Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

KUTANA NA SAMAKI ANAYE TUMIKA KAMA DAWA KANDA YA ZIWA

$
0
0
Dkt. Ngwatya mganga wa jadi na miti shamba aliyerithishwa tangu mwaka 1984 akiwa na umri wa miaka 25-30, mkononi akiwa ameshika samaki wa dawa aitwaye 'Shilonge'.
 Licha ya Ziwa Victoria kutumika kama moja ya njia za usafiri kupitia vyombo vya usafiri majini, kuzalisha samaki watamu aina kwa aina huku maji yake yakitumika kama lishe kwa wanyama (akiwemo binadamu),  mimea na huduma kwa viwanda.


Kuna samaki aitwaye 'Shilonge' hili ni jina toka kwa watu kabila la Wasukuma (Sukuma) samaki ambaye hutumika si kwa chakula bali kama dawa.



Sifa kuu ya samaki huyu (Shilonge) ni kuwa hakai tumboni ni sumu kwa samaki wengine, akiliwa na samaki anatoka mzima mzima kama alivyo hivyo samaki wengi wanaokula samaki wenzao kama vile Sangara humkwepa samaki huyu.



Ili atumike kama dawa, samaki huyu hukaushwa juani kisha husagwa na kuwa kwenye form ya unga, ambao ndiyo dawa akinywa mtu anasafisha tumbo na kuondoa sumu nyinginezo mwilini. (Zaidi Bofya Play kusikiliza)


Samaki Shilonge kwa ukaribu zaidi...

Dawa nyingine zinazouzwa hapa kwa mujibu wa Dkt. Ngwatya anasema kuwa ni pamoja na dawa ya kuvuta bahati iitwayo 'Samba', dawa za kumvuta mpenzi, kuvimba miguu, chango la uzazi, pumu na kadhalika na kadhalika......

Chachandu. na bangili..

Nilikutana na mdau huyu katika mnada wa kata ya Lugeye wilayani Magu mkoani Mwanza kama vipi mzukie upate ukitakacho...Umefuraaaaaaahi mwenyewe..By G SENGO.

Diamond Platinumz aingia mkataba na Vodacom Tanzania

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa offer ya miito ya simu jijini Dar es Salaam. Kupitio ofa hio, wateja wanaweza kuchukua wimbo wa Diamond Platinumz kama Ring Back Tone (RBT) na wajishindie Tsh50,000 kwa siku. Kushoto ni msanii wa muziki ya kizazi kipya, Diamond Platinumz na kulia ni Meneja wa Mahusiano ya Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim.
Msanii wa muziki ya kizazi kipya Diamond Platinumz (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa offer ya miito ya simu jijini Dar es Salaam. Kupitia ofa hio, wateja wanaweza kuchukua wimbo wa Diamond Platinumz kama Ring Back Tone (RBT) na wajishindie Tsh50,000 kwa siku. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (katikati) na kulia ni Salum Mwalim, Mejena wa Mahusiano ya Nje, Vodacom Tanzania.
Msanii wa muziki ya kizazi kipya Diamond Platinumz (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, punde baada ya kusaini mkataba utakaowezesha wateja kuchukua wimbo wa Diamond Platinumz kama Ring Back Tone (RBT) na wajishindie Tsh50,000 kwa siku. Anayeshuhudia ni Salum Mwalim , Mejena wa Mahusiano ya Nje, Vodacom Tanzania.
Msanii wa muziki ya kizazi kipya Diamond Platinumz (mwenye fulana nyekundu) akiucheza wimbo wake mpya ujuikanao kama My Number One, wakati wa uzinduzi wa mkataba utakaowezesha wateja kuchukua wimbo huo kama Ring Back Tone (RBT) na wajishindie Tsh50,000 kwa siku. Mkataba huo ni baina ya Diamond Platinumz na Vodacom Tanzania.

music system Sony inauzwa

$
0
0
 Nauza Used music system Sony kwa mawasiliano unaweza kuwasiliana kwa number 0768808819 ama kwa email misasophie@yahoo.com


SHIWATA YAKABIDHI NYUMBA ZA WANACHAMA WAO KWA AJILI YA MAKAZI

$
0
0
Mchezaji na Kepteni wa zamani wa Timu ya  Taifa Stars, Jella Mtagwa (kushoto) akipokea cheti cha nyumba aliyokabidhiwa na SHIWATA na eneo la robo ekari ambalo anatarajia kujenga nyumba kubwa
Mwanachama huyu wa SHIWATA kulia ameamua kujijengea nyumba yake pole pole hapa akikabidhiwa cheti chake
Mmoja wa wanachama wa SHIWATA, Emmanuel Ntumbii na mkewe wakipokea cheti cha kumilikishwa nyumba yake akishuhudiwa na wanachama wenzake.
Mwandishi wa Habari, Josephine Joseph akionesha cheti alichokabidhiwa na SHIWATA mbele ya nyumba yake katika sherehe ya kukabidhi nyumba za wasanii,Mkuranga.
Mkuu wa wilaya mstaafu, Bw. Henry Clemence akizungumza katika sherehe ya kukabidhi nyumba 38 za wasanii wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga.

MAJIBU YA REGINALD MENGI JUU YA GESI

$
0
0
Septemba 7, 2013 nilipokea barua pepe (email) yenye kichwa cha habari kisemacho “ubinafsi/ufisadi wa MENGI na Chuki/Fitina kwenye Maendeleo”.  Aliyetuma email hiyo alijitambulisha kama “CCM TANZANIA” na email ilisambazwa kwa vyombo vya habari, waandishi na watu wengine wengi wakiwamo wanasiasa. Kabla ya hapo nilifowadiwa nakala ya ujumbe (SMS) na watu ambao walitumiwa na Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge inayosema;



“Ambieni Watanzania: Kampuni za Mengi zimeshikilia vitalu 59 vya madini vyenye ukubwa wa mita za mraba 3,752.37 (sq km) Amevishikilia, ameshindwa kuviendeleza. Watanzania wanakosa mapato na ajira! Sasa anataka vitalu vya gesi na mafuta. Je huu ndio uzawa?|


Na

“Mengi hana uzawa bali ubinafsi. Anataka kufanya udalali wa vitalu vya raslimali zetu. Waelezeni Watanzania ukweli huu.”


