Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1611 | 1612 | (Page 1613) | 1614 | 1615 | .... | 1898 | newer

  0 0  Baadhi ya wafanyakazi katika banda la maonesho la ASAS DAIRIERS LTD wakihudumia wananchi waliotembelea kwenye banda hilo katika Maonesho ya Biashara ya Sabasaba TANTRADE barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo.
  Wananchi mbalimbali wakijinunulia bidhaa mbalimbali katika banda la ASAS DAIRIERS LTD kwenye Maonesho ya Biashara ya Sabasaba TANTRADE barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo.
  Msanii na Mtangazaji wa kituo cha redio cha EFM Ummy Wenceslaus (Dokii) akiwa na baadhi ya wafanyakazi katika banda la ASAS DAIRIERS LTD.


  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  KAMPUNI ya Asas Dairies imesema inatarajia kuanza kutoa zawadi za aina mbalimbali katika banda lao lililopo kwenye Maonesho ya Biashara ya kimataiafa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam baada ya maonesho hayo kuzinduliwa rasmi.

  Baadhi ya zawadi ambazo zitatolewa na Asas katika msimu huu wa maoneshao hayo ziko nyingi na miongoni mwa zawadi hizo ni Gym Bag , Power Bank,Peni, fulana, na kofia.Akizungumza leo kwenye banda la Asas lililopo kwenye maonesho hayo Meneja Masoko na Matukio wa kampuni hiyo Jimmy Kiwelu amesema kuwa wanatambua kuwa maziwa ya Asas yanapendwa na kukubalika na Watanzania wengi na hivyo wameamua kutoa zawadi kwa wananchi ambao watafika kwenye banda lao.

  Kiwelu amesema utoaji wa zawadi hizo utaanza baada ya kufanyika kwa uzinduzi rasmi wa maonesho hayo na kueleza wamejipanga kuhakikisha kila anayefika kwenye banda lao anapata zawadi na zitatolewa kupitia mashindano mbalimbali ambayo yameandaliwa katika kipindi hiki.

  Akizungumzia mahudhurio ya wananchi kwenye banda lao amesema ni mkubwa mno na hiyo inatokana na kukubalika kwa bidhaa zao na kufahamika na walio wengi.Kiwelu amesema ni jambo la faraja kwa kuona wananchi wameendelea kuwaunga mkono kwa kunununua bidhaa zao katika maonesho hayo kwa wingi ambapo pia wameamua kutenga eneo kwa ajili ya kuchezea watoto wakati wakinywa maziwa ya Asas.

  0 0

  Na Said Mwishehe, Globu ya jamii.

  WAHITIMU wa Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro wameamua kutumia taaluma ambayo wameipata chuoni hapo kufanya shughuli za ujasirimali kwa kubuni bidhaa za kipekee.

  Baadhi za wahitimu hao ambao wamepikwa vema na Chuo Kikuu cha Mzumbe wameonesha kwa vitendo kuwa elimu ambayo wanaipata chuoni hapo ni mkombozi kwa Watanzania huku wakijivunia bidhaa ambazo wanazalisha kwa ubora wa hali ya juu.Mmoja wa wahitimu wa Chuo kikuu cha Mzumbe Sia Mshiu akiwa kwenye Banda la Chuo hicho katika Maonesho ya biashara ya kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam amesema kuwa kutokana na elimu ambayo ameipata ameweza kuzalisha Wine na Kahawa.

  “Elimu ambayo nimeipata darasani imenifanya sasa niwe mjasiriamali na nimeweza kubuni bidhaa zangu ambapo kwa sasa natengeneza Kahawa na Wine.“Kahawa ambayo naitengeneza ina ladha ya aina yake ambapo pia wakati wa kuitengeneza nachanganya na viungo na hivyo kuwa na aina Fulani ya ladha ambayo huwezi kuipata kokote zaidi ya kahawa ambayo natengeneza,”amesema Mshiu.

  Amefafanua kutokana na kufanikiwa kutengeneza bidhaa hizo lengo lake ni kuhakikisha anasajili Mamkala ya Chakula na Dawa(TFDA)na baadae Shirika la Viwango Tanzania(TBS) ili kuifanya iwe rasmi na kuingiza sokoni.Ametoa ombi kwa Rais Dk.John Magufuli kuwa iwapo itawezekana anatamani kuona kunaandaliwa mazingira mazuri ambayo yatajenga daraja la kuunganisha wajasiriamali wadogo kama yeye na kisha kuwaunganisha na wawekezaji wakubwa ili kuhakikisha siku moja nchi yetu inapiga hatua ya kimaendeleo.

  Chuo kikuu cha Mzumbe kimeweka utaratibu wa kuhakikisha wanafunzi ambao wamemaliza kwenye chuo hicho kuendelea kuwafuatilia na kuwaendeleza katika shughuli ambazo wanazifanya.


  Mkuu wa Mawasiliano Chuo Kikuu cha Mzumbe Bi. Sylivia Lupembe akimtambulisha Sia Nshiu mhitimu wa Programu ya Intrepreneuship "Trade Promotion For Industrial Development" katika Chuo hicho ambaye yupo katika maonyesho hayo akionyesha bidhaa zake za kahawa na mvinyo katika maonesho ya biashara ya Sabasaba kwenye viwanja vya TANTRADE barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo huku Waziri wa viwanda na Biashara Mh. Charles Mwijage akimsikiliza wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara RANTRADE Bw. Edwin Rutageruka.
  Sia Nshiu mhitimu wa Programu ya Intrepreneuship "Trade Promotion For Industrial Development" katika Chuo Kiku cha Mzumbe akitoa maelezo ya bidhaa zake kwa Waziri wa viwanda na Biashara Mh. Charles Mwijage wakati alipotembelea banda la chuo hicho katika maonyesho ya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam kulia ni Mkuu wa Mawasiliano Chuo Kikuu cha Mzumbe na wa pili kutoka ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara RANTRADE Bw. Edwin Rutageruka.
  Waziri wa viwanda na Biashara Mh. Charles Mwijageakifurahia jambo na Mkuu wa Mawasiliano wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Bi. Sylivia Lupembe wakati alipomaliza kutembelea katika banda hilo kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara RANTRADE Bw. Edwin Rutageruka.
  Bw Innocent Mgeta Afisa Udahili Mwandamizi akiwapa maelezo baadhi ya wananchi waliofika katika banda hilo.
  Bi Sia Nshiu akitoa maelezo kwa Bi Masha Kimaku aliyetembelea katika banda hilo.

  0 0

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itafanya uchaguzi mdogo kwenye Jimbo la Buyungu, Mkoani Kigoma na kwenye Kata 79 za Tanzania Bara, Mwenyekiti wa NEC, Jaji (R), Semistocles Kaijage amesema.

  Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana, Jaji Kaijage amesema uchaguzi huo utafanyika tarehe 12 mwezi ujao (Agosti) na fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kuanzia tarehe 8 hadi 14 mwenzi huu (Julai).

  "Uteuzi wa Wagombea utafanyika tarehe 14 Julai, mwaka huu. Kampeni za Uchaguzi zitafanyika kati ya tarehe 15 Julai, hadi tarehe 11 Agosti, mwaka huu na siku ya uchaguzi itakuwa ni tarehe 12 Agosti mwaka huu,” alisema.

  Jaji Kaijage amebainisha kwamba Tume imetangaza uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge kwenye Jimbo hilo la Buyungu baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Ndugu Job Ndugai.

