Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 154 | 155 | (Page 156) | 157 | 158 | .... | 1903 | newer

  0 0

  Wakili Israel Magesa aliyekuwa mmiliki wa kampuni ya Mawakili ya Magesa &Co. Advocates ataagwa rasmi Jumamosi 7/9/2013  kuanzia saa 6 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar Es Salaam. 
  Wakili Magesa ni baba mzazi wa Phares Magesa(MNEC), Kalimba Magesa, Makongo Magesa, Yusuh (Yohana) Magesa, Rose Magesa, Salome Magesa, Rachel Magesa, Emmanuel (Sospeter )Magesa , Marehemu Elisha Magesa (RIP) na baba Mkwe wa Mrs. Haika Lawere(Mkurugenzi - Mbezi Garden Hotel), Dr. Julius Keyyu (Mkurugenzi wa Utafiti- TAWRI) na Ndg. Charanga ( Mkurugenzi - Tanzania Aviation Training College). 
  Marehemu ameacha mjane Rhoda Magesa na wajukuu 8. 

   Wakili Magesa enzi za uhai wake aliwahi kuwa Hakimu Mkazi Mkuu Mahakama ya Kisutu, Katibu wa bodi na Mwanasheria Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya kusini, Mwenyekiti wa Baraza la Nyumba Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa Amnesty International - Tanzania Chapter, Mwenyekiti wa Lions Club -Singida, pia ni mmoja wa wanasiasa waanzilishi wa siasa za vyama vingi nchini. 

   Enzi za uhai wake alifanya kazi ya uhakimu Mkazi mikoa ya Mbeya, Kilimanjaro, Singida, Kagera, Mtwara na Dar Es Salaam, Wakili Magesa ni miongoni mwa wanasheria waliomaliza shahada ya Sheria LLB katika Chuo Kikuu Cha East Africa miaka ya sabini mwanzoni na baadae kupata shahada ya Uzamili LLM toka Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam. Pia alipata nafasi ya kujiendeleza zaidi kimasomo katika nchi za Uingereza, Uholanzi na Sweden. 

   Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa Marehemu Ukonga, Majumba Sita na shughuli rasmi ya kuaga itafanyika Jumamosi tarehe 7/9/2013 kuanzia Saa 2-3 nyumbani kwa marehemu, saa 3-6 ibada kanisa la Mennonite Tanzanai-Upanga, saa 6-10 jioni shughuli rasmi ya kuaga na kutoa heshima za mwisho - Mnazi Mmoja, Dar Es Salaam na mazishi yatafanyika siku ya jumatatu 9/9/2013 kijijini Chitare, Majita, Musoma Vijijini.

  0 0

  Mgeni rasmi akipiga picha ya pamja na kamati ya maandalizi ya shughuli hii.
  Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Tanzania  Mh. Benjamin Mkapa  ambaye alikuwa mgeni rasmi akitoa risala ya ufunguzi wa awamu ya pili ya  mpango mkakati wa kuendeleza sekta ya Afya kwa wananchi wa Vijijini mwaka 2013-2018  katika halfa ya  chakula cha usiku kilichoandaliwa  na Taasisi ya Benjamin William Mkapa iliyofanyika  Serena Hoteli jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Benjamin William Mkapa Dkt.Ellen Senkoro  akitoa historia fupi wakati wa ufunguzi wa mpango mkakati wa Taasisi hiyo kwa mwaka 2013-2018 katika halfa ya  chakula cha usiku kilichoandaliwa na Taasisi hiyo na kuhudhuliwa wadau mbalimbali katika Hoteli ya   Serena jijini Dar es Salaam.
  Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Tanzania kulia  Mh. Benjamin Mkapa  ambaye alikuwa mgeni rasmi akifungua rasmi Mpango mkakati wa awamu ya pili kwa mwaka 2013-2018  wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Benjamin William Mkapa  katika  halfa ya chakula cha usiku kilichoandaliwa  na  Taasisi  hiyo katika Hoteli ya   Serena jijini Dar es Salaam,kushoto ni Mkuregenzi wa Taasisi hiyo Dkt.Ellen Senkoro.                              
  Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Tanzania  Mh. Benjamin Mkapa  ambaye alikuwa mgeni rasmi akikabidhi cheti cha shukrani kwa Bi .Mera Mathew Mkurugenzi wa Maendeleo wa Shirika la Irish  wakati wa ufunguzi wa  Mpango mkakati wa awamu ya pili kwa mwaka 2013-2018  wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Benjamin William Mkapa  wakati wa hafla ya  chakula cha usiku kilichoandaliwa  na  Taasisi  hiyo katika Hoteli ya   Serena jijini Dar es Salaam. 
  Rais Mstaafu wa awamu ya tatuTanzania  Mh. Benjamin Mkapa  ambaye alikuwa mgeni rasmi akikabidhi cheti cha shukrani kwa Bw .Jonson Mshana mwakilishi kutoka Banki M katika ufunguzi wa Mpango mkakati wa awamu ya pili kwa mwaka 2013-2018  wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Benjamin William Mkapa   wakati  wa halfa ya chakula cha  usiku kilichoandaliwa  na Taasisi  hiyo katika Hoteli ya   Serena jijini Dar es Salaam. 
  Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Tanzania  Mh. Benjamin Mkapa  ambaye alikuwa mgeni rasmi akikabidhi  cheti cha shukrani kwa Bi .Rahel Sheiza Mkurugenzi Mipango wa  Taasisi isiyo ya kiserikali ya Benjamin William Mkapa  katika ufunguzi wa Mpango mkakati wa awamu ya pili kwa mwaka 2013-2018    katika  wa halfa ya chakula cha usiku kilichoandaliwa  na  Taasisi  hiyo  katika Hoteli ya   Serena jijini Dar es Salaam.


