Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 152 | 153 | (Page 154) | 155 | 156 | .... | 1897 | newer

  0 0
 • 09/04/13--02:12: Neno La Leo; Vita Na Meza..!
 • Ndugu zangu,

  Bado inaunguruma milio ya ' ngoma za vita' kwenye Ukanda wetu wa Nchi za Maziwa Makuu.

  Ngoma hizi ni za kuzimwa haraka kabla ya waliomo na wasiomo wakalazimishwa kuchanganyika kucheza. Na hakika ni ngoma ya vita vya kiwendawazimu.

  Mama Mary Robinson, Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Nchi za Maziwa Makuu ametua kwenye ukanda wetu. Ana ujumbe mmoja tu katika kupata suluhu ya vita ya Congo; MAZUNGUMZO.

  Na kawaida ya wanadamu hawazungumzi kulimaliza jambo wakiwa wamesimama. Huitafuta MEZA. Ndio, meza ya mazungumzo. Yaweza kuwa meza ya duara au mstatiri, lakini, lililo muhimu ni MEZA.

  Kabla ya ujio wa Wareno hatukuwa na neno meza. Hili ni neno la Kireno, linatamkwa ' Mesa'.  Mama Mary Robinsson anatukumbusha umuhimu wa MEZA. Na ni ukweli, kuwa kwenye mgogoro wowote mwanadamu ni nadra sana akaikimbia meza ili kupata suluhu ya mgogoro. Maana, hata ukipigana vita, bado utaihitaji meza kumaliza vita.

  Wenye kupiga na kufurahia ' ngoma za vita' hawajapendezwa na msimamo wa Mama Mary Robinson. Wao wanataka ' Vita ipiganwe leo' wakiamini shughuli yote inaweza kuisha kesho.

  Hawajui, kuwa Mama Mary Robinson anaposhauri Serikali ya DRC Congo izungumze na M23 kuwa ana uelewa mpana na wa kina wa historia ya Congo. Kimsingi M23 ni tone tu kwenye dimbwi la matatizo ya Congo yenye chimbuko la kihistoria.

  Tusingependa kuona tena mamilioni ya raia wasio na hatia na hususan akina mama na watoto wakitembea maelfu ya kilomita kukimbia makazi yao. Kuishi ukimbizini ndani na nje ya mipaka ya Congo. Tusingependa tena kusikia maelfu kwa maelfu ya akina mama na watoto wakibakwa mchana wa jua kali kwa sababu ya vita. Tusingependa kuona picha za raia wasio na hatia wakiuawa au kujeruhiwa kwenye vita vya kiwendawazimu. Vita ambavyo vingeweza kuepukwa kama hekima na busara ingetangulizwa.

  Ni imani yangu, ni imani ya wengi pia, kuwa juhudi za Mama Mary Robinson za kuzikutanisha pande zote kwenye meza ya mazungumzo zitazaa matunda.

  Na kwa kuanzia, tunataraji Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu unaotarajiwa kuanza kesho pale Kampala utafanyika, na hivyo, kuwa hatua ya kwanza muhimu kwa wahusika kuikaribia meza.

  Mungu Ibariki Afrika.

  Maggid.
  Iringa.
  0754 678 252

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya SILAFRICA Bw Alpesh Patel ambao ni watengenezaji wa vifaa vya plastiki yakiwemo matanki ya kuhifadhia maji ya SIMTANK akisoma taarifa fupi mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa Tanki jipya la Kuhifadhia maji liitwalo SIMTANK la Bluu lenye Ubora wa hali ya juu wakati wa uzinduzi wa SIMTANK jipya uliofanyika katika ofisi zao zilizopo Chang'ombe Jijini Dar Es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu Wa Kampuni ya SILAFRICA Alpesh Patel akimuonyesha Mwanafunzi Wa Shule ya Msingi sehemu ya Kukata Utepe Ikiwa kama Ishara ya Uzinduzi wa SIMTANK jipya lenye ubora wa hali ya juu wakati wa uzinduzi wa SIMTANK jipya uliofanyika katika Ofisi zao zilizopo Chang'ombe Jijini Dar Es Salaam
  Baadhi ya wanafunzi wanaosomeshwa na Kampuni ya SILAFRICA ikiwa kama sehemu ya kurudisha faida kwa jamii wakiwa makini katika uzinduzi wa SIMTANK jipya lenye ubora wa hali ya juu.
  Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya SILAFRICA Alpesh Patel Akikata keki yenye mfano wa SIMTANK lililozinduliwa leo jijini Dar Es Salaam pamoja na Mwanafunzi wa Shule ya Msingi kama Ishara ya Kuzindua tanki Jipya la SIMTANK la Bluu linalotengenezwa na kuuza na Kampuni ya SILAFRICA kupitia kwa mawakala wake
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya SILAFRICA Alpesh Patel ambao ni watengenezaji wa bidhaa za plastiki yakiwemo matanki ya kuhifadhia maji ya SIMTANK akionyesha ubora wa tanki hilo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) endapo tanki hilo la SIMTANK la bluu hata kama likikanyagwa au kukandamizwa baadae linarudi kwenye hali yake ya kawaida bila kuwa na nyufa au kupasuka
  SIMTANK jipya kutoka Kampuni ya SILAFRICA ambao ni watengenezaji wa bidhaa za plastiki yakiwemo Mantaki ya SIMTANK likiwa limeminywa Na gari la kubeba vitu vizito wakati wa uzinduzi wa SIMTANKI jipya la Bluu katika ofisi zao zilizopo Maeneo ya Chang'ombe Jijini Dar Es Salaam jana
   Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya SILAFRICA Bw Alpesh Patel ambao ndio watengenezaji wa bidhaa za plastiki yakiwemo matanki ya SIMTANK akionyesha tanki la SIMTANK jipya lililominywa na gari la kubeba vitu vizito wakati wa uzinduzi wa SIMTANK jipya lenye ubora wa hali ya Juu baada ya kuanza kurudi kwenye hali yake ya kawaida mara baada ya kuminywa na gari la kubeba vitu vizito wakati wa uzinduzi wa SIMTANK jipya la bluu uliofanyika jana Katika Ofisi zao zilizopo Maeneo ya Chang'ombe jijini Dar Es Salaam
  Baunsa wa Wa SIMTANK akionyesha uwezo wake wa kutunisha misuli ikiwa kama ishara ya kuonyesha kuwa matanki yote yanayotengenezwa na kampuni ya SILAFRICA yana ubora wa hali ya juu na magumu na yenye kuaminika na wateja zaidi ya Milioni Moja Afrika Mashariki.

  0 0

  WASHINGTON, September 4, 2013 – Children in sub-Saharan Africa are now less likely to die from diarrhea and pneumonia, but these illnesses are still the most common causes of childhood death and sickness in most African countries, according to a new report published today.   Loss of health due to diarrheal diseases dropped 34% between 1990 and 2010, lower respiratory infections (LRIs) such as pneumonia dropped 22%, and protein-energy malnutrition was down 17%. Several countries documented striking progress, with Malawi reducing diarrheal diseases by 65%, Burundi decreasing LRIs by 44%, and Benin reducing measles by 84% during this time.   Malaria and HIV/AIDS were the leading causes of premature death and disability in 2010 for the region. But in some countries, there has been significant progress in recent years. Between 2000 and 2010, Rwanda recorded a 56% decrease in the rate of healthy years of life lost from malaria, while Botswana cut the rate of premature death and disability from HIV/AIDS by 66%.  These are some of the findings from the new report The Global Burden of Disease: Generating Evidence, Guiding Policy – Sub-Saharan Africa Regional Edition, published today by the World Bank and the Institute for Health Metrics and Evaluation (IHME). 
  “The rapid shifts in disease burden place poor people in low- and middle-income countries at high risk of not having access to appropriate services and incurring payments for health care that push them deeper into poverty,” said Timothy Evans, Director of Health, Nutrition, and Population at the World Bank Group. “The data in these new reports are critical inputs to the efforts of policymakers in countries towards universal health coverage that aim to improve the health of their people, communities, and economies.”   The report also finds that nutritional deficiencies were the leading cause for disability in childhood, mental and behavioral disorders accounted for the most illness during adolescence and young adulthood, while musculoskeletal disorders were the largest drivers of disability in adulthood.   In the region’s upper- and middle-income countries, non-communicable diseases emerged as a significant health threat. From 1990 to 2010, substantial increases in premature mortality and disability were recorded from stroke (up by 31%), depression (up by 61%), diabetes (up by 88%), and ischemic heart disease (or coronary artery disease, up by 37%). Amidst the region’s rapid economic growth, early death and illness from road injuries increased by 76% between 1990 and 2010. Health loss from interpersonal violence also climbed during this time, particularly in the Democratic Republic of the Congo and Lesotho.   “The health landscape in sub-Saharan Africa is changing in unexpected ways,” said Dr. Christopher Murray, IHME Director and one of the lead authors of the GBD study. “Addressing chronic disease and certain communicable diseases will continue to be important, but people in sub-Saharan Africa are dealing with a greater range of illnesses today that aren’t fatal but are definitely disabling.”  The report also identifies trends in leading risk factors that cause the most disability in the region. Under-nutrition during childhood and household air pollution were among the leading factors behind premature death and disability.   Detailed findings for Sub-Saharan Africa and each country in the region are available online in a series of country profiles and data visualization tools


   Watch a live webcast on the presentation of the reports on September 4, 2013, from 10-11:30 a.m. EDThttp://live.worldbank.org/global-burden-disease-webcast.
   On Twitter, join the conversation at @worldbankhealth and @IHME_UW, or follow #GBD2010.


   0 0

   Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania Limited yesterday confirmed receipt of a full operating license issued to them by the Bank of Tanzania.  The license empowers Dun & Bradstreet to offer Credit Bureau and related services in Tanzania.

   The issuance of an operating license by Bank of Tanzania to Dun & Bradstreet brings an end to the long wait of the financial sector for D&B’s services and opens up a new and expectedly rewarding chapter for lenders who seek secure lending, borrowers who seek easy access to credit and other stakeholders who are keen on seeing a stronger and more vibrant economy driven by Tanzania’s financial sector.


   According to Mr. Miguel Llenas, CEO of Dun & Bradstreet Credit Bureaus, the news of the issuance of an operating license to Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania Limited by Bank of Tanzania was received with pleasant delight but also with the understanding that this is an immense responsibility. 

   According to him, “We are delighted at the news of the issuance of the license by Bank of Tanzania and we thank them for taking this positive step by giving us the opportunity to bring our expertise to the benefit of all Tanzanians and everyone who does business in Tanzania.  We consider ourselves a vital part of the financial sector and are well prepared to play our role in protecting and strengthening Tanzania’s economy through its financial sector.”


   Also speaking on the news of the issuance of the license by BoT, General Manager Dun & Bradstreet Credit Bureau in Tanzania – Adebowale Atobatele expressed high optimism that with the support of the B.o.T and the collaborative efforts of all stakeholders, the Credit Reference System as championed by BoT delivers the much anticipated benefits. 

   Mr. Atobatele said, “We are glad that we are finally kicking-off operations in Tanzania and we are very optimistic that with everyone playing their role responsibly, we will be able to create and deliver superior value to all stakeholders.  With the commencement of operations by Dun and Bradstreet Credit Bureau in Tanzania, Banks can now look forward to processing loan applications faster, reducing operational costs and with better information; furthermore, the banking public can now look forward to getting easy access to credit.”