  “Tumeilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifaya Uchaguzi, Suraya 343, aliitarifu Tume uwepo wa nafasi wazi ya Mbunge wa Jimbo la Buyungu katika Halmashauri ya Kakonko Mkoani Kigoma kufuatia kufariki kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mheshimiwa Kasuku Samson Bilago,” alisema.

  Kwa upande wa nafasi wazi za Udiwani, Mwenyekiti huyo alisema Tumeilipokea taarifa kutoka kwa waziri mwenye dhamana akiitaarifu juu ya uwepo wa nafasi hizo na taratibu za uchaguzi mdogo zikaanza mara moja.

  “Tumeimepokea Taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa ambaye kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali zaMitaa, Sura ya 292, aliitarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata 79 za Tanzania Bara,” alisema.

  Akitoa wito kwa vyama vya siasa, Jaji Kaijage amesema “tunapenda kuvikumbusha Vyama vya Siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia Sheria, Kanuni, Maadiliya Uchaguzi, Taratibu, Miongozo na maelekezo yote wakati wa kipindi cha Uchaguzi mdogo”.

  JajiKaijagealisemakwambauchaguzihuomdogoutafanyikandaniyaHalmashauri 43zilizopokwenyeMikoa 24ya Tanzania Bara.

  Mikoa hiyo ni pamoja na, Kigoma, Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Lindi, Manyara, Mara, Mbeya, Mtwara, Morogoro, Mwanza, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Simiyu, Singida, Songwe, TaboranaTanga.

  Halmashauri hizo ni pamoja na Moshi, Ruangwa, Mbulu, Hanang, Babati, Serengeti, Tarime, Kyela, Mtwara, Newala, Kilombero, Kilosa, Kwimba, Makete, Wanging’ombe, Kalambo, Songea, Msalala, Meatu, Singida, Songwe, Tunduma, Tabora, Nzega, UrambonaTanga.

  Halmashauri nyingine ni pamoja na Karatu, Longido, Arusha, Ngorongoro, Monduli, Meru, Ubungo, Kondoa, Mpwapwa, Chamwino, Iringa, Kyerwa, Misenyi, Muleba, Nsimbo, KasulunaSame.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji (R), SemistoclesKaijage.

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda akielezea jambo kwa wawakilishi wa mradi wa TACIP baada ya kupokea barua yao. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Nicholaus William na katikati ni Mratibu wa mradi huo, Bw. Macmillan George.
  Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda akiongea na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Nicholaus William baada ya kupokea zawadi ya picha ya kuchora ya simba iliyotolewa na wawakilishi wa mradi wa TACIP.
  Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda akimsikiliza Rais wa TAFCA na Mtendaji Mkuu Mshirika wa Mradi wa Utambuzi wa Sanaa za Ufundi Tanzania (TACIP), Bw. Adrian Nyangamalle wakati yeye na wenzake walipomtembelea nyumbani kwake, kijiji cha Nzinje, nje kidogo ya Jiji la Dodoma kumuomba awe mlezi wa mradi huo.

  0 0

  Songwe: Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amezindua rasmi maonesho ya tatu ya Utalii Karibu Kusini 2018 yatakayofanyika mkoani Iringa Septemba 26 hadi 30 mwaka huu, huku akiwataka wakuu wa mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini kuandaa kalenda ya pamoja itakayoainisha matukio ya kimkakati katika kutangaza vivutio vya utalii katika mikoa hiyo.

  Agizo hilo, Waziri Kigwangalla alilitoa mwishoni mwa wiki mkoani Songwe wakati akifunga rasmi maonesho ya utalii ya Kimondo yaliyoratibiwa kwa mafanikio makubwa na Mkoa huo huku pia akitumia fursa hiyo kuzindua rasmi Maonesho ya tatu ya Utalii Karibu Kusini 2018 yanayohusisha mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kupitia uratibu wa mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii.Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ni Iringa,Mbeya,Songwe,Ruvuma,Njombe,Katavi na Rukwa.

  Akifafanua kuhusu agizo hilo, Dk Kigwangalla alisema ipo haja ya mikoa hiyo kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuhakikisha kwamba inabuni kalenda ya pamoja itakayoainisha matukio ya kiutalii kwa kila mkoa kisha kuyapanga katika mtiririko maalumu katika kipindi cha mwaka.

  "Uwepo wa kalenda ya pamoja kwenye hili utawasaidia kufahamu mkoa upi unafanya nini kwa wakati fulani na hivyo kuwa rahisi kwa mikoa jirani kuweza kutoa ushirikiano kuhakikisha tukio hilo linakuwa kubwa zaidi bila muingiliano lakini pia itatoa fursa kwa walengwa ambao ni watalii na wadau wengine kufahamu kipi kinaendelea katika ukanda huu kwa wakati husika ili na wao pia waweze kujipanga'' alifafanua.

  Alisema wingi wa vivutio vya utalii katika Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini ni sababu tosha kuweza kuvutia zaidi idadi kubwa ya watalii haswa kama mikoa hiyo itashirikiana kuvitangaza kwa pamoja kupitia matukio ya kimkakati yakiwemo maonesho ya Utalii Karibu Kusini ambayo yanafanyika mara ya tatu mkoani Iringa.

  Akizungumzia agizo hilo la Dk Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Galawa alisema tayari mazungumzo yameanza miongoni mwa wakuu wa mikoa hiyo kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) kuangalia namna bora ya kuandaa kalenda itayoainisha matukio makubwa ya kiutalii na kiuwekezaji kwa kila mkoa ili yaingizwe kwenye agenda ya pamoja.

  "Mheshimiwa Waziri tayari tumeshaanza mazungumzo ya awali kuhusu uwepo wa kalenda ya pamoja ambapo kila mkoa utajipambanua kwa tukio lake kubwa litakalotambuliwa na mikoa mingine ndani ya kanda yetu ili kuongeza ushirikiano na hivyo kufanya kila tukio la mkoa husika miongoni mwetu liwe kubwa zaidi kwa kuwa litahusisha ushiriki wa pamoja.'' alisema

  Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William alisema katika kufanikisha maonesho ya Utalii Karibu Kusini kwa mwaka huu mkoa huo umejipanga kushirikisha wadau kutoka mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini pamoja na kutoa mwaliko kwa mikoa jirani ili kuhakikisha kwamba vivutio vyote vya utalii katika ukanda huo vinatangazwa kupitia maonesho hayo.

  Akifafanua kuhusu maandalizi ya maonesho hayo, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alisema pamoja na maonesho ya Utalii yatakayoanza Septemba 26 hadi 30 mwaka huu, pia maonesho hayo yatahusisha michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa gofu utakaoanza Julai 27 hadi 29 wilayani Mufindi.

  "Kuanzia Septemba 26 hadi 30 ndio kutakuwa na mfululizo wa matukio mengi zaidi ikiwemo kongamano la Utalii Nyanda za Juu Kusini, Mbio za baiskeli, mashindano ya kumpata ya mlimbwende wa utalii kanda yetu, maonesho ya ngoma za asili na mwisho kabisa tutakuwa na nusu marathon itakayofanyika Septemba 30 ambayo ndio siku ya kufunga maonesho yetu,'' alifafanua.

  Mratibu wa maonesho ya Utalii Karibu Kusini kutoka Kampuni ya Capital Plus Internantional (CPI) inayoshirikiana na Mkoa wa Iringa kuratibu maonesho hayo, Bw Clement Mshana alisema kwa mwaka huu yana maboresho makubwa ambapo mbali na kuongeza uhusishwaji wa sekta binafsi wao, kama waratibu wamejipanga kuhakikisha yanaandaliwa katika viwango vya kimataifa.

