More Channels
Showcase
Articles on this Page
(showing articles 3081 to 3100 of 37921)
- 09/05/13--01:09: _SHINDANO JIPYA LA T...
- 09/05/13--01:11: _Siku ya Pili ya Tam...
- 09/05/13--01:13: _THE BEAT FESTIVAL F...
- 09/05/13--01:18: _MSTAHIKI MEYA MH. J...
- 09/05/13--05:22: _WAFANYE WATABASAMU
- 09/05/13--05:28: _KINANA KUFANYA ZIAR...
- 09/05/13--05:38: _Davis Mosha, DRFA, ...
- 09/05/13--05:58: _ Nyota wa Airtel Ri...
- 09/05/13--07:14: _MAKAMU WA RAIS DKT....
- 09/05/13--09:27: _CHEKA ATINGA BUNGEN...
- 09/05/13--09:36: _THE UN SECRETARY-GE...
- 09/05/13--09:41: _TAZAMA HABARI YA MT...
- 09/05/13--10:03: _Airtel yatangaza m...
- 09/05/13--10:07: _SERIKALI YAZINDUA A...
- 09/05/13--10:21: _Fi¬rst National Hum...
- 09/05/13--10:24: _SHIGELA, SIXTUS WAK...
- 09/05/13--10:35: _RAIS KIKWETE AKUTAN...
- 09/05/13--10:41: _Du...! Shughuli ime...
- 09/05/13--13:59: _TAZAMA PALIVYOCHIMB...
- 09/05/13--23:38: _WAANDISHI WANNE WAJ...
(showing articles 3081 to 3100 of 37921)
Channel Description:
Karibuni Jamvini Wanajamii
Pichani chini ni Mkurugenzi wa Kamati ya Tanzania TOP Model Jackson Kalikumtima akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jana kwenye mgahawa wa City Sports Lounge.































0 |
|
0 |
|
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akikabidhi rasmi Magodoro 50 kwa Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akimshukuru Mwenyekiti wa kikundi cha Neema Womans Power Bi.Maryam Dedes (mwenye hijabu nyekundu) mara baada ya kukabidhi Magodoro hayo.
Mwenyekiti wa kikundi cha Neema Womans Power Bi.Maryam Dedes katika picha ya pamoja na Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Wakinamama wa Kikundi cha Neema Womans Power.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa kikundi cha Neema Womans Power Bi.Maryam Dedes kuelekea kwenye chumba cha mikutano katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kabla ya kukabidhi msaada wa Magodoro kwenye Hospitali hiyo.
Mkurugenzi wa Wauguzi Hospitali ya Muhimbili Bi. Agnes Jonathan Mtawa akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili katika uotaji huduma kwa wananchi mbele ya mgeni rasmi Mstahihiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa katika hafla fupi ya kukabidhi Magodoro 50 kwa Hospitali hiyo.
Katibu wa Neema Womans Power Mgeni Ottow akisoma risala yao mbele ya mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi Magodoro 50 kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Na. Ripota wetu.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala MH.JERRY SILAA amekabidhi magodoro 50 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupitia kikundi cha wakimama "NEEMA WOMANS POWER".
Neema Womens Power ni kikundi cha wakina mama kilichoanzishwa mwaka 2005 kwa kuanza na Madrasa mbili ya akinamama na wasichana akiwa na wanafunzi 18 tu. Madrasa hizo zipo Kinondoni na Buguruni chini ya Mwenyekiti wa kikundi hicho Bi.Maryam Dedes. Jumuiya hii pamoja na kuwa na Elimu ya dini, husaidia jamii kwa michango mbalimbali ikiwemo kulipia ada za shule kwa wanafunzi wasiokuwa na uwezo, kusaidia Walemavu na Wajane pamoja na familia duni.