   Dun & Bradstreet is present in 200 countries and has deployed its Credit Bureau solutions in several countries across Africa, Middle-East and Asia.


   For more information:

   Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania Limited

   Tel No: +255-715-DBCBTZ (322289) or +255-716-DBCBTZ (322289)   0 0


   Ndugu, jamaa na marafiki ! 


   Nasikitika kuwataarifu kuwa baba yangu mzazi Wakili Israel Magesa amefariki leo asubuhi ghafla, msiba uko nyumbani kwa marehemu Ukonga Majumba sita.   Taratibu za mazishi zinafanywa hapo, na tunatarajia kumuaga rasmi siku ya ijumaa 6/9/2013 hapa Dar Es Salaam na mazishi yatafanyika kijijini kwetu Chitare, Majita, Musoma Vijijini siku ya jumapili tarehe 8/9/2013.   Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.   Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.   RIP my Dad Israel, one of the very best and dedicated lawyer, a great friend and my mentor.   Phares  Magesa,
   Member of NEC- CCM
   Ag. Director of ICT- TPA
   President - TPN
   Vice President- TBF

   0 0

    Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kushoto), akimpatia tiketi ya ndege na nyaraka zinginezo, Nuru Sinna ambaye ametimiza vigezo kwenda kufanya kazi Dubai, Falme za Kiarabu katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam hivi karibuni. Wanaoshuhudia  ni  Jaffari Kingwande  (wa pili kulia) ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bravo Job Centre iliyofanikisha kupata kazi hiyo pamoja wengine wengi watakaokwenda siku za usoni.Wa pili kushoto ni Mohamed Omari Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo.
    Mtemvu akionesha nyaraka ikiwemo viza, vibali vya kazi pamoja na tiketi ya Nuru Sunna kwenda Dubai. Jaffari Kingwande  (wa pili kulia) ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bravo Job Centre iliyofanikisha kupata kazi hiyokufanyakazi.
    Mtemvu akizungumza katika mkuta na waandishi wa habari, Dar es Salaam, kuhusu changamoto mbalimbali ambazo anazipata katika jitihada zake za kuwatafutia kazi watanzania Falme za Kiarabu. Alisema kuwa baadhi ya maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwemo Waziri Belnald Membe wanashiriki kukwamisha jitihada hizo.
    Mtemvu  (mbele katikati) akiwa katika hafla hiyo.
   Nuru Sunna (kushoto) akiwa na mdogo wake katika hafla hiyo.

   0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kuzindua Benki mpya ya UBL, iliyopo Mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika leo Sept 4, 2013. Kushoto na kulia kwa Makamu wa ni baadhi ya viongozi wa juu wa benki hiyo, Anwar Pervez na Atif Bakhari.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa benki ya UBL iliyozinduliwa leo Sept 4, 2013 jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBL, Zamees Ghudrey, akizungumza wakati alitoa shukrani baada ya uzinduzi huo, uliofanyika leo Sept 4, 2013.
   Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa benki hiyo, wakimsikiliza Makamu wa Rais , wakati alipokuwa akiwahutubia kwenye uzinduzi huo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata Keki maalum iliyoandaliwa kuashiria uzinduzi wa benki hiyo mpya ya UBL, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika leo Sept 4, 2013.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa benki mpya ya UBL, baada ya uzinduzi wa benki hiyo uliofanyika leo, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR.

   0 0

   Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N.Rufunga akizungumza na Maafisa Tarafa wa Mkoa wa Shinyanga kabla hajawakabidhi pikipiki zao jana ofisini kwake ( ofisi ya Mkuu wa Mkoa). 
    Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Dkt.Anselm Tarimo akitoa maelekezo ya utendaji kazi kwa Maafisa  Tarafa Mkoani Shinyanga jana.
    Baadhi ya Maafisa Tarafa wa Mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza Mhe.Mkuu wa Mkoa kabla hawajakabidhiwa pikipiki.
    Hizi ni baadhi ya pikipiki walizokabidhiwa Maafisa tarafa  Mkoani Shy ili ziwasaidiekatika katika utendaji wa kazi zao za serikali.
   =======  =====  =====
   SERIKALI YAGAWA PIKPIKI KWA MAAFISA TARAFA MKOANI SHINYANGA


   Serikali mkoani Shinyanga imewataka Maafisa Tarafa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya maadili ya utumishi wa umma ili kuiboresha kada hiyo inayoonekana kusahaulika siku hadi siku.

   Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Ally N. Rufunga amewaasa Maafisa Tarafa ofisini kwake jana,kabla ya  kuwakabidhi pikipiki 14 aina ya YAMAHA kwa ajili ya tarafa zote za mkoa wa Shinyanga, ili kuwasaidia kuboresha utendaji wao wa kazi za serikali.


   Mhe. Rufunga amewaeleza kuwa,serikali ya mkoa wa Shinyanga imeamua kubadili mfumo, na kuanzia sasa itawatumia Maafisa Tarafa kikamilifu kwani wao wanawajibika kwa Serikali kuu na Mamlaka za serikali za mitaa katika shughuli zote kuanzia kusimamia ulinzi na usalama hadi usimamizi wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao.


   Amewakumbusha pia kuhusu utaratibu wa kuratibu utendaji kazi za serikali katika shughuli mbalimbali katika tarafa zao, na jukumu la kutunza pikipiki hizo.


   Nae Katibu Tawala Mkoa Dkt. Anselm Tarimo amewakumbusha Maafisa Tarafa hao wajibu na maadili ya kazi yao na kuwaeleza kuwa wanatarajiwa sana na serikali katika kupata taarifa sahihi za utekelezaji wa shughuli mbalimbali kwenye tarafa, ili serikali iongeze nguvu pale ambapo wenyewe watakwama.


   Awali, Maafisa tarafa walieleza changamoto zinazowakabili ni pamoja na kutoshirikishwa katika shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hata kutoitwa kwenye vikao vya kisheria na hivyo inakuwa vigumu kwao kuwajibika kwenye shughuli hizo, ambapo uongozi wa Mkoa umeahidi kuzifanyia kazi changamoto hizo kwa kukutana na Wakurugenzi wa Halmashauri zote, ili sheria na kanuni zilizowekwa zifuatwe.

   Na Magdalena Nkulu

   Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Shinyanga.
   0 0

   Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano Mallya akiongea kuhusu kuboreshwa kwa huduma mpya ya Airtel Yatosha inayomwenzesha mteja wa Airtel kupata kifurushi cha maongezi , sms na internet na kuwasiliana na mitandao yoyote nchini, sasa kwa shilingi 499 mteja anapata dakika 20, sms 300 pamoja na kifurushi cha internet cha 125MB.

   Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza kuboresha vifurushi vyake vya huduma ya Airtel yatosha hivyo kuvifanya kuwa bora, vya ushindani na gharama nafuu nchini.

   Akiongea kuhusu kuboreshwa kwa huduma hiyo , Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano Mallya alisema "huduma ya Airtel Yatosha inaendelea kutosha kuliko yoyote nchini! sasa vifurushi vya Airtel yatosha vya siku zimeendelea kuboreshwa na kuwa vya gharama nafuu zaidi, kwa shilingi 499 mteja anapata dakika 20, sms 300 pamoja na kifurushi cha internet cha 125MB. Bei ni poa na ya gharama nafuu ukilinganisha na huduma nyingine za vifurushi zinazotelewa sokoni"

   Bi Singano alisema Sambamba na hili vifurushi vya Airtel yatosha vinamuwezesha mteja kupiga simu kwenda mtandao wowote ule nchini wakati wowote masaa 25 yaani mteja anafaidika na vifurushi hivi kwa masaa 24 na 1 la nyongeza siku saba za wiki.

   Kikubwa na kizuri zaidi mteja anapojiunga na vifurushi hivi anapata nafasi ya kuingia kwenye promosheni yetu kabambe ya Airtel Yatosha Shinda Nyumba na kujishindia pesa taslimu au nyumba za kisasa zilizoko Kigamboni jijini Dar es saalam".

   "Airtel inaendelea na dhamira yake ya kuboresha huduma zake ikiwemo Airtel money yatosha pamoja na vifurushi vya Airtel yatosha vilivyo na gharama nafuu na kukuwezesha kuwasiliana kwa gharama nafuu zaidi ndani na nje ya nchi". aliongeza mmbando.

   Kujiunga na vifurushi mbalimbali vya Airtel yatosha mteja anatakiwa kupiga *149*99# na kuchagua kifurushi kinachokithi mahitaji yake. Airtel yatosha inapatikana katika vifurushi vya siku, wiki au mwezi na vifurushi vyake vinadumu kwa masaa 25 kwa siku.

   0 0

   KITAMBI  SASA  BASI
   ONDOA  KITAMBI KWA  SIKU KUMI NA  NNE

   SHIRIKI  KATIKA  UTAFITI  KUHUSU  UFANISI  WA  TIBA  ASILIA  NA  VYAKULA  LISHE   KATIKA  KUKABILIANA  NA  TATIZO  LA  VITAMBI, UNENE  NA  UZITO..

   Unakabiliwa  na  tatizo  la  kitambi?  Unataka  kuondoa  kitambi  kwa  njia  asilia ? Unataka  kupunguza  uzito  na  unene ? Unataka  kuondoa  manyama  uzembe?

   Kama  jibu  ni  ndio, basi  hii  ni  habari njema  sana  kwako. Neema  Herbalist  &  Nutritional  Foods  Clinic  ni  kituo  cha   Utafiti  wa  Tiba  Asilia . Tunakualika  kushiriki  katika  utafiti   kuhusu  UFANISI  WA  TIBA  ASILIA  KATIKA  KUKABILIANA  NA  TATIZO  LA  VITAMBI, UNENE, & UZITO  KUPITA  KIASI.

   FAIDA  ZA  KUSHIRIKI  KATIKA  UTAFITI  HUU:
   Faida  za  kushiriki  kwenye  utafiti  huu  ni  pamoja:
   ·       Kupatiwa  dawa  ya  asili  ya  kuondoa  kitambi, kupunguza  uzito  na  unene  au  vyote  kwa   pamoja , pamoja   na  kitabu  cha diet  ya  kupunguza  mwili  na  uzito  kwa   PUNGUZO  LA  ASILIMIA  SIHIRINI  (20%)  ya  bei  kamili  ya  dawa .

   ·       Kila  atakaye  shiriki  katika  utafiti  huu, atapewa mwaliko  maalumu  wa  kuhudhuria  bure  kwenye  semina  maalumu  za  kila  mwezi  kuhusu  kuondoa  vitambi, unene  na  uzito   kwa  kutumia  dawa  asilia   na  vyakula  lishe ambazo  zinaandaliwa  na  kituo  chetu   chini  ya  Mradi  wa  Flatbelly   Project  wenye  kauli mbiu  flatbelly  Is  Sexy!


