Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46329 articles
Browse latest View live

Camera aina ya Kodak 10 megapixels inauzwa

$
0
0
 Camera aina ya Kodak 10 megapixels inauzwa,kwa mtu anayehitaji anaweza kuwasiliana kwa simu 0768808819 ama email misasophie@yahoo.com

Taswa SC, Taswa Queens zatesa bonanza la waandishi Arusha

$
0
0
 Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taswa SC wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya bonanza la waandishi wa habari lililofanyika kwenye uwanja wa General Tyre, Arusha. 
Mchezaji wa timu ya Taswa SC, Juma Pinto akituliza mpira huku akilindwa na mchezaji wa Triple A. katika mchezo huo uliofanyika kwenye viwanja vya General Tyre, mkoani Arusha, Taswa SC ilishinda kwa mabao 3-1.
=======  =====   ======
Taswa SC, Taswa Queens zatesa bonanza la waandishi Arusha
Mwandishi Wetu, Arusha
Timu ya Mpira wa pete (netball) ya wanahabari wa jijini Dar es Salaam,Taswa Queen   juzi ilitwaa ushindi katika bonanza la nane la Waandishi mkoa wa Arusha, baada ya kuichapa timu ya chuo cha uandishi wa habari Arusha Arusha(AJTC) magoli 21-1.
Wakati Taswa Queen walikitwaa ubingwa kaka zao, TASWA SC , walishindwa kunyakuwa kombe, baada ya kutoka suluhu na timu ya AJTC katika mchezo mkali wa fainali, ambao ulisitishwa kutoka na kiza wakati wa mikwaju ya penati timu hizo, zikiwa zimefungana 1-1.
Kutokana na matokeo hayo, Meneja wa kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL), Endrew Warden alikabidhi Mwenyekiti wa Taswa SC Majuto Omar fedha taslim 200,000 na meneja wa AJTC Modaha Lucas alikabidhiwa kiasi cha sh 200,000.
Taswa  SC, walifanikiwa kuingia fainali baada ya kuichapa timu ya Radio 5 magoli 3-1 na baadaye kuifungua timu ya Arusha 1-0 katika mchezo mkali wa nusu fainali.
 Kwa Upande wa AJTC, waliingia fainali baada ya kuichapa timu ya  Taswa Arusha, 1-0 na baadaye waliwatoa Sunrise radio kwa penati 11-12 baada ya timu hizo kutoka sale.
 Katika mchezo wa fainali ya mpira wa pete   uliochezwa uwanja wa general Tyre jijini Arusha, Taswa Queen iliicharaza Taswa Arusha 45-0 katika mchezo wa nusu fainali na kuisambaratisha AJTC ambao walikuwa mabingwa watetezi kwa mabao 53-1 katika mchezo wa fainali.
Kutokana na ushindi huo, Taswa Queen walikabidhiwa kikombe na Meneja mauzo wa kampuni ya Megatrade, Gudluck Kway na fedha taslimu 150,000.
 Katika soka Taswa Dar pia ilifanikiwa kuingia fainali na timu ya AJTC na licha ya kupigiana mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya kutofungana, mshindi alishindwa kupatikana kutokana na kiza uwanjani.
 Katika michezo mingine, timu ya ORS kutoka Manyara, ilifungwa  na Sunrise 2-1 na baadaye ORS iliwafungua TBL Arusha goli 1-0 na hivyo kutwaa zawadi ya timu yenye nidhamu.
 Katika tamasha hilo, katika mchezo wa kuku, wanahabari kutoka Taswa SC, AJTC na Taswa Arusha walitamba na kushinda.
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliwapongeza wachezaji wake kwa ushindi huo huku akiwapongeza wadhamini wao, Delina Group of Companies, Said Salim Bakhresa & Co Ltd  (Azam), DRFA na Kassim Dewji.
Tamasha hilo la nane la vyombo vya habari mkoa wa Arusha, liliandaliwa na TASWA Arusha kwa ushirikiano na kampuni ya Ms Unique na kudhaminiwa na TBL,TANAPA, Megatrade,AICC,Cocacola, Pepsi na Wazee Klabu.

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KAHAMA

$
0
0
 
1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali pamoja na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa tanki la maji katika kata ya Kagongwa Wilayani Kahama wakati alipoanza rasmi ziara yake ya siku nne katika mkoa wa shinyanga leo na kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo na za kukiimarisha chama katika mkoa huo, Katika picha wanaoshuhudia kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi na katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Ndugu Khamis Mngeja.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KAHAMA2Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi3Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi naye akishiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa tanki hilo la maji katika kata ya Kagongwa4Hili niyo tanki linalojengwa katika kata ya Kagogwa wilayani Kahama
19Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria uzinduzi wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa jengo la Kituo cha afya katika kata ya Mwendakulima kijiji cha Mwendakulima iliyojengwa na kampuni ya Kuchimba madini ya mgodi wa Buzwagi wilayani Kahama , kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa mgodi wa Buzwagi Bw. Richard Otendo wa pili kutoka kulia. 20Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na mwakilishi wa mkuu wa mgodi wa Buzwagi Richard Otendo wakati alipotembelea jengo la kituo cha afya cha Mwendakulima lililojengwa na mgodi huo. 21Hili ndilo jengo lenyewe. 22Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananc hi katika kata ya Mwendakulima mara baada ya kutembelea ujenzi wa jengo la kituo cha afya cha kata hiyo kulia ni Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi na katikati ni Diwani wa Kata hiyo kutoka TLP Bw. Ntabi  -
 
5Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi akisoma ujumbe katika mabango yaliyoandikwa na wana CCM kuelezea kero zao Nape amepokea kero ya wanaCCM hao na kuahidi kulishughulikia mara moja.6Umati uliojitokeza katika mkutano wa hadhara mjini Kahama.7Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Kahama.8 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Ndugu Khamis Mngeja akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.9Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Kahama leo.12Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika kata ya Kagongwa wilayani Kahama13Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikbidhi kadi kwa mwanachama mpya wa CCM Ndeke Mdaki katika kata ya Isaka Wilayani Kahama.17Ndugu Ezekiel Maige mbunge wa Msalala akiwahutubia wananchi katika Kata ya Isaka Wilayani Kahama. Majabi. 23Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti katika kituo cha afya cha Mwendakulima. 24Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi naye akishiriki kupanda mti katika kituo cha afya cha Mwendakulima.25Wana CCM wakiwa katika mkutano wa Ndani mjini Kahama.27Kikundi cha Sarakasi kikionyesha uwezo wao katika sarakasi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sinjita mjini Kahama.

