Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

MANISPAA YA UBUNGO YAIKABIDHI CRDB BANK BILLIONI 1.947 YA MIKOPO YA WANAWAKE NA VIJANA.

$
0
0
Leo Tarehe 18 April 2018,Halmashauri Ya Manispaa ya Ubungo,Imeingia Mkataba wa Makabidhiano na Kutoa Huduma ya Mikopo ya Wanawake,Vijana na walemavu na Benki ya CRDB,Kwa Niaba ya Halamshauri.

Mstahiki meya,Boniface Jacob ametiliana Saini ya Mkataba na Benki ya CRDB ambapo  wametiliana saini Ya utoaji wa Huduma hiyo.

 Fedha za Kuanzia Shughuli hiyo Kiasi cha Shillingi Billioni 1.947 Zitapelekwa Benki ya CRDB kwa ajili ya Ugawaji wa Fedha hizo kwenye Vikundi Mbalimbali vya wanawake(40%) Vijana(40) na walemavu(20)*

Ambapo kiasi kikubwa Billioni 1.947 kitaifanya Halamshauri Kuvunja Rekodi kwa Kuwa Halmashauri Ya kwanza DSM na Tanzania kuwahi kutoa kiasi kingi cha fedha kwa ajili ya Mikopo ya Vijana,wanawake na kundi Maalum la walemavu

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo,Bw.John Kayombo,ameeeleza kuwa fedha hizo ni sehemu ya asilimia 10,za Mapato ya ndani yaliyokuwa yakitengwa na Halmashauri,Kwa Muda wa Mwaka Mmoja,Pamoja na fedha za Mgawanyo wa Halamshauri kutoka Manispaa ya Kinondoni.

Aidha Mstahiki Meya,Boniface Jacob Ameeleza kuwa; Halamashauri Ya Manispaa ya Ubungo imefikia hatua ya  kutiliana Saini na Benki ya CRDB baada ya Kushindanisha Mabenki yote ya Tanzania,na Kuangalia Benki yenye Huduma Nzuri kwa wajasiriamali  wake,itakayo kubali kutoa Riba ndogo kwa Wajasiriamali,Na kukubali kuchangia shughuli za Utoaji Huduma hiyo ya kukagua na kuvisaidia Vikundi vya wakopaji.

Mpaka Leo wakina mama 11,312 na Vijana 1,224 wameshajaza fomu za Maombi ya Mikopo kutoka  Halmashauri,kwa kata zote 14 na Mitaa 91 ,Huku wito ukitolewa kwa vijana baada ya  Idadi Ndogo ya Vijana kujotokea kulinganisha na akina Mama.

Mstahiki meya Amewashukuru Wataalamu wakiongozwa na Mkurugenzi,wabunge na Madiwani wote,kwa Ushirikiano na Jitihada za Kuibadilisha Manispaa ya Ubungo

IMETOLEWA Na
OFISI YA MSTAHIKI MEYA
MANISPAA YA UBUNGO
18-04-2018

Wadau wa dawa na vifaa tiba nchini watakiwa kuchangamkia fursa

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Josephat Kandege amewataka wauzaji, waagizaji, wasambazaji na wadau wote wa dawa pamoja na Vifaa Tiba Nchini kuchangamkia fursa inayotolewa na Serikali ya kuwa Mshitiri mteule ‘Prime Vendor’ kusaidia katika utoaji wa dawa katika Mikoa yote Tanzania.

Kandege ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Wadau wa dawa  ‘Vendors Forum’ kilichoandaliwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na wadau wa Afya ‘HPSS’ chenye lengo la kuweka uelewa wa pamoja kuhusu uanzishwaji na utekelezaji wa mfumo wa Mshitiri.

Amesema “mfumo huu utatumika kupata mahitaji ya bidhaa za Afya pale ambapo vituo vya kutolea huduma za Afya vya Umma vitakosa au kupata kiwango pungufu toka Bohari Kuu ya Dawa na pia utasaidia kupunguza kero za Afya ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya”.

Sasa basi ninyi kama wazabuni muhimu katika sekta hii ya Afya wenye Uzalendo na nia njema na Nchi ya Tanzania mnatakiwa kujitokeza katika mchakato wa kumpata Mshitiri (Prime Vendor) wa kila Mkoa ambaye atakidhi vigezo kwa mujibu wa taratibu manunuzi alisema Mhe. Kandege.

Wakati huo huo Naibu Waziri Kandege aliwafahamisha wadau wa dawa kuwa Serikali imagatua mipango na bajeti kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya na inapeleka Fedha moja kwa moja kwenye akaunti za benki zilizofunguliwa katika kila kituo hii itasaidia katika kufanya manunuzi ya dawa hizo na kurahisha mchakato wa malipo.

“Hivyo niwahakikishie kuwa utaratibu wa malipo utakua ni rahisi na wa haraka zaidi kwa kuwa Hospital, Vituo vya Afya na Zahanati husika zitahusika kuagiza dawa kwa Mshitiri pale mahitaji ya dawa hizo zitakapokosekana kutoka MSD” alisema Mhe. Kandege.

Alimalizia kwa kuwataka Wadau wote wa Dawa kutumia kikao hiki kuelewa kwa undani kuhusu utaratibu huu na kujitokeza kwa wingi katika mchakato wa kumpata Mshitiri Mteule kwani zoezi hili litaendeshwa kwa uwazi na kwa usindani mkubwa.

Mkurugenzi wa Afya Ofisi ya Rais Tamisemi Dr. Ntuli Kapologwe amesema hivi sasa wako katika uwekezaji Mkubwa katika Sekta ya Afya kwa kuzingatia kuwa Bajeti ya Dawa imeongezwa kutoka Bil 31 kwa mwaka 2015/16 hadi kufikia Bil 269 kwa mwaka 2017/18 hivyo ongezeko hili la bajeti linatakiwa kwenda sambamba na uhakika wa upatikanaji wa dawa na zenye ubora chini ya usimamizi makini wa wataalamu wa Afya.

Dr. Ntuli alisema mpango huu utaleta manufaa kwa wananchi wote ambao watakua chini ya mpango wa Tele kwa Tele na wale wanaopata huduma kupitia mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa; Tunataka kila mmoja apate dawa anayoihitaji kwa wakati.

Naye Mfamasia toka Ofisi ya Rais Tamisemi Regina Richard alisema mfumo wa Mshitiri Mteule umeanzishwa kwa sababu ya changamoto zilizoonekana awali za kutumia mzabuni kama vile taratibu za manunuzi kuchukua muda mrefu na gharama za manunuzi kuwa kubwa na zinazotofautiana kati ya Halmashauri moja na nyingine ndani ya Mkoa mmoja.