   ·       UHAKIKA  WA  KUONDOA  KITAMBI, KUFANYA  TUMBO  LIWE  FLAT, KUPUNGUZA  UNENE  &  UZITO  KWA  ASILIMIA  MIA  MOJA

   Kila  atakaye  shiriki  katika  utafiti  huu, 
   atapewa guarantee  ya  kupata  matokeo  anayo  yahitaji, iwe  ni  kuondoa  kitambi, kupunguza  tumbo  kabisa  na  kulifanya kuwa  flat, kupunguza  unene na  uzito  au  vyote  kwa  pamoja  kwa  kutumia  tiba  asilia  na   vyakula  lishe. Sisi  kama  kituo  cha  utafiti  wa  tiba  asilia  na  vyakula dawa  tutahakikisha  kila  mtu  anaye shiriki  katika  utafiti  huu  anafikia  asilimia  mia  ya   malengo  ya  kupungua  aliyo  jiwekea.
    

   JINSI  YA  KUSHIRIKI  KATIKA  UTAFITI  HUU : Unaweza  kushiriki  katika  utafiti  huu  kwa  kujaza    dodoso  yetu, kisha  kupatiwa  dawa   ya  kuondoa  kitambi, au  ya  kupunguza  unene  na  uzito(mwili mzima )  pamoja  na   kitabu  cha  diet (lishe)  ya  kupungua  kwa   nusu  gharama  ya  bei  ya  dawa . Bei  ya kawaida  ya  dawa  hii  ni  shilingi  ELFU  HAMSINI  lakini  kwa  wewe  unaye  shiriki    katika  utafiti  huu  utapatiwa  dawa  hii  kwa  punguzo  la  asilimia  hamsini  ya  bei  kamili  ya  dawa, ambapo  utapatiwa  dawa  hii  kwa  shilingi  ELFU  ISHIRINI  NA  TANO   tu.
   UTARATIBU  WA  KUSHIRIKI  KATIKA  UTAFITI  HUU :  Utaratibu  wa  kushiriki  katika  utafiti  huu   upo  kama  ifuatavyo :
   i.                    Kuomba  kushiriki  kwenye  utafiti  huu. Unaweza  kuomba  kushiriki  kwenye  utafiti  huu  kwa  kutuandikia   kwenye  barua  pepe  yetu  ambayo  ni  : neemaherbalist @gmail.com    au  kutupigia  simu  0766538384  au  0767010756  ukiomba  kushiriki  katika  utafiti  huu.

   ii.                Kujaza  dodoso  ya  utafiti  huu  ambapo  utaweka  taarifa  zako  kuhusiana  na  urefu  wako, uzito  wako, unene  na  kitambi  pamoja  na   jambo  unalolitaka mfano; kupunguza  kitambi pekee  na  kulitengeneza  tumbo  kulifanya  kuwa  flat,  au kupunguza  kitambi, unene  na  uzito kwa  pamoja.

   iii.              Baada  ya  hapo utapatiwa  dawa  na  kitabu  pamoja  na  maelekezo  mengine  ya muhimu  kama  vile   ratiba  ya  kushiriki  kwenye  semina  maalumu  kuhusu  kuondoa  vitambi, na  kupunguza  uzito,& unene  kwa  njia  ya  dawa  asilia  na  vyakula  dawa

   iv.              Baada  ya  kumaliza    kutumia  dawa  pamoja  na diet , tutarejea  kwako  kwa  ajili  ya  kuchukua  taarifa  za  matokeo  ya  dawa  yetu.

   v.                 Taarifa  zako  zitatumika  katika   ripoti  ya  matokeo  ya  utafiti  wetu  itakayo  tolewa   mwezi  Januari 2014.


   Kama  una  tatizo  la  kitambi, unene, na  au  uzito, na  unataka  kushiriki  katika  utafiti  huu, wasiliana  nasi  kwa  simu  ;0766538384  AU  0767010756  AU  tuandikie  barua  pepe
   neemaherbalist@ gmail.com   AU  Tutembelee  katika  ofisi zetu  zilizopo  jijini  Dar  Es  salaam, katika  eneo  la  CHANGANYIKENI  lilipo  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU.

   Kwa  maelezo  zaidi  kuhusu  huduma  za  Neema  Herbalist, tembelea


   0 0

    Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akimkaribisha Balozi wa Sudan hapa nchini, Dk. Yassir Mohamed Ali,kabla ya mazungumzo naye, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza na Balozi wa Sudan hapa nchini, Dk. Yassir Mohamed Ali, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Saloaam.(Picha na Bashir Nkoromo).

   0 0

    

   Kamati ya Ushauri ya Ugawaji wa Vitalu vya Utalii ikiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Suedi Kagasheki  (mwenye kaunda suti) na Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Ibrahim Mussa (wa kwanza kulia).


   Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamis Suedi Kagasheki amezindua rasmi Kamati ya Ushauri ya Ugawaji wa Vitalu vya Utalii  nchini.

   Kamati hiyo inaundwa na wajumbe 10 kutoka sekta mbalimbali inajukumu la kumshauri waziri katika masuala yote yalioainishwa  kwenye sheria na kanuni za Wanyamapori juu ya ugawaji vitalu. 

   Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Selous uliopo Wizara ya Maliasili na Utalii Makao Makuu, Dar es Salaam, Mhe. Kagasheki alisema anaimani kamati hiyo itamsaidia kwa kumpa ushauri utakaokuwa umefanyiwa utafiti wakina kutokana na kamati hiyo kuundwa na watu wenye uweledi na uzoefu mbalimbali katika masuala ya usimamizi wa raslimali na maliasili.

   Aidha, Mhe. Kagasheki aliwataka wajumbe wa kamati hiyo kutekeleza majukumu waliopewa kwa kushirikiana kikamilifu na kwa kuzingatia maslahi ya taifa.

   Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Ugawaji wa Vitalu, Prof. Leticia Rutashobya alimshukuru Mhe. Waziri kwa kumpa jukumu la kuongoza kamati hiyo na kuahidi kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kwa uadilifu.

   Kamati ya Ushauri wa Ugawaji wa Vitalu inaundwa na Prof. Leticia Rutashobya (mwenyekiti) na wajumbe wake Mhe. Zakhia Hamdan Meghji, Bw. Alli Mufuruki, Bw. Mohamed Abdukadir, Bw. Raymond Mbilinyi, Dkt. Simon Mduma, Bw. Allan Kijazi, Dkt. Fred Manongi, Prof. Alexander N. Songorwa na Bi. Agnes Ndumati; na itahudumu hadi tarehe 15 Julai, 2016.   0 0

    Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Said Meck Sadiki (kulia) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Skauti Mkuuwa Chama cha Skauti Tanzania Hajati Mwantum Mahiza (kushoto) katika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.
    Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo(kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania  Hajati Mwantum Mahiza (kushoto) kwa ajili ya kuukabidhi Mwenge kwa Mkoa wa Dar es Salaam, katika makabidhiano yaliyofanyika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.

    Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Barnabas Ndunguru akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa kabla ya Mwenge huo kukabidhiwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam Kulia ni Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Assah Mwambene. 

    Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mmoja wa wakimbiza Mwenge Kitaifa Zamda John (Tanga) katika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.

   Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Juma Ali Simai akitoa salamu za shukrani kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Hajati Mwantum Mahiza (aliyevaa Miwani) kabla ya kuukabithi Mwenge huo kwa Mkoa wa Dar es Salaam, katika makabidhiano yaliyofanyika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.


    Kaimu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo(kushoto) akipokea Mwenge wa uhuru kutoka kwa Mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa, katika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.

   Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Said Meck Sadiki akitoa taarifa fupi mara baada ya kupokea Mwege wa Uhuru leo Jijini Dar es Salaam katika uwanja wa ndege wa Terminal one. Picha na Hassan Silayo-MAELEZO   0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. M.K.Tarishi amemteua Bw. Chikambi Karugendo Rumisha (57) kuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
   Katibu Mkuu amefanya uteuzi huo kwa mamlaka aliyo nayo chini ya Kifungu cha 6 (b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 2003.

   Bw. Rumisha ameitumikiwa Wizara tangu mwaka 1984 katika idara mbalimbali hali inayompa uzoefu na uelewa mkubwa wa masuala mbalimbali yanayohusu Wizara ya Maliasili na Utalii.

   Kabla ya uteuzi huo Bw. Rumishaalikuwa akitumikia Wizara ya Maliasili na Utalii katika Idara ya Sera na Mipango.


   Bw. Chikambi Rumisha ambaye ni mtaalam wa elimu viumbe alihitimu Shahada ya Sayansi – Ekolojia ya Bahari na Wanyama katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1984.     Bw. Rumisha ameitumikia Serikali katika vituo mbalimbali, pamoja na Makao Makuu ya Wizara idara ya Uvuvi alipohudumu kama Afisa Uvuvi, Kilichokuwa Chuo cha Uvuvi Nyegezi- Mwanza alipohudumu kama mkufunzi, Marine Parks alipohudumu Kama Meneja na Mwazilishi wa Taasisi hiyo na  Makao Makuu ya Wizara -Idara ya Sera na Mipango kitengo cha Ufuatiliaji .


   Uteuzi huu wa Bw. C.K.Rumisha unafuatia kustafu kwa aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino ya Serikali wa Wizara, Bw. George Matiko kustaafu tangu tarehe 15/06/2013.


   Bw. Chikambi K Rumisha uteuzi wake unanzia tarehe 15/8/2013na utadumu hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo.


   Katibu Mkuu


   Wizara ya Maliasili na Utalii


   0 0

    WALE MABINGWA WA COSMETICS ZA UKWELI KUTOKA MBELE MBELE, AK CLASSIC COSMETICS SASA WAMEWASHUSHIA MZIGO WA VITU VYA TOFAUTI KABISA!!  KUANZIA PRODUCTs ZA KUPUNGUA,TIBA ZA CHUNUSI,PRODUCTs ZA KUNG'ARISHA NGOZI YAKO,DAWA ZA KUONDOA STRETCH MARKS, BODY SHAPERs...SASA LEO KUNA BIDHAAA ZINGINE LUKUKI MUPYAAAAAA!!EM TUONGOZANE HAPA..

    KWA MAELEZO NA PICHA ZAIDI WATEMBELEE www.akclassic.blogspot.com
    KUWEKA ODA NA KUFIKISHIWA BIDHAA MPAKA ULIPO PIGA  0753-482909/0713-468393.

   0 0

   MAONI YA MSEMAJI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA SHERIA NA KATIBA, MHESHIMIWA TUNDU A.M. LISSU KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA, YA MWAKA 2013 (Kanuni ya 86(6) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2013)
    
   UTANGULIZI

   Mheshimiwa Spika,

   Huu ni Muswada wa marekebisho ya pili ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Sheria za Tanzania. Kama Bunge lako tukufu litakavyokumbuka, Sheria hii ilifanyiwa marekebisho ya kwanza kwa kupitishwa kwa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Na. 2 ya mwaka 2012, mwezi Februari ya mwaka jana. Mabadiliko hayo ya kwanza yalihusu Sehemu ya Tatu na ya Nne ya Sheria hii, na yalilenga vifungu mbali mbali vinavyohusu Tume ya Mabadiliko ya Katiba na utekelezaji wa majukumu yake.

   Muswada huu wa sasa unalenga kufanya marekebisho katika Sehemu ya Tano ya Sheria inayohusu ‘Kuitisha Bunge Maalum.’ Sambamba na mapendekezo haya, kuna mapendekezo ya kufanya marekebisho katika Sehemu ya Sita kwa kufuta vifungu vya 32 hadi 36 vya Sheria vinavyohusu utaratibu wa kura ya maoni kwa ajili ya kuhalalisha ‘Katiba Inayopendekezwa.’ Marekebisho haya yamewekwa katika aya ya 57 ya Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni, 2013. Mapendekezo ya Muswada huu ni muhimu lakini yana utata mkubwa.

