Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

RUTA KUFANYA MAANDAMANO KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS DK. MAGUFULI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

UMOJA wa wananchi ujulikanao kama Rudisha Uzalendo Tanzania (RUTA) unatarajia kufanya maandamano ya amani ya kumuunga mkono Rais John Magufuli kutokana na juhudi na uthubutu anaoonesha katika utendaji wake wa kazi yatakayofanyika jijini Dar es salaam.

Akizungumza na vyombo vya habari Mwenyekiti wa Kamati ya maandamo hayo Charles Maselle ameeleza kuwa Juni 21, mwaka huu watafanya maandamano ya amani yasiyohusisha itikadi za vyama vya kisiasa wala dini ila wananchi wa kada zote jijini wataandamana kutoka Karume na kumalizikia katika viwanja vya mnazi mmoja na wanategemea mgeni rasmi atakuwa Rais.

Aidha amesema kuwa kama wananchi wameona ni bora kumpongeza Rais kwa sasa ili kumpa nguvu na kumtia moyo katika kazi anazofanya hasa dhamira yake ya dhati, ukweli na uthubutu katika kuleta maendeleo na wameanza kwa mkoa wa Dar es salaam na baadaye yataendelea nchini kote.

Pia Maselle ameeleza kama wananchi wameamua kurudisha uzalendo kutokana na mambo yanayofanywa na Rais kama kuboresha huduma za afya, elimu na miundombinu.

Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya maandamano Kigoro Athumani hayo ameeleza kuwa wanamuunga mkono Rais kutokana na juhudi na dhamira yake ya dhati katika kulipeleka taifa katika maendeleo zaidi hasa katika kuziba mianya ya rushwa  na kusimamia uadilifu katika taasisi za umma na binafsi  na kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo.

Pia amewaomba wananchi kujitokeza siku hiyo kumuunga mkono Rais kutokana na mapinduzi anayoleta bila kujali vyama wala dini.

Hali kadharika RUTA wamezindua nembo maalumu itakochapishwa katika tisheti zitakazovaliwa siku hiyo na wameomba wadau mbalimbali kutumia nembo hizo kwa kuchapa fulana na kugawa kwa wananchi siku hiyo.
 Mwenyekiti wa maandamano ya Rudisha Uzalendo Tanzania(RUTA) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya maandamano ya amani yasiyohusisha itikadi za vya vya siasa yatakayo fanyika Juni 21 mwaka huu jijini Dar as Salaam.picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii.
Mwenyekiti wa kamati ya maandamano ya Rudisha Uzalendo  Tanzania  (RUTA) Charles Maselle(kulia)akiwa na wajumbe wameonesha   ya umoja huo.

WAZIRI DK. MWIGULU NCHEMBA AMSIMAMISHA KAZI MSAJILI WA TAASISI ZA KIDINI WIZARANI

$
0
0

*Wizara yake yaanza kumchunguza aliyesambaza nyaraka na matamko mitandaoni 

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba ametangaza kumsimamisha kazi Msajili wa Taasisi za kidini Maryline Komba, huku akiwaomba viongozi wa dini kuendelea na shughuli zao za kutoa huduma za kiroho.

Pia amesema kwa sasa Wizara yake inaendelea kuchunguza aliyeandika na kusambaza nyaraka katika mitandao ya kijamii ambayo imeibua sintofahamu kwa viongozi wa dini mbalimbali na Watanzania kwa ujumla ili sheria ichukue mkondo wake.

Ameongeza kuwa viongozi wa dini na watanzania kwa ujumla wafahamu kuwa nyaraka na matamko ambayo yamesambazwa kwenye mitandao ya kijamii hazina baraka za Wizara husika wala Serikali na hivyo ni vema zikapuuzwa tu.

"Tuwaombe viongozi wa dini kupuuza nyaraka ambazo zinasambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Endeleeni na shughuli zenu kama kawaida kwani nchi hii inaendeshwa kwa mujibu wa Katiba na hivyo msiwe na hofu.

"Serikali na viongozi wa dini wamekuwa na ushirikiano mkubwa na hakuna mahali ambapo wanaonekana kutoaminiana. Hivyo aliyesambaza nyaraka hizo tunachunguza na kisha tutachukua hatua zinazostahili,"amesema Dk. Mwigulu.

Akizungumza leo wizarani hapo Dk. Mwigulu amesema msajili huyo amesimamishwa kupisha uchungu wa kina na iwapo atabainika kutohusika na matamko hayo au nyaraka ambazo zinasambaa mtandaoni basi atarudi kwenye majukumu yake.

Amesisitiza kuwa Serikali inaheshimu viongozi wa dini zote huku akionya wanaotaka kutumia dini kama kigezo cha kufanya siasa au kuigawa nchini.

"Wale ambao wanataka kutugawa kwa misingi ya kidini ni vema wakaacha kwani haitakuwa na tija kwao wala kwa Taifa letu. Hivyo tusiwe sehemu ya kushabikia mambo yanayohusu dini,"amesema.

DK. KIKWETE AISHAURI CMSA KUTOA ELIMU KUHUSIANA NA FAIDA ZA HISA

$
0
0
CMSA yairudisha NICOL soko la hisa

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne , Dk.Jakaya Mrisho Kikwete ameishauriwa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA) kutoa elimu kwa watanzania kuhusiana na ununuaji wa hisa katika soko la hisa.

Kikwete ameyasema wakati hafla ya Kampuni ya NICOL kurudishwa katika Soko la Hisa Dar es Salaam(DSE) baada ya kukidhi vigezo vya kisheria kuongia katika soko hilo, amesema CMSA ikitoa elimu kwa wananchi kutafanya kuongeza hamasa ya ununuaji hisa kuliko ilivyo sasa.

Dk.Kikwete amesema kuwa CMSA ikitoa elimu kutafanya kampuni nyingi kuorodheshwa katika soko la hisa na kufanya uwekezaji wa miradi mingine.Aidha amesema kutokana na ukuaji wa teknolojia katika masoko CMSA imeshauriwa kuboresha zaidi manada wa soko la Hisa wakati wa kufungua na kufunga.Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete alisema kwamba lengo la kuisajili Nocol ilikuwa ni kuwasaidia .

"Nakumbuka wakati serikali inauza hisa zake NMB kulikuwa na mjadala mkali wa kuhoji kwanini nicol wapewe asilimia tano, lakini kwa imani kwamba hii ni kampuni ya wazalendo, basi tukachukua uamuzi kuwapa wazalendo," alisema.Kikwete kwamba hakuwahi kuusikia mgogoro wa NICOL wakati wa utawala wake.

"Lengo lilikuwa kusaidia wazawa kujijenga kuichumi na kukuza maendeleo, nimesikia leo (jana) hadithi ya Nicol katika uongozi wangu sikusikia kabisa mgogoro wao," alisema Kikwete.Aidha aliipongeza CMSA kwa utendaji kazi wake, ikiwemo kusimamia kwa madhubuti masoko ya mitaji.

Nae Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama,amesema kuwa imefanikiwa kuorodhesha hisa 69,165,170 za Kampuni ya Uwekezaji wa Pamoja ya National Investment Company Limited (NICOL) katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) ni kutokana na kukidhi vigezo vya kisheria .

Amesema NICOL iliondolewa katika orodha ya kampuni ya kampuni zilizoorodheshwa DSE Juni 2011 kutokana na matatizo ya kiutendaji katika uwekezaji katika uwekezaji.mamlaka iliidhinisha mauzo ya awali ya hisa za Kampuni ya NICOL kwa umma yaani (Initial Public Offers – IPO). 

Amesema kwamba mauzo hayo yalifanyika katika awamu mbili, moja ikiwa ni Novemba 2004 ambapo Kampuni NICOL ilifanikiwa kukusanya sh. bilioni 3.9 na awamu nyingine ilifanyika Oktoba mwaka 2007, ambapo jumla ya sh. bilioni 5.6 zilikusanywa. 

"Kutokana na mwenendo mzuri wa mauzo ya hisa, Kampuni hii ilifanikiwa kuorodheshwa katika soko la hisa la Dar Es Salaam Julai 15, 2008. Hata hivyo, kutokana na matatizo ya uongozi na kiutendaji katika uwekezaji,kampuni hii tuliiondoa sokoni Juni mwaka 2011 na CMSA iliamuru kuwasimamishwa kwa Wakurugenzi wa Bodi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya NICOL ili kuwezesha uongozi mpya kuteuliwa na wanahisa wote,"alisema.

