Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1603 | 1604 | (Page 1605) | 1606 | 1607 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mheshimiwa Hamid Mahmoud Hamid kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.

  Dkt. Shein amefanya uteuzi huo kwa kutumia uwezo aliopewa chini ya Kifungu 119 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 .

  Aidha amewateua wajumbe sita wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ambao ni Bwana Mabrouk Jabu Makame, Bwana Feteh Saad Mgeni, Bwana Makame Juma Pandu, Dkt. Kombo Khamis Hassan, Jaji Khamis Ramadhan Abdalla na Bibi Jokha Khamis Makame.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotiwa saini na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee, uteuzi huo umeanza leo tarehe 20 Juni 2018.

  Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi walioteuliwa wataapishwa siku ya Ijumaa tarehe 22 Juni 2018 saa 4.00 asubuhi Ikulu Mjini Zanzibar.

  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

  Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.

  KONGAMANO la kimataifa la madaktari wa mifupa duniani limeanza kufanyika leo hadi Juni 23 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

  Ambapo linaratibiwa na Taasisi za IGOT, SIGN, OTA, OA ALLIANCE na Chuo Kikuu cha Calfonia San Fransisco cha Marekani na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.Akizungumza leo Dar es salaam Daktari bingwa wa mifupa Bill Aonga amesema kuwa mafunzo hayo yatatolewa na madaktari bingwa wa Mifupa wa MOI kwa kishirikiana na wakufunzi kutoka Marekani, Uingereza na Switzerland.

  Amefafanua mafunzo hayo yatalenga mbinu mpya za matibabu ya mivunjiko mbalimbali ya Mifupa, magonjwa yatokanayo na ajali na namna ya kufidia kilande cha mfupa kilichopotea kutokana na ajali.Ameeleza washiriki sita kutoka Tanzania watapewa mafunzo hayo na baadaye watakuwa wakufunzi wa mafunzo hayo bila kutegemea wageni.

  Pia daktari bingwa wa mifupa aliyebobea katika nyonga na kiuno Joseph Mwanga amesema idadi kubwa ya watanzania walioshiriki katika mafunzo hayo watanufaika na ujuzi waliopata utanufaisha na kuendeleza wengi.Mafunzo hayo wamelenga kuangalia namna ya kuunga mifupa na misuli mara baada ya kuchanika na kupoteza misuli.

  Aidha imeelezwa taasisi ya MOI inatambulika kama kitovu cha weledi katika matibabu ya mifupa kwa muda mrefu wa paja kwa kutumia teknolojia ya kuweka chuma ndani ya mfupa.Na teknolojia hiyo hutumika zaidi duniani na hadi sasa taasisi ya MOI imefikisha wagonjwa zaidi ya 8,000 idadi ambayo haijafikiwa na hospitali yoyote duniani.

  Pia mafunzo hayo hufanyika kila mwaka kwa miaka 6 mfululizo ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani na kuwapa mbinu mpya madaktari bingwa ili waweze kuendana na teknolojia ya matibabu duniani inayobadilika mara kwa mara.
  Daktari Bingwa wa Uhamishaji wa ngozi Profesa kutoka Marekani,Profesa Michael Terry akizungumza na Madakri wa mifupa Duniani katika kongamano lililo fanyika leo jijini Dar as Salaam.
   Daktari Bingwa wa upasuaji Mifupa na Muhadhiri wa chuo Kikuu cha Afya Mhuhimbili,Bill Aonga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano lililo fanyika leo jijini Dar as Salaam.(picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
  Wadau mbalimbali wa afya wakiwa katika kongamano hilo.

  0 0

   Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akiweka jiwe la msingi Mradi wa ukarabati na uboreshwaji katika Kituo Cha Afya Mdemu kilichopo Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma leo.kulia ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mzee na Mbunge wa Bahi Bw. Omari Baduel.
   Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikagua majengo ya wodi ya wajawazito,jengo la upasuaji wa dharura ,Mochwari ,sehemu ya kuchomea taka na maabara katika Kituo Cha Afya Mdemu kilichopo Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma kabla ya kuweka jiwe la msingi leo.
   Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikagua majengo ya wodi ya wajawazito,jengo la upasuaji wa dharura ,Mochwari ,sehemu ya kuchomea taka na maabara katika Kituo Cha Afya Mdemu kilichopo Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma kabla ya kuweka jiwe la msingi leo.

   Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwasalimia wanakijiji waliojitokeza  wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo cha Afya Mdemu kilichopo wilayani Bahi mkoa wa Dodoma .
   Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na wanakijiji wa kata ya Mdemu hawapo pichani wakati wa uwekaji jiwe la msingi katika kituo cha Afya Mdemu wilayani Bahi  jijini Dodoma.
   Mbunge wa Jimbo la Bahi Bw. Omari Baduel akiongea na wanakijiji wa kata ya Mdemu hawapo pichani wakati wa uwekaji jiwe la msingi katika kituo cha Afya Mdemu wilayani Bahi  jijini Dodoma, kushoto waliokaa ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Bi. Elizabeth Kitundu 
   Baadhi ya wanakijiji waliojitokeza kumsikiliza na kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi katika Kituo cha afya Mdemu uliofanywa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wilayani Bahi  jijini Dodoma.
   Baadhi ya wanakijiji waliojitokeza kumsikiliza na kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi katika Kituo cha afya Mdemu uliofanywa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wilayani Bahi  jijini Dodoma.
  Mafundi wakiwa katika hatua ya mwisho ya kumalizia jengo la Mochwari lilipo katika Kituo cha Afya Mdemu Wilayani Bahi Mkoa Dodoma .PICHA NA WIZARA YA AFYA -DODOMA

  0 0


  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Binafsi ya kusaidia sekta ya kilimo nchini (PASS) Bw,Nicomed Bohay akizungumza wakati wa kutambulisha fursa mpya kwa Wadau wa sekta ya Kilimo. 
   Baadhi ya Wadau wa Sekta ya Kilimo wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya PASS wakati wa utambulishaji wa fursa mpya kwa wadau wa sekta ya Kilimo. 
   Mwakilishi wa AATIF, Bwana Samuel Ndonga akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam

  0 0

  Na Frankius Cleophace BUTIAMA

  Wazee wa Mila Muungano wa koo 12 kabila la Wakurya kwa kushirikiana na Shirika la ATFGM Masanga Tarime, wameendelea kutoa Elimu ya Kupinga suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa kike kwa lengo la Kumnusuru ili atimize ndoto yake ya kupata Elimu na kutimiza Serikali ya Viwanda.

  Wazee hao Muungano wa Koo 12 wamezungukia Koo 12 Wilayani Tarime kwa Kutoa Elimu ya kupinga Ukeketaji huku wakitoa Matamko ya Kuondoa Miiko ambayo imekuwa ikikandamiza Mtoto wa kike ambaye hajakeketwa kupitia Mikutano ya hadhara lengo  ikiwa ni kufikisha Ujumbe.

  Licha ya kutoa Elimu hiyo sasa wazee hao wameamua kwenda Wilaya ya Butiama kwa lengo la kufikisha ujumbe huo uliokusudiwa, lengo ni kunusuru Mtoto wa kike.

  Akitoa Elimu hiyo Mwita Nyasibora ambaye ni Katibu Msaidizi wa koo hiyo amesema kuwa ,Koo ya Bukenye ni kubwa imesambaa mpaka Wilaya ya  jirani ya Butiama, hivyo wameona ni vyema kufikisha Elimu hiyo ili wasije kukiuka na kukeketa Mtoto wa kike kwa kuwa wazee tayari wamekataa Ukeketaji.

  “Sisi kama Wazee Muungano wa Koo12 tumeisha kataa Ukeketaji na Koo itakayokiuka iwajibishwe yenyewe” alisema Mwita.

