Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel Catalog



Channel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1564 | 1565 | (Page 1566) | 1567 | 1568 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akifungua Mafunzo ya Ujasiriamali yaliyowashirikisha zaidi ya wajasiriamali 2000 kutoa viunga mbalimbali vya Manispaa ya Dodoma.
   Baadhi ya wajasiriamali walioshiriki mafunzo.
   Baadhi ya wajasiriamali walioshiriki mafunzo.
   Baadhi ya wajasiriamali walioshiriki mafunzo.
   Wajasiriamali walioshiriki.
  Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na mmoja wa washiriki wa semina.

  ...........................................................

  Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Peter Mavunde ameahidi kuwapatia vikundi vya wajasiriamali mafunzo ya UJASIRIAMALI na kuviwezesha vikundi katika kata zote 41 zilizopo Jimbo la Dodoma Mjini.

  Mavunde ameyasema hayo leo katika ukumbi wa Cavillam wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Ujasiriamali yaliyowashirikisha zaidi ya wajasiriamali 2000 kutoka viunga mbalimbali vya Manispaa ya Dodoma,ambapo mafunzo hayo sasa yataanza kutolewa kwa kila kata  ili kuhakikisha idadi kubwa zaidi ya wajasiriamali inafikiwa na kupata mafunzo haya yenye lengo la kumuandaa mjasiriamali wa Dodoma kupata ujuzi wa utengenezaji wa bidhaa mbalimbali.

  Aidha Mavunde amewataka wajasiriamali hao kutumia fursa za ujio wa shughuli za Serikali Mjini Dodoma kama sehemu ya kukuza uchumi wao na kujiletea maendeleo binafsi.

  Akimkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mafunzo hayo,Mkurugenzi wa Taasisi ya MJASIRIAMALI KWANZA , Dk.Mujungu amemshukuru Mbunge Mavunde kwa udhamini wa mafunzo hayo na pia kumpongeza kwa kugawa mashine ndogo ndogo zenye thamani ya Tsh 55,000,000 kwa Vikundi vya Wajasiriamali katika kata 31 za Manispaa ya Dodoma.

  0 0



  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati), akizungumza na Uongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati alipofika kwenye Ofisi za shirika hilo, kukagua utendaji katika Idara mbalimbali za shirika hilo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo na kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.
  Meneja Masoko wa Shirika la Posta, David George akimpatia maelezo Waziri Profesa Mbarawa kuhusu mikataba ya Kibiashara iliyoingiwa na shirika.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akiangalia baadhi ya mikataba iliyoingiwa na shirika hilo.
  Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe (katikati), akimweleza jambo Waziri Profesa Mbarawa (kulia), katika ziara hiyo.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa Idara ya Kompyuta ya Shirika la Posta, Agnes Mtango. Kushoto ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akielekeza jambo katika Idara ya Kompyuta ya Shirika la Posta. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo na kushoto ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akielekeza jambo katika Idara ya Usafirishaji ya Shirika la Posta, alipoangalia mfumo wa usafirishaji kwenye moja ya kompyuta za idara hiyo.
  Afisa Msimamizi wa Magari ya Shirika (Transport Officer), Mhandisi Lameck Francis (kulia), akimweleza Waziri Profesa Mbarawa namna ya mfumo wa Udhibiti wa magari na mafuta kwenye moja ya kompyuta za idara hiyo, unavyofanyakazi.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akikagua mfumo wa Udhibiti wa magari na mafuta ya shirika ya kwenye moja ya kompyuta za idara hiyo.
  Meneja Fedha wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Rajab Mngong'e (kushoto), akimweleza jambo Waziri Profesa Makame Mbarawa, alipofika katika Idara ya Fedha katika ziara hiyo.
  Meneja Msaidizi Idara ya Fedha, Aron Samwel (kushoto), akimuonesha Waziri Profesa Makame Mbarawa, mfumo wa utunzaji wa fedha za shirika unavyofanya kazi.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akisindikizwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo (wa pili kulia), Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Elia Madulesi, mara baada ya kumaliza ziara hiyo.


  WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Profesa Makame Mbarawa (MB) leo tarehe 17 Aprili, 2018 amefanya ziara ya kushtukiza Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania.

  Mhe. Profesa Mbarawa ametembelea Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania kwa lengo la kukagua utendaji na uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Posta, katika ziara hiyo Mhe. Waziri aliongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Posta Luteni Kanali mstaafu Dr. Haruni Kondo.

  Katika ziara hiyo Mhe. Waziri alitaka kujionea matumizi ya mifumo ya kielektronik na namna ambavyo Shirika limejipanga kuitumia mifumo mbalimbali ili kusimamia utendaji kwa ukaribu. Mhe. Waziri Mbarawa alitembelea idara ya Fedha, Idara ya Barua na Logistiki, Idara ya Sheria, Idara ya Masoko na pia alikagua mifumo udhibiti wa gharama za mafuta na mwenendo wa magari ya Shirika yanayosafiri kati ya Dar es salaam na mikoani.

  Katika ziara hiyo Mh. Waziri ameitaka menejimenti ya Shirika kusimamia utendaji kazi na kuzingatia weledi na matumizi ya mifumo ya kielektroniki na kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia kasi ya Serikali ya awamu ya tano na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

  Mhe. Waziri alitoa msisitizo wa kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi na kukuza tija kwa kila Idara ndani ya Shirka la Posta. Waziri amemwaagiza Kaimu Postamasta Mkuu Hassan Mwang’ombe kufuatilia utendaji wa kila idara na kupata taarifa za mara kwa mara ili kuimarisha utendaji wa shirika.


  Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Posta alimshukuru Waziri Mhe. Mbarawa kwa kutembelea Shirika la Posta na kuahidi kuwa maagizo yote na maelekezo aliyoyatoa atayasimamia kikamilifu ili kuleta tija na Ufanisi zaidi.

  0 0

  wanawamke wawili waliojulikana kwa majina ,TEOFRIDA NJAKO miaka 27 na INVOLATA KOMBA miaka 61 kabila lao ni wamatengo kutoka wilayani MBINGA,mkoani RUVUMA wanashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kukutwa Wanamiliki MAshamba ya bhangi hekali moja kwa kila mtuhuwa.

   Hayo yamebainishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma SACP GIMMIN MUSHY wakati akiongea na RUVUMATV. HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akimtambulisha mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza (mwenye ushungu) huku mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere akifuatilia kwa karibu wakati wa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu lililofanyika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita.
  Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela (kushoto) akifurahia burudani iliyokuwa ikitolewa na msanii wa Muziki wa Singeli, Dulla Makabila wakati wa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu lililofanyika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita.
   Msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda nae hakuwa nyuma kutoa burudani. Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akizungumza na wana-Iringa waliojitokeza katika amasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu lililofanyika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita. Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Msanii wa Bongo Movies, Steve Nyerere ambao ndiyo waandaaji wa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu akizungumza machache na wakazi wa Iringa juu ya kutunza Amani, Upendo na Mshikamano wetu katika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita.
  Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiwatambulisha wasanii wa Bongo Movie waliofika katika Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu lililofanyika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita. Mratibu wa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu, Msanii wa Bongo movies, Single Mtambalike (Rich Rich) akizungumza machache wakati wa tamasha hilo lililofanyika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita. Msanii maarufu wa Bongo Movies Jacob Steven 'JB ' akieleza machache. Msanii maarufu wa Bongo Movies Jacob Steven 'JB ' akimtambulisha msanii mwenzake Weru Sengo. Msanii wa Kundi la Ze Komed akitoa burudani. Mchekeshaji maarufu, Mama Asha Boko akitoa burudani. Dj Choka nae alipata wasaa wa kutoa neno kwa wana-Iringa. Msanii wa Bongo Movies, Anti Ezekiel akiwasalimu wakazi wa Iringa.
  Msanii wa Bongo Movies, Jackline Wolper toa burudani.
  Wanamuziki wa bendi ya Fm Academia Wazee wa Ngwasuma wakitoa burudani.
  Wasanii wa Bongo movies wakipata picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mhe. Richard Kasesela na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza na viongozi wengine wa Mkoa mara baada ya kumalizika kwa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu.

  0 0

  Zaidi ya wakulima mia moja wa korosho katika Kijiji cha Namiungo Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma waliokuwa wametapeliwa Tani 15 za korosho zenye thamani ya Shilingi Milioni 56 na Kampuni ya ZUMA CARGO wameanza kulipwa fedha zao.

  0 0

   Mwenyekiti wa Bodi ya Tanzania Microfinance Association (TAMFI), Joel Mwakitalu (kulia) akikabidhi cheti kwa mshindi wa tatu wa tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation, Lydia Majoro wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
   Mjasiriamali mlemavu aliyefanya vyema Aneth Geraw ambaye aliondoka na kitita cha dola za Marekani 2000 wakati hafla ya kukabidhi tuzo za ujasiriamali za Citi Foundation zilizofanyika jijini Dar es Salaam
   Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia) akikabidhi cheti kwa mshindi wa pili wa tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation, Anney Sekulasa (kushoto) katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo katikati ni Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila.
   Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia) na Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila (katikati) kwa pamoja wakikabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Yetu Microfinance, Attemius Millinga (kushoto) ambapo taasisi yake imekuwa na ubunifu mkubwa wa bidhaa zake sambamba na mifumo ya kutolea huduma na methodolojia wakati wa hafla fupi ya tuzo za ujasiriamali za Citi Foundation zilizofanyika jijini Dar es Salaam.
   Mwanamke aliyefanya vyema kwenye ujasiriamali mdogo, Lucy Kiongosi akipozi baada ya kupokea cheti kilichoambatana na dola za Marekani 2000 wakati wa hafla ya tuzo za ujasiriamali za Citi Foundation zilizofanyika mwishoni wa wiki jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso.
   Mshindi wa tatu wa tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation, Lydia Majoro akifurahi na kupozi na cheti pamoja na tuzo yake.
   Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila (katikati)  akikabidhi cheti kwa Mjasiriamali mdogo aliyefanya vyema mwenye umri wa miaka 18-25 tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation, Mopaya Madi (kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia).
   Mshindi wa jumla wa tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Beula Seed and Co & Sons, Zabron Mbwaga (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Tanzania Microfinance Association (TAMFI), Joel Mwakitalu (wa pili kushoto), Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia).
  Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia) akikabidhi cheti kwa Ofisa mikopo Rose Chacha (kushoto) wakati wa hafla fupi za tuzo za ujasiriamali za Citi Foundation zilizofanyika jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo ni ni Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila.

  Na Mwandishi Wetu
  Zabron Mbwaga ambaye ni Mzalishaji mbegu, aliyepo Viwanja vya NaneNane, Njiro mkoani Arusha ametwaa tuzo ya mshindi wa jumla wa tuzo za Ujasiriamali ya Citi Foundation. Tuzo hiyo inaambatana na fedha taslimu dola za Marekani 7,500.