Agizo la Rais JK ! juu ya Wahamiaji haramu ! lazima litekelezwe !

$
0
0
Kwanini ? Vibali vyote vya kuishi wageni visifutwe na kusajiliwa upya.Msako lazima uwe na kasi kubwa tena uanzie mji mikubwa kama Dar,Arusha...

Kuanzia mwezi julai 2013 kiongozi mkuu wa nchi yetu rais Dk.Jakaya Kikwete katoka agizo kuwa raia wote wa kigeni ambao ni wahamiaji haramu wamepewa siku 14,kuondoka au kujisalimisha katika vyombo vya dola.

Agizo hili la rais lina lengo zuri tu kwa watanzania na usalama wa watanzania,lakini utekelezwaji wake umekuwa hauna kasi,kwani idadi ya wahamiaji haramu walio jisalimisha ni ndogo kulingana na waliopo nchini,na kati ya hao walijisalimisha ni wahamiaji waliopo nje ya miji mkubwa sio katika miji mikubwa kama Dar ,Arusha na
kwingineko !

Cha kushangaza kwamba kuna baadhi ya wahamiaji haramu au halali wanakiuka kwa namna moja au nyingine sababu zinazowafanya kuwepo nchini Tanzania.

mfano raia wa kigeni aliyekuja nchini kwa kufanya kazi fulani na akapewa kibali kwa ajili hiyo anakiuka kwa taratibu za uhamiaji na kuanza kuwa mfanyi biashara
ya baa au dangulo fulani! au pengine kujiingiza katika biashara ambayo mzawa anaweza kuifanya, na huku vyombo vya usalama vikimwangalia !

Hivi kuna uhalali wa kisheria Raia wa kigeni asiye na hata asili ya Tanzania kumiliki nyumba au Ardhi ?

Watanzania wengi wamekuwa wakilalamika juu ya ongezeko la raia wa kigeni hususan raia wa nchi za ulaya,Asia na nchi za kiarabu kumiliki au kununua
nyumba na ardhi nchini ,mfano wachina wanamiliki majumba au ardhi uenda wakawa wanakiuka sheria fulani za nchi,na watanzania wanao wauzia nyumba
wageni hao nao pia wanajisaliti au kuisaliti nchi.

Ukiwikaji wa sheria za ajira ! mchina anapofanya ya kuuza duka na mitumba au kubeba zege !  Mzungu anapokuja kutalii na baadaye 
kupata ajira ya muhudumu wa hotel ! hili nalo neno?

Bendi za muziki zinapo ajiri wanenguaji kutoka nje ya nchi!

Ndio maana watanzania walio wengi wanaona kuwa hipo haja kwa serikali kuvifuta vibali vyote vya wageni na kuanza zoezi la kuvitoa upya na kuvihakiki
kwa kupitia Wizara ya mambo ya ndani.

Kama Rais JK kesha toa agizo tangu mwezi julai mbona utekelezaji wake una mwendo wa pole ? wakati kiongozi mkuu wa nchi,ambaye ndiye amri jeshi mkuu kishaagiza siku 14 tu kila muhamiaji haramu aondoke sasa
tena msako kwanini? usianze katika kutekeleza agizo la mkuu wa nchi.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Rais JK

MGODI UNAOTEMBEA; Nashangaa malumbano na mnyukano huu wa CCM

$
0
0
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.

NI wazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndio chama kikongwe na chenye historia kubwa na Taifa hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Tangu Uhuru, wakati lipo chini ya Chama kimoja na sasa vyama vingi, CCM imefanikiwa kwa miaka kadhaa kuunda serikali kwa kutoa Rais wa Bara na Visiwani.

Ni CCM ndio iliyoiweka nchi katika hatua hii nzuri ya kuungwa mkono ndani na nje ya mipaka yetu. Waswahili wamesema, mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. CCM pamoja na mapungufu kadhaa yanayosemwa na baadhi yao, ila imefanya mengi mazuri.

Ni kutokana na hilo, muasisi wa Taifa hili, Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kuelezea umuhimu wa serikali ya CCM kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bila kuficha, Nyerere alisema wazi kuwa bila CCM imara, nchi itayumba. Ni kauli nzuri inayoendelea kukumbukwa hadi wakati huu. Mara kadhaa CCM imekuwa ikifanikiwa kutoa rais na kuunda serikali kwa ujumla wake.

Kwa wale wanaopingana na suala hili; wanapaswa kukaa na kuwaza haya machache kabla ya kutoa uamuzi wa kukichukia chama hiki kikongwe. 

Mosi; kwanini CCM imekuwa ikichanganya vichwa vya Watanzania kila inapofikia chaguzi zake za ndani?

Kwanini ni wagombea urais wa CCM pekee wamekuwa na mguso na kuangaliwa sana kiasi cha kuumiza watu wengine mtaani? Hawa wengine wa upinzani wapo wapi, wanafanya nini? Angalia, licha ya kuwa Uchaguzi Mkuu utafanyika tena mwaka 2015, lakini ni makada wa CCM na baadhi ya viongozi wanaotajwa zaidi kwenye kinyang’anyiro cha urais.

Watu kama vile Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, Samuel Sitta, Dkt Asha Rose Migiro na John Magufuli, hawa wanatajwa mno kuwa wana mipango ya kuwania nafasi hiyo inayoshikiliwa kwa sasa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Ukiacha hao, pia wapo vijana wachache akiwamo Naibu Waziri wa Sayansi na Technology, January Makamba anayetajwa katika nafasi hiyo, bila kuangalia kuwa umri wake bado haumruhu kuwania kiti hicho.

Sio kama hakuna wengine wanaotajwa katika nafasi hiyo, hasa kutoka vyama vya upinzani, akiwamo Dk Willbroad Slaa kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Profesa Ibrahim Haruna Lipumba kutoka Chama Cha Wananchi (CUF), ambao pia waliwania nafasi hiyo Uchaguzi wa  mwaka 2010.

Ndio hao wanatajwa, ila si kama wanavyotajwa makada wa CCM. Kila mtu ndani na nje ya nchi amekuwa akitumia muda mwingi kuangalia majina hayo. Hii ni kwasababu wanatokea katika chama kikongwe na kinachokuwa na nafasi kubwa yaa kutoa rais wan chi kwa miaka kadhaa ijayo.