  Mmoja wa wazee wa Mila ametoa ushuhudi jinsi gani Mwanamke zamani alivyokuwa akinyanyaswa wakati mwingine kukeketwa wakati akijifungua jambo ambalo lilikuwa linamwongezea Uchungu mara mbili na kuendeleaza Ukatili lakini kwa sasa wazee hao wameona hakuna faida ya kukeketaji bali hasara ndo nyingi kuliko faida.

  Wambura Mwema ni Mwenyekiti wa kijiji cha Buswahili Wilaya ya Butiama anasema kuwa kuna haja kubwa ya Wazee hao wa Mila kula kiapo kuhusu Matamko yao ili atakayekiuka ka kukeketa Mtoto wa kike achukuliwe hatua peke yake huku akisema kuwa Serikali inaungana na wazee hao kutokomeza Ukeketaji.

  “Sasa wazee mmetamka hapa mbele yetu kuna haja kubwa ya kula kiapo ili atakayekiuka tunachukua hatua kali na serikali inapinga sana suala ili na nyie mmeongea sasa ni jukumu letu kuungana pamoja” alisema Wambura.

  Licha ya kuzungumzia suala la kuipinga Ukeketaji kushirikiana na Shirika la Kupinga Ukeketaji Wilaya ya Tarime ATFGM Masanga Wazee hao wanaongeza kuwa kuna haja ya kuungana kwa pamoja sasa kukomesha suala la Wizi wa Mifugo huku wakituhumu kuwa Mifugo mingi inayoibiwa Wilaya ya Butiama inaishia Tarime.

  Wazee hoa kutoka Wilaya ya Butiama wameomba Wazee wa Mila kuwa watumie mbinu ambayo walitumia Tarime na kupunguza Wizi wa Ng’ombe ili jamii iendelee kunufaika na Mifugo yao.

  “Ng’ombe Wetu Wengi wanaibiwa kijijini hapa Nyao zinaishi Kijiji cha Nkerege Wilaya ya Tarime na wakati Mwingine Wilaya ya Serengeti sasa ni jukumu letu Kuungana kama Wazee na kumaliza Wizi huu” alisemaWerema Isombe Mzee wa Mila Koo ya Bukenye Butiama.

  Aidha Chacha Magera ambaye ni Mwenyekiti wa Mila Koo ya Bukenye Wilayani Butiama anazidi kusisitiza suala la Amani huku Mwenyekiti wa Muungano wa Koo12 Wilaya ya Tarime Nchagwa Mtongori akisema kuwa ni jukumu la Wazee ni kurudisha heshima iliyokuwepo tangu enzi za mababu kwa kufundisha maadili mazuri likiwemo suala la Malezi na Makuzi..

  Shirika la ATFGM Masanga limekuwa Mkombozi kwa watoto wa kike kioindi cha tohara uwahifadhi ili wasikeketwe mpka msimu unamalizika hivyo Serikai haina budi kuendelea kushirikiana Vyema na Shirika hilo ili Mtoto wa kike aweze kutimiza ndoto zake za Msingi ikiwemo kupata Elimu.
  Picha ya Pamoja Wazee wa Mila Muungano wa Koo12 Kabila la Wakurya Wilayani Tarime Mkoani Marea na Koo ya Bukenye Wilayani Butiama baada ya kikao cha pamoja kilichofanyika kijiji cha Kongoto Kata ya Buswahili Wilayani Butiama lengo ni kuzungumzia Mikakati ya Kupiga Vita Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.
  Katibu Msaidizi wazee wa Mila Muungano wa Koo12 ,
  Mwita Nyasibora 
  akitoa Elimu kwa wazee hao juu ya madhara ya Ukeketaji kwa Mtoto wa kike, ambapo amesema kuwa Wilaya ya Tarime wamezunguka na kutoa Elimu hiyo kwa jamii,hivyo wameamua kufikia Koo ya Bukenye ambayo inaenda mpaka Wilaya ya Butiama.
  wazee wa Mila wakiwa katika Kikao cha pamoja
  Baadhi ya Wazee wa Mila  wakiwa katika Kikao cha pamoja
   Mzee wa Mila kutoka Koo ya Bukenye Wilaya ya Butiama 
  Werema Osombe 
  akiomba aWazee hao kupiga Vita suala la Wizi wa Mifugo ambayo inaibiwa kutoka Wilayani humo na kupelekwa Tarime.
  Mwenyekiti wa Muungano wa wazee wa Mila kabila la Wakurya Wilayani Tarime Mkoani Mara,
  Nchagwa Mtongori 
   akijibu baadhi ya Maswali katika kikao hicho likiwemo suala la kutokomeza Wizi wa Mifugo na Suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Binafsi ya kusaidia sekta ya kilimo nchini (PASS) Bw,Nicomed Bohay akizungumza wakati wa kutambulisha fursa mpya kwa Wadau wa sekta ya Kilimo. 

  Baadhi ya Wadau wa Sekta ya Kilimo wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya PASS wakati wa utambulishaji wa fursa mpya kwa wadau wa sekta ya Kilimo.
  Mwakilishi wa AATIF, Bwana Samuel Ndonga akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam .
  Meneja uwekezaji Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Mfuko wa UGEAP,Sonja Riedke akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya PASS. 
  Balozi wa Denmark nchini Tanzania ,Einar Jensen akizungumza wakati wa hafla hiyo.
  Wadau wa sekt ya Kilimo wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa taasisi ya PASS ,AATIF pamoja na Balozi wa Denmark nchi Tanzania ,Einar Jensen.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Binafsi ya kusaidia sekta ya kilimo nchini (PASS) Bwana Nicomed Bohayakizungumza na Wanahabari muda mfupi baada ya kumalizika kwa hafla hiyo.  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii .

  Taasisi ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo nchini (PASS) imeingia makubaliano na Mfuko wa uwekezaji wa biashara na kilimo Afrika (AATIF) kusaidia wadau wa sekta ya Kilimo nchini kwa kutoa mikopo mikubwa itakayowezesha utekelezwaji wa miradi mikubwa ya kilimo.

  Makubaliano haya baina ya PASS na AATIF yanatajwa kuwa mkombozi wa changamoto za muda mrefu za wadau wa sekta ya Kilimo ambao wamekuwa wakipitia kwa kushindwa kupata mikopo ya muda mrefu kutoka kwa taasisi za kifedha hapa nchini kutokana na ufinyu wa muda wa urejeshwaji wa mikopo hiyo. 

  Kwa kiasi kikubwa hali hii imekuwa ikitajwa kama sababu ya sekta hii kushindwa kuwa na maendeleo makubwa kutokana na mipango mingi kujikita katika uwekezaji wa muda mfupi. 

  Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutambulisha fursa hiyo kwa wadau wa kilimo na baadhi ya taasisi za fedha iliyofanyika mapema leo asubuhi katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa PASS Bwana Nicomed Bohay amesema.hatua ya upatikanaji wa mikopo mikubwa na ya muda mrefu kwa wadau wakubwa wa kilimo utachochea ukuaji wa sekta ya kilimo. 

  “Malengo yetu sisi ni kutengeneza mashirikiano baina ya taasisi hizi ili ziweze kupata mikopo hii, imani yetu kama PASS nikuwa itachochea uwekezaji mkubwa katika maeneo mbalimbali ya kilimo na hivyo kuifanya sekta ya kilimo nchini kuwa mdau mkubwa wa falsafa ya serikali ya awamu ya tano ya kuziwezesha sekta binafsi na hasa kilimo katika kushiriki katika uchumi wa viwanda” Amesema Bwana Nicomed Bohay. 

  Naye Mwakilishi wa AATIF, Bwana Samuel Ndonga akizungumza katika hafla hiyo amesema, makubaliano hayo ni sehemu ya jitihada za taasisi yake kuunga mkono kiu ya siku nyingi ya Taasisi ya PASS, ambayo imekuwa ikitamani kumpunguzia changamoto mdau wa kilimo kwa kumhakikishia upatikanaji wa mikopo ya uhakika na nafuu kupitia taasisi za kifedha. 