  Wageni waalikwa wakifuatilia kwa umakini matukio mbalimbali katika wa halfa ya chakula cha usiku kilichoandaliwa na Taasisi isiyo ya kiserikali  ya Benjamin William Mkapa wakati wa ufunguzi wa mpango mkakati  wa  awamu ya pili kwa mwaka 2013-2018 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 
  Wanamuziki wa  nyumba ya vipaji Tanzania(THT) wakitoa burudani kwa wageni waalikwa waliofika katika halfa ya chakula cha usiku kilichoandaliwa na Taasisi isyo ya kiserikali ya Benjamin William Mkapa wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya mpango makakati kwa  mwaka 20013-2018 wa Taasisi hiyo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.  Picha zote na  Lorietha Laurence -Maelezo

  0 0

        Usaili kuanza kesho:

  Tusker Project Fame, shoo halisi ya muziki ambayo inapagawisha watazamaji na mashabiki kwa ujumla Mashariki mwa Afrika. Sasa imerudi tena katika msimu wa 6 ambapo msimu huu itakua ya aina yake kwa ukubwa na nzuri zaidi kulinganisha na misimu iliyopita.


  Miliki jukwaa! Tusker inawaalika wale wote wenye vipaji vya kuimba kufika katika usaili tarehe 7 na 8 Septemba, 2013 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Baada ya hapo washiriki wa Tanzania watapata nafasi ya kuingia katika jumba la Tusker project Fame na kushindanishwa jukwaani na vinara kutoka Kenya, Uganda, Rwanda na Sudan Kusini.


  Zawadi ni nono msimu huu, na mshindi wa Tusker project Fame atajinyakulia kitita cha Sh. 100,000,000 za kitanzania na kupata mkataba mnono wa mwaka wa  kurekodi wenye thamani ya Sh. 200,000,000 za kitanzania. Ni imani yetu kwamba fedha zitabebwa na mtanzania kwani vipaji tunavyo vya kutosha kikubwa watanzania wajitokeze kwa wingi katika usaili huu.


  Katika msimu huu mpya watu wengi zaidi watahusika katika shughuli mbalimbali uwanjani hata kumiliki jukwaa. Kujiunga na hayo yote shiriki katika promosheni zinazoendelea katika bar mbalimbali na upate ofa za Tusker.


  KUHUSU USAILI

  Tusker Project Fame kupitia bia yake ya Tusker Lager inatafuta vijana wenye vipaji vya kuimba nawenye uwezo wa kuleta mabadiliko katika soko la muziki pia wenye utaalamu wa hali ya juu katika kuimba na kutumia vifaa vya muziki ipasavyo. Wapenzi wote wa muziki ambao wana weledi wa kutosha kuiwakilisha Tanzania na kuonesha kuwa wanaweza kufanikiwa na kujulikana kama nyota katika muziki wanakaribishwa sana.


  Wale wenye vipaji vya muziki wanaweza kujaribu bahati kwa kujitokeza katika usahili wa Tusker project fame. Siku mbili za usaili kwa ajili ya kusaka mastaa wa msimu wa 6 wa Tusker Project fame utakaofanyika jijini Dar es Salaam kama ifuatavyo:


  Tarehe 7 Septemba 2013, Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa mbili asubuhi

  Tarehe 8 Septemba 2013, Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa mbili asubuhi


  Washiriki waje wakiwa tayari kuwakabili majaji wetu ambao wataangalia kipaji, kujiamini na kubwa zaidi wataangalia washiriki ambao wateweza kufundishika na wale watakaoibuka vinara kwa wenzie.


  Usahili wa Tusker Project Fame ni kwa wale wenye umri zaidi ya miaka 18.


  ITAONYESHWA


  Msimu wa sita wa Tusker Project Fame inarushwa hewani kupitia katika vituo vya televisheni vya EATV saa 2 usiku na ITV saa 4 usiku.


