Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

DKT TIZEBA AMALIZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI SINGIDA ATUA TABORA

$
0
0

Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza kwenye kikao kazi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida. Picha Zote Na Mathias Canal, WK. Juzi 8 Juni 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Kushoto) na Mkuu wa Wilya ya Singida Mhe Elias Tarimo wakifatilia kikao cha kazi kilichoongozwa na waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba, Juzi 8 Juni 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza jambo mbele ya waziri wa kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba alipotembelea ofisi ya Mkoa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili, Juzi 8 Juni 2018.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza kwenye kikao kazi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida. Juzi 9 Juni 2018.

Na Mathias Canal-WK, Tabora


Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amemaliza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Singida na tayari amewasili mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku moja hapo kesho 10 Juni 2018.


Akiwa Mkoani Singida Mhe Dkt. Tizeba ametembelea vituo mbalimbali vya ukusanyaji wa pamba na kujionea msimu wa ununuzi wa pamba katika Wilaya ya Ikungi na Iramba.


Miongoni mwa mambo ya msisitizo katika maeneo yote hayo ni pamoja na kuwashauri wakulima kutouza pamba chafu kwa kudhani kuwa watapata kilo nyingi kwani jambo hilo linafifihisha soko la zao hilo kwa wanunuzi.


Katika hatua nyingine ametoa onyo kwa viongozi wa vyama vya ushirika AMKOS kutojihusisha na ubadhilifu wa fedha za wakulima huku akielekeza kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa wale wote waliobainika kuiba fedha za wakulima katika maeneo mbalimbali nchini.


Aidha, ametangaza neema kwa wakulima wa pamba kote nchini kuwa msimu ujao wa kilimo wa mwaka 2018/2019 wakulima watapatiwa mbegu na dawa bure pasina malipo.


Akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Tizeba amewasisitiza watendaji wote mkoani humo kutoa ushirikiano mahususi kwa wakulima ili kuongeza tija katika uzalishaji wa zao la pamba na mazao mengine yakiwemo mahindi, mtama, alizeti N.k


Zao la pamba ni miongoni mwa mazao ya biashara yanayolimwa katika mkoa wa Singida, Katika msimu huu wa mwaka 2017/2018, mkoa ulipokea mbegu bora za pamba aina ya UKM 08 tani 381.48 na kusambazwa kwa wakulima ambapo jumla ya ekari 35,889 zilipandwa. Aidha, sumu chupa 137,970 zimesambazwa kwa wakulima na mabomba ya kunyunyizia sumu 365 yamesambazwa pia.


Pia amesisitiza kuwa uongozi wa mkoa huo unapaswa kujipanga kikamilifu kusimamia ununuzi wa pamba kupitia utaratibu uliowekwa wa kuvitumia Vyama vya Ushirika vya Kilimo na Masoko (AMCOS) pamoja Vyama vya Awali vya Ushirika  (Pre Cooperative Societies).


Katika mkoa huo jumla ya AMCOS 36 na “Pre Cooperatives” 20 zitahusika katika ununuzi wa zao la pamba katika msimu huu wa kilimo wa mwaka 2017/2018.


Akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt Rehema Nchimbi alisema kuwa mkoa huo ulikuwa na matarajio ya awali ya mavuno kwa tani 21,533.4 ambapo matarajio haya yameshuka mpaka kufikia tani 14,015.2 zinazotarajiwa kuvunwa kutokana na athari za wadudu waharibifu.


Alisema jumla ya vituo vitakavyotumika kukusanya na kununua pamba ni 117 ambavyo vimesambaa katika maeneo yote yanayolima pamba yaliyopo katika Halmashauri saba za Mkoa huo.


Aliongeza kuwa maghala yatakayotumika kununulia pamba katika vituo hivyo  yamesafishwa na kufukiziwa sumu ya kuuwa wadudu. Kampuni iliyoruhusiwa kununua pamba katika Mkoa huo ni BioSustain (T) LTD ambayo ni mdau mkubwa wa kilimo cha zao la pamba katika mkoa wa Singida kwani imewekeza kiwanda cha kuchambua pamba kilichopo Manispaa ya Singida.

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA DKT MNDOLWA KUUPATIA UFUMBUZI MGOGORO WA MACHIMBO YA DHAHABU MKOANI GEITA

$
0
0


Na Bashir Nkoromo, Geita.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa ameahidi kuupatia ufumbuzi mgogoro wa machimbo ya dhahabu wa Lwamgasa mkoani Geita uliopo kati ya Jumuuya ya Wazazi mkoa wa Geita na Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mwanza.

Mgogoro huo umeibuka tangu Geita ilipomegwa kuwa mkoa, na hivyo leseni ya machimbo hayo yaliyopo Geita huhodhiwa na Jumuiya Wazazi Mwanza huku machimbo yenyewe yakiwa kwenye mkoa wa Geita.

Mvutano wa umiliki wa machimbo hayo umekuja kutokana na Jumuuya ya Wazazi Geita kuona kuwa ni rasilimali yake lakini haipati chochote badala yake wanaofaidika nayo ni Mwanza. "Ninayo majembe (viongozi) ambao nikikaa nao tutaumaliza mgogoro huu, na hii ni Geita isiwasumbue sana hasa mkizingatia kuwa mali za jumuia ni mali za Chama". alisema Dk. Mndolwa.

Dk. Mndolwa ambaye alikuwa akizungumza katika kikao cha ndani na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Geita na Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya za Chama kutoka wilaya za mkoa huo alisema, moja ya tatizo ni kwamba rasilimali nyingi za Chama na jumuiya zake kwa sasa nyingi zimo mikononi mwa watu binafsi.

Alisema kwa kuwa CCM imelitafutia ufumbuzi tatizo hilo sasa litakwisha na mali zote zitanilikiwa na Chama kikamilifu na hivyo migogoro mingi kuhusu mali za Chama itapungua au kuisha kabisa .Dk. Mndolwa alisema yeye pamoja na safu ya uongozi wake watahakikisha Jumuiya ya Wazazi inakuwa Jumuiya ya mfano zaidi Kwa kuhakikisha rasilimali zake zinakuwa endelevu na hivyo mambo mengi ndani ya Jumuiya hiyo yatakwenda vizuri.

" Jumuiya hii kama ni kipele sasa kimepata mkunaji, nataka niwahakikishie wana CCM wenzangu kwamba sikuja katika Jumuiya hii kuganga njaa, nimekuja kufanya Kazi bila kubabaisha, ninyi wenyewe ni mashahidi tangu uongozi huu mpya mishahara inawahi na mambo mengi ikiwemo bima ya afya Kwa watumishi wetu tumehakikisha tunasimamia vilivyo" Aliseama

Dk. Mndolwa alisema Tanzania chini ya Rais Dk Magufuli had I kufikia 2023 itakuwa imeingia katika hadhi ya uchumi wa kati

Dk Mndolwa yupo katika ziara ya mikoa ya Kagera, Geita, Mara, Simiyu na Singida kushukuru Kwa kuchaguliwa na pia kuwatambulisha Makamu wake upande wa Zanzibar Haidar Haji Abdallah na Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Wazazi Erasto Sima ambao ameambatana nao kwenye ziara hiyo.

DTB BENKI YAFUTURISHA WATEJA WAO MKOANI TANGA

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Tanga ,Martine Shigella akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na Benki ya DTB kwa waislama mkoani Tanga iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort.
Shehe wa mkoa wa Tanga Juma Luwuchu akizungumza katika Futari hiyo

Meneja wa Benki ya DTB Mkoa wa Tanga Athumani Juhudi akizungumza katika futari hyo
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza katika futari hiyo
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto akiteta jambo na Meneja wa Benki ya DTB Juhudi Athumani wakati wa futari hiyo
Wakiteta jambo
Mkuu wa Mkoa wa Tanga akipokea zawadi kutoka kwa Benki ya DTB mara baada ya kumalizika kwa futar hiyo
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akiagana na Meneja wa Hotel ya Tanga Beach Resort Joseph Ngoyo mara baada ya kumalizika kwa futari iliyoandaliwa na Benki ya DTB Benki
Sehemu ya waumini wa dini ya kiislamu wakipata wakipata futari
Sehemu ya waumini wa dini hya kiislama wakiwa kwenye futari hiyo
Sehemu ya waumini wa dini ya kiislama wakipata futari iliyoandaliwa na Benki ya DTB
Mkuu wa mkoa wa Tanga akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wengine baada ya kumalizika kwa futari hiyo


WATANZANIA TUSIKUBALI KUCHONGANISHWA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wasikubali kuchonganishwa na kwamba Serikali haiongozwi kwa misingi ya kidini bali imeziachia taasisi za kidini zifanye kazi kwa kuzingatia Katiba , Sheria za nchi na malengo yaliyokusudiwa katika uanzishwaji wake. 
Aliyasema hayo jana jioni (Jumamosi, Juni 9, 2018) alipozungumza na viongozi na wananchi wa Mkoa wa Mwanza baada ya kushirikiana nao katika futari aliyowaandalia. Shughuli hiyo ilihudhuriwa na waumini wa dini mbalimbali.

