Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

JAFO AZIAGIZA HALMASHAURI KUKAMILISHA MAJENGO YA KUPOKEA KIDATO CHA TANO

$
0
0

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akikagua ujenzi unaoendelea katika Shule ya Sokoine Memorial wilayani Mvomero
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akisisitiza jambo kwa viongozi na watendaji wa mkoa wa Morogoro na wilaya ya Mvomero wakati wa ukaguzi wa sekondari ya sokoine memorial
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo  akiongea na wananchi katika kituo cha afya Chazi wilayani Mvomero
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo  akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa afya wa Hopitali Teule ya Bwagala iliyopo Turiani wilayani Mvomero
Ukaguzi wa nyumba za watumishi ukiendelea katika sekondari ya sokoine memorial

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo ameziagiza halmashauri ambazo zinaendelea na ujenzi wa mabweni na madarasa kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi wa kudato cha tano Julai mwaka huu kuongeza kasi ya ujenzi huo ili ziweze kuwapokea wanafunzi watakaopangwa katika shule hizo. 

Waziri Jafo aliyasema hayo leo mkoani Morogoro alipokuwa akikagua ujenzi wa shule ya wasichana ya Sokoine Memorial inayojengwa wilayani Mvomero. 

Alipokuwa wilayani humo, Waziri Jafo amemsisitiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero kuongeza idadi ya mafundi ili kazi hiyo ifanyike kwa kasi pindi fedha zilizoombwa za umaliziaji sh.millioni 900 kutoka wizara ya elimu zitakapotolewa. 

Katika ziara hiyo, Jafo aliongozana na Mkuu wa mkoa Morogoro Dk.Steven Kebwe ambapo miradi mbalimbali ya elimu na afya ilikaguliwa ikijumuisha Sekondari mpya ya wasichana ya Sokoine Memorial,  kituo cha afya Chazi, Hospitali Teule ya Bwagala , pamoja na sekondari ya Lusanga.

BALOZI WA KUWAIT AKABIDHI VIFAA TIBA KWA HOSPITALI KIGAMBONI

$
0
0
Ubalozi wa Kuwait umekabidhi zawadi ya vifaa tiba katika Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni ya Vijibweni vyenye thamani ya shilingi milioni 12 za kitanzania ikiwa ni utekelezaji wa mwanzo wa ushirikiano mzuri baina ya Kigamboni na Taifa la Kuwait. 

Akizungumza jana kwenye mapokezi ya vifaa tiba hivyo Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Mgandilwa ameshukuru kwa zawadi hizo alizozitoa Balozi wa kuwait ikiwa ni ahadi aliyoitoa alipotembelea Hospitalini hapo wiki mbili zilizopita. Mhe. Mgandilwa alisema kuwa matembezi ya Balozi wa Kuwait katika Hospitali ya vijibweni yalimfanya kubaini changamoto ya baadhi ya vifaa, hivyo kuahidi kurudi kabla ya mwezi wa ramadhani kuisha. 

Aliesma kuwa Kuwait na Tanzania ni marafiki na kuna kila sababu ya kuendelea kusapotiana na kudumisha urafiki uliopo huku akimuomba Balozi wa Kuwait kuendelea kusaidia baadhi ya vifaa ambavyo ameahidi atavileta kama vile vitanda vya kung'olea meno vitakavyosaidia kuboresha huduma za afya kwa ubora zaidi. 

"Naomba usiishie hapa kwa chochote utakaachona unaweza kusapoti kwenye sekta hizi tatu usisite kutusaidia na mimi kama Mkuu wa Wilaya naahidi kudumisha urafiki wetu" Alisema Mkuu wa Wilaya. Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem alisema zawadi alizozitoa ni mwanzo wa ushirikiano mzuri uliotokana na mapokezi mazuri aliyoyapata kipindi chote kutoka kwa Mkuu wa Wialaya ya Kigamboni pindi alipotembelea Wilayani kwake. 

Aliongeza kuwa Ubalozi wa Kuwait umetoa Vitanza 3 vya watoto, vitanda3 vya kujifungulia kinamama, mashine za oksijeni, mabeseni 8 ya watoto waliozaliwa , mashine ya kutolea uchafu pindi mtoto anapokunywa maji machafu wakati wa kujifungua na vifaa vingine ili kuboresha huduma za afya zinazotolea na Hopsitali ya Vijibweni. 

Balozi Jasem aliongeza kusema kuwa ataangalia namna atakavyoweza kusaidia kutoa mashine za moyo zilizoombwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni na kuahidi kuendeleza ushirikano uliopo na Kigamboni na Tanzania kwa ujumla. Aidha alisema kuwa Kuwait ina mpango unaojulikana kama Kuwait Blood Bank yenye lengo la kutunza damu salama hivyo atajitahidi kuhakikisha Kigamboni inakua miongoni mwa wanufaika wa mpango huo hususani Hospitali ya Vijibweni ambapo viataletwa vifaa vitakavyotumika kuhifadhia damu salama kwaajili ya kuokoa maisha ya Wananchi wa Tanzania. 

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe.Hoja Maabad alimshukuru Balozi wa Kuwait kwa zawadi alizozitoa na kumuomba kuendeleza urafiki na ushirikiano mzuri ulioanzishwa kwa manufaa ya wote. 

Imeandaliwa na: 
Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano 
Halmshauri ya Manispaa ya Kigamboni 
11/06/2018
 Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, leo tarehe 10/6/2018 amepokea ugeni wa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najem.

Mapema akimkaribisha mgeni wake, DC Mgandilwa amemshukuru Balozi Najem kwa moyo wake wa upendo kwa  watanzania hususani wakazi wa Kigamboni. Ameeleza kuwa vifaa ambavyo vimetolewa ni vya zaidi ya Shilingi milioni kumi na moja na vinalenga kuondoa changamoto iliyokuwepo katika wodi za akina mama na watoto. 
Vifaa vilivyopokelewa ni pamoja na mashine za kusaidia wakati wa upasuaji, mashine za kusaidia kupumua, vifaa vya kupima moyo, vitanda vya watoto na beseni maalum kwa ajili ya akina mama wanaojifungua. 

DC Mgandilwa amesema kuwa nchi ya Kuwait ni miongoni mwa nchi ambazo ni marafiki wazuri wa Tanzania na kuwa Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kigamboni itaendeleza ushirikiano huo mwema. Kwa upande wake, Balozi Jasem Al Najem amewapongeza viongozi wa wilaya ya Kigamboni kwa ushirikiano mzuri ambao wamekuwa wakimpatia mara zote alipotembelea wilaya hiyo. 

Balozi Jasem ameeleza kuwa vifaa tiba alivyovikabidhi sio msaada bali ni zawadi kutoka kwa watu wa Kuwait kwenda kwa marafiki zao walioko Tanzania. 
Balozi Najem ameongeza kuwa huo ni mwanzo tu kwani baadhi ya vifaa tiba vingine vilivyoombwa na DC Mgandilwa atahakikisha vinapatikana na kuletwa ili kusaidia watu wa Kigamboni na watanzania kwa ujumla. 

Hafla ya kukabidhi vifaa tiba imefanyika katika hospitali ya  Vijibweni na baadae DC Mgandilwa alimkaribisha mgeni wake iftar iliyoandaliwa katika viwanja vya Msikiti wa Gaddafi uliopo Kigambobi.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa akipokea sehemu ya vifaa tiba kutoka kwa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najem.