  Mbwaga ambaye aliwezeshwa upanuzi wa shughuli zake kwa mikopo kutoka BRAC Tanzania, alianza kazi zake akiwa na mtaji wa shilingi milioni 2 kabla ya kuongezewa nguvu na BRAC.

  Tuzo hizo zilizofanyika mwishoni mwa wiki zilitolewa kwa wajasiriamali 16 na ofisa mikopo mmoja.

  Mshindi wa pili ni Anney Sekulasa akiondoka na dola za Marekani 6000 huku mshindi wa tatu ni Lydia Majoro ambaye aliondoka na dola za Marekani 4000. Nafasi ya mjasiriamali mlemavu ilitwaliwa na Aneth Geraw aliyepata dola za Marekani 2000.

   Zaidi ya shilingi milioni 70 za kitanzania zimetolewa kwa washindi wa kwanza hadi wa 16 . Pia Taasisi za kifedha za wajasiriamali wadogo na wa kati (MFI) zenye ubunifu mkubwa wa bidhaa zake na huduma, mifumo ya kutolea huduma na methodolojia pia ilipata  tuzo. Safari hii Yetu Microfinance ndio walioinyakua.

  Tuzo hizo za Citi Bank Foundation zimeendeshwa na Mtandao wa Asasi zinazotoa huduma za kifedha kwa wajasiriamali wadogo (TAMFI) ‘TAMFI’ na washindi wametangazwa na majaji walioshiriki kufanyakazi hiyo.

  Tuzo hizo zimelenga kuhamasisha  wajasiriamali kutumia taasisi za kifedha za watu wa kati na chini na kufaidika nazo.

  Takribani wajasiriamali 209 waliwasilisha miradi yao lakini 22 pekee ndio waliweza kupenya na 16 ndio walipata ushindi wa tuzo tofauti.

  Safari hii washiriki walitoka maeneo mbalimbali nje ya Dar es Salaam tofauti na ilivyokuwa kwa mwaka 2016 ambapo washiriki wake walikuwa ni wa Dar es Salaam pekee.

  Washindi wengine ni Comelord  Swai $ 1000, Prisca Kayombo $ 1000, Rahim Kalyango $ 1000, Emmanuel Lazaro $ 1000, Jumanne Findisha $ 1000, Salma Said $ 1000, Editha Lukindo $ 1000, Amon Kalumuna $ 1000, Salum Chumu $ 1000 na Doroth Sambi $ 1000.


  0 0

  Picha na Habari za Freddy Macha

   Ulikuwa mkutano mfupi uliokusudia kutoa shukrani kwa wafadhili na Watanzania London wanaosaidia nyumbani. Fadhila hupitia Jumuiya ya Waingereza na Watanzania  (BTS) na kitengo chake cha TDT = shirika la Mfuko wa Maendeleo Tanzania.  BTS ilianzishwa mwaka 1975, na mlezi wake sasa hivi ni Rais mstaafu Ali Mwinyi.

  BTS ilimkaribisha Makamu wa Rais Mheshimiwa Suluhu Samia, aliyekuja London wiki hii kudhuruia mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Madola.
  Kawaida viongozi hutegemewa  hotuba ndefu zenye maelezo yanayochosha masikio.

  Mhe Suluhu alitua chuo kikuu cha lugha za Afrika na Mashariki ya Kati (SOAS)  akasalimiana na kupeana mikono na wananchi wa pande zote mbili. Hiyo tu ilitosha kuonesha imani yake kwa wananchi wachapa kazi wa pande hizi mbili.
   Makamu wa Rais Mhe Suluhu Samia akizungumza na Dk Mohammed Hamza, kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Uingereza
  Balozi wa Tanzania nchini  Uingereza, Dk Asha Rose Migiro akiwa na Kaimu Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe Marc Thayre
   Mwenyekiti wa Jumuiya Ya Uingereza na Tanzania (BTS)  Dk Andrew Coulson aliyefungua na kufunga kikao cha Brunei Gallery, SOAS.
  Baadhi ya Watanzania waliohudhuria katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Kiondo Wilkins, Dk Alex Paurine, Simon Mzuwanda na Joe Warioba

  0 0

  Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano jana jioni alikuwa ni miongoni mwa Jopo lililojadili kuhusu sera za kumwinua mwanamke kiuchumi wakati wa mkutano wa Jukwaa la Wanawake linalofanyika kama sehemu ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) unaoendelea hapa London.

  Kwenye jopo hilo Mheshimiwa Makamu wa Rais aliungana na Mhe. Dkt. Joseph Muscat, Waziri Mkuu wa Malta na wadau wengine wa masuala ya maendeleo ya wanawake.
   


  0 0


  Kaimu Mkurugenzi wa TBS, Tumaini Mtitu, akizungumza katika hafla ya kukabidhi leseni na nyeti kwa wazalishaji 59 waliogawanyika katika sekta mbalimbali.

  Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mati Super Brands Ltd, inayotengeneza vinywaji vikali aina ya Sed Cane Spirit na Strong, Castro Temba (kushoto), akipokea Leseni ya kutumia Alama ya Ubora kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Tumaini Mtitu, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya washiriki wa hafla hiyo.

  Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mati Super Brands Ltd, Castro Temba, akionyesha Leseni ya Ubora

  Mwanasheria wa Kampuni ya Mati Super Brands Ltd, Charlotte Lupembe, akiwa katika hafla hiyo.

  Meneja Uzalishaji wa Kampuni ya Mati Super Brands Ltd, Gasper Mlay, akiuliza swali wakati wa hafla ya kukabidhiwa Leseni ya kutumia Alama ya Ubora kutoka TBS.
  Washiriki kutoka makampuni mbalimbali.

  Meneja Uzalishaji wa Kampuni ya Mati Super Brands Ltd, Gasper Mlay, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kampuni hiyo kukabidhiwa Leseni ya kutumia Alama ya Ubora kutoka TBS.

  Wafanyakazi wa Kampuni ya Mati Super Brands Ltd, inayotengeneza vinywaji vikali aina ya Sed na Strong wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa Leseni ya kutumia Alama ya Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya bidhaa zilizopata Leseni ya kutumia Alama ya Ubora kutoka TBS. 


  KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Shirikaka la Viwango Tanzania (TBS), Mhandisi Tumaini Mtitu, amesema alama ya ubora kwa bidhaa ni chachu ya maendeleo ya biashara kitaifa na kimaifa.

  Mtitu aliyasema hao juzi jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhi leseni na nyeti kwa wazalishaji 59, waliogawanyika katika sekta mbalimbali ikiwamo usindikaji wa vyakula vya kuku, uhandisi mitambo na umeme.

  Mhanisi Mtitu alisema: "alama hii mliyopewa ni uthibitisho kuwa bidhaa zenu zimekaguliwa na kupimwa kwenye maabara za TBS zenye umahiri wa kimatifa na kutambulika,” alisema.

  Akuzungumza baada ya kupata leseni na vyeti vya ubora, Meneja Uzalishaji wa Kampuni Mati Super Brands Ltd, Gasper Mlay, alisema kuwa kampuni yao inatengeneza bidhaa kwa kukidhi masoko ya ndani na ya nje.

  "Bidhaa zetu tunatengeneza bidhaa ambayo inakidhi masoko ya ndani na ya nje,"alisema Mlay.

  0 0

  KUZIONA SIMBA SIMBA NA YANGA ELFU 7

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara(VPL) msimu wa 2017/2018 kati ya Simba na Yanga utakaochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

  Katika mchezo huo namba 178 utakaofanyika saa 10 jioni Kiingilio cha chini kitakuwa shilingi Elfu Saba (7,000) wakati kiingilio cha juu kitakuwa shilingi Elfu Thelathini.

  Jukwaa la VIP A itakuwa shilingi Elfu Thelathini (30,000),VIP B na C shilingi Elfu Ishirini (20,000) na Upande wa Mzunguko kwenye viti vya rangi ya Chungwa,Bluu na Kijani itakuwa shilingi Elfu Saba (7,000)

  Tiketi tayari zimeanza kupatikana kuanzia sasa kupitia Selcom


  FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM(ASFC) KUPIGWA JUNI 2,2018 SHEIKH AMRI ABEID

  Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) inatarajia kuchezwa Juni 2,2018 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid,Arusha.

  Katika mashindano ya ASFC mwaka huu kumefanyika maboresho ya kuongeza zawadi ambapo awali mshindi wa pili alikuwa hapati zawadi na katika msimu huu wa mashindano hayo mshindi wa pili atajikusanyia kiasi cha shilingi Milioni Kumi huku bingwa akibeba kitita cha shilingi Milioni Hamsini.

  Zawadi nyingine zitakazotolewa ni pamoja na Mchezaji bora wa mashindano atakayezawadiwa shilingi milioni Moja,Kipa Bora atapata shilingi Milioni Moja huku mfungaji Bora pia akipata shilingi Milioni Moja wakati mchezaji Bora wa mchezo wa fainali akijizolea shilingi Laki Tano.


  TFF YAVITAKA VILABU KUFUATA UTARATIBU,YASISITIZA HAITASITA KUVIKATA FEDHA KWA KUKIUKA MIKATABA.

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) linavitaka vilabu vyote kuwa makini na mikataba wanayoingia na Wachezaji pamoja na makocha wao.

  TFF haitasita kuzikata fedha klabu zote zitakazokuwa na madeni yanayodaiwa iwe kwa kukiuka mikataba yao na wachezaji,makocha au kwa namna nyingine yoyote.

  Kumekuwa na klabu zinalalamika kinyume na utaratibu tunazitahadharisha kufuata utaratibu unaofahamika kinyume cha hapo hatutasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayekiuka utaratibu.

  TFF inaendelea kusisitiza kwa klabu kutoa malalimiko yao kwa njia za kikanuni ili kuepuka hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa dhidi yao kama Ibara ya 50 ya katiba ya TFF inavyozungumza pamoja na Kanuni za Maadili.

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

  0 0
 • 04/18/18--05:57: MPRU YAPATA MTENDAJI MPYA
 • Na John Mapepele, Dodoma

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina amemteua John David Komakoma kukaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu nchini (MPRU) baada ya kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa awali Dkt. Milali Machumu kutokana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kubaini dosari katika usimamizi wa Kitengo hicho.

  Pia Waziri Mpina amevunja Bodi ya Wadhamini ya MPRU iliyokuwa chini ya Uenyekiti wa Profesa John Machiwa ambayo ilikuwa na Wajumbe nane.Mpina alisema ameamua kuvunja bodi na kumsimamisha Mtendaji huyo kwa mamlaka aliyonayo kulingana na Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, Na 29 ya mwaka 1994.