  "Kwa kushirikiana na ofisi ya mkoa wa Iringa tumejipanga kuhakikisha kwamba maonesho ya mwaka huu yanakuwa na tofauti kubwa sana kuanzia kwenye ubora wa maandalizi, idadi ya washiriki si tu kutoka ndani ya nchi bali pia kutoka nje ya nchi na mwisho kabisa kuhakikisha kila tukio la kimchezo kwenye maonyesho haya si tu linafana bali pia linaleta tija tunayohitaji katika kutangaza utalii wa Nyanda za juu Kusini,'' alisema.Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018 yanalenga kutangaza vivutio pamoja na fursa za kitalii katika mikoa hiyo huku yakiwa na kauli mbiu "Utalii ni Nguzo ya Uchumi wa Viwanda''.
   Baada ya uzinduzi huo ikawa  ni furaha tupu!
  Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangalla akikata utepe kuashiria uzinduzi wa maonesho ya tatu ya Utalii Karibu Kusini 2018 yatakayofanyika Septemba 26 hadi 26 mwaka huu mkoani Iringa wakati wa hafla ya ufungaji wa maonesho ya Utalii ya Kimondo yaliyohitimishwa  mkoani Songwe mwisho wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga ( wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Galawa (kulia kwa waziri Kigwangalla) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela (kushoto).

  0 0

  MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez ametembelea maonesho ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam. Akiwa katika maonesho hayo, maarufu kama ya Sabasaba alikutana na Mkurugenzi Mkuu wa Tan Trade, Bw. Edwin Rutageruka.

  Katika mazungumzo hayo walijadiliana masuala mbalimbali zikiwamo changamoto na fursa za kibiashara na viwanda zinazojitokeza kwa sababu ya kuwapo kwa maonesho hayo kwa Tanzania na Afrika Mashariki. Baada ya mazungumzo hayo, Mratibu huo alifanya ziara katika mabanda kadhaa akianzia na banda la Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.

  Mwaka huu banda la Umoja wa Mataifa lina wabunifui vijana watatu ikiwa ni sehemu ya shughuli ya Umoja huo ya kuibua na kukuza ubunifu kwa maendeleo endelevu. Ukitembelea banda hilo utakutana na Gracious Fanuel ambaye alivumbua mkono wa roboti ambao unaweza kuendeshwa na simu ya mkononi.

  Ni matumaini yake kwamba uvumbuzi huo unaweza kuboreshwa zaidi na kutumika katika viwanda mbalimbali. Mbunifu mwingine ni Latifa Mohammad Ngea kutoka Zanzibar ambaye amevumbua mfumo wa umwagiliaji ambao ni automatiki na inatumia ‘sensa’ kutambua kama ardhi ina unyevunyevu na kupeleka maji katika maeneo makavu.

  Pia katika banda hilo la Umoja wa Mataifa utakutana na Amos Mtambala ambaye anatumia uwezo wake wa kiusanii kufanya ujasiriamali. Amos ambaye amefunzwa na kupewa ufadhili na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ametanua shughuli zake na kuingiza vijana zaidi ya 100.
   Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bw. Edwin Rutageruka alipotembelea viwanja vya Sabasaba vilivyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam .
   Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bw. Edwin Rutageruka katika chumba maalum cha wageni mashuhuri alipotembelea maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
   Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akizungumza jambo na Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (wa pili kulia) pamoja na Afisa Uhusiano wa Shirika la Kazi nchini (ILO), Magnus Minja wakati wakielekea kwenye banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
   Afisa Uhusiano wa Shirika la Kazi nchini (ILO), Magnus Minja (kushoto aliyenyoosha kidole) akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez kuhusu uvumbuzi uliofanywa na kijana Gracious Fanuel wa roboti anayeweza kufanyakazi kwa kupitia mifumo ya simu, roboti huyo anaweza kutumika katika shughuli mbalimbali za viwandani wakati alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
   Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez akiwasilikiliza vijana wabunifu Gracious Fanuel na Latifa Mohammad Ngea kutoka Zanzibar wakati alipotembelea Banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
   Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na Ofisa wa Mawasiliano kwa Umma wa TanTrade, Daniel Diha wakati alipotembelea Banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
   Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez akipata maelezo kutoka mwanamke mjasiariamali kutoka Zanzibar alipotembelea banda la SIDO katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.


  0 0


  NA WAMJJW-DAR ES SALAAM

  WIZARA ya afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imetangaza rasmi kuanzia Juali 1 2018 imepokea Hospitali 28 za Rufaa za Mikoa ambazo zilikuwa chini ya usimamizi wa OR-TAMISEMI .

  Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala. “Hospitali ambazo tumezipokea zina jumla ya vitanda 7,474 na jumla ya watumishi 8,671 ambao, kati yao Wauguzi ni 3,960, Madaktari 536, Madaktari Bingwa wa fani mbalimbali ni 182, na waliobakia ni watumishi wa kada zingine mbalimbali za Afya” alisema Waziri Ummy.

  Waziri Ummy amesema kuwa Hospitali ambazo Wizara imezipokea ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mount Meru (Arusha), Dodoma General (Dodoma), Kitete (Tabora), Shinyanga, Geita, Singida, Mpanda (Katavi), Mawenzi (Kilimanjaro), Bombo (Tanga), Morogoro, Ligula (Mtwara), Sokoine (Lindi), Maweni (Kigoma), Sekou Toure (Mwanza), Mwananyamala, Amana, Temeke (Dar es Salaam), Songwe, Kibena (Njombe), Iringa, Tumbi (Pwani), Sumbawanga (Rukwa), Bariadi (Simiyu), Musoma (Mara), Songea (Ruvuma), Mbeya, Babati (Manyara) na Bukoba (Kagera).

  Waziri Ummy alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2018/19, Wizara imetenga shilingi Bilioni 30 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya kipaumbele katika Hospitali za Rufaa za Mikoa ambako tayari huduma zinatolewa ikiwemo Matibabu kwa wagonjwa wa dharura ,Huduma za upasuaji wa dharura hususan wakati wa ujauzito na uzazi pamoja na Huduma za tiba kwa wagonjwa mahututi zikiwemo za watoto wachanga .

  Mbali na hayo Waziri Ummy amesikitishwa na upungufu wa wodi pamoja na vitanda kwa ajili ya wanawake wanaofika kujifungua katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala na kuahidi kulifanyia kazi mara moja iwezekanavo. “Kama Mama,na nimeumia sana na lazima tulifanyie ufumbuzi mara moja kwahiyo namuagiza katibu mkuu alete mtaalamu wa majengo na tupandishe fedha za kujenga ghorofa mbili mara moja kwakweli halii hii haikubaliki” alisema Waziri Ummy.

  Mnamo Novemba 25, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizindua Hospitali ya Taaluma na Tiba (MAMC) ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) aliagiza kuwa Hospitali za Rufaa za Mikoa zihamishiwe kwenye usimamizi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (WAMJW) kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI.

