Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1602 | 1603 | (Page 1604) | 1605 | 1606 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe ashiriki maadhimisho ya siku ya mtoto Afrika Wilayani Gairo akiwa mgeni rasmi.
  Maadhimisho hayo yamefanywa na Vituo vya huduma ya mtoto vilivyopo kwenye makanisa 13 ya Injili yaliyopo Wilaya ya Gairo na Kongwa chini ya "Compassion International Centre".
  Katika hotuba yake Mhe. Mchembe aliwakumbusha chimbuko la siku ya mtoto ambapo watoto zaidi ya 2000 waliuwawa na makaburu Kitongoji cha Soweto Afrika Kusini.
  Vifo hivyo vilitokana na watoto hao kuandamana wakipinga elimu ikiyokuwa ikitolewa na makaburi kwa mrengo na manufaa ya utawala wa kibaguzi.
  Umoja wa Afrika kwa kukumbuka siku hiyo kila mwaka tarehe 16/6 tangu mwaka 1991 wamekuwa wakiadhimisha siku hiyo na Tanzania ni miongoni mwa nchi hizo.
  Mhe. Mchembe alipokea maandamano ya watoto wakiwa na mabango mbalimbali yaliyolenga kufikisha ujumbe wa kauli mbiu ya mwaka 2018 " KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA TUSIMUACHE MTOTO NYUMA".
  Mabango hayo, maigizo, ngonjera, mashairi, shuhuda na nyimbo vililenga kufikisha ujumbe wa vilio vya watoto. Maeneo yaliyogusiwa ni kama vile ubakaji, ukawiti, unyanyasaji, ukeketaji, ndoa na mimba za utotoni.
  Mhe. Mchembe alitoa taarifa ya Serikali akieleza jinsi ambavyo Serikali imekuwa mstari wa mbele ikishirikiana na wadau mbalimbali kulinda haki za mtoto hasa wenye mazingira magumu:-
  ūüĎČ Kutoa elimu bila malipoūüĎČ Vituo vya Polisi kuunda dawati la jinsia kwa ajili ya wanawake na watoto. Ubakaji, ukeketaji, ulawiti na mimba za utotoni unaripotiwa na kushughulikiwa.ūüĎČ Uundwaji wa dawati la ulinzi na usalama mashuleni, kwenye vitongoji hadi kata.ūüĎČ Wizara kuandaa mwongozo kama nyenzo ya kushughulikia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake.
  Mhe. Mchembe aliwaeleza mikakati ya Wilaya katika kukabiliana na changamoto ya mtoto ikiwemo:-
  ūüĎČ Mwezi wa nne 2018, Mhe. Mchembe kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama waliunda kamati maalum ya ulinzi na usalama kuchunguza suala zima la mimba za utotoni kuanzia chanzo, visababishi na mikakati ya kulimaliza tatizo hilo.ūüĎČ Kupiga marufuku maridhiano nje ya mahakama na wazazi watakaokamatwa watashughulikiwa.ūüĎČ Elimu kwa wazazi kuepuka lugha zisizofaa kwa watoto.ūüĎČ Kukemea vipigo vinavyopitiliza utu wa mtoto.
  ūüĎČ Kukamata wazazi wa wanafunzi watoro na wanaobainika kuwazuia watoto wasifanye vizuri wakati wa mitihani.ūüĎČ Kukemea mila potofu hasa ukeketaji na kuoza watoto. Wazazi watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Hadi sasa kesi zipo Mahakama ya Wilaya ya Kilosa.¬†
  ūüĎČ Aidha Mhe. Mchembe aliwaasa watoto kujilinda na kulindana. Pia watoe taarifa haraka wanapobaini kufanyiwa vitendo hivyo au mwenzao kufanyiwa.
  Katika kuelezea kauli mbiu ya kuelekea uchumi wa viwanda tusimuache nyuma mtoto Mhe. Mchembe alielezea mambo yafuatayo:-ūüĎČ Kwenye sekta ya elimu watoto wanapata elimu bora na sio bora elimu. Serikali ya Magufuli imehakikisha kuna madawati, madarasa, maabara, nyumba za waalimu, kuboresha ufundishwaji pamoja na stadi za kazi.ūüĎČ Malezi bora ni ya wote kuanzia familia, koo, jamii, makanisa na misikiti nk

  0 0

    
  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeihakikishia Serikali ya Norway kuwa inaendelea kuelekeza nguvu zake kwenye kuweka mikakati sahihi ya kuvutia uwekezaji kutoka nje ya nchi, ikiwemo nchi ya Norway, ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa Tanzania.

  Hayo yamesemwa na Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania alipokutana na Bw. Jon Lamoy, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Norway lijulikanalo kwa kifupi kama NORAD mwanzoni mwa ziara yake ya kikazi ya siku tatu Mjini Oslo, makao makuu ya Norway.

  Katika mazungumzo yao, Mkurugenzi Lamoy alimueleza Waziri Mahiga kuwa shirika hilo limekuwa na uhusiano wa karibu na wa kindugu kwa zaidi ya miongo mitano na nchi ya Tanzania. Yeye binafsi na washirika wengi wa Tanzania nchini humo wanasifu utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli hususan kwenye mapambano dhidi ya rushwa. 

  Rushwa inarudisha nyuma maendeleo kwa kuikosesha nchi mapato, hivyo jitihada za Tanzania za kupambana na rushwa, hususan kwenye ukusanyaji kodi, zitawawezesha wananchi wa Tanzania kunufaika na huduma za kijamii na hatimaye kupata maendeleo kwa haraka.

  Hata hivyo mkurugenzi huyo alitoa angalizo kuwa nia nzuri ya Serikali ya Tanzania ya kuweka mifumo thabiti ya uwekezaji wenye faida  ukiwemo ule wa sekta ya madini, ni muhimu ikakamilika mapema ili kutoa fursa kwa wawekezaji wapya kuwekeza kwenye sekta hiyo kwa wakati.

  Kwa upande wake, Mheshimiwa Mahiga alielezea kuwa suala hilo tayari linafanyiwa kazi ambapo pamoja na Serikali kuweka mazingira rafiki  kwa wawekezaji, uwekezaji huo ni lazima uwe na faida kwa Watanzania na kwa maendeleo ya nchi.

  ‚ÄúSerikali ya Rais Magufuli imedhamiria kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa kati unaoongozwa na sekta ya viwanda. Katika kutekeleza hilo, Serikali imepitia na kurekebisha baadhi ya sheria na mikataba ambayo ilikua inanufaisha upande mmoja. Marekebisho yanayofanyika sasa yanalenga kwenye kuleta faida kwa pande zote mbili yaani win win situation‚ÄĚalisisitiza Dkt. Mahiga.

  Kwenye mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Prof. Adolf Mkenda, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Balozi wa Tanzania nchini Norway, Dkt. Wilbroad Slaa mwenye makazi yake nchini Sweden kwa pamoja walielezea kuwa marekebisho hayo, yatakapokamilika, yatarutubisha mazingira ya uwekezaji Tanzania ikiwemo mikataba itakayoridhiwa na Bunge ambayo italeta manufaa kwa pande zote mbili kama zifanyavyo nchi nyingi duniani, ikiwemo Norway.

  Awali kabla ya mkutano huo, Mheshimiwa Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya STATOIL yenye makao yake makuu Mjini Oslo, ambayo kwa sasa nchini humo inajulikana kama Equinor. Kampuni ya STATOIL Tanzania ni mshirika mkubwa nchini Tanzania kwenye shughuli za utafutaji na upatikanaji wa gesi.

  Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya Statoil Bw. Lars Christian Bacher alielezea shughuli za kampuni hiyo Tanzania ikiwemo kujenga uwezo wa ndani ya nchi kwa Watanzania kuijua na kuendesha sekta hiyo muhimu kwa ukuaji wa uchumi. Kwa sasa kampuni hiyo inatoa ufadhili wa masomo ya shahada ya uzamili kwa Watanzania kumi kila mwaka kwenye eneo la mafuta na gesi.

  Bw. Bacher pia alieleza kuwa uwekezaji wa kampuni hiyo kwenye masuala ya gesi ni wa muda mrefu, na matunda yake yanachukua muda kuonekana. Lakini yakishatoka yataongeza mara mbili upatikanaji wa nishati ya umeme nchini Tanzania, ambapo itaongeza uzalishaji wa viwanda pamoja na faida nyingine nyingi za kiuchumi.

  Ujumbe wa Waziri Mahiga ulisifu jitihada za kujenga uwezo kwa Watanzania na kuelezea kuwa hatua hiyo itasadia sana kwenye kutoa elimu kwa Watanzania ili wawe na matarajio sahihi ya matokeo ya shuguli za uwekezaji wa kampuni hiyo nchini Tanzania. Waziri Mahiga aliwasihi kuendelea kujenga uwezo wa kada ya kati ya wataalam wa gesi kwa kushirikiana pia na vyuo vya ndani ya nchi ili utaalamu huo uendelezwe nchi nzima.

