Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 159 | 160 | (Page 161) | 162 | 163 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmmbando (kushoto)  akiongea na wanahabari kabla ya kukabidhi cheti Mshindi wa Nyumba ya pili ya  Airtel Yatosha Anna G. Lyimo (kati) 
   Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmmbando (kushoto)  akimkabidhi cheti Mshindi wa Nyumba wa Airtel Yatosha bi. Anna G.Lyimo mkazi (kulia) wa  Dar Es Salaam  akishuhudiwa na Meneja masoko wa Airtel Tanzania Anethy Muga.


  Mshindi wa Nyumba wa pili wa Airtel Yatosha  bi. Anna G. Lyimo akionyesha cheti chake alichokabidhiwa na Meneja wa uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando (kulia), wakishuhudiwa na Meneja masoko wa Airtel Anethy Muga (kushoto).
   Wanahabari wakirekodi tukio wakati Anna G. Lyimo anakabidhiwa cheti chake cha nyumba leo jijini Dar es salaam.
  ========  =====  =======


  Mshindi wa nyumba ya pili ya Airtel Yatosha yenye thamani ya shilingi milioni 65/- amekabidhiwa cheti cha ushindi leo ikiwa ni uthibitisho maalum mbele ya wanahabari ambapo ni muda mfupi baada ya mshindi huyo kuibuka mshindi kupitia droo kubwa ya mwisho wa mwezi iliyochezeshwa wiki iliyopita Airtel Tanzania kupitia promosheni hiyo imekuwa ikitoa zawadi mbalimbali kwa wateja wake zikiwemo pesa taslim pamoja na nyumba 3 ambapo kila mwezi nyumba moja huenda kwa mshindi mmoja .

  Akizungumza kwa furaha Mshindi wa nyumba hiyo ya pili Bi Anna Gustav Lyimo ambae ni mkazi wa Dar es salaam alisema “namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kuwa mshindi wa nyumba ya Airtel Yatosha, Nilipopigiwa nilijua ni matapeli, mpaka siku ya pili nilipopigiwa kwa mara ya pili na Airtel ndipo nilipojua si utapeli” “Nawashukuru sana Airtel kwa zawadi hii kwani imenirahisishia mipango yangu ya kuanza ujenzi wa Nyumba mwishoni mwa mwaka huu. ,” alisisitiza Bi, Lyimo “Ninawashauri wateja wengine wa airtel kuendela kutumia huduma ya Airtel yatosha ili na wao waibuke washindi kama mimi” alimalizia kusema Bi Anna Lymo .

  Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando alisema “makabidhiano ya cheti hiki ni taratibu za awali ambapo hivi karibuni mshindi huyu atakabidhiwa rasmi nyumba yake iliyopo maeneo ya Kigamboni jijini Dar es salaam. “Airtel tutaendelea kutoa zawadi bora kwa wateja wetu nchi nzima kupitia promosheni mbalimbali tulizonato” 

  “Kama alivyo na furaha mshindi wetu ndivyo na sisi tunavyofurahi na hii sio kikomo bado tunatoa zawadi za pesa taslim kila siku kwa wateja mbalimbali wa Airtel nchi nzima. Njia ni rahisi tu! Jiunge sasa na vifurushi mbalimbali vinavyopatikana kupitia Yatosha na utapata nafasi ya kuingia kwenye droo ya kushinda,” alisema Mmbando.
  Kujiunga na vifurushi hivyo mteja anapaswa kupiga *149*99# na kuchagua 1 au 2 kisha aweze kujiunga na kifurushi chochote cha Wiki, Siku au Mwenzi. Airtel kupitia promosheni ya Airtel yatosha imeshatoa zaidi ya shilingi milioni 60 kwa wateja wake kupitia promosheni hii ambapo Promosheni hii inadumu kwa siku 90 toka ianze, hadi sasa bado kuna nyumba moja kati ya tatu zilizopo Kigamboni itashindaniwa kwa mwezi huu.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Sixtus Mapunda, leo amekutana na wazee waasisi wa Jumuia hiyo, Ofisini kwake, Makao Makuu ya UVCCM, Barabara ya Morogoro, jijini Dar es Salaam. na kuwa na mazungumzo ya kina na waasisi hao.Pichani, Mapundfa (kushoto) akiwasikiliza waasisi hao. Wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM, Mfaume Ally Kizigo. (Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0