  0 0

   Sehemu ya vijana waliojitokeza kwa wingi kwenye semina hiyo ya Fursa kwa vijana wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa ikijadiliwa ukumbini humo.
  Muwakilishi wa NSSF-Makao Makuu Bwa,Salim Khalfan akizungumza mbele ya vijana mbalimbali waliojitokeza kwenye semina ya Fursa kwa vijana,iliofanyika mapema leo  kwenye ukumbi wa  chuo cha Teofilo Kisanji kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya. Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil,TPSF.
  Mmoja wa Vijana Wajasiliamali ,ambaye ana mradi mkubwa wa kuuza juisi,Gasto Sony mkazi Uyole mkoani Mbeya,akieleza zaidi kwa vijana wenzake waliojitokeza kwa wingi kwenye semina hiyo,namna ambayo ameweza kuitumia fursa alioipata na kuwa mjasiliamali wa kuuza juisi kisasa kabisa.
    Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Eprahim Mafuru akizungumza na wakazi wa Mbeya (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye semina ya Fursa kwa vijana,filiofanyika leo asubuhi ndani ya ukumbi wa  chuo cha Teofilo Kisanji (TEKU),kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya.Kampuni ya Serengiti ndio wadhamini wakuu wa tamasha la Fiesta 2013 linalotarajiwa kufanyika jioni ya leo kwenye uwanja Sokoine.
    Baadhi ya vijana mbalimbali kutoka ndani ya mkoa wa Mbeya  wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo mapema leo asubuhi kwenye ukumbi wa  chuo cha Teofilo Kisanji kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya. 
   Semina ya Fursa kwa vijana ikiendelea
   Mkali wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akifafanua jambo mbele ya wakazi mbalimbali wa mji wa Mbeya,alipokuwa akiielezea mada mojawapo iliyohusiana na fursa mbalimbali zilizomo ndani ya mkoa huo namna ya kuzitumia,Semina hiyo imefanyika leo ndani ya ukumbi wa chuo cha Teofilo Kisanji kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya.
    Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Eprahim Mafuru akizungumza jambo na msanii wa muziki wa kizazi kipya aitway Niki wa Pili ndani ya semina ya Fursa kwa vijana.
  Muwakilishi kutoka shirika la TPSF,Bwa.Louis Accaro akifunguka kuhusiana na mambo ya fursa kwa vijana na nanmna ya kuzichangamkia mara zipatikanapo.
   Mdau wa Kilimo kutoka mkoani Mbeya,Bwa.Yona Daniel akizungumzia fursa zinazopatikana kwenye kilimo,ambapo amewaasa vijana kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye suala zima la kilimo.

   Semina ya Fursa kwa vijana ikiendelea.Semina kama hii imekweíshafanyika kwenye mikoa ya Kigoma,Singida,Tabora,Mtwara na leo mkoani Mbeya.

  0 0

  Mabingwa wa Airtel Rising Stars 2013 Mwanza wakisheherekea ushindi kwenye Uwanja wa Kumbu Kumbu ya Karume jijini Dar es Salaam Julai 6. 

  Wasichana walionyesha vipaji vya hali ya juu vya kusakata kabumbu wakati wa fainali za Airtel Rising Stars jijini Dar es Salaam mwaka huu.

  Vijana wakipambana vikali wakati wa fainali za Airtel Rising Stars jijini Dar es Salaam mwaka huu.

  =======   ======  ======
  Bharti Airtel imetangaza leo kwamba michuano ya kimataifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars itaanza kutimua vumbi katika jiji la Lagos nchini Nigeria kuanzia September 16 hadi 22 ambapo Tanzania itawakilishwa na timu za wasichana na wavulana. 

   Michuano hii inafanyika kwa mara ya pili mfululizo kwa lengo la kutoa fursa kwa vijana chipukizi kutoka sehemu mbali mbali barani Afrika kuonyesha vipaji vyao na kuchochea maendeleo ya mpira wa miguu. 

   Akizungumzia mashindano hayo Mkurugenzi Mtendani wa Airtel Tanzania Sunil Colaso amesema: “Michuano ya Afrika ya Airtel Rising Stars itasaidia kuinua kiwango cha soka barani Afrika na Airtel inafarijika kupata fursa hii ya kuendeleza vipaji vya wachezaji chipukizi”. 

  Huu ni mwaka wa tatu tangu kuanzishwa kwa programu hii ya Airtel Rising Stars barani Afrika ambapo maelfu ya vijana wamepata nafasi ya kushiriki katika nchi 16 kuanzia ngazi ya chini, mkoa hadi Taifa. 
   Wachezaji nyota kutoka katika kila nchi hizo sasa wanaelekea nchini Nigeria kuchuana kwa lengo kuonyesha vipaji vyao zaidi na kupata mshindi ambaye ndiye atakuwa kinara wa Airtel Rising Stars barani Afrika mwaka huu. 