Changamoto zingine alizozibainisha ni kubadilika kwa bei mara kwa mara kila manunuzi yanapofanyika, kutokuwa na uhakika wa ubora wa bidhaa kutokana na kuhifadhiwa na kusafirishwa katika mazingira mbayo si salama na zaidi baadhi ya wazabuni na watumishi kutokuwa waaminifu.

Matumizi ya mfumo huu umeelekezwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi, Sera ya Afya ya Taifa ya mwaka 2007, Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya na Sera ya Mashirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi.
Kikao hiki cha wadau wa dawa ‘Vendor Forum’ kimefanyika kwa mara ya kwanza na kimehusisha wadau kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.
 Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege(mbele) akifungua kikao cha wadau wa Afya ‘Vendor Forum’ kilichofanyika katika Ukumbi wa Dodoma Hotel.
  Mkurugenzi wa Afya Ofisi ya Rais Tamisemi Dr. Ntuli Kapologwe akitoa maelezo ya awali kabla hajamkaribisha mgeni rasmi kufungua kikao cha wadau wa Afya Vendor Forum.
 Mfamasia Mwandamizi  toka Ofisi ya Rais Tamisemi Regina Richard akielezea malengo la kikao cha Wadau wa Dawa ‘Vendor Forum’ kilichofanyika katika ukumbi wa Dodoma Hotel mapema leo.
  Wataalam toka Idara ya Afya Ofisi ya Rais-TAMISEMI pamoja na wadau wa Dawa wakiwa katika kikao maalum cha wadau wa dawa.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege(mbele katikati) katika picha ya pamoja na baadhi ya wataalamu na wadau wa dawa.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke, ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke, ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

UJANGILI NCHINI WAPUNGUA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 - DK. KIGWANGALLA

$
0
0

Na Hamza Temba-Dodoma

Serikali imefanikiwa kudhibiti vitendo vya ujangili hapa nchini kwa zaidi ya asilimia 50.

Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla wakati akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma.

Mazungumzo hayo yalilenga kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta ya uhifadhi na maendeleo ya utalii.Dk. Kigwangalla alisema katika kipindi cha miezi sita iliyopita hakuna mauaji mapya ya wanyamapori yaliyoripotiwa na kwamba nyara zinazokamatwa hivi sasa ikiwemo meno ya tembo na ngozi za wanyamapori ni masalia ya zamani.

Amesema mafanikio hayo yametokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali kudhibiti vitendo vya ujangili ikiwemo doria za mara kwa mara za kiitelijensia ambazo zimekuwa zikishirikisha vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama pamoja na raia wema. 

Alisema Serikali itaendelea kudhibiti vitendo hivyo kwa kuimarisha ulinzi katika maeneo ya hifadhi nchini ikiwa ni pamoja na kuanzisha jeshi maalum la usimamizi wa Misitu na Wanyamapori, Sheria ya wanyamapori na za taasisi za uhifadhi zimeanza kufanyiwa marekebisho kuwezesha mabadiliko hayo.

Katika hatua nyingine Dk. Kigwangalla amemueleza balozi Cooke kuwa, Serikali kupitia Wizara yake inaendelea kuimarisha  vivutio vya utalii hapa nchini kwa kupanua jeografia ya maeneo ya utalii sambamba na kuongeza vivutio ili kuongeza idadi ya watalii na mapato.

Amesema Serikali itajenga makumbusho ya Marais Wastaafu wa Tanzania mjini Dodoma pamoja kuanzisha makumbusho ya meno ya tembo katika miji ya Dar es Salaam, Arusha, Iringa na Dodoma.

Sambamba na hayo amesema Serikali itaanzisha mwezi maalum wa maadhimisho ya urithi wa Mtanzania ambao utafanyika mwezi Septemba kila mwaka pamoja na kuendeleza utalii wa mikutano.

Amesema Serikali pia itaanzisha Mamlaka ya Usimamizi na Uendelezaji wa Fukwe nchini ili kuimarisha utalii wa fukwe pamoja na kutambua barabara iliyokuwa ikitumika katika biashara ya utumwa wakati wa ukoloni ili iweze kutumika kiutalii.

Akizungumzia migogoro ya mipaka iliyopo baina ya wananchi na maeneo ya hifadhi, Dk. Kigwangalla alisema Serikali itatatua migogoro hiyo kwa kushirikisha wananchi sambamba na kuwasaidia kutatua changamoto za msingi ambazo ni kuimarisha maeneo ya malisho ya mifugo, upatikanaji wa maji kwa ajili ya wananchi na mifugo, mpango bora wa matumizi ya ardhi na uendelezaji wa kilimo na ufugaji.

Kwa upande wake balozi Cooke alisema nchi yake itaendelea kuimarisha ushirikiano inaoutoa kwa Serikali ya Tanzania katika kudhibiti mtandao wa uhalifu wa madawa ya kulevya, rushwa na ujangili.

Alisema kwa sasa watalii zaidi ya 75,000 wa Uingereza hutembelea Tanzania kila mwaka na wengine wamewekeza katika sekta utalii hapa nchini, hivyo akaiomba Serikali kurekebisha baadhi ya changamoto chache zilizopo katika sekta hiyo kwenye mtiririko wa kodi. 


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma jana ambapo walijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya uhifadhi na maendeleo ya utalii.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma jana ambapo walijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya uhifadhi na maendeleo ya utalii.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla.
 Balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiaga na balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma jana baada ya mazungumzo yaliyolenga walijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya uhifadhi na maendeleo ya utalii.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na msafara wa balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma jana ambapo walijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya uhifadhi na maendeleo ya utalii.

ALI KIBA AFUNGA NDOA YA KIFAHARI MJINI MOMBASA NCHINI KENYA,KURUSHWA LIVE JIONI YA LEO

$
0
0
 
Mwanamuziki mahiri wa Bongofleva nchini Ali Kiba, leo amefunga ndoa na Binti wa Kimombasa ajulikanae kwa jina la Bi.Amina Khalef,ndoa hiyo imefungwa katika msikiti wa Ummu Kulthum uliopo mjini Mombasa nchini Kenya,ambapo hafla hiyo imehudhuriwa na watu wa aina mbalimbali wakiwemo mashuhuri .Aidha taarifa zinaeleza kuwa Harusi hiyo itakayokuwa ya aina yake itarushwa LIVE  na kituo cha televisheni ya AZAM jioni ya leo.
Mwanamuziki mahiri wa Bongofleva nchini  Ali Kiba akizungumza na 'mpambe' wake leo wakati akifunga ndoa na Binti wa Kimombasa ajulikanae kwa jina la Bi.Amina Khalef,ndoa hiyo imefungwa katika msikiti wa Ummu Kulthum uliopo mjini Mombasa nchini Kenya.
 Alikiba akifurahia jambo na marafiki zake mara baada kufunga ndoa 
 Ali Kiba akifurahia jambo akiwa na ndugu,jamaa na marafiki zake waliomsindikiza kwenye kuchukua 'jiko' mapema leo asubuhi huko mjini Mombasa. 
Msanii alikiba na Wapambe wake wakielekea kufunga ndoa.