Mkama alisema kwamba Aprili 14, 2012, Kampuni ya NICOL ilifanikiwa kupata uongozi mpya chini ya Mwenyekiti wake Dk. Gideon Kaunda na ofisa Mtendaji Adam Kinoni ambao ulithibitishwa kupitia Mkutano mkuu wa wanahisa wote.

"Uongozi huu umeweza kushughulikia matatizo ya uendeshaji wa kampuni na uwekezaji ambayo yalisababisha Kampuni hii kuondolewa katika soko la hisa,NICOL pia imeweza kutekeleza maelekezo yote yaliyokuwa yametolewa na CMSA Mamlaka ili kukidhi hadhi ya kuendelea kuwa kwenye Soko la Hisa.

Mkama aliyataja masharti ambayo CMSA ilitoa kwa NICOL nikutoa notisi kwa wanahisa kuwaelezea kile kinachoendelea ndani ya kampuni na kutayarisha mkutano mkuu wa wanahisa,kuhakikisha mahesabu ya NICOL tokea mwaka 2009 yanakamilishwa kama ilivyopangwa, Kuteua wakaguzi wa nje (External Auditos) kwa ajili ya hesabu za kampuni kwa miaka ya fedha 2010-2015 ili kuhakikisha kuwa mkutano mkuu unafanyika Octoba.

Amesema masharti mengine waliyowapa ni Kutayarisha taarifa ya shughuli za kampuni ikiwemo kuiwezesha kuanza kutekeleza kazi zake na kuangalia uwezekano wa kuirudisha kampuni sokoni. 

Mkama alisema NICOL imefanya mabadiliko ikiwa ni pamoja na kuandaa mkakati mpya wa uwekezaji unaohusisha kuugawa uwekezaji wake kwenye dhamana za serikali kwa lengo la kupata anuwai, kuleta ulinzi wa mtaji na uongozi madhubuti. 

"Mageuzi makubwa ya kiutendaji na matokeo mazuri ya mwenendo wa Kampuni ya NICOL ni matokeo ya usimamizi madhubuti wa CMSA uliodhihirika katika kusimamia sheria, miongozo na kanuni za masoko ya mitaji. Misingi hiyo ndiyo iliyotumika kuiwakilisha serikali kulinda masilahi ya wawekezaji katika kampuni ya NICOL, na hivyo kukuza thamani ya uwekezaji kutoka sh. 4.6 bilioni Mwaka 2004 mpaka Sh. Bilioni 96.2 mwaka 2017, sawa na ongezeko la asilimia 1,991,"alisema.

Mwenyekiti wa DSE, Jonathan Njau, alisemakwamba DSE wana furaha kuiona Nikol ikirejea tena katika soko la hisa kwaajili ya kuuza, kununua, na kukuza uchumi wa kampuni pamoja na taifa.

Aliwaasa viongozi wa Nicol kufuata taratibu ikiwa wanataka kuendelea kukaa katika soko lazima wafuate sheria na utaratibu ikiwemo kutengeneza mahesabu na kukaguliwa kwa uwazi.Mwenyekiti bodi ya NICOL, Dk. Gideon Kaunda, alisema kwamba wamerudi sokoni kwa kasi hivyo itauza, kununua na kuzalisha zaidi.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akigonga kengele kwa ajili ya kufungua soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) kuingia kampuni ya NICOL.
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama akitoa maelezo kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kuhusiana na kuingia NICOL katika Soko la Hisa la Dar es Salaam , jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti bodi ya NICOL, Dk. Gideon Kaunda akitoa maelezo kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kuhusiana na kuingia NICOL katika soko hisa na changamoto walizoweza kukabiliana nazo .
Picha za pamoja za makundi mbalimbali katika hafla ya CMSA kuisajili NICOL kwa mara nyingine
Picha za pamoja za makundi mbalimbali katika hafla ya CMSA kuisajili NICOL kwa mara nyingine

Picha za pamoja za makundi mbalimbali katika hafla ya CMSA kuisajili NICOL kwa mara nyingine

Picha za pamoja za makundi mbalimbali katika hafla ya CMSA kuisajili NICOL kwa mara nyingine

Mfumuko wa bei wapungua hadi kufikia asilimia 3.6

$
0
0


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

MFUMUKO  wa bei wa Taifa  wa Mei 2018  umepungua  hadi kufikia asilimia 3.6 ikilinganishwa na asilimia 3.8 ilivyokuwa Mwezi Aprili 2018 mwaka huu .

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo amesema kupungua kwa bei kumechangiwa sana na kupungua kwa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula.

Amesema  baadhi ya bidhaa za chakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na mahindi kwa asilimia 10.3, unga wa mahindi kwa asilimia 12.5, mtama kwa asilimia 13.8, unga wa mihogo kwa asilimia 15.2, viazi mviringo kwa asilimia 9.0 na mihogo mibichi kwa asilimia 12.6, alisema bwana Kwesigabo.

Ameongeza kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2018 imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili 2018.

Hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2018 nchini Uganda umepungua hadi asilimia 1.7 kutoka asilimia 1.8 kwa mwaka ulioishia mwezi aprili 2018.

Aidha kwa upande wa Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2018 umeongezeka kidogo hadi asilimia 3.95 kutoka asilimia 3.73 kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2018.

Mfumuko wa bei unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mfumko wa bei wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam, Mfumuko wa bei umeshuka toka asilimia 3.8 mwezi Aprili hadi kufikia 3.6 Mei. Kushoto ni Meneja wa Ajira na Bei toka NBS, Ruth Minja.

WANAWAKE WASHIRIKI KUJENGA WODI YA MAMA NA MTOTO CHEMBA

$
0
0

Wanawake washiriki kujenga Wodi ya mama na mtoto - Chemba

Wanawake wa Kata ya Songolo, katika Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma wamejitoa katika ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto lililojengwa katika kituo cha afya cha Hamai kilichopo katika Wilaya hiyo kwa lengo la kuchangia nguvukazi ili kupunguza changamoto za kutembea muda mrefu kutafuta huduma za afya.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa kituo hicho Bw. Saidi Msigwa mbele ya timu ya ukaguzi wa ujenzi wa vituo vya afya katika Mkoa wa Dodoma walipokuwa wakikagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya mkoani Dodoma.

Amesema kuwa asilimia kubwa ya wanawake wa Kata ya Songolo walijitokeza katika ujenzi wa kituo hicho kwa kuwa ndicho kilikuwa kilio chao cha muda mrefu cha kujengewa Wodi ya mama na Mtoto jambo lililopelekea wanawake wengi hasa wajawazito kwenda kujifungulia katika Hospitali ya Wialaya ya Kondoa.

Amesema kukamilika kwa Kituo cha afya cha Hamai kutasaidia wananchi wengi kupata huduma ya afya hasa vijiji vya jirani ambavyo ni Murongia, Itolwa , Jangalo, Jinjo, Kinkima na Kirerechangombena ambao wote hupata huduma katika kituo hicho.

Bw. Msigwa amesema mwaka 2015 wanawake wa Kata ya Songolo waliamua kijutolea kujenga jengo la Wodi ya Mama na mtoto kutokana na kuwepo kwa jengo moja la wodi ya Mama na Mtoto jambo ambalo lilikuwa likisababisha msongamano wa wamama wajawazito sababu hii ilipelekea wanawake kuamua kuchimba msingi na kukusanya mawe kwa ajili ya ujenzi wa wodi hiyo ndipo serikali ilipoamua kujenga jengo hilo mwaka 2018.

Bw. Msigwa ameishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kujenga kituo cha afya cha Hamai ambacho kitasaidia wananchi maskini ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu kwenda kutafuta huduma za afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.Amesema kituo hicho kimejengewa wodi ya mama na mtoto, jengo la upasuaji, maabara, chumba cha kuhifadhia maiti na nyumba ya mtumishi ambapo mpaka sasa tayari zimetumika zaidi ya shilingi milioni 291.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Charles Kiologwe ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya chemba kwa usimamizi mzuri wa majengo yaliyojengwa ambayo yanaonyesha uhalisia wa matumizi ya fedha zilizotumika ukilinganisha na ubora wa majengo.

