Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

TFDA KUWAENDELEZA WAJASIRIAMALI WA CHAKULA

$
0
0
 Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Bi. Gaudensia Simwanza KUSHOTO akieleza kwa waandishi wa Habari kuhusu mpango wa mafunzo na Ufuatiliaji kwa wazalishaji wadogo wa bidhaa za Chakula unaoratibiwa na mamlaka hiyo, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari leo Jijini Dar es Salaam KULIA ni Mkaguzi wa Chakula toka Mamlaka Hiyo Bw. John Mwingira.

Mkaguzi wa Chakula toka Mamlaka ya Chakula na Dawa Bw. John Mwingira akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu mpango wa ukaguzi wa vyakula kutoka kwa wazalishaji, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari leo Jijini Dar es Salaam KULIA ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Bi. Gaudensia Simwanza


PICHA NA HASSAN SILAYO> MAELEZO

========  ========  =========


MAELEZO KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MPANGO WA MAFUNZO NA UFUATILIAJI KWA WAZALISHAJI WADOGO WA BIDHAA ZA CHAKULA , UKUMBI WA IDARA YA HABARI MAELEZO, TAREHE 16 SEPTEMBA 2013



*      Wakurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo,

*       Ndugu Waandishi wa Habari,

*      Mabibi na Mabwana.


Ndugu wanahabari,

Napenda kwa heshima na taadhima kutumia fursa hii kwa niaba ya Menejimenti ya TFDA na wafanyakazi wote kwa ujumla kuwakaribisha katika mkutano huu.  TFDA ni taasisi ya Serikali iliyopo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iliyoundwa chini ya sheria namba 1 ya Chakula, Dawa na Vipodozi  Sura 219 kwa lengo la kudhibiti ubora na usalama wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya za wananchi. Hii inamaanisha kuwa wanaolindwa ni sisi sote ikiwa ni pamoja na jamaa zetu na wananchi kwa ujumla.


Ndugu wanahabari,

Leo tumekutana hapa kwa lengo la kupeana taarifa kuhusu mkakati wa TFDA katika kuwaendeleza wajasiriamali wa chakula kwa lengo la kulinda afya ya walaji, lakini pia kufanya vyakula hivyo kuweza kumudu ushindani wa soko la ndani na nje na kuleta matokeo makubwa sasa.



Ndugu wanahabari,

Suala la usalama wa vyakula ni la msingi kwa sababu lina athari kubwa kiafya, kiuchumi na kijamii.  Hata hivyo, kama hazikudhibitiwa ipasavyo matumizi ya bidhaa hizi yanaweza kuleta madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kusababisha ulemavu, kupoteza maisha na hata kudhoofisha uchumi wa nchi. Kwa sababu hiyo TFDA kama taasisi iliyopewa dhamana ya usimamizi wa bidhaa hizo inahakikisha kwamba vyakula vinavyouzwa katika soko la Tanzania vinakidhi viwango vya usalama, ubora na ufanisi.

TFDA ina majukumu mengi kwa mujibu wa Sheria. 

Miongoni mwa majukumu hayo ni pamoja na udhibiti wa uhifadhi, usafirishaji, usindikaji, uagizaji na usambazaji vyakula. Katika kutekeleza jukumu lake, TFDA inasajili majengo yote yanayotumika katika usindikaji wa vyakula ikiwa ni pamoja na utoaji wa vibali vya usindikaji, uingizaji na usafirishaji nje vyakula. Majukumu mengine yanayofanywa na TFDA ni pamoja na ufuatiliaji usalama wa vyakula kwenye soko na utoaji wa elimu kwa wadau mbalimbali.


Ufanisi wa utekelezaji wa majukumu haya unawezekana kutokana na  mifumo mizuri ya utendaji kazi iliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kulingana na viwango vya kimataifa vya ISO 9001: 2008.


Ndugu wanahabari,

TFDA kama taasisi ya udhibiti wa vyakula, tunatambua kuwa tuna wajibu wa kuwasaidia wasindikaji wadogo wa vyakula ili waweze kukua na kuzalisha vyakula kwa mujibu wa Kanuni bora za uzalishaji ili viweze kumudu ushindani wa soko la  ndani na  nje kutokana na biashara huria na kuzalisha chakula salama.


Takwimu zinaonesha asilimia 75 ya viwanda vya vyakula nchini ni viwanda vidogo (Kwa mujibu wa upembuzi yakinifu uliofanyika 2004/5) ambapo kukua kwa viwanda hivi kutakuwa na mchango mkubwa katika; kuongeza ajira na kipato katika ngazi ya kaya, kukuza kilimo cha mazao ya chakula kutokana na kuwepo na soko la mazao ya vyakula na kuchangia katika pato la taifa.


TFDA inatambua kuwa viwanda vidogo vina nafasi kubwa ya kuchangia katika pato la Taifa kutokana na uwingi wake lakini pia vinaweza kutoa mchango mkubwa katika kuleta athari za kiafya ikiwa bidhaa zake hazitakidhi viwango vya usalama na ubora.


Ndugu wanahabari,

Kwa kuzingatia mambo hayo niliyotaja, TFDA imeamua kuja na mkakati wa kuwafundisha wajasiriamali wadogo wa vyakula ili kuwawezesha wasindikaji hawa kujua sheria, kanuni na miongozo inayohusu usindikaji wa chakula salama pamoja na kuongeza kiwango cha uzingatiaji wa kanuni bora za uzalishaji wa vyakula.

Hadi sasa mafunzo hayo yametolewa kwa wajasiriamali 417 kutoka katika Kanda zote katika mikoa ya Dar es Salaam (90), Singida (44), Mbeya (76), Arusha (54), Dodoma (98) na Mwanza (55).


Ndugu wanahabari,


Aidha, kutoka mwaka 2012/13, TFDA imekuwa inaendesha mpango wa majaribio kwa wasindikaji wadogo wa mafuta ya alizeti mkoani Singida  ili kuelekeza namna ya kuboresha uzingatiaji wa matakwa ya Sheria kuhusu misingi ya usafi na uzalishaji bora.