Vile vile Septemba 5, 2013 Profesa Muhongo akijibu swali la Mwandishi wa habari lililouliza;

“Mhe. Waziri tunataka ufafanuzi kuhusu kauli yako ya hivi karibuni kwamba waTanzania hawana uwezo wa kuwekeza katika uwekezaji wa gesi asilia. Kwanza kauli hii ni kweli? Pili kauli kwamba   Watanzania wanaweza kuwekeza kwenye sekta ya machungwa tu huoni kwamba si kwamba unawavunja moyo bali unadhalilisha wewekezaji wazalendo?”


Na Profesa Muhongo akajibu:

“Kila mtu alitoa mawazo ya sera ya gesi wakiwemo TPSF. Mengi na wenzake wanataka vitalu wafanye ulanguzi wa gesi na mafuta yetu. Tutatoa orodha ya vitalu vya madini vilivyoko mikononi wa Mengi ambavyo anafanya ulanguzi. Ukweli utaonyesha ubabaishaji na ulanguzi wa Mengi wa genge lake.”


Nimeona ni vyema nitumie haki yangu ya kujibu (right of reply), lakini kwa wale wanaohusika kusambaza taarifa hizo kuchafua jina langu wajue kwamba kujibu kwangu hakuondoi haki yangu ya kuchukua hatua za kisheria.

Kuingizwa kwa vitalu vya madini katika hoja ya gesi
Huo ni upotoshwaji wenye lengo la kututoa kwenye hoja ya msingi ya rasilimali yetu ya gesi. Sijawahi kufanya udalali kwenye vitalu vya madini. Huu ni uongo wa hali ya juu.

Tamko la TPSF na majibu ya Profesa Muhongo
Siku ya Agosti 28, 2013 Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) ilifanya kikao chake cha Bodi na baadaye kufanya mkutano na waandishi wa habari. Mambo mengi yalizungumzwa katika kikao hicho ikiwa ni pamoja na uwezeshaji wa Watanzania (Economic Empowerment).

Kuhusu uwezeshaji Watanzania, mambo muhimu matatu yalijadiliwa na kutolewa mapendekezo. Mambo hayo ni 1) Manunuzi ya Umma (Public Procurement); 2) Ardhi na uvuvi; na 3) suala la gesi asilia.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari, mimi nikiwa Mwenyekiti wa TPSF, niliwasilisha maoni ya TPSF kuhusiana na Manunuzi ya Umma, wakati Makamu Mwenyekiti wangu, Salum Shamte, aliwasilisha maoni yetu kuhusiana na sekta ya ardhi na uvuvi na mwishoni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye, aliwasilisha maoni TPSF kuhusiana na gesi asilia.

Katika maoni yake TPSF ilisisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa Watanzania katika uchumi wa gesi na kushauri kusitishwa ugawaji wa vitalu vya gesi hadi hapo sera ya gesi itakapokua tayari. Mwisho Bwana Simbeye alisema kwamba TPSF itaomba kukutana na Profesa Muhongo kuwasilisha mawazo na mapendekezo ya taasisi hiyo.


Siku chache baada ya TPSF kutoa maoni yake mambo mawili yalitokea. Kwanza Profesa Muhongo alijibu kupitia vyombo vya habari kwamba mpango wa kugawa vitalu vya gesi na kuingia mikataba utaendelea. Profesa Muhongo pia alisema wazi kwamba hana mpango wa kukutana TPSF, kwani kufanya hivyo ni kupoteza muda.

Matokeo yake Profesa Muhongo hajajibu hoja kuhusiana na barua aliyoandikiwa na TPSF. Binafsi nilishitushwa na msimamo wa Profesa Muhongo kwani Serikali ya awamu ya nne imepiga hatua kubwa katika kudhihirisha kuwa ni “serikali sikivu”. Ingemgharimu nini Profesa Muhongo kukaa na kutusikiliza? Hakuna ambacho angepoteza zaidi ya dakika chache za muda wake.
Jambo la pili ambalo lilitokea ni mimi binafsi kushambuliwa kana kwamba maoni yaliyotolewa kuhusiana na gesi ni maoni yangu binafsi na si ya TPSF.
Mifano ya mashambulizi dhidi yangu ni kama nilivyoonyesha hapo juu katika email na ujumbe mfupi wa simu (SMS).
Msimamo wa Profesa Muhongo katika gesi ni upi?
Msimamo wa Profesa Muhongo mara baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini ulikuwa ni kutaka kupitishwa kwanza kwa sera ya gesi asilia kabla ya kuendelea na ugawaji wa vitalu vya gesi.
Septemba 2012, Profesa Muhongo alisema;

“Some of the agreements are really shoddy and they need to be revoked” and “I can’t tolerate agreements which are not in the country’s interests but they benefit a few individuals”.
Tafsiri yake ni:

“Baadhi ya mikataba ni ya ovyo, na inahitaji kuvunjwa” na “Sitovumilia mikataba ambayo haina maslahi kwa nchi na inawanufaisha wachache”. 
Baada ya hapo, Profesa Muhongo aliamrisha Bodi mpya ya TPDC kusitisha ugawaji wa vitalu vya gesi ambao ulipangwa kufanyika mwezi Septemba 2012 na kupitia upya mikataba yote. Profesa Muhongo alinukuliwa akisema:

‘Earlier this month, the state-run Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) delayed a licensing round for nine deep-sea oil and gas blocks previously set for this month until a parliamentary vote on a new gas policy in October. "Right now as a country, we are in the gas boom and we don't have gas policy in place.”


[…]


Recent gas strikes off east Africa's   seaboard have led to predictions the region could become the third largest exporter of natural gas on the planet.


"Our country is reviewing its policy. Is that something new?" he said. "We want both the companies that are investing in the country and Tanzanians to benefit from the oil and gas projects."


[…]


"This is completely new business to us. We are learning," Muhongo said.’

Tafsiri yake ni:



‘Mwanzoni wa mwezi huu TPDC ilihairisha mchakato wa ugawaji wa vitalu tisa vya gesi asilia vilivyoko baharini hadi hapo Bunge litakapopitisha sera mpya ya gesi iliyowasilishwa bungeni mwezi Oktoba;
"Kwa sasa kama Taifa, tuko katika mazonge ya gesi na hatuna sera ya gesi. 
"Nchi yetu inaandaa sera (ya gesi). Hicho ni kitu kipya?..." 
"Tunataka kampuni zote, kampuni zinazowekeza nchini mwetu na Watanzania tunufaike na miradi ya gesi na mafuta."
"Hii  ni biashara mpya kabisa kwetu. Tunajifunza."


