Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1601 | 1602 | (Page 1603) | 1604 | 1605 | .... | 1896 | newer

  0 0


  0 0

  NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

  BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limesema halitakubali kuonewa na watu wachache na limedhamiria kurejesha mali za Waislamu zilizohodhiwa kwa maslahi ya wachache.

  Pia limesema waumini wa dini Kiislamu wameridhia kuwa chini ya kiongozi mmoja Sheikh Mkuu wa Tanzania na kuwataka wengine wote kufuata Katiba ya BAKWATA ili kuepusha vurugu.

  Kauli hiyo ilitolewa ja juzi jijini Mwanza kwenye Baraza la Idd El Fitri na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA Taifa Sheikh Hassan Kabeke ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuendeleza Quraan na Suna Tanzania (JUQUSUTA).

  Alisema BAKWATA hitakubali kuporwa mali za Waislamu na kuwanufaisha wachache ambao wamelifanya baraza hilo kuwa ombaomba wakati lina mtandao mkubwa kuliko taasisi nyingi za dini nchini kwa kuwa lina mtandao wa uongozi hadi vijijini.

  Sheikh Kabeke alisema kuwa wamejipanga kurejesha mali za waislamu na kuwataka waumini na viongozi wa dini hiyo kuwa imara na wahakikishe mali zote za Waislamu zinarudishwa lakini wakilegea zote zitakwisha.“Tunataka BAKWATA yenye nguvu itakayopambana na watu wanaopuuza maelekezo ya baraza hilo na hatuna sababu ya kuwa ombaomba wakati tumeweka mizizi hadi vijijini, isipokuwa tunazidiwa na CCM tu.

  "Lakini pia tumsaidie Mufti wa Tanzania pamoja na kudumisha amani na utulivu nchini,” alisema Sheikh Kabeke ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Mwanza.Awali katika risala yake kwa mgeni rasmi John Mongela, Kaimu Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza Sina Mwagalazi alisema kutokana na uhusiano uliopo baina ya baraza hilo na serikali aliiomba iwape ushirikiano waweze kurejesha mali za Waislamu kwa sababu orodha ya mali hizo zilizohodhiwa na kuwanufaifa watu wachache badala ya Waislamu ipo.

  “BAKWATA ndiyo msimamizi wa mali za Waislamu kwa mujibu wa katiba ya baraza hilo.Tunawaomba watu waliojimilikisha mali hizo wajitokeze kwa mazungumzo ili kuwwka mambo sawa,”alisema Mwagalazi.Wakati huohuo Kaimu Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Sheikh Hassan bin Almasi aliwataka waumini wa dini ya Kiislamu kuwa siku 30 za mfungo wa mwezi wa Ramadhani liwe darasa la kujitathmini kutokana na semina aliyowapa Mwenyezi Mungu.

  Alisema Waislamu waliokuwa kwenye semina (wamefunga) wafanye tathmini je, wataendelea kufanya kama walivyofanya wakati wa mwezi wa Ramadhani, wafikiri vizuri safari yao ya kuondoka duniani je, wataimaliza salama na watakwenda kama ilivyokuwa mwezi Mtukufu?

  “Kukutana kwenye baraza la Idd tafsiri yake ni kupata heri ya Ramadhani na tunakusanyika kukumbushana semina aliyotuletea Mwenyezi Mungu na kwamba ameingia kwenye vifua vyetu.Hebu tujiulize semina hiyo itaendelea ama imefika mwisho? ”alisema Sheikh Almasi.

  Alisisitiza semina hiyo waliyopewa iwe endelevu kwa kuwa na madarasa ya dini badala ya kuishia kwenye siku ya Idd el Fitri na kuonya misikiti kukosa madarasa kunaifanya safari yao ya kwenda peponi isiwe nzuri sababu watu hawasomi aya za quraan na kusababisha wawatete wengine bila sababu.

  “ Mambo hayo ndiyo balaa ya kuigia kaburini na huwezi kufunga wakati unamsengenya mtu ndiyo maana tunataka Waislamu waliokuwa wamefunga kufanya tathmini.Je, wataendelea kuwa kama walivyokuwa kwenye mwezi wa Ramadhani? Alieleza kaimu Sheikh huyo wa Mkoa wa Mwanza.

  Aidha alidai zipo changamoto za kufarakana kwa waumini wa dini hiyo wanaume na wanawake na kuonya kila mmoja abebe mzigo wake mwenyewe badala ya kuwabebesha wengine.
  Sheikh Hassan Kabeke akizungumza kwenye Baraza la Idd jijini Mwanza ambalo lilifanyika katika ukumbi wa Makutano wa New Mwanza Hotel juzi.Picha na Baltazar Mashaka

  0 0

  Na Jumia Food Tanzania

  Kikiwa kimeanzishwa takribani miaka 10 iliyopita, kituo cha kulea watoto yatima cha Maunga kilichopo Kinondoni jijini Dar es Salaam kinakumbwa na changamoto kadhaa zikiwemo eneo la kutosha kuwalea na kuwahifadhi watoto pamoja na bima ya afya.
  Kituo hiki ambacho mpaka hivi sasa kina jumla ya watoto 48 wakiwemo wavulana 26 huku 22 ni wasichana. Watoto hao wanaolelewa na Bi. Zainab Bakari ambaye ndiye mwanzilishi na mlezi wa watoto hao, anawahudumia kwa mahitaji yao yote muhimu yakiwemo malazi, chakula, mavazi, shule, afya na mengineyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile serikali, sekta na watu binafsi kupitia misaada inayopelekwa kituoni hapo.

  Akizungumza wakati akipokea msaada wa chakula na mahitaji ya shule kutoka kampuni ya Jumia Food, Bi. Bakari ameelezea kuwa watoto wanazidi kuongezeka kituoni kwake hali inayopelekea kuwa ni changamoto kuwahifadhi na kuwalea katika eneo moja kama inavyotakiwa.
  “Kituo hiki nilikianzisha takribani miaka 10 iliyopita nikiwa na watoto wachache hapa kwenye hii nyumba yetu. Na kwa kipindi chote hiko nimekuwa nikipokea watoto na kuwalea hapahapa. Hivyo, kadri miaka inavyozidi kwenda ndivyo ninavyozidi kupokea watoto, wakizidi kukua na mahitaji kuongezeka. Hali hiyo imepelekea suala la kuwalea wote kwa pamoja kuwa ni changamoto kwasababu kituo hiki hakina uzio na kimezungukwa na nyumba za watu wengine,” alielezea Mwanzilishi na Mlezi wa Kituo cha Maunga.

  Jumia Food, kampuni inayojihusisha na huduma ya chakula kwa njia ya mtandao ilikuwa ikiendesha kampeni iliyokwenda kwa jina la “STAND BY ME” katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kampeni hii iliwashirikisha wateja wake kwa kuwataka kuagiza chakula kwa kutumia nenosiri ‘ASANTE’ ili kuchangia mahitaji ya chakula kituoni hapo.
  Mpaka kampeni inamalizika jumla ya huduma za chakula zilizofanyika kwa kutumia nenosiri ‘ASANTE’ zilikuwa zaidi ya 200. Hii inamaanisha kwamba idadi hiyo ya wateja wa Jumia Food ndiyo waliounga mkono kampeni hiyo ili kufanikisha watoto wa kituoni hapo kuwa na tabasamu katika msimu huu wa sikukuu za Eid al-Fitr kama watoto wengine.