Mpango huu umehusisha hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na;

i.   Kufanya tathmini ya kiwango cha uzingatiaji wa sheria

ii.Kuainisha maeneo yenye mapungufu

iii.  Kuandaa mafunzo yanayozingatia mapungufu yaliyojionesha

iv.  Kuwasilisha taarifa ya tathmini kwa wadau pamoja na wasimamizi wa sheria katika eneo husika

v.    Kukubaliana namna ya kutatua upungufu na kuwa na ratiba ya utekelezaji kwa mambo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu

vi.  Ufuatiliaji wa makubaliano

vii.Tathmini ya jumla kwa makubaliano ya muda mfupi na wa kati ili kujua kiwango cha utekelezaji.

Lengo la mpango huu ni kusambazwa nchi nzima ikiwa utaleta matokeo mazuri kwa mkoa huu wa Singida ambao ni wa majaribio ifikapo mwaka 2016/17.


Ndugu wanahabari,


Kwa kuhitimisha, TFDA inatoa shukurani kwa ushirikiano ambao mmekuwa mkiuonesha katika kutoa taarifa za kiudhibiti pale inapotokea pamoja na kuelimisha jamii.


Rai yetu kwenu ni kuendelea kutumia kalamu zenu katika kuwaondolea hofu wananchi kuhusu usalama na ubora wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na Vifaa tiba vilivyopo katika soko kutokana na mifumo thabiti iliyowekwa na TFDA.


Aidha, tunatoa wito kwa wananchi kwamba ikiwa mtu atabaini au kuwa na mashaka juu ya usalama na ubora wa bidhaa hizo basi asisite kuwasiliana nasi kupitia ofisi zetu za Makao Makuu na za Kanda zilizopo Extenal Mabibo, Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma na Ofisi za Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya au kutoa taarifa katika kituo chochote cha polisi kilicho jirani naye.


Asanteni kwa kunisikiliza!



SERIKALI KUIMARISHA UDHIBITI WA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE NCHINI

$
0
0
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa akiwatambulisha kwa waandishi wa habari wawasilishaji toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika mzunguko wa pili wa Taasisi za Serikali kuongea na  waandishi wa habari, KATIKATI ni Mratibu wa Taifa wa Mpango wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira na KULIA ni Afisa Habari Bi.Catherine Sungura wote kutoka Wizara hiyo, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari leo Jijini Dar es Salaam.

 Mratibu wa Taifa wa Mpango wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Upendo Mwingira KUSHOTO akiwaonesha waandishi wa habari Dawa za Kingatiba za Magonjwa yasiyopewa kipaumbele yaliyosambazwa katika wilaya 97 kupitia Bohari kuu ya Madawa. KULIA ni Afisa Habari Bi.Catherine Sungura wote kutoka Wizara hiyo, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari leo Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA HASSAN SILAYO> MAELEZO. 
Mratibu wa Taifa wa Mpango wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Upendo Mwingira KUSHOTO akieleza kwa waandishi wa habari juu ya mpango wa serikali kuendelea kuimarisha udhibiti wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchini, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari leo Jijini Dar es Salaam KULIA ni Afisa Habari wa Wizara hiyo Bi.Catherine Sungura.



======  ======= ======
SERIKALI KUIMARISHA UDHIBITI WA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE NCHINI


Sera ya afya ina lengo la kuinua hali ya maisha kwa wananchi wote mahali popote walipo ikiwa mjini au vijijini kwa kupunguza maradhi na vifo kwa wananchi na kuongeza umri wa maisha yao kwa kuwa na afya thabiti kimwili, kiakili na kijamii. Vilevile ieleweke kwamba afya bora ni rasilimali kubwa kwa maendeleo ya kiuchumi na kiakili.


Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imejikita  katika kuimarisha, kuboresha na kusambaza huduma za afya na ustawi wa jamii nchini, kwa kuzingatia Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi(MMAM-2007-2017),imejikita katika kudhibiti  magonjwa yasiyopewa kipaumbele.


Magonjwa yasiyopewa kipaumbele ni magonjwa ambayo yanaathiri jamii  ya watu hususani wenye kipato cha chini wanaoishi katika maeneo duni, maeneo ambayo  hata upatikanaji wa  huduma za afya ni  mgumu.


Magonjwa hayo ni pamoja na Matende na mabusha, Usubi, Trakoma, Kichocho, Minyoo ya tumbo,Homa ya malale,Kichaa cha mbwa,tauni,Tegu na mengineyo.Maambukizi ya Magonjwa haya yanatokana na  kuenezwa  na wadudu kama vile mbu, nzi na konokono. Udhibiti wa magonjwa haya unaelekezwa kwenye kinga tiba,usafi binafsi wa mazingira na udhibiti wa wadudu waenezao magonjwa hayo.


Athari za magonjwa  haya yasipotibiwa mapema  ni pamoja  na saratani ya kibofu cha mkojo na ini,upofu,utumbo kujifunga na dalili za kifafa.Magonjwa haya husabababisha pia ulemavu wa kudumu hali ambayo inapunguza uwezo wa wananchi wetu kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya kiuchumi.


Magonjwa haya huathiri pia watoto  na hivyo  kupunguza mahudhurio ya watoto shuleni hatimaye maendeleo yao katika masomo  kuathirika. Magonjwa haya husababisha usumbufu mkubwa kwa waathirika wake na  yanaongeza matumizi ya rasilimali chache tulizonazo katika kuyakabili kwa gharama kubwa mno. Pamoja na athari zote hizo, waathirika wa magonjwa haya  wakabiliwa na unyapaa katika jamii.


Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imepiga hatua kubwa katika  udhibiti wa magonjwa hayo kwa kuimarisha, kuboresha na kusambaza huduma za Mpango wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele kwa jamii zilizoathirika nchini. Katika mwaka 2012/2013, wizara kwa kuzingatia Mpango wa Taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele imefanikiwa kutekeleza yafuatayo:

·        Kuzindua rasmi Mpango Mkakati wa Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele (2012-2017).

