONYESHO YA SABASABA

$
0
0

Afisa Habari wa RITA Jaffar Malema akiendelea na zoezi la kuita majina kwa ajili kuwapatia vyeti vya kuzaliwa kwenye maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa RITA wakiwa wanatoa huduma kwa wananchi waliojitokeza katika banda hilo kupata huduma ya vyeti vya kuzaliwa kwenye maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Wananchi waliojitokeza katika Banda la Mamlaka ya Vitambulisho ya Taifa (NIDA) kwa ajili ya kujipatia huduma za vyeti vya kuzaliwa kwenye maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)



Wananchi waliojitokeza katika Banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA kwa ajili ya kujipatia huduma ya vitambulisho vya Taifa kwenye maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

JIJI HALINA MAMLAKA KUTOA KIBALI CHOCHOTE BILA MAMLAKA HUSIKA KUJUA-DC HAPI

WAZIRI KIGWANGALLA AHITIMISHA ZIARA YAKE MKOANI MBEYA, ATEMBELEA MAPOROMOKO YA KIMANI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga picha ya pamoja (Selfie) kwa kutumia simu yake ya mkononi na baadhi ya wafanyakazi wa Pori la Akiba Mpanga Kipengere alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi. Nyuma yao ni Maporomoko ya Mto Kimani ambayo yana urefu wa mita 70, na ni chanzo kikuu cha maji yanayounda mto Ruaha hadi mto Rufiji. 

Mbali na maporomoko hayo pori hilo pia lina wanyamapori mbalimbali ikiwemo Tumbili, Nyani, Tandala, jamii ya ndege mbalimbali ikiwemo wahamao kutoka ulaya wakati wa baridi kali na aina mbalimbali za maua ya asili ya kuvutia. 

Dk. Kigwangalla amesema maporomoko hayo hayakuwahi kutumika ipasavyo kiutalii kutokana na kukosekana kwa miundombinu muhimu ikiwemo barabara ya kufika eneo hilo. Amesema katika mwaka huu wa fedha Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuboresha barabara hizo pamoja na kujenga ngazi kushuka kwenye kina cha maporomoko hayo hadi upande wa pili. Pori hilo pia lina kivutio cha pango alilojificha chief Mkwawa wakati wa vita ya pili ya dunia. 

Kuna aina mbalimbali za utalii katika pori hilo ikiwemo utalii wa kupanda mlima, utalii wa kuogelea, utalii wa kutembea kwa miguu na utalii wa picha.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua shughuli za uhifadhi katika Pori la Akiba Mpanga Kipengere ambalo lipo katika wilaya za Mbarali (Mbeya), Makete na Wanging'ombe (Njombe) jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua shughuli za uhifadhi katika Pori la Akiba Mpanga Kipengere ambalo lipo katika wilaya za Mbarali (Mbeya), Makete na Wanging'ombe (Njombe) jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga jaramba wakati akikagua shughuli za uhifadhi katika Pori la Akiba Mpanga Kipengere ambalo lipo katika wilaya za Mbarali (Mbeya), Makete na Wanging'ombe (Njombe) jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa Maporomoko ya Mto Kimani (hayako pichani) na Meneja wa Pori la Akiba Mpanga Kipengere, Stanslaus Odhiambo alipotembelea pori hilo kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Makete mkoani Njombe jana. Maporomoko hayo yenye urefu wa mita 70 ni chanzo kikuu cha mto Ruaha Mkuu na Mdogo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa ramani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo, Dk. Chris Timbuka (wa pili kulia) alipotembelea bonde la Ihefu kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Mbeya jana. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani Nkuwi na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfaume.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa Maporomoko ya Mto Kimani na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani Nkuwi alipotembelea Pori la Akiba Mpanga Kipengere ambalo lipo katika wilaya za Mbarali (Mbeya), Makete na Wanging'ombe (Njombe). Maporomoko hayo yenye urefu wa mita 70 ni chanzo kikuu cha mto Ruaha Mkuu na Mdogo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Wawindi iliyopo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo iliyofadhiliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) shuleni hapo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Igaza iliyopo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo iliyofadhiliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) shuleni hapo.

DAWASCO YATAKIWA KUWEKA MITA ZA KIELEKTRONIKI

$
0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO) wakati wa ziara ya kujitambulisha mapema leo ofisi za DAWASCO. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja alitoa maelekezo machache wakati wa ziara ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa ofisi za DAWASCO mapema leo alipofanya ziara ya kujitambulisha.
Wafanyakazi wa DAWASCO wakifuatilia maelezo ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa akipokelewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati akipokelewa ofisi za DAWASCO mapema leo alipofanya ziara ya kujitambulisha.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa akiagana na wafanyakazi wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO) wakati wa ziara ya kujitambulisha mapema leo ofisi za DAWASCO.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Makame Mbarawa. 

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

Waziri wa Maji na umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa ameliagiza Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASCO) kuhakikisha linabadili mfumo wa mita zinazotumika sasa kuhamia kwenye mfumo wa kieletroniki ambao utawafanya wateja wake walipe kabla ya kutumia hatua ambayo itasaidia katika ukusanyaji wa mapato na kudhibiti upotevu wa mapato. 

Maagizo hayo ameyatoa mapema leo Julai 4, 2018 alipotembelea shirika hilo mara baada ya kuteuliwa mwishoni mwa wiki kuingia kwenye wizara ambapo amesema awali aliwahi kuteuliwa lakini alikaa muda mfupi ambapo aliacha maagizo kadhaa ikiwemo hilo la mita ambalo kwa sasa amewataka walitilie mkazo. 