Ni chama kilichowafanyia mema Watanzania tangu Uhuru. CCM iliyozaliwa mwaka 1977, imeitoa Tanzania katika vipindi tofauti mno. Hata kama mabaya yake yapo na wachache wao wanayajadili, ila kwakuwa ndani yake kuna mazuri, basi ni vyema tukawa wepesi pia kuyaweka mbele.

Pamoja na hayo, ila ni wakati sasa wa kuangalia namna gani viongozi wa serikali kutoka CCM, viongozi wao wa chama na makada kwa ujumla kujaribu kutafakari hayo ili iwe njia yao ya kubakia madarakani.

Watanzania tunahitaji maendeleo. Na hapana shaka maendeleo hayo yataendelea kupatikana kutokana na uzalendo, ushirikiano kutoka kwa watu wote, wakiwamo viongozi wanaotoka CCM.

Huwezi kukwepa mazuri ya Tanzania yaliyopatikana ndani ya utawala wa serikali ya CCM, inayoongozwa na Kikwete. Sasa katika mikoa mbalimbali kumeunganishwa barabara za lami.

Sera nyingi zinazotekelezeka zimeendelea kuwa chachu ya maendeleo ya Taifa hili. Miaka ya 2005 kushuka chini ilikuwa kazi kupata shule ya kusoma elimu ya sekondari. Leo hii kila Kata kumejengwa shule.

Zamani mtu anayesoma Chuo Kikuu alionekana ni wa ajabu sana au pia kuonekana tajiri. Lakini hii Vyuo Vikuu na vinginevyo vimeendelea kujengwa katika mikoa mbalimbali kwa ajili ya watoto wa Tanzania kuipata elimu ya juu.

Haya na mengine ni maatunda ya CCM. Ni vyema tukayatambua na kuyaheshimu ili iwe nafasi ya kutafuta mengine hata kwa vyama vya upinzani kama wanavyohitaji baadhi yao, ukizingatia kuwa hii ni nchi ya demokrasia.

Tunajua wapo wanaohitaji vyama vingi, ila si sababu ya kutufanya tuponde na kuchukia kila jema linalofanywa na CCM, ati kwasababu ni chama tawala. Kama hivyo ndivyo, hawa viongozi wa CCM wanafanya nini?

Kuanzia viongozi wa matawi hadi Taifa wanajua thamani yao? Wanafahamu ni namna gani wanapaswa kulitumikia Taifa na wananchi wao ili mazuri yao yawe mbeleko leo na hata kesho pia?

Wakati nasema haya, natambua kuwa katika sehemu nyingi za nchi yetu, Bara na Visiwani kumekuwa na msuguano wa aina yake kwa viongozi wa ndani ya CCM. Kila mara kumekuwa na msuguano unaotishia uhai wa CCM.

Utakuta Meya anasuguana na mbunge wa jimbo husika. Kama hivyo haitoshi, wakati mwingine diwani kumenyana na mwenyekiti au Katibu wa CCM na pengine msuguano huo kuingia hadi kwa Mkuu wa Wilaya na kuharibu kabisa ufanisi katika maeneo hayo, maana linapotokea huwakumbuka watu wengi.

Ni juzi tu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM Taifa, Kikwete, alipowataka Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Khamis Kagasheki kumaliza mgogoro wake na Meya wa Kagera, Anatory Amani, ambaye naye anatoka kwenye chama hicho kikongwe Barani Afrika.

Mgogoro wa viongozi hao ulisababisha kuzaliwa kwa makundi yasiyokuwa na tija kwa serikali na chama kwa ujumla, hasa baada ya kuibua malumbano kutoka chini hadi juu, huku kila mmoja akiona yupo sahihi.

Akiwa mkoani Kagera, Kikwete aliwataka watu hao wamalize mzozo wao kwa sababu za kuijenga nchi inayoongozwa na CCM. Hata hivyo, hayo yalikolezwa pale madiwani nane wa CCM kuvuliwa uanachama mkoani humo.

Madiwani hao waliofukuzwa ambao baadaye walitetewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliyepinga uamuzi wa viongozi wa chama Kagera ni Richard Gaspar (Miembeni), Murungi Kichwabuta (Viti Maalumu), Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe), Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai), Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga), Robert Katunzi (Hamugembe), Samwel Ruhangisa (Kitendagulo) na Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).

Ingawa Kamati Kuu ya CCM iliwaita tena mahasimu hao, yani Kagasheki na Amani ili waangalie tatizo lililopokuwa, ila bado msuguano huo upo na umeenea katika maeneo mengi ya Tanzania.

Kwa bahati mbaya, matokeo hayo mara kadhaa yamekuwa machungu kwa CCM,  hasa pale vyama vya upinzani vinapogeuka kuwa fisi anayesubiri mifupa. Mara baada ya madiwani hao kufukuzwa kama ilivyotangazwa na CCM mkoani Kagera, Mwenyekiti wa Chadema, Mbowe aliibuka na kuwaita wajiunge na chama chao.

Mbowe alizungumza mengi, hasa madai ya ufisadi unaofanywa na Amani, hivyo kuwakera madiwani hao wa CCM. Hii ni nzuri, ila nathubutu kusema kuwa maneno ya Mbowe yamekuja huku yakionyesha kuwa inategemea zaidi mnyukano huo ili iwe tija kwao.

Sio mbaya pia, ila lazima viongozi wa CCM wenyewe wafahamu kuwa wao ndio kila kitu kwa chama chao. Msemo wa vita vya panzi faida ya kunguru unaweza kuchukua nafasi kubwa katika kadhia hii.

Bado vyama vya upinzani haviwezi kufanya vizuri bila kuhitaji Baraka kutoka kwa makada au viongozi wa CCM. Hivyo sitaona ajabu hata leo Mbowe akamuita Lowassa, Membe, Sitta na wengineo akiamini kuja kwao hao ni faida kwa Chadema, ukizingatia kuwa miamba hiyo itakuja na watu wao.

Katika mchezo wa siasa, hakuna mwanasiasa mdogo. Diwani mmoja tu alitepita kwa haki na ambaye ni chaguo la wananchi wake, basi ni wazi kuwa akihamia upinzani, bado anaweza kutetea nafasi yake hiyo.

Kama hivyo ndivyo, diwani aliyefukuzwa ndani ya CCM akahamia Chadema au CUF, nafasi ya kutetea nafasi yake ni kubwa, hivyo Kata hiyo itapotea. Je, CCM matawi, Kata, Wilaya na Taifa wanafahamu hili?