·        Kuongeza idadi ya wilaya zinazotekeleza mpango huu kutoka 76 mwaka 2011 hadi  halmashauri 93 kati ya 155 yaani asilimia 60%  halmashauri zote kwa nchi nzima

·        Kutibu na kukinga   watu  milioni 15.4 kwa dozi million 36 za dawa za Mectizan, Albendazole, praziquantel na Zithromax.

·        Kufanya Tathminini ya awali ya  ugonjwa wa Trachoma katika wilaya 9. Matokeo yanaonyesha Wilaya 10 zilizofanyiwa tathmini hiyo hazihitaji  kinga tiba i.e MDA

·        Uzinduzi wa kampeni ya  ugawaji wa dawa  katika jiji la Dar (kwa jamii) pamoja na Mwanza ( mashuleni).



Kwa kiasi kikubwa serikali imejitahidi kuboresha huduma za  udhibiti wa magonjwa hawa kwa  kusambaza dawa za kingatiba za magonjwa haya katika wilaya 97 kupitia Bohari kuu ya Madawa,kuwa na waratibu wa Mpango huu katika ngazi za Mkoa na wilaya.Waratibu hawa wanapatiwa Mafunzo na maelekezo ya utekelezaji wa mpango  kila mwaka.Utekelezaji  wa Mpango huu unafanyika katika ngazi ya wilaya na hivyo Halmashauri zote zilizoathirika zimeelekezwa kutenga  rasilimali katika mipango yao ya Afya kupitia  Muongozo  wa CCHP.


Mwisho napenda kutoa wito kwa wananchi wote kumeza dawa hizi za Kingatiba kama wanavyoelekezwa na wataalam wakati wa Kampeni husika.Dawa hizi zimethibitishwa na shirika la afya duniani pamoja na mamlaka ya Chakula na dawa nchini kuwa ni salama na hazina Madhara yeyote.


CLARA BAYO ALIVYO SHINDA TAJI LA REDD'S MISS TANZANIA SPORTS WOMAN 2013

$
0
0
 Mrembo Clara Bayo akipunga mkono mara baada ya kutangwazwa kuwa mshindi wa Taji la Redd's Miss Tanzania Sports Woman 2013 juzi wakati wa tamasha la michezo la warembo wanao wania taji la Miss Tanzania 2013. Bayo alifanya vyema katika michezo kadhaa na kujizolea point nyingi na kuwashinda warembo wengine 29.

Kwa Taji hilo Clara Bayo ambaye anatoka Kanda ya Ilala, amekuwa mrembo wa nne kuingia nusu fainali za Mashindano hayo makubwa ya urembo nchini ambayo fainali zake zitafanyika Ukumbi wa Mlimani City Septemba 21 mwaka huu.
 
 Warembo walichuana vikali kaika soka huku timu za Redd's na Zanzi zikichuana na Zanzi iliyoongozwa na nahodha na mfungaji bora Happines Watimanywa ikishinda kwa goli 2-1.
Michezo mingene mbalimbali ilifanyika kama kukimbia, kukimbia na magunia, kuruka chini, Volleyball na kuogelea ilifanyika. 

KINANA AWATAKA MAWAZIRI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakazi wa kata ya Mwandoya ,kijiji cha Mandoya tarafa ya Kisesa ambapo Katibu Mkuu alipata maelezo ya utekelezaji wa ilani ya CCM.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amewataka mawaziri husika kutatua kero za wananchi baada ya watendaji wa chini kushindwa kufanya kazi zao, alisema sasa baadhi ya watendaji wamegeuza kero za wananchi mitaji  na kuwachajisha pesa nyingi hasa wafugaji.

Akihutubia wakazi wa kata ya Mwasengela alisema mawaziri lazima wachukue jukumu la moja kwa moja kutatua matatizo ya wananchi, alisema wafugaji wa kata ya Mwasengela wamekuwa wakibughudhiwa na watu wa hifadhi ya Maswa  kupita kiasi, alisema sheria zingine ziangalia wakati zinaweza zikawa zimepitwa na wakati hivyo ni vyema zikarekebishwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Mwangesela wilayani Meatu mkoani Simiyu.
 Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina akiwatambulisha wazazi wake kwenye mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia wananchi ilimchukua miezi mitatu kukubaliwa kwa ombi lake la kutaka kugombea ubunge jimboni kwake.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na Mbunge wa Kisesa Ndugu Luhaga Mpina pamoja na wazazi wa mbunge huyo.

TIB TOKA TAASISI YA FEDHA MPAKA BENKI YA MAENDELEO NCHINI

$
0
0
01
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro (kulika) akikata utepe kuzindua ofisi za Makao Makuu ya Benki ya Maendelea Tanzania (TIB) ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Tawi la benki hiyo Mkoa wa Mbeya iliyofanyika jijini Mbeya jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa TIB, Peter Noni na Mwenyekiti wa Bodi ya TIB, Prof. William Lyakurwa.
02
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo Tanzania (TIB), Prof. William Lyakurwa (kushoto), akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa ofisi za Makao Makuu ya TIB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Tawi la benki hiyo Mkoa wa Mbeya iliyofanyika jijini Mbeya. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na Mkurugenzi Mwezeshaji wa TIB, Peter Noni.
03
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro (katikati) akijaza fomu ili kufunguliwa akaunti ya Benki ya Maendeleo Tanzania (TIB) Tawi la Mbeya, katika hafla ya ufunguzi wa ofisi za Makao Makuu ya TIB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini pamoja na tawi hilo Mkoa wa Mbeya iliyofanyika jijini humo. wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa TIB, Peter Noni na anayeongea naye ni Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi.