  Aidha Mpina amemwagiza Katibu Mkuu wa Uvuvi kuunda Kamati ya kuchunguza utendaji wa kazi wa Mtendaji wa awali.Akizungumza mara baada ya uteuzi huo Komakoma ambaye ni mtaalam wa Bailojia ya Baharini amesema atahakikisha kuwa maeneo yote ya bahari yaliyotengwa yanahifadhiwa kikamilifu ili kuleta Mchango mkubwa katika taifa letu.

  “Nina imani kwamba maeneo haya ni muhimu sana kwa uhifadhi wa raslimali za bahari na utalii endelevu hivyo hatuna budi kuyasimamia kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo” alisisitiza Komakoma.Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu kiliundwa na sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu  Mwaka 1994 ambapo baadhi ya majukumu yake makuu yameanishwa katika sehemu ya VI kifungu cha 10 ambayo ni pamoja na kulinda na kuhifadhi maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa bioanuai pamoja na mifumo ya ikolojia ya baharini na mwambao wa pwani.

  Kuhamasisha wananchi kutumia kwa busara raslimali ambazo hazitumiki kabisa au hazitumiki kikamilifu kwa sasa, kusimamia maeneo ya bahari na mwambao wa pwani ili kuwezesha matumizi endelevu ya raslimali na ukarabati wa maeneo yaliyoharibiwa.Kuhakikisha kuwa wananchi wanaoishi ndani ya hifadhi wanashirikishwa katika nyanja zote za upangaji,uendelezaji na usimamizi wa raslimali.

  Hadi sasa kuna Hifadhi za Bahari tatu na Maeneo Tengefu 15 hapa nchini katika mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es Salaam na Mtwara.Kabla ya uteuzi huu Komakoma alikuwa akikaimu nafasi ya Mkurugenzi Msaidizi wa Uvuvi katika Kitengo cha Udhibiti Ubora, Usalama, Viwango na Masoko ya Mazao ya Uvuvi katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina(aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati Ndogo ya Kutathmini Utendaji wa Sekta ya Uvuvi katika Ziwa Victoria baada ya kukabidhi taarifa hiyo mjini Dodoma hivi karibuni.Waliokaa kuanzia kushoto Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhandisi Bonaventure Baya Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi, Dk Yohana Budeba, aliyesimama kuanzia kushoto John Komakoma Kaimu Meneja wa MPRU.


  0 0

   Mwenyekiti wa Afrika wa World Association of Girl Guides and Girl Scouts (WAGGGS), Zoe Rakotondratovo (kushoto0 na Mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Zakia Meghji wakipia saluti salamu ya kiskauti baada ya Meghji kuvishwa beji na skafu wakati wa hafla iliyoandaliwa  na TGGA kwa mwenyekiti huyo  jana katika Makao Makuu ya TGGA, Upanga Dar es Salaam. 

  Rakotondratovo ambaye aliambatana na Meneja Mahusiano, Marie Rafenoarisoa alikuwa  nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo alitembelea Makao Makuu ya TGGA Upanga na miradi ya chama hiyo. Ziara hiyo ilikuwa maalumu kwa ajili ya kuipongeza TGGA kwa kuwa wa kwanza Afrika kusajiri wanachama wengi wakifuatiwa na Kenya na Nigeria. IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG;0715264202,0754264203

  Mwenyekiti wa Afrika wa World Association 
  of Girl Guides and Girl Scouts (WAGGGS), 
  Zoe Rakotondratovo akionesha zawadi ya kitenge alichozawadiwa na Kamishna wa Kimataifa wa TGGA, Miryam Mjema wakati wa hafla hiyo ya kumuaga.
   Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya TGGA, Grace Makenya akimvalisha khanga Meneja Mahusiano,Marie Rafenoarisoa 


   Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya TGGA, Grace Makenya  akimvalisha Rakotondratovo khanga baada ya zawadi hiyo kumkabidhi.

   Kamishna Mkuu wa TGGA, Symporosa Hangi (kushoto) na Kamishna wa Kimataifa wa TGGA,  Miryam Mjema (kulia0 wakitoka kumpokea Mwenyekiti wa Afrika wa World Association of Girl Guides and Girl Scouts (WAGGGS), Zoe Rakotondratovo tayari kuingia kwenye hafla ya chakula cha usiku Makao Makuu ya TGGA, Uapanga
   Meghji akimlaki Meneja Mahusiano wa WAGGGS Afrika, Marie Rafenoarisoa 
   Kamishna Mkuu wa TGGA, Symporosa Hangi  akitoa utambulisho wa baadhi ya waalikwa kwenye hafla hiyo
   Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya TGGA, Grace Makenya akitambulishwa
   Kamishna wa Kimataifa wa TGGA,  Miryam Mjema akitambulishwa
   Marafiki wa TGGA wakitambulishwa
   Viongozi wa TGGA kutoka Mkoa wa Lindi wakitambulishwa
   Girl Guides wakitambulishwa
   Wafanyakazi wa TGGA Makao Makuu, wakitambulishwa
  Saada El Maamry akimtuza msanii
   Msanii aliyekuwa akitumbuiza katika hafla hiyo akituzwa na Kamishna Mkuu wa TGGA, Hangi na Rafiki wa chama hichoClara Makenya.(kulia)