   Mshindi pia atajinyakulia kitita cha dola za Mimarekani 10,000 ambazo ni zaidi ya milioni kumi na sita za Tanzania.  Fedha hizi zitatumika kuwaendeleza vijana hao kielimu. Michuano hii ya Afrika mwaka jana ilifanyika jijini Nairobi ambapo timu ya wasichana kutoka Ghana ilinyakua taji huku timu ya wavulana kutoka Niger ikiukwaa ubingwa kwa upande wa wavulana. 

  Mchuano unatarajiwa kuwa mkali zaidi mwaka huu huku timu mwenyeji Nigeria ikiwa imejianda vilivyo kuhakikisha kwamba wanawapa raha mashabiki wao na hatimaye kutwaa ubingwa wa mashindano hayo. 
  Timu nyingine zinazotarajiwa kutoa upinzani mkali na hata kuiadhili Nigeria nyumbani kwao ni Ghana na Zambia. 

  Kwa kuendesha mashindano haya ya vijana Airtel inaelekea kutimiza lengo lake ililojiwekea awali la kuwa mdhamini mkubwa wa mchezo wa soka kwa vijana barani Africa. Wachezaji bora kutoka katika mashindano hayo ya Afrika watapata fursa ya kushiriki kliniki mbili zitakazofanyika chini ya usimamizi wa klabu maarufu duniani: Arsenal na Manchester United. 

  Kliniki hizo zitafanyika Lagos (Nigeria) na Lubumbashi (Democratic Republic of Congo) mwezi Aprili 2014 na kusimamiwa na makocha wa Manchester United na Arsenal. Akizungumzia umuhimu ya kliniki za Airtel Rising Stars Colaso amesema: 


  “Zitasaidiwa kuwaendeleza vijana kisoka na kuwapa hamasa ya kutaka kuwa wachezaji wa kulipwa”. Kliniki hizo ndizo zitakazozindua rasmi mwaka wa nne mwezi Aprili 2014.   Awali kliniki hizo zilipangwa kufanyika baada ya mashindano ya kimataifa lakini zimelazimika kusongezwa mbele ili kuwa na muda zaidi wa maandalizi ya kuziboresha.

  0 0

  Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa kituo cha Televisheni cha Star TV Abdala Tilata akishauriana jambo na Meneja wa Vodacom wilaya ya Missungwi Gift Tesha(katikati) na MenejaUhusiano wa Nje wa Kampuni hiyo Salum Mwalim muda mfupi kabla ya Vodacom kukabidhi vifaa vya michezo kwa shule ya MsingiLukungu iliyopo Wilayani Missungiwi Mkoani Mwanza.
  MenejaUhusiano wa Njewa Vodacom Salum Mwalim akiongea kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo vilivyotolewa na Vodacom kwa shule ya Msingi Lukugu iliyopo Wilaya ya Missungwi mkani Mwanza. Kushoto kwake ni Meneja wa Vodacom Missungwi Gift Tesha na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Kishiwa Maleba (wapilikushoto).
  Meneja wa Vodacom Wilaya ya Missungwi Gift Tesha akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lukungu jezi zilizotolewa na Vodacom.Kampuni hiyo imeipatia shule hiyo jezi za mpira wa pete na soka pamoja na mipira ili kuendeleza michezo shuleni hapo ya kukuza michezo nchini. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
  Meneja Uhusiano wa Njewa Vodacom Salum Mwalim akimkabidhi Mwalimu wa Michezo wa Shule ya Msingi Lukungu iliyopo Wilaya ya Missungwi Vicent Ndulu moja ya mipira iliyotolewa na Vodacom pamoja na jezi kuendeleza michezo shuleni hapo. Katikati ni Menejawa Vodacom Missungwi Gift Tesha.
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lukungu iliyopo Wilaya ya Missungi Mkoani Mwanza wakifurahia kupokea vifaa vya michezo kutoka kampuni yaVodacom walivyokabidhiwa ilikushiriki vema katika shughuli za michezo wawepo shuleni. Vifaa vilivyotolewa ni jezi seti mbili za mpira wa soka, seti moja ya mpira wa pete, mipira na fulana za mazoezi.

  0 0


  0 0

   .Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Mwanzilishi na Mkurugenzi waShirika la Africa School House Bi.Ainee Bessire (watatu kushoto) pamoja naMbunge wa Misungwi Charles Kitwangwa(kushoto) na mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo(kulia) wakikata utepe kuzindua rasmi shule ya msingi Ntulya katika kata ya Mondo wilayani Misungwi.Shule hiyo imejengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la kiserikali la Africa School House lenye makao yake nchini Marekani.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza ambapo atakagua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Ntulya muda mfupi baada ya kuizindua katika kata ya Mondo wilayani Misungwi leo. Shule hiyo imejengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la kiserikali la Africa School House lenye makao yake nchini Marekani.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza ambapo atakagua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo. 
  Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

  0 0

  Mkazi wa Kawe Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam anayefahamika kwa jina la Musa Senkando anatafutwa na polisi kwa mahojiano baada ya kutoweka akisadikika kumuua mke wake aliyetambulika kwa jina la Yusta Mkali.