BRAC YATOA VIFAA VYA SH MIL 69 KWA WASICHANA TANGA

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa vyenye thamani ya ya sh Mil 69 kwa wasichana 924 kwa ajili ya kuanza shughuli za ujasirimali ili kuweza kujikwamua kiuchum ambavyo ni vyerahani na madraya ya saloon na vifaa vyengine kushoto ni Mkurungenzi Mkuu wa Brac Assan Golowa.
Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga DAS Faidha Salimu akizungumza katika halfa hiyo
Mkurungenzi Mkuu wa Brac Assan Golowa akizungumza katika halfa hiyo
PRO wa shirika la BRAC SEcilia Bosco akizungumza katika halfa hiyo
Meneja wa Miradi wa Shirika la BRAC Mkoani Tanga William Manoah akizungumza katika halfa hiyo
Afisa Elimu Msingi Jiji la Tanga Enedy Mzava ambaye pia ni Kaimu Afisa Kilimo na Mazingira akizungumzxa katika halfa hiyo
sehemu ya vyarahani vilivyotolewa
sehemu ya wasichana wanufaika na vifaa wakivitazama kabla ya kukabidhiwa
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akimkabidhi vifaa vya saloni moja wa wasichana waliopatiwa mafunzo na shirika la BRAC
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akiangalia baadhi ya vifaa v ya shuleni kabla ya kuvikabihdhi kwa wahusika 
Sehemu ya wasichana walionufaika na vifaa hivyo wakimsikiliza mgeni rasmi
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kulia akifurahia jmbo na Mkurungenzi Mkuu wa Brac Assan Golowa
mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo akitoa ushuhuda kwa mgeni rasmi



SHIRIKA la Brac limetoa vifaa vya kazi vyenye thamani ya sh Mil 69 kwa wasichana 924 kwa ajili ya kuanza shughuli za ujasirimali ili kuweza kujikwamua kiuchumi .

Vifaa hivyo ambavyo vimetolewa maalum kupitia mradi wake wa kuwajengea uwezo na kujiajiri wasichana ambao wameshindwa kuendelea masomo ya sekondari mkoani Tanga.Akikabidhi msaada huo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa alisema kuwa vifaa hivyo vitaweza kuwasaidia wasichana hao kuweza kujiendeleza kiuchumi kwa kujihakikishi kipato chao.

“Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ili kuweza kufikia uchumi wa viwanda lakini kupitia Brac tunaona walivyofanikiwa kuwawezesha wasichana hao ili waweze kujikwamua kiuchumi”alisema DC Mwilapwa.

Kwa upande wake Mkurungenzi Mkuu wa Brac Assan Golowa alisema kuwa tayari mradi huo umefanikiwa kuwafikia wasichana 240 toka ulipoanzishwa mwaka 2016 mkoani humo.Alisema kuwa mradai huo unatoa fursa ya pili kwa wasichana walioshindwa kuendelea na masomo waweze kujifunza ujuzi wa mikono na kuweza kujiajiri ili kuweza kuwa wazalishaji mali.

“Mradi huu upo katika mikoa 23 hapa nchini lakini kwa mkoa wa Tanga umeonyesha mafanikio zaidi kutokana na muitikio mkubwa wa wasicahna kujivutika kujiunga na mradi huo”alisema Golowa.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA BALOZI WA VATICAN NCHINI IKULU, AKAGUA UJENZI WA MSIKITI WA BAKWATA KINONDONI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane wakati akiwasili kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wakandarasi wa ujenzi wakati akiwasili kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameongozana  na Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane akikagua  maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa  Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane alipokagua  maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
  Sehemu ya  msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa  na Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally akimshukuru Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane   baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wananchi baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa  na Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane  na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akimsikiliza  mjumbe wa Nyumba Kumi wa Konondoni Shamba Bw. Rashidi Mohamed Mashaushi anayeeelezea kuhusu changamoto ya barabara na mfereji wa maji eneo lao baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga wananchi  baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally aliye na Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane  aliye  na Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Vatican Nchini Mhashama Askofu Mkuu Mrek Solezyriski Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Balozi wa Vatican Nchini Mhashama Askofu Mkuu Mrek Solezyriski baada ya kukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Vatican Nchini Mhashama Askofu Mkuu Mrek Solezyriski baada ya kukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018

PICHA NA IKULU

RC KAGERA -VIONGOZI WA WILAYA WATOE USHIRIKIANO KUTAMBUA VIKUNDI ILI WANUFAIKE NA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII(NSSF)

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya Jamii Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera amewataka viongozi wote wa Wilaya kuhakikisha wanatoa ushirikiano katika kutambua vikundi vyote katika maeneo yao ili Mfuko wa Hifadhi ya jamii Taifa (NSSF) waweze kuwafikia na kuweza kuingia katika mpango wa hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu katika ufunguzi wa semina juu ya mpango wa hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi.

"Maafisa biashara na maafisa ushirika natambua mnazo orodha za vikundi vyote vilivyopo kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Mkoa niwaombe muwapatie hizo orodha NSSF na muwaunganishe na vikundi husika ili waweze kuwafikia wote na kuwapa elimu ya manufaa yanayopatikana iwapo watakuwa wanachama wa NSSF"alisema

Kinawilo aliwataka viongozi wote wa vikundi waliohudhuria semina hiyo kuhakikisha ujumbe unawafikia wale wanaowaongoza na kuandaa mazingira ambayo yatawawezesha kufikiwa na NSSF kwaajili ya kunufaika nayo.Alisema wajasiriamali wengi wamekuwa na kilio cha mitaji,na mara nyingi wanapoomba mikopo wanapewa kwa riba za juu kiasi cha kuwafanya washindwe kupata faida inayositahili na kushindwa kuendelea.

"Nimeelezwa mpango huu wa hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi hasa kwa wanachama wa saccos na waliojiunga NSSF ambao wapo katika vikundi vyenye sifa husika wanaweza kukopeshwa kupitia usimamizi wa benki ya Azania na NMB tunaomba mtoe mikopo kwa riba nafuu na kwakuwa wahusika mpo mtaje kiwango cha riba wazi hapa"alisema

Mariam Muhaji Mwenyekiti wa kamati ya kuratibu sera ya hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi alisema kuwa serekali ya awamu ya tano ni serekali inayomjali kila mtu hasa watu wa hali ya kipato cha chini,kwa kutambua umuhimu huo bunge limeshapitisha sheria mpya namba 2 ya mwaka 2018 inayoboresha hifadhi ya jamii nchini ambapo sheria hiyo imeacha mifuko miwili ambayo ni PSSSF na NSSF.

Alisema mpango huo una manufaa mengi ikiwemo kugharamia matibabu,kinga za majanga,pensheni za uzee mafao ya uzazi na mafao mengine muhimu.

"Tunafahamu zamani swala la hifadhi ya jamii lilikuwa linalenga waajiriwa na kuacha nje waliojiajiri,takwimu zinaonyesha wastani watu 2000 kati ya zaidi ya watanzania milioni 50 wanaopata huduma ya hifadhi ya jamii na katika nchi yetu walioajiriwa ni wachache ukilinganisha na wale waliojiajiri"alisema.
Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawilo akisoma hotuba yake kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu katika ufunguzi wa semina ya mpango wa hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi kwa viongozi wa vikundi vya wajasiliamali na vyama vya ushirika Mkoani Kagera.
Baadhi ya viongozi 82 wa vikundi vya ujasiliamari na vyama vya ushirika Mkoani Kagera wakifuatilia mada mbalimbali zinazotolewa kuhusu mpango wa hifadhi ya jamii kwa sekta zisizo rasmi.

TAARIFA KWA UMMA

DKT TIZEBA AFUNGUA MASOKO YA TUMBAKU KITAIFA WILAYANI KAHAMA

$
0
0
Mgeni rasmi-Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati wa sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018. Picha Zote Na Mathias Canal, WK
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akimkabidhi cheti cha pongezi Mkulima Jonas Blakali kutoka Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita ambaye ameshika nafasi ya tatu katika msimu wa kilimo cha tumbaku wa mwaka 2017/2018 wakati wa sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.
Mgeni rasmi-Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akikata utepew kuashiria ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa katika sherehe iliyofanyika kwenye viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akishuhudia ununuzi wa tumbaku wakati wa sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.
Baadhi ya wakulima wa tumbaku wakishuhudia sherehe za uzinduzi wa ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Zainab Telack akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba wakati wa sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.