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelekezo juu ya matangazo yaliyo kwenye mbao mapema leo wakati alipofanya ziara ya kukagua huduma za Afya zinazotolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimsikiliza moja kati ya wagonjwa waliofika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala wakati alipofanya ziara mapema leo katika Hospitali hiyo.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimsikiliza kwa makini Bi Halima Said aliyefika kupata huduma za matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala pindi alipofanya ziara mapema leo katika Hospitali hiyo.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na Bi. Angelina Erasto juu ya umuhimu wa kukata Bima ya Afya ya TOTO AFYA KADI itakayomsaidia kupunguza gharama za matibabu kwa mtoto wake
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akishangaa idadi kubwa ya wakina mama iliyozidi kiasi katika wodi ya kupumzikia wakina mama baada ya kujifungua, akiwa katika ziara yake ya kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala kukagua ubora wa Huduma zitolewazo katika Hospitali hiyo.  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 02 Juni 2018, amezindua kitabu chenye historia ya maisha ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Abraham Mengi kinachoitwa I CAN, I MUST I WILL jijini Dar es Salaam.

  Mhe. Rais Dkt. Magufuli amewataka wafanyabiashara nchini kuiga mfano wa Dkt Mengi na kupuuza maneno ya baadhi ya watu wanaowakatisha tamaa kwani hakuna Serikali yoyote duniani iliyopata maendeleo bila ya kushirikiana na sekta binafsi. Amesema hata Serikali imekuwa ikikatishwa tamaa katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile ujenzi wa Reli ya Kisasa, utoaji elimu bila malipo, ununuzi wa ndege mpya saba na ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa Stiglers Gorge na mingine mingi.

  Pamoja na kukatishwa tamaa huko na baadhi ya watu wasioitakia nchi maendeleo Serikali haikukata tamaa na imekuwa ikiendelea na utekelezaji wa miradi yake kwa lengo la kuwaletea watanzania maendeleo.

   ‘’Ninachotaka kuwaambia Wafanyabiashara wa Tanzania na watanzania kwa ujumla ni kuwa kitabu cha Mzee Mengi kiwe fundisho kwetu sote tunaweza kwelikweli,na mimi napenda nitoe wito kwa wafanyabiashara wote nchini ninarudia wito wangu msisikilize maneno ya watu wanaowakatisha tamaa fanyeni biashara zenu kwelikweli, wekeni uwekezaji wenu wote hakuna Serikali inayoweza kuendelea bila kutegemea sekta binafsi’’ amesema Rais Magufuli.

  Rais Magufuli amesema watanzania wakiamua wanaweza kwani Dkt. Mengi alizaliwa katika familia masikini lakini kwa kuwa aliukataa umasikini ameweza kufikia maendeleo aliyonayo hivi sasa na hivyo kuwataka watanzania wote kujiamini na kuukataa umasikini kwani tunaweza.

  Aidha Rais Magufuli amewataka Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini kuwahamasisha wafanyabiashara katika nchi zao kuja kuwekeza hapa nchini kwani Tanzania ni sehemu salama kwa uwekezaji. Amesema katika historia ya mzee Mengi yapo mengi amekutana nayo ya kumkatisha tamaa lakini yeye hakukata tamaa bali aliamini anaweza na akaamua kufanya  na akaweza hivyo watanzania tuache kukatishana tamaa ili tuweze kufikia mafanikio ya kweli. Dkt. Magufuli amesema Dkt. Reginald Mengi ni mfanyabiashara wa kuigwa hapa nchini kutokana na jitihada zake mbalimbali katika mchango wa Taifa kwa kuwa chanzo cha ajira kwa watanzania na kulipa kodi kwa serikali inayokwenda kutoa huduma mbalimbali kwa watanzania wote.

  Kwa upande wake Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi amempongeza Dkt. Mengi kwa uamuzi wa kuandika historia ya maisha yake na kuonyesha hatua mbalimbali alizopitia hadi kufikia mafanikio aliyonayo kwani ni watu wachache wanaoweza kufanya kitu kama hicho hasa kwa Afrika. Amesema ipo fikra kwamba watu wenye uwezo wa uandishi ni wale wenye taaluma na wasomi katika vyuo mbalimbali lakini Dkt. Mengi amevunja dhana hiyo na kuweza kuandika kitabu hicho.

  Nae Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi amemshukuru Rais Dkt. John Pombne Magufuli kwa kukubali kumzindulia kitabu hicho na kuwataka watanzania kutokata tamaa katika kufikia hatua ya maendeleo kwani alichoandika yeye ni uhalisia wa maisha yake tangu akiwa masikini hadi kufikia mafanikio aliyonayo.

  Dkt. Mengi amepata msukumo wa kuandika kitabu hicho cha historia ya maisha yake ili kutimiza azma ya marehemu mtoto wake Rodney Mutie Mengi aliyemtaka kuandika kitabu hicho na mambo mengine ambayo atayatimiza kadri awezavyo.

  Jaffar Haniu
  Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  02 Julai, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu chenye historia ya maisha ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Abraham Mengi (wa tatu kulia) kinachoitwa I CAN, I MUST, I WILL kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo. Wengine pichani ni Rais Mstaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Prof Rwekaza Mukandala, Mke wa Dkt. Mengi, Jacquline Mengi, Bi. Jane Goodall pamoja na watoto wa Dkt. Mengi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akionyesha kitabu chenye historia ya maisha ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Abraham Mengi kinachoitwa I CAN, I MUST, I WILL baada ya kukizindua kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akitoa hotuba yake katika hafla ya uzinduzi wa kitabu chenye historia ya maisha ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Abraham Mengi kinachoitwa I CAN, I MUST, I WILL iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
  Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP na Muandishi wa kitabu hicho,  Dkt. Reginald Abraham Mengi akizungumza na hadhara iliyofika kwenye uzinduzi wa kitabu chenye historia ya maisha yake.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Binti Wakonta Kapunda ambaye ni mlemavu aliyejishidia kiasi cha Dola elfu 20 kwa kutoa wazo zuri la kibiashara. Rais Magufuli amemuongezea binti hiyo kiasi cha Shilingi Milioni 10. PICHA NA IKULU

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema wameyapokea maoni ya wadau na watayafanyia kazi ili kuongeza ufanisi katika utoaji na urejeshaji wa mikopo.

  Badru aliyasema hayo wakati akizungumza katika banda la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kwenye maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere. Amesema kuwa HESLB inashiriki katika maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kwa wazazi, wanafunzi pamoja wanufaika wa mikopo.

  Amesema kuwa wadau wakifika katika banda la bodi watapata ufafanuzi wa vipengele kwa waombaji mikopo katika bodi hiyo utakaomalizika Julai 15 mwaka huu kwa waombaji hao kupata taarifa sahihi.Badru amesema kuwa wanufaika wa mikopo pia watapata elimu ya urejeshaji wa mikopo iliyoiva ili kuweza kurejesha katika mfuko kwa ajili wengine kunufaika ikiwa ni pamoja na kujua ankara zao kwa ajili ya kulipa kutokana na kuwepo na changamoto katika malipo.

  Aidha amesema kuwa baadhi ya waajiri wamekuwa na mwamko wa kukata asilimia 15 ya mshahara huku wengine wakikata bila kupeleka bodi kwa wakati muafaka.Amesema waajiri ambao wamekuwa wakishindwa kufanya malipo kwa wafanyakazi wao wamekuwa wakiwapeleka mahakamani na wakifika huko wanaomba wazungumze nje ya mahakama na matokeo yake wanalipa.

  Badru amesema kuwa mikopo inatolewa kwa wenye mahitaji maalum na vipaumbele ikiwa kwa watoto yatima, kipato duni, wenye ulemavu na wale ambao wanasomea sekta ambazo zinahitaji wataalam katika kuziba nafasi za utalaam huo.“Changamoto kubwa tuliyonayo ni kuwa waombaji wengi hawasomi mwongozo tunaoutoa na hivyo wanakosea kujaza fomu za maombi mtandaoni. wito wetu kwao ni kuwa wausome kwa makini na kuuzingatia,” amesema Bw. Badru.