.ilianzishwa mwaka 1970 ina takribani miaka 40 kwenye huduma za kifedha
.sasa kuwekeza kwenye miundombinu ya reli, mawasiliano na barabara
.Benki ya wanyonge, mafanikio kichelee, wakulima nao kunufaika

Na Damas Makangale, Moblog
Baada ya kujiendesha Kwa faida Kwa takribani muongo mmoja, Benki ya Maendeleo Tanzania (TIB) iliyoanzishwa mwaka 1970 Kama Taasisi ya Maendeleo ya fedha, Development Finance Institution (DFI), TIB inakusudia kuanza kuwekeza katika miradi mikubwa yenye kuleta matokeo makubwa na kuendana na kauli mbiu mpya ya Serikali “Matokeo Makubwa sasa” (Big Results Now).

Baada ya kufanya kazi Kama taasisi ya maendeleo ya fedha Kwa miaka 25, TIB ilikuja kubadilishwa na kuwa benki ya uwekezaji (Tanzania Investment Bank) ili kuongeza uwezo wake wa kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya soko hapa nchini.

TIB lengo lake kuu ni kutoa Fedha na huduma za uwekezaji na maendeleo katika Nyanja mbalimbali kama vile kilimo kupitia dirisha lake maalum la kukopesha wakulima wadogo wadogo (Special Agriculture Window), mikopo kwa wafanyabiashara na watu wa kipato cha chini ili kuweza kuinua maisha yao na kuondokana na umaskini.
Kusoma makala hii kwa kina ingia hapa

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII,MHE. UMMY MWALIMU KATIKA MKOA WA PWANI

$
0
0

 Mhe. Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na watoto wa shule ya awali ya Mtakatifu Stephano Shahidi,Wakuu wa Shule hiyo,Walimu na Baadhi ya Watendaji wa Halmashauri
 Mhe.Ummy Mwalimu akiwasalimia watoto wanaosoma katika Shule ya Awali ya Mtakatifu Stephano Shahidi, alipowatembelea leo
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na baadhi ya Wanafunzi wa Sekondari za Chanzige na Kimani Wilayani Kisarawe.
Naibu Waziri Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati wa mkutano kati ya Wananfunzi, Watendaji wa Halmashauri na Madiwani, Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Fatma Kimario
=========  ========   ========
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  ameanza Ziara yake MKoa wa Pwani katika Wilaya za Kisarawe,Rufiji,  Mkuranga, na Mafia ambapo anatarajia kutembelea Utekelezaji wa Miradi  na Shughuli za Maendeleo ya Jamii Mkoani humo.



  Katika Ziara yake leo Mhe.Ummy amepata nafasi ya kukutana na
Watendaji Wakuu wa Wilaya ya Kisarawe ambapo taarifa ya utekelezaji wa  
Wilaya imewasilishwa kwake, Vilevile amefanya kikao na Maafisa   
Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii , Amekutana na
Wananfunzi wa Sekondari za Kimani na  Chanzige, na ametembelea Shule
ya Watoto ya Awali ya Mtakatifu Stephano.

KINANA: MAWAZIRI TATUENI KERO ZA WANANCHI MOJA KWA MOJA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia maendeleo ya hatua za awali za ujenzi wa daraja la Mongobakama ambalo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM akipokelewa na umati wa wakazi wa kijiji cha Mwasengela ambao kwa ni nadra kupata viongozi wa kitaifa kwenye kijiji chao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakazi wa kata ya Mwandoya ,kijiji cha Mandoya tarafa ya Kisesa ambapo Katibu Mkuu alipata maelezo ya utekelezaji wa ilani ya CCM.
 Mkuu wa Wilaya ya Meatu Rosemary Kirigini akisalimia wakazi wa kata ya Mwasengela wakati wa mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alihutubia.
 Mbunge wa Kisesa Ndugu Luhaga Mpina akihutubia wakazi ya kata ya Mwasengela kwenye mkutano wa hadhara ambao mgeni wa heshima alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wakazi wa kata ya Mwasengela ambapo yupo kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mkoani   Simiyu .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na aliyekuwa mgombea wa udiwani kwa tiketi ya TLP lakini sasa amejiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi Zunzu Ndatulu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mwasengela.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Mwangesela wilayani Meatu mkoani Simiyu ambapo aliwasifu wakazi wa kata hiyo kwa kuichagua CCM na kupata viongozi wanaoleta maendeleo.
 :Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina akiwatambulisha wazazi wake kwenye mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia wananchi ilimchukua miezi mitatu kukubaliwa kwa ombi lake la kutaka kugombea ubunge jimboni kwake.
 Chifu Kilabanja Abdulrahman Kinana akiwaaga wakazi wa kata ya Mwasengela baada ya kumaliza Mkutano wa hadhara.
Sehemu ya umati uliofika kwenye mkutano wa hadhara kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya mikoa mitatu ambapo kwa sasa yupo mkoani Simiyu na atamalizia mkoa wa Mara, tayari Katibu Mkuu ameshamaliza ziara ya mkoa wa Shinyanga na kuleta neema kwa wakulima wa pamba na wafugaji.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na mbunge wa Kisesa Ndugu Luhaga Mpina na wazazi wa mbunge huyo mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amewataka mawaziri husika kutatua kero za wananchi baada ya watendaji wa chini kushindwa kufanya kazi zao, alisema sasa baadhi ya watendaji wamegeuza kero za wananchi mitaji  na kuwachajisha pesa nyingi hasa wafugaji.

Akihutubia wakazi wa kata ya Mwasengela alisema mawaziri lazima wachukue jukumu la moja kwa moja kutatua matatizo ya wananchi, alisema wafugaji wa kata ya Mwasengela wamekuwa wakibughudhiwa na watu wa hifadhi ya Maswa  kupita kiasi, alisema sheria zingine ziangalia wakati zinaweza zikawa zimepitwa na wakati hivyo ni vyema zikarekebishwa.

HOSPITALI ZA TUMBI, MOROGORO NA USALAMA BARABARANI ZANUFAIKA NA MSAADA WA TBL

$
0
0
 AFISA Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Dorris Malulu mwenye iwani akikabidhi hundi yenye thamani ya sh. Mil. 13 kwa Daktari wa Upasuaji katika hospitali ya  Tumbi Kibaha, Pwani,hiyo Dkt. Petter Datan, katikati ni Mkuu wa Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani mkoani Pwani Nassoro Sisiwaya katikati ni mmoja wa madaktari wa hospitali hiyo. (PICHA NA MWENGE  SAID).

Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro dk Godfrey Mtey kushoto akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Afisa Uhusiano wa kampuni ya bia ya TBL, Doris Malulu yenye thamani ya sh14.6 milioni ili kuweza kutumika wakati wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ikihusisha madereva wa nagari kupima afya katika mizani ya Mikese mkoa wa Morogoro, katikati ni Mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Boniface Mbao.

WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA NA BIASHARA WATEMBELEA KIWANDA CHA TBL IYUNGA MBEYA

$
0
0

 Wajumbe wa Mamati maalumu Bunge ya Viwanda na Biashara wakitembelea Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) Iyunga Jijini Mbeya hivi karibuni.
 Wajumbe wa Mamati maalumu Bunge ya Viwanda na Biashara wakitembelea Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) Iyunga Jijini Mbeya hivi karibuni.

 Wajumbe wa Mamati maalumu Bunge ya Viwanda na Biashara wakioneshwa namna Bia aina ya Safari Lager inavyozalishwa katika kiwanda cha Bia cha TBL kilichopo Iyunga Jijini Mbeya.
Wajumbe wa Mamati maalumu Bunge ya Viwanda na Biashara wakioneshwa namna Bia aina ya Safari Lager inavyozalishwa katika kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) kilichopo Iyunga Jijini Mbeya.

SEVERINA LWINGA ATWAA TAJI LA MISS TANZANIA PERSONALITY 2013

$
0
0
Mrembo Severina Lwinga juzi alifanikiwa kuwa mrembo wa tano kuingia nusu fainali ya shindano la Redd's Miss Tanzania 2013 baada ya kutwaa taji la Miss Personality 2013. Mshindi wa taji hilo anapatikana kwa kupigigiwa kura na warembo wenzake.

Severina ameungana na Miss Tanzania Photogenic 2013, Happiness Watimanywa, Miss Tanzania Talent 2013, Prisca Clement, Miss Tanzania Top Model 2013, Narietha Boniface na Miss Tanzania Sports Woman, Clara Bayo kuingia katika nusu fainali ya Miss Tanzania ambayo itafanyika Jumamosi hii ukumbi wa Mlimani City. Shindano hilo lilifanyika Mgahawa wa AK'S ulipo mtaa wa Samora.
 Warembo walioingia tano bora ya Miss Personality 2013 shindano lililofanyika katika magahawa wa AK'S uliopo Mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam.

Warembo watano ambao wamefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya Redd’s Miss Tanzania 2013 wakiwa katika picha ya pamoja mara jana. Kutoka kushoto  ni Miss Tanzania Photogenic 2013, Happiness Watimanywa, Miss Tanzania Talent 2013, Prisca Clement, Miss Tanzania Personality, Severina Lwinga, Miss Tanzania Top Model 2013, Narietha Boniface na Miss Tanzania Sports Woman, Clara Bayo.
Warembo wakiingia katika Mgahawa wa AK'S uliopo mtaa wa somora Dar es Salaam kushiriki shindano la Miss Personality.
 
 Warembo wakiwa ndani ya mgahawa wa AK'S jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga ambao ndio waandaaji wa Miss Tanzania akiwa na Mkurugenzi wa Mgahawa wa AK'S, Kishan.
 Warembo wakiwa eneo la juu la mgahawa huo ambako kuna patikana viywaji vya kila namna pamoja na burudani kali ya muziki.
Warembo wakiburudika kwa Disco safi lililopo ndani ya mgahawa huo wa Kimataifa wa AK'S.

Timu ya Copa Coca-Cola yarejea nchini baada kushiriki michuano ya kimataifa ya Copa Coca-Cola nchini Afrika Kusini

$
0
0
 Timu ya Copa Coca-Cola iliyoshiriki katika michuano ya kimataifa ya Copa Coca-Cola nchini Afrika Kusini wiki iliyopita ikiwasili kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu jioni. Timu hiyo ilitolewa katika hatua ya makundi na Zimbabwe kuibuka mabingwa.

 Afisa maendeleo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Salum Madadi akiipokea timu ya vijana ya Copa Coca-Cola iliyoshiriki katika michuano ya kimataifa ya Copa Coca-Cola nchini Afrika Kusini wiki iliyopita. Timu hiyo ilitolewa katika hatua ya makundi na Zimbabwe kuibuka mabingwa.

Zimbabwe waliibuka mabingwa wa 2013 wa mashindano ya kimataifa ya COPA Coca-Cola kwa kuwafunga Uganda 3-0 katika mchezo wa fainali iliyochezwa High Performance Center, Pretoria, Afrika Kusini.



Match details in group that featured Tanzanian team

No

Matches

Results

1

Tanzanite vs Chipolopolo (Zambia)

0-2

2

Tanzanite vs Dream Team (DRC, Congo, Kazakstan)

2-0

3

Tanzanite vs African United (SA, Swaziland, Rwanda, Lesotho

2-2

4

Tanzanite vs Phoros (Egypt)

0-1


140 players from 15 countries participated







“Busara Promotions Looks Ahead: Strategic Planning for the Next 5 Years of ‘Sounds of Wisdom’”

$
0
0



Busara Promotions, the NGO behind the renowned annual music festival Sauti za Busara, recently convened its Board of Trustees, management, senior staff, and distinguished guests from Tanzania’s arts and culture sector for a weekend Strategic Planning retreat at Bluebay Beach Resort in Kiwengwa, Zanzibar, to review its achievements over the last decade and to plan its next five years of activities.

Supported by the Dutch foundation Hivos, Bluebay Beach Resort Zanzibar, and with facilitators from PEN Kenya, the Busara Promotions team got together in order to chart a new course for  the organisation, which has built a strong reputation for excellence in promoting East African music and culture, locally, regionally and worldwide over the ten years of its existence.