   Mheshimiwa Spika,

   Katika kutekeleza majukumu yake ya kuuchambua Muswada huu, Kamati ya Bunge lako tukufu ya Katiba, Sheria na Utawala ilikutana na wadau wengi mbali mbali. Hivyo, kwa mfano, Kamati ilipata maoni ya taasisi za kidini na za kiraia; taasisi za elimu ya juu na za kitaaluma; vyama vya siasa na asasi nyingine. Kwa sababu ambazo Kamati haikuelezwa vizuri na uongozi wa Bunge hili tukufu, mapendekezo ya Kamati kwenda Zanzibar kwa lengo la kukusanya maoni ya wadau wa Zanzibar juu ya Muswada huu muhimu kwa mustakbala wa Jamhuri ya Muungano yalikataliwa.

   Kwa maana hiyo, ni muhimu Bunge lako tukufu lifahamu ukweli huu kwamba wadau pekee walioshirikishwa kutoa maoni yao juu ya Muswada ni Watanzania Bara tu. Wazanzibari hawakupatiwa fursa hiyo na hawakushirikishwa kabisa, licha ya Sheria yenyewe kuwa na mambo mengi yanayoihusu Zanzibar. Kwa vile wadau wa Zanzibar walishirikishwa kikamilifu kutoa maoni yao kuhusu Muswada uliopelekea Sheria hii kutungwa mwaka 2011, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka kujua ni kwa nini uongozi wa Bunge na wa Serikali umeona si busara na sahihi kuwapatia Wazanzibari fursa ya kutoa maoni yao kuhusu Muswada huu wa kurekebisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inawahusu pia Wazanzibari na nchi yao.

   URAIS WA KIFALME KWA MARA NYINGINE TENA!!!!

   Mheshimiwa Spika,

   Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imepigia kelele jitihada za serikali hii ya CCM kudhibiti mchakato wa Katiba Mpya kwa kuendeleza kile tulichokiita miaka miwili iliyopita, “... kivuli kirefu cha Urais wa Kifalme katika mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya.” Hapo tulikuwa tunazungumzia mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wajumbe na watendaji wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, na tulisema kwamba mamlaka hayo yalikuwa na lengo moja tu: “kuhakikisha kwamba matokeo ya kazi ya Tume hiyo ni yale tu yanayotakiwa na Rais na Serikali yake na chama chake cha CCM.”

   Mheshimiwa Spika,

   Katika Maoni yetu wakati wa kutungwa kwa Sheria hii mwezi Novemba mwaka 2011, Kambi Rasmi ya Upinzani ilipinga vikali mapendekezo ya kumwezesha Rais kuteua Wajumbe wa Bunge Maalum wasiotokana na Bunge lako tukufu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Tulisema yafuatayo kuhusiana na jambo hili: “... wajumbe ... wanaopendekezwa kuteuliwa kwenye Bunge la Katiba kwa mujibu wa ibara ya 20(2)(e) na (4) ya Muswada Mpya sio, na hawawezi kuwa, wawakilishi wa wananchi. Kwanza, hawajachaguliwa na mtu yeyote na wala taasisi zao kuwawakilisha katika Bunge la Katiba kwa sababu Muswada Mpya unapendekeza wateuliwe na Rais.”

   Kwa sababu ya upinzani huo, mapendekezo ya kumfanya Rais kuwa mteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum wasiokuwa wabunge na Wawakilishi yaliondolewa katika Muswada huo wa Sheria hii. Badala yake, kifungu cha 22(1)(c) cha Sheria iliyotungwa na Bunge lako tukufu kiliweka wazi kwamba “wajumbe mia moja sitini na sita [watateuliwa] kutoka ...” taasisi zilizotajwa katika kifungu hicho.

   Mheshimiwa Spika,

   Ni kweli kwamba kifungu cha 22(1)(c) kama kilivyotungwa kilileta giza badala ya mwanga katika suala la uteuzi wa wajumbe hao. Kama tulivyoieleza timu ya wataalamu wa Serikali kufuatia mkutano wetu na Rais Jakaya Kikwete uliofanyika Ikulu tarehe 26 Novemba, 2011: “Toleo la Kiswahili la Sheria linasema kwamba wawakilishi wa makundi mengine ‘watakaoteuliwa kutoka’ kwenye makundi yaliyoorodheshwa. Toleo la Kiingereza linasema wajumbe hao watakuwa ‘drawn from’ (kwa tafsiri ya Kiswahili ‘watachukuliwa kutoka’). Maana za maneno haya hazifanani na wala hayako wazi kuhusu nani ‘atakayewateua’ au ‘kuwachukua’ wajumbe hao kutoka kwenye taasisi zao.”

   Kwingineko katika mkutano wetu na Rais Kikwete tulimweleza kwamba: “Wajumbe 166 wengine wanaowakilisha taasisi nje ya Wabunge na Wawakilishi hawajachaguliwa na mtu yeyote na wala na taasisi zao kwani Sheria haisemi ni nani atakayewateua na/au kuwachagua.” Kwa sababu hiyo, tulipendekeza kwamba “Sheria iweke wazi kwamba wajumbe hawa ‘watateuliwa na’ taasisi zilizotajwa. Hii itaondoa utata juu ya uwakilishi wao na juu ya mamlaka yao ya uteuzi.”

   Mheshimiwa Spika,

   Mapendekezo ya marekebisho yaliyoko kwenye Muswada huu yanaonyesha wazi kwamba ushauri wetu kwa Rais Kikwete na kwa timu yake ya watalaamu umepuuzwa. Badala yake, serikali hii sikivu ya CCM imeamua kuturudisha nyuma kwa zaidi ya miaka miwili kwa kuibua tena pendekezo la kumfanya Rais kuwa mteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum wasiotokana na Wabunge au Wawakilishi wa Zanzibar. Hii ni kwa sababu aya ya 3 ya Muswada inapendekeza kwamba wajumbe hao sasa wateuliwe Rais. Hiyo ni sawa na kusema kwamba kilichokuwa hakifai miaka miwili iliyopita sasa kinafaa; na kilichokataliwa wakati ule sasa kinakubalika!

   Ili kuficha ukweli kwamba mwenye mamlaka ya uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum wasiokuwa Wabunge au Wawakilishi ni Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, Muswada unapendekeza kuongezwa kwa vifungu vidogo vipya viwili katika kifungu cha 22. Kwanza, inapendekezwa kuwe na kifungu kidogo cha (2A) ambacho kitamruhusu Rais kualika kila kundi lilioainishwa katika kifungu kidogo cha 1(c) “kuwasilisha kwake orodha ya majina ya watu wasiozidi watatu ili kuteuliwa kuwa wajumbe.” Pili, inapendekezwa kuwe na kifungu kidogo cha (2B) kitakachomlazimu Rais kuzingatia sifa na uzoefu wa watu waliopendekezwa, na usawa wa jinsia wakati wa kufanya uteuzi wa wajumbe hao.

   Mheshimiwa Spika,

   Mapendekezo ya kumpa Rais mamlaka ya kuteua wajumbe wa Bunge Maalum hayakubaliki na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaliomba Bunge lako tukufu lisiyapitishe kuwa Sheria. Kwanza, mapendekezo haya yanarudisha dhana kwamba wajumbe hawa watakuwa watu wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM. Rais Kikwete na chama anachokiongoza ni wadau wakubwa wa mchakato wa Katiba Mpya na wana maslahi halisi na makubwa ya kuhakikisha kwamba matakwa ya chama chao ndio yanakuwa Katiba Mpya ya nchi yetu.

   Ushahidi wa maslahi haya ya CCM ni kile kinachoitwa Ufafanuzi Kuhusu Rasimu ya Kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Wanachama na Viongozi wa CCM uliotolewa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM tarehe 10 Juni, 2013. Katika Ufafanuzi huo, CCM imekataa mapendekezo yote muhimu yaliyoko kwenye Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume. Needless to say, Rais Kikwete ni Mwenyekiti wa vikao vyote vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM. Kumpa Rais, na Mwenyekiti wa CCM Taifa, mamlaka ya kuteua wajumbe wa Bunge Maalum litakaloijadili – na kuikubali au kuikataa – Rasimu ya Katiba ambayo chama chake kimekwishaikataa ni sawa na kuipa CCM fursa nyingine ya kujaza Bunge hilo na makada wake kwa lengo la kutekeleza matakwa ya chama hicho.

   Pili, hata bila wajumbe hawa kuteuliwa kwa namna inayopendekezwa, tayari CCM peke yake ina zaidi ya 72% ya wajumbe wote wa Bunge Maalum wanaotokana na Wabunge na Wawakilishi. Kumpa Mwenyekiti wa CCM mamlaka ya kuteua wajumbe wengine zaidi, kama inavyopendekezwa katika Muswada huu, ni kutoa mwanya kwa CCM kutumia kivuli cha makundi ya kiraia, taasisi za kidini na makundi mengine ili kujiongezea wajumbe wengine zaidi, na hivyo kuhakikisha kwamba Bunge Maalum litatekekeleza matakwa ya kuendeleza status quo.

   Kwa maneno mengine, Serikali hii ya CCM na Wabunge wake inataka Mwenyekiti wao wa Taifa ayachagulie makanisa na awachagulie Wakristo wawakilishi wao katika Bunge Maalum; awachagulie Waislamu wa BAKWATA, Baraza Kuu, JUMAZA na taasisi nyingine za Kiislamu wawakilishi wao katika Bunge hilo; avichagulie vyama vya siasa vinavyoipinga CCM wawakilishi wao; awachagulie wafanyakazi, wakulima, wafugaji, wahadhiri, wanafunzi, wafanyabiashara, walemavu na makundi mengine ya kijamii wawakilishi wao katika Bunge Maalum! Kama ni hivyo, hilo halitakuwa Bunge Maalum la Watanzania, bali litakuwa Bunge Maalum la CCM na Mwenyekiti wao. Hili halikubaliki kwa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na, tunaamini, halitakubalika kwa wananchi wa Tanzania katika ujumla wao.

   Tatu, kwa jinsi yalivyo kwa sasa, mapendekezo haya hayawezi kutekeleza matakwa ya kifungu cha 22(1)(c) cha Sheria kinachotaka wajumbe wa Bunge Maalum wasiotokana na wabunge au wawakilishi kuwa mia moja sitini na sita. Hii ni kwa sababu, hata kama watu wote waliopendekezwa na makundi yaliyoainishwa na kifungu hicho watateuliwa kuwa wajumbe, bado idadi yao itakuwa wajumbe ishirini na saba kwa kuwa makundi yenyewe yako tisa tu! Muswada uko kimya juu ya wajumbe wengine mia moja thelathini na tisa watatoka wapi na watateuliwa na nani na kwa utaratibu upi.

   Kuna hoja kwamba utaratibu wa uteuzi wa wajumbe unaopendekezwa na Muswada unafanana na uteuzi wa wajumbe wa Tume ulioko kwenye kifungu cha 6(6) cha Sheria ambapo Rais alialika vyama vya siasa, jumuiya za kidini, asasi za kiraia, n.k., kuwasilisha orodha ya majina ya watu ili kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume. Hoja hii sio sahihi. Kwanza, Tume ya Katiba sio sawa na Bunge Maalum. Tume ni chombo cha kitaalamu chenye majukumu ya kitaalamu ya kukusanya maoni ya wananchi, kuandaa ripoti pamoja na Rasimu ya Katiba. Uhalali wa Tume unatokana na utaalamu wa wajumbe wake na weledi katika kutekeleza majukumu yao ya kitaalamu.