Zoezi wa la kugawa vitalu vya gesi asilia lilisitishwa lakini hadi sasa matokeo ya kupitia upya mikataba hayajatolewa hadharani.
Miezi michache baadaye, Februari 26, 2013, Profesa Muhongo alisisitiza msimamo wake wa kutaka Tanzania kuwa na sera ya gesi kabla ya kugawa vitalu zaidi. Aliyasema hayo alipokua akihutubia mkutano uliofanyika Chatham House, mjini London. Mkutano huo uliopewa jina “Tanzania: An Emerging Energy Producer”. Ulikuwa na madhumuni ya:

“Tanzania is drawing growing attention as a pivotal country in East Africa for oil and natural gas exploration, having led the region in terms of new discoveries of natural gas in 2012. With known gas reserves of approximately 7.5 billion cubic feet, the potential to transform Tanzania's international standing and domestic electricity production is considerable. However, recent protests against the construction of a pipeline to Dar es Salaam highlight the challenges that Tanzania faces in ensuring that the benefits of its natural resources are widely felt.

Tafsiri yake ni:

“Tanzania inaonyesha kuja juu katika Afrika Mashariki kwa uvumbuzi wa mafuta na gesi asilia baada ya kuongoza kwa uvumbuzi wa gesi asilia mwaka 2012. Ikiwa na wastani wa futi za ujazo bilioni 7.5, ni dhahiri itasaidia Tanzania kupaa katika anga za Kimataifa na kusaidia uzalishaji wa umeme kwa matumizi ya ndani. Hata hivyo, vurugu za hivi karibuni kupinga ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam inaashiria changamoto mpya ambazo Tanzania sasa inakabiliana nazo kuhakikisha kwamba manufaa ya gesi asilia yanawafikia watu wengi zaidi wa chini.”

Alichowasilisha Profesa Muhongo katika mkutano huo kwa ufupi kinapatikana katika tovuti hii;
Kama inavyonekana kwenye kiambatanisho, moja ya nyaraka aliyowasilisha Profesa Muhongo inaonyesha kwamba mchakato wa kuanza ugawaji wa vitalu ungeanza baada ya kupitishwa kwa sera ya gesi.
 Hadi sasa hatuna sera ya gesi asilia.
Lakini jambo la kushangaza, Profesa Muhongo amebadilika na anataka vitalu vigawiwe kabla ya kuwapo kwa sera gesi.
Sababu za kubadilika kwa Profesa Muhongo hazina mashiko
Profesa Muhongo amenukuliwa na gazeti la Daily News la Agosti 31, 2013 akieleza sababu zake za kutaka vitalu vigawanywe kabla ya kupitishwa kwa sera ya gesi. Sababu kuu alizozisema ni tatu; (1) Ushindani wa soko na majirani zetu akitolea mfano wa Msumbiji (2) Sheria ya mwaka 1960 iliyoanzisha TPDC na Sheria ya Petroli ya mwaka 1980 kwamba zinatosha kusimamia ugawaji wa vitalu akimaanisha sera na sheria mpya zitafuata baada ya ugawaji wa vitalu; na (3) Watanzania hawana uwezo wa kuwekeza katika sekta hii akimaanisha waachiwe wageni peke yao.
Maelezo kwamba tunashindana na Msumbiji haya halalishi ugawaji vitalu kabla ya sera. Utafiti wa gesi asilia ni jambo linachokua muda mrefu, ndio maana TPDC wanaingia kwenye mikataba ya muda mrefu (isiyozidi miaka 11 kwenye utafiti na miaka 25 kwenye uchimbaji). Kwa hiyo kusubiri miezi michache ili Bunge letu liidhinishe sera, haiwezi kuathiri ushindani wa kibiashara. Hata nchi Msumbiji anayoizungumzia hivi sasa inapitia upya mpango wake wa uwekezaji katika gesi asilia na kuingiza sera na sheria mpya zitakazo simamia rasilimali hiyo. Katika mahojiano yaliofanyika na jarida la Africa Report mwezi Julai mwaka huu, Naibu Waziri wa Nishati wa Msumbiji, Mh. Abdul Razak Noormahomed, alisema madhumuni ya mabadiliko hayo ni kuwapa kipaumbele wananchi wa Msumbiji.
Mohojiano haya yanapatikana katika anuani ifuatayo:
Kama nilivyoeleza hapo juu, mara baada ya Profesa Muhongo kuingia wizarani alisema kinaga ubaga kwamba sheria iliyopo haikidhi mahitaji ya sekta ya gesi asilia ndiyo maana akasimamisha ugawaji wa vitalu vya gesi na kuamrisha mikataba ipitiwe upya na sera ipatikane. Leo tunashuhudia Profesa Muhongo akila matapishi yake na kusema kwamba sheria zile zile alizoziponda sasa zinafaa.
Kauli ya Profesa Muhongo kwamba wafanyabiashara wa Tanzania wanaweza tu kushiriki biashara ya juisi na soda na hawana uwezo wa kushiriki katika biashara ya gesi yao ni dharau.
Kigezo gani Profesa Muhongo anatumia kutoa kauli ya jumla yenye kutawaliwa na hisia? Amefanya utafiti gani kupima uwezo wa kifedha wa wafanyabiashara wa kitanzania? Kwa taarifa yake, wapo wafanyabiashara wengi ambao wanaweza kupata fedha kwa ajili ya kuchimba visima vya gesi. 
Ni dhahiri kwamba Profesa Muhongo anathamini tu kampuni za kigeni, anasahau kwamba kuna mifano ya kuwapo kampuni za kigeni ambazo zimekua zikifanya udalali hapa nchini kwa miaka mingi kwenye rasilimali za nchi yetu ikiwa ni pamoja na madini na gesi.
Uzalendo wangu:
Ningependa kupuuza tuhuma kwamba mimi si mzalendo Wantanzania wanafahamu ukweli. Vile vile ningependa kupuuza tuhuma kwamba mimi ni mbinafsi na sipendi maendeleo ya Watanzania wenzangu kwa hili pia Watanzania wanafahamu ukweli
Kuhusu Kilimanjaro Hoteli na mgogoro na Yussuf Manji n.k, mtizamo wako unategemea wewe upo katika kundi lipi kati ya kundi safi la waadilifu au kundi chafu la wala rushwa. Watanzania wanafahamu msimamo wangu kwenye hili.
Mimi sipingi kuwepo kwa wawekezaje wageni katika sekta ya gesi lakini kuna mambo mawili napigania. Kwanza Watanzania wanufaike na rasilimali yao ya gesi na pili iwepo sera ya gesi inayotoa kipaumbele kwa Watanzania
Mimi napenda maendeleo ya nchi yangu; kwa hiyo hata siku moja siwezi kupinga uwekezaji ama ubia na wawekezaji. Ninachosimamia ni manufaa kwa nchi yangu.
Tuhuma kwamba nafanya kampeni dhidi ya wizara
Tuhuma kwamba nimeandaa kongamano kwa ajili ya vijana wa Chadema si za kweli. Huu ni uzushi usio na kichwa wala miguu. Vile vile madai kwamba naitumia vibaya vyombo vya habari vya IPP Media si ya kweli hata kidogo ikizingatiwa kwamba hata mahojiano ya Profesa Muhongo kwa simu akiwa Austria, yalirushwa na kituo cha redio cha Radio Stereo kinachomilikiwa na kampuni yangu ya ITV-Independent Television Limited.
Hitimisho
Julai mwaka huu, Rais wa Marekani Barack Obama, alihitimisha ziara yake ya Kiserikali nchini Tanzania, kwa kusema;