   Rais Mh.  Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi mpya  Dkt. Luigi Scotto (Kulia) kutoka Italia  katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu- Dar es Salaam..
   Rais Mh. Dkt, Jakaya Kikwete (kulia) akizungumza na Balozi mpya anaewakilisha nchi ya  Italia nchini Tanzania Balozi  Dkt. Luigi Scotto( kushoto) leo Ikulu Dar es Salaam.
   Rais  Mh.Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) akisikiliza taarifa ya utambulisho kutoka kwa  Balozi  mpya wa Italia nchini Tanzania Mh, Dkt. Luigi  Scotto (kulia) leo  Ikulu Dar es Salaam.
  Balozi mpya wa Italia nchini Tanzania Mh. Dkt. Luigi Scotto akisaini kitabu cha wageni leo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokwenda kuwasilisha hati za utambulisho kwa Mh, Rais Dkt. Jakaya Kikwete(hayupo pichani). 
  Bolozi mpya wa Italia nchini Tanzania Mh. Dkt, Luigi Scotto (kulia) akisalimiana na baadhi ya maafisa  kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, leo katika hafla hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Balozi mpya anaewakilisha nchi ya Italia nchini Tanzania Dkt, Luigi Scotto (katikati waliovaa suti) pamoja na maafisa wakuu wa Itifaki wakiwa katika wimbo wa taifa.leo katika hafla hiyo ya utambulisho Ikulu Dar es Salaam. Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akijaribu kuendesha gari maalum ya kuinulia mizigo huku akipata maelezo kutoka kwa Balozi wa China nchini Lu Youqinq alipotembelea kiwanda cha nguo cha Dahong Textile kinachojengwa mkoa wa Shinyanga.
   Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Balozi wa China nchini Lu Youqinq kuhusu mipango ya China katika kuwekeza Tanzania.Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman leo ametembelea vkiwanda cha nguo cha Dahong Textile kilichopo Shinyanga. 
  Balozi wa China nchini Lu Youqinq akimkabidhi zawadi Laptop Katibu wa CCM wa Wilaya ya Shinyanga Charles Charles .
  Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa China nchini Lu Youqinq na wawekezaji baada ya kumaliza kukagua maendeleo ya viwanda hivyo ambavyo vitaajiri maelfu ya Watanzania mara vitakapokamilika..Picha na Adam Mzee

  0 0

  Press Release 1IMG_5989
  Sheria Ngowi Company Limited, Assistant Director and Marketing Manager, Mr Deogratius Kessy (centre) elaborate a point to reporters not in picture about the invitation of Sheria Ngowi to the New York Fashion Week Show this week. Right is Communication Manager Miss Julda Makundi and left is Jesca Ngowi who is also a designer for the women clothes.
  IMG_6005
  Assistant Director and Marketing Manager, Mr Deogratius Kessy (right) from Sheria Ngowi Company Ltd displays a bronchure of fashion and design which was created and designed by their company which shows some of the new collections. Left Ms Jesca Ngowi.


  IMG_6036
  Jesca Ngowi a designer specialized in women clothes stresses a point and sharing her experience in fashion and design industry.
  IMG_6089
  Communication Manager Miss Julda Makundi from Sheria Ngowi Company Ltd emphasis a point when speaking to reporters during a news conference at Habari Maelezo.
  IMG_5972
  Sheria Ngowi Company Limited, Assistant Director and Marketing Manager, Mr Deogratius Kessy (centre) responding questions to reporters.
  IMG_6013
  A cross section of journalist and other participants who attended the press conference in Dar es Salaam which was organized by Sheria Ngowi Company Ltd who is popular and young designer who is attending the New York Fashion Week Show in US.

  By Special Correspondent.
  Popular Tanzanian fashion designer Sheria Ngowi, plans to build a modern textile manufacturing plant which is current based in Bangalore, India as part of his efforts to foster the development of fashion and design industry in the country.

  Speaking to reporters in a news conference in Dar es Salaam yesterday, Sheria Ngowi Company, Assistant Director and Marketing Manager Deogratius Kessy said that the firm plans to build a modern manufacturing plant that would create employment opportunities to Tanzanian youths.

  “A modern manufacturing plant would be a solution for those Tanzanians who always travel to abroad for shopping because it will reduce the cost and time spent in the queue at the various international airports,” he said.

  Kessy underscored that the Sheria Ngowi firm will also provides their services in neighboring countries such as South Africa, Nigeria, DRC Congo and Kenya at the popular city of Nairobi.
  He said Sheria Ngowi, who recently opened his flagship store in Tanzania, is known for his custom tailored suits, using only superior fabrics, meticulous hand tailoring, and quality that is hard to find. “No one tells an authentic African story better that Africans themselves, through my designs the west and the east merge to create a beautiful journey of various culture and heritage,” he explained.