  “Kwa sasa changamoto kubwa ninayokumbana nayo kituoni hapa ni ufinyu wa eneo ambalo nawalea watoto hawa. Eneo ni lilelile tangu nilipofanya uamuzi nyumba hii kuwa kituo cha kulea watoto yatima. Idadi ya watoto inazidi kuongezeka kadri siku zinavyokwenda, kwasababu siwezi kukataa mtoto anayehitaji msaada.
   
   Ningependa kutumia fursa hii kuwaomba wadau na serikali kwa ujumla kunisaidia eneo ambalo litajengwa kituo kikubwa cha kutosha tofauti na hapa ili kuwatosheleza hawa nilionao na wengine watakaokuja,” alisema na kuhitimisha Bi. Bakari, “Kwa kuongezea, ningependa kutoa wito kwa wafadhili wajitokeze kunisaidia bima ya afya ili kusaidia pindi pale matibabu yanapohitajika. Matibabu ni gharama, huwa natumia gharama kubwa ili watoto waweze kupatiwa tiba.”
  Naye kwa upande wake Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Jumia Food Tanzania, Bi. Sayi Makwaia amesema kuwa, “tumeona ni vema kuleta msaada huu wa mahitaji machache ya chakula na vifaa vya shule kituoni hapa. Waswahili husema, ‘Wema huanzia nyumbani.’ Kampuni yetu ipo jirani na kituo hiki, hivyo ni busara kuwathamini.”

  “Maunga inakabiliana na changamoto kadhaa lakini kwa msaada huu wetu mdogo tunaamini utawasaidia kwa kiasi fulani na tunaahidi kuwakumbuka zaidi pale tutakapopata fursa. Ningeziomba pia taasisi na kampuni zingine ambazo zinafanya shughuli zao jirani na kituo kuweza kuwasaidia watoto hawa ili nao waweze kuishi maisha sawa na watoto wengine wenye wazazi na kuwalea,” alimalizia Bi. Makwaia.

  Msaada wa mahitaji ya chakula na vifaa vya shule uliotolewa katika kituo cha kulea watoto yatima cha Maunga kutoka Jumia Food kwa niaba ya wateja wake ni pamoja na mchele, unga wa mahindi, maharage, sukari, mafuta ya kupikia, sabuni za kufulia, madaftari, penseli nakadhalika.

  0 0

  Na Frankius Cleophace Tarime.

  Wasichana 40 kutoka katika kata tofauti Wilayani Tarime Mkoani Mara wamepatiwa mafunzo ya uelimishaji rika katika Maeneo wanayotoka kwa lengo la kupinga Ukeketaji kwa Mtoto wa kike ili aweze kutimiza ndoto zake ikiwemo kupata Elimu.

  Sarah Bedah ni Afisa Mawasiliano kutoka Shirika la Msihana Initiative lililopo Jijini Dar Es Salaam amesema kuwa wao kama Shirika kwa kushirikiana na Shirila la ATFGM Masanga lililopo Tarime wameamua kutoa Elimu hiyo kwa lengo la kuwajengea Uwezo wasichana hao ili kuwa mabalozi wazuri katika kufikisha Elimu ya kupinga Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la ATFGM Masanga Sister Stella Mgaya amesema kuwa wao kama shirika wameamua kutoa Pia Mafunzo hayo kwa wasichana ambao wamekeketwa tayari na ambao hawajakeketwa ili kuzidi kuwaelimisha Wasicha ambao hawajakeketwa ili wasikeketwe.

  Pia Mgaya ameongeza kuwa licha ya kutoa Elimukwa Wasichana hao bado wanazunguka na wazee wa Mila Muungano wa Koo12 kwa lengo la kutoa Elimu kwa jamii ili kuondoa Ukeketaji ikiwa ni pamoja na Kupiga Vita Miiko ambayo inakandamiza Mtoto wa kike ambaye hajakeketwa ili asitengwe Kwenye Jamii.

  Aidha Washiriki wa Semina hiyo ya Siku mbili wamesema kuwa Elimu watakayopewa itakuwa chachu kwao na kuitumia Vyema kwa lengo la kukomboa Mtoto wa Kike Wilayani Tarime Mkoani Mara.

  Naye Mratibu wa Huduma ya Afya ambaye pia ni Mwezeshaji katika Mafunzo hayo Abel Gichaine amesema kuwa baada ya kutoa Elimu kwa jamii endepo itakiuka lazima Sheria itumike ili kuwatia hatiani wale ambao watakao keketa Msichana kwani Mwaka huu unaogawanyika Kwa Mbili wenda koo Nyingi za kabila la Wakurya Wilayani Tarime zikakeketa ili kutimiza Mila zao.
  Meneja Miradi Shirika la ATFGM Masanga Tarime ambao wanapiga Vita Ukatili wa kijinsia akitoa Somo kwa Mabinti hao ambao baadhi yao wamekeketwa na kuolewa katika Umri Mdogo wakipewa Elimu ili waweze kuwa mabalozi wazuri wa kuopiga Vita Ukaili Maeneoo wanayotoka.

  0 0
  Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko akiongea na wananchi wa kijiji cha Ipanko juu ya changamoto ambazo wanakabiliwa nazo na kuunda timu maalum ya wataalam kwa ajili ya kuchunguza migodi yote na aina ya madini yanayopatika katika migodi iliyopo halmashauri ya wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro kwa lengo la kuhakikisha kuwa Tanzania haiendelei kuibiwa na wawekezaji katika seckta ya madini.

  Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa umakini Naibu waziri wa madini mheshimiwa Doto Bitoke alifanya ziara ya kutatua mgogoro baina ya wawekezaji na wananchi kwenye sekta ya madini
  NA FREDY MGUNDA,MOROGORO.

  Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amesema kuwa ataunda timu maalum ya wataalam kwa ajili ya kuchunguza migodi yote nchini ikiwa ni pamoja na utambuzi wa aina ya madini yanayopatika katika migodi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro kwa lengo la kuhakikisha kuwa Tanzania haiendelei kuibiwa na wawekezaji katika sekta ya madini.

  Akizungumza wakati wa ziara ya siku mbili Mkoani Morogoro Mh Biteko alisema kuwa madini yote yaliyopo katika ardhi ya Tanzania ni mali ya watanzania hivyo yanapaswa kuwanufaisha watanzania kwanza ndipo watu wengine wafuate.