  “AATIF kwa kushirikiana na PASS tumedhamiria kuwawezesha wakulima wakubwa kwa wadogo kufikia ndoto ya kuendesha miradi mikubwa ya Kilimo hapa Tanzania,imani yetu ni kuwa Wadau mbalimbali kama vile Taasisi za fedha zinazo toa mikopo kwa wakulima, Wazalishaji,Wasindikaji,Wafanyabiashara na Wajasiliamali wengine katika sekta ya Kilimo watachangamkia fursa hii” Amesema Bwana Samuel Ndonga 

  Kwa miaka mingi upatikanaji wa mitaji na mikopo kwa sekta ya Kilimo imekuwa ni changamoto kubwa, na kwa ujio huu wa Taasisi ya AATIF sasa tumaini la sekta ya kilimo nchini kupata mikopo kati ya dola za kimarekani milioni tano mpaka thelathini ni la uhakika jambo ambalo linaelezwa kuwa litaleta mapinduzi makubwa ya uchumi nchini kupitia sekta hii ya kilimo.


  0 0  0 0

  Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

  WAKIMBIZI mkoani Kigoma wametakiwa kurejea nchini kwao, ili waanze kujishughulisha na masuala ya maendeleo kwani kwa sasa nchi zao ziko salama na amani imerejea.

  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala katika kambi ya Mtendeli wakati wa Siku ya Wakimbikiz Duniani.

  Amesema sasa ni wakati wa wakimbizi waliko chini kurudi katika nchi zao kuendelea na majukumu mengine.Amefafanua mkapa sasa baadhi ya wakimbizi 6000 wamerejea nchini mwao kwa hiyari. "Wapo wengine bado wapo nchini kwetu kutokana na kushawishiwa na baadhi ya watu kwa maslahi yao binafsi,"amesema.

  Amewaambia wakimbizi hao ni vema wakarejea nchini kwao na kuendelea na maisha yao badala ya kubaki Tanzania kwasababu kuna watu wanawashawishi.Aidha amesema Serikali haitawavumilia wakimbizi wanaoishi katika kambi zilizopo wilayani hapo ambao watabainika kujihusisha na vitendo vya kiualifu.

  "Serikali imewahakikishia kuishi kwa amani na usalama wao pamoja na mali katika kambi yao na sambamba na kuilinda amani hiyo ambayo waliikuta nchini," amesema Ndagala Amefafanua kila mkimbizi anatakiwa kufata taratibu na sheria za nchi na kwa kila atakayekiuka taratibu hizo sheria haitamuacha salama lazima itafata mkondo wake.Pia amesema kuna changamoto ya uhalifu, kwani kuna baadhi ya wakimbizi wamekuwa wakitoka kambini na kwekuharibu mazao katika mashamba ya watanzania.

  Awali akisoma hotuba Mwenyekiti wa kambi hiyo Mtena Nizigiyumukiza ameiomba Serikali ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi(UNHCR), kufanya mahojiano na wakimbizi ambao hawako tayari kurudi nchini kwako ili wasikilizwe matatizo yao. "Tunaomba pia mtuongezee sabuni pamoja na chakula ikiwa sambamba na kubadilishiwa chakula kwani tumekuwa tukila ugali na imetufanya kutamani wali,"amesema Nizigiyumukiza.

  Mkuu wa kambi hiyo Lulu Malima, amewataka wakimbizi hao kutunza mazingira ndani na nje ya kambi na kuacha tabia ya kukata miti ovyo.
  Baadhi ya Wakimbizi wa kambi ya Mtendeli iliyopo wilayani Kakonko Mkoani Kigoma wakiadhimisha  katika siku ya wakimbizi duniani,
   Shughuli za burudani hapa na pale zilitolewa katika maadhimisho hayo hapo jana
   Baadhi ya Wakimbizi wa kambi ya Mtendeli iliyopo wilayani Kakonko Mkoani Kigoma wakiadhimisha  katika siku ya wakimbizi duniani,
   

  0 0

  *Rural Water System to benefit remote areas through solar-powered project
  The United States Agency for International Development (USAID) and The Coca Cola Foundation (TCCF), through their Water and Development Alliance (WADA) global partnership, commemorated the launch of activities that will transform the lives of more than 70,000 rural Tanzanians. The Coca-Cola Foundation and USAID are supporting project activities with a combined investment of more than US$1 million, primarily focused on an innovative water access project.

  “USAID is pleased to contribute to this enterprising approach to use clean technology to access safe water,” said USAID Tanzania Director of Economic Growth Randall Chester. “The project brings opportunity and know-how to villages to manage their own resilient water system. USAID is proud to join international and Tanzanian public and private partners in a worthwhile investment that can transform lives.”

  Tanzania has been facing unprecedented water stress. Rural villages often rely on out-of-date and inefficient water point technology for their water systems, resulting in expensive fuel costs, breakdowns, and consequently, a lack of access to safe water for the community. The WADA Tanzania project will install or upgrade solar-powered water systems in 36 villages identified by the Tanzanian Ministry of Water and Irrigation across theDodoma, Kilimanjaro, Mara, Mwanza, Singida, and Tabora regions.

  The WADA project will enhance the technical knowledge held in Tanzania’s workforce, through field work and capacity-building collaboration with the University of Dodoma. “The WADA project is a key link for the University of Dodoma academia and students to provide the much needed community service in ensuring sustainability of the village water supplies.” said Professor Flora Fabian, the University of Dodoma’s Director of Research and Publications, Innovations, Consultancy, and Institutional Collaboration.

  “For over a decade, The Coca-Cola Company and its Foundation have partnered with USAID, bringing shared opportunity to communities. We are pleased to launch this innovating new project to rural communities in Tanzania, building healthy and resilient villages through improved access to water and sanitation,” said Ahmed Rady, General Manager for Coca-Cola East & Central Franchise.

  The sustainability of these systems will be ensured through WADA’s provision of two years of technical support to train and develop water service entrepreneurs in performing basic operations and maintenance tasks. This training will increase the self-reliance of the rural villages, enabling sustained access to a safe water supply. In addition, this project will collaborate with the Ministry of Water and Irrigation, theirRegional and District Water Engineers, and staff and students at the University of Dodoma to improve management of groundwater suppliers across the nation. This will include installing a solar-powered water systemtraining program at the University of Dodoma.

  According to Marty Kress, Executive Director of the Global Water Institute at Ohio State, "The Ohio State model for sustainable water systems being deployed through this WADA project is focused not just on the installation of wells but also on the deployment of sustainable operating systems – enabling communities to thrive long after this project ends, rather than becoming reliant on its presence in the region."

  WADA Tanzania is being implemented by a consortium of partners led by The Ohio State University and managed inTanzania byWorldServe International. Together, WorldServe International andWaterboys, an American charity founded by US National Football League (NFL) athlete Chris Long, are contributing U.S. $1 million in co-financing to scale project activities.
  Mr. Randall Chester, Director of Economic Growth, USAID Tanzania (first left) explains a point during the launch of Resilient Village Water Systems in Dodoma. Looking on is (second left) Catherine Bamwenzaki, Assistant Director, Rural Water Supply Division, Ministry of Water and Irrigation, David Karamagi, Coca-Cola Tanzania Country Manager ( center), UDOM Deputy Vice Chancellor Prof. Peter Msofee (second right) and Haji Ally from Kwanza Bottlers Ltd.

  0 0

  Jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku sita  inayofanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya mjini Mumbai nchini India .

  Wagonjwa hao wamefanyiwa upasuaji wa   kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) na kubadili milango miwili hadi mitatu ya  moyo (Valve Replacement).

  Wagonjwa wote waliofanyiwa upasuaji hali zao zinaendelea vizuri na wanne kati yao wameruhusiwa kutoka  katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) na kupelekwa wodini kwa ajili ya kuendelea na matibabu.