  Having studies Law Ngowi’s sentrance into design is not an accident but a choice made due to an unwavering obsession with fashion and a keen awareness of its power.
  Shy and humble by nature, Sheria is uncomfortable speaking about himself and what he has achieved. That said, the honor of being able to showcase in New York during fashion week does not go unnoticed.

  Sheria Ngowi, who recently opened his flagship store in the country, has been invited to attend New York Fashion Week show and become the first Tanzanian designer to attend in the history of fashion and design industry.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi katika uzinduzi wa mradi wa vibanda vya biashara katika uwanja wa Kambarage huku akishuhudiwa na Balozi wa China nchini Dr.Lu Youqinq.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka kwa baiskeli kutoka Uwanja wa Kambarage kuelekea uwanja wa Shycom kwenye mkutano wa hadhara.
   Balozi wa China nchini Dk.Lu Youqinq akiwapungia wananchi wakati akielekea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Shycom,Shinyanga mjini.
   Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Balozi wa China nchini wakiwasubiri wenzao tayari kuelekea kwenye uwanja wa Shycom ambapo mkutano mkubwa ulifanyika.
   Kutoka kushoto ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Balozi wa China nchini na Mbunge wa Shinyanga mjini Steven Masele wakiendesha baiskeli kuelekea kwenye uwanja wa Shycom ambapo mkutano mkubwa na wa kihistoria ulifanyika leo tarehe 13 Septemba 2013.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiingia kwenye uwanja wa Shycom na baiskeli tayari kuhutubia kwenye mkutano wa hadhara.


   Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto),Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqinq na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye , Balozi wa China alipata fursa ya kuelezea kwa wananchi wa Shinyanga namna uwekezaji utaweza kuunufaisha mkoa huo ambapo viwanda vya nguo, kusindika mafuta, asali na bidhaa zitokanazo na mifugo vinategemewa kujengwa katika mkuo huo na kutoa nafasi kwa ajira ,kuinua uchumi ,elimu na kuondoa kabisa umasikini.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini katika mkutano wa hadhara uliofanyiaka kwenye uwanja wa Shycom mkoani Shinyanga.
   Mbunge wa Shinyanga mjini Ndugu Steven Masele akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini na kuwaambia yeye anachofanya ni kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM na kwake maendeleo kwa wana Shinyanga ndio kitu cha msingi.
   MNEC wa Wilaya ya Shinyanga mjini Ndugu Gasper Kileo akihutubia wakazi wa Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shycom,mkoani Shinyanga leo.
   Mbunge wa Viti maalum kupitia UWT Shinyanga Ndugu Lucy Mayenga akiwahutubia wakazi wa Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu alikuwa anahitimisha ziara yake mkoani hapo.
   Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Ndugu Azah Hilal Hamad akiwasalimu wakazi wa Shinyanga mjini wakati wa kuhitimisha ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini  ambapo aliwaasa wananchi waepuke 'makanjanja wa siasa' na badala yake washirikiane na viongozi wao katika kuleta maendeleo.
   Umati wa watu uliofurika wakati wa mkutano wa mwisho wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye viwanja vya Shycom.
   Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisoma vijiji vitavyofaidika na mradi wa umeme vijijini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shycom leo tarehe 13 Septemba 2013.
   Mbunge wa Kishapu akiruka kwa furaha baada ya kusikia vijiji vya wilaya yake vitafaidika na mradi wa umeme wa vijiji.
   Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akijaribu pikipiki mpya watakazopewa makatibu kata wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini.
  Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiondoka uwanja wa Shycom baada ya kumaliza mkutano wenye mafanikio makubwa kwa wakazi wa Shinyanga kwani walipata fursa ya kutambua namna mkoa wao utakavyobadilika ndani ya miaka 10 ijayo kwani wawekezaji wa kutoka China wameanza kuwekeza viwanda amabavyo vitatoa ajira za kutosha, kuinua uchumi kwa wakulima na pia kutoa elimu ya kilimo na teknolojia.