  Waziri Mahiga yupo nchini Norway kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 18 hadi 20 Juni 2018, kufuatia mualiko wa mwenyeji wake Mhe. Ine Eriksen Soreide, Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway. Ziara hiyo imekuja baada ya Tanzania na Norway kusaini makubaliano ya ushirikiano mwaka 2017. 

  Mbali na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Mheshimiwa Mahiga na ujumbe wake wanatarajiwa kukutana na makampuni ya Norway yanayowekeza Tanzania pamoja na kuzungumza kwenye Jukwaa la Oslo kuhusu uthabiti wa amani kwenye Eneo la Maziwa Makuu na mchango wa nchi jirani.

  Jukwaa la Oslo linakutanisha watu mashuhuri duniani wanaoshughulika na utatuzi wa migogoro duniani akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Mkutano huu hufanyika mara moja kila mwaka kujadili masuala ya utatuzi wa migogoro duniani.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  Dar es Salaam, 19 Juni, 2018

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumzana Balozi wa Sweden nchini Mhe. Katarina Rangnitt ambaye amemaliza muda wake wa kazi .Balozi Katarina Rangnitt alifika ofisi kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumuaga rasmi Makamu wa Rais. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi zawadi Balozi wa Sweden nchini Mhe. Katarina Rangnitt ambaye amemaliza muda wake wa kazi .Balozi Katarina Rangnitt alifika ofisi kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumuaga rasmi Makamu wa Rais
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Katarina Rangnitt aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kumuaga baada ya muda wake wa kazi nchini kumalizika. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Katarina Rangnitt ambaye amemaliza muda wake wa kazi .Balozi Katarina Rangnitt alifika ofisi kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumuaga rasmi Makamu wa Rais

  0 0


  Na Frankius Cleophace Tarime

  Wanawake wametakiwa kujenga Umoja na Ushirikiano na Waume zao pamoja nakuwa waaminifu katika kutunza mali zao ikiwemo fedha ili kujiinua na kuongeza Uchumi wa Nchi kwa Ujumla.

  Hayo yamebainishwa na Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mara Conference George Ezekiel katika Uzinduzi wa Nyumba ya Kulala wageni iliyojengwa na Kampuni ya SOJEMA Mjini Tarime Mkoani Mara.

  Askofu huyo amesema kuwa Wanawake wengi siyo waaminifu katika suala zima la fedha jambo ambalo linapelekea waume zao kushindwa kuwaamini na kuwapa Miradi Mikubwa ili waweze kusimamia hivyo amezidi kusisitiza suala la Uaminifu kwa waume zao ili waweze kupewa Mitata na kusimamia Miradi yao kwa lengo la kujikomboa Kiuchumi.

  Askofu ameshukuru Kampuni ya SOJEMA kwa kushirikisha Viongozi wa Dini na Serikali katika ufunguzi wa Nyumba ya Kulala Wagenzi iliyopo Mtaa wa Mwangaza Mjini Tarime huku akisihi jamii kuiga Mfano huo wa kufanyia Maombezi Nyumba zao za biashara ili Mwenyezi Mungu azidi kuzibariki na kuepuka Majaribu.

  ‚ÄúWengi waliobarikiwa na Mwenyezi Mungu wamekuwa wakijenga Nyumba zaao ata za kuishi lakini hawashirikishi Mwenyezi Mungu hivyo sasa huu ni mfano mzuri wa Kuigwa‚ÄĚ alisema Askofu.

  Eziekieli amezungumzia Pia suala la Jamii kuendelea Kutumikia Mwenyezi Mungu na siyo kukumbatia Mila potofu ambzo zinanyima Mwanamke uhuru katika Jamii inayomzunguka likiwemo suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa kike.

  Angela Godfrey kutoka kampuni ya SOJEMA anazidi kusisitiza suala la Mwanamke kudhubutu na kudai kuwa wanawake wanaweza hivyo sasa wanaume waweze kuwapa Mitaji na kuwaamini ili kuendesha Biashara zao

  ‚ÄúMimi nimeweza kushirikiana vyema katika Ujenzi wa Nyumba hii ya kulala wageni na mme wangu ameniamini nimekuja kuifungua hayupo yote ni kwa sababu ya uaminifu‚ÄĚ alisema Angela.  Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mara Conference George Ezikiel Ojwang akikata Utepe kama ishara ya uzinduzi rasmi Nyumba ya Kulala wageni iliyojengwa na Kampuni ya SOJEMA Katika Mtaa wa Mwangaza Mjini Tarime Mkoani Mara.
   Sehemu ya jengo hilo kama lionekanavyo nje
  Baadhi ya Wageni mbalimbali walioshiriki kwenye hafla hiyo

  0 0

  Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa akikata utepe katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu iliyofanfyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. 

  Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa (wa pili toka kulia) akipokea ngao ya heshima kutoka kwa mawaziri kuanzia kushoto, Selemani Jafo (TAMISEMI), Jenista Mhagama (Waziri wa Nchi ‚Äď Ofisi ya Waziri Mkuu) na Ummy Mwalimu (Afya) kulia kabisa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu iliyofanfyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo.

  Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti mojawapo ya mabalozi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu katika uzinduzi uliofanfyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. 

  Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wageni mbali mbali wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu iliyofanfyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. 

  Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa akihutubia katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu iliyofanfyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. 

  Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) , Dkt Leonard Maboko akihutubia wageni waalikwa katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu iliyofanfyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa.

  Baadhi ya wakuu wa mikoa mbali mbali wakishiriki katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu iliyofanfyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa.

  Baadhi ya wageni waalikwa kutoka taasisi na mashirika mbali mbali pamoja na wananchi wakishiriki katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu iliyofanfyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa.  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu akihutubia katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu iliyofanfyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ‚Äď Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mhe Jenista Mhagama akihutubia katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu iliyofanfyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa.  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ‚Äď Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe Selemani Jafo akihutubia katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu iliyofanfyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa.¬†

  Msanii Nandy akitumbuiza wananchi na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni Waziri mkuu, Mhe Kassim Majaliwa. 

  Wananchi mbali mbali wakisubiri kupima afya zao wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu iliyofanfyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni Waziri mkuu, Mhe Kassim Majaliwa.

  0 0

  Picha ya pamoja nje ya jengo jipya la kisasa la Mahakama ya Mwanzo na Mahakama ya Wilaya Kigamboni, Mhe. Gadenya ameisifu Mahakama kwa maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika na ambayo tayari ameshafanyika kwa ustawi wa Wananchi.(Picha na Mary Gwera, Mahakama)
  ¬†Jaji wa Mahakama Kuu ya Uganda, Mhe. Paul Gadenya akitia saini kitabu cha wageni pindi alipowasili katika Mahakama ya Wilaya Kigamboni kujionea jengo hilo la kisasa lililojengwa kwa teknolojia ya ujenzi ya Moladi, mbali na kutembelea jengo hilo Jaji Gadenya ametembelea Ofisi za Kitengo cha Maboresho ya Mahakama ‚ÄėJDU‚Äô kupata taarifa ya maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika ndani ya Mahakama kwa lengo la kuboresha huduma za utoaji haki nchini, aliyesimama kulia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kigamboni, Mhe. Sundi Fimbo.
   Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kigamboni, Mhe. Sundi Fimbo, akimpitisha Mhe. Jaji Gadenya kukagua sehemu mbalimbali za jengo hilo la kisasa, aliyepo nyuma ya Mhe. Gadenya ni Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji na Tathmini, Mahakama, Bw. Sebastian Lacha. 
   Mhe. Jaji Gadenya (kushoto) akijadili jambo na wenzake, kulia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kigamboni, Mhe. Sundi Fimbo na katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji na Tathmini, Mahakama, Bw. Sebastian Lacha.
  0 0

  Ramadhani Ali ‚Äď Maelezo Zanzibar

  Wakala wa Chakula na Dawa  Zanzibar (ZFDA) imezuia kusambazwa bidhaa za chakula na vipodozi zilizoingizwa nchini kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na siku kuu ya Idd el Fitri kinyume na taratibu na zilizokuwa hazifai kwa matumizi ya binadamu.

  Mkurugenzi Mtendaji wa ZFDA Dkt. Burhan Othman Simai alisema bidhaa hizo zilikamatwa kufuatia operesheni maalumu waliyoifanya katika kipindi cha miezi miwili kwenye maghala ya wafanyabiashara na baadhi ziligundulika zimetupwa katika jaa la Kibele na eneo la Migombani.

  Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Mombasa Dkt. Burhani alizitaja bidhaa zilizokamatwa na zilizotupwa kuwa ni mchele tani 40, unga wa sembe tani 75,  sukari tani 25 na lita 15,000 za mafuta ya kula.