Waziri Mkuu alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanaishi kwa amani na utulivu, jambo litakalowawezesha kufanya shughuli zao kikamilifu, hivyo wasikubali kuchonganishwa kwa misingi yoyote.

“Nawaasa viongozi wa dini msikubali kutumia makundi mengine nje ya taasisi zenu kwa ajili ya kuwazungumzia masuala yenu kwa sababu watawachonganisha na Serikali ambayo haipo kwa ajili ya kugombana na taasisi yoyote,” alisisitiza.

Waziri Mkuu alisema jukumu kubwa la taasisi za kidini ni kuhakikisha wanawalinda waumini wao pamoja na kuwaongoza kwa kuwapa mafundisho mema yanayompendeza Mwenyezi Mungu, ambayo yatawawezesha kuishi kwa amani .

Alisema misingi ya amani na utulivu ikiwa pamoja na mshikamano walionao  wananchi umesababisha Tanzania kupata heshima kubwa dunia kote, hivyo ni vema kila mwananchi ahakikishe suala la kudumisha amani linapewa kipaumbele.

Pia Waziri Mkuu  alisema amefurahi sana kujumuika na wananchi wa Mkoa wa Mwanza katika futari hiyo, ambapo aliwapongeza kwa kukamilisha uundaji wa kamani za amani kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. John Mongella amlishukuru Waziri Mkuu kwa ukarimu wake kwa kuwaalika wakazi wa Mwanza katika hafla hiyo, ambapo alisema Mwanza ni kitovu cha amani kwa kanda ya Ziwa na nchi za Maziwa Makuu. T

“Mwanza tumejipanga na tunashirikiana na taasisi zote kwenye njanja zote , tupo pamoja na tunashirikiana katika kuimarisha amani na utulivu. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli kwa kutuamini na  tunamuahidi tutafuata falsafa zake katika utendaji wetu,”.

Kwa upande wake, Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza na Askofu wa Kanisa la Charismatic Episcopal Church of Tanzania (CECT), Charles Sekelwa alisema wao wanaiunga mkono Serikali katika kudumisha amani na wataendelea kushirikiana nayo.

Alisema awali kulikuwa na changamoto ya matabaka ya kidini iliyobabisha na kutoelewana baina ya waislamu na wakiristo, ambapo kamati yao ilifanya kazi ya kuyasulisha na sasa hali ni shwari. “Matabaka ya kiimani yameisha na watu wa dini zote wanashirikiana vizuri,”.

Askofu Sekelwa alisema wao kama viongozi wa pande hizo mbili hawawezi  kukubali kuona kunakuwa na matabaka ya kiimani miongoni mwa waumini, hivyo watakikisha wanaendelea kuwafundisha waumini wao umuhimu wa amani.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Akson, Naibu Waziri waNchi, OR – TAMISEMI, Joseph Kakunda, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali baadhi ya wananchi wa mkoa wa Mwanza

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JUNI 10, 2018.

JAFO AZITAKA TAASISI ZA SERIKALI ZINAZOJISHUGHULISHA NA UJENZI KUWA KINARA WA UBORA KWENYE KAZI.

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Selemani Jafo amezitaka Taasisi za serikali zinazo shughulika na masuala ya ujenzi kuwa kinara kwa ubora wa kazi zinazotekelezwa na taasisi hizo.

 Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa akikagua ujenzi wa jengo la halmashauri ya Makambako mkoani Njombe linalo jengwa na kampuni ya  MZINGA CORPORATION.

Katika ukaguzi huo, jafo ameagiza kazi hiyo ifanyike kwa ubora wa hali ya juu ili kuliwezesha jengo hilo kudumu kwa miaka mingi. 

Waziri Jafo kabla ya kukagua ujenzi huo amepata fursa ya kutembelea shule ya sekondari Makambako ambapo serikali imetoa sh.Million 150 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili. 

Akiwa katika shule hiyo, Waziri Jafo amefurahishwa na kazi iliyofanywa na halmashauri kupitia kamati ya ujenzi ya shule ambapo mabweni hayo mawili yamekamilika kwa kutumia "Force account'.

Aidha Waziri Jafo amempongeza Mbunge wa Makambako Deo Sanga kwa jitihada kubwa anayo ifanya kuwaletea maendeleo wananchi wake wa Makambako.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Jimbo la Makambako Deo Sanga pamoja na viongozi wengine wakiwa katika ukaguzi wa ofisi za halmashauri ya mji wa makambako.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo  akiwapongeza viongozi wa Mji wa Makambako kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa mabweni ya wasichana katika sekondari ya makambako.
 Majengo ya halmashauri ya mji wa makambako yanayo endelea kujengwa.
Mbunge wa Jimbo la Makambako Mhe. Deo Sanga pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Jombe.  Mhe. Lucy Msafiri wakifurahia jambo wakati wa Ziara ya waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo Jimboni humo.

ELIMU BORA KUIWEZESHA TANZANIA KUPIGA HATUA YA UCHUMI WA VIWANDA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge (wa pili kushoto) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kulia) , wakiwasili katika viwanja vya Shule ye Sekondari Amani Abeid Karume, iliyoko Kata ya Pahi, Wilayani Kondoa, mkoani Dodoma, kushiriki tukio la uzinduzi wa Kambi ya masomo ya wanafunzi 442 wa Kidato cha Pili na cha Nne kutoka shule za sekondari 23 za wilaya ya Kondoa, wanaojiandaa na mitihani yao ya kitaifa.
Wanafunzi 442 wa shule za Sekondari katika wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, walioshika nafasi ya kwanza hadi ya kumi katika shule zao, wakiwa katika kambi katika Shule ye Sekondari Amani Abeid Karume, iliyoko kata ya Pahi, Wilayani Kondoa, kujiandaa na mitihani yao ya kitaifa ikiwa ni mkakati wa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji wa kuinua kiwango cha ufaulu na elimu wilayani humo ambapo mfuko wake wa Jimbo umetumia zaidi ya shilingi milioni 90 kufanikisha makambi hayo katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
Baadhi ya wanafunzi wa kike wa Kidato cha Pili na cha Nne wa shule za Sekondari katika wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, walioshika nafasi ya kwanza hadi ya kumi katika shule zao wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge, akizungumza kabla ya kuzindua rasmi ya kambi ya masomo katika Shule ye Sekondari Amani Abeid Karume, iliyoko kata ya Pahi, Wilayani Kondoa, kujiandaa na mitihani yao ya kitaifa.
Baadhi ya wanafunzi wa kike wa Kidato cha Pili na cha Nne wa shule za Sekondari katika wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, walioshika nafasi ya kwanza hadi ya kumi katika shule zao wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge, akizungumza kabla ya kuzindua rasmi ya kambi ya masomo katika Shule ye Sekondari Amani Abeid Karume, iliyoko kata ya Pahi, Wilayani Kondoa, kujiandaa na mitihani yao ya kitaifa.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Bi. Sezaria Makota, akielezea namna wilaya yake ilivyopiga hatua kubwa kielimu kufuatia hatua ya Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, kuwekeza zaidi ya shilingi milioni 90 za Mfuko wa Jimbo katika Sekta ya Elimu kwa kipindi cha miaka mitatu.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akielezea namna Serikali ya Awamu ya Tano ilivyojipanga kuboresha elimu nchini baada ya kuamua kutoa elimu bure kuanzia shule za msingi hadi sekondari na uamuazi wake wa kutumia zaidi ya asilimia 80 ya Mfuko wake wa Jimbo kuwekeza katika elimu kwa kuwa ndicho kipaumbele chake cha kwanza.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akielezea namna Serikali ya Awamu ya Tano ilivyojipanga kuboresha elimu nchini baada ya kuamua kutoa elimu bure kuanzia shule za msingi hadi sekondari na uamuazi wake wa kutumia zaidi ya asilimia 80 ya Mfuko wake wa Jimbo kuwekeza katika elimu kwa kuwa ndicho kipaumbele chake cha kwanza.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge (wa sita kushoto), Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (Mb), Dkt. Ashatu Kijaji (wa tano kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Kondoa Bi. Sezaria Makota (wa tano kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wa Sekondari waliojitolea kuwafundisha wanafunzi 442 wanaoshiriki kambi maalumu kwa ajili ya kujiandaa na mitahani yao ya kitaifa, katika shule ya Sekondari Amani Abeid Karume, iliyoko Kata ya Pahi, Wilayani Kondoa mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa, mkoani Dodoma, Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Bi. Sezaria Makota, wakipongezana baada ya kufanikisha uzinduzi wa kambi maalumu ya wanafunzi wa kitado cha Pili na cha Nne kutoka shule 23 za Sekondari wilayani Kondoa, mkoani humo, mpango uliofanikisha kuongeza kiwango cha ufaulu wilayani humo.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)


Benny Mwaipaja, WFM, Kondoa

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa uwekezaji katika elimu bora kwa vijana wa kike na wa kiume kutaiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati wa viwanda hata kabla ya mwaka 2025.