  “Naombeni watanzania wote mjue kuwa madini haya ni mali ya watanzania wote hivyo tunapaswa kuyalinda na kutoa taarifa sahihi kwa serikali kama kuna mtu anaiibia serikali kwa namna moja au nyingine ili serikali iweze kuchukua hatua za kisheria dhidi yake, Na mimi nawaambieni watanzania tuache uoga tuseme ukweli kama Rais wetu Mhe Dkt John Pombe Magufuli anavyosisitiza utendaji wa uwazi na uwajibikaji katika serikali” Alikaririwa Mhe Biteko

  Biteko amepiga marufuku wawekezaji kutumia fedha zao kuwanyanyasa wananchi waliopo kwenye maeneo ambayo kuna migodi kwa ajili ya kuwaibia watanzania ambao bado wana kipato cha chini katika maeneo yanapopatikana madini.
  “Najua hawa wawekezaji wanapesa nyingi sana hivyo isiwe sababu ya kuwarubuni baadhi ya wananchi na kuwatesa wananchi wengi hususani waliopo kwenye maeneo ya madini na leo nataka niwaambie ukweli wawekezaji wote nchini najua ambavyo mnatumia pesa zenu kuwanyanyasa wananchi, sasa ndio mwisho wenu maana serikali ya awamu ya tano inataka haki kwa kila mwananchi” Alisisitiza Biteko

  Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Bitoke alifanya ziara ya kikazi katika kijiji cha Ipanko kilichopo katika wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro na kugundua kuwa kuna wawekezaji wanaidanganya serikali na wananchi kwa kutoweka wazi kiasi gani ambacho wanakipata kwenye migodi iliyopo katika kijiji hicho.

  “Jamani wana Ipanko nchi hii tumeibiwa sana sasa ifike mwisho tusema hapana haiwezekani tena kwenye serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli tuendelee kuibiwa madini yetu na kuwanufaisha watanzania ambao wapo nje ya nchi yetu, Rais kashasema na sisi wasaidizi wake tunaungana naye kwamba iwe mwisho kuchezewa kwa rasilimali zetu”

  “Chonde chonde nyie viongozi wetu wa ngazi za vijiji, kata, tarafa, wilaya na mkoa tunaomba msituangushe kwa kupokea rushwa kutoka kwa wawekezaji na kuisaliti nchi yako kuendelea kuibia kirahisi namna hii” alisema Biteko

  Biteko alieleza kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli inawapenda sana kuwa na wawekezaji wengi wenye tija ambao sio wababaisha na ambao wamekuja nchi kuiba rasilimali za watanzania.

  Aidha, Biteko alisema kuwa haiwekani muwekezaji akawekeza Bilioni 42 halafu akachangia madawati na mifuko ya saruji katika jamii kama ndio mchango wake, haiwezekani wanapaswa kuchangia kulingana na kiasi ambacho wamewekaza kwa faida na manufaa ya wananchi.

  “Mimi binafsi hainiingi akilini kuona muwekezaji amewekeza pesa nyingi kama hizo halafu kwenye shughuli za kimendeleo amechangia kiasi kidogo namna hiyo kwangu nasema haiwezekani na nchi hii kwa sasa sio yakuchezewa tena” alisema Biteko

  Lakini pia Naibu waziri huyo alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mhe Goodluck Mlinga kwa kuwapigania wananchi wake kwa kuzifikisha kero mahali husika na kutafutiwa ufumbuzi.

  Nao baadhi ya wananchi akiwemo Pangarasi Kanyali, Cyprian Kanyali, Micky Sengo, Doedatus Moholeli, Hilda Linoma na Fredrick Kazimoto walimpongeza Naibu Waziri wa Madini Mhe Biteko kwa kufika kijiji hapo na kusiliza kero zao kwani wana amini zitatafutiwa ufumbuzi kwa kufuata sheria na katiba ya nchi.

  “Toka sisi tuzaliwe hatujawahi kutembelewa na waziri na kusikiliza kero zetu kama ambavyo wewe umefika kijijini kwetu leo hii tunajisikia wenye amani na furaha kwa kuwa tunajua kero zetu tunazifikisha moja kwa moja kwa kwa Rais wetu kupitia wewe waziri” Walisema wananchi hao

  Awali Mbunge wa Jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga alisema kuwa lengo la waziri kufika katika kijiji hapo ni kujionea kero wanazokumbana nazo wananchi kupitia wawekezaji wa sekta ya madini na kuzitafutia ufumbuzi.

  “Huku ni mbali sana Mheshimiwa Naibu Waziri lakini kuna madini mengi ambayo ndio utajiri wa nchi hii hivyo tunapaswa kuwa makini na hawa wawekezaji maana wamekuwa wakiibia sana serikali yetu” Alisema Mlinga

  0 0

  Na Woinde Shizza,Arusha

   WADAU mbalimbali wa zao la alizeti wameanza jitihada za  kujadili mikakati ya kuhakikisha wanainua zao hilo hasa kwa kuzingatia mafuta ya alizeti ni bora kwa afya ya binadamu. 

  Wanasema kuwa alizeti ni moja kati ya mazao yanayostahimili ukame na kumpa mkulima faida kubwa kutokana na ukwel kwamba mbali ya alizeti kutoa mafuta pia hitoa malighafi nyingine ka
  dhaa. 

  Wakizungunza leo wadau hao wanasema zao hilo pia hutumika katika kukamua mafuta ya kula pamoja na kutengeneza chakula cha mifugo ikiwemo mashudu yanayotumiwa na ng`ombe na kuku ili kunenepesha mifugo pamoja na sabuni.

  Hivyo kutokana na umuhimu wa zao hilo pamoja na kuwa na faida nyingi bado jalijapewa kipaumbele  stahiki ili Taifa lipate mafuta ya kutosha na kupunguza uingizwaji wa mafuta kutoka nje ya nchi.Wamesema wameanza juhudi za kuhamasisha kilimo cha zao hilo ambalo ni muhimu katika kuchochea uchumi wa viwanda kwani wako wasindikaji  wadogo na wakubwa wa mafuta ya alizeti ambao wananunua alizeti kutoka kwa wakulima.

  Mkurugenzi wa Taasisi hiyo isiyokua ya kiserikali ya Gola Foundation Salaiwe Elisha Maghembe amesema ili kuhasisha kilimo cha zao hilo wameanzisha shamba la mfano  la ekari 30.Ambapo wanalima alizeti kama njia mojawapo ya kuwafundisha wakulima na kukuza uchumi wa taasisi hiyo.

  Maghembe amesema tayari wametenga kiasi She. milioni 60 kwa ajili ya kutoa mashine za kusindika mafuta ya alizeti kwa vikundi vya wakulima walioko katika Mikoa ya Mwanza na Kagera .Elisha anasema zao la alizeti linaweza kutumika kuchochea uchumi wa viwanda kwa kuwa na vikundi vya wakulima wanaolima na kusindika zao hilo kwa maana ya kuongeza thamani na kuuza mafuta pamoja na chakula cha mifugo.