  Alisema dawa na vipodozi vilivyokamatwa ni vichupa 4000 vya chanjo aina ya ATS kutoka China zilizoingizwa nchini kinyume na miongozo ya uingizaji na utoaji wa dawa nchini, na tani tisa za vipodozi vyenye viambata vya sumu kali inayosababisha saratani ya ngozi.

  Dkt. Burhan alieleza masikitiko yako kwa baadhi ya wafanyabiashara kutoa sadaka bidhaa hizo bila kuangalia athari inayoweza kuwapata wananchi wenzao baada ya kuzitumia.
  MKURUGENZI Mtendaji Bodi ya Chakula na Dawa Zanzibar, Dkt. Burhan Othman Simai (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na zoezi la Kukamata bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya Binaadamu miezi miwili iliyopita. 
   Mkuu wa Ukaguzi wa Chakula Mohammed Shadhil (kushoto) na Muangalizi wa Ofisi Mussa Bakar Othman wakionesha  vipodozi vyenye chemicali za sumu zilizoingizwa kwa ajili ya siku kuu
  Aina za Bidhaa za Mchele, Unga wa Ngano,Mafuta ya Kula na vipodozi zilizokamatwa na ZFDA ambazo  hazifai kwa  matumizi ya Binaadamu.
  Picha na Abdalla omar Maelezo ‚Äď Zanzibar.


  0 0

  Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Juni 19,2018 imeadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa kila mwaka Juni 16 huku Shirika la Kimataifa la Save The Children limetumia maadhimisho hayo kugawa vitabu vinavyohusu haki na wajibu wa watoto kwa maslahi chanya.
  Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo Kambarage Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
  Shirika la Save the Children limegawa vitabu vinavyozungumzia Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto katika lugha rahisi kwa watoto ili kutetea haki na wajibu wa mtoto kwa maslahi chanya lakini pia vitabu vinavyohusu malezi bora kwa watoto.
  Akizungumza wakati wa kugawa vitabu hivyo,Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto mkoa wa Shinyanga, Antonio Chuhila alisema vitabu hivyo vitawasaidia kwa kiasi kikubwa watoto kujua wajibu na haki zao ili kukabiliana na vitendo vya kikatili ambavyo wamekuwa wakifanyiwa.
  ‚ÄúVitabu hivi vimeandikwa na kuchapishwa na shirika la Save The Children na vimeandikwa kwa lugha rahisi kabisa kuwezesha watoto kuelewa haki na wajibu wao‚ÄĚ,alisema Chuhila.
  Kwa Upande wake,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro alilipongeza shirika la Save The Children kwa kugawa vitabu kwa watoto kwani hiyo ni njia ya kuwasaidia watoto kujua haki zao.
  ‚ÄúNiwashukuru sana Save The Children kwa kutoa vitabu vigumu sana kutetea haki za watoto kama watoto hawajui haki zao,lakini kama watoto watajua haki zao itakuwa rahisi kuripoti matukio yanayowasibu,hivyo naomba watoto mkasome vitabu hivi ili mjue haki zenu‚ÄĚ,alisema Matiro.
  Hata hivyo Matiro aliitaka jamii na wadau wote kushirikiana katika kulinda haki za watoto huku akiwaasa watoto kutonyamazia kimya vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa.Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika manispaa ya Shinyanga yametanguliwa na maandamano ya watoto kutoka Viwanja vya Shycom hadi Viwanja vya Sabasaba,kasha Mkuu wa wilaya Josephine Matiro kukagua vibanda ili kujionea shughuli za maendeleo zinazofanywa na watoto. 
  Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika mwaka huu ni ‚ÄúKuelekea uchumi wa viwanda,Tusimuache mtoto nyuma‚ÄĚ.

  Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto mkoa wa Shinyanga, Antonio Chuhila akimuonesha Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro vitabu vinavyozungumzia Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto vilivyotolewa na shirika la Save The Children leo wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika katika Manispaa ya Shinyanga 
  Muonekano wa moja ya vitabu vilivyotolewa na Shirika la Save The Children kwa watoto wa Manispaa ya Shinyanga
  Muonekano wa vitabu hivyo
  Katibu wa Baraza la Watoto Mkoa wa Shinyanga Victoria Deogratius akimkabidhi vitabu vinavyohusu haki za watoto mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia vitabu vinavyohusu haki za watoto
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati akiangalia vitabu vinavyohusu haki za watoto vilivyotolewa na shirika la Save The Children
  Getruda George kutoka shirika la Save The Children akigawa vitabu kwa watoto wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika manispaa ya Shinyanga.
  Getruda George kutoka shirika la Save The Children akiendelea kugawa vitabu kwa watoto
  Watoto wakisoma vitabu vinavyohusu haki za watoto
  Watoto wakionesha vitabu vya haki za watoto
  Watoto wakiwa katika viwanja vya Sabasaba wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika manispaa ya Shinyanga.
  Watoto wakiandamana kutoka Viwanja vya Shycom kuelekea viwanja vya Sabasaba mjini Shinyanga wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika manispaa ya Shinyanga.
  Watoto wakiwa wameshikilia bango wakati wa maandamano hayo.
  Watoto wakiwa wameshikilia bango wakati wa maandamano hayo.
  Maandamano yanaendelea..
  Watoto wakiendelea kuandamana
  Meza kuu wakiwa wamesimama kupokea maandamano ya watoto katika viwanja vya Sabasaba Mjini Shinyanga
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika manispaa ya Shinyanga.
  Wadau wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa maadhimisho hayo.
  Watoto wakiwa eneo la tukio
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika katika manispaa ya Shinyanga
  Wadau wa haki za watoto wakionesha bidhaa zinazozalishwa na watoto
  Watoto wakitoa burudani ya wimbo wakati wa maadhimisho hayo
  Fatuma Omary akisoma risala ya watoto
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa zawadi ya madaftari na kalamu kwa watoto/vijana wanaoishi katika mazingira magumu zilizotolewa na wadau wa haki za watoto katika manispaa ya Shinyanga.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa zawadi ya madaftari na kalamu kwa mtoto
  Wanafunzi wa Tuseme Klabu kutoka shule ya Sekondari Mwasele wakiimba shairi.
  Watoto kutoka baraza la watoto kata ya Kambarage wakionesha mchezo wa igizo kuhusu haki za watoto
  Wadau wa haki za watoto wakiwa katika viwanja vya Sabasaba mjini Shinyanga.
  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

  Na Estom Sanga- TASAF

  Maafisa kutoka nchini Nigeria walioko nchini kujifunza namna Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF unavyotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wameipongeza serikali ya Tanzania kwa kutekeleza kwa mafanikio Mpango huo wenye lengo la kupambana na umaskini.

  Wakizungumza baada ya kutembelea eneo la Nzasa A katika halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam, Wataalamu hao kutoka Nigeria pamoja na mambo mengine wameshuhudia Walengwa wa TASAF wakijishughulisha na uzalishaji wa bidhaa kama mikeka, vikapu ,vyungu kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.

  Aidha maafisa hao kutoka Nigeria wameshuhudia namna Walengwa walivyoboresha makazi yao kwa kujenga nyumba huku wakielezwa kuwa suala la elimu na afya limepewa kipaumbele kwa Kaya za Walengwa ikiwa ni mkakati maalum wa Mpango huo kujenga rasilimali watu .

  Wakiwa katika eneo hilo la Nzasa A wageni hao walioko nchini pamoja na wageni wengine kutoka Sudan Kusini wamejionea namna walengwa wanavyopata ruzuku kwa njia ya simu ikiwa ni mkakati maalum wa kuboresha huduma hiyo kupitia TASAF.

  Hata hivyo katika ziara hiyo kilio cha Walengwa juu ya upatikanaji wa soko la bidhaa wanazozalisha baada ya kupata ruzuku kutoka TASAF kimeendelea kusikika huku walengwa hao wakiomba mfumo bora zaidi wa kutafuta masoko ya bidhaa wanazozalisha ili waweze kunufaika vizuri zaidi.

  Hii leo (Jumatano)maafisa hao kutoka Nigeria na Sudan Kusini wanatembelea na kukuitana na Walengwa wa TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha na Bagamoyo kujifunza namna Mpango huo unavyowanufaisha Walengwa hao.