   Rakotondratovo akipata mlo wa usiku ulioandaliwa kwa ajili yake wakati wa hafla ya kumuaga
  Kamishna wa Kimataifa wa TGGA, Miryam Mjema akiwa na marafiki wa chama hicho Mecy Mchechu na Saada El-Maamry walipokuwa wakichukua mlo wa usiku
   Sasa ni wakati wa maakuli







   Wakicheza muziki
   Mwenyekiti wa Afrika wa World Association of Girl Guides and Girl Scouts (WAGGGS), Zoe Rakotondratovo (kushoto), akimvisha beji Mbunge wa Viti Maalumu, Hamida Abdallah ikiwa ni shukrani baada ya mbunge huyo kutoka Mkoa wa Lindi kuhudhuria hafla hiyo
  Mwenyekiti wa Afrika wa World Association of Girl Guides and Girl Scouts (WAGGGS), Zoe Rakotondratovo akitoa neno la shukrani
   Viongozi wa TGGA wakiwa na marafiki wa chama hicho
   Viongozi wa TGGA, wakiwa na wafanyakazi wa TGGA Makao Makuu
    Mjumbe wa Kamati ya WAGGGS Afrika, Florentina Mganga akimvisha zawadi ya skafu Zakia Meghji

   Meghji akivishwa beji ya WAGGGS


  0 0

  Kiongozi wa mbio za mwenge,Charles Kabeho akifungua bomba kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji wa Kasanda iliofadhiliwa na Water Mission Tanzania.
   Shamrashamra za uzinduzi wa mradi
  Kiongozi wa mbio za mwenge, Charles Kabeho, akiongea na wananchi wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji Kasanda,(kushoto) ni Mkurugenzi wa Kanda wa shirika la kimataifa la Water Mission, Will Furlong Shirika la kimataifa la Water Mission Tanzania lafanikisha mradi wa maji safi na salama katika Kijiji cha Kasanda Wakazi wa kata ya Kasanda, wilayani Kakonko mkoani Kigoma, jana,wameanza kupata maji safi na salama kutokana na kuzinduliwa kwa mradi mpya wa maji chini ya ufadhili wa Shirika la kimataifa la Water Mission Tanzania. 

  Mradi huu utanufaisha zaidi ya kaya 729 zinazoishi maeneo hayo. Miradi ya Kakonko na Kasanda, ni miongoni mwa miradi zaidi ya 20 ya kuwapatia wananchi maji safi na salama ambayo imetekelezwa na shirika la Water Mission Tanzania tangu mwaka 2014. Miradi ya Kasanda na Kakonko ni tofauti na ile iliyotekelezwa maeneo mengine kwa kuwa iko katika maeneo yaliyopo karibu na kambi ya wakimbizi ya Mtendeli. 

   Mkurugenzi wa Kanda wa shirika la kimataifa la Water Mission, Will Furlong alisema “Water Mission Tanzania, kupitia ufadhili wa taasisi ya Poul Due Jensen Foundation ambayo zaidi inajulikana kama, Grundfos Foundation, imewezesha ufanikishaji miradi 8 ya maji safi na salama kwa jamii mbalimbali nchini. 

  Mradi mwingine wa Zeze mkoani Kigoma nao tayari umezinduliwa mwezi huu. Mashirika ya Water Mission Tanzania na Grundfos Foundation, yanashirikiana kuhakikisha huduma za maji safi na salama zinafikia jamii zenye changamoto katika kanda ya Afrika Mashariki”. 

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi huu mkubwa wa maji ulioambatana na sherehe za mbio za Mwenge katika kata hiyo,Kiongozi wa mbio za mwenge,Charles Kabeho,alisema kuwa kuzinduliwa kwa mradi huo ni jambo la kihistoria kwa wakazi wa eneo hilo ambalo kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kupata maji safi na salama.

   “Kwa niaba ya serikali napenda kutoa shukrani kwa wadau wa maendeleo wanaounga mkono jitihada za serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazokabili jamii kama ambavyo hawa wenzetu wa Water Mission Tanzania ,wamekuwa mstari wa mbele kufanikisha miradi ya maji sehemu mbalimbali hapa nchini”alisema Kabeho. 

  Alisema kero ya ukosefu wa maji safi na salama kwa muda mrefu ilisababisha akina mama kutembea mwendo mrefu kutafuta maji sambamba na wananchi wengi kuathirika kwa kupata magonjwa mbalimbali kutokana na kutumia maji yasio salama kwa matumizi ya binadamu. Kabeho,alitoa wito kwa wakazi wote wa eneo hilo kujiona ni sehemu ya mradi huu na kuhakikisha wanatunza miundo mbinu ya mradi wakati wote sambamba na kutoa ushirikiano kwa wataalamu wanaofanya ushauri wa uendeshaji mradi.

  0 0


  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kupitia Katibu wake wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole kimesema Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe(ACT-Wazalendo) ni mpotoshaji mkubwa na vyombo vya kisheria vinastahili kumchukulia hatua.

  Kimesema Ziito kupotosha kuwa kuna fedha Sh.Trilioni 1.5 za Serikali zimeibiwa si kweli na kwamba wameipitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) hakuna fedha ambayo imepota au kuibiwa na kiasi ambacho kimetajwa kwenye ripoti cha makusanyo na matumizi kipo sahihi .