Naheshimu mno busara za Kikwete katika kukiendesha chama cha CCM, akiamini kuwa yeye ndio dreva wa kuliongoza jahazi hili. Ni CCM tu yenye mamlaka ya kuunda serikali ya kuwaongoza Watanzania.

Kwa bahati mbaya, CCM hii imekuwa na mnyukano wa kila wakati, hivyo ni wakati wao sasa kukaa chini kwa ajili ya kukijenga chama chao. Mwaka 2014, ikiwa ni miezi michache kutoka sasa itaingia kwenye Uchaguzi wa serikali za mitaa.

Uachaguzi huo ni muhimu kuliko hata ule wa ndani ya chama. Ni kipimo kikubwa kuonyesha CCM ya miaka mitano ijayo itakuwaje. Kama CCM itaanguka kwenye mitaa mingi, basi matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 yatashangaza wengi.

Lakini kama ikifanikiwa kushika serikali za mitaa kama kawaida yake, basi viongozi hao watakaochaguliwa na wananchi, wakawa ni machaguo yao halisi, wakawatumikia kama inavyotakiwa, kwanini wasiwaunge mkono kwenye Uchaguzi Mkuu?

Hatuhitaji uchakachuaji wala mihemko ya kisiasa. Tunahitaji busara, unyenyekevu na moyo wa uzalendo kwa ajili ya Watanzania wote. Hayo yakifanyika kwa mikono miwili, hata hayo maisha bora kwa kila Mtanzania yapatikana.

Na kama yakipatikana kwa vitendo na sio maneno ya kisiasa, sasa kwanini watu waichukie serikali ya CCM wakati inawapatia kila wanachohitaji? Haya ni mambo yanayotakiwa yawekwe vichwani mwa viongozi wote wa CCM.

Viongozi hawa wanaowezo mkubwa wa kuwasimamia watendaji wengine wa serikali kwa ajili ya kusimamia sera na utekelezaji wote uliokusudiwa kwa ajili ya kuwaongoza vyema wananchi wanaounda serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Huu ndio ukweli na kuna kila sababu ya kuangalia nyendo zote zenye tija, maana CCM wasipokuwa makini, suala hili la mnyukano litawaathiri.

Mvutano Wa Marekani Na Urusi (DK 90 ZA DUNIA Capital Radio)

$
0
0
Na watangazaji wetu Bahati Alex kutoka Capital Radio Jijini Dar es Salaam  akiwa na  Mubelwa Bandio wa Jamii Production Washington DC.Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania. Hii ilikuwa ripoti ya Septemba 7, 2013

Bi.Asha Mandela Mwanamke mwenye nywele ndevu kuliko mtu yeyote duniani

$
0
0
Bi.Asha Mandela ,Mwanamke aliyevunja rekodi ya Guiness kwa kuwa na nywere ndevu kuliko binadamu yeyote duniani

FFU Ughaibuni Wapongeza Bi.Hafsa Ngazinja ! Kuibua dhahabu ya Mzee Gurumo.

$
0
0
Bendi Maarufu ya Muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band,inampongeza mwanamuziki Bi.Hafsa Ngazinja  kuwa mwamuziki mfano wa kuigwa baadala ya mwanadada huyo kuingia Studio na kurekodi mmoja ya nyimbo ya NUTA kwa ajili ya kumuenzi Mkongwe wa muziki wa dansi ambeye amejiuzulu Mzee Muhidin Maalimu Gurumo.

Ngoma Africa band aka FFU ughaibuni wamemtaja mwanamuziki Bi.Hafsa Ngazinja kuwa ni moto wa kuotea mbali ,pia ni mfano kwa wengine,kwani mwanamuziki huyo amewashirikisha wakongwe  akina "Salvador" na Omary Mkali katika kurekodi Studio, wimbo huo "Nimuokoe Nani" ni sawa na dhahabu iliyoibuliwa upya.

MGAHAWA MPYA WA SIX DEGREES SOUTH WAZINDULIWA ZANZIBAR

$
0
0
DHL_5976
Wakati upepo mzuri wa kipindi cha joto kutoka bahari ya Hindi ukipuliza, uzinduzi wa mgahawa mjini Zanzibar, Six Degrees South, ulikuwa hauna mfano! Huku kukiwa na fataki za ndani, chupa za Moet zikifunguliwa kwa madaha usiku kucha mpaka mida ya usubuhi, uzinduzi wa Six Degrees South uliwaacha wengi mjini Zanzibar wamepigwa na butwa wakiwa hawana la kusema.
6Deg Launch (220)
6Deg Launch (223)
6Deg Launch (270)
6Deg Launch (176)
6Deg Launch (294)
Huku Wazanzibari wengi wakiwa wana hamu ya mgahawa kama huu, muundo wa mgahawa huu wa kisasa wenye ghorofa tatu umedhihirisha hadhi yake ya kuwa na eneo la nyama choma na baa ya mvinyo. Kuanzia ordha ya vyakula vya moto vya asubuhi mpaka mchanganyiko murua wa vyakula vya siku nzima na vitafunio vidogo vidogo, sehemu hii imeinua viwango vya biashara ya migahawa mjini Zanzibar na kuifikisha juu kabisa.
PBF_6038
DHL_5927
Six Degrees South ipo eneo la mji mkongwe na inawapa wageni utulivu wa hali ya juu ili kuwawezesha kupumzika na kujichanganya. Ukichanganya mazingira ya utulivu na na huduma ya bure ya mtandao wa internet, sehemu hii inamfaa mtu yoyote kupata kinywaji anachopendelea na vitafunwa. 

Mgahawa una vibaraza kwenye ghorofa tatu vyenye eneo kubwa kwa ajili ya wageni kutazama jua likizima kwenye mandhari ya Bahari ya Hindi.
PBF_6064
PBF_6090-Edit
Vyakula kutoka mataifa mbalimbali pia vitapikana kwa ya wateja wenye ladha na uwezo tofauti. Orodha ya chakula iliyoandaliwa na Mpishi Mkuu kutoka Afrika Kusini, Louise Serfontein, inatoa fursa kwa watu kutoka bara na visiwani kufuruhia chakula. Six Degrees South inajisifia kwa kuwa na viwango vya hali ya juu ya utoaji huduma wakati wakiwaridhisha wateja kwa chakula na mandhari nzuri.