Dokta Kijaji ameyasema hayo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma, wakati wa uzinduzi wa kambi inayowahusisha wanafunzi 260 wa kidato cha pili na cha nne kutoka shule 23 za Sekondari wilayani humo wanaopatiwa mafunzo ya kina ili kujiandaa na mitihani yao.

Kambi hiyo inafanyika kwa mwaka wa tatu mfululizo ambapo kiasi cha shilingi milioni 90 za mfuko wa Jimbo la Kondoa zimetumika na kuiwezesha wilaya hiyo kupanda daraja kielimu kutoka nafasi za mwisho kitaifa hadi kufikia nafasi za juu kabisa.

“Athari chanya ambayo ninataka kuiacha Kondoa ni elimu bora kwa vijana wetu inayokwenda sambamba na uamuzi wa Mhe. Rais wetu Dkt. Jihn Magufuli, wa kutoa elimu ya msingi na Sekondari bure kwa wanafunzi hivyo kuongeza thamani ya uamuzi huo wa Serikali” Alisema Dkt. Kijaji

Alisema kuwa baada ya hatua ya Halmashauri ya wilaya hiyo kutoa mtihani wa aina moja wa majaribio kwa shule za msingi na kuonesha mafanikio makubwa, hatua hiyo sasa itaelekezwa kwenye elimu ya Sekondari ili kuwapima vyema wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani yao ya kitaifa.

Akizungumza kabla ya kuzindua kambi hiyo ya siku 25, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge, amesema kuwa taifa lenye wasomi waliobobea katika nyanja mbalimbali wataisaidia nchi kukabiliana na mikataba mibovu inayo pora rasilimali za nchi.

Aliwataka wanafunzi hao kutumia vizuri fursa waliyoipata kwa kusoma kwa bidii na maarifa ili waje kulitumikia taifa ili liweze kufikia maendeleo ya haraka kwa kuhakikisha kuwa wanalinda kwa nguvu zao zote rasilimali hizo za Taifa yakiwemo madini, gesi na mazingira.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Bi. Sezaria Makota, amempongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Dkt. Ashatu Kijaji, kwa kusimamia kidete suala la elimu ya watoto wa wilaya yake kupitia mfuko wa jimbo, hatua iliyoifanya wilaya hiyo kupata tuzo mbalimbali za ubora wa elimu katika kipindi cha miaka mitatu

Makamu wa Rais ashiriki ibada ya kumuweka Wakfu na kumuingiza kazini Askofu Mteule Mch. Dkt. Isaac Kissiri Laiser wa KKKT mkoani Tabora

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa Dini nchini kuunga mkono azma ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda.

Makamu wa Rais ameyasema haya wakati wa Ibada ya Kuzindua Dayosisi ya Magharibi Kati na Kumuweka Wakfu na Kumuingiza kazini Askofu Mteule Mchungaji Dkt. Isaac Kissiri Laiser na kuingizwa kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Newton John Maganga katika Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri Tabora. Makamu wa Rais amesema hivi karibuni Serikali imepitisha mabadiliko na mpango mpya wa uwekezaji Tanzania.

Makamu wa Rais amesema kuwa kudumisha Amani na usalama ni jukumu la wote “ Endeleeni kuhubiri Amani na kwa upande wa Serikali niwahakikishie Watanzania Wote kwamba Amani na Usalama ni kipaumbele chetu hatuta vumilia kumstahimilia mtu yeyote yule ambaye ana lengo la kuharibu Amani ya Tanzania hatutamvumilia tutamshughulikia ipasavyo”

Makamu wa Rais amesema “Tukosoeni pale tunapokosea nasi tunawaahidi tutarekebisha na twende mbele kwani Mwalimu Nyerere alituambia kuongoza nikuonyesha njia na katika kuonyesha njia lazima ukubali kukosolewa nasi tunakubali kukosolewa hilo nalo ni jukumu la utumishi wa kiroho kwa hiyo endeleeni kutukosoa kwa ile lugha ambayo tutafahamiana”

Makamu wa Rais amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Taasisi za dini katika masuala ya maendeleo na kuboresha huduma za kijamii. Makamu wa Rais amelishukuru na kulipongeza Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kwa mchango wake mkubwa unatoa katika nchi yetu hususani katika Nyanja za Elimu, Huduma za Afya na Maji.

Nae Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Baba Askofu Fredrick Shoo alisema kuwa wameona jitihada za Mheshimiwa za Rais na wataendelea kumuunga mkono na wapo pamoja kushirikiana na Serikali kwa nia njema kabisa. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt. Fredrick Shoo mara baada ya kuwasili kwenye Ibada ya Kuzindua Dayosisi ya Magharibi Kati na kumuweka Wakfu na kumuingiza kazini Askofu Mteule Mch. Dkt. Isaac Kissiri Laiser na kuingizwa kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mch. Newton John Maganga, mkoani Tabora leo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt. Fredrick Shoo mara baada ya kuwasili kwenye Ibada ya Kuzindua Dayosisi ya Magharibi Kati na kumuweka Wakfu na kumuingiza kazini Askofu Mteule Mch. Dkt. Isaac Kissiri Laiser na kuingizwa kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mch. Newton John Maganga, mkoani Tabora leo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais akisalimiana na Askofu Mteule Mchungaji Dkt. Isaac Kissiri Laiser wakati wa ibada ya ya Kuzindua Dayosisi ya Magharibi Kati na Kumuweka Wakfu na Kumuingiza kazini katika Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri Tabora
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kamba kama ishara ya zawadi ya ng'ombe wa maziwa kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Baba Askofu Fredrick Shoo wakati wa Ibada ya Kuzindua Dayosisi ya Magharibi Kati na Kumuweka Wakfu na Kumuingiza kazini Askofu Mteule Mchungaji Dkt. Isaac Kissiri Laiser na kuingizwa kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Newton John Maganga katika Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Maaskofu wote kutoka Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania mara baada ya kumalizika kwa Ibada ya Kuzindua Dayosisi ya Magharibi Kati na Kumuweka Wakfu na Kumuingiza kazini Askofu Mteule Mchungaji Dkt. Isaac Kissiri Laiser na kuingizwa kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Newton John Maganga katika Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri Tabora

 

WAZIRI WA KILIMO AAGIZA KURUDIWA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA USHIRIKA KILA MAHALI PENYE DOSARI WILAYANI IKUNGI

$
0
0

Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza jambo kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mkunguakihendo kilichopo katika kata ya Kikio, Wilaya ya Ikungi wakati wa ziara ya kukagua vituo vya ununuzi na ukusanyaji wa pamba Mkoani Singida, Jana 8 juni 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-WK
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akishuhudia ununuzi na ukusanyaji wa pamba baada ya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mkunguakihendo kilichopo katika kata ya Kikio, Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Jana 8 juni 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mkunguakihendo kilichopo katika kata ya Kikio kabla ya kumkaribisha Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba , Jana 8 juni 2018.
Waziri wa kilimo akijadili jambo na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani Singida.
Baadhi ya wananchi wakifatilia mkutano wa hadhara




Na Mathias Canal-WK, Singida

Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amemuagiza Afisa ushirika wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Ndg Gurisha Msemo kufanya ziara ya kikazi maeneo yote kuliko fanyika uchaguzi wa viongozi wa vyama vya ushirika ili kubaini uhalali wa uwepo wao.

Mhe Tizeba ametoa kauli hiyo mara baada ya wakazi wa Kijiji cha Mkunguakihendo na Misughaa Wilayani Ikungi kuonyesha kutotambua namna walivyochaguliwa viongozi waliopo madarakani kukiongoza chama hicho katika ngazi mbalimbali jambo ambalo lina ashiria kupatikana kwa viongozi hao kinyume na utaratibu.


