Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1610 | 1611 | (Page 1612) | 1613 | 1614 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Bi. Rose Joseph Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA akifafanua jambo wakati alipkuwa akihijiwa na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya biashara ya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam yanayoandaliwa na Mamlaka ya Mendeleo ya Biashara TANTRADE.
  Baadhi ya wananchi mbalimbali wakipata maelezo kwa mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika Maonesho ya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo.
  Muonekano wa Banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA katika maonesho ya Sabasaba.


  MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)imewataka wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao hawana vitambulisho vya Taifa kufika kwenye banda lao lililopo Maonesho ya biashara ya kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam ili wapate vitambulisho.

  Akizungumza leo kwenye maonesho hayo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Rose Joseph amesema pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu NIDA na majukumu yake pia wameamua kutumia maonesho hayo kutoa vitambulisho kwa wananchi wa mkoa huo.

  Amesema kuwa hivyo kwa anayehitaji kitambulisho cha Taifa atatakiwa kuwa na viambatanisho muhimu vikiwemo cheti cha kuzaliwa, cheti cha taaluma, leseni au kadi ya bima ya afya.Amesema kwa watakaofika wakiwa na vielelezo vyao itakuwa rahisi kujaziwa fomu na kisha kupata kitambulisho cha taifa ambacho kina umuhimu mkubwa na ni vema kila mwananchi mwenye sifa akikapata.

  “Tumeamua kutumia maonesho ya biashara ya kimataifa ya 42 kuhakikisha wananchi wa Dar es salaam ambao hawakuwa na vitambulisho vya taifa basi wanavipata.“Kwa hapa kwenye maonesho tutatoa vitambulisho kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam tu na wale wananchi wa mikoa mingine wao watapata kupitia ofisi zetu zilizoko mikoani,”amesema.

  Amefafanua changamoto kubwa iliyopo katika kuandikisha vitambulisho vya taifa ni baadhi ya watu kutokuwa na viambatanishi muhimu ,hivyo wanashauri ni vema kila anayekwenda kuchukua kitambulisho akawa na vilelezo vyote muhimu.Wakati huo amesema NIDA kwa kutambua uwepo wa makundi yenye mahitaji maalumu nchini , ipo katika mchakato wa kutoa vitambulisho kwa kundi la watu wenye ulemavu wa kusikia.

  Amefafanua baada ya hapo watakwenda kwenye makundi mengine na lengo ni kuhakikisha nao wanakuwa na vitambulisho vya taifa.

  “Ni jukumu letu kuhakikisha vitambulisho vya taifa kila mtanzania mwenye sifa anakuwa nacho, hivyo tumeamua kuanzisha mpango maalum ambao huu utajikita kusajili makundi maalumu na tutaanza na kundi la watu wenye ulemevu wa kusikia.Tutakuwa na wakalimani ili kuhakikisha tunafanikisha mpango huo na tunatarajia kupata ushirikiano kutoka kwa viongozi wao,”amesema.

  0 0

  Habari njema kwa Watanzania wapenda maendeleo kwa fursa kubwa huko ughaibuni katika tamasha kubwa la kimataifa linaloitwa Afrobeats Summer Festival litakalofanyika Tubingen nchini Ujerumani.

  Mratibu wa tamasha hilo nchini, Shamsa Danga, amesema, hii ni kwa wale wote wenye nia ya dhati ya kukutana na wadau na wawekezaji wa Ujerumani kwa lengo la kupanua wigo wa kibiashara kimataifa katika nyanja zote ikiwemo sanaa ya muziki, uchongaji, uchoraji na ngoma za asili.

  Tamasha hilo litakalochukua siku nne kufanyika kuanzia Agosti 9-12 mwaka huu, litahusisha mambo mbalimbali yanayotoa fursa kwa fani zote zitakazopata wahusika. Ndio maana msisitizo mkubwa umewekwa kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki.Aidha, tamasha hilo linawakaribisha watu binafsi, taasisi, makampuni, wajasiriamali, wakulima, wafanyabiashara na wadau wa kada mbalimbali.

  Kwa watakaokuwa tayari na kutaka maelezo zaidi wapige simu namba +255713 457743 (Shamsa Danga) au +491715176779 au watembelee: www.gabs-germany.com

  0 0

  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo alipotangaza kuwa kwa mwaka wa tatu mfululizo, Tigo ndio mdhamini mkuu wa mawasiliano katika Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam ya Biashara (DITF) ambayo yanaandaliwa na Mamlaka ya Ukuzaji wa Biashara Tanzania (Tantrade). Kushoto ni Meneja wa Ukuzaji wa Biashara wa Tantrade, Stephen Koberou 
   

   Tigo yatoa ofa murwa kwaa simu janja za kisasa zenye vifurushi vya intaneti katika maonesho hayo

  Dar es Salaam, Tanzania– Juni 29, 2018: Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo ndio mdhamini mkuu wa mawasiliano katika Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam ya Biashara (DITF) ambayo yanaandaliwa na Mamlaka ya Ukuzaji wa Biashara Tanzania (Tantrade). Kauli mbiu ya maonesho hayo almaarufu Sabasaba yanayofanyika kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2018 ni ‘Ukuzaji wa Biashara kwa Maendeleo ya Viwanda’.

  Akitambulisha udhamini huo jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa hii ni mara ya tatu mfululizo kwa Tigo kudhamini maonesho hayo. Ushirikiano huu ni sehemu mojawapo ya azma ya Tigo kuchangia juhudi za serikali kukuza biashara kama njia mojawapo ya kukuza uchumi wa viwanda nchini.
   
  ‘Tigo inatambua kuwa Tanzania ni mojawapo ya nchi za Afrika ambapo uchumi wake unakua kwa kasi ya juu na kuwa bado kuna fursa nyingi zinazopatikana nchini. Kila mwaka kwa kipindi cha miaka 42 sasa, Maonesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam ya Biashara (DITF) yamekuwa chachu kubwa ya kukuza uchumi wa viwanda kwani yanatoa fursa kubwa kwa wafanyabiashara wakubwa, wadogo na wa kati kuonesha ubunifu katika bidhaa na huduma, pamoja na teknologia mpya kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. Vilevile, Sabasaba ni chachu ya maendeleo ya kiuchumi kwani inatoa fursa za ajira na mapato kwa sekta tofauti,’ Woinde alisema.