Amesema kuwa malengo ya wizara yake kuwa ni kuwafikishia wananchi wanyonge huduma ambayo ni muhimu na hivyo amewataka watendaji wa DAWASCO kutoka na kwenda kushughulikia kero za wananchi na kuhakikisha zinatatuliwa kwa wakati. "Nawaomba tufanye kazi kwa uadilifu na kuacha kuwanyanyasa wananchi kwa kuwapelekea bili zisizoeleweka kabisa maana hizi mita za zamani zinapoteza maji na vile vile fedha ya shirika," 

Amesema Prof. Mbarawa. Aidha ameongeza suala la wafanyakazi kuingia mikataba ya kiutendaji ambayo anaamini endapo itafuatwa itaweza kubadilisha sura ya shirika hilo huku akiigiza bodi ya wakurugenzi kuhakikisha inaongeza wateja kutoka 290,000 waliopo sasa hadi kufikia 850,000 kwa mwaka hatua ambayo itaongeza mapato zaidi ya mara tatu lakini pia amesema suala la upotevu wa maji lipewe kipaumbele ili kudhibiti fedha nyingi zinazopotea kupitia upotevu huo. 

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kwa sasa DAWASCO ina mipango mingi ambayo inakwenda kutekelezwa na ndiyo maana ameamua kuingia mikataba na watumishi wa shirika hilo ili kufikai malengo hayo kwa urahisi huku likiendelea kubuni mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamaoto zinazojitokeza ikiwemo upotevu wa maji ambapo mita 155 zitabadilishwa ambazo zilikuwa chakavu.

Watoto wa Kitanzania waweka lengo la kuipeleka Tanzania Kombe la Dunia

$
0
0

RAIA wa Tanzania Laigwanani Mollel na Ziporah Godfrey Mollel walioshiriki michuano ya soka kimataifa ya Football for Friendship(F4F) wameondoka Urusi kurejea Tanzania wakiwa na ndoto yakuiwakilisha Tanzania katika Kombe la Dunia siku moja.

Michuano hiyo ya F4F ilishirikisha watoto wenye miaka 12 kutoka nchi 211 na imefanyika kwa mwaka wa sita tangu kuanzishwa kwake. Laigwanani na Ziporah wakitokea akademi ya Lengo Football ya Arusha Tanzania wameondoka Urusi kurejea Tanzania wakisema ndoto yao kubwa ni kuiwakilisha Tanzania katika Kombe la Dunia siku za usoni.

“Niiwakilisha vizuri Tanzania kwa kupeperusha bendera ya taifa kwenye sherehe za ufunguzi wa Kombe la Dunia mwaka huu, ilikuwa kabla ya mechi ya ufunguzi ya Urusi na Saudi Arabia. “Nilikuwa na uchovu sana baada ya kazi ya siku ile lakini naamini nimepata hamasa ya kuiwakilisha nchi yangu katika Kombe la Dunia siku zijazo kwa mimi mwenyewe kucheza uwanjani,” alisema Laigwanani.

Kwa upande wake, Ziporah alisema; “Nitakua na faraja sana kwa sababu Tanzania haijawahi kufuzu katika fainali za Kombe la Dunia, hivyo nitakuwa ni mimi ninaye iwakilisha nchi yangu. “Nitajisikia ujasiri na nitaiwakilisha nchi yangu vizuri na najua katika mawazo yangu kuwa siku moja Tanzania itakuwa hapa katika fainali za Kombe la Dunia.”

Program hii ya Kijamii ya F4F ni programu ya kijamii inayojumuisha siku tatu za mafunzo ya soka na kila timu kati ya timu 32 kutoka duniani kote zilizipewa majina ya wanyama walio hatarini kupotea. Timu zilizoundwa zilijumuisha wachezaji kutoka kila pembe ya dunia, kutoka mataifa makubwa na wadogo bila kujali, dini, tamaduni na ushawishi wa kisiasa na wa kiitikadi.


KIWANDA CHA ASAS DAIRIERS LTD CHAIBUKA MSHINDI KIPENGELE CHA "FOOD AND BEVERAGES" MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akimkabidhi kikombe cha ushindi wa jumla kipengele cha (Foods and Beverages) Bw. Jimmy Kiwelu Meneja wa Masoko na Matukio kiwanda cha ASAS DAIRIERS LTD katika maonyesho ya biashara ya Sabasaba kwenye viwanja vya TANTRADE barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-TANTRADE)
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akipokea zawadi kutoka kwa Meneja wa Masoko na Matukio kiwanda cha ASAS DAIRIERS LTD Bw. Jimmy Kiwelu wakati alipotembelea katika banda hilo katika maonyesho ya biashara ya Sabasaba kwenye viwanja vya TANTRADE barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Masoko na Matukio kiwanda cha ASAS DAIRIERS LTD Bw. Jimmy Kiwelu wakati alipotembelea katika banda hilo leo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiakionyeshwa na Meneja wa Masoko na Matukio kiwanda cha ASAS DAIRIERS LTD Bw. Jimmy Kiwelu vikombe mbalimbali ambavyo Kiwanda hicho kimewahi kujishindia wakati alipotembelea katika banda hilo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akitembelea kitengo cha wateja wakubwa cha kiwanda cha ASAS DAIRIERS LTD wakati alipotembelea katika banda hilo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akitoka nje ya banda la kiwanda cha ASAS DAIRIERS LTD wakati alipolitembelea leo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi kwa kuwapungia mkono mara baada ya kutoka katika banda la kiwanda cha ASAS DAIRIERS LTD wakati alipolitembelea
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiendelea kutembelea mabanda mengine katika viwanja vya Sabasaba mara baada ya kuzindua rasmi maonesho hayo.

GPSA YAUNGA MKONO JUHUDI ZA KUTOA ELIMU BURE KWA KUSAIDIA VIFAA VYA KUFUNDISHIA KWA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAKALA wa Huduma ya Ununuzi Serikalini(GPSA)umetoa msaada wa vifaa vya kufundishia kwa shule za msingi na sekondari wenye thamani ya zaidi ya Sh.milioni tisa.