Dkt Tizeba ameyasema hayo jana 8 Juni 2018 wakati akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara katika vijiji hivyo ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Singida.“Pamoja na maelekezo yangu ya kutazamwa mahali penye matatizo na kufanyika upya uchaguzi lakini pia nawasihi pindi utakapofanyika uchaguzi mchague viongozi waadilifu ambao watawasimamia katika kweli na haki”

“Kwa muda mrefu sana kwenye vyama vya ushirika karibu nchi nzima watu walikuwa wanagawana vyeo badala ya kuchagua viongozi bora kwa maslahi ya wananchi, lakini katika kipindi hiki tumedhamiria kwa dhati kabisa kuwa na haki katika upatikanaji wa viongozi wa chama chenu” Alikaririwa Mhe Tizeba

Sambamba na agizo hilo pia amewasihi viongozi mbalimbali wa vyama vya ushirika kote nchini kutojihusisha na wizi wa fedha za wananchi kwani kufanya hivyo sio kosa la wizi pekee bali ni kosa la uhujumu uchumi.Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi katika mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amewasihi maafisa ugani kuongeza ufanisi katika usimamizi kwenye kilimo ili kuongeza tija itakayopelekea kuwa na mavuno mazuri yenye manufaa makubwa kwa wakulima.

Aliwaomba wataalamu wa utafiti kote nchini kupitia upya katika maeneo mbalimbali nchini ili kubaini dawa bora za kuua wadudu wanaoathiri mazao mbalimbali likiwemo zao la pamba.

DK. MNDOLWA AUNGURUMA JIJINI MWANZA, LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akizungumza na viongozi wa CCM na wa Jumuiya hiyo mkoani Mwanza, katika mkutano uliofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Erasto Sima, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Dk. Anthony Diallo na kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mwanza Cornel Magembe na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania upande wa Zanziar Haidar Haji Abdallah. 
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania upande wa Zanzibar Haidar Haji Abdallah akizungumza wakati wa mkutano huo. 

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Erasto Sima akizungumza wakati wa mkutano huo. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Cornel Magembe akizungumza kwenye mkutano huo. 
Malenga Omari Kupnda kutoka Nyamagana, akighani shairi wakati wa kikao hicho. 
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Christina Joram akizungumza, alioopewa nafasi ya kusakimia kwenye kikao hicho. 

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania na Mjumbe wa Kamati ndogo ya Uchumi, fedha na Uwekezaji wa Jumuiya hiyo Dk. John Palangyo akisalimia baada ya jutambulishwa kwenye kikao hicho.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ambaye alikuwa mjumbe katika Kamati ya kuhakiki mali za Chama Ndugu Sitwala akizungumza baada ya kutambulishwa kwenye kikao hicho. 

"Nashangaa CCM kila niendapo naikuta..." Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akiiongoza kuimba wimbo wenye maneno hayo, kabla ya kuzungumza na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake katika kikao hicho. 
Baadhi ya viongozi na watumishi wa Jumuiya ya Wazazi wakiwa kwenye kikao hicho. 
Baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho. 




Baadhi ya viongozi na watumishi wa Jumuiya ya Wazazi wakiwa kwenye kikao hicho. 
Baadhi ya viongozi na watumishi wa Jumuiya ya Wazazi wakiwa kwenye kikao hicho. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akiagana na Katibu wa Jumuiya hiyo mkoa wa Mwanza, Adam Soud kabla ya kuondoka Mwanza kwenda mkoani Mara baada ya kikao hicho .
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mwanza Cornel Magembe akimuonyesha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Edmund Mndolwa kiwanja cha Jumuiya hiyo kilichopo eneo la Nyamagana, Dk. Mndolwa alipokagua kiwanja hicho, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza, leo. Wapili kusho ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania upande wa Zanzibar Haidar Haji Abdallah na watatu ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoa wa Mwanza Dk. Anthony Diallo. (Picha zote na Bashir Nkoromo).

TANESCO MANYARA KUWACHUKULIA HATUA KALI WALE WOTE WANAOHUJUMU MIUNDOMBINU

$
0
0
Maneja wa Tanesco mkoa wa Manyara Gerson Manase akiongea na waandishi wa habari hawapo kwenye picha hivi karibuni katika kampeni ya kuhamasisha wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu karibu na miundombinu ya shirika hilo. 

 Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Manyara limewatahadharisha wakazi wanaoendelea kufanya shughuli za kibinadamu karibu na miundombinu ya shirika hilo na kusema kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Tahadhari hiyo imetolewa na meneja wa Tanesco mkoa huo hivi karibuni, Gerson Manase kupitia kampeni maalumu inayofanywa na Tanesco makao makuu ikiwa na lengo la kuhamasisha juu ya athari za kuhujumu miundombinu ya shirika na kufanya shughuli karibu. 

 “Kuanzia sasa mkazi yoyote atakaye kiuka sheria na kufanya shughuli za kibinadamu karibu na miundombinu ya umeme, tutafyeka mazao yake yote na hatua nyingine za kisheria zitafuata,” alisema meneja huyo Kwa sasa Tanesco Manyara inahudumia wilaya tatu ikiwemo Babati, Mbulu na Kateshi ambapo kuna wateja wapatao 28,000 na lengo ni kuongeza idadi zaidi. Mitambo iliyosimikwa ina uwezo wa kuzalisha megawati 50 ila kwa sasa matumizi ni megawati 15 tu na kukaribisha wawekezaji kwani umeme upo wa kutosha. Alisema wakazi hao walishalipwa fidia zao na shirika ili kupisha maeneo hayo ambayo ni hatarishi kwa maisha yao lakini kuna baadhi bado wanafanya shughuli za kilimo. 

Aidha, alisema katika maeneo hayo kuna vyombo vya moto huwa vinatakiwa kupita kwa ajili ya ukaguzi wa miundombinu sasa wakati mwingine inashindikana kutokana na watu kupanda mazao katika njia hizo, matokeo yake kazi zinashindwa kufanyika kwa wakati. Meneja alisema, “Tunatoa wito kwa wakazi wote waheshimu sharia kwani tulishaandika barua kwa wenyeviti wa vijiji kuhusiana na amza yetu. Lengo la shirika sio kumkomoa mtu ila na kuhakikisha maisha ya watu yanakuwa salama na umeme unapatikana kwa wakati,” Katika hatua nyingine meneja huyo aliomba wakazi kuachana na tabia ya kuhujumu miundombinu hiyo na kuongeza mkoa huo umekithiri kwa wizi wa nyaya za umeme. 

 Alisema wizi huo unarudisha jitihada za shirika nyuma na maendeleo kwa ujumla kwani serikali inatumia gharama kubwa kwa ajili ya marekebisho. Akitolea mfano hivi karibuni kuna wizi wa transformer ulitokea na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wateja na shirika kwa ujumla, “Vitendo hivi vinaweza kuleta maafa makubwa, badala ya kuhujumu tunaomba washirikiane na sisi kukomesha wizi huu,” 

Naye Kaimu Meneja Kitengo cha Mawasiliano Tanesco Leila Muhaji alisisitiza kwamba zoezi la uhamasishaji linafanyika nchi nzima lengo ni kutoa elimu ya madhara yanayoweza kupata watu wanaojaribu kuiba vifaa au kufanya shughuli karibu ya miundombinu ya umeme. “Hili ni shirika lenu tunaomba ushirikiano wenu ili kuhakikisha tunakuwa na umeme wa kutosha na kuvutia wawekezaji wengi nchini, serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili ya kufanya marekebisho,” alisema Muhaji.

JAFO AMUAGIZA MKANDARASI KUBOMOA SAKAFU ILIYOJENGWA CHINI YA KIWANGO

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo amemuagiza mkandarasi anayekarabati shule kongwe ya sekondari ya Malangali iliyopo wilayani Mufindi mkoani Iringa kubomoa Sakafu iliyowekwa kwenye madarasani kutokana na kuwa chini ya kiwango.

Hali hiyo imetokea leo wakati Waziri Jafo alipokuwa mkoani Iringa katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo.

Akiwa katika ziara hiyo, Waziri Jafo amefika katika shule hiyo na kukagua moja ya darasa ambalo tayari lilikuwa limekamilika na kubaini kuwa sakafu yake imewekwa chini ya kiwango baada ya kugonga gonga kwa viatu na kutokea nyufa. Kufuatia hali hiyo, Waziri Jafo amemuagiza Mkandarasi huyo kubomoa sakafu hiyo na kuanza kazi upya.

Jafo ameoneshwa kukerwa na hali hiyo na kuagiza msimamizi wa kazi hiyo ambaye ni Wakala wa Majengo nchini(TBA) kuhakikisha sakafu hiyo inavunjwa na kujengwa upya katika ubora unaotakiwa.Shule ya Malangali ni miongoni mwa shule kongwe 89 ambazo serikali imeamua kuzikarabati upya ili zirudi katika ubora wake.

Katika hatua nyingine, Waziri Jafo ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi kwa usimamizi mzuri wa ukarabati kituo cha afya Malangali ambapo majengo yake yamejengwa kwa ubora wa hali ya juu. 