  Aliwahamasisha Watanzania kujiandaa kupokea ofa kabambe za simu janja za kisasa zenye ofa murua za vifurushi vya intaneti kwa kipindi cha hadi miezi sita kutoka Tigo. ‘Tumeingia ubia na watengenezaji wakubwa wa simu duniani kama vile Tecno, Samsung, Nokia na Freetel kuhakikisha kuwa wateja na wananchi watakaofika katika viwanja vya Sabasaba, Dar es salaam au katika maduka yote ya Tigo nchi nzima wanafaidika na simu janja kwa bei nafuu kuanzia TSH 69,000 pekee katika msimu huu wa Sabasaba.’

  Kwa upande wake, Meneja wa Ukuzaji wa Biashara wa Tantrade, Stephen Koberou aliwashukuru Tigo kwa kuchukua jukumu la kuthamini maonesho ya mwaka huu ya Sabasaba ili kukuza biashara. Pia aliwahamasisha wananchi wote kujitokeza kwa wingi ili waweze kujionea ubunifu na teknologia mpya, kujifunza, kujenga mahusiano mapya ya kibiashara pamoja na kuwa sehemu ya fursa kubwa zaidi ya kufanya manunuzi na kupata huduma muhimu kwa bei nafuu.

  ‘Maandalizi yako tayari na nawakaribisha wafanyabiashara wote kujitokeza kwa wingi kuunga mkono wafanyabiashara wenzao wa ndani na nje ya nchi ambao wameleta bidhaa na huduma zao katika  maonesho ya mwaka huu, huku wakipata fursa ya kujionea hatua kubwa tulizopiga katika kukuza uchumi wa viwanda nchini,’ alisema. 

  Sabasaba imejizolea umaarufu kama maonesho yanayoongoza nchini kwa kuvutia mamia ya wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi pamoja na maelfu ya wageni wanaovutiwa na bidhaa bora na bei nafuu zinazopatikana katika maeonesho hayo.

  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,  akipongezana na kumshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Bank, Joseph Iha, baada ya kukabidhiwa na kuzindua Kituo cha Polisi kinachohamishika kilichojengwa eneo la Kisasa jijini Dodoma jana wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi moja kati ya vituo vitano vilivyofadhiliwa na benki hiyo vyenye thamani ya Sh. milioni 250. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamadi Masauni (kulia) ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu na Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde.Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Giles Mroto, alipokuwa akifafanua kuhusu mali na Pikipiki za wizi zilizokamatwa na Jeshi hilo kwa nyakati tofauti wakati wa hafla ya kukabidhiwa na kuzindua Kituo cha Polisi kinachohamishika kilichojengwa eneo la Kisasa jijini Dodoma wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi moja kati ya vituo vitano vilivyofadhiliwa na benki hiyo vyenye thamani ya Sh. milioni 250. 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Giles Mroto, alipokuwa akifafanua kuhusu Televisheni za wizi zilizokamatwa na Jeshi hilo kwa nyakati tofauti wakati wa hafla ya kukabidhiwa na kuzindua Kituo cha Polisi kinachohamishika kilichojengwa eneo la Kisasa jijini Dodoma wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi moja kati ya vituo vitano vilivyofadhiliwa na benki hiyo vyenye thamani ya Sh. milioni 250. 

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akihutubia wananchi na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Kisasa jijini Dodoma jana. 
  Sehemu ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo wakimsikiliza Waziri Mkuu wakati akihutubia
   Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Bank, Joseph Iha, akizungumza wakati wa hafla hiyo
   Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma,  Giles Mroto, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
   Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamadi Masauni, akizungumza wakati wa hafla hiyo
   Sehemu ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo......
    Baadhi ya wakiondoka mbele ya jukwaa kuu baada ya kuimba wimbo wa maadili wa jeshi hiyo kwa Waziri Mkuu jana,
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi baada ya kuzindua kituo hicho.
   Picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Equity Bank baada ya uzinduzi huo
   Picha ya pamoja na jeshi la Polisi
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage, Teddy Mapunda, baada ya hafla ya uzinduzi huo
   Askari Polisi wakiwa ndani ya Kaunta ya Kituo hicho baada ya uzinduzi
   Mazungumzo ya hapa na pale yakiendelea baada ya uzinduzi huo
   Mkurugenzi wa Equity Bank, Joseph Iha, akipongezana na baadhi ya askari
   Picha ya pamoja baadhi ya wafanyakazi wa Equity Bank na Viongozi wa Polisi mkoa wa Dodoma.
   Ubize wa mawasiliano.........
   Picha ya pamoja na ''Watapata Taabu sanaaana'' kila mmoja aliyekuwapo eneo hili alitamani kujiselfie na mtu huyo muhimu katika kipindi hiki anayeendelea kukiki na slogan yake ya ''WATAPATA TAABU SANA, WATAPA KIPIGO CHA MBWA KOKO''
   Muonekano wa jengo hilo
   Wasanii wa kikundi cha Sanaa cha Mzee Choya chenye maskani yake jijini Dodoma, wakitoa burudani wakati wa hafla ya uzinduzi wa kimoja kati ya vituo vitano vya Polisi vinavyohamishika kilichowekwa eneo la Kisasa chini ya ufadhili wa Equity Bank. Vituo hivyo vina thamani ya sh. milioni 250. Hafla hiyo ilifanyika juzi jijini humo. 
   Muonekano wa kituo hicho kwa nje
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua gwaride baada ya kuwasili eneo hilo kuzindua kituo hicho.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Bank, Joseph Iha, baada ya kuwasili eneo hilo kuzindua kituo hicho.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Meneja wa Equity Bank, mkoa wa Dodoma, baada ya kuwasili eneo hilo kuzindua kituo hicho.
   Mbwa wa Polisi akionyesha jinsi anavyoweza kumdhibiti mhalifu.

  0 0

  Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

  MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya JKT na Mgambo na hawana kazi wafike katika ofisi ili kushirikiana katika kuweka jiji katika hali ya usafi.

  Makonda ameeleza hayo jana alipokuwa akifanya mazungumzo na viongozi wa Jeshi la kujenga taifa watokao katika Wilaya 5 za jiji, Makonda ameeleza kuwa licha ya kuweka  kila mkakati ikiwemo kutoa wito na rai kuhusu suala la usafi lakini bado jiji limekuwa chafu.

  Ameeleza kuwa vijana hao watokao katika jiji la Dar es salaam wafike ofisini kwake Julai 6 ili kupata maelekezo kuhusiana na utaratibu mpya.