Na Mathias Canal, WK, Kahama-Shinyanga


Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amefungua masoko ya tumbaku Kitaifa huku akitoa onyo kali kwa wakulima waliolima zao hilo nje ya mfumo wa ushirika kwa mujibu wa sheria ya zao hilo kwa kuwataka kuacha mara moja kwani serikali itashughulika na wote wanaokiuka taratibu za kilimo hicho.

Dkt Tizeba ameyasema hayo leo 12 Juni 2018 katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga wakati akihutubia mamia ya wakulima wa tumbaku kwenye sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa.

Dkt Tizeba amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Zainabu Telack kufanya kikao na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Wilaya zote za Mkoa huo kuhakikisha wanazuia wananchi kulima nje ya mfumo wa ushirika kwa mujibu ya sheria ya zao la tumbaku.Alisema kuwa wigo wa soko la tumbaku unazidi kuwa finyu kutokana na viongozi mbalimbali kuwakumbatia baadhi ya wakulima wa tumbaku wanaolima nje ya mfumo wa zao hilo.

Katika sherehe hiyo Mhe Dkt. Tizeba amekabidhi vyeti vya pongezi kwa wakulima waliofanya vizuri katika msimu wa kilimo wa mwaka 2017/2018 ambao ni mkulima Emmanuel Cherehani kutoka Wilaya ya Ushetu aliyeshika nafasi ya kwanza, nafasi ya pili ni Jimson Mwanjwenga kutoka Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya na Jonas Blakali kutoka Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wakulima wa zao la tumbaku Tanzania Kaimu Meneja Mkuu TCJE Ndg Bakari Kisia alisema kuwa zao la tumbaku limeanza kulimwa nchini Tanzania enzi za ukoloni kwa kuanzia mikoa ya Ruvuma (Tumbaku ya Moshi) na Iringa (Tumbaku ya mvuke) huku akisema kuwa umaarufu wa zao hilo umekuja mara baada ya masoko huria kuanzishwa.

Kisia amepongeza juhudi za serikali katika misimu miwili ya mwaka 2016/2017 na 2017/2018 kwa kutatua suala la kupanda kwa bei ya pembejeo huku akizitaja changamoto katika zao la tumbaku kuwa ni pamoja na kupungua kwa mahitaji ya tumbaku, Kushuka kwa bei ya wastani ya tumbaku, pamoja na Ukubwa wa riba za mikopo.

Akisoma taarifa ya maendeleo ya zao la tumbaku Tanzania Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya tumbaku Tanzania Dkt Julius Ningu ameitaja mikoa inayolima tumbaku kwa wingi kuwa ni pamoja na Shinyanga, Kagera, Geita, Kigoma, Tabora, Rukwa, Mbeya, Morogoro, Iringa, Ruvuma na Mara huku akiutaja mkoa wa Tabora kuongoza kwa uzalishaji kwa takribani asilimia 50 ya tumbaku yote inayozalishwa nchini.

Alisema kuwa zao la tumbaku lina mchango mkubwa katika pato la Taifa ambapo pato la mkulima limeongezeka kutoka shilingi za kitanzania 2,242,030 mwaka 2011/2012 hadi shilingi 5,982,745 mwaka 2016/2017 ambapo ongezeko hilo ni sawa na asilimia 166.8

Makusanyo ya ushuru wa Halmashauri za Wilaya yameongezeka kutoka shilingi bilioni 10.8 mwaka 2011/2012 hadi shilingi bilioni 14.8 mwaka 2016/2017 ongezeko la asilimia 37. Huku mapato ya fedha za kigeni yakiwa yameongezeka kutoka dola milioni 302.8 mwaka 2011 hadi dola milioni 343.9 mwaka 2016/2017 ongezeko la asilimia 14.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MGENI RASMI KAMPENI YA UPIMAJI VIRUSI VYA UKIWMI


TANROAD YADAIWA KUKWAMISHA MRADI KUFUNGULIWA

$
0
0
Wakala wa barabara Mkoani Ruvuma TANROAD walikwamisha mradi wa ujenzi wa Daraja mto Litete lililopo katika kijiji cha Mkongo Gulioni wilayani Namtumbo liweze kufunguliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Charles Fransis Kabeho.

Akitoa maelezo ya kutofungua mradi huo kwa mkuu wa wilaya ya Namtumbo kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge kitaifa alisema kuwa hawezi kufungua mradi huo kutokana na kumkosa mtu sahihi wa kumwuliza maswali ili aweze kujiridhisha na ujenzi wa daraja hilo .

Bwana Kabeho aliongeza kwa kumwambia mkuu wa wilaya kuwa haiwezekani kufungua mradi wakati wahusika waliojenga Mradi hawapo katika mradi wao na kina nipa wasiwasi kwa nini hawajafika katika mradi wao na mimi kukosa kujiridhisha kwa maswali ambayo ningeweza kuwauliza alisema Kabeho.

Pamoja na kukagua mradi wa ujenzi wa Daraja hilo alitaka kuwauliza maswali wahusika wa mradi TANROAD ambao hawakujitokeza kuhudhuria ufunguzi wa daraja hilo na kuwashangaza wananchi wa kijiji cha Mkongo ambao walitegemea daraja hilo liweze kufunguliwa.

Awali akisoma taarifa ya daraja hilo kaimu Ofisa mipango wa Halmashuri ya wilaya ya Namtumbo bwana Hancy Ngogo alisema kuwa Daraja hilo mpaka kukamilika kwake limegharimu shilingi 64,682,172 .na alipotakiwa kueleza kuhusu ukubwa wa eneo la kujenga daraja hilo alionesha kutojua na kumweleza kiongozi wa mbio za mwenge kuwa taarifa hiyo ilitakiwa isomwe na waliojenga daraja hilo na baada ya kuona hawapo katika eneo hili nimeamua niisome kwa kuwa taarifa yao walishaiwasilisha katika ofisi ya mkuu wa wilaya Namtumbo.

Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Luckness Adrian Amlima alimwambia mkimbiza mwenge kitaifa kuwa ameshangazwa na wakala wa barabara TANROAD kutofika kwenye mradi wao kwani mawasiliano na taarifa zote za mradi wao kuwa moja ya miradi ya kufunguliwa na mwenge wa uhuru walikuwa nayo alisema mkuu wa wilaya huyo.

Mwenge wa uhuru wilayani Namtumbo ulipita katika vijiji 19 kata 9 na Tarafa 2 ambapo wanachi wa wilaya ya Namtumbo waliweza kushiriki katika kuushangilia kila ulipokuwa ukipita na kufanya kazi ya kukagua kuzindua na kutembelea miradi mbalimbali wilayani humo.

Maonesho ya Utumishi wa Umma Kuanza Juni 18 Muhimbili

$
0
0

Hospitali ya Taifa Muhimbili  (MNH) inatarajia kufanya maonesho ya Utumishi wa Umma-siku tatu mfululizo ambayo yatafanyika ndani ya hospitali hiyo kuanzia Juni 18 hadi 20, 2018.

Maonesho hayo ambayo yatazinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu yamebeba kaulil mbiu inayosema “Mapambano dhidi ya rushwa kwa kushirikisha wadau na kujenga uongozi bora ili kufikia malengo ya ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika  na malengo ya maendeleo endelevu’’.

Akizungumza na waandishi wa habari leo  jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Bw. Aminiel Aligaesha amesema Hospitali itafanya maonesho hayo kwa kipindi cha siku tatu kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa11jioni ili wananchi waweze kuona shughuli zinazofanywa na Hospitali ya Taifa Muhimbili.