Umefafanua kuwa wanatambua juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli ya kutoa elimu bure,hivyo wameamua kuunga mkono juhudi hizo kwa vitendo kwa kutoa msaada huo.

Akizungumza leo katika Shule ya Msingi Kilimahewa iliyopo wilayani Temeke jijini Dar es Salaam Kaimu Mtendaji Mkuu wa GPSA Lilian Mwinuka amefafanua utoaji wa msaada huo pia ni sehemu ya kuadhimisha miaka 10 tangu wakala huo ulipoanzishwa. Amefafanua kutokana na kutimiza miaka 10 tangu kuanza kwa wakala huo wameona ipo haja ya kurudisha shukrani kwa jamii na wakaona haja ya kusaidia vifaa vya kufundishia.

"Kwa leo tumekabidhi msaada huo wa vifaa vya kufundishia kwa shule nne za Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Tumekabidhi kwa shule hizi kwa niaba ya shule zote za Dar es Salaam."Nijukumu letu kurudisha fadhila na shukrani zetu kwa jamii na tumeona tutoe vifaa vya kufundishia shuleni. Ni jukumu letu kuunga mkono uamuzi wa Serikali wa kutoa elimu bure,"amesema Mwinuka.

Ametaja baadhi ya msaada ambao wameutoa ni chaki, daftari, ufutio wa ubaoni, kalamu, na vifaa vya kuhifadhia taka. Mwinuka ameongeza baada ya kutoa msaada huo Dar es Salaam watakwenda kutoa msaada kama huo wa vifaa kwa shule zilizopo mkoani Dodoma siku za karibuni. Akizungumzia kuhusu GPSA Mwinuka amesema vifaa ambazo wanauza bei yake iko chini ukilinganisha na maeneo mengine kwasababu wao hawapo kwa ajili ya kupata faida kubwa.

Hivyo amewashauri Watanzania kwenda uununuzi kwao kwani mbali ya unafuu wa gharama pia ziko imara."Bidhaa zetu ni bora na zinapatikana kwa bei nafuu, sababu kubwa sisi tunaagiza moja kwa moja kwa wazalishaji, hivyo bei yetu ni yakawaida,"amesema. Hivyo amewahamiza Watanzania kununua bidhaa zao na kufafanua kauli mbiu yao inasemaje "Okoa fedha za umma kwa kufanya ununuzi kupitia GPSA.

Kwa upande wao baadhi ya walimu kutoka shule ambazo wamepatiwa msaada huo wakiongozwa na Kaimu Ofisa Elimu wa Wilaya Bakari Mnondwa wameahukuru kwa msaada huo. Pia ameomba wadau wengine nao kusaidia sekta ya elimu na kufafanua msaada ambao wameupata umeongezeka chache ya wao kufanyakazi ya kufundishia kwa amri zaidi.
Kuhusu changamoto ambayo wanakabilana kwa Wilaya yake Temeke ni uhaba wa vyumbo vya madarasa 2,162 huku idadi ya wanafunzi wa shule ni 161,313.

.Kaimu Mtendaji Mkuu wa GPSA LIlian Mwinuka akikabihi vifaa kwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Karume iliyopo wilayani Temeke jijini Dar es Salaam Hillgaro Lwambusha.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kilimahewa, walimu wa shule nne ambazo zimekabidhiwa msaada huo pamoja na uongozi wa GPSA ukiongozwa na Kaimu Mtendaji wao Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) Lilian Mwinuka(kulia) akizungumza katika Shule ya Msingi Kilimahewa baada ya kukabidhi msaada wa vifaa vya kufundishia kwa shule za msingi wenye thamani ya zaidi ya Sh.Milioni tisa.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa GPSA LIlian Mwinuka (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wengine baada ya kukabidhi msaada wa vifaa vya kufundishia kwa shule za msingi na sekondari ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kutoa elimu bure.

BENKI YA CRDB YAVUTIA WENGI MAONYESHO YA SABASABA 2018

$
0
0
 Wananchi waliofika katika Maonyesho ya Sabasaba wakipata huduma za kutoa pesa na kuweka katika Mobile Branch.
Wananchi wakipata huduma za kifedha katika banda la Benki ya CRDB katika Maonyesho ya Sabasaba.
 Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Lumumba, Pendo Assey (kushoto), akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Jessica Nyachiro, alipotembelea Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa 'Sabasaba'.
Wateja wa Benki ya CRDB wakijaza fomu kwa ajili ya kupata huduma.
Baadhi ya wateja waliofika katika banda la Benki ya CRDB katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa 'Sabasaba' wakipata huduma za kutoa na kuweka fedha kwa wakala wa benki hiyo.
Mteja akipata huduma kwa Wakala wa Fahari Huduma.
Mteja akipata huduma.

Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Lumumba, Mamertus Luena, akitoa huduma kwa mteja.
Watu wakipata huduma katika Banda laBenki ya CRDB.
Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Jessica Nyachiro, akisaini kitabu cha wageni alipofika katika banda la Benki ya CRDB katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa 'Sabasaba' inayoendelea jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Benki Kidigitali wa Benki ya CRDB, Mangire Kibanda, akisaini kitabu cha wageni.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa benki hiyo.

Halmashauri ya yatenga Millioni 370 kuchimba Visima katika Vijiji 16 Tarime.

$
0
0
Na Frankius Cleophace Tarime.

Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini Mkoani Mara,  imeanza rasmi kazi ya kuchimba Visima Virefu Vya Maji katika Vijiji 16 kati ya Vijiji 88 vyenye thamani ya Shilingi Millini 370, kwa lengo la kupunguza adha ya upatikanaji wa Maji na akina Mama kutembea umbali mrefu ili kutafuta Maji.