  0 0

   Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) akiongozana na baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Tabora,wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Tabora Mjini,mchana wa leo Septemba 13,2013.
   Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM Wilaya ya Tabora waliofika kumlaki alipokuwa akiwasili Mkoani Tabora mchana wa leo Septemba 13,2013.
   Msafara wa Pikipiki (maarufu kama Boda Boda) Mkoani Tabora ukiwa barabarani wakati wa kumpokea Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa alipokuwa akiwasili Mkoani Tabora leo,ambapo alitembelea Ofisi za Chama cha Waendesha Pikipiki (Bodaboda) Mkoani Tabora.
   Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na baadhi ya wanachama wa Chama cha Waendesha Pikipiki (Bodaboda) Mkoani Tabora wakati alipokitembelea Chama hicho jioni ya leo Septemba 13,2013.Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama hicho,Waziri Kipusi.
   Mwenyekiti wa Chama Waendesha Pikipiki (Bodaboda) Mkoani Tabora,Waziri Kipusi (kushoto) akisoma taarifa fupi mbele ya Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa juu ya mwenyendo wa Chama hicho pamoja na malengo yake.ambapo Mh. Lowassa ameahidi kuwapatia pikipiki tatu,ikiwa ni sehemu ya mchango wake kwenye Chama hicho.

   Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza machache kwenye mkutano wake ya Waendesha Boda Boda wa Mkoa wa Tabora.


   Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza jambo na Watoto waliojitokeza kumsalimia wakati alipokuwa akiwasili Mkoani Tabora leo,Septemba 13,2013.
   Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akifurahia jambo na Watoto Chipukizi waliokuwepo nje ya Ofisi za CCM Wilaya ya Tabora Mjini.
   Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (mwenye kipaza sauti) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wanafunzi wa Vyo mbali mbali Mkoani Tabora,waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Ukumbi wa Chuo cha Utumishi,Mkoani Tabora leo Septemba 13,2013.
   Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Tabora Mjini,Seif Gulamali akizungumza machache mbele ya Wanafunzi wa Vyuo mbali mbali Mkoani Tabora leo.
   Mbunge wa Jimbo la Urambo,Mh. Athuman Kapuya akijibu moja ya Maswali yaliyokuwa yakiulizwa na Wanafunzi hao wa Vyuo mbali mbali Mkoani Tabora waliokuwa wamefurika kwa wingi ndani ya Ukumbi wa Chuo cha Utumishi Mkoani humo,kumsikiliza Mh. Lowassa.
   Baadhi ya wanafunzi hao kutoka Vyuo mbali mbali Mkoani Tabora,wakiuliza maswali.


  0 0


  TAMASHA Kubwa la Filamu litakaloandika historia ya tasnia ya filamu Tanzania la Dar Filamu Festival (DFF 2013) linamtambulisha Elizabeth Michael kama Official Actress for DFF 2013/14 katika muonekano mpya akiwa kama balozi wetu wa kwanza kutambulishwa kutoka DFF, alafu utapata muonekano wa Official Director/ Producer DFF 2013/2014 Vincent Kigosi ‘Ray the Greatest’.  Dar Filamu Festival 2013 awali ilitambulishwa kwa wadau na wanahabari wiki iliyopita na sasa tupo katika hatua nyingine ya kuwatangaza na kuwapa majukumu mabalozi wetu ambao ni Ray na Lulu katika kuhakikisha kampeni ya kupenda filamu za Kiswahili na kuzipa thamani zinafanikiwa na kuwa ni soko lenye nguvu zaidi katika tasnia ya filamu Ulimwenguni.  Tamasha la Dar Filamu Festival (DFF 2013) litafanyika katika viwanja vya CoICT- UDSM- Kijitonyama kuanzia tarehe 24 hadi 26 Septemba 2013, filamu za Kitanzania kama ufunguzi wa tamasha hilo zitaonyeshwa kwa kiingilio cha Bure kabisa  kiingilio chako ni kufika katika viwanja vya Posta pale Kijitonyama na kushuhudia filamu kutoka kwa wakali wa filamu Bongo Movie.


  Sasa ni zamu yako kukutana na Lulu kisha kuongea naye kuhusu filamu na soko jipya la Filamu,  kupitia Projector kubwa  na kuona filamu kwa uzuri zaidi huku ukiburudika kwa kazi nzuri kutoka nyumbani.