   Kwa upande mwingine, Bunge Maalum ni chombo cha uwakilishi ambacho wajumbe wake wana majukumu ya kisiasa ya kuwakilisha wananchi wa makundi mbali mbali kwenye kazi ya kisiasa ya kuandika Katiba Mpya. Uhalali wa Bunge Maalum unatokana na upana na ubora wa uwakilishi wake wa makundi mbali mbali ya kisiasa na kijamii. Chombo cha uwakilishi cha aina hii lazima kitokane na wananchi na/au makundi ya kijamii kinachoyawakilisha ili kiwe na uhalali wa kisiasa. Dhana ya Rais – na Mwenyekiti wa CCM – kuteua Wajumbe wa Bunge Maalum inavuruga au kuondoa kabisa dhana ya uwakilishi wa wananchi na uhalali wa kisiasa katika mchakato wa Katiba Mpya.

   Pili, kumpa Rais mamlaka ya kuteua wajumbe wasiokuwa Wabunge au Wawakilishi wa Zanzibar kunaleta dhana ya ubaguzi. Hii ni kwa sababu, Rais hana mamlaka ya kuteua wajumbe wa Bunge Maalum watakaotoka kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Hawa wataingia katika Bunge Maalum kwa mujibu wa nafasi zao Bungeni au katika Baraza na sio kwa fadhila ya Rais. Swali la kujiuliza hapa ni kwa nini Rais awe na mamlaka ya kuteua wajumbe wasiokuwa Wabunge au Wawakilishi wakati hana mamlaka hayo kuhusu Wabunge na Wawakilishi? Needless to say, ubaguzi huu unaenda kinyume na matakwa ya ibara ya 13(2) ya Katiba ya sasa na, kwa hiyo, haukubaliki.

   Tatu, uteuzi wa wajumbe wa Tume uliofanywa na Rais na ambao unatumiwa kama mfano wenyewe ulikuwa na walakini kubwa. Katika hili, kuna ushahidi wa wawakilishi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Kikristo Tanzania (CCT) na asasi mbali mbali za kiraia zikiwemo za walemavu waliowasilisha maoni ya taasisi zao kwa Kamati juu ya Muswada huu. Wawakilishi hao waliiambia Kamati kwamba ijapokuwa waliandikiwa na Rais kuwasilisha majina ya wajumbe wao kwa ajili ya kuteuliwa kwenye Tume, na walifanya hivyo, hakuna hata moja ya majina waliyopendekeza aliyeteuliwa na Rais kuwa wajumbe wa Tume.

   Badala yake, Rais aliteua watu aliowaona yeye na washauri wake wanafaa. Kama taarifa za wadau hawa ni za kweli maana yake ni kwamba Rais na Mwenyekiti huyu wa CCM Taifa hawezi kuaminika tena kuteua wajumbe halisi wa taasisi hizi katika Bunge Maalum ambalo ndilo litakalojadili na kuipitisha – au kuikataa - Rasimu ya Katiba Mpya ambayo tayari CCM na wapambe wao wametamka wazi kwamba wanaikataa!

   WAJUMBE WA BUNGE MAALUM WAONGEZWE

   Mheshimiwa Spika,

   Ili kutatua mkanganyiko huu, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza Bunge lako tukufu lirejee na kukubali mapendekezo yetu kwa Timu ya Wataalamu wa Serikali ya Januari mwaka jana:

    “Sheria iweke wazi kwamba wajumbe hawa ‘watateuliwa na’ taasisi zilizotajwa. Hii itaondoa utata juu ya uwakilishi wao na juu ya mamlaka yao ya uteuzi;
    

    “Sheria itaje kwamba idadi ya wajumbe wa Bunge Maalum watakaotokana na kila taasisi iliyoorodheshwa katika kifungu cha 22(1)(c) itakuwa 354 kama walivyoorodheshwa hapa chini:
   (a) “Asasi zisizokuwa za kiserikali zilizotajwa katika aya (i) zifafanuliwe kuwa ni makundi yanayounganisha asasi hizo, yaani, ANGOZA, TANGO, TACOSODE na Jukwaa la Katiba na kila moja ya makundi hayo itakuwa na wajumbe watano kwa jumla ya wajumbe 20;
   (b) “Asasi za kidini zilizotajwa katika aya (ii) zifafanuliwe kuwa ni makundi yanayounganisha asasi hizo, yaani, BAKWATA, Baraza Kuu, JUMAZA, TEC, CCT na PCT na kila moja ya makundi hayo itakuwa na wajumbe watano kwa jumla ya wajumbe 30. Aidha, Waadventista wa Sabato (SDA), Hindu, Shia Ithnaasheri na Sikh watakuwa na mjumbe mmoja mmoja, kwa jumla ya wawakilishi 35 wa taasisi za kidini;
    

   (c) “Vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu vilivyotajwa katika aya (iii) vitakuwa na wajumbe 72 watakaogawanywa katika makundi mawili: 1) vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu vitakuwa na wajumbe 42 ikiwa ni wajumbe wawili kwa kila chama; 2) vyama vya siasa vyenye uwakilishi Bungeni vitakuwa na wajumbe 30 ikiwa ni CCM 18, CHADEMA 7, CUF 3 na NCCR-Mageuzi, TLP na UDP 3 kwa ujumla wao. Hii ni kufuatana na uwiano wa kura zote za Wabunge ambazo vyama hivyo vilizipata kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2010;
    

   (d) “Taasisi za elimu ya juu zilizotajwa katika aya (iv) zifafanuliwe kuwa ni vyuo vikuu 28 vinavyotambuliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na vyuo vya elimu ya juu 16 vinavyotambuliwa na Baraza la Elimu ya Ufundi la Taifa (NACTE). Taasisi hizi zitakuwa na mjumbe mmoja kwa kila moja kwa jumla ya wajumbe 44;
    

   (e) “Taasisi za elimu ya juu zinahusisha pia vyama vya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ambavyo vitakuwa na mjumbe mmoja mmoja kwa chama cha wanafunzi kwa jumla ya wajumbe 44;
    

   (f) Taasisi za elimu ya juu zinahusisha pia vyama wahadhiri/wakufunzi wa vyuo vya elimu ya juu ambavyo vitakuwa na mjumbe mmoja mmoja kwa kila chama kwa jumla ya wajumbe 44;
    

   (g) “Makundi yenye mahitaji maalum yaliyotajwa katika aya (v) yafafanuliwe kuwa ni mashirika yanayowakilisha wenye ulemavu wa macho, ngozi, viziwi/bubu, viwete na walemavu wa aina nyingine ambayo yatakuwa na wajumbe 10 kwa ujumla wao;
    

   (h) “Vyama vya wafanyakazi vilivyotajwa katika aya (vi) vifafanuliwe kuwa ni vile vilivyosajiliwa na vitakuwa na wajumbe 40 ikiwa ni wajumbe wawili kutoka kila chama cha wafanyakazi kilichosajiliwa;
    

   (i) “Jumuiya ya wakulima iliyotajwa katika aya (vii) itakuwa na wajumbe 10 watakaotokana na vyama vya wakulima wa mazao kama vile pamba, kahawa, korosho, chai, katani, karafuu, miwa na wavuvi;
    

   (j) “Jumuiya ya wafugaji iliyotajwa katika aya (viii) itakuwa na wajumbe 10 watakaotoka Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Wafugaji na Wawindaji/wakusanya matunda ya porini (PINGOS Forum);
    

   (k) “Vikundi vingine vya watu wenye malengo yanayofanana vilivyotajwa katika aya (ix) vifafanuliwe kumaanisha Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Chama cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC); Chama cha Wafanyabiashara ya Madini na Nishati (TCME); vyama/mashirika ya wachimbaji madini wadogo wadogo; Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOWAT), Chama cha Waandishi Habari/Jukwaa la Wahariri Tanzania, Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Chama cha Mawakili Zanzibar (ZLS), Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET) na Chama cha Wakandarasi Tanzania (CATA). Makundi haya yatakuwa na wajumbe wawili kwa kila moja kwa jumla ya wajumbe 26.”
    

   Mheshimiwa Spika,

   Kwa mujibu wa kifungu cha 22(1) cha Sheria kama ilivyo sasa, Bunge Maalum litakuwa na jumla ya wajumbe 604, yaani Wabunge 357, Wawakilishi 81 na wajumbe 166 wanaowakilisha makundi mbali mbali. Mapendekezo haya ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni yatafanya uwakilishi katika Bunge Maalum kupanuka hadi wajumbe 792 kwa Tanzania yenye idadi ya watu milioni 45 kwa takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.

   Hili, kwa vyovyote vile, ni ongezeko kubwa la wajumbe wa Bunge Maalum. Hata hivyo, ukubwa huu unaopendekezwa hauna tofauti kubwa sana na Mabunge Maalum ya nchi nyingine ambazo zimekamilisha utungaji wa Katiba Mpya kwa kutumia utaratibu huu. Kwa mfano, Bunge Maalum la Jamhuri ya Nepal la mwaka 2011 lilikuwa na wajumbe 601 kwa nchi yenye idadi ya watu milioni 26; Bolivia (2009) lilikuwa na wajumbe 255 katika nchi yenye watu milioni 9; Kenya (2005) lilikuwa na wajumbe 629 kwa idadi ya watu milioni 31; Eritrea (1997) lilikuwa na wajumbe 527 kwa idadi ya watu milioni 3.2, wakati Bunge Maalum la Ufaransa ya Mapinduzi ya 1789 lilikuwa na wajumbe 1145 katika nchi iliyokuwa na idadi ya watu milioni 28.

   Kikubwa na muhimu zaidi, kwa mapendekezo haya, ni kwamba Bunge Maalum la Katiba litakuwa na sura ya Kitanzania zaidi badala ya utaratibu wa sasa unaolifanya Bunge Maalum kuonekana la kiCCM zaidi. Kwa kuongezea tu, Mheshimiwa Spika, wadau karibu wote waliotoa maoni yao kwenye Kamati walipendekeza kuongezwa kwa idadi ya wajumbe wa Bunge Maalum. Kwa kigezo chochote kile, kwa hiyo, mapendekezo haya ni ya kidemokrasia na tunaliomba Bunge lako tukufu liyaunge mkono ili kuiwezesha nchi yetu kujipatia Katiba Mpya yenye sura halisi ya kitaifa kuliko inavyopendekezwa sasa.

   UWAKILISHI WA ZANZIBAR KATIKA BUNGE MAALUM

   Mheshimiwa Spika,

   Tume ya Mabadiliko ya Katiba imekwishatoa Rasimu ya Katiba kwa mujibu wa kifungu cha 19(1)(d) cha Sheria. Rasimu hiyo imepndekeza mabadiliko makubwa katika muundo wa Jamhuri ya Muungano kwa kupendekeza muundo wa shirikisho lenye serikali tatu. Baada ya kukamilika kwa mchakato wa kutoa maoni juu ya Rasimu hii kwa mujibu wa kifungu cha 18, Tume itawasilisha ripoti kwa Rais na kwa Rais wa Zanzibar kwa mujibu wa kifungu cha 20(1). Baada ya hapo, Rais, “... atachapisha Rasimu ya Katiba katika Gazeti la Serikali na kwenye magazeti mengine pamoja na maelezo kwamba Rasimu ya Katiba itawasilishwa kwenye Bunge Maalum kwa ajili ya kupitishwa Katiba inayopendekezwa.”