  "Tumepitia kwa usahihi taarifa ya CAG na kujiridhisha hakuna fedha iliyobwa kama Zitto anavyopotosha na kutaka kuaaminisha umma.Huu ni upotoshaji mkubwa na lazima tuukemee maana unaleta sintofahamu kwenye jamii."Zitto siku hizi amekuwa na tabia ya uongo.Nimetoa tafsiri yangu na kuelezea ukweli kuhusu fedha hizo anazodai kuwa hazipo.CCM hatuwezi kukaa kimya wakati kuna muongo mmoja anafanya kazi ya kupotosha na kuaminisha umma kitu ambacho si cha kweli,"amsema Polepole.

  Amefafanua taarifa ya CAG kuwekwa wazi ni msimamo wa Serikali na hawana tatizo na kuongeza kwa bahati mbaya kuna utamaduni wa baadhi ya watu kila jambo la Serikali hata liwe nzuri wao lazima walififishwe Pia amekiri Serikali ya CCM imeanza kuchukua hatua kwa kuwawajibisha waliosababisha ufujaji wa fedha za umma na mtindo huo uendelee na mtu akibainika mkosaji achukuliwe hatua .

  "Mkaguzi amefanya ukaguzi na kubaini kuna maeneo yanaviashiria vya ubadhirifu hatua zimechukuliwa.Uongozi wa awamu ya tano unajinasibu kwa uongozi bora ambao umejikita kwenye kufanya kazi na haupo tayari kuona ubadhirifu unafumbiwa macho uwe ndani ya Serikali, kwa taasisi za umma au binafsi na hata kwenye vyama vya siasa"amesema.

  Amesema ni utaratibu mzuri na ndio maana yote ambayo CAG ameona wamekubaliana yafanyiwe kazi na kusisitiza wanafahamu Zitto amelelewa vibaya huko nyuma lakini anatakiwa kufahamu sasa ni Serikali ya Awamu ya Tano na CCM ni mpya haipo tayari kuwavumilia wapotoshaji.

  "Zitto amekuwa na tabia ya uongo uongo sana, siku za nyuma alianza kuongopa kuhusu njaa wakati njaa hakuna na anaongopa kuhusu ripoti ya CAG.Vyombo vya kisheria vimchukulie hatua maana kuongopa ndani ya nchi yetu ni kosa,"amesisitiza.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo baada ya kuwasili mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia ya Mzee Mashaka Gambo kwa kufiwa na mkewe ambaye pia ni mama mzazi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli  leo Aprili 18, 2018. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpa pole Mzee Mashaka Gambo kwa kufiwa na mkewe Marehemu Rehema Paul Mumbuli ambaye pia ni mama  wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo  leo Aprili 18, 2018.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpa pole  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo alipofika nyumbani kwao mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam kumfariji kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli  leo Aprili 18, 2018.
   Mama janeth Magufuli akimpa pole  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo alipofika nyumbani kwao mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam kumfariji kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli  leo Aprili 18, 2018.
   Mama Janeth Magufuli akimpa pole Mzee Mashaka Gumbo kwa kufiwa na mkewe ambaye pia ni mama mzazi wa  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo alipofika nyumbani kwao mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam kuwafariji  leo Aprili 18, 2018.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia ya Mzee Mashaka Gambo kwa kufiwa na mkewe ambaye pia ni mama mzazi wa  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli leo Aprili 18, 2018.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiaga waombolezaji baada ya kutoa mkono wa pole kwa familia ya Mzee Mashaka Gambo kwa kufiwa na mkewe ambaye pia ni mama mzazi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli  leo Aprili 18, 2018. Picha na IKULU

  0 0






  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakimjulia hali Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara Dkt. Juma Ngasongwa walipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam kuwajulia hali wagonjwa leo Aprili 18, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakimjulia hali Mzee Celestine Bulima walipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam kuwajulia hali wagonjwa leo Aprili 18, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakipata maelezo toka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam Profesa Mohamed Janabi walipotembelea taasisi hiyo kuwajulia hali wagonjwa leo Aprili 18, 2018

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli nakiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam Profesa Mohamed Janabi walipotembelea taasisi hiyo kuwajulia hali wagonjwa leo Aprili 18, 2018 .Picha na IKULU