  0 0
 • 09/13/13--13:54: Article 9

 • 0 0

   Mmoja wa wasanii wanaokuja kwa kasi kwenye anga ya muziki wa Bongofleva a.k.a hip hop,Stamina akiwaimbisha wakazi wa Dodoma na vitongoji vyake waliojitokeza kwa wingi usiku huu ndani ya uwanja wa Jamuhuri,wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea.
   Msanii mahiri ambaye kwa sasa anasumbua vilivyo anga ya muziki wa Bongofleva,Diamond akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013,linalofanyika usiku huu kwenye uwanja wa Jamuhuri.
  Haaaa haaaa...ukitaka kubana pua kabane nyumbani kwenu,hapa ni hip hop tuuu.....Msanii wa Bongofleva Ney wa Mitego wakioneshana umahiri umwamba wa jukwaani na msanii mwenzake  Dimond  kupitia wimbo wa Muziki Gani.
   Sehemu ya mashabiki wakishangweka vilivyo usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
  Mmoja wa wakongwe wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Wateule Skwadi,atambulikae kwa jia la kisanii Mchizi Mox akiimba jukwaani usiku huu.  
  Maelfu ya Watu wakiwa kwenye uwanja wa jamuhuri,usiku huu wakishangweka na tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
  Mkali mwingine wa Bongofleva,Dullysykes akiimba jukwaani usiku huu wakati tamasha la Serengeti fiesta likiendelea.
   Young Killer na Stamina  kama kawaida yao wakilishambulia jukwaa la fiesta usiku huu,huku maelfu ya watu wakiwa ndani ya uwanja wa Jamuhuri,mkoani 
   Ni burudani murua kabisa usiku huu ndani ya uwanja wa Jamuhuri,wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea. 
   Mwanadada ambaye wengi wanadai amerithi viuno na sauti kutoka mwanamuziki Ray C,anaitwa Rachael kutoka nyumba ya vipaji a.k.a THT akiimba jukwaani huku akionesha umahiri wake wa kukata mauno.
  Mkongwe wa muziki wa kizaz kipya a.k.a Bongofleva Afande Sele a.k.a Baba Tunda a.k.a Simba Mzee akidhihirisha ukongwe juu ya steji ya tamasha la Serengeti linalofanyika usiku huu ndani ya uwanja wa Jamuhuri mkoani Dodoma,ambapo maelfu ya watu washabiki wamejitokeza kushuhudia tamasha hilo ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka.
   Makamuzi yakiendelea usiku huu 
   sehemu ya umati wa watu. 
   Dj Mully B akikamua mangoma
   wakishangweka.
  Kutoka TMK Wanaume Halisi,alyewahi kuwa ndani ya kundi la mabaga flesh akishusha mistari yake mbele ya mashabiki wake usiku huu.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano kushoto mh. Samia suluhu Hassan kwa Niaba ya waziri wa nchi wa nchi Ofisi ya makamu wa Rais Mazingira Dkt Terezya Hufisa, akisoma hotuba kwa waandishi wa habari hawapo pichani kuelekea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya hifadhi ya tabaka la Ozone, ambayo huadhimishwa kila mwaka Sepetember 16 kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Julius Ningu (Picha na Ofisia ya Makamu wa Rais)
  ======== ========  ========= 
  MAADHIMISHA YA SIKU YA KIMATAIFA YA HIFADHI YA TABAKA LA OZONI 16 SEPTEMBER 2013.

  Na Evelyn Mkokoi & Rashda Rashid


  Ili kufanikisha utekelezaji wa mkataba wa Montreal, serikali imeandaa na kutekeleza programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali haribifu kwa tabaka la ozoni.

   Akiongea kwa Niaba ya ya waziri wanchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira waziri mwenye dhamana ya kushughulikia masuala ya Muungano Mh. Samia Hassan Suluhu alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, amesema mikakati ya kitaifa ndani ya Programu hii ni pamoja na kujenga uwezo wa taasisi zinazosimamia utekelezaji wa mkataba. , kutoa elimu kwa wadau na umma  wa watanzania kuhusu umuhimu wa Tabaka la Ozoni na hatari zinazolikabili.

  Mheshimiwa suluhu aliongeza kwa kusema kuwa kubadilisha technolojia katika viwanda vinavyotumia kemikali haribifu na kutoa mafunzo yanayolenga kuimarisha ujuzi katika sekta ya kuhudumia  viyoyozi na majokofu na kuhamasisha na kuhimiza matumizi ya kemikali na technolojia mbadala na rafiki kwa tabaka la Ozoni ni njia ambazo serikali inatumia kunusuru kuharibika kwa tabaka la hewa ya Ozoni

   “Ni muhimu tuzingatie kwamba juhudi za kila mmoja wetu zinatakiwa kupunguza na kuondosha mathara katika Tabaka la Ozoni yanayo sababishwa na bidhaa tunazo nunua na kutumia majumbani au sehemu za biashara alisisitiza.”