   Mheshimiwa Spika,

   Ili kutimiza matakwa haya ya Sheria na kwa kuzingatia mapendekezo ya Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume, Bunge lako tukufu linahitaji kuangalia upya suala la uwakilishi wa Zanzibar katika Bunge Maalum. Kwa mujibu wa kifungu cha 22(2) cha Sheria, idadi ya wajumbe wa Zanzibar katika Bunge Maalum watakaotokana na makundi yaliyoainishwa katika kifungu cha 22(1)(c) “... haitapungua theluthi moja ya wajumbe hao.” Hii ina maana kwamba, kwa uchache kabisa, wajumbe hao wa Zanzibar hawatapungua 55.

   Rasimu ya Katiba itakayojadiliwa na Bunge Maalum inahusu Katiba ya Jamhuri ya Muungano peke yake. Rasimu hiyo imependekeza kwamba masuala yote yasiyo ya Muungano ya Washirika wa Muungano, yaani Tanzania Bara na Zanzibar, yashughulikiwe na Katiba za Washirika hao.

   Kwa sasa Wabunge wanaotoka Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano ni 83, wakati Baraza la Wawakilishi Zanzibar lina wajumbe 76. Kwa ujumla, kwa hiyo, ili kutekeleza matakwa ya kifungu cha 22(1) na (2) cha Sheria, Zanzibar itakuwa na wajumbe 219 katika Bunge Maalum lenye wajumbe 604, sawa na takriban 36% ya wajumbe wote. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka kujua: kama ilikuwa busara na sahihi kwa nusu ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoka Zanzibar, kwa nini isiwe busara na sahihi vile vile kwa nusu ya wajumbe wa Bunge Maalum litakaloijadili na kuipitisha Katiba Mpya hiyo kutoka Zanzibar? Au ndio kusema kwamba hoja za usawa kati ya nchi Washirika wa Muungano huu ni kelele za majukwaani tu?

   Mheshimiwa Spika,

   Profesa Palamagamba J.A.M. Kabudi wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mjumbe wa Tume aliwahi kusema kwenye Semina ya Wabunge Juu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba iliyofanyika hapa Dodoma tarehe 12 Novemba 2011 kwamba: “Katika kuandika katiba mpya, wabia wa Muungano wanarudi kwa usawa.” Kwa sababu hiyo, na kwa kuzingatia mapendekezo ya ‘hadhi na haki sawa’ baina ya Washirika wa Muungano yaliyoko katika Rasimu ya Katiba, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba idadi ya wawakilishi wa Zanzibar katika Bunge Maalum iongezwe hadi kufikia nusu ya wajumbe wote wa Bunge Maalum.

   Hili linawezekana kwa namna mbili. Kwanza, kwa kuongeza idadi ya wajumbe waliotajwa katika kifungu cha 22(1)(c) hadi 354 kama tulivyopendekeza katika Maoni haya. Na pili, kwa kurekebisha kifungu cha 22(2) ili kisomeke kwamba idadi ya wajumbe kutoka Zanzibar ‘haitapungua asilimia hamsini na tano ya wajumbe hao.’ Kama pendekezo hili litakubaliwa na Bunge lako tukufu, wajumbe wa Bunge Maalum kutoka Zanzibar wataongezeka kutoka 214 kwa mujibu wa Sheria ilivyo sasa, hadi 323. Muhimu zaidi, Bunge Maalum litakuwa limetimiza matakwa ya usawa wa Washirika wa Muungano kwa kuwa na idadi sawa ya wajumbe katika Bunge hilo. Hili litaondoa manung’uniko yanayoweza kujitokeza baadae kwamba Wazanzibari hawakutendewa haki sawa katika Bunge la Katiba.

   WATUMISHI WA BUNGE MAALUM

   Mheshimiwa Spika,

   Muswada unapendekeza marekebisho mengine katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Hivyo basi, aya ya 4 inapendekeza marekebisho ya kifungu cha 24(4) kama ifuatavyo: “Katibu wa Bunge Maalum baada ya kushauriana na Naibu wake na taasisi husika, atateua kutoka katika Bunge, Baraza la Wawakilishi na taasisi husika idadi ya watumishi kama itakavyoonekana inafaa kwa utekelezaji wa majukumu na mamlaka ya Bunge Maalum.” Kama kilivyo hivi sasa, kifungu hicho kinasomeka kama ifuatavyo: “Katibu wa Bunge Maalum baada ya kushauriana na Naibu Katibu wa Bunge Maalum watateua watumishi kutoka kwenye Bunge na Baraza la Wawakilishi kwa idadi watakayoona inafaa kwa ajili ya kutekeleza kwa ufanisi majukumu ya Bunge Maalum.”

   Mheshimiwa Spika,

   Kama inavyoonekana wazi, mabadiliko pekee yanayopendekezwa na Muswada ni maneno ‘taasisi husika.’ Maneno haya hayajatafsiriwa mahali popote katika Sheria, na Muswada uko kimya juu ya maana yake. Hata Maelezo ya Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria mbele ya Kamati yako kimya juu ya maneno hayo.

   Ukimya huu una mwangwi mkubwa. Kama pendekezo hili litakubaliwa, kutakuwa na uwezekano wa watumishi wa Bunge Maalum la Katiba kuteuliwa kutoka katika taasisi na idara mbali mbali za serikali, au hata taasisi zisizokuwa za kiserikali. Kwa sababu Bunge Maalum litatekeleza majukumu yake kwa muda maalum unaopendekezwa katika aya ya 6 ya Muswada huu, ni wazi watumishi hao watatumikia Bunge Maalum on secondment kutoka kwenye taasisi zao za mwanzo. Kwa maana hiyo, watumishi hao watawajibika kwa taasisi zao na wanaweza kutumiwa na taasisi zao kutoa taarifa au siri muhimu juu ya shughuli za Bunge Maalum kwa taasisi zao.

   Kwa upande mwingine, watumishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wamepewa kinga ya kikatiba inayowakataza kupokea maelekezo kutoka taasisi nyingine nje ya Bunge. Kama kifungu cha 4(3) cha Sheria ya Uendeshaji Bunge, Na. 14 ya 2008, inavyoweka wazi, katika utekelezaji wa majukumu yao, watumishi wa Bunge “... hawatapokea maelekezo kutoka mahali popote nje ya Utumishi (wa Bunge).” Katika mazingira haya, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba mapendekezo ya kurekebisha kifungu cha 24(4) hayakidhi matakwa ya uhuru wa Bunge Maalum na, kwa sababu hiyo, yasikubaliwe na Bunge lako tukufu.

   Mheshimiwa Spika,

   Kuna hoja kubwa zaidi juu ya pendekezo hili. Hoja hii inahusu mamlaka ya Katibu wa Bunge Maalum na Naibu wake kuteua watumishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Mapinduzi Zanzibar kuwa watumishi wa Bunge Maalum chini ya kifungu cha 24(4) cha Sheria, na pendekezo la Muswada la kukifanyia marekebisho.

   Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Bunge, Katibu wa Bunge hana mamlaka ya kuteua watumishi wa Bunge peke yake. Hayo, kwa mujibu wa Sheria hiyo, ni mamlaka ya pamoja kati ya Katibu na Tume ya Utumishi wa Bunge na utekelezaji wake unahitaji mashauriano kati ya vyombo hivyo viwili. Kwa sababu hiyo, na kwa kuzingatia utaratibu wa Sheria hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza watumishi wa Bunge Maalum wateuliwe kutoka miongoni mwa watumishi wa Bunge na Baraza la Wawakilishi baada ya mashauriano kati ya Katibu wa Bunge Maalum na Naibu wake pamoja na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum. Pendekezo hili lina faida kwamba watumishi wa Bunge Maalum watakuwa wameteuliwa na watawajibika kwa Bunge Maalum na siyo kwa taasisi nyingine nje ya Bunge Maalum. Kwa maana hiyo, pendekezo la Muswada juu ya uteuzi wa watumishi wa Bunge Maalum nje ya Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi Zanzibar halina umuhimu na linapaswa kukataliwa.

   TAFSIRI YA RASIMU YA KATIBA

   Mheshimiwa Spika,

   Muswada unapendekeza marekebisho ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inayohusu tafsiri ya maneno mbali mbali. Mapendekezo ya Muswada yanahusu tafsiri ya maneno ‘Rasimu ya Katiba’ na ‘Kanuni.’ Pendekezo la kutafsiri neno ‘Kanuni’ halina utatanishi wowote na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaliunga mkono. Kwa upande mwingine, Kambi Rasmi Upinzani Bungeni inapinga tafsiri inayopendekezwa ya maneno ‘Rasimu ya Katiba.’ Kwa mujibu wa aya ya 2 ya Muswada, maneno ‘Rasimu ya Katiba’ yatakuwa na maana ya “... Rasimu ya Katiba ambayo imetayarishwa na Tume kutokana na maoni na mapendekezo ya wananchi chini ya Sheria.”

   Pendekezo hili linapingana na maudhui ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Kwanza, pamoja na kwamba maoni ya wananchi ni chanzo muhimu cha ripoti ya Tume na Rasimu ya Katiba, maoni hayo sio chanzo pekee cha ripoti ya Tume na Rasimu ya Katiba. Kwa mujibu wa kifungu cha 17(4) cha Sheria, Tume inatakiwa kupitia “na kuchambua michango, mawazo, maoni, taarifa na mapendekezo yaliyokusanywa na kufanyiwa tathmini siku za nyuma....” Kifungu hicho kimeorodhesha nyaraka nyingi muhimu na za kihistoria ambazo zimejenga taswira ya kikatiba ya nchi yetu tangu uhuru wa Tanganyika mwaka 1961. Tume inawajibika kuzipitia na kuzichambua nyaraka zote hizo “katika kutekeleza majukumu yake chini ya Sheria hii....”

   Pili, Tume pia inawajibika kutumia “tafiti za kiuchambuzi na kitaalam zitakazofanywa na Tume”, na “nyaraka nyingine zozote ambazo Tume itaona ni muhimu.” Vyanzo vyote hivi vinatakiwa kutumika katika matayarisho ya Rasimu ya Katiba. Kwa maana hiyo, madhara ya mapendekezo ya Muswada juu ya tafsiri ya maneno ‘Rasimu ya Katiba’ ni ya wazi na mabaya. Kama yatakubaliwa na kuwa Sheria, vyanzo vyote hivi vya ripoti ya Tume na Rasimu ya Katiba vitakuwa redundant.

   Aidha, mapendekezo ya Tume na Rasimu ya Katiba yanayotokana na vyanzo hivyo yatakuwa kinyume cha Sheria na yatabidi yaondolewe kwenye ripoti na Rasimu ya Katiba. Kwa sababu hizi, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba maneno ‘Rasimu ya Katiba’ yatafsiriwe kumaanisha “... Rasimu ya Katiba ambayo imetayarishwa na Tume kwa mujibu wa Sheria hii.” Tafsiri hii inayopendekezwa inajumuisha maoni ya wananchi pamoja na vyanzo vingine vyote vya ripoti ya Tume na Rasimu ya Katiba vilivyoainishwa kwenye Sheria.