  Katika kambi hiyo iliyoanza tarehe 18 hadi tarehe 23 mwezi huu  inaenda sambamba na utoaji wa elimu pamoja na kubadilishana ujuzi wa kazi kwa madaktari wetu pamoja na wauguzi. Jumla ya wagonjwa 20  ambao ni watu wazima  wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji.
   Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu kutoka Hospitali ya Saifee ya mjini Mumbai nchini India  Ali Ascar Beliranwalwa akivuna mshipa wa damu ndani ya kifua na kuunganisha kwenye misuli ya moyo ili kuuongezea moyo damu katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo ya siku sita inayofanywa na Hospitali hiyo kwa kushirikiana na  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Tangu kuanza kwa kambi hiyo jumla ya wagonjwa 11 kati ya  wagonjwa 20 waliopangwa kufanyiwa  upasuaji  wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) na  kubadili milango miwili hadi mitatu ya  moyo (Valve Replacement) wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri. 
    Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa  Hospitali ya Saifee ya mjini Mumbai nchini India wakimfanyia mgonjwa  upasuaji  wa  kubadili milango ya moyo  (Valve Replacement) ambayo haipitishi damu vizuri kwenye moyo katika kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku sita inayoendelea katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa  20 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo.
   Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa  Hospitali ya Saifee ya mjini Mumbai nchini India wakimfanyia mgonjwa  upasuaji  wa  kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) katika kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku sita inayoendelea katika Taasisi hiyo. Kwa kipindi cha siku tatu tangu kuanza kwa kambi hiyo jumla ya wagonjwa  11 wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri.
  Picha na JKCI

  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  WANAMUZI walio wanachama wa Umoja wa Muziki Tanzania (TAMUFO) wiki ijayo watatembelea Bunge kwa ajili ya kuona mambo mbalimbali yanayofanyika ndani ya Bunge hilo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Akizungumza Dar es Salaam jana, Rais wa Umoja huo, Dk.Donald Kisanga alisema kwa umoja huo kwao ni fursa kubwa ya kutembelea Bunge."Kwetu sisi Tamufo kutembelea Bunge ni fursa kubwa na tunaenda kuona jinsi Bunge linavyofanya kazi yake" alisema Kisanga.

  Kisanga alisema msafara wao utaondoka jijini Dar es Salaam Juni 23 na Bungeni watakuwepo Juni 25 mwaka huu na mwenyeji wao ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk.Harrison Mwakyembe.

  Kisanga aliyataja baadhi ya makundi ya wanamuziki watakaokuwepo kwenye msafara huo kuwa ni wanamuziki wa dansi ambalo litaongozwa na Mwanamuziki mkongwe Boniface Kikumbi Mwanza Mpango au King Kik na Hamza Kalala.

  Alitaja kundi la muziki wa Injili kuwa litaongozwa na Stella Joel na Emanuel Mbasha wakati Bongo Fleva litaongozwa na Witness Kibonge Mwepesi huko taarabu likiongozwa na Sizer Masogelo na Muziki wa Asili likiongozwa na Grace Kayinga.Katibu wa Tamufo, Stellah Joel alisema wanamuziki kutoka mikoa yote waliotayari watakuwepo kwenye msafara huo.
  Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dk. Donald Kisanga, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Tamufo, Morocco Dar es Salaam jana wakati wa kujadili masuala mbalimbali ya umoja huo pamoja na safari ya baadhi ya wanachama wa Tamufo kwenda Bungeni Dodoma.
  Mhandisi Abdallah Ally kutoka Kampuni ya CogsNet ambayo inasimia kazi za wasanii akizungumza kwenye mkutano huo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo.
  Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dk. Donald Kisanga, akiteta jambo na Katibu wa umoja huo, Stellah Joel wakati wa mkutano huo.
  Msemaji wa Kampuni ya CogsNet ambayo inasimia kazi za wasanii, Ahmed Kipozi akizungumza kwenye mkutano huo
  Mwanamuziki Hamza Kalala akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mwanamuziki mkongwe Boniface Kikumbi Mwanza Mpango au King Kiki.
  Katibu wa umoja Tamufo, Stellah Joel, akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
  Mwanamuzi mahiri Kitenzogu Makassy, akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mwanamuziki Hamza Kalala.
  Mwanamuziki mkongwe Boniface Kikumbi Mwanza Mpango au King Kiki akichangia jambo kwenye mkutano huo.
  Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Witness Kibonge, akizungumza kwenye mkutano huo.
  Katibu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Stellah Joel, akizungumza kwenye mkutano wa kujadili safari hiyo ya Bungeni Dodoma.
  Wanamuziki Hamza Kalala na Mzee Makassy wakiteta jambo kwenye mkutano huo.

  0 0   


    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na meza kuu wakitumia mawasiliano ya Video Conference wakati baada ya kupokea gawio la shilingi Bilioni 1.5 kwa serikali  toka kwa viongozi wa TTCL Corporation kwenye hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 21, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akijiandaa kupokea mfano wa hundi ya gawio la shilingi Bilioni 1.5 kwa serikali  toka kwa viongozi wa TTCL Corporation kwenye hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 21, 2018
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisaidiwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu akipokea mfano wa hundi ya gawio la shilingi Bilioni 1.5 kwa serikali  toka kwa viongozi wa TTCL Corporation kwenye hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 21, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia baada ya kupokea gawio la shilingi Bilioni 1.5 kwa serikali toka kwa viongozi wa  TTCL Corporation kwenye hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo  Juni 21, 2018

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma za mawasiliano za kampuni ya TTCL nchi nzima baada ya kupokea gawio la shilingi Bilioni 1.5 toka kwa viongozi wa TTCL Corporation kwenye hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 21, 2018. 

  Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

  UONGOZI wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bernard Konga umekutana na uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kujadili namna ya kuboresha huduma kwa wanachama wakati wanapofika kupata huduma za matibabu hosptalini hapo.

  Majadiliano ya huduma kati ya watoa huduma na Mfuko yamekuwa yakifanyika kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa wanachama wa Mfuko.

  Akizungumza leo kwenye kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa NHIF  Konga amesema kuwa suala la huduma bora kwa wanachama ni kipaumbele cha Mfuko kwa kuwa wamelipia huduma hizo kabla ya kuugua.

  "NHIF na watoa huduma lazima tuwe na lugha moja ya kuwapa huduma bora wanachama wetu na kama kuna tatizo linajitokeza tulishughulikie wenyewe na sio kuwahusisha wanachama wetu.

  "Na kwa kufanya hivi mwanachama atapata huduma bila usumbufu wowote na itavutia wengine kujiunga na huduma zetu," amesema Magoha.
  Uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bernard Konga umekutana na uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kujadili namna ya kuboresha huduma kwa wanachama wakati wanapofika kupata huduma za matibabu hosptalini hapo.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  SERIKALI imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni hali inayotishia afya ya mama na mtoto wakati wa kijifungua pindi wanapofika hospitalini.

  Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza kutoka Wizara ya Afya,Maedeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk . Sara Maongezi wakati akifungua Programu ya AstraZeneca ya Healthy Heart Africa (HHA).

  Programu hiyo inatokana na ushirikiano wa Touch Foundation na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.Lengo ni  kupunguza maradhi ya shinikizo la damu wakati wa mimba.

  Maongezi amefafanua ubia uliozinduliwa leo katika mradi huo utakaoongeza utekelezaji wa programu hiyo nchini Tanzania.  

  "Ubia huo unakusudia kwa kiasi kikubwa kupunguza kuenea kwa maradhi ya shinikizo la damu, hasa miongoni mwa wanawake wajawazito ikiwa ni kuunga mkono mpango mkakati wa Serikali wa kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza,"amesema Dk. Maongezi.