  Mauaji hayo yalitokea usiku wa kuamkia leo(jana)habari za kuaminika za mauaji hayo kutendeka zilizibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema kwa uchunguzi wa awali mauaji hayo yanasadikika kutokea usiku wa kuamkia leo.

  “Yusta ameuwawa na kitu chenye ncha kali kilichomchoma kwenye koromeo na inasadikika mume huyo ameshatoweka na jeshi la polisi linamtafuta kwa uchunguzi zaidi kwani yeye ndiye aliekuwa mtu wa mwisho kuwa nae ndani,” alisema.

  Wambura alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

  Naye Mtoto wa dada yake marehemu ambaye alikuwa anaishi naye, Joshua Zebedayo alisema yeye ameshtukizwa na mauaji hayo pale alipo amka asubuhi kuelekea kufanya usafi chumbani mwa mama yake mdogo kwani yeye huwa analala chumba kingine na ndipo alipoukuta mwili wa marehemu ukiwa na majeraha pamoja na damu.

  “Ilikuwa majira ya saa mbili asubuhi nilipoamka kufanya usafi chumbani kwa mama kama ilivyokawaida yangu mama na baba waendapo kazini, ila cha kushangaza nilimkuta mama bado amelala wakati alitakiwa kuwepo kazini. Nilimwita mama bila mafanikio nikafunua shuka alilojifunika na kumkuta amekwisha fariki dunia,” alisema kijana huyo huku akibubujikwa na machozi.

  Marehemu Yusta wakati wa uhai wake,alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya umma Frontline Porter Novelli(PR COMPANY)
  Huyu ndiyo Mtuhumiwa Musa Senkando anaetafutwa na polisi.
  Marehemu Yusta Mkali enzi za uhai wake.
  Wakazi wa Kawe wakiwa na nyuso za huzuni wakati mwili wa marehemu ukitolewa ndani kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
  Mwili wa Marehemu Yusta Mkali ukitolewa kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala. 

  0 0

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya,ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga za muziki huo,Neylee akiimba kwa hisi jukwaani huu wakati tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea kwa shangwe ndani ya uwanja wa Sokonine.
  Wakazi wa jiji la Mbeya wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Sokoine,ndio kwanza shoo inaanza ambapo msanii aliyewahi kuiwakilisa shindano la BSS,Walter Chilambo ndiye aliyefungua pazia la onesho hilo usiku huu.
   Mama wa miduara ya Kibongofleva,Shilole akiwa na madensa wake wakitumbuiza jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
   Sehemu ya umati wa watu
   Wakazi wa jiji la Mbeya wakitoa heshima kwa baadhi ya wasanii waliotangulia mbele za haki, kwa kuwasha tochi za simu zao usiku huu.
   Rich Mavoko na skwadi lake wakilishambulia jukwaa. 
   Shilole akiimba jukwaani.
  Wasanii mahiri katika miondoko ya hip hop,Stamina na Young Killer wakilishambulia jukwaa la Serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Sokoine usiku huu.
   Ni shangwe tu kwa wakazi wa jiji la Mbeya usiku huu ndani ya uwanja wa Sokoine. 
  Mmoja wa sanii mahati wa kizazi kipya,Ommy Dimpo akiwaimbia mashabiki wake singo yake mpya iitwayo Tupogo usiku huu ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013.
   MKali wa kukamua mangoma kutoka Clouds FM,Dj Zero akiwarusha maelfu ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wanaondelea kumiminika kwenye uwanja wa Sokoine usiku huu.
  Msanii aliyewahi kulwakilisa shindano la BSS,Walter Chilambo ndiye aliyefungua pazia la onesho hilo usiku huu,pichani akitumbuiza mbele ya mashabiki wake.
  Baadhi ya watu wakifuatilia yanayojiri usiku huu kwenye tamasha la Seremgeto Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
  Mkali wa Mahaba,a.k.a tajiri wa Mahapa kutoka mwambao wa Pwani,Cassi Mganga akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013,kwenye uwanja wa Sokoine mkoanni Mbeya.

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni wakati alipowasili katika Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kuanza ziara ya kikazi 
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu muda mfupi baada ya kuzindua rasmi Shule ya msingi Ntulya,iliyopo kata ya Mondo, Wilayani Misungwi,Mkoa wa Mwanza.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na bvaadhi ya watoto waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa Shule ya Msingi Ntulya,katika kata ya Mondo,wilayani Misungwi
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amembeba motto Paulo Muhangwa muda mfupi baada ya kuzindua shule ya Msingi Ntulya wilayani Misungwi,Mkoani Mwanza
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalmiana na baadhi ya wauguzi katika hospitali ya wilaya ya Misungwi wakati wa uzinduzi wa huduma ya X Ray katika hospitali hiyo,
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo katika hospitali ya wilaya ya Misungwi wakati wa uzinduzi wa huduma ya X Ray katika hospitali hiyo,

  0 0


  Na Edwin Moshi, Makete.