Aidha ameutaka uongozi wahuo kukamilisha ujenzi huo kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma za afya katika maeneo ya karibu na wanapoishi.Naye Bi Martha Mariki Afisa afya Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ameutaka uongozi wa Halamashauri ya Wilaya ya Chemba kuhakikisha maeneo ya taasisi yanapimwa na kuwa na hati miliki, pia kuhakikisha wanaweka kwenye bajeti kama kipaombele cha kuweka uzio wa maeneo ya taasisi ili kuepusha maeneo mengi kuvamiwa na wananchi.
Jengo la Mama na Mtoto liliojengwa katika Kituo cha afya cha Hamai, kilichopo katika Kata ya Songolo, Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.
Timu ya ufuatiliaji na ukarabari wa vituo vya afya nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Charles Kiologwe wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Bw.Jofrey Shima walipotembelea Kituo cha afya cha Hamai, kilichopo katika Kata ya Songolo Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Charles Kiologwe akitoa maelekezo kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Hamai kilichopo katika Wilaya ya Chemba, Mkoani Dodoma.
Timu ya ufuatiliaji na ukarabari wa vituo vya afya nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Charles Kiologwe wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Bw.Jofrey Shima wakati walipotembelea Kituo cha afya cha Hamai, kilichopo katika Kata ya Songolo Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.

SERIKALI YASHAURIWA KUJENGA MAHABUSU ZA WATOTO KWENYE MIKOA NA WILAYA HAPA NCHINI

$
0
0



















 Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga Latiba Ayoub akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo ya siku moja iliyokuwa na lengo la kujaribu kujadili changamoto kwenye sheria za mtoto na kanunuzi zake hususani waliopo kwenye ukinzani nazo wakiwemo kama wadau iliyofanyika mjini hapa .
Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (Tawla) Mwanaidi Kombo akizungumza wakati wa warsha hiyo ya siku moja iliyofanyika ukumbi wa YDCP Jijini Tanga
Afisa wa Dawati Jeshi la Magereza mkoani Tanga ASP Halima Mswagilla akichangia jambo kwenye warsha hiyo 
Wakili wa Serikali Rebbeca Msalangi akisisistiza jambo kwenye warsha hiyo wakati akiwasilisha mada 
 Wakifuatilia hoja mbalimbali za wajumbe wa warsha hiyo 
 Sehemu ya washiriki wakiendelea kufuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwang’ombe Jijini Tanga Husna Abdi wa pili kutoka kulia akichukua baadhi ya dondoo kwenye warsha hiyo 




SERIKALI imeshauriwa kujenga mahabusu za watoto kwenye mikoa na wilaya hapa nchini ili kuwaweka watoto waliokuwa katika ukinzani wa kisheria ambao wamekuwa wakifanya vitendo viovu. 

Hatua hiyo itakuwa sehemu ya kuwaweka watoto happy wakiwa wanasubiri kesi zao kusikilizwa badala ya ilivyokuwa hivi sasa watoto hao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na uhaba uliopo. 

Hayo yalisemwa juzi na Mratibu wa Chama cha Wanasheria wanawake mkoani Tanga (TAWLA) Latifa Ayoub wakati wa warsha ya siku moja iliyokuwa na lengo la kujaribu kujadili changamoto kwenye sheria za mtoto na kanunuzi zake hususani waliopo kwenye ukinzani nazo wakiwemo kama wadau iliyofanyika mjini hapa 

Alisema kutokana na uhaba wa mahabusu za watoto wamekuwa wakati mwengine wakikumbana na changamoto kadhaa wakati wakisubiri utaratibu wa kusikilizwa kesi zao wanazokabiliana nazo kabla ya kutolewa hukumu. 

“Hivi sasa kuna watoto wanakuwa kuzidi umri wao na wanafanya vitendo viovu huku wazazi wakiwa hawana uwezo hivyo kupelekea wimbi lao kuwa wengi na mahabusu yao ni chache hivyo kuna umuhimu wa serikali kuliangalia jambo hili kwa mapana kwa kuziongeza angalau mkoa na wilaya “Alisema 

Hata hivyo alisema pia sehemu hizo ambazo watakuwa wakiwekwa watoto hao itakuwa ni eneo ambalo watakaa wale ambao wapo kwenye ukinzani wa kisheria wakisubiri hitimisho la kesi zao ambazo wanatuhumiwa kuhusika nazo. 

Naye kwa upande wake Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwang’ombe Jijini Tanga Husna Abdi alisema watoto wanaokinzana na sheria wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kuchanganywa na watu wazima watoto kutokupewa haki zao. 

Alisema kupitia warsha hiyo ambayo wamekutana wadau mbalimbali wakiwemo ustawi wa Jamii,Jeshi la Polisi,Mahakamani wawe chachu ya kuielimisha jamii kuhusu haki zao ili kuhakikisha haki inatendeka vema kwa mujibu wa sheria.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

MAAFISA UUGUZI CHUO KIKUU CHA NEW YORK NCHINI MAREKANI KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KATIKA KUBORESHA UTOAJI HUDUMA KWA WAGONJWA

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Shirikishi ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Delila Kimambo akimkabidhi zawadi ya kinyago Afisa Muuguzi wa Chuo Kikuu cha New York cha nchini Marekani Linda Herrmann wakati wa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Maafisa uuguzi wawili kutoka chuo hicho walifika katika Taasisi hiyo kwaajili ya kuangalia namna ya kushirikiana katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wagonjwa.
Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Shirikishi ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Delila Kimambo akimkabidhi zawadi Afisa Muuguzi wa Chuo Kikuu cha New York cha nchini Marekani Mary Brennan wakati wa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Maafisa uuguzi wawili kutoka chuo hicho walifika katika Taasisi hiyo kwaajili ya kuangalia namna ya kushirikiana katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wagonjwa.
Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi Robert ally pamoja na Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Uuguzi wa Chuo Kikuu cha New York cha nchini Marekani Mary Brennan mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Maafisa uuguzi wawili kutoka chuo hicho walifika katika Taasisi hiyo kwaajili ya kuangalia namna ya kushirikiana katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wagonjwa.Picha na JKCI

MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA DUNIA ATEMBELEA MAHAKAMA YA WILAYA KIGAMBONI: AISIFU MAHAKAMA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA MOLADI KTK UJENZI

$
0
0

 MAKAMU  wa Rais wa  Benki ya Dunia Bi.Sandie Okoro ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa utekelezaji wa mradi ya ujenzi wa Mahakama kwa kutumia teknolojia ya Moladi na kutaka iwe mfano wa kuigwa katika nchi nyingine za Afrika.

Pia,  ameipongeza Mahakama hiyo kwa uwiano wa jinsia kwa uwepo wa watumishi wengi wanawake. Sandie alitoa pongezi leo, Juni 08 jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea jengo la Mahakama ya Wilaya na  ya Mwanzo Kigamboni ambalo limejengwa kwa kutumia teknolojia ya Moladi na kupata fursa ya kujionea mahakama inayotembea 'Mobile Court'.

 "Nashukuru kwa mada zilizowasilishwa. Ujenzi wa muda mfupi na majengo mazuri ambayo ni ya mfano wa kuigwa kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla," alisema Sandie. Alisema taarifa za ujenzi wa majengo hayo inapendeza kuzifikia nchi nyingi kwa kuwa majengo yake ni mazuri na yamejengwa kwa viwango vizuri kuendana na thamani ya fedha.

Makamu huyo wa Rais wa Benki ya Dunia, Sandie ambaye yuko nchini kuhudhuria mkutano wa kimataifa juu ya upatikanaji wa haki na jinsia kwa bara la Afrika na kutembelea Mahakama ya Tanzania kujionea Mradi wa Maboresho wa huduma za Mahakama unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, alipongeza Mahakama ya Tanzania kwa uwiano wa jinsia.

Alitoa pongezi hizo baada ya kushuhudia watumishi wengi wa mahakama hiyo wakiwa wanawake na wanawake kushuriki katika ujenzi wa majengo ya mahakama kwa kutumia teknolojia ya Moladi.

Kuhusu Mahakama inayotembea, Sandie alisema ni ubunifu mzuri ambao katika utendaji haki utaweza kuwafikia wananchi kwa urahisi hivyo kusaidia kutatua migogoro mbalimbali katika jamii kwa haraka na kwa wakati.

Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Joachim Tiganga, alisema ujenzi wa Mahakama hiyo unarahisisha upatikanaji wa haki kwa wakazi wa Kigamboni ambao walikuwa wakisafirisha kilomita 50 kwenda Temeke kufuata huduma ya Mahakama ya Wilaya.
Alisema eneo lililojengwa mahakama hiyo,  awali lilikuwa na Mahakama ya Mwanzo na jengo hilo jipya lina miundombinu muhimu ikiwemo ya walemavu na lina mfumo wa teknolojia.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Dk. Daniel Mbisso, alieleza teknolojia ya Moladi ilivyotumika kujenga majengo mbalimbali ya Mahakama na kusema ujenzi wake ni rahisi na wa gharama nafuu na huchukua muda mfupi.
Alisema teknolojia hiyo inatumika kujenga majengo ya Mahakama kutokana na changamoto ya majengo ya mahakama.