“Wananchi watapata elimu juu ya utaratibu wa kupata huduma, kutoa elimu ya afya kuhusiana na magonjwa mbalimbali na pia kuwapa fursa wananchi kutoa maoni na malalamiko juu ya huduma tunazotoa,’’amesema Bw. Aminiel.

Kupitia kauli mbiu hiyo amesema MNH  itaeleza ni namna gani wanapambana na vitendo au viashiria vya rushwa katika utoaji wa huduma kwa wananchi na pia kuwaeleza wananchi mipango iliyopo katika kutoa huduma za afya ambazo ni endelevu.

Katika maonesho hayo watalaam waliobobea kutoka maeneo mbalimbali ya Hospitali watakuwepo ambao ni washauri,wachunguzi,tiba na upasuaji ili kukutana na wananchi watakaojitokeza.

Maadhimisho hayo ni moja ya matukio katika kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo nchi wanachama huadhimisha kwa kufanya maonesho ya kazi mbalimbali zinazofanywa na serikali pamoja na taasisi zake na pia kongamano kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma.

Maonesho hayo huratibiwa na Ofisi ya Rais Menejiment ya Umma na Utwala Bora ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Wateja katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha akiwaonesha waandishi wa habari idara mbalimbali zitakazoshiriki kwenye maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2018. Maonesho hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 18 hadi 20 Juni, mwaka huu kwenye viwanja vya Muhimbili.
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo leo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Wateja katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha akisisitiza jambo kwa waandhishi wa habari.


SPRITE BBALL KINGS MSIMU WA PILI WAZINDULIWA, USAILI KUFANYIKA JUNI 16 MLIMANI CITY

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 

MASHINDANO ya Mpira wa Kikapu ya Sprite BBall Kings yamezinduliwa jana huku usaili ukitarajiwa kufanyika Mei 16 mwezi huu katika Viwanja vya Mlimani City Mall Jijini Dar es salaam kuanzia saa 3 asubuhi hadi sa 10 jioni.

Kituo cha East African Television (EATV), East Africa Radio kwa kushirikiana na Kinywaji cha Sprite wameanzisha mashindano hayo kwa lengo la kuinua na kurejesha heshima ya mpira wa kikapu.Mashindano ya Sprite BBall Kings yanafanyika kwa mara ya pili ambapo mwaka 2017 timu ya Mchenga BBall Stars wakiondoka na ubingwa na kujinyakulia kitita cha Sh.Milion 10 na kombe na mshindi wa pili akijinyakulia Milion 3 huku mchezaji bora wa mashindano (MVP) akipata Milion 2 na kikombe.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Masoko wa East Africa Television Basilisa Biseko amesema kuwa dhumuni kuu la mashindano haya ni kuutangaza na kuibua vipaji katika mchezo wa mpira wa kikapu nchini.Basilisa amesema," mashindano haya yamelenga kuinua mchezo wa mpira wa kikapu hususani kwa vijana pia kurejesha heshima ya mchezo huu unaopendwa sana na watu.

"Nawashukuru sana TBF tulikua nao mwaka jana na mwaka tunaendelea tena kuwa nao katika kuhakikisha tunarejesha heshima ya mpira wa kikapu,"amesema Basilisa.Meneja Mauzo wa Kinywaji cha Sprite Sialouise Shayo amesema kuwa hiyo ni fursa nzuri ya kuinua mpira wa kikapu nchini kupitia kwa vijana walioko mtaani.

Amesema kwa muda sasa Sprite wamekuwa wanatafuta vipaji vya mpira wa kikapu katika mashule ila kwa sasa vijana wote watashiriki kuupeleka mchezo wa kikapu mbele  na lengo kuu likiwa ni kusapoti mchezo huo.Sialouise ameongezea na kusema kupitia mashindano haya watapata wachezaji wazuri zaidi hata ikiwemo kwenda kucheza nje ya nchi.

Kwa upande wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini, Katibu Mkuu Mike Mwita amesema kuwa aanawashukuru EATV kwa kuanzisha mashindano haya yanayofanyika kwa mara ya pili na anaamini awamu hii yatakuwa mazuri zaidi.Mwita ameongezea kuwa mwamko kwa mwaka huu umekuwa mkubwa sana ingawa kulikuwa na changamoto ila liliweza kutatuliwa na mashindano kuendelea huku akitoa ushauri kwa EATV na Sprite kupeleka mashindano hayo mikoani.

Katika usaili wa timu siku hiyo, atahitajika kufika nahodha wa timu husika akiwa na majina ya wachezaji wasiopungua 10, wakiwa ni raia wa Tanzania na wenye umri usiopungua miaka 16 pamoja na kwenye kikosi chao wasizidi wachezaji watatu wa ligi daraja la kwanza nchini.Mashindano hayo yatakuwa na hatua kuu sita ambazo usaili, kufuzu, kumi na sita bora, robo fainali, nusu fainali  na fainali.
Afisa Masoko wa East Africa Television ( EATV)  Basilisa Biseko (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa mpira wa kikapu nchini wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Sprite BBall Kings 2018 ikiwa ni kwa mwaka wa pili yanayotarajiwa kuanza mwishoni kwa mwezi June, kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini (TBF) Mike Mwita na Kushoto ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Vinywaji ya Sprite Sialouise Shayo.

WAZIRI JAFO: MABARAZA YA BIASHARA NI CHACHU YA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA

$
0
0
Uwepo wa Mabaraza ya Biashara nchini unachochea azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya Tanzania inakuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati.

Haya yamebainishwa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo wakati wa akifungua warsha ya viongozi wa ngazi ya Mikoa na Wilaya kuhusu uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara iliyoandaliwa na Mradi wa uboreshaji mazingira ya Biashara na Uwekezaji nchini (LIC) kwa kushirikiana na TAMISEMI.

"Mabaraza ya biashara ni muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi yetu hivyo ni vyema kuendelea kuimarisha vyombo hivi vya majadiliano na kupanga mipango ya pamoja kati ya Serikali na Sekta Binafsi,"alisisitiza Jafo.Warsha hiyo ya siku mbili imelenga kuwajengea uwezo viongozi hao ili kutambua fursa na umuhimu wa mabaraza hayo katika kujenga uchumi imara.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge amepongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi kwa kuandaa warsha kama hizo ambazo zinasaidia kuwaongezea na kuwajengea uwezo pamoja na kuvutia wawekezaji nchini.

"Mkoa wa Dodoma tumeweza kutumia fursa kupitia warsha hizi na zimesaidia uwekezaji kuongezeka katika sekta ya kilimo cha Alizeti na Zabibu, ambapo viwanda vidogo vidogo vya kuchakata mafuta ya alizeti na vinywaji vya mvinyo vimeweza kufunguliwa," alisisitiza Dkt. Mahenge

Naye Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TNBC), Bi. Oliver Ligula amesema kuwa semina hiyo itasaidia kuwajengea uwezo viongozi hao wa Mikoa na Wilaya pamoja na wadau mbalimbali juu ya fursa zitokanazo na mabaraza hayo ya biashara.

“Baraza la Taifa la Biashara kwa kushirikiana na TAMISEMI na wadau mbalimbali wameweza kushiriki katika semina hii ambayo itawajengea uelewa wadau na sekta binafsi ili kuweza kuleta maendeleo ya pamoja na yenye ufanisi.” alisema Bi. Ligula.