Aidha, Jafo ameitembelea hospitali ya Frelimo iliyopo Manispaa ya Iringa na kujionea changamoto zinazoikabili hospitali hiyo ambazo zimekuwa zikiwasilishwa mara kwa mara bungeni na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Ritta Kabati.

Kutokana na changamoto hizo, Jafo amesema hospitali hiyo inapaswa kupewa kipaumbele kwa upande wa majengo ya Wodi pamoja na jengo la uchunguzi ili iweze kutoa huduma stahiki kwa wagonjwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akifanya ukaguzi wa vyumba vya madarasa katika sekondari kongwe ya Malangali ambapo ameagiza sakafu kufumuliwa kutokana na kutokuwa na ubora.
Viongozi wakifanya Ukaguzi wa miundombinu inayojengwa katika kituo cha afya Malangali
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo na Mbunge wa Viti Maalum Ritta kabati walipo watembelea akina mama waliojifungua katika hospitali ya Frelimo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza, Mbunge Ritta Kabati pamoja na wafanyakazi wa hospitali ya Frelimo

UWEKEZAJI WENYE MTAZAMO ENDELEVU WA BIASHARA UTAFANIKISHA MPANGO WA KUJENGA TANZANIA YA VIWAND

$
0
0
Lisa akiwa (kushoto) akiwa na mwenzake katika mpango wa GMT, Raj Chandarana wakipanda mti wilayani Hai katika mradi wa mazingira wa TBL.
Lisa (wa pili kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake wa TBL baada ya kushiriki katika mradi wa mazingira mkoani Kilimanjaro hivi karibuni “Wakati serikali ya Tanzania inakwenda kasi katika kutekeleza mpango wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda,kunahitajiwa uwekezaji wenye mipango mikubwa ya kuvifanya viwanda vilivyopo na vinavyoanzishwa kuwa endelevu.

Sio tu kuwekeza kwenye fedha na teknolojia bali kunahitajika kuwekeza katika kupata wataalamu wa kuviendesha kwa kipindi cha sasa na miaka ya mbele ili viweze kuwa endelevu”,anasema Lisa Cheche, mhitimu wa Chuo Kikuu ambaye kwa sasa yupo katika programu ya kipekee, ya mafunzo ya kuwandaa wahitimu wa vyuo vikuu kushika nafasi za uongozi ijulikanayo kama, Global Management Trainee Program (GMT), ya kampuni ya kimataifa ya ABinBev ambayo ni kampuni mama ya Tanzania Breweries Limited Group (TBL Group) akiwa anafanyika kazi katika kiwanda cha (TBL).

Lisa, anaeleza kuwa bila kufanya uwekezaji wenye mtazamo wa kujenga biashara endelevu kwa miaka mingi, kuna hatari ya biashara nyingi hususani viwanda vinavyoanzishwa kutofika mbali; badala yake historia ya nyuma kujirudia ambapo Tanzania ilikuwa na viwanda vingi kuanzia katika awamu ya kwanza ya utawala ambapo vingi vilikufa kutokana na sababu mbalimbali mojawapo ikiwa ni kukosekana kwa mipango endelevu katika uwekezaji. 

 Akiwa msomi aliyehitimu Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika mchepuo wa Viwanda, Utawala,Uhusiano katika masuala ya kazi na Kifaransa, kutoka Chuo Kikuu cha Cornell nchini, Marekani, anashauri kuwa kuna haja ya kuanzishwa Progamu mbalimbali za kuwanoa vijana wa kitanzania wahitimu wa vyuo vikuu na vyuo vya ufundi kwa kuwapatia mafunzo ya vitendo kwa ajili ya kuwaanda kushika nafasi za uongozi katika miaka ya mbele. 

 Akiongea kuhusu kupata nafasi ya kujiunga na Programu ya kuwaandaa vijana wahitimu wa vyuo vikuu kushika nafasi za uongozi ya ABInBev na TBL, Lisa, anaeleza kuwa anajivunia kuwa miongoni mwa wahitimu waliochaguliwa kwenye programu hii kwa kuwa ushindani wa kuipata nafasi ulikuwa mkubwa sambamba na mchujo mkali uliofanywa na wataalamu mbalimbali ili kuhakikisha na kujiridhisha kuwa wanachukua watu wenye uwezo,, makini na waliopo tayari kujifunza.

 “Kwa muda mfupi ambao nimeanza mafunzo ya vitendo katika kampuni ya TBL nimegundua kuwa programu hii ni muhimu sana kwa kuwa katika kipindi cha muda mfupi nimejifunza mambo mengi ambayo huko nyuma sikupata kukumbana nayo na kila kukicha nakutana na mambo mengi mageni ya kujifunza”, anasema Lisam

Anasema moja ya ndoto kubwa aliyokuwa nayo katika maisha yake ni kufanya kazi katika kampuni kubwa na yenye mifumo mizuri ya kazi, jambo ambalo limetimia kutokana na mazingira ya kazi aliyoyakuta kwenye kampuni ya TBL,amekuta na timu ya wafanyakazi waliobobea katika fani mbalimbali na ambao wako tayari kutoa utaalamu wao kwa wengine wanaojifunza. 

 Kitu kingine ambacho kinamfurahisha Lisa ,katika safari yake ya mafunzo kupitia programu ya GMT ni kukuta kampuni aliyojiunga nayo, ina mifumo thabiti iliyotokana na uwekezaji makini,kuanzia mifumo ya uzalishaji,usambazaji wa bidhaa,masoko na mauzo na kuwa na sera zenye mtazamo wa kujenga jamii endelevu zinazoenda sambamba na utekelezaji wa malengo endelevu ya milenia ya umoja wa mataifa.

 “Inafurahisha kuona kampuni inayapa kipaumbele masuala ya msingi katika kujenga biashara endelevu kama vile utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji,usalama wa wafanyakazi wake ,kushirikiana na jamii zilizopo katika maeneo inakofanyia biashara zake kama ambavyo inafanya kazi na wakulima wa zao la Shahiri na mazao mengine,kuhakikisha inapata malighafi zake nchini ,kuendesha mafunzo ya ujasiriamali wadogo wanaosambaza biashara zake ili nao biashara zao ziwe endelevu bila kusahau kufanikisha miradi mbalimbali ya kusaidia jamii mojawapo ikiwa ni miradi ya maji ,kelimisha jamii matumizi ya vinywaji kistaarabu na kushirikiana na serikali na wadau wengine kutoa elimu ya usalama barabarani” .

Anaeleza kuwa katika safari yake ya mafunzo atafanya kazi katika vitengo mbalimbali vya kampuni ndani na nje ya nchi ili kupata ujuzi,na katika kipindi cha muda mfupi tayari ameshiriki katika miradi ya mazingira,ukuzaji wa vipaji vya wanafunzi na mradi wa promosheni ya bia ya Kilimanjaro inayowezesha washindi kwenda nchini Urusi,kushuhudia mashindano ya kombe la Dunia mubashara. 

 Lisa, anaeleza kuwa anaamini kuwa hadi kufikia mwishoni mwa programu hii ya mafunzo atakuwa amejifunza mambo mengi yatakayomsaidia katika safari yake ndefu ya kukabiliana na changamoto za uongozi sambamba na ubunifu na kutoa mawazo ya kitaalamu yanayowezesha kukabili changamoto na kusonga mbele kibiashara kwa mafanikio.

 Lisa,alimalizia kwa kutoa ushauri kwa wawekezaji wengine nchini kuwa na mtazamo wa kujenga biashara endelevu sambamba na kuwa na programu za kuandaa wataalamu wa kuendesha biashara wanaopata mafunzo ya vitendo kutoka kwa wataalamu waliopo kama ilivyo programu ya GMT ya ABInBev na TBL.”Programu kama hii ni muhimu kwa kuwanoa vijana wasomi kupata ujuzi na uzoefu zaidi,natamani kuona pia idadi ya vijana wanaochukuliwa katika Programu hii kuongezwa zaidi ya sasa ili inufaishe vijana wengi zaidi”alisisitiza. 

 Akiongea juu ya Programu ya Global Management Trainee (GMT),Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa TBL,David Magese,alisema hii ni progamu inayolenga vijana wasomi ambapo wanaobahatika kujiunga nayo hupatiwa mafunzo ya vitendo kwa kipindi cha miezi 10 kwa ajili ya kuwaandaa kushika nafasi za juu za uongozi ndani ya biashara za kampuni mama ya TBL ya ABIn Bev. 