“Ultimately the goal here is for Africa to build Africa for Africans.”



Akimaanisha kwamba, Hatimaye Lengo ni Africa kujenga Africa kwaajili ya Waafrica

                                                        
Profesa Muhongo asipingane na ushauri huu mzuri.
Nimalizie kwa kuwahakikishia Watanzania kwamba mashambulizi binafsi dhidi yangu yenye nia mbaya ya kunishushia heshima hayatakaa yafanikiwe.
Wenu,

Dk. Reginald A. Mengi

JENGO LA SHAMO TOWERS SASA LIMEFUNGULIWA

$
0
0
JENGO LA SHAMO TOWERS SASA LIMEFUNGULIWA NA UNAWEZA KUPATA HUDUMA ZIFWATAZO:

- Huduma  za ki Benki - STANDARD CHARTERED & DIAMOND TRUST BANK
- ATM machines - FNB, ECO BANK, STANBIC, STANDARD CHARTERED, DIAMOND TRUST BANK
- Huduma za afya na pharmacy  - AGAKHAN MEDICAL CENTRE.
- Boutiques za kisasa 
- Baby shop & Gift Shops- FUN ZONE & BABY VILLAGE
- Electronics and IT shop - HTC
- Huduma za internet - Smile communications
- BOOGIE WOOGIE Coffee Shop & fast food restaurant. Open from 8am to 10pm at night
- stationary Shops.
- Furniture shop- FURNITURE CENTRE
Dry cleaners -3 SECONDS DRY CLEANERS
- Legal Aid - GRACE ATTORNEYS
 
-VILLAGE SUPERMARKET, BUREAU DE CHANGE & VODASHOP- KUFUNGULIWA HIVI KARIBUNI
 
TEMBELEA SHAMO TOWERS KWA MAHITAJI YAKO YOTE.

SHAMO TOWERS ipo Mbezi Beach, karibu na tangi bovu. 
 
Kwa maelezo zaidi juu kupangisha Ofisi au maduka piga namba zifwatazo:
 
Mobile: 0713-472200 or 0777-472200
 
au
 Tembelea ofisi za Shamo Towers ambazo zipo ghorofa ya kwanza kwenye jengo hilo.

TAMASHA LA VIPAJI VYA WASANII MBALIMBALI KUFANYIKA OKTOBA

$
0
0

African Star Entertainment – ASET  ikishirikiana na  studio ya  Fleva   Inc  Audio Records and Video Production   Pamoja na Makubi Sports Promotion imeandaa Tamasha la vipaji vya Wasanii wa fani  mbalimbali  za sanaa kwa Wasanii ambao bado hawajapata fursa ya kutoka na kufanikiwa kupitia sanaa zao, tamasha hilo linatarajiwa kufanyika katikati ya mwezi  Octoba ambalo litaitwa  Tamasha  la  Vipaji  2013.

Ndugu Waandishi , Malengo mahsusi ya Tamasha  la Vipaji  2013   ni kuvionesha vipaji mbalimbali vya Wasanii ambao bado hawajapata fursa ya kuonekana  pia kuhamasisha, kuendeleza na kulinda  vipaji vya wasanii  hao ili vipawa hivyo viwe ni sehemu ya nyenzo muhimu ya ajira za uhakika  katika maisha ya vijana mbalimbali ambao wamejiingiza katika taaluma ya sanaa. Tamasha hili pia litasaidia ukuzaji wa ajira za Wasanii mbalimbali  wataojitokeza.

Ndugu Waandishi, walengwa wakuu wa Tamasha  la Vipaji  2013 ni
Wasanii wa Maigizo ya jukwaani (Matangazo , Filamu & Tamthilia),Wasanii wa Vichekesho,Wasanii wa Muziki Bongofleva (R & B, Raga, Hiphop n.k),Wasanii wa Kupiga na kucheza Ngoma za Asili,Wasanii wa kucheza muziki wa Wasanii wa ndani au nje ya nchi,Kucheza show za nyimbo mbalimbali za ndani na nje Kuigiza Sauti za watu mbalimbali walio maarufu wa hapa Tanzania,Kuigiza kazi za Watangazaji maarufu wa vipindi vya Radio na Televisheni vya Tanzania.

Wasanii wa Ubunifu wa michoroWasanii wenye vipaji vya utangazaji wa vipindi vya radio na televisheni,pamoja na wale wa Sanaa za maonesho ya mavazi

Ndugu Waandishi,Wasanii wataofanya vizuri katika tamasha hilo wapata fursa ya kufanya kazi (lebo) na Studio ya Fleva Inc Record, pia kushiriki katika kazi zinazoandaliwa na ASET ikiwemo filamu, tamthilia kuimba ,kucheza dance n.k. Pamoja na pia tunakaribisha kampuni /taasisi mbalimbali kusaidia kufanikisha tamasha hili pamoja na kuwasaidia Wasanii hawa  kufikia malengo

Ndugu Waandishi,Fursa hii ni adimu kwa Wasanii wengi hivyo Wasanii wanaohitaji  kushiriki wafike Ofisi za ASET au Fleva Inc Studio zilizopo Ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni  kwa ajili ya Kujiandikisha, mwisho wa kujiandikisha ni  tarehe 30 Septemba 2013 saa kumi jioni,tamasha linatarajiwa kufanyika 21 Octoba 2013 katika Ukumbi wa Vijana Hall uliopo Kinondoni mjini Dar es Salaam.