Though the NGO is best-known for its annual music festival, Sauti za Busara [Sounds of Wisdom], Busara Promotions is also active year round behind-the-scenes in the music industry, building appreciation worldwide for the region’s music, developing skills and opportunities for musicians and music industry professionals, strengthening the local arts infrastructure, and building regional and international networks.

The next five-year plan builds on the previous successes of Busara Promotions while also introducing some exciting new ideas and projects, including the addition of more cultural events to the NGO’s annual calendar.

Busara Promotions also hopes to be more active in linking artists and music professionals with jobs, workshops, and networking opportunities, as well as strengthening the visibility and accessibility of African music and information online.

Busara Promotions is also pleased to announce that during the retreat, the Board of Trustees confirmed three new members. Ally Saleh, one of Zanzibar’s foremost journalists, first worked with Busara Promotions during the Zanzibar Leaders for Culture and Economic Growth Forum in November 2011. He moderated an important discussion about how stakeholders in business, tourism and other industries can work together with cultural organisations for the benefit of local people. 

Julia Bishop, a professional consultant and former director of the Zanzibar Association of Tourism Investors (ZATI), brings her expertise in cultural tourism and business to the Busara Promotions Board. Verena Knippel helped produce some of Tanzania’s first TV programmes and films. She lived and worked in Zanzibar for many years before re-locating to Dar es Salaam to work for DFID as a budget specialist. All three new board members will help guide Busara Promotions and fulfil its goals in the coming years, contributing their diverse skills and experiences to the team.

At the same time, the Board of Trustees saw two founding members, Hilda Kiel and Emerson Skeens, step down from their Trustee positions and into their new roles as Busara Advisory Council members. The Chairman of the Board, Simai Mohammed Said, thanked them for their many years of loyal service to the organisation and for their continuing commitment as advisors.

Busara Promotions is looking forward to the 11th edition of the Sauti za Busara music festival, to take place during 13-16 February 2014, in Stone Town, Zanzibar. The festival will feature a host of top names and emerging acts in African music. For any inquiries, please contact the Managing Director of Busara Promotions, Rebecca Corey, at rebecca@busara.or.tz.

With special thanks to Bluebay Beach Resort, Zanzibar and our Sauti za Busara 2014 sponsors: Royal Norwegian Embassy, Hivos, Goethe Institute, Memories of Zanzibar, Azam Marine, Ultimate Security, Zanzibar Unique Ltd., SMOLE II and all of our other sponsors and supporters

BLOGGERS TANZANIA WAPIGWA MSASA NA TCRA JIJINI DAR LEO.

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akiwasilisha mada ya kwanza juu ya Ukubwa wa Sekta ya Mawasiliano  na changamoto zake hapa nchini wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy akitoa utambulishao wa baadhi ya watoa mada wakuu wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Wakurugenzi kitengo cha Watoa Huduma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Dkt. Raynold Mfungahema akiwasilisha mada yake ya Haki,wajibu na utoaji huduma wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya Wapiga Picha kutoka Vyombo mbali mbali vya habari ambao pia walifika kwenye warsha hiyo  ikiwa ni sehemu ya kuihabarisha jamii kuhusiana na Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Blogggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.

KUONA PICHA ZAIDI,BOFYA HAPA

PLATINUM CREDIT LTD YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA AJILI YA SHIMIWI.

$
0
0
Na Benedict Liwenga-MAELEZO-Dar es Salaam.

KAMPUNI inayojishughulisha na utoaji wa mikopo kwa watumishi wa Serikali na kampuni zilizothibitishwa ijulikanayo kama Platinum Credit Ltd leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Jeshi la Magereza na TAMISEMI kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya Shimiwi inayotarajiwa kuanza hivi karibuni mjini Dodoma.


Akikabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni hiyo Bw. Elias Samwel amesema kuwa kampuni yake inajihusisha na utoaji wa mikopo ya fedha kwa watumishi wa serikali na kampuni zilizothibitishwa na kiasi cha ziada wanachokipata wanakitumia katika kusaidia jamii katika shughuli mbalimbali ikiwemo michezo.


Aidha, kampuni hiyo imekabidhi jezi, tisheti na kofia zenye thamani ya shilingi milioni 10 ili ziweze kusaidia katika michezo ya Shimiwi itakayofanyika hivi karibuni mjini Dodoma.


“Thamani ya vifaa hivi ni ndogo lakini ninaamini kuwa vitasaidia katika kuleta chachu ya maendeleo katika michezo ya shimiwi”. Alisema Samwel. Kwa upande wake Katibu wa Klabu ya Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Saidi Marusu ameishukuru kampuni ya Platinum Credit Ltd kwa mchango wao mkubwa waliojitolea katika kusaidia kutoa vifaa vya michezo.

“Kwa niaba ya Wizara Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo napenda kutoa shukurani kwa kupokea vifaa hivi kwani ninaamini kuwa vitaleta chachu katika mashindano haya ya Shimiwi”. Alisema Bw. Marusu.


Naye Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza Mkwanda Hassid Mkwanda ameishukuru kampuni hiyo kwa kupata vifaa hivyo na amesema kuwa vitasaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha malengo yao katika michezo ya Shimiwi. “Vifaa hivi vitatumika kwa lengo lililokusudiwa na sio vinginevyo”. Alisema Mkwanda.

Naye mwakilishi wa TAMISEMI ambaye ni Katibu Mkuu wa Shimiwi Bw. Ramadhani Sululu ameishukuru kampuni hiyo kwa mchango wake mkubwa wa kutoa vifaa hivyo vya michezo na ameongeza kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuleta hamasa katika michezo.


“Katika mashindano ya Shimiwi tumejiandaa vizuri na tunaamini kuwa tutashiriki vema katika michezo hiyo”. Alisema Sululu. Mashindano ya Shimiwi yanahusisha Wizara zote za Serikali na Taasisi zake ambapo itajumuisha michezo ya kuvuta kamba, mpira wa miguu, pete, riadha, drafti, bao, karata na kurusha tufe.