 Alisema programu ni moja ya mkakati wa kampuni wa kuendeleza vipaji vya vijana na kuongeza kuwa waliochaguliwa kwenye GMT mwaka huu ambao ni 2 kwa hapa nchini mbali na kupata mafunzo ndani ya nchi pia watapata mafunzo kwenye viwanda mbalimbali vya kampuni vilivyopo nje ya nchi kwa kuwa wanaandaliwa kuwa viongozi sio kwa hapa Tanzania bali wanaweza kufanya kazi katika nchi yoyote. 

 Magese,alimalizia kwa kusema kuwa kampuni itaendelea na mpango wa kuendeleza wahitimu wa vyuo vikuu nchini kwa kuwapatia fursa za kukuza vipaji vyao kupitia programu hii ya GMT ambayo imepata mafanikio makubwa katika nchi mbalimbali zilipo biashara za kampuni ya ABInBev.

USAID YAPONGEZA MCHANGO WA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII-TASAF KATIKA KUBORESHA MAISHA YA WANANCHI.

$
0
0
Na. Estom Sanga-TASAF 

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa -USAID, Andy Karas amefanya ziara katika mkoa wa Kagera na kukagua shughuli zinazofanywa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF na kuridhishwa na maendeleo yaliyofikiwa katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani humo.

Akiwa katika kijiji cha Mishenyi kata ya Butelankuzi wilaya ya Bukoba Vijijini ,Mkurugenzi Mkazi huyo wa USAID alitembelea Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambako alijionea namna Walengwa hao walivyoboresha makazi yao kwa kujenga nyumba bora kwa kutumia ruzuku itolewayo na TASAF .

Aidha Karas alipata ushuhuda wa Walengwa namna wanavyotumia ruzuku hiyo katika kuboresha huduma za elimu na afya kwa kaya zao huku pia wakitilia mkazo suala la uanzishwaji wa miradi midogo midogo ya uzalishaji mali kwa lengo la kujiongezea kipato chao.

“huu ni mwelekeo sahihi na unaopaswa kuungwa mkono na wapenda maendeleo kama USAID kwani unatekelezwa kwa misingi endelevu” alisisitiza Mkurugenzi Mkazi huyo wa USAID.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mkazi huyo wa USAID alikagua miradi na bidhaa mbalimbali inayotekelezwa na Walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Mishenyi kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato na kukuza uchumi wao. Miongoni mwa bidhaa hizo ni mbuzi, kuku,vikapu, mayai,vikapu na Mikungu ya ndizi.

Nao Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji hicho cha Mishenyi waliipongeza serikali kwa kubuni Mpango huo kupitia TASAF ambao wamesema umesaidia kurejesha utu wao kwani hapo awali waliishi katika hali ya ufukara na sasa wanaona nuru ikiwarejea kwa kuanza kumiliki mali na kumudu kuendesha maisha yao kaya zao.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF,Amadeus Kamagenge,aliwahakikishia walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini kote kuwa Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii imeweka mkakati madhubuti wa kuwashirikisha walengwa katika kupunguza umaskini huku mkazo ukiwa ni kwa wao kufanya kazi za uzalishaji mali.
Mkurugenzi Mkazi wa USAID  Andy Karas (wanne kulia )katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa miradi wa TASAF Amadeus Kamagenge (wa pili kulia )nje ya nyumba iliyojengwa na mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa kutumia fedha za Mpango huo  katika kijiji cha Mishenye kata ya Butelankuzi wilaya ya Bukoba mkoani Kagera. 
 Mkurugenzi  Mkazi wa USAID  Andy Karas  na Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF Amadeus Kamagenge wakiangalia bidhaa zilizotengenezwa na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Mishenye kata ya Butelankuzi halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera.
 Mkurugenzi  Mkazi wa USAID  Andy Karas (aliyeshika daftari) akiangalia bidhaa zilizotengenezwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na TASAF  katika kijiji cha Mishenyi  kata ya Butelankuzi wilaya ya Bukoba mkoani Kagera kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato na kupambana na umaskini..
 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa ,USAID, Andy Karas akikagua moja ya mabanda ya kufugia mbuzi lililoanzishwa na mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, katika kijiji cha Mishenyi wilaya ya Bukoba mkoani Kagera kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.
Hapa ni mwendo wa zawadi tu, Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na TASAF katika kijiji cha Mishenye kata ya Butelankuzi wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wakimpatia zawadi mgeni wao Mkurugenzi Mkazi wa USAID baada ya kuzungumza nao na kuwatia moyo wa kufanya kazi ili waweze kuondokana na umaskini.

Rais Magufuli amteua Bw. Fidelis Mutakyamirwa kuwa Mwenyekiti Baraza la Taifa la Ushauri wa Ardhi

SERIKALI YAPOKEA GAWIO LA SH. BILIONI 10.1 KUTOKA NMB

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Benki ya NMB imetoa gawio la Sh. bilioni 10.1 kwa Serikali ambayo inamiliki asilimia 32 ya hisa za Benki hiyo baada ya kupata faida ya Sh. bilioni 94.8 baada ya kodi kwa mwaka 2017/2018.

Tukio hilo la kukabidhi hundi kifani ya gawio hilo limefanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma, kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango, kwa niaba ya Serikali, na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ineke Bussemaker. 

Dkt. Mpango amezipongeza juhudi za watendaji wa Benki hiyo waliofanikisha kupatikana kwa faida iliyowezesha Serikali kupata gawio licha ya changamoto zilizoikumba Sekta ya Benki likiwemo suala la mikopo chechefu.

“Mikopo chechefu imekua tatizo kwa Benki nyingi nchini hivyo ninatoa rai kwa Benki ya NMB kuhakikisha inafuata taratibu za kukopesha na kuendelea kusimamia vizuri wakopaji ili kuondoa tatizo la mikopo chechefu” alieleza Dkt. Mpango. 

Aidha ameipongeza Benki hiyo kwa kutoa huduma katika Sekta ya kilimo na kuitaka ipanue wigo zaidi na kuziwezesha sekta za uvuvi na ufugaji kutokana na umuhimu wake katika ukuaji wa uchumi wa taifa. 

Alisema kuwa anatarajia Benki hiyo itatoa gawio zaidi mwaka ujao wa fedha na amemwagiza Msajili wa Hazina, kuzihakiki taasisi zote ambazo Serikali imewekeza hisa zake ili zitoe gawio lasivyo ametishia Serikali kuondoa hisa zake kwakuwa uwekezaji huo hautakuwa na tija. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ineke Bussemaker alieleza kuwa licha ya Benki yake kutoa gawio hilo la shilingi bilioni 10.1 kwa Serikali, pia inalipa kodi za Serikali vizuri ambapo katika kipindi cha mwaka 2017/18 imetoa kodi ya shilingi bilioni 127.

Aliongeza kuwa tangu mwaka 2014 hadi 2017 benki hiyo imetoa kodi zinazofikia zaidi ya shilingi bilioni 460 na kwamba itaendelea kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za kibenki ili iweze kupata faida na kulipa gawio kubwa zaidi kwa wana hisa wake ikiwemo Serikali inayomiliki silimia 31.8 ya hisa 500.

Aidha, amesema kuwa Benki yake imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Sekta ya Kilimo kwa kutoa huduma za kifedha kwa wakulima wakiwemo wakulima wa Tumbaku na Korosho katika mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara, ambapo imefungua zaidi ya akaunti 300,000 na kuweza kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 250 mwezi Novemba mwaka jana.

Bi. Bussemaker alisema kuwa Benki yake inajitahidi kuhakikisha kunakua na huduma jumuishi za kifedha kwa wananchi kote nchini kwa kuweka Mawakala na kuongeza Matawi ya Benki hiyo na pia kuhamasisha wananchi wafungue Akaunti ya Benki hiyo.

Alisema kuwa ili kufanikisha utoaji wa huduma hiyo ya kifedha kwa watanzania, Benki hiyo imejipanga kutumia teknolojia ya kisasa ya masuala ya fedha ambayo itarahisisha kuwafikia watu wengi ikiwemo huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi. 