Katika hafla hiyo fupi Mgeni rasmi Mh. Jerry Silaa ametoa wito kwa wadau mbalimbali kuweza kujitoa kwa kusaidia jamii kwani mzigo uliopo kwa Serikali peke yake haiwezi, na ukizingatia ya kwamba hakuna mtu asiyeijua Hospitali kama si Muhimbili basi Amana, Temeke au Mwananyamala na Hospitali nyingine nyingi zinahitaji msaada vifaa mbalimbali na endapo kila mwananchi angeweza kuchangia japo kifaa kimoja sasa tungekuwa mbali sana na inawezekana kabisa tusingekuwa na matatizo sugu katika Hospitali zetu.
Mh.Jerry ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha huduma zinaboreshwa ndani ya Halmashauri yake na anayesifika kwa uchapakazi wake na umakini aliwashukuru kwa dhati kabisa uongozi wa Neema Womans Power pamoja na wanachama wao kwa kuliona tatizo hilo na kwa uwezo walionao leo hii wameweza kutoa magodoro hayo 50 na kuwaasa waendelee kujitoa zaidi na wasife moyo maana kazi ya jamii haina malipo zaidi ya fadhira mbele za Mungu.
Hafla hiyo fupi ya kukabidhi Magodoro imehudhuriwa na Bi.Maryam Dedes ambaye ni Mwenyekiti wa kikundi hicho, Agnes Jonathan Mtawa- Mkurugenzi wa Wauguzi Hospitali ya Muhimbili, Mgeni Ottow Katibu wa Neema Womans Power pamoja na Khadija Mwita Makamu mwenyekiti na wajumbe wao 30 na Uongozi wa Hospitali ya muhimbili.
Marafiki wa Wafanye Watabasabu, watabasamu na watoto wagonjwa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Mratibu, Nathan Mpangala, anatoa shukrani za kumwaga kwa marafiki waliochangia mawazo, muda na zawadi. Pia Rich Mavoko kwa kuruhusu wimbo wake kutumika kwenye video hii. Share TABASAMU kwa kusambaza video hii.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahaman Kinana septemba 10 anatarajiwa kuanza ziara ya kawaida katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara.
Ziara hiyo itaanzia katika mkoa wa Shinyanga septemba 10 mpaka 13 mwaka huu, kwa kutembelea wilaya zote nne za mkoa huo na kufuatiwa na mkoa mpya wa Simiyu kuanzia Septemba 14 mpaka septemba 19 kwa kutembelea wilaya zote tano Kabla ya kuhitimisha ziara hiyo kwa kutembelea wilaya Sita za mkoa wa Mara kuanzia Septemba 20 Mpaka 25 mwaka huu.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM ataambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM anayeshughulikia Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye.
Kwa mujibu wa Ratiba ya ziara hiyo, Wajumbe hao wa sekretarieti watakagua uhai wa Chama ikiwa ni pamoja na kupokea wanachama wapya sanjari na kuhamasisha wananchi kujituma katika shughuli za uzalishaji ili Kuleta tija katika maisha Yao na ya taifa kwa ujumla.
Aidha watakagua maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015 hasa katika miradi ya kimaendeleo Kama vile Ujenzi wa majosho kwa ajili ya wafugaji, maendeleo ya maboresho ya kilimo cha Pamba, uvuvi wenye tija pamoja na maboresho ya sekta za Afya, elimu na miundombinu zikiwemo Barabara.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu atapata fursa ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kwa kushauriana na serikali kutafuta namna ya kuzitafutia ufumbuzi.Katibu mkuu pia atafanya mikutano ya ndani, na ya hadhara katika kila wilaya za mikoa hiyo.
Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
05/09/2013
Kampuni ya Delina Group na Chama Cha soka cha Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kimeipiga tafu klabu waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa SC) kiasi cha sh milioni 4.2 ili kuwawezesha kushiriki katika mashindano ya wana-habari yaliyopangwa kufanyika Jumapili ijayo mkoani Arusha.
Makabidhiano hayo yalifanyika jana kwenye mgahawa maarufu wa City Sports and Lounge uliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam. Katika makabidhiano hayo, mjumbe wa DRFA kupitia vilabu katika mkutano mkuu wa TFF, Benny Kisaka alikabidhi kiasi cha sh 1.2 huku Mkurugenzi wa kampuni ya Delina ambaye ni mdau mkubwa wa michezo nchini, Davis Mosha alikabidhi shs milioni 3 kwa mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto “Ronaldo De Lima” Omary.