Moses Misiwa Yomami ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini amesema kuwa katika Mwaka wa fedha 2016-2017 Halmashauri ilitenga kiasi cha Fedha Mill 150 lakini kwa ajili ya kuchimba Visima Vijiji vya Matongo na Kemambo lakini zoezi hilo halikufanikiwa kwa sababu ya ukosefu wa pesa zilizotengwaambapo Mwaka wa Fedha ambao unamalizika 2017-2018 wametenga Kiasi cha Shilingi Millioni 370 na Vijiji 16 kati ya 88 Vinaenda kunufaika na Mradi wa Kuchimba Visima Vya Maji.

“Tuna Mikaba Miwili hapa Kuna Mkataba wa Visima Nane Virefu vya pampu  Vyenye Thamani ya Shilingi 204 katika Vijiji Nane na Mkataba wa Pili Visima Shilingi Mill 170 ambapo jumla ya fedha tunazitoa kwa ajili ya Uchimbaji wa Visima kupitia Mapato ya ndani itakuwa Jumla ya Shilingi 370” alisema Misiwa.

Yomami ametaja kuwa Vijiji 16 katika Halmashauri hiyo vitanufaika na Mradi kuwa ni Gibaso, Kitawasi, Mutana, Surubu, Nyantira, Boga A Kwisarara na Mangucha pia katika mkataba wa Pili Vijiji Vitakavyonufaika ni Weigita, Nyamirambaro, Mutana, Kimusi, Kewanja, Mjini Kati na Nyangongo jumla Vijiji 16 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini.

Licha ya Serikali kuletea Maendeleo Wananchi wananchi hao wamekuwa wakidai fidia pale Miradi inapopita ambapo Mwenyekiti amessma kuwa wananachi wamekubali Miradi hiyo hivyo hakuna haja ya kuomba Fidia pale miradi inapofanyika.

Yomami ameongeza kuwa Nyuma kampuni iiyopewa kazi ilikuwa ikifanya Utafiti na kuchukua Mchanga na Kampuni nyingine inakuja kuchimba ikikosa Maji wanashindwa kuwabana kwa madai wao hawakufanya utafiti kazi yao ilikuwa ni Kuchimba Maji lakini kwa Mikaba iliyotolewa kwa sasa imeboreshwa anayechimba Visima hivyo ndiye atakayefanya Utafiti wa eneo lenye maji hiyo yakikosa lazima awajibike yeye mwenyewe na siyo mtu mwingine.

Mwenyekiti amesisitiza Wananchi kulinda Miundombinu ya Maji itakayojengwa Maeneo tofauti kwani Miradi ya Maji imekuwa ikiharibika kwa sababu ya kuaribu Miundombinu hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Moses Misiwa Yomami akiwa ofisi kwake baada ya Kuongea na Vyombo vya habari kuhusu Mradi huo wa kuchimba Visima hivyo.

WAZIRI KIGWANGALLA AAGIZA TFS KUCHANGIA MILIONI 20 KWA AJILI YA UJENZI WA ZAHANATI SUMBAWANGA

$
0
0


Na Hamza Temba, Rukwa


Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS kuchangia shilingi milioni 20 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Mponda katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

Ametoa agizo hilo kufuatia taarifa iliyowasilishwa kwake na Mtendaji wa Kata ya Majengo, Matage Bikaniko Mjarifu alipotembelea kijiji hicho kinachopakana na Msitu wa Mbizi ambapo amesema wananchi wa kijiji hicho husafiri umbali mrefu wa zaidi ya kilomita 11 kwa ajili ya kufuata huduma za afya mjini Sumbawanga.

Amesema mpaka sasa wananchi wa kijiji hicho wameshachangia shilingi laki 9 na Mbunge wa Sumbawanga mjini shlingi milioni 5. Hata hivyo amesema jumla ya shilingi milioni 134 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo.

Kufuatia taarifa hiyo, Waziri Kigwangalla alisema Wizara yake kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS itachangia shilingi Milioni ishirini hivyo wananchi wapambane kwa kushirikiana na halmashauri yao ili jengo hilo lisimame na hatimaye fedha hizo ziwasilishwe kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wake.  

Alisema Falsafa ya Uhifadhi Endelevu ni Uhifadhi Shirikishi Jamii, hivyo wizara yake itaendelea kusimamia sera ya kuhakikisha wananchi hususan wanaoishi jirani na maeneo ya hifadhi wananufaika moja kwa moja na hifadhi hizo kupitia miradi ya maendeleo.

Dk. Kigwangalla ameziagiza taasisi zote za uhifadhi nchini kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya jamii ili wananchi wanaoishi jirani na hifadhi hizo waone umuhimu wa hifadhi hizo moja kwa moja na hivyo kutoa ushirikiano kwenye uhifadhi.

Katika hatua nyingine, Waziri Kigwangalla amemsimamisha kazi Meneja wa Pori la Akiba Uwanda, katika wailaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Mark Chuwa kwa tuhuma za kushindwa kuondoa mifugo zaidi ya 12,000 iliyopo ndani ya hifadhi hiyo.

Kabla ya uamuzi huo, akisoma taarifa ya mkoa kwa Waziri huyo, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Dk. Khalfan Haule alisema uvamizi katika pori hilo umekuwa wa kiasi kikubwa  ambapo wafugaji huingia na makundi makubwa ya mifugo na kugeuza eneo hilo sehemu ya malisho.Alisema licha ya na kufanyika kwa opresheni za mara kwa mara za kuondoa mifugo hiyo, baada ya muda mfupi wafugaji hao hurejea na makundi makubwa ya mifugo kwa ajili ya malisho.

Hata hivyo Dk. Kigwangalla alishangazwa na uongozi wa mkoa na wilaya kwa kushindwa kuchukua hatua za kuondoa mifugo hiyo hifadhini wakati sheria za uhifadhi haziruhusu mifugo hifadhini.