  Serikali kupitia TASAF imefanikiwa kuandikisha zaidi ya Kaya Milioni MOJA NA LAKI MOJA nchini kote katika Mpango huo ambao pamoja na kupata ruzuku ya fedha ya kilamwezi, lakini pia wamekuwa wakipewa mafunzo ya namna ya kukuza kipato chao kwa kuanzisha miradi midogo midogo kwenye maeneo yao.
   Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na serikali kupitia TASAF moja ya malengo yake ni kuihamasisha Walengwa wa Mpango huo kufanya shughuli za uzalishaji mali ikiwemo ususi wa vikapo,mikeka na kuuza kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato. Pichani hapo juu wageni kutoka nchini Nigeria walioko nchini kujifunza na TASAF inavyotekeleza majukumu yake wakiangali bidhaa zilizotengenezwa na Walengwa wa Mpango huo.
   Mmoja wa Wageni kutoka Nigeria akiwa ameshika kikapo alichokinunua kutoka kwa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF katika eneo la Nzasa B katika kata ya Charambe wilaya ya Temeke mkoani Dar es salaam.
   Baadhi ya maafisa kutoka nchini Nigeria walioko nchini kujifunza namna Mfuko wa Maendeleo  ya Jamii TASAF unavyotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini  wakiangalia bidhaa zinazouzwa na Wanufaika wa Mpango huo  katika eneo la Nzasa B wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.
   Maafisa kutoka Nigeria wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke na TASAF baada ya kupata maelezo ya namna halmashauri hiyo inavyotekeleza  Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini .
   Wageni kutoka nchini Nigeria wakiangalia baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- katika  mtaa wa Nzasa B kata ya Charambe wilaya ya Temeke mkoani Dar es salaam.

  0 0

  Na Nelson Nchobe wa LITA

  Duniani kote taka ni kero au adha ndogo katika familia kwa sababu moja tu: katika ngazi ya kaya watu ni wachache na taka ni adha ambayo watu hao wachache wanaweza kuimudu. Ili kuondokana na kero hiyo, kwa desturi, wanakaya hukusanya taka na kuziweka eneo moja.

  Lakini kaya nyingi katika mtaa au kijiji zinapokusanya taka nakuzirundika eneo moja, ubaya wa taka unapanda daraja; taka inakuwa siyo adha au changamoto ndogo tena bali taka inageuka nakuwa ni tatizo KUBWA; rundo hilo la ataka linakuwa ni jambo la hatari. Hivyo ndivyo ilivyo duniani kote.

  Kwa hiyo katika nchi zote duniani ukusanyaji na uhifadhi salama wa taka vimekuwa ni tatizo sugu kwa sababu kila siku taka huzalishwa majumbani, ofisini na viwandani. Taka hizo sasa zimekuwa ni kitu cha hatari kwa uhayi wa mwanadamu na viumbe wengine. Taka zimekuwa jambo la hatari kwa sababu kimsingi taka ni uchafu na uchafu ni chanzo cha magonjwa karibu yote. Lakini si hayo tu, taka zingine ni sumu inayoharibu mazingira na kuangamiza viumbe hai, wakiwemo wanadamu.

  Kwa kuwa ukusanyaji na uhifadhi salama wa taka ni tatizo la kidunia, mataifa yote yamekuwa yakihangaika ili kushinda tatizo hilo. Sasa dalili za kupambana vilivyo na tatizo hili kidunia zinaanza kuonekana mwisho wa upeo wa macho kwa sababu kuna juhudi zinazoratibika zikiongozwa na asasi ijukanayo kama Let’s Do It World chini ya taasisi iitwayo Let’s Do It Global Foundation. 

  Japo ukusanyaji na uhifadhi salama wa taka nchini Tanzania bado ni ndoto, Tanzania tayari imesajiliwa na taasisi ya Let’s Do It Global Foundation kuwa ni kati ya nchi zenye dhamira ya kweli katika kupambana na taka na kulinda mazingira. Lakini kusajilika tu hakutoshi; kikubwa ni bidii ya kweli ya kukusanya na kuhifadhi salama taka zizalishwazo nchini kwa mujibu wa sheria. Afrika ina nchi 42 ambazo zimesajiliwa katika zoezi hili wanachi wan chi hizo tayari wameishapata mafunzo.

  Kihistoria msukumo wa hiari wa kupambana na taka ulianzia katika nchi ndogo ya Estonia huko Ulaya mwaka 2008. Msisimko huu sasa umesambaa duniani na nchi 133 and watu takribani milioni 20 wanashiriki katika ukusanyaji wa hiari wa taka zinazozagaa sehemu zisizo rasmi au taka zilizo nje ya madapo yanayotambuliwa na mamlaka husika katika nchi.

  Huko Estonia msisimko huu wa kushangaza tarehe 3 Mei, 2008 uliamsha ari ya watu kuchukia taka katika nchi yao hata watu 50,000 wakaungana pamoja na kuisafisha nchi yao yote katika muda wa saa tano tu! Na Waestonia waliisafisha nchi yao chini kauli mbiu ya Let’s Do it ( yaani basi na tulifanye jambo hili). 

   Wao walikusanya taka bila shuruti kwa mapenzi ya taifa lao, kwa uelewa na dhamira ya kweli ya kujitegemea, pasipokujua kwamba wanawasha moto wa heri utakaosambaa duniani kote na kuzaa asasi iitwayo Let’s Do It World na taasisi mama ya Let’s Do It Global Foundation.

  Mtu anaweza kusema, jambo hili liliwezekana kwa sababu Estonia ni nchi ndogo. Hapana. Jambo hili liliwezekana kwa sababu ya umakini wa na ari ya wananchi na umahili wa viongozi waasisi wa jambo hili wakiungwa mkono na serikali kuu na serikali za mitaa za nchi hiyo. Hakuna muujiza mwingine! 

  Kama Watanzania tunataka kufanikiwa katika jambo hili ni budi kuwa makini na kuiga umahili wa Waestonia. Maneno na hotuba nzuri vitu vizuri na muhimu, lakini umahili na vitendo ni vitu vizuri na muhimu zaidi. Wananchi wa Estonia walichagua kutenda kwa hiari ndiyo maana wanapigiwa mafano na mataifa 133 kote duniani.

  Chini ya uratibu wa asasi ya Let’s Do It World na taasisi Let’s Do It Global Foundation, sasa dunia imechagua tarehe 15 Septemba, mwaka huu kuwa siku ya kukusanya taka kwa hiari duniani. Jambo hili serikali ya Tanzania imelikubali. Kauli ya serikali ya kuunga mkono rasmi jambo hili imo katika barua ya tarehe 28 Februari, 2018 iliyoandikwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

  Kabla ya kauli hiyo rasmi, tarehe 15 Februari, 2018 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Bw Selemani Jafo, alizindua kampeni hii ya Let’s Do It-Tanzania na kueleza shahuku yake ya kuona zoezi hili linafanikiwa. Aliueleza mkutano wa wadau kuwa udhibiti wa taka, hasa katika miji ya Tanzania, ni changamoto kubwa sana na kwamba waadhirika wakubwa ni watu maskini. Alieleza kwamba taka zitupwazo ovyo tayari zimeanza kuingia mitoni na baharini na kuchafua vyanzo hivyo vya maji.

  Heshima ya Tanzania na umakini wa baadhi ya taasisi zake umeifanya taasisi inayosimamia na kuendeleza moto wa mageuzi ya kuchukia taka, yaani Let’s Do It Global Foundation, kuiteua asasi isiyo ya kiserikali ya Nipe Fagio kuongoza, hapa Tanzania, harakati au kampeni ya kukusanya na kuhifadhi salama taka zilizokusanywa. Kiongozi wa Taasisi hii, Bi Tania Hamilton, anasema asasi yao haikuchaguliwa tu, bali ina historia ya kufanyakazi na raia.

  ‚ÄúTazama suala la kuwaendea watu na kuwa karibu nao, kuwapa elimu na uelewa juu ya taka na kuwaongoza wabadili tabia, ni kazi yetu ya msingi toka 2013. Kwa hiyo ni jambo linaloingia akilini kuona asasi yetu inateuliewa kuwa kiongozi wa shughuli hii nchini. Tunakiri pia kuwa ni heshima kubwa kwetu,‚ÄĚ ameeleza Bi Tania. Amesema asasi yake itatumia mtandao wake wa wabai kufanikisha jambo hili. Lakini mafanikio ya jambo hili yatategemea hasa mwitiko wa Watanzania wote, hasa watu wazima.

  Tarehe 25 Mei, asasi ya Nipe Fagio iliandaa mkutano Jijini Dar es Salaam kuashiria kukamilika kwa maandalizi ya kampeni kwa upande wa Tanzania.

  Katika mkutano huo walitambulishwa wadau mbali mbali na kuelezwa mkakati wa kitaifa wa Let‚Äôs Do It Tanzania (LDI-T). Kauli mbiu ya kidunia ya LDI ni ‚Äúwatu kwa ajili ya kuwa na sayari safi‚ÄĚ (people for a clean planet).

  Bi Hamilton, ambaye peia ni muasisi wa Nabaki Afrika, ameeleza mkutano huo kuwa kampeni hii ya usafi ni endelevu na kwamba nguvu na msingi wake ni harakati ya kujitolea ya kiraia (civic movement). Katika Tanzania miji sita imeteuliwa kwa zoezi hili ambayo ni Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha, Moshi, na Mbeya.

  Bi.Hamilton amesema mwaka 2012 jarida la Forbes liliitaja Dar es Salaam kuwa jiji la 12 kwa uchafu duniani, na kuwaomba wadau kuzingatia elimu ya mazingira kwa wananchi hasa viongozi wa serikali za mtaa. 