  Pia licha ya kuhamasisha kilimo cha alizeti  wanahasisha ufugaji kuku kwani mabaki ya alizeti baada ya kukamuliwa mafuta hutumika kama chakula bora cha kuku hivyo wakulima hao wakifuga kuku wanaweza kupata kipato cha ziada na kuondokana na umasikini.“Pia tumejikita katika kutoa mafunzo ya kilimo bora cha alizeti kinachofanywa kwa kanuni na taratibu pamoja na utengenezwaji wa kalenda ya zao hilo muhimu,”amesema Elisha

  Anaeleza kuwa taasisi hiyo ina mpango wa miaka 10 wa kuwekeza kwenye kilimo cha alizeti pamoja na kutoa mashine rahisi za kukamua alizeti kuwawezesha wakulima kuongeza thamani zao hilo.Amefafanua kwa sasa Gola inashirikiana na Shirika la Kagera Edible Oil katika kuwafikia wakulima wa alizeti mkoani Kagera ambapo wameanzisha Ofisi ya pamoja ili kuwahudumia wakulima kwa karibu ikiwemo mafunzo na vitendea kazi.

  Kwa upande wake Mkurugenzi  Mtendaji wa Kagera Edible Oil  Kibambi Ibrahim anasema zao la alizeti linastawi katika maeoneo yote na linastahimili ukame.Pia halitumii viuatilifu vyenye sumu kali ambavyo ni hatari kwa afya ya mlaji pia kumgharimu mkulima fedha nyingi.Anaeleza kwa Mkoa wa Kagera wamejipanga kuhamasisha wadau kujenga kiwanda cha sabuni ambacho kitatumia malighafi zinazotokana na alizeti kwani mkoa huo bado hauna kiwanda cha sabuni.

  Ameongeza tayari wameweka mikakati ya kuhakikisha zao hilo linalimwa kwa wingi na kuongezewa thamani ili yapatikane mafuta ya kutosha ya kuuza ndani na nje ya nchi ikiwemo nchi za Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi."Juhudi za kuwaweka wakulima pamoja katika makundi na kuwapatia elimu kuhusu kilimo bora cha alizeti zinaendelea lengo ni kukuza kilimo cha alizeti katika mkoa huo,"amesisitiza. 

  Imeelezwa ushirikiano baina ya Gola Foundation na Kagera Edible Oil unatarajia kuzaa matunda kwa kuunganisha nguvu kwa pamoja na kuwafikia wakulima na kutatua changamoto zao ikiwemo za kielimu na teknolijia ya usindikaji.Huku wakiwaomba wadua wengine wajitokeze ili kuunga mkono juhudi hizo.

  “Tumepanga kuwa na mkutano wa wadau wa alizeti Juni 25 ili kujadili kwa pamoja namna ya kulipeleka mbele zao la alizeti wadau watakutana Bukoba mjini vikundi vyote vya wakulima wa alizeti pamoja na vyama vya ushirika,” anafafanua  Kibambi.Anasisitiza zao la alizeti ni mkombozi kwa wakulima kwani mazao mengine yamekua yakiporomoka bei kama kahawa lakini zao la alizeti huwa haliporomoki bei kirahisi na linaweza kuvunwa kwa mwaka mara 3 tofauti na mazao mengine ambayo huvunwa kwa mwaka mara moja.


  Kagera Edible oil inatoa mafunzo kwa wakulima 3000 wa alizeti katika Mkoa wa Kagera na kwa mwaka huu mavuno yanatarajia kufikia tani 60 kipindi cha nyuma ilikua na makunsanyo ya tani 4. Pia wanatarajia kuwa na kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti ambacho kitakua chachu ya kilimo cha alizeti kwani wakulima watakua karibu na soko la mazao yao.

  Tayari Gola Foundation na Kagera Edible Oil ina mkataba wa kufanya kazi kwa pamoja na kushirikiana katika masuala ya uwekezaji katika mkoa wa Kagera.

  0 0

  Na Veronica Kazimoto,Iringa

  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere amewapongeza Wafanyabiashara mkoani Iringa kwa kuwa na mwitikio mkubwa wa kutumia Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFD) ambazo husaidia kutunza kumbukumbu za mauzo ya wafanyabiashara hao na kurahisisha ukusanyaji mapato ya Serikali.

  Akizungumza leo mara baada ya kutembelea baadhi ya maduka na vituo vya mafuta mkoani hapa, Kichere amesema kwamba, mwamko wa matumizi ya Mashine za EFD umeongezeka kwa kiasi kikubwa na wafanyabiashara wengi wanatumia mashine hizo kwa ufasaha.

  "Nichukue nafasi hii kuwapongeza wafanyabiashra wa Iringa mjini kwa mwitikio wao mkubwa wa kutumia Mashine hizi za EFD. Nimeona maduka mengi na wafanyabiashara wengi sana wakitumia mashine za EFD katika maduka na vituo mbalimbali vya mafuta hapa mjini," alisema Kichere.

  Aidha, Kamishna Mkuu Kichere amewahimiza wafanyabiashara hao na wananchi kwa ujumla kuendelea kutoa na kudai risiti kila wanapofanya mauzo na kununua bidhaa na huduma mbalimbali.Kwa upande wake mfanyabiashara maarufu wa Kampuni ya ASAS iliyopo mkoani hapa, Feisal Abri amesema kuwa, ujio wa Kamishna Mkuu wa TRA ni wa muhimu kwa wafanyabiashara hao kwani huwasaidia kutambua Sheria mbalimbali za Kodi zikiwemo zile zinazohusiana na matumizi ya Mashine za EFD.

  "Ujio wa Kamishna Mkuu unatupa nguvu sisi wafanyabiashara na kuona kwamba hatuko peke yetu ila kuna watu wanatufuatilia kwa maana ya kutusaidia kujua Sheria mbalimbali za Kodi. Hivyo, ninaomba utamaduni huu uendelee na uwe wa mara kwa mara," alieleza Abri.Naye, Rehema Shabani mfanyabiasha wa duka la nguo lililopo katika soko la Miyomboni alisema kuwa amefurahishwa sana na ziara ya Kamshina Mkuu wa TRA katika soko hilo kwa sababu amepata fursa ya kumueleza kero na malalamiko yake.

  "Nimefurahi sana kumuona Kamishna Mkuu wa TRA kwa sababu nimetoa kero zangu na nimemueleza malalamiko yangu na amewaagiza viongozi wa TRA hapa mkoani kuyafanyia kazi," alisema Rehema.Kamishna Mkuu Charles Kichere amehitimisha ziara yake mkoani Iringa ambapo amefanikiwa kutembelea jumla ya maduka ya bidhaa mbalimbali 36 pamoja na vituo vya mafuta vinne.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akisikiliza maoni kutoka kwa mfanyabiasha wa duka la nguo lililopo katika soko la Miyomboni mkoani Iringa Bi. Rehema Shabani wakati alipofanya ukaguzi wa matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) kwenye maduka na vituo mbalimbali vya mafuta leo mkoani hapo.
  Mfanyabiashara wa Kampuni ya ASAS iliyopo mkoani Iringa Feisal Abri akitoa maelezo kuhusu namna Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) inavyofanya kazi katika kituo chake cha mafuta wakati Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere alipofanya ukaguzi wa matumizi ya mashine za EFD kwenye maduka na vituo mbalimbali vya mafuta leo mkoani Iringa.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (aliyevaa kofia kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa moja ya kituo cha mafuta mkoani Iringa wakati alipofanya ukaguzi wa matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) kwenye maduka na vituo mbalimbali vya mafuta leo mkoani hapo. (PICHA NA TRA).