  Kuhusiana na kazi zitakazofanywa na vijana hao Makonda ameeleza, watakaa na watendaji na kujua makampuni yanayofanya usafi na kama yanatekeleza majukumu hayo, kujua mahali ambapo wananchi wanatupa taka na kama kampuni zinazokusanya taka zinatoa risiti na kukamata kila anayetupa na asilimia 50 ya faini itakuwa sehemu ya ujira kwa vijana hao na atakayekamatwa akiwa hana fedha atafanya usafi kwa juma zima.

  Aidha ameziagiza Manispaa zote ndani ya mwezi huu wa saba kila mfanyabiashara aliyepewa leseni awe na sehemu ya kutupa taka na vituo vya daladala viwe na sehemu maalumu ya kutupa ,Aidha amewataka makandarasi wote wa usafi katika ngazi zote kuwasilisha mikataba yao katika ofisi yake kuanzia Julai 4 hadi 6 ili iweze kupitiwa na tume iliyoundwa.

  Pia amewashukuru wananchi na vyama mbalimbali ambavyo hujitolea kufanya usafi ili kuliweka jiji katika hali ya usafi.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na vyombo vya habari juu ya mkakati wa kusimamia usafi katika jiji la Dar es salaam.

  0 0

  Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii 

  MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametangaza vita na watu wenye tabia za kuwachukuwa watoto yatima,walemavu na waishio katika Maisha magumu kama mitaji ya kujinufaisha watakamatwa na kuchukuliwa hatua Kali za kisheria.

  Makonda ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya matokeo ya utafiti wa idadi ya Watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani kinyume na Sheria hali inayosababisha kushindwa kutumia fursa ya elimu bure iliyotolewa na Rais John Magufuli jambo ambalo Makonda ameapa kulivalia njuga.

  Kwa mujibu wa utafiti huo umebaini Mkoa wa Dar es salaam pekee una jumla ya watoto 3,312 wanafanya kazi mitaani na kati ya hao watoto 2,984 walionekana wakifanya kazi nyakati za mchana na 328 wanafanya kazi nyakati za usiku.

  "Idadi hiyo ya watoto wanaoishi mitaani ni matokeo ya kukosekana kwa misingi bora ya familia na mmonyoko wa maadili ndio maana niliamua kuunda tume ya kupitia sheria ya mtoto na mikataba ya kimataifa ambayo itasaidia kuweka haki stahiki za watoto,"amefafanua. 

  Aidha amewaonya watu wenye tabia ya kuwapatia ombaomba fedha barabarani kuwa ndio wanaohalalisha uwepo wa watu hao ambapo amesema kama mtu anataka kweli kusaidia waishio maisha magumu wapeleke misaada kwenye vituo vilivyopo kwa mujibu wa sheria kwani vituo hivyo vinafuatilia mienendo ya watoto kitabia, elimu na matibabu.

  Ambapo ukimpa fedha mtoto barabarani unatengeneza mazingira ya kuwa na fedha ambayo hana uhalali nayo na anapokuwa mtu mzima anakuwa mkabaji,mporaji na kuchoma visu watu wasio na hatia.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la Babawatoto Center Bwana Mgunga Mwa Mnyenyelwa amempongeza Makonda kwa kutafuta haki ya mtoto alietelekezwa kwani kupitia mchakato huo limewezesha watoto wengi kuingia kwenye mfumo rasmi wa kupata fedha ya matunzo kila mwezi pamoja na bima ya matibabu Bure.

  Amesema utafiti huo umefanywa na shirika la Babawatoto Center for Children and Youth.kupitia mradi wa USAID Kizazi Kipya kwenye mikoa mitano ambapo wamebaini nusu ya watoto wa mitaani wanapatikana mkoa wa Dar es salaam
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wanaowatumia watoto yatima,walemavu waishio,mazingira magumu kama mitaji ya kujinufaisha,ameeleza kuwa watu hao wakibainika watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
  Mkurugenzi wa Shirika la Babawatoto Sente,Mgunga Mwa Mnyenyelwa akimkabidhi ripoti ya matokeo ya utafiti wa idadi ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani kinyume cha sheria,Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda.
  Picha ya pamoja

  0 0

  Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere ametoa wito kwa wananchi kujenga tabia ya kulipa kodi mbalimbali kwa wakati ikiwepo Kodi ya Majengo ili kuepuka usumbufu unajitokeza tarehe za mwisho za kulipa kodi hizo.

  Akizungumza leo na wananchi waliotembelea banda la TRA katika maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba, Kamishna Mkuu huyo amesema kuwa, wananchi wengi husubiri tarehe za mwisho ili kulipa kodi suala linalosababisha foleni na malalamiko kutoka kwa wananchi hao.

  “Tumetangaza kwa muda mrefu kuhusu kulipa Kodi hii ya Majengo lakini hamkutaka kulipa kwa wakati, matokeo yake foleni imekuwa kubwa na sasa mnaanza kulalamika kwamba mnachelewa kupata huduma. Jengeni tabia ya kulipa kodi kwa wakati ili muweze kuondokana na usumbufu huu usio wa lazima,” alisema Kichere.

  Kamishna Mkuu Kichere ameongeza kuwa, kodi ya majengo ya mwaka 2018/19 inaaza kulipwa tarehe 1 Julai 2018 na mwisho wa kulipa kodi hiyo ni tarehe 30 Juni, 2019. Hivyo, wananchi waanze kulipa mapema ili kuondoa usumbufu wa kukaa kwenye foleni.Naye mwananchi aliyetembelea banda la TRA kwa ajili ya kulipa Kodi ya Majengo Shabani Mkolimwa, amefurahishwa na huduma alizozipata katika banda hilo na kuiomba Mamlaka kusogeza huduma hizo karibu na maeneo wanayoishi.