  0 0

  Watanzania wamehimizwa kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu kwa ajiri ya kuibua fursa mbalimbali za kimaendeleo na kuacha tabia ya  kutumia vitabu kama sehemu salama ya kuhifadhia fedha ,  kama ilivyo kwa baadhi ya watu maeneo ya vijijin na mjini  huku waandishi wa vitabu wakitakiwa kuendelea kuandika vitabu kwa lengo la kujenga Taifa lenye wasomi.
  Hayo yamesemwa na mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Prof, Ganka Nyamusogoro wakati wa uzinduzi wa siku ya kusoma vitabu duniani katika chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro, ambapo amesema  jamii nyingi za kitanzania zimejenga tabia ya kutosoma vitabu kama njia ya kuibua fursa  na kuongeza maarifa baadala yake wanatumia  vitabu kama sehemu ya kuhifadhia fedha  jambo ambalo ni kinyume na na malengo ya waandishi wa vitabu.
   Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe  Prof,Ganka Nyamusogoro akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa siku ya kusoma vitabu Duniani katika chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.
   Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe  prof,Ganka Nyamusogoro akikagua moja ya vitabu vilivyooneshwa na chuo cha mzumbe wakati wa maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu Duniani,ambapo chuo cha mzumbe kimetoa nafasi kwa watu mbalimbali kusoma vitabu katika eneo hilo ambalo lipo maalumu kwa siku tatu chuoni hapo kuadhimisha siku hiyo ya kusoma vitabu.
   Wanafunzi wa chuo kikuu cha mzumbe  mkoani Morogoro na shule ya sekondari Mzumbe wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi  katika maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani ambaye pia ni makamu mkuu wa chuo hicho Prof, Ganka Nyamusongoro hayupo pichani.
   Diwani wa kata ya Mzumbe mkoani Morogoro Recho Kungi wa kwanza kushoto  akisisitizia wanafunzi  juu ya umuhimu wa kusoma vitabu katika maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani yaliyo fanyika chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.
    Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe  Prof,Ganka Nyamusogoro ambaye pia ni Mgeni rasimi katika maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani chuo kikuu Mzumbe  Mkoani Morogoro  akisoma vitabu vya tafiti vilivyofanywa na wanazuoni wa chuo kikuu cha mzumbe mara baada ya kuzindua hafla hiyo.
   Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Mzumbe mkoani Morogoro Alfred  Joseph King akijisomea jarida wakati wa maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu  duniani, jarida hilo  limechapishwa na chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.
   Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe  Prof,Ganka Nyamusogoro (katikati) akiangalia hotuba inayohusu maadhimisho ya siku ya vitabu  duniani ambapo kushoto kwake ni mkuu wa idara ya huduma za wasomaji chuo kikuu cha mzumbe Sarah Mwambalaswa na kulia ni Mkurugenzi maktaba na huduma za kiufundi chuo kikuu mzumbe Dk Arobogasti Musabila .
  Wa kwanza kushoto ni David Onyango mkutubi wa maktaba ya chuo kikuu cha mzumbe akimuonesha vitabu vilivyo pangwa katika maktaba maalumu ya madhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani,wa pili kushoto Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe  Prof,Ganka Nyamusogoro anae fatia ni Diwani wa kata ya Mzumbe mkaoni Morogoro Recho Kungi wa mwisho ni  mkurugenzi maktaba na huduma za kiufundi chuo kikuu mzumbe Dk Arobogasti Musabila

  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  CHAMA Cha Mapinduzi(CCM), Mkoa wa Dar es Salaam kimetoa pole kwa familia ambazo zimepoteza ndugu zao kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha huku kikitoa ushauri kwa Serikali kuwaondoa waliojenga kwenye njia za maji kwa lengo la kupunguza maafa.

  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Cylivia Katekamba amewaambia leo waandishi wa habari kuwa chama hicho kinatoa pole kwa wote ambao wamefikwa na maafa na kuomba wenye uwezo wa kusaidia walioathrika na mvua hizo kujitokeza kusaidia.

  " Mkoa wa Dar es Salaam umekumbwa na mafuriko na kusababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha.CCM mkoa tunatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kutokana na kuondokewa na ndugu zetu kutokana na mvua.

  "Tunafahamu matatizo ya mafuriko yametokea kwetu na hata maeneo mengine duniani nayo wakati mwingine hukumbwa na mafuriko.Kubwa ni kuendelea kushikamana na kusaidia kwenye kipindi hiki.CCM tunatoa pole,"amesema Katekamba.

  Pia ametoa mwito kwa walio maeneo hatarishi ni vema wakaondoka maeneo hayo na kufafanua kutokana kuzibwa kwa mitaro na njia za maji imesababisha hata maeneo ambayo huwa hayapati mafuriko safari hii maji yamejaa.

  Amefafanua yapo maeneo ambayo watu wamejenga lakini kiuhalisia ni maeneo ambayo yapo kwa ajili ya kupitisha maji na matokeo yake yanakosa pakupita na kwenda kwenye makazi ya watu na kusababisha maafa.

  Ameshauri watu wa mipango miji kuangalia namna ya kuondoa changamoto hiyo na kuongeza kamati ya siasa ya Mkoa wa Dar es Salaam jana usiku imekutana kujadili hali ya mafuriko."Moja ya jambo tulilokubaliana maeneo ambayo yanatakiwa kubaki wazi ili maji yapite lazima mipango miji kuangalia namna ya kufanya,"amesema na kuongeza ni vema wananchi wa wakazingatia utunzaji wa mazingira kwa kutoziba njia za maji na kutokata miti ovyo.

  Alipoulizwa kuhusu waliojenga kwenye njia za maji, Katekamba amejibu kuwa kazi ya Chama ni kuisimamia Serikali na hivyo moja ya jambo ambalo wanataka kuona linafanyika ni kuwaondoa waliojenga maeneo hayo.

  Pia ameomba wananchi kuibua na kuwabainisha watu ambao wamejenga kwenye mifereji ya kupitisha maji badala ya kukaa kimya huku akielezea CCM Mkoa wa Dar es Salaam walikuwa na sherehe yao ya familia ya Wana-CCM Aprili 21 mwaka huu ambayo Mwenyekiti wake ni Idd Azan lakini wameiahirisha kutokana na mafuriko ya mvua na athari zilizotokea. 

  Hata hivyo, Katekamba pamoja na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali ya mkoa wamefanya ziara ya kukagua mitaa iliyokumbwa na mafuriko na kuona hali halisi.
  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Cylivia Katekamba(wa kwanza kushoto) akizungumza ma waandishi wa habari leo jijini wakati anatoa pole kwa waliokumbwa na mafuriko na familia ambazo zimepoteza wapendwa wao kwasababu ya mvua zinazonyesha.

  0 0


older | 1 | .... | 1564 | 1565 | (Page 1566) | 1567 | 1568 | .... | 1897 | newer