  HESLB ilianzishwa kwa sheria mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji na kukusanya mikopo iliyoiva ambayo imetolewa na Serikali tangu mwaka 1994/1995.Wadau mbalimbali wameendelea kutembelea banda la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es salaam na kushauri HESLB ishirikishe wadau katika kutatua changamoto za urejeshaji mikopo iliyoiva.

  Akizungumza katika banda la HESLB, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Prof. Joe Lugalla amesema wanufaika wengi wa mikopo ya elimu ya juu hawana ajira rasmi na hivyo kuhitajika ushirikishwaji mkubwa zaidi ili kuwafikia na kuongeza makusanyo.

  “Kuna wanafunzi wengi wamemaliza masomo na wapo vijijini wanaendelea na shughuli zao binafsi…ni vizuri wadau mbalimbali kama taasisi za elimu ya juu zishirikishwe ili kuwabaini,” amesema Prof. Lugalla.

  Naye Mussa Sayenda ambaye ni mnufaika wa mkopo wa elimu ya juu na mhitimu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam amesema HESLB inapaswa kuboresha matumizi ya teknolojia kwa kuwa na mfumo unaomwezesha mnufaika kupata taarifa za deni lake popote alipo.

  Kwa upande wake, Bi. Severine Mwakalukwa ambaye ni mlezi wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es salaam (DUCE) ameishauri HESLB kuboresha vigezo vya utoaji mikopo ili kuondoa malalamiko ya upangaji mikopo kutoka kwa baadhi ya wanafunzi.
  01.Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru akizungumza na Mwandishi wa Michuzi Blog katika banda la bodi hiyo katika maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru akiwapa huduma wananchi waliotembelea banda la bodi katika maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Prof. Joe Lugalla akipata maelezo katika banda la bodi ya mikopo alipotembelea maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Kippi Warioba akizunguza wakati wa Mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika la Hifadhi ya Jamii(NSSF)  kwa Wajasiliamali ikiwa ni njia mojawapo ya kuwaingiza wote walio kwenye sekta isiyo rasmi katika Mifuko ya Jamaa .
  Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo hayo wakiwemo wawakilishi wa Benki za Azania na NMB.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kuratibisha Sera wa Shirika la Mifuko ya Jamii,(NSSF) Mariam Muhaji akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
  Baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo.
  Baadhi ya Viongozi wa NSSF walioshiriki pia katika Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa NSSF mkoani Kilimanjaro.
  Muwakilishi wa Benki ya NMB  Tawi la Nelson Mandela Moses Koda akichangia jambo wakati wa mafunzo hayo.
  Muwakilishi wa Benki ya NMB ,Adeline Gabriel akichangia jambo  wakati wa Mafnzo hayo.
  Mgeni rasmi ,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Kippi Warioba akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo hayo yanayoendelea maeneo mbalimbali nchi nzima.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .

  SHIRIKA la Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeingia mkataba na Benki za Azania,NMB na NBC  kwa  ajili ya utoaji wa mikopo kwa wanachama wake watakao ingia kwenye mpango wa Hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi, lengo likiwa ni kupunguza hali ya umaskini.
  NSSF  imeanza utekelezaji wa mpango huu baada ya maboresho ya sheria namba 2 ya mwaka 2018 iliyotoa majukumu kwa shirika hilo kuboresha na kushuhulikia sekta isiyo rasmi ambayo inatajwa kuwa kwa muda mrefu imetelekezwa.
  Katika kuhakikisha elimu hii ya inawafikia wananchi wengi ,NSSF imeanza kufanya mafunzo kwa viongozi wa vikundi vya wajasiriamali ili kutoa hamasa na baadae kuwaingiza katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wananchi wote ambao wako kwenye sekta isyo rasmi..
  Mgeni rasmi katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa NSSF mjini Moshi,Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Kippi Warioba akatumia nafasi hiyo kutoa rai kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika kuacha tabia ya ubadhirifu.
  Kwa upande wao washiriki wa Semina hiyo wakiwemo viongozi wa Benki zilizoingia mkataba na NSSF katika kuboresha utoaji wa mikopo kwa wanachama walio kwenye sekta isiyo rasmi wakiwemo wajasiliamali wadogowadogo wameelezea matumani yao juu ya mpango huo wa NSSF.
  Wanachama ambao watanufaika na mpango huu ni wale watakao toka kwenye vikundi vyenye sifa za mikopo ambayo itasimamiwa na Benki ya Azania zikiwemo Saccos na Amcos zaidi ya 100.
  Mwisho.
   

  0 0

  Wafanyabiashara wa soko la Kisutu jijini Dar es salaam wameishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kulijenga upya soko lao ili waweze kufanya biashara zao katika mazingira mazuri.

  Shukrani hizo wamezitoa leo katika ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo alipotembelea sokoni hapo kukagua maandalizi ya mradi huo mkubwa wa ujenzi wa soko la Kisutu. 

  Wafanyabiashara hao kwasasa wamejengewa soko la muda katika eneo la kituo cha mabasi cha Kisutu ya zamani. Wakizungumza mbele ya Waziri Jafo, Wamesema hatua hiyo ya serikali itawawezesha kufanya biashara zao kwenye mazingira rafiki.

  Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amewapongeza viongozi wa wilaya ya Ilala kwa maandalizi mazuri ya mradi huo kwa kujenga soko la muda litakalochukua wafanyabiashara hao wakati soko lao likiwa katika ujenzi.Aidha ameagiza uongozi wa wilaya hiyo kuwapa kipaumbele wafanyabiashara waliokuwepo sasa katika soko hilo pindi soko jipya litakapo kamilika.

  Ujenzi wa soko jipya utagharimu sh.Bilioni 13 ambazo tayari Manispaa hiyo ya Ilala imeshapokea kupitia Mpango wa serikali wa miradi mkakati.Katika mpango huo, serikali imeshatoa zaidi ya Sh.Bilioni 146 katika Mamlaka mbalimbali za serikali za mitaa hapa nchini.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya Ilala pamoja na wafanyabiashara wa soko la kisutu.
  Wafanyabiashara wa soko la kisutu wakitoa maoni yao wakati wa ujio wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo sokoni hapo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za itaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akifanya ukaguzi wa soko la muda lililo andaliwa kwaajili ya wafanya biashara kutoka soko la kisutu.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za itaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akitembelea maeneo mbalimbali ya soko la kisutu lililo katika mpango wa kuboreshwa.

  0 0

  *Yasema ni marufuku kufanya biashara pembezoni mwa reli, yaiomba jamii kulinda miundombinu

  Na Said Mwishehe, Globu ya jamiiSHIRIKA la Reli Tanzania(TRC)limesema linaendelea na mkakati wa uboreshaji wa reli ya kati kutoka Dar es Salaam hadi Isaka ambapo dola za Marekani milioni 300 zitatumika katika uboreshaji huo.

  Limesema lengo la kuboresha reli hiyo ni muendelezo wa kuhakikisha usafiri wa treni nchini unakuwa wa uhakika zaidi na hiyo itafungua fursa za kiuchumi hasa katika kipindi hiki cha mchakato wa ujenzi wa viwanda nchini.Hayo yamesemwa leo na Mratibu wa Uboreshaji wa reli ya kati Mhandisi Mlemba Singo akiwa katika banda la TRC lililopo kwenye maonesho ya bishara yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam.