 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa mkoa wa Rukwa wakikagua eneo shamba la miti kwenye Msitu wa Mbizi wilayani Sumbawanga jana. Aliiagiza TFS kuchangia milioni 20 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Mponda.
 Waziri wa Maliasili na Ualii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia eneo linalojengwa zahanati ya kijiji cha Mponda ambayo ameahidi wizara yake kuchangia ujenzi wake wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi wilayani Sumbawanga jana. Ambapo aliiagiza TFS kuchangia milioni 20 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Mponda. Wapili kulia kwake ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk. Khalfan Haule. 
 Waziri wa Maliasili na Ualii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwapungia mkono wananchi wa kijiji cha Mponda katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi wilayani humo jana. Aliiagiza TFS kuchangia milioni 20 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Mponda. Kulia kwake ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk. Khalfan Haule.
 Waziri wa Maliasili na Ualii, Dk. Hamisi Kigwangalla akicheza ngoma na wananchi wa kijiji cha Mponda katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi wilayani humo jana. Aliiagiza TFS kuchangia milioni 20 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Mponda. Kulia kwake ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk. Khalfan Haule.
 Waziri wa Maliasili na Ualii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mponda katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi wilayani humo jana ambapo aliiagiza TFS kuchangia milioni 20 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Mponda. Kulia kwake ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk. Khalfan Haule.
 Waziri wa Maliasili na Ualii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya wanafunzi katika kijiji cha Mponda Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi wilayani humo jana. Aliiagiza TFS kuchangia milioni 20 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Mponda. Kulia kwake ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk. Khalfan Haule.
Waziri wa Maliasili na Ualii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata ufafanuzi kuhusu upandaji wa miti kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Zawadi Mbwambo wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi katika msitu wa Mbizi wilayani Sumbawanga jana. Aliiagiza TFS kuchangia milioni 20 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Mponda.


Watumishi Muhimbili Wapigwa msasa Kuhusu Maadili, Rushwa

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeendesha mafunzo ya siku mbili ambayo yamelenga kuwakumbusha watumishi wa hospitali hiyo kuzingatia sheria ya kupambana na rushwa mahali pa kazi sambamba na maadili katika utumishi wa umma.

Watumishi walikumbushwa kutojihusisha na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa pamoja na madhara yanayotokana na vitendo hivyo.

Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Bw. Steven Agwanda aliwataka watumishi wa hospitali hiyo kuzingatia maadili kwa sababu makosa mengi ya rushwa yanasababishwa na ukiukwaji wa maadili.

“Kuna uhusiano mkubwa kati ya rushwa na maadili, mtumishi au viongozi hawachukui rushwa kwa sababu hawana hela, hapa tatizo ni ukosefu wa maadili, zikiwamo tamaa ambazo zinasababishwa na watumishi au viongozi,” alisema Agwanda.

Mafunzo hayo ya siku mbili yalifunguliwa na Mkuu wa Idara ya Ajira na Mafunzo, Bw. Abdallah Kiwanga na yaliwalenga wakuu wa vitengo na wasimamizi wa wodi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).


Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Bw. Steven Agwanda akitoa mada katika semina ya siku mbili kuhusu rushwa mahali pa kazi kwa watumishi wa umma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Sehemu ya watumishi wa umma wa Muhimbili wakimsikiliza mtoa mada kwenye semina hiyo.
Sehemu ya watumishi wa umma wa Muhimbili wakimsikiliza mtoa mada kwenye semina hiyo.

RC TEMEKE AWAMWAGIA SIFA WOISO ORIGINAL PRODUCTS KWA KUNYAKUA TUZO YA BIDHAA ZA NGUO NA NGOZI

$
0
0

Na Leandra Gabriel , Globu ya Jamii.

MKUU wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amewataka wananchi hasa watokao katika Manispaa ya  Temeke kujitokeza kwa wingi kushuhudia maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba ili kujipatia elimu ya ujasiriamali.

Lyaniva ametembelea mabanda mbalimbali katika maonesho hayo na kujionea kazi za wazalendo wakiwa na bidhaa tofauti zilizotengenezwa hapa nchini wakitilia mkazo kauli ya Rais wa John Pombe Magufuli ya uchumi wa viwanda.

Akizungumza na Globu ya Jamii akiwa ndani  ya banda la bidhaa za nguo na ngozi la Woiso Orginal Company Ltd Lyaniva ameeleza kuwa maonesho hayo yameboreshwa na washiriki wamekuwa wengi kutoka katika nchini mbalimbali duniani.

"Maonesho ya mwaka huu zaidi ya mataifa 50 kutoka nje ya nchi wameweza kushiriki na wameleta bidhaa bidhaa nzuri zikiwa zenye ubora wa hali ya juu,"amesema Lyaniva.

Lyaniva amewapongeza wazalishaji wa bidhaa za nguo na ngozi kutoka kampuni ya Woiso Original Products kwa kuzalisha bidhaa nzuri na zenye ubora wa hali ya juu na kwa bei nzuri ambayo unanunua kitu na utadumu nacho kwa mda mrefu na amewataka wananchi kujitokeza sasa kuona na kujifunza namna bidhaa za kitanzania hasa za ngozi zilivyoshika hatamu kwa ubora wa hali ya juu.

Aidha amewashukuru watanzania walioelewa na kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika masuala ya kiuchumi na wamekuja vizuri sana na kuboresha maonesho hayo ambayo kwa namna moja au nyingine yana tija kwa taifa letu.

Naye Meneja masoko wa Woiso Original Products Company Ltd bi. Teya Herman ameeleza kuwa wao kama kampuni wanajituma sana katika kuhakikisha wanatoa bidhaa bora za ngozi na nguo kama vile viatu, mikanda, pamoja na nguo na mapazia.