  “Leo nimefurahi sana kwasababu nimepata huduma za TRA na huduma za benki ndani ya banda moja. Ninaiomba TRA ituletee huduma hizi kwenye Serikali zetu za Mitaa ili iwe rahisi kwetu kupata huduma hizi za TRA kwa haraka,” alisema Mkolimwa.Mamlaka ya Mapato Tanzania imeshiriki katika Maonyesho ya Sabasaba na banda lake lipo mkabala na banda la Azam ambapo pamoja na kupokea maoni kutoka kwa wananchi, huduma mbalimbali zinatolewa ikiwa ni pamoja na Kulipa Kodi ya Majengo, Usajili wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) na Elimu ya Mlipakodi
   Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (kulia) akizungumza na wananchi waliotembelea Banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba kwa ajili ya kulipa Kodi ya Majengo wakati Kamishna Mkuu huyo alipotembelea banda hilo kuona huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wananchi. 
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (katikati) akikagua bili ya Kodi ya Majengo aliyopewa mteja (kulia) wakati alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba kuona huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wananchi. Kushoto ni Meneja wa Huduma wa TRA Bi. Honester Ndunguru.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (katikati) akijibu hoja za mteja aliyempigia simu wakati alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba kuona huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wananchi. Kushoto ni Afisa Kodi Bi. Levina Shirima na kulia ni Meneja wa Huduma Bi. Honester Ndunguru.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere akimsikiliza Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Temboni iliyopo jijini Dar es Salaam Ally abdallah (kulia) wakati alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba kuona huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wananchi. Kushoto ni Mwanafunzi mwenzake Safinia Shani. 
  Baadhi ya wateja wakitoka katika Banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) lililopo mkabala na banda la Azam ndani viwanja vya Sabasaba. PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO

  0 0  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Waziri Mkuu wa Mauritania Mhe. Yahya Hademine mara baada ya kupokelewa kwenye uwanja wa ndege wa Nouakchott usiku huu tayari kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika .
  23
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mkuu wa Mauritania Mhe. Yahya Hademine mara baada ya kupokelewa kwenye uwanja wa ndege wa Nouakchott usiku huu tayari kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0


  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akikabidhi hati za uteuzi kwa baadhi ya Mahakimu Wafawidhi wa Mikoa wakati wa sherehe za kuwakabidhi hati Mahakimu hao 24 pamoja na kuwaapisha Naibu Wasajili 9. Sherehe hizo zimefanyika leo jijini Dodoma.
  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akisaini kiapo cha uadilifu cha mmoja wa Naibu Wasajili katika sherehe za kuwakabidhi hati Mahakimu 24 pamoja na kuwaapisha Naibu Wasajili 9. Sherehe hizo zimefanyika leo jijini Dodoma.
  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akishuhudia mmoja wa Naibu Wasajili akisaini kiapo cha maadili katika sherehe za kuwakabidhi hati Mahakimu 24 pamoja na kuwaapisha Naibu Wasajili 9. Sherehe hizo zimefanyika leo jijini Dodoma.


  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Majaji wakati wa sherehe za kuwakabidhi hati Mahakimu 24 pamoja na kuwaapisha Naibu Wasajili 9. Sherehe hizo zimefanyika leo jijini Dodoma.Kushoto kwake ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi 

  Baadhi ya Naibu Wasajili na Mahakimu Wafawidhi wa Mikoa wakiwa katika picha wakati wa sherehe za kuwakabidhi hati Mahakimu 24 pamoja na kuwaapisha Naibu Wasajili 9. Sherehe hizo zimefanyika leo jijini Dodoma.

  ………………

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.


  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewakumbusha viongozi wa Mahakama kusimamia kwa makini upangaji na utendaji wa madalali ili kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za wadaawa.

  Jaji Mkuu, Prof. Juma ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akikabidhi hati 24 za uteuzi kwa Mahakimu Wafawidhi wa Mikoa pamoja na kushuhudia uapisho wa Naibu Wasajili 9 uliofanywa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dkt. Eliezer Feleshi.

  Prof. Juma amesema kuwa mara nyingi shughuli za madalali hulalamikiwa, wananchi wanafahamu kuwa madalali ni sehemu ya Mahakama kwahiyo eneo hilo lazima liangaliwe kwa umakini hasa pale fedha za wadaawa zinapotumiwa vibaya na baadhi ya madalali.

  “Pamoja na Kanuni za sasa kuwataka madalali wapitie mafunzo lakini bado mna wajibu wa kusimamia majukumu yao, pia tunazifanyia mabadiliko kanuni za madalali ambapo watalazimika kuweka fedha zote kwenye akaunti ya Mahakama kabla ya kuweka katika akaunti zao ili tuweze kudhibiti matumizi mabaya ya fedha ambazo ni dhamana kwa wananchi,” alisema Prof. Juma.

  Prof. Juma ameongeza kuwa upangaji wa kesi ni eneo lingine linalotakiwa kusimamiwa kwa umakini kwani kesi zinatakiwa zipangwe kwa kuzingatia muda wa kusajiliwa au vipaumbele maalum kama maelekezo yanavyotolewa na viongozi wa Mahakama hali itakayosaidia kuepusha malalamiko kutoka kwa wananchi.

  Aidha, amewataka viongozi hao kuwa kichocheo cha maboresho ya Mahakama ya Tanzania pamoja na kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu mkubwa na bila upendeleo wowote huku wakizingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali iliyowekwa.

  Vile vile amewakumbusha kuwa uteuzi wao ni ishara tosha kwamba wameaminiwa kutekeleza majukumu yaliyoainishwa katika ngazi hizo za uteuzi na wameshakuwa walezi wa watumishi katika maeneo yao hivyo ni jukumu lao kuwatambua viongozi wa baadae ambao watachukua nafasi zao.

  Akiongelea kuhusu mfumo wa kisasa wa kielektroniki katika utoaji wa huduma, Prof. Juma amesema kuwa mfumo huo wa kufungua mashauri kwa njia ya kielektroniki utasimamiwa na Msajili Mkuu ambapo vitaanzishwa vibanda vya kuwasaidia wananchi kufungua mashauri kwa kielektroniki lengo likiwa ni kumaliza kabisa tatizo la upoteaji wa majalada.

  0 0


  Na Heri Shaaban

  MKUU wa Wilaya Ilala jijini Dar es Salaam Sophia Mjema afanya ziara kutembelea kambi ya warembo wa Miss ILALA na kutangaza zawadi za warembo.

  Mjema ametangaza zawadi za walimbwende hao alipokwenda kambini kwao na kuwapa faraja Miss Ilala .

  "Nawaomba Miss Ilala mjiamini kila mmoja mzuri na huu ni mwanzo wa mashindano ya Miss Ilala matarajio yetu wana Ilala mrembo wa Miss Tanzania atatokea Wilaya ya Ilala,"amesema Mjema .

  Mjema amesema warembo wa Wilaya Ilala wote ni wazuri na kila mmoja anamshinda mwezake,hivyo majaji siku hiyo watakuwa na kazi kubwa ya kumpata malikia wa wilaya ya Ilala atakayewakilisha Miss Tanzania.