Nawashukuru  kwa  usikivu wenu tunaomba ushirikiano.

W.R  MAKUBI
Project Meneja

Kwa  Niaba
ASHA  BARAKA
Mkurugenzi
  ASET/FLEVA  INC RECORDS.

Global Publishers wachangia milioni 15 Ujenzi wa Mabweni

$
0
0
Mkurugenzi wa Global Publishers, Masha Bukumbi akimkabidhi mfano wa hundi hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Rosemary Lulabuka. Kulia ni Meneja Mkuu wa Global Publishers Abdallah Mrisho, na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Ukuzaji Rasilimali (TEA), Sylvia Gunze.
Masha Bukumbi akimkabidhi Rosemary hundi halisi.
Bukumbi akiwashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha tamasha hilo na kueleza jinsi walivyotimiza ahadi ya kuisaidia elimu hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa TEA akitoa shukrani baada ya kupokea hundi hiyo.


Na Richard Bukos.
Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Amani, Ijumaa, Championi, Risasi na Ijumaa Wikienda leo imeikabidhi Mamlaka la Elimu Tanzania (TEA) kiasi cha shilingi milioni 15, ambazo ni sehemu ya mapato yaliyopatikana kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Julai 7 mwaka huu.'



Akipokea hundi ya fedha hizo kutoka kwa Mkurugenzi wa Global Publishers, Masha Bukumbi, Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Rosemary Lulabuka aliishukuru kampuni hii kwa uchangiaji huo na kuziomba kampuni, taasisi, watu binafsi na wadau wengine kuiga mfano huo. Rosemary amesema mpaka sasa mfuko wa mamlaka hiyo umekusanya jumla ya shilingi milioni mia tano na kuwashukuru wadau wote waliochangia ambapo kiasi hicho cha fedha kinatarajiwa kuanza kutumika hivi karibuni kwa kujenga mabweni 30, ya Shule ya Sekondari ya Kibaigwa ambayo yatatumika na wanafunzi wapatao 1504.



Mkurugenzi huyo ameiomba Kampuni ya Global Publishers kuliendeleza tamasha hilo kila mwaka na kuwaomba wadau watakaoshirikishwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwani lengo lake kuu ni kukuza elimu hapa nchini jambo ambalo ni ukumbozi wa taifa letu.

(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL)

wachezaji watakaoshiriki miachuano ya Airtel Rising stars nchini Nigeria wakabidhiwa daruga

$
0
0
 Afisa uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde Akikabithi viatu vya kuchezea mpira kwa wachezaji watakaoshiriki miachuano ya Airtel Rising stars nchini Nigeria itakayoanza jumatatu wiki ijayo na kushirikisha nchi 17 barani Afrika, wakipokea vifaa hivyo ni makaptani wa  timu hizo  Athanas Mdam na Stumai  Athumani. wa pili kushoto ni kocha wa timu ya wavulana ya Airtel Rising Stars Abel Mtweve

 Afisa uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde Akikabithi viatu vya kuchezea mpira  kamptaini wa timu ya kike Stumai  Athumani wakati Airtel ilipogawa vifaa kwa timu itakayosafiri kwenda kwenye michuano ya Airtel Rising stars Nchini Nigeria, Michauno hiyo itashirikisha nchi 17 barani Afrika, wakishuhudia ni kikosi cha timu ya Airtel Rising stars Tanzania

 Baadhi ya wachezaji  watakaoshiriki miachuano ya Airtel Rising stars nchini Nigeria wakijaribu viatu mara baada ya kukabithiwa vifaa vya michezo na Airtel kwaajili ya  miachuano ya Airtel Rising stars nchini Nigeria itakayoanza jumatatu wiki ijayo na kushirikisha nchi 17 barani Afrika

Baadhi ya wachezaji  watakaoshiriki miachuano ya Airtel Rising stars nchini Nigeria wakijaribu viatu mara baada ya kukabithiwa vifaa vya michezo na Airtel kwaajili ya  miachuano ya Airtel Rising stars nchini Nigeria itakayoanza jumatatu wiki ijayo na kushirikisha nchi 17 barani Afrika

Dr Maria Kamm Public Lecture on Girls' Education

$
0
0
When you speak about Weruweru Girls School,you directly speak of Dr Maria Kamm. She is the iconic woman who glorified that school and groomed hundreds of today's strong women in Tanzania,in various fields. The likes of Dr Asha Rose Migiro, Dr Mary Nagu, Ambassador Zainab Maajar, Hellen Kijo-Bisimba and so many more! She is the reason why many of us had that golden chance to have our foundation made in concrete.
 Today from 10a.m at the Julius Nyerere Conference Hall, Dr. Kamm gave a Public lecture on "The Power of Educating the Girl Child", a gathering that was attended by hundreds of Weruweru Alumni and members of the public.
 It was epic!!
 One of Weruweru Alumni Foundation committee member,June...rocking a blazer made out of  the Weruweru Golden Jubilee khanga .
 Mama Kamm was estounded by the love in the conference hall....
 Seeing many of her students,all grown up now and holding high positions in the society.
 Among many of her points, Dr Kamm insisted that, no one will change our education system in Tanzania BUT Tanzanians ourselves. She stressed the fact that, educating a girl and grooming her from her tender age is equal to educating the other half of the population for the development of the country.
 " Weruweru brought up competitive,innovative,respective and time conscious ladies,and I am proud of all of you"she said.


 Let's just say,it was a very emotional get together for many Weruweru alumni

 "The role of a woman remains the same,no matter how educated she is. But we need to have equal opportunities among us"..she added. According to Dr Kamm, in 1954,only 9 girls graduated their Form Two level,which was the highest level then...and She was among those. However,there were discrimination on women in terms of salaries...and even the girls' certificates were marked "Women education certificate"


 The moderator of the symposium was Dr Mwele Malecela,a Weruweru product and now Director General of NIMR.
 Ambassador Zainab Maajar who is the chairperson of the Weruweru Alumni Foundation committee for the Golden Jubilee introduced some of the influential Weruweru alumni who were present at the event.