   UHALALISHAJI WA KATIBA MPYA

   Mheshimiwa Spika,

   Muswada unapendekeza marekebisho katika kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kinachohusu ‘uendeshaji wa kura ya maoni.’ Inapendekezwa kwamba kifungu hicho kifutwe na badala yake kiwekwe kifungu kipya kitakachosema kwamba “masharti yote yanayohusu uendeshaji wa kura ya maoni utawekwa na Sheria ya Kura ya Maoni.” Kwa vile tayari kuna Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni, 2013, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inakubaliana na pendekezo hili.

   Hata hivyo, kifungu cha 31 sio kifungu pekee katika Sheria hii chenye masharti ya uendeshaji wa kura ya maoni. Kuna vifungu vingine vinavyotaja au kuweka utaratibu wa kura ya maoni. Ukweli ni kwamba Sehemu ya Sita yote inayohusu ‘uhalalishaji wa Katiba Inayopendekezwa’ inahusika na masuala mbali mbali ya kura ya maoni. Vile vile, kifungu cha 4(1)(n) na (2) navyo pia vinataja kura ya maoni. Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, vifungu hivi pamoja na Sehemu ya Sita yote vinahitaji kurekebishwa kwa kufutwa.

   Mheshimiwa Spika,

   Muswada unapendekeza kufanya marekebisho katika kifungu cha 27(2) cha Sheria kinachohifadhi ‘uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge Maalum’ kwa kuweka kinga ya mashtaka dhidi ya wajumbe wa Bunge Maalum. Zaidi ya hayo, Muswada unapendekeza muda usiozidi siku sabini kwa Bunge Maalum kujadili Rasimu ya Katiba. Muda huo unaweza kuongezwa kwa siku nyingine zisizozidi ishirini kwa ridhaa ya Rais “baada ya kukubaliana na Rais wa Zanzibar....” Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inakubaliana na mapendekezo yote haya ya Muswada kwa caveat kwamba pendekezo la muda wa nyongeza lisiwekewe muda mahsusi. Hii ni kwa lengo la kuwezesha muda kuongezwa kulingana na hali halisi ya majadiliano ndani ya Bunge Maalum.

   JEDWALI LA MAREKEBISHO LA SERIKALI

   Mheshimiwa Spika,

   Serikali iliwasilisha Jedwali la Marekebisho ya Muswada huu mbele ya Kamati ikipendekeza marekebisho kadhaa katika Muswada na katika Sheria mama. Mapendekezo haya ni ya aina mbili. Kwanza, ni mapendekezo ya marekebisho ya Muswada uliosomwa mbele ya Bunge lako tukufu katika Bunge la Kumi na Moja, na ambayo yalijadiliwa na Kamati na wadau mbali mbali. Haya ni marekebisho yanayopendekezwa katika sehemu A, B na D ya Jedwali la Marekebisho ya Serikali. Marekebisho haya yanaenda sambamba na matakwa ya kanuni ya 84(3) na (4) ya Kanuni za Kudumu na kwa hiyo yanakubalika kikanuni.

   Kwa upande mwingine, marekebisho yanayopendekezwa katika sehemu C na E za Jedwali la Marekebisho ya Serikali ni mambo mapya ambayo hayakuwepo kwenye Muswada uliosomwa kwa Mara ya Kwanza katika Bunge lililopita. Marekebisho haya hayakujadiliwa na wadau wan je ya Bunge, na hayajulikani kwa Wabunge wasiokuwa wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala. Kwa sababu hiyo, marekebisho haya yanakiuka masharti ya kanuni ya 86(7) ya Kanuni za Kudumu inayoelekeza kwamba “mjadala wakati wa Muswada wa Sheria Kusomwa Mara ya Pili utahusu ubora na misingi ya Muswada huo tu.” Ili kulinda heshima ya Bunge lako tukufu, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inakuomba, Mheshimiwa Spika, utekeleze wajibu wako chini ya kanuni ya 5(2) ya Kanuni za Kudumu kwa kufutilia mbali sehemu C na E za Jedwali la Marekebisho ya Serikali kwa sababu zinakiuka matakwa ya kanuni tajwa ya Bunge lako tukufu.

   Mheshimiwa Spika,

   Sehemu C ya Jedwali la Marekebisho ya Serikali tunaokuomba uifutilie mbali inapendekeza kuongezwa kwa kifungu kipya cha 22A katika Sheria. Katika pendekezo la awali kuhusu kifungu hicho, ilikuwa inapendekezwa kumfanya Spika wa Bunge hili tukufu kuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum kwa ajili ya kutengeneza Kanuni za Kudumu za Bunge Maalum, na kwa ajili ya uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum. Baada ya Kamati kuhoji na kuelezwa kwamba Spika/Mwenyekiti wa Muda atakuwa pia na haki ya kugombea kuwa Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum na hivyo kutengeneza mgongano wa wazi wa maslahi, Kamati ilielekeza kwamba Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum watasimamia uchaguzi wa Mwenyekiti wa Muda ambaye hatakuwa na haki ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum. Hata hivyo, hoja ya msingi kwamba hili ni pendekezo jipya ambalo halikuwepo kwenye Muswada uliosomwa Mara ya Kwanza inabaki pale pale.

   Kuhusu sehemu E ya Jedwali la Marekebisho ya Serikali, sehemu hiyo inapendekeza kufifisha matakwa ya kifungu cha 26(2) cha Sheria inayoweka masharti ya kupitisha Katiba inayopendekezwa kwa theluthi mbili ya wajumbe wote wa Bunge Maalum wanaotoka Tanzania Bara na idadi hiyo hiyo ya wajumbe wanaotoka Zanzibar. Pendekezo jipya ni kupunguza idadi ya uungwaji mkono hadi wingi wa kawaida (simple majority) ya wajumbe wote wanaotoka Tanzania Bara na idadi hiyo hiyo ya wajumbe wanaotoka Zanzibar endapo Bunge Maalum litashindwa kupitisha Katiba inayopendekezwa kwa theluthi mbili baada ya kupiga kura mara mbili. Pendekezo hili nalo linakiuka matakwa ya kanuni ya 86(7) na linapaswa kuondolewa katika mjadala wa Muswada huu.

   MENGINEYO

   KUITISHWA TENA BUNGE MAALUM?

   Mheshimiwa Spika,

   Kuna maeneo mengine ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo, kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, yanahitaji kufanyiwa marekebisho ili kuwezesha utekelezaji bora wa Sheria hii. Eneo mojawapo ni masharti ya kifungu cha 28(2) yanayoruhusu Bunge Maalum kuitishwa tena baada ya kukamilisha majukumu yake kwa mujibu wa Sheria na kuvunjwa chini ya kifungu cha 28(1) cha Sheria hii.

   Kifungu cha 28(1) kinasema: “Baada ya kutunga Katiba Inayopendekezwa, masharti yatokanayo na mashrti ya mpito, Bunge Maalum litavunjwa na mamlaka ya kutunga masharti ya Katiba inayopendekezwa, masharti yatokanayo na masharti ya mpito yatakoma.” Kwa upande mwingine, kifungu cha 28(2) kinatengua masharti ya kifungu cha 28(1) kwa maneno yafuatayo: "Kuvunjwa na kukoma kwa mamlaka ya Bunge Maalum hakutachukuliwa kuwa kunaondoa mamlaka ya Rais kuliitisha tena Bunge hilo kwa lengo la kuboresha masharti yaliyomo kwenye Katiba inayopendekezwa.”

   Mheshimiwa Spika,

   Misingi mikuu ya tafsiri za kisheria inaelekeza kwamba chombo chenye mamlaka au majukumu ya kisheria ya kufanya jambo fulani kikishakamilisha kutekeleza mamlaka au majukumu yake hayo kinakuwa functus officio katika jambo hilo, yaani kinakuwa hakina mamlaka tena kisheria juu ya jambo hilo. Huu ndio msingi wa kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Athari ya kifungu cha 28(2) ni kulifufua kutoka katika wafu Bunge Maalum ambalo, kwa mujibu wa kifungu cha 28(1), linakuwa limekuwa functus officio baada ya kupitisha Katiba Mpya na masharti ya mpito. Na hii inafanywa na Rais ambaye – na chama cha siasa anachokiongoza – ni mdau mkubwa wa mchakato wa Katiba Mpya.

   Katika Maoni yetu wakati wa mjadala wa kupitishwa kwa Sheria hii mwezi Novemba 2011, tulisema yafuatayo juu ya kifungu hiki: “Maana halisi ya maneno haya ni kwamba Rais atakuwa na mamlaka ya kuita tena Bunge la Katiba ili lifanye marekebisho ya mambo ambayo yeye au serikali yake au chama chake hawayapendi katika Katiba Mpya kabla haijapigiwa kura ya maoni na wananchi! Kama chombo huru cha wananchi, Rais hawezi kujipa madaraka ya kupingana na kauli ya wananchi kupitia Bunge la Katiba.”

   Katika mapendekezo yake kwa timu ya Wataalam wa Serikali iliyoundwa kufuatia mkutano wa tarehe 26 Novemba, 2011 kati ya CHADEMA na Rais Jakaya Kikwete, CHADEMA ilipendekeza kwamba kifungu cha 28(2) kifutwe kabisa. Huu ni wakati muafaka kukiangalia upya kifungu hiki ambacho kinaweza kuleta mgogoro usiokuwa na sababu endapo Rais ataamua kuliitisha tena Bunge Maalum kwa sababu Serikali au chama chake hakikubaliani na Katiba Mpya iliyopitishwa na Bunge Maalum.

   MCHAKATO WA KATIBA YA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

   Mheshimiwa Spika,

   Tarehe 3 Juni, 2013 Tume ilichapisha Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 2013. Kwa kufanya hivyo, na kwa mujibu wa kifungu cha 18(5) cha Sheria, Tume imekamilisha jukumu lake la kwanza baada ya kukamilisha zoezi la kukusanya maoni ya Watanzania juu ya Katiba Mpya. Rasimu hii inapendekeza mambo mengi na muhimu kwa mustakbala mzima wa nchi yetu na tayari imezua mjadala mkali wa kitaifa. Mwanazuoni mmoja maarufu nchini ameyaita mapendekezo ya Rasimu ‘Mapinduzi ya Kimya Kimya’; wakati mwingine amehoji kama Rasimu hii ni ‘Mwarobaini au Sanduku la Pandora?’ Aidha, Profesa Issa G. Shivji ambaye pengine ni msomi maarufu wa masuala ya kikatiba katika sehemu hii ya Afrika, ameonyesha kile ambacho amekiita ‘Utatanishi na Ukimya Katika Rasimu ya Katiba Mpya.’

   Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kama ilivyo kwa wadau wengine ambao wamezungumzia Rasimu hiyo ya Katiba, eneo muhimu pengine kuliko yote ni muundo wa Jamhuri ya Muungano kama shirikisho lenye serikali tatu. Kwa sababu hiyo, Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume imejikita katika masuala ya Muungano tu. Na kwa mujibu wa Mwenyekiti wake, Tume haikushughulikia masuala yasiyokuwa ya Muungano ya Tanganyika na Zanzibar kwa sababu mambo hayo yanatakiwa kushughulikiwa na Katiba za Washirika wa Muungano.