  0 0

  Na Frankius Cleophace, Tarime

  NCHI za Kenya na Tanzania zimeshauriwa kuendelea kushirikiana vema katika kupinga na kulaani vitendo vya ukeketaji kwa mtoto wa kike huku zikitakiwa kumthamini na kumpa kipaumbele katika elimu.

  Ushauri huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Wazee wa Mila kutoka nchini Kenya Zacharia Ghati wakati wa mkutano wa hadhara ulioandaliwa na wazee wa Mila Kijiji cha Pemba kwa kushirikiana na Shirika la ATFGM Masanga ambao wanapiga vita ukeketaji.Zacharia amesema kuna koo ambazo zinapatikana Tarime kwa upande wa Tanzania pia zinapatikana nchini Kenya, hivyo wote wanatamaduni moja.

  " kama ni suala la ukeketaji wengine wanaenda Kenya ili kutimiza azma yao na wengine kutoka Kenya na kuja Tanzana, hivyo sasa kuna haja kubwa ya kushirikiana baina ya nchi zote mbili ili kukomesha ukeketeji,"amesema.

  Kwa upande wa Mzee wa Mila kutoka Koo ya Bukenye Elias Maganya anasema wao kama wazee wa mila tayari wamepaza sauti zao na kudai kuwa mwaka huu hapatakuwa na ukeketaji kwa mtoto wa kike.

  "Na suala la kupaka unga tutapaka watoto kuanzia miaka 15 si watoto wadogo na lengo ni kutimiza mila na ili suala litamalizika polepole kama zamani tulikuwa tunatoboa masikio."Wajaruo wanangoa Meno lakini Vyote kwa sasa vimeisha na suala la Ukeketaji litaisha lenyewe,"amesema Elias.

  Kwa Upande wake Mratibu wa Afya na Ustwai wa Jamii Wilaya ya Tarime Abel Gichaine amesema kusisitiza mikataba ambayo nchi ilisaini kwa lengo la Kulinda haki za binadamu ili zisikiukwe.Hivyo suala la ukeketaji linapotendeka linakikua sheria hizo ikiwemo Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 huku Mkurugenzi wa Shirika la ATFGM Masana Stella Mgaya amehimiza amehimiza umuhimu wa kumjua ili jamii iondokane na ukeketaji.

  Ametumia fursa hiyo kuwataka mabinti kipindi cha tohara inapoanza waende Kituo cha kuhifadhi mabinti hao Masanga ili kupatiwa elimu ikiwemo elimu ya makuzi, kupinga ndoa na mimba za utotoni.
  Zacharia Ghati Mzee wa Mila kutoka Nchini Kenya akitoa Elimu kwa Wananchi wa kata ya Pemba .
  Wazee wa Mila Muungano wa Koo12 Kabila la Wakurya na Wazee wa Mila kutoaka Nchini Kenya wakiwa katika Mkutano huo wa kutoa Elimu ya Kupinga Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.
  Wangubo Mtongori Mzee wa Mila kutoka Koo ya Bukira Tanzania na Kenya akitoa Elimu kwa Wananchi wa kata ya Pemba.
  Wanaanchi wa Kijiji cha Pemba kata ya Pemba wakiwasikiliza Wazee wa Mila Muungano wa Koo12 kipindi wakitoa Elimu Hiyo ya kupinga Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.
  Abel Gichaine ambaye ni Mratibu wa Huduma ya Afya na Ustawi wa Jamii Wilaya ya Tarime akitoa Elimu kwa Wananchi hao na kutaja madhara yanayompata Mwanamke aliyekeketwa wakati wa kijifungua na kufafanua sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009.

  0 0


  Katibu wa Rais Ngusa Samike akimkabidhi Rehema Kadogosa ambaye ni Mama wa Mtoto Latifa Kadogosa (13) aliyelala kitandani kiasi cha Shilingi milioni tano (5,000,000/-) fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kumsaidia mtoto huyo ambaye ana matatizo ya kiafya jijini Dar es Salaam.
  Katibu wa Rais Ngusa Samike akimuangalia mtoto huyo Latifa Kadogosa(13) ambaye amepakatwa na Mama yake Rehema Kadogosa Mwenge jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa Tawi la Benki ya CRDB Mikocheni Rehema Moyo akimkabidhi Kadi ya Benki Rehema Kadogosa mama mzazi wa Latifa Kadogosa mara baada ya kufungua Akaunti katika tawi hilo kwa ajili ya kutunza fedha hizo alizopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na fedha nyingine atakazosaidiwa na wadau wengine. PICHA NA IKULU

  0 0

  Na.Estom Sanga-TASAF. 

  Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF yameanza kuvutia Mataifa mbalimbali ya kiafrika kuja nchini kujifunza namna Mpango huo unavyotekelezwa. 

  Miongoni mwa nchi ambazo zimetuma wataalamu kujifunza namna serikali ya Tanzania kupitia TASAF inavyotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaohudumia takribani kaya Milioni Moja na Laki Moja ni pamoja na Sudan Kusini na Nigeria. 

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa Ujumbe huo ambao umeanza ziara katika Ofisi za TASAF jijini Dar es salaam,wamepongeza hatua ya Serikali ya Tanzania kutekeleza Mpango huo ambao wamesema unawagusa moja kwa moja wananchi wanaokabiliwa na umaskini. 

  Wamesema mkakati huo wa kupunguza umaskini kwa njia ya hifadhi ya jamii unaonyesha mafanikio makubwa nchini Tanzania na hivyo kuvutia nchi nyingine kuja kujifunza namna Mpango huo uliyofanikiwa. 

  Aidha wajumbe hao kutoka Sudan Kusini na Nigeria wamesema utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaofanywa na Serikali ya Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umefanikiwa kwa kiwango kikubwa kutokana na dhamira ya dhati inayoonyeshwa na serikali katika kupambana na umaskini kwa kuwashirikisha wananchi. 

  Akitoa maelezo kwa Wageni hao,Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga amesema mafanikio ya shughuli za Mpango yametokana kwa kiasi kikubwa na ushirikishaji wa Wananchi tangu katika hatua za awali hadi sasa,huku akiipongeza Serikali kwa kuratibu kwa ufanisi utekelezaji wa shughuli za Mpango huo. 

  Ametaja baadhi ya mafanikio ya Mpango kuwa ni kuhamaisha walengwa wa Mpango kufanya kazi za uzalishaji mali kwa kutumia ruzuku wanayoipata na kuboresha makazi yao kwa kujenga nyumba bora, huku msisitizo pia ukiwekwa katiamsekta za elimu, afya na lishe hususani kwa watoto na mama wajawazito. 