Alitaja mahakama zilizojengwa kwa kutumia teknolojia hiyo kuwa ni Kibaha, Bagamoyo, nyumba za watumishi Bagamoyo, Kituo cha Mafunzo kilichoko Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Kigamboni, Mkuranga na Kawe.

Mhadhiri Mwandamizi wa Mfumo: Court Mapping kutoka chuo cha Ardhi Job Chaula, akieleza jinsi mfumo wa kutoa taarifa mbali mbali za mahakama una vyofanya kazi katika Mahakama ya Mwanzo na Wilaya ya Kigamboni kupitia mradi wa Court Mapping. 
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Dk. Daniel Mbisso, akieleza jinsi teknolojia ya Moladi ilivyotumika kujenga majengo mbalimbali ya Mahakama na kufanikisha kwa mafaniko makubwa mahakama zaidi ya tano zilizojengwa kwa muda mfupi na garama nafuu.
Makamu wa rais wa Benki ya dunia, Sandie Okoro (katikati) aliyevaa miwani akiwa katika Picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mahakama ya Mwanzo Kigamboni na Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni, Mara baada ya kupokea taarifa (presentation) juu ya utekelezwaji wa miradi wa Court Mapping na mradi wa ujenzi wa mahakama kwa garama nafuu wa kupitia mladi wa Moladi.
Makamu wa rais wa Benki ya dunia, Sandie Okoro kulia akizungumza na wadau mbali mbali wa Mahakama ya Mwanzo Kigamboni na Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni, Mara baada ya kupokea taarifa (presentation) juu ya utekelezwaji wa miradi wa Court Mapping na mradi wa ujenzi wa mahakama kwa garama nafuu wa kupitia mladi wa Moladi. Pembeni yake ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Hussein Katanga.



NAIBU WAZIRI WA NISHATI SUBIRA MGALU, ATEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MITA ZA LUKU ZA KISASA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
NAIBU Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, akiwa ameshika moja ya mita ya kisasa ya LUKU, (Smart Meter), iliyotengenezwa na kiwanda cha Baobab Engineering System Tanzania kilichoko Mbezi jijini Dar es Salaam, wakati alipokitembelea kujionea mita hizo leo Juni 8, 2018.


NA K-VIS BLOG/KhalfanSaid

NAIBU Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, ametembelea kiwanda cha kutengeneza mita za LUKU kilichoko Mbezi jijini Dar es Salaam leo Juni 8, 2018 na kuridhishwa na ubora wa mita hizo.

Alisema tatizo la mita lilikuwa ni changamoto kubwa iliyopelekea kasi ya kuwafikishia umeme Watanzania kuwa na kikwazo kwani TANESCO iliagiza mita hizo kutoka nje.

Kampuni ya Baobab Engineering System Tanzania ndiyo watengenezaji wa mita hizo za kisasa za LUKU (Smart Meters) na uongozi wa kiwanda umeahidi kuzalisha mita za kutosha ili kutatua changamoto iliyokuwa ikiikabili TANESCO kuhusu upatikanaji wa mita.

“Sisi katika kutaka shirika letu la TANESCO lifanye vizuri tumewapa maelekezo yako ndani ya Sera na mipango yetu lazima waunganishie umeme wateja wengi na moja ya component inayotakiwa ni mita, kumekuwa na changamoto ya mita kama mlivyosema, na hasa inatokana na utaratibu wa uagizaji na hata kufika kwa vifaa hivyo ilichukua muda sana, sasa uwepo wa kiwanda cha kutengeneza mita hapa nyumbani ninaamini tatizo hili sasa halitakuwepo.” Alisema Mhe. Naibu Waziri Mgalu.

Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshuhghulikia Mauzo na Masoko Mhandisi Theodory Bayona amesema, tayari Shirika limeanza kutekeleza agizo hilo la serikali na mchakato wa manunuzi umeanza kwa kuhakikisha vifaa vyote vya Shirika vinanunuliwa kutoka ndani na tayari TANESCO imeanza kwa kununua nguzo za umeme hapa hapa nchini, lakini kuhusu mita za umeme TANESCO inampango wa kununua mita 350,000 kutoka kwa wawekezaji wa ndani na mita hizo hasa zitatumika kubadilisha zile mita zile za zamani ambapo zilikuwa haziendi sawasawa lakinin pia kuwaunga na wateja wapya., Alisema Mhandisi Bayona.

Awali Mhe. Naibu Waziri alipatiwa maelezo ya kiuntendaji ya kiwanda hicho kabla ya kupata fursa ya kutembelea eneo la uzalishaji na kujionea jinsi mafundi wazawa wa kiwanda hicho wanavyotengeneza mita hizo la LUKU 
Mheshimiwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizunguzma jambo baada ya kujionea mita hizo.
Mhe. Naibu Waziri akimsikiliza Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshuhghulikia Mauzo na Masoko, Mhandisi Theodory Bayona.
Wataalamu wa kiwanda ambao wote ni Watanzania wakiwa kazini.
Mhe. Naibu Waziri akiangalia utaalamu wa kutengeneza mitab hizo.
Mhe. Naibu Waziri akiangalia utaalamu wa kutengeneza mitab hizo.
Moja ya mita hizo ikiwa katika hatua za mwisho za matengenezo.
Wataalamu wa kiwanda ambao wote ni Watanzania wakiwa kazini.
Wataalamu wa kiwanda ambao wote ni Watanzania wakiwa kazini.
Mhe. Subira Mgalu, akizunhuzma. Kulia ni Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshuhhulikia Mauzo na Masoko, Mhandisi Theodory Bayona.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwanda cha Baobab Engineering System Tanzania, Bw.Allan Magoma, akizungumza.
Picha ya pamoja

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AWAVISHWA VYEO MAOFISA WAANDAMIZI TISAWA JESHI LA MAGEREZA JIJINI DAR

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) akimvalisha cheo akimvalisha cheo Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila kuwa Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 8, 2018.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) akimvalisha cheo Mkuu wa Magereza Mkoani Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga kuwa Naibu wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 8, 2018.
Makamishina na Manaibu Kamishna wa Magereza wakisoma Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma baada ya kuvalishwa vyeo na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2018. 

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt Juma Malewa akikagua gwaride maalum katika hafla ya uvishaji vyeo kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza.
Baadhi ya Maafisa Wastaafu na waliopo sasa wa Jeshi la Magereza wakifuatilia hafla fupi ya uvishaji vyeo kama inavyoonekana katika picha.
amishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza waliowavalisha vyeo hivyo kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli ambapo hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni, 8, 2018.Picha zote na Jeshi la Magereza



KAMISHNA Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa, kwa niaba ya Amiri jeshi mkuu Rais John Magufuli amewavisha vyeo maafisa wa ngazi ya juu 9 wa Jeshi la Magereza waliopandishwa vyeo hivyo hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Miongoni mwa maafisa 9 waliovishwa vyeo ni manaibu kamishna wa magereza – DCP wanne wa Jeshi hilo ambao wamepandishwa vyeo na kuwa Makamishna wa magereza, huku makamishna wasaidizi waandamizi wa Magereza -SACP watano wakipandishwa vyeo kuwa Manaibu Kamishna – DCP wa Jeshi hilo.

Waliovishwa vyeo kuwa Makamishna wa Magereza ni Naibu Kamishna wa Magereza Uwesu Ngarama, Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza Tusekile Mwaisabila, Mkuu wa Divisheni ya Huduma za Urekebishaji, Naibu Kamishna wa Magereza Augustine Mboje, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Naibu Kamishna wa Magereza Gideon Nkana ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga, Dar es Salaam.

Wengine waliovishwa vyeo kuwa Manaibu Kamishna wa Magereza ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Julius Sang’udi, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Afwilile Mwakijungu, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Phaustine Kasike, Mkuu wa Kitengo cha Parole pamoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Jeremiah Katungu ambaye ni Katibu Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Magereza.

Akizungumza mara baada ya kuwavisha vyeo Maafisa hao wa magereza(Ijumaa, Juni 8, 2018) katika hafla ya kuwavisha vyeo hivyo iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Ukonga, jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa amewataka makamishna hao wa Jeshi la magereza wa ngazi zote kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uadilifu sambamba na kusimamia haki na usawa katika utekelezaji wa majukumu yao kila siku.

Aidha, Jenerali Malewa amemshukru Amiri jeshi mkuu Rais John Magufuli kwa kuwapandishwa vyeo maafisa hao ambao watajaza nafasi mbalimbali za juu za uongozi ndani ya Jeshi la Magereza kwani kwa muda mrefu safu ya juu ya uongozi ilikuwa na upungufu mkubwa wa kada ya maafisa wa vyeo hivyo hali iliyopelekea kuathiri utendaji kazi wa Jeshi hilo.