Timu zinazoshiriki michuano ya vijana ya Airtel Rising Stars zawasili nchini Nigeria

$
0
0
 Kikosi cha timu ya wavulana kinachoshiriki michuano ya Airtel Rising stars nchi Nigeria wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuondoka katika uwanja wa Julius Kambarage nyerer kuelekea Nigeria kwenye michuano ya Afrika inayoshirikisha timu kutoka nchi 17 barani Afrika .Wa kwanza kulia ni mwakilishi wa Airtel Bi Lilian Kibiriti
 Kikosi cha timu ya wasichana kinachoshiriki michuano ya Airtel Rising stars nchi Nigeria wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuondoka katika uwanja wa Julius Kambarage nyerer kuelekea Nigeria kwenye michuano ya Afrika inayoshirikisha timu kutoka nchi 17 barani Afrika. (mwenye shuti)  ni kocha wa timu hiyo Rogacian Kaijage . 

Kikosi cha timu ya Airtel Rising stars  wakati wa ufunguzi wa michuano ya Airtel Rising Stars ya Afrika  inayozinduliwa rasmi jana (jumatatu) Nchini Nigeria na kushirikisha timu kutoka katika nchi 17 barani Afrika

========  ======  ========
Timu zinazoshiriki michuano ya vijana ya Airtel Rising Stars zawasili nchini Nigeria
·      michuano hiyo inafanyika  Lagos, Nigeria kuanzia 16 hadi  22 September 2013.
Timu zinazoshiriki michauano ya pili ya Afrika ya Airtel rising Stars inayofanyika nchini Nigeria mwaka huu zimewasili ambapo michuano hiyo imeanza rasmi jana  katika viwajnja vya Agege. michuano hiyo imeudhuriwa na wachezaji guru wakiwemo Rober Pires mchezaji nyota wa zamani wa kablu ya Arsenal
Timu ya Zambia ilikuwa yakwanza kutua siku ya Ijumaa ikifatiwa na timu ya Ghana iliyotua muda mchache baadaye siku hiyo. timu ya mabigwa watetezi kutoka Niger ilitua katika uwanja wa ndege wa Murtala Mohammed International  siku ya jumamosi  mchana pamoja na timu kutoka Congo Brazzaville
kikosi cha timu ya Tanzania kiliwasili siku ya jumapaili chini ya kocha Abel Mtweve na timu nyingine zinategemea kuwasili kabla ya michuano hiyo kuanza siku ya jumatatu
michuano ya Airtel Rising stars ni michuano ya kipekee ya nchi za Afrika yenye lengo la kuvumbua na kukuza vipaji  huku ikiwezesha nchi za Afrika kupata wachezaji wa timu za taifa
kwa kupitia mashindano haya Airtel inatoa nafasi kwa vijana hawa kutimiza ndoto zao, na kuonyesha uwezo wao kwa zaidi ya mamilioni ya watu alisema mkurugenzi mkuu wa Airtel Nigeria bwana Segun Ogunsanya
aliongeza "wachezaji wengi wameshiriki michuano mikubwa kama hii kwa mara ya kwanza na wanafurahia kupata nafasi ya kushindana na wachezaji nyota wengine toka katika nchi mbalimbali. kwa wiki nzima tunaamini wachezaji hawa watabaki na kumbukumbu ya mpira ambayo wataifurahia katika maisha yao siku zote"
michuano ya Airtel Rising stars itafanyika nchini lagos Nigeria kuanzia tarehe 16 hadi 22 septemba 2013. wachezaji nyota waliochaguliwa watashiriki katika clinic  itakayosimamiwa na makocha wa Manchester united inayotegemea kufanyiaka mwaka kesho April 2014 nchini   Lubumbashi (Democratic Republic of Congo).

maadhimisho ya siku ya ozone jijini mwanza

$
0
0
 Pichani kulia ni Bwana  Sheejo Varghsese, meneja katika kiwanda cha kutengeneza samaki cha Tanpearch cha jijini Mwanza akiwaonyesha washiriki wa mafunzo katika maadhimisho ya siku ya ozone, namna mitambo ya kuupozea katika kiwanda hicho yenye kemikali rafiki kwa tabaka la ozone inavyofanya kazi.
 Bwana Robnson Swai mwalimu wa VETA Moshi, akitoa mada wakati wa mafunzo kwa mafundi na washiriki wengine jijini Mwanza katika siku ya pili baada ya maadhimisho ya siku ya Ozone Duniani
Baadhi ya washiriki katika mafunzo ya hifadhi ya tabaka la ozone jijini Mwanza (Picha na Evelyn Mkokoi).
========  ========= ======

TRA WANUFAIKA NA UKUSANYAJI WA KODI KWA NJIA YA MITANDAO

$
0
0
Na Denis Mlowe,Iringa
 
UKUSANYAJI wa mapato kupitia mitandao ya simu M-Pesa,Tigo Pesa na Airtel Money umeleta mafanikio  makubwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) tangu mfumo huo uanze kutumika Tanzania.
 
Mkurugenzi  wa  Elimu kwa  Walipa kodi Nchini Richard Kayombo  amebainisha hayo alipokutana na waandishi wa habari  jana katika  ukumbi  wa Hotel ya M.R mjini hapa  kuhusu utaratibu mpya  wa ulipaji  wa kodi kwa wafanyabiashara  na faida zake.

Kayombo alisema kwa kipindi cha mwaka jana kwa muda wa wiki nne TRA alifanikiwa kukusanya kiasi cha bilioni 3.6 tofauti na mwaka huu kipindi cha wiki 3 wamefanikiwa kuingiza bilioni 4.7 ikiwa ni ongezeko la bilioni 1.1 zaidi kwa muda mchache.

Alisema matumizi ya mitandao ya simu imerahisisha ulipaji wa kodi na kuweza kutokomeza kabisa vishoka tangu mfumo huo uanze kutumika nchini Tanzania.
 