Mabaraza ya Biashara Tanzania yalianzishwa kwa mujibu wa Wakala wa Rais Na.1 wa mwaka 2001 na kuchapishwa katika Gazeti la Serikali Na.691 la tarehe 28Septemba, 2001.Madhumuni ya kuanzishwa kwa Mabaraza haya ni kuunda jukwaa la majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta ya Biashara katika kila jukwaa la utawala ili kujadiliana namna bora ya kuboresha mazingira ya boashara na uwekezaji Nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR -TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha ya viongozi wa ngazi za Mikoa na Wilaya kuhusu uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara ya mikoa ya Dodoma na Kigoma Juni12, 2018 Jijini Dodoma. 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya viongozi wa ngazi za Mikoa na Wilaya kuhusu uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara ya mikoa ya Dodoma na Kigoma Juni12, 2018 Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR -TAMISEMI), Selemani Jafo akipitia nyaraka wakati wa ufunguzi wa warsha ya viongozi wa ngazi za Mikoa na Wilaya kuhusu uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara ya mikoa ya Dodoma na Kigoma Juni12, 2018 Jijini Dodoma.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa toka TAMISEMI,Charles mhina.


Baadhi ya washiriki wa warsha ya viongozi wa ngazi za mikoa na wilaya kuhusu uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara ya mikoa ya Dodoma na Kigoma wakifuatilia hafla ya uziduzi wa warsha hiyo leo Juni12, 2018 Jijini Dodoma.

Mwezeshaji wa warsha ya viongozi wa ngazi za mikoa na Wilaya kuhusu uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara ya Mikoa ya Dodoma na Kigoma, Profesa Lucian Msambichaka akiwasilisha mada kuhusu nafasi ya Sekta ya Umma katika kuboresha mazingira ya biashara leo Juni12, 2018 Jijini Dodoma.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

CHINA YAIOMBA TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA KIDUNIA WA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeombwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa kidunia wa viongozi wa vyama vya kisiasa, maombi haya yamewasilishwa na Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke alipotembelea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba kuonana na Ndg. Bashiru Ally Kakurwa, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Balozi Wang Ke amefika Ofisi Ndogo za CCM kumletea Ndg. Bashiru Kakurwa ujumbe wa salamu za pongezi kwa kuteuliwa na Ndg. John Pombe Joseph Magufuli, Mwenyekiti wa CCM na kwa kauli moja kuchaguliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Katika salamu zake Balozi Wang Ke ameeleza China na Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) kinampongeza Ndg. Bashiru na kwamba wako tayari kushirikiana naye katika masuala mbalimbali kama sehemu ya mahusiano ya muda mrefu kati ya Tanzania na China na vyama vya CCM na CPC. Aidha, Balozi Wang ametumia mkutano huo kuwasilisha ombi la China kwa Chama Cha Mapinduzi kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kidunia wa Viongozi wa Vyama vya Siasa ambao kwa mara ya kwanza unafanyika barani Afrika na unaotarajiwa kufanyika mwezi wa Julai 2018.
Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) kimeichagua Tanzania na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mwenyeji wa mkutano huu mkubwa na wa kihistoria "CPC Dialogue with World Political Leaders in Africa". Mkutano huu wa kidunia unabeba kauli mbiu isemayo nadharia na vitendo katika kutambua njia sahihi za maendeleo ambazo ni endelevu na halisia kwa nchi zetu. Tunayo furaha na heshima kubwa kuwa na mkutano huu mkubwa Afrika na Tanzania kama sehemu ya Mpango wa kuiunganisha dunia kwa barabara na usafiri wa maji ulioasisiwa na Ndg. Xi Jinping Katibu Mkuu wa CPC na Rais wa China amesema Bi. Wang Ke.

Akipokea salamu hizo za pongezi Ndg. Bashiru Ally amemhakikishia Balozi Wang kwamba Chama Cha Mapinduzi kitaendeleza mahusiano ya kidugu na ya kihistoria kati ya CCM na CPC na nchi zetu mbili.
Tunataka kujifunza zaidi kutoka China na hasa namna ya kujipanga kimkakati katika kushughulika na kuendeleza mapambano dhidi ya dhuluma na unyonyaji ili nchi yetu iinuke na kuleta manufaa makubwa kwa watu wetu wa Tanzania. Ndg. John Pombe Joseph Magufuli, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayo kazi ya kujenga uchumi utakaowezesha kujitegemea, uchumi wa kitaifa, uchumi utakaowaondoa watanzania kutoka katika maisha ya umasikini kama China na kwa msingi huu kama Chama na Ilani tumejitambulisha kuhudumia wanyonge na kushughulika na shida za watu amesema Ndg. Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa CCM

Huu ni mwendelezo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuimarisha mahusiano ya ndani na ya nje katika eneo la siasa, diplomasia na uchumi.

Imetolewa na,

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
OND LUMUMBA

WAZIRI UMMY KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LA TIKA WAGAWA VYAKULA VYA SIKUKUU YA EID EL FITRI KWA WAKAZI WA JIJI LA TANGA

$
0
0

 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia Mbunge wa Viti Maalumu (CCM)Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu katika akigawa vyakula vyenye thamani ya sh.milioni 29.9 kwa kaya 500 za wakazi wa Jiji la Tanga ambavyo ni Mchele Kg 5,Maharage Kg 5,Sukari Kg 5,Unga wa Ugali kg 5,Unga wa Ngano Kg 5,Chumvi Kg 1 na Mafuta ya kupikia lita 5 kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Fitri vilivyotolewa na Shirika la Maendeleo la Uturuki (TIKA) baada ya kuwapa maombi ya mahitaji hayo kwa wakazi hao kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella katika halfa iliyofanyika kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga
  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia Mbunge wa Viti Maalumu (CCM)Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu  akigawa vyakula vyenye thamani ya sh.milioni 29.9 kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Fitri kwa kaya 500 za Jiji la Tanga ambavyo ni Mchele Kg 5,Maharage Kg 5,Sukari Kg 5,Unga wa Ugali kg 5,Unga wa Ngano Kg 5,Chumvi Kg 1 na Mafuta ya kupikia lita 5vilivyotolewa na Shirika la Maendeleo la Uturuki(TIKA) baada ya kuwapa maombi ya mahitaji hayo kwa wakazi hao kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella katika halfa iliyofanyika kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga
  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia Mbunge wa Viti Maalumu (CCM)Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu kushoto akimkabidhi vyakula mkazi wa Jiji la Tanga vyenye thamani ya sh.milioni 29.9 kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Fitri kwa kaya 500 za wakazi  Jiji la Tanga ambavyo ni Mchele Kg 5,Maharage Kg 5,Sukari Kg 5,Unga wa Ugali kg 5,Unga wa Ngano Kg 5,Chumvi Kg 1 na Mafuta ya kupikia lita 5 vilivyotolewa na Shirika la Maendeleo la Uturuki(TIKA) baada ya kuwapa maombi ya mahitaji hayo kwa wakazi hao kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella katika halfa iliyofanyika kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia Mbunge wa Viti Maalumu (CCM)Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu kulia akiteta jambo na Mratibu wa Shirika la Tika Hikmet Ozdenoglu kabla ya kuanza zoezi la ugawaji wa vyakula kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Fitri  katikati ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella
  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia Mbunge wa Viti Maalumu (CCM)Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu kushoto akiwa na Mratibu wa Shirika la Maendeleo Uturuki (TIKA) Hikmet Ozdenoglu wakifuatilia ugawaji wa vyakula kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Fitri
  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia Mbunge wa Viti Maalumu (CCM)Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu katikati akiwa na Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto wakiwa na Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Uturuki (TIKA) Hikmet Ozdenoglu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye halfa hiyo ya ugawaji wa vyakula ambavyo ni Mchele Kg 5,Maharage Kg 5,Sukari Kg 5,Unga wa Ugali kg 5,Unga wa Ngano Kg 5,Chumvi Kg 1 na Mafuta ya kupikia lita 5
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga akizungumza wakati wa halfa hiyo
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza katika halfa hiyo
 Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Allan Kingazi akizungumza katika halfa hiyo
 MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza katika halfa hiyo
  Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Allan Kingazi katikati akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakati wa halfa hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Hamisi Mkoba
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto wakati wa halfa hiyo

 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga katikati akiteta jambo na Mratibu wa Shirika la Tika Hikmet Ozdenoglu kabla ya kuanza zoezi  ugawaji wa vyakula kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Fitri kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella
 Sehemu ya wananchi wakisubiri kupatiwa vyakula hivyo

Sehemu ya wananchi waliojitokeza kupata vyakula hivyo kwa ajili ya sikukuu

Sehemu ya vyakula vilivyotolewa
 Sehemu ya vyakula vikishushwa kwenye gari tayari kwa ajili ya kugawiwa wakazi 500 wa Jiji la Tanga ambavyo vimetolewa na Shirika la Maendeleo la Uturuki (TIKA)


MADEREVA WALEVI WAONYWA

$
0
0
JOSEPH MPANGALA,MTWARA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara DCP Lucas Mkondya amewaonya Madereva wa Magari na Pikipiki Kuacha Kutumia Kilevi na baadaye Kuendesha Hasa katika Sikukuu ijayo ya Idd El Fitri.

Akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake Kamanda Mkondya amewataka watu woote wanaotumia Kilevi kuhakikisha wanatafuta madereva watakao wandesha kwa lengo la kuepuka Ajali.

“Tukikumata umelewa na unaendesha gari Utakaa mahabusu ya Polisi Mpaka Sikukuu itakapokwisha ndio tutakupeleka Mahakamani,Kwa hiyo Tukikukamata siku ya Iddi Utakuja kupelekwa Mahakaman siku ya Jumatatu lakini kama unaona Huwezi Sikumbili haziwez kupita Bila kunywa Pombe ni Bora Utafute Dereva aweze kukuendesha”

Aidha ameongeza kuwa katika siku ya Idi Watu woote wanaopenda kukaa maeneo ya ufukweni wahakikishe wanaondoka na kurudi majumbani Pindi inapofika Mida ya saa 12 Jioni.

“Inapofika Saa12 jioni hatutaruhusu watu kuendelea kuogelea baharini kwa hiyo tunawaomba waende mapema na itakapofika saa12 jioni werejee majumbani”

AZANIA BANK YAWAFUTURISHA WATEJA WAKE NA WATOTO YATIMA DAR

$
0
0
AZANIA Benki inajivunia uzalishaji wa huduma kwa kila mmoja kwa wateja wake bila kujali dini, kabila na jinsia kwa faida na hasara kwa kuandaa futari pamoja na waislamu walioungana na wateja wa benki hiyo.
Akizungumza juzi katika hafla ya futari iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara  wa Benki hiyo, Rhimo Nyansaho alisema wameungana na waislam katika futari hiyo ikiwa ni sehemu yao ya kushirikiana na jamii.
Nyansaho alisema benki hiyo inasonga mbele kwa sababu ya michango ya jamii katika benki hiyo ndio maana kipindi cha mfungo wakaona ni sahihi kurudisha pato hilo kwa kufuturu na jamii yenye uhitaji kama watoto yatima na wengineo.
Mkurugenzi huyo alitumia fursa hiyo kuisifia benki yake kwamba wanatoa huduma bora na ndio maana faida inayoongezeka wanairudisha kwa jamii.
Aliipongeza serikali kwa kuweka mazingira ya kushuka kwa riba katika benki mbalimbali ingawa wao walishashusha riba zao muda mrefu.
Mwakilishi wa wateja wa benki hiyo, Deogratius Kifumani aliipongeza benki hiyo kwa huduma zake inazotoa na kutoa wito kwa jamii kuelekeza mikakati yao ya kiuchumi huko.Kifumani alisema ubora wa huduma zao ndio maana inafanikisha matukio muhimu kama hayo katika jamii kwa kurudisha sehemu ya pato lao.  
Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Maulid Kidebe alisema kilichofanywa na benki ya Azania kina maana kubwa kwa jamii, tukio hilo ni thawabu kubwa zinapatikana kwa sababu imewakumbuka yatima ambao wanatakiwa kuwa karibu zaidi na jamii.
Sheikh Kidebe alitoa wito kwa benki na taasisi nyingine kuiga mfano uliofanywa na Azania ili kusaidia jamii katika mahitaji muhimu.
Mtoto yatima aliyekuwepo katika futari hiyo, Safina Muhsin aliishukuru na kuiomba benki hiyo kuendelea kuwa karibu nao kwa masuala mbalimbali.
Katika hafla hiyo ya futari iliyoandaliwa na benki ya Azania iliwahusisha watoto wa kituo cha Yatima cha Ijango Zaidia cha Sinza jijini Dar es Salaam.
 Watoto wa wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Ijango Zaidia cha Sinza jijini Dar es Salaam wakiswali kabla ya kujumuika na wateja wa Azania Bank katika futari.
 Sheikh wa Wilaya ya Ubungo, Shjeikh Maulid Kidebe. akiwaongoza wateja wa Azania Bank wakati wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo iliyowahusisha watoto wa kituo cha watoto yatima cha Ijango zaidia cha Sinza jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wateja wa Azania Bank wakipata futari iliyoandaliwa na benki hiyo na kuwahusisha watoto wa kituo cha yatima cha Ijango Zaidia cha Sinza jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wateja wa Azania Bank wakipata futari iliyoandaliwa na benki hiyo na kuwahusisha watoto wa kituo cha yatima cha Ijango Zaidia cha Sinza jijini Dar es Salaam.
Watoto wakipata futari.
Wateja wakipata futari.
Watu mbalimbali wakipata futari.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Azania Bank pamoja na wateja wa benki hiyo wakipata futari.
Watoto Yatima wanaolelewa na Kituo cha Ijango Zaidia wakipata futari.
 Baadhi ya Watoto Yatima wanaolelewa na Kituo cha Ijango Zaidia wakipata futari.
Watoto wa kituo cha Yatima cha Ijango Zaidia wakisoma duwa.
Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea, akizunguma katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake pamoja na watoto yatima wa kituo cha Ijango Zaidia cha Sinza.
 Mteja wa Azania Bank, Deogratius Kufumani, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wateja wa benki hiyo.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara  wa Azania Bank, Rhimo Nyansaho, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake na kuwahusisha watoto yatima wa kituo cha Ijango Zaidia cha Sinza.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara  wa Azania Bank, Rhimo Nyansaho, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake na kuwahusisha watoto yatima wa kituo cha Ijango Zaidia cha Sinza.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara  wa Azania Bank, Rhimo Nyansaho, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake na kuwahusisha watoto yatima wa kituo cha Ijango Zaidia cha Sinza.
 Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Maulid Kidebe, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Azania Bank kwa ajili ya wateja wake pamoja na watoto yatima.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara  wa Azania Bank, Rhimo Nyansaho, akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo.

KAMISHNA MKUU WA TRA AWASHUKURU WAFANYABIASHARA JIJINI DODOMA

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Dodoma 

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amewashukuru wafanyabiashara jijini Dodoma kwa mchango wao wa kulipa kodi na kuiwezesha Serikali kutekeleza wajibu wake wa kukuza uchumi na kutoa huduma mbalimbali za jamii hapa nchini. 

Akizungumza wakati akifuturisha wafanyabiashara na wafanyakazi wa TRA katika ukumbi wa LAPF jijini hapa, Kichere alisifia uhusiano mzuri uliopo kati ya wafanyabiashara hao na ofisi ya TRA Mkoa wa Dodoma. 

"Nachukua nafasi hii kuwashukuru wafanyabiashara wa Dodoma kwa kuwa walipakodi wazuri na kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu na ofisi yetu ya TRA hapa mkoani Dodoma ambapo kutokana na uhusiano huu uliopo, tunapata urahisi wa kutekeleza jukumu letu la kukusanya mapato ya Serikali kwa manufaa ya watanzania wote," alisema Kichere. 