Maafisa hao kabla ya kuvishwa vyeo hivyo walivyotunukiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuanzia Juni 02, 2018, walipata fursa ya kula kiapo cha Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma mbele ya katibu wa sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma.

WANANCHI WA KIGOMBE WATAKIWA KUACHANA NA BIASHARA ZA MAGENDO

$
0
0
 MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kigombe Kata ya Kigombe wilayani Muheza umuhimu wa kulipa kodi na kuacha kujihusisha na uingizaji wa bidhaa kwa njia za magendo.
 MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kigombe Kata ya Kigombe wilayani Muheza ambao hawapo pichani juu ya umuhimu wa kulipa kodi na kuacha kujihusisha na uingizaji wa bidhaa kwa njia za magendo kulia ni Kaimu Meneja wa TRA Mkoani Tanga Nazarius Mfikwa kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kigombe Bakari Akida Ally.
 Kaimu Meneja wa TRA Mkoani Tanga Nazarius Mfikwa akizngumza wakati wa mkutano huo kushoto ni MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo.
AFISA Mfawidhi wa Forodha Bandari ya Tanga Zahor Makame akizungumza katika mkutano huo 
MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo kushoto akiwa na Kaimu Meneja wa TRA Mkoani Tanga Nazarius Mfikwa wakifuatilia kwa umakini hoja za wananchi wa kijiji cha Kigombe leo 
Mkazi wa Kijiji cha Kigombe Kata ya Kigombe wilayani Muheza mkoani Tanga Tajiri Twaha akiuliza swali kwenye mkutano
 Sehemu ya wananchi wa Kijiji cha Kigombe kata ya Kigombe wilayani Muheza wakimsikiliza kwa umakini MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo ambaye hayupo pichani wakati alipokwenda kuzungumza nao kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na na kuacha kujihusisha na uingizaji wa bidhaa kwa njia za magendo

MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo kulia akimsikiliza kwa umakini Mwenyekiti wa Kijiji cha Kigombe wilayani Muheza Bakari Akida mara baada ya kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.



WANANCHI wa Kijiji cha Kigombe Kata ya Kigombe wilayani Muheza mkoani Tanga wametakiwa kuacha kushiriki kwenye biashara za magendo badala yake watumie maeneo yaliyorasmi kwa kisheria kwa ajili ya upitishaji wa bidhaa. 

Wito huo ulitolewa leo na Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo wakati akizungumza na wananchi hao kwenye mkutano uliofanyika kwenye eneo la sokoni akiwa ameambatana na maafisa wa TRA mkoa wa Tanga. 

Alisema kitendo cha wananchi kuacha kutumia bandari ya Pangani ambayo ipo kusheria wanafanya makosa makubwa na kuwataka kuitumia kupitisha bidhaa badala ya kutumia zile ambazo hazitambuliki ambazo watakapokamatwa watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria. 

“Tumefika hapa kigombe kutoa elimu kwa kuzungumza na wananchi kutokana na changamoto za mara kwa mara biashara za magendo ambazo zimekuwa zikipitishwa eneo hilo na kuona kutumia muda huo kuzungumza na wananchi kuwaambia madhara yake ni yapi”Alisema. 

Aidha alisema kuwa katika eneo hilo ambalo lipo kilomita 10 kutoka wilayani Pangani ambako kuna Bandari rasmi waendelee kuitumia hiyo na kuchana na matumizi ya bandari bubu ya Kigombe kwani kuendelea kuitumia wanakuwa wakivunja sheria zilizopo

Pia aliwataka wananchi hao kupitisha bidhaa zao kwenye Bandari za Tanga na Pangani ambazo zipo kisheria ili bidhaa zao ziweze kuhakikiwa ili walipwe ushuru ikiwemo kuepukana na kukimbizana na gharama kubwa wanazoingia kukumbizana na wafanyabiashara za magendo.

Hata hivyo alisema hivi sasa chombo cha baharini, nyumba ambazo zitakutwa zimehifadhiwa bidhaa za magendo zitataifishwa ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha biashara za namna hiyo zinakwisha kwenye jamii na hivyo kumfanya kila anayeingiza bidhaa kutumia maeneo yaliyopo kisheria.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Tigo Yaanda Futari Kwa Waamini wa Dini ya Kiislamu Tanga

$
0
0
  Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani George Lugata akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu mkoani Tanga wakati wa futari walioiandaa iliyoandaliwa  na Tugo katika  shule ya Sekondari Jumuiya mjini Tanga juzi. Kulia ni Shehe wa mkoa wa Tanga, Juma Luwuchu

 Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, George Lugata (katikati) akijumuika na waumini wa dini ya kiislamu mkoani Tanga katika futari  iloyoandaliwa na Tigo liyofanyika katika Shule ya Sekondari Jumuiya mjini Tanga juzi.

KIGWANGALLA AFUTURISHA WABUNGE DODOMA, ASISITIZA UPENDO, UMOJA NA MSHIKAMANO WA KITAIFA

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amefuturisha wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika makazi yake yaliyopo Area D Jijini Dodoma.

Futari hiyo ilihudhauriwa na wabunge mbalimbali wa chama tawala CCM na wa vyama vya upinzani wakiongozwa na Spika, Job Ndugai na Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson.

Dkt. Kigwangalla aliwashukuru wabunge wote waliohudhuria hafla hiyo na kusema kuwa imelenga kudumisha upendo, mshikamano na umoja wa kitaifa uliopo baina ya wabunge hao bila ya kujali mipaka ya vyama vyao hususan katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

"Nimefarijika sana kuwapokea waheshimiwa wabunge wenzangu hapa nyumbani kwangu, ninawashukuru sana kwa kuja maana shughuli ni watu, tuliandaa futari nyingi kwa ajili ya wabunge wote, sasa msingefika tungepata mtihani ni wapi pa kuipeleka. "Hafla kama hii ya Iftar inatuunganisha sisi sote bila kujali dini zetu, inajenga na kudumisha upendo, mshikamano na umoja wetu wa kitaifa bila kujali mipaka ya vyama vyetu" alisisitiza Dkt. Kigwangalla. 

Alisema zamani kulikuwa na utamaduni wa watu kufuturu nje ya nyumba zao ili wapita njia au majirani wakikuta wanafuturu nao wanajumuika, "Siku hizi tumeanza kufuturia ndani kila mtu na familia yake, basi siku moja moja kama hivi inatokea tunaamua kuukumbuka utamaduni wetu na kualikana kufuturu pamoja" alisema. 

Kwa upande Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alikua mgeni rasmi kwenye hafla hiyo, Job Ndugai alimpongeza na kumshukuru Dkt. Kigwangalla kwa kuandaa hafla hiyo na kusema kuwa inajenga mshikamano baina ya wabunge bila kujali itikadi za vyama na dini zao. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akimkaribisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai nyumbani kwake kwa ajili ya kujumuika na wabunge wengine kwenye hafla ya futari aliyoiandaa kwa ajili yao nyumbani kwake Jijini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum, Janeth Massaburi akimuombea dua Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla katika hafla ya futari aliyoiandaa jana kwa ajili ya wabunge nyumbani kwake Jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimkaribisha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson kwanye hafla ya futari aliyoiandaa kwa ajili ya wabunge nyumbani kwake Jijini Dodoma. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Mama Salma Kikwete kwenye hafla ya futari aliyoiandaa kwa ajili ya wabunge nyumbani kwake Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (wa tatu kulia) akizungumza na baadhi ya wabunge kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla nyumbani kwake jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao aliwaalika kwenye futari ya pamoja nyumbani kwake Jijini Dodoma.
Mbunge wa Vunjo, James Mbatia akichukua futari katika hafla ya kufuturu iliyoandaliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla kwa ajili ya wabunge nyumbani kwake Jijini Dodoma.
Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hillal akisalimiana na mbunge wa Vunjo, James Mbatia katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla kwa ajili ya wabunge nyumbani kwake Jijini Dodoma. Kushoto ni Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliowaalika kujumuika naye kwenye futari ya pamoja nyumbani kwake Jijini Dodoma.

WAZIRI MKUU ATAKA WANAOTOA TAARIFA ZA UONGO WADHIBITIWE

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wawachukulie hatua kali wananchi wote wanaotumia vibaya namba za mawasiliano za jeshi hilo kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu matukio ya majanga ya moto.

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini kuendelea kutoa mafunzo kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na kupambana na majanga ya moto pindi yanapotokea katika maeneo yao.