  Kiongozi huyu pia aligusia suala la kubadili mtazamo wa watu kuhusu taka. Katika kampeni hii kidunia na hapa Tanzania, amesema suala la kubadili mtazamo na fikira za watu kuhusu taka ni muhimu sana na wanalichagiza kama ‚Äúupofu dhidi ya uchafu‚ÄĚ (trash blindness). Ameomba katika harakati hizi, chagizo hili liwe ni mbinu ya kubadili mtazamo na tabia za watu juu ya taka zinazowazunguka. Iwe ni mbinu ya kuwafanya Watanzania wachukie taka.

  Sasa, kuliko nyakati nyingine za nyuma, mawazo na mbinu za kutekeleza kampeni ya usafi kitaifa na kidunia vimepatikana. Lengo ni kuzifanya kaya, mitaa na vijiji vichukie taka na kuwa na ari ya kuzikusanya na kuhakikisha zinapelekwa na mamlaka husika katika mahali salama.

  LITA ni mtandao wa waandishi wa habariza sayansi, ubunifu na teknolojia.

  0 0

  Na Frankius Cleophace Rorya

  Serikali Wilayani Rorya Mkoani Mara imepiga Marufuku Jamii kumaliza kesi zinazohusu Ukatili wa Kijinsia Ukiwemo Ubakaji, Utelekezaji wa watoto wadogo, Kuchomwa Moto na Kuwatenga kwa watoto wenye Ulemavu bila kuripoti Kwenye Vyombo vya Sheria ili kuchukua hatua kali kwa wanaotenda Ukatili huo na kumaliza kiundugu jambo ambalo linazidi kunyima Mtoto haki zake za Msingi na hawatalifumbia Macho Kamwe.

  Hayo yamebainishwa na Gabriel Paul ambaye ni Afisa elimu Sekondari Wilayani Rorya kwa niamba ya mkuu wa Wilaya hiyo Simon Chacha katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Kwenye Viwanja vya Obwere Mji Mdogo wa Shirati.

  Gabriel amesema kuwa katika Maeneo mengi vitendo vya Ukatili dhidi ya mtoto vimekuwa vikifanyika lakini jamii wanamaliza Matatizo hayo kiundugu bila kushirikisha Vyombo vya Sheria ili kulinda Mtoto dhidi ya Ukatili huo.

  Pia Gabriel amezitaka idara zote ikiwemo idara ya Maendeleo ya Jamii pamoja na Mashirika Mbalimbali kuendelea kutoa Elimu kwa Jamii juu ya Madhara ya Ukatili wa kijinsia ikiwa nipamoja na kujua Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009.

  Wilaya ya Rorya Imekuwa ikikumbwa na Changamoto ya Mimba kwa Watoto wa Shule za Msingi na Sekondari ambapo Afisa Elimu Sekondari Gabriel Paul anaeleza Mikakati ya Serikali ili kunusuru Mabinti hao huku akisema kuwa tayari watumiwa saba wamefikishwa Mahakani na wamejenga Mabweni saba na wanaendelea kuhamasisha jamii kujenga Mabweni kwa lengo la kuwapunguzia Umbali mrefu mabinti kwa ajili ya kutafuta Elimu na wakati Mwingine kushawishika na kujiingiza kwenye Mapenzi na kupata Mimba zisizojarajiwa.

  Ossoro Siris ambaye ni Mwenyekiti Shirika la Shirika la Tanzaia Education Aid (TEA) amesemakuwa Shirika hilo limekuwa likiwasaidia Watoto hususani mabinti wanaotoka katika Mazingira Magumu kwa kuwalipia ada katika Shule za Serikali na Binafsi kabla ya Elimu bure lakini wa shule binafsi bado wanalipiwa.

  Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma ya Mtoto TZ 704 Wilayani Rorya Justin Lugoye Nyanswede ameiomba Serikali kutoa bure Tauro za Watoto wa Kike Mashuleni ili kutatua Chnagamoto inayowakabili na kushindwa kuudhulia Masomo pale mabadiliko ya Mwili yanapotokea.

  Aidha Watoto hao wamesema kuwa kupitia Kauli mbiu ya Mwaka huu kuwa Kuelekea Uchumi wa Viwanda Usimwache Mtoto Nyuma hivyo wameomba Wazazi kuendelea kuwapatia haki zao za msingi ikiwemo Elimu na kupiga Vita Mimba za Utoto ambazo zinakatisha ndoto zao.
    Afisa elimu Sekondari Wilayani Rorya Gabriel Paul kwa niaba ya mkuu wa Wilaya hiyo Simon Chacha akizungumza  katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Kwenye Viwanja vya Obwere Mji Mdogo wa Shirati.
   Afisa elimu Sekondari Wilayani Rorya Gabriel Paul kwa niaba ya mkuu wa Wilaya hiyo Simon Chacha akipata maaelezo kwa mmoja wa Watoto Mbunifu katika sanaa ya Uchoraji na Uchingaji  katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Kwenye Viwanja vya Obwere Mji Mdogo wa Shirati.
   Afisa elimu Sekondari Wilayani Rorya Gabriel Paul kwa niaba ya mkuu wa Wilaya hiyo Simon Chacha akipata maaelezo kwa baadhi ya Wajasiriamali kuhusua bidhaa zao mbalimbali katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Kwenye Viwanja vya Obwere Mji Mdogo wa Shirati.

  0 0

   Meneja wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi Tigo kanda ya kaskazini, ,Aidan Komba akikabidhi mfano wa Hundi ya Sh Milioni mbili kwa mshindi wa kwanza, Kanda ya Kaskazini wa Promosheni iliyowahusisha Mawakala mtandao wa Tigo kupitia Tigo Pesa,Real Stationary kutoka wilaya ya Same.
   Meneja wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi Tigo kanda ya Kaskazini, ,Aidan Komba akikabidhi mfano wa Hundi ya Sh Milioni moja kwa mshindi wa Pili, Kanda ya Kaskazini wa Promosheni iliyowahusisha Mawakala mtandao wa Tigo kupitia Tigo Pesa,Justin Mbazi kutoka wilaya ya Same.
  Washindi wa Promosehni ya Mawakala wa Mtandao wa Simu za Mkononi ya Tigo kupitia Tigo Pesa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Kampuni ya Tigo mara baada ya kukabidhiwa mifano ya Hundi baada ya kujishindia zawadi za Pesa katika Promosehini hiyo.

  0 0

  KUNA maswali mengi sana yanayoulizwa na watu mbalimbali kuhusu mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Dk. Reginald Mengi, alivyoweza kufikia nafasi aliyonayo kwa sasa akimiliki makampuni kadhaa na mengine kuwa na hisa hapa nchini na ughaibuni.

  Majibu ya maswali hayo na maelezo mengine yatapatikana katika kitabu chake cha kumbukumbu kuelekea utajiri ambacho kitazinduliwa Juni 30 mwaka huu. Kitabu hicho chenye taarifa muhimu kwanza za kumfahamu Mengi ni nani kisha safari yake ndefu kufikia ustawi alionao leo akiwa na makampuni yaliyotawanyika nchini na katika nchi za majirani na mataifa tajiri duniani. 

  Ndani ya kitabu hiki ambapo wakali wa tafakari kimataifa wameandikia maelezo yao ya kukiafiki kama kitabu bora kinachostahili hata kufundishia. Kitabu hicho ambacho kinaelezea safari ya maisha ya Dk. Mengi kutoka kwenye maisha ya kimaskini mpaka kufikia kuwa miongoni mwa wafanyabiashara wenye mafanikio makubwa hapa nchini kitafanyiwa uzinduzi Dar es salaam na kinatarajiwa kuwa mwongozo kwa wasomaji, hususan vijana wanaotaka kuwa wajasiriamali. 

  Kitabu hiki ambacho kinaitwa ‚ÄúI Can, I Will, I Must‚ĶThe Spirit of Success‚ÄĚ (Naweza, Nitaweza, Nitafanya na Moyo wa Mafanikio‚ÄĚ, na kinaelezea kwa undani mambo aliyoyapitia Dk. Mengi mpaka kufikia mafanikio aliyoyapata.¬†Mambo ambayo yanaelezewa kwenye kitabu hicho yamekuwa yakichambua kiini cha msongo kwani majaribu, matatizo, changamoto pamoja na maeneo aliyoshindwa lakini hakukata tamaa kutokana na nia madhubuti na malengo ya kutaka kufanikiwa.¬†

  Mpaka hivi sasa kitabu hicho kimeshapongezwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Juma Mwapachu, ambaye amekielezea kuwa ni simulizi ya mafanikio ya hali ya juu na ni cha kwanza cha aina yake barani Afrika. Ameongeza kuwa simulizi ya kitabu hicho imeweza kuelezea kwa ufasaha na kiufundi jinsi mifumo ya kiuchumi na kisiasa iliyokuwa ikibadilika kwa miongo minne iliyopita ilivyoweza kuathiri jitihada za ujasiriamali nchini Tanzania na kuelezea nini kinahitajika katika kutafuta mafanikio. 