 BOT was also present and they communicated to all guests on the Mwl Nyerere Foundation scholarship which sponsors girls studying Mathematics and Science. The scholarship involves payments of all costs,living expenses and a laptop,for undergraduate students...and a partial scholarship for Masters
 We also sang the Weruweru school song!! Can you imagine,Dr Kamm remembers every word of the song and she sang along,throughout!

 Until the ed of the symposium,it was clear that,Alumni of all schools in Tanzania have responsibilities to bring back and develop the quality of the education provided by their schools. Weruweru Alumni Foundation has been formed to do just that.
 The issue of Girls' pregancies while in school was also discussed. Mama Kamm advised for both parents and teachers to find means of helping these children finish their education,regardless.

 Teachers lacking the passion for their job was found as one of the problems in Tanzania's education. As one of the guests pointed out,many of our current teachers chose the field only because of the University Loans provided...

 And ...that marked another highlight on the Weruweru Golden Jubilee! For videos of the various occasion of this event,visit our Youtube page,Missie Popular.
 If you are on Twitter, search for #Weruweru50 to read all the points discussed in this symposium.

 Ooooppss...the Khangas,Mugs,T shirts of all Weruweru colors are already on sale!
 Can you spot Mama Sambaya? :))...the mugs come in various designs and colors...
Come for the Sunday meeting at Cine Club from 3p.m (Saa Tisa Alasiri) and get your khanga, Tshirt and/or mugs....

See you all,on Sunday 15th,Septermber....Cine Club

xoxo

onyesho maalum la kumuaga Mwanamuziki mkongwe hapa nchini,Maalim Gurumo kufanyika Oktoba 11 Diamond Jubilee, jijini Dar.

$
0
0
Mwenyekiti wa kamati ya kumuenzi Muhidin Maalim Gurumo, Asha Baraka, akizungumza jambo katika kutambulisha onyesho maalum la Gurumo litakalofanyika Oktoba 11 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam. Anayefuata upande wa kushoto wa Asha ni mzee Muhdini Gurumo, Juma Mbizo, na Said Kibiriti.
Asha Baraka na wanakamati katika kutambulisha onyesho maalum la Gurumo litakalofanyika Oktoba 11 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam. Anayefuata upande wa kushoto wa Asha ni mzee Muhdini Gurumo, Juma Mbizo, Cosmas Chidumule na Said Kibiriti. Kulia ni Katibu wa kamati Saidi Mdoe
Juma Mbizo, mratibu wa shoo hiyo, akionyesha mfano wa cd itakayouzwa ikiwa ni juhudi za kumuwekea mazingira mazuri mwanamuziki Muhdini Gurumo, baada ya kutangaza kustaafu muziki. Picha zote na Kambi Mbwana.
======== ===== =====
MWANAMUZIKI mkongwe aliyestaafu muziki akiwa na bendi ya Msondo Ngoma, Muhidini Maalim Gurumo, ameandaliwa shoo mbili za kumuaga, moja wapo ikipangwa kufanyika Oktoba 11, ikiwa ni VIP, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee. 

Shoo nyingine kwa wapenzi wote itafanyika Novemba Mosi mwaka huu katika Ukumbi wa TCC Sigara Chang’ombe, jijini Dar es Salaam, zote zikiwa na lengo la kumuaga kwa heshima mwanamuziki huyo na kumpa nafasi ya kuyamudu maisha yake baada ya kuachana na muziki. 

 Akizungumza leo na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa shoo hiyo iliyopewa jina la (Gurumo 53), Asha Baraka, alisema kuwa ni heshima kuwa na mwanamuziki kama Gurumo, hivyo wadau wameamua kuandaa shoo hizo za kumtafutia fedha mkali huyo. 

 Alisema wazo hilo limefanyiwa kazi kwa pamoja, akiwa na wadau kadhaa, akiwamo Said Mdoe Katibu wa Kamati hiyo, Richard Sakala mjumbe, Cosmas Chidumule, Waziri Ally, Said Kibiriti na Juma Mbizo, ambaye ndio mratibu wa Kamati hiyo. 

 ”Lengo si kumpa karatasi za kuthamini mchango wake katika tasnia ya muziki wa dansi Tanzania, ila kuhakikisha kuwa anapata mwangaza wa maisha yake baada ya kuachana na muziki. 

 ”Huyu ni mwanamuziki mwenye uwezo wa juu wakati huo, hivyo kwa sasa lazima sisi wadau tuhakikishe anajiweka katika ramani nzuri, ikiwa ni kutambua ataishi vipi nje ya muziki,” alisema. Naye Gurumo aliwaambia waandishi wa habari kuwa ameamua kuachana na muziki kwa sababu umri na afya yake hairuhusu kufanya kazi hiyo, hivyo asitokee mtu wa kupotosha ukweli wake huo. 

 ”Nasikia watu wanasema naachana na muziki Msondo nikiwa na lengo la kurudi tena Sikinde, jambo ambalo si kweli kwa kuwa sioni nitamuimbia nani wakati nimechoka.  ”Naomba kwa sasa kuwapa nafasi watu waliojitolea kunisaidia hasa kwa kuunda kamati hii ambayo nitapanda jukwaani kuimba mara ya mwisho, ukizingatia kuwa kazi yangu inahitaji kuagana na mashabiki wangu jukwaani na si mahali pengine,” alisema. 

 Katika hatua nyingine, mwanamuziki Cosmas Chidumule, alisema kuwa licha ya kuwa ameokoka, ila atapanda jukwaani kuimba na mzee Gurumo kama sehemu ya kutambua mchango wake. ”Nimeokoka lakini si sababu ya kunifanya nishindwe kumheshimu mwanamuziki ambaye nina uhakika mchango wake ulinifanya niwe juu katika muziki wa dansi Tanzania,” alisema.

 Kwa mujibu wa Kamati hiyo ambayo Mdoe ndio Katibu wake, taratibu zote zinaendelea ikiwa ni kuandaa nyimbo alizowahi kuimba na kuziweka katika mfumo wa kibiashara, ikiwamo mpango wa kuuza nyimbo zake katika makampuni ya simu za mikononi.

January Makamba azindua tume ya tehama leo jijiini Dar.