Kuhusu tuzo waliyokabidhiwa leo wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Kassim ya watayarishaji bora wa bidhaa za nguo na ngozi bi. Teya ameeleza kuwa ni mara yao ya 4 kushiriki maonesho hayo na ni mara ya 4 kushinda tuzo hiyo ambapo awali ilijikita katika bidhaa za ngozi na ila kwa sasa imejumuisha bidhaa za ngozi na nguo.

Akielezea changamoto wanazokutana nazo hasa kwenye upatikanaji wa ngozi bi. Taya amesema kuwa upatikanaji wa bidhaa hiyo hauko vizuri  kutokana na uwepo wa alama zilizowekwa na wafugaji na zile zinazotokana na kuchinjwa hali inayopelekea ugumu wakati wa kuandaa bidhaa hizo.

Na ameungana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke akiwaomba watanzania kuunga mkono juhudi za serikali katika kuelekea uchumi wa viwanda kwa kupenda vya nyumbani.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akimuelezea mwananchi aliyefika kwenye banda la Woiso Original Products Company Ltd wanaojihusisha na uuzaji wa bidhaa za nguo na ngozi wakiwa washindi kwenye kipengele hicho kwa mara ya nne mfululizo katika maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba 
Meneja Masoko wa Kampuni ya Woiso Original Products Ltd Teya Herman akieleza jambo kwa mkuu wa  Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva katika maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akieleza jambo kwa Meneja Masoko wa kampuni ya Woiso Original Products Ltd Teya Herman  alipotembelea banda hilo na kujionea bidhaa zinazotengenezwa na watanzania zikiwa zenye ubora katika maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba
Meneja Masoko wa kampuni ya Woiso Original Products Ltd Teya Herman akizungunza na Globu ya Jamii akielezea tuzo ya ushindi waliyoipata katika kipengele cha Bidhaa za nguo na ngozi kutoka Tanzania ikiwa ni mara ya nne mfululizo wakishinda katika maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akizungumza na Globu ya Jamii akiwa ndani ya banda la washindi wa bidhaa za nguo na ngozi akielezea umuhimu wa watanzania kupenda vitu vya nyumbani ikiwemo kuwaunga mkono Wazalishaji wa ndani wa Viwanda vidogo na vikubwa.

Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)

NIC KIDEDEA SABASABA, YANYAKUA TUZO MBILI KWA MPIGO

$
0
0


Big Boss: Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga akiwa amebeba vikombe vya mshindi wa kwanza katika sekta ya bima (kushoto), na cha ushindi wa pili (kulia) katika washindi wa jumla miongoni mwa washiriki wa maonyesho hayo ya 42 ya sasasaba yanayoendelea katika viwanja vya mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga kikombe cha mshindi wa kwanza katika sekta ya bima , NIC pia imekuwa mshindi wa pili katika washindi wa jumla miongoni mwa washiriki wa maonyesho hayo ya 42 ya sasasaba yanayoendelea katika viwanja vya mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam
Vigogo NIC:Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Bima za Mali,Ajali na Shehena Romanus Hokororo,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NIC Thomas Msongole,Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Sam Kamanga na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko Elisante Maleko
Picha ya pamoja, wafanyakazi wa NIC waliosimama mbele na viongozi wao mstari wa nyuma

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje atembelea maonesho ya 42 ya biashara ya kimataifa (sabasaba)

$
0
0
Mhe. Dkt. Susan Kolimba Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga pamoja na watumishi wa Wizara. 

Dkt. Kolimba alifurahishwa na ushiriki wa Wizara kwenye maonyesho ya sabasaba, ambapo aliwasisitiza watumishi wa Wizara kuendelea kutumia fursa hiyo kutoa elimu kwa umma kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara. 
Mhe.Dkt. Kolimba akipata maelezo kutoka kwa Bi. Mindi Kasiga 
Mhe. Dkt. Susan Kolimba akizungumza na watumishi alipotembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba 
Mkurugenzi wa Masomo wa Chuo cha Diplomasia Prof. Watengere Kitojo akizungumza na watumishi alipotembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye maonesho ya sabasaba . 
Wanafunzi kutoka Chuo cha Diplomasia wakipata maelezo kutoka kwa watumishi wa Wizara walipotembelea bandala kwenye maonesho ya saba.Wanafunzi hao walipata fursa ya kuelezwa kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kikanda na kimataifa sambamba na fursa na faida zinazopatikana. 
Bw. Teodos Komba Afisa Mawasilino, akielezea jambo kwa wananchi waliojitokeza kwenye banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Bw. Hassan Mnondwa akielezea jambo kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara. 
Mhe.Dkt. Susan Kolimba akiwa katika Picha ya pamoja na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipotembelea banda la Wizara

Watafiti wa afya waombwa kubaini sababu ya wanaume kukwepa kupima VVU

$
0
0

Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile ametoa wito kwa watafiti wa afya nchini kufanya utafiti ili kubaini sababu na suluhisho kuhusiana na uwepo wa idadi ndogo ya wanaume wanaojitokeza kupima virusi vya Ukimwi (HIV) hapa nchini.

Dk Ndugulile alitoa wito huo jijini Dar es Salaam jana wakati akifunga Mkutano wa sita wa kisayansi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS).

Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2016/2017 ulioangalia maambukizi mapya na kiwango cha kufubaza VVU, wanawake wanaongoza katika maambukizi mapya lakini ni wepesi kupima na kutumia dawa kikamilifu ikilinganishwa na wanaume.

“Lengo hasa tunahitaji kuona idadi kubwa ya wanaume ikijitokeza kupima VVU ili tuweze kupunguza kasi ya maambukizi mapya ifikapo 2030. Ili tuweze kufanikisha hili ni lazima tuwe na majibu ya kitafiti yatakayotupa muongozo kuhusu sababu za wanaume kukwepa kupima VVU na nini hasa kifanyike kuondoa changamoto hizo,’’ alisema.