Pia ameziagiza Halmashauri zote nchini kuwa na magari ya zimamoto pamoja na magari ya kubeba wagonjwa kwenye vituo vyote vya Zimamoto na Uokoaji katika maeneo yao.Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Juni 8, 2018) wakati alipofanya ziara katika Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura ya Maafa pamoja na Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha mkoa wa Ilala.

Amesema ili kudhibiti wananchi wanaopiga simu za kuomba msaada wa kutaka kuokolewa, huku kukiwa hakuna tukio lolote la janga la moto lililotokea kwenye maeneo yao, ni vema watu hao wachukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye kumweleza baadhi ya changamoto zinazolikabili jeshi hilo kuwa ni pamoja na wananchi kupiga simu wakidai kuna ajali ya moto imetokea katika maeneo yao na baada watu wa uokoaji kufika wanabaini ni uongo.

Hata hivyo, Waziri Mkuu aziagiza Halmashauri zote nchini kuwa na magari ya zimamoto pamoja na ya kubebea wagonjwa kwa ajili ya kutoa huduma pindi majanga yanapotokea kwenye maeneo yao ili kuharakisha utoaji wa huduma za dharura.

Pia amelitaka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kila Mtanzania aweze kuwa na uelewa wa kutoa huduma za awali pindi majanga ya moto yanapotokea katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kutumia vifaa vya kuzima moto.Waziri Mkuu ambaye alitembelea kituo cha Jeshi la Zimamoto cha Ilala amejionea magari ya kuzimia moto likiwemo la aina ya Bronto Sky Lift lenye uwezo wa kufika futi 54 na kuzunguka nyuzi 360. 

Alielezwa kuwa katika Bara la Afrika, magari ya aina hiyo yapo matatu tu, ambayo yapo nchini Tanzania, Misri na Afrika Kusini. Kwa upande wa Tanzania, gari hilo lilinunuliwa miaka 10 iliyopita kwa sh. bilioni 1.5. 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alitembelea Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura ya Maafa, ambapo aliwasisitiza viongozi wa kituo hicho kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara yatokanayo na kuishi kwenye maeneo hatarishi hususan mabondeni.

Waziri Mkuu alisema licha ya kuwapa elimu, pia wanatakiwa kuwashawishi wakazi wa maeneo hayo kuondoka kabla ya kutokea kwa maafa badala ya kusubiri majanga yatokee. Pia aliwataka wawe na mpango wa kuonesha eneo lenye maafa na kuujulisha umma.Pia aliwataka watendaji wanaohusika na kamati za maafa waimarishe mawasiliano katika ngazi zote kuanzia ya kijiji hadi Taifa na wafanye kazi kwa ushirikiano ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi pindi maafa yanapotokea.

Awali, Waziri Mkuualitembelea Ofisi za Mpiga Chapa wa Serikali jijini Dar es salaam ambapo mbali na mambo mengine alijionea moja kati ya mitambo ya kwanza ya Mpiga Chapa wa Serikali uitwao Original Heidelberg wenye zaidi ya miaka 100 ambao bado unafanya kazi vizuri. 


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, Juni 8, 2018.

Muogeleaji Natalia atamba kushinda mashindano ya kuogelea ya Marekani

$
0
0
Dar es Salaam. Muogeleaji wa Tanzania, Natalia Ladha ametamba kufanya vyema katika mashindano ya kuogelea ya kutafuta tiketi ya kufuzu kwa mashindano ya Olimpiki ya jimbo la Florida nchini Marekani yajulikanayo kwa jina la Florida Gold Coast Junior Olympic.

Natalia aliondoka nchini jana tayari kwa mashindano hayo yaliyopangwa kufanyika Martin County Juni 16 ambapo atajiunga na waogeleaji wa klabu ya Swimfast.

Muogeleaji huyo ambaye ni nyota kwa waogeleaji wa Tanzania wenye umri kati ya miaka tisa na 10, anashindana katika mashindano hayo makubwa matano Marekani kwa mara ya pili mfulilizo.

“Nimejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo na natarajia kufanya vyema kwa waogeleaji wenye umri kama wangu, nimejiandaa vyema katika nikiwa na makocha wangu wa klabu ya Taliss,” alisema Natalia.

Katika mashindano yam waka jana ya Miami, Natalia alishinda medali ya shaba kwa mita 50 na 100 kwa upande wa staili ya backstroke.

Natalia pia alitamba katika mashindano ya staili nyingine ambapo alitwaa medali ya dhahabu kwa mita 200 freestyle, 200 ( individual medley), 100m (backstroke),50m (butterfly) na medali ya fedha kwa mita 100 katika staili ya butterfly. Pia alishinda medali ya dhahabu kwa mita 100 katika freestyle.

Mbali ya mashindano hayo, Natalia pia atashiriki katika mashindano ya umri ya Coral Spring ambayo yataanza Juni 15 na kumalizika Juni 17 na vile vile mashindano ya Fort Lauderdale yaliyopangwa kuanza Juni 22 mpaka 24.

Vile vile atashiriki katika mashindano ya Sectionals, yaliyopangwa kuanza Julai 6 mpaka 9 ma Area championships yaliyopangwa kuanza Julai 13 mpaka 15, mjini Sunrise.

POLISI MORO WATOA UFAFANUZI MWANAMKE ALIYEJIFUNGUA NJIANI

$
0
0
Na John Nditi, Morogoro

POLISI mkoani Morogoro inaendelea na uchunguzi zaidi kuhusu mwanamke aliyejifungua mtoto wakati akiwa njiani kupelekwa Kituo cha Afya Mang’ula, wilaya ya Kilombero mkoani humo mara baada ya kutolewa mahabusu ili kubaini kama kuna uzembe wowote umefanywa na watendaji ama askari na ikibainika hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Mugabo Wekwe ,alisema hayo jana katika taarifa yake kwa waandishi wa habari juu ya tukio la kujifungua mtoto njiani mwanamke Amina Rafael Mbunda (27) mkazi wa Kijiji cha Kiswanywa , Tarafa ya Mang’ula , wilayani Kilombero , mkoa wa Morogoro.

Alisema , Polisi inaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio la mwanamke huyo aliyefikishwa katika kituo cha Polisi Mang’ula kwa kosa la kukutwa na mali ya wizi kisha kujifungua akiwa njiani kuelekea katika Kituo  cha Afya Mang’ula.

Alisema , Mei 31, mwaka huu ilifunguliwa kesi ya wizi wa samani mbalimbali zenye thamani ya Sh 1,040,000 katika kituo cha Polisi Mang’ula kilichopo wilayani Kilombero mkoani Morogoro zilizoibwa kwa vipindi tofauti katika karakana ya Joseph Mdee iliyopo maeneo ya Posta Mang’ula .

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa huyo alisema, baada ya tukio uchunguzi ulianza mara moja na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja alitwaje Ridhiwani Athuman na kukiri kuiba kisha kuwauzia watu mbalimbali akiwemo Abdallah Mohamed Mrisho (40) mkazi wa Kijiji cha Kiswanywa ,Tarafa ya Mang’ula.

Alisema ,askari walifika nyumbani kwa Mrisho kwa ajii ya upekuzi wakiwa na Mwenyekiti wa kijiji hicho pamoja na mlalamikaji na kumkuta mke wake aitwaye Amina Rafael Mbunda na kujitambulisha kisha kumweleza kuwa wanahitaji kufanya upekuzi.

Alisema , wakati wa upekuzi huo mlalamikaji alibaini kuwa fumbati “ base” ya mbele ya kitanda ikiwa katika kitanda kilichofungwa ni ya kwake na ilichukuliwa kama kielelezo pamoja na mwanamke huyo kwani ndiye aliyekutwa na mali hiyo ya wizi kisha kupelekwa kituo cha Polisi Mang’ula siku hiyo ya Mei 31, mwaka huu majira ya saa 12 jioni kwa hatua zaidi.

Alisema , kabla ya kuondoka na mtuhumiwa huyo, Mwenyekiti wa kijiji pamoja na askari walimjulisha mume wa mama huyo kwa njia ya simu kuwa mke wake amechukuliwa baada ya kukutwa na mali ya wizi na kupelekwa kituo cha Polisi Mang’ula na dhamana iko wazi na mume wa mama huyo aliahidi kuwa atafika kituoni akitoka katika shughuli zake.

Kaimu Kamanda huyo alisema ,mume wa mama huyo hakufika kituoni hapo na hakukuwa na ndugu wala jirani aliyefika kituoni kwa ajili ya kumwona au kuomba dhamana , hivyo ililazimika awekwe mahabusu kwa mujibu wa taratibu.