Kisaka alisema kuwa wameamua kutoa msaada huo kutokana na mchango wa waandishi wa habari za michezo nchini kwa mkoa wa Dar es salaam kwani ni wadau wao wakubwa.
“Waandishi wa habari za Michezo wametoa mchango mkubwa wa maendeleo ya michezo nchini, sit u kwa DRFA, bali kwa vyama vyote vya michezo, sisi DRFA tumekuwa wa kwanza kuonyesha mfano mfano na tunaamini wengine watatuunga mkono ili kufanikisha jambo hili,” alisema Kisaka.
Mosha alisema kuwa amesukumwa sana na mwamko wa waandishi wa habari ambao wameamua kuonyesha kwa mfano kwa kucheza soka na mpira wa pete (netiboli).
Alisema kuwa kampuni ya Delina Group imeamua kutoa mchango huo ili kuwawezesha kufanya vizuri katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na kampuni ya Ms Unique kwa kushirikiana na Taswa Arusha na kudhaminiwa na TBL, Tanapa, Mega Trade, Pepsi, AICC na Wazee Klabu.
“Huu ni mchango wangu nikiwa kama mdau mkubwa wa michezo, nimefarijika sana na tunaamini kuwa mtafanya vizuri katika mashindano hayo ambapo nimeambiwa Taswa SC ni mabingwa mara mbili mfululizo,” alisema Mosha.
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliwapongeza wadau hao kwa msaada huo mkubwa. “Mbali ya DRFA na Davis Mosha, pia Azam imetupiga tafu safari hii ambapo mbali ya fedha pia wametoa jezi mbili,” alisema Majuto.
Aliwataja wadhamini wengine kuwa ni Bodi ya Ligi (TPL Board) na Kassim Dewji ambao wamechangia kufanikisha ziara hiyo. “Bado tunahitaji msaada wa hali na mali ili kuweza kufikia bajeti yetu, kwa ajili ya safari hiyo,” alisema Majuto.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo , Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde alisema wachezaji hao chipukizi watashughulikia na kukamilisha hati zao za kusafiria kati ya kesho, Alhamisi na Ijumaa. “Kwa upende wetu kila kitu kimekamilika kwa ajili ya safari kuelekea kwenye mashindano hayo ya kimataifa ambayo yatashirikisha timu kutoka sehemu mbali mbali barani Afrika,” alisema.
Jumla ya wavulana na wasichana 32 walifuzu kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu wakati wa fainali za Taifa za Airtel Rising Stars zilizofanyika jijini Dar es Salaam mwezi Juni.
Mashindano haya ya kimataifa yanafanyika kwa mara ya pili mwaka huu yakiwa na lengo la kutoa fursa zaidi kwa wachezaji chipukizi kuendeleza vipaji vyao. Kwa mara ya kwanza mashindano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars yalifanyika jijini Nairobi mwaka jana ambapo Tanzania iliwakilishwa na timu ya wavulana pekee ambayo hata hivyo ilitolewa hatua za awali huku timu ya Nigeria ikitawazwa kuwa mabingwa.
“Kulingana na kiwango cha kuridhisha cha wachezaji waliochaguliwa mwaka huu nina imani kwamba timu zetu za Tanzania – wasichana na wavulana – wana nafasi nzuri ya kufanya vizuri,” anasema Matinde ambaye ni mmoja wa maofisa wa Airtel Tanzania waliongoza na timu kwenye mashindano hayo.
Airtel imeanzisha mashindano haya ya vijana barani Afrika kwa nia ya kusaidia upatikanaji wa vijana wenye vipaji vya soka kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi ngazi ya Taifa. Airtel Rising Stars inatoa fursa kwa vijana kudhihirisha uwezo wao kwa makocha wa Taifa na kimataifa na kuweza kujiendeleza zaidi kisoka..