Katika Mwaka wa Fedha 2016/2017, Benki hiyo ilitoa gawio la shilingi bilioni 16.5 kwa Serikali, huku kukiwa na pungufu ya shilingi bilioni 6 mwaka huu hatua iliyomlazimu Dkt. Mpango kuiagiza Benki hiyi ihakikishe inaboresha huduma zake ili Serikali ipate gawio kubwa zaidi kwa ajili ya kutumia fedha hizo kuwaletea wananchi maendeleo katika sekta za maji, afya, elimu, na miundombinu mingine muhimu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker (kulia), akieleza kuhusu mkakati wa Benki yake wa kuhakikisha inaongeza ufanisi na kufungua akaunti za wateja wengi zaidi, wakati wa hafla ya kutoa gawio la Sh. bilioni 10.1 kwa Serikali ambayo ni mwanahisa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
 Msajili wa Hazina Bw. Athuman Mbuttuka (Kushoto), Kaimu Kamisha wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benedict Mgonya (katikati) na Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara hiyo Bw. John Rubuga, wakisikiliza kwa makini maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor. Mpango (Mb), kuhusu taasisi za fedha kutakiwa kuwafikia wafugaji na wavuvi wakati wa kupokea gawio la Sh. bilioni 10.1 kutoka Benki ya NMB, Jijini Dodoma.
 Kaimu Kamishna wa Sera Bw. William Mhoja (kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Bajeti Bw. Pius Mponzi, wakifuatilia tukio la Benki ya NMB kuipatia Serikali inayomiliki asilimia 32 ya hisa za Benki hiyo, mgao wa Shilingi bilioni 10.1, baada ya kupata faida katika biashara mwaka 2017.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor. Mpango (Mb) (mbele),  akitoa maelekezo kwa taasisi za fedha kuzingatia kanuni za kukopesha ili kuondoa mikopo chechefu,  wakati wa hafla ya Benki ya NMB kutoa gawio la Sh. bilioni 10.1 kwa Serikali ambayo ni mwanahisa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor. Mpango (Mb),  akitoa maelekezo kwa Msajili wa Hazina, Bw. Athuman Mbuttuka, kuzihakiki taasisi zote ambazo Serikali imewekeza hisa zake ili zitoe gawio kwa Serikali, wakati wa hafla ya Benki ya NMB kutoa gawio la Sh. bilioni 10.1 kwa Serikali ambayo ni mwanahisa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor. Mpango (Mb) (wa sita kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker (wa saba kushoto) na Maafisa waandamizi kutoka Benki ya NMB na Wizara hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Serikali kupokea gawio la Sh. bilioni 10.1 kutoka NMB, Jijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor. Mpango (Mb) (kushoto) akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker, baada ya kupokea gawio la Sh. bilioni 10.1 kutoka NMB, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor. Mpango (Mb) (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker, wakiangalia hundi kifani yenye thamani ya shilingi bilioni 10.1, ambayo ni gawio lililotolewa na Benki ya NMB kwa Serikali, Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor. Mpango (Mb) (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker, wakipeana mkono wakati wa makabidhiano ya hundi kifani yenye thamani ya shilingi bilioni 10.1, ambayo ni gawio lililotolewa na Benki ya NMB kwa Serikali, Jijini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

CCM YAIHAKIKISHIA JUMUIA YA KIMATAIFA MAZINGIRA WEZESHI NA RAFIKI YA UWEKEZESHAJI NCHINI

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeihakikishia Jumuia ya kimataifa mazingira mazuri, wezeshi na rafiki kwa uwekezaji nchini. Kauli ya CCM imetolewa leo na Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.

Akiambatana na Maafisa wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Ndg. Polepole amefanya mazungunzo ya kirafiki na Mabalozi wawili Bi. Matli na Bwana Arthur Matli wa nchi ya Uswisi wanaowakilisha Tanzania pamoja na Afrika Mashariki na Zambia.
Katika mazungumzo hayo Ndg. Polepole amefafanua juu ya Mageuzi makubwa ambayo CCM inayafanya katika Chama na Serikali na ambayo yanalenga kuongeza tija, ufanisi na utumishi wa watu. Aidha amewajulisha Mabalozi hao kuwa Chama kimeielekeza Serikali kupitia mikataba ya Madini ili kuhakikisha haki ya Tanzania inapatikana na kwamba baada ya mapitio kumefanyika majadiliano na mashauriano na wawekezaji ambao wameridhia kwa moyo mmoja kuingia katika utaratibu mpya ambao unalinda haki ya watanzania na wawekezaji pia. 

"Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kuielekeza Serikali kuendelea kuweka mazingira rafiki, wezeshi na mazuri kwa wawekezaji ambao wako tayari kuja kuwekeza hapa Tanzania na hasa katika eneo la viwanda. Serikali imetenga ardhi ya kutosha kwa uwekezaji mkubwa, imeweka utaratibu mzuri kupitia kituo cha uwekezaji (TIC) na hivyo yeyote mwenye nia ya kuwekeza anakaribishwa. Kama kuna mwekezaji ambaye amepata changamoto katika mchakato wa kuwekeza nchini au anapata ugumu wowote asisite kutoa taarifa na Serikali ya CCM itashughulikia changamoto hizo" amesema Ndg. Polepole.
Naye Balozi wa Uswisi nchini Tanzania amesema amefarijika sana kwa mazungumzo na yamemwongezea Imani zaidi kwasababu amepata kujua mambo mengi tofauti na habari ambazo anazisikia zikiwemo zinazopotoshwa. "Nakuhakikishia kwamba wakati wowote atakapopatikana mwekezaji nitamleta mara moja Tanzania, na ninapendekeza utaratibu huu wa mazungumzo uendelee" amesema Bi. Matli Balozi wa Uswisi Nchini Tanzania  

Huu ni mwendelezo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuimarisha mahusiano ya ndani na nje katika eneo la siasa, diplomasia na uchumi.

Imetolewa na,

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
OND LUMUMBA

Tigo na StarTimes Wanakuletea Tukio Kubwa Zaidi la Soka kwa Mwaka 2018 Moja Kwa Moja Kwenye Simu Yako ya Kiganjani, Laivu Kupitia Tigo 4G

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo, William Mpinga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya Tukio Kubwa Zaidi la Soka Duniani. Mashabiki wa soka sasa wanaweza kutazama mechi za Kombe la Dunia laivu kwenye simu zao za mkononi kupitia Star Times App na kupata dondoo muhimu za tukio kubwa zaidi la michezo kwa kupiga *147*00# au kwenye Tigo Sports Portal. Kulia ni Meneja wa Masoko na Matangazo wa StarTimes, David Malisa 
Meneja wa Masoko na Matangazo wa StarTimes, David Malisa akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya Tukio Kubwa Zaidi la Soka Duniani. Mashabiki wa soka sasa wanaweza kutazama mechi za Kombe la Dunia laivu kwenye simu zao za mkononi kupitia Star Times App na kupata dondoo muhimu za tukio kubwa zaidi la michezo kwa kupiga *147*00# au kwenye Tigo Sports Portal. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo, William Mpinga .
Afisa wa Habari wa StarTimes, Sam Gisayi akionesha hatu aza kujiunga na huduma mpya ya StarTimes App itakayowezesha wapenzi wa soka kutazama mechi zote 64 za kombe la Dunia laivu kwenye simu zao za mkononi. Hii ilikuwa katika katika uzinduzi wa kampeni ya Tukio Kubwa Zaidi la Soka Duniani ambapo Tigo Tanzania na StarTimes walitangaza ushirikiano huo utakaowezesha wapenzi wa soka pia kupata dondoo muhimu za tukio kubwa zaidi la michezo kwa kujisajili kupitia Tigo namba *147*00# au kwenye Tigo Sports Portal.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo, William Mpinga (kushoto) akikabidhiana mpira na Meneja wa Masoko na Matangazo wa StarTimes, David Malisa katika uzinduzi wa kampeni ya Tukio Kubwa Zaidi la Soka Duniani. Mashabiki wa soka sasa wanaweza kutazama mechi za Kombe la Dunia laivu kwenye simu zao za mkononi kupitia Star Times App na kupata dondoo muhimu za tukio kubwa zaidi la michezo kwa kupiga *147*00# au kwenye Tigo Sports Portal. 

Baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa kampuni za Tigo Tanzania na Startimes wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa kampeni ya Tukio Kubwa Zaidi la Soka Duniani jijini Dar es Salaam.. Mashabiki wa soka sasa wanaweza kutazama mechi za Kombe la Dunia laivu kwenye simu zao za mkononi kupitia Star Times App na kupata dondoo muhimu za tukio kubwa zaidi la michezo kwa kujisajili kupitia Tigo namba *147*00# au kwenye Tigo Sports Portal. 


……………………………………………………………………………

Mashabiki wa soka nchi nzima wana sababu ya kushangilia kufuatia ushirikiano mkubwa kati ya Tigo Tanzania na StarTimes utakaowezesha Watanzania kutazama laivu kwenye simu zao za mkononi mechi zote za tukio kubwa zaidi la mpira wa miggu kwa mwaka 2018.

Huku joto la msimu mkubwa zaidi wa soka kwa mwaka 2018 likizidi kupanda, kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidigitali ya Tigo Tanzania imetambulisha tovuti ya michezo ya www.tigosports.co.tz itakayokuwa hewani kuanzia tarehe 14 Juni mwaka huu. Tigo pia imeungana na mrushaji rasmi wa Kombe la Dunia, StarTimes kuzindua StarTimes Application, itakayowezesha wapenzi wote wa soka kuwa sehemu ya msisimko, furaha na huzuni yanayoendana na tukio hilo linalotazamwa zaidi duniani.