Waziri Mhandisi Kamwelwe aainisha mikakati ya Serikali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya Maji

WAGONJWA 19,371 WATIBIWA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KUTOKA JANUARI HADI MACHI 2018.

$
0
0
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kipindi cha miezi mitatu ya Januari hadi Machi 2018 imeona jumla ya wagonjwa 19,371 wenye matatizo mbalimbali ya moyo kati ya hao wagonjwa wa nje ni 18,481 na waliolazwa ni 890.

Wagonjwa 105 walifanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua kati ya hao watu wazima 53 na watoto 52. Kati ya wagonjwa 105 waliofanyiwa upasuaji 66 walifanyiwa na madaktari wetu bingwa wa magonjwa ya moyo watoto wakiwa ni 35 na watu wazima 31.

Upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab ulifanyika kwa wagonjwa 231 kati ya hao watoto ni 20 na wakubwa 211. Kati ya wagonjwa 231 waliotibiwa wagonjwa watu wazima 211 walifanyiwa upasuaji na madaktari wetu wa ndani.

Kwa kipindi cha miezi mitatu tumekuwa na jumla ya kambi za matibabu nane (8) ambapo tulifanya matibabu kwa kushirikiana na washirika wetu kutoka nchi za Ujerumani, Israel, Australia , Marekani, India na Falme za Kiarabu. Katika kambi hizo jumla ya wagonjwa 39 walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua kati ya hao watoto 17 na watu wazima 22. Wagonjwa 72 walifanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua kati ya hao watoto 20 na watu wazima 52.

Tumefanya upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu (AVF- Arterio Venous Fistula) kwa ajili ya kusafishia damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo (Hemodialysis) 36.

Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo ni wagonjwa wengi tunaowapokea mioyo yao kutokuwa katika hali nzuri hivyo basi tunawaomba wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hii itawasaidia kujuwa kama wana matatizo ya moyo au la na kama wanamatatizo wataweza kupata tiba kwa wakati.

Wazazi na walezi tunawaomba wasisahau kupima afya za watoto wao pale watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi ya moyo yanaanzia utotoni. Mtoto akianza kuuguwa magonjwa ya moyo wazazi wengi wanadhani ni matatizo ya kifua baada ya kumfikisha Hospitali na kufanyiwa vipimo ndipo inagundulika mtoto anasumbuliwa na magonjwa ya moyo. Kwa wamama wajawazito wafanye uchunguzi (Fetal Echocardiography) wa kuangalia kama mtoto aliyeko tumboni anamatatizo ya moyo.

Aidha kwa upande wa gharama za matibabu Taasisi yetu imeyagawa katika makundi manne (4) tuna wagonjwa wanaotibiwa kwa bima mbalimbali ambazo tumeingia makataba nazo. Wagonjwa wanaolipia gharama zote wenyewe, wagonjwa wanaochangia kidogo huku gharama zingine zikilipwa na Serikali. Kundi la mwisho ni wagonjwa ambao hawalipii kabisa gharama za matibabu ikiwa watakidhi vigezo vyote vya kutokulipa.

Huduma zetu za matibabu ya moyo zinatolewa kwa watanzania wote wa Bara na Visiwani. Ifahamike kwamba fedha za matibabu zinazolipwa na wagonjwa zinatumika kununua vifaa tiba vya moyo kama mlango wa moyo (Valve), betri ya moyo (Pacemaker) na vinginevyo.

Kutokana na matibabu ya moyo kuwa ya gharama kubwa tunaendelea kuwasisitiza wananchi wajiunge na mifuko ya bima za afya ambayo itawasaidia kulipa gharama za matibabu pindi watakapohitaji kutibiwa. Pia itasaidia Hospitali yetu kuendelea kujiendesha yenyewe kwa kushirikiana na Serikali na wadau wengine.

Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
19/04/2018

TCAA YAAGIZWA KUSIMAMIA USAFIRI WA ANGA

$
0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari wakati akitoa maelezo ya awali kabla ya ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la Mamlaka hiyo, mjini Dodoma.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la Mamlaka hiyo, lililofanyika mjini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari nyaraka mbalimbali mara baada ya kulifungua mjini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) lililofanyika mjini Dodoma. 


……………


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ameitaka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), kusimamia usafiri wa anga kwa kuzingatia taratibu na kanuni za usafiri huo ili kuweka uwiano wa haki kwa waendeshaji na abiria wanaotumia usafiri huo.


Ametoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati akizindua rasmi Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo na kuwapongeza kwa kuamua kuweka mikakati ya kununua rada nne kwa kutumia fedha za ndani.


“Lazima msimamie kanuni na taratibu zilizopo, wajibu wenu ni kutoa haki kwa watumiaji na abiria kwa usawa, hatutaki kusikia mnakandamiza watumiaji wa usafiri na mkisimamia vizuri eneo hili mtafanya idadi ya watumiaji kuongezeka na makampuni kuendelea kuwekeza zaidi kwenye usafiri” amesisitiza Prof. Mbarawa.

Waziri Prof. Mbarawa amesema yeyote anaevunja taratibu zilizowekwa kwenye usafiri wa anga Mamlaka hiyo ichukue hatua stahiki kulingana na taratibu zilizopo ili usafiri huo uweze kuwa na nidhamu.

“Kila Kampuni mkiiachia ifanye inavyotaka hatutafika popote na malalamiko kwenye usafiri wa anga yataendelea kuwepo, hivyo naomba msimamie makampuni haya kwa ukaribu mkubwa,’ amesisitiza Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa ili mamlaka ifikie lengo na kufanikiwa lazima Menejimenti ishirikishe watumishi kwa karibu ili kutimiza malengo iliyojiwekea.Prof. Mbarawa amesisitiza umuhimu wa TCAA kuwawezesha watumishi wake kitaaluma na kimaslahi ili kuongeza tija katika kazi na kufikia malengo ya utendaji Kitaifa na Kimataifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Bw, Hamza Johari, amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa TCAA imejipanga kutekeleza miradi mbalimbali kwa kutumia vyanzo vya ndani ili kuvutia makampuni ya ndege ya ndani na nje ya nchi.“Nikuhakikishie kuwa tumejipanga kutekeleza miradi mingi zaidi kwenye usafiri wa ndani ili kuchochea kasi ya usafiri huo lakini pia kutimiza amza ya kuboresha usafiri huo, ”amesema Johari.