Kichere amewaahidi wafanyabiashara hao kuwa, TRA itaendelea kudumisha ushirikiano huo na kukaribisha mazungumzo ya pamoja na viongozi wa TRA mkoani hapa ili kufikia muafaka wa masuala mbalimbali yanayohusu kodi badala ya kulalamika mitaani bila kupata suluhisho. 

Aidha, Kamishna Mkuu Kichere amewahimiza wafanyabiashara hao kuendelea kulipa kodi mbalimbali kwa wakati kwani kodi hizo hutumika katika kujenga uchumi wa nchi na kutoa huduma mbalimbali za jamii ikiwa ni pamoja na huduma za afya, maji safi na salama, elimu, kulipa mishahara ya watumishi wa Umma, miundombinu ya barabara na umeme. 

"Nachukua fursa hii kutoa rai kwenu wafanyabiashara kuendelea kulipa kodi zote kwa wakati ikiwa ni pamoja na Kodi ya Majengo na Kodi ya Mapato awamu ya pili ambapo mwisho wa kulipa kodi hizi ni tarehe 30 Juni, mwaka huu. Kodi nyingine ni Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo hulipwa tarehe 20 ya kila mwezi. Hivyo, uhiari wenu wa kulipa kodi hizi kwa wakati ndio chachu ya kujenga uchumi wetu na kuharakisha kutoa huduma za jamii kwa watanzania wote", alisema Kichere. 

Naye Katibu Mtendaji wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) mkoani Dodoma ambaye pia ni Katibu wa Sekta Binafsi mkoani hapa Idd Senge amesema kwamba, sekta binafsi itaendelea kushirikiana na TRA kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanalipa kodi kwa wakati ili kuepuka faini ambazo zinarudisha nyuma maendeleo ya biashara zao. 

"Sisi kama wafanyabiashara wa hapa mkoani Dodoma tutaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania na pale patakapotokea sintofahamu yoyote tutafanya mawasiliano na viongozi wa TRA ili kupata muafaka wa pamoja," alieleza Senge. 

Mamlaka ya Mapato Tanzania imejiwekea utaratibu wa kufuturisha wafanyabiashara na wafanyakazi wake kila ifikapo Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa lengo la kumshukuru Mwenyezi Mungu katika shughuli mbalimbali wanazozifanya hususani za ukusanyaji mapato ya Serikali.



Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akitoa hotuba fupi kwa Wafanyabiashara wa Jijini Dodoma wakati wa hafla fupi ya Iftar aliyowaandalia wafanyabiashara hao ikiwa ni sehemu ya kuwathamini walipakodi nchini.
Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (aliyevaa miwani) akiwekewa futari wakati wa hafla fupi ya Iftar aliyowaandalia wafanyabiashara wa Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuwathamini walipakodi nchini.
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Jijini Dodoma wakichukua futari wakati wa hafla fupi ya Iftar iliyoandaliwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere kwa wafanyabiashara hao ikiwa ni sehemu ya kuwathamini walipakodi nchini.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (aliyevaa kofia kulia) akiwa na baadhi ya wafanyabiashara na watumishi wa TRA wakifuturu wakati wa hafla fupi ya Iftar iliyoandaliwa na Kamishna Mkuu huyo ikiwa ni sehemu ya kuwathamini walipakodi nchini.
Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wakiwa katika hafla fupi ya Iftar jijini Dododma aliyoiandaa Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Charles Kichere ikiwa ni sehemu ya kuwathamini walipakodi nchini.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyabiashara na watoto yatima wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Rahman kilichopo jijini Dodoma wakati wa hafla fupi ya Iftar aliyowaandalia wafanyabiashara na watumishi wa TRA ikiwa ni sehemu ya kuwathamini walipakodi nchini. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi la LAPF jijini Dodoma.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyabiashara na watumishi wa TRA mara baada ya hafla ya Iftar aliyowaandalia wafanyabiashara hao ikiwa ni sehemu ya kuwathamini walipakodi nchini. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi la LAPF jijini Dodoma. (PICHA ZOTE NA TRA)

UBA-TANZANIA MEETS LEGENDARY INSPIRATIONAL FIGURE AND PROFFESIONAL ATHLETE JOHN STEVEN AKHWARI.

$
0
0
On 29th May 2018, Lucky United Bank for Africa - Tanzania staff were visited by a legendary figure from the summer Olympics of 1968, Mr. John Steven Akwari who is famous for his quote "My country did not send me 5,000 miles to start the race; they sent me 5,000 miles to finish the race."

Executive Director Emeke E. Iweriebor was pleased to host Mr. Akhwari,s as he always referred to his story to motivate the team to making success stories through resilience and commitment.The ED/RCEO charged all staff members to be strongly committed and positively inclined to creating a difference.

He urged staff to become believers, be resilient and always go the extra miles to achieve exceptional results.During his dialogue, the ED/RCEO largely used the example of John Steven Akhwari a marathon runner during the 1968 Olympic games in Mexico City. Akhwari was a world class runner of the 1960’s and 1970’s where he participated in different Olympic games across the world. His 1968’s Olympics in Mexico is regarded the most heroic story to date.

This is because during his 42 Kilometre marathon mission Akhwari was Cramped up due to the high altitude of the city. He had not trained at such an altitude back in his country. At the 30 -kilometre point there was jockeying for position between some runners and he was hit. He fell badly wounding his knee and dislocating that joint plus his shoulder hit hard against the pavement.

He however continued running, finishing last among the 57 competitors who completed the race started by 75 runners.The winner of the marathon was Mamo Wolde of Ethiopia who finished in 2:20:26. Akhwari finished in 3:25:27 one hour later when there were only a few thousand people left in the stadium, and the sun had set and television crew sent out.

As he finally crossed the finish line a cheer came from the small crowd. When interviewed later and asked why he continued running, he said, "My country did not send me 5,000 miles to start the race; they sent me 5,000 miles to finish the race."

During his engagement with UBA- Tanzania staff Mr. Akhwari reminded the agile audience that he did not finish the race to prove a point but simply to ensure that he finished what he was set to do.

Managing Director UBA - Tanzania honoured the iconic figure and urged his staff to always be the first to do things differently saying “the historical moment demonstrates resilience, consistency and Focus the ultimate goal must be achieved regardless the circumstances and strive to complete what is started and not rely on obstacles as excuses”.

He said each individual is born with an inner talent and it is important to let shine the talent and become more productive than being timid and live without achieving significant results.

During the 1968 race, Akhwari’s body was exhausted but not his spirit; his competitors crossed him one by one but his determination rewarded him in tremendous pain. Akhwari never won any Olympic gold medal but he became the greatest example of never-give-up spirit, and a tale of courage and his story has widely been told across the world especially in education institutions.

John Stephen Akhwari has been honoured and symbolized as the living example of courage and determination. In 1983, he was awarded a National Hero Medal of Honour. In 2000, he was invited to the Olympics in Sydney, Australia and 2008 he was invited in Beijing as a goodwill ambassador to inspire the Olympic athletes for the 2008 Games.
From Left Mr. Mathias Ninga, HR Business Partner East and Southern Africa UBA Group, next is Mr. Emeke Iweriebor, Executive Director East and Southern Africa UBA Group, next is the Renowned Olympian Mr.John Akhwari and Right is Mr.Usman Isiaka the Managing Director UBA Tanzania.
Mr. John Akhwari stressing a point during his visit to UBA Tanzania. On his right hand is Mr. Emeke Iweriebor the Executive Director East and Southern Africa UBA Group.
UBA Staff members pose with Mr. John Akhwari during his visit to UBA Tanzania Head Office.