Hivi sasa Airtel Rising Stars ni moja ya matukio muhimu ya kisoka kwenye kalenda ya Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF). Huanzia katika hatua ya usajili ikifuatiwa na mechi za mtoano ili kupata wachezaji nyota wa kuunda timu za mikoa ambazo huchuana katika ngazi ya Taifa.
Airtel inaendesha muchuano hii kwa kushirikiana na klabu maarufu duniani ya Manchester United ambayo hutoa ushauri wa kiufundi na michuano hii imekuwa na hamasa kubwa katika nchi zote zinazoshiriki.
For more information, check out our website (www.airtel-football.com) or our mobile site (www.airtel-football.mobi). Please also take the time to like our facebook page (facebook.com/airtelfootball).
0 |
|
0 |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Simu za mkononi Zantel, Pratap Ghose, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Sept 5, 2013 akiwa na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zante, waliofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Sept 5, 2013 kwa ajili ya mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Viongozi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Sept 5, 2013. Picha na OMR
Waziri Mkuu Mh,Mizengo Pinda wanne kushoto akiwa na bingwa wa dunia wa mchezo wa masumbwi nchini Fransic Cheka baada ya kukaribishwa bungeni mjini Dodoma. wengine kushoto Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' na bingwa wa mabara Fransic Miyeyusho, kulia ni promota wa mchezo wa masumbwi nchini Mohamed Bawaziri, na promota wa mpambano wa ubingwa wa Dunia ambao cheka anao kwa sasa Catherini Matili .
MAJI MAREFU AKIWA NA MABINGWA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI |
Bondia fransic Cheka akiwa na wabunge mbalimbali pamoja na mwanaseria mkuu wa Selikari le alipotembelea bungeni. |
Waziri wa Wizara ya Habari ,Vijana,utamauni na michezo, Dkt,Fenela Mukangala wa pili kushoto akiwa na Rais wa TPBO Yassini Abdala pamoja na mapromota Mohamedi Bawazir kulia na Catherini Matili . |
Waziri Mkuu Mh,Mizengo Pinda katikati akiwa na mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Fransic Cheka wakati walipo tembelea bungeni Dodoma kwa ajili ya kutambua mchango wao na kuwapongeza picha na www.superdboxingcoach. |
Charity plays an important role in upholding the values and advancing the work of the United Nations. Donations of time or money; volunteer engagement in one’s own community or on the other side of the world; acts of caring and kindness with no thought of recompense; these and other expressions of global solidarity help us in our shared quest to live together in harmony and build a peaceful future for all.
I welcome this first observance of the International Day of Charity, which was proclaimed last year by the United Nations General Assembly and which coincides with the anniversary of the death of Mother Teresa, whose life and good works for some of the human family’s poorest and most vulnerable members inspired emulation across the world.
Strangely, charity sometimes gets dismissed, as if it is ineffective, inappropriate or even somehow demeaning to the recipient. “This isn’t charity”, some donors take pains to claim, “this is an investment”. Let us recognize charity for what it is at heart: a noble enterprise aimed at bettering the human condition.
At a time when we aim to accelerate our efforts to achieve the Millennium Development Goals and define a bold agenda for the period beyond 2015, the role of charity can and should grow.
UN bodies such as the UN Volunteers Programme and UNICEF offer venues for people across the world to get involved. In establishing the Day, the General Assembly asked that charity be encouraged through education and awareness-raising activities; initiatives such as the United Nations Academic Impact's ASPIRE -- Action by Students to Promote Innovation and Reform through Education -- have encouraged young women and men to take on the responsibility of ensuring that their less fortunate peers have the financial opportunity to go to school.
The UN’s humanitarian agencies rely on charitable donations from the public as well as the generosity of governments to continue their lifesaving work in response to natural disasters, armed conflicts and other emergencies.
On this new International Day, I call on people everywhere, of all ages, to act on the charitable impulse that resides in every human being.

sehemu ya tatu
sehemu ya pili
sehemu ya kwanza
Hii ni story ya mtoto wa miaka 12 aliyeishi kwenye ndoa tangu akiwa na miaka 8, kupitia kipindi kinachorushwa na EATV cha Wanawake Live chini ya Super Woman Joyce Kiria.