  Ujumbe huo utapata fursa ya kutembelea mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambako utakutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na kujionea namna wanavyonufaika na Mpango huo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akizungumza na wageni kutoka Sudan Kusini na Nigeria (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa mikutano wa TASAF jijijini Dar es salaam,wageni hao wako nchini kujifunza namna TASAF inavyotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
  Mmoja wa wageni kutoka Sudan Kusini akizungumza kwenye ukumbi wa mikutano wa TASAF jijini Dar es salaam juu ya azma ya serikali yao kujifunza utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ili kwenda kuutekeleza nchini kwao.
  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akizungumza na wageni kutoka Sudan Kusini na Nigeria (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa mikutano wa TASAF jijijini Dar es salaam,wageni hao wako nchini kujifunza namna TASAF inavyotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
  Wajumbe kutoka Sudan Kusini,Nigeria,na baadhi ya Watumishi wa TASAF makao makuu wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ofisi za TASAF jijini Dar es salaam.

  0 0


  HelpAge International in partnership with Jb Geriatrics and HIV Center, Pwani DPA and GSST have been implementing a project on Measuring Healthy Aging and Co Designing Health in Tanzania. The project is being implemented in Kibaha township and Kibaha Municipal council.

  Judith Bagachwa director of Jb geriatrics says Mwendapole A is one of the communities that has successfully been engaged in the implementation of the project. The beginning was really tough because the practice of community life competence requires members to use/utilize their own resources so as to solve their problems. 

  The process of using their own resources took a very long time before community members realized they were capable of doing something by themselves. CLCP has helped Mwendapole A community members learn to appreciate their strengths and take actions towards challenges that they face.

  So as to live a healthy living style Mwendapole A started a vegetable garden where community members could grow vegetables to improve on their nutrition. Community members worked together and through the help of their local leader they managed to secure a piece of land where they could grow their vegetables. 

   Mr Desdery Masawe who works at the Local government office, confirmed that a piece of land was secured for community members to implement on their project. Community members immediately took actions and started to work on their project.

  Salum Chambuli a group chairperson explained that the steps taken gave community members a sense of progress and believed that anything is possible. Before the land was secured people had lost hope and others left. But now that the land is available people have put all their strengths in making sure that the community project becomes a success. 

   Despite the success that Mwendapole A received in achieving their goals, a community was struck by a loss of land after the original owner decided to take his land for personal use. This was a big turning point to community members. Members became devastated and lost hope.

  Community members gathered and encouraged themselves that there was a solution to every problem. They then came up with another plan. This time one of them decided to provide for the community a piece of land where they could start a fresh and resume on the normal routine like they had before. The SALT, (S-Stimulate, A-Appreciate, L- Listen/Learn, T-Transfer) provides confidence to community members that they are capable of solving their problems. Communities come to realize the strengths that they have and use the strengths to take necessary actions

  Elizabeth Nkwela says “ I was approached and asked if I could provide an area for the community project. I had participated and seen the benefits of the first project. I saw the community strength and efforts that members had put to achieve our community dream. Without hesitation I said yes and gave a portion of my land to the community. The place is big enough to run our community dream and we can grow anything we want.”

  Judith further said “We take the competence approach to communities to make them competent but becoming competent is like journey. It does not happen suddenly. The CLCP approach provides community members with confidence to practically take ownership and deal with their own problems.

  Community members at their new farm
  Elizabeth Nkwela at the community farm
   

  0 0

  Mhamasishaji wa Afya kutoka shirika la FHI 360, Happiness Swai akimhamasisha mmoja wa wakaazi wa eneo la Chamgombe jijini Dodoma ambaye ni mhudumu wa duka la dawa kujitokeza katika zoezi la kitaifa la upimaji na tiba wa VVU linaloratajiwa kuzinduliwa rasmi na Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa tarehe 19 mwezi huu katika uwanja wa Jamhuri jijini humo.
  Wahamasishaji wa Afya kutoka shirika la FHI 360 wakiwa katika harakati za kuwahamasisha wakaazi wa eneo la Changombe jijini Dodoma kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kitaifa la upimaji wa VVU na kuanza kutumia dawa mapema ambalo linatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa tarehe 19 mwezi huu katika uwanja wa Jamhuri jijini humo.
  Mhamasishaji wa Afya kutoka shirika la FHI 360, Getruda Francis akimhamasisha mmoja wa maderava wa bodaboda na mkaazi wa jijini Dodoma, eneo la Mipango kujitokeza katika zoezi la kitaifa la upimaji na tiba wa VVU linaloratajiwa kuzinduliwa rasmi na Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa tarehe 19 mwezi huu katika uwanja wa Jamhuri jijini humo. 
  5. Mhamasishaji wa Afya kutoka shirika la FHI 360, Getruda Francis akimhamasisha mmoja wa wakaazi wa Area A, jijini Dodoma ambaye ni mama wa nyumbani, kujitokeza katika zoezi la kitaifa la upimaji na tiba wa VVU linaloratajiwa kuzinduliwa rasmi na Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa tarehe 19 mwezi huu katika uwanja wa Jamhuri jijini humo.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanafaniyika kwa siku tatu mfulilizo. Wananchi mbalimbali wamefika kwa wingi katika hospitali hiyo kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na hospitali hiyo pamoja na kupima afya bure. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Muhimbili, Bw. Juma Muhimbi na Mkurugenzi wa Tiba katika wizara hiyo, Dkt. Doroth Gwajima.
  Wananchi mbalimbali wakiwamo wataalamu wa MNH wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizungumza kwenye viwanja vya Muhimbili.
  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Dkt. Onesmo Kisanga akifafanua jambo kwa Waziri Ummy Mwalimu kuhusu magonjwa ya figo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru wakati kulia ni mjumbe wa bodi ya Muhimbili, Bw. Juma Muhimbi.
  Bw. Paul Mayengo akipima dawa ya methadone kwa watu wenye tatizo la uraibu wa heroin katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Dawa hiyo inatumiwa na wataalamu wa afya kwa ajili ya kutibu uraibu.
  Prisca akimweleza waziri kuhusu maendeleo yake baada ya kupandikizwa figo katika hospitali hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Mahonjwa ya Figo, Dkt. Jacqueline Shoo.
  Waziri Ummy Mwalimu akiwa kwenye banda la lishe ambako ampatiwa maelezo kuhusu lishe bora. Kushoto ni mmoja wa watu akipimwa afya baada ya kutembelea banda hilo leo.
  Ofisa Ustawi wa Jamii wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), John Mwakyusa akitoa huduma ya ushauri kwa mmoja wa watu waliotembelea banda hilo.
  Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akimsikiliza Msimamizi wa wodi ya Kangaroo, Cleopatra Mtei jinsi ya kuwabeba watoto wanaozaliwa kabla ya muda (premature).
  Mtoto, Mnyaman Omary Mohammed akizungumza na Waziri Ummy Mwalimu leo katika viwanja vya Muhimbili ambako maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yanaendelea.
  Mkuu wa Idara ya Afya ya Akili, Dkt. Frank Masao akieleza shughuli mbalimbali za tiba zinazofanywa na idara hiyo.