Huku wakiwa na orodha ya mivinyo zaidi ya 80 ambayo mteja anaweza kunywa kwa glasi au chupa, Six Degrees South inatoa fursa nzuri ya kunywa, kula na kufanya matembezi wakati mwezi ukiangaza kwenye bahari. Sehemu yenye kutoa ukarimu wa hali ya juu, Six Degrees South ni sehemu ambayo kila mtu anatakiwa kutembelea.
PBF_6146-Edit
PBF_0767
6Deg Launch (254)
DHL_5973

TANGAZO NAFASI ZA KAZI MMK MEDIA GROUP

$
0
0
Kampuni ya MMK MEDIA GROUP
Inayomiliki SWAHILI TV,SWAHILI RADIO ONLINE, SWAHILITV.BLOGSPOT.COM na DMK11.BLOGSPOT.COM Inatangaza nafasi za kazi kwa watu wa masoko na matangazo.
Wenye uzoefu na wanaojituma.
Maombi ya kazi yatumwe katika 
email
career@mmkmediagroup.com

WAIGIZAJI KUPEWA MAFUNZO.

$
0
0
Mdhamini mkuu wa mafunzo ya Uigizaji na utayarishaji wa Filamu kwa wasanii wa mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na asasi ya TCDA na shirikisho la filamu Tanzania (TAFF) Fredrick Mwakalebela.
=====  =====  ======
WAIGIZAJI KUPEWA MAFUNZO

Na Denis Mlowe,Iringa

SHIRIKISHO la Filamu Tanzania(TAFF) kwa kushirikiana na asasi isiyo ya Kiserikali ya Tanganyika Centre For Development and Advocacy (TCDA) wameandaa mafunzo ya uigizaji na utayarishaj wa filamu kwa wasaniin wa mkoa wa Iringa na maeneo ya jirani.


Akizungumza na Daraja letu mkurugenzi wa asasi hiyo, Jackson Kiyeyeu alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwapa upeo na ujuzi zaidi wasanii wa Iringa katika kuweza kuandaa filamu bora na kuwa na ujuzi wa katika uigizaji.


Alisema mafunzo hayo yatakuwa ya mwezi mmoja na yatatolewa na wasanii wakali wa filamu Tanzania akiwemo msanii nguli  Haji Adam maarufu kama Baba Haji akiambatana na walimu wa sanaa kutoka Dar es Salaam.


Kiyeyeu alisema wahitimu wa mafunzo hayo watapatiwa vyeti vinavyotambulikana shirikisho la filamu Tanzania na wasanii bora 10 watapatiwa fursa ya kushiriki filamu ya No Option itakayochezwa na wakali wa Bongo Movie.

“ Mafunzo yatatolewa kwa watu wote kuanzia elimu ya shule ya msingi hadi kidato cha sita na vyeti vitakavyotolewa vitawawezesha kufanya kazi za filamu popote pale Tanzania na ni wakati wa wasanii sasa kuwa na elimu ya ugizaji na utayarishaji wa filamu kuliko ilivyo sasa wengi wao kutokuwa na elimu.” Alisema Kiyeyeu

Mafunzo ya ugizaji na utayarishaji wa filamu yatakakuwa ni mara ya kwanza kwa mkoa wa Iringa yamedhaminiwa na aliyekuwa katibu mkuu wa TFF Fredrick Mwakalebela aliyetoa asilimia 75 ya ada za mafunzo hayo kwa wasanii wa Iringa.


Kwa upande wake Daraja Letu lilipozungumza na Mwakalebela alisema  lengo ni kuwasaidia wasanii wa Iringa kuweza kuwa na ufahamu wa uigizaji na utayarishaji wa filamu bora Tanzania na kuwakomboa vijana katika umaskini.


Alisema sanaa ya uigizaji wa filamu una faida kubwa sana katika kuondokana na tatizo la ajira kwa vijana natoa wito wajitokeze kwa wingi na kuwataka wadau kuweza kuwasaidia vijana katika kuondokana na tatizo la umasikini katika kuwaidia kutimiza ndoto zao.

“Kutokana na kupenda sanaa  na michezo kwa ujumla ameguswa sana na wazo la TCDA kuweza kunipa mawazo yao hivyo sikuwa na budi kuweza kuwadhamini katika hilo nachoomba wadau wengine waweze kujitokeza kuwasaidia wasanii wa Iringa kuweza kutambulika kitaifa na kimataifa katika tasnia ya Filamu.” Alisema Mwakalebela

Alisema Iringa kuna wasanii wengi wanaojitahidi kupambana kwa uwezo wao binafsi kufanya sanaa kwa kile anachofikiria bila elimu ya sanaa ya ugizaji na utayarishaji wa filamu.

Mwakalebela alisema wasanii watakaofanya vizuri katika mafunzo hayo watashirkishwa katika filamu mbalimbali ambazo zinaandaliwa na wasanii wakubwa kutoka jiji Dar es salaam kwa lengo la kuwainua mbeleni waweze kujitegemea.

MSAFARA WA KINANA WAWASILI SHINYANGA VIJIJINI

$
0
0
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ,Mbunge wa Jimbo la Swola ndugu Ahmed Salum na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakicheza na nyoka aina ya chatu wakati wa mapokezi katika kata ya Didia, Luhambo wilaya ya Shinyanga Vijijini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akisalimiana na wanachama wa chama cha Mapinduzi waliokuja kumpokea alipowasili  Wilaya ya Shinyanga Vijijini.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Ndugu Hamisi Mgeja akisalimia wakazi wa Luhambo Didia wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wakazi wa kata ya Didia na kuwashukuru kwa mapokezi mazuri waliyowapa.

USAID Supported SERA POLICY Project conducts a one day seminar on Food Security in Dar today.

$
0
0
 Senior Agriculture Advisor at SERA Policy Project, Alex Mkindi (R ) briefs journalists at a one day seminar on food security in Dar es Salaam today. SERA is the policy arm of the Feed the Future Initiative supported by the American people through the United States Agency for International Development (USAID) with him is the USAID supported Feed the Future Senior Advisor, Tom Hobgood. 
 Ministry of Agriculture and Food Security National Food  Director Karimu Mtambo talking to media during the SERA Policy project workshop in Dar es Salaam today. 
 A cross section of journalists during the SERA Policy Project workshop on Food Security in Dar es Salaam today.
 A cross section of participants attending the USAID supported SERA Policy Project workshop to present the results of cutting edge research studies on food security in Dar es Salaam today. 