Tazama hizi link hapa chini
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuchezesha droo ya pili ya mshindi wa nyumba wa promosheni ya Airtel yatosha Jishindie nyumba 3 ambapo bi Anna Gustav Lyimo (29) Afisa wa benki kuu na mkazi wa Dar es salaamu ameibuka kuwa mshindi wa nyumba ya kisasa iliyopo kigamboni jijini Dar es salaam , akishuhudia ni Meneja Msoko wa Airtel Aneth Muga ( kulia) na mwakilishi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Emmanuel Ndaki.
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na mshindi wa nyumba ya pili wa promosheni ya Airtel yatosha Jishindie nyumba 3 mara baada ya kuibuka mshindi katika droo iliyochezeshwa katika ofisi za Airtel na kushuhudiwa na waandishi wa habari. bi Anna Gustav Lyimo (29) Afisa wa benki kuu na mkazi wa Dar es salaamu ameibuka kuwa mshindi wa nyumba ya kisasa iliyopo kigamboni jijini Dar es salaam , akishuhudia ni Meneja Msoko wa Airtel Aneth Muga ( kulia) na mwakilishi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Emmanuel Ndaki.
Mganga mkuu wa Serikali Dkt Donan Mmbando akizindua awamu ya pili ya kampeni ya tuko wangapi? tulizana! Inayosimamiwa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja wa mpango wa taifa wa kudhibiti ukimwi Dkt Angela Ramadhan akitoa takwimu wakati wa awamu ya pili ya kampeni ya tuko wangapi? tulizana! Inayosimamiwa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanamuziki wa bendi ya Fm Academia, ambaye ni rais wa Vijana, Nyoshi El Sadat akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya tuko wangapi? tulizana! Inayosimamiwa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
MSanii wa muziki wa bongofleva H.Baba akitoa burudani wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya tuko wangapi? tulizana! Inayosimamiwa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakifuatilia uzinduzi huo.
President Jakaya Kikwete (left) cuts a ribbon to open an exhibition shortly after opening of the three day National Human Resources for Health Conference held in Dar es Salaam this week.
President Jakaya Kikwete addresses health sector stakeholders during the opening of the three day National Human Resources for Health Conference held in Dar es Salaam this week.
The Benjamin William Mkapa HIV/AIDS Foundation (BMAF) Chief Executive Officer, Dr Ellen Mkondya Senkoro addresses participants during the opening of the three day National Human Resources for Health Conference held in Dar es Salaam this week
Health sector stakeholders follow up the President’s speech during the opening of the three day National Human Resources for Health Conference held in Dar es Salaam this week.
President Jakaya Kikwete (centre) poses for a group photo with health sector stakeholders shortly after opening of the three day National Human Resources for Health Conference held in Dar es Salaam this week
Health sector stakeholders follow up the President’s speech during the opening of the three day National Human Resources for Health Conference held in Dar es Salaam this week.
Participants pose for a photo during a break session shortly after opening of thethree day National Human Resources for Health Conference held in Dar es Salaam this week.
President Jakaya Kikwete (left) stresses a point to the former President Benjamin Mkapa (right) shortly after opening of thethree day National Human Resources for Health Conference held in Dar es Salaam this week.
The Minister for Health and Social Welfare, Dr. Hussein Mwinyi briefs reporters shortly after opening of the three day National Human Resources for Health Conference held in Dar es Salaam this week.
KATIBU Mkuu mstaafu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Martine Shigela (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu mpya wa UVCCM, Sixtus Mapunda, faili wakati wa makabidhiano ya Ofisi, waliyofanya leo, Makao Makuu ya UVCCM, mjini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni, Naibu Katibu Mkuu UVCCM (Bara), Mfaume Ally Kizigo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Utekelezaji UVCCM Taifa, Seki Kasuga. (Picha na Bashir Nkoromo).