HOSPITALI YA TAALUMA NA TIBA MAMC, MLOGANZILA WAADHIMISHA SIKU YA KUCHANGIA DAMU

$
0
0
Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili MAMC, Mloganzila imeanza maadhimisho ya siku ya kuchangia damu kwa kufanya zoezi la uchangishaji damu kwa wafanyakazi wa Mkombozi Commercial Bank, tawi la Msimbazi Center ili kukidhi mahitaji ya huduma hiyo kwa wagonjwa wanaohitaji. 

Katika zoezi hili la uchangizaji damu Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Mkombozi Bw.George R. Shumbusho alitoa msaada wa kitanda kimoja kwa hospitali ya MAMC kwa ajili ya kusaidia wakati wa zoezi la utoaji damu kwa watu mbalimbali wanaojitolea na mabox 20 (cooler boxes) za kuhifadhia damu wakati wa kupeleka damu wodini kwa wagonjwa. Msaada huu wa vifaa unagharimu pesa ya kitanzania shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000).

Akiongea wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi Mtendaji Bw. Shumbusho “Kama taasisi ya benki kwa kuona umuhimu wa mahitaji ya damu ndiyo maana tumeadhimisha siku hii ya leo kwa kuwaamasisha wafanyakazi wetu wachangie damu ili tuweze kuokoa maisha ya watanzania na kutoa msaada ya vifaa vitakavyoweza kusaidia zoezi la uchangishaji damu”, alisema Vile Vile aliwapongeza wafanyakazi waliojitokeza kuchangia damu, “Ni jambo la umuhimu mmefanya kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa”, aliongeza. 

Naye Mkuu wa kitengo cha kuchangia damu katika Hospitali ya Taaluma na Tiba MAMC, Mloganzila Dkt. Ivan Nyamhanga amewashukuru uongozi mzima wa Benki ya Mkombozi kwa kuhamasisha zoezi hili la kuchangia damu na pia kwa vifaa walivyotoa ambavyo vitasaidia wakati wa zoezi la uchangishaji damu. Pia aliwashukuru wafanyakazi wote wa benki ya Mkombozi kwa kujitolea kuchangia damu kwa wahitaji. 

"Kama mnavyojua mahitaji ya damu ni makubwa hasa katika hospitali yetu ambayo bado ni changa na hivyo tunatoa shukrani zetu za dhati kwa kuhamasika kuchangia damu", alisema Dkt. Nyamhanga. Zoezi hili la maadhimisho ya siku ya kuchangia damu lilifanyika katika Benki ya Mkombozi, tawi la Msimbazi center na vile vile baadhi ya maaskari kutoka SUMA JKT, Mloganzila waliweza kuchangia damu.
Mtaalamu kutoka kitengo cha kuchangia Damu katika Hospitali ya Taaluma na Tiba (MAMC) akielezea faida za kuchangia damu na sifa za mtu anayetakiwa kuchangia damu kwa wafanyakazi ya Benki ya Mkombozi waliojitolea kuchangia damu katika kuadhimisha siku ya kuchangia damu duniani. 
Wataalamu kutoka kitengo cha cha kuchangia Damu katika Hospitali ya Taaluma na Tiba (MAMC) wakiwa wanapima vipimo mbalimbali kwa wachangiaji kabla ya kuanza zoezi la kuchangia damu 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Mkombozi, Bw. George R. Shumbusho (kulia) akishiriki katika maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu duniani.
Baadhi ya wafanyakazi wakisubiri kuchangia damu katika kuadhimbisha siku ya kuchangia damu duniani 
Kwa Niaba ya Mkurugenzi mtendaji Bw.Antony Mnyambo akimkabidhi kitanda na mabox 20 (cooler boxes) kwa Mkuu wa kitengo cha kuchangia damu katika Hospitali ya Taaluma na Tiba (MAMC) Dkt. Ivan Nyamhanga kwa ajili ya kusaidia zoezi la uchangishaji damu. 
Mkuu wa kitengo cha kuchangia damu katika Hospitali ya Taaluma na Tiba (MAMC) Dkt. Ivan Nyamhanga akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Mkombozi Benki baada ya kupokea vifaa vya kutumika wakati wa zoezi la uchangishaji damu. 
Picha ya Pamoja ya wataalamu kutoka Kitengo cha Kuchangia Damu katika Hospitali ya Taaluma na Tiba (MAMC) wakati wa maadhimisho ya siku ya kuchangia damu duniani. 

MASAUNI AFANYA ZIARA MKOANI GEITA, AKAGUA UJENZI WA KITUO KIPYA CHA POLISI, GEREZA NA UJENZI WA NYUMBA 100 ZA ASKARI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akionyeshwa na Mkuu wa Gereza Chato, Joseph Busumabu, maeneo mbalimbali ya Gereza hilo ambalo tayari linahifadhi wafungwa na mahabusu na pia linaendelea kupanuliwa kwa kujengwa majengo mapya zaidi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Geita, Shabaan Ntarambe. Masauni alifanya ziara katika Mkoa wa Geita kwa kukagua ujenzi wa Kituo cha Polisi Chato, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi ambazo zimeanza kujengwa mjini Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulamboakimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), Kituo kipya cha Polisi mjini Chato ambacho kipo katika hatua ya mwisho kukamilika. . Masauni alifanya ziara katika Mkoa wa Geita kwa kukagua ujenzi wa Kituo cha Polisi Chato, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi ambazo zimeanza kujengwa mjini Geita.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akitoka kukagua ujenzi wa Gereza Chato, mkoani Geita, ambalo licha ya kua tayari Gereza hilo jipya limenza kuhifadhi wafungwa na mahabusu lakini linaendelea kupanuliwa kwa kuongezwa majengo zaidi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Shaaban Ntarambe, na kulia alyevaa sare, ni Mkuu wa Gereza hilo, Joseph Busumabu. Masauni alifanya ziara katika Mkoa wa Geita kwa kukagua ujenzi wa Kituo cha Polisi Chato, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi ambazo zimeanza kujengwa mjini Geita.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimpa maelekezo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo, mara baada ya kumaliza kukikagua Kituo Kikuu cha Polisi cha Wilaya ya Chato (nyuma pichani) ambapo ujenzi wake upo katika hatua ya mwisho kukamilika. Masauni alifanya ziara katika Mkoa wa Geita kwa kukagua ujenzi wa Kituo cha Polisi hicho, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi ambazo zimeanza kujengwa mjini Geita. 
 Mkuu wa Wilaya ya Chato, Shaaban Ntarambe, akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) eneo la pembezoni mwa Ziwa Victoria ambalo linaweza kufaa kujengwa Kituo cha Polisi cha Wanamaji katika eneo hilo ili kuweza kuimarisha ulinzi zaidi. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo. Masauni alifanya ziara katika Mkoa wa Geita kwa kukagua ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi Geita, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi ambazo zimeanza kujengwa mjini Geita. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi zinazojengwa nje kidogo mwa mji wa Geita. Masauni alisema ujenzi wa nyumba hizo utapunguza ukosefu wa nyumba kwa askari wa mkoa huo mpya, hata hivyo nyumba zaidi ya elfu moja zinatarajiwa kujengwa mkoani humo. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo. Masauni alifanya ziara mkoani humo  kwa kukagua ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi Chato, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa nyumba hizo 100 kwa ajili ya makazi ya askari polisi.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi, akimpa maneno ya kumuagaNaibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) mara baada ya kufanya mazungumzo naye ofisini kwake, jana. Mkuu wa Mkoa huyo alimuambia Masauni wanashirikiana vizuri na vyombo vilivyopo ndani ya Wizara yake na hali ya ulinzi na usalama ipo vizuri mkoani humo. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Selestine Gesimba. Masauni amemaliza ziara yake mkoani humo, ambapo alifanya ukaguzi wa ujenzi wa Kituo kipya  cha Polisi Chato, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi ambazo zimeanza kujengwa mjini Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images