ABASI TARIMBA, MWENYEKITI WA MTAA WA HANANASIFU WAMKACHA ASHA BARAKA ZOEZI LA UBOMOAJI

$
0
0

 Mkurugenzi wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', ambaye pia ni Mjumbe wa Nec CCM, Asha Baraka, akiwaka wakati akizungumza  na mtandao huu jana jioni alipokuwa akisimamia zoezi la kuwazuia wabomoaji kutobomoa nyumba na vibanda vya wananchi katika eneo hilo la Hanansifu bila kufikia muafaka kwa mazungumzo na wahusika.

Zoezi hilo la kubomoa eneo hilo ili kujengwa barabara ya mtaa lilianza tangu mwezi wa tano mwaka huu, ambapo wenye nyumba zizizopo eneo hilo baada ya mazungumzo na wasimamizi wa zoezi hilo na Diwani na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, walikubaliana na kuwekewa alama eneo linalotakiwa kubomolewa ili kupisha upanuzi huo.

Baada ya alama hizo ulifanyika ubomoaji na kuchimba barabara hiyo kana kwamba zoezi la ujenzi lilikuwa likianza muda mfupi tu baada ya ubomoaji, lakini cha kushangaza watu wao baada ya kubomoa waliondoka zao na kuacha eneo hilo likiwa na madimbwi makubwa yaliyojaa maji na kusababisha eneo hilo kutopitika kwa wenye magari na waenda kwa miguu.

Aidha baada ya kumalizika kwa ubomoaji huo, wahusika wenye nyumba zao na fremu za maduka eneo hilo, walikaa kwa muda wa miezi miwili na walipohakikishiwa kuwa zoezi hilo limemalizika na hakuna ubomoaji utakaoongezeka, walianza kukarabati nyumba na fremu zao upya ili kuendelea na biashara.

Cha kushangaza ghfla watu hao walirejea tena jana na kuchora alama mpya kwa kutumia mkaa, na kuanza kubomoa jana hiyo hiyo jambo lililowaacha hoi wananchi wa eneo hilo na wenye frem zao, kutokana na kutotolewa kwa taarifa wala watu hao kutokuwa na kiongozi hata mmoja wa Eneo hilo yaani Diwani au Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, ambao walitakiwa kuwepo ili kutoa ufafanuzi wa tukio hilo.

Lakini cha kushangaza wakati wa zoezi hilo, hakuwepo Mwenyekiti wala Diwani, jambo lililowafanya wananchi kuhoji juu ya uhalali wa zoezi hilo.

Wakati wa zoezi hilo Asha Baraka, alimpigia simu Diwani, Abasi Tarimba, lakini naye alimjibu kuwa hajui lolote kama Diwani na kumtumia namba ya simu ya mtu mwingine ili azungumze naye, wakati yeye ndiye hasa alitakiwa kuwapo eneo hilo na kuwatetea wapiga kura wake.

Hata hivyo watu waliokuwapo eneo hilo walishangazwa na kitendo cha jamaa hao kuendelea kumoboa upande mmoja wa eneo hilo huku wakikwepa ukuta wa ghorofa lililopo eneo hilo ambalo ni jipya lililojengwa hivi karibuni kwa kukwepa gharama, wakati alama za awali zinaonyesha kuwa hata ukuta wa ghorofa hilo ulitakiwa kubomolewa.
 Katapila likiendelea kubomoa....
 Asha Baraka akisimama mbele ya Frem zake eneo hilo kuwazuia jamaa hao kuendelea na zoezi hilo hadi upatikane muafaka na wahusika kwanza.
 Asha Baraka, akionyesha alama ya pili iliyowekwa jana na kuanza kubomoa jana hiyo hiyo.....
 Wananchi wakimsikiliza Asha Baraka.....
 Sehemu ya madimbwi yaliyoachwa na wachimbaji hao mara ya kwanza ambayo kwa sasaa yameanza kukauka.
 Nyumba ya Asha Baraka (kushoto) inayotakiwa kubomolewa na (kulia) ndiyo Ghorofa lilalokwepwa ili kupindisha barabara hiyo jambo linalofanya kubomolewa kwa nyumba za upande mmoja.
 Asha Baraka, akionyesha alama za awali zilizowekwa kwa rangi nyekundu ambazo zinaonyesha kuwa hadi ukuta wa ghorofa unatakiwa kuondoka...
 Alama hiyo ipo kwenye kibanda hiki cha mkaa ambacho kipo sambamba na ghorofa hilo..
 Alama iliypchorwa kwa mkaa mara ya pili jana.......
Sehemu ya uhalibifu uliotokea jana wakati wa zoezi hilo.....katika moja ya fremu zilizopo eneo hilo..!
Na www.sufianimafoto.com

WAREMBO REDD'S MISS TANZNIA 2013 WALIPOTEMBELEA MARIA STOP KANDA YA KASKAZINI

$
0
0
 Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Maria Stop ya jijini Arusha wakisalimiana na warembo wa Redd’s Miss Tanzania 2013 wakati warembo hao walipotembelea Makao Makuu ya Kanda ya Kaskazini mjini Arusha hivi karibuni na kupatiwa mafunzo juu ya uzazi wa mpango
 Warembo wakiwa mapokezi
Warembo wa Miss Tanzania wakifuatilia mafunzo juu ya uzazi wa mpango na wakati salama wa umri wa kuanza kupata mtoto.
 Meneja wa Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa wa Maria Stop Tanzania, Dk Abraham Msaki akizungumza na warembo wanaoshiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania 2013 na kuwapatia elimu ya uzazi wa mpango wakati warembo hao walepotembelea taasisi hiyo mjini Arusha hivi karibuni.
 Meneja wa Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa wa Maria Stop Tanzania, Dk Abraham Msaki akizungumza na warembo wanaoshiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania 2013 na kuwapatia elimu ya uzazi wa mpango wakati warembo hao walepotembelea taasisi hiyo mjini Arusha hivi karibuni.
 Mmoja wa washiriki Salsha Isdori  akiuliza swali...
 Meneja wa Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa wa Maria Stop Tanzania, Dk Abraham Msaki akiendelea kutoa darasa kwa warembo hao.
 Mrembo Prisca Paul akigawa mpira ya kiume 'Condom' kwa warembo wenzake. Mipira hiyo pia hutumika katika njia za uzazi wa mpango pamoja na kujikinga na magonjwa ya zinaa na Virusi vya ukimwi.
 Picha ya pamoja kati ya warembo na wafanyakazi wa Maria Stop Kanda ya Kaskazini ilipigwa.
Meneja wa Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa wa Maria Stop Tanzania, Dk Abraham Msaki akizungumza na warembo wanaoshiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania 2013 na kuwapatia elimu ya uzazi wa mpango wakati warembo hao walepotembelea taasisi hiyo mjini Arusha hivi karibuni.