  Mh Suluhu aliwaasa wananchi kushiriki katika kuhifadhi Tabaka la Ozoni kwa kuzingatia  kuepuka kuingiza nchini gesi zilizopigwa marufuku, kuepuka kutupa ovyo majokofu na viyoyozi chakavu ama vifaa vya kuzuia moto vyenye kemikali zinazomong’onyoa tabaka la Ozoni,


  Alitoa wito kwa mafundi wa majokofu na viyoyozi waakikishe kuwa wananasa kwa kutumia tena vipoozi  (refrigerants) kutoka kwenye viyoyozi, na majokofu wanayo hudumia badala ya kuviachia huru ili visisambae angani na amewashauri mafundi hao watoe elimu kwa wateja wao juu ya njia raisi za kutambua uvujaji wa vipoozi.


  Maadhimisho hayo ya siku ya Ozoni duniani ambayo huadhimishwa tarehe 19 ya mwezi wa September kila mwaka, mwaka huu yatafanyika katika chuo cha VETA-Nyakato jijini Mwanza yakiambatana na maonyesho ya bidhaa na technolojia mbadala na rafiki kwa Tabaka la Ozoni Pamoja na mafunzo na njia bora za technologia sahahi ya kuuudumia viyoyozi, majokofu na mitambo ya kupoozea viwandani.


  Walengwa wakubwa wa maadhimisho haya ni mafundi wa kuudumia majokofu viyoyozi mitambo ya kupoozea kutoka viwandani vya kusindika minofu ya samaki vinywaji na taasisi za ufundi zenye fani ya kuudumia majokofu na viyoyozi. Lengo kuu ni kuelimisha mafundi kuhusu technolojia mpya. 

  0 0
 • 09/14/13--08:36: TANGAZO


 • 0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa pole Nassoro Rashid Tinde mmiliki wa duka la vipuri vya magari Tinde Store lililotekea kwa moto jana usiku,Shinyanga.
   Katibu Mokuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia jinsi moto ulivyoteketeza  Duka la Tinde Store  lililopo mtaa wa Nkurumah ,Shinyanga mjini kushoto ni mmiliki wa duka hilo Rashid Nassoro.
   Seif Ally akionyesha namna duka lilivyoteketea.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapa pole majirani waliomsaidia Ndugu Nassoro Rashid kuzima moto uliounguza Duka la Vipuri vya magari pamoja na nyumba.


  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akivishwa vazi maalum la Kichifu pamoja na kukabidhiwa Mkuki na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe,Chifu Msagata Fundikira ikiwa ni ishara ya kumsimika kuwa Chifu wa Kabila hilo,wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124 iliyopita.Sherehe hizo zimefanyika jana kwenye Kijiji cha Itetemya,Mkoani Tabora.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akisikiliza kwa makini Wasifu wa Marehemu,Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124 iliyopita.Wasifu huo Ulisomwa na Bw. Richard Mchembe.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa pamoja na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe,Chifu Msagata Fundikira wakishirikiana kuweka jiwe la msingi katika eneo litakalojengwa Mnara wa kumuenzi Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124 iliyopita.Sherehe hizo zimefanyika jana kwenye Kijiji cha Itetemya,Mkoani Tabora.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa pamoja na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe,Chifu Msagata Fundikira wakiwa kwenye picha ya pamoja na Machifu kutoka mikoa mbali mbali hapa nchini walioshiriki kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124 iliyopita.Sherehe hizo zimefanyika jana kwenye Kijiji cha Itetemya,Mkoani Tabora.


  0 0

   Kikosi cha Mapacha Watatu Band FC
  Kikosi cha Mashujaa Band FC
  MECHI iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa kati ya Mapacha Watatu FC na Mashujaa Band FC  imeisha vizuri huku timu zote mbili zikifungana bao 1-1, katika mchezo uliochezwa jana katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
  Mchezo huo uliondaliwa na kundi la Bongo Dansi linalopatikana kataika mtandao wa kijamii wa facebook kwa nia ya kuletaa ushirikiano na undugu kwa wanamuziki.

  Ilikuwa ni mechi ya kukata na shoka iliyoacha simulizi kubwa kwa  wote walioishuhudia. Hadi Mapumziko, Mapacha Watatu walikuwa mbele kwa kwa bao lililofungwa na Hija Ugando dakika ya 19.
  Mfungaji alifunga kufuatia kazi kubwa iliyofanywa na Hamis Dacota aliyeichambua ngome ya Mashujaa kabla ya kutoa pande kwa mchezaji mwalikwa Mathew Kiongozi ambaye naye bila hiyana alimsogezea Hajji aliyeujaza mpira wavuni.