  Pia kitabu kimepongezwa na wanazuoni wastaafu wa Chuo Kikuu Cha Harvard, Profesa Daniel Isenberg na Profesa Sujata Bhatia. 

  Kwa taarifa zaidi kuelekea uzinduzi wa kitabu chake ‚Äėlike‚Äô na ‚Äėfollow‚Äô akaunti zake za mitandao ya kijamii kupitia twitter¬†@regmengi¬†na instagram¬†@regmengi

  0 0

  *Azindua kitabu cha Mafunzo ya umeme wa jua 
  *Atashauri kisambazwe kwa wataalam ,mafundi mitambo 

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

  RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa amewataka watalaam wote na taasisi zinazohusika na nishati ya umeme-jua kuangalia namna ya kupanua wigo wa matumizi ya nishati hiyo ya jua ambayo ipo kwa wingi katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwamo Tanzania. 

  Amefafanua katika kiwango cha Gigawatt 400 za umeme jua zinazotumika duniani kwa sasa bado ni Gigawatt moja tu ndio zimefungwa na kutumika katika nchi za Afrika ,Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa namna mbili. 

  Mkapa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazindua Kitabu cha Mafunzo ya Umeme wa Jua ambacho mtunzi na mwandishi wake ni Godwin Msigwa.Kitabu hicho ambacho kimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili kitasaidia kusambaza taaluma na maarifa katika eneo la nishati ya umeme wa jua nchini. 

  Akizungumza kabla ya kuzindua kitabu hicho ambacho ameomba kisambazwe kwa watalaamu wa nishati ya umeme jua na mafundi mitambo wa umeme jua, amesema pamoja na duniani kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme unaotokana na jua bado nchi za Afrika zipo chini kwenye matumizi. 

  Mkapa amefafanua kwa mujibu wa taarifa za Mtandao wa jarida la kimataifa la nishati Jadidifu linaloitwa REN 21 ya 2018 hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2017 jumla ya zaidi ya Gigawatt 400 za umeme jua zimefungwa duniani kote kwa ajili ya kuzalisha nishati ya umeme ambayo sote tunaifahamu kuwa ni nishati muhimu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. 

  Aidha amesema ongezeko la uzalishaji wa umeme duniani kote linatokana na  uzalishaji kwa kutumia umeme-jua lilifikia Gigawatt 380 katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2017. "Ongezeko hilo ni la kasi sana, jambo ambalo linaashiria kuwa kuna mwelekezo mkubwa duniani wa matumizi ya nishati ya umeme unaozalishwa kwa kutumia nishati ya jua. 

  "Kutokana na ukweli huu ni faraja kubwa kuona hata sisi Watanzania tuko pamoja na wenzetu wa nchi nyingine katika kukuza matumizi na teknolojia ya umeme-jua kupitia njia mbalimbali ikiwemo mafunzo kwa vijana wetu. "Uzinduzi wa kitabu hiki tunaoufanya hapa ni ushahidi tosha wa jitihada zetu kama nchi kuelekea matumizi makubwa ya umeme wa nishati ya jua,"amesema. 

  Mkapa amesema pamoja na ongezeko hilo nchi zote za Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara .Ukweli huo unakinzana na hali halisi ya eneo hilo kwa maana mbili;kwanza nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ndizo zenye maeneo mengi ambayo hayajafikiwa na umeme. 

  Pili nchi hizo zipo ukanda wa Tropiki ambao una jua jingi muda wote wa mwaka ambalo linaweza kutumika kuzalisha nishati hiyo ya jua. "Nichukue fursa hii kuwataka watalaam wote na taasisi husika zinazoshughulikia masuala ya nishati kuangalia jinsi ya kupanua wigo wa matumizi ya nishati hii ya jua ambayo tunayo kwa wingi katika eneo la Kusini mwa Jagwa la Sahara ikiwemo Tanzania ili kuzalisha umeme wa uhakika na gharama nafuu kwa wananchi wetu. 

  "Hii itasaidia kuharakisha upatikanaji wa umeme jambo ambalo litaharakisha ukuaji wa uchumi wa viwanda na kuongeza ajira kwa vijana.Wenzetu wa nchi za Ulaya,China ,Marekani ,Japan na India licha ya kuwa na vyanzo vingine na vikubwa vya uzalishaji umeme kama vinu makaa ya mawe na nyukilia bado wanaendeleza uzalishaji umeme kwa kutumia teknolojia ya umeme jua,"amesema. 

  Mkapa ametoa mfano nchi ya Ujeruman pekee tayari imefunga zaidi ya Gigawatt 400 za umeme-jua zilizounganishwa kwenye mtandao (grid) wao wa umeme , nchi ya China zaidi ya Gigawatt za umeme-jua.Hiyo inaonesha teknolojia ya umeme huo imekuwa , imekomaa na sasa inaweza kutumika bila mashaka yoyote katika kukidhi mahitaji. 

  Amefafanua kinachohitajika kwa sasa ni kuweka mipango madhubuti na kuitekeleza lakini ili kufanikisha hilo wanahitaji taasisi muhimu za Serikali kama COSTECH kusimamia mipango hiyo kwa kushirikisha wabia wa maendeleo na watalaam mbalimbali kutoka serikalini na sekta binafsi. 

  Amesema ushirikishwaji wa tasnia za mafunzo na uandishi wa vitabu kama alivyofanya mtunzi wa kitabu hicho Godwin Msigwa ni muhimu maana mafunzo na vitabu vya teknolojia hiyo vitasaidia kwa kiwango kikubwa katika kufikia malengo ya nchi. 

  Ameongeza maendeleo endelevu yanategemea mazingira endelevu;mazingira endelevu yanategemea jinsi wanadamu wanavyotumia mazingira hayo katika shughuli za kawaida na uzalishaji mali ikiwa pamoja na rasilimali za uzalishaji umeme.  
  Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akizungumza katika uzinduzi wa Kitabu cha Mafunzo ya Umeme Jua Kilichoandikwa na Godwin Msigwa katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Costech jijini Dar es Salaam.
  .Mwenyekiti wa Bodi ya Costech, Profesa Makenya Maboko akitoa shukrani kwa Mgeni Rasmi Benjamin Mkapa.
  Rais wa Awamu ya Tatu akitoa kitabu baada ya kukata utepe.
  Rais wa Awamu ya Tatu akitoa kitabu baada ya kukata utepe.
  Baadhi ya Wadau waliohudhuria hafla hiyo
  Mtunzi wa Kitabu cha Mafunzo ya Umeme Jua, Godwin Msigwa akieleza malengo ya kitabu hicho na hatua alizozipitia, hafla ilifanyika katika ukumbi wa Costech kijiji Dar es Salaam.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa yote nchini washirikiane na wadau wa mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI kuanzisha kampeni ya kuhamasisha wananchi hususani wanaume kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema.

  Kadhalika, amewaagiza Wakuu hao wa Mikoa na Wilaya kwa kusaidiana na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wasimamie kwa uzito unaostahili kampeni hiyo itakayoendeshwa kwa muda wa miezi sita mfululizo.

  Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumanne, Juni 19, 2018) wakati akizindua kampeni ya Kitaifa ya kuhamasisha wananchi hususani wanaume kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema, iliyofanyika katika Uwanja wa Jamuhuri, jijini Dodoma.

  ‚ÄúKwa vile tunazindua kampeni ya kupima na kuanza ARV mara moja (Test and Treat) natoa rai kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI, mhakikishe vitendanishi na dawa za ARV zipo za kutosheleza katika kila kituo kinachotoa huduma katika kila Mkoa na Wilaya,‚ÄĚ amesema.¬†

  Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwahamasisha watu wote watakaogundulika na maambukizo ya VVU waelewe kuwa utaratibu wa sasa ni kuanza dawa mara moja pasipo kujali kiwango cha kinga mwilini, yaani CD4.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizindua Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipokea tuzo ya kutambua kukubali kuwa Balozi wa kuhamasisha wanaume kupima VVU nchini, kwenye Uzinduzi wa Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018, kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia wakati alipozindua Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, kwenye uwanja vya Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018.

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Afisa Muuguzi Msaidizi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Flora Kamwela, wakati alipozindua Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU  na kuanza dawa mapema, kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihamasisha upimaji wa Virusi vya  Ukimwi hususani kwa wanaume, wakati alipozindua Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018, kulia ni Sajenti Deogratius Peter. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa maelezo na kapteni Geofrey Mwajombe katika Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018, katikati ni Sajenti Deogratius Peter.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo, akihamasisha pimaji wa VVU hususan kwa wanaume, wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018, kulia ni Sajenti Deogratius Peter. 