MTANDAO WA WASANII TANZANIA SHIWATA watoa shukurani

$
0
0
BAADA ya kukabidhi nyumba kwa wanachama 38, SHIWATA inatoa shukurani kwa viongozi wa kijiji cha Mwanzega Kata ya Mbezi, Tarafa ya Shungubweni,wanavijiji pamoja na viongozi wa wilaya ya Mkuranga akiwepo Mkuu wa wilaya, Mercy Silla kwa kufanisha sherehe ya ugawaji nyumba na vyeti.

Wanachama zaidi ya 70 wamejitokeza kuchangia ujenzi wa nyumba ili wakabidhiwe Desemba 28, 2013 katika sherehe nyingine ya kukabidhi nyumba ambayo inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali ambao waliomba udhuru sherehe ya awali.

SHIWATA inawahimiza wanachama wake wasifanye mzaha na kudharau mpango wa kuchangia ujenzi kwani utawanufaish na kuwamilikisha nyumba zao wenyewe kwa gharama nafuu.

Mtandao wa wasanii unatoa bure viwanja baada ya mwanachama kulipa gharama zote za kujiunga uanachama ambaye ataruhusiwa kujenga mwenyewe au kuchangia ujenzi wa nyumba kwa pamoja.

SHIWATA  inakusudia kujenga Shule ya Msingi, Sekondari na vyuo vya fani za utamaduni, Uandishi wa Habari na michezo mbalimbali ikiwemo soka kwa malengo ya kupata wachezaji bora ambao watanyanyua viwango vya michezo hiyo ndani na nje ya nchi ili kuwapatia vipato zaidi.

Pia inawahitaji wasanii, wanamichezo, wanahabari wenye vipaji na elimu ya juu katika fani zao wajiunge na SHIWATA ili waweze kuwa walimu wa sanaa na michezo mbalimbali ambayo itaanza kufundishwa kutoka ngazi ya Shule ya Msingi, Sekondari hadi Chuo katika kijiji cha Mwanzega.

Shule ya msingi itakapoanzishwa itatoa kipaumbele kwa masomo ya sanaa na michezo ili kupata wasanii na wanamichezo bora katika taifa letu.

SHIWATA pia inatarajia kujenga viwanja vya michezo, kumbi za Maonesho na Studio za kurekodia muziki na filamu zenye ubora ambazo zitauzwa ndani na nje ya nchi. 

KLABU YA SUNDERLAND YA UINGEREZA KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA UTALII NA KUINUA MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU HAPA NCHINI

$
0
0
 Mkurugenzi wa Biashara wa Timu ya Sunderland ya nchini Uingereza Gary Hutchinson(wa pili kutoka kulia) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam  juu mazungumzo ya awali ya timu hiyo kuanzisha ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania nchini Uingereza na vilevile kuendeleza michezo hapa nchini.Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Tadeo(kushoto) , Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Dkt. Alyoce Nzuki(wa pili kutoka kushoto) na Mwakilishi wa timu ya Sunderland hapa nchini Edmund Hazzal(kulia).
 Mkurugenzi wa Biashara wa Timu ya Sunderland ya nchini Uingereza Gary Hutchinson( kulia) akimkabidhi jezi ya timu yake Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Tadeo(kushoto) leo jijini Dar es salaam mara baada ya mazungumzo ya awali ya kuimarisha ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania nchini Uingereza na vilevile kuendeleza michezo hapa nchini. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Dkt. Alyoce Nzuki. 
 Mkurugenzi wa Biashara wa Timu ya Sunderland ya nchini Uingereza Gary Hutchinson( kulia) akimkabidhi jezi ya timu yake leo mjini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Dkt. Alyoce Nzuki (KUSHOTO),mara baada ya mazungumzo ya awali ya kuimarisha ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania nchini Uingereza na vilevile kuendeleza michezo hapa nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Tadeo.
 Mkurugenzi wa Biashara wa Timu ya Sunderland ya nchini Uingereza Gary Hutchinson(kulia) akiongea na waandishi wa habari hapo pichani jana jijini Dar es salaam  juu ya timu hiyo kuanzisha ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania nchini Uingereza na vilevile kuendeleza michezo hapa nchini.Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Dkt. Alyoce Nzuki (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Tadeo (kushoto).
 Mkurugenzi wa Biashara wa Timu ya Sunderland ya nchini Uingereza Gary Hutchinson(wa pili kutoka kulia) akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam  juu mazungumzo ya awali ya timu hiyo kuanzisha ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania nchini Uingereza na vilevile kuendeleza michezo hapa nchini.Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Tadeo(kushoto) , Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Dkt. Alyoce Nzuki(wa pili kutoka kushoto) na Mwakilishi wa timu ya Sunderland hapa nchini Edmund Hazzal(kulia).Picha zote na Idara ya Habari(MAELEZO).  
 Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Dkt. Alyoce Nzuki akiongea na waandishi wa habari leo  jijini Dar es salaam  juu ya mazungumzo ya awali kati ya timu ya Sunderland ya Uingereza ya kuanzisha ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania nchini Uingereza na vilevile kuendeleza michezo hapa nchini.Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Biashara wa Timu ya Sunderland ya nchini Uingereza Gary Hutchinson( kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Tadeo(kushoto).

KATIBU MKUU WA CCM ABULRAHMAN KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE SHINYANGA VIJIJINI LEO

$
0
0


01Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye wakishiriki katika ujenzi wa Birika la Kunyweshea mifugo linalojengwa katika Kata ya Didia Jimbo la Solwa Katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga vijijini mkoani Shinyanga, ambapo leo katibu Mkuu huyo ameendelea na ziara yake ya siku nne mkoani humo na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika kuimarisha uhai wa chama hicho na utekelezaji wa Ilani ya ya Uchaguzi.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE -SHINYANGA.