  Wachezaji wa Mapacha wakiongozwa na Jose Mara, Khalid Chokoraa, Kasongo, Dacota , Dulla Ngoma na wengineo, waliendelea kulisakama lango la Mashujaa kwa muda wote wa kipindi cha kwanza.
  Lakini Upepo ulibadilika kipindi cha pili ambapo Chaz Baba, Abdul Tall, Jado FFU na wengineo walianza kuumiliki mpira na na kuwafunika Mapacha Watatu.

  Zikiwa zimesalia dakika 3 mpira kumalizika, Mashujaa walisawazisha kwa bao lililofungwa na Hamis Tanya, ikiwa ni hatua nzuri ya maendeleo ya kundi hilo la Bongo Dansi, lililoanzishwa na kuongozwa na wadau wa muziki, akiwamo Said Mdoe, Mathew Kawogo ama Mathew Kiongozi, Engi Muro Mwanamachame, William Kaijage na Abdulfareed Hussein, Deo Mutta Mwanatanga na Khamis Dacota.

  0 0
  0 0  Tübingen  will once again host the International Africa festival 2014. The 5th Edition will bring you the best in African diversity, culture, music from the continent and beyond. Save this date now, and join us in Tübingen for world-class performances, unbeatable atmosphere, meet and make new friends.  We welcome you to the African Village in Tübingen - 4days non-stop, spice up your life and be amongst the thousands of people that will celebrate the 5th anniversay of Tübingen Africa Festival.  Stay online for more detailswww.afrikafestival.net

  Call for Artist 2014
  Are you interested in performing next year at the 5th International African Festival in Tübingen - Stuttgart south of Germany? Are you a band on tour, looking for festivals to promote and sell your CDS? Are you interested in supporting the aims and objectives of our festival with a free concerts?
  Are you musicians or a band that support the spirit of freedom, love and non descrimination?


  Our festival is open to all nationalities, denominations,  age groups, poor and rich , simple and uncomplicated! We believe that no amount of money can compensate freedom, love and peace and that another way of life is possible – a lifestyle in which people, humans, everything that has breath, comes first!
  Bands and artist that are interested to perform at our festival shall possess the same spirit –
   Applications are now open to apply for the chance to perform at the 5th edition of International Africa Festival Tübingen- Stuttgart, south of Germany. The festival features live as well as soundsystem music, traditional dance and music groups, acrobatic shows, theater, comedy and more.  Note that we receive hundreds of applications every year and not all applications shall be considered. All artists have to complete  and send recordings to reach our us  before 15 May 2013. Selected acts will be informed per mail.

  Call for Sponsors & Donors

  Daily solidarity entry fee for the 5th International African festival is 2Euros. To help keep it this way we rely on support from donors and sponsors. We have ingenious ways your organisation can be seen as part of the Festival's success. If you are interested in sponsoring the festival Email:  kontakt@afrikafestival.net

  Call for festival / Eventsmanagement Internship
  The International African Festival Tübingen is founded and developed on the principles of being a family oriented event where the surrounding communities could gather for socializing, entertainment, education and friendly competition. Those founding principles have continued to play an integral role in the fair’s purpose throughout the past three years because of the dedication of past and present fair board members, staff, exhibitors and fair patrons.
  Our Festival offers an exciting opportunity for experiences. If you´re seeking an outstanding interns for a fun,
  unique, fast-paced, Festival/Event Management Internship within diversed departments . Broaden your know-how and  
   build experience in a number of event management areas including:
  • Social Media Marketing
  • Sponsorships
  • Commercial Vendor Accounting
  • Entertainment Attraction Marketing
  • Client Services
  • Advertising
  The ideal candidate will enjoy working on a variety of tasks and may have the opportunity to work in must exhibit a strong work ethic, be detail-oriented, display a professional demeanor, and have the ability to multi-task when needed. The Festival/Event Management interns will have a measurable impact on the success of the Festival, a 4-day event which will occur July 17 -20 2014. Interested applicants should submit cover letter, resume and availability to kontakt@afrikafestival.net


  Call for Volunteers 2014
  The International african festival depends on a large team of talented and dedicated volunteers who take part in all aspects of the Festival. Volunteer opportunities range from working with the Festival’s operations team to ushering, administration, and special events. We invite you to lend your time and talents and be a part of the incredible experience of the Festival.