Ameongeza kuwa kwa sasa mamlaka iko kwenye hatua za awali za utekelezaji wa mradi wa kufunga vifaa maalum vya kuwezesha ndege kwa usalama katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Zanzibar ambapo mradi huo ukikamilika utaimarisha huduma za kuongozea ndege katika kiwanja hicho.

MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA WANUNUZI WA PAMBA NCHINI NA WAKUU WA MIKOA INAYOLIMA PAMBA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Chama Wanunuzi wa Zao la Pamba Tanzania pamoja na Wakuu wa Mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma, Mara, Morogoro, Manyara, Mwanza, Singida, Simiyu, Shinyanga na Tabora, Ofisini kwa Waziri Mkuu, bungeni mjini Dodoma, Aprili 19, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI MBADALA BENKI YA DUNIA, KANDA YA AFRIKA

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wakwanza kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe (hayumo pichani) kuhusu mpango kazi wa kuboresha uwekezaji Tanzania. Kushoto kwake ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga na Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha Dkt. Yamungu Kayandabila.
Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe (kulia) akimsikiliza kwa makini Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayumo pichani) wakati wa majadiliano ya namna ya kuendeleza miradi ya maendeleo nchini Tanzania, kushoto kwake ni Mshauri wa Mkurugenzi huyo Bw, Zarau Kibwe.
Picha ya pamoja ya wajumbe walioshiriki majadiliano ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe kuhusu uboreshaji wa sekta binafsi, miradi ya maendeleo, ukuaji wa uchumi pamoja na sekta ya ukuaji wa viwanda. Wanaopeana mikono kulia Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)kushoto Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe. Kutoka kulia ni Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha Dkt. Yamungu Kayandabila, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere, wa pili kushoto ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga na wa pili kushoto ni Mshauri wa Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, kanda ya Afrika Bw, Zarau Kibwe.


………………


Na. WFM- Washngton DC

Mikutano ya Bodi ya Magavana ya Shirika la Fedha la Kimataifa na kundi la Benki ya Dunia kwa mwaka 2018 imeanza rasmi mjini Washington D.C. Katika mikutano hiyo kutakuwa na Magavana, Mawaziri wa Fedha, Sekta Binafsi pamoja na Wanataaluma mbalimbali kuweza kujadili hali ya uchumi wa dunia pamoja na kupunguza umasikini.

Katika mikutano hiyo Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) alifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe, kuhusu maendeleo ya hali ya uchumi wa Tanzania huku akisisitiza kwamba ni wakati mzuri sasa wa kusemea hali ya uchumi wetu kwa nguvu zote.

Akiendelea kutoa ufafanuzi Dkt Mpango alieleza hatua ambazo Serikali imezifanya ili kuweka mazingira mazuri katika sekta binafsi, na kwamba Serikali imeandaa mpango kazi wa kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji katika Taifa la Tanzania.

Pia Waziri Mpango alielezea miradi mikubwa ambayo nchi imeanza kuitekeleza, ikiwamo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa na Ujenzi wa Bwawa kubwa la kuzalisha Umeme wa Megawati 2100 la ‘Steigler’s Gorge’ katika Maporomoko ya Maji ya Mto Rufiji. 

Kupitia miradi hiyo ambayo Serikali imepanga kuifanikisha kwa wakati Dkt. Mpango alimuomba Bw. Bvumbe kuendelea kuzungumza na uongozi wa Benki ya Dunia ili uweze kutusaidia katika kuwezesha uwekeza katika miradi hiyo.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe alisema kuwa anaipongeza Tanzania kwa jitihada inazozionesha hasa katika kupambana na rushwa na ametutia moyo tuendelee na juhudi zetu za kuimarisha uchumi wetu hususani katika sekta ya kilimo na pia amefurahishwa na hatua mbalimbali zinazofanya kwa ajili ya kuendeleza sekta ya viwanda.

DK.SHEIN AKUTANA NA MAKAMU WA SHIRIKA LA NDEGE LA MISRI EGYPTAIR LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Makamo wa Rais wa Shirika la Ndege la Misri EGYPTAIR Bw.Mohamed Alabbady alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na Ujumbe aliofuatana nao
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Makamo wa Rais wa Shirika la Ndege la Misri EGYPTAIR Bw.Mohamed Alabbady (katikati) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na Ujumbe aliofuatana nao
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Makamo wa Rais wa Shirika la Ndege la Misri EGYPTAIR Bw.Mohamed Alabbady alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na Ujumbe aliofuatana nao (hawapo pichani),
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akibadilishana mawazo na Makamo wa Rais wa Shirika la Ndege la Misri EGYPTAIR Bw.Mohamed Alabbady (kushoto) mara baada ya mazungumzo yao yalifanyifika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na Ujumbe aliofuatana nao (wa pili kulia) Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Misri Meja Jenerali Issa Suleiman Nassor na Kaimu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ofisi ya Zanzibar Bw.Mohamed Haji Hamza(wa pili kulia),

Picha na Ikulu

SERIKALI ITAHAKIKISHA INAULINDA, INADUMISHA NA KUUENZI MUUNGANO WETU

TANZANIA KUNADI VIVUTIO VYA UTALII DUNIANI KUPITIA TAMASHA LA URITHI WA UTAMADUNI WA MABARA NCHINI UFARANSA

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha pili cha wadau wa utalii kutoka nchi mbalimbali zinazohusika na tamasha la ‘Urithi wa Utamaduni wa Mabara’ Jijini Dar es Saalam jana.

...........................................

Tanzania ni miongoni mwa nchi 54 za bara la Afrika zitakazoshiriki katika tamasha la ‘Urithi wa Utamaduni wa Mabara’ linalotarajiwa kufanyika nchini Ufaransa katika mji wa ‘Cherbourg’ mwezi Julai mwaka huu.

Tanzania inashiriki tamasha hilo la kihistoria kwa mara ya kwanza ambapo itapata fursa ya kutangaza utamaduni wake na vivutio vya utalii vya mambo ya kale hivyo kuongeza idadi ya watalii na mapato.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha pili cha wadau wa utalii kutoka nchi mbalimbali zinazohusika na tamasha hilo Jijini Dar es Saalam jana, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, alisema tamasha hilo litatoa fursa pana kwa nchi kutangaza vivutio vyake ikiwemo vile vya Zamadamu.

“Kimsingi tamasha hilo linatarajiwa kutoa fursa kwa Tanzania kutangaza vivutio vyake na hivyo kuvutia watalii wengi kuja nchini, kila nchi itapewa banda lake la kuonyesha vivutio vyake , Tanzania naamini inakuwa na vivutio vingi vyenye kupendeza watalii kama vile Zinjathropus, Ngoma za makabila mbalimbali pamoja na nyimbo.

“Baada ya tamasha hilo, kutakuwa na ongezeko kubwa la watalii nchini na ninaamini hata zile nchi ambazo hazina rekodi nzuri ya kuja Tanzania kwa wingi  zilizopo Bara la Asia zitaanza kuja,’’. alisema Kigwangla.