Alisema kwasasa serikali ipo kwenye mchakato wa kuandaa sera ya afya hivyo tafiti mbalimbali kuhusu masuala ya afya ni muhimu ili kuiwezesha sera hiyo kuhakisi ualisia wa masuala muhimu katika sekta hiyo.

Aliongeza kuwa kwasasa taifa linakabiliwa zaidi na magonjwa yasiyoyakuambukiza ikiwemo kisukari, shinikizo la damu, kiarusi pamoja na ugonjwa wa figo huku akitaja sababu kuwa ni pamoja na mfumo wa maisha usiozingatia miongozo ya lishe, matumizi ya pombe kupitiliza na uhaba wa mazoezi miongoni mwa wana jamiii.

“Upande wetu serikali tunaendelea kuboresha huduma za kibingwa kuhakikisha magonjwa kama figo na mengine ambayo tulikuwa tunatumia fedha nyingi kusafirisha wagonjwa nje ya nchi sasa yanatibiwa hapa nchini.,’’ alisema huku akitolea mfano matibabu ya figo ambayo kwasasa yanafanyika ndani ya nchi kwa sh mil 21 badala ya mil 100 zilizokuwa zikitumika nje ya nchi kwa kila mgonjwa.

Kuhusu suala la upatikanaji wa dawa hapa nchini, Dk Ndugulile alisema; “ Kwasasa serikali imetoa muongozo wa utoaji wa dawa ambapo badala ya kuruhusu soko liamue dawa gani zitumike kwasasa serikali ndio inaamua dawa ipi itumike kutibu ugonjwa upi, sehemu gani na kwa utaalamu gani,’’ alisisitiza.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa MUHAS, Prof. Prof Andrew Pembe alisema nyingi kati ya tafiti zilizowasilishwa kwenye mkutano huo wa siku mbili zilijikita katika vipaumbele vya taifa yakiwemo masuala ya HIV/AIDS, kifua kikuu, afya ya uzazi na mtoto, magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ajali pamoja na magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika.

“Mkutano huu umewakutanisha wataalamu wa afya katika ngazi tofauti wakiwemo wale waliobobea pamoja na wanafunzi ili kuruhusumbadilishano wa mawazo na ujuzi. Zaidi ya tafiti tofauti 200 zimewasilishwa kupitia mkutano huu’’ alisema. Aliishukuru serikali ya Sweden kupitia Shirika la Sida ambao kwa kushirikiana na wadau wengine wamewezesha mkutano huo.
Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile (kulia) akizungumza wakati akifunga Mkutano wa sita wa kisayansi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS)jijini Dar es Salaam jana.
Makamu Mkuu wa MUHAS, Prof. Prof Andrew Pembe (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile (katikati) kuhusu dawa zinazaondaliwa na wataalamu wa Kitengo cha Dawa asili kutoka Chuo cha MUHAS muda mfupi kabla hajafunga Mkutano wa sita wa kisayansi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS)jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni pamoja na Naibu Makamu Mkuu wa MUHAS, Prof. Appolinary Kamuhabwa (wa tatu kulia)
Makamu Mkuu wa MUHAS, Prof. Prof Andrew Pembe akizungumza wakati wa kuhitimisha Mkutano huo
Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile (kushoto) akibadilishana mawazo na Naibu Makamu Mkuu wa MUHAS, Prof. Appolinary Kamuhabwa kabla hajafunga Mkutano wa sita wa kisayansi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS)jijini Dar es Salaam jana.
Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa huo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) mara tu baada ya kufunga Mkutano wa sita wa kisayansi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS)jijini Dar es Salaam jana.
Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa huo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) pamoja na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa sita wa kisayansi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS)jijini Dar es Salaam jana.

MKUU WA MAJESHI YA ULINZI JENERALI VENANCE MABEYO ATEMBELEA BANDA LA NSSF KATIKA MAONESHO YA SABNASABA

$
0
0
 Mkuu wa Majeshi  ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akizungumza  alipotembelea banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF  na kuwapongeza NSSF kwa ushindi wa Jumla alipotembelea Banda la NSSF katika maonyesho ya Sabasaba , pembeni ni baadhi ya wafanyakazi wa NSSF. Picha na Mwandishi wetu. Picha na Mwandishi wetu
 Mkuu wa Majeshi  ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akipata maelezo mbalimbali kuhusu huduma za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kutoka kwa Kaimu meneja wa Uhusiano na Masoko Ndugu Salim Khalfan alipotembelea Banda la NSSF katika maonyesho ya Sabasaba
 Afisa Uhusiano wa NSSF Bi. Angella Msangi akimkabidhi zawadi za vitabu na vipeperushi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo alipotembelea banda  la NSSF katika maonyesho yanayoendelea ya sabasaba. Picha na Mwandishi wetu
Mkuu wa Majeshi  ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akifurahia jambo na Kaimu Meneja uhusiano na Masoko wa NSSF Ndugu Salim Khalfan alipotembelea banda  la NSSF katika maonyesho yanayoendelea ya sabasaba. Picha na Mwandishi wetu. Picha na Mwandishi wetu

SPIKA NDUGAI AONGOZA WAHESHIMIWA WABUNGE KATIKA MAZISHI YA ALIYEKUWA MBUNGE WA KOROGWE VIJIJINI MHE. STEPHEN NGONYANI

$
0
0
 Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza wakati wa wa mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini Marehemu Stephen Hillary Ngonyani yaliyofanyika leo nyumbani kwake Korogwe Jijini Tanga. kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama na Kushoto ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakari Zuberi
 Mawaziri, Manaibu Waziri, Waheshimiwa Wabunge na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa wakiwa katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini Marehemu Stephen Hillary Ngonyani yaliyofanyika leo kijijini kwake Kwamndolwa Wilayani Korogwe Jijini Tanga.
 Wapambe wa Bunge wakibeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini Marehemu Stephen Hillary Ngonyani tayari kwa mazishi yaliyofanyika leo Kijijini kwake Kwamndolwa Wilayani Korogwe Jijini Tanga. 

 Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini Marehemu Stephen Hillary Ngonyani katika mazishi yaliyofanyika leo kijijini kwake Kwamndolwa Wilayani Korogwe Jijini Tanga.PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE

TFDA ATOA NENO KWA WAJASIRIAMALI NCHINI, YAWAKUMBUSHA KUJISAJILI

$
0
0



Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Agnes Kijo akizungumza na wajasiriamali wa bidha za Chakula katika Banda la Mfuko wa Fursa kwa Wote katika Maonesho ya 42 ya Biashara Kimataifa katika Viwanja vya Mwalim Julius Nyerere kijiji Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Agnes Kijo akingalia moja ya bidhaa katika banda la Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote wakati alipotembelea maonesho ya Sabasaba.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Agnes Kijo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Mamlaka hiyo .



Said Mwishehe,Globu ya jamii

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) imewahimiza wajasiriamali kuhakikisha katika mamlaka hiyo kwa lengo la kutambulika na hatimaye kuwa na uhakika wa kuuz bidhaa zao mahali popote.

Pia imewashauri wajasiriamali nchini kutafuta maalumu ambalo litatumika kwa ajili ya kuuza bidhaa zao na hiyo itawafanya wanaohitaji kununua bidhaa kutambua mahali walipo na kufika kwa urahisi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Agnes Kijo baada ya kutembelea mabanda mbalimbali yaliyopo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Amesema ujumbe wake mkubwa kwa wajasiriamali wa ndani ambao amewatembelea kwenye mabanda yao ni kuwataka kujisajili TFDA na kufafanunua gharama ya kujisajili ni Sh.50,000.

Pia amesema amewahimiza wajasiriamali hao kuangalia namna ya kuwa na eneo moja ambalo watapanga bidhaa zao mbalimbali kwani kufanya hivyo kutasaidia kutambulika waliko na hatimaye kufanyabiashara.“Tunahimiza wajasiriamali kujisali maana bidhaa inapokuwa inatambulika na TFDA na TBS inasaidia kumfanya anayehitaji kuinunua kuwa na uhakika na ubora na usalama wa bidhaa,”amesema.

Ameongeza kikubwa ambacho kimemfurahia ni namna ambavyo wajasiriamali wamekuwa na muamko mkubwa kuhusu TFDA na majukumu yake na wengi zaidi wamejisajiri tayari.ia amewashauri Watanzania kupenda na kuthamini bidhaa za ndani kwani hiyo itawasaidia kuwainua kiuchumi wa wajasiriamali nchini.

Amefafanua kuwa kwa sasa wananchi walio wengi wameanza kuthamini vya ndani na kutoa mifano mbalimbali lakini akashauri kuthamini huko sasa kuende na kwenye bidhaa.Pia amewahimiza wajasiriamali nchini ambao wanataka kusajili bidhaa zao kufika kwenye ofisi za TFDA ambazo zipo katika kanda saba na kwamba wakifika katika ofisi hizo watahudumiwa vizuri kwani jukumu lao ni kuwahumia Watanzania.

CHUO CHA KODI CHAFUNGUA MILANGO KWA WANAOTAKA KUJIUNGA KWA MWAKA WA MASOMO WA 2018/2019

$
0
0

Bi Oliver Njunwa MKuu wa Kitengo cha Mawasiliano Chuo cha Kodi akizungumza na mwandishi wa habari Said Mwishehe katika banda la TRA kwenye maonesho ya biashara ya Sabasaba katika viwanja vya TANTRADE barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo. Rachel Mkundai Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA akimkabidhi zawadi mmoja wa wananchi aliyejiunga na mitandao ya kijamii ya TRA ili kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na mamlaka hiyo.

...........................................................................

Na Said Mwishehe Blogu ya Jamii

CHUO cha Kodi (ITA) kimesema kwa sasa kimeanza kupokea maombi ya wanaotaka kujiunga na chuo hicho kwa mwaka wa masomo wa 2018/2019 na kwamba wamekuwa wakielezea program ambazo wanazitoa.

Pia kimesema wanafunzi wote wenye sifa watume maombi kwa kozi ambazo wanahitaji kusoma na kwamba wanaosoa chuoni hapo na kumaliza wanaweza kufanya kazi mahali popote kwa kuajiriwa au kujiajiri.

Akizungumza na Michuzi Blog leo katika Banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ambako ndani yake kuna banda la Chuo cha Kodi Mkuu wa Mawasiliano wa chuo hicho Oliver Njunwa amesema wanaombaji watumie maombi kwa njia ya mtandao kupitia www.ita.ac.tz au http://212.71.252.209/ita-oas/.

Ametaja kozi ambazo zinatolewa na chuo hicho ni Astashahada ya Forodha na Usimamizi wa kodi na Stashahada ya Forodha na Usimamizi wa Kodi.Pia Shahada ya Forodha na Usimamizi wa kodi, Stashahada ya Uzamili wa Usimamizi wa kodi, Cheti Afrika Mashariki cha Uwakala wa Forodha pamoja na Shahada ya Uzamili ya Sheria ya kodi na usimamizi.

Alipoulizwa ni kitu gani hasa ambacho wanakifanya katika maonesho hayo, amejibu kuwa wanatumia maonesho hayo kwa ajili ya kuzungumza na watanzania kuhusu uwepo wa chuo hicho na faida zake na kubwa ni kuwahamasisha kujiunga na chuo hicho.“Chuo cha Kodi ni chuo pekee kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini katika utoaji wa mafunzo ya forodha na kodi.

“Chuo chetu kinatoa mafunzo kwa wadau mbalimbali na hiyo imetufanya tupokee wanafunzi kutoka nchi nyingi za Afrika,”amesema Njunwa.
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images