   Kwa maana hiyo, masuala haya sasa itabidi yashughulikiwe kwa utaratibu mwingine wa kisheria Zanzibar na Tanganyika vile vile, ambao utakuwa tofauti na utaratibu uliowekwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Kutokana na mapendekezo ya Rasimu ya Katiba, mchakato wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano hautakamilika bila ya kuwepo, na kukamilika, kwa mchakato wa Katiba Mpya kwa masuala yasiyokuwa ya Muungano ya Tanganyika na ya Zanzibar.

   Mheshimiwa Spika,

   Kuanza na kukamilika kwa mchakato wa Katiba Mpya kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano ya Tanganyika na Zanzibar ni suala muhimu kwa muundo wowote wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano au hata bila Muungano kuwepo, kwa sababu zifuatazo. Kwanza, hata kama muundo wa Muungano utakuwa wa serikali moja, au mbili za sasa, au tatu zinazopendekezwa na Rasimu, ni lazima masuala yote yanayoihusu Tanganyika yaingizwe kwenye mchakato wa Katiba Mpya. Hii ni kwa sababu Rasimu inahusu masuala saba ya Muungano tu, na Zanzibar ina Katiba yake tayari. Pili, hata kama wananchi wa Tanzania watakataa kuendelea na Muungano wa aina yoyote na kudai uhuru kamili wa Washirika wa Muungano, bado masuala ya Katiba Mpya ya Tanganyika na Zanzibar yatahitajika kufanyiwa kazi. Tatu, bila masuala ya Tanganyika kuamuliwa katika Katiba Mpya, mchakato mzima hautakamilika, na kwa maana hiyo, hakuwezi kukawa na uchaguzi wowote wa Jamhuri ya Muungano kwa upande wa Tanganyika.

   Kwa vyovyote vile, constitutional gridlock hii lazima ipatiwe suluhisho. Kwa sababu hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba mchakato wa Katiba Mpya ya Tanganyika na marekebisho ya Katiba ya Zanzibar, 1984 uanze mara moja ili uendane sambamba na mchakato wa Katiba Mpya ya Jambhuri ya Muungano. Kwa vyovyote vile, kwa maoni yetu, Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kama ilivyo sasa haiwezi kutumika kwa ajili ya mchakato huo kwa sababu sheria hiyo ilitungwa kwa ajili ya mchakato wa Katiba ya Muungano tu.

   Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliundwa kwa ajili ya mchakato wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Na Tume yenyewe imekiri kwamba haikujishughulisha na masuala yasiyokuwa ya Muungano kwa sababu hayakuwa sehemu ya majukumu iliyokabidhiwa kisheria. Kwa muundo wake, Tume hiyo haiwezi kujibadilisha na kuwa Tume ya Katiba ya Tanganyika. Kwa maana hiyo, mchakato wa Katiba ya Tanganyika unatakiwa kuwekewa utaratibu mpya na tofauti kabisa wa kisheria na wa kitaasisi. Hii itahitaji kutungwa kwa sheria mpya kwa ajili ya mchakato huo.

   Sambamba na mchakato wa Katiba ya Tanganyika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kuanzishwa kwa mjadala juu ya masuala ya mpito kwa sababu kuna uwezekano mkubwa kwamba Katiba Mpya, ya Muungano peke yake au ya Muungano na za Washirika wake, yaani Tanganyika na Zanzibar, zisiwe tayari kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015. Au hata kama zitakuwa tayari kabla ya Uchaguzi Mkuu, kuna uwezekano mabadiliko makubwa ya kisheria na ya kitaasisi yatakayohitajika kwa ajili ya utekelezaji wa Katiba Mpya, yasiwe tayari kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao. Kwa kuangalia mfano wa Kenya, Katiba Mpya ya nchi hiyo ilikamilika mwezi Agosti, 2010. Hata hivyo, mabadiliko mbali mbali ya kisheria na kitaasisi kwa ajili ya utekelezaji wa Katiba hiyo yalichukua zaidi ya miaka miwili na nusu hadi Uchaguzi Mkuu wa mwezi Machi, 2013.

   Ikumbukwe kuwa Kenya haikuwa na suala la Muungano kama Tanzania. Sisi tuna Muungano wa muundo ambao upande mmoja wa Muungano huo una dola yenye Katiba na taasisi kamili za dola, wakati upande mwingine hauna dola wala Katiba na taasisi kamili za dola. Hii ina maana kwamba maandalizi yetu ya kisheria na kitaasisi yanaweza kuhitaji muda mrefu zaidi kuliko ilivyokuwa kwa Kenya. Hatuna budi kuanza kuyafikiria na kuyajadili mambo haya muhimu sasa.

    ---------------------------------------
   TUNDU A.M. LISSU
   WAZIRI KIVULI & MSEMAJI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

   0 0


   0 0

   Na James Festo,

   Zaidi ya wanafunzi mia mbili wameacha shule  sababu zisizojulikana katika shule ya sekondari ikuwo iliyopo katika wilaya ya Makete Mkoani njombe Katika Kipindi Kuanzia mwezi januari 2012 hadi Mwezi agasti mwaka huu.

   Hayo yamebainika wakati akiwasilisha taarifa  ya maendeleo ya shule hiyo kwa   mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilayani hapa bw Francis Chaula alipokuwa kwenye ziara yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo  katika
   kata ya kigala na ikuwo iliyomo kwenye irani ya uchaguzi 2010/2015, ambapo makamu mkuu wa chule hiyo mwalimu Fred Mbopa   amesema kuwa wananfunzi hao haijulikani wameacha shule kwa sababu gani.

   Pia makam mkuu wa shule hiyo  bw Mbopa amelezea mahusiano duni baina wazazi na walimu hali inayopelekea kushindwa kudhibiti hali hiyo na Wanafunzi waliopo shuleni hivi sasa ni 206 kati ya 508 ambao walitakiwa kuwepo shuleni
   hapo.

   Aidha wanafunzi hao wakizungumza na katibu wa wazazi wa chama cha mapinduzi bw Adam Mwampashi na kutoa sababu za wenzao kuacha shule walisema  kuwa wameacha shule kwa sababu ya mazingira magumu hali inayopelekea kushindwa kuchangia michango mbalimbali kutokana na hali ngumu kimaisha waliyonayo wazazi .

   Aidha Wanafunzi wakiendelea Kutoa sababu za wanafunzi wenzao Kuacha Shule walisema kuwa   wanafunzi hao walisema kuwa wanapata chakula tofauti na michango  wanayochangia shuleni hapo na wanafunzi wenyewe kutopenda elimu.

   Hata hivyo kwa Upande wake afisa Elimu sekondari wa halmashauri ya wilaya ya makete bw Jacob Mena alionyesha kutounga mkono  kwa idadi ya wanafunzi waliotajwa makamu wa shule hiyo.

   sijajua idadi hiyo iliyotajwa je imeunganishwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao hawajaripoti kwa mwaka huu,alisema bw Bw Mena . Pia amewataka wazazi  wa watoto wanaosoma katika shule hiyo kutoa ushirikiano kwa walimu ili kuweza kuzuia suala hilo lisiweze kuendelea na
   walioacha shule kurejea na kuendelea na masomo.

   Akizungumzia kwa upande wa wanafunzi hao kutambua wajibu wao kama wanafunzi hao ikiwa pamoja na kuzitumia fursa za nafasi za masomo ya  sekondari  kwani ndio mkombozi pekee aliyebaki kwao.

   Katika hatua nyingine  Afisa huyo ameitaja shule ya Sekondari ya Ipepo kuwa ndio shule ambayo ina idadi kubwa ya wanafunzi wa kidato cha kwanza  ambao hawakuweza kuripoti kuanza masomo hayo  ya kidato cha kwanza ambapo katika wilaya nzima zaidi ya wanafunzi mia nne hawakuripoti idadi ambayo ni kubwa ikilinganishwa na miaka mingine.

   Akielezea njia ambazo wanakabiliana .na tatizo hilo afisa huyo amesema kuwa kwa sasa wamekwisha mpeleka mwalimu mkuu katika shule hiyo na kumuagiza kuzungukia katika  vijiji vya jirani na shule hiyo ili kuweza kujua sababu
   zilizopelekea tatizo hilo katika shule hiyo.

   0 0

    Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifunga Kongamano la Kimataifa kuhusu Historia ya Ustaarabu wa Kiislamu Afrika Mashariki kwa niaba ya makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Hoteli ya lagema, Nungwi.
    Muhadhir Hajjat Aiseta Aisha toka Uganda akiwasilisha mada katika Kongamano la kimataifa kuhusu historia ya kiislam Afrika Mashariki  katika Hoteli ya Lagema Kaskazini Unguja. 
    Baadhi ya washiriki  wakifuatilia mada zilizowasilishwa katika Kongamano la kimataifa kuhusu historia ya ustaarabu wa Kiislam katika Afrika Mashariki kwenye ukumbi wa Hoteli ya Lagema Nungwi kaskazini Unguja.
    Muhadhir Amour Abdalla wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) akiwasilisha mada ya athari ya utandawazi katika Kongamano la Kimataifa kuhusu historia ya ustaarabu wa Kiislam Afrika Mashariki, katika ukumbi wa Hoteli ya Lagema Nungwi kaskazini Unguja.
    Mwenyekiti wa Mamlaka ya kutunza Nyaraka, Ufalme wa Oman Dkt. Hamadi Moh'd Al-Dhawiani, akitoa  mapendekezo katika ufungaji wa Kongamano la Kimataifa kuhusu historia ya ustaarabu wa Kiislam katika Afrika Mashariki katika ukumbi wa Hoteli ya Lagema Nungwi kaskazini Unguja.
   Picha ya pamoja kati ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa kuhusu Historia ya Ustaarabu wa kiislam  Afrika Mashariki katika Hoteli ya lagema Nungwi. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

   0 0

    Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya bilionea wa madini Erasto Msuya,Sharifu Mohamed na Musa Mangu wakiwa mahakamani.
    Ndugu wa marehemu Erasto Msuya wakiwa mahakamani.
    Ndugu wa marehemu Erasto Msuya wakiwa mahakamani.
    Wakazi wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha walifurika mahakamani kusikiliza kesi hiyo.
    Mtuhumiwa Sharifu Mohamed akiteta jambo na wakili wake Mhe. Hudson Ndusyepo mara baada ya kuhairishwa kwa kesi hiyo .

    Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja Msuya baada ya  kupoteza fahamu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi.
    Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja Msuya baada ya kupoteza fahamu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi.
    Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja Msuya akiangua kilio na baadae kupoteza fahamu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi.
    Mdogo wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Bahati Msuya akiwa anasaidiwa kupelekwa kwenye gari mara baada ya kuahirishwa kwa kesi
   hiyo.
    Mdogo wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Bahati Msuya akiwa anasaidiwa kupelekwa kwenye gari mara baada ya kuahirishwa kwa kesi
   hiyo.
    Mama mzazi wa marehemu Erasto akisindikizwa na wanandugu kwenda kwenye gari la familia.
   Umati mkubwa wa wananchi ulifurika mahakamani hapo 
   Picha na  Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi.

  older | 1 | .... | 152 | 153 | (Page 154) | 155 | 156 | .... | 1897 | newer