  Amefafanua mradi huo umefadhiliwa na Benki ya Dunia na utatekelezwa na TRC katika kipindi cha muda wa miaka miwili kuanzia Juni mwaka huu hadi Juni mwaka 2020.Amesema lengo la uboreshaji wa reli ya kati ni kutoa usafiri wa kuaminika na kukuza upatikanaji wa huduma bora nchini na maboresho hayo yatasaidia kuinua uwezo wa kubeba mzigo toka tani 13.5 za uzito wa ekseli hadi tani 18.5.

  Mhandisi Singo amesema maboresho hayo yataenda sambamba na kutandika upya njia za reli zenye uzani wa paundi 80 kwa urefu wa kilometa 312, kufanya ukarabati wa njia ya reli iliyosalia kwa urefu wa kilometa 658 na kufanya ukarabati wa makaravati na madaraja 442.Pia kuboresha mfumo wa mawasiliano , kuboresha vituo vya kupakia na kupakua mizigo vya bandari ya Dar es Salaam ,Ilala na Bandari kavu ya Isaka.

  Amesema kuwa katika maboresho hayo wamejipanga kuboresha na kuongeza kiwango cha ubebaji mizigo kwa miundombinu ya reli na madaraja na kuongeza mwendokasi wa treni kutoka kilometa 35 kwa saa hadi kufikia kilometa 70 kwa saa.Ameongeza kupitia mradi huo TRC pia imetengeneza mpango endelevu wa matengenezo ya miundombinu ili kufanya njia ya huo kuwa wa uhakika na kuaminika.

  “Kuimarika kwa usafiri wa reli kutapunguza gharama za matengenezo ya barabara na hivyo Serikali kuendeleza bajeti iliyookolewa kwenda kwenye huduma nyingine za kijamii.Mhandisi Singo amesema lengo lao pia ni kupunguza gharama na muda wa usafiri wa mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi bandari kavu ya Isaka hadi kufikia saa 24 kutoka zaidi ya saa 36 ya sasa.

  Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa TRC Jamila Mbarouk amewataka Watanzania kuhakikisha wanakuwa walinzi wa miundombinu ya reli na kufafanua kuna baadhi ya wananchi wamekuwa wakiharibu miundombinu na kufanya hujuma ikiwamo ya kuiba kokoto.Pia amesma ni marufuku kufanya biashara pembezoni mwa reli na kwamba anayateka kufanya biashara pembeni ya reli itawezekana pale tu atakapopata kibali maalumu.

  Mbarouk amesema ni marufu kupitisha mifugo kwenye reli na kueleza dhamira ya TRC ni kuona wananchi wananufaka na mradi huo na hakuna madhara yanayoweza kutokea.

  Mratibu wa Uboreshaji wa reli ya kati Mhandisi Mlemba Singo akizungumza na waandishi wa habari katika banda la TRC lililopo kwenye maonesho ya bishara yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam leo kuhusu uboreshaji wa Reli ya kati.
  Mratibu wa Uboreshaji wa reli ya kati Mhandisi Mlemba Singo akimsikiliza  Meneja Mawasiliano wa TRC Jamila Mbarouk wakati alipokua akifafanua jambo katika banda la TRC lililopo kwenye maonesho ya bishara yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam.

  0 0
 • 07/02/18--08:15: TAARIFA KWA UMMA


 • 0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Makame Mnyaa Mbarawa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Eng. Isack Kamwelwe kuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Eng. Isack Kamwelwe kuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Jacob Kingu kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kailima Ramadhani kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Thomas Mihayo kuwa Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Omar Ramandani Mapuri kuwa Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Viongozi mbalimbali walioapishwa wakila Kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Viongozi mbalimbali walioapishwa wakitia saini viapo vyao vya maadili kwa Viongozi wa Umma mara baada ya kuapa.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Moses Kusiluka kuwa Katibu Mkuu Ikulu. PICHA NA IKULU


  0 0  Na Hamza Temba, Songwe
  ....................................................................
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa miezi mitatu kwa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kufanya utafiti na sensa ya mamba katika ziwa Rukwa ili kubaini idadi yake na hatimaye kuishauri Serikali namna ya kudhibiti madhara yanayosababishwa na mamba hao kwa wananchi hususan wa jimbo la Songwe ikiwemo kuwavuna kama idadi yao itabainika kuwa kubwa kupita kiasi.

  Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana katika kijiji cha Maleza, kata ya Mbangala, wilaya ya Songwe mkoani Songwe alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kwa ajili ya kutatua mgogoro uliopo baina ya wananchi na Mamba wa ziwa Rukwa.

  "Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori ambayo ipo chini ya wizara yangu, nawaagiza wafike hapa mara moja, ndani ya miezi mitatu wanipe majibu nini kifanyike kupunguza madhara yanayotokana na mamba kwenye ziwa Rukwa, wafanye sensa watuambie kuna Mamba wangapi lakini pia watushauri nini tufanye ili kudhibiti mamba hao wasiendelee kusababiaha athari kubwa kwenye maisha ya watu wanaoishi jirani, lakini pia wanaoutumia ziwa.

  "Kwa sababu madhara yanaweza yakawa mengi, inawezekana mamba wameshakuwa wengi na samaki wamebaki wachache, kwahivyo hata mamba nao mwishowe wataanza kufa ama wataanza kutafuta chanzo kingine cha chakula pengine ndio maana wameanza kutafuta binadamu wanakwenda ziwani kwasababu wanakuwa na njaa, inabidi wasogee ufukweni wawinde chochote kinachosogea karibu na maji" alifafanua Dk. Kigwangalla. 

  Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo kufuatia malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa kwake na mbunge wa Jimbo la Songwe, Phillipo Mulugo ambaye amesema kumekuwepo na matukio mengi ya mamba kushambulia na kuuwa wananchi wa vijiji jirani wanaofata huduma mwambao wa ziwa Rukwa. 

  Katika hatua nyingine Dk. Kigwangalla ametoa miezi mitatu kwa Wakala wa Huduma za misitu Tanzania kuandaa mpango wa kitaifa kwa kila wilaya na vijiji nchini utakaoweka utaratibu maalum wa namna na sehemu wananchi watakayopata huduma ya kuni mkaa.

  "Utaratibu uwekwe na muuweke nchi nzima, kila wilaya, kila kata, kila kijiji uwekwe utaratibu wananchi watapata wapi mkaa, watapata wapi kuni, kibali cha kuvuna kitapatikana wapi, utaratibu uwe wazi, sio kusubiri kwenye mageti unakamata, hapana weka utaratibu kwanza, ukishaweka utaratibu atakayevunja sheria hata ukimkamata ukimpeleka polisi utakuwa umemrahisishia OCD kazi. 

  "Kwa sababu hata OCD atakuwa anajua kwamba katika hii wilaya ninayoiongoza hapa ndio mipaka ya mkaa, hapa ni mipaka ya kuni, wewe umetoa wapi, kibali chako kiko wapi, umevunja sheria, mahakamani" ameeleza Dk. Kigwangalla. 

  Wakati huo huo, Dk. Kigwangalla ametangaza kutaifishwa kwa greda ambalo limekutwa likiwa limetelekezwa na watu wasiojulikana ambao walikuwa wakichimba mchanga wa dhahabu (makinikia) kinyume cha sheria ndani ya Hifadhi ya msitu wa Patamela wakati wa ziara yake wilayani Songwe.