Alisema , ilipofika saa tisa usiku mama huyo ( Mtuhumiwa) alianza kulalamika kuwa anajisikia vibaya na anadhani huwenda ikawa ni uchungu ndipo askari walitafuta gari la kumpekea katika kituo cha afya na kutofanikiwa kuupata usafiri huo .

Kaimu Kamanda wa Polisi huyo alisema , mmoja kati ya askari aliyopo kituoni hapo aliamua kuchukua pikipiki yake kumbeba mama huyo pamoja na kukodi pikipiki nyingine ( Bodaboda) kisha kumpakia mama mmoja aliyeishi jirani na eneo la tukio aitwaye mama Kipangula kuelekea katika kituo cha afya Mang’ula.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi huyo ,mara tu baada ya kutoka Kituo cha Polisi wakielekea kituo cha Afya mama huyo alilalamika kuwa anataka kujisaidia , waliposimamisha pikipiki na mama huyo (mtuhumiwa )alishuka ndipo alipoanza kijifungua na kusaidiwa na mama Kipangula kisha kukimbizwa katika Zahanati iliyokuwa jirani na eneo hilo iitwayo Lugusha na kupatiwa huduma ya kwanza.

Alisema ,mara baada ya huduma hiyo, mama huyo aliwahishwa katika Kituo cha Afya Mang’ula ambapo alipokelewa akiwa salama yenye pamoja na mtoto ambaye ni wa kike na kuendelea kupata huduma kama akina mama wengine wanaojifungua nje ya Hospitali.

Katika hatua nyingine Mganga wa Kituo cha Afya Mang’ula ,Samweli Msomba akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu alisema licha ya yenye kutokuwepo siku ya tukio hilo , lakini mama huyo aliletwa katika Kituo hicho akiwa tayari amejifungua na kulazwa kwa uangalizi kwa muda wa siku tatu na baadaye aliruhusiwa kwenda nyumbani.

‘ Alisema , mtoto huyo ni wakike na alizaliwa akiwa na uzito wa kilo 3.5 na kwamba mama wa mtoto huyo hakuwa na tatizo baada ya kujifungua na alilazwa wodini kwa siku tatu ili kuona kama yapo madhara aliyapata wakati wa kujifungua .

“ Hakuwa na tatizo lolote baada ya kulazwa kwa muda wa siku tatu na aliruhusiwa , ambapo hali ya mwanake na mtoto walikuwa ni salama “ alisema Dk Msomba.

SERIKALI YASHAURIWA KUKABILIANA NA UKOSEFU WA USAWA KATIKA ULIPAJI KODI

$
0
0

Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU), Rashid Mtima (wa tatu kulia) akiwaongoza wajumbe wa warsha ya siku mbili iliyojadili usawa katika ulipaji wa kodi na manufaa yake katika kuboresha huduma za umma wakiimba wimbo wa ‘Mshikamano Daima’ wakati wa ufungaji wa warsha hiyo jijini Dar es Salaam. Walipendekeza serikali kupitia upya misamaha na mikataba ya kodi, kuwepo uwazi wa umiliki na faida wanazopata makampuni mbalimbali kuongeza uwezo wa TRA ili ikusanye mapato na fedha zitakazowezesha kujenga miundombinu na kuboresha huduma kwa umma. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)
Sehemu ya washiriki toka vyama vya wafanyakazi, asasi za kiraia makundi ya wanafunzi na vijana uliofanyika Tarehe 7 hadi 8 jijini Dar es Salaam wakifuatilia matukio wakati wa warsha iliyojadili maswala ya usawa katika ulipaji wa kodi na manufaa yake katika kuboresha huduma za umma. 
Mmoja wa washiriki akitoa mchango wake katika warsha iliyojadili maswala ya usawa katika ulipaji wa kodi na manufaa yake katika kuboresha huduma za umma.
 Everline Aketch mjumbe kutoka Nchini Togo na mjumbe mwingine Daniel Oberko pia toka nchini humo wakijadili jambo waliposhiriki warsha ya siku mbili iliyojadili usawa katika ulipaji wa kodi na manufaa yake katika kuboresha huduma za umma wakiimba wimbo wa ‘Mshikamano Daima’ wakati wa ufungaji wa warsha hiyo. 
Mmoja wa washiriki akitoa mchango wake katika warsha iliyojadili maswala ya usawa katika ulipaji wa kodi na manufaa yake katika kuboresha huduma za umma. 
Sehemu ya washiriki toka vyama vya wafanyakazi, asasi za kiraia makundi ya wanafunzi na vijana uliofanyika Tarehe 7 hadi 8 jijini Dar es Salaam wakifuatilia matukio wakati wa warsha iliyojadili maswala ya usawa katika ulipaji wa kodi na manufaa yake katika kuboresha huduma za umma. 

Sehemu ya washiriki wa warsha ya siku mbili iliyojadili usawa katika ulipaji wa kodi na manufaa yake katika kuboresha huduma za umma wakiimba wimbo wa ‘Mshikamano Daima’ wakati wa ufungaji wa warsha hiyo jijini Dar es Salaam. Walipendekeza serikali kupitia upya misamaha na mikataba ya kodi, kuwepo uwazi wa umiliki na faida wanazopata makampuni kuongeza uwezo wa TRA ili ikusanye mapato na fedha zitakazowezesha kujenga na kuboresha huduma kwa umma.
Mwakilishi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU), Shani Kibwasali akisoma maazimio ya wajumbe wa warsha ya siku mbili iliyojadili usawa katika ulipaji wa kodi na manufaa yake katika kuboresha huduma za umma Juni 8 2018. Walipendekeza serikali kupitia upya misamaha na mikataba ya kodi, kuwepo uwazi wa umiliki na faida wanazopata makampuni kuongeza uwezo wa TRA ili ikusanye mapato na fedha zitakazowezesha kujenga na kuboresha huduma kwa umma.
Sehemu ya washiriki toka vyama vya wafanyakazi, asasi za kiraia makundi ya wanafunzi na vijana uliofanyika Tarehe 7 hadi 8 jijini Dar es Salaam wakifuatilia matukio wakati wa warsha hiyo.
Sehemu ya washiriki toka vyama vya wafanyakazi, asasi za kiraia makundi ya wanafunzi na vijana uliofanyika Tarehe 7 hadi 8 jijini Dar es Salaam wakifuatilia matukio wakati wa warsha iliyojadili maswala ya usawa katika ulipaji wa kodi na manufaa yake katika kuboresha huduma za umma. 
Mwezeshaji Profesa wa Uchumi wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prosper Ngowi akitoa mada kuhusu Usawa katika ulipaji wa Kodi na manufaa yake kuboresha huduma za jamii kwa washiriki toka vyama vya wafanyakazi, asasi za kiraia makundi ya wanafunzi na vijana uliofanyika Tarehe 7 hadi 8 jijini Dar es Salaam wakifuatilia matukio wakati wa warsha iliyojadili maswala ya usawa katika ulipaji wa kodi na manufaa yake katika kuboresha huduma za umma. 

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA HOSPITALI YA MLOGANZILA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema ufumbuzi umepatikana wa changamoto kubwa ya umeme inayoikabili hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila na kuahidi kusimamia utendaji ili umeme upatikane muda wote.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila. Makamu wa Rais amesema kwa vifaa vya kisasa vya umeme vilivyopo hospitalini hapo havipaswi kupata umeme wa mashaka .

Makamu wa Rais amesema kuwa wananchi wengi hawajajua umuhimu wa kuwa na bima ya afya hivyo elimu zaidi itolewe ili wananchi wengi wachangie huduma ya afya kwa kupitia bima zao hii itawapunguzia gharama sana wakati wa matibabu.

Makamu wa Rais aliutaka uongozi wa Mloganzila kutangaza kwa wananchi huduma zinazopatikana hospitalini hapo ambapo wana vifaa vya kisasa kabisa kwa ajili ya uchunguzi wa afya, Makamu wa Rais alisema huduma ya kupima saratani ya matiti katika hospitali ya Mloganzila ni shilingi elfu 30 tu. Akiongea na Watumishi wa hospitali hiyo Makamu wa Rais amesema “ Mnaofanya kazi sekta ya afya mnafanya kazi ya Uungu”

Makamu wa Rais pia aliwasikiliza wananchi waliofika kwenye kupata huduma hospitalini hapo na kusema kuwa Serikali itajitahidi kushughulikia changamoto zinazojitokeza lakini aliwahimiza wananchi kuhakikisha wanakuwa na bima ya afya.

Mapema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alimuambia Makamu wa Rais kuwa (MAMC) Mloganzila ni kati ya hospitali saba zinazomilikiwa na serikali ambazo zinatoa huduma za matibabu ya kibingwa ngazi ya juu pia alimpongeza Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa kuweka msukumo wake katika huduma ya mama na mtoto ambapo juhudi za Makamu wa Rais zimezaa matunda ambapo leo hii kuna vituo 208 vimeboreshwa na kutoa huduma.