  Ameongeza kupanda kwa shinikizo la damu ni moja ya vihatarishi vikubwa vya ugonjwa wa moyo hali ambayo msukumo wa damu katika moyo  huzuizwa au kukatizwa na chembe chembe za mafuta kwenye mishipa ya koronari  na mwishowe huenda ikasababisha kiharusi.

  Amefafanua kwa bahati mbaya, ugonjwa wa moyo ni moja ya vyanzo vikubwa vya kifo nchini Tanzania hasa kwa wajawazito wakati wa kujifungua.

  Amesema  kupitia ufadhili wa AstraZeneca, shirika la Touch Foundation litaendeleza mpango wa Healthy Heart Africa  ambao tayari unatekelezwa huko Kenya na Ethiopia, kwa kufuata mazingira halisi ya Tanzania kama linavyotekelezwa mpango wake wa Mobilizing Maternal Health (MMH) katika mikoa ya Shinyanga na Mwanza.

   "Serikali tunaukaribisha ubia huu mpya kwa vile unakwenda sambamba na azma yetu inayolenga kinga kwa jamii, kuboresha afya, kupima, na kutoa matibabu mapema, na kuwasaidia waathirika. 

  "Ubia huu pia unajikita katika imani aliyonayo Rais John Magufuli kwamba kazi ya kujenga uchumi na kupambana na umaskini inategemea zaidi afya bora ya raia wake.

  "Kwa hiyo, nausifu mpango huu na kuwa na matarajio mema katika safari yetu ya kuboresha maisha ya Watanzania kwa kupambana na maradhi ya shinikizo la damu nchini mwetu,"amesema.

  Ameongeza shinikizo la damu kwa asilimia 16 unasababisha vifo vya mama wajawazito nchini Tanzania na kwamba ingawa kiwango cha kuenea kwa ugonjwa huo ni kikubwa.

  Ambapo watu milioni 150 katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wakitarajiwa kuathiriwa na maradhi hayo ifikapo 2025.Viwango vya uelewa na tiba bado viko chini, hali inayoonyesha ipo haja kwa programu nzima kujielekeza zaidi katika kukuza uelewa na tiba ya shinikizo la damu.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mwandamizi wa Programu ya Healthy Heart Africa ya AstraZeneca, Ashling Mulvaney, amesema wao kama kampuni ya dawa duniani yenye urithi mkubwa wa kisayansi, uboreshaji wa mfumo wa afya imekuwa ndio nguzo yao kubwa.

  Amesema waamini nguvu ya pamoja itakuwa ni silaha kubwa katika mapambano dhidi ya changamoto zinazoikabili sekta ya afya kama magonjwa yasiyoambukiza ambayo sasa ndio chanzo kikubwa cha vifo duniani.

  Ameweka wazi kuwa  lengo la programu ya Healthy Heart Africa nchini Tanzania ni kukuza uwezo wa mfumo wa sekta ya afya kukabiliana na maradhi ya shinikizo la damu miongoni mwa wanawake  wajazito kwa kuimarisha uwezo wa wafanyakazi wa sekta ya afya na kuimarisha mbinu za kuwasaidia akina mama katika wilaya sita.

  "Lengo la mpango huu ni kutoa mafunzo kwa wafanyakazi 350 kuhusu mbinu za kutoa huduma pamoja na kuwapima wafanyikazi 1,800 na  wanawake wajawazito 50,000 katika kipindi cha miaka mitatu kwa kuwashauri wajiunge na matibabu, iwapo itahitajika,"amesema Mulvaney.

  Wakati huo huo Mganga Mkuu wa Shirika la Touch Foundation, Steven Justus, amesema tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004, taasisi hiyo imeelekeza nguvu zake kuboresha sekta ya afya nchini Tanzania.

  "Ubia huu na kampuni ya kimataifa ya AstraZeneca na Serikali ya Tanzania ni fursa pekee ya kuunganisha juhudi za pamoja za mapambano dhidi ya maradhi ya shinikizo la damu kwa wajawazito kwa kuwahusisha wahudumu wa afya ili kuleta mafanikio katika mfumo wa afya na maisha ya watu,"amesema.

  Programu ya Healthy Heart Africa, ambayo ilianzishwa nchini Kenya mwaka 2014, ina lengo la kuwafikia watu milioni 10 wanaokabiliwa na shinikizo la damu barani Afrika katika jitihada za kuliunga mkono Shirika la Afya Duniani (WHO).

  0 0

  KAMPENI ya kitaifa ya kuhamasisha watu binafsi pamoja na walioko kwenye sekta isiyorasmi kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) ya 'zamu yako', imeanza kutoa matokeo chanya baada ya zaidi ya watu elfu 80 kujiunga na mfuko huo hadi sasa.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye kikao na viongozi wa vikundi vya wajasiriliamali na vyama vya ushirika mkoa wa Arusha, Mwenyekiti  wa kamati ya kuratibisha sera ya hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi, Maryam Muhaji alisema kampeni hiyo ilianza Juni mosi mwaka huu katika Jiji la Dar es salaam.

  Alisema  tangu kuanza kwa kampeni hiyo iliyoanzia katika mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Kagera, Mara na Arusha, tayari wanachama elfu 80 wamejiunga na mfuko wa NSSF na wameanza kupata huduma.

  “Hii kampeni ya ‘Zamu Yako’ ni kampeni maalum ya kuhamasisha watu walioko katika sekta isiyo rasmi kujiunga na mfuko wa NSSF kwa kuwa katiba inamtaka kila mwananchi kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii ni haki yake, hivyo baada ya kugawanywa kwa mifuko hii tumeanzisha kampeni hiui ili kutoa fursa kwa watu wote,”alisema.

  Alisema  kwa kuwa lengo la Serikali ni kuwafikia wananchi wenye kipato cha chini kuweza kupata huduma muhimu, mfuko wa NSSF utaendelea na kampeni hiyo katika mikoa mbalimbali nchini na imepanga hadi kufikia Juni 2019 iwe imeshaandikisha wanachama laki 3.

  Maryam alisema wanachama wanapaswa kujiunga na mfuko wa NSSF na kufaidika na mafao saba ya muda mrefu na muda mfupi yanayotolewa na mfuko huo ikiwemo pensheni, uzee, afya, uzazi, mazishi na kuumia kazini.

  “Kwa kuanzia mtu anayetaka kujiunga na mfuko wa NSSF anapaswa kuchangia kiasi cha Tsh 20,000 kila mwezi ambapo pesa hiyo itamwezesha kupata huduma mbalimbali, kiwango hiki ni kidogo kulinganisha na huduma ambayo mwanachama ataipata, na hata atakapostaafu atapata mafao yatakayomwezesha kuendelea kuishi bila wasiwasi,”alisema.

  Akifungua kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo aliwaagiza viongozi wote wa Wilaya ikiwemo maafisa ushirika kutambua vikundi vyote vilivyopo katika maeneo yao na kuviwasilisha katika ofisi za NSSF ili viweze kufikiwa na kuunganishwa na mfuko huo.

  Kwa upande wake Meneja wa Saccos ya Kimandolu Utu Family, Charles Isaya aliipongeza NSSF kwa kuanzisha mpango huo wa kuandikisha wanachama kutoka sekta isiyorasmi na kudai kuwa atahakikisha wanachama wenzake wote wanajiunga ili kunufaika na huduma hiyo.