  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Jinana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufungua Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kongamano la Tatu la Uwezeshaji  Wananchi Kiuchumi kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 9 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Kongamano hilo kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na baadhi ya viongozi walioshiriki katika Ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi wakipiga makaofi baada ya Waziri Mkuu kufungua Kongamano hilo kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa, Faustine Kamuzora, Meya wa jiji la Dodoma,Profesa Davis Mwamfupe, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng'i Issa. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizinduaTaarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mei 2017 Mpaka Mei 2018  baada  ya kufungua Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha Taarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mei 2017 Mpaka Mei 2018  baada  ya kuizindua  katika Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mhandisi, Salome Kabunda  kutoka TANROADS  Tuzo ya Uwezeshaji Kiuchumi, baada ya TANROADS kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Wizara, Wakala na Idara za Serikali kwenye  Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofunguliwa na Waziri Mkuu katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mku, Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama  (katikati) Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mku, Profesa Faustine Kamuzora baada ya kufungua Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018.

  0 0

  MEYA Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Yusuph Mwenda ameishauri jamii kuendelea kudumisha amani na upendo hasa kipindi hiki ambacho Taifa linapopiga hatua za kimaendeleo chini ya Uongozi wa Rais Dk.John Magufuli.

  Mwenda aliyasema hayo jijini Dar es Salaam baada ya kuandaa Chakula maalumu kwa ajili ya watoto wanaoishi katika Mazingira magumu wanaolelewa katika Kituo cha Malaika.Amesema katika kipindi hiki ambacho Tanzania inaendelea 'kujengwa' kiuchumi kupitia miradi mbalimbali ya kimaendeleo, kuna kila sababu kwa wananchi wote kudumisha amani iliyopo nchini, kama hatua ya kuungana mkono maendeleo hayo.

  Amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Serikali ya awamu ya tano, Taifa limeshuhudia likitekeleza miradi mikubwa ya kimaendeleo.Ametaja baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa Reli ya Kisasa(Standard Gauge),Bwawa la kuzalisha umeme la Mto Rufiji(Stiggler's George) na kuiunganisha mikoa mbalimbali kwa barabara za lami.

  "Sote tunashuhudia namna ambavyo Taifa letu linazidi kupiga hatua kuelekea mikakati ya Serikali ya ujenzi wa uchumi wa viwanda ifikapo 2025."Ambayo kimsingi kama watanzania tunapaswa kuipongeza,lakini ili hayo yafanyike kwa ufasaha tunapaswa kwanza kudumisha amani yetu tuliyonayo,"amesema Mwenda.

  Aidha Mwenda ameiomba jamii kuwa na upendo kwa watoto wadogo hasa yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu ili kujiona kuwa sehemu ya familia zingine ambazo hazipo katika maisha wanayoyapitia.Amesema watoto hao ambao wengi wao wamepoteza wazazi wao wana kila sababu ya kuoneshwa upendo ili kuwajenga kisaikolojia wakati wote wanapokuwa katika maeneo wanayoelelewa.

  "Hiyo itasaidia kuwapa nguvu ya kuwafikisha katika malengo yao mbalimbali ya kimaisha.Tuwapende ili wajione na wao ni sehemu ya jamii kama ilivyo kwa watoto wengine,"amesema.

  0 0

  Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo ametoa wiki mbili kuanzia leo kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha wanabainisha maeneo ya ujenzi na mafundi watakaojenga madarasa 478 na mabweni 269.

  Ameayasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa leo yanayofanyika katika ukumbi wa chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Jijini Dodoma.

  Mhe. Jafo alisema kuwa tayari Serikali imetenga shilingi bilioni 29 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 478 mapya na Mabweni 269 ili kuhakikisha wananfunzi wote waliokosa nafasi ya kupangiwa kujiunga na kidato cha tano awamu ya kwanza wanapata katika uchaguzi wa awamu ya pili.

  Mhe. Jafo amewataka Wakurugenzi hao kuhakikisha wanatumia muda mdogo kubainisha maeneo yatakayojengwa madarasa na mabweni kwa kutumia njia ya “Force Account” ili uchaguzi wa wanafunzi awamu ya pili uatakapofanyika na ujenzi huo uwe umekamilika. 

  Mhe. Jafo aliwaagiza Wakurugenzi hao kusimamia ujenzi huo na kuhakikisha unakamilika tarehe 30/08/2018 ili wanafunzi waliokosa nafasi ya kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya kwanza wanachaguliwa katika awamu ya pili na kutimiza ndoto za wanafunzi hao .

  Mhe Jafo aliwaagiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha wanasimamia kwa weledi ujenzi wa miradi mbalimbali katika Halmashauri zao ikiwemo ya ujenzi wa madarasa na Mabweni ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa madarasa nchini.

  “Ninawaagiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Nchini kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ujenzi wa madarasa na mabweni kwa umakini wa hali ya juu ili dhamani ya fedha inayotolewa na Serikali iendane na majengo yatakayojengwa. Alisema Jafo

  Aidha Mhe. Jafo alisema sambamba na ujenzi huo Serikali imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya vingine 98 na kuwataka kuhakikisha wanafanyakazi kwa weledi na umakini wa hali ya juu hasa katika suala zima la usimamizi wa miradi mbalimbali ili dhamani ya fedha zinazotolewa iendane na majengo yatakayojengwa. 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akitoa maagizo kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa leo yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Jijini Dodoma.

  Mkurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Dkt. Charles Mhina akiongea na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye mafunzo ya siku mbili kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa leo yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Jijini Dodoma.
  Baadhi ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa leo yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Jijini Dodoma.
  Baadhi ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa leo yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Jijini Dodoma

  0 0

   

  0 0

  Na Veronica Simba – Dodoma

  Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, amefurahishwa na maombi ya wawekezaji wa Kampuni ya CTC Power Equipment Co. Ltd, kutoka China, wenye nia ya kujenga Kiwanda cha kutengeneza vifaa maalum vinavyotumika kuzuia upotevu wa umeme vijulikanavyo kitaalam kama ‘Insulators.’

  Wawekezaji hao ambao wameingia ubia na Kampuni ya kizalendo iitwayo Interbest Investment Co. Ltd, waliambatana na Mkurugenzi wake, Augustine Masonga na kuwasilisha maombi hayo kwa Waziri, Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma, Juni 18, 2018.

  Waziri Kalemani alisema kuwa, lengo la Serikali ni kuhakikisha vifaa vyote vinavyotumika kuunganisha umeme vinanunuliwa hapa nchini na tayari imekwishapiga marufuku kuagiza vifaa kama transfoma, nguzo na nyaya mbalimbali, ambavyo vinapatikana hapa nchini.

  “Kwa upande wa ‘insulators’, tumeshindwa kutoa zuio hilo kwakuwa, hazipatikani nchini na hivyo tunalazimika kuziagiza kutoka nje ya nchi,” alisema Waziri na kuongeza kuwa, itakuwa ni faraja kubwa kwa Serikali endapo wawekezaji hao watafanikiwa kuanzisha Kiwanda husika ili kuepusha gharama kubwa zinazotumika kuagiza vifaa hivyo nje na pia kupunguza muda mrefu unaotumika katika kuvisafirisha.