Wakati huo huo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Ole Nasha amesema wanafunzi 350 wa shahada ya kwanza wameanza kupata mafunzo ya udaktari na udaktari bingwa na kuishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuona umuhimu wa maendeleo ya upanuzi wa kamapsi hii ili kuruhusu udahili wa wanafunzi wengi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Dkt. Lulu Sakafu juu ya mashine ya kupimia saratani ya matiti wakati wa ziara yake katika hospitali yaTaaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu na Mwalimu wa masuala ya Meno Dkt. Elison Simon wakati wa ziara yake katika hospitali yaTaaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Amani Ahmada mwenye umri ya miaka 6, wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.
  Muonekano wa hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na wafanyakazi wa hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila wakati wa ziara yake iliyofanyika leo.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wanaopata huduma ya matibabu Mloganzila wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa Mradi Mhandisi Elly Kisoreka juu ya maendeleo ya ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi wakati wa ziara yake katika hospitali yaTaaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUTURISHA JIJINI MWANZA, AWATAKA WATANZANIA WASIKUBALI KUCHONGANISHWA

$
0
0
 Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wasikubali kuchonganishwa na kwamba Serikali haiongozwi kwa misingi ya kidini bali imeziachia taasisi za kidini zifanye kazi kwa kuzingatia Katiba , Sheria za nchi na malengo yaliyokusudiwa katika uanzishwaji wake. 

 Aliyasema hayo jana jioni (Jumamosi, Juni 9, 2018) alipozungumza na viongozi na wananchi wa Mkoa wa Mwanza baada ya kushirikiana nao katika futari aliyowaandalia. Shughuli hiyo ilihudhuriwa na waumini wa dini mbalimbali. 
 Waziri Mkuu alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanaishi kwa amani na utulivu, jambo litakalowawezesha kufanya shughuli zao kikamilifu, hivyo wasikubali kuchonganishwa kwa misingi yoyote. 

 “Nawaasa viongozi wa dini msikubali kutumia makundi mengine nje ya taasisi zenu kwa ajili ya kuwazungumzia masuala yenu kwa sababu watawachonganisha na Serikali ambayo haipo kwa ajili ya kugombana na taasisi yoyote,” alisisitiza. 
 Waziri Mkuu alisema jukumu kubwa la taasisi za kidini ni kuhakikisha wanawalinda waumini wao pamoja na kuwaongoza kwa kuwapa mafundisho mema yanayompendeza Mwenyezi Mungu, ambayo yatawawezesha kuishi kwa amani . 

 Alisema misingi ya amani na utulivu ikiwa pamoja na mshikamano walionao wananchi umesababisha Tanzania kupata heshima kubwa dunia kote, hivyo ni vema kila mwananchi ahakikishe suala la kudumisha amani linapewa kipaumbele. 

 Pia Waziri Mkuu alisema amefurahi sana kujumuika na wananchi wa Mkoa wa Mwanza katika futari hiyo, ambapo aliwapongeza kwa kukamilisha uundaji wa kamani za amani kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa. Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. John Mongella amlishukuru Waziri Mkuu kwa ukarimu wake kwa kuwaalika wakazi wa Mwanza katika hafla hiyo, ambapo alisema Mwanza ni kitovu cha amani kwa kanda ya Ziwa na nchi za Maziwa Makuu. 

 “Mwanza tumejipanga na tunashirikiana na taasisi zote kwenye njanja zote , tupo pamoja na tunashirikiana katika kuimarisha amani na utulivu. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli kwa kutuamini na tunamuahidi tutafuata falsafa zake katika utendaji wetu,”. 

 Kwa upande wake, Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza na Askofu wa Kanisa la Charismatic Episcopal Church of Tanzania (CECT), Charles Sekelwa alisema wao wanaiunga mkono Serikali katika kudumisha amani na wataendelea kushirikiana nayo. 

 Alisema awali kulikuwa na changamoto ya matabaka ya kidini iliyobabisha na kutoelewana baina ya waislamu na wakiristo, ambapo kamati yao ilifanya kazi ya kuyasulisha na sasa hali ni shwari. “Matabaka ya kiimani yameisha na watu wa dini zote wanashirikiana vizuri,”

Askofu Sekelwa alisema wao kama viongozi wa pande hizo mbili hawawezi kukubali kuona kunakuwa na matabaka ya kiimani miongoni mwa waumini, hivyo watakikisha wanaendelea kuwafundisha waumini wao umuhimu wa amani. 

 Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Akson, Naibu Waziri waNchi, OR – TAMISEMI, Joseph Kakunda, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali baadhi ya wananchi wa mkoa wa Mwanza

 Sehemu ya wakazi wa jiji la Mwanza wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika futari aliyoiandaa kwenye viwanja vya Benki Kuu jijini Mwanza Juni 9, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofuturisha kwenye viwanja vya Benki Kuu jijini Mwanza Juni 9, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika dua iliyoongozwa na Sheikh Khamis Almasi (wanne kushoto) baada ya kufuturisha kwenye viwanja vya Benki Kuu jijini Mwanza Juni 9, 2018.  Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI, Joseph Kakunda, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Jamal Abdul Babu na Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani inayojumuisha  viongozi wa dini zote ya mkoa wa Mwanza, Askofu Charles Sekelwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akigana na Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani inayojumuisha viongozi wa dini zote ya mkoa wa Mwanza, Askofu Charles Sekela baada ya kufuturisha kwenye viwanja vya Benki Kuu jijini Mwanza Juni 9, 2018.  Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI, Charles Kakunda na  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na Sheikh Khamisi Almasi. 
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha wakati alipowasili kwenye viwanja vya Benki Kuu jijini Mwanza kushiriki katika futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Juni 9, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu baada ya kufuturisha kwenye viwanja vya  Benki Kuu jijini Mwanza Juni 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

JAFO AKERWA NA KUSUASUA KWA UJENZI WA KITUO CHA MABASI MJI WA NJOMBE

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo ameonyesha kukerwa kutokamilika kwa ujenzi wa kituo cha mabasi cha mji wa Njombe licha ya serikali fedha zote za gharama ya ujenzi huo zaidi ya Sh. bilioni 10. 

Ujenzi wa kituo hicho ulianza tangu Desemba 2013 lakini hadi sasa haijakamilika. Kufuatia hali hiyo, Waziri Jafo amemjia juu mkandarasi aliyepewa kazi hiyo pamoja na upande wa usimamizi wa ujenzi huo na kudai kuwa umechelewa kukamilika kutokana na uzembe wao. 

“Hapo awali kazi hiyo ilikuwa ikifanywa na MASASI CONSTRUCTION kwa kujenga awamu ya kwanza na ya pili ambapo katika awamu hizo zimekamilika lakini kwa kuchelewa sana na kulazimika kutafutwa mkandarasi mwingine ili akamilishe awamu ya tatu ambayo ni ya mwisho kwa mradi huo,”amesema. 

Amebainisha kuwa awamu ya tatu Halmashauri ya mji wa Njombe wamempata mkandarasi mpya ambaye ni kampuni ya HAINAN INTERNATIONAL na amesaini mkataba mwezi Mei 2018 na anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo mwezi Februari 2019. 

Jafo amewaonya wakandarasi ambao wanachukua kazi lakini wanapopewa kazi wanaleta ubabaishaji katika kukamilisha kazi hizo. Amemuagiza mkandarasi huyo mpya kukamilisha mradi huo ndani ya muda uliopangwa ili wananchi waweze kupata huduma bora kama serikali ilivyokusudia. 
Waziri Jafo, kabla ya kutembelea kituo hicho, alisimamia harambee ya kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati wa shule ya sekondari Makoga iliyopo wikayani Wanging’ombe ili iweze kupokea wanafunzi wa kidato cha tano hapo mwezi Julai 2018. 

Katika harambe hiyo kiasi cha sh.Milioni 137 zilichangwa na wananchi wa Wanging'ombe na wadau mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Njombe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akisisitiza jambo kwa wakandarasi wapya wanaojenga Kituo cha mabasi cha Mji wa Njombe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe baada ya kukagua ujenzi wa Kituo cha mabasi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akisikiliza taarifa ya ujenzi wa Kituo cha mabasi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akipanda mti wa Matumaini kabla ya Harambee ya shule ya Makoga mkoani Njombe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akiendesha zoezi la Harambee katika wilaya ya wanging'ombe kwa ajili ya sekondari ya Makoga.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images