  Alitaja zawadi za mshindi wa kwanza atajinyakulia kiwanja chenye hati, mshindi wa pili Sh. Milioni moja na duka la biashara, mshindi wa tatu draya za saloon ya kike, mshindi wa tatu atapelekwa katika chuo cha Urembo kilichopo wilayani Kinondoni kusomea Urembo, mshindi wa nne atapekwa katika hoteli kubwa five star, mshindi wa tano Daraya ya saloon ya kike.

  Amesema zawadi hiyo ni sehemu ya motisha lakini kila mrembo wa Ilala ambaye ameshiriki amewekewa mazingira bora ya kazi ndani ya Manispaa ya Ilala. Aidha amesema warembo wote wanatambulika mpaka sasa wamepanda daraja wasiwe na wasiwasi waendelee kujiamini waandaji wamewawekea mazingira mazuri. .

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miss Ilala Lucas Lutainurwa amesema jumla ya warembo 17 ambao wapo kambini Lamada wanajifua kwa mazoezi. Lucas amesema fainali ya mashindano hayo yanatarajia kufanyika Julai 6 mwaka huu na washindi watakao ingia tatu bora watashiriki ngazi ya TAIFA.

  Amesema warembo wake wote wazuri wamejiandaa vizuri fainali hiyo ambayo itafanyika Julai 6 .


  Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akiwa na warembo wa Miss ILALA Katika Hotel ya Lamada Dar es Salaam jana,fainali ya kumtafuta miss ILALA inatarajia kufanyika Julai 6 mwaka huu (PICHA NA HERI SHAABAN)
  Baadhi ya Washiriki wa shindano la Miss Ilala wakiwa Katika pozi hotel ya Lamada kwa ajili ya kujiandaa na kilele cha mashindano Julai 6 mwaka huu Picha na Heri Shaaban).
  Katibu Tawala wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (kushoto) akisalimiana na wasimamizi wa Miss Ilala Mbaraka Mwinyi MKUU na Said Side (katikati ),Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema (Picha na Heri Shaaban)

  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  KAMPUNI ya Cholemu Investment Limited ambayo inajihusisha na na uaazaji aridhi ikiwemo viwanja na mashamba imesema kwa kutambua kauli mbiu ya Tanzania ya Viwanda imesema ipo katika mchakato wa kuanza kuuza maeneo yaliyopimwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.

  Hayo yamesmwa leo kwenye Maonesho ya biashara ya kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam na Meneja Masoko wa Kampuni ya Cholemu Investment Limited Swaumu Mohamed.

  Asema kampuni yao kwa muda mrefu imejikita katika uuzaji wa viwanja kwa gharama nafuu mbayo kila mwenye kuhitaji kiwanja atamudu na kutokana na unafuu wao wa bei idadi kubwa ya wananchi wamenunua viwanja kutoka kwenye kampuni yao.mesema pamoja na kukijita katika uuzaji wa viwanja na mashamba wamejijenga sifa kwani kampuni yao uhakikisha aliyenunua kiwanja kutoka kwao anapata hati ya Wizara ya Maendeleo ya Adrhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

  “Tupo mbioni kuanza mchakato wa kuanza kuuza na maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.Ni wajibu wetu kama kampuni ya kizalendo kuhakikisha tunaunga mkono kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda.Hivyo tumeamua kuunga mkono kwa vitendo kwa kuanza kuuza maeneo ambayo yatatumika kwa ujenzi wa viwanda,”amesma.Mohamed.

  Kuhusu uwepo wao kwenye maoesho hayo amesema kikubwa wanataka kuwaambia wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla shughuli ambazo kampuni yao inafanya.Akizungumzia baadhi ya maeneo ambayo wanayo kwa ajili ya viwanja ni Kigamboni, Bagamoyo, Kibaha, Chanika, Morogoro, Mbweni(Kilakala), Mabwe pande, Arusha eneo la Kisongo.

  Amewaomba wananchi wanaofika kwenye maonesho hayo kufika kwenye banda lao ili kupata maeleo kuhusu viwanja na bei zake na kubwa zaidi lengo lao ni kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na uhakika wa eneo ambalo limepimwa kwa ajili ya makazi.
  Meneja Masoko wa Kampuni ya Cholemu Investment,Swaumu Mohamed  akizungumza na Globu ya jamii  leo jijini Dar as Salaam juu ya kuuza mashamba,viwanja bila riba wala dhamana yoyote katika
  maonyesho ya biashara ya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam yanayoandaliwa na Mamlaka ya Mendeleo ya Biashara TANTRADE.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Julai 1, 2018 ameungana na waumini wengine kusali Ibada ya Jumapili, Dominika ya 13, katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Julai 1, 2018 ameungana na waumini wengine kusali Ibada ya Jumapili, Dominika ya 13, katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Jaji Mstaafu Mhe. Thomas  Mihayo, ambaye ni mmoja wa wazee wa kanisa  leo Julai 1, 2018 alipoungana na waumini wengine kusali Ibada ya Jumapili, Dominika ya 13, katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana amani na  waumini wengine kusali Ibada ya Jumapili, Dominika ya 13, katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es salaam.Picha na IKULU

  0 0

  Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaendelea kutoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupokea maoni na mrejesho kutoka kwa wananchi, usajili wa walipakodi na kutoa elimu juu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa manufaa ya wananchi wote kwa ujumla.

  Akizungumzia juu ya TRA ilivyojipanga katika kutoa huduma kwa wananchi katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Richard Kayombo amesema kuwa, wananchi watumie fursa hii kujifunza masuala mbalimbali ya kodi ili kuongeza uelewa na uhiari wa ulipaji kodi.

  "Sisi kama Mamlaka tumejipanga kuhakikisha kuwa, tunatoa huduma kwa kila mwananchi atakayetembelea banda letu na tunapokea maoni na mrejesho kutoka kwa wananchi. Vilevile tunasajili walipakodi, tunawaelimisha wananchi umuhimu wa kulipa kodi, tunaelezea haki na wajibu wa Mlipakodi kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Huduma na Mlipakodi pamoja na kuwaonyesha makusanyo yote ya miaka mitatu ya fedha iliyopita yaani kuanzia 2015/16, 2016/17 na 2017/18," alisema Kayombo.