  Kufuatia tukio hilo, amemuagiza Kamanda wa Polisi wa wilaya hiyo kulinda eneo hilo na kutafuta dereva atakayeendesha greda hilo hadi kituo cha polisi kwa ajili ya kufuata taratibu za sheria za kulitaifisha na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Maleza kata ya Mbangala wilaya ya Songwe mkoani Songwe alipofanya ziara ya kikazi katika kijiji hicho jana kwa ajili ya kutatua mgogoro wa mamba wa ziwa Rukwa ambao wamekuwa wakidhiru wananchi wa kijiji hicho na vijiji jirani.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akitoa agizo la kutaifishwa kwa greda (pichani nyuma) lililokutwa ndani Hifadhi ya Msitu wa Patamela baada ya kutelekezwa na watu watu wasiojulikana waliokuwa wakichimba mchanga wa dhahabu (makinikia) kinyume cha sheria ndani ya Hifadhi hiyo katika wilaya ya Songwe mkoani Songwe jana.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akitoa maelekezo kwa uongozi wa wilaya ya Songwe kufuatia greda lililokutwa ndani Hifadhi ya Msitu wa Patamela ambalo limetelekezwa na watu wasiojulikana waliokuwa wakichimba mchanga wa dhahabu (makinikia) kinyume cha sheria ndani ya Hifadhi hiyo katika wilaya ya Songwe mkoani Songwe jana.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akishirikiana na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Songwe kuzima moto uliokutwa ukiwaka ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Patamela wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo jana.
  Dk Hamisi Kigwangalla akishirikiana na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Songwe kuzima moto uliokutwa ukiwaka ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Patamela wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo jana.
  Juhudi za kuzima moto zikiwa zinaendela.
  Dk Kigwangalla akiwa anazungumza na wananchi wa kijiji Maleza.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Songwe, Philipo Mulugo alipokuwa akiwasilisha malalamiko ya wananchi wa jimbo lake ambao wamekuwa wakipata madhara makubwa ya mamba wa ziwa Rukwa.

  0 0

  Na Humphrey Shao , Globu ya Jamii

  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako leo amefungua Mkutano wa sita wa kisayansi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es Salaam huku akitoa wito kwa taasisi za elimu ya afya na mashirika mbalimbali yanayofanya tafiti za afya hapa nchini kuhakikisha tafiti hizo zinafika kwa wadau na wananchi.

  “Kwa sasa tunaelekea kwenye uchumi wa viwanda na miongoni mwa sekta muhimu ambazo pia zinatarajia wawekezaji ni pamoja na sekta ya afya hivyo basi muelekeo na mapendekezo ya tafiti za afya ndio zitakazoweza kuwasaidia wadau na serikali kufahamu aina ya ukwekezaji huo pamoja na maeneo gani yanafaa kulingana na mahitaji.”Alibainisha.

  Aliongeza kuwa Serikali kwa kiasi kikubwa inajitahidi kutumia tafiti hizo katika kuandaa sera mbalimbali zinazohusiana na masuala ya afya huku akitoa pongezi kwa uongozi wa chuo hicho kwa kuendelea kuandaa wataalamu wanaoandaa tafiti hizo kwa weledi na ufanisi mkubwa.

  Awali, akizungumza kwenye hafla hiyo Makamu Mkuu wa MUHAS, Prof. Prof Andrew Pembe alisema nyingi kati ya tafiti zitazowasilishwa kwenye mkutano huo wa siku mbili zitajikita katika vipaumbele vya taifa yakiwemo masuala ya HIV/AIDS, kifua kikuu, afya ya uzazi na mtoto, magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ajali pamoja na magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika.

  “Zaidi umuhimu wa mkutano huu ni kuwa unawakutanisha wataalamu wa afya tena katika ngazi tofauti wakiwemo wale waliobobea pamoja na wanafunzi na hivyo kuwa kama jukwaa kwa wao kuweza kubadilishana ujuzi. Zaidi ya tafiti tofauti 200 zitawasilishwa kupitia mkutano huu’’ alisema.

  Aliishukuru serikali ya Sweden kupitia Shirika la Sida ambao kwa kushirikiana na wadau wengine wamewezesha mkutano huo.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako (kulia) akizungumza wakati akifungua Mkutano wa sita wa kisayansi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es Salaam
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako (kulia) akizungumza wakati akifungua Mkutano wa sita wa kisayansi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es Salaam
  Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakisikiliza kwa umakini hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako wakati akifungua mkutano huo.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano hilo

  0 0


  Afisa Mwandamizi wa Uchambuzi wa Mifumo ya Biashara wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Bw. Mathias Chanila akimhudumia mwananchi aliyetembelea Banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa Huduma kwa Mlipakodi ambaye pia ni Mratibu wa Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba kwa upande wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Honester Ndunguru (kushoto) akiwaelezea Maafisa wa SIDO haki na wajibu wa Mlipakodi kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Huduma na Mlipakodi wakati walipotembelea Banda la TRA kwenye Maonyesho hayo yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Afisa Elimu na Huduma kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi Temeke Bw. Paul Maghembe akimhudumia mwananchi aliyetembelea Banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Afisa wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi Temeke Bi. Jacqueline Fairom akimhudumia mwananchi aliyetembelea Banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

  0 0

  ·       Sasa wataweza kutuma na kupokea pesa kutoka mitandao mingine.
   Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel imeondoa gharama za kutuma pesa kwa wateja wanaotumia huduma ya kifedha ya Halopesa, na hivi sasa wataweza kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa, huku pia ikipunguza gharama za kutuma fedha kutoka Halopesa kwenda mitandao mingine.
  Kuondolewa kwa makato hayo inatafsiriwa na kampuni hiyo kama njia pekee ya kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa mamilioni ya Watanzania ambao wanatumia huduma za kifedha kwa njia ya simu.
  Mkurugenzi wa Kitengo cha Halopesa, Vu Tuan Long, amesema kuwa kuondolewa kwa gharama hizo kutawezesha wateja wa mtandao huo hasa walioko katika maeneo ya vijijini kuweza kufanya miamala ya simu na kuondokana na usumbufu ambao wangeweza kuepuka kwa kutumia njia nyingine kutuma fedha ili kuokoa gharama za makato ya kufanya miamala.
  “Tuna mamilioni ya watanzania ambao kwa mara ya kwanza walipata mawasiliano ya simu tulipoanzisha huduma zetu, na baada ya kuanzishwa kwa huduma ya Halopesa kwa miaka miwili sasa wateja wetu katika maeneo mbalimbali wanaweza kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa,” Alisema Long na kuongeza.
  “Hii ni hatua nyingine ya kuhakikisha kwamba wateja wanakuwa na wigo mkubwa wa kuweza kukidhi mahitaji yao katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, na kijamii kupitia huduma ya kifedha ya mtandao kwa ubora, ukaribu, uhakika  na usalama zaidi na kuepuka kwenda umbali mrefu kwaajili ya kufuata huduma za kifedha kupitia benki”. Aliongeza Long.
  Aidha Mkurugenzi huyo, alibainisha kuwa, licha ya kuondoa gharama katika kutuma fedha, huduma ya kutuma fedha kutoka Halopesa kwenda mitandao mingine imepunguzwa gharama ili iwe rahisi zaidi kwa wateja wanaotuma pesa kwenda mitandao mingine ya simu pia waweze kutuma pesa kwa gharama nafuu.
  “Habari njema tuliyonayo kwa wateja wetu ni kuwezeshwa kwa huduma ya Halopesa kuweza kutuma pesa kwenda mitandao yote, sasa wateja wetu wataweza kutuma pesa kwenda mitandao mingine kwa gharama nafuu zaidi kabisa,” Alihitimisha Long
  Tangu kuanzishwa kwa huduma ya Halopesa tayari Mawakala Zaidi ya elfu 55,000 tayari wamejisajili na wanatoa huduma kwa zaidi ya wateja milioni moja na nusu walioenea nchi nzima.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Nguyen Van Son pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo,Mhina Semwenda wakifungua shampeni kuashiria uzinduzi wa huduma ya wateja wa Halopesa kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa, wanaoshuhudia ni Mkuu wa kitengo cah Halopesa Vu Tuan Longa (Kulia) na Meneja biashara wa Halopesa Magesa Wandwi (Kushoto). 
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Van Nguyen Son pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo,Mhina Semwenda wakishika glasi za shampeni katika uzinduzi wa huduma ya wateja wa Halopesa itakao wawezesha kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa, wanaoshuhudia ni Mkuu wa kitengo cah Halopesa Vu Tuan Longa (Kulia) na Meneja biashara wa Halopesa Magesa Wandwi (Kushoto).
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Van Nguyen Son pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo,Mhina Semwenda pamoja wa wafanyakazi wengine wa Halotel wakigonga glass za shampeni kuashiria uzinduzi wa huduma ya wateja wa Halopesa itakao wawezesha kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa, wanaoshuhudia ni Mkuu wa kitengo cah Halopesa Vu Tuan Longa (Kulia) na Meneja biashara wa Halopesa Magesa Wandwi (Kushoto).