Alisema tamasha hilo linalotarajiwa kuhusisha takriban nchi zote za bara la Afrika, zaidi limelenga kutangaza tamaduni na vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo katika mataifa yote yatakayoshiriki  huku likitajwa kuwa tamasha bora na kubwa  la utalii pengine kuliko matamasha mengine yote kutokana na kila nchi kujitokeza kuonyesha vivutio vinavyopatikana katika mataifa yao.

“Tanzania tunavyo vivutio mbalimbali tunavyotarajia kwenda kuvionyesha katika tamasha hilo, ukiacha vivutio vya mambo kale, tuna bonde la Olduvai Gorge na mengineyo, tunayoamini kuwa  kupitia tamasha hilo tutaweza kuyatangaza na hivyo kuvutia watalii wengi kuja nchini” alisema Dkt. Kigwangalla. 

Hata hivyo alisema baada ya kukamilika kwa tamasha hilo, Septemba mwaka huu hapa nchini kutakuwa na tamasha la ‘Urithi wa Mtanzania’ linalotarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza na litakuwa likifanyika kila mwaka kuadhimisha urithi wa Mtanzania.

Alisema tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika kwa kipindi cha mwezi
mzima, pia litatoa fursa kwa kila wilaya kutangaza vivutio vyake, huku akizitaka kila wilaya kujiandaa na tamasha hilo, litakalotoa fursa pia kwa mikoa na wilaya hizo kukuza utalii wa maeneo yao.
 Waziri Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.
 Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Asngya Bangu akiongoza zoezi la utambulisho.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha pili cha wadau wa utalii kutoka nchi mbalimbali zinazohusika na tamasha la ‘Urithi wa Utamaduni wa Mabara’ Jijini Dar es Saalam jana.
 Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Prof. Audax mabula akizungumza katika mkutano huo.
 Picha ya pamoja ya Waziri Kigwangalla na washiriki wa mkutano huo.
 Waziri Kigwangalla akifurahia jambo na baadhi ya washiriki wa mkutano huo.

UTT AMIS PLC YATOA ELIMU YA UWEKEZAJI WA PAMOJA KWA WASTAAFU WATARAJIWA WA WAKALA WA MISITU TANZANIA

$
0
0
Ofisa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS PLC, Bi. Martha Mashiku, akitoa elimu ya uwekezaji wa pamoja kwa wastaafu watarajiwa wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania katika Ukumbi wa Mkutano wa Hoteli ya Kings Way mkoani Morogoro. (Na Mpiga Picha Wetu).
 Baadhi ya washiriki wakipata elimu juu ya Uwekezaji wa Pamoja kwa wastaafu watarajiwa wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom yaingia ubia wa kibiashara kampuni ya iflix

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix, Paul Coogan (Kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi (katikati) wakati alipokuwa akiongea kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya iflix na Vodacom. Wateja watapakua apllication ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix, Paul Coogan (Kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi (katikati) wakati alipokuwa akiongea kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya iflix na Vodacom. Wateja watapakua apllication ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix, Paul Coogan (Kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi (katikati) wakati alipokuwa akiongea kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya iflix na Vodacom. Wateja watapakua apllication ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya iflix na Vodacom. Wateja watapakua aprication ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# . Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix Paul Coogan na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix Tanzania, Paul Coogan (Kushoto) Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Hisham Hendi (katikati) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia) wakiwa kwenye uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya iflix na Vodacom. Jijini Dar es Salaam. Wateja wa Vodacom watapakua aprication ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# . Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Hisham Hendi (kulia) akikabiziwa zawadi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix Tanzania, Paul Coogan (Kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya iflix na Vodacom. Jijini Dar es Salaam. Wateja wa Vodacom watapakua aprication ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# . Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia) akiteta jambo na Meneja Masoko wa Kampuni ya Iflix Afrika Mashariki, Bernice Macharia, jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya iflix na Vodacom. Wateja mtandao wa wa Vodacom watapakua aprication ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# . Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia akikabiziwa zawadi na Meneja Masoko wa Kampuni ya Iflix Afrika Mashariki, Bernice Macharia, jijini Dar es Salaam, (wapili kushoto) wakati wa uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya iflix na Vodacom. Wateja mtandao wa wa Vodacom watapakua aprication ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# . Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix Tanzania, Paul Coogan na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi.


Kutana na burudani bila kikomo: Vodacom Tanzania yaingia ubia na iflix

Dar Es Salaam, 19 Aprili, 2018 – Kampuni yenye mtandao wa simu za mkononi unaoongoza, Vodacom Tanzania PLC leo imetia saini mkataba wa ubia na kampuni ya iflix, yenye kutoa huduma ya burudani inayoongoza katika nchi zinazoendelea ili kuwapa wateja wa Vodacom huduma hiyo ya iflix bila kikomo. Kampuni hii ya burudani inawapa wateja wa Vodacom uwezo wa kuangalia maelfu ya vipindi bora duniani, sinema na mengine mengi kwenye kila kifaa walicho nacho.

Mteja anatakiwa kupakua App ya iflix, ambapo hakutakuwa na malipo ya aina yeyote. Lakini kuna vifurushi maalum Mteja atabonyeza *149*01# kisha chagua intanet halafu kifurushi ikifuatiwa na iflix. Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 na cha mwezi kwa shilingi 18,000.

Akiongea na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa kitengo cha Biashara Hashim Hendi alisema: “Vodacom, kampuni ya mawasiliano inayoongoza nchini imedhamiria kuiingiza Tanzania katika dunia ya kidijitali na njia mojawapo ya kudhihirisha hili ni kwa dhamira yetu ya kuwapatia wateja burudani isiyo na kifani ya kidijitali. Leo hili linahakikishwa kwa ubia wa kihistoria na kampuni ya iflix. Kuwahakikishia lengo letu la kutoa huduma inayomlenga mteja, siyo tu kuwa tunawapa wateja wetu uwezo wa kufikia burudani bora duniani lakini pia tunajenga jukwaa ambalo wasanii wataweza kutumia kuuza kazi zao. Hii ni hatua kubwa sana kwa Vodacom ikielekea kuwa kampuni ya kidijitali inayoongoza barani Afrika ambayo inawezesha maisha ya kidijitali ya wateja wetu. Tunafurahia sana kuwaleta wateja wetu zaidi ya milioni 12 kwenye huduma za iflix.”