  0 0
 • 06/20/18--04:33: DATA ANALYSIS TRAINING
 • Download Application form here https://goo.gl/forms/w1cS7MccCxg8o4Kq2

  0 0

  JIOGRAFIA/MAHALI LILIPO SOKO

  Soko la Katengele linapatikana katika vilele vya milima yenye msitu ujulikanao kama Iyondo - Mswima wenye miti ya asili na ile ya kupandwa ukizungukwa na Kata za Kalembo, Sange, Ibaba, Ngulugulu na Kufule.
  Pia soko hili hupitiwa na  Barabara ya Mkoa ya Ibungu - Ileje hadi  KKK Wilayani Rungwe ikiligawa katikati na kuacha upande mmoja kuwa  Kata ya Sange na upande mwingine Kata za Kafule na Sange.

  HISTORIA YA SOKO:

  Soko hili limekuwepo kwa muda mrefu likianzia kabla ya wakoloni, wakati wa ukoloni na baada ya Uhuru wa wetu mnamo 1961 hadi sasa.
  Katengele awali palijulikana kama Katengele Bhalindu (yaani mabinti) ikielezwa kuwa ndipo palikutanisha vijana waliotaka kuoa au kuolewa kwa kabila la Wandali ambalo ni kubwa kwa Wilaya hii na maarufu kwa Mkoa wa Songwe na Mbeya kutokana na uchapaji kazi hususani zile za kutumia nguvu.
  Kuhusu ‚ÄúKatengele Bhalindu‚ÄĚ (yaani mabinti) hapa ndipo palipokuwa soko la awali pakiwa na msitu mdogo ambapo inasemekana kuwa mabinti wawili walipotea bila kupatikana katika mazingira ya kutatanisha kwa muda mrefu na imebaki kuwa simulizi inayoendelea ¬†kila linapotajwa neno katengele.
  Awali lilikutanisha watu wa maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ileje na Wilaya za Mbozi, Rungwe na Kyela wakiuza bidhaa kwa fedha tasilimu pamoja na biashara ya kubadilishana bidhaa kwa bidhaa.  
  Kwa miaka ya hivi karibuni limekuwa maarufu sana kwa biashara ya ng’ombe, bidhaa za asili pamoja na zile za viwandani likiwavutia hata raia wa Nchi jirani ya Malawi.

  KUANZISHWA KWA MRADI WA SHAMBA LA MITI

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Misitu (TFS) imeamua kuanzisha Shamba la Miti la Iyondo - Mswima ukiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya 2015/2020 ibara ya 31 vifungu vya b,c,d,e na f kuhusiana sekta ya Maliasili.
  Kwa mujibu wa Meneja wa Mradi wa Iyondo ‚Äď Mswima Ndg. Deograsian Kavishe upandaji miti utaanza rasmi katika mwaka wa Fedha 2018/2019 ikiwa baadhi ya kazi zilianza kutekelezwa na Mradi katika mwaka wa fedha 2017/2018.
  Kuanzishwa kwa shamba hili la Katengele kunaifanya Tanzania kuwa na mashamba ya miti ya kupandwa 23 yakiwa yanapatikana katika Kanda mbalimbali kati ya hayo manne yapo katika hatua ya uanzishwaji likiwemo hilo la Iyondo ‚Äď Mswima (Ileje).

  KUHAMISHWA KWA MNADA WA SOKO LA KATENGELE

  Kutokana na soko hili kuwa ndani ya msitu wa hifadhi na kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa kufuata Kanuni, Sheria na taratibu za uanzishwaji na uendeshaji wa miradi ya upandaji miti hapa Nchini, soko hilo halistahili  kuendelea kuwepo mahali lilipo, hivyo linatakiwa kuhamishiwa sehemu nyingine nje ya hifadhi zikiwemo kaya 13 zinazoishi ndani ya eneo hilo.
  Ujenzi wa miundombinu katika eneo lililochaguliwa utafanywa na serikali kupitia wakala wa Misitu (TFS).

  MICHAKATO YA KUHAMISHA SOKO

  Ili kuendeleza mahusiano mazuri na wadau mbalimbali wa maendeleo TFS imeshirikisha Baraza la Madiwani, wataalam wa Halmashauri pamoja na Serikali Kuu.
  Michakato hiyo ilianzia kwenye vikao vya CMT, Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira, Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango pamoja na Baraza la Madiwani ambalo liliridhia kuhama kwa Mnada wa Soko hilo kutoka mahali lilipo na kwenda sehemu nyingine.
  KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI
  Baraza la Madiwani baada ya kujadili na kupitia mapendekezo ya vikao vilivyotangulia kisheria liliridhia juu ya kuhama kwa soko la Katengele kutoka mahali lilipo na kwenda Njiapanda ya Shule ya Msingi Mbangala katika barabara ya Ibaba - Katengele ili kupisha uanzishwaji wa Mradi wa Shamba la Miti la Iyondo - Mswima.

  Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya upigaji kura kufanyika ambapo Wah. Madiwani wane waliliridhia mnada wa Katengele uhamishiwe eneo la Ghala - Sange huku Madiwani 18 wakiridhia Mnada wa Katengele uhamishiwe Njiapanda ya Shule ya Msingi Mbangala.

  MAONI YA BARAZA LA MADIWANI

  Baraza lilishauri kuwa wakati wa kuhamisha Mnada wa Katengele ufanyike utaratibu wa kukutanisha wananchi waliokuwa katika eneo la mnada pamoja na wadau wa mnada huo wakiwemo viongozi wa maeneo yanayozunguka mnada, machifu na Wah. Madiwani ili kuwajengea uelewa na kuwajulisha mchakato wa kuhamisha mnada.
  Aidha ilishauriwa kutoa mwaliko kwa wadau kutoka maeneo mbalimbali ili kuwajulisha juu ya mabadiliko ya eneo jipya la mnada

  GHARAMA ZA UJENZI WA MIUNDO MBINU KWENYE ENEO JIPYA LA MNADA

  Serikali kupitia Wakala wa Misitu (TFS) inatarajia kujenga miundombinu katika eneo jipya la mnada ili kutoathiri bajeti ya Halmashauri ambayo tayari ilishatekelezwa kwenye soko la awali ukiwemo ujenzi wa machinjio.

  MANUFAA YA MRADI WA UPANDAJI MITI WA IYONDO MSWIMA-ILEJE

  Meneja wa Mradi huu Ndg. Deograsian Kavishe alibainisha faida kadha zitakazotokana na kuwepo kwa Mradi huu kiwilaya, kitaifa na kimataifa ambazo ni pamoja na:
  Ajira kwa jamii ambapo mpaka sasa wananchi wa maeneo hayo wameshaanza kufanya kazi za awali katika Mradi huo, ongezeko la viwanda ndani na nje ya Wilaya vinavyochakata mazao ya magogo, kukabiliana na ongezeko la uvunaji miti michanga (pre mature) na  jamii kupata elimu ya upandaji miti.
  Faida zingine ni uanzishwaji na uboreshaji wa huduma za jamii, kuwezesha Mashamba Darasa ya miti kwa Taasisi za Serikali kama vile shule na magereza pamoja na kugawa miche ya miti kwa jamii ikiwa ni njia mojawapo ya uhamasishaji wa upandaji miti.
  Kuanzishwa kwa Mradi huu kutaitangaza Ileje kitaifa na kimataifa kutokana na shughuli za kitalii zinazoweza kufanywa katika eneo hilo lenye jiografia ya kipekee katika Mkoa wa Songwe pamoja na uwepo wa nyani aina ya mbega ambao hupatikana sehemu zenye baridi kali.

  CHANGAMOTO ZA UANZISHWAJI WA SHAMBA LA IYONDO MSWIMA NA UHAMISHAJI WA MNADA WA KATENGELE

  Zipo chanagamoto kadha zinazokabili juu ya kuanzishwa kwa Mradi huu, moja ni mshituko na hofu kwa watumiaji wa soko hilo ambao wanaona giza mbele yao hili linatokana na mazoea ya uendeshaji wa mambo.
  Pia hofu nyingine ni juu ya hatima ya miti ya watu binafsi ambayo imebainika kuwa ipo ndani ya hifadhi ya Msitu wa Iyondo ‚Äď Mswima ambao walitumia gharama kubwa katka kuipanda ikiwa ni sehemu ya uwekezaji.