  Serikali wilayani Makete mkoani Njombe imewataka wananchi kutoa ushirikiano wa pamoja kuwakamata ama kutoa taarifa kwa ngazi husika pindi wanapowaona watu wakijisaidia ovyo maeneo yasiyo rasmi

  Hayo yamesemwa na afisa afya wilaya ya Makete Bw Boniphace Sanga wakati akizungumza na mtandao huu na kuongeza kuwa kumekuwa na ongezako la magonjwa hasa ya kuhara ambayo yanatokana na watu wanaojisaidia ovyo na kuchafua mazingira

  Bw sanga amesema jukumu la usafi ni la kila mmoja na si la bwana ama bibi afya pekee na kwa kuwa wananchi ndio wanaoshinda maeneo mbalimbali wanawaona wale wanaojisaidia hovyo na kuomba watoe taarifa kwenye ofisi yake ili wachukuliwe hatua za kisheria

  Amesema inashangaza kuona hadi sasa wapo watu ambao hawana vyoo na wanaongoza kwa kuchafua mazingira kutokana na kujisaidia ovyo, na kutoa wito kuwa msimu huu ni wa kiangazi hivyo wanatakiwa kujenga vyoo kabla mvua haijanyesha

  "Kwa kweli natoa wito nyumba bila choo haijakamilika, acheni kun***a(akimaaisha kujisaidia) maeneo ambayo si kwa ajili hiyo, unakuta mtu kavaa vizuri lakini ni namba moja kujisaidia maporini, huu si ustaarabu na watu wa namna hii ndio wanaoleta magonjwa kwenye wilaya yetu

  Katika hatua nyingine Bw. sanga amewaomba wananchi kuendelea kujijengea utaratibu wa kutupa taka maeneo yanayoruhusiwa( kwenye vizimba vya taka) na kuwaasa kuacha tabia ya kutupa chupa za soda na maji mitaani kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaokamatwa

  0 0

  Mtangazaji wa kipindi cha burudani cha Funika Base kutoka Radio 5 ya Mjini Arusha , Julius Kamafa (kushoto) akifanya mahojiano na Washiriki wa Shindano la Redd’s Miss Tanzania 2013 katika studio za redio hiyo jana.
   Baadhi ya warembo wakijieleza Live Redio 5 hii leo walipotebelea kituo hicho.  Meneja Biashara wa TAN MEDIA, Angela Maina akizungumza na warembo wa Redd’s Miss Tanzania 2013 wakati warembo hao walipotembelea Kituo cha Redio cha Radio 5 cha mjini  Arusha leo kujionea shughuli mbalimbali na kufanya mahojiano maalum. Warembo wa Redd’s Miss Tanzania wapo mkoani Arusha kwa ziara ya kimafunzo.
   Baadhi ya wafanyakazi wa TAN MEDIA wakisikiliza kwa makini mkutano huo baina ya warembo na Viongozi wa TAN MEDIA.
  Meneja Biashara wa TAN MEDIA, Angela Maina akizungumza na warembo wa Redd’s Miss Tanzania 2013 wakati warembo hao walipotembelea Kituo cha Redio cha Radio 5 cha mjini  Arusha jana kujionea shughuli mbalimbali na kufanya mahojiano maalum.
   Warembo wakipiga picha za Pozi
   Walimbwende na Viongozi wa TAN MEDIA na watangazaji wa Radio 5 walipiga picha ya kumbukumbu.
  Warembo wakiondoka Radio 5

  0 0

  Mpendwa msomaji tunashukuru kwa mapendekezo kupitia kura zako, hatimaye blog hii yahttp://eddymoblaze.blogspot.com/ imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kugombea tuzo ya THE BEST DESIGN/GRAPHIC DESIGN BLOG, Tunakuomba hivi sasa uipigie kura blog hii ili iweze kuchukua tuzo hiyo. 

  Ili kupiga kura yako tafadhali bonyeza link ifuatayo na uchague palipoandikwa eddymoblaze.blogspot.com:-


  Asante kwa ushirikiano wako, piga mara nyingi uwezavyo

  0 0


  0 0

  For all who believe in Girls' Education....

  See you on September 12th, at Julius Nyerere Conference Hall...

  xoxo
  Missie Popular

  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akisalimiana na wananchi wa eneo la Ruaha Buyuni waliokuja kumpokea tayari kwa uzinduzi wa Mbio za Bendera.
   Wamama kutoka mkoa wa Iringa wakicheza ngoma ya kihehe wakati wa uzinduzi wa Mbio za Bendera.
   Wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wakishangilia salaam walizokuwa wanapewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndugu Sixtus Mapunda.
   Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Sixtus Mapunda akisalimia wakazi wa Ruaha Buyuni wakati wa uzinduzi wa  wa Mbio za Bendera ya Chama mkoani Iringa
   Wananchi akifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wa chama waliofika wakati wa uzinduzi wa Mbio za Bendera ya Chama mkoani Iringa.