WAZIRI WA WA NCHI AFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS BI. FATMA ABDULHABIB FEREJI AZINDUA BODI YA MAKAMISHNA WA TUME YA UKIMWI

$
0
0

WAZIRI WA WA NCHI AFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS BI. FATMA ABDULHABIB FEREJI AKIZINDUA BODI MPYA YA MAKAMISHNA WA TUME YA UKIMWI ZANZIBAR KWENYE OFISI YA TUME YA UKIMWI SHANGANI.
========  =======  ==========
NA RAMADHANI ALI / HABARI MAELEZO ZANZIBAR.  
                          
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Ferej leo amezindua Bodi mpya ya Makamishna wa Tume ya Ukimwi Zanzibar na kuitaka kushirikiana kwa karibu zaidi na wadau mbali mbali kuanzia ngazi ya chini ili kuhakikisha maambukizi ya janga la Ukimwi yanapungua na kufikia lengo la  Zanzibar bila Ukimwi inawezekana. Waziri Ferji amewaeleza wajumbe hao kwamba Ukimwi ni janga la Taifa, na mapambano ya ya gonjwa hilo yamejaa changamoto nyingi ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi kwani  bado wapo watu hawataki kuelewa ingawa juhudi kubwa za kuwaelimisha zimechukuliwa.

Katika kuanza kazi zake, Waziri wa Nchi Afisi ya Mkamu wa Kwanza wa Rais ameieitaka safu  mpya ya Makamishna  kufanya ziara za mara kwa mara sio katika maofisi tu bali  kuwapitia wadau kujua changamoto zinazowakabili kwa lengo la kunagalia namna Tume inavyoweza kusaidiana nazo katika kuzitatua. “Hilo  ni jambo muhimu sana na tukifanya hivyo tutaweza sote kujiridhisha na yale tunayojipangia kuyatekeleza katika mipango yetu ya mwaka au robo mwaka,”alisisitiza Waziri Fatma Abdulhabib Ferej.

Amewashauri Makamishna  wapya  katika kipindi  cha miaka mitatu ya kazi, kuendelea kuwa karibu zaidi na watendaji  na Wafanyakazi wa Tume katika kusimamia  utendaji na uwajibikaji ili kufikia lengo  la kuanzishwa sheria namba 3 ya mwaka 2002 ya  Tume ya Ukimwi Zanzibar. Amesema kwa upande wake na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa jumla wapo tayari kutoa kila msaada kwa Tume kila itapohitajika ili kufanikisha kazi zao kwa ufanisi mkubwa. 

Ameeleza matumaini yake kuwa kutokana na Tume hiyo mpya kusheheni Makamishna wenye uzoefu mkubwa na shughuli  za Bodi na mapambano dhidi ya ukimwi  hategemei kama shughuli zitazozorota.

Amewapongeza wajumbe  waliomaliza muda wao kwa namna walivyoisaidia Tume ya Ukimwi licha ya changamoto nyingi walizokabiliana nazo lakini busara zao na uwezo wao umesaidia sana ufanisi katika shughuli za Tume.  ‘Ni imani yangu ya dhati  kwamba mafanikio yaliyopatikana ndani ya Tume yametokana na michango yao kutokana na uzoefu wao pamoja na maelekezo yao, ’alisema Waziri Ferej.

Alitaja moja  ya fanikio la kujivunia kwa Makamishna hao ambalo ni la kupigiwa mfano ni kwamba wakati baadhi ya nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wamefikia kiwango cha maambukizo cha asilimia kati ya ishirini na thelathini katika miaka ya hivi karibuni, Zanzibar imeweza kudhibiti kiwango cha maambukizo chini ya asilimia moja.

Amewaomba wajumbe hao kuwa tayari kuendelea kuisaida Tume mpya kila watakapohitajiwa kufanya hivyo kwa vile ni watu wenye uwezo mkubwa katika kusaidia maendeleo ya Tume ya Ukimwi.

Katika uzinduzi wa Bodi uliofanyika Tume ya Ukimwi Shangani, limpongeza Mwenyekiti aliemaliza muda wake Professa Saleh Idrissa Mohammed kwa kuteuliwa tena na Rais kwa kipindi chengine  cha miaka mitatu na kueleza kuwa ni kutokana na uwezo wake mkubwa alioonyesha katika kuiongoza Bodi hiyo.

Kwa upande wake Professa Idrissa amemuhakikishi Waziri kwamba watatekeleza wajibu wao waliokabidhiwa na Taif na kuhakikisha huduma za Tume zinawafikia wananchi wote na kufikia lengo la kuhakikisha janga la ukimwi linapungua kwa kiasi kikubwa na vizazi vijavyo visome historia kuwa kulikuwa na Ukimwi Zanzibar. 

Makamishna  wapya wa Tume ya Ukimwi Zanzibar ni Abeid Saad Said kutoka Taasisi zisizo za Kiserikali, Sheikh Mziwanda Ahmed Taasisi za Dini, Hasina Hamad kutoka vyombo vya Habari, Munira Humud Taasisi za Biashara na mjumbe mmoja kutoka Jumuiya ya watu wanaoishi na Viruza vya ukimwi Zanzibar.

Wajumbe  wanaoingi moja kwa moja kwa mujibu wa nyadhifa zao ni Makatibu Wakuu wa Wizara ya Elimu, Wizara ya Afya, Wizara ya Vijana, Wanawake na watoto na Uwezeshaji wananchi kiuchumi pamoja na Wizara ya Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ.
                                                       
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR                          

PRESIDENT KIKWETE ARRIVES IN NAMIBIA FOR A ONE DAY SUMMIT OF THE SADC TROIKA-ORGAN ON POLITICS, DEFENCE AND SECURITY

$
0
0
H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania is received by Namibia’s Minister for Home Affairs, Mrs. Rosalia Nghidinwa at the Hosea Kutako International Airport in Windhoek Namibia ahead of a one-day Summit of the Southern Africa Development Community (SADC) Troika-Organ on Politics, Defence and Security Summit today September 11, 2013 held at the State House in Windhoek.
H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania ( attends a one-day Summit of the Southern Africa Development Community (SADC) Troika-Organ on Politics, Defence and Security today September 11, 2013 at the State House in Windhoek, Namibia, under its chairman President Hifikepunye Pohamba of Namibia. Second left if the SADC Chairperson Dr Joyce Banda,second right is President Joseph Kabila of the Democratic Republic of Congo.STATE HOUSE PHOTOS.
Viewing all 46329 articles
Browse latest View live




Latest Images