$
0
0
 Mgeni rasmi Naibu Waziri Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba akitoa salamu zake kwa wadau mbalimbali (hawako pichani) waliohudhuria mkutano kabla ya kutoa hotuba yake wakati alipokuwa akizindua rasmi Mkutano wa wadau wa uanzishwaji wa Tume ya TEHAMA uliofanyika leo Peacock Hotels jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Prof. Patrick Makungu na kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dkt. John Mngodo.  
 Baadhi ya wadau mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi wa Mkutano wa wadau juu ya uanzishwaji wa Tume ya TEHAMA wakifauatilia kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi . Mkutano huo umefanyika leo Peacock Hotels jijini Dar es Salaam. 
 Naibu Waziri Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba akijibu maswali mbalimbali toka kwa waaandishi wa habari mara alipomaliza kuzindua rasmi Mkutano wa wadau wa uanzishwaji wa Tume ya TEHAMA uliofanyika leo Peacock Hotels jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba (wa pili toka kushoto mstari wa mbele), wa kwanza wake toka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dkt. John Mngodo. Wa kwanza kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Mawasiliano Bi. Clarence Ichwekelezwa na anayemfuatia ni Katibu Mkuu Prof. Patrick Makungu.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.

======= =====  ======
UZINDUZI WA MKUTANO WA UANZISHWAJI WA TUME YA TEHAMA.

Na Benedict Liwenga-MAELEZO.

12/09/2013.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba amezindua rasmi mkutano wa Washikadua juu ya uanzishwaji wa Tume ya TEHAMA leo jijini Dar es Salaam.¨


Mhe. Makamba amesema kuwa TEHAMA kitakuwa chombo kikubwa ambacho kitashirikisha wadau wengi hapa nchini kwa lengo la kuhakikisha kuwa matumizi ya TEHAMA yanasonga mbele na inatoa fursa mbalimbali zenye kuweza kutatua changamoto za kimaisha kwa watanzania.


Mhe. Makamba aliongeza kuwa TEHAMA ndiyo inaleta mabadiliko na kuleta maendeleo makubwa hivyo amesisitiza juu matumizi ya TEHAMA katika ofisi za serikali na sekta binafsi. Aidha, amewashauri wadau wote kuangalia wenzetu nchi zilizoendelea jinsi wafanyavyo ili kuhakikisha kuwa matumizi ya TEHAMA nchini Tanzania yanasonga mbele. “Kama Taifa hakuna sehemu ambapo tunakutana kutafakari juu hali ilivyo katika matumizi ya TEHAMA hapa nchini”. Alisema Mhe. Makamba.

Kwa upande mwingine Mhe. Makamba alisisitiza juu ya wanataaluma wa TEHAMA wawe wanajulikana na amesema kuwa katika uundaji wa Tume hiyo ni vema wataalamu na ufanisi wa kazi zao ujulikane ili kuepukana na kuwa na wataalamu ambao ni Makanjanja. “Hapa nchini Tanzania hatuna uhakika wa wahitimu katika mambo ya TEHAMA hivyo kuna uwepo wa vyuo na tasisi ndogondogo nyingi zilizosambaa ambazo zinajikita kutoa taaluma hiyo, katika masuala ya TEHAMA ni lazima wataalamu wajulikane na kusajiliwa kama ilivyo katika bodi nyingine za serikali hapa nchini”. Alisema Naibu Waziri.

Aidha, Mhe. Makamba alimalizia kwa kuipongeza Serikali kwa kazi kubwa inayofanya kwa upande wa TEHAMA kwani mpaka hivi sasa nchi imefikia mahali pazuri katika mambo ya mawasiliano pia ameshauri juu ya ushirikishwaji wa sekta binafsi katika uundaji wa tume ya TEHAMA. 

Uzinduzi wa Rock City Marathon awamu ya tano kufanyika Septemba 19

$
0
0
UZINDUZI wa mbio za Rock City Marathon awamu ya tano unatarajia kufanyika tarehe 19 mwezi Septemba mwaka 2013 katika hotel ya New Afrika jijini Dar es Salaam.

Mbio hizo za kila mwaka zinazoandaliwa na kampuni ya Capital Plus International (CPI) kwa ushirikiano na Chama cha Riadha Tanzania (RT) pamoja na Chama cha Riadha Mkoani Mwanza (MRAA) zimeendelea kuwavutia washiriki wengu huku waandaji wakizidi kuboresha viwango vya mbio hizo za riadha.

Taarifa iliyotolewa na Mratibu wa mbio hizo, Bw. Mathew Kasonta Jijini Dar es Salaam jana, ilisema kuwa mbio hizo kwa mwaka huu zitakuwa kubwa na bora zaidi ukilinganisha na miaka iliyopita.

“Tuko tayari kwa mbio za mwaka huu za Rock City Marathon. Kamati ya maandalizi imeweka mikakati mizuri ili kuhakikisha mbio za mwaka huu zinakuwa na mafanikio zaidi,” alisema.

Bw. Kasonta alisema mbio hizo zitakuwa na vipengele vitano kwa msimu huu, akitaja kuwa kipengele kimojawapo cha mbio hizo kuwa  ni zile za kilometa 21 kwa wanawake na wanaume.

Alitaja vipengele vingine vya mbio hizo kuwa ni kilometa tano kwa wakimbiaji kutoka makampuni mbali mbali, mbio za kilometa tatu kwa watu wenye ulemavu, mbio za kilometa tatu kwa watu wazima (zaidi ya miaka 55) na kilometa mbili kwa watoto walio kati ya miaka 7 mpaka 10. 

Bw. Kasonta alisema kuwa mbio hizo zimeendelea kupata mafanikio tangu zilipoanza mnamo mwaka 2009, zikiwa na lengo la kukuza utalii wa ndani kupitia michezo.

Alibainisha kuwa kilele cha tukio hilo kubwa kwa kanda ya ziwa kitakuwa tarehe 27 mwezi wa Oktoba 2013, ambapo wanariadha wa ndani, nchi za jirani na kimataifa watapata nafasi ya kushiriki mbio hizo.

Bw. Kasonta alisema kutokana na uzoefu wa mwaka jana kwa wanariadha wengi kujitokeza kushiriki, kamati ya maandalizi imeongeza idadi ya waongozaji watakaosaidia katika kuzifanikisha mbio hizo.

 “Tunatarajia watu wengi kujitokeza mwaka huu, kwa kuwa tuna vitu vizuri kwa msimu huu. Kutokana na kujifunza kwa mbio za mwaka jana, kamati ya maandalizi imekuja na mpango madhubuti utakao saidia kuboresha mbio za Rock City Marathon zaidi mwaka huu,” alisema.

patakuwa hapatoshi viwanja vya leaders club.!