Makubaliano haya yanakuja wakati wa mabadiliko makubwa kwenye vyombo vya habari duniani, mabadiliko yanayoleta ongezeko la uhitaji wa maudhui bora kwenye mifumo mbalimbali. Ikiwa imeshasaini makubaliano na zaidi ya kampuni 240 za usambazaji duniani, iflix inawapa watazamaji wake chaguo kubwa la vipindi vya TV vinavyosifika pamoja na sinema zinazopendwa na mashabiki kitaifa na kimataifa kama vile ICE, Saints I Sinners, Riviera, Britannia, Tin Star, Being Mary Jane, Medici Masters of Florence na Luther, pamoja na nyinginezo. Hii ikiambatana na sinema kubwa za Bollywood kama Love Shagun, Sharafat Gayi Tel Lene, Golmaal Returns and Dedh Ishqiya.

Muanzilishi wa iflix na Mkurugenzi Mkuu Mark Britt alisema: “Leo ni siku muhimu kwa iflix. Tunafurahi sana kufikisha huduma yetu yenye ubora wa kimataifa nchini Tanzania na kuingia ubia na Vodacom, kampuni ya mawasiliano inayoongoza nchini. Sisi iflix tunashauku kubwa kuwahudumia wateja wa ndani ya nchi ya Tanzania. Tumedhamiria kuwapatia chaguo kubwa kabisa la vipindi vya burudani, kwa uhitaji na matakwa yao wenyewe waweze kutazama au kupakua kwenye kifaa chochote atakachopenda mteja.”

Upande wa maudhui ya KiAfrika, iflix inatoa sinema za Bongo kama vile Akili Nyingi, Mama Kubwa, Mapenzi Yamerogwa, Family, Perfect Command, Omega na nyingine nyingi huku kukiwa na sinema na vipindi vitakvyokuwa maalum kwa iflix ambavyo vitatangazwa baadae.

Mkuu wa iflix Afrika Mashariki, Bw. Paul Coogan aliongeza “Tumefurahishwa sana kuileta huduma ya kimataifa ya iflix nchini Tanzania. Ikiwa na vipindi bora kabisa vya TV na sinema kutoka duniani kote, iflix iko tayari kubadilisha kabisa namna ya upatikanaji wa burudani nchini Tanzania. Tunauelewa mkubwa wa watazamaji wa Tanzania na tuna mategemeo mazuri katika ubia wetu na Vodacom kuwafikishia hayo. Huduma yetu nchini Tanzania inawalenga watazamaji wa KiTanzania! Kuanzia uchaguzi wa maudhui hadi jinsi inavyonadiwa, mteja ni kiini wa yote tunayoyafanya.”


Kwa sasa ikiwa inapatikana katika nchi 27 barani Asia, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini pamoja na barani Afrika kusini mwa Sahara, iflix inawapatia watazamaji maudhui mengi ya sinema kubwa za Hollywood na vipindi vya TV vya kikanda na kitaifa, nyingi kati ya sinema na vipindi vikiwa ni vipya na ndiyo vinarushwa kwa mara ya kwanza. Kila mteja atakapojiandikisha ataweza kuipata huduma hii kwenye vifaa vitano, ikiwa ni pamoja na simu za kiganjani, laptop, tablet na kwenye TV za nyumbani ili aweze kutazama popote na wakati wowote.






WAZIRI MKUU KUZINDUA MRADI WA KUONGEZA UWEZO WA KUHIFADHI NAFAKA TANZANIA JUMAMOSI 21 APRILI 2018

$
0
0
 
 
Na Mathias Canal, NFRA-Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) Tarehe 21 Apili 2018 atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa kuongeza uwezo wa uhifadhi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) katika dhifa itakayofanyika kwenye viwanja vya Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula zilizopo Mtaa wa Kizota eneo la Viwanda Mjini Dodoma.

Mradi huo utagharimu Dola za Kimarekani Milioni 55, ambao ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Poland ikiwa ni sehemu ya kiasi cha Dola milioni 110 kilichotolewa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, mikataba ya ujenzi ilianza kutekelewa tarehe 9 Disemba 2017 ambapo Mradi huo utatekelezwa na kampuni mbili za Kandarasi kutoka Poland ambazo ni (Feerum S.A na Unia Araj Realizacje Sp.o.o) huku msimamizi wa mradi ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandashi wa habari na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba ameeleza kuwa Mradi huo utahusisha ujenzi wa vihenge vya kisasa, maghala ya kisasa, ujenzi wa ofisi na kutekelezwa katika maeneo nane ambayo ni (Babati)-Manyara, Dodoma, Makambako-Njombe, Mbozi-Songwe, Shinyanga, Songea-Ruvuma, Sumbawanga-Rukwa na Mpanda-Katavi.  

Baada ya mradi kukamilika Wakala utakuwa umeongeza uwezo wa kuhifahi kwa 250,000 MT zaidi (vihenge vya kisasa 190,000MT na maghala 60,000 MT) jambo ambalo litakuwa chachu na mafanikio yenye tija katika kuunga mkono Juhudi za utendaji wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.

Kupatikana kwa Mradi huo nchini ni jitihada za Serikali ambazo zitapelekea ukuaji wa uchumi nchini na kuchangia kuwezesha Tanzania ya viwanda ambapo kutawezesha maghala ya Wakala kuweza kuhifadhi akiba ya Chakula ambayo itaendana na mahitaji halisi ya dharura kulinganisha na ongezeko la watu nchini.

Hifadhi ya Chakula inayohitajika kukidhi mahitaji ya dharula kwa miezi mitatu ni zaidi ya tani 500,000 ukilinganisha na tani 150,000 iliyokuwa inahitajika miaka ya 2008 Wakala ulipoanzishwa.

Aidha, Zikankuba alisema kuwa technolojia itakayotumika katika ujenzi wa vihenge vya kisasa, itawezesha Wakala kupunguza gharama za uendeshaji; kuhifadhi chakula kwa muda mrefu zaidi; kupunguza upotevu wa zao la mahindi baada ya kuvuna (posthaverst loss), kuongeza soko la mahindi nchini na kuimarisha usalama wa nafaka inayohifadhiwa kwa kudhibiti sumukuvu (Aflatoxin) kwa mahindi yaliyohifadhiwa. Jitihada hizi zinalenga katika kuimarisha uwezo wa Taifa katika kuimarisha usalama wa chakula nchini.

WAGENI WAMIMINIKA BANDA LA TANZANIA WTM AFRIKA

$
0
0

Meneja Utafiti na Maendeleowa Bodi ya Utalii Tanzania, Ndugu Gladstone Mlay akitoamaelezo kwa wageni waliyotembelea banda la Tanzania katika maonesho ya utalii “World Travel Market (WTM)” yanayofanyika nchini Afrika Kusini.
Baadhi ya mawakala wa utalii wa Tanzania waliyoshirikikatika maonesho ya Utalii ya WTM Afrika 2018 wakiuza huduma za utalii wanazozitoa kwa wageni waliyotembelea Banda la Tanzania.
Baadhi ya mawakala wa utalii wa Tanzania waliyoshirikikatika maonesho ya Utalii ya WTM Afrika 2018 wakiuza huduma za utalii wanazozitoa kwa wageni waliyotembelea Banda la Tanzania.