  0 0

  Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) inayoongozwa na Mwenyekiti Prof. John Kondoro imeshiriki mafunzo ya siku mbili ya uongozi kwa wajumbe wa Bodi (Board Leadership Training) yalioandaliwa na Menejimenti ya shirika la Reli na kuratibiwa na Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (Institute of Directors in Tanzania) kuanzia tarehe 2 - 3 Juni katika ukumbi wa Bodi, jengo la LAPF jijini Dodoma.

  Lengo la kuandaa mafunzo ni kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi katika shughuli za uendeshaji wa Shirika. Bodi ya Shirika la Reli Tanzania imeundwa na wajumbe nane (8) wenye ujuzi mbalimbali kwa kufuata sheria mpya ya Reli namba 10 ya Mwaka 2017. Bodi ya Shirika la Reli ilizinduliwa rasmi tarehe 11 mwezi Juni 2018 na aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.

  Wajumbe.

  1. Prof. John Kondoro-Mwenyekiti
  2. Eng. Karim Mattaka-Mjumbe
  3. Dkt. Jabiri Bakari-Mjumbe
  4. Masanja Kadogosa-Katibu wa bodi
  5. Eng. Rogers Mativila
  6. Rukia Shamte-Mjumbe
  7. Edson Mweyunge-Mjumbe
  8. Wolfgang Ephraim Salia-Mjumbe 9. MahamudMabuyu-Mjumbe


  Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kadogosa akitoa mfano alipokuwa akifafanua jambo walilokuwa wakijadili katika mafunzo ya wajumbe wa Bodi mpya ya TRC yaliyofanyika jijini Dodoma, tarehe 2 Juni 2018.
  Katibu wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Ndg. Masanja Kadogosa akiwakaribisha wajumbe wa Bodi mpya ya TRC wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na menejimenti ya TRC.
  Mjumbe wa Bodi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (wa kwanza kulia) Eng. Mattaka akielezea jambo kwa kina huku mwenyekiti Prof. Kondoro na mwezeshaji Ndugu Said Kambi wakifuatilia kwa makini.

  Dr. Jabiri Bakari (katikati) akielezea jambo kwa msisitizo wakati wa mafunzo ya wajumbe wa Bodi ya TRC yaliyoandaliwa na menejimenti ya Shirika la Reli Tanzania na kufanyika jijini Dodoma.
  Picha ya pamoja ya wajumbe wa Bodi mpya ya Shirika la Reli Tanzania, waratibu kutoka Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania na Sektretarieti ya Shirika la Reli Tanzania katika jengo la LAPF jijini Dodoma.

  0 0


  SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limedhamiria kutoa mikopo ya riba nafuu kwa sekta isiyo rasmi wakiwamo wajasiriamali, waendesha bodaboda, mamalishe, wakulima, wavuvi na wote waliojiunga kwenye vikundi rasmi vya uzalishaji mali kama VIBINDO, AMCOS, VICOBA na  SACCOS  

  Akizunngumza leo kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendeelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam ,Kaimu Meneja na Uhusiano wa NSSF Salim Khalfan amewaambia waandishi kuwa NSSF imedhamiria kuinua maisha ya Watanzania kwa kupitia fursa hii ya mikopo ambayo itawawezesha katika kufanya maendeleo yao ya sasa na baadae.

  Amesema wafaidika na mikopo hii ni wale ambao wamejiunga tayari kwenye vikundi mbali mbali ambavyo tayari vimesajiliwa na kutambulika vitawezeshwa kuweza kupata mikopo hii kupitia katika benki ya AZANIA.

  Hii ni fursa pekee kwa wale ambao wako kwenye sekta isiyorasmi kuweza kujikwamua kiuchumi kupitia mikopo ya riba nafuu. Shirika la Taifa Hifadhi za jamii (NSSF) linatoa mkopo huo kwa walengwa wenye masharti na fuu na riba ndogo ya kiasi cha asilimia 12.5 ambapo kwa mtu wa kawaida anaweza kukopa na kufanyia maendeleo yoyote.

  Pia mbali na wananchi waliopo kwenye sekta isiyo rasmi pia hata wananchi waliopo kwenye sekta iliyorasmi nao wananafasi ya kupata mkopo kupitia vyama vyao vya ushirika. Mbali na mikopo hiyo, wanachama watapata mafao yote sita yanayotolewa na NSSF yakiwemo matibabu bure kwa mwanachama na wategemezi wake wanne, mafao ya uzazi ambapo mwanachama mwanamke atapata asilimia 300 ya kipato chake cha mwezi pale mwanachama anapokuwa ameka akiba kwa muda wa miezi 36.

  Vile vile mwanachama atapata mafao ya uzeeni pale atakapokuwa amefikisha umri wa miaka 55-60 na mwanachama awe ameshachangia angalau miezi 180. Pamoja na hayo mwanachama atapata mafao ya ulemamu pale itakapothibitika kwamba amepoteza uwezo wake wa kufanya kazi, mafao ya urithi kwa wategemezi wa mwanachama pindi mwanachama atakapofariki pamoja na msaada wa mazishi kwa mwanachama .


  Waaandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyarara alipozungumza nao leo kuhusu dhamira ya Shirika hilo kutoa Mikopo ya Riba nafuu kwa sekta isiyo rasmi kama vile wajasiliamali,waendesha boda boda,Mamalishe,Wakulima,Wavuvi na wote waliojiunga kwenye vikundi rasmi vya uzalishaji mali kama AMCOS,VICOBA  pamoja na SACCOS, ndani ya Banda la Shirika hilo
   katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyarara akitoa ufafanuzi wa shughuli mbalimbali zitolewazo na shirika hilo mapema leo mbele ya Waaandishi wa Habari (hawapo pichani) wndani ya Banda la Shirika hilo 
  katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

older | 1 | .... | 1611 | 1612 | (Page 1613) | 1614 | 1615 | .... | 1898 | newer