  Hadi hivi sasa mfuko wa hifadhi ya jamii wa NSSF una wanachama laki2, wakati takwimu za serikali zinaonyesha kuwa sekta isiyorasmi ina zaidi ya watu milioni 18 ambao hawajajiunga na mfuko wowote wa hifadhi ya jamii jambo ambalo limekuwa likiwakosesha fursa mbalimbali za kupata mafao.
  Mwenyekiti wa kamati ya kuratibisha sera ya hifadhi ya jamii katika sekta isiyorasmi  kupitia mfuko wa NSSF, Maryam Muhaji akizungumza na viongozi wa vikundi vya ujasiriamali na saccos mkoa wa Arusha katika ukumbi wa NSSF Arusha kuhamasisha kujiunga na mfuko huo.
  Washiriki wa kikao cha semina kwa viongozi wa vikundi vya wajasiriamali na  vyama vya  ushirika mkoa wa Arusha wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati ya kuratibisha sera ya hifadhi ya jamii katika sekta isiyorasmi kupitia mfuko wa NSSF Maryam Muhaji (hayuko pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao hicho.

  0 0

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  wa nne kulia akikata utepe kuzindua majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) uliofanyika leo jijini Dodoma na wanne kutoka kushoto ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu. 
  aziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  wa Tatu kulia akizindua majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) uliofanyika leo jijini Dodoma, wa pili kulia ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kulia akipokea cheti cha umalizaji wa ujenzi wa majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi kutoka kwa Waziri wa Afya,Maendeleo ya amii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa majengo hayo uliofanyika leo jijini Dodoma.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa mwenye suti ya bluu akikagua baadhi ya sehemu za majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi baada ya kuzindua majengo hayo yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) yaliyozinduliwa leo jijini Dodoma.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kulia akipata ufafanuzi wa kina kutoka kwa Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa majengo majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) uliofanyika leo jijini Dodoma.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi wakati wa uzinduzi wa majengo ya Taasisi hiyo yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) uliofanyika leo jijini Dodoma, wa tatu kutoka kushoto ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
   aadhi ya viongozi na wananchi  wa Mvumi wilayani Chamwino waliojitokeza kumsikiliza na kushuhudia uzinduzi wa Majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) uliofanya na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo jijini Dodoma.PICHA NA WIZARA YA AFYA.   SERIKALI ITAENDELEA KUTOA KIPAUMBELE KWA  WATAALAM WA AFYA
  NA WAMJW-DODOMA

  SERIKALI itaendelea kutoa kipaumbele kwenye sekta ya  afya hususan swala la kuajiri wataalam wa kada mbalimbali za afya nchini kwa kuzingatia maeneo yenye uhaba mkubwa wa watumishi hasa maeneo ya vijijini.

  Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tan
  zania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa kuzindua majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) uliofanyika leo jijini Dodoma.
  Mhe. Majaliwa aliendelea kusema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kutekeleza Malengo Endelevu ya Milenia hususan lengo nambari tatu linalohusu kuboresha afya za watu pamoja na ustawi wao.

  “Miongoni mwa hatua hizo ni kuhakikisha tunashirikiana na wadau wote ili kuongeza idada ya wataalam wa afya nchini kwa kuvijengea uwezo wa kimiundombinu vyuo vya elimu ya afya nchini ili viweze kuongeza udahili na kuzalisha wataalam bora wa afya” alisema Mhe. Majaliwa.

  Aidha, Mhe. Majaliwa aliwataka wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali za kuongeza idadi ya watumishi wa afya nchini watakaotekeleza majukumu yao kwa uadilifu na weredi mkubwa kwani Taifa bora linajengwa na wananchi wenye afya bora na afya bora kwa wananchi itapatikana iwapo watahudumiwa ipasavyo.
  Mbali na hayo Mhe. Majaliwa alisema kuwa nchi bado inakabiliwa na changamoto  ya magonjwa ya Kifua kikuu na Malaria ,hata hivyo Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya afya nchini imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za ugunduzi wa magonjwa hayo kwa kutumia vipimo vya vina saba (gene -expert).

  “Tumefanikiwa kusambaza mashine za “gene expert” 191 kwenye Hospitali zote za Rufaa za Kanda ,Mikoa,Wilaya na baadhi ya vituo vikubwa vya afya ili kuwezeza kupata majibu ya vipimo vya utambuzi wa kifua kikuu ndani ya masaa mawili badala ya kipimo cha hadumini kinachotoa majibu baada ya masaa 24” alisema Mhe. Majaliwa 

  Aidha , Mhe. Majaliwa amewataka wananchi kujikinga na maambukizi ya Malaria kwa kuzuia mazalia ya mbu kupitia usafi wa mazingira wanayoishi na kutumia vyandarua kwa usahihi ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

  Kwa uapnde Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto mhe. Ummy Mwalimu  ametoa shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kutoa kipaumbele kikubwa katika masuala ya afya za Watanzania.

  “Serikali kupitia Wizara yangu itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye sekta ya afya yenye lengo la kuboresha huduma za afya na  vyuo vya kutolea mafunzo ya kada za afya ili kuimarisha afya za wananchi” alisema waziri Ummy.

  Naye Mkurugenzi wa Tume ya Kikristo ya Huduma za jamii Bw. Peter Maduki amesema kuwa mradi wa ukarabati ,upanuzi na ujenzi wa majengo mapya pamoja na vifaa tiba na tahama ulioanza April 2015  katika chuo hicho umegharimu shilingi Bilioni 5.2 ikiwa na malengo ya kuongeza 

  0 0  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kushoto) akipeana mkono na Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia mara baada ya mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro. Kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi.
  Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akipeana mkono na Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo (kulia) mara baada ya kumalizika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro. Katikati ni Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi.
  Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akifurahi jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na ziara yake ya kwanza katika bara la Afrika na Tanzania ikiwa ni nchi yake ya kwanza kutembelea huku wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro.Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani.
  Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na ziara yake ya kwanza katika bara la Afrika na Tanzania ikiwa ni nchi yake ya kwanza kutembelea huku wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani na kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kulia) akiwa ameongozana na Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mkutano na waandishi wa habari kuhusu ujio wa Gwiji huyo wa Liverpool nchini. Wengine katika picha nyuma kutoka kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba, Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo pamoja na Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi.
  Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na ujio wa Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (katikati) uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani 
   

  Sami Hyypia veteran wa timu ya Liverpool yupo nchini kwa mwaliko wa benki ya Standard Chartered. 
  Mchezaji huyo mwenye haiba ya aina yake aliwasili nchini Jumanne, kuhudhuria michuano ya kombe la Standard Chartered inayotarajiwa kuanza jumamosi wiki hii. Akizungumza klatika mkutano na waandishi wa habari Ofisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Bank nchini Tanzania, Bw. Sanjay Rughani, alisema benki yake imefurahjishwa sana na ujio wa mchezaji huyo wa zamani. 

  “Tumefurahi sana kuwa na Sami nchini na kumshirikisha katika michuano ya tatu ya kombe la Standard Chartered . Sami pia atatumia uwepo wake kufanya kazi na timu ya vijana chini ya miaka 17– Serengeti Boys” Sami Hyypia ni mmoja wa viungo hatari ambao walivaa fulana nyekundu wakati wa utawala wa makocha Gerard Houllier na Rafael Benitez na kumfanya kuwa mmoja wa walinzi hodari barani Ulaya. 

  Mchango wa Hyypia katika soka la England kulimfanya atambuliwe kwao (Finland) kwa kupewa tuzo za mwanasoka bora wa mwaka kwa miaka saba. (1999, 2001, 2002, 2003, 2005, 2006 na 2008). Baada ya kusaidia timu yake dhidi ya Sheffield Wednesday hapo Agosti 7, 1999, Hyypia akawa katika mahusiano mazuri ya kisoka na Stephane Henchoz na kuwa na viungo bora wa ulinzi 2000-01. 

  Aidha uchezaji wake na Jamie Carragher ulitengeneza kitu kilichokubalika kuwa ngome thabiti baada ya Liverpool baada ya kutwaa Champions League katika viwanja vya Ataturk. Hyypia ndiye aliyefunga goli la kukumbukwa sana wakati alipofunga goli dhidi ya Juve katika robo fainali. Historia ya soka, alisema mtendaji huyo wa Benki, itamweka katika eneo zuri kabisa la kibiashara mchezaji huyo ambaye wapenzi walimweka katika orodha ya kuwa mtu wa 38 kati ya watu 100 waliofanya vyema katika klabu hiyo. 