Na: Geofrey Tengeneza-Capetown Afrika Kusini

Banda la Tanzania katika maonesho ya Kimataifa ya WTM Afrika yanayofanyika jijini Capetown Afrika Kusini limeendelea kutembelewa na watu wengi wanaotembelea maonesho haya kwa lengo la kupata taarifa mbalimbali zinazohusu Tanzania na vivutio vyake vya utalii sambamba na kufanyamzungumzo ya kibiashara na wafanyabiashara katika sekta ya utalii kutoka Tanzania.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi umebaini kuwa watu wengi wanaotembelea banda la Tanzania wamekuwa wakivutiwa zaidi na yanayotolewa kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo nchini kama vile mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, pori la akiba la Selous n.k

Kwa upande wa wadau wa utalii kutoka sekta binafsi kutoka Tanzania wanaoshiriki maonesho haya wameelezea kuridhishwa kwao na namna wanavyoendelea kukutana na kuingia makubaliano na wafanyabiashara wenzao wa utalii wakubwa wa kimataifa.

“ Namshukuru Mungu maonesho ni mazuri na nimefanikiwa kukutana na wafanyabiashara ya utalii kutoka mataifa mbalimbali na kufanya makubaliano katika biashara yetu hii” anasema Bw. Naiman Meyassy Mkurugenzi wa kampuni ya usafirishaji watalii ya Quest Horizonya jijini Arusha.

Mapema Naibu balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Bi Rosemary Jairo alitembelea banda la Tanzania na kuelezea kufurahishwa kwake namna ilivyojipanga na kushiriki vema katika onesho hili.

“Nimefurahishwa sana na banda letu na namna mnavyoitangaza nchi yetu, napenda niwaponze sana Bodi ya Utalii kwa uratibu mzuri wa ushiriki wetu kama nchi” alisema naibu Balozi.

Katika onesho hili la WTM Afrika mwaka huu Tanzania inawakilishwa na makampuni 17 kutoka sekta binafi chini ya uratibu wa Bodi ya utalii Tanzania (TTB) wanaoshiriki katika banda la Tanzania wakati makampuni mengine zaidi ya 10 yanashiriki binafsi yakiwa na mabanda yao katika maonesho hayo. Mbali tna TTB taasisi nyingine zinazoshiriki maonesho hayo ni Shirika la Hifadhi za Taifa, Mamlaka ya hifadhi ya Bonde la Ngorongoro na Kamisheni ya utalii Zanzibar.

SERIKALI YASISITIZA HAKUNA UPOTEVU WA SHILINGI TRILIONI 1.5

$
0
0
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akitoa taarifa ya Serikali kuhusu hoja ya kutoonekana kwenye matumizi ya Serikali shilingi trilioni 1.51 leo Bungeni mjini Dodoma. 


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akitoa maelezo kuhusu mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa kila kipande cha ardhi hapa nchini kinapimwa ili kuchochea maendeleo wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma. 

Mbunge wa viti maalum (CCM) Mkoa wa Kagera Mhe. Oliver Semuguruka akichangia hoja ya Bajeti ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kuhusu maboresho yanayopaswa kufanywa katika sekta ya afya ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi katika Mkoa wa Kagera na katika hosipitali zote za umma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akisisitiza kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi kuendelea kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao kote nchini leo Bungeni mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akijibu miongozo ya wabunge mapema leo Bungeni mjini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Sehemu ya wageni waliofika Bungeni kwa ziara ya mafunzo wakifutilia kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO


Serikali leo imelithibitishia Bunge na umma kwa ujumla kuwa kufuatia maneno ya baadhi ya watu yaliyosheheni upotofu, siasa na yenye nia ya kuchafua taswira ya nchi kwamba kuna Shilingi trilioni 1.5 zimepotea, ukweli ni kwamba hakuna upotevu huo na mchanganuo wa matumizi uko wazi.

Akitoa taarifa hiyo ya kina Bungeni leo, huku akiainisha mchanganuo wa matumizi ya fedha hizo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amesisitiza kuwa chini ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, fedha za umma ziko salama na wanaojaribu kufanya ufujaji hatua kali zinachukuliwa. Taarifa kamili yenye aya 12 ni kama ifuatavyo:

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 49 ya Kanuni za Bunge Toleo la Januari 2016, naomba kuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu Kauli ya Serikali juu ya madai ya kutoonekana kwa matumizi ya shilingi trilioni 1.51 kwenye matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2012/13 hadi 2016/17, Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango ilikuwa kwenye kipindi cha mpito cha miaka mitano ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kuandaa hesabu za Serikali kwa kutumia mfumo wa Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (International Public-Sector Accounting Standards – IPSAS Accrual). Katika kipindi hicho, Serikali iliendelea kukusanya taarifa mbalimbali kwa kutumia mfumo huu ili kutuwezesha kutambua kikamilifu hesabu za mali, madeni pamoja na mapato yanayotokana na kodi. “IPSAS Accrual” ni mfumo wa kiuhasibu ambapo mapato yanatambuliwa baada ya muamala husika kukamilika na sio wakati fedha taslimu inapopokelewa; na matumizi yanatambuliwa wakati muamala wa matumizi umekamilika na sio wakati fedha inalipwa. Mfumo huu ni mzuri na una faida nyingi ikiwa ni pamoja na miamala ya Mapato na Matumizi kutambuliwa wakati husika na siyo wakati wa fedha taslimu inapopokelewa au kulipwa. 

Mheshimiwa Spika, matokeo ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa uandaaji wa hesabu kwa mfumo wa “IPSAS Accrual” umeiwezesha Serikali na taasisi zake kutoa taarifa za kina na zinazoonesha uwazi na uwajibikaji wa taasisi husika, hususan katika usimamizi wa mali na madeni ya taasisi. Kuongezeka kwa uwazi, kumewawezesha watumiaji wa hesabu kupata taarifa zinazowasaidia kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, kutokana na matumizi ya mfumo huu wa viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika sekta ya umma, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu na Watanzania kwa ujumla kwamba hakuna fedha taslimu ya shilingi trilioni 1.51 iliyopotea au kutumika kwenye matumizi ambayo hayakuidhinishwa na Bunge. Hivyo basi, madai ya baadhi ya watu wasiolitakia mema Taifa letu na Serikali yetu ya Awamu ya Tano hayana msingi wowote wenye mantiki. Haya yanadhihirishwa na aya zifuatazo kwenye tamko hili la Serikali.