  Kayombo ameongeza kuwa, makusanyo yanayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania ndiyo hutumika katika kutoa huduma mbalimbali za jamii ikiwemo miundombinu ya barabara na umeme, maji safi na salama, elimu pamoja na huduma za afya.Naye Meneja wa Huduma kwa Mlipakodi ambaye pia ni Mratibu wa maonyesho hayo kwa upande wa TRA Bi. Honester Ndunguru ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika banda la TRA ili waweze kupata elimu sahihi ya kodi na hatimaye waweze kulipa kodi stahiki na kwa wakati.

  "Kila mwaka tunashiriki maonyesho haya ya Sabasaba lakini kwa mwaka huu tumejipanga vizuri zaidi hivyo nachukua fursa hii kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika banda letu ili tuwahudumie na kuwaelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kodi na hatimaye waweze kulipa kodi sahihi na kwa wakati unaotakiwa," alisema Ndunguru.Banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania linapatikana ndani ya viwanja vya Sabasaba na lipo mkabala na banda la Azam ambapo wananchi wanaendelea kupata huduma mbalimbali zinazotolewa ndani ya banda hilo.

  Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Richard Kayombo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akizungumzia juu ya TRA ilivyojipanga katika kutoa huduma kwa wananchi katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yaliyoanza tarehe 28 Julai, 2018 jijini Dar es Salaam.
   Meneja wa Huduma kwa Mlipakodi ambaye pia ni Mratibu wa Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba kwa upande wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  Bi. Honester Ndunguru (kushoto) akijadiliana jambo na Maafisa wa Kodi wakati wa maonyesho hayo yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 
    Afisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Mercy Macha akitoa elimu ya kodi kwa wananchi waliotembelea Banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
   Afisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Judith Lwaikondo akimhudumia mwanachi aliyetembelea Banda la TRA kwa ajili ya kupata huduma wakati wa Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 
  Baadhi ya wateja wakitoka katika Banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Banda la TRA lipo mkabala na banda la Azam ndani viwanja vya Sabasaba. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu leo amehudhuria ufunguzi wa Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) katika mji Nouakchott, Mauritania. 

  Pamoja na mambo mengine mkutano huu umejikita katika masuala ya Kupambana na Rushwa katika bara la Afrika, Mkakati wa Biashara ya Pamoja ,masuala ya Ulinzi na Amani katika nchi za Congo DRC, Burundi na Sahara Magharibi, pamoja na kujadili masuala ya mabadiliko yatakayoleta tija katika Utawala na kuboresha uchumi. 

  Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Katika hotuba ya Ufunguzi wa mkutano huo, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ,Rais wa Rwanda Paul Kagame alisema “ Kama umoja, tupo pamoja na watu Ethiopia na Zimbabwe, kufuatia mabadiliko ya kisiasa ya amani. Tunashutumu mashambulizi yaliotaka kuvuruga amani na tunatoa pole kwa waliopoteza maisha”. 

  Kagame amesema pia wameridhiswa na hatua zinazoendelea za kuleta Amani Sudani ya Kusini. Mkutano huo unatarajiwa kumalizika kesho ambapo kuna uwezekano mkubwa Viongozi hawa wa Afrika watakutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa chakula cha mchana .
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine pamoja na Viongozi waandamizi wakati ufunguzi wa Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) katika mji Nouakchott, Mauritania Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia kwa makini yanayoendelea kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) katika mji Nouakchott, Mauritania ambako anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).Picha zaidi: Makamu wa Rais ahudhuria ufunguzi wa Mkutano wa AU Mauritania​.

  0 0

  Na Emmanuel Massaka ,Globu ya jamii

  WAKAZI wa  Kata ya Somangila  wilayani Kigamboni mkoani Dar es Salaam  wamemuomba  Rais Dk.John Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es SalaamPaul Magufuli kuingilia kati suala la mgogoro uliopo kwenye Kata hiyo uliokwamisha miundombinu ya barabara kusimama.

  Hayo yamebainishwa jana na wakazi wa eneo hilo wakati wakizungumza na waandishi wa habari walipokuwa wamekutana na  Diwani wa Kata hiyo,Chichi Masanja na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo Sadick Mohamed ambapo wameelezea kuhusu kero yao ya miundombinu ya barabara ambayo imekwamishwa na mmoja wa Mkurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam. 

  Wakazi hao wakizungumza kwa nyakati tofauti wameelezea kwamba Mkurugenzi huyo(wakamtaja )  amezungushia uzio kwenye eneo la barabara hivyo kusababisha usumbufu hasa kwa akina mama wajawazito wanapohitaji kwenda kujifungua.

  Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo kijiji cha Dege Kata ya Somangila, Sadick Mohamed, amesema kuwa Mkurugenzi huyo amejimilikisha zaidi ya ekari 100 ambazo haziendelezwi na hivyo zimesababisha kuwepo kwa wahalifu wanaojificha kwenye vichaka vilivyopo kwenye mashamba hayo.

  Amesema kuwa mbali  na wahalifu pia amekwamisha miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa Barabara unaosimamiwa na Wakala wa Barabara vijijini na mijini  (TARULA) ambayo tayari fedha zake zilikwisha tengwa katika bajeti ya 2017/18 hivyo ujenzi huo ukiendelea kusimama fadha hizo zinaweza kurudi Serikali kuu.

  Wakati huo huo Diwani wa Kata hiyo Chichi Masanja amesema ni vema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuingila kati suala hilo kwani linakwamisha maendeleo katika wilaya hiyo.Na iwapo ipo haja ya Rais Magufuli kuingilia kati utakuwa jambo jema zaidi.

  0 0  Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza na wadau wa Sanaa na Utamaduni ( hawapo katika Picha), wakati wa ufunguzi wa tamasha la TAMANI FESTIVAL lililopewa jina la TANZANIA MAMA NI WA THAMANI ASANTE MAMA 2018, chini ya uratibu wa Tanzania Gospel Artist Network (TAGOANE) Jijini Arusha.

  Rais wa Taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network(TAGOANE) Dkt. Godwin Maimu akisoma risala ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (Hayupo katika picha), wakati wa ufunguzi wa TAMANI FESTIVAL Jijini Arusha.
  Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (Kushoto) akisalimiana na Mjasiriamali wa bidhaa za chupa za urembo Bibi . Glory Silayo (kulia) anayemiliki kampuni ya AfricanBae, katika uzinduzi wa TAMANI FESTIVAL Jijini Arusha.
  Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akisalimiana na wakina mama wa jamii ya kimasai waliohudhuria uzinduzi wa TAMANI FESTIVAL katia viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

  Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akisikiliza maelekezo ya namna ya kumsaidia mtu aliyepata ajali kutoka kwa Mkufunzi wa Huduma ya Kwanza wa Msalaba Mwekundu Bw. Tisian Temba (kulia) katika uzinduzi wa TAMANI FESTIVAL Jijini Arusha.
  Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akipimwa presha na Muuguzi Mkuu Mwandamizi kutoka Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru Bibi. Patricia Khatibu , alipotembelea banda hilo wakati wa uzinduzi wa TAMANI FESTIVAL lililoandaliwa na Taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha,(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha


  Na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha.

  Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ameeleza kuwa Serikali inatambua juhudi zinazofanywa na wadau mbalimbali katika kutangaza utamaduni wa Mtanzania pamoja na kukuza soko la ajira kupitia kazi za sanaa nchini.

  Hayo ameyasema leo Jijini Arusha , alipokuwa akifungua Tamasha la TANZANIA MAMA NI WATHAMANI “TAMANI FESTIVAL” ASANTE MAMA 2018 lililoandaliwa na Tanzania Gospal Nertwork Artist (TAGOANE ) lenye lengo la kulinda na kuendeleza utu wa mwanamke.

  “Naipongeza timu nzima ya TAGOANE kwa juhudi kubwa walioifanya katika kujenga misingi imara ya utamaduni wa kumuwezesha, kumuendeleza na kulinda UTU wa mwanamke kwa ustawi wa taifa letu ” amesema Mhe. Juliana Shonza.

  Aidha Mhe. Shonza aliongeza kwa kueleza kuwa Wizara kupitia Idara ya Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa itashirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali katika kuhakikisha inaweka mazingira mazuri ya kufanya kazi kwa ufanisi zaidi ambapo kwa sasa sanaa imekuwa kiwanda kinachozalisha ajira kwa wingi.

  Alizidi kufafanua kuwa Tamasha la TAMANI FESTIVAL ni kichochea kikubwa katika kutangaza fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya sanaa, ubunifu na ujasiriamali hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kuweza kushiriki katika kuonyesha bidhaa zao.

  Naye Rais wa Taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network Dkt. Godwin Maimu ameeleza kuwa uongozi wa taasisis hiyo utahakikisha unatangaza na kuhubiri maadili mema na kuhimiza uzalendo kwa vijana ili kuwa na jamii bora yenye kuleta maendeleo.

  Tamasha la TAMANI FESTIVAl limefanyika kwa mara ya kwanza na kuzinduliwa katika Jiji la Arusha , ambapo baadaye wamedhamilia kuendelea kulitambulisha katika mikoa mingine ya Tanzania

  0 0

  Kamati ya bunge ya kudumu inayosimamia miundo mbinu,Mwenyekiti wa kamati Ndugu Seleman Kakoso,wakiambata na Katibu  Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Dkt.Leornad Chamuriho pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania, Ndugu Masanja Kadogosa,kukagua njia ya reli Tanga,Moshi,Arusha kwa lengo la kufanya maandalizi ya Uboreshaji wa njia ili iweze kafanya kazi kama awali.

  Shirika la Reli linaendelea na mikakati ya  ufufuaji wa njia za reli zilizokuwa hazifanyi kazi kwa muda mrefu na kuboresha reli zinazoendelea kutoa huduma bora za uhakika kwa gharama nafuu, kukamilika kwa mikakati kunatarajia kuongeza tija katika kuendeleza na kukuza uchukuzi wa viwanda Nchini.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Ndugu Masanja Kadogosa akitoa maelezo kwa kamati ya bunge ya kudumu inayosimamia miundo mbinu mikakati ya Uboreshaji wa njia ya Reli Tanga,Arusha ,Moshi baada ya kusimama kutoa huduma kwa takribani miaka kumi. 
  Kamati ya bunge ya kudumu inayosimamia miundo mbinu ikiendelea kupata ufafanuzi wa Uboreshaji wa njia ya Reli Tanga,Arusha na Moshi walipofanya ziara ya kutembelea njia hizo.

  0 0

  Na Frankius Cleophace Tarime.

  Waliokuwa Ngariba Wilayani Tarime Mkoani Mara wamepatiwa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa lengo la kujikwamua Kiuchumi ili wasirudie tena suala Ukeketaji kwa Mtoto wa ni baada ya kupatiwa Elimu juu ya Madhara ya Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.

  Ngariba hao wamedai kuwa kipindi cha Ukeketaji hupata pesa Nyingi zinazotokana na Ukeketaji jambo ambalo uwangumu kuacha kitendo hicho licha ya Mashirika mbalimbali likiwemo Shirika la AFGM Masanga kuendelea kutoa Elimu juu ya Madhara ya Ukeketaji ili Jmii iweze kubadilika.

  Kwa kuliona hilo Shirika la ATFGM Masanga ambao ni wadau wa Kupinga Ukatili katika Jamii wameamua kutoa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa Waliokuwa Ngariba lakini kwa sasa wameachana na Kitendo hicho baada ya kupewa Elimu ili waweze kufanya kazi zinazotambulika na Serikali kwa lengo la kujipatia kipato na siyo kutegemea tena Ukeketaji.

  Mafunzo hayo ya Ujasirimali pia yamewashirikisha Mabinti lengo ni kuwajengea Uwezo ili kuendelea kutoa Elimu hiyo katika Jamii inayowazunguka huku walikuwa Ngariba hao wakipatiwa Mafunzo ili kuendeleza Biashara zao na kuondokana na mawazo ya kurudia kukeketa tena.

  Wamedai kuwa katika Kukeketaji wamekuwa wakipata zaidi ya Mill Nane mpaka Tisa Ukeketaji unamalizika huku Binti Mmoja akikeketwa kuanzia Elfu Kumi na zaidi.“Sisi kipindi cha Ukeketaji tulikuwa tunapata Pesa Nyingi lakini kwa sasa wazee wamekataa hatutakeketa tena hivyo tunaomba Serikali itupatie Mitaji baada ya Mafunzo haya tuliyoyapata” alisema Mmoja wa Walikuwa Ngariba.

  Akifunga mafunzo hayo katibu wa afya wilaya ya Tarime Neema Alphonce amewataka Waliokuwa Ngariba pamoja na Mabinti hao kuendelea kuwa mabarozi wazuri katika Jamii inayowazunguka huku wakitumia Vizuri Vikundi vilivyoundwa na kupewa Elimu ya Ujasiriamali.

  Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo Stella Tungalaza amezidi kusisitiza kuzingatia vyema kile Walichofundishwa darasani kwa lengo la kujikomboa na kuongeza Uchumi

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la ATFGM Masanga Sister Stella Mgaya ambao ni wadau wa kuipiga Vita Ukatili wa Kijinsia Wilayani Tarime Mkoani Mara anazidi kusisitiza Wazee wa Mila kusimia Vyema Kauli ya kuwa Mwaka huu hapatakuwa na Ukeketaji na Kuomba Serikali kuendelea Kushirikiana Vyema na Mashirika hayo ili kuchukua hatua kali kwa wale watakaokiuka na Kukeketa Mtoto wa Kike.

  “Wazee walishatoa Kauli kuwa hakuna Ukeketaji lakini Wakurya wanatabia ya Kujaribu hivyo wanaweza Kujaribu kukeketa na Serikali isipofuatilia wanaongeza kasi ya kukeketa sasa tushirikiane zaidi japo tunashirikiana Vizuri” alisema Stella Mgaya.

  Mgeni rasmi ambaye ni Katibu wa Afya Wilaya ya Tarime Neema Alphonce akikabidhi cheti cha Mafunzo ya Ujasiriamali kwa mmoja wa waliokuwa ngariiba baadaya kupata Elimu hiyo.
  Picha ya pamoja na Mgeni rasmi na Washiriki baada ya kupata Mafunzo hayo.
  Stella Tingalaza ambaye ni Mwezeshaji wa Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la ATFGM Masanga akiendelea kutoa Elimu kwa washiriki hao wakiwemo Mabinti kutoka Maeneo tofauti.
  Mkurugenzi wa Shirika la ATFGM Masanga Sister Stella Mgaya akiongea na Washiriki wa Mafunzo hayo na kusisitiza suala kuendelea kuelimisha jamii katika Maeeo wanayotoka.
  Washiriki wakiendelea na Mafunzo hayo.
  Mkurugenzi wa Shirika la ATFGM Masanga Sister Stella Mgaya akipongeza Mmoja wa washiriki wa Mafunzo hayo.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 hatua ya mchujo imemalizika kwa timu 15 kuingia hatua inayofuata  baada ya michezo 25 kupigwa ndani ya Viwanja vya JMK Youth Park Kidongo Chekundu Jijini Dar es Salaam.

   Mechi hizo zilizoanza saa 2 asubuhi ilizikutanisha timu 50 zote zikiwania nafasi ili ziweze kuingia hatua inayofuata ya 16 bora kuungana na mabingwa watetezi wa Mchenga BBall Stars.

  Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini (TBF) Manase Zablon amesema timu hizo zilizofanikiwa kutinga hatua ya 16 bora wameweza kutumia vigezo vya utofauti wa alama za kushinda na kufungwa.

  Manase amesema," mechi zilichezwa 25 na washindi 25 walipatikana katika mchezo vigezo vilivyotumika ili kuwapata wakaoenda hatua ya 16 bora tuliangalia utofauti wa vikapu vya kushinda na kufungwa."

  Amesema, mechi zilikua na ushindani mkubwa sana na ushindani huo ulipelekea hata zile timu zilizoshiriki mwaka jana zitoke mapema kwakuwa kila timi imejiandaa kuhakikisha wanakuwa mabingwa wapya wa mwaka 2018.

  Timu zilizofanikiwa kuingia hatua inayofuata  kuungana na mabingwa watetezi ili kutimiza idadi ya timu 16 ni The Team Kiza, Stylers, St Joseph, Oysterbay, Flying Dribblers, Portrands, Raptors, Ukonga Hitmen, Ukonga Warriors.

  Zingine ni Temeke Heroes,Water Institute, Fast Heat, Mbezi Beach KKKT, Air Wings na DMI na ratiba ya hatua ya 16 bora itapangwa mbashara leo kwenye kituo cha EATV saa 3:30 kupitia kipindi cha 5 Sports.

  Michuano ya Sprite BBall Kings imeandaliwa na kituo cha Televishen cha EATV na Radio yakidhamiwa na kinywaji cha Sprite wakiwa na lengo la kurejesha heshima ya mpira ya kikapu nchini.

  Bingwa wa michuano hiyo atajinyakulia kitita cha Shilling Milioni 10 na kikombe, mshindi wa pili akibeba Milioni 3 na mchezaji bora wa mashindano ( MVP) akibeba milioni 2.
   Mchezaji wa timu ya St Joseph Jermaine Ishengoma akiifungua timu yake dhidi ya Madena Ballers. Ambapo St joseph aliibuka mshindi katika hatua ya mchujo  uliofanyika jumamosi jijini Dar es salaam katika viwanja vya JMK Youth Park kidongo chekundu.
   Mchezaji wa Oysterbay Godfrey Swai akijaribu kumtoka mchezaji wa Ilala East Zone Ally Salum Bakari wakati wa mashindano ya mpira wa kikapu ya sprite bball kings hatua ya mchujo uliofanyika jumamosi jijiji dar es salaam katika viwanja vya JMK Youth Park kidongo chekundu, Ambapo Timu ya Oysterbay iliibuka ushindi wa vikapu 48 kwa 19.
   
   Mchezaji wa timu ya Montifort  akijaribu kumshambulia mpinzani wake wa timu ya Goldent Talent  wakati wa mashindano ya mpira wa kikapu ambapo tmt iliondoka na ushindi.Ambapo Timu ya Montifort  iliibuka ushindi wa vikapu 24 dhidi ya 22 ya Goldent Talents.
  Bampa to Bampa......

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na huduma kwa wateja Shirika la Bima (NIC) Elisante Maleko,katikati akimkabidhi zawadi mfanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Zodo M Zodo(kushoto) baada ya kutembelea banda la maonesho ya 42 katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam jana.kulia ni Ofisa Bima za Maisha Honest Valence. 
  Huduma zikiendelea katika banda la NIC 
  Mchungaji wa KKKT Mtaa wa Bonyukwa Bongye Lameck akijaza fomu ya moja ya huduma za bima zinazotolewa na Shirika la Bima la Taifa (NIC) jana wakati wa maonyesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam, kulia ni Honest Valence Afisa Bima wa NIC.
  Picha ya Pamoja ya baadhi ya wafanyakazi wa NIC wakiwa katika banda lao kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendele jijini Dar es Salaam

older | 1 | .... | 1610 | 1611 | (Page 1612) | 1613 | 1614 | .... | 1897 | newer