Aidha alisema TRA imetoa muda hadi Novemba 15 mwaka  huu kwa  wafanyabiashara wote nchi nzima kununua mashine za kutolea risiti kutokana na kutoa muda mrefu kwa wadau hao kuweza kumiliki mashine huzo.
 
“Wafanyabiashara wote tanzania tumewapa muda mrefu sana wa kuweza kumiliki mashine za kutolea risiti hivyo hadi novemba 15 mfanyabiashara yoyote ambaye hana mashine hizo atachukuliwa hatua za kisheria na kulipishwa faini” alisema Kayombo

Alisema baada ya  kupita  Novemba 15 mwaka  huu TRA itafanya msako mkali kwa  wale  wote  watakaoshindwa kununua mashine  hizo na  wale ambao wamenunua mashine  hizo na kushindwa kuzitumia watahusika katika mkumbo huo wa sheria kuchukua mkondo wake.
 
Alisema  kuwa mashine  hizo  za utoaji risiti zitasaidia  serikali katika  kukusanya mapato na zitamsaidia mfanyabiashara  kutunza  kumbukumbu  zake na kuepuka  kuibiwa na  wafanyakazi wake  wasio waaminifu.

Kayombo TRA   itaendelea  kuboresha  ulipaji kodi na kuwa lazima  wafanyabiashara  kutambua kuwa suala la ulipaji kodi ni wajibu na sio adhabu kama ambavyo wafanyabiashara wengi wanachukulia ni unyanyasaji.
 

Rais Kikwete afungua ubalozi wa Heshima San Francisco.

$
0
0
                                                                  
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Heshima wa Tanzania jijini San FranciscoMh.Ahmed Issa,(wapili kushoto) muda mfupi baada ya kufungua ofisi za ubalozi wa Tanzania jijini San Francisco nchini Marekani leo jioni.Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula na kulia ni mke wa balozi Ahmed Mama Sherry julin Issa.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi ofisi ya ubalozi wa heshima(Honorary Consulate) wa Tanzania jijini San Francisco nchini Marekani leo jioni.Kulia ni Balozi wa heshima wa Tanzania jijini San Francisco Mh.Ahmed Issa na kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula na wapili kushoto ni Mke wa Balozi Mama Sherry Julin Issa.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya Watanzania waishio jijini San Francisco Marekani muda mfupi baadaya kufungua ubalozi wa heshima wa Tanzania na kuzungumza nao leo jioni.
 Rais Dkt.Jakaya MrishoKikwete akizungumza na baadhi ya Watanzania waishio jijini San Francisco Marekani leo jioni.Rais Kikwete yupo nchini Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine atahutubia kikao cha 68 cha Umoja wa Mataifa Jijini New York Marekani(picha na Freddy Maro). 

VITUO VYA MIZANI YA BARABARANI MKOANI IRINGA KUCHUNGUZWA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mbaye yuko katika ziara ya kikazi mkoani Iringa ameagiza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu utendaji wa vituo vya mizani mkoani Iringa. Agizo hilo lilitolewa katika mkutano ambao Waziri huyo wa Ujenzi alikutana na wafanyakazi wa taasisi zinazosimamiwa na Wizara ya Ujenzi mkoani humo.


Meneja wa Tanroads wa mkoa wa Iringa Injinia Poul Lyakurwa alimtaarifu Waziri Magufuli kuwa kiasi cha Shilingi milioni 31.9 kilikusanywa katika kipindi hicho cha mwezi mmoja.


Akishitushwa na kiwango hicho Waziri Magufuli  alibainisha kuwa, kiasi hicho kilichosomwa katika taarifa kimetokana na magari 735 yaliyokamatwa kati ya magari 20,700 yaliyopimwa sawa na asiliamia 3.5.

“Takwimu hizi sizikubali kwani wastani wa magari yanayokamatwa katika nchi nzima unakaribia asiliamia 40 iweje barabara kuu kama hii iwe na kiwango kidogo kiasi hicho cha magari yaliyokutwa na makosa” hapa ni lazima pafanyike uchunguzi” alisisitiza Mheshimiwa Magufuli na kueleza kuwa hali hiyo hawezi kuiruhusu hata kidogo kuendelea.


Katika hatua nyingine Waziri Magufuli amempongeza Meneja huyo wa Tanroads kwa kufukuza wafanyakazi 18 katika Kituo cha Mizani cha Makambako kwa kutokuwa waaminifu katika kazi zao. Waziri huyo wa Ujenzi aliendelea kubainisha kuwa, takriban asilimia 70 ya wafanyakazi waliokuwa katika vituo mbali mbali vya mizani ya barabara nchi nzima wamebadilishwa baada ya kukamilika kwa zoezi la kutangaza nafasi hizo upya.


Akisisitiza zaidi, Waziri Magufuli alisema “Wizara ya Ujenzi itaendelea kushirikia na taasisi mbali mmbai zikiwemo PCCB, Jeshi la Polisi, TRA na hata kwa kutumia makondakta na wasaidizi katika magari ya usafirishaji ili kuendelea kubaini mbinu mbali mbali ambazo zinaendelea kutumika katika suala zima la vitendo vya rushwa katika vituo vya mizani hapa nchini”.


Kwa upande mwingine Wakala wa Majengo Nchini pamoja na Wakala wa Ufundi na Umeme wametakiwa kuwa wabunifu ili waweze kukabiliana kikamilifu na changamoto mbali mbali zinazowakabili.

Katibu Mkuu wa CCM aapishwa uchifu Machibola

$
0
0
 Kinana asimikwa kuwa Chifu Machibola katika kijiji cha  migato katta ya Migato wilaya ya Itilima,Katibu Mkuu leo yupo wilaya ya Itilima kukagua na kuimarisha uhai wa Chama na kusimamia ilani ya Uchaguzi ya CCM
Katibu Mkuu akinywa maji kwa kwa Upeyu .Picha na Adam Mzee
Katibu mkuu akila chakula cha kimila cha kisukuma kinafahamika kama Michembe.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images