Mheshimiwa Spika, taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeeleza jumla ya mapato yote ya Serikali kwa mwaka 2016/17, yalikuwa shilingi trilioni 25.3 ambapo fedha hizi zinajumuisha mapato ya kodi, mapato yasiyo ya kodi, mikopo ya ndani na nje pamoja na misaada na mikopo nafuu kutoka kwa Washirika wa Maendeleo.

Mheshimiwa Spika, napenda kulitaarifu Bunge lako Tukufu kwamba, kuanzia mwaka 2016/17, Mamlaka ya Mapato Tanzania ilianza rasmi kuyatambua mapato kwa mfumo wa Accrual. Hivyo basi, kati ya mapato haya ya shilingi trilioni 25.3, yalikuwemo pia mapato tarajiwa (receivables) kama mapato ya kodi yenye jumla ya shilingi bilioni 687.3 pamoja na mapato ya kodi yaliyokusanywa kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya jumla ya shilingi bilioni 203.92 (transfer to Zanzibar).

Mheshimiwa Spika, katika uandishi wa taarifa ya ukaguzi, CAG alitumia taarifa za hesabu na nyaraka mbalimbali ikiwa ni pamoja na Taarifa za Utekelezaji wa Bajeti (Budget Execution Report) ambapo hadi kufikia tarehe 30 Juni 2017, mapato yalikuwa jumla ya shilingi trilioni 25.3 na matumizi yalikuwa shilingi trilioni 23.79. Matumizi haya hayakujumuisha shilingi bilioni 697.85 zilizotumika kulipa dhamana na hati fungani za Serikali zilizoiva. Matumizi haya yalikuwa hayajafanyiwa uhamisho (re-allocation) wakati ukaguzi unakamilika. Hivyo basi, baada ya kufanya uhamisho jumla ya matumizi yote kwa kutumia Ridhaa za Matumizi (Exchequer issues) yalikuwa shilingi trilioni 24.4.

Mheshimiwa Spika, kutokana na ufafanuzi huo, shilingi trilioni 1.51 zilizodaiwa kutoonekana kwenye matumizi ya Serikali zilitokana na mchanganuo ufuatao:



Maelezo Shilingi Trilioni
Matumizi ya dhamana na hati fungani zilizoiva 0.6979
Mapato tarajiwa (Receivables) 0.6873
Mapato ya kodi yaliyokusanywa kwa niaba ya Serikali ya Zanzibar 0.2039
Jumla 1.5891
Fedha iliyotolewa zaidi ya mapato (Bank Overdraft) (0.0791)
Fedha zilizodaiwa kutoonekana kwenye matumizi 1.51

Mheshimiwa Spika, hii inamaanisha kwamba, baada ya kupunguza mapato ya Zanzibar ya shilingi bilioni 203.92 na kupunguza mapato tarajiwa ya shilingi bilioni 687.3, mapato halisi kwa mwaka 2016/17 yalikuwa shilingi trilioni 24.41. Aidha, baada ya kujumlisha matumizi ya dhamana na hati fungani zilizoiva za kiasi cha shilingi bilioni 697.85 kwenye matumizi ya shilingi trilioni 23.79 yaliyooneshwa katika Taarifa ya CAG, ridhaa za matumizi zilizotolewa zilikuwa shilingi trilioni 24.49 na kuleta ziada ya matumizi ya shilingi bilioni 79.07 ikilinganishwa na mapato. Kwa mchanganuo huu, ni dhahiri kwamba kwa mwaka 2016/2017 matumizi ya Serikali yalikuwa makubwa kuliko mapato kwa shilingi bilioni 79.09 ambazo ni Overdraft kutoka Benki Kuu ya Tanzania. Utaratibu wa kutoa fedha zaidi ya mapato (Overdraft facility) uko kwa mujibu wa kifungu cha 34 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006.

Hitimisho

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imepata mafanikio makubwa katika uandaaji wa Hesabu za Serikali kwa kutumia mfumo huo wa Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (IPSAS Accrual). Itakumbukwa kwamba, katika Afrika, Tanzania ndio nchi pekee iliyofanikiwa kwa kiwango kikubwa kuandaa hesabu kwa kuzingatia matakwa ya IPSAS na kufanikisha kuandaa hesabu za Majumuisho kwa kuzingatia mfumo huo.

Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo haya ya Serikali, napenda kulitaarifa Bunge lako Tukufu na wananchi kwa ujumla kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ipo makini na haiwezi kuruhusu upotevu wa aina yoyote wa fedha za umma. Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuona kwamba, kila mapato yanayokusanywa yanatumika ipasavyo na kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii, na naomba kuwasilisha.

UFUNGUZI SHEREHE ZA MAONESHO WIKI YA UTAFITI WA SAYANSI YA BAHARI WAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
Mgeni Rasmi Mkuu wa Kitengo cha Uratibu wa Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Aida Juma akitoa hotuba ya ufunguzi wa Sherehe za Nne za Maonesho ya Wiki ya Utafiti wa  Sayansi ya Bahari iliofanywa na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Bahari Dar es Salaam Buyu Wilaya ya Magharibi B Unguja.
 Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi ya Bahari Chuo Kikuu Dar es salaam Zanzibar Dk. Matern S.P.Mtolera akitoa hotuba ya Makaribisho kwa Mgeni rasmi  katika Ufunguzi wa Sherehe za Nne za Maonesho ya Wiki ya Utafiti wa  Sayansi ya Bahari iliofanywa na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Bahari Dar es Salaam Buyu Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Kitengo cha Uratibu wa Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Aida Juma kushoto akipatiwa maelezo kuhusiana na utafiti wa mwani na Mtafiti wa Mwani Dk. Flower Ezekiel Msuya katika ufunguzi wa Sherehe za Nne za Maonesho ya Wiki ya Utafiti wa Sayansi ya Bahari iliofanywa na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Bahari Dar es Salaam Buyu Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika Ufunguzi wa Sherehe za Nne za Maonesho ya Wiki ya Utafiti wa Sayansi ya Bahari iliofanywa na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Bahari Dar es Salaam Buyu Wilaya ya Magharibi B Unguja.
 Baadhi ya wanafunzi wa Sayansi  waliohudhuria katika Ufunguzi wa Sherehe za Nne za Maonesho ya Wiki ya Utafiti wa  Sayansi ya Bahari iliofanywa na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Bahari Dar es Salaam Buyu Wilaya ya Magharibi B Unguja.
 Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi ya Bahari Chuo Kikuu Dar es salaam Zanzibar, Dk. Matern S.P. Mtolera akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya ufunguzi wa Sherehe za Nne za Maonesho ya Wiki ya Utafiti wa  Sayansi ya Bahari iliofanywa na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Bahari Dar es Salaam Buyu Wilaya ya Magharibi B Unguja. Picha Na Yussuf Simai/Maelezo Zanzibar.


MAMA NI MUNGU WA PILI DUNIANI: AUNTY EZEKIEL

Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images