  0 0

  Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara amewateua Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspapers Ltd (TSN) baada ya bodi ya awali kumaliza muda wake mwishoni mwa mwezi Machi, 2013.

  Uteuzi wa Mhe. Waziri unafuatia uteuzi alioufanya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania kwa Profesa Moses Wariobi kuwa wa Mwenyekiti wa Bodi ya TSN. Wajumbe wa Bodi ni kama Ifuatavyo:

  1. Dkt. Consolata Ishebabi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara
  2. Everlyn Richard kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam
  3. Alfred Nchimbi, Chuo cha Utumishi wa Umma
  4. Glorious Luoga, Mwanasheria

  Uteuzi huu ni kuanzia tarehe 6 Septemba, 2013

  0 0

   Ankal akipongezwa na blogger gwiji duniani kaka Ndesanjo Machas iku alipoanzisha rasmi Globu ya Jamii katika ukumbi wa mikutano wa Finlandia jijini Helsinki, Finland, Septemba 8, 2005 (BOFYA HAPA)
   Ankal na mai waifu wake na toto tundu Sellah wakikata keki kuadhimisha miaka 9 ya Globu ya Jamii usiku huu
  Ankal na familia yake wakisherehekea kimya kimya hepi besdei ya kuzaliwa kwa Globu ya Jamii usiku huu.
  -----------------------------------------------------------
  Ilikuwa siku ya Alhamisi tarehe kama ya leo (Septemba 8,) miaka TISA iliyopita wakati Globu ya Jamii ilipozaliwa rasmi katika ukumbi wa mikutano wa Finlandia jijini Helsinki Finland, kama utani tu. Kwa msemo mwingine, ni miaka TISA kamili leo toka Globu ya Jamii ianze Libeneke la kuhabarisha wadau kwa mapicha na habari kemkem bila kukosa hata siku moja  Kikosi kazi cha Globu ya Jamii kingependa kutoa shukrani za dhati kwa wadau wote duniani kote kwa kampani mnayotupa kila saa, siku, wiki, miezi na hadi sasa ikiwa ni MIAKA TISA kamili.  Si jambo dogo, ukizingatia katika safari hii njiani tumekutana na kila aina ya changamoto, kubwa kuliko yote ikiwa ni kufanya kila tuwezalo kubakia hapa tulipo kwa kufuata weledi pamoja na sera ya HATUBAGUI, HATUCHAGUI; ATAYETUZIKA HATUMJUI, pamoja na kauli mbiu kwa wadau watoa maoni ya kuwa waangalifu kutochafua hali ya hewa wala kujeruhi hisia ya mtu wakati wa kutoa maoni.  Si rahisi kumridhisha kila mdau, na kwa mujibu wa usemi wa Kimombo wa “What’s good for the goose is bad for the hen” unaomaanisha hivyo. Yaani “Kilicho kizuri kwa bata mzinga, ni kibaya kwa kuku”.

  Katika kuadhimisha hii MIAKA TISA ya Libeneke, Globu ya Jamii haitofanya sherehe ya pamoja na wadau kama ilivyotarajiwa. Badala yake Ankal kajikakamua na kununua kajikeki na kukata na kula na familia kwa niaba ya wadau. Ila ahadi yetu ni kwamba, panapo majaaliwa, sherehe kubwa itaandaliwa mwakani wakati wa kuadhimisha MIAKA KUMI. Ni mapema mno kusema itakuwaje, ila panapo uhai itakuwa  SHEREHE KUBWA na inayostahili.  Kwanza kabisa tunamshukuru Jalali Muumba wa vyote kwa tunu hii aliyoitupa. Tunatambua kuwa tuna bahati ya sisi kuwa sisi, na kamwe bahati hiyo uliyotupa, EWE MOLA, hatutoichezea...
  Globu ya Jamii pia inachukua nafasi hii kuwashukuru wadhamini wake, ikiwa ni pamoja na VODACOM, AIRTEL, UHURU ONE,  TTCL, NMB, NBC, AZANIA BANK, CRDB, NHC, PRECISION AIR, AIR UGANDA, NSSF, PSPF, DSTV, SKYLINK, SERENGETI FREIGHT FORWADERS  ‘WAZEE WA KAZI’, SWIFT FREIGHT, GIRAFFE OCEAN VIW HOTEL, DR MKOMBOZI,  na wengineo wote. Tunashukuru kwa kutuamini na kuendelea kuendeleza nasi Libeneke. 