  0 0
 • 09/16/13--09:35: Special Announcement
 • Dear Weruweru Golden Girls... Our Khanga, T shirts and Mugs for the Weruweru Golden Jubilee are all in the MARKET now...The Khanga designs incorporates our school skirt colors,so you get to wear something that reminds you of those good old days.
   With the Stars that represents us,the shining stars from Weruweru...You can tailor it in any design you want! A dress,a blazer, a skirt,trousers etc...it's all in your choice.
   For the mugs,you can either have the ones with Mama Kamm,or the ones with all the legendary women who groomed us throughout. Dr. Maria Kamm, Sister Mary, Mama Msuya, Mama Sambaya...all of them!
   Where to get them? Here are the selling points;
  1. Masaki, Chole Road at the Nature's Rumour Dhow Furniture Shop located at the shopping center just before making the turn going to Yatch Club. Contact person is Pamella on tel# 0713 251 703

  2. Sinza Kijiweni at Puma Petrol Station super market along Shekilango Road. Contact person is Anna Mushi a Weruweru alumni
  Tel# is 0715 307 780
  Did you know; You can send in your CONTRIBUTIONS according to your pledges through Tigo Pesa, Airtel Money na M-Pesa..... 0713213771 and 0786213771( Mwanaimani Tuli )... and/or 0763475506-Naelijwa Gadiely.

  Kumanya Kupenda Huduma...

  0 0

   Mkurugenzi idara ya mazingira ofisi yamakamu wa Rais Dkt Julius Ningu akisoma hotuba ya ufunguzi katika maadhimisho ya siku ya kimaifa ya hifadhi ya tabaka la ozone inayofanyika kitaifa mjini mwanza leo. 
  Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya hifadhi ya tabaka la ozone inayofanyika kitaifa mjini mwanza leo.picha na habari na (Evelyn Mkokoi)
  =======  ========   ==========
  Evelyn Mkokoi,

  Mwanza 16/9/2013


  Imelezwa kuwa kuharibiwa kwa tabaka la ozoni husababisha kuongezeka kwa magonjwa, kama vile saratani ya ngozi, uharibifu wa macho kama vile "mtoto wa jicho" unaosababisha upofu, na upungufu wa uwezo wa mwili kujikinga na maradhi.  hayo yameelezwa leo Jijini Mwanza  na mkurugenzi wa idara ya mazingira kutoka ofisi ya makamu wa rais Dkt Julius Ningu katika kilele cha maadhimisho ya siku ya kimataifa ya hifadhi ya tabaka la ozoni.


  Dkt. Ningu amesema kuwa  watoto wako katika hatari zaidi ya kupata madhara haya, na madhara mengine  katika viumbe hai, pamoja na  kuharibika kwa fiziolojia ya mimea na utaratibu wa ukuaji wake.


  Dkt Ningu ameendelea kusema kuwa, madhara haya yanaweza kuchangia mabadiliko katika muundo wa spishi, hivyo kuathiri  bioanuwai katika mifumo ikolojia mbalimbali, na yaweza kuchangia kuathiri uzalishaji, ukuaji na uwezo wa kuzaliana wa viumbe wa majini,  na uharibifu wa vifaa mbalimbali vya aina ya plastiki.


  Awali akifungua mafunzo kwa washiriki ikiwa ni sehemu ya kazi katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya hifadhi ya tabaka la ozoni, Mgurugenzi msaidizi osifi ya kamau wa rais mazingira bi Magdalena Mtengu amesema kuwakumong’onyoka kwa  tabaka hilo kutokana na mlundikano wa gesi aina mbali mbali.


  alitolea mfano wa gesi hizo kuwa  kuwa  ni pamoja na, chloroflourocarbons (CFCs), halons, methyl choroform, methyl bromide, carbon tertrachoridena ambazo ni sehemu ya kemikali zinazotumika katika majokofu, viyoyozi, vifaa vya kuzimia moto, ushafishaji chuma, utengenezaji wa magodoro, madawa na manukato ya kupulizia, ufukizaji wa udongo katika vitalu vya tumbaku na mashamba ya maua na upiliziaji wa madawa kwenye mazao katika maghala.


  Na  Ili kunusuru uharibifu wa tabaka la ozone na madhara yake kwa viumbe hai na mimea serikali za jumuiya ya umoja wa kimataifa kwa pamoja ziliridhia Mikataba mbali mbali ukiwemo wa Montreal wenye lengo la  kudhibiti utengenezaji na matumizi ya kemikali zinazomong’onyoa Tabaka hilo.


  maadhimisho haya kitaifa mwaka huu yanafanyika mjini mwanza yakiwa na malengo ya kutoa mafunzo kwa mafundi, wenye viwanda na elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari.
older | 1 | .... | 159 | 160 | (Page 161) | 162 | 163 | .... | 1898 | newer