  Aliwataka wawekezaji hao kukutana na wataalam wa Shirika l
  a Umeme Tanzania (TANESCO) ili kujadiliana nao kuhusu suala la viwango vinavyotakiwa kwa ajili ya vifaa husika. Pia, aliwataka kukutana na wataalam kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), ili waweze kufahamishwa viwango vinavyotakiwa nchini.

  Waziri aliwapongeza wawekezaji hao kuingia ubia na mzalendo kwani ni moja ya vigezo vya kisera vinavyohitajika katika uwekezaji wa aina hiyo nchini.
  Alisema kuwa, mbali na kuwapatia ajira wananchi lakini pia itasaidia kuwapa fursa ya kujifunza teknolojia husika ili baadaye waweze wao wenyewe kuanzisha aina hiyo ya uwekezaji na kuisimamia kikamilifu.

  Wawekezaji hao waliahidi kutekeleza yale yote waliyoelekezwa na Waziri na kusema kwamba wanatarajia kukamilisha kazi zote za maandalizi ndani ya kipindi cha miezi zita kutoka sasa, na hivyo Kiwanda kuanza kazi ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu au Januari mwakani.
   Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, akiwa katika mazungumzo na Ujumbe kutoka Kampuni ya CTC Power Equipment ya China, waliwasilisha maombi ya kujenga kiwanda cha kutengeneza vifaa vya kuzuia upotevu wa umeme (Insulators), Juni 18, 2018, Makao Makuu ya Wizara Dodoma. Wengine pichani ni wataalam wa Nishati wa Wizara.
   Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akiagana na Augustine Masonga, ambaye kampuni yake imeingia ubia na Kampuni ya CTC Power Equipment kutoka China waliowasilisha maombi ya kujenga kiwanda cha kutengeneza vifaa vya kuzuia upotevu wa umeme (Insulators) nchini, Juni 18, 2018, Makao Makuu ya Wizara Dodoma.
  Wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Salum Inegeja (wa pili kutoka kulia), Sebastian Shana (wa tatu kutoka kulia) na Mhandisi Ahmed Chinemba (wa pili kutoka kushoto), wakijadiliana na Ujumbe kutoka Kampuni ya CTC Power Equipment kutoka China, baada ya kikao chao na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) ambapo waliwasilisha maombi ya kujenga kiwanda cha kutengeneza vifaa vya kuzuia upotevu wa umeme (Insulators) nchini. Kikao hicho kilifanyika Juni 18, 2018 Makao Makuu ya Wizara Dodoma.

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe Jenista Mhagama (wa pili kushoto) akiwa ameandamana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Bilinith Mahenge (kushoto),  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu  Prof Faustin Kamuzora (wa pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS  Dk Leonard Maboko (kulia) wakijadili jambo wakati wa ukaguzi wa maandalizi ya uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema inayojulikana kama Furaha Yangu. Kampeni  hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe Jenista Mhagama (wa pili kulia) akipokea maelezo kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema inayojulikana kama Furaha Yangu wakati alipotembelea uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ambapo kampeni  hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe Jenista Mhagama (wa kwanza kulia) akikagua mabanda ambayo yatatumiwa na wananchi kupima VVU  katika Kampeni ya Kitaifa ya Kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema inayojulikana kama Furaha Yangu. Kampeni  hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma. Mhe Mhagama alikuwa ameandamana na kamati ya maadalizi wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Bilinith Mahenge,  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu  Prof Faustin Kamuzora pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS  Dk Leonard Maboko.  “FURAHA YANGU – PIMA, JITAMBUE, ISHI”

  Utangulizi

  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI kwa kushirikiana  na FHI360 mradi wa USAID –Tulonge Afyana wadau wengine inatarajia kufanya kampeni ya Kitaifa ya Upimaji wa VVU na Kuanza Kutumia ARV Mapema. Kampeni hii inasimamiwa na kikosi kazi kilichoundwa kwa kujumuisha wataalamu toka Wizara yetu, TACAIDS, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na wadau wa VVU na UKIMWI. Jukumu kuu la kikosi kazi ni kusimamia maandalizi, utekelezaji na tathimini ya kampeni ikiwemo  kupitia matangazo na machapisho mbalimbali. Kamati hii inaongozwa na wenyeviti ambao NACP na TACAIDS, wakishirikiana na wawakilishi wa TAMISEMI, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na kazi za kuweka kumbukumbu zimeongozwa FHI360 Kupitia mradi wa USAID Tulonge Afya.

  Hali hali halisi ya maambukizi nchini Utafiti wa nne uliofanyika katika ngazi ya kaya kuanzia mwezi Oktoba 2016 hadi Agosti 2017 ulibainisha kuwa wastani wa kitaifa wa maambukizi ya VVU kwa watu wenye umri wa miaka 15 hadi 49 ni asilimia 4.7. Wanawake ni asilimia 6.2 na wanaume ni asilimia 3.1.

  Nchi yetu imeridhia na kuanza utekelezaji wa kauli mbiu ya kidunia ya TISINI TATU ifikapo 2020 (asilimia 90 ya watu wanaoishi na VVU wawe wamejua hali zao za maambukizo; asilimia 90 ya waliopimwa VVU na kugundulika kuwa wana maambukizo wapatiwe dawa za kufubaza makali ya VVU; na asilimia 90 ya watu wanaotumia dawa wawe wamefubaza VVU). 

  Hali halisi ya utekelezaji wa kufikia hizi tisini tatu ni Kama ifuatavyo:
  Tisini ya Kwanza: Nchini Tanzania ni asilimia 52.2 tu ya wanaoishi na VVU wenye umri wa miaka 15 – 64 walitoa taarifa kuwa wanajua hali zao za maambukizo ya VVU (Wanawake  ni asilimia 55.9 na Wanaume  ni asilimia 45.3)

  Tisini ya Pili: Kati ya watu wanaoishi na VVU wenye umri wa miaka 15 – 64 ambao wanajua hali zao za maambukizo, asilimia 90.9 walitoa taarifa kuwa wanatumia dawa za kufubaza VVU (Wanawake  ni asilimia 92.9 na Wanaume ni asilimia 86.1)

  Tisini ya Tatu: Kati ya watu wanaoishi na VVU wenye umri wa miaka 15 – 64 ambao wametoa taarifa kuwa wanatumia dawa za kufubaza VVU, asilimia 87.7 ya watu hao inaonyesha kiasi cha VVU kimefubazwa (Wanawake  ni asilimia 89.2 na Wanaume ni asilimia 84).

  Hivyo basi, Tanzania inafanya vizuri sana katika Tisini ya pili na tatu, lakini tatizo kubwa ni katika kufikia 90 ya kwanza, kwani ni asilimia 52.2 tu ya wenye VVU wanajua hali zao. Tatizo hili ni kubwa zaidi miongoni mwa wanaume, kwani ni asilimia 45.3 tu ya wanaume wanaoishi na VVU wanajua hali zao.
   older | 1 | .... | 1601 | 1602 | (Page 1603) | 1604 | 1605 | .... | 1896 | newer