‘Tigo sports portal www.tigosports.co.tz itawezesha Watanzania kufurahia msisimko wa dakika zote tukio kubwa zaidi la soka duniani kupitia mtandao mpana zaidi wa Tigo 4G, pamoja na kupata habari za matukio na dondoo muhimu za tukio hilo kubwa zaidi la mpira wa miguu duniani. Kwa kujiunga kupitia huduma iliyoboreshwa ya *147*00#, wateja wetu pia wanaweza kushiriki katika shindano litakalowapa nafasi ya kushinda zawadi za hadi TSH 10 milioni,’ alisema William Mpinga, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo.

Tigo inajivunia kwa mara ya kwanza kabisa, kuwaletea mashabiki wa soka maajabu ya tukio hili kubwa zaidi la soka moja kwa moja kwenye simu zao za mkononi. Hii inaendana na sifa kuu ya Tigo ya kuwaelewa wateja wake na kuwapa bidhaa na huduma bunifu zinazoboresha maisha yao ya kidigitali.

Kwa kupakua StarTimes Application inayopatikana kupitia Applestore au Play Store, Watanzania sasa wanaweza kuchagua bando za saa, siku, wiki au mwezi kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00#. Kisha wataweza kutazama mechi zote 64 za tukio kubwa zaidi la soka duniani kwa mwaka 2018 moja kwa moja kwenye simu zao janja wakiwa popote nchini huku wakifurahia ubora wa hali ya juu wa huduma za intaneti za Tigo 4G, mtandao mpana, wenye kasi ya juu na wa uhakika zaidi nchini.

‘Teknologia yetu ya StarTimes App inawezesha wateja wetu kuokoa gharama kubwa za intaneti, hivyo kuwasaidia kufurahia Kombe la Dunia muda wowote na popote walipo. Hii ni muhimu hasa ukizingatia kuwa baadhi ya mechi zinaanza saa 11 jioni, muda ambapo wengi wetu bado tupo ofisini au njiani kuelekea majumbani. Kwa hiyo Startimes App na Tigo intaneti zitahakikisha kuwa hukosi mechi yoyote,’ Meneja wa Masoko na Matangazo wa StarTimes, David Malisa alibainisha.

‘Mtandao wetu mkubwa zaidi wa Tigo 4G unaopatikana katika miji 22 nchini, pamoja na uzinduzi wa sports portal na ushirikiano huu na Startimes ambayo ni kampuni kubwa ya kidigitali nchini, tutahakikisha kuwa hakuna shabiki anayepata kisingizio cha kukosa kutazama mechi laivu, kujua matokeo na kufuatilia dondoo mbalimblai za tukio hili kubwa zaidi la soka duniani kwa mwaka 2018,’ William Mpinga, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo alimalizia.

RIDHIWANI APATA FUTARI NA VITUO VITANO VYA WATOTO YATIMA NYUMBANI KWAO MSOGA

$
0
0

Mbunge wa Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ridhiwani Kikwete akiwa ana swali kabla ya Iftar iliyoandaliwa na Tasisi ya Ko Innoavate kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Chalinze kwa Vituo Vitano vya Watototo Yatima Iftar hiyo ilifanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu Ikulu ndogo Msoga

Mmoja ya Wadau kutoka Tasisi ya K Innovates Nasra Kaseja akizungumz ajuu ya umuhimu wa kuwasaidia watoto yatima wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Tasisi ya Ko Innoavate kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Chalinze kwa Vituo Vitano vya Watototo Yatima Iftar hiyo ilifanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu Ikulu ndogo Msoga
Msherehesjai wakati wa Iftar hiyo Mtangazajoi wa Raidio Masoud Kipanya akizungumza juu ya utaratibu na umuhimu wa kufutirisha makundi ya watu maalum katika kipindi hichi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Mbunge wa Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ridhiwani Kikwete akiwa ana swali kabla ya Iftar iliyoandaliwa na Tasisi ya Ko Innoavate kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Chalinze kwa Vituo Vitano vya Watototo Yatima Iftar hiyo ilifanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu Ikulu ndogo Msoga
Mbunge wa Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ridhiwani Kikwete akipakuwa chakula wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Tasisi ya Ko Innoavate kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Chalinze kwa Vituo Vitano vya Watototo Yatima Iftar hiyo ilifanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu Ikulu ndogo Msoga
Wadau wa Tasisi ya Ko Innoavate Pink Ijab wakiwa katika picha ya kabla ya Iftar hiyo ilifanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu Ikulu ndogo Msoga
Mbunge wa Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ridhiwani Kikwete katikati akiwa na Wadau waliotoa Vifaa kwa ajili ya Watoto Yatima wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Tasisi ya Ko Innoavate kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Chalinze kwa Vituo Vitano vya Watototo Yatima Iftar hiyo ilifanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu Ikulu ndogo Msoga

Baadi ya wadau waliofika katika Iftar iliyofanyika nyumbani kwa Rais Mstaafu Ikulu ndogo Msoga

KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MRATIBU MKAZI WA MASHIRIKA YA UN NCHINI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda (kulia) akizungumza na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez alipofika Wizarani tarehe 11 Juni, 2018 kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Serikali ya Tanzania pamoja na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) hapa nchini. Kwa upande wake, Prof. Mkenda alipongeza Mpango wa One UN unaotekelezwa na Ofisi za Umoja wa Mataifa hapa nchini kwa vile unarahisisha utekelezaji wa majukumu na kushukuru ushirikiano mzuri uliopo kati ya Umoja wa Mataifa na Tanzania hususan katika program za kupunguza umaskini na maendeleo endelevu. 
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimatifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy akiwa na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Eva Ng'itu wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Mkenda na Bw. Rodriguez hawapo pichani 
Bw. Rodriguez nae akimweleza jambo Prof. Mkenda 
Mazungumzo yakiendelea 
Picha ya pamoja

MKUTANO WA KIMATAIFA WA MASUALA YA JINSIA NA MAHAKAMA WAFUNGULIWA LEO MJINI ARUSHA

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Licha ya changamoto kadhaa, Tanzania Imepiga hatua kubwa katika jitihada zake za kupunguza unyanyasaji na ubaguzi wa kijinsia.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa Mkutano wa Kimataifa unaohusu masuala ya Jinsia na Mahakama Afrika ulioandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na kuhudhuriwa na Majaji Wakuu kutoka nchi za Afrika.

Makamu wa Rais amesema Tanzania imepiga hatua kwa Marekebisho ya sheria kupitia makosa ya kijinsia ya mwaka 1998 ,pili Utekelezaji wa Sheria ya Ardhi na Sheria ya Ardhi ya Kijiji mwaka 1999 ilifanya mabadiliko makubwa katika kuzingatia haki za wanawake juu ya upatikanaji wa ardhi, Tatu Utekelezaji wa sheria ya sheria ya mtoto mwaka 2009, ambayo kati ya mambo mengine, imewekwa kwa namna sahihi ya haki za mtoto na kuanzishwa kwa madawati maalum kwenye vituo vya polisi ili kuboresha msaada kwa waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia.

Makamu wa Rais aliwaambia Majaji Wakuu kutoka nchi za Afrika kuwa pamoja na uzoefu walionao, wana nafasi ya kufahamu umuhimu wa kuimarisha jinsia katika mfumo wa haki.“Ni matumaini yangu kwamba mkutano huu utakuja na mapendekezo yenye manufaa ambayo yatafungua njia ya kuwa na mifumo ya mahakama yenye uaminifu wa kijinsia na wajibu”

Akizungumzia Mkutano uliofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Jaji Mkuu wa Tanzania profesa Ibrahim Hamis Juma mkutano huo umejikita kuona namna gani kunakuwa na usawa katika kutoa haki, kusogeza huduma za kimahakama kuangalia sheria za mirathi ambapo bado mwanamke ameonekana kukandamizwa na sheria ya kujamiiana.

Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Bi. Sandie Okoro, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird, Majaji Wakuu kutoka nchi za Afrika na wadau mbali mbali wa sekta za kimahakama na sheria.










Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Majaji Wakuu kutoka nchi za Afrika waliohudhuria Mkutano wa Kimataifa unaohusu Jinsia na Mahakama Afrika ulioandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na kufanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Wengine pichani kulia ni Jaji Mkuu wa Ghana Sophia Akuffo,Jaji Mkuu wa Zimbabwe Luke Malaba na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu wengine kushoto ni Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu na Jaji Mkuu wa Benin Batoko Ousmane.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhan mara baada ya kufungua Mkutano wa Kimataifa unaohusu Jinsia na Mahakama Afrika ulioandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na kufanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC)
  
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais




Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images