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika mazungumzo na Marais Paul Kagame wa Rwanda(kushoto), Rais Salva Kiir wa Sudan ya kusini na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakati walipokutana na kufanya mazungumzo ya faragha, katika Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, jijini Kampala, Uganda.
Imetolewa na;
Ikulu,
Baadhi ya viongozi wan chi za jumuiya ya Maziwa Makuu wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Mkutano wa wakuu wa nchi hizo uliofanyika jijini Kampala Uganda leo.Kutoka kushoto ni Rais Salva Kiir wa Sudani ya Kusini,Rais Joseph Kabila wa DRC,Rais Dkt.Jakaya Kikwete,Rais Yoweri Museveni wa Uganda,Mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika Dkt.Nkosazana Dlamini Zuma na Rais Paul Kagame wa Rwanda..Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.
======== ===== ======
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Septemba 5, 2013, amekutana kwa faragha na Rais wa Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame katika mazungumzo yaliyokwenda vizuri na kuwaridhisha viongozi hao wawili wa nchi jirani.
Viongozi hao wamekutana kwa zaidi kidogo ya saa moja katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, nje kidogo ya mji wa Kampala, Uganda.
Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete na Rais Kagame wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika kujenga uhusiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Viongozi hao wawili wako nchini Uganda kuhudhuria Mkutano wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Kimataifa wa Maziwa Makuu – “International Conference on the Great Lakes Region (ICGLR)” unaofanyika leo Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort.
Viongozi wengine ambao wanahudhuria Mkutano huo ni pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye ni Mwenyekiti wa ICGLR na mwenyeji wa Mkutano huo, Rais Silva Kiir wa Sudan Kusini, Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU).
Rais Kikwete na ujumbe wake amewasili Kampala asubuhi ya leo akitokea mjini Dodoma ambako aliwasili jana jioni kwa ajili ya hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu watatu na Naibu Makatibu Wakuuu wawili iliyofanyika Ikulu Ndogo, Dodoma.
Rais Kikwete aliwasili Dodoma akitokea Mwanza ambako alihudhuria mazishi ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Askofu Mkuu Dkt. Moses Samwel Kulola yaliyofanyika kwenye Kanisa la Bugando Calvary Temple, mjini Mwanza.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
05 Septemba, 2013
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aakiwa ameng'ang'ania Microphone ya sehemu ya Kuzungumzia wapinzani Bungeni wakati polisi walipokuwa wakimtoa Bungeni Mjini Dodoma leo
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akiwa ameng'ang'ania Microphone ya sehemu ya Kuzungumzia wapinzani Bungeni wakati polisi walipokuwa wakimtoa Bungeni Mjini Dodoma leo. hata hivyo Microphone hiyo iling'oka na polisi wakafaikiwa kumtoa nje
Microphone hiyo iling'oka na polisi wakafanikiwa kumtoa nje-
Mbunge wa Kuteuliwa na Mwenyekiti wa NCCR_MAGEUZI, James Mbatia akisahangaa kuona mapambano kati ya wabunge wa CHADEMA na Polisi Bungeni
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi akitolewa na Askari Polisi nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo
Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiongoza wabunge wa CHADEMA kutoka Bungeni mjini Dododma baada ya kuamriwa kufanya hivyo na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai
Mbunge wa Mbeya Mjini akizuiwa na wabunge wa CHADEMA ili asiambane na polisi, Bungeni Mjini Dodoma leo.
Wabunge wa Chadema wakiwa wamesimama kukaidi amri ya Naibu spika, Job Ndugai ya kuwataka wakae chini
Wabunge wa CHADEMA wakipambana na Polisi, Bungeni Mjini Dodoma leo
Baadhi ya waandishi wa habari wakipatiwa huduma ya kwanza baada ya kutokea ajali ya gari walilokuwa wamepanda katika msafara wa wabunge waliokuwa safarini kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro jana ambalo lilipindua eneo la Karatu na kuwajeruhi waandishi wanne ambao walipelekwa kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Karatu.
Baadhi yao wakipatiwa huduma ya kwanza wakipepewa baada ya ajali hiyo.
Hili ndilo gari walilokuwa wamepanda waandishi hao..