  Shukrani zingine  za kipekee ziende kwa familia yangu kwa uvumilivu wanaoonesha kwangu, pia kwa wadau kadhaa ambao tukiamua kuwataja wote hapa itachukua ukurasa wote hu na tusiwe tumetaja japo robo yao. Kwa uchache tu, na ambao ni kwa niaba ya wale ambao hatutotaja kwa ufinyu wa nafasi na pia si  kwa ubora wao, shukrani hizo zimwendee kaka Ndesanjo Macha kwa kuwa wa kwanza kutufungulia na kutuongoza njia na kutupa maudhui ambao baada ya kuyafuata, tumeona faida yake.  Washauri wakuu wetu pia hatuwasahau katika hili. Nao  ni Profesa Mark Mwandosya, Mhe. January Makamba, Freddy Macha, Balozi Peter Kallaghe, Othman Michuzi, Ahmad Michuzi, Christopher Makwaia MK, Steve Wassira jnr., Nathan Chiume, DJ Luke Joe wa Vijimambo, Waziri Ally, John Kitime, Alex Perullo, Muhidin Maalim Gurumo, kaka Jeff Msangi, Boniface Makene, Kirk Gills, Oscar Shelukindo, Ephraim Mafuru, Imani Kajula, Profesa Mbele, Da' Chemi Chemponda, Ankal Beda Msimbe, kaka Assah Mwambene, Da' Tagie Daisy Mwakawago, Shamim Zeze wa 8020 Fashions, Mama wa Mitindo Asia Idarous na mumewe Mzee Khamsin, Ainde, kaka Asimwe Kabuga, Abdallah Ezza na Fide Tungaraza wa Heslsinki na wengineo wengi tu. Ushauri wenu tunauthamini na kuuheshimu!

  Wengine ni viongozi wote wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Spika, Naibu Spika na maofisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waheshimiwa Wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano pamoja na wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Viongozi  maofisa wote wa vyama vya siasa, Viongozi wote na watumishi  wa taasisi za umma na binafsi, Mablogger wote na mwisho ni wadau wote wanaotupa moyo kila kukicha. Asanteni sana, sana,  sana, sana. Hatuna cha kuwapa zaidi ya hizo SHUKURANI kutoka katika kilindi cha moyo wetu. MOLA AWE NANYI, NA AWAZIDISHIE PALE PALIPOPUNGUA.  Hatuna la zaidi la kusema zaidi ya kuahidi kwamba tutaendeleza Libeneke kwa moyo wetu wote huku tukipiga magoti kuwaomba wapendwa wadau wetu duniani kote muendelee kutupa kampani, kwani bila ninyi sisi si lolote si chochote. Pia tunaomba radhi pale tunapoteleza kama binaadamu yeyote ambaye daima duni si mkamilifu, ambapo likitokea litalotokea si kwa makusudi ama nia mbaya bali ni kwa udhaifu huo huo wa kibinaadamu.


  Naomba kuwasilisha,

  Wenu Mnyenyekevu,

  Muhidin Issa Michuzi “Ankal”

  0 0

  Katibu wa Taswa Jijini Arusha,Mussa Juma akiongea na waandishi wa habari kuhusiana Tamasha la Taswa linalotarajiwa kufanyika leo katika kiwanja cha general tyre,jijini humo.Kushoto ni Afisa wa Kinywaji cha Vita Malt ambao ni sehemu ya wadhamini wa Tamasha hilo,Deogratius Katambi.

  Na Woinde Shizza,Arusha

  Tamasha la michezo la waandishi wa habari za Michezo nchini (TASWA) linatarajiwa kufanyika leo September 8 katika viwanja vya general tyre vilivyopo njiro jijini hapa.

  Akiongelea tamasha hilo katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo mkoani wa Arusha,Musa Juma alisema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika na jumla ya timu 12 zinatarajiwa kushiriki katika tamasha hilo.

  Alisema kuwa michezo mbali mbali itachezwa katika tamasha hili ikiwa ni pamoja na kufukuza kuku,kukimbia na magunia,mpira wa miguu ,mpira wa pete pamoja na michezo mingine mbalimbali sambamba na burudani mbalimbali za muzikikutoka katika sehemu na bendi mbalimbali.

  Alisema kuwa hili nitamasha la nane kufanyika na kwa mara hii wameboresha zaidi kwani zawadi zimeongezeka tofauti na kipindi kingine.

  Amewasihi wadau mbalimbali kujitokeza katika tamasha hili kwani tamasha hili ni lakihistoria kutoka na waandishi mbalimbali kushiriki kutoka katika mikoa mbalimbali.

  Alitaja baadhi ya timu zitakazo shiriki katika tamasha hili kuwa ni pamoja na timu ya taswa ya jijini dar es salaamu ambapo inatarajiwa kuwasili leo timu ya taswa arusha ambao ni wenyeji wa bonanza hili,timu ya taswa manyara ,timu ya triple a fm ,sunrise fm,radio five pamoja na timu nyingine nyingi ikiwemo timu ya tbl ambao ni wathamini wakuu pamoja na timu ya wazee klabu.

older | 1 | .... | 154 | 155 | (Page 156) | 157 | 158 | .... | 1903 | newer