  MAONI YA MWANDISHI WA TAARIFA HII

  Kila jambo linapoanzishwa huwa na changomoto zake, hata ujenzi wa barabara ya Mpembe - Isongole ambayo kwa muda mrefu tumekuwa tukiihitaji imeshawathiri baadhi ya watu hata kuhamia kwa Serikali yetu huko Dodoma kumewaathiri baadhi ya watu.
  Kinachotakiwa ni kutathmini faida na hasara juu ya jambo tunalolihitaji si lazima tulio hai sasa tukanufaika bali twaweza kuwa washiriki wa ujenzi wa misingi imara kwa vizazi vijavyo kama walivyofanya babu zetu ambao licha ya kutokuwa na ‚ÄúElimu ya Kimagharibi‚ÄĚ kuna mambo walifanya ambayo mpaka leo tunayafaidi ukiwemo ulinzi wa mazingira.
  Kamwe tusikubali ujio wa miradi kama hii kutugawa  bali tukae pamoja kwa kujadiliana ili tuweze kuimba wimbo mmoja kwa kufuata midundo ya ngoma inayopigwa.
  Imeandaliwa na:
  Daniel J. Mwambene
  KITENGO CHA HABARI
  ILEJE
  Eneo la Mnada wa Katengele Wilayani Ileje mkoani Songwe unaotakiwa kuhamishwa ili kupisha Mradi wa Upandaji Miti.
  Askari Jeshi USU (ambalo ni jina geni kwa wengi ) Deograsian Kavishe Meneja Mradiwa Upandaji Miti wa Iyondo-Mswima akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ileje.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mhe.Ubatizo Songa akiongoza Wahe. Madiwani na Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje walipotembelea eneo la Mradiwa Upandaji Miti la Iyondo-Mswima  Sehemu ya Msitu wa Iyondo-Mswima ikionesha msitu wa asili na kupandwa.
  Kitalu cha miti kilichopo Katengele-Ileje kikitarajiwa kubadilisha sura ya msitu wa Iyondo-Mswima wiyani Ileje
  Eneo la Njiapanda ya Shule ya Msingi Mbangala panapotarajiwa kuhamishiwa Mnada wa Katengele.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Ndugu Haji Mnasi (aliyesimama) akizungumza kwenye Baraza Maalum kuhusu Mnada wa Katengele
  0 0


  Na Mwashungi Tahir - Maelezo Zanzibar 

  Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Kimataifa linaloshuhulikia Idadi ya watu Duniani UNFPA Jaqline Mohan amesema Shirika lake litaendelea kutoa mashirikiano katika sekta ya afya hasa katika uzazi salama ili kuweza kuyanusuru maisha ya mama na mtoto.

  Hayo ameyasema huko katika ofisi ya Wizara ya Afya Mnazi Mmoja wakati alipokuwa akielezea lengo la matarajio yao katika kusaidia mpango wa uzazi salama wa mama na mtoto.

  Alisema afya na mama na mtoto ni muhimu katika jamii hivyo wataendelea kusaidia sekta hiyo ya afya ili kuhakikisha kuwa kinamama wanapata huduma bora wakati wa kujifungua pamoja na watoto kupata makuzi yaliyo salama ili kupunguza vifo wakati wa uzazi.

  Alisema vifo vingi vya akinamama na watoto hutokea wakati wa kujifungua hivyo huduma hiyo itaweza kupunguza vifo na kusaidia kuwapa uzazi salama kwa kujenga afya bora na makuzi mazuri wa watoto.

  ‚ÄúTuna mpango wa kusaidia Wizara ya Afya katika mambo ya kijamii , uzazi salama kwa mama na mtoto na kushuhulikia vijana katika kujua afya zao‚ÄĚ alisema mwakilishi huyo.

  Alieleza kuwa Shirika lake pia lina lengo la kuwasaidia vijana kwa kuhakikisha kuwa wanaishi na afya bora , kuwapa uhuru wa kujipanga katika kujiletea maendeleo yao pamoja na kuwasaidia kwenye mambo ya kiuchumi. kwani ndio nguvu kazi ya Taifa

  Nae Waziri wa Afya Hamadi Rashid Mohammed amelishukuru shirika hilo kwa kutoa mashirikiano katika kuboresha afya za mama na watoto katika uzazi ulio salama.

  Alisema watazidi kushirikiana kwenye kutoa elimu zaidi ya uzazi wa mpango ulio salama ili kupunguza vifo vya mama na mtoto, kwani elimu ya uzazi bado uzazi wa mpango iko chini na kuwataka akinamama kuwa na muamko wa kupanga uzazi ilikunusuru maisha yao pamoja na kuwa na afya bora

  ‚ÄúElimu inahitajika zaidi kwa jamii na iendelee kutolewa katika suala zima la uzazi wa mpango salama kwa mama na mtoto na pia kuwashauri akina baba kuwapa fursa akina mama kujiunga na uzazi salama‚ÄĚ, alieleza Waziri Hamad .

  Waziri Hamad alisema shirika hilo limesaidia kutoa dawa kwa ajili ya jamii ikiwemo vifaa vya uzazi kwenye wodi ya uzazi katika Hospitali ya Mnazo Mmoja na mwembeladu pamoja na kutoa mafunzo wafanyakazi ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

  ‚Äú Uzazi wa mpango ulio salama umo mpaka katika vitabu vya dini yetu ya kiislamu hivyo tujitahidini ili kuweza kuleta afya iliyo bora kwa mama na mtoto na kupata nguvu ya kulea mtoto miaka miwili na kupumzika angalau mwaka mmoja‚ÄĚ, alisema Waziri huyo.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Ali Salim alisifu jitihada wanazozitoa shirika hilo katika kuboresha sekta ya afya ya mama na mtoto jinsi wanavyoweza kutoa juhudi za Afya za mama na mtoto katika kuweka uzazi ulio salama.
     MWAKILISHI wa UNFPA Tanzania Jacguline Mahon akizungumza na Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed kuhusu kuongeza ushirikiano juu ya uzazi salama na kuimarisha afya ya Mama na Mtoto, (kulia kwake)  ni Mwakilishi wa (UNICEF) Maniza Zaman 
  WAZIRI wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
  WAZIRI wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed katika akipiga picha ya pamoja na Wawakilisi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania, (kushoto) Mania Zaman wa UNICEF na  Jacguline Mahon wa UNFPA (Picha na Abdalla Omar  Maelezo - Zanzibar).

  0 0

  Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akisalimiana na Makamu wa Rais wa Abbott Fund kutoka Marekani Bw. Andy Wilson wakati Makamu wa Rais wa Mfuko huo alipomtembelea leo Ofisi kwake Jijini Dodoma ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali yahusuyo utoaji wa huduma kwa watoto waishio katika mazingira magumu nchini.
  Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akifurahia jambo na Makamu wa Rais wa Abbott Fund kutoka Marekani Bw. Andy Wilson wakati Makamu wa Rais wa Mfuko huo alipomtembelea leo Ofisi kwake Jijini Dodoma ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali yahusuyo utoaji wa huduma kwa watoto waishio katika mazingira magumu nchini.
  Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Abbott Fund kutoka Marekani Bw. Andy Wilson (wa pili kushoto) mara baada ya mazungumzo wakati Makamu wa Rais wa Mfuko huo alipomtembelea leo Ofisi kwake Jijini Dodoma ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali yahusuyo utoaji wa huduma kwa watoto waishio katika mazingira magumu nchini kushoto ni Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt Naftali Ng’ondi na kulia ni Meneja Programu wa Abbott Fund Bw. Alfred Magalla.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

  0 0

   Meza kuu
  Wajumbe wa Sekretariet ya CCM wakiimba wimbo alipowasili Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu Ndg Abdulrahman Kinana katika hafla iliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga  na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma leo.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipeana Mkono na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana mara baada ya kumkabidhi zawadi mbalimbali alizotoa kwa niaba ya Kamati ya Wabunge wa CCM katika hafla iliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga  na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma leo.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Kmati ya Wabunge wa CCM Mhe Majaliwa Kassim akimkabidhi zawadi mbalimbali Katibu Mkuu wa CCM  kwa niaba ya Kamati ya Wabunge wa CCM katika hafla iliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga Ndg Abdulrahman Kinana   na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma leo.
   Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wabunge katika hafla aliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga  na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma leo.
   Katibu Mkuu Dkt. Bashiru Ally akizungumza na wabunge katika hafla ya kumuaga Katibu Mkuu Mstafu Abdulrahman Kinana iliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga  na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma leo.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya wabungea wa CCM akizungumza  katika hafla ya kumuaga Katibu Mkuu Mstafu Abdulrahman Kinana   na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma leo.
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na wabunge katika hafla aliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga  na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma leo.
   Sehemu ya wabunge wakifuatilia Hafla hiyo
   Wajumbe wa Sekretariet ya CCM wakifuatilia Hafla hiyo
  Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu Abdurahmani Kinana akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mwenyekiti wa Kamati Mhe Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya kitenge aina ya Wax Mke wa Katibu mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally katika hafla iliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga Ktibu mkuu Mstaafu Ndg Abdulrahman Kinana na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma leo.
  Katibu Mkuu Mstaafu Ndg. Abdulrahman Kinana akifurahi jambo na Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Ndg Hamphley Polepole katika hafla iliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga  na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma leo.
   Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula akimuaga Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana katika hafla iliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga  na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma leo.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM akizungumza na Mbunge wa CCM anaewakilisha Vijana Mhe Khadija ALLY wakati wa hafla iliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga  na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma leo.(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI CCM)

older | 1 | .... | 1602 | 1603 | (Page 1604) | 1605 | 1606 | .... | 1897 | newer