MAANDAMANO YA KUPINGA UJANGILI WA TEMBO NCHINI YAFANYIKA JIJINI DAR

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) (watano kutoka kushoto msitari wa mbele) akiwa anandamana pamoja na waandamanaji wanaopinga ujangili wa tembo ‘Tembea kwa ajili ya Tembo’ mara baada ya kuwapokea leo, Ubungo  jijini Dar es Salaam asubuhi. Maandamano hayo yamechukua muda wa siku 19 na waandamanaji wametembea kilomita 650, kutoka Jijini Arusha.


Matembezi hayo ya kupinga ujangili yameandaliwa Bw. Patric Patel, Mkurugenzi, African Wildlife Trust (wanne kutoka kulia msitari wa mbele) yakiwa na lengo la kuelimisha wananchi na Ulimwengu mzima kwa ujumla juu ya madhara ya ujangili. Matembezi yamehusisha raia wa nchi mbalimbali duniani.



Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) ambaye ndiye mgeni rasmi katika kilele cha matembezi hayo ametoa wito kwa wananchi wote waendelee kushirikiana na serikali kupiga vita ujangili kwa kuwafichua majangili popote wanapowaona; na taasisi zote za umma zishirikiane kupambana na ujangili ili kuutokomeza kabisa.

Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexander Songorwa (aliyeshika karatasi nyeupe mstari wa mbele) akiwa ameungana na msafara wa waandamanaji eneo la Ubungo kutembea nao hadi viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo atapokea risala kutoka kwa waandamanaji. 

KINANA AHITIMISHA ZIARA YAKE KISHAPU KWA MAFANIKIO MAKUBWA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi waliofika kumpokea kwenye wilaya ya Kishapu katika eneo la Maganzo ambapo Katibu Mkuu alikuwa na ziara katika wilaya ya Kishapu.
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi moja ya madarasa katika shule ya Sekondari Mwigumbi.
Moja ya Nyumba mpya iliyojengwa kwa ajili ya makazi ya Walimu wa Shule ya Sekondari Mwigumbi, wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga ambayo ilizinduliwa leo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitumia usafiri wa baiskeli kufika kijiji cha  Mwigumbi ambapo kulikuwa na shughuli za kuzindua mradi wa maji.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kuzindua mradi wa maji wa kata ya Mondo,kijiji cha Mwigumbi wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga.
 Mbunge wa Kishapu Suleiman Masoud Mchambi akishiriki kucheza ngoma ya kiasili wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji uliofanyiaka kata ya Mondo kijiji cha Mwigumbi.
 Tanki la maji litakalowasaidia wakazi zaidi ya 4000 katika kijiji cha Mwigumbi ,pichani wakazi wa kijiji hicho wakiwa wamekusanyika kushuhudia uzinduzi rasmi wa tanki hilo.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mwigumbi mara tu baada ya kuzindua mradi wa maji utakaosaidia zaidi ya watu 4000.
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Ndugu Azah Hilal Hamad akiwahutubia wakazi wa kata ya Mondo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Mwigumbi.
 Mbunge wa Kishapu Ndugu Suleiman Masoud Mchambiakihutubia wakazi wa kata ya Mondo na kuelezea namna gani jimbo lake limekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiingia kwenye viwanja vya Mabela kwa staili ya aina yake tayari kuhutubia wakazi wa Wilaya ya Kishapu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza  Balozi wa China hapa nchini ndugu Lu Youqinq wakati wa mkutano wahadhara uliofanyika katika viwanja vya Mabela, kushoto kwake ni Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

TANGAZO LA UFUNGUZI WA TAWI LA CCM CALIFORNIA

vijana wenye vipaji vya muziki & sanaa

Sales Executive Job Opportunity

SEMINA YA KAMATA FURSA TWENDZETU YAFANYIKA MKOANI DODOMA LEO.

$
0
0
 Mwakilishi wa NSSF-Makao Makuu,Salim Khalfan akifafanua masuala mbalimbali yatokanayo na faida za kujiunga na shirika hilo la NSS,ndani ya semina ya kamata fursa twendzetu iliofanyika mapema leo kwenye moja ya ukumbi wa hotel ya  Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma.
  Sehemu ya ya watu wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri kwenye semina hiyo.
 Meneja wa  NSSF mkoani Dodoma,Bwa.Kirondera Nyabuyenze akizungumza fursa mbalimbali zitokanazo na shirika la NSSF,Nyabuyenze amewataka watu mbalimbali wajitokeze kwa wingi kujiunga na NSSF,ili kujipatia fursa mbalimbali zikiwemo mikopo,matibabu na mambo mengiyo mbalimbali.
 Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Maxmalipo,Bernard Munubi akizungumza kwenye semina ya Kamata Fursa Twenzetu kwa vijana,kuhusiana na masuala mbalimbali yanayofanywa na kampuni yake katika kusaidia huduma za jamii,ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya  Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma.
 Sehemu ya wakazi wa mji wa Dodoma wakiwa wamejitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya fursa kwa vijana
 Sehemu ya meza kuu ya watoayo mada wakishangilia jambo.

 Wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye semina hiyo ya kamata fursa twendzetu,mapema leo asubuhi mkoani Dodoma.
 Mmoja wa Watangazaji mahiri wa Clouds FM,akizungumzia fursa mbalimbali alizokumbana nazo na namna alivyozifanyia kati na kujipatia sehemu ya  mafanikio katika kupambana na maisha.Semina ya Kamata Fursa twendzetu inayoratibiwa na Clouds Media Group,imekwishafanyika mikoa zaidi ya mitano ikiwemo  Kigoma,Tabora,Singida,Mtwara,Mbeya,Iringa sambamba na leo ndani ya Dodoma,ambo semina hizo zote zimeonesha mafanikio makubwa kwa vijana kwali walikuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye ushiriki.


 Baadhi ya wasanii ambao wamenufaika mara baada ya kujiunga na Shirika la NSSF,shoto ni Queen Doreen na Mwasiti wakijadiliana jambo na mdau Phillipon mapema leo,wakati semina ya Kamata fursa twendzetu ilipokuwa ikiendelea. 
Msanii mahiri wa Kughani Mashairi kwa mtindo wa kisasa kabisa,Mrisho mpoto akizungumza mbele ya sehemu ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma na vitongoji vyake waliojitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya kamata Fursa twendzetu,iliofanyika ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya  Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma. 
 Sehemu ya washiriki wa semina hiyo ilipokuwa ikiendelea mapema leo asubuhi.
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images