  Akiwa nchini pamoja na kufanya kliniki ya soka kwa vijana wa Serengeti Boys atakutana na vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi na wale wenye akaunti katika benki ya Standard Chartered. Sami pia atahudhuria michuano ya Standard Chartered inayoanza Dar es salaam Jumamosi hii. Michuano ya soka ya Standard Chartered hufanyika kwa kila mchezo kutumia dakika 10 na mshindi atapata zawadi ya kwenda Anfield kuiona klabu ya Liverpool. 

  Michuano hii ya tatu nchini Tanzania toka ianzishwe mwaka 2005 itashirikisha timu 32 zinazotokana pia na wateja wa benki hiyo. Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Salum Madadi, katika mkutano huo na waandishi wa habari aliishukuru benki ya Standard Chartered kwa kusaidia kukuza michezo na hasa soka. Naye kocha wa Serengeti Boys, Bw. Oscar Mirambo aliipongeza benki hiyo kwa kumleta Sami Hyypia nchini Tanzania na kusema itakuwa ni fursa nzuri kwa timu ya Serengeti kuwa naye 

  Akizungumza kuhusiana na ziara yake na uzinduzi wa michuano hiyo akishirikiana na Waziri wa Habari, Sanaa, Wasanii na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, gwiji huyo wa Liverpool, Hyypia alisema kuwa amefurahi kuhudhuria mashindano hayo na kufika kwa mara ya kwanza nchini huku akitoa wito kwa wachezaji wenye vipaji wa Afrika pamoja na Tanzania kujitahidi ili kupata fursa ya kucheza soka la kulipwa nchini Uingereza na nchi nyingine. 

  Hyypia amesema kuwa kwa sasa kuna wachezaji wengi wenye vipaji ambao wanatamba Uingereza kutokana na kuongeza bidii. Amesema kuwa tokea enzi ya Tony Yeboah ambaye alicheza naye, kwa sasa kuna wachezaji kama Sadio Mane, Mohamed Salah na wengine wengi wanaotamba katika ligi mbalimbali barani Ulaya na mabara mengine. 

  Amesema kuwa atafanya mazungumzo na Shirikisho la Kandanda nchini (TFF) kupitia benki ya Standard Chartered ili kuona namna ya kuwawezesha wachezaji wa Tanzania kucheza soka nchini Uiengereza na nchi nyingine kama Finland. 

  “Kwa sasa nipo nchini na bahati nimekutana na viongozi wa TFF hasa kocha wa Serengeti Boys, Oscar Mirambo na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi, pia nitakutana na Waziri wa Michezo, nini kitafanyika, naomba msubiri,” alisema Hyypia.
   

  0 0

  Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakzi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, (kushoto), akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa waajri jijini Tanga kuhusu wajibu wa waajiri kufanya tathmini mara kwa mara ya viwango hatarishi mahala pa kazi.

  WAAJIRI wanao wajibu wa kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wao unapewa umuhimu wa kwanza na moja ya njia ya kutekelza hilo ni kufanya tathmni ya viwango hatarishi mara kwa mara.
  Hayo yamesemwa leo Juni 21, 2018 na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Thathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa waajiri jijini Tanga kuhusu wajibu wa waajiri katika kuhakikisha usalama na afya ya mfanyakazi unazingatiwa.
  Lakini pia aliwataka wafanyakazi nao watekeleza wajibu wao kwa kutumia vifaa kinga walivyopewa na waajiri wao pale wanapotekeleza majukumu yao ya kikazi ili kupunguza ajali zinazoweza kuzuilika.
  Alisema ili kutekeleza awajibu huo wa kisheria, wajiri wanapaswa kufanya tathmini ya mara kwa mara ili kubaini vihatarishi mahala pa kazi ili kuchukua hatua ya kuzuia majanga yatokanayo na kazi.
  “Ifahamike kuwa sisi WCF wajibu wetu wa msingi ni kulipa fidia stahiki na kwa wakati kwa mfanyakzi aliyeumia, kuugua au kufariki wakati akitekeleza wajibu wake wa kazi, ikiwa ni pamoja na kusajili na kupokea michango kutoka kwa waajiri walio katika sekta ya umma na binafsi Tanzania Bara, lakini pia tunalo jukumu la kisheria la kukuza mbinu za kuzuia ajali na vifo kazini kwa kutoa elimu kwa waajiri lakini pia wafanyakazi wenyewe na hiki ndicho tunachokifanya hapa leo.” Alisema Dkt. Omary amabaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba.
  Katika kuhakikisha wadau wanapata uelewa wa kutosha kuhusu majukumu ya Mfuko na wajibu wao katika kutekeleza sheria iliyoanzisha Mfuko, tumekuwa tukikutana na waajiri na kuwapa elimu kupitia semina kama hii ya leo, lakini pia tumekuwa tukitembelea maeneo ya kazi na kwa kushirikiana na waajiri wenyewe tumekuwa tukitoa elimu kwa wafanyakazi pia, alisema Mkurugenzi huyo wa hudumaz a Tiba na Tathmini.
  “Na kwa hakika kumekuwepo na kukua kwa uelewa miongoni mwa waajiri, kuhusu shughuli za Mfuko, awali waajiri walidhani Mfuko kazi yake ni kusajili na kukusanya michango tu, lakini kupitia elimu hii tunayotoa kuhusu shughuli za Mfuko, kumekuwepo na mabadiliko makubwa, tumekuwa tukipokea maombi mengi kutoka kwa waajiri wakitaka tutembelee maeneo yao ya kazi, ili kutoa elimu hii kwa wafanyakazi pia, jambo ambalo hapo awaali wakati tunaanza halikuwepo na hakika kwetu sisi haya ni mafanikio.”
  Dkt. Omary alisema, kwa sasa Mfuko umekuwa ukitekeleza majukumu yake kwa mafanikio makubwa ambapo zaidi ya waajiri 14,224 wamesajiliwa na wengine wapya wanaendelea kujisajili.
  Mafaniukio mengine yaliyopatikana katika kipoindi kifupi, Mfuko umeweza kutekeleza jukumu lake la msingi la kulipa fidia satahiki na kwa wakati kwa wafanyakazi walioumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi kwa mafanikio makubwa.
  “Pamoja na uchanga wake, Mfuko umeshalipa fidia  kiasi cha shilingi bilioni 2.52 kwa wafanyakazi walioumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi, haya ni mafanikio makubwa ambayo Mfuko umeyapata katika kipindi kifupi”.
  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ni taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoanzishwa kwa mujibu kifungu namba 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura ya 263 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2015, lengo kuu likiwa ni kulipa fidia stahiki na kwa wakati lakini pia kusajili na kukusanya michango kutoka kwa waajiri walio katika sekta ya umma na binafsi Tanzania Bara.
  Mfuko ulianzishwa mnamo mwaka 2015 na Serikali ilitoa kipindi cha mpito cha mwaka mmoja ili kujiweka sawa na ilipofika Julai 2016 tulianza  kupokea madai ya fidia.
   Washiriki wakiendelea kuchukua nafasi zao.
   Baadhi ya washiriki wakisoma majarida ya WCF yenye maelezo mbalimbali kuhusu shughuli za Mfuko.


   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa WCF, Bi. Laura Kunenge, (katikati), Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi (kushoto) na Afisa Matekelezo wa Mfuko huo, Bw. George Faustine wakipitia taarifa mwanzoni mwa mafunzo hayo.
   Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa WCF, Bi. Laura Kunenge, akiongoza mafunzo hayo.

   Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakzi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, (kulia aliyesimama), akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa waajri jijini Tanga kuhusu wajibu wa waajiri kufanya tathmini mara kwa mara ya viwango hatarishi mahala pa kazi.
   Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakzi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, (kushoto aliyesimama), akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa waajri jijini Tanga kuhusu wajibu wa waajiri kufanya tathmini mara kwa mara ya viwango hatarishi mahala pa kazi.
   Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakzi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, (kulia aliyesimama), akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa waajri jijini Tanga kuhusu wajibu wa waajiri kufanya tathmini mara kwa mara ya viwango hatarishi mahala pa kazi. wengine pichani meza meza kuu ni, Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi (kushoto) na Afisa Matekelezo wa Mfuko huo, Bw. George Faustine
   Afisa Matekelezo wa Mfuko huo, Bw. George Faustine, akizungumza.
   Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.
   Picha ya kwzna ya pamoja.
  Picha ya pamoja ya pili.
  Mshiriki (kulia), akipatiwa vipeperushi na vifaa vingine wezeshi vya mafunzo.
  Mshiriki akijiandikisha.

  0 0


  Na Jumia Travel Tanzania

  Jumia Travel ilibahatika kuhudhuria maonyesho ya utalii ya KARIBU KILIFAIR 2018 yaliyofanyika kuanzia Juni 1 mpaka Juni 3 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.


  Haya ni miongoni mwa maonyesho makubwa ya Utalii katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na Kati ambapo zaidi ya washiriki 350 walishiriki kuonyesha bidhaa na huduma zao, zaidi ya mawakala 300 wa ndani na kimataifa walikaribishwa, pamoja na takribani wageni 4000 walihudhuria ndani ya siku tatu za maonyesho.
  Ni dhahiri kwamba kuendelea kufanyika kwa maonyesho haya kila mwaka kunazidi kukuza vivutio vya kitalii na watalii kwa ujumla nchini. Tanzania imebarikiwa na vivutio lukuki vya kitalii kwa upande wa nyanda za Kaskazini vikiwemo Mlima Kilimanjaro (mlima mrefu zaidi barani Afrika) na Hifadhi za Kitaifa za Mbuga za Wanyama (Arusha, Mkomazi, Ziwa Manyara, Serengeti, na Tarangire). 

  Kufanyika kwa maonyesho kadhaa ya kitalii katika ukanda huo hususani Kilimanjaro na Arusha kumesaidia kwa kiasi kikubwa kuvitangaza vivutio vilivyopo maeneo yale, kukuza uwekezaji katika sekta mbalimbali pamoja na kuneemesha wananchi kwa ujumla. 

  Licha ya kuwepo kwa vivutio vya kitalii pia miundombinu katika mikoa ya Kaskazini ni rafiki kwa watalii kufika kwa urahisi. Ukiachana na uwepo wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro ambao ndio kiungo kikuu cha watalii wanaofikia jijini Dar es Salaam na nchi jirani lakini pia kuna barabara nzuri za lami, hoteli nyingi zinazokidhi viwango vya kitalii, mawakala wa shughuli za kitalii pamoja na hali ya hewa nzuri inayowapendeza watalii wa aina mbalimbali.
  Umeshawahi kujiuliza ingekuwaje endepo kila ukanda nchini Tanzania ungekuwa na onyesho angalau moja kwa mwaka? 

  Tanzania inayo mikoa takribani 30 kwa sasa ukijumuisha pamoja na ya Visiwani Zanzibar. Katika upande wa shughuli za kitalii Tanzania bara imegawanywa katika kanda nne ambazo ni Ukanda wa Kaskazini - unaoundwa na Hifadhi za Taifa za Mbuga za Wanyama (Arusha, Mkomazi, Ziwa Manyara, Serengeti, Tarangire na Mlima Kilimanjaro); Ukanda wa Magharibi - unaoundwa na Hifadhi za Taifa za Mbuga za Wanyama (Gombe, Katavi, Mahale, Rubondo na Saanane); Ukanda wa Kusini - unaoundwa na Hifadhi za Taifa za Mbuga za Wanyama (Kitulo, Mikumi, Ruaha na Udzungwa) na Ukanda wa Mashariki - unaoundwa na Hifadhi ya Taifa ya Mbuga ya Wanyama ya Saadani. 

  Tayari Ukanda wa Kaskazini unawakilishwa vema na maoinyesho ya KARIBU KILIFAIR, ambapo kuanzia mwaka huu wametangaza rasmi kuwa yataanza kufanyika kwa kupokezana. Mwaka 2018 yamefanyika Moshi, Kilimanjaro na mwakani 2019 yatafanyika mkoani Arusha.

  Kwa upande wa Ukanda wa Mashariki, kuna maonyesho ya S!TE (Swahili International Tourism Expo) ambayo huandaliwa na Bodi ya Utalii ya Tanzania (TTB) kila mwaka ifikapo mwezi Oktoba. Kwa mwaka huu maonyesho haya yatafanyika kuanzia Oktoba 12 mpaka 14 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Jiji hili ni mashuhuri kwa shughuli za kibiashara nchini Tanzania na kwa asilimia kubwa ndipo shughuli mbalimbali za kiuchumi zinapofanyika na wawekezaji walipo. 
  Kwa upande wa Zanzibar kuna matamasha makubwa mawili ya Sauti za Busara na Zanzibar International Film Festival (ZIFF) ambayo hufanyika kila mwaka. Ingawa matamasha haya hayahusiani na utalii moja kwa moja lakini shughuli za kitalii hutumika kwa asilimia kubwa kuwavutia wahudhuriaji. Uwepo wa fukwe safi, utajiri wa kihistoria na tamaduni, hoteli zenye hadhi ya juu, uwanja wa ndege, usafiri rahisi na nafuu wa maji pamoja na ukaribu wake na Dar es Salaam ni sababu tosha kwa wahudhuriaji na watalii. 

  Kwa mara ya kwanza visiwani humo, mwaka huu yatafanyika Maonyesho ya Utalii ya Zanzibar (Zanzibar Tourism Show) kuanzia Oktoba 17 mpaka 20, yakiwa na lengo ya kutangaza vivutio vilivyopo pamoja na kuvutia wadau kwa ujumla.

  Vipi kwa upande wa kanda za Kusini na Magharibi? 

  Kwa muda mrefu mikoa ya Kusini na Magharibi imekuwa ipo kimya hususani kwenye upande wa maonyesho ya shughuli za kitalii. Licha ya kuwa na vivutio vya kila aina vilivyopo bado kuna jitihada hafifu za kuvitangaza na kuwavutia wadau wengi.Mikoa inayopatikana kwenye kanda hizi mbili imebarikiwa na vivutio vya kipekee ambavyo havipatikani maeneo mengine nchini. Hivyo basi, hivi ni vigezo tosha kwa serikali na wadau wa utalii kutupia jicho maeneo haya ili taifa linufaike na wananchi wa maeneo ya karibu.
  Kwa mfano, yanapofanyika maonyesho kama KILIFAIR wanaonufaika moja kwa moja si wadau wa utalii pekee. Katika msimu wa tamasha hili wafanyabiashara wa mahoteli, migahawa, usafiri wa bodaboda na teksi, huduma za kibenki na sehemu za starehe hunufaika kwa kiasi kikubwa kwani huduma zao huwa zinatumika kwa viwango vikubwa.

  Kwa kuhitimisha, utamaduni wa maonyesho kama haya ungesambaa nchi nzima angalau kuwe na onyesho kubwa mara moja kwa mwaka, watalii wa ndani na nje wangejua vivutio vya kila pembe ya Tanzania. Lakini hatutoweza kufanikiwa hilo endapo hatutohamasisha ujengaji wa hoteli za kisasa zinazokidhi vigezo vya kitalii, viwanja bora vya ndege, barabara nzuri za lami pamoja na huduma nyinginezo za jamii kama vile benki, hospitali nakadhalika.

older | 1 | .... | 1603 | 1604 | (Page 1605) | 1606